Simulizi: Lisa

“Jason amekupa nyumba, lakini sijui nikupe nini. Nitakupa tu ubao wa kuogea.” Wendy alitabasamu na kutoa ubao. "Kama Rodney anakukasirisha, mfanye apige magoti juu yake. Akikataa kupiga magoti, unaweza kunipigia simu tu.”

“Mama...” Rodney akawa hana furaha.


“Asante Aunty. Naipenda sana zawadi hii.” Pamela alitabasamu sana.


"Aunty? Unapaswa kuniita 'Mama' sasa." Wendy alitingisha kichwa chake, katika mood nzuri. Hamu yake ilitimizwa hatimaye.

Saa kumi jioni, Jason aliwachukua wawili hao hadi Shangwe Corporation kufanya mkutano na waandishi wa habari. Kwa kuwa suala hili lilihusisha Rais wa baadaye, waandishi wengi wa habari kutoka kila kona ya nchini walihudhuria.

“Mwenyekiti Shangwe, kwa nini uko hapa? Waziri Shangwe yuko wapi? Je, hajapanga kueleza kisa cha bintiye wa kike kuwadhulumu wengine?”

"Je, Pamela Masanja ana nia ya kuomba msamaha? Lakini kuna umuhimu gani wa kuomba msamaha? Alisababisha bei ya hisa ya Jackson & Sons Company kushuka kwa siku kadhaa. Mabilioni yametoka kwenye soko la hisa."

"Nilisikia kwamba Bi Masanja alichumbiana na Bwana Jackson kutoka Jackson & Sons Company hapo awali. Baadaye, alipendekeza kuachana. Lakini alipomwona Patrick Jackson akipata mpenzi mpya, alikosa furaha na kumtishia Patrick kwamba ikiwa hataachana na mpenzi wake, ataiharibu Jackson & Sons Company.”

"Pia nilisikia kwamba Binti Mkubwa wa Shangwe anataka kushughulika na Jackson & Sons Company na familia ya Shei. Je, hii ni kweli?”

"Familia ya Shangwe lazima iombe msamaha kwa suala hili."

"Je, familia ya Shangwe haikumfukuza Rodney Shangwe kutoka kwa familia muda mfupi uliopita? Mbona amerudi haraka hivyo? Je! familia ya Shangwe ilikuwa ikionyesha tu maonyesho?"

Baadhi ya wanahabari walikuwa wamehongwa na washindani wa Nathan na kuuliza maswali kadhaa ya kufedhehesha. Hata hivyo, Jason alikuwa mtu ambaye alikuwa amepitia mambo mengi maishani. Alibaki mtulivu mwanzo-mwisho.

Baada ya zaidi ya dakika kumi, makoo ya waandishi hao yalitoka kwa sauti ya kupiga kelele. Hatimaye hawakuweza kujizuia na kusema, “Kwa nini hujibu lolote kati ya maswali yetu? Una hatia?"

“Mmetupa nafasi ya kujibu?” Macho makali ya Jason yakatua kwa waandishi. Ilikuwa sura moja tu na sentensi moja, lakini iliwafanya waandishi wa habari kutetemeka.

“Ninafanya mkutano na waandishi wa habari leo kwa sababu tukio hili linazidi kuwa kubwa. Imeleta shida nyingi kwa familia ya Shangwe," Jason alisema kwa unyogovu, "nilikuja hapa leo na mwanangu na binti-mkwe wangu kuomba msamaha."

"Kwa hivyo unakubali kwamba ulikosea, na unakubali kwamba familia ya Shangwe ilikuwa ikiwanyanyasa wengine?" waandishi wa habari mara moja walipiga bomba tena.

"Kwa kweli ni makosa kuwapiga watu." Jason alikunja uso. "Lakini ninaamini kwamba mtu yeyote atakasirika akiona mke wake mwenye ujauzito wa miezi minne akipigwa kofi."

Waandishi wa habari walikuwa katika ghasia. “Hiyo ina maana gani? Bi Masanja ana mimba? Rodney Shangwe alikua mume wake lini?"

Jason alimtazama Rodney, Rodney akasimama. "Ninaamini kila mtu anajua kuwa wakati wa karamu ya uzinduzi wa bidhaa ya Osher Corporation, kuna mtu alipanga njama dhidi yangu na Pamela, na kutufanya tulale pamoja. Sikutarajia angepata ujauzito usiku huo na niligundua hivi majuzi tu. Tayari nimeachana na Sarah Njau, na Pamela kwa sasa ni mke wangu.

“Jana, nilikuwa nikimpelekea kitu nilipomwona akipigwa kofi na Patrick Jackson. Akili yangu ilizimika kutokana na hasira. Ana ujauzito wa miezi minne, na kuna wakati ulikaribia kuharibika. Familia ya Shangwe imekuwa makini sana wakati huu, lakini... samahani.”

Aliinama na kusema, “Kuhusu mimi kumpiga Linda Shebi, ni kweli nilimpiga. Alikuwa amesimama mbele ya Patrick na sikuweza kuzuia hasira yangu wakati huo.”

Waandishi walipigwa na butwaa. Hakuna aliyetarajia Pamela kuwa mjamzito.

"Hiyo haiwezekani. Haonekani kuwa na ujauzito wa miezi minne hata kidogo. ” Baadhi ya wanahabari waliibua shaka.

"Hizi ni risiti za uchunguzi wa ujauzito na uchunguzi unaohusiana nao. Amekuwa akienda kufanyiwa uchunguzi wa uzazi kila mwezi.”
 
Rodney alionyesha ripoti za ujauzito moja kwa moja kwenye skrini kubwa nyuma yake. “Ungefanya nini ukiona mkeo wa miezi minne anapigwa? Ninakubali kwamba nilikuwa na msukumo, na ninaomba msamaha. Lakini katika hali kama hiyo, sikuweza kujizuia kupoteza busara yangu.”

Mwandishi alisema, “Lakini tunavyojua, Miss Masanja alilenga Jackson & Sons Company kwanza. Vinginevyo, Linda Shebi asingemsumbua Miss Masanja. Pia, alipiga magoti kuomba msamaha, lakini Bi Masanja hakujali na akawa mwenye kiburi.”

Pamela alikunja uso. “Ninaamini lazima nyote mlitazama video hiyo. Katika hali hiyo, unapaswa kujua kwamba sijawahi kumgusa Linda mwanzo hadi mwisho. Alitokea ghafla, akapiga magoti mbele yangu bila kuchokozwa na kuniomba msamaha. Nilichanganyikiwa. Kusema ukweli, simfahamu vizuri na hatuna uhusiano mzuri. Kwa nini niongee naye? Nilihisi kuumwa kwa kusikia tu sauti yake, kwa hivyo nilitaka kuondoka moja kwa moja. Yeye ndiye aliyekuwa akining’ang’ania.”


“Huoni kama ulienda mbali sana?” mwandishi wa habari alimshtaki.


“Je, ni lazima nijifanye kuwa na nia njema kuelekea mtu kama Linda? Kama mbwai na iwe mbwai tu, na chuki ni chuki. Patrick na mimi tulipokuwa tukichumbiana, Linda alizunguka nasi kila mara akitumia utambulisho wake kama rafiki wa utotoni wa Patrick. Je, umewahi kuona jinsi mpenzi wako anavyokuja na msichana mwingine wakati nyinyi wawili mnanunua vitu, mkitazama sinema, mkienda kutembea, na mkila pamoja?”

Pamela alisema huku akionyesha kuchukizwa, “Niliachana na Patrick kwa sababu sikuweza kuvumilia. Ninaamini wafanyakazi wengi katika makao makuu ya Jackson & Sons Company huko Dar es Salaam wanaweza kuthibitisha hili. Wakati Patrick na mimi tulipokuwa tukichumbiana, Linda alishikamana na Patrick kila wakati Samahani, lakini mimi si mtu mahiri hivyo. Namchukia mwanamke huyu.”

"Kwa hiyo ulilenga Jackson & Sons Company kwa sababu unamchukia?" mwandishi aliuliza kwa ukali.

Jason akachukua ripoti nyingine. "Tumeuliza idara ya usimamizi kuhusu hili. Idadi ya bidhaa zinazouzwa sana na Jackson & Sons Company zina acrylamide. Idara ya usimamizi inachunguza kampuni yao kwa sababu kiwango cha acrylamide kwenye vyakula vyao kinazidi viwango vya kimataifa. Wakati huo huo, kiwango cha sukari pia kinazidi wastani.

"Ikiwa huniamini, unaweza kuangalia vipimo hivi vya maabara. Hili ni jambo zito, kwa hivyo Jackson & Sons Company iliombwa kusitisha uzalishaji na kurekebisha tatizo hilo. Lakini, Jackson & Sons Company ilisisitiza kufungua tawi katika nchi ya Kenya. Kwa kuwa Patrick hana uwezo wa kusuluhisha mzozo huu, alimwandama Pamela na kusema kwamba alikuwa akimlenga. Alitaka kumtumia Pamela kuisaidia Jackson & Sons Company kupitia shida hii.

Waandishi walitazamana.

Macho ya Jason yalipita katikati ya kundi la wanahabari mmoja baada ya mwingine. " Kwa kweli ni makosa kuwapiga watu, na familia ya Shangwe inaomba msamaha kwa hilo. Lakini tetesi za kwenye mtandao kuhusu Pamela kutumia hadhi yake kuwadhulumu wengine zilitoka wapi? Familia ya Shangwe itachukua hatua za kisheria dhidi ya wale wanaothubutu kukashifu sifa yetu. Mkutano na waandishi wa habari leo unaishia hapa.”

Alizima kipaza sauti na kuondoka na Rodney na Pamela.

Sura ya: 698



Mkutano huo wa wanahabari ulikuwa umerushwa moja kwa moja.
Watu kwenye mtandao walikuwa wanazungumza juu yake kama wazimu.

[Holy Sh*t! Pamela ana ujauzito wa miezi minne? Sikuweza kujua hata kidogo. Bado ni mrembo sana akiwa na mimba ya miezi minne.]

[Tafadhali, hilo si jambo la maana, sawa? Jambo ni kwamba Pamela hakuwahi kuilenga kampuni ya Jackson hata kidogo.]

[Je, uliona arifa ya dharura ambayo idara ya usimamizi imetoa sasa hivi? Kwa kweli kuna kitu kibaya na biskuti na keki za Jackson & Sons Company. Usizinunue siku zijazo.]

[Nilikuwa nikifanya kazi katika kampuni ya Jackson & Sons Company. Uhusiano wa Patrick na Linda ndivyo Pamela alivyouelezea. Wakati huo, ingawa kila mtu alijua kuwa anatoka na Pamela, lakini kila siku alikuwa akija kazini na kutoka kazini na Linda. Wageni wengi katika kampuni hawakuelewa kuwa wao ndio walikuwa kwenye uhusiano badala yake.]
 
[Si kwenda tu na kutoka kazini. Mara nyingi nilimwona Patrick akifanya shopping na Linda wakati huo. Nilikuwa tayari nimechanganyikiwa wakati huo. Nilikuwa nikijiuliza ikiwa Pamela kweli hakujali.]

[Nilikwenda chuo kikuu na Patrick na Pamela. Ninaweza kushuhudia kwamba Pamela alikuwa mzuri sana kwa Patrick. Alikuwa mtiifu kwake, lakini siku zote alikuwa akimjali. Siku moja, Pamela alipougua, nilimtazama akinywa dawa peke yake.]
[Katika siku ya kuzaliwa ya Patrick, Pamela aliwaita wanafunzi wengi wa zamani kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja, lakini hata hakutokea.]

[Hiyo si kitu. Patrick alipotakiwa kukutana na wazazi wa Pamela ili wazungumze kuhusu ndoa yao, badala yake alikimbia kukutana na Linda. Kama matokeo, aliwasimamisha wazazi wa Pamela na kuwafanya wasubiri masaa mawawili.]

[Holy sh*t, ni kweli? Yeye ni mpuuzi sana. Anaweza kushindana na Kelvin Mushi.]

[Kelvin ni mtu wa kudharauliwa asiye na maadili. Patrick ni fisadi aliyepoteza ujana wa Pamela.]

Lisa alimjibu Mwanamtandao mmoja: [Patrick hajawahi kutambua jinsi alivyo mtupu. Anafikiri kwamba Pamela hapaswi kujali kuwepo kwa Linda. Alichumbiana na Pamela kwa miaka mitano, lakini mtu ambaye alisafiri naye Pamela alikuwa ni mimi, mtu ambaye huwa anakula nae ni mimi, mtu ambaye alikuwa anatazama naye filamu ni mimi, niliyeenda naye shopping pia ni mimi. Hakuwahi kufanya chochote kwa Pamela. Aliongozana na Linda kwa kila kitu na bado angelalamika kuwa Pamela hakuwa mzuri. Hah. Je, anafikiri kwamba Pamela bado angekuwa na mapenzi ya zamani kwake? Katika ndoto zake!]

[MUNGU WANGU. Lisa alinijibu. Ninaota?]

[Lisa na Pamela ni marafiki wakubwa.]

[Hatimaye ninaelewa kwanini Pamela alimpuuza Linda. Ikiwa ningekuwa mimi, ningeweza kupata wehu. Ninahisi ghafla kuwa Pamela ana hasira nzuri.]

Alvin alimjibu Lisa: [Nakuunga mkono, babe. Ndiyo, Patrick Jackson si mzuri. Yeye ni takataka.]
Lisa alimjibu Alvin: [Hmph. Alimtumia Pamela kukata uhusiano nami, akisema kwamba niliwatia moyo waachane. Ikiwa ningeweza kufanya hivyo tena, nisingemtia moyo tu kuachana naye. Ningemkasirisha pia.]

Alvin akamjibu Lisa: [Ngoja nifanye hivyo. Usichoke mikono yako.]

Wanamtandao: [Aha, Bwana Kimaro anacheza kimapenzi na Bibi Jones tena.]


Kwa upande mwingine.
Katika Jackson & Sons Company.

Baba na mama ya Patrick walikimbilia jijini Nairobi mara tu walipopata habari juu ya mkutano wa waandishi wa habari na familia ya Shangwe.

Bwana Jackson alipomuona Patrick, kitu cha kwanza alichokifanya ni kumpiga kofi kali. “Mjinga wewe! Ulikuwa mjinga kiasi cha kuwa kibaraka wa wale vigogo wanaopigana dhidi ya Nathan Shangwe. Unafikiri wewe ni nani? Unathubutu kweli kwenda kinyume na familia ya Shangwe na Rais wa baadaye?! Umerukwa na akili?"

Kichwa cha Patrick kikaunguruma kutokana na kofi lile.
Hakuwahi kufikiria kuwa Pamela angekuwa mjamzito. Alikuwa mjamzito na kuolewa? Kwa sababu fulani, mara tu alipopata habari hiyo, akili yake ikawa tupu sana.

“Uncle...” Linda alikimbia na kusimama mbele ya Patrick. “Usimlaumu Patrick. Pamela kweli alilenga Jackson & Sons Company, lakini wao ni matajiri na wenye nguvu, kwa hivyo wanakataa kukubali. Jana katika kituo cha polisi, Jessica Shangwe pia alionya kwamba hataruhusu familia za Jackson na Shebi kusimama. Patrick alikata tamaa na hakuwa na chaguo.”

"Nyamaza! ” Bwana Jackson aliwahi kuwa na picha nzuri ya Linda. Baada ya yote, familia zao zilikuwa na uhusiano mzuri, lakini alipoona maoni kwenye mtandao, hakuweza kujizuia kumchukia sasa. Patrick na Pamela walikuwa karibu kufunga ndoa wakati huo, lakini waliachana kwa sababu yake.
Chini ya uongozi wa Forrest, Kampuni ya familia ya Masanja lilistawi na hata kuipita Jackson & Sons Company. Ikiwa sivyo kwa Linda, familia za Jackson na Masanja zingeunganishwa kwa ndoa. Sasa, kuhusu Jackson & Sons Company, kinachowangojea kinaweza kuwa mwisho wao.

“Uncle...” Mwili wa Linda ulitetemeka huku macho yake yakimtoka.

“Baba usimlaumu Linda. Ilikuwa chaguo langu,” Patrick alisema kwa unyonge.
 
Bw. Jackson alisema kwa hasira, “Wale vigogo walipanda ushahidi wa uongo dhidi ya Rais wa baadaye. Je, unafikiri familia ya Shangwe itaiacha tu? Jason Shangwe tayari alisema kwamba wataifuatilia hadi mwisho. Watu wanaoshindana dhidi ya Nathan Shangwe watajificha mara moja na kukusukuma nje kuwa mbuzi wa sadaka. Unafikiri kuna ugumu kwa wao kuiharibifu Jackson & Sons Company? Familia ya Shangwe ina kila sababu ya kusema kwamba wewe ndiye mpangaji mkuu. Umesababisha matatizo mengi kwa familia ya Shangwe wakati huu. Hawatakuacha kamwe.

"Nathan Shangwe atakutumia kama mfano kwa wengine na kuonya ulimwengu wa nje kwamba familia ya Shangwe si rahisi kuhangaika nayo. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuikasirisha familia ya Shangwe."

Mwili wa Patrick ukatetemeka.
Bibi Jackson naye alilia. “Mwanangu, wewe ni mpumbavu sana! Familia yetu inatakiwa kupiganaje na familia ya Shangwe?”


Mara tu maneno hayo yalipoanguka, kundi kubwa la maafisa wa polisi liliingia kutoka nje. "Samahani, tulipokea ripoti kutoka kwa familia ya Shangwe kwamba Patrick Jackson aliajiri watu mtandaoni kumpaka matope Waziri Shangwe na bintiye. Patrick Jackson, uko chini ya ulinzi.”
Afisa mmoja aliifunga mikono ya Patrick nyuma ya mgongo wake.

“Sikufanya hivyo!” Patrick aliingiwa na hofu kabisa.
“Unathubutu kusema kwamba si wewe uliyepakia video hiyo?”
Afisa huyo aliuliza kwa ukali, “Ni kwa sababu ulipakia video hiyo ndipo ulimwengu wa nje ulianza kufikiria kwamba Waziri Shangwe aliruhusu familia yake kuwanyanyasa wengine. Jambo hilo lilipozidi kuwa mbaya, ulikaa kimya na kuruhusu wanamtandao kukemea familia ya Shangwe, ambayo ni sawa na kukubaliana na maneno yao kimya kimya. Wakati huo huo, ulipata watu wa kueneza uvumi kwamba Pamela Masanja alilipiza kisasi kibinafsi dhidi ya Jackson & Sons Company. Anwani ya IP iliturudisha kwenye kampuni yako."

Sura ya: 699



Moyo wa Patrick ukasisimka. Alikiri kwamba alikubaliana kimyakimya na matusi ya wanamtandao, lakini hakuwahi kupata mtu wa kueneza uvumi.
Alimtazama Linda bila kujua.

Moyo wa Linda ulitetemeka. Alilia na kuwatazama polisi. “Hatukufanya hivyo. Hii ni tuhuma ya uwongo."

Afisa huyo alidhihaki, “Imetosha. Ni shtaka la uwongo la familia ya Shangwe kwamba kuna tatizo na bidhaa za Jackson & Sons Company, na ni shtaka la uwongo la polisi kwamba ulikashifu familia ya Shangwe...”

“Hilo silo alilomaanisha...” Patrick alieleza kwa haraka.

"Mwondoe." Maafisa wawili wakamtoa Patrick nje moja kwa moja.

“Patrick...” Bi. Jackson alilia kwa wasiwasi. “Tunapaswa kufanya nini sasa? Mpendwa, fikiria njia. Tunapaswa kumuokoa Patrick.”

Bwana Jackson alikunja ngumi. “Tunapaswa kumuokoa vipi? Nani atathubutu kuwaudhi familia ya Shangwe ili kumwokoa sasa? Linda, ulikuwa unafanya nini? Kwanini hukumzuia Patrick kufanya vile?”

Linda alipauka kwa hofu. Sio tu kwamba hakumzuia, lakini kwa kweli yeye ndiye alianzisha jambo hilo. Alikasirishwa tu kwamba Pamela alikua binti wa hiari wa Nathan. Alifikiri kwamba ikiwa sifa ya Nathan ingeharibiwa, Pamela pia asingekuwa na wakati mzuri.

"Tutaenda ... na kumsihi Pamela.” Baada ya muda mrefu, Bwana Jackson alishusha pumzi nzito.

“Basi... kwanini tusimuambie Linda akaombe msamaha?” Bibi Jackson aliuliza kwa kuhema.

“Kuna maana gani kumwambia aende? Ili akapige magoti na kubamiza kichwa chake chini? Au kung'ang'ania mkono wa Pamela na kukataa kuondoka?" Bwana Jackson alitupa mkono wake na kuondoka.

Bibi Jackson alimfuata. Baada ya wao kuondoka ofisini, alimwambia mumewe, “Umeenda mbali sana sasa hivi. Najua umemkasirikia Linda, lakini ikiwa Jackson & Sons Company itaanguka kweli, Patrick ataweza tu kutegemea familia ya Shebi.”

“Huelewi? Familia ya Shangwe haitaruhusu familia ya Jackson kunyanyuka, na pia hawatairuhusu familia ya Shebi Mbali na hilo ... Tutazungumza juu yake ikiwa Patrick ataachiliwa. Ninachohofia ni kwamba... familia ya Shangwe haitamwacha aende zake.” Bwana Jackson alihema sana.

Bibi Jackson aliganda.
•••
Katika makazi ya Shangwe.
 
Pamela alikuwa amemaliza chakula chake cha jioni kwenye meza kubwa ya duara wakati Jessica alipokea simu na kumwambia Nathan, "Ba mdogo, Patrick Jackson amekamatwa."
“Mh.” Nathan alikunja uso sana na kunywa chai. "Hali ikoje kwa familia ya Karama?"

"Waziri Karama anadaiwa kuwa ni mgonjwa na haonani wageni wowote. Amechukua likizo ya siku chache,” Jessica alisema kwa unyogovu, “nadhani atakuwa na tabia nzuri huku mkia wake ukiwekwa katikati ya miguu yake kwa sasa.”

"Ataweka mkia wake katikati ya miguu yake kwa muda mfupi na kisha kufufuka ili kunipa wakati mgumu tena?" Nathan alimtazama Ian. "Hapo awali nilifikiria kumwacha Waziri Karama afurahie maisha yake wakati wa kustaafu, lakini inaonekana hakuna haja ya hilo. Ondoa familia ya Karama kwenye nyadhifa zao zote ndani ya siku mbili. Wanaweza kutupwa kwenye vyeo vya chini.”

“Sawa.” Ian alitikisa kichwa kwa sura kali kwenye uso wake mzuri ambao Pamela hakuwahi kuuona hapo awali.

Pamela alipigwa na butwaa. Nathan daima alikuwa mkarimu mbele yake, kiasi kwamba alikuwa karibu kusahau kwamba hakuna mtu katika siasa ambaye angekuwa rahisi hivyo.

“Kuhusu Patrick...” Nathan alitabasamu na kumtazama Pamela. "Kwa kuwa alimuudhi bintiye mdogo wa familia yetu, mwache akae gerezani kwa muda."

Pamela akavuta pumzi ya baridi.

Ian alimtazama. "Kwa kuwa alithubutu kwenda kinyume na familia ya Shangwe, anapaswa kuwa tayari kwa mabaya zaidi. Mbali na hilo, ikiwa hatutamfundisha somo baya, watu wengine watajuaje kuitendea familia ya Shangwe kwa heshima?”

"Familia ya Shangwe daima ilikuwa na sifa nzuri, lakini ilikuwa karibu kuharibiwa na Patrick Jackson. ” Mzee Shangwe alitikisa kichwa kukubaliana na maneno ya Ian.
Midomo myekundu ya Pamela ilisogea, lakini mwishowe, hakujua la kusema.
Alimchukia sana Patrick, lakini si kiasi kwamba alitaka aoze gerezani maisha yake yote. Hata hivyo, alikuwa amemchukiza Rais wa baadaye, ambaye mamlaka yake hayangevumilia kuudhiwa.

"Lakini, Rodney," Wendy alisema ghafla, "Kwa kuwa umeoa sasa, unapaswa kuandamana na Pamela kwenda Dar es Salaam na kukutana na wazazi-wakwe wako. Nenda kesho.”

“Sawa. ” Rodney alitii na kumtazama Pamela. “Um... Alvin na Chester walisikia kwamba nimepata jiko na wakaniomba nijumuike no kwenye klabu jioni hii.”

“Mmh.” Pamela alicheka kwa kukiri. “Kama unataka kwenda we nenda tu.”

Ikiwa alitaka kwenda, basi aende tu. Kwanini alikuwa akimwambia hivi?
Rodney alijisikia vibaya kidogo na tabia yake ya kutojali. “Nakwambia tu endapo utafikiri nitamwona Sarah.”

“Ukithubutu kumuona Sarah tena, nitakuvunja miguu,” Jason alimuonya.

Miguu ya Rodney ilitetemeka huku akitabasamu. "Sina uhusiano naye tena."

Baada ya chakula cha jioni, Rodney aliendesha gari hadi ClubHouse.
Chester alifika kwanza na kukaa kwenye sofa peke yake. Alikuwa anacheza na sigara mdomoni mwake kwa mawazo.

“Unawaza nini? Umepoteza mawazo.” Rodney akaketi karibu naye.

“Alvin yuko wapi?”

“Anapaswa kuwa njiani. Nilipopiga simu saa moja iliyopita, alisema atakuja baada ya kucheza mpira wa kikapu na watoto wake. Anapaswa kuwa njiani sasa,” Chester alijibu kwa kawaida.
Rodney alikosa la kusema. “Kuna tatizo gani la kuwa na mwanamke na watoto? Lakini ... hehe. Nina mwanamke na mtoto pia sasa. Chester, wewe tu na Sam bado hamjaoa. Naam, bahati nzuri."

“Siwaonei wivu wale waliofunga ndoa,” Chester alisema kwa unyonge.

"Hiyo ni kweli. Afadhali ujinyonge juu ya mti,” Rodney alitania.

“Unaonekana kuwa na furaha sana kuhusu ndoa yako. Tulipokuomba umwoe Pamela hapo awali, ulifanya kama ungependa kufa." Chester alimtazama na kumpa tabasamu lisiloeleweka.

“Nina furaha?” Rodney alionekana kuchanganyikiwa. “Mimi nipo kawaida tu. ”

“Kawaida?”
Chester alikoroma.

Uso wa Rodney ulikuwa umejaa kiburi, lakini yeye mwenyewe hakuliona hilo. “Nahisi tu... unajua, watu lazima wafunge ndoa mapema au baadaye. Hata kama sitamuoa Pamela, mama yangu ataendelea kunipangia watu nisiowajua. Angalau Pamela amembeba mtoto wangu. Yeye ni mrembo na mwenye talanta. Familia yangu inampenda sana pia, kwa hivyo yeye ni mwenzi mzuri wa ndoa,” Rodney alikariri na kusema.
 
“Hongera sana. Lakini kama si tukio hili na Patrick, Pamela ungemsikia kwenye bomba tu.” Chester akatabasamu. "Umepata mwisho mzuri wa mzozo."

“Usiseme hivyo. Mimi pia si mbaya.”

Rodney alikuwa amemaliza kuzungumza mara mlango wa chumba hicho ulisukumwa. Alvin aliingia huku mikono yake ikiwa mfukoni. “Tunazungumza nini? Haraka na umalize. Nataka kwenda nyumbani kwa mke wangu na watoto wangu.”

“Hata huwezi kufanya hivyo. Kuna faida gani ya kuja?” Rodney alimvamia bila huruma.
Uso wa Alvin ulitiwa giza. "Rodney Shangwe, unataka kufa?"

Chester alitabasamu. "Ameoa leo, kwa hivyo mpongeze kidogo.

“Njoo, Rodney, furahia. Nakutakia usiku mwema wa harusi! ”

Rodney alijikaza. Chester alimnong’oneza kwa siri sikioni, “Mimba ya mwanamke hutulia baada ya miezi mitatu. Haijakuwa rahisi kwako. Ulifanya mara moja tu katika miaka 3o ya maisha yako, na haukufanya katika hali ya ufahamu pia. Je!... unataka nikufundishe mbinu chache?”

“Ondoka nje!” Rodney akaruka juu akiwa na uso mwekundu.

“Sisi sote ni wanaume hapa. Kunanini cha kuwa na aibu?" Chester hakujua acheke au alie.

Rodney alitaka kulia. “Unawaza sana. Kabla hatujafunga ndoa, Pamela alitia saini makubaliano nami. Siruhusiwi kumshika baada ya ndoa. Sisi ni wanandoa tu kwa jina."

Alvin alifurahi kwa msiba wake. "Hiyo ni nzuri."

“Ina uzuri gani? Mimi ni mwanamume wa kawaida—”


“Je, si umekuwa ukiishi hivi kwa muda wote? Usimguse tu.” Chester alitabasamu.

"Hapana. Sikuwa nimeoa hapo awali, lakini kwa kuwa sasa nimeoa, jambo la aina hii ni sawa. Kwanini siwezi kumgusa?” Rodney hakuweza kukubali hili. "Nisaidieni kufikiria njia."

“Hakuna cha kufikiria. Ni mjamzito sasa, hivyo huwezi kutumia nguvu kwani itamuumiza mtoto.” Chester alimpa maneno matatu, "vumilia."

Rodney, akaguna. Kwa hasira akapiga funda kubwa kutoka kwenye glasi yake.
Alvin naye taratibu akanywa glasi mbili hadi tatu. Hakuthubutu kunywa pombe kupita kiasi kwa kuogopa kulewa.

Sura ya: 700


Saa tatu za usiku, Alvin alikuwa anaenda kuondoka.

“Pole sana, Alvin. Unachosha sana. ” Rodney alikasirika. "Leo ni siku ya ndoa yangu, lakini unaondoka mapema sana."

“Unaweza kujifunza kutoka kwangu. Jizoeze kuandamana na mkeo na mtoto wako.” Alvin alitabasamu na kuondoka kwa upole.

Alipofika nyumbani, Lisa alikuwa bado
akiwasomea hadithi wale watoto wawili.
Akapanda kitandani na kumkumbatia kwa nyuma. "Lisa, nimelewa."

Suzie alimtazama kwa unyonge. "Lo, baba mchafu, huna aibu sana. Wewe ni mtu mzima lakini bado unaigiza kwa kubembelezwa.”

"Aibu kwako!" Lucas naye alitema maneno haya mawili.

“Mnajua nini wawili? Ni kawaida kumtendea mke wako hivyo.” Alvin alimkumbatia Lisa bila kumwachia, na kuwafanya watoto wahisi hasira kwa mama yao.

Lisa alishtuka kidogo kwa kukosa aibu. "Pamela na Rodney watarejea Dar kesho. Ninapanga kwenda nao. Kesho ni siku ya kuzaliwa kwa bibi yangu, kwa hiyo nataka kwenda kumpa heshima zangu kwenye kaburi lake.”

“Mbona hukuniambia mapema?” Alvin alikunja uso. "Hans tayari amepanga ratiba yangu kwa siku mbili zijazo..."
“Ni sawa. Naweza kwenda peke yangu. Pamela atakuwa nami...” Lisa alimfariji.

"Yeye ni yeye, na mimi ni mimi. Ni tofauti. Isitoshe, ni bibi yetu. Bila shaka, ni lazima niende nawe.” Alvin alizika uso wake kwenye shingo yake.

“Ahem. Je, unaweza kuwa makini na mazingira yako? Kuna watoto wawili wasio na hatia hapa." Suzie aliweka mikono yake kwenye makalio yake.

Lucas alikunja uso. “Unachukua wakati wote wa Mama sasa. Hatimaye ana muda wa bure leo kutusomea hadithi, lakini unataka kushikamana naye tena. Huwezi kumwacha kidogo?”

“Ndiyo,” Suzie alilalamika, “Kama ningalijua kwamba mngekuwa mnanga’nga’aniana sana, nisingeweza kamwe kuwaunga mkono nyinyi wawili kurudiana pamoja.”

Uso wa Alvin ulijawa na huzuni na aibu kutokana na maneno ya watoto hao.

"Pfft." Lisa alishindwa kujizuia kucheka. Alimsukuma Alvin na kuchukua watoto wake wawili mikononi mwake.

"Mama, tunaweza kwenda nawe?" Suzie alicheza kwa kubembelezwa.

"Hapana, bado mko hatarini." Lisa akatikisa kichwa. "Nitarudi baada ya siku mbili."
 
Baada ya kusimama, alirudi kwa Alvin. “Si lazima ushikamane nami siku nzima. Wakati mwingine, umbali ni mzuri pia."

“Umechoka na mimi?” Alvin alipata pigo.

Lisa alishtuka. "Naona uso wako kila siku. Nitashindwa kuona hata kile kinachopendeza kwako tena.”
Uso wa Alvin wa kupendeza ukawa giza mara moja. Suzie na Lucas walicheka kwa furaha, hasa Suzie.

"Baba mchafu, mama yuko sahihi. Nilidhani ulikuwa mzuri hapo awali, lakini baada ya kukutazama sana, sijisikii chochote tena. Uso wako umepoteza mvuto.”

Alvin alitaka kutapika damu. Siku zote alikuwa akijiamini katika sura yake, hivyo hakutarajia kupata pigo kutoka kwa mke na binti yake. Sahau. Wakati mwingine, umbali kidogo ulihitajika.

“Sawa, nitakubali uende Lisa, lakini lazima urudi kwa wakati. Usinifanye nisubiri peke yangu kwa muda mrefu,” Alvin alisema huku uso wake ukiwa hoi.

“Unaonekana umekosea. Sihitaji ruhusa yako kwenda popote. nakujulisha tu,” Lisa alimkumbusha huku akitabasamu.

Alvin alikuwa na huzuni. “Uko sahihi. Katika familia hii, wewe ndiye mwenye sauti ya mwisho.”

"Mama, wewe ni wa kushangaza." Suzie na Lucas walimsifu kwa unyonge.

Ilikuwa ni kawaida kwa Suzie kusema hivyo, lakini si Lucas. Lisa alimtazama Lucas. Ingawa mtoto bado alikuwa baridi na asiye na hisia, baada ya yeye na Alvin kurudiana pamoja, alionekana kuwa mchanga zaidi.
•••

Siku inayofuata.

Alvin binafsi alimpeleka Lisa kwenye uwanja wa ndege. Rodney na Pamela walikuwa tayari wamefika. Walipomwona Lisa, Pamela mara moja akaenda kumshika mkono.

“Lisa! Nikiwa na wewe, kurudi Dar hakutakuwa jambo la kuchosha sana wakati huu. Kaa nyumbani kwetu usiku huu.”

“Oh, hakika.” Lisa alitabasamu.

“Niangalizie mwanamke wangu,” Alvin alimtazama Rodney na kumuelekeza.

“Nimekupata. Lakini inapofika kwa mwanamke wako, kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba yeye ndiye atanitunza,” Rodney alisema kwa sauti ya chini, “Kusema kweli, kwanini ulikubali kumruhusu Lisa aende nasi?”

“Hukumkaribisha?” Alvin hakuwa na furaha. "Ni heshima yako kuwa naye kwenye safari hii."

Rodney alikasirika. “Inatosha. Lisa ni hazina moyoni mwako, lakini hayuko ndani yangu. Hujui kuwa yeye ni gurudumu la tatu hapa? Nilipanga... nitumie nafasi hii ili mimi na Pamela tufahamiane zaidi. Labda tunaweza…” Akatulia huku uso wake mzuri ukibadilika na kuwa mwekundu kidogo.

Alvin alimtazama kwa dharau. “Usijali, hata kama Lisa asingeenda na wewe, bado isingewezekana. Acha kuota.”

Rodney ambaye gwaride lake lilinyeshewa na mvua, hakutaka kuhangaika tena na Alvin.

“Lisa, kuwa makini. ” Alvin alimsogelea Lisa na kumgusa uso wake mdogo. Alionya, “Jitenge na watu wengine.”

"Hifadhi mstari huo kwako mwenyewe." Lisa alimrudishia maneno yale na kutembea akiwa ameshikana mkono na Pamela hadi kwenye geti la kutokea.

Alvin alikodoa macho baada ya kuwaona yeye na Pamela wakiwa wameshikana mikono, moyo wake ukiwa na wasiwasi kidogo. Hakupenda aliposhikana mikono na wengine, hata kama mtu huyo alikuwa mwanamke.

Kwenye ndege, Pamela na Lisa walikaa pamoja. Wanawake hao wawili walinong'ona na kupiga soga, wakionekana kuwa na mada zisizo na kikomo za kuzungumza.

Rodney aliketi nyuma yao, na wanawake hao wakampuuza. Akiwa amechoka, alifumba macho tu na kulala mpaka wakafika Dar es Salaam.
Ndege hiyo ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Forrest alikuwa akingoja kwa muda mrefu, amevaa suti kamili. Alipomuona Rodney, uso wake mzuri ulijaa kutojali. “Bwana Shangwe, unaweza kujipanga mahali pa kufikia. Sio lazima kuja kwa familia ya Masanja. Kila mtu anajua kuwa ulioa dada yangu mdogo tu kwa sababu ulilazimishwa, kwa hivyo sio lazima kujaribu kumfurahisha baba na mama mkwe wako. Pande zote mbili zitahisi shida."

Rodney alionekana kuwa na aibu. Lilikuwa kosa lake. Alipokuwa na chakula cha jioni na familia ya Masanja wakati uliopita, bado alikuwa na Sarah moyoni mwake hivyo mtazamo wake wakati huo haukuwa mzuri sana. “Hata tukilazimishwa kuoana, ni ukweli kwamba tumefunga ndoa. Nchi nzima inajua kuhusu hilo. Ikiwa niko hapa Dar es Salaam lakini nisitembelee familia ya Masanja, utaaibika pia habari zinapoenea.”
 
"Tayari umesababisha familia ya Masanja kuwa na aibu mara nyingi. ” Forrest hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo.

Rodney aligusa pua yake. “Hata unikaribishe kiasi gani, bado natakiwa kutekeleza majukumu yangu. Wazazi wangu walitayarisha zawadi nyingi za uchumba, kwa hiyo sina budi kuzipeleka kwa familia ya Masanja.”

Forrest alimtazama kwa ubaridi kabla ya kugeuka na kumshika Pamelamabegani. “Twende nyumbani. Lisa, kaa nasi kwa siku chache.”

"Lazima niende makaburini kwanza ili kutoa heshima kwa bibi na babu yangu." Lisa alikataa huku akitabasamu.

“Basi nitakupangia gari la kukupeleka huko...”

“Hakuna haja. Ofisi ya tawi imepanga gari la kunichukua. Rudi nyumbani mapema. Nitakuja kukusumbua usiku.” Lisa akatikisa mkono.

Forrest aliitikia kwa kichwa. Alipokaribia kuondoka na Pamela, alionekana kuwaza kitu na ghafla akasimama. "Lisa. Nimesikia kwamba... shangazi na mjomba wako watatoka gerezani hivi karibuni.”

"Nini?" Pamela aliuliza kabla Lisa hajafungua mdomo wake. “Walishukiwa kuiba urithi wa Lisa na hata kumuua Bibi Masawe. Wanapaswa kutumia maisha yao yote gerezani. Kwa nini wanaachiliwa haraka sana?”

"Nilisikia kwamba ... wamekuwa na tabia nzuri gerezani na pia walitoa michango inayostahili. ” Forrest alikunja uso na kusema, “Wanapangwa kutolewa wiki ijayo.”

Lisa alikunja uso sana. Alikuwa ametumia juhudi nyingi kuwaweka jela John Jones Masawena mkewe. Bila kutarajia, wangeachiliwa kabla hata miaka minne haijapita? Hakuna mtu angeweza kukubali kitu kama hiki.

"Michango yao ilikuwa nini?" Lisa aliuliza kwa udadisi.

"Sina uhakika." Forrest akatikisa kichwa.

Uso wa Lisa ulikunjamana. “Haina maana. Je, ni michango gani inaweza kuondoa zaidi ya miaka 20 ya kifungo chao gerezani? Nashangaa kama... ina uhusiano fulani na Lina.”

Pamela alishangaa. “Unashuku kuwa amerudi? Hiyo haiwezekani. Baada ya Jones Masawe na mkewe kwenda jela, Lina alikimbia bila uangalizi wa wazazi wake na hakuwajali kabisa. Mtu wa aina hiyo hana dhamiri hata kidogo.”
"Sijui, lakini Dar es Salaam ni nyumbani kwake. Ni lazima kwake kurudi.” Lisa akahema. "Lakini ana uwezo gani wa kumuokoa John Jones na mkewe? Amekuwa akijificha gizani, na sijawahi kushinda dhidi yake katika makabiliano yetu ya baadaye. Ikiwa amerejea kweli, lazima atakuwa amefanya maandalizi.” Wasiwasi mkubwa ukatanda machoni mwa Lisa.

Suala lake na Kelvin lilikuwa bado halijatatuliwa, na Alvin alikuwa anapigana na familia ya Campos. Ikiwa Lina angerudi sasa, ingekuwa shida.

Rodney alitazama kushoto na kulia. “Lina ni nani?”

Pamela alimkazia macho. “Binamu wa Lisa. Yeye ni mwanamke mbaya, labda mbaya zaidi kuliko Sarah.

Rodney alipigwa na butwaa. Alitapeliwa na Sara kwa zaidi ya miaka kumi, lakini kuna mtu ambaye alikuwa bora zaidi katika kuwadanganya wengine kuliko Sara?

“Tuache kuongea mambo haya yasiyofurahisha. Hali yako si ya chini sasa. Hata kama amerudi, hakuna haja ya kuogopa,” Forrest alisema kwa tabasamu hafifu.

"Hiyo ni kweli. Lisa, mimi sasa ni binti wa Rais ajaye sasa. hakika nitakusaidia.” Pamela alimfunga Lisa mkono. "Kwa kweli, ni vizuri ikiwa atarudi. Tunaweza kusuluhisha alama zote tulizo nazo naye. Wakati huu, tutahakikisha kwamba hawezi kutoroka.”

“Asante, lakini ni mawazo tu. Labda hakurudi kabisa.”
Lisa alitabasamu.

Baada ya Pamela na wengine kuondoka, alitembea kuelekea kwenye maegesho ya magari. Muda si muda, mwanamume mmoja wa makamo akaja haraka. “Mwenyekiti Jones, samahani. Nilichelewa kwa sababu ya trafiki. Hili ndilo gari ulilotaka…”

“Ni sawa.” Lisa alichukua funguo za gari. "Unaweza kurudi kazini."

Baada ya kuingia kwenye gari, alienda na kununua maua.
Duka lilikuwa kwenye barabara kuu ya Nyerere inayotoka uwanja wa ndege kwenda mjini.
Aliingia kwenye duka kubwa la maua na kusema, “Bwana, nipe maua tafadhali.”

"Yamekwisha." Mwanaume huyo alijibu haraka.

“Hauna mashada ya maua?” Lisa aliuliza, aliona ni ajabu.

"Hapana." Mwanaume akatikisa kichwa. "Kuna kijana alifika mapema na kununua maua yote.

Lisa alipigwa na butwaa. Ilionekana kana kwamba kulikuwa na mambo ya ajabu kila mahali. "Sawa, nitaangalia mahali pengine."
 
Hata hivyo, baada ya kutembelea maduka matano, aligundua kuwa mashada ya maua yalikuwa yamenunuliwa na mtu mmoja.


ITAENDELEA LISA KITABU CHA: 15
 




Jamani mwendelezo utakua mgumu mana mwandishi mefungia copying en forwading kama mnavoona hapo kwenye picha[emoji3064][emoji3064] ko sijui tufanyaje wakuu?? leteni mawazo
 




na kama mnavoona story ni bado sanaa kuisha[emoji16][emoji2356] leteni mawazo tufanyaje??
 
Chubbyladdy naona umeamua kutupooza moyo😇🤤
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…