mireille
JF-Expert Member
- Mar 4, 2020
- 529
- 589
- Thread starter
- #941
Sura ya 1288
Ilionekana kana kwamba Cindy alikuwa na kiburi kweli.
“Unawezaje kuongea na Cindy hivyo?” Walinzi waliokuwa nyuma ya Cindy walisonga mbele na kusema kwa majivuno, “Mwombe msamaha Cindy mara moja, la sivyo, itabidi ukabiliane na matokeo yake.”
“Unafikiri ninaogopa kuingia kwenye matatizo?” Eliza alimkazia macho Cindy kwa ubaridi. "Cindy, Felix Media sio kampuni yako. Japo sijui ni njia gani uliyotumia kumfanya Chester akulinde kiasi hicho, unapaswa kuujua vizuri mtazamo wake. ”
Hofu fupi ilitanda moyoni mwa Cindy. Hata hivyo, alipokumbuka kwamba Eliza alimpiga makofi ya jeuri juzi kati, alicheka kicheko na kumwendea Eliza. Alipunguza sauti yake na kusema, “Eliza, huenda bado hujaelewa ni kwa nini kashfa zako za zamani zilifichuliwa kwa usiku mmoja. Ili kukuepusha na simanzi, ngoja nikuambie ukweli. Muda fulani nyuma, mtandao ulijaa habari kuhusu mimi na Simwendo. Kwa hivyo, Chester na mimi tulikuja na wazo hili ili kuifunika na kutumia kashfa yako kugeuza umakini. Angalia jinsi Chester anavyonitendea vizuri. Sentensi moja kutoka kwangu imesababisha kazi yako yote kuanguka. Hii ndiyo bei ya kunipiga makofi.”
Eliza alishangaa. Baada ya kuwa katika sintofahamu kwa sekunde kadhaa, haraka haraka akagundua kuwa ni kweli wazo hilo lilipendekezwa na Cindy.
Hata hivyo, kando na kuondoa kashfa ya Cindy, ingeweza pia kuwasahaulisha watu kuhusu tukio la kampuni hiyo kutozwa faini. Kwa maneno mengine, kujitolea kwake kulifanya Cindy ashinde na kufaidika na kampuni. Ni yeye tu ndiye aliyenyonywa kikamilifu.
Uso mzuri wa Eliza ukawa giza bila kujua. Cindy alishangaa sana kuona hivyo. "Lazima ulifikiri wewe ni kitu cha kuweza kushindana nami. Hii inathibitisha kuwa wewe si kitu moyoni mwa Chester."
Baada ya kutulia, aliwadokezea walinzi waliokuwa nyuma yake kwa macho. “Eliza alinionea. Mnaweza kumpiga makofi mawili usoni.”
Cindy alikuwa akimzaba kofi Eliza sawa na jinsi Eliza alivyompiga mbele ya watu wengi siku nyingine.
Walinzi wawili mara moja walikunja mikono na kuelekea kwa Eliza. Waliinua mikono yao na kuushika mkono wa Eliza pande zote mbili. Eliza alikodoa macho. Alikuwa karibu kupinga.
Ghafla, Shedrick alitembea kwa kasi. “Acha.”
Cindy hakuridhika. Alisema, “Mkurugenzi Mutui, Eliza alinifedhehesha sasa hivi majuzi. Nina hasira sana, kwa hivyo nimewaomba wamfundishe somo. Usinizuie. Lazima nitoe hasira yangu.”
Eliza alicheka kwa baridi. "Nilisema tu kwamba unawatendea watu tofauti kulingana na hali yao. Je, hiyo inahesabika kama kukukemea? Kuwa mkweli tu ikiwa unataka kunidhalilisha. Hakuna haja ya kunidharau na kuleta walinzi wawili wenye misuli pamoja nawe kwenye kampuni.”
“Nani alikuambia unipige kwenye kampuni mara ya mwisho? Ninaleta mabaunsa ili kujilinda tu.”
“Sawa, Cindy. Usiwe mkali sana.” Shedrick alimtazama Cindy bila furaha kama onyo.
Kusema kweli, hakumpenda Cindy. Hakuwa na ustadi wa kuigiza, na uimbaji wake ulikuwa mbaya. Hata hivyo, alikuwa na kiburi. Isingekuwa Chester kumlinda, asingemuunga mkono hata kidogo.
Sura ya Cindy ikabadilika, akauma mdomo. Alitoa msonyo mkali na kuwaondoa watu wake.
Shedrick alikasirika kidogo. Cindy alikuwa na kiburi sana. Alikuwa Mkurugenzi. Hakumheshimu kwa sababu tu alikuwa na ulinzi wa familia ya Choka.
“Eliza, nifuate.” Shedrick alipanda juu kwa hatua ndefu.
Eliza akafuata.
Walipoingia ofisini na mlango ukafungwa, alisema, “Mkurugenzi Mutui, asante kwa kunisaidia kutoka kwenye matatizo sasa hivi.”
“Eliza, mimi ndiye nasema asante. Na samahani.” Maneno ya Eliza yalimfanya Shedrick aingiwe na hatia. "Ilikuwa kinyume cha maadili kwa kampuni yetu kukufanya dhabihu wakati huu. Nilipaswa kujadili suala hilo na wewe, lakini…”
"Lakini lilikuwa wazo la Chester, sawa?" Eliza aliendelea na sentensi ya Shedrick kwa utunzi.
Ishara ya aibu ilitanda usoni mwa Shedrick. Kwa kweli, alimuhurumia sana Eliza.
Wanawake wengi walikuwa wamekaa na Chester, lakini Eliza ndiye angeweza kuingiza mapato mengi zaidi kwa kampuni. Hata hivyo, kampuni hiyo ilimkandamiza sana hivi kwamba aliishia kuwa dhabihu ya kampuni hiyo.