Detective Kipepeo
New Member
- Jul 28, 2022
- 4
- 7
Sehemu ya 1.
Jakson Maiga.Koplo, kutoka kituo kikuu cha Polisi Arusha, alionekana na mawazo mengi kichwani kuhusu hatma ya maisha yake ya baadae, akiwa ndani ya gari dogo la polisi, nje ya benki ya Meridian iliyoko Clock Tower .
Koplo Maiga ni kijana mwenye miaka 27, mrefu, maji ya kunde, mwenye umbo kakamavu.mwenye malengo ya kuwa Sajenti wa polisi hapo baadae, cheo kitakachomuwezesha kufikia malengo yake ya kuoa, kuwa na watoto, na kuwa na maisha mazuri hapo baadae.Kitu ambacho hakiwezekani mpaka pale Sajenti Kimaro atakapostaafu, au kufariki.
Sajenti Kimaro, ambae ameshapita muda wake wa kustaafu wa miaka 65, pamoja na uchapakazi wake wa kiwango cha juu, ilitakiwa awe amestaafu na kumpisha Maiga kuchukua cheo chake cha Usajenti, Cheo ambacho kitampatia nafasi koplo Maiga ya kupata mshahara mkubwa utakaomuwezesha kumuoa mchumba wake anaempenda sana Hadija.
Ukiacha mawazo haya ya kupanda cheo, Koplo Maiga alikuwa na hasira za kupangwa lindo kwenye benki ya Meridian siku hii ya jumamosi jioni, muda ambao alitakiwa awe na mchumba wake Hadija, na hii ilisababishwa na taarifa ya dharura kutoka kwa Sajenti Kimaro,baada ya meneja wa benki ya Meridian ndugu Joseph Kigai, kupata ugonjwa wa mshtuko wa moyo ghafla.
"Samahani kijana wangu" Sajenti
Kimaro alimwambia Maiga," nimepata dharura kuna mambo muhimu naenda kuyashughulikia", kaa hapa ulinde benki, huwei jua, anaweza kutokea mwehu akapata wazo baya,na pia ndani ya benki yuko Janet, anamsubiri meneja mpya kutoka makao makuu ,aje kuchukua nafasi ya meneja wa sasa, ndugu Kigai ambae anaumwa, najua ulikuwa na miadi na mchumba wako Hadija,lakini hii ni dharura, utapata muda mwingine wa kukutana na mchumba wako, lakini sio leo" Sajenti Kimaro alimwambia koplo Maiga.
Koplo Maiga amekaa kwa muda wa masaa mannne sasa toka apate maagizo kutoka kwa Kimaro, na matumaini yake ya kuonana na mchumba wake yametoweka, Akaona gari dogo aina ya toyota corola taratibu inasimama kwenye parking za benki ya Meridian,akamuona kijana wa makamo, mrefu, mwenye umbo la kimazoezi anashuka kutoka ndani ya gari,na kuekea kwenye mlango mkuu wa kuingia benki, koplo Maiga kwa haraka akashuka nje ya gari.
"Wewe! ", Koplo Maiga akaita, " hebu subiri, benki imefungwa," koplo Maiga akafoka kwa hasira, Yule jamaa akasimama na kumwangalia Kolplo Maiga, alivyomuona Maiga anamkaribia, akatabasamu. " Jina langu ni Chriss Ruge," akajitambulisha kwa Koplo Maiga, " ni meneja mpya wa Meridian Benki",Koplo Maiga akamuangalia kwa makini Chriss, halafu akampa mkono,"Mimi ni Koplo Maiga, ninaweza kuona kitambulisho chako"?. Koplo Maiga akamuuliza, Chriss akaingiza mkono kwenye mfuko wake wa nyuma wa suruali, akchomoa wallet yake,na kutoa kitambulisho chake cha benki na kumpa Koplo Maiga,"hiki kitatosha"? Koplo Maiga akapokea kitambulisho cha Chriss, akakiangalia kwa makini, aliporidhika akamrudishia Chriss kitambulisho chake."Sajenti Kimaro hakutaka Janet abaki mwenyewe ndani ya benki,akaniagiza nimlinde, lakini kwa sababu umekuja,mimi naondoka", Koplo Maiga akamwambia Chriss.
"Vipi hali ya Joseph Kigai, ana unafuu"? Chriss akamuuliza koplo Maiga, "Mhh, bado hali yake sio nzuri, daktari kasema labda tumwangalie mpaka kesho, labda mambo yanaweza kubadilika",Koplo Maiga akasema."Ngoja nimuangalie Janet huku ndani ya benki,atakuwa amechoka,anataka kwenda nyumbani", Chriss akamuambia Koplo Maiga. ""Mhh kweli , maana alimkuta meneja yuko chini amedondoka, Janet atakuwa na mshtuko bado", koplo Maiga akamuambia Chrriss. Chriss na koplo Maiga wakaanza kutembea kuelekea kwenye lango la benki, mbele yao katikati ya mlango wa benki, wakamuona binti mrembo mwenye umri kati ya miaka ishirini na tano mpaka ishirini na saba amesimama."Huyu ni bwana Chriss",koplo Maiga akamuambia Janet.Janet akamuangalia Chriss kwa mshtuko, mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio" What a man!" Janet akatahayari utanashati wa Chriss. "Samahani kwa kukuchelewesha Janet", Chriss akasema."Hakuna shida"Janet akamuambia Chriss, "unaingia ndani"? Janet akauliza, Koplo Maiga akasema, Acha mimi niondoke, sina kitu kingine cha kufanya hapa", Chriss akaagana na koplo Maiga, akaanza kuongozana na Jenet kuingia ndani ya benki.Koplo Maiga akaenda kwenye gari lake na kuondoka.
Chriss akaingia ndani ya benki na kufunga mlango,akaanza kuangaza macho ndani ya benki, mbele kuna kaunta yenye nondo za chuma, nyuma ya nondo kuna dirisha la vioo, kushoto kwake kuna mlango, na mlango mwingine uko nyuma ya kaunta, pembeni kuna viti vya sofa ,na meza iliyojaa magazeti mbele ya viti. Janet akamuangalia usoni, "Pole sana kuhusu Kigai",najua bado una mshtuko, ni vizuri ukaenda nyumbani kupumzika", Chriss akamuambia Janet, "Unaweza kunipa funguo za benki, halafu uondoke"? "Hakuna kitu tunaweza kufanya sasa,mpaka Jumatatu",Chriss akamuambia Janet.
"Hutaki kukagua mahesabu"? Janet akamuuliza Chriss."Sio sasa hivi, nitakagua mahesabu Jumatatu", Chriss akasema,Chriss akafungua mlango wa ofisi ya meneja, Ofisi nzuri yenye kapeti chini, viti viwili vya kifahari vinavyoangalia meza, pamoja na kabati zuri nyuma ya kiti."Ingia na ukae kwenye kiti", Chriss akamuambia Janet, "Sigara"?, Chriss akamuuliza Janet, "Hapana, sivuti sigara", Janet akamuambia Chriss na kukaa kwenye kiti."Funguo ziko wapi"? Chriss akauliza, "Ziko kwenye droo ya juu ya kabati" Janet akajibu. Chriss akafungua droo na kuchukua funguo. "Wewe unakaa na funguo gani"?. Chriss akamuuliza Janet."Ninakaa na funguo za mlango wa mbele, pamoja na funguo za kwenye kabati la kuhifadhia fedha", Janet akamjibu Chriss,. Chriss akatabasamu na kusema,"Kwa hiyo siwezi kutoa fedha kwenye kwenye kabati, mpaka nipate ruhusa yako"?. Janet akatingisha kichwa kukubali. "Janet, mimi ndio nimefika leo kutoka Dar es Salaam ,,..sina sehemu ya kukaa, wapi ninaweza kupata nyumba nzuri ya kupanga"? Chriss akamuuliza Janet,... Mmh kwa sasa hivi ni ngumu, lakini pale ninapoishi kuna vyumba self container ni vizuri havina mpangaji.", Janet akamuambia Chriss. Chriss hakutaka kuishi karibu na Janet, lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali mapendekezo ya Janet, "Sawa, nitaenda kuviangalia,"Chriss akamuambia Janet. "Janet, kwa nini haukai na wazazi wako"? Chris akauliza, "Sina, walikufa kwenye ajali ya gari miaka mitano iliyopita", Janet akajibu. "Pole sana Janet", Chriss akamuambia. "Asante", Janet akajibu. Chriss akanyanyuka kwenye kiti na kuanza kuondoka ofisini, akamuambia Janet afunge ofisi mpaka Jumatatu watakapofungua benki, Janet akafunga mlango wa benki na kuondoka.
Chriss akawasha gari na kuelekea nyumbani kwa bwana Kigai, anaeishi kwenye nyumba ya benki, alipofika ,akaanza kuikagua nyumba, Nyumba ya kizamani ya matofali ya kuchoma, bati limechakaa na kuanza kutoa kutu, rangi ya kuta imepauka, Chriss akawaza, ", Kwa hiyo bwana Kigai asipopata nafuu mapema, mimi ndio nitakujaa kuishi kwenye hili pango"?.Chriss akawaza.Chriss akarudi kwenye gari lake, akaondoka na kuelekea Sakina Bar, alipofika, akashuka, akaingia ndani, akaenda kaunta kwenye viti virefu,akakaa na kuagiza bia.."Kwa hiyo bwana Kigai asipopata nafuu, nitakaa hapa kwenye huu mji wa wamasai kwa miezi mingi"!.. Tena inawezekana nikakaa moja kwa moja kama mambo hayatakuwa mazuri kwa bwana Kigai.."Inawezekana nikazeekea hapa benki, pamoja na Janet...tutatoka mvi pamoja na kustaafu hapa Benki.... lakini Janet hata akifikisha miaka hamsini, bado ataonekana mrembo..miaka kumi na tano jela Kisongo sio mingi."Chriss akawaza.
Chriss akaondoka Sakina Bar, akapanda gari lake na kuelekea Sekei.Akasimamisha gari mbele ya geti la nyumba nzuri, akashuka kwenye gari na kugonga geti. Baada ya muda kidogo, geti likafunguliwa na mwanamke mmoja wa makamo, mwenye umbo la namba nane. "Mimi ni Chriss Ruge", Chriss akasema, "Janet nimemkuta"?. " Oooh, karibu bwana Chriss, Janet alinitaarifu utakuja", yule mwanamke akajibu. "Asante", Chriss akajibu na kuingia ndani, Nyumba ina floor tiles kuanzia getini, Juu bati la Msouth, na milango yenye grill nzuri za rangi nyekundu iliyopauka. Chriss akamuangalia kwa makini yule mwanamke aliemkaribisha. Mwanamama mnene wastani, mweupe, mwenye hips nene, kiuono chembamba, matiti makubwa yaliyojaa na kuchongoka, shingo ya michirizi, kichwa chembamba kilichorembwa na pua ndefu na midomo minene, nywele nyingi zilizodondoka mpaka mabegani, " Bila shaka huyu ni mmeru", Chriss akawaza. "Mimi ni mama Hadija, ndio mama mwenye nyumba, ukiamua kuishi hapa, nitafurahi", Yule mwanamke akamuambia Chriss. "Na mimi pia nitafurahi kuishi hapa", Chriss akajibu. " Sijui nitakaa hapa muda gani, inategemea na muda meneja wetu bwana Kigai atapata nafuu, nimesikia yuko kwenye hali mbaya". "Ndio, Janet ameniambia, namuonea huruma mke wake", mama Hadija akajibu.
" "Najua umechoka, njoo nikuonyeshe vyumba, kuna vyumba viwili double vina vyoo ndani, unaweza kuchagua kimoja wapo", mama hadija akasema. Chriss akageuza shingo na kumuangalia mama Hadija usoni, mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio, "Shilingi ngapi kwa mwezi"?. Chriss akauliza. "Laki moja kwa mwezi", mama Hadija akajibu. Chriss akaingia ndani ya chumba kimoja wapo, akaona kuna milango miwili, " Huu ni mlango wa kuelekea chooni"?. Chriss akauliza, na kunyoosha kidole kuelekea mlango mmojawapo, "Hapana, mlango huo hautumiki, unaelekea kwenye chumba changu, huo mwingine ndio unaelekea chooni,"Mama Hadija akajibu. "Nitachukua chumba hiki, kama unakubali", Chriss akajisema. "Hakuna shida", mama Hadija akasema. "Unaweza kuleta vitu vyako sasa." Mama Hadija akamuambia Chriss. "Nina begi moja tu dogo la nguo, vitu vingine nitanunua kesho", Chriss akajibu. "Sawa, naelekea jikoni kupika ," Mama Hadija akamuambia Chriss na kuanza kuondoka kuelekea jikoni, Chriss akamuangalia nyuma jinsi makalio yanavyotingishika, mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio. "Mmh ,huyu mwanamke kweli ameumbika". Chriss akawaza. Chriss akaenda kwenye mlango unaounganisha chumba chake na cha mama Hadija, Akakunja kitasa kutaka kufungua, akakuta umefungwa, akatoka nje ya geti, na kuelekea kwenye gari yake, akawasha gari akaelekea mjini.
Nyumba aliyopanga Janet na Chriss, pia kuna wapangaji wengine wawili wazee wastaafu, bibi Maureen, pamoja na mzee Kijazi. Kesho yake, baada ya Chriss kununua vitu vya ndani na kuhamia rasmi, jioni akakaa na bibi Maureen , Janet, pamoja na mzee Kijazi kwenye maongezi ya kawaida ya wapangaji. Mzee Kijazi akamuambia Chriss, "Unajua bwana, Mama Hadija ni mpambanaji sana, hakuna mwanamke anaejua kupika mtaa huu zaidi yake, Mume wake, baba Hadija alikuwa mfanyakazi wa shirika la bima, mume wake alikuwa muhuni sana, alikuwa na wanawake wengi, kila siku walikuwa wanagombana, walifanikiwa kupata mtoto mmoja, mume wake alipata ajalivya gari akafariki, akimuachia mama Hadija pesa kidogo, hizo pesa ndio amejenga hii nyumba". "Binti wa Mama Hadija, na yeye anaishi hapa",? Chriss akamuuliza Mzee Kijazi, Mzee Kijazi akamjibu Chriss," Ndio, anaishi hapa, yeye pamoja na koplo Maiga ni wachumba, Hadija anafanya kazi Mount Meru Hotel, mara nyingi anaingia zamu ya usiku, ni ngumu sana kuonana nae, anarudi nyumbani saa tisa usiku, akienda kulala muda huo, kuamka ni baada ya saa tano asubuhi", Mzee Kijazi akamuambia Chriss. Baada ya muda Chriss akajisikia uchovu, akawaaga wapangaji wenzake,akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake, akajitupa kitandani, na kuanza kuwaza. "Inaonekana huu mwaka nitaupoteza hivi hivi bila kufanya chochote", Chriss aliwaza, Sasa hivi nina miaka thelathini na nane, nina akiba benki isiyofika hata milioni, nina madeni, nisipofanya kitu sasa hivi, sitaweza tena kufanya kitu chochote milele, najua mimi sio mfanyakazi hodari wa benki, kutokuwa mfanyakazi mzuri wa benki, hakunifanyi nishindwe kufanya kitu kingine.. Lazima nitafute pesa, tena pesa nyingi za kuniwezesha kuishi maisha ya kifahari kufanya biashara kubwa za maana. Hapa Arusha kuna pesa ya maana kweli nitapata"? Chriss aliwaza. Wakati anawaza hayo, mara akasikia sauti ya mama Hadija anaingia chumbani kwake.Akaamka kutoka kitandani, akaenda kwenye mlango unaounganisha chumba chake na na cha mama hadija, akainama na kuchungulia chumbani kwa mama Hadija, kupitia kwenye tundu la kwenye kitasa cha mlango,. .... akaona kitanda kikubbwa tano kwa sita, chupi, sidiria ziko juu ya kitanda, mama Hadija akavua nguo, akachukua taulo na kulizungurusha kwenye mabega, akaelekea bafuni kuoga, Chriss mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, akahema kwa nguvu, akarudi kitandani, "Huu sio muda muafaka", Chriss akaongea mwenyewe taratibu na kupitiwa na usingizi.
Itaendelea..................................
kwa mawasiliano zaidi.
0678 85 47 50.