Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ArostooooSEHEMU INAYOFUATA.....
Aaaamh samahani dada vipi Kuna tatizo? aliuliza dada wa kazi,
Hakuna,alijibu mke wangu Huku akiinuka pale ili waende usawa wa jikoni akamsikilize zaidi.
Nilitulia pale sebuleni huku nikicheka peke yangu,,
Leo hii ni Kali sana aiseeh yaani mke wangu kaniita jina kabisa,ndiyo naitwa Daniel,lakini yeye hajazoea kuniita hivyo Leo kakasirika tena sana,ila afadhali katema nyongo maana inawezekana alikuwa nayo haya muda mrefu .
Ila ni kweli maana Kila alichoongea si kibaya,halafu..,
Kumbe kajua kuwa kubeba kwake ujauzito sikufurahi,,ni kweli lazima hili nitalikataa katakata.
Ni kweli nilifikiria hivyo lakini hapaswi kujua kama sijapenda.
Usiku wa siku hiyo,hakukuwa na stori kama tulivyozoea,ila ile saa kumi na moja alfajiri nikiwa Sina usingizi niligundua hata mke wangu naye Hana usingizi,
Nikavunja ukimya.
Mke wangu,akaitika
Hivi unanipenda?
Hivi mume wanguuu,samahani lakini tuna Kuna vitu vingi vya kuviongelea usianze na habari sijui nakupenda sijui nini,hizi habari ziache kwenye matamthilia huko .alijibu
Nikaona ohooo naianza siku vibaya hii,Bora hata ningepiga kimya,
Wewe ni mume wangu na Mimi ni mkeo hatuna haja ya kukumbushana vitu vilivyokaa kitoto kama hivyo,Mimi na wewe hatuko kwenye mahusiano.
Bali tuko kwenye NDOA ,tunaitumikia ndoa tuliyokula kiapo kanisani Mimi na wewe kwamba tutavumiliana kwenye shida na raha,Kuna vilima na mabonde,kama zilivyo nyakati za mvua na jua.
Nikaona nisharikoroga hapa,nikamjibu
Siyo hivyo mke wangu Mimi nakupenda ila Kuna jambo umenisingizia Jana,limeniumiza sana,
Jambo lipi Hilo? alidakia
Ni kuhusu ujauzito wako, unadai eti sijapenda jambo ambalo si kweli,mke wangu kwani uwaze tofauti,?
Alicheka kidogo Kisha akaendelea,
Sikia mume wangu,Mimi najua unanipenda sana,na kitendo Cha Mimi kushika ujauzito,si kwamba hujafurahia,ila ulishituka kwasababu ya nyakati unazopitia,
Laiti ungekuwa na kazi yako halafu nikahisi hivi pengine ingeniwia vigumu kutambua,lakini wewe umetishwa na vile ambavyo huna kazi ya uhakika,lakini nikwambie tu mi nakuombea Kila kitu kitakaa sawa kwa upande wako tena tutaishi kwa furaha kama mwanzo, na safari hii huyu mtoto atakuwa wa kidume,
We umejuaje, niliuliza
Hakukuwa na majibu zaidi ya vicheko kwa Kila mmoja.
Tuliamka huku maandalizi ya kwenda kanisani yakiwa yamepamba moto,
Mume wangu vipi,naona upo nyuma nyuma kulikoni,
Huendi kanisani,tena ujue huu ndiyo muda wa wewe kuwa karibu na kanisa,kule Kuna maombi mbalimbali unaweza kuungana na wengi wenye matatizo Tena Leo Kuna maombi
Maalumu kwa wenye uhitaji na wewe kwangu naona ni WA muhimu mno.
Nilicheka sana,
Hivi nahitaji kuwa karibu na kanisa au kuwa karibu na MUNGU.niliuliza
Ohooo ushaanza,si tunatangulia huwa siyawezi maswali yako.wakaondoka wakiniacha mwenyewe,akili ikiwaza ifike siku ya kesho jumatatu nikaitike wito wa barua yangu.
Nani aende kanisani, Mimi hahahaaa ngoja kwanza,Mimi nimebatizwa utotoni baba yangu alikuwa Katekista kabla hajaacha kutokana na uzee akaona apumzike,Mimi ni mbatizwa wa tangu utotoni,nikapata kitubio na kipaimara nikiwa shule ya msingi,
Kutokana na mzee kuwa maarufu nikawa kiongozi tangu nikiwa primary sekondari mpaka chuo nilikuwa na rundo la uongozi.
Nimezunguka mikoa mingapi Mimi kwenye matamasha,makongamano na semina mbalimbali huku safari nyingi zikijaa kujitolea zaidi ya hela za mfukoni ndiyo zaidi.
Mbaya zaidi ikaja kuibwa hela ya harambee na nikawa mtuhumiwa Mimi wakati siyo muhasibu Wala mweka hazina,
Walinionea sana halafu,licha ya kubadilisha kanisa japo ni like lile catholic bado Nako nilikula za uso nikituhumiwa na jamaa mmoja kuwa natembea na mke wake jambo ambalo si kweli
Mpaka alipogundua yeye mwenyewe kuwa si Mimi wakati mambo yashaharibika, anyway mke wangu ana haki ya kuniambia hivyo yuko sahihi kabisa.
Lingine ni michango,michango,michango naamini nikienda huko itakuwa kero tu maana hata jumuiya waliyoipa jina linalofanana na Mimi nimeitelekeza kulingana na kuwa bize na mambo yangu zaidi.
Ah wewe nitasimangwa huko tukashikana mashati bure maana vichwa vyenyewe vimepata moto halafu mtu akakuulize maswali huko si mnaweza kugombania bure?
Acha niweke mambo yangu vizuri huko nitaenda tu,
Mwenyezi MUNGU nisamehe mja wako nakiri Mimi ni mwenye dhambi.
Nikainuka baada ya kujikumbusha mengi yahusuyo kanisani ,yalitosha kabisa kuona Mimi sipaswi kwenda kanisani kana kwamba kanisa ni night club Tena V.I.P.
Itoshe kusema kwa siku hiyo,shetani alishinda,Tena tatu bila.
Nikaingia ndani nizisabahi suti zangu huku nikiwa makini kwamba lazima nitafute nguo itakayonipendeza lakini itabidi nisipendeze zaidi kuliko wao mabosi japo sijui watavaaje,lakini Nina uzoefu mkubwa kwenye hizi mambo unaweza kukosa kazi kwenye jambo dogo,halafu usijue Nini kilisababisha mpaka unaingia kaburini.
Kumbe labda ulikuwa more than smarter,ni hatari sana.
Nikaona pia ni muda wa kwenda saloon nikapunguze hizi ndevu ,khaaaa wewe nakua kama mwigizaji ambaye anataka uhalisia kwenye movie zake,nilizugazuga pale home nikiwa karibu na PC yangu ili kujikumbusha Documents fulani
Maana sipaswi kuwa mzembe ,wakati najiandaa kutoka nielekee saloon,ilisikika hodi .ni sauti ya mke wangu,najua akiwa na wageni huwa anabisha hodi akiwa mbali ili kama mtu upo vibaya,...
...hili linaeleweka kwa Kila mtu.
Nikawakaribisha ndani, mke wangu,dada wa Kazi na mgeni wa kike ambaye sura haikuwa ngeni,kama naliwahi kumwona sehemu,vijana wanaita pisi Kali yes, ni pisi yaani unaweza kuapa nakuweka nadhiri kwamba kwa Sasa sitaki ukaribu na wanawake na kuwa bize na mambo yangu,nakwambia usije kuapa hivyo utakufuru
Ukaja pata LAANA bure.
Kuna watu wameumbika jamani yaani,namlaumu mke wangu unamletaje mtu kama yule ndani kwako hata Kama ni kwa maongezi ya dakika tatu?
Itaendelea..........
mambo ya ngoswe hayaSEHEMU INAYOFUATA.......
Tarehe 17 mwezi wa kumi mwaka 2011 Mimi,boss na mke wa boss tulikaa kwenye hoteli fulani huku tukipata Chakula Cha pamoja ikiwa ni kuonesha upendo tu kwangu lakini kuagana tayari Mimi kwenda mkoani ,
Tulimaliza nikapewa pesa nyingi tu za kuacha nyumbani, dharula yaani nilikuwa full,hata ingekuwa kusafiri kwa flight nauli ingetosha ya kwenda na kurudi lakini nilichagua usafiri wa bus,huku nikipata taarifa kuwa yule fundi yeye kaenda Leo,
Nikajua yote hayo hataki kuongozana na mimi,
Nilikuja ubungo,nikakata ticket, Kisha nikampigia simu mke wangu,nimpe maelekezo kuwa sitarudi naunganisha tu maana nikisema nirudi, nyumbani ni mbali yaani pembeni kabisa ya mji kwahiyo nikachukua chumba lodge nikalala.
Kutokana na hizi kampuni za mabasi kuwa na ushindani mkubwa kwenye mwendo saa kumi na nusu tayari nilikuwa mkoani,nikapokelewa vizuri nikajitambulisha kwa watu wa ile yard wakaniambia taarifa zangu wanazo,lakini wakaomba vitambulisho wajiridhishe,nikafanya hivyo huku nikiwaambia kuwa Mimi ni mwenyeji wa mkoa ule na pale ndiyo maeneo ya nyumbani kwahiyo wasinione mgeni,
Mmoja akadakia kwa kusema siyo kweli mbona naonekana haiba yangu haifanani na watu wa mkoa ule,
Huyo ni muongo bwana,aseme ukweli mbona Mimi kabila langu ni ******** akataja kabila lake,maneno haya anayasema yule fundi aliyenitangulia jana.
Nikaona ni kawaida kwa mtu ambaye hakupendi ,atakukosoa na kukupinga kwa Kila jambo ili uonekane we hufai,lakini huyu ni mshamba nadhani pia umri wake ni tatizo ni kijana bado lakini pia hajafanya kazi sehemu nyingi ,pili hata hilo kabila alilolitaja kama si lake,maana ana mchanganyiko wa uarabu huyu si msomali huyu,any way pengine ni kabila lake,
Ikabidi baadhi waniongeleshe lugha ya pale ,hatimaye wakajiridhisha,nikawaambia hata hivyo Mimi ndiyo mwenyeji wenu maana wengi wenu siyo wa hapa tukataniana tukacheka,
Yule fundi kusikia vile akawa Hana la kufanya akawa Sasa yupo karibu na Mimi ananiongelesha na vijistori vya hapa na pale huku akiwa anainanga ile kampuni,
Yaani bro hili Chaka uliloingia siyo kabisa,hii siyo kampuni kaka,hebu fikiria we spea inawezekanaje ikosekane mjini ifatwe huku mkoani, ndiyo ujue jinsi yule boss alivyombahili yaani yule dawa yake ni moja,kumpiga tu (kumuibia)
Nikacheka kwakuwa nilishapewa taarifa kuwa yule HR na huyu fundi ni watu wa kuwaangalia sana,hata hivyo boss huwa hawafukuzi kazi sijui kwanini,
Nikamjibu,kwani wewe na mafundi wenzio si mmezunguka jiji Zima kutafuta spare mkadai hamjaiona,
Hamna bro,spea zipo ila bosi wako mkuda kinoma, aliona eti zinauzwa bei ya juu mno.
Nikamuona ni mpuuzi tu,nikamuaga kuwa Mimi nitalala nyumbani kwa wazazi wangu ili kesho nije tuendelee na kazi,Cha ajabu tulitumia karibu wiki nzima Kila akija anagusa gusa tu kwa madai ni ngumu kufunguka lakini pia ni inatakiwa itolewe kiutaalamu tusije haribu nikaona mbona Kama ananifanyia mchezo,
Hatimaye boss wa kike akaanza kupiga simu maana mume wake alishasafiri,alikuwa akilaumu mbona siku zinazidi kwenda na kazi zinakwama Mimi nikawa Kila lawama naielekeza kwa fundi Hadi alipotishiwa kuwa ataletewa fundi mwingine ,ndipo akaitoa.
Huku kwa ndugu zangu tuliongea mengi huku nikipewa baraka na kufanyiwa mambo ya kimila,japo si muumini sana wa mambo yale lakini lazima uheshimu taratibu ambazo unaelekezwa na wazazi
Unajua mwanangu Daniel una dharau sana wewe ndiyo maana mitihani haiishi kwako, Dunia hadaa ulimwengu shujaa mwanangu,alisema mama huku nikimpata kwa umakini mkubwa sana.
Kwakuwa pesa nilikuwa nayo nikawaachia kiasi fulani,huku nikipanga safari hii naenda kulala na ESTA mwanamke ambaye ningemuoa pengine na licha ya kuwa ni kama kachuja lakini bado ni mzuri sana tu,kwakuwa namba zake ninazo baada ya kuziiba kwenye simu ya wife ngoja nimpigie kabisa ili nikifika tu mjini nijue pa kuonana naye.
Nikampigia ,nikampiga sound nyingi sana japo kulikuwa na ugumu kutokana na misimamo ya kilokole lakini hakuwa ESTA wa zamani,ESTA huyu alikuwa na njaa,Tena alipigika hivyo asingechomoka kwa kile nilichomuahidi,
Kwakuwa bosi alisema yule fundi kazi yake ni kufungua tu,kuhusu kuisafirisha lilikuwa ni jukumu langu kwakuwa wale mafundi hawakuwa waaminifu,
Nikaipakia kwenye gari,nikihakikisha ipo salama kwenye ile buti,nikaagana na baadhi ya ndugu zangu huku wakiniombea Kila la kheri,huku njiani simu za ESTA zikawa nyingi kuliko za mtu yoyote yule,nikaona kumbe je,
Pesa ni sabuni ya roho vingi tunashindwa kuvipata shida ni umasikini.
Hatimaye tukawa Ubungo stand kuu,
Hapa Kuna kitu vitu wale wabeba mizigo kwenye toroli walinichanganya wakati mizigo inashushwa toka kwenye buti Mimi Niko bize na simu, ESTA kanichanganya.
Mzigo ukapakiliwa kwenye kitoroli Cha mtu mwingine,Mimi nikaomba mzigo wangu uwekwe stoo ili baadaye nitapiga simu ili gari ndogo ije kufuata yule dogo mbeba mizigo akaniambia si huu ndiyo unaenda stoo nikamjibu ndiyo,yaani chuma hiki nakiona kabisa,lakini alijichanganya akapewa mtu mwingine bila Mimi kujua.
Nilikuwa naweza kuufikisha mzigo vizuri tu,lakini tamaa za ngono ziliniambia nenda huku kwanza Kisha mzigo utapeleka tu,
Weeeeeee ningejua.....
Itaendelea.......
Weee kumbee basi usipotee sana jackHii ni simulizi ya kweli ya maisha yangu,ila majina yanayotumika humu ni ya kufikirika,ndiyo maana sitaji hata location mbali mbalimbali ili watu wasiunganishe matukio
Simulizi haiko kwaajili ya mtu kujitambulisha Bali ni kufundisha,kuelimisha na kuburudisha
Mambo mazuri yanakuja Kila siku usikose kufuatilia
[emoji1787][emoji1787]kaona tumesifia kapotea mazima