LISA KITABU CHA......... (13) SIMULIZI...........................LISA
KURASA....................626- 630
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY
Sura ya: 626 Katika wodi.
Lisa hakusema neno. Maumivu yalikuwa yameandikwa kwenye uso wake mdogo mzuri.
Alvin alimmenyea machungwa kwa uangalifu pembeni. Alielewa kuwa Charity ni jeraha kwake. Sasa, hata kuomba msamaha itakuwa muhimu. Uharibifu ulikuwa tayari umefanywa, kwa hivyo asingeweza kurekebisha.
"Lisa, mimi na wewe tutachunguza ukweli wa mwaka huo ili wahalifu wa kweli waadhibiwe na sheria." Alvin alimenya kipande cha chungwa na kumpa.
“Sina hamu ya kula,” Lisa alisema kwa unyonge. “Sijasema hayo yote ili
kukulaumu tu. Najilaumu pia. Kama ningekuwa nadhifu wakati huo, singemruhusu Kelvin kumuundia njama Charity. Hata niliolewa na mtu aliyemuumiza rafiki yangu.”
“Sio kosa lako. Kelvin ni mnafiki sana. Si ajabu nilizoea kumwona kama mtu aliyeshindwa.” Alvin alijidhihaki huku akimliwaza.
Kwa siku mbili zilizofuata, Lisa alikaa hospitalini.
Hakusoma habari zozote kwenye simu yake, kwa hiyo hakuona matusi makubwa dhidi yake kwenye mtandao. Angeweza kunyamaza, lakini Pamela hakuweza. Matusi ya wanamtandao yalimtia hasira. Alipomuona Lisa, alianza kulaani mara tu alipoingia mlangoni.
“Watu hao kwenye Mtandao hawajui
ukweli. Wanaamini kila aina ya uvumi. Nimekasirika. Kelvin ni mkatili sana. Jambo la kuchukiza zaidi ni kwamba polisi walimfungia kwa siku tano tu. Alipata siku tano tu za kukupiga hivi. Hujakasirika kuhusu hilo?”
"Hakuna kitakachosaidia hata kama nitakasirika. Alijisalimisha, na ana tabia nzuri. Mbali na hilo, Mtandao pia unamuunga mkono, kwa hivyo polisi hawatathubutu kumpa adhabu kali zaidi ya hiyo," Lisa alisema kwa upole.
“Kwa nini usitoe kauli chache? Watukane tu kama wanavyokufanyia. Kelvin ni wa ajabu sana. Amekuwa kwenye habari zinaovuma kwa kwa siku chache sasa, na joto halijapungua hata kidogo.” Moyo wa Pamela uliumia aliposema, “Wewe ni kama vile mimi nilivyokuwa zamani. Utarushiwa mayai vinza ukitoka nje.”
“Siyo kama sijawahi kukaripiwa hapo awali. Nilipotekwa na Alvin enzi hizo, nilielekezwa maneno popote nilipokwenda, nimezoea.” Lisa alisema bila kujali, "Tofauti pekee ni kukemewa vikali na kukemewa vikali zaidi."
“Lakini ukiacha hali iendelee kuwa hivi utaathiri sifa ya kampuni yako... ” Pamela alionekana kuwa na wasiwasi.
"Hilo sio muhimu hata kidogo. Mimi ndiye mbia pekee wa kampuni hata hivyo. Kwa hiyo hata sifa ikishuka, ni pesa zangu tu.” Lisa alikuwa mtulivu.
Pamela alitaka sana kumpa dole gumba kwa kustaajabisha kwa mtazamo huo wa kutokushindwa.
“Sasa, mimba yako ikoje?” Lisa aliuliza kwa wasiwasi.
“Ni sawa. Nimekuwa nikitapika sana hivi
karibuni na sina hamu ya kula.” Pamela akainama sikioni mwa Lisa na kumtazama Alvin aliyekuwa akipika jikoni. “Vipi nyinyi wawili mambo yanaendeleaje? Je, mnarudi pamoja? Pia, anajua kupika? Atachoma jiko... "
Uso wa Lisa ulikua mgumu. Hakujua jinsi ya kuelezea hali yake na Alvin pia. Siku hizi, amekuwa akitunza hali yake kutoka asubuhi hadi usiku badala ya kwenda kwenye kampuni. Hata alimfulia nguo na kumpikia chakula. Ingawa hakikuweza kuchukuliwa kuwa kitamu, aliweza kusema kwamba alikuwa makini, na hakikuwa na ladha mbaya kama hapo awali.
Hata hivyo, kurudiana pamoja na Alvin? Bado hakuweza kujifanya kana kwamba hakuna kilichotokea huko nyuma.
Pamela alisugua kidevu chake na kusema kwa kumaanisha, “Ninahisi kwa jinsi Alvin anavyokung’ang’ania,
hutaweza kumtoa katika maisha yako yote...”
Lisa alikosa la kusema.
“Kwanini usimruhusu tu?” Pamela alipumua. “Acha kupingana na hisia zako. Kadiri unavyokazana, ndivyo anavyozidi kukung'ang'ania wewe."
"Sis, nimeolewa sasa, sawa?" Akiwa amechanganyikiwa, Lisa alimkumbusha. “Vipi kama ungekuwa mimi? Katika ndoa yangu ya kwanza, mume wangu alichukuliwa na mwanamke mwingine, nami nilitendewa kama mgonjwa wa akili. Katika ndoa yangu ya pili, niliolewa na shetani na mnafiki ambaye alinipiga usoni katika hali hii. Unafikiri bado nina matarajio ya hisia na ndoa? karibu nipatwe na kiwewe.”
"Hiyo ni kweli, shoga yangu maskini." Kwa haraka Pamela alinyoosha mkono
na kumkumbatia kwa shida. “Hatutaolewa. Hatutapata wapenzi. Tutalea tu wapenzi wetu watatu na kila mmoja katika siku zijazo."
Alvin ambaye alikuwa akikata mboga jikoni, aliwaona wale wanawake wawili wakiwa wamekumbatiana, na uso wake mzuri ukawa mweusi.
Alijua walikuwa marafiki wazuri, lakini bado hakuweza kuvumilia hilo.
"Aende zake." Hakuweza kupinga kutoka nje kumwonya Pamela.
“Kwa nini?” Pamela aliinua kidevu chake kwa hasira. "Sote ni wanawake ambao tumejeruhiwa na mapenzi. Mwishowe, tumegundua kuwa wanaume sio wa kutegemewa. Wanawake pekee wanaweza kutejigemea. Lisa alisema anataka kuwa nami katika siku zijazo. Isitoshe, tayari tuna watoto, hivyo hatuhitaji mbegu za kiume ili kuendeleza jina la
familia.”
“Una kichaa.” Alvin akauma meno. “Ukitaka kupata mwanamke, tafuta mtu mwingine. Usimsumbue.”
Pamela alikoroma. “Unawaza kupita kiasi. Mtu ambaye amekuwa akiumizwa sana na wanaume ni Lisa. Ana kiwewe cha wanaume. Kuanzia sasa, mtu pekee atakayempenda ni mwanamke kama mimi."
Lisa alikosa la kusema. Yalikuwa ni maoni ya kawaida tu, lakini Pamela aliweza kusimulia hadithi kama hiyo. Lisa alivutiwa sana.
“Sawa. Saa za kutembelea wageni zimekwisha. Unaweza kuondoka sasa. ” Alvin alimshika Pamela na kumburuta hadi mlangoni.
“Alvin Kimaro, niachie. Unawezaje
kuthubutu kuweka mikono yako juu ya mwanamke mjamzito? Lisa hatakusamehe...”
Akiwa na 'ghadhabu, Alvin alifunga mlango kwenye uso wa Pamela.
"Kwanini ulifanya hivyo kwa rafiki yangu?" Lisa alimfokea.
"Ana tamaa mbaya kwako. Nilifanya hivyo ili kukomesha mawazo yake kama hayo.” Alvinalisema kwa umakini, “Lisa, wanaume bado ni bora kuliko wanawake. Angalau, wanaume wana nguvu zaidi kuliko wanawake. Ikiwa balbu ndani ya nyumba itavunjika, Ninaweza kuibadilisha. Ikiwa choo kimeziba, naweza kukizibua...”
“Naweza... piga simu mtu wa kazi asaidie katika hayo yote” Lisa alikosa la kusema.
Alvin aliinua uso wake. “Unapokuwa katika hali mbaya, nitakuruhusu unikaripie na kunipiga upendavyo. Ukiwa umechoka kwa ununuzi, ninaweza kukusaidia kubeba vitu vyako. Ninaweza pia kuwafundisha watoto, kuwalinda, na kuwa baba mzuri kwao. Majukumu haya siwezi kumpa mtu mwingine tena...”
“Inatosha.” Kichwa cha Lisa kilianza kumuuma kutokana na maneno yake. “Bado sijatalikiana na Kelvin, na sitaki kufikiria mambo haya. Hata nikipata talaka, nitakaa mwenyewe kwa miaka michache. Nimechoshwa na nyie wanaume. Ninataka kuishi kwa utulivu na uhuru peke yangu."
“Miaka michache?” Uso mzuri wa Alvin ulianguka.
"Ndio, miaka michache. Una shida na hilo?" Lisa aliinua nuso wake
kumtazama.
“Hapana. Chochote unachosema, ni sawa. Ni miaka michache tu. Hakika nitakuwa nimepona kabisa kufikia wakati huo. ” Alvin alijifariji na kurudi jikoni kupika.
Sura ya: 627
Lisa alifumba macho ili apumzike kwa muda mara ghafla simu ya Alvin iliyokuwa juu ya meza ya kitanda ikaita. Aliitazama na kuona jina la 'Hannah Gituro' likiwaka kwenye skrini. Alikuwa anawasiliana na huyo mwanamke?
Aliposikia simu hiyo, Alvin alitoka jikoni na kuona pia jina la mpigaji. Alimtazama Lisa kwa siri kabla ya kukandamiza kitufe cha kujibu mbele yake. Pia aliiweka kwenye laudispika.
"Hi, Alvin, hatimaye ulijibu simu yangu.
Nilidhani hautapokea." Kicheko cha Hannah kilisikika.
“Unahitaji kitu?” Alvin aliuliza bila kujieleza.
“Bado unaongozana na Lisa Jones hospitalini kila siku? Sielewi kwanini unajali sana mwanamke mzee kama yeye. Hata ameolewa na mtu mwingine. Anawezaje kulinganisha na mimi?" Hannah alikasirika kidogo kwa sauti yake ya baridi.
Lisaalikosa la kusema. Mwanamke mzee? Alikuwa mwanamke mzee? B*tch, tafadhali. Alikuwa na miaka ishirini na sita tu, sawa?
Alvin alisema kwa unyonge, “Bi. Gituro, unaonekana una yako tena. Baadhi ya wanawake wa umri wako tayari wameolewa na wana watoto, lakini
wewe bado, unajifanya kama una umri wa miaka 17 au 18.”
“Wewe... Nimesema kitu kibaya? Nina umri wa miaka ishirini tu, sawa?" Hannah alisema kwa hasira, “Alvin Kimaro, tayari nimekuonyesha heshima kubwa. Je, unapaswa kuwa na hasira na mimi? Sijasuluhisha matokeo na wewe mara ya mwisho kutokana na tukio lile la bafuni.”
“Inatosha. Sijamalizana na wewe kwa kuniwekea dawa mara ya mwisho pia.” Uvumilivu wa Alvin ulikuwa unatoweka kwa kasi. “Hannah Gituro, kaa mbali nami. Ninaumwa ninapoona wanawake wasio waadilifu kama wewe.”
“Oh, kweli? Je, utaniamini nikisema nitasimama na kuuambia ulimwengu kwamba ulikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa siri na Lisa Jones kwenye bafu wakati wa siku yangu ya kuzaliwa?
Ninaahidi kuwa utadharauliwa na kila mtu nchini. Familia zote tajiri na za kifahari zitakuona kama mtu asiye na haya, na hakuna mtu atakayekualika siku zijazo." Hannah alidhihaki.
Macho ya Alvin yalimtoka kwa ubaridi. Kwa utambulisho wa Hannah, Lisa bila shaka angekemewa vikali zaidi ikiwa Hannah kweli angesimama na kusema hivyo. Hakujijali mwenyewe, lakini alikuwa na wasiwasi juu ya Lisa...
Mkono mweupe na mwembamba ghafla ukampokonya simu yake. Lisa alisema huku akitabasamu, “Hakika, endelea kusema. Mwandishi wa habari akiniuliza, nitajibu tu kwa kueleza ukweli wa mambo ulivyokuwa. Alikuwa Bi. Gituro ambaye alimpa dawa mume wangu wa zamani bila aibu, kwa hiyo sikuwa na budi ila kujitokeza kwa ujasiri na kumsaidia.”
“Lisa Jones, wewe...” Hannah nusura aingiwe na hasira. Hakutarajia Lisa angekuwepo na kusikia kila kitu. Alikuwa karibu sana na Alvin?
“Lisa, huna aibu. Umeolewa lakini bado haujaridhika na hali yako. Sijawahi kuona mwanamke mwenye kudharauliwa kama wewe.”
“Asante. Ninafurahi tu kwamba ni Alvin pekee ndiye anayeweza kunipenda hata kama ulimwengu wote utanidharau. Lo, by the way, usiendelee kuniita mwanamke mzee. Ingawa nahisi kuwa umri wangu ni mkubwa zaidi kuliko wako, hakika wanaume watapenda urembo wangu zaidi kuliko wako. Wanaume kwa kawaida hawapendi aina za wanawake kama wewe."
Lisa alikata simu moja kwa moja bila kujali kama Hannah alikuwa na hasira. Kisha, akairusha simu kwa mtu fulani
aliyepigwa na butwaa pembeni yake.
"Nini? Je, umeumia moyoni kwamba nilimfokea mpenzi wako na kupoteza nafasi yako ya kuoa kwa Seneta Gituro?” Lisa aliuliza huku akitabasamu.
Uso wa mshangao wa Alvin ulimtazama, na tabasamu machoni pake lilikuwa tamu kama asali. “Sikulaumu. Je, Hannah Gituro anawezaje kulinganishwa na wewe? Ni msichana ambaye ni ushahidi wa mwanamke tu lakini ndani yake hakuna mwanamke, amechezewa maelfu ya mara elfu nje ya nchi. Na wewe...” Macho yake yakasimama kwenye eneo fulani la mwili wake. "Unamjua mwanamume mmoja tu, nami namjua mwanamke mmoja tu, sawa? Mmoja tu duniani kote."
“...Potea.” Lisa alihisi macho yake yanaishiwa nguvu kwa haya.
Alishtuka na kuvuta shuka kwa haraka huku akimkazia macho.
"Hayo yalikuwa maneno yako." Alvin alicheka na kunyata. "Lisa, napenda sana jinsi unavyoonekana sasa hivi, mtawala na mwenye wivu."
“Nani mwenye wivu? Sipendi Hannah anitumie kama tishio.” Lisa alimrukia. “Hata nilipokuwa nikikufukuzia wakati huo, sikuwa mtupu kama Hannah. Kukosa aibu ni jambo moja, lakini kuwachafua wengine ili upate unachotaka ni jambo lingine.”
"Ndio, mimi pia simpendi, lakini ... Labda tulimkosea sasa hivi, na atasema kwa hadhara. Ikiwa mtu mwenye sifa ya familia ya Gituro ataeneza uvumi huo, sifa yako ita...” Alvin alisita kuzungumza.
Lisa alimkazia macho. “Alvin Kimaro,
mbona unazidi kukosa maamuzi? Hana hata alikutishia sasa hivi. Uko wapi msimamo wako wa wakati huo na ukatili?"
Aibu ilitanda usoni mwa Alvin. "Sikuwa na udhaifu hapo awali, lakini sasa, wewe, Suzie, na Lucas ni udhaifu wangu."
Lisa alimtazama kwa macho yake safi kwa muda kabla ya kusema, “Alvin, sipendi kutishiwa. Wewe baba wa Lucas na Suzie, kwa hivyo sipendi utishwe kirahisi pia. Pesa na umaarufu ni za kupita. Tangu nilipokuja Nairobi, siku zote nimekuwa nikijulikana na watu wengi sana wakinizomea. Lakini vipi kuhusu hilo? Je, wanaweza kuniathiri vipi kando na kunikaripia mtandaoni? Ikiwa mbaya zaidi ni mbaya zaidi, nitawachukua watoto na kuondoka Kenya. Dunia ni kubwa sana. Kwanini niwe chini ya watu hao?”
Alvin alishtuka kidogo. Ghafla aligundua kuwa hakuelewa ni kiasi gani alikuwa amebadilika. Hata hivyo, mtazamo wake wa utulivu na kutojali kuhusu wakati ujao ulimfanya aone aibu.
“Umesema kweli Lisa. Ikiwa hali itakuwa mbaya zaidi, nitaondoka na wewe. Ikiwa Kenya haina nafasi kwetu, tunaweza kuishi katika nchi nyingine. Nina ujuzi wa lugha nne au tano za kigeni, hivyo bado ninaweza kupata pesa.” Alvin akatabasamu.
"Sikusema nitaondoka pamoja na wewe." Lisa alimtazama.
“Hata usipoondoka na mimi, nitakufuata mwenyewe. Nina miguu.” Alvin alitabasamu.” Lisa alikosa la kusema. “Sawa, ni wakati wa kula. Siwezi kukuacha ufe njaa.” Alvin akasimama.
Alasiri hiyo, wakati Lisa anaamka kutoka usingizini ili kuangalia simu yake, alikutana na habari ya Hannah ikiwa kwenye habari zinazovuma: [Ungamo la Hannah Gituro.]
Alibonyeza kuona kwamba wakati Hannah alipokuwa akihudhuria hafla iliyoandaliwa na brand moja maarufu, mwandishi alimuuliza, “Bi. Gituro, nilisikia kwamba kwenye sherehe yako ya kuzaliwa, mke wa Kelvin Mushi, Lisa Jones, alijificha bafuni na Alvin Kimaro. Je, hii ni kweli? Umesikia kuhusu hili?"
Hannah alitabasamu kwa huzuni. “Jambo hilo ndilo jambo lisilo la furaha kuwahi kunipata. Hata nilipigana na Lisa juu yake. Sikufikiri ingetokea hivyo. Yote ni makosa yangu, na sikupaswa kumwalika Alvin. Aliniokoa siku chache kabla ya hapo, kwa hiyo nilimshukuru sana, lakini sikutarajia kwamba ... yeye na Lisa wangefanya hivyo. Si ajabu
kwamba sikuweza kumwona usiku kucha.”
Mwandishi alishtuka. “Bi. Gituro, unampenda ... "
"Inatosha. Hatajibu maswali ya kibinafsi." Kabla Hannah hajazungumza, mlinzi aliyekuwa nyuma yake alikuwa amepanda na kumsimamisha mwandishi.
Mwandishi pia aliogopa utambulisho wa Hannah na hakufuatilia swali hilo. Lakini, sehemu hiyo tayari ilitosha kwa watumiaji wa mtandao kuunda mjadala mkali.
[Kwa hivyo, ni kweli kwamba Lisa na Alvin walimzunguka Kelvin kwa siri kwenye karamu ya Hannah?]
[Duh. Hannah hakukataa, kwa hivyo alikubali. Hakuweza kusema kwa uwazi
sana.]
[F*ck. Kwa nini ninaweza kuhisi ladha ya uchungu na huzuni katika sauti ya Hannah? Je anampenda Alvin, sawa? Asingepigana na Lisa vinginevyo.]
[Bado nashangaa sana kuhusu Alvin. Kweli sielewi. Yeye si mtu tajiri zaidi tena, na bado ana matatizo katika kipengele hicho, kwa nini wanawake wengi wanampenda?]
[Huwezi kusema hivyo. Alvin si mtanashati kidogo tu, ni mtanashati sana tu, sawa?]
[Hata hivyo, ninahisi kama Lisa na yeye ni kama saratani. Kama anampenda Alvin kwanini alikubali kuolewa na Kelvin. Kwanini wanapaswa kuwadhuru watu wasio na hatia na waaminifu?]
[Ninajihisi mgonjwa ninapoona picha za
Lisa sasa.]
[Lisa ni mrembo na anavutia. Kwa kumtazama tu usoni, unaweza kujua kwamba amelegea na hana haya. Ikiwa unatafuta mwanamke, kamwe usimtafute mtu kama yeye kwa sababu hakika atakusumbua. Kila mtu anaweza kuja kwangu ikiwa unataka kuona uso wake. Namba yangu ya WhatsApp ni ****** *]
[Nilisikia kwamba Lisa ana binti. Je! binti yake atakua kama yeye?]
[Ndio, nilisikia kwamba yuko katika Shule ya Awali ya Sunshine. Sitaki binti yake awe katika darasa moja na mtoto wangu. Hakika atajifunza jinsi ya kutongoza wanaume akiwa bado mdogo.]
[Kama mama, kama binti.]
Sura ya: 628
Karibu na mwisho, uso wa Lisa ulikuwa mbaya sana. Hakujali watu walisema nini juu yake, lakini hawakutakiwa kuwavuta watoto wao ndani yake. Hilo ndilo jambo moja ambalo asingeweza kuvumilia.
Muda si muda, alipokea simu kutoka kwa mwalimu wa shule ya awali. “Bi. Jones, unaweza kuwahamisha Suzie na Lucas hadi shule tofauti? Samahani. Lakini kwa sababu ya sifa yako mbaya ya hivi majuzi, wazazi wengi wamekuja shule ya chekechea kulalamika. Hawataki watoto wao wawe katika darasa moja na Suzie na Lucas. Mkurugenzi pia hataki iathiri kiwango cha uandikishaji wa shule, kwa hivyo tafadhali unaweza kujaza fomu za uhamisho? Ada ya masomo itarudishwa kwako."
“Sawa.” Lisa hakutaka kubishana.
Ikiwa shule ya chekechea inaweza kuwalazimisha watoto wake kuacha shule kwa sababu hii, haikuwa shule nzuri ya chekechea. Kwa bahati nzuri, watoto walikuwa wamechukua likizo wakati huo. Angeweza kufikiria kwamba ikiwa wangeenda shule, bila shaka wangeshambuliwa na watu wengi.
“Kelvin, kweli... umevuka mipaka.”
“Lisa, nimempigia Chester. Habari na picha za Lucas na Suzy zitafutwa mara moja.” Alvin pia alikuwa ameliona hilo, na alieleza kwa uso wa ukali, “niliweka mtu wa kulichunguza. Anwani na picha za shule ya awali ya Suzie zilitumwa na mtu ambaye alichochewa nyuma ya pazia. Inapaswa kuwa kazi ya Kelvin.”
“Ndio. Sitaki kuwaingiza watoto katika
hili.” Lisa alifumba macho.
Alipoona jinsi alivyokuwa akijaribu kuzuia hasira yake, Alvin aliweza kujilazimisha tu kutoka nje ya wodi ile. Alikunja ngumi kwa shida.
Kisha, Mike Tikisa alimpigia. "Niliona habari kwenye mtandao. Ninajua kwamba watoto waliathiriwa, na una hasira sana. Lakini haijalishi ni nini, unapaswa kuvumilia. Sio wakati wa kufichua nguvu zako bado."
“Najua.” Maumivu yalimuosha usoni mwa Alvin. "Nimekuwa nikivumilia, lakini siwezi hata kumlinda mwanamke wangu na watoto wangu. Najiona sina maana sana.”
"Hii ni ya muda tu." Mike alisema, "Kelvin anathubutu tu kuwa na kiburi kwa sasa kwa sababu ana familia ya Campos inayomuunga mkono. Mara
baada ya familia ya Campos kuanguka, atapunguzwa kuwa si chochote. Kufikia wakati huo, kutakuwa na fursa nyingi za kumwadhibu.”
Baada ya wiki katika hospitali, Lisa aliruhusiwa. Siku ya kuruhusiwa, mlango wa hospitali ulikuwa umejaa waandishi wa habari, hivyo Chester akapanga waondoke kwa siri kutoka kwenye lifti ya maegesho ya chini ya ardhi. Hata hivyo, walipotoka nje ya eneo la maegesho, bado walikuwa wamezuiwa na waandishi wa habari. Kila aina ya majani ya mboga, mayai yaliyooza, na nyama iliyooza vilitupwa kwenye gari. Walirundikana kwenye gari, na kuifanya iwe ngumu kusonga. Baadhi ya watu walifungua hata mlango wa siti ya dereva na kumburuza dereva wa familia ya Ngosha chini kwa nguvu. Kisha, waandishi wa habari kadhaa waliingia.
"Mnafanya nini? Bado kuna sheria?" Joel alikasirika sana alipoona kundi la waandishi wa habari vichaa.
Waandishi walimpuuza tu na kuelekeza kamera zao kwa Alvin na Lisa. “Wow, Alvin kweli yuko hapa. Uhusiano wa Lisa umekamatwa kwa njia isiyofaa.”
"Si tayari mmetupiga picha nilipomleta hospitali?" Alvin alishika kamera ya mwandishi huyo akiwa na uso baridi. "Ondokeni, au msinilaumu kwa kukosa adabu."
“Hatutoki. Utatufanya nini? Utatupiga?” Waandishi hawakuwa waoga. “Nyie wanandoa mnaodanganya. Mnathubutuje kuwa na kiburi wakati mna uhusiano batili wa kimapenzi? Ninataka kukupiga picha wazi na kuruhusu ulimwengu uone vitendo vyako vibaya."
“Unataka kutupiga picha?” Lisa ghafla alifunua tabasamu la hasira. Baada ya kulazwa hospitalini kwa siku chache zilizopita, uvimbe usoni mwake ulikuwa umepungua sana, lakini uso wake mdogo ulikuwa bado umepauka.
“Sio tu kuwa nataka kupiga picha, lakini pia nataka kukuhoji...” Mwandishi alifoka. “Je, vitu vilivyoibiwa ni vyema zaidi ya vile ulivyo navyo? Je, umewahi kumpenda Kelvin hapo awali? Yeye ndiye mtu aliyekupa kila kitu na kukupenda kimya kimya, lakini ulimtumia bila huruma na kumkanyaga. Je, hujisikii kuwa na hatia hata kidogo? Je, umepoteza dhamiri yote? Hakuna mtu aliyekufundisha maadili hapo awali?"
“Lisa, puuza. nitamfukuza.” Alvin alitazama sura za waandishi wa habari
zenye jeuri na akashindwa kuvumilia tena.
“Kwanini ufanye hivyo? Waache tu wanihoji. La sivyo, watatuwinda kama mbwa.” Lisa alitabasamu sana akimtazama mwandishi. "Haya, haipendezi ikiwa mtauliza tu maswali ya kushosha. Kwanini tusifanye jambo la kusisimua zaidi?”
Kisha, ghafla akageuza uso wa Alvin na kumbusu kwa nguvu midomo yake myembamba. Alvin, ambaye alikuwa amepitia kila aina ya hali hapo awali, pia alikuwa ameganda.
Joel aliyekuwa na Alvin na Lisa alikasirika na kutaka kugonga mlango kwa kichwa. "Lisa, unafanya nini?"
Baadhi ya waandishi wa habari walipigwa na butwaa, huku wengine wakaanza kupiga picha. Ilikuwa ni mara
ya kwanza kukutana na wahojiwa kama hao. Baada ya kumaliza kupiga picha, ghafla walipata fahamu zao.
"Je, unajaribu kutuambia wazi kwamba ulimsaliti Kelvin katika ndoa?"
“Hapana, najaribu kumwambia Kelvin kupitia wewe kuwa simpendi na ninahisi kuchukizwa naye. Afadhali niwe na Alvin kuliko kuendelea kuishi naye. Nyote mnadhani ananipenda sana, sivyo? Ni sawa. Saa 8:00 asubuhi kesho, nitawajulisha wote jinsi alivyo na upendo,” Lisa alitabasamu kwa mbwembwe na kupepesa kope zake.
“Hiyo ina maana gani?” Waandishi hawakuwa na wakati wa kujibu.
Alvin aliingia kwenye kiti cha dereva na kumshusha mwandishi. Alipunguza dirisha na kuiambia kamera, “Unanitazama sana. Wakati mimi
nilishambuliwa kwenye kituo cha polisi mara ya mwisho, sehemu fulani yangu ilipatwa na kiwewe. Tangu wakati huo, nimekuwa nikienda kwa mtaalamu kwa ziara ya kufuatilia kila wiki. Siwezi kumfanya chochote. Unaweza kuangalia na kujua kwamba Chester Choka alianza kutafuta madaktari mashuhuri wa andrology nje ya nchi takriban mwezi mmoja uliopita.” Waandishi walipigwa na butwaa. “Usitudanganye. Hapo awali, ulisema kwamba huwezi kufanya hivyo na ulienda kwa idara ya androlojia, lakini ulipomkabili Sarah Njau mahakamani mara ya mwisho, wakili wao aliwasilisha ushahidi kwamba ulinunua dawa za kupanga uzazi.”
“Kwa kweli sikuwahi kufanya hivyo na Sarah. Sikuwa na shida na mwanamke ninayempenda, lakini nina shida sasa. Kama nilivyosema, utajua ukiafuatilia. Nimekuwa natumia dawa,” Alvin
alisema kwa unyonge.
"Lakini mara ya mwisho ulipokuja hospitalini na Lisa, tuliona wazi kuwa amefunikwa na alama za busu na wewe pia," mwandishi alisema kwa ukaidi.
"Ndio, nilifanya hivyo," Alvin alitikisa kichwa kwa jazba. "Kwa bahati mbaya, naweza kumbusu tu. Siwezi kufanya lolote lingine.”
"Kwa kifupi, Lisa alidanganya kwenye ndoa na nyinyi wawili mna uhusiano usio halali," mwandishi alikashifu kwa dharau.
Alvin alicheka gizani. “Kwa kuwa nilikuwa na ujasiri wa kumpokonya mke, unadhani bado ninajali sifa yangu? Nampenda. Iwe ameolewa au la, nitamsumbua milele. Hatawahi kuepuka makucha yangu katika maisha haya. Endelea kunikaripia ukipenda.” Alisema
hivyo kwa uwazi na kiburi.
Waandishi wa habari waliokuwapo pia walipigwa na butwaa.
Kulingana na uzoefu, hii haikuwa jinsi walivyotegemea. Walitegemea huenda Alvin na Lisa wangejitenga na kujiweka mbali na kila mmoja huku wakijitetea.
“Nyinyi wawili hamna aibu. Ni washawishi wabaya kwa jamii, "waandishi wa habari waliwashutumu.
Alvin alicheka. "Najua tu kwamba kama si Kelvin, nisingeweza kuachana na Lisa kwanza. Tangu miaka mitatu iliyopita, alianza kuchokonoa uhusiano wangu na Lisa kwa siri. Anapanga na kuhesabu bado anajifanya kama muungwana. Nitafichua sura halisi ya mnafiki huyo mapema au baadaye.” Kisha akawasha gari. Alipoona bado waandishi hawafanyi njia, akakanyanga moto kwa nguvu.
Muungurumo wa injini uliwatisha waandishi wa habari. Alvin alitabasamu kwa madaha. Baada ya kubadilisha gia, gari liliondoka bila kizuizi.
Sura ya: 629
Ndani ya gari, Joel alitaka kulipuka kwa hasira kutoka kwa watu hawa wawili.
“Lisa, ulikuwa unawaza nini? Tayari umekemewa vya kutosha na watu, na bado ulimbusu hata mbele ya waandishi wa habari. Unafikiria kurudiana pamoja naye?” Kisha akamkabili Alvin, “na wewe Alvin, mbona unakuwa kama mzimu ambao hauachi kumsumbua? Huwezi kufanya tena, kwanini usimruhusu binti yangu aende? Unataka kumkanyaga maisha yote?"
Alvin hakuongea chochote akamuacha Joel amkemee.
Masikio ya Lisa yalipohisi kama yangeanguka kutokana na kuhangaika, hakuweza kujizuia kusema,
“Baba, huoni? Waandishi wa habari hawataniamini hata niseme nini, kwa hivyo hakuna haja ya kuificha. ”
“Wewe...” Joel alikabwa. "Lakini huwezi kumbusu tu mbele ya kamera. Je, hakuna wanaume waliobaki duniani? Hajakuumiza vya kutosha?”
Alvin alionekana kuumia na kuita kwa upole, “Baba...”
“Acha. Unamuita nani baba? Sina mwana wala mkwe kama wewe,” Joel alisema kwa hasira.
"Anko Joel..." Alvin angeweza tu kubadilisha utambulisho wake kwa jinsi Joel alivyokuwa amefadhaika. "Ilikuwa kosa langu hapo awali. Inaeleweka kwa wewe kunifokea, lakini huwezi
kusukuma lawama zote kwangu. Ukiwa baba yake Lisa, hukupata mkwe mzuri na ukamruhusu aolewe na fisadi kama Kelvin anayepiga wanawake.”
Joel alikosa la kusema tena kusikia maneno ya Alvin. Ilikuwa ni aibu. Ndiyo, alichosema Alvin kilikuwa kweli. Kama baba, alishindwa kabisa. Hapo awali, kila mara alimsifu Kelvin, lakini Kelvin aliishia kuwa fisadi.
“Lisa, kosa ni la Baba. Baba amechanganyikiwa—,” Joel alipumua kwa sana. “Baada ya tukio hili, ninahisi kama hakuna wanaume wengi wazuri katika ulimwengu huu. Sitakushauri uolewe tena siku zijazo. Rudi nyumbani na Baba atakulea na kukutunza. Sitajisikia raha ukiolewa na mwanaume mwingine. Ni bora nikuhudumie mimi mwenyewe.”
“Sawa, Baba. Sina mpango wa kuolewa
tena,” Lisa aliitikia kwa kichwa.
Moyo wa Alvin uliruka kwa hofu. “Anko Joel, huwezi kusema hivyo. Tayari uko katika hamsini zako. Huwezi kuandamana na Lisa milele. Siku moja, utaondoka mbele yake.”
"Basi bado ana watoto wake," Joel alisema kwa upole. “Nikifa, Suzie na Lucas watakuwa watu wazima. Pia ni jukumu lao kama watoto kumtunza.”
"Lakini pia watakuwa na mke au mume na watoto. Lisa bado anahitaji kupata mume anayeaminika. Mimi ndiye chaguo bora. Ninajua mizizi yangu ndani ... "
"Ndio, unaijua vizuri mizizi yako," Joel alicheka na kumtazama. "Unajua kwamba mizizi yako pia imevunjika."
Alvin alikosa la kusema. Lisa aliona
sura iliyopigwa ya Alvin na akachungulia dirishani tu kujibaraguza. Baba yake alikuwa katili wa maneno bila kutarajia. Walipofika kwenye jumba la Ngosha, Alvin alifukuzwa bila huruma na Joel. Lisa alizungumza na Suzie na Lucas kupitia ‘Hangout’ ya Video kwa muda mrefu kabla ya kutafuta habari zilizokuwa zinavuma. Video ya Alvin na yeye hospitalini ilifikia maoni zaidi ya elfu kumi.
[LisaJones ameenea sana. Ana kiburi sana hata akiwa na mume. Atapata adhabu mapema au baadaye.]
[Kelvinni muungwana sana, lakini bado alimdharau. Hana aibu sana.]
[Hapana, Lisa na Alvin walimaanisha nini kwa kitendo hichi? Je! walikuwa wakidokeza kwamba Kelvin ni mnafiki?]
[Kwa mtoa maoni hapo juu,
usidanganywe na Lisa. Mwanamke huyo anajaribu kupaka matope kwa wengine ili kugeuza usikivu kutoka kwake, lakini sisi sote tuna macho makali.]
[Lisa alisema atatujulisha jambo saa 8:00 asubuhi kesho, nadhani lazima atakuwa amepata jambo la kusema hivyo.]
[Haijalishi anafunua nini, ni bora ikiwa hatuamini. Kwa vyovyote vile, ni ukweli kwamba alimsaliti mumewe.]
Iwapo angekuwa Lisa Jones wa miaka mitatu iliyopita, angekasirishwa sana na maneno ya wanamtandao hao hivi kwamba angetaka kutapika damu. Hata hivyo, ilimbidi akubali kwamba sasa moyo wake ulikuwa na nguvu zaidi. Hakuwa tena mtu ambaye angeweza kuyumbishwa kihisia na wengine.
Simu yake iliita ghafla. Alitazama chini kwenye simu na ubaridi ukamtoka machoni mwake. Aliitikia wito na sauti ya Kelvin ikasikika kwa sauti ya upole sana, “Lisa, tukutane.”
Aliposikia sauti ya Alvin, Lisa alihisi kama nyoka mwenye sumu amemrukia. Siku hiyo, Kelvin alimpiga kana kwamba alikuwa shetani. Lakini, alikuwa mpole kama malaika alipoongea kwenye simu. “Umetoka jela?” Lisa aliuliza kwa ubaridi.
"Ndio, polisi pia walinihurumia, lakini nilikuwa na wakati mbaya sana gerezani wiki hii iliyopita. Lisa, nimekukumbuka...” Maneno mawili ya mwisho yalitamkwa haswa kwa maana.
"Ni bahati mbaya. Nimekukumbuka sana pia,” Lisa alisema kwa sauti ya chini. “Lakini sithubutu kukutana nawe tena. Nani anajua kama utaniongezea
kitu kwenye maji yangu, au utanipiga tena.”
“Lisa, sikufanya makusudi. Nilipoteza udhibiti siku hiyo. Ni kwa sababu nakujali sana. Hutazungumza kuhusu talaka, sivyo?” Kelvin alihema. “Sitasema mengi kwenye simu. Nani anajua ikiwa unairekodi?"
Lisa aliitupia jicho simu iliyokuwa ikirekodi simu hiyo na kuguna kuwa kweli Kelvin alikuwa mjanja na makini sana.
“Ikiwa hutakutana nami, basi sitalazimika kukupa talaka,” Kelvin alitabasamu. “Ni vyema tukifungwa pamoja hivi. Utakuwa mke wangu daima. Hata ukifa, bado utakuwa wa familia ya Mushi.”
Lisa alicheka na kusema, “Kelvin, usinitishe. Hilo halitafanya kazi kwangu.
Unafikiri ninashikilia ushahidi ili kujadiliana na wewe kwa talaka? Hiyo ndiyo niliyopanga awali, lakini kutokuwa na haya kwako kulibadilisha mawazo yangu. Unapenda kuigiza, sivyo? Natazamia jinsi wengine watakavyokutazama wakati barakoa yako inapovuliwa.”
Upumuaji wa Kelvin ulikuwa mzito zaidi, “Lisa, unazungumzia ushahidi gani? Je, nimefanya jambo baya?”
“Ndio, endelea kuigiza, Kelvin. Nataka kukuambia kuwa hunijui vizuri.”
Lisa akakata simu.
•••
Ndani ya gari.
Simu ikakatika na Kelvinakahisi huzuni. Lisa alimaanisha nini? Je, alitaka kuachia video ya Regina na yeye? Vipi yeye. Ikiwa angethubutu kuiachilia,
asingemtaliki hata kama angekufa.
“Bwana Mushi, kamera hizi mbili zilipatikana ofisini kwako,” Regina alipauka huku akizitoa zile kamera mbili ndogo.
Hakuthubutu kufikiria kuwa vitendo vyake vya kipuuzi na Kelvin siku hizo vilirekodiwa. Kelvin alizitazama kamera na kumpiga kofi usoni. "Wewe mjinga. Nani alikuruhusu kunitongoza ofisini kwa uzembe?”
Regina alikasirishwa na kipigo. Ndio, alichukua hatua wakati mwingine, lakini ilichukua vidole viwili kuvunja chawa. Ikiwa asingeanza, Kelvin angeenda kwa Sara badala yake. Alitaka tu kupata nafasi yake.
"Samahani, Bwana Mushi." Regina hakuthubutu kujibu na aliweza tu kuomba msamaha kwa sauti ya kimya.
Kelvin akashusha pumzi ndefu. Wakati huo, Mason alimpigia simu ghafla. "Kelvin, hali yako na Lisa imekuwa gumzo hivi karibuni."
Kelvin alikasirika na kusema, "Bwana Campos "Ninataka tu kujua ikiwa Lisa ana chochote kibaya dhidi yako,"
Mason alisema kwa upole. "Sitaki familia yangu iingie kwenye matatizo."
"Hapana, amepata tu jambo fulani kuhusu uhusiano wangu," Kelvin alisema kwa sauti ya chini. “Bwana Campos, unaweza kunisaidia? Sitaki hili lifichuliwe.”
"Sijakusaidia vya kutosha?" Mason alicheka kwa baridi. “Unafikiri nilikuwa sijui? Hapo awali, ulitaka kundi hilo la wauaji wawaue mapacha wa Lisa.”
Kelvin alikunja ngumi.
"Kelvin, hata hauwaachi watoto wa miaka mitatu? Ukatili wangu hauwezi kulinganishwa na wako,” Mason alisema kwa makini. “Unataka nikusaidie, lakini natakiwa kukusaidiaje? Kumteka Joel Ngosha? Au kuwateka nyara watoto wawili ili kumtishia Lisa? Unafikiri watakuwa hawajajiandaa? Je, unafikiri mimi ndiye ninayesimamia nchi au nina uwezo wa kudanganya umma na kufanya lolote nipendalo?”
Moyo wa Kelvin ulirukaruka. "Hicho sio nilichomaanisha."
Mason alipumua. "Mara ya mwisho ulipomsihi Jerome amdhuru Alvin, karibu umuue Hannah Gituro. Je! unajua ilinigharimu kiasi gani kusuluhisha hilo?"
“Samahani, Bwana Campos. Sikujua
ingeisha hivyo. Niliona kuwa Jerome Campos alitaka Alvin afe...”
“Nakwambia, watu si wajinga. Watoto hao wawili walipokaribia kupata ajali mara ya mwisho, iliibua mashaka ya polisi. Jambo kama hilo likitokea tena, polisi hakika watafuata dalili. Unapaswa kufikiria tena na usilete shida yoyote." Mason alikata simu.
Sura ya: 630
Kelvin alikasirika sana akataka kuponda simu yake. Kwa hakika aliweza kusema kwamba Mason hakutaka kumsaidia. Alifanya mambo mengi kwa ajili ya familia ya Campos siku za nyuma. Sasa baada ya familia ya Campos kufikia cheo cha juu, hawakumthamini tena. Kwa bahati nzuri, alifanya mipango mingine, lakini jambo lingine lilipaswa kufanywa kwa wakati mmoja.
Kwa haraka akapiga namba ya Sarah.
Nusu saa baadaye, wote wawili walikutana katika jumba la kibinafsi la Kelvin.
“Bwana Mushi, karibu tena,” Sarah alimtazama kwa tabasamu. "Nini tatizo? Uko katika hali mbaya?"
“Vipi Rodney sasa hivi? Familia ya Shangwe bado inampuuza?" Kelvin aliuliza kwa ubaridi.
Uso wa Sarah ukawa ngumu. Alijua kwamba Kelvin alimsaidia tu wakati huo kwa sababu ya familia ya Shangwe nyuma ya Rodney. "Familia ya Shangwe bado ina hasira, lakini usijali. Baada ya yote, Rodney ni mtoto wa Jason. Haiwezekani wampuuze.”
"Itachukua miaka mingapi?" Kelvin akatoa chupa ya mvinyo na kuifungua. Tafakari ya macho yake katika mvinyo mwekundu wa giza ilionekana kuwa ya
ajabu sana. "Sarah, wakati mwingine, lazima utumie ubongo wako. Ikiwa Rodney ataendelea hivi, una subira vya kutosha kukaa naye kwa miaka michache zaidi?”
Sarah alishikwa na butwaa ghafla. Kitu pekee ambacho angeweza kufanya sasa kilikuwa ni kushikilia kwa uthabiti na mti mkubwa kama Kelvin.
"Muache Rodney kwa muda na umruhusu arudi kwa familia ya Shangwe."
Kelvin alimmiminia glasi ya divai na kumshauri, “Mradi tu atakuacha, familia ya Shangwe itampa nafasi nyingine. Nathan Shangwe hivi karibuni atapanda kiti cha Urais. Na mtu kama yeye kumuunga mkono Rodney, mustakabali wake hautakuwa na kikomo. Yeye ndiye mjukuu mkubwa zaidi wa wajukuu wa familia ya Shangwe. Hivi karibuni au baadaye, atachukua familia ya
Shangwe. Kadiri mtu anavyopanda juu, ndivyo anavyozidi kukosa mapenzi yake ya kwanza.”
Macho ya Sarah yakaangaza. Kelvin alitabasamu. "Ikiwa utaendelea kuandamana naye kama mjinga, hata kama una mtoto wake, familia ya Shangwe inaweza kutokubali. Lakini siku moja atakapokuwa na mamlaka, nami nikimsaidia kwa siri, nafasi ya Bibi Shangwe itakuwa si nyingine ila yako.”
Sarah alifurahishwa na maneno yake.
Kelvin alimtazama. “Sarah inabidi uelewe kuwa haiwezekani nikuoe. Ulikuwa na Rodney na Alvin, na vijana kutoka kwa familia zenye ushawishi wataogopa kuwa karibu na wewe zaidi na hakuna uwezekano wa wao kukuoa. Sasa, kitu pekee unachoweza kufanya ni kumruhusu Rodney kurudi kwenye familia ya Shangwe."
“Nimekupata.” Uso wa Sarah ulibadilika rangi kutokana na maneno ya Kelvin. Alijua kwamba sifa yake haikuwa nzuri, lakini Kelvin alikuwa anazungumzia fursa.
Baada ya kuondoka, Kelvin alienda haraka kwenye jumba la familia la Ngosha. Hata hivyo, alizuiwa na mlinzi huyo mara tu alipofika getini. Joel mara moja alitoka nje na mlinzi baada ya kujua ujio wake.
“Kelvin, uko kwa wakati tu. Nilikuwa karibu kwenda kukutafuta. Wewe mnyama, unawezaje kuthubutu kuinua mikono yako dhidi ya binti yangu." Joel alikasirika sana hadi akamsalimia Kelvin kwa ufagio.
“Baba, endelea kunipiga. Ilikuwa ni kosa langu kumuumiza Lisa.” Kelvin hakukwepa akapiga magoti chini huku
akionyesha uchungu.
Joel aliganda, lakini alielewa mara moja alipoona wanahabari kadhaa wamejificha karibu. “Kelvin, wewe ni mjanja. Nikikupiga nitaona kwenye vichwa vya habari vya kesho Joel Ngosha alikuonea bila kutofautisha mema na mabaya.” Joel alidhihaki.
“Baba...” Ghafla Kelvin alisema kwa sauti ya chini, “Nimekuja kukuambia kwamba mtu akiwa kichaa anaweza kufanya lolote. Alvin sio vile alivyokuwa. Hawezi kuwalinda wazee au wajukuu zako, hasa wazee wawili wa familia ya Ngosha. Unapaswa kumwambia Lisa afikirie kwa makini."
Uso wa Joel ulibadilika. “Mnyama wewe. Unathubutuje kuwatumia wazazi wangu kunitisha?"
“Baba, mshawishi. Chukua ushahidi tukae chini tuongee. Anaweza hata
kunitaliki mapema,” Kelvin aliinamisha kichwa chake chini na kuondoka.
Joel alizuia hamu ya kumpiga hadi kufa na akarudi kwenye jumba lake kumwambia Lisa juu ya hili.
“Lisa, Kelvin ni mwendawazimu. Yeye ni mwendawazimu. Vipi... unamtaliki kwanza?”
"Acha nifikirie juu yake, baba." Lisa alijifanya kukasirika na kuhema.
Logan akamtazama. Walipopanda ghorofani, aliuliza, “Hutamtaliki?’
"Bila shaka hapana. Nilimdanganya tu baba yangu. Siku zote yeye ni mwoga na hana maamuzi linapokuja suala la familia yake. Sitaki kutishiwa na Kelvin. Isitoshe, mtu anayenitisha hataruhusu watu walio karibu nami waende kwa sababu tu ninakubali kutishika.” Lisa aliongeza kwa ubaridi, “Kadiri Kelvin
anavyonitisha, ndivyo anavyojali zaidi. Kwa kuwa alinifanyia fujo, siwezi kamwe kumruhusu awe rahisi hata nikilazimika kupigana hadi mwisho wa uchungu.”
Logan alimtazama kwa kupendeza. “Nimegundua kuwa unanivutia zaidi na zaidi. Ikiwa ungekuwa mwanamume, ningeweza hata kukuangukia.”
Pembe za mdomo wa Lisa zilitetemeka. “Usiongee kana kwamba wewe ni mwanamke. Kumbe siku hiyo nilichanganyikiwa. Sikufanya chochote kwako, sawa? Ninaogopa kwamba Austin ananichukia.”
Pengine hakuna mtu zaidi yake aliyejua kwamba wanaume hao wawili walipendana. Alipomwokoa Logan wakati huo, Austin pia alimshukuru. Hakutaka kumuacha Logan, hivyo Austin aliongozana naye na kumfanyia kazi Lisa pia. Lisa alikuwa wazi na
hakujali sana mambo haya. Baada ya yote, aliamini upendo haukuwa na jinsia.
Uso mzuri wa Logan ulijawa na aibu. “Ulichangamka sana siku hiyo. Nisingejilinda vizuri, ungenivua nguo kabisa.”
Lisa alikosa la kusema. Je, alikuwa mwendawazimu kiasi hicho?
“Kwa hiyo ulinipeleka kwa Alvin?”
"Ndiyo ... Uliponivua nguo, uliendelea kuita jina la Alvin," Logan alisema kwa unyogovu.
"...Inawezekanaje?" Macho ya Lisa yalimtoka. Alikataa kuamini kwamba alifanya hivyo.
Logan alimkazia macho kimyakimya kana kwamba anasema “Hilo haliwezekani vipi?”.
"Samahani..." Lisa aliinamisha kichwa chini akiomba msamaha.
Alvin alimkata kidole Logan, lakini sio tu kwamba hakulipiza kisasi, lakini pia bado alikuwa amenaswa na Alvin. “Sahau, mimi si mtu mdogo kiasi hicho. Ni kidole tu. Unaweza kuwa na yeyote unayemtaka, kwa hivyo usiwe na mashaka kwa sababu yangu. Kando na hilo, Alvin pia aliangukia katika njama za Sarah na Kelvin.” Logan alipunga mkono wake kwa kujieleza bila wasiwasi.
Hilo lilimfanya Lisa ajisikie vibaya zaidi. Angewezaje kuliita jina la Alvin wakati huo? Hakuweza kufanya mapenzi tena. Kulikuwa na maana gani ya kumwita? Lisa alihema kwa huzuni. Ni kweli aliuzoea mwili wa Alvin?
"By the way, kata baadhi ya matukio potovu na ya kusisimua ya Kelvin na
uyaedit vizuri," Lisa alitabasamu. "Kesho, nitaonyesha umma sura halisi ya Kelvin."
TUKUTANE KURASA 631-635
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully.