Simulizi: Mpaka Kieleweke

Simulizi: Mpaka Kieleweke

SEHEMU YA 10

“aisee hawezi kuthubutu kumchukua mke wanguuuuu! Sitokubaliiiii” nilisema kwa uchungu lakini Mnaro aliniangalia kisha atabasamu na kusema “akiamua huna jinsi ya kuzuia hilo, kama kungekuwa na njia basi mimi ningekuwa wa kwanza kumzuia asinipokonye Sauda wangu”...









pamoja na kuumizwa sana na kauli ile nilijitahidi kuvumilia kwakuwa nilikuwa najua fika hali ya kutokuwa mvumilivu ingenirudisha nyuma kama ambavyo imetokea mara kadhaa ninapokuwa na bwana Mnaro, safari hii nikafanikiwa na kushusha kabisa hasira nilizokuwanazo na kuonesha utulivu ambao najua hata Mnaro mwenyewe hakuutegemea. “tunafanyaje sasa? Nadhani muda wa kwenda Muifufu umefikia, hatupaswi kumuacha huyo Magugi aendelee kufanya atakacho, ni bora kumuwahi mapema kwamaana kadri muda uendavyo na yeye anajipanga” nilianzisha upya maongezi ili kumshawishi bwana yule nikijaribu kuonesha utulivu wa hali ya juu ili nisionekane mwenye kukurupuka.



“ni muda muafaka wa kwenda Muifufu sikatai, ila jambo la msingi zaidi ni wewe kujifunza mbinu ambazo zitakuwezesha kuwa salama ndani ya Muifufu, kama ambavyo nilikueleza awali itakubidi kuwa mchawi, na sasa niko tayari kuanza kukufundisha mbinu hizo” aliweka kituo akanitizama nami nikauliza kwa shauku “ni lini tutaanza sasa mafunzo hayo” naye akanijibu “muda wowote ukiwa tayari, hata leo kama ukitaka” nikajikuta nimeingiwa na faraja moyoni mwangu na matumaini ya kumpata mke wangu yakanijia tena kwa kasi kubwa “mafunzo haya yatatuchukua muda gani mpaka kuyamaliza?” niliuliza tena ili kujua ni muda kiasi gani ulikuwa umesalia mpaka safari ya Muifufu. “hiyo inategemea kasi yako ya kuelewa, siku tatu zinaweza kutosha kama una kasi nzuri, lakini kama huna kasi ya kutosha inaweza kutuchukua miaka” kitu pekee ambacho nilikua nikikitaka kwa wakati ule ni kwenda mahali alipo mke wangu kwa gharama yoyote kuingia kwenye mafunzo ya uchawi sikuona kama ni tatizo na nikaamini haitonichukua muda kufuzu mafunzo hayo kwa maana siku zote penye nia pana njia “naomba tuanze leo hayo mafunzo” niliomba na Mnaro akakubali na kunitaka nijiandae kwa jambo hilo usiku wa siku hiyo kisha akaondoka.



Niliendelea kujipumzisha pale kitandani baada ya kuangalia muda na kuona ni saa moja tu toka tuingie kupumzika na kuona haukuwa wakati muafaka wa kuongea na baba yangu juu ya jambo lile baadala yake nilipaswa kumuacha apumzike huku na mimi nikijipatia nafasi ya kupumzika zaidi nikiamini kazi ya usiku wa siku hiyo itakuwa sio ya kitoto, na kweli usingizi ulinichukua kama ambavyo nilitaka.





Nilifumbua macho kutoka kwenye ndoto ambayo nilikuwa nikiota kuwa Mnaro ananiita na kweli nikamkuta akiwa amesimama kando ya kitanda changu pale chumbani.. “amka haraka tuwahi kabla hakujapambazuka, na leo itakuwa mara ya mwisho kukufuata itabidi uwe unakuja mwenyewe mafunzoni” alisema Mnaro ambaye alikuwa amevalia kivazi mfano wa nguo ya ndani ila kilikuwa kimetengenezwa kwa ngozi, alikuwa ni karibu tu na mtu aliye uchi. Nikawa naomba kimoyomoyo mafunzo hayo yasiwe ya uchawi ule wa kutembea uchi ambao huwa nausikia.



Alinipa kitu kama kijiti kidogo mithili ya njiti ya kibiriti akanitaka nikishike kwa kukibana katika kidole changu cha mwisho cha mkono wa kushoto na kisha kuniambia “ukiwa umekibana kijiti hicho namna hiyo unaweza kupenya kupita hapa ukutani na kutokea nnje, unatakiwa tu kuhakikisha mlango umefungwa kwa maana ukiwa wazi hauwezi kupenya, jambo lingine ni imani, unatakiwa kuamnini unachokifaya vinginevyo uchawi huwa unashindwa kukusaidia” niligeuka na kuangalia mlango wa chumba changu na kuona ukiwa umefungwa, ikabaki tukio la kupenya kupitia ukutani kutoka nnje ya nyumba! “Basi wacha nimuage baba maana anweza kuamka akanikosa kisha akapatwa na wasiwasi” nilitoa ombi nikianza kuongoza kuuelekea mlango wa chumba changu “hapana, haina haja. Lengo la uondokaji wa aina hii ni kumfanya mtu anayebakia kutojua kama haupo, ataendelea kukuona ukiwa umelala palepale mpaka utakaporudi” alielezea Mnaro maelezo ambayo yalinishangaza sana “vipi kama ataamua kuniamsha sasa? Si nitashindwa kuamka na kumtia wasiwasi uleule?” niliuliza swali lingine ambalo nalo alilijibu “unatakiwa kunuia ambavyo unataka mambo yatokee ukiwa haupo, kwa mfano unaweza kunuia kuwa iwapo mtu ataingia chumbani asikuamshe naye atakuwa mzito kufanya uamuzi wa kukuamsha na kuamua kukuacha ulale” niliyaelewa vizuri maelezo yake lakini nilishangaa kwanini anakwepa sana wazo la kumuaga baba hali ya kuwa hili sio jambo la siri kwake kwamaana anaijua mipango inayoendelea “kwani kuna ubaya wowote kama nikimuaga?” niliamua kuuliza baada ya kushindwa kujipatia mwenyewe najibu ya maswali yangu.. “wachawi huwa hawaagi wanapotoka kwaajili ya kwenda kwenye shughuli za kichawi, mafanikio huwa sio makubwa kwenye safari kama mchawi ataaga” nilimuelewa na kuamua kufanya kama ambavyo likuwa akiniagiza. “kibane vizuri hicho kijiti kisha upite hapo utokee nnje” alinielezea Mnaro akinioneshea kwenye ukuta wa chumba kile, nami nikatembea polepole kuelekea kwenye ukuta ule nikiuvaa polepole kuona kama utaniruhusu kupita baadala yake nilijikuta nikijigonga ukutani, sikufanikiwa kupenya.
 
SEHEMU YA 11

Nikageuka na kutizama Mnaro ambaye alikuwa akitikisa kichwa kusikitika “nimekwambia mambo mawila ambayo ni lazima yatimie ili uweze kupenya, kwanza mlango uwe umefungwa na pili uamini ambacho unakifanya, lakini wewe umeusogelea ukuta huo kwa wasiwasi mkubwa na nilijua tu kama hautofanikiwa” aliongea Mnaro na kisha akaendelea “haya bwana mimi nakuacha, kama kweli unataka kwenda kwenye mafunzo leo utaniwahi, ukinikosa hapo nnje ujue nimeshaondoka tayari” baada ya kusema hayo alitembea kwa mwendo wa kawaida akauvaa ukuta ambao ulimpokea na akapotea pale chumbani, nikapatwa na hofu ya kuchwa pale na kushindwa kupiga hatua kuelekea kumkomboa mke wangu kwa mara nyingine, nikajikuta nimepatwa na ujasiri wa ajabu kisha nikakibana vizuri kijiti kile katika kidole kile cha mwisho kisha nikauvaa ukuta ule kwa mwendo wa kasi sana, nilijikuta nimepita kupitia ukuta ule kama vile ulikuwa ni pazia na nikajikuta nnje ya nyumba ile, Mnaro alikuwaa amesimama mbele yangu akiwa amepanda juu ya paka mkubwa sana na pembeni yake alikuwepo paka mwingine mweusi sana na mkubwa kama yule wake, paka wale walikuwa na macho mekundu sanaaa na walikuwa waanatisha kwa kweli ila nilijikaza sana nikatembea kuelekea pale alipo Mnaro “usafiri wako huo hapo


” alisema Mnaro akinionesha paka yule ambaye sikuwa nikitamani hata kumuangalia, lakini nikajikaza na kusogea mpaka karibu ya paka yule nikabaki nimesimama bila kusema lolote kwa maana hata sikujua pakuanzia nikawa nikingojea muongozo wa Mnaro. “ unangoja nini? Panda twende” Mnaro aliongea nami nikabaki nikiwa na bumbuwazi kwa maana paka yule alikuwa ni mkubwa sana na sikuona namna gani naweza kupanda mpaka juu ya paka yule! “mvute shingo yake chini atashuka na utaweza kupanda” Alielekeza Mnaro baada ya kuona nimebaki nikiwa nashangaa bila kujua cha kufanya, nami nikanyoosho mkono wangu juu na kuanza kuvuta shingo ya paka yule nikiwa nimefumba macho kwa uoga. Haikuwa kazi rahisi kama ambavyo nilidhani, paka yule alikuwa kama ambaye anapingana na nguvu ya mimi kumvuta chini na alionekana kuwa na nguvu kwelikweli nami nikajitahidi kuongeza nguvu zaidi lakini sikufanikiwa baadala yake nikamkasirisha, akatoa mlio mkali kama ambao hutokea paka wakipigana lakini huu ulikuwa mlio mkubwa zaidi, nadhani ni kutokana na paka mwenyewe kuwa mkubwa sana tofauti na paka ambao nimezoea kuwaona na kusikia wakilia. Nilishtushwa na mlio ule na kumuachia paka yule haraka sana na kuruka nikasimama mbali kidogo na paka yule macho yang yakiwa kwa Mnaro kama ishara ya kutaka msaada wake

“wewe na mgumu sana kuelewa ndugu yangu, nimekwambia bila kuamini ambacho unafanya huwezi kufanikiwa” aalisema Mnaro akianza kuonesha kuchoshwa na ugumu wangu wa kuelewa, ingawa sio kweli kwamba mimi nilikuwa mgumu wa kuelewa ila nilikuwa najifunza jambo la kutisha na halikuwa jambo ambalo nilikuwa na uzoefu nalo. Sikusubiri Mnaro aongee neno lingine lolote nikakaza moyo na kumsogelea tena paka yule, safari hii kwa ujasiri wa hali ya juu, nikamshika shingo na kumvuta chini, tofauti na mwanzo mara hii paka yule alionekana mtii, akachuchumaa chini taratibu mpaka kufikia kimo ambacho kilinitosha kumpanda nikampanda naye akaanza kurudi juu, nilijikuta nikiyumba na kutaka kuanguka nikakosa pakushika na kushika manyoya ya paka yule lakini yaling'oka baadhi ya paka yule akatoa kelele ya maumivu na kuanza kukimbia ovyo ovyo, hali ilikuwa ya kutisha sana nikijitahidi kuhakikisha kuwa sianguki kwa kung'ang'ania vyema manyoya ambayo nilikuwa nimeyashika huku mengine yakiendelea kung'oka na paka yule kuzidi kuwa kuchaa “MSHIKE KWENYE MASIKIOOOOO”

Mnaro alikuwa akipiga kelele huku akija kwa kasi kufuata uelekeo ambao paka yule alikuwa akielekea, nilijitahidi nikaachia manyoya ya paka yule upande wa mkono wangu wa kushoto na kushika sikio la kushoto la paka yule kisha nikaachia na manyoya ambayo nimeyashika kwa mkono wa kulia na na kushika sikio la kulia la paka yule. Paka yule akapunguza mwendo taratibu kisha akasimama kabisa. Mnaro alikuja mpaka paka yule alipo akanitizama akitabasamu.. “masikio yake ndio mjuongozo wako, ukitaka aende mbele unayavuta mbele, ukitaka asimame unayavuta nyuma, ukitaka aruke unayavuta juu na kuelekea kushoto ama kulia ni hivyohivyo, unaelekeza masiko ya paka huyu kuelekea uelekeo wowote ambao unataka aende” alimaliza kusema kisha akanivuka na kuendelea kwenda mbele, nami nikavuta masikio ya paka yule kuelekea huko ambako alikuwa akielekea yeye. Tukaenda tukikimbia juu ya wanyama wale tukipita mitaa mbalimbali mpaka nikajikuta nikimzoea mnyama yule na kuona kama naendesha tu pikipiki yangu ambayo nimeizoea sana! Nikajikuta nikifurahia kumuendesha myama yule mwendo wake ulikuwa wa kuruka ruka hivyo kwenda mwendo mrefu ndani ya muda mfupi Mno!
 
SEHEMU YA 12

Wakati mwingine nikawa navuta sana masikio yake naye akawa anaruka juu sana kama wafanyavyo ndege, nikawa navutiwa na usafiri ule nikizidi kumfuata Mnaro ambaye alionekana kuwa dereva mzuri sana kwenye usafiri ule.



Mara nilisikia ngurumo kubwa sana nyuma yangu, kugeuka niliona wanyama watatu wakubwa kuliko wale ambao tumepanda sisi wakija kwa kasi kubwa sana, wanyama wale walikuwa na macho ambayo yalitoa mwanga wa kutisha sanaaa! “Kimbiaaaaaaa, hao wanyama ni maadui wakubwa sanaaa” alisema Mnaro huku yeye akikaza mwendo zaidi na hatimaye kutokomea kizani, nami nikajitahidi kuvuta zaidi masikio ya paka yule mkubwa lakini hakuwa na mwendo mkubwa kama yule paka wa Mnaro, nikaona wanyama wale wakizidi kunikaribia na hatimaye mmoja wao akawa karibu kabisa, hatimaye akaja kama anakuja kunigonga! Nikamrusha paka wangu juu zaidi mnyama yule akapita lakini nikaona wanyama wawili waliokuwa nyuma yangu wakinifuata hukohuko juu, nikashuka chini nao wakaja. Wakawa wananikimbiza nikijitahidi kulazimisha mwendo wa paka yule, lakini kwa mbele nilimuona mnya yule mwingine ambaye alipitiliza aliwa anakuja kwa kasi upande ule ambao mimi nilikuwa nikitokea! Nilijaribu kuangalia huku na huko lakini sikumuona Mnaro, wasiwasi ukatanda moyoni mwangu.......









Nilijikaza nikaamua kuwa nitafanya lolote kukabiliana na wanyama wale, niliamini haukuwa wakati wangu wa kufa kwa maana niliishajiapiza kuwa sitokufa kabla ya kumrudisha mke wangu kipenzi katika maisha ambayo ameyazoea.

Muda huu nilikuwa nimewekwa kati, wanyama wawili wakiwa nyuma yangu na mmoja akiwa mbele yangu, wote wakiniijia kwa kasi huku nami nikikazana kuelekea mbele kama sikuwa nikimuona mnyama yule wa mbele yangu.

Nikajikuta nikitazamana usokwa uso na mnyama yule tukiwa tumeelekeana kama ambao tunataka kugongana, na unaelekea nia ya mnyama yule ilikuwa ni kugongana maana alizidi kuongeza mwendo akiwa ameikaza mno sura yake ya kutisha kama ambaye amedhamiria ubaya. Nami nikajifanya kama sina akili kama yeye na ninakusudia kugongana lakini nilipomfikia nikakwepa haraka akapitiliza kwa kasi kubwa huku mimi nikiyumba vibaya juu ya paka niliyekuwa nimempanda, nusura nianguke ila nikajikaza na kuendelea huku nikizibana mbavu za paka yule kwa miguu yangu ili nisianguke lakini nikajikuta nikiwa nimegundua kitu, kwa kumbana paka yule kwenye mbavu alikuwa akiongeza kasi kiasi ambacho sikutegemea.

Nikaendelea kubana mbavu z a paka yule ambaye akakazana mpaka kuwa wapoteza kabisa wanyama wale kwenye upeo wa macho yangu! Nikaenda nikipunguza kasi na hatimaye nikasimama na kujaribu kufikiri nawezaje kumpata Mnaro lakini sikupata jibu, wakati huo pia sikujua ilikuwa saa ngapi. Hofu ikaanza kunipanda nikijiuliza nitafanyaje kama kutakucha na watu wakanikuta katika mazingira yale nikiendesha nyau!

Nikaamua kurudi nyumbani kupitia njia ambayo ilinileta pale huku nikiwa najiuliza kipi kitanipata iwapo nitakutana na wanyama wale ambao walinikimbiza muda mfupi uliopita, lakini nilikwenda mpaka nikawa napaona nyumbani bila kukutana na wanyama wale, Mnaro pia sikuwa nimemuona na sasa nikawa najiuliza itakuwaje kuhusu mnyama yule kama mimi nitaenda nyumbani, je nitamuweka wapi. Nilikosa majibu na bado nilikuwa nina wasiwasi wa asubuhi kufika na kunikuta katika hali ile, hivyo nikaamua kumuacha mnyama yule achague pa kwenda nami niingie ndani. Nikaenda mojakwa moja mpaka kwenye ukuta ambapo tulipita wakati wa kutoka nichukua kijiti kile alichonipa Mnaro, nikakibana kwenye kidole cha mwisho kama ambavyo alinielekeza na kukwenda kujaribu kupenya kwenye ukuta lakini cha ajabu nilishindwa, nikajaribu tena na tena lakini ukuta ulikuwa imara. Nikajiuliza nakosea wapi lakini bado nilijijibu kuwa niko sahihi, nikajaribu tena ila kwa mara nyingine nikakwama. Nikiwa naendelea kuwaza hili na lile nikasikia sauti ya baba akikohoa sebuleni, hapo nikajua atakuwa ameamka na kufungua wa chumbachumbauchanguuachkuuacha wazio haitowwzekana tena ktenaimi kuingikuingiaikupitiamlangoni, hivyo nikaenda kugonga mlango mkubwa ambapo baba alinifungulia nikaingia na kumkuta akiwa na maswali mengi sana ikanibidi kumuhadithia safari nitokayo kuanzia mwanzo hadi mwisho, baada ya kisikia maelezo yangu baba alionekana kuhofia sana juu yapaka yule.

Akaamua kutoka nnje ili kuangalia kama atamuona, ila akarudi akiwa na amani kabisa "nadhani litakuwa limeondoka, unadhani lingebaki hapa asubuhi tungewaeleza nini majirani kama wangeliona?.. alisema baba, maneno ambayo yalikuwa ni yakweli kabisa..

nami nikaridhika na kuamua kwenda kulala maana nilikuwa nimechoka sana.

Nikaingia chumbani kwangu na kujifungia kisha nikapanda kitandani kwaajili ya kulala lakini kabla hata usingizi haujanichukua

Nikasikia mtu akipiga makofi ya kupongeza, nilijishangaa kuona hata sikushituliwa na hali ile, nadhani nilikuwa nimeanza kuzoea maisha yale ya mauzauza..
 
SEHEMU YA 13

"Umenifurahisha sana safari hii" ilisema sauti ile ambayo niliitambua moja kwa moja kuwa ni ya Mnaro, kisha ikaendelea "ukiendelea kuwa na ujasili kama ambao umeuonesha leo basi tutafanikiwa haraka kuliko ambavyo tulitegemea" maneno haya ya mwisho yakanisisimua na kuirudisha hali yangu ya uchangamfu kutoka kwenye uchovu na uvivu niliokuwanao pale kitandani, nikaamka na kuwasha taa, nikaweza kumuona Mnaro ambaye alikuwa kwenye pembe moja ya chumba kile kisha akaja moja kwa moja na kukaa na mimi pale kitandani.. "uliniacha katika wakati mgumu sana nilipokuwa sikuoni, nilikuwa na hofu sana iwapo watu wangenikuta katika mazingira yale ningefanyaje" nilifungulia maongezi kwa kumuelezea Mnaro juu ya wakati mgumu ambao nilibakinao baada ya kukosa muongozo.. "unadhani ni sisi pekeyetu tulikuwa tukifanya shughuli za kichawi huko nnje?" Aliuliza Mnaro lakini akaendelea kabla sijamjibu "kuna maelfu ya wachawi ambao walikuwepo huko mtaani lakini hakuna hata mmoja ambaye alikuwa akiogopa" kufika hapo nikagundua kuwa alikuwa anataka kuonesha ni namna gani mimi ni muoga.. "tatizo hata muda wenyewe sikuwa nikiujua nikahofia pengine panaweza kukucha nikiwa bado sijarudi" nilijaribu kujitetea.

"Wachawi hufanya shughuli zao hata mchana, kukucha kungekuzuia nini? Kuns mengi sana yanaendelea hata kwenye jamii ya hapa mtaani, ni macho yenu tu hayaoni" baada ya kusema hayo akatoa kachupa kutoka kwenye mkoba wake ule wa ngozi na kunikabidhi..

Nikajaribu kuitikisa kujua kulikuwa na nini ndani yake, nikagundua kulikuwa na kitu kama chumvi hivi..."iwapo utapaka dawa hiyo usoni, hamna ambacho hautokiona" alinieleze nami nikafungua na kujaribu kujioaka kidogo, kweli ilikuwa ni kama chumvi na haikuwa ikibaki usoni, baadala yake ilikiwa ikianguka chini wakati naipaka, naye akaniambia haina shida, lengo limetimia tayar. Nilivutiwa kuona haibaki usoni kwa maana kumbe ningeweza kuipaka na kutembea nayo kuelekea popote.



Mnaro hakuwa na jambo lingine la kuzungumza na mimi kwa usiku ule hivyo akaniaga na kuondoka nami usingizi ukanichukua.

Nilikuja kuamka asubuhi majira kama ya saa moja na robo na kuamua kuelekea bafuni kujiswafi kabla ya kuendelea na mipango mingine, lakini nilipofika bafuni nikagundua kuwa sabuni ilikuwa imeisha hivyo nikaamua kwenda dukani kwanza kununua sabuni, lakini nilipotoka nnje tu nikapatwa na mshangao kuona paka yule mkubwa ambaye nilikuwa nikimfanya usafiri usiku akiwa amesimama katikati ya uwanja wa nyumbani pale. Nikarudi ndani na kumuita baba na kumuelezea ambacho nilikiona pale nnje kwa maana yeye alinihakikishia usiku kuwa paka yule alikuwa aneondoka. Tukatoka nnje pamoja ilikumuona paka yule ila baba hakuwa akimuona. Nikagundua kuwa ni ile dawa ambayo nilijipaka usoni ndiyo inayonitofautisha uwezo wangu wa kuona na wababa hivyo nikajifanya kama ambaye nilijichanganya na kumruhusu baba arudi ndani, "acha mawazo mwangu, utachanganyikiwa. Matatizo ni sehemu ya maisha" alisema baba huku akirudi ndani nami nikafarijika kuwa hata watu wengine hawatoweza kumuona paka yule hivyo nikaendelea na safari ya dukani.



Nilipata sabuni kisha nikaanza safari ya kirudi nyimbani, njiani nilikitana na dada ambaye huwa anatembeza vitafunwa asubuhi kwenye majumba, hata kwangu huwa anapita na wakati mwingine huwa tunanunua, lakini kitu cha ajabu leo alikuwa uchi, uchi kabisa wa mnyama "habari za asubuhi kaka, vipi nikiletee vitumbua ?" Alinisalimia na kuuliza dada yule, nadhani hakijua kama niligundua kuwa alikuwa uchi. "Hapana, sitaki vitumbua vinavyouzwa uchi" nilimjibu kikorofi dada yule baada ya kumuona kuwa anajaribu kunifanya mjinga ikiwa ninaona kinachoendelea, nilijutia pia muda wote wa nyuma ambao nilinunua bidhaa zake. Dada yule alioneshwa kushtushwa na kauli yangu ila akajikaza na kujifanya kama hanielewi, "haya kama huhitaji, nitakuletea siku nyingine" alisema dada yule akijichejeshachekesha nami nikamjibu "usikanyage tena kwangu machawi mkubwa wee" kufikia hapo alionekana kukasirika waziwazi "kwani wewe sio mchawi? Usingekuwa mchawi usingejua kama mimi ni mchawi.. kwanza huna lolote nimeshawachezea mara ngapi pale kwako, kama unajiona umekua tutaonana usiku" alibwata dada yule huku akiendelea na safari yake kwa kasi, nami nikaendelea na safari yangu kuelekea nyumbani.



Nikiwa hatua chache kutoka nyumbani nikaona watu wengi sana wakiwa pale kwangu, nikashtuka na kukaza zaidi mwendo, nilipokaribia zaidi niliweza kumuona na yule paka mkubwa katikati ya wale watu..







Nilifika nikiwa na shauku ya kujua ambacho kinaendelea huku nikiwa na hofu pia, watu wale watanifanya nini kama uwepo wa yule paka ndiyo sababu ya kuwepo kwao pale, nilijiuliza.
 
57261115_784255105292832_6521996195043213312_n.jpg
 
SEHEMU YA 14

Mchawi ni adui mkubwa sana kwenye jamii yoyote, hakuna ambaye angeweza kunielewa kuwa nafanya jambo lile kwa nia njema kwa maana hajawahi kuonekana mchawi mwema. "Vipi jamani kwema hapa?" Niliuliza kwa sauti yenye kitetemeshi cha uoga ndani yake mara baada ya kufika na watu wote wakasitisha mazungumzo na kunipokea kwa macho. "Sio kwema sana bwana, si unajua tena mambo ya kidunia haya" aliongea bwana mmoja wa makamo kwenye lile kundi na kisha akaendelea "huyu bwana ni miongoni mwa wakazi wa eneo hili" alianza kuelezea bwana yule huku akimnyooshea kidole bwana mwingine ambaye kwa harakaharaka alionekana ana matatizo "bwana huyu, amepatwa na tatizo ambalo linafanana sana na ambalo limekupata wewe hivyo tumeelekezwa tukuone pengine tunaweza kusaidiana mawazo" alimaliza bwana yule akaweka kituo kunipa nafasi yaniingie vyema kisha akaendelea "bwana huyu amepotelewa na binti yake siku ya tatu sasa, jitihada za kumtafuta mpaka sasa hazijafanikiwa pamoja na polisi kujitahidi kadri ya uwezo wao. Mwisho tumefikia kuamini kuwa huenda amepotea kama alivyopotea mkeo na wanawake wengine wengi wenye ujauzito, sijui tunaweza kusaidianaje?" Aliweka kituo bwana yule na macho ya watu wote yakawa kwangu, muda huu mimi nilikuwa kimya nikishukuru kimoyomoyo kuwa umati ule haukuwepo pale kwaajili ya paka yule wa kichawi.. "ndugu yangu tunaomba utusaidie, niko tayari kukupa chochote kwaajili ya binti yangu...." alisema bwana yule mwenye kupotelewa na binti yake nami nikamuwahi kabla hajaongea zaidi "hata mimi sijampata mke wangu mpaka leo ndugu yangu, bado nahangaika bila mafanikio na wala sijui ni kwavipi nikusaidie" baada ya maelezo haya bwana yule alionekana kuchanganyikiwa, akasimama akitembea kama mtu ambaye anataka kuondoka lakini ghafla akanirudia "sikiliza bwana, kuna tetesi mitaani kuwa wewe umepata mbinu ya kumrudisha mkeo ndio maana hata huangaiki tena" alisema bwana yule akibaki amenitumbulia macho kama ambaye ananitaka kuthibitisha habari zile... "ni kina nani wanaeneza habari hizo, hakuna mtu ambaye amewahi kunifuatilia hata kwa kuuliza kujua habari za kumtafuta mke wangu, leo wanayajuaje hayo maendeleo? ni uzushi tu ambao wala hauna ukweli wowote" nilijitahidi kutoa maelezo yale ya kujitetea lakini bwana yule alionekana waziwazi kutoamini.. "kama utaona una chochote cha kunisaidia tafadhali nitafute, alisema huku akinikabidhi business card yake ambayo niliitupia macho haraka haraka na kujua kuwa alikuwa ni hakimu mkuu wa mahakama ya wilaya..

Umati ule ukaanza kuondoka taratibu huku nikibaki mimi na maswali mengi ambayo sikuwa na pakuyapatia majibu yake, je nilipaswa kuwaeleza watu wale juu ya safari ya kwenda Muifufu? Kwanini jamii inafikiri kuwa ninayo njia ya kumpata mke wangu? Pengine mzee Miale atakuwa amewaeleza juu ya ujio wa sauti ya Mnaro nyumbani kwake siku ile, au inawezekana ni fikra za watu tu baada ya kuona jitihada zangu za kumtafuta mke wangu zilisimama ghafla mbele ya macho yao.

Niliingia ndani nikaendelea na shughuli zangu za kawaida kisha nikaamua kutoka angalau ninyooshe miguu maana nilichoka kukaa peke yangu ndani kwa maana baba pia alikuwa ametoka.

Kabla sijatoka nikaamua tena kupaka ile dawa kwa maana nilikuwa nimeoga hivyo kuiondoa, na kuamua kuitumia safari ile kujionea ambayo yanaendelea kwa siri kwenye jamii ile.

Kumbe jamii ile ilikuwa imejawa sana na mambo ya kishirikina, hasa katika sehemu za biashara. Niliona vitu vingi sanaaa, vingine vilikuwa vikinitisha ingawa nilikuwa nikivumilia na kujifanya kama sivioni.

Nikatembea sana mpaka nikajikuta nimechoka na kuamua kukaa chini ya mti na kupumzika. Nikiwa pale nikapata wazo la kwenda kwa mzee Miale angalau nikapate kujua kama ni yeye aliyewaambia wale watu waliokuja nyumbani kuwa mimi nimepata njia ya kumpata mke wangu, nikaanza safari ya kuelekea kwa mzee Miale ambapo nilifika na kupokelewa na yeye mwenyewe, tukakaa na kuanza mazungumzo..

"Umefikia wapi kwenye jitihada zako mwanangu?" Hili lilikuwa swali la kwanza la mzee Miale ambalo sikuliona kama lilikuwa la kumaanisha kwa maana kwake na kwangu sio mbali, kama kweli alikuwa na nia ya kujua lazima angekuja na kuniuliza "bado napambana mzee" nilimjibu kwa kifupi na kisha nikahamia kwenye swala ambalo lilinileta pale "mzee kuna watu wamenitembelea nyumbani kwangu leo,..." nilianza kuongea ila mzee Miale hakuruhusu nimalizie akadakia "ninafahamu, walianzia hapa kabla ya kuja kwako" wakati mzee huyu akiendelea kuongea alikatiza paka mweusi, mbaya, na mkubwa kama yule ambaye ninaye kule nyumbani akitoka ndani kwenye vyumba kuelekea nnje ya kajumba kale kadogo, nilishangaa nikawa najiuliza kumbe mzee huyu naye ni mchawi, nilikuwa nimetoka kabisa katika mazungumzo na kumsindikiza nyau yule mbaya kwa macho akielekea nnje jambo ambalo mzee Miale aliligundua naye akaacha kuongea na kubaki akinitizama mimi, nadhani hata yeye alishangaa nimewezaje kumuona paka yule.
 
SEHEMU YA 15

"hana matatizo huyo achana naye" alisema mzee yule kisha akarudi kwenye mada husika ili kulipoteza swala la paka yule "wale watu walifika mpaka hapa na lengo kubwa lilikuwa ni kujua wewe umefanikiwa kwa kiasi gani katika utafutaji wako, nami nikawajibu kuwa sikuwa nikijua lolote hivyo wakaamua kuja kwako" aliweka nukta mzee Miale. "Kwahivyo hukuwaambia jambo lingine lolote?" Niliuliza na mzee yule akatikisa kichwa kukataa nami nikabaki bila neno la ziada la kusema, nikaamua kuondoka na kurudi nyumbani kupumzika.



Ilikuwa ni majira ya saa 12 jioni ambapo nilikuwa nimejipumzisha chumbani kwangu nikiangalia filamu, nikachoka na kupitiwa na usingizi.

Katikati ya usingizi nilisikia kama kuna mtu anazungumza ndani ya chumba kile nikashtuka na kufumbua macho. Nikakutana na sura ya dada yule ambaye alitaka kuniuzia vitumbua akiwa uchi asubuhi tukashindwana akiwa amenikalia tumboni.

Dada yule alishtuka sana alipoona nimefumbua macho nadhani hakutegemea kama nitaamka, akainuka haraka na kutaka kukimbia lakini nilimvuta akaanguka chini pembeni ya kitanda nami nikaamka haraka na kumuwahi pale chini, akaniwahi na kukimbia akiuelekea ukuta huku nikimsindikiza kwa kofi zito sana la mgongo ambalo lilimfanya apepesuke ila akajikaza na kutoroka kupitia ukutani, na mimi sikusubiri nikapitia hapohapo kumfuata dada yule ambaye nilimuona kwa mbali akikimbia nami nikamfuata kwa kasi ya ajabu. Nilikuwa na kasi ambayo sikuwahi kuwa nayo kabla siku hiyo mpaka mimi mwenyewe nilijishangaa, lakini nikaendelea kumkimbiza dada yule ambaye naye alikuwa na mbio kwakweli, safari yetu ilitupeleka mpaka kwenye shule ya msingi ambayo ilikuwa jirani na dada yule akakimbia kuelekea kwenye uwanja wa shule hiyo huku mimi nikimfuata lakini nilisimama ghafla mara baada kuona kundi kubwa la watu wakiwa wamekaa wakitengeneza mduara pale uwanjani, dada yule akaenda moja kwa moja na kukaa katikati ya mduara ule huku watu wote waliokuwepo pale wakigeuza macho yao na kuangalia kule alikotokea ambako ndipo nilipokuwa nimesimama mimi. Nikaona eneo lile halikuwa salama hata kidogo hivyo nikaondoka kwa mwendo wa kasi kurudi nilikotokea. Nikitembea harakaharaka huku nikigeuka nyuma kila mara kuhakikisha kuwa sifuatwi. Nilitoka nnje ya shule ile na kushika njia kubwa ambayo ingenipeleka moja kwa moja nyumbani lakini baada ya hatua chache ilisimama gari mbele yangu ikiwa imewashwa taa kubwa na kunimulika vizuri, nikiweza kuitambua mara moja gari ile kuwa ilikuwa ya polisi.. "simama hapo mara moja" iliamuru kwa ukali sauti kutoka ndani ya gari, nami nikatii. Wakashuka askari wawili wakiwa na silaha wakawa wakija upande ule ambao nilikuwepo. Nilikuwa nimevaa suruali ya michezo na flana nyepesi lakini chini sikuwa na viatu, nitawaambia natoka wapi askari wale? Sikuwa na jibu. " wewe ni nani na unatoka wapi?" Aliuliza askari mmoja wa askari wale, akili yangu ikafanya kazi harakaharaka nikajikuta nimejibu, "natoka kumsindikiza mgeni afande" askari wale waliangaliana kwa mshangao kisha mmoja wao akauliza "unajua ni saa ngapi saa hizi?" Kwakweli hata sikuwa nikijua muda, ninachokumbuka tu ni kuwa nililala mida kama ya saa 12. Sikujaribu kujibu swali lile kwa maana nilijua naweza kuharibu zaidi. Askari mmojawapo akaangalia saa yake na kisha kusema "ni mgeni gani huyo ambaye unamsindikiza saa saba kasoro?" Duuh! Muda umeenda kiasi hiki? Nimewezaje kulala muda wote huo? Nilikuwa nikijiuliza bila hata kujibu swali la mapolisi wale.. "tunaomba kitambulisho chako" alisema askari yule mwingine, sikuwa na kitambulisho pia, jambo ambalo askari wale walilitegemea bila shaka.. "hana kitambulisho, twende naye kituoni tu huyu" alishauri askari mmoja baada ya kuona nimekuwa kimya baada ya kuombwa kitambulisho. "Jamani mimi ni mtu mwema, haina...." kabla sijamalizia sentensi yangu askari yule akafoka "unatufundisha kazi? Twende kituoni" nikabaki nimeduwaa, sikuwa na neno lolote la kusema.. "bwana tunaenda ama umegoma?" Aliuliza askari mmoja, ikanibidi kukubaliana na matakwa yao. Tukaongozana mimi nikitangulia, wao wakifuata nyuma hadi kwenye gari yao ambapo tulipanda na kuelekea kituoni.

Tulifika, wakanichukua maelezo na kuniweka mahabusu. Muda huo niliweza kukadiria kuwa ilikuwa majira ya saa saba na nusu, nikajiuliza itakuwaje kama Mnaro atanifuata kwa ajili ya muendelezo wa mafunzo yetu? Sikuwa nikitaka kupoteza hata siku moja. Nikaamua kuwa niondoke kupitia ukutani, nikafanye ya kufanya usiku huo kisha nirudi mahabusu mule kabla hakujakucha. Nikatoroka na kuelekea nyumbani ambapo nilijilaza na kumngojea Mnaro kwakuwa sikua hata nikijua namna ya kumpata, ilikuwa ni lazima aje yeye kama ulivyo utaratibu wetu siku zote.

Niliendelea kujilaza pale mpaka usingizi ukanipitia ambapo nilikuja kushtuka mlango wa chumba changu ukigongwa. Nilikurupuka na kuangalia saa ya ukutani pale chumbani ambayo ilionesha kuwa ilikuwa saa mbili na dakika kumi asubuhi.. "khaaaaaa" nilihamaki sana baada ya kugundua kulikuwa kumekucha bila kurudi mahabusu..


ITAENDELEA BAADAE JIONI
BURE SERIES
 
SEHEMU YA 16

Nilikurupuka nikaenda moja kwa moja na kufungua mlango. Alikuwa ni baba akiniamsha na kunipa taarifa juu ya mama yangu kuumwa, alisema mama alikuwa amelazwa akiwa na hali mbaya sana. Tukakubaliana kuwa yeye aondoke kwenda kumuuguza mama huku akiniacha mimi nikiendelea na jukumu la kumtafuta mke wangu, baba akaondoka.

Nilibaki pale ndani nikijiuliza cha kufanya juu ya kutoroka kwangu mahabusu, mpaka sasa lazima watakuwa wamegundu kutokuwepo kwangu, lazima watakuwa wameshangazwa na jambo lile kwa maana niliondoka nikiacha chumba kile cha mahabusu kikiwa kimefungwa kama ambavyo walikiacha. Je nirudi mahabusu? Lakini nitawaeleza nini iwapo watanikuta mule ndani wakati wamegundua tayari kuwa sikuwepo?

Au niache tu kwenda? Hili pia ni jambo gumu kwa maana nilitoa maelezo yote kunihusu mimi, tena kwa usahihi kabisa, hivyo wana uwezo wa kunipata iwapo watanihitaji.. niliendelea kujiuliza maswali mwisho nikaamua kutoenda mahabusu, liwalo na liwe kwanza serikali haiutambuwi uchawi, niliwaza.

Nilipumzika pale nyumbani mpaka majira ya saa tano asubuhi kisha nikaamua kwenda benki nikatoe pesa kwa maana nilikuwa karibu kuishiwa.

Nikatoka na kwenda benki, nikachukua pesa na kisha kuamua kuingia kazini angalau nikawaone watu wangu kwa maana sasa ulikaribia mwezi toka niombe likizo ile ya bila malipo.

Nilifika kazini nikakutana na wafanyakazi wenzangu, tukaongea mengi huku wengi wakinipa pole na kunitaka nirundi kazini. Kwa muda ule mfupi wa kuongea na wafanyakazi wenzangu nilijikuta nikipata ari ya kufanya kazi. Ninaweza kufanya kazi na mambo mengine yakaendelea, isitoshe mchana nakuwa bila kazi kwa maana mambo mengine hufanyika usiku, niliwaza na kufikia maamuzi kuwa nirudi kazini.

Nikaamua kwenda kwenye ofisi ya mkuu wa kitengo ili kuzungumza naye juu ya kurudi kwangu kazini. Tukaongea na kukubaliana, kisha nikabaki tukiongea mengine kuhusu maisha kwani alikuwa rafiki yangu pia. Tulipomaliza maongezi nikatoka nikikusudia kwenda nyumbani lakini secretary wa mkuu wa kitengo akanipa taarifa "kaka Abuu, kuna wageni wako mapokezi" wageni wangu mapokezi? nani anaweza kuwa mgeni wangu ikiwa sikuwepo kazini kwa muda wote huu?, nilijiuliza huku nikielekea mapokezi kuonana na hao wageni wangu.

Sasa nilikuwa nikiutizama mlango wa mapokezi lakini kabla sijaingia ndani akili ikaniambia nimeingia mtegoni, nilipokamatwa na polisi niliwapa maelezo yote kunihusu ikiwa ni pamoja na mahala pangu pa kazi, kivyovyote baada ya kutoroka sehemu ya kwanza kutafutwa ingekuwa hapa kazini kwakuwa hawana taarifa kuwa sipo kazini.

Baada ya kupata wazo hilo nikaamua kugeuka haraka ili kutoka nnje ya ofisi lakini nilikutana na askari polisi akiwa ndani ya sare "bwana Abubakar Saire uko chini ya ulinzi" niliishiwa nguvu, mwili ukanyong`onyea na kujuhisi kama sina uzito. Askari yule akaja na kunitaka kumpatia mikono yangu kisha akanifunga pingu na kuwaita wenzake kwa simu nao wakaja kutokea mapokezi, safari ya kuelekea kituoni ikaanza huku wafanyakazi wenzangu wakibaki wamepigwa na butwaa wasielewe nimefanya kosa gani la kuwindwa na polisi.



Tulifika kituoni nikaingizwa mahabusu, lakini kilikuwa ni chumba tofauti na kile ambacho niliingizwa mwanzo.

Nilitamani sana kutoroka mule mahabusu ila nilishindwa kutoka kutokana na kutokuwa na vijiti vile ambavyo vingeniwezesha kupenya kichawi.

Nikakaa humo kwa nusu saa kisha wakaja askari watatu na kuanza kunihoji, askari wale walikuwa wakiamini kuwa kutoroka kwangu kituoni pale kulitokana na kusaidiwa na askari mmojawapo mule ndani na walikuwa wakitaka kumjua askari huyo "bwana, sisi unachotaka kujua ni kimoja tu, nani alikusaidia kutoka mahabusu na si kingine chochote" alisema askari mmoja ambaye alikuwa akizungumza lafudhi ya Kihaya na alionekana mwenye roho ya kikatili.

Kwa haraka haraka sikuwa na jibu la kutoa nikabaki nikiwaangalia tu kitendo ambacho walikitafsiri kama dharau. "Tumewahi kukutana na wajeuri kuliko wewe lakini walitii bila kupenda, hakuna ambaye huingia humu akaacha kutupa habari ambazo tunazitaka" alisema askari yule Muhaya akionekana amekasirika, "kwanini mpaka uumizwe? Bora useme mapema tu kwa maana kusema lazima utasema" aliongea askari mwingine lakini bado niliendelea kuwa kimya, niwajibu nini sasa? Kuwa nilitoroka kichawi? Kwanza hawawezi kuniamini, niliwaza.

Ghafla nilizabwa kofi kali la shavuni na yule askari ambaye hakuwa ameongea chochote toka ameingia mule ndani, lilikuwa kofi zito kiasi kwamba sikuamini kuwa lilitoka kwa askari yule ambaye nilimuona kuwa alikuwa mpole kuliko wale wengine, ama kweli umdhaniae ndie kumbe siye.
 
SEHEMU YA 17

Damu zilikuwa zikinitoka puani kutokana na kofi lile ambalo lilinifanya pia Nikapatwa na kizunguzungu cha hali ya juu. "Uko tayari kusema ama show iendelee?" Aliuliza askari yule ambaye aliyenizaba kofi ambaye alikuwa ni mdogo wangu kiumri, lakini kwa mara nyingine nilikuwa kimya akanizaba kofi lingine kali mpaka nihisi harufu ya damu kisha akanibaki akinikazia macho kama ambaye anangoja nitoe majibu lakini sikuwa na chakusema, nikamuona akinyanyua mkono wake ili kuninasa kibao kingine nikasimama na haraka huku nikikinga mikono kuzuia kofi lile zito ambalo lilitua juu ya mikono yangu.. askari wale wote watatu wakanikabili kunidhibiti kila mmoja akipiga alipopaona mpaka nikaanguka chini.

Askari mmoja akatoka na kurudi mara moja akiwa amebeba kiti cha mbao na kamba, wakaninyanyua na kunikalisha kitini kisha wakanifunga wakinishikanisha vyema na kiti kile kutia mikono yangu ambayo ilizungushwa nyuma ya kiti na kukazwa na kamba vizuri kisha miguu nayo ikafungiwa viziri kwenye miguu ya mbele ya kiti kile.

"Tunakuuliza kwa mara ya mwisho, nani alikutorosha kituoni jana" aliongea askari ambaye sasa nilimgundua kuwa alikuwa miongoni mwa wale ambao walinikamata usiku na kunileta pale kituoni kabla sijatoroka kichawi..

Nilitamani kujieleza ili adhabu ile iondoke lakini nini niseme ndio tatizo ambalo sikujua kulitatua.

"Endelea afande" alizungumza askari aliyenifunga kamba baada ya kuona sitoi maelezo na askari yule mtaalamu wa kupiga makofi akanisogelea tayari kwa muendelezo wa adhabu ile..

"NGOJENI JAMANI NASEMAAA" nilijikuta nikisema kwa sauti kubwa yenye hofu ndani yake.. "kusema tunajua utasema tu unataka ama hutaki" alisema askari yule mdogo lakini katili huku akinizaba kofi lingine zito nikajihisi kuchanganyikiwa.. "haya sema sasa" aliamuru askari mwingine, wakati huu damu zilikuwa zinazidi kutoka puani, na mdomo wangu wa chini ulikuwa umevimba kutokana na kupatwa na kofi mojawapo, lakini nilijikaza nikaanza kujieleza harakaharaka kabla askari yule asiyerudi nyuma akiamua kupiga hajaamua tena.. "jamani mimi nilitoroka kichawi, nilipenya kwenye ukuta" nilijieleza lakini kama ambavyo nilitegemea askari wale hawakuniamini, waliangalian, wakacheka kisha wakanirudia "wewe ni mchawi? toroka sasa uende" alisema askari mmoja kimzaha huku wenzake wakicheka.

Askari wale waliona kama nimepania kutomtaja ambaye alinitorosha hivyo wakaamua kunining`niniza kweye kamba ambayo iliifunga mikono yangu ikiiunganisha pamoja na kisha askari yule mpenda kupiga akawa ananishindilia ngumi nzito za tumbo huku akisema mchezo ule ungesita iwapo nitawaeleza nilitorokaje mahabusu..

"Kama hutomtaja ambaye alikusaidia kutoka mahabusu utakufa kwa adhabu humu ndani" alisema askari ambaye alionekana yeye ndiye mwenye kuagiza wenzake lakini yeye hakuwa akifanya chochote zaidi ya kuongea.

"Kwanini unaacha niteseke ikiwa unajua ni wewe ambaye ulinitorosha, nirudishie pesa zangu basi" niliropoka kumwambia askari yule akabaki mdomo wazi huku askiri aliyekuwa akinipiga akisitisha zoezi ya kumgeukia askari mwenzao, wakawa wanamtazama bila kusema neno naye akagutuka na kutaka kuniamia lakini wenzie walimdhibiti wakamtoa mule chumbani.. "kumbe tunapoteza muda ikiwa unajua ulichokifanya" alisema askari yule aliyekuwa akinipiga wakati wakimvutia nnje askari mwenzao ambaye nilimvika kesi isiyomuhusu ili mimi nipumzike na kipigo kile.

Nikabaki pekeyangu kwenye chumba kile ambacho niligundua kuwa kilikuwa cha mateso, huku nikiwa nimening`inizwa kwa kamba nikiwa na maumivu makali.

Nikawa nikiwaza juu ya hatma yangu, nilitamani kutoroka lakini sikuwa na vifaa, Mnaro pia sikuwa nimemuona toka nipatwe na matatizo yale ya polisi na sikujua kama alikuwa anajua kama nilikuwa polisi. Mipango ya kumkomboa mke wangu itafanikiwaje kwa mimi kiwemo mule ndani, na roho iliniuma sana na nikauchukia uchawi kwakua haukua na chakunisaidia.



Baada ya kama dakika ishirini aliingia askari yule mwenye lafudhi ya Kihaya akanifungua na kunihamishia kwenye chumba kile cha mahabusu ambacho nilitoroka. "Tulikuwa tunajua yule bwana ndiye ambaye atakuwa amekutorosha, hatukua na ishahidi tu, ila hakuna askari mwingine angeweza kufanya kitu cha aina hiyo hapa" alisema askari yule akinibwaga chini, nikagumia kwa maumivu ya tumbo.. "ungetueleza haraka wala yasingekupata hayo, sisi tulikuwa tunamtaka mpumbavu huyu ambaye anataka kututia matatizoni kwaajili ya tamaa zake, alisema askari yule huku akiondoka..

"Sasa nini hatma yangu afande?" Nilimuuliza polisi yule naye akajibu "tunawapeleka mahakamani kesho, wewe ni mshtakiwa namba moja na huyo mwenzio ni mshtakiwa namba 2" alisema askari yule akatoka nnje na kuniacha nikimuonea huruma polisi yule ambaye nimemsababishia matatizo.. lakini sikuwa na jambo la kufanya zaidi ya lile, pengine mpaka sasa ningekuwa bado napigwa. Niliwaza.

Mida ya saa 8 wafanyakazi wenzangu wawili walikuja kiniona wakaniletea na chakula. Walijaribu kuniwekea dhamana nitoke ila ikashindikana, ikanibidi kulala pale bila mpango wowote juu ya kutoka kwangu.
 
Back
Top Bottom