Simulizi: Lisa

Simulizi: Lisa

Wapendwa ni usiku mtulivu pande hizi lakini ili uwe mzuri zaidi kumekosekana vipande kadhaa vya simulizi yetu pendwa "Lisa" hima kwa mwandishi ikikupendeza naomba utupe mwendelezo[emoji39][emoji39]
 
Nipo standby ikiletwa tu naidaka. Story nzuri sana
 
Sura ya: 680

Uso wa Cindy ulipauka hasa kwa kuiona midomo ya Chester iliyotapakaa damu na macho yake yaliyokuwa yakiungua kwa uchu. Pia aliweza kujua kutoka kwa ‘mtarimbo’ wake uliokuwa umetuna kwamba alikuwa amesisimka.
Cindy hakuwa mjinga. Hakuweza kujizuia kwa ukweli kwamba Chester alikuwa akimpuuza siku za karibuni bila kujali jinsi alivyomtongoza wakati huo. Hata alikuwa na shaka kwamba amerudia tabia yake ya kuwa na wanawake wengi kama hapo awali. Kwa wakati huo, aliamini. Haikuwa kwa sababu Chester alipendezwa na wanawake bali kwa sababu tu hakuwa na hamu naye.
Lakini, bila kutarajia, alifurahi sana alipokuwa na Eliza. Kwa wivu, alihisi kama kifua kitamlipuka. Je, Eliza angeweza kulinganishwaje naye? Eliza lazima awe alitumia mbinu za hila kumtongoza Chester.
B*tch! Ikiwa Eliza alikuwa amesimama mbele yake, Cindy angekuwa tayari amempiga makofi mawili ili kuonyesha hasira yake.
Baada ya kufahamu kinachoendelea, Ada, msaidizi wa Cindy alipigwa na butwaa huku akibaki amesimama nyuma ya Cindy.
Chester, ambaye alihusika katika suala hilo, aliweka miguu yake juu ya meza ya kahawa na kuwasha sigara. Alionekana kuchukizwa na ujio wa Cindy. “Kwanini upo hapa?”
“Unapaswa kuondoka.” Cindy alimpiga jicho Ada.
Ada aliitikia kwa kichwa na kuhema. Alikuwa chini ya hisia kwamba Chester alikuwa na wasiwasi sana kuhusu Cindy, lakini ikawa kwamba haikuwa hivyo. Iwapo Chester angemjali sana Cindy, asingekuwa mtulivu na asiyejali bila hata hisia ya hofu baada ya kushikwa na hatia.
Baada ya mlango wa ofisi kufungwa, macho ya Cindy yalibadilika na kuwa mekundu huku machozi yakimtoka. “Chester, kwanini hukunitafuta kama ulitaka kukidhi mahitaji yako—”
“Wewe?” Chester alimkatisha huku akimtupia jicho la mawe. "Samahani, siwezi kulala na wewe."
Akiwa ameumizwa na maneno yake, Cindy alipigwa na butwaa na uso wake ukageuka kuwa wa kinyonge. Nini? Hakuweza kulala naye, kumbe hakuwa na tatizo na Eliza?
Chester aliinua macho yake na kumtazama kwa baridi. "Bado unaota, huh? Unajua kabisa kwanini nilikubali kukuoa. Ukitaka kufuatilia suala hili, ninaweza kukuvua hadhi yako kama mke wangu mtarajiwa wakati wowote.”
“Hapana... Hapana...” Midomo ya Cindy ilitetemeka, lakini bado hakuridhika. “Mimi tu... nakupenda sana tu. siwezi kuvumilia.”
“Kama huwezi kustahimili, niache basi. Vinginevyo, nitakupa moyo mwingine ili uweze kustahimili, sawa?" Chester alimkumbusha kwa tabasamu lisilo na furaha.
Cindy akatetemeka. Huenda wengine wasiamini kwamba Chester alikuwa mkatili, lakini alikuwa mkatili kuliko alivyoonekana.
Mtu huyu alikuwa tofauti alipokuwa na Rodney na Alvin. Hakika, alikuwa mtu asiye na moyo, asiyejali, na hatari.
“Potelea mbali.” Maneno hayo yalimponyoka Chester kwenye midomo myembamba. Cindy akasaga meno. “Sawa, nitaondoka.”
Tone la machozi lilimdondoka. Alipogeuka na kuelekea mlangoni, alitazama tena. “Chester, najua huna furaha na mimi na haishangazi kwamba unatamani kuwa na mwanamke mwingine, lakini natumai utamtafuta mwanamke mwingine isipokuwa Eliza. Eliza sio rahisi kama unavyofikiria. Zaidi ya hayo, hastahili kuwa na wewe.”
“Unajaribu kusema nini?” Chester alikodoa macho. "Kweli, labda haujui hii."
Cindy akauma mdomo. "Eliza alikuwa mwanamke wa Monte Karanja. Alipokuwa chuo kikuu, akawa mwanamke wake kwa miaka minne. Eliza alifanikiwa kusaini mkataba na Felix Media kwa sababu tu Monte alivutana na Shedrick. Lakini utendaji wake ulikuwa duni sana katika miaka michache ya kwanza. Hata baada ya Monte kutumia pesa nyingi juu yake, alishindwa kumfanya kuwa maarufu.
"Baadaye, akina Karanja walimfanya Monte amchumbie na mwanamke mchanga kutoka kwa familia mashuhuri kama wao, walimdharau Eliza kutokana na historia yake. Kwa hivyo, Eliza aliachwa na Monte miaka miwili iliyopita.
Monte Karanja? Macho ya Chester yalikuwa na baridi ya kutisha.
Cindy akatetemeka. ” Sikudanganyi. Mkurugenzi Mutui na watu wengi wanajua kuhusu hili pia. ”
 
“Sawa, nimeelewa. Potelea mbali.” Chester aliongea bila huruma.
Wale ambao hawakumfahamu vizuri wangefikiri kwamba Chester hakusumbuliwa kabisa na suala hilo. Hata hivyo, Cindy alimuelewa vyema, ukizingatia kwamba alikuwa naye kwa muda mrefu. Kadiri Chester alivyokasirika zaidi ndivyo alivyoonekana kutojali zaidi. Cindy hakutarajia kwamba Chester angejali sana kuhusu Eliza. Alianza kusaga meno.

Shooting ya filamu ya Mke Mwenza ilikuwa karibu kuanza, na Eliza angeigiza kama Mke Mwenza, na Cindy angeigiza kama mke wa kwanza. Bila shaka Cindy angechomoa hila fulani kwenye mkono wake ili kumfanya Eliza atambue matokeo ya kujithamini kupita kiasi na kumwendea mume wake.
Muda mfupi baada ya Cindy kuondoka, Chester alipiga teke meza ya kahawa kwa nguvu. Kwa teke lake, kila kitu kwenye meza kubwa ya kahawa kiliharibika.
Uso wake mzuri ulitiwa giza, huku macho yake yakionekana kuwa ya ajabu kwa hisia zisizoeleweka. Shedrick aliingia ndani na kuziona zile damu pembeni ya mdomo wa Chester. Alishtuka kwa mshtuko kabla ya kufoka. “Ulisema unataka kuongea na Eliza ofisini kwangu. Tsk, sasa ninajiuliza ikiwa ulikuwa unazungumza naye au unamnyonya damu. Ni hali mbaya kama nini. Kama ningelijua hili mapema, ningekuandalia kondomu.”
Chester alimtazama kwa ubaridi. "Nilisikia Eliza alikuwa mwanamke wa Monte."
Shedrick alipigwa na butwaa kwa muda kabla hajatikisa kichwa. “Ndiyo.”
Mara Shedrick alipojibu, aliweza kuhisi kabisa hali ya hewa ndani ya ofisi ile ilikuwa ya baridi kana kwamba kiyoyozi kimewashwa.
“Mbona…sikusikia ukisema hapo awali?” Macho ya Chester yaliangaza kwa chuki kubwa.
“Unapocheza na wanawake... hujawahi kusumbuliwa ikiwa ni mara yao ya kwanza. Sivyo?" Shedrick aliongea.
Chester alishindwa cha kusema. Kwa kweli, hakuwahi kuwa na wasiwasi juu ya hili. Lakini, wazo la kwamba Eliza alikuwa na mtu mwingine lilipomjia, angekuwa na huzuni kwa sababu fulani. Kutokana na majivuno yake, hakuamini kama Eliza aliwahi kuwa na mwanamume hapo awali. Baada ya yote, mwanamke huyu alikuwa na kiburi sana.

“Sawa. Ni vizuri kwamba hujihusishi naye,” Shedrick alisema ghafla, “Ingawa hii ilikuwa miaka miwili iliyopita, Monte alimbembeleza kama mtoto wakati huo. Eliza alionekana kumpenda Monte na hata kujaribu kujiua kwa ajili yake miaka miwili iliyopita "
“Kujiua?" Chester alishangaa. Kulingana na tabia ya Eliza, hakuwahi kutarajia kuwa angekuwa aina ya mtu ambaye angejaribu kujiua.
“Umesikia vizuri.” Shedrick alijibu. “Wakala wake alisema kwamba alidhamiria kujiua wakati huo baada ya Monte kupangiwa mke mwingine na wazazi wake, na angeweza kupoteza maisha yake, na aliponea chupuchupu. Nilipomtembelea hospitalini baadaye, niligongana na Monte. Monte alisema kwamba alijaribu kujiua kimakusudi kwa matumaini kwamba angebadilisha mawazo yake. Monte alikasirika sana juu yake. Baada ya kufika nyumbani kutoka hospitalini, wazazi wake walipanga afunge ndoa.”
Shedrick alipokuwa akieleza, alimkabidhi Chester sigara. Chester akaichukua na kucheza nayo. Kope zake ndefu ziliweka kivuli chini ya macho yake. Alionekana kutabasamu, lakini sura ya chuki machoni mwake ilizidi kuimarika. Hakutarajia kwamba Eliza angekuwa mwanamke wa kudharauliwa, asiye na maana.
"Baadaye, alipopona, Eliza alionekana kubadilika na kuwa mtu tofauti.” Shedrick alicheka. “Alikua mwenye bidii, mwenye kujituma, na asiyejali. Hata uigizaji wake ukawa mzuri. Hmm, nampenda sana Eliza wa sasa. Angalau, yeye ndiye msanii anayeleta faida nyingi zaidi kwa kampuni.
“Inatosha. Usiniambie kitu kingine chochote kumhusu. ” Chester aliinuka kwa chuki.
Hapo awali, alimwona Eliza kuwa wa kipekee, lakini hakuwa na hisia kwake tena. Eliza alikuwa mwanamke mjanja sana. Ikiwa angejihusisha naye, angekuwa katika matatizo makubwa. Kwa namna fulani, alikuwa katika hali mbaya. Kifua chake kilionekana kujawa na uhasama.

Sura ya: 681


Baada ya kuingia kwenye gari, simu yake iliita. Ilikuwa ni simu kutoka kwa Rodney. “Nimekuomba uongee na Eliza, imekuwaje?”
"Nilisahau," Chester alisema kwa hasira, "usimtaje mwanamke huyu tena."
 
"Nini tatizo?" Rodney hakuweza kumjua Chester.
"Baada ya kuuliza juu ya Eliza, niligundua kuwa alikuwa na wakati mgumu. Afadhali umzuie Pamela asijichanganye naye sana.” Chester alikata simu mara baada ya kumaliza kuongea. Kisha akatoa sigara na kuvuta kwa raha ndani ya gari.
Mbali na harufu ya moshi, harufu ya midomo ya Eliza ilikuwa bado ikiendelea kutanda mdomoni mwake. Ilikuwa tamu sana. lakini, aliiona kuwa tamu na ya kuchukiza kwa wakati huu.
•••
Saa tano asubuhi, Alvin alikodi katapila na kuliendesha hadi kwenye jumba lake la kifahari alilomhonga Sarah. Alianza kwa kuchimbua maua yote ambayo Sarah alikuwa ameotesha.
Kusikia makelele hayo, Sarah akatoka nje huku akiwa amepauka. Baada kuona kilichokuwa kikiendelea, alikaribia kuvunjika. "Alvin, unafanya nini?" Maua aliyapenda zaidi, lakini yalikuwa yaking’olewa yote kikatili.
Alvin alikuwa amevaa miwani ya jua. Alishusha dirisha na kuutoa uso wake wa kupendeza usiojali nje. “Bila shaka ninaharibu. Jana, hakimu alisema kwamba lazima unirudishe jumba hili. Nilipokumbuka kwamba umekuwa ukikaa mahali hapa ambapo palipokuwa nyumbani kwangu na kwa Lisa kwa miaka mingi, ninahisi kuchukizwa sana hivi kwamba nataka kupaharibu mara moja.”
“Alvin, wewe...” Sarah alianza kutetemeka kwa hasira.
"Mahali hapa si mali yako tena." Alvin aliongeza, “Hapana, haijawahi kuwa mali yako. Fungasha vitu vyako na utoke sasa hivi."
“Mahakama imenipa wiki moja. Huna haki ya kunifanya niondoke sasa,” Sarah alifoka kwa kutoridhika.
“Sawa. Unaweza kukaa hapa kwa wiki moja nyingine, lakini mahakama haikusema kwamba siwezi kuharibu mahali hapa. Ni sawa ikiwa utaendelea kukaa hapa mradi tu usijali kulala kwenye vifusi.” Alvin alikoroma kabla hajalivulumisha katapila kuelekea ndani.
Mkonga wa katapila uligonga kwenye dirisha, na kusababisha kishindo kikubwa. Kwa hiyo, dirisha lote lilivunjika.
Sarah akawa anafadhaika. “Acha, Alvin! Basi, imetosha. Nipe saa moja niondoke.”
Kulikuwa na vitu vingi vya thamani ndani, nguo, na vito ndani. Asingekuwa na wakati wa kutosha kuvipakia vyote.
"Nitakupa ... dakika kumi zaidi," Alvin alidhihaki.
“Wewe...”
“Zimesalia dakika tisa.” Alvin aliinua uso wake.
Damu ya Sarah ilikuwa ikichemka. Aliogopa kusema kitu tena kwani angebakiwa na dakika nane tu. Mara moja alipanda ghorofani na kuingiza vito vya gharama kubwa zaidi chumbani ndani ya sanduku. Kabla hajamaliza kufungasha kila kitu, katapila lilikuwa limeingia sebuleni.
"Alvin, wewe ni mwendawazimu sana!" Sarah alitoka nje ya chumba cha kulala mbio kwa hasira.
“Muda umekwisha.” Alvin alipoona sanduku lile mkononi mwake na mkufu wa gharama kubwa uliokuwa umebanwa kwenye zipu, macho yake yalimtoka kwa chuki. Alikuwa mtu wa kufuja pesa kiasi gani? Alichukizwa sana na ukweli kwamba alikuwa mpenzi wake wa kwanza.
Kwa hasira, katapila liliendelea kuharibu kila mahali, punde, jumba zima liliharibiwa. Sarah alilitazama tukio hilo kwa macho ya damu huku akiwa amesimama nje.
'Alvin Kimaro, wewe subiri.’ Asingesahau kamwe fedheha aliyopata siku hiyo. Aliapa kumuweka kuzimu. Alichukua koti na kuondoka mahali hapo na nywele zilizovurugika.

Baada ya Alvin kumaliza kuharibu kila mahali, alimpigia Lisa simu ya video.
"Angalia, Lisa. Niliharibu jumba lote alokuwa anaishi Sarah.”
Lisa aliyekuwa ofisini alipigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa baada ya kumuona Alvin akiwa amesimama katikati ya magofu. Labda hakutarajia jumba lile kuharibiwa kwa kiwango hicho.
"Wewe una wazimu sana, huh?" Hakuwa na la kusema. “Ulisema unaenda kazini asubuhi ya leo, lakini ukaishia kubomoa jumba. Uliiharibu vipi?”
"Na katapila."
"Unajua jinsi ya kuendesha katapila?" Lisa alipigwa na butwaa.
 
“Mm. Nimejifunza asubuhi ya leo.” Alvin alitabasamu kwa unyonge.
Lisa alishindwa cha kusema. Aliposema hivyo, je, alifikiria hisia za wale wanaojifunza jinsi ya kuendesha katapila? Kwa kawaida wangetumia nusu mwaka, au angalau miezi mitatu hadi minne kukamilisha mafunzo.
“Hongera sana. Umepata ujuzi mwingine wa kutengeneza pesa,” Lisa alimtania huku akicheka.
“Lisa, nilitaka kuharibu eneo hili mwenyewe kwa sababu nyumba yetu ilichafuliwa na Sarah. Sitaki iwe kichefuchefu kwako,” Alvin alisema kwa bidii.
Macho ya Lisa yalidhihirisha ladha ya upole. “Sarah yuko wapi?”
“Nilimfukuza. Alipakia vito vya thamani kwenye sanduku kabla ya kuondoka.” Uso wa Alvin ulionyesha kejeli na huzuni. “... Kwa nini nilikutana na mwanamke wa namna hiyo enzi hizo? Ninahisi kuchukizwa ninapokumbuka kuwa alikuwa mpenzi wangu.”
"Fikiria juu yangu na hautajisikia kuchukizwa, basi." Lisa alipepesa macho kwa utani.
Alvin aliyeyuka. "Lisa, kula chakula cha mchana nami leo, sawa? Ninakukosa rohoni."
"Tumeachana chini ya masaa mawili yaliyopita." Huku akimtazama kwa upendo, Lisa uso wake ulikunjamana.
"Lakini Nakutamani. Usipokuja, nitakuja ofisini kwako na kula nawe,” Alvin alisema kwa tabasamu.
“Chakula cha ofisini kwetu ni hivyo...”
“Haijalishi. Chochote kitakuwa kitamu maadamu niko na wewe.” Alvin hakuweza kusubiri kumuona.

Uso wa Lisa ulikuwa unawaka. Baada ya kukata simu, alitulia ili kupunguza dukuduku moyoni mwake. Kisha, akamwomba Ambah aingie. “Uliza jikoni kuandaa sehemu ya ziada ya chakula. Alvin atakuwa hapa kula chakula cha mchana.”
Harvey alikosa la kusema. "Bwana Kimaro amekukomalia sana."
“Ndiyo.” Tabasamu tamu likatanda usoni mwa Lisa.
Labda hakuna mtu ambaye angetarajia Alvin kuwa mshikaji sana wakati yuko kwenye uhusiano.
•••
Wakati huohuo, Sarah hatimaye alionekana mbele ya Kelvin baada ya mapambano fulani. Kwa wakati huu, hakuwa na chochote kilichobaki.
Jumba lilikuwa limekwenda. Zaidi ya hayo, ilimbidi kurudisha bilioni 1o za Alvin. Hakuwahi kufikiria hivyo, Asingekuwa na mtu mwingine wa kumtegemea isipokuwa Kelvin. Hata hivyo, mara tu alipoona hali ya huzuni ya Kelvin, alikata tamaa. Alijua kwamba Kelvin alikuwa mkatili na asiyejali kuliko yeye. Alikuwa akimweka karibu naye muda wote tu kwa sababu alikuwa bado anatumika.
“Nilifikiri ulikuwa kibaraka cha manufaa, lakini bila kutarajia...” Kelvin akatikisa kichwa. Ni wazi kwamba alikatishwa tamaa sana na Sara. "Hata umepoteza bilioni 1o sasa. Wewe ni tofauti gani na mwanamke wa kawaida huko nje?"
Sarah akauma meno. “Mimi ni tofauti. Namchukia Alvin, na ninataka kumuua.”
Kelvin aliinua uso wake kwa uzito. Sarah akamsogelea taratibu. “Nina suluhu, bila shaka. Nilipomlaza hapo awali, nilimfanyia kitu.”
Kelvin aliyakazia macho yake meusi taratibu. “Kweli?”
“Hakika.” Sarah akaitikia kwa kichwa. "Amini usiami ataanguka chini siku moja. Nadhani utafurahi kusikia hivyo, sivyo? Ingawa hamjaachana na Lisa, Alvin na Lisa tayari wamejitokeza pamoja hadharani. Wanalala hata usiku pamoja. Je, hujisikii vibaya moyoni?”
Kelvin alikunja ngumi. Baada ya kuchochewa na maneno yake, uso wake ukawa mkali. “Sarah, nakupa nafasi ya mwisho kunionyesha thamani yako. ”
“Sawa.” Sarah akasaga meno. “Kabla ya hili, nataka Thomas afe.”
Kelvin aliinua uso wake na kumtazama. Kisha akatabasamu. “Je! unajua ninachokipenda zaidi kwako? Wewe ni mwanamke wa pili katili ambaye nimekutana naye. Una roho mbaya sana hivi kwamba unaweza kufikia hatua ya kuua familia yako mwenyewe.”
"Ni kwa sababu alinisaliti." Sarah alipandwa na hasira. "Yule d*ckhead alidai kuwa nilimteka nyara wakati hata sikufanya hivyo."
"Kwa kweli, jambo hili lina mashaka kidogo. Nadhani ulikuwa mtego wa Alvin.” Kelvin alikunja uso. "Baada ya kusema hivyo, Thomas sasa yuko chini ya ulinzi wa familia ya Choka, kwa hivyo siwezi kufanya chochote juu yake."
Sarah aliuma mdomo wake bila kuridhika.
"Lakini hii ni ya muda tu," Kelvin aliongeza bila kujali, "Baada ya miezi miwili zaidi, Alvin, Chester, na wengine wote hawataweza kunifanya chochote."

Sura ya: 682
 
Kwa hofu, Sarah akampiga jicho kali na kumtazama kwa haraka. Kwa kadiri alivyojua, Kelvin kwa sasa alikuwa chini ya huruma ya familia ya Choka na kwenye kona kali. Je, angefanya nini ambacho kinaweza hata kumfanya Chester ashindwe kukabiliana naye?
Alifungua kinywa chake kwa kusitasita. "Huenda usijue uwezo wa kweli wa familia ya Choka. Hata kama Mason atakabiliana na familia ya Choka, hatakuwa na makali juu yao...”
“Najua. Hivi karibuni, utaelewa. ” Kelvin alitoa tabasamu baridi.
Akiwa ameingiwa na mawazo, Sarah akauliza ghafla, “Ulisema mimi ni mwanamke wa pili katili zaidi uliyekutana naye, kwa hiyo unamaanisha kwamba kuna mwanamke mwingine ambaye ni mkatili kuliko mimi?
"Nadhani nyote wawili hamna huruma sawa. Pia... Kwa bahati mbaya, anawachukia Alvin na Lisa pia,” Kelvin alijibu kwa tabasamu lisilo na furaha.
Sarah mara moja akanyamaza. Mwanamke huyu anaweza kuwa nani? Lakini, kwa kuwa walikuwa na maadui sawa, wangeweza kufanya kazi pamoja katika siku zijazo.
•••
Lubumbashi Kongo. Casino Royale Resto Terrasse.
Zamani likiitwa jiji la Elisabethville, Lubumbashi ni jiji la pili kwa ukubwa nchini Kongo, na pia ni bandari ya nchi kavu. Mtu tajiri zaidi aliyekuwa anayedhibiti jiji hili aliitwa Titus Tshombe. Sio tu kwamba familia ya Tshombe ilikuwa na udhibiti wa mauzo ya madini ya Colbat ulimwenguni, lakini pia ilidhibiti migodi ya chuma, copper na Zinc huko Katanga, walimiliki mahoteli makubwa ya kifahari karibu miji mikubwa yote nchini Kongo, na mnyororo wa mabenki yao pia ulikuwa na matawi hadi Ulaya.
Kwa wakati huo, mwanamke wa Kitanzania tayari alikuwa ameshinda pesa nyingi kwa kucheza kamari siku tatu mfululizo kwenye kasino kubwa zaidi ndani ya jiji la Lubumbashi, Casino Royale Resto Terrasse, iliyomilikiwa na familia ya Tshombe.
Nywele nene, za rangi ya hudhurungi na sifa nzuri za mwanamke huyu zilisababisha wanaume wengi kutoka sehemu mbalimbali za dunia waliokuwa wakicheza kamari ndani ya Casino hilo kumlemea. Mwanamke huyu hakuwa mwingine ila Lina Jones, ambaye alikuwa ametoweka kwa miaka mingi.
"Samahani, nimeshinda tena." Lina alifungua kadi yake ya mwisho kwa namna ya moyo mwepesi. Chini ya macho ya umati wa watu, alijikongoja na sura yake iliyopinda.
Alikuwa hapo kwa wiki moja. Kabla hajaja, alikuwa ametumia pesa nyingi kumwajiri mcheza kamari mmoja ili kumfundisha ustadi fulani wa kucheza kamari ili tu ashinde. Lakini, ikiwa angeendelea kufanya hivi, hakika asingeweza kushinda tena kesho yake.
Kwanini mtu huyo alikuwa bado hajajitokeza? Je, Kelvin angeweza kumdanganya? Hapana. Hata kama angeachwa na nafasi ya mwisho, ilimbidi atende kulingana na mpango. Hakuweza kumudu kufanya makosa.
Lina hakujua kwamba kulikuwa na mtu amesimama nyuma ya dirisha la kioo kwenye ghorofa ya tano, akimwangalia akiondoka. Mtu huyo aliingiza mikono yake mfukoni kwa utulivu. Taa zilizokuwa juu yake ziliangazia nywele zake za mtindo wa Ras zilizoanguka juu ya mabega yake. Wanaume wengi walimtazama, hakuwa na mvuto mwenye nywele zake ndefu zilizosokotwa, lakini alikuwa na sura ya kuvutia iliyofanana na ya shetani.
Hata hivyo, mtu yeyote ambaye angemwona angejawa na woga kwa sababu ya macho yake ya ajabu ya ukungu. Macho yake yangeweza kupelekea mtu kuwa na baridi hadi kwenye uti wake wa mgongo.
Kila mtu alijua kwamba tajiri mkubwa wa Lubumbashi, Titus Tshombe, alikuwa na aina hiyo ya macho. Mtu huyo alikuwa mwana wa Titus, Matthew Tshombe—mrithi wa baadaye wa familia ya Tshombe.
“Bwana Mkubwa..” Mhudumu alitembea. “Nimeulizia kuhusu hilo. Jina lake la mwisho ni Jones, na alitoka Tanzania.
“Jones?” Mathew alikodoa macho taratibu. "Hufikirii ... anafanana na mama yangu?"
Baada ya kukaa kimya kwa muda, msaidizi alijibu, "Baada ya kumtazama kwa karibu, nadhani alifanyiwa upasuaji wa plastiki hapo awali. Pengine aligundua sura ya Madam na kufanyiwa upasuaji wa plastiki ili kufanana naye.”
 
"Mama yangu haonyeshi uso wake hadharani, hakuna mtu aliyewahi kumuona. Isitoshe, maneno na tabia yake ni kama ya mama yangu pia.” Matthew alisema kwa sauti ya kutatanisha, “Mama yangu aliniambia kwamba alijifungua mtoto kabla hajafika Kongo. Hii inamaanisha kuwa nina dada wa kambo huko Tanzania ambaye anashea mama mmoja na mimi.”
“Unashuku kuwa ni yeye?” Mhudumu alishangaa.
“Waambie wafanyakazi wa hoteli watafute njia ya kupata nyuzi mbili za nywele zake. Ninataka vipimo vya DNA vifanyike kwa ajili yake na mama yangu haraka iwezekanavyo. Nataka kujua matokeo kesho asubuhi.”
Baada ya Mathew kutoa agizo hilo, aligeuka na kuondoka.
Kulipopambazuka asubuhi iliyofuata, msaidizi alimwendea na matokeo. “Bwana Mkubwa, ikawa kweli ana uhusiano na wewe. DNA yake ni sawa na asilimia 90 na ya mama yako. Hii pia inamaanisha kuwa hakika una uhusiano naye. ”
Mathew alichukua ripoti ili kuangalia. Macho yake yalionyesha sura ya furaha. Ikiwa mama yake angejua kwamba alikuwa amempata binti yake aliyepotea kwa muda mrefu, angefurahi sana. Mara moja alichukua ripoti na kuchukua ndege ya haraka hadi Paris Ufaransa, jiji ambalo wazazi wake waliishi kwa miaka mingi.
Baada ya kujua mahali alipo mama yake, mara moja alielekea kwenye bwawa lililo nyuma ya jumba.
Wenzi hao wa ndoa walikuwa wakivua samaki kando ya bwawa. Licha ya kuwa katika umri wao wa makamo, wawili hao walidumisha sura ya ujana. Mwanamke huyo alikuwa mzuri, wakati mwanamume alikuwa mtanashati sana. Wote wawili walionekana kana kwamba walikuwa na miaka 30 tu licha ya kwamba walikuwa wakikaribia kuingia miaka ya 5o.
“Mpenzi, usiweke macho yako kwenye fimbo ya kuvulia samaki. Niangalie." Kwa wakati huu, Titus, tajiri mkuu wa Lubumbashi, alikuwa mbali na kiburi na kutawala kama jinsi wengine walivyomwona kuwa. Alimng'ang'ania mke wake kama kupe na ng’ombe.
“Nyamaza na ukae kimya. Usiongee samaki wangu atakimbia.” Sheryl alimpiga Titus mng’ao mkali.
Titus alipepesa macho kwa huzuni. "Wewe, unanipenda mimi au samaki zaidi?"
Sheryl alikosa la kusema. “Wewe bado ni mtoto katika uzee huu. Acha ujinga."
“Mimi ni mzee hivyo? Ninahisi nina umri wa miaka 30 tu,” Titus alijibu kwa tabasamu.
Sheryl alishindwa cha kusema.
“Mama...” Mathew alimkimbilia kwa haraka.
Titus alimtupia jicho la dharau. “Mbona umerudi? Si tulikuambia ubaki Kongo usimamie biashara ya familia yetu? Siku zote unasafiri kwenda na kurudi.”
Kwa kudharauliwa na baba yake, Mathew alikosa la kusema. Alijihisi kana kwamba ni zawadi ambayo mama yake alimpa baba yake na hakukaribishwa hata kidogo.

Kwa mawazo kwamba baba yake angejisikia vibaya baadaye, Matthew alifurahi sana.
"Mama, nina kipande cha habari ya kushangaza kwa ajili yako wakati huu." Uso wa Matthew ulijawa na msisimko.
"Habari gani?" Sheryl alimtazama kwa mshangao.
“Nilimpata mtoto uliyemzaa hapo awali. ” Mathew alipomaliza kusema tu, Titus alimvuta kola.
“Umesema nini?” Macho ya Titus yalimfanya aonekane kuwa anataka kummeza Mathew.
“Shoo! ” Sheryl alimsukuma Titus. “Uliponioa, uliahidi kwamba utamkubali mtoto wangu mwingine ikiwa nitampata baadaye.”
Mdomo wa Titus ulining’inia, na uso wake ulionyesha masikitiko yake.
“Usijali, nitamkubali mtoto tu na sitakuwa na uhusiano wowote na mpenzi wangu wa zamani,” Sheryl alisema kwa sauti laini.

Sura ya: 683
 
Back
Top Bottom