SEHEMU INAYOFUATA.....
Aaaamh samahani dada vipi Kuna tatizo? aliuliza dada wa kazi,
Hakuna,alijibu mke wangu Huku akiinuka pale ili waende usawa wa jikoni akamsikilize zaidi.
Nilitulia pale sebuleni huku nikicheka peke yangu,,
Leo hii ni Kali sana aiseeh yaani mke wangu kaniita jina kabisa,ndiyo naitwa Daniel,lakini yeye hajazoea kuniita hivyo Leo kakasirika tena sana,ila afadhali katema nyongo maana inawezekana alikuwa nayo haya muda mrefu .
Ila ni kweli maana Kila alichoongea si kibaya,halafu..,
Kumbe kajua kuwa kubeba kwake ujauzito sikufurahi,,ni kweli lazima hili nitalikataa katakata.
Ni kweli nilifikiria hivyo lakini hapaswi kujua kama sijapenda.
Usiku wa siku hiyo,hakukuwa na stori kama tulivyozoea,ila ile saa kumi na moja alfajiri nikiwa Sina usingizi niligundua hata mke wangu naye Hana usingizi,
Nikavunja ukimya.
Mke wangu,akaitika
Hivi unanipenda?
Hivi mume wanguuu,samahani lakini tuna Kuna vitu vingi vya kuviongelea usianze na habari sijui nakupenda sijui nini,hizi habari ziache kwenye matamthilia huko .alijibu
Nikaona ohooo naianza siku vibaya hii,Bora hata ningepiga kimya,
Wewe ni mume wangu na Mimi ni mkeo hatuna haja ya kukumbushana vitu vilivyokaa kitoto kama hivyo,Mimi na wewe hatuko kwenye mahusiano.
Bali tuko kwenye NDOA ,tunaitumikia ndoa tuliyokula kiapo kanisani Mimi na wewe kwamba tutavumiliana kwenye shida na raha,Kuna vilima na mabonde,kama zilivyo nyakati za mvua na jua.
Nikaona nisharikoroga hapa,nikamjibu
Siyo hivyo mke wangu Mimi nakupenda ila Kuna jambo umenisingizia Jana,limeniumiza sana,
Jambo lipi Hilo? alidakia
Ni kuhusu ujauzito wako, unadai eti sijapenda jambo ambalo si kweli,mke wangu kwani uwaze tofauti,?
Alicheka kidogo Kisha akaendelea,
Sikia mume wangu,Mimi najua unanipenda sana,na kitendo Cha Mimi kushika ujauzito,si kwamba hujafurahia,ila ulishituka kwasababu ya nyakati unazopitia,
Laiti ungekuwa na kazi yako halafu nikahisi hivi pengine ingeniwia vigumu kutambua,lakini wewe umetishwa na vile ambavyo huna kazi ya uhakika,lakini nikwambie tu mi nakuombea Kila kitu kitakaa sawa kwa upande wako tena tutaishi kwa furaha kama mwanzo, na safari hii huyu mtoto atakuwa wa kidume,
We umejuaje, niliuliza
Hakukuwa na majibu zaidi ya vicheko kwa Kila mmoja.
Tuliamka huku maandalizi ya kwenda kanisani yakiwa yamepamba moto,
Mume wangu vipi,naona upo nyuma nyuma kulikoni,
Huendi kanisani,tena ujue huu ndiyo muda wa wewe kuwa karibu na kanisa,kule Kuna maombi mbalimbali unaweza kuungana na wengi wenye matatizo Tena Leo Kuna maombi
Maalumu kwa wenye uhitaji na wewe kwangu naona ni WA muhimu mno.
Nilicheka sana,
Hivi nahitaji kuwa karibu na kanisa au kuwa karibu na MUNGU.niliuliza
Ohooo ushaanza,si tunatangulia huwa siyawezi maswali yako.wakaondoka wakiniacha mwenyewe,akili ikiwaza ifike siku ya kesho jumatatu nikaitike wito wa barua yangu.
Nani aende kanisani, Mimi hahahaaa ngoja kwanza,Mimi nimebatizwa utotoni baba yangu alikuwa Katekista kabla hajaacha kutokana na uzee akaona apumzike,Mimi ni mbatizwa wa tangu utotoni,nikapata kitubio na kipaimara nikiwa shule ya msingi,
Kutokana na mzee kuwa maarufu nikawa kiongozi tangu nikiwa primary sekondari mpaka chuo nilikuwa na rundo la uongozi.
Nimezunguka mikoa mingapi Mimi kwenye matamasha,makongamano na semina mbalimbali huku safari nyingi zikijaa kujitolea zaidi ya hela za mfukoni ndiyo zaidi.
Mbaya zaidi ikaja kuibwa hela ya harambee na nikawa mtuhumiwa Mimi wakati siyo muhasibu Wala mweka hazina,
Walinionea sana halafu,licha ya kubadilisha kanisa japo ni like lile catholic bado Nako nilikula za uso nikituhumiwa na jamaa mmoja kuwa natembea na mke wake jambo ambalo si kweli
Mpaka alipogundua yeye mwenyewe kuwa si Mimi wakati mambo yashaharibika, anyway mke wangu ana haki ya kuniambia hivyo yuko sahihi kabisa.
Lingine ni michango,michango,michango naamini nikienda huko itakuwa kero tu maana hata jumuiya waliyoipa jina linalofanana na Mimi nimeitelekeza kulingana na kuwa bize na mambo yangu zaidi.
Ah wewe nitasimangwa huko tukashikana mashati bure maana vichwa vyenyewe vimepata moto halafu mtu akakuulize maswali huko si mnaweza kugombania bure?
Acha niweke mambo yangu vizuri huko nitaenda tu,
Mwenyezi MUNGU nisamehe mja wako nakiri Mimi ni mwenye dhambi.
Nikainuka baada ya kujikumbusha mengi yahusuyo kanisani ,yalitosha kabisa kuona Mimi sipaswi kwenda kanisani kana kwamba kanisa ni night club Tena V.I.P.
Itoshe kusema kwa siku hiyo,shetani alishinda,Tena tatu bila.
Nikaingia ndani nizisabahi suti zangu huku nikiwa makini kwamba lazima nitafute nguo itakayonipendeza lakini itabidi nisipendeze zaidi kuliko wao mabosi japo sijui watavaaje,lakini Nina uzoefu mkubwa kwenye hizi mambo unaweza kukosa kazi kwenye jambo dogo,halafu usijue Nini kilisababisha mpaka unaingia kaburini.
Kumbe labda ulikuwa more than smarter,ni hatari sana.
Nikaona pia ni muda wa kwenda saloon nikapunguze hizi ndevu ,khaaaa wewe nakua kama mwigizaji ambaye anataka uhalisia kwenye movie zake,nilizugazuga pale home nikiwa karibu na PC yangu ili kujikumbusha Documents fulani
Maana sipaswi kuwa mzembe ,wakati najiandaa kutoka nielekee saloon,ilisikika hodi .ni sauti ya mke wangu,najua akiwa na wageni huwa anabisha hodi akiwa mbali ili kama mtu upo vibaya,...
...hili linaeleweka kwa Kila mtu.
Nikawakaribisha ndani, mke wangu,dada wa Kazi na mgeni wa kike ambaye sura haikuwa ngeni,kama naliwahi kumwona sehemu,vijana wanaita pisi Kali yes, ni pisi yaani unaweza kuapa nakuweka nadhiri kwamba kwa Sasa sitaki ukaribu na wanawake na kuwa bize na mambo yangu,nakwambia usije kuapa hivyo utakufuru
Ukaja pata LAANA bure.
Kuna watu wameumbika jamani yaani,namlaumu mke wangu unamletaje mtu kama yule ndani kwako hata Kama ni kwa maongezi ya dakika tatu?
Itaendelea..........