Baada ya wale jamaa kutia timu nyumbani kwangu,kijihasira kikaanza kuninyemelea,kwakuwa nilishajua lengo lao.
Hivi huyu fundi ni mtu wa aina gani,mtu gani asiyeelewa? Ndiyo,?! Lazima mtu akikataa Chake ujue kakataa kuendelea kubembeleza inakuwa kero itakayosababisha ukahisiwa vingine. niliwaza sana.
Kaka,kamkubwa samahani bwana kwa usumbufu,tumerudi tena.aliongea yule fundi huku akijichekesha chekesha.
Kwani wanataka nini hawa?
Kuna usalama kweli hapa mume wangu? Nikamjibu,
Hakuna shida ngoja tuwasikilize,
Oy, bro eeh unajua nini babu mwanaume ukiamua kunyoosha jambo lako fanya kweli, wee umemwambia mwanetu kuwa una chombo unataka kusukuma,mkakubaliana ile fresh yaani, Sasa tumesikia unarusha yaani ile sitaki nataka,
Mchizi hapa alikuambia anatembea kilomita miatano au vipi,wee ukaona ni karibu,ni vyema ukafu....ukafunguka unataka kilomita ngapi ziongezeke,usikae kinyonge tiririka mwamba.
Aliongea kijana mmoja ambaye, haya majani mabaya yanayokatazwa na serikali,ni kama yanalimwa nyumbani kwake.
Kwa kifupi nilishakasirika,
Sikia wewe fundi,kuzoeana na wewe isiwe sababu ya wewe kuja kila unapojisikia hapa nyumbani kwangu,halafu unaleta watu design tofauti tofauti Mimi siwajui, heshima na Imani ninakupa wewe ndiyo maana huwa unafika kwangu Kila unapohitajika,kwahiyo nakuomba uondoke hapa hakuna biashara Mimi na wewe,
Halafu hivi,mbona hujiheshimu huyooooo mpaka uwanjani kwa watu kwahiyo hi fence kutomalizika ndiyo kigezo Cha nyinyi kujikuta mnaweza kufika muda wowote ule .nilibwata.
Baada ya kuona hapa maelewano hakuna wakaondoka bila kuaga wale wengine huku huyu fundi,akiniomba msamaha ambapo kwa muda huu sikuwa nakamatika,Kila mtu akawa ananiogopa,ikabidi yule fundi naye aondoke maana hali ya hewa ilishakuwa mbaya.
Twende ndani mume wangu,aliongea mke wangu Huku akiwa akinitazama kwa woga,maana tangu anijue sijawahi kuwa wa moto hivyo mbele yake,akawa ananiangalia sana , nikamwita kwa ishara ya kufumba na kufumbua kiganja, taratibu akaja mpaka pale kwenye kiti nilipokaa.
Usiogope mke wangu ni lazima kuweka mipaka,kwa baadhi ya watu ili kulinda heshima na hadhi yetu ,si Kila mtu lazima kuzoeana naye,
Au nimekosea mke wangu,?
Siwezi sema umekosea, au umepatia kwakuwa sijui chanzo Cha ugomvi wenu mume wangu.ni vyema ukanieleza Nini kilitokea.....
Nikamueleza Kila kitu tangu mwanzo mpaka nawapiga mkwara siku hiyo.
Lakini mume wangu,wewe uliwatamanisha sana, kwamba unauza Mali yako wakawa na Imani kuwa muda si mrefu watapata bidhaa,kifupi umewachanganya ndiyo maana wakafika hapa,
Ila kiukweli sijapenda,stahili waliyokuja nayo Mimi nikajua unadaiwa ,maana maisha tunayoishi tunayajua wenyewe.
Alisisitiza.
Mke wanguuuuu,yaani hata Kama nadaiwaaaa,ndiyo nidaiwe na wale wavuta bangi ,
Haaaaaa Dani my husband usiseme hivyo,hapa unajiona una maisha magumu lakini unaweza kushuka zaidi ya hapa ukajikuta wale ndiyo kampani yako.
Ila ni kweli mke wangu, tuachane na hizo stori naona kama unanitisha.niliongeza.
Siyo tuachane na hii stori,kwanza kwanini ulitaka kuiuza hii TV bila kushauriana ma mimi,najua Mimi hapa kwako Sina nachomiliki.mwenzangu ulisoma kwa kiasi fulani Mimi sikusoma.
Uliuza pikipiki bila kunitaarifu au kushauriana na Mimi,nilisikitika moyoni lakini sikuwa na namna ni vitu vyako kwanini nihoji,
Umeuza vitu vidogo vidogo vingi tu,sikuulizi,siyo kwamba siwezi Bali naepusha maneno madogo madogo
Najivunia kuwa na wewe mume wangu,Kila unachokileta ama kukitafuta huwa nafurahi na kukuombea uzidi kupata zaidi huku nikiringa na kutamba kuwa na mume Bora,ulinioa miaka nane nikiwa kwenye uyatima wa kukosa wazazi wote wawili,lakini baada ya kuolewa na wewe nikajikuta, nimepata mfariji,mlezi,baba wa watoto wangu na la mwisho nimepata mume mwema,
Leo hii,unauza vitu vidogo sana bila kuniambia,unadhani utaniambia kwenye mambo makubwa!
Una Mashamba lakini una hii nyumba
Na siku zote najivunia kuwa na wewe ni mpambanaji,naamini Sina Cha kukulipa zaidi ya kukuzalia watoto.
Najua kuwa hata hiki kiumbe kingine kilichoko tumboni mume wangu hujapenda lakini nikwambie tu kuwa najua ni wajibu wangu,kukuzawadia watoto ili ukuze jina lako mume wangu.
Mmmmmmmh mume wangu ipo siku utauza hii nyumba,Tena baada ya kuwa ushaanza udalali baada yakuwa huna kazi,na sifa za madalali nazijua wakikosa vya kuuza, huuza hata vitu vyao,
Hamna mke wangu, kamwe siwezi kuuza nyumba,.niliropoka,
Na nikiuza,au ukisikia tu tetesi za kuuza nipeleke mahakamani.
Nani akupeleke mahakamani,Daniel Mimi Sina huo muda,wa kugombania Mali sizizo kuwa zangu,we ukiuza utakuwa umeuza Mali zako.aliongea huku akilengwa na machozi,nilimuhurumia nikamkumbatia,muda huo hata sikuwa na Cha kumwambia zaidi ya kuona aibu tu,tulikumbatiana kitambo mpaka tuliposhituliwa na sauti ya dada wa kazi,
Akiita DADAA,!!!!!!.....
Itaendelea.........
Usichoke huu ni utangulizi tu mambo mazuri yanakuja.