Simulizi: Mpenzi wangu Amina

Simulizi: Mpenzi wangu Amina

kallase

Member
Joined
Mar 18, 2020
Posts
27
Reaction score
43
Simulizi: Mpenzi wangu Amina.(01)

Mwandishi: Salum Kalase

Sehemu ya kwanza.


Maisha ni kuchagua na mimi nilichagua kumpenda Amina katika maisha yangu yote bila kujali ni nini kitakachotokea katikati yetu.

Ngoja kwanza, kwa majina naitwa Gift Mathayo Lugwisha ni mtoto wa pekee nyumbani kwetu, baba huwa anadai hakutaka iwe hivyo lakini ndio ishakuwa hivyo, ndoto yake ilikuwa ni kuwa na watoto kumi na mbili yaani alipanga kumiliki timu nzima na kocha wake lakini haikuwa hivyo kwani mama alimsaliti baba, hivyo baba akaamua kumpatia talaka yake mama na akanichukua mimi kwenda kuishi nae. Sijawahi kumwona tena mama yangu hadi leo.

Baba naye hakutaka tena kujiingiza kwenye ndoa , hivyo alinilea peke yake kwa msaada mkubwa wa bibi yaani mama yake baba.

Kiukweli nilipatiwa malezi bora sana anayopaswa kupatiwa mtoto hadi nafikia umri wa kujitegemea sikumbuki kujihisi mpweke kabisa kila nilipokuwa nyumbani.

Naposema nyumbani namaanisha nyumbani tu, yaani nyumbani kwa baba na bibi yangu ila tofauti na hapo maisha yangu yamekua na upweke mkubwa sana na hiyo ni kwa sababu ya machaguzi yangu.
Kama nilivyosema mwanzo maisha ni kuchagua, na mimi niliamua kuchagua maisha ya upweke kwa sababu ya kumpenda mwanamke mmoja tu naye si mwingine bali ni Amina, Kivipi?

Mimi na Amina tulikutana mara ya kwanza mwaka 2014 wakati naingia kidato cha nne katika shule moja inayopatikana huko Mwadui Shinyanga ya kuitwa Mwadui Secondary School. Mimi nilikua muhamiaji katika shule ile vivyo hivyo kwa Amina naye alikuwa muhamiaji pale.

Kwa kuwa wote tulikua wahamiaji haikutuwia ugumu kufahamiana kwani nakumbuka mimi ndio nilitangulia kufika shuleni, na baada ya wiki moja Amina naye akafatia, Siwezi kuisahau siku ya kwanza namuona Amina, naikumbuka vizuri sana siku ile hadi hii leo, ilikuwa ni kwenye kipindi cha Mathematics, kipindi changu pendwa sana lakini cha ajabu siku hiyo nilikua najihisi usingizi balaa, hivyo sikuwa namsikiliza kabisa mwalimu kwani usingizi ulikua umenizidia na nilikua nalala kila nilipokua napata muda japo kwa kuiba ili nisionekane na mwalimu.

Ndipo mlango wa darasa letu ukafunguliwa, macho ya wanafunzi wote darasani yakatazama mlangoni kuona ni nani anayeingia Kasoro mimi ambae nilikua bado nipo bize na usingizi wangu.

Akaingia mwalimu wa nidhamu Mr Justus akiwa anaongozana na Amina kisha akasalimiana na mwalimu mwenzake na kumweleza ametuletea mwanafunzi mpya ambae alimuamuru ajitambulishe “Hi!!! My name is Amina Rashid(Habari zenu, Majina yangu naitwa Amina Rashid)” Amina alijitambulisha kwa sauti moja nyororo ambayo sikuwahi kuisikia kutoka kwa mtu yeyote yule tangu dunia hii iumbwe, sauti ile ilinifanya niamke kutoka usingizini na kutazama mbele, La haula!!! Haikuwa sauti tu, hata urembo aliokuwa nao Amina nikiri kusema kuwa hakuna mwanafunzi wa kiume mle darasani ambae hakummezea mate.

“Gift hiyo siti pembeni yako anakaa nani?” Mwalimu aliniuliza
“Haina mtu mwalimu” Nilimjibu haraka haraka mwalimu ambae alimwelekeza Amina aje kuketi kwenye siti ya pembeni na ninapokaa.

Ni kama Mungu alikua upande wangu, kwani niliona kama kila kitu kinatokea kwa haraka sana “Mambo" Amina alinisalimia huku akiwa anatabasamu, tabasamu lile likanifanya niione sifa nyingine ya Amina kwenye uso wake, Amina alikua na vishimo viwili kwenye mashavu yake yaani dimpozi, ugonjwa wangu mimi huo, kiukweli niliweweseka nikashindwa hata kuijibu ile salamu, nikabaki namtazama tu nisiongee kitu.

Washikaji zangu walikuwa wananichora (wananitazama) wakaanza kucheka chini chini kwa kuniona domo zege. Amina hakujali sana mimi kutokumuitikia salamu yake, akavuta kiti chake na kuketi ili amsikilize mwalimu aliyokuwa anayafundisha.

Kipindi hakikupanda tena, akili yangu yote ilikuwa kwa Amina , muda mwingi niliutumia kumtazama tu, sikuwa na nguvu za kuacha kuitazama sura yake iliyokuwa imejua kupangiliwa na mwenyeji Mungu.
“Unanitazama sana shida nini?” Huo ulikuwa ni ujumbe wa kikaratasi ambacho Amina aliamua kuniandikia baada ya kuona namtazama sana. Ujumbe ule ulinifanya niache kumtazama na kuangalia mbele bila kumjibu chochote kile.

“Mbona haujanijibu, nimekuuliza shida nini" Amina alinipatia kiujumbe kingine tena, nikakisoma, na nikaamua kukijibu
“Nikisema wewe ni mrembo sana utaniamini?” Amina alisoma ujumbe wangu wa karatasi, nikamwona anatabasamu lakini hakunijibu chochote kile zaidi ya kukikunja kile kikaratasi na kukiweka kwenye begi lake.
“Nimekwambia wewe ni mrembo sana" Nilimtumia meseji nyingine Amina ambayo nayo aliisoma na kuiweka kwenye begi lake

Kitendo kile kikanitia unyonge sana, nikajihisi nimewahi sana kuzicheza karata zangu “Dah itakuwa ameshaniona muhuni" nilijiwazia na tayari nilijipatia majibu kuwa ndio hivyo nishampoteza Amina wangu kizembe namna hiyo.

Kipindi cha Mathematics kiliisha, vikafatia Vipindi vingine ambavyo navyo vilianza na kuisha bila ya mimi na Amina kusemezana. Wakati tupo kipindi cha mwisho kabisa cha siku hiyo zikiwa zimebaki kama dakika ishirini hivi kipindi kuisha, nikawaza kama kumpoteza Amina nishampoteza sasa kwanini nisimpoteze mazima kwa kujilipua kabisa na kuzielezea hisia zangu kwake ndipo nikaamua kuchukua karatasi na kumwandikia maneno haya,

“Mbona hivyo Amina unanitisha ujue" kisha nikampatia asome huku mimi nikiwa nimetazama mbele.
Haikuchukua dakika Amina akanigusa na kunipatia kikaratasi alichokuwa amenijibu “Kwanini unasema hivyo?”
“Kosa langu nini sasa hapa kukusifia au, mbona umeninunia ghafla"
“Hapana hata sijakununia mbona"
“Sasa kama haujaninunia mbona hukunijibu sms yangu nilivyokwambia wewe ni mrembo?”
“Naomba basi tuzungumze kipindi kikiisha wanafunzi wenzetu wakishaondoka darasani sawa" Maneno ya Amina yalinishtua kidogo moyo wangu, sikutegemea kama angeweza kuniambia vile, yaani atake kuzungumza na mimi baada ya vipindi kuisha, tena peke yetu mimi na yeye tu.
“Sawa" Nilimkubalia.

Kipindi cha mwisho kiliisha, wanafunzi wakaanza kuondoka kurudi mabwenini kwa lengo la kwenda kujiandaa na chakula cha mchana. Mimi na Amina hatukuondoka, tulibaki tumeketi kwenye siti zetu tukiwa kimya bila kuongea chochote kile. Sijui Amina alikua anawaza nini muda ule lakini kwa upande wangu sikuwa najua cha kuongea baada ya wanafunzi wote kuisha mle darasani.
“Vipi unanitaka?”

“U....u...Unasema?” Nilijikuta nauliza swali baada ya kujibu swali aliloniuliza Amina.
“Nimekuuliza kama unataka kuwa na mimi kwenye mahusiano? Amina aliniuliza tena swali lake na mara hiyo alikuwa amelifafania zaidi ili nimwelewe alichokuwa ameniuliza. Nilimtazama kwa muda kabla ya kumjibu, Amina alikua amenikazia macho, hakuwa na aibu hata kidogo Tofauti na mimi niliyekuwa naona aibu hata kumtazama,
“Nimekuuliza swali mbona haunijibu" Amina alinisemesha tena
“Swali lako gumu sana ujue"
“Kwahiyo haujui unachotaka kutoka kwangu si ndio?”
“Hapana sio hivyo Amina"
“Ila kumbe nini sasa.......”
“Nikisema kwamba sitaki kuwa na wewe nitakuwa nakudanganya nahitaji sana kuwa na wewe lakini..........” Kabla hata sijamalizia kuongea Amina alinikatiza

“Sawa tutakua wapenzi kuanzia leo sitaki kujua hizo sababu nyingine" Amina aliniambia vile huku akitabasamu. Nadhani udhaifu wangu mkubwa kwa Amina ni tabasamu lake naweza kusema hivyo kwani nazikumbuka vyema hisia zangu muda ule Amina ananiambia kuwa tumeshakuwa wapenzi, ukweli ni kwamba sikuwa tayari bado kuwa na Amina kimapenzi lakini lile tabasamu lake ndilo lililoninyima ujasiri wa kumkatalia alichokuwa amenieleza.

Sijui hata kwanini nilitaka kukataa kuwa naye kwani Amina alikuwa na kila sifa za mwanamke ambazo mwanaume rijali alizihitaji kutoka kwa mwanamke wake.
“Tutakutana jioni sasa mpenzi wangu" Amina alinieleza vile kisha akachukua begi lake na kuondoka zake kwenda bwenini kwao, aliniacha nikiwa bado nimesimama pale kwenye siti yangu nikiwa siamini kilichokuwa kimetokea.

ITAENDELEA.

WhatsApp No: 0625000557
#KakaMkubwa.
 
MPENZI WANGU AMINA.
MWANDISHI: SALUM KALASE
MAWASILIANO: 0625000557

SEHEMU YA PILI.
Nguvu za kwenda hata bwenini sikuwa nazo kabisa, nilibaki nimeketi tu mule darasani nikijisikilizia. Baada ya muda kupita niliamua kuelekea moja kwa moja hadi dining Hall (Sehemu ya kupatia chakula) ambako nilijua nitakutana na mshkaji wangu Elias ambae kivyovyote vile nilijua tu ni lazima atakuwa amekuja na vyombo vyangu.

Kweli kama nilivyowaza, Elias alikuwa ameshanichukulia na chakula changu,
“Oii G mbona umechelewa hivyo nina ubao kish***nzi leo ujue" Elias alinisemesha, tayari alikua ameshaanza kula bila kusubiria jibu langu.

“Gift...... Gift.......”,Nilisikia kama jina langu unaitwa na hata kabla sijageuka kutazama ni nani aliyekuwa ananiita, nilishangaa narukiwa na mtu mgongoni kwangu kitu kilichofanya nishtuke kidogo, nikageuka na kutazama kuona ni nani huyo aliyenirukia,

“Hahahahahah mbona umeshtuka hivyo" Amina aliniuliza swali lililonifanya nibaki nimeduwaa nisijue cha kumjibu.

Sikuwa peke yangu ambae nilionekana kushangazwa na ujio wa Amina pale kwangu, bali hata mshkaji wangu Elias naye alionekana kushangaa, wanafunzi wenzangu pia mule Dining wengi wao walikuwa wanatutazama, kitendo cha Amina kunirukia kiliwashangaza wengi kwani hakuelewa ukaribu wangu mimi na Amina umeanza tangu lini.

“Yaani huwa sipendi kula peke yangu vipi naweza kujumuika nanyi hapa tule wote?” Amina alituuliza mimi na Elias,

“Ndio karibu haina shida” Elias alimjibu Amina ambae aliweka chakula chake kwenye meza yetu na kuanza kula.

“Vipi G wewe hauli au" Elias aliniuliza baada ya kuniona bado nimesimama bila kuketi kwenye kiti kwa ajili ya kula chakula changu.

Swali lile lilimfanya Amina ahairishe Kula, akaanza kunitazama, ni kama alikuwa anataka kuona ni nini nitakachokiamua pale, mimi sikutaka shida yoyote ile, hivyo niliamua kuketi na kuanza kula jambo lililomfanya Amina atabasamu, nadhani alitabasamu kwa furaha.

“Namfahamu mwenzako tu kwani unaitwa nani wewe?” Amina alimuuliza Elias wakati tunaendelea kula,

“Naitwa Elias na wewe nani vile?”

“Amina........... Nyie ni marafiki sio?”

“Sio marafiki tu sisi ni zaidi ya ndugu kwa hapa tulipofikia au naongopa G?”

“Ni kweli tulishapita Levo ya urafiki sie"

Nililijibu swali la Elias ambae alionekana kuchangamka wakati anaongea na Amina.

“Kumbe, basi hata nikikueleza siri ya rafiki yako unaweza kuitunza kama siri yako eti” Amina alimuuliza Elias

“Hilo ni swali kwani? Nina siri nyingi sana za mwamba hapa na hakuna hata moja iliyovuja hadi leo" Elias alitamba,

“Basi sawa nimefurahi kusikia hivyo"

“Vipi kwani kuna jambo unataka kunieleza au?”

“Lipo ndio sema sidhani kama ndugu yako atafurahia nikikweleza"

“Usijali hata, G hanaga noma weh nieleze tu Amina"

“Kweli kabisa?”

“Niamini mimi Amina"

Amina kusikia vile alinitazama, ni kama alikuwa anataka kuniomba jambo lakini alishindwa, muda wote huo mie nilikuwa kimya nawasikiliza tu wanavyozungumza bila kutia neno lolote lile.

“Kwakuwa umetaka kujua shemeji yangu nitakwambia, Gift na mimi ni wapenzi" Amina alimweleza Elias

“Weeeeeh acha basi kunitania" Elias alionekana kushangaa

“Naanzaje kukutania sasa shemeji yangu si umuulize G kama nakudanganya sasa" Amina alijitetea.

Elias kusikia vile alinitazama, mie sikumtazama, Elias moja kwa moja akajua taarifa zile alizokuwa ameambiwa na Amina zilikuwa ni za ukweli. Bila kutarajia Elias alianza kucheka, sio kucheka tu alicheka sana kiasi cha kufanya wanafunzi wengine waanze kututazama pale tulipokuwa tumekaa.

“Kweli watu wasiri sana, nashukuru kukufahamu shemeji yangu, jisikie huru kabisa kwangu kama ni shemeji umepata sasa” Elias alijitapa.

“Naomba ukimaliza kula tuzungumze kidogo pembeni” Amina aliniomba, sikuwa na kipingamizi zaidi ya kumkubalia.

Kweli tulivyomaliza kula Elias aliondoka na vyombo vyangu na kutuacha mimi na Amina tunazungumza,

“Mbona kama sikuelewi G" Amina aliniuliza swali ambalo sikulielewa

“Haunielewi vipi?”

“Naona kama haujafurahia mimi kujitambulisha kwa Elias au nimekosea"

“Sijafurahia vipi sasa, au nini kinachokufanya useme hivyo?”

“Nakuona tu kama huna raha hivi au labda nalazimisha mahusiano kwako nambie nijue" Amina aliniuliza

“Hapana, mbona umefika mbali hivyo Amina siko poa tu” Nilijitetea.

“Kweli?”

“Kweli kabisa Amina, kwanini nisipende sasa wewe kujuana na Elias" Nilijitahidi kumwondolea hofu Amina ambae alikubaliana nami japo sikumuona kama ameridhishwa na majibu yangu. Tukaagana akarudi bwenini kwao na mimi nikaenda bwenini kwetu.

Huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yetu mimi na Amina, mwanzoni sikuwa huru kabisa kujionesha kwa watu kuwa tulikua wapenzi, tofauti na Amina yeye muda wote ni kama alitaka kila mtu afahamu kuwa alikuwa kwenye mahusiano na mimi.

Amina alikuwa huru sana kufanya chochote na mimi bila kujali macho ya watu, alipenda sana kutembea na mimi huku tukiwa tumeshikana mikono, hakuona aibu kunikumbatia kila mara tulipokuwa tunakutana na wakati mwingine kunipiga mabusu kabisa.

Kama nilivyosema mwanzoni sikuwa huru kabisa lakini kadri siku zilivyokuwa zinakwenda mbele ndivyo nilivyojikuta naanza kuzoea na kujikuta nakuwa huru na mimi kufanya chochote na Amina wangu bila woga wowote ule.

Amina alinieleza kuwa kabla hata ya kuhamia shuleni kwetu alikuwa ameshanuia moyoni mwake kuwa mwanaume wa kwanza atakayemtongoza hapo shuleni basi ndiye atakayekuwa mpenzi wake na atafanya lolote lile kwa ajili ya mpenzi wake huyo. Naona kama bahati hiyo iliniangukia mimi kwani ukiachana na kwamba mimi ndiye niliyeanza kumtongoza Amina, kumbe hata jibu langu lilikuwa limeshaandaliwa hata kabla ya Amina kufika shuleni kwetu.

Shule yetu ya Mwadui ilikuwa ni shule inayoendeshwa kwa kusimamia maadili ya dini ya kikristo kwani ilikuwa chini ya kanisa la KKKT (Lutheran). Hivyo kuna mambo ambayo yalikua yanapingwa sana shuleni kwetu hasa mahusiano. Tayari mimi na Amina tulikuwa tumeshapewa onyo na mwalimu wa nidhamu kuwa kama tutaendelea kuonekana tupo pamoja basi wazazi wetu wangeitwa shuleni na sisi kupewa taarifa ya kufukuzwa shule.

Pamoja na yote hayo hatukuonekana kutaka kusikia, ndio kwanza kila siku penzi letu lilizidi kukua, hakuna kitu ambacho hatukuwahi kufanya mimi na Amina kama wapenzi, ndio hakuna kitu ambacho hatukuwahi kufanya, kila kitu kinachotakiwa kufanywa na wapenzi basi sie tulikifanya bila kujali mazingira yaliyokuwa yanatuzunguka.

Siku moja tukiwa darasani tunajisomea mwalimu wa nidhamu alitufuata wote n a kutueleza tumfuate ofisini kwake. Wito ule haukuwa wa kushangaza kwetu kwani tulikuwa tumeshauzoea.

Tulifatana na mwalimu hadi ofisini kwake, kufika ofisini kwake tulishangaa kuwakuta wazazi wetu wanatusubiria huko, yaani baba yangu na mama yake AAmina. Walipotuona kwa pamoja walitabasamu, tabasamu ambalo kiuhalisia lilinitia woga moyoni mwangu, sijui mwenzangu Amina yeye alilichukulia vipi lile tabasamu.

“Wazazi wenu wanataka kuzungumza na nyie mie nipo nje nawasubiria" Mwalimu wa nidhamu aliongea vile kisha akatupisha.

Tulianza kwa kuwasalimia wazazi wetu, kisha wakatuomba tukae ili wazungumze na sie
“Huyu ndio kijana wangu Gift” Mzee wangu alimweleza mama Amina ambae alinitazama kwa tabasamu pana usoni mwake,

“Nashukuru kukufahamu mwanangu" Mama Amina aliongea vile huku akinipatia mkono wake, tukashikana mikono kisha naye akamtazama mwanae Amina na kumweleza baba yangu,

“Na mimi huyu ndio binti yangu Amina naona wanalingana lingana tu na mwanao Gift" Mama Amina alimalizia kuongea maneno yaliyomfanya baba yangu acheke kidogo kitu kilichozidi kunichanganya kwani sikujua kilichokuwa kinaendelea pale.

“Mama, huyu ndiye mwanaume uliyeniambia unamleta kumtambulisha kwangu kama mumeo ajae?” Amina alimuuliza mama yake swali lililonichanganya kidogo

“Unasema? Mume? Au sijaelewa nini hapa........ Unaongea nini Amina huyu ni baba yangu ujue" Nilijikuta nauliza maswali mfululizo kwa paniki kitu kilichofanya baba yangu aniombe nitulie kwanza anielezee.

“Mwanangu sitaki kuwa mpweke tena, nahitaji kuwa na msaidizi na mimi” Mzee wangu alinieleza.

Hakujua maneno yale yalivyokuwa yananichoma moyoni mwangu, niliwaza itawezekana vipi mama wa mpenzi wangu awe mke wa baba yangu mzazi, yaani ni kama nilikuwa napewa taarifa za kuanza kumuheshimu Amina na kumchukulia kama dada yangu, nitaweza vipi mie niliwaza.

Kiukweli nilijihisi kutaka kuchanganyikiwa ghafla.............

ITAENDELEA...


WhatsApp Number: 0625000557
 
MPENZI WANGU AMINA..........(03)
MWANDISHI:SALUM KALASE
MAWASILIANO: 0625000557

SEHEMU YA TATU.
“Vipi Gift mbona sikuelewi" Baba aliniuliza

“Hapana baba nipo kawaida tu" Nilimjibu baba kumuondoa wasiwasi lakini kiukweli sikuwa sawa kabisa, taarifa zile ziliichanganya sana akili yangu. Mbaya zaidi sikuona kama ni taarifa zilizomchanganya Amina ambae muda wote alionekana kuwa sawa kabisa.

“Nashukuru kukufahamu sana baba yangu" Amina aliongea na baba yangu huku akiwa ametabasamu.

“Nashukuru pia kukufahamu" Baba yangu aliitikia

“Unaona sasa mume wangu hapakuwa na ugumu wowote ule ulikua unaogopa bure” Mama Amina aliongea na baba yangu ambae alionekana kufurahia sana kila kitu kilichokuwa kinaendelea pale.

Muda wa wazazi wetu ulifika kuondoka, wakaondoka huku wakiwa na furaha sana. Ni mimi tu ndiye niliyeonekana kujali sana taarifa zile. Ilinibidi nimwombe Amina tuzungumze kwanza kabla ya kurudi darasani.

“Unaonekana kama haujashtushwa kabisa na taarifa hizi za wazazi wetu" Nilimuuliza Amina

“Cha kunishtua nini sasa hapo? Au kipi cha ajabu ambacho haujawahi kukishuhudia hapa? Hebu waache wazazi wetu waufurahie uzee wao bhana"

“Haujanielewa Amina, sipo hata huko mie, nachojaribu kuwaza hapa ni kuhusu mahusiano yetu, itawezekana vipi mimi na wewe kuwa pamoja huku wazazi wetu nao wanataka kuoana?”

“Hahahahahaahahah" Amina alianza kucheka sana kitu ambacho sikukielewa.

“Unacheka nini sasa mbona sikuelewi”

“Gift..... unafurahisha sana ujue inamaana hadi sasa haujajua bado kama tumeshaachana" Amina alinieleza maneno hayo huku akiwa anacheka, nikadhani ananitania hivyo ikanibidi nimuulize kama yupo siriazi au ananitania.

“Nipo siriazi mie, mahusiano yetu yameishia pale wazazi wetu walivyojitambulisha kuwa wapo pamoja na wanahitaji kuishi pamoja"

“Amina...... acha basi kunitania mbona Unaongea maneno makali hivyo alafu kiwepesi sana"

“Gift naona unanichelewesha tu hapa naomba uniache nirudi zangu darasani “ Amina aliongea maneno yale kisha akaanza kuondoka.

Sikutaka kukubaliana na ukweli uliokuwa mbele yangu,nilimkimbilia Amina na kumzuia asiendelee na safari yake.

“Amina mbona hivyo mpenzi wangu, haya mambo mbona yanazungumzika usinifanyie hivyo mwenzako” Nilimweleza Amina maneno hayo kwa hisia, tayari machozi yalikua yameanza kunitoka.

“Gift nakuomba kuwa mwelewa basi"

“Nakuwaje mwelewa sasa kwenye suala kama hili Amina wewe ndio sio mwelewa"

Amina kuona kama sipo tayari kumuelewa alianza kuondoka lakini nilimzuia, akawa analazimisha kuondoka hivyo hivyo kwa nguvu lakini alishindwa kwani tayari nilikua nimeshamkamata mkono wake kwa nguvu kitendo kilichofanya tuonekane kama tunagombana.

Wanafunzi waliokuwa kwenye madarasa ya karibu walianza kutuchungulia kupitia madirisha ya madarasa yao. Wapo walioanza kupiga kelele za shangwe ambazo sikuzijali hata kidogo. Nia na dhumuni langu kwa muda ule lilikuwa ni kumtaka Amina anielewe na si vinginevyo.

Baada ya mvutano wa kama dakika tano, walimu kadhaa walifika pale, mwalimu wa nidhamu akatutaka tuelekee ofisini kwake .

“To my office right now (Nendeni ofisini kwangu sasa hivi)” Mwalimu yule wa nidhamu kwa majina ya Justus aliongea kwa hasira.

Tulielekea hadi ofisi ya nidhamu, huko mwalimu alitueleza tupige magoti kabla ya kuanza kuzungumza naye.

“Eenhe nyie wapendanao leo imekuwaje hadi mkaanza kupigana hadharani" Mwalimu Justus alituuliza kwa ukali kidogo.

Mie sikuwa na nguvu za kuzungumza kabisa kwani hasira zilizokuwa zimenijaa kifuani mwangu hazikuelezeka, na nilijikuta nalia mfululizo, sikuweza kujizuia kabisa. Ila pamoja na yote hayo Amina alionekana kuwa Tofauti na mimi. Ukiachana na hasira alizokuwa nazo juu yangu, Amina alitaka kunieleza msimamo wake bayana tena mbele ya mwalimu wetu

“Mwalimu, nimeshamweleza mara kibao Gift kuwa simtaki na sitaki kuwa nae labda unisaidie wewe kumweleza labda atakuelewa" Amina aliongea maneno makali yaliyoshindilia zaidi Msumali wa moto kifuani mwangu.

Kusikia vile mwalimu Justus alinitazama kwa muda bila kuongea chochote kile kisha akamtazana Amina na kumweleza kuwa aelekee darasani na aniache mie mule ofisini. Amina akaondoka zake.

Baada ya Amina kuondoka mwalimu Justus aliniamuru ninyanyuke kisha niketi kwenye kiti cha mule ofisini, nikafanya vile kisha mwalimu Justus akaniambia nimueleze ukweli wa kila kilichotokea na kinachoendelea kuhusu mimi na Amina. Sikuona Haja ya kumficha tena mwalimu hivyo Nilimweleza ukweli wa kila kilichokuwa kimetokea.

Mwalimu alinisikiliza kwa umakini sana, hakutaka kuniingilia, aliniacha nizungumze hadi nimalize, kisha akanyanyuka na kuchukua karatasi moja na kalamu ya kuandika.

“Mdogo wangu huu ni mwezi wa ngapi?” Aliniuliza

“Ni mwezi wa tisa mwalimu” Nilimjibu

“Sasa nisikilize kwa makini mdogo wangu, mwezi kesho kutwa unaingia kufanya mitihan yako ya mwisho kumaliza kidato cha nne, namaanisha nini kusema hivyo, huu ni muda wako wa kuwa makini sana na masomo na si kitu kingine chochote kile, si umesema Amina mnaenda kuishi nae pamoja mtakaporudi nyumbani?” Aliniuliza na nikamkubalia

“Sasa hebu fanya hivi kwa muda huu uliobakia......Komaa na kitabu mdogo wangu, soma sana na usiiruhusu akili yako iwaze mambo mengine, najua ni ngumu ila inawezekana kama utaamua alafu mtakaporudi nyumbani ndio ukakomae na Amina wako si umesema unampenda sana na huwezi ishi bila yeye?” Aliniuliza tena na nikamjibu Ndio.

“Basi hakikisha unafaulu mitihani yako, hakuna mwanamke anayependa mwanaume zezeta sawa mdogo wangu"

Mwalimu Justus alinieleza mambo mengi sana kuhusu maisha siku ile, hakuwa tena mwalimu wangu bali aliamua kuwa kama kaka yangu, kikubwa alichonishauri nisisahau kilichonipeleka shule na nilimwelewa sana hivyo akaniambia nirudi darasani kujisomea.

Nilikwenda hadi darasani, huko nilifika na kumkuta Amina akiwa ameketi kwenye siti yake, hatukusalimiana zaidi ya kubaki tukimsikiliza mwalimu aliyekuwamo darasani anafundisha. Mwalimu alipomaliza kufundisha aliondoka na kutuacha sie tukijiandaa kutoka kwani hicho ndio kilikuwa kipindi cha mwisho kwa siku hiyo.

“Samahanini jamani wanadarasa naombeni kuzungumza nanyi kabla hamjaondoka" Amina alisimama na kuwaomba wanadarasa wasiondoke kwani anataka kuzungumza nao. Kweli wote waliketi na kumsikiliza nikiwemo na mimi.

“Kama mlivyoona tukio la pale nje lililomfanya mwanafunzi mwenzenu hapa (huku akinishika begani) hadi akalia, ujumbe ni mfupi tu ya kuwa mimi na Gift tumeachana kwa hiyo jimbo lipo wazi" Amina aliongea vile kisha akaanza kucheka.

Wanafunzi wote darasani walibaki wanamtazama Amina, hakuna aliyemwelewa, lakini hiyo haikuwa sababu ya yeye kuacha kuendelea kucheka

“Mimi na Gift tumeachana jamani msichoelewa nini hapa mbona kama mnanishangaa" Amina alikazia.

Hasira zilinijaa kifuani, kicheko kile cha Amina pia kilizidi kunizidishia hasira zangu, niliwaza ni kama kweli kulikuwa na ulazima kiasi hicho cha kuwatangazia wanafunzi wenzetu kuhusu mimi na yeye kuachana, jibu likawa ni hapana.

Bila kutarajia nilijikuta nimenyanyuka pale nilipokua nimekaa kisha nikamshika Amina kwa nguvu, nikamtwanga ngumi mbili za nguvu kwenye pua yake zilizompeleka chini moja kwa moja na kumfanya azime pale pale. Wanafunzi wenzangu wote walishtuka pia kwa kudhania kuwa labda naweza kuwa nimeua.

ITAENDELEA

Tafadhari usiache kutoa maoni yako ni muhimu sana kwangu

#KaKaMkubwa
 
MPENZI WANGU AMINA...........(04)
Na SALUM KALASE

SEHEMU YA NNE

Hasira Hasara!!! Ni msemo wa kawaida ila wenye maana kubwa sana. Binafsi msemo huo nilikua sijawahi kuuelewa hadi siku hiyo ambapo nilimshuhudia Amina akianguka chini kama mzoga mbele ya macho yangu.

Kelele za wanafunzi wenzangu mule darasani ndio zilizonitia hofu zaidi. Elias mshkaji wangu hakutaka kupoteza muda, alihitaji kuchukua maamuzi ya haraka ili anisaidie rafiki yake hivyo alimfuata Amina pale chini alipokuwa ameanguka kisha akaanza kujaribu kumuamsha bila mafanikio.

Wanafunzi wenzangu kadhaa nao walimsogelea Amina na kuanza kumsaidia Elias kumuamsha. Lakini hakuna kilichobadilika, Amina aliendelea kuwa kimya pale chini kitu kilichofanya wanafunzi wenzangu washauriane kumbeba na kumuwahisha kwa nesi wa shule.Wakafanya hivyo upesi baada ya wote kuwa wameafikiana.

Taarifa zilifika ofisini kuhusu tukio lile, mwalimu Justus akaniita tena ofisini kwake na hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa siku hiyo. Nilipofika tu ofisini mwalimu Justus hakutaka kusikiliza maelezo yangu zaidi ya kunishushia viboko mfululizo hadi pale aliporidhika ndio akaamua kuchukua barua aliyokuwa ameshaindaa tayari kwa ajili yangu.

“Nenda nyumbani ukaniletee wazazi wako" Mwalimu Justus alinieleza huku akiwa ananipatia ile barua.

Maneno ya mwalimu Justus yalikua yameeleweka sana lakini nilitaka kuyapinga kwa kujaribu kuomba msamaha labda nitaeleweka lakini ilikua ni kama natwanga maji kwenye kinu kwani mwalimu hakuelewa na alisisitiza niondoke shuleni mara moja bila kupoteza muda.

Hivyo ilibidi nielekee bwenini kwetu, huko nilikwenda kubadilisha nguo zangu na kuchukua baadhi ya vitu ambavyo nilivihitaji kurudi navyo nyumbani.

Safari yangu ya kurudi nyumbani ikaanza. Nakumbuka safari ile ilikuwa fupi sana kufika nyumbani, nafikiri ni kwa sababu ya mawazo mengi niliyokuwa nayo kichwani mwangu. Cha ajabu sikuwa nawaza kabisa kuhusu baba yangu, akili na mawazo yangu yote yalikuwa kwa Amina mpenzi wangu. Muda wote nilikuwa nawaza kama atakuwa amezinduka huko shuleni nilikomuacha. Nilijikuta najiona mjinga na nilizilaumu sana hasira zangu ambazo niliona ni kama ndio zilikuwa zimepigilia msumali wa mwisho wa mimi na Amina kuachana.

Nilifika nyumbani lakini sikumkuta mzee hivyo nikafanya utaratibu wa kuwasiliana nae, akanieleza kuwa yupo njiani anaelekea Arusha na mama yake Amina hivyo nifanye kwenda kwa bibi nikamsubiri huko. Sikubisha hivyo nikaanza safari nyingine ya kuelekea kwa bibi kwenda kumsubiri baba atakaporejea.
☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆
Amina alizinduka baada ya nusu saa toka afikishwe kwa nesi wa shule, mkononi mwake alikuwa ameshachomwa sindano na kutundikiwa dripu ya maji kwa ajili ya kumuongezea nguvu.

Nesi alimtoa hofu kwa kumueleza kuwa asijali kwani baada ya muda atakua sawa. Elias hakutaka kutoka ndani ya chumba kile tangu Amina alipokuwa amezimia. Alitaka kumwona Amina akiwa sawa hivyo hakutaka kuwa mbali naye. Yote hayo alifanya kama kuniwakilisha rafiki yake ambaye muda wote huo nilikua nimesharudishwa nyumbani bila hata kuagana nae.

“Gift yuko wapi?” Amina alimuuliza Elias

“Yupo bwenini amepumzika, hawezi kuja huku" Elias aliamua kumuongopea Amina, hakutaka kumpatia wasiwasi kwani lengo lake kubwa lilikuwa ni kuhakikisha anaona afya ya Amina inakuwa sawa tena.

“Kwanini asiweze kuja? Au hataki kuniona mimi?”

“Hapana sio hivyo, mwalimu Justus ndio ameelekeza hivyo, amemzuia kusogea kabisa karibu na wewe kuepusha maafa zaidi"

Kusikia vile Amina alianza kulia kwa kugugumia taratibu, hakutaka kutoa sauti japo machozi yaliyokuwa yanambubujika mashavuni mwake yalimsaliti.

“Shem shida nini tena mbona unalia"

“Jamani Gift wangu najua atakua ananichukia sana muda huu" Amina alijibu

“Hapana hata usiwaze hivyo shem, G anakupenda sana zaidi ya unavyofikiria"

“Nalijua hilo lakini nitafanya nini sasa mie? Ni lazima mmoja wetu alipaswa kuchukua maamuzi magumu ili kuweka mambo sawa, na mimi ndio nimechagua kuwa mbaya Elia”

Amina aliongea maneno ambayo Elias hakuyaelewa, hivyo ikabidi amuulize Amina ni nini alichokuwa anamaanisha kwa kusema hivyo.

Amina ilimbidi amwambie Elias kila kitu kilichokuwa kinaendelea, hakumficha hata kitu kimoja. Amina alimweleza Elias kuwa bado ananipenda sana lakini ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kuachana na mimi mapema kwani anaona sio sawa kuwa na mimi tena hali ya kuwa wazazi wetu wanakwenda kuoana, hivyo ameamua kuepusha mengi mabaya yanayoweza kuja kutokea huko mbele.

Elias alimuelewa sana Amina,pia alimuonea huruma sana kwani muda wote aliokuwa anaongea machozi yalikuwa yanamtoka na alijaribu kujizuia bila Mafanikio. Elias alimtia moyo Amina ya kuwa hilo nalo litapita.

Elias na Amina walizungumza sana siku ile kitendo kilichowafanya watengeneze ukaribu ambao hawakuwa nao mwanzo.

Elias aliamua kuchukua jukumu la kumlea Amina kipindi chote ambacho alikua anaumwa. Mazoea yaliongezeka hadi pale alipopona lakini hawakuacha kuendelea kuwa karibu. Amina alimuomba Elias abadili siti yake ya darasani na kwenda kuketi nae pale nilipokua nakaa mimi hadi pale nitakaporejea, Elias hakubisha akafanya hivyo.

Ukaribu wao haukuwa wa kawaida kwani kila sehemu walikuwa pamoja. Walipenda Kula pamoja dining, walipenda kuketi pamoja mida ya ibada za kanisani hata shughuli zote za shule walifanya pamoja.

Wanafunzi wenzangu wakaanza kuhisi labda Elias na Amina ni wapenzi lakini walikanusha kila mara walipoulizwa. Hakuna kati yao aliyekubali japo nafsi zao ni kama zilikuwa zinatamani skendo hiyo ingekuwa ni ya ukweli. Tayari hisia za kimapenzi juu yao zilikuwa zimeshajengeka. Kila mtu alikuwa anamtamani mwenzake lakini hakuna aliyeweza kuzieleza hisia zake. Labda ni kwa sababu ya ukaribu wangu kwao ndio maana walijikuta wanashindwa kuongea kile kilichokuwa kinawatafuna nafsi zao.

Amina yeye hisia zilimzidia hivyo aliamua kuchukua maamuzi magumu ambayo alijua fika yataniumiza sana. Amina aliamua kumweleza Elias kuwa anahitaji kuzungumza nae usiku wa siku hiyo baada ya kumaliza kujisomea masomo ya jioni. Elias hakuwa na hiyana zaidi ya kuitikia wito wa Amina.

Kweli usiku masomo yalipokwisha wanafunzi wote walitawanyika na kwenda mabwenini kwa ajili ya kulala isipokuwa Elias na Amina ambao walikuwa na miahadi ya kuzungumza usiku huo.

“Nakusikiliza Amina, naona upo kimya sana wakati watu wote wameshaondoka........” Elias alishindwa kuendelea kuongea kwani Amina alikuwa amemsogelea na kumchumu mdomoni mwake kisha akarudi nyuma na kuanza kumtazama bila kuzungumza chochote kile.

Elias hakutaka kupewa ishara nyingine tena, tayari alikuwa ameshaelewa ni nini ambacho Amina alikuwa anakihitaji kwa muda ule. Taratibu alimsogelea Amina kisha akazipeleka lipsi zake na kuzikutanisha na lipsi za Amina ambae alizipokea bila kipingamizi chochote kile kisha wote kwa pamoja wakaanza kubadilishana mate.

ITAENDELEA.

#KaKaMkubwa.
 
Kesho nitaposti SEHEMU YA TANO Alafu kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa wiki ijayo nitakuwa naposti kipande kimoja tu kwa siku

Jumamosi na Jumapili ni Mapumziko.
 
MPENZI WANGU AMINA..........(05)

Imeandikwa Na SALUM KALASE.

WhatsApp Number: 0625000557

SEHEMU YA TANO.

Ukurasa rasmi wa mahusiano kati ya Elias na Amina ulifunguliwa rasmi usiku ule. Kila mmoja wao kati ya Amina na Elias walionekana kukifurahia kitendo chao cha kubadilishana mate. Hawakutaka kujali tena kuhusu mimi, hisia zao ndicho kitu pekee walichokitazama kwa muda ule. Mioyo yao iliwaaminisha ya kuwa wanapendana sana na hawawezi kuacha kuwa pamoja kisa mimi.

Mimi nyumbani nilikaa kwa muda wa wiki tatu kabla ya baba yangu kurudi kutoka Arusha na kuniomba nirudi nyumbani kutoka kwa bibi yangu nilikokuwa nimeenda.

Baba yangu alitaka kujua ni kwanini anahitajika shuleni, Nilimweleza ukweli ya kuwa nimepigana ila sikumwambia kama mtu niliyepigana nae alikua ni Amina. Babba yangu kusikia vile alikasirika sana na alitaka kuniadhibu lakini alizuiriwa na mama Amina ambae alikuwepo muda wote ule tuliokuwa tunazungumza.

Baba alinieleza ya kuwa nimshukuru mama yangu kwa kunitetea kwani isingekuwa hivyo angenibutua sana. Kwa upande wangu mama Amina sikumuona kama mkombozi wangu bali nilimuona kama adui yangu kwani nilimuona kama mtu aliyesababisha mimi na Amina tuachane, hivyo sikuwa na nia ya kumshukuru kwani bila yeye nisingefikia hatua hiyo ya kumpiga Amina.

Usiku ulifika tukalala, kesho yake mapema tuliamka kwa ajili ya safari kuelekea shuleni. Tulivyofika shule, mwalimu Justus alitupokea ofisini kwake na alimweleza baba yangu kuwa anataka kunirudisha nyumbani rasmi nikasubirie muda wa kufanya mitihani ya kumaliza shule ndio nirudi kufanya mitihani.

Baba yangu alijitahidi sana kunitetea lakini msimamo wa mwalimu Justus ulikua vile vile, haukubadilika

“Nisamehe sana mzazi mwenzangu, lakini hatuwezi kuvumilia matukio kama haya na tunafanya yote haya ili kuepusha kujirudia kwa matukio kama haya kwa wanafunzi wengine" Mwalimu Justus alikazia.

Baba yangu hakuwa na cha kufanya zaidi ya kukubaliana na ukweli, hivyo alinieleza niende nikachukue vitu vyangu kwa ajili ya kuondoka.

Nilielekea bwenini kisha nikachukua vitu vyangu kwa lengo la kuondoka lakini kabla sijaondoka Elias alifika bwenini. Nilifurahi sana kumuona na tulikumbatiana kwa furaha, Elias aliniuliza kama nilikuwa na mpango wa kuondoka bila kumuaga,

“Hapana sio hivyo mshkaj wangu, nisingeweza kuja darasani si unajua tena ni muda wa masomo huu na mimi siruhusiwi kuwa hapa shuleni" Nilijitetea

“Hata kama mshikaji wangu, ila vipi umeambiwaje ofisini” Elias aliniuliza

“Nimeambiwa nirudi nyumbani, nitarudi shule muda wa mitihani kuja kufanya mitihani tu"

“Duh!!! Pole sana ila hapa sijaja kwa ajili yangu, Amina ameniagiza mwanangu" Elias alinieleza maneno ambayo sikuyaamini.

“Amina amekuagiza? Kwangu mimi? Anataka nini tena?!” Nilijikuta nauliza maswali mfululizo

“Usiwe hivyo bwana, Amina anahitaji kuzungumza na wewe anaumia sana kuona yeye na wewe hampo sawa twende ukamsikilize” Elias alinieleza.

Ikabidi tutoke bwenini na kuelekea maeneo ya vyoo vya wanawake, huko ndiko Elias aliniambia ya kuwa Amina yupo huko ananisubiria. Nilifika maeneo hayo na kumkuta Amina akiwa ameegemea ukuta mmoja wa choo kwa nje, na alikua ameinama kama mtu mwenye mawazo hivi,

“We mrembo mbona hivyo stress zote hizo za nini?” Nilimuuliza Amina baada ya kuwa nimemkaribia pale alipokuwa.

Amina alinyanyua kichwa chake na kunitazama, alionekana kuwa mnyonge sana, na aliponiona tu machozi yalianza kumtoka. Ilinibidi nimsogelee hadi pale alipokuwa kisha nikamuuliza anasumbuliwa na nini mbona analia.

“Gift nisamehe sana..... Nisamehe G .......” Amina aliniomba msamaha huku akiendelea kulia

“Haujanikosea chochote kile mbona, ni mimi ndiye nayepaswa kukuomba msamaha Amina"

“Hapana G, najuta sana mwenzio nisamehe sana" Amina aliongeza, na aliendelea kulia sana.

Hivyo ilinibidi nimsogelee karibu zaidi kisha nikamkumbatia na kuanza kumbembeleza huku nikimweleza ya kuwa asijisikie vibaya kwa sababu yangu kwani kila nilichokifanya nilikifanya nikiwa na akili zangu timamu na hapo nilikua nalipia gharama za maamuzi yangu. Pia nilimuomba msamaha kwa kumpiga siku ile, Amina alinielewa na baada ya muda alinyamaza ndipo nikapata muda wa kuzungumza nae. Muda wote huo Elias alikuwa amesimama pembeni yetu akitutazama na pia alikua anaangalia mazingira kuhakikisha usalama wa eneo lile tusije kukutwa na mtu yeyote eneo lile.

“Vipi Amina upo poa lakini" Nilimuuliza Amina

“Ndio, mie nipo salama sana, vipi nyumbani baba yako hajakasirika sana"

“Hapana hata, mama yako kanitetea sana, mzee hajanigusa kabisa"

“Usinitanie bhana, kwani mama yangu tayari ameshaamia kwenu?” Amina aliniuliza

“Ndio, sasa hivi wazazi wetu wanaishi pamoja”

“Aaanh sawa" Amina alinijibu, ukimya kidogo ukapita tukitazamana, ni kama nilikua na mambo mengi kichwani mwangu niliyohitaji kuzungumza na Amina lakini nilishindwa kufanya hivyo. Hivyo ikanibidi nimuage tu.

“Mie niondoke sasa, mzee ananisubiria nisimuweke sana"

“Okay sawa, au twende pamoja na mimi nikamsalimie baba"

“Hapana haina haja, wewe nenda darasani tu usijali sana kuhusu mzee wangu" Nilimkatalia Amina, nadhani hofu ya ukweli kujulikana ilikuwa imenitawala, sikutaka kabisa baba ajue kama mtu niliyegombana nae alikua ni Amina.

Nilirudi bwenini na kuchukua mizigo yangu, ofisini nilimkuta baba akiwa ananisubiri.

“Nimeongea na mwalimu wako hapa ameniruhusu nionane na Amina naomba uende ukaniitie kwanza nimsalimie kabla hatujaondoka.” Baba alinieleza maneno ambayo sikutaka kuyasikia kwa muda ule japo uwezo wa kumkatalia sikuwa nao hivyo ilibidi nimkubalie japo kishingo upande kumridhisha.

“Sawa baba wacha nikamuite"

Nilijua sehemu ya kumpata haraka ilikuwa ni darasani kwao, nilielekea huko kwani wakati naachana nae kule chooni alinieleza kuwa anarudi darasani muda huo huo.

Nilifika darasani, nikabisha hodi kisha nikamsalimia mwalimu niliyemkuta mule darasani kisha nikamuulizia Amina. Mwalimu alijaribu kumuita bila Mafanikio, wanafunzi wenzangu wakaniambia kuwa ametoka darasani muda sana hivyo nikawaza haraka haraka huenda labda akawa bado yupo ile mitaa ya chooni na akili yangu ilinieleza nielekee huko nikamtazame.

Nilielekea hadi huko chooni, ni kama nilikuwa nashauku ya kumuona tena Amina, kwani muda wote niliokuwa natembea kuelekea kule chooni sikuacha kuangaza macho yangu huku na huko kutazama labda naweza kukutana nae njiani.

Ile nafika chooni pale nje nilipokuwa nimemuacha Amina, sikutaka kuamini nilichokiona, Amina alikuwa ukutani ameegemea kwenye ukuta ule, alafu mbele yake Elias alikuwa amesimama karibu yake, mkono wake mmoja alikuwa ameupitisha kukizunguka kiuno cha Amina na mkono wake mwingine alikuwa amemshikilia vyema Amina shingoni kwake. Elias alikuwa ameinama kidogo ili alingane na Amina ambae yeye alikuwa ameinyanyua miguu yake kidogo ili kumsaidia Elias amfikie vyema pale alipokuwa na alikuwa amenyanyua mikono yake yote miwili kuzunguka nyuma ya shingo ya Elias.

Tukio lililokuwa linaendelea pale lilikuwa ni tukio la kubadilishana juisi za vinywa vyao. Amina alikuwa anampatia Elias juisi yangu ambayo alikuwa amezoea kunipatia mimi kila mara ninapoihitaji. Mbaya zaidi Amina alionekana kufurahia kitendo kile kwani alionekana kumpatia ushirikiano aliouhitaji Elias.

Nilijikuta naanza kutetemeka, hasira zilinijaa kifuani, nilihisi kama nakabwa kwenye koo langu, machungu niliyoyahisi pale hayakuelezeka, sikuwahi kuwaza kushuhudia jambo kama hilo tena mapema kiasi hicho, yaani wiki tatu tu zilitosha kabisa kumfanya Amina anisaliti, tena na mshkaji wangu wa karibu sana? Hapana, sikutaka kuamini.

“Aminaaaaa..............” Nilijikuta namuita Amina kwa hasira.

ITAENDELEA

WhatsApp Number: 0625000557

#KaKaMkubwa.
 
MPENZI WANGU AMINA...........(06)
Imeandikwa Na SALUM KALASE
WhatsApp Number: 0625000557

SEHEMU YA SITA.

Amina na Elias walishituka sana baada ya kunisikia nikimuita Amina. Wakaachiana haraka sana, Elias alinitazama na alionekana kuingiwa na woga ndani yake. Amina hakutikisika zaidi ya kubaki ananitazama huku akiwa bado ameegemea pale pale ukutani alipokuwa ameegemea.

Sikutaka kusikiliza maelezo yoyote yale kutoka kwao kwani tayari nilikuwa nimeshashuhudia kila kitu nilichopaswa kukishuhudia. Kwa hasira nilimkimbilia Elias alipokuwa amesimama kisha nikaruka juu huku nikiwa nimekunja ngumi ambayo niliipeleka moja kwa moja kwa Elias ikalisalimie shavu lake.

“Paaah!!!” Ngumi yangu nzito ilitua shavuni kwa Elias ambae alijitahidi kujizuia asianguke lakini uzito wa ngumi yyangu ulimpeleka chini moja kwa moja.
Sikuwa na muda wa kumsubiri anyanyuke kwani nilimfuata pale pale chini na kumkaba shingoni, kisha nikammiminia ngumi tatu za haraka haraka usoni kwake jambo lililomfanya Elias anaanze kulia kama mtoto mdogo kwa maumivu aliyoyahisi.

Amina kuona vile alinifuata na kunikumbatia kwa nyuma, mgongoni akinitaka nimuachie Elias lakini nilimsukuma pembeni kama karatasi. Sijui hata zile nguvu nilizitolea wapi, kisha nikaendelea kumshushia makonde Elias ambae alikua anajitahidi kujiziba uso wake ili nisimuumize zaidi. Mie sikulijari hilo kwani nilidhamiria kabisa kumdhuru Elias hivyo nilikuwa nampiga popote pale ambapo ngumi zangu ziliweza kutua.

Amina kuona vile aliona ni bora akaombe msaada kwa wanafunzi wenzetu. Kwa haraka sana alinyanyuka kisha akaanza kukimbia kuelekea kwenye darasa lililokuwa karibu na pale nilipokuwa nampigia Elias.

“Elias anakufa huku Jamani msaada Giiii atauwa.....” Amina aliongea huku akiwa analia baada ya kuingia kwenye darasa la karibu ambalo lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha tatu.

“Unasemaje hebu ongea taratibu nikuelewe" Mwalimu aliyekuwamo mule darasani alimuuliza Amina amwelezee kinachoendelea.

“Mwalimu Gift na Elias wanapigana huku, watauana hao" Amina alimweleza mwalimu yule huku akiwa analia.

Mwalimu kusikia vile, aliamua kuongozana na Amina kuelekea huko alikoelekezwa. Wanafunzi nao hawakuwa mbali kwani walifuatia msafara kwa nyuma kwenda kushuhudia tukio lile.

Mwalimu pamoja na wanafunzi wote hawakuamini walichokiona. Walimkuta Elias akiwa amelala chini kama mfu, huku damu nyingi zikiwa zinamvuja. Muda huo mimi nilikua nimesimama huku nikihema juu juu kwa hasira. Akili yangu ilikuwa haijakaa sawa bado kwani kitendo kile nilichokuwa nimekifanya nilikua naona kipo sawa kabisa.

Mwalimu alinisogelea nilipokuwa kisha akaanza kunipiga makofi mfululizo ambayo sikuwa hata nayahisi ukali wake. Moyo na akili yangu vilikuwa na maumivu zaidi hata ya hayo makofi ambayo niliona kama mwalimu ananipapasa tu,

“Mbebeni mwenzenu mumuwahishe hospitali" Mwalimu aliwaamuru wanafunzi wenzangu wambebe Elias. Na aliendelea kunishushia kipigo ambacho sikuwa nakihisi kabisa.

Mbele za macho yangu nilikuwa namtazama Amina ambae alionekana kuwa analia, ndio Amina alikua analia!!! Na muda ule nilijua fika aliyekuwa analiliwa pale hakuwa mimi bali ni Elias. Ukweli ule uliuvunja sana moyo wangu, maumivu niliyokuwa nayahisi pale hayakuwa ya kuelezeka kwa kinywa hiki hiki cha mwanadamu. Akili yangu iilikuwa inawaza mengi yasiyotamkika, kubwa zaidi niliwaza ni kosa gani kubwa nililomtendea Amina kiasi cha kuniadhibu kiasi kile, niliwaza, inamaana Amina amekosa wanaume wengine wote huko nje hadi akatoke na rafiki yangu kweli, sikuwa na majibu.

Nilipelekwa ofisini, huko nilifika na kufungiwa kwenye moja ya ofisi za pale shuleni, tayari mwalimu alikuwa ameshapiga simu polisi kuwajulisha kuhusu tukio lile, alifanya hivyo ili kusaidia upatikanaji wa PF3 mapema kwa ajili ya matibabu ya Elias pindi atakapofikishwa hospitali.

Baba yangu hakuwa na neno zaidi ya kubaki akishangaa, alijaribu kujiuliza ni nini kilichonikumba hadi kufikia hatua ile ya kumpiga mtu nusu kumuua, hakupata majibu.

“Kwahiyo mwalimu unanisaidiaje juu ya mwanangu najua polisi wakishafika hapa watahitaji kuondoka nae" Baba yangu alimuuliza mwalimu Justus

“Mzee wangu sina msaada wowote ule zaidi ya kukuomba tuwasubiri polisi wafike maana haya ni maagizo yao kuwa mwanao afungiwe mahala peke yake hadi watakapofika” Mwalimu Justus alimjibu baba yangu

“Sawa mwalimu naelewa hilo lakini kumbuka huyo ni mtoto bado tunapaswa kumkingia kifua"

“Mzee wangu..... Naona kama unapoteza muda wako hapa cha kukuomba labda hebu fanya kuiombea afya ya Elias huko aliko asije kufariki maana akishafariki tutazungumza mengine hapa" Mwalimu Justus alimwambia baba yangu kauli nzito yenye ukweli ndani yake iliyomfanya awe mpole.

Maombi na sala kichwani mwa baba yangu viliongezeka, pamoja na kwamba nilikuwa nimekosea kupigana lakini hilo halikubadilisha uhalisia wa kwamba mimi nilikua bado ni mwanae hivyo ilikuwa ni wajibu wake kunitetea.

Polisi walifika na kuelezwa kila kilichokuwa kimetokea. Baada ya kuwa wamejiridhisha na maelezo ya mwalimu walimuomba baba yangu wazungumze nae. Baba aliwaitikia na walimweleza uhalisia wa mambo jinsi yalivyokuwa.

“Hadi muda huu hali ya mgonjwa ni mbaya sana huko hospitali na haijulikan kama ataamka au lah hivyo basi mzee wetu tutaondoka na mwanao hadi kituoni huko tutakaa nae hadi pale mgonjwa atakapozinduka”.

“Sawa nawaelewa sana ndugu zangu vipi hakuna namna yoyote ya kunisaidia ili mwanangu asiende kulala polisi"

“Mzee wetu bila kukuficha kitu, hakuna tunaloweza kukusaidia zaidi ya kukuomba uzidishe maombi zaidi kesi hii isije badilika na kuwa kesi ya mauaji" Polisi yule alimalizia kuongea kisha akamuomba mwalimu Justus awaelekeze walikokuwa wameniweka.

Polisi walikuja na kunichukua, moja kwa moja hadi kituoni. Huko nilifika na kukabidhi vitu nilivyokuwa navyo mapokezi kama viatu, mkanda wa suruali na karamu za kuandikia kisha nikaelekezwa niingie rumande.
Labda niseme jambo moja hapa, katika umri wangu huu wa miaka thelathini na saba nadhani hilo ni moja ya tukio ambalo sintokaa nilisahau hadi naingia kaburini.

Nakumbuka wakati naingia rumande kwa mara ya kwanza siku ile nilikuwa na miaka kumi na saba tu. Nakumbuka nilipokelewa na harufu kali iliyokuwamo mule ndani, joto kali iliyokuwamo mule ilifanya midume yote iliyokuwamo mule ndani ivuje jasho lililokuwa linatoa harufu kali kwani mule ndani hakuna aliyepewa nafasi ya kuoga bila kujali umekaemo kwa muda gani.

Mbaya zaidi ndoo kubwa iliyokuwa mule rumande kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo na kubwa ilifanya hali ya hewa ibadilike zaidi kila ilipofunuliwa ili watu wajisaidie.

Cha ajabu kuna watu niliwakuta mule ndani wakiwa wameshaizoea ile hali na hawakuonekana kusumbuliwa kabisa na ile hali kwani walikuwa wanapiga stori zao kama kawaida huku wakicheka sana.

Kwangu mimi nilijihisi Kufa kufa hivi, joto kali jumlisha na ile harufu kali vilinizidia kiasi cha kunifanya nianze kuhisi kizunguzungu hivyo ilibidi nitafute mahala na kuketi.

Nikiwa nimeketi pale, geti la rumande lilianza kupigwa pigwa kwa nguvu na afande aliyekuwa nje akiashiria watu wote wasogee nyuma. Haraka haraka watu wote walirudi nyuma kwa woga kisha geti lile likafunguliwa na katika hali nisiyoitarajia askari wale waliingia ndani wakiwa wamemshikiria jamaa mmoja aliyekuwa amevalia chupi tu, yaani hakuwa na kitu kingine kwenye mwili wake zaidi ya hiyo chupi kisha wakamrushia ndani kwa nguvu jambo lililopelekea yule jamaa aanguke chini kwa nguvu na kuanza kuugulia maumivu.

Kwa kumtazama tu alionekana kuwa ni mtu aliyetoka kupigwa sana. Mwili wake wote ulikuwa unamtetemeka na alionekana kutokuwa na nguvu hata za kujigeuza zaidi ya kubaki pale pale chini ametulia akiugulia maumivu.

Huruma ilinijaa, nilijikuta namuonea huruma yule jamaa, ni kama niliyasahau matatizo yangu kwa muda, hali aliyokuwa nayo ilionekana kuwa mbaya sana lakini hakuna aliyeonekana kujali

“Braza kwani jamaa kafanya nini hadi apigwe hivyo?” Nilimuuliza Mshikaji mmoja aliyekuwa amekaa pembeni yangu

“Mwenzio ana mada kesi hapo alipo"

“Mada kesi?!!, unamaanisha nini kaka"

“Kaua mwenzako hapo alipo, huna haja hata ya kumuonea huruma anastahili kabisa kipigo hicho” Yule mshkaji alinieleza, na alionekana kumaanisha kila alichokiongea.

Ilibidi nimtazame tena yule jamaa aliyekuwa amelala pale chini jinsi alivyokuwa ameumia vibaya kwa kipigo kisha nikawaza inamaana na mimi kama Elias akifariki huko hospitali basi kipigo kama cha huyo jamaa kinaweza kunikuta.Nilijikuta naanza kupata woga na kujutia maamuzi yangu ya kumpiga Elias. Na jambo pekee nililokuwa nimebakisha ni kuuombea uhai wa Elias ili nitoke salama mule rumande.........

ITAENDELEA.

#KAKAMKUBWA

WhatsApp Namba: 0625000557
IMG_20240811_111042.jpg
 
MPENZI WANGU AMINA...........(07)

Imeandikwa na SALUM KALASE

Mawasiliano: 0625000557

SEHEMU YA SABA.

Elias alifikishwa hospitali ya Mwadui na kuanza kupatiwa matibabu. Madaktari walitumia zaidi ya lisaa limoja kumshona uso wake ambao nilikua nimeuhatibu vibaya sana. Amina yeye muda wote alikua amekaa nje ya wodi aliyokuwa anatibiwa Elias na muda wote alikua analia tu. Mwalimu na wanafunzi kadhaa pia walikuwapo, na wote kwa pamoja walionekana kuwa na mawazo juu ya hali ya Elias ambae walimfikisha hospitali pale akiwa hajielewi kabisa.

“Dokta vipi hali ya mgonjwa” Mwalimu Justus alimuuliza daktari baada ya kumuona akitokea katika chumba cha matibabu.

“Mgonjwa wenu anaendelea vizuri, na hivi tunavyoongea ameshapelekwa wodini akapumzike lakini itahitajika watu watatu wajitokeze kwa ajili ya kumchangia damu kwani amepoteza damu nyingi sana" Dokta alimaliza kuzungumza kisha akaondoka zake na kumuacha mwalimu Justus na wanafunzi wake wakijadili kuhusu suala lililokuwa mbele yao la kuchangia damu.

Siku mbili zilipita ndio Elias akaruhusiwa kurudi shule, taarifa zile zilikuwa nzuri sana kwa wazazi wangu maam Amina na baba yangu ambao wote walikuja kituoni kwa pamoja kwa lengo la kunitoa rumande. Baba alifanya mambo yote aliyoelekezwa na polisi na baada ya kumaliza niliruhusiwa kutoka.

Nilikua na furaha sana ya kutoka siku hiyo kwani siku tatu hizo nilizokuwa nimelala mule mahabusu kwangu niliziona kama ni mwaka vile. Mama Amina alinikumbatia baada ya kuniona na kunipatia pole lakini baba yangu yeye aliishia kunitazama tu na zaidi alitueleza mimi na mama Amina tufanye haraka tuondoke tusije chelewa usafiri wa kuturudisha nyumbani Kahama.

Tukiwa njiani, njia nzima sikuwa naongea, japo mama Amina alijitahidi sana kunisemesha bila Mafanikio. Akili yangu haikuwa sawa, mambo niliyokuwa nimeyashuhudia mule mahabusu yalinifikirisha sana. Nadhani nilipaswa kupelekwa humo ili nikajifunze zaidi kuhusu maisha. Jambo moja kubwa nililojifunza nikiwa rumande ni ushirikiano, kwani kwa siku zote zile mbili kamili nilizokuwamo mule ndani baba yangu hakuwahi kuniletea hata andazi moja lakini sikulala njaa kwa sababu ya ushirikiano waliokuwa nao wale watuhumiwa wenzangu, kwani hakuna mtu aliyeletewa chakula na akakila peke yake, ilikua ni kama amri ya kuwa atakayeletewa chakula basi wote lazima tutakigawana chakula kile.

Tulipofika nyumbani moja kwa moja nilikwenda kulala. Sikutaka hata kula chakula chao walichokuwa wameniandalia,

“Usiwaze sana mke wangu bado anamawazo huyo atakuwa sawa" Baba yangu alimtoa hofu mama Amina ambae muda wote alionekana kuwa na wasiwasi na mimi.

BAADA YA MIEZI MIWILI

Penzi la Amina na Elias lilishamiri, hakuna ambae hakujua tena kuhusu mahusiano mapya kati ya Elias na Amina. Wapo waliowabariki na wapo waliomuona Elias kama msaliti kwani Amina alikua ni mpenzi wa rafiki yake wa karibu sana. Elias hakujari hilo kwani alikua ameshampenda Amina na Amina aliridhia kuwa naye kwa moyo wake wote.

Vidonda na maumivu aliyoachiwa na Gift hakuyakumbuka tena kwani tangu atoke hospitali Amina alikuwa mstari wa mbele kumuhudumia. Kiufupi Elias hakupata tabu ya kujihudumia kwani alihudumiwa na Amina kimwili na kiroho pia, hivyo kupona kwake lilikua ni suala la muda tu.

Muda ulizidi kwenda na mitihani ilizidi kukaribia, lakini kadri muda ulivyozidi kwenda Amina alianza kuhisi mabadiliko makubwa kwenye mwili wake ambayo hakuwa anayaelewa. Kwanza alianza kuwa ni mtu anayekuwa anahisi uvivu sana na mara kadhaa alianza kuwa anasumbuliwa na kizunguzungu ambacho kila mara alipokuwa anamweleza Elias aliishia kuambiwa ajitahidi kunywa maji mengi yatamsaidia.

Amina pia alianza kubagua vyakula, mara nyingi alikuwa anajikuta anashindwa kula wali na badala yake akawa anakula ugali tu. Jambo hilo hakuwa analielewa kabisa kwani kiuhalisia Amina alikuwa anajifahamu sana ya kuwa anapenda sana wali kuliko ugali, sasa vipi mara hiyo aanze kukataa kula wali na badala yake apende kula ugali tu, Hakuelewa.

Ukiachana na yote hayo Amina alianza kuwa mtu wa kuhisi kichefu chefu sana kilichompelekea awe anatapika mara kwa mara kitu kilichomfanya ahisi kuwa atakuwa anaumwa sana hivyo akaomba ruhusa ya kwenda hospitali akapime ili ajue shida ni nini hasa iliyokuwa inamsumbua.

“Tumekupima vipimo kadhaa na tumegundua kuwa wewe ni mjamzito" Daktari alimueleza Amina ambae hakutaka kuamini alichokisikia,

“Dokta unasema? Mimi nina nini? Mimba!!!! Acha basi kunitania dokta” Amina aliuliza mfululizo kutaka apatiwe majibu aliyoyahitaji

“Ndio vipimo vinavyoonesha binti yangu, nadhani huu ni muda wa kutulia na kujipanga ujue utailea vipi hiyo mimba, baba wa mtoto si unamfahamu?” Daktari alimalizia kwa kuuliza swali ambalo Amina aliliona ni kama anaoneshwa dharau hivi.

“Unamaanisha nini kuniuliza kama baba wa mtoto namfahamu? Au unahisi mimi ni Kahaba sio?” Amina alimuuliza daktari kwa jazba

“Hapana sio hivyo nili............”

“Nyamaza huko usije kunivuruga zaidi, eti baba wa mtoto namfahamu?!! Kwa kunionaje labda, huo udaktari wako usikupe haki ya kujaji maisha ya wenzako kirahisi rahisi hivyo" Amina aliongea kwa hasira sana kisha akatoka ndani ya chumba cha daktari akiwa na hasira sana.

Hasira zile hazikuwa ni hasira kwa ajili ya daktari yule bali hasira zile zilikuwa ni hasira dhidi yake. Amina alihisi kujichukia kwa uzembe alioufanya wa kuruhusu kubeba mimba hali ya kuwa anajijua yeye bado ni mwanafunzi.

“Ooh!! Mungu wangu nitaanzia wapi kumweleza taarifa hizi Elias hadi anielewe" Amina aliwaza bila kupata majibu, akawaza hata kama atawaza sana hakuna kitakachobadilika hivyo palikua na ulazima wa kumfuata Elias na kumueleza hali halisi ili aamue yeye mwenyewe ni nini cha kufanya.

“Mpenzi wangu mbona leo unaonekana kama haupo sawa" Elias alimuuliza Amina baada ya kumuona yupo kimya sana.

Tayari Amina alikuwa ameshamuomba Elias wakutane mahala wazungumzo lakini tangu wakutane Amina alikuwa kimya tu asije cha kuongea.

“Mmmh!! Unasema" Amina aliuliza kana kwamba hakumsikia Elias alichoongea

“Nakuuliza hivi mpenzi wangu..... Upo sawa kweli? Nakuona upo kimya sana"

“Aanh!! Eti eeh nipo kimya sana"

“Ndio upo kimya sana hadi unanitisha niambie shida nini Amina wangu"

“Elias mimi ni mjamzito" Amina aliona aongee moja kwa moja kilichomfanya amuite Elias pale kwani alikuwa anakosa kabisa maneno sahihi ya kumueleza.

“Wewe ni mjamzito,........Amina unamaanisha nini kusema hivyo?!!” Elias aliuliza

“Nina mimba yako Elia"

“Mimba yangu?!! Hebu kuwa siriazi bhana, hiyo mimba iko wapi hadi useme ni ya kwangu"

“Swali gani hilo sasa Elia, mimba si ipo tumboni kwangu, nitaibebea wapi unadhani kama sio tumboni kwangu”

“Aanh kumbe!!! Sasa kama mimba ipo tumboni kwako unauhakika gani ni ya kwangu?” Elias alimuuliza Amina swali ambalo hakulielewa

“Unamaana gani kuniuliza hivyo Elia"

“Nina maana gani? Huelewi? Au ndio unajitoa akili tu hapa, unadhani nitaamini vipi kuwa hiyo mimba ni ya kwangu wakati upo nayo wewe Amina” Elias aliongea maneno yaliyomfanya Amina akose cha kuongea, akabaki anamtazama kwa muda Elias ambae alionekana kubadilika sana, hakuwa Elias yule tena wa dakika kumi zilizopita kwani Elias huyu alikuwa na sura Tofauti kabisa, sura yenye ndita na iliyoonekana kuwa na hasira sana.

“Ndio unataka kusema hii mimba nimejipachika mwenyewe au?” Amina alimuuliza Elias

“Hayo umeyasema wewe sasa, hebu fikiria hata ungekuwa wewe ungeikubali wakati unajua kabisa mpenzi wako hajatulia" Elias aliongea maneno ambayo yalimchanganya zaidi Amina

“Unamaanisha nini kusema sijatulia?”

“Usichokielewa nini hapa, kama kweli ungekuwa umetulia ungekubali kutoka na mimi wakati unajua nilikua rafiki wa mwanaume wako?....... Aya tuachane na hayo labda nikuulize swali moja tu kama kweli uliweza kumsaliti mshkaji wangu kwangu ni kipi kitakachokufanya ushindwe kunisaliti mimi kwa watu wengine huko? Nijibu"

Amina kusikia vile aliishiwa nguvu kabisa, na taratibu alijikuta anaanza kukaa chini na kuanza kulia. Alijikuta anajutia maamuzi yake ya kuwa na Elias. Ni kweli alikuwa ameachana na Gift lakini kutoka na Elias kimapenzi hakuwahi kuwaza kama kutakuja kumuadhibu hivyo,

“Naomba uniambie Elia kama hii mimba umeikataa au vipi ili nijue moja" Amina alimuuliza Elias huku akiwa analia,

“Hapana, umenielewa vibaya, sio kwamba nimeikataa hiyo mimba lakini nachojaribu kukueleza hapa ni kuwa fanya kuipeleka hiyo mimba kwa baba yake halali, tatizo haujatulia Amina nitakuamini vipi mimi" Elias alimaliza kuongea kisha akaondoka zake huku akimweleza Amina aache mazoea naye kabisa.

Amina alijikuta anaanza kulia kama mtoto mdogo. Hakutaka kuamini kama Elias ndiye aliyembadilikia kiasi kile. Hakujua ni nini afanye tena baada ya hapo. Wazo kubwa kwa muda ule lililokuwa limeitawala akili yake ni kuitoa ile mimba, hakutaka kulea kiumbe kisichokuwa na baba hivyo alihitaji kuchukua maamuzi ya haraka sana kutimiza lengo lake hilo,

“Sidhani kama nitaweza kufanya suala hili peke yangu nitahitaji msaada wa nje" Amina aliwaza, tayari alikuwa ameshafikiria jambo la kufanya. Hivyo aliamua kunyanyuka pale chini alipokuwa amekaa na kisha akajifuta machozi yake kisha akaanza kutembea kuelekea ofisini kwa mwalimu wa zamu.

Alipofika alimuomba mwalimu yule simu yake apige nyumbani kwao. Mwalimu hakumnyima kwani hiyo nayo ilikua ni kazi yake kuwasaidia wanafunzi wawasiliane na wazazi wao. Amina akapiga simu ile ambayo ilianza kusikika ikiita upande wa pili,Amina akaamua kusogea pembeni ili kuepusha mwalimu asisikie atakachokiongea,

“Halloo!!!” Niliongea baada ya kupokea ile simu

“Gift, ni wewe?” Amina aliniuliza,sikuwa na haja ya kuuliza ni nani anayeniuliza kwani sauti yake nilikuwa naifahamu sana.

“Ndio ni mimi Amina niambie" Amina kusikia nimemjibu alianza kulia kilio ambacho sikukielewa japo kiliniumiza na mimi pia kwani sikupenda kabisa kusikia Amina akiwa na huzuni, furaha ndicho kitu pekee nilichohitaji awe nacho Amina wangu

“Amina mbona hivyo unashida gani” Nilimuuliza Amina

“Giiih naomba unisaidie" Amina aliongea huku akiwa anaendelea kulia

“Nambie Amina niambie chochote kile nitakusaidia.......” Nilimweleza Amina kwa kujiamini sana kwani sikupenda kumuona Amina akiwa na shida au tatizo lolote lile

“Naogopa sana Gift sijui hata nifanye nini yani"

“Huna haja ya kuogopa Amina wee nieleze tu sawa"

“Aya sawa, Giiih nina mimba mwenzio na nina hitaji kuitoa"

Amina alinieleza maneno ambayo yaliupatia ganzi moyo wangu nikajikuta namuuliza bila kutarajia

“Mimba?!! Ya nani Amina?!! Elias au?!!”


ITAENDELEA.

WhatsApp Number; 0625000557

#KAKAMKUBWA.
 
MPENZI WANGU AMINA........(08)

Imeandikwa Na SALUM KALASE

Mawasiliano: 0625000557

SEHEMU YA NANE.

“Mbona una maswali mengi hivyo, jibu ni moja tu hapa unanisaidia au?” Amina alionekana kukasilishwa na maswali yangu

“Ni lazima nikusaidie Amina niambie nachopaswa kufanya sasa” Ilibidi nimkubalie kwani sikutaka kumkwaza.

Amina aliposikia nimemkubalia ombi lake alinipatia mpango wake wa jinsi alivyokuwa amewaza. Nilimsikiliza kwa makini kisha tukakubaliana mpango huo tutautimiza kuanzia siku inayofuata aniache kwanza nijiandae kwa ajili ya zoezi hilo lililokuwa mbele yetu. Tukakubaliana na kuagana. Amina akakata simu.

Baada ya Amina kukata simu nilijikuta naanza kupata maswali kadhaa kichwani mwangu yasiyokuwa na majibu. Kubwa zaidi nilichojiuliza ni kuhusu huo ujauzito wa Amina, niliwaza, kama ni kweli Amina ana mimba ni kwa nini anataka kuitoa? Na je baba wa mtoto ni nani?!! Mimi au Elias, nilikosa majibu. hivyo ikanibidi niachane na mawazo yale ambayo nilijua fika hata nikiwaza vipi siwezi kupata majibu yake.

Jambo la kwanza nililowaza kufanya ni kwenda duka la dawa lililokuwa karibu na nyumbani kwetu, huko nilikwenda na kuulizia dawa za kutolea mimba,

“Mimba mnayotaka kuitoa ni ya miezi mingapi" Dada aliyekuwa ndani ya lile duka aliniuliza

“Umri?!! Nadhani ni miezi miwili sasa" Nilimjibu

“Una uhakika ni ya miezi miwili” Yule dada aliniuliza

“Ndio nina uhakika" Nilimkubalia japo sikuwa na uhakika, ilibidi nimuongopee ili kutimiza lengo langu lililokuwa limenipeleka pale dukani.

Yule dada aliniomba elfu arobaini kwa ajili ya dawa nikampatia, kisha akanielekeza matumizi ya zile dawa ambayo niliyasikiliza kwa umakini sana nisije kuyakosea wakati wa zoezi lile la utoaji wa mimba.

“Najua itakuwa ni kazi sana ila usiogope, kila kitu kitakuwa sawa" Yule dada alimalizia maelezo yake kwa kunieleza kauli hiyo ambayo sikuizingatia sana.

Nilirudi nyumbani, moja kwa moja hadi kwenye kibubu changu nikakivunja na kisha nikachukua pesa zote nilizokuwa nimezitunza. Nilihitaji kuondoka jioni ile ile ili kesho yake nikafanye mpango wa kumchukua Amina shuleni. Baada ya kuwa nimeshajiandaa niliondoka nyumbani bila hata kuaga, kwani nilijua sitakua na majibu sahihi ya kuwaeleza wazazi wangu watakaponiuliza nakokwenda.

Safari yangu ya kutoka Kahama iliishia Maganzo Shinyanga ambapo nilichukua chumba cha kulala kwa lengo la kulala usiku ule hadi kesho yake asubuhi.

Asubuhi ilipofika, nilikwenda moja kwa moja hadi kituo cha maboda boda nikakodi boda moja kwa lengo la kunipeleka hospitali ya Mwadui iliyokuwa inapatikana ndani ya kijiji cha Mwadui ambacho chote kiujumla kilikuwa kimezungushiwa uzio nadhani ni kwa sababu za kiusalama za kulinda madini ya Almasi yanayopatikana pale.

Ilikuwa ni safari ya zaidi ya dakika ishirini kwa boda kutoka hapo Maganzo hadi Mwadui hivyo malipo yake yalikuwa juu kidogo ambayo hayakunipa shida kuyalipa,

“Kuna mtu tunakwenda kumchukua na kurudi nae hapa mjini lakini hatakiwi kuonekana wakati tunatoka nae humo ndani" Nilimweleza yule boda.

“Usijali kaka hizi ndio kazi zetu zinazotuweka hapa mjini shaka Ondoa kabisa" Yule boda alinitoa wasi wasi.

Mpango wetu mimi na Amina ulikuwa ni kwenda kumtorosha hospitali Amina ambako atakwenda kwa kisingizio cha kuwa anakwenda kupima afya yake kwani bado anajihisi kuumwa.

Kwa kuwa tulikuwa na lengo la kumtorosha Amina, yule boda alinishauri tupitie njia za siri kwenda na kurudi ili kuepusha mambo ya kuonekana na walinzi waliokuwa wanalilinda geti kuu la kijiji cha Mwadui, nikamkubalia. Safari yetu ilianza mida ya saa mbili asubuhi, yule boda alikuwa anaijua kazi yake kweli kwani hatukupata shida kabisa kuingia Mwadui hadi tunafika hospitali hakuna kipingamizi chochote kile tulichokutana nacho njiani.

Ile kufika hospitalini, tulimkuta Amina akiwa anatusubiria,

“Mbona umechelewa hivyo” Amina aliniuliza

“Usafiri ulikuwa wa shida sana” Nilimjibu

“Mzigo wangu uko wapi kwanza" Amina aliniuliza, nikampatia begi nililokuwa nalo akalichukua na kwenda nalo ndani ya hospitali huku akitutaka tumsubirie pale nje ya kuwa atarudi baada ya muda.

Ndani ya lile begi kulikuwa na nguo za nyumbani ambazo nilimnunulia kwa lengo la kubadilisha. Amina alibadilisha nguo zake za shule na kuziweka ndani ya lile begi alilokwenda nalo mule ndani ya hospitali kisha akavaa zile nguo nilizokuwa nimemnunulia. Baada ya kuhakikisha yupo tayari alitoka nje na safari ya kurudi mjini ikaanza.

Safari yetu ya kurudi mjini pia haikuwa na changamoto yoyote ile kwani yule bodaboda alitumia njia ile ile tuliyokuja nayo mwanzo ambayo ilionekana kuwa na usalama. Tulifika maganzo mida ya saa nne za asubuhi. Moja kwa moja tukaelekea kwenye lodge niliyokuwa nimefikia huko tulifika na kuagiza chai kwanza kabla ya kuanza mambo mengine.

Nilimweleza Amina kuwa nimeshauriwa dawa zile azitumie usiku ndio muda mzuri kwani hadi kufikia asubuhi kesho yake kila kitu kitakuwa kimeshamalizika, akanielewa. Nikamweleza ila kabla ya yote hayo kuna vitu nilihitaji kuzungumza nae

“Sidhani kama nitakuwa nina majibu ya maswali yako unayotaka kuniuliza” Amina alinieleza baada ya kusikia nataka kuzungumza nae

“Lakini huoni kama nina haki ya kujua kila kitu kwanza kabla ya yote?" Nilimuuliza

“Itakusaidia nini hata kama ukishajua"

“Haya basi sawa naomba unieleze tu jambo moja. ....... Mimba hii tunayoitoa ni ya nani?!!”

Amina alinitazama kwa muda kabla hajanijibu,

“Hivi kweli katika maswali yako yote hilo ndilo umeona ni swali la msingi sana kulijua jibu lake?”

“Ndio nadhani napaswa kujua hata jibu ya hilo swali langu moja au nakosea?"

“Aya sawa kwa kuwa umetaka kujua....... Hii mimba ni ya Elias na sio yako kama unavyowaza" Amina alinijibu, jibu lililonifanya nijikute nashusha pumzi nzito sana, ni kama nilikuwa nashukuru Mungu hivi, kiukweli sikuwa nataka kushiriki kukitoa kiumbe changu kwa Amina.

“Mbona kama umefurahi kusikia mimba hii sio yako?” Amina aliniuliza

“Hapana hata sijafurahia ila nawaza ni kwanini umeamua kuchukua maamuzi hayo ya kuitoa mimba hiyo" Nilimjibu kwa swali ambalo nilijua hatoweza kulijibu

“Nadhani swali lako nimeshalijibu, hayo mengine niachie mwenyewe” Amina alinijibu kisha akapanda kitandani kwa lengo la kulala, sikutaka kumzuia kwa sababu sikuwa na kitu kingine cha kuongea naye zaidi. Kitu pekee kilichokuwa kimebakia mbele yetu ni kusubiria ifike jioni kwa ajili ya kuanza zoezi letu la kuitoa ile mimba.

“Amina..... Amina....... amka basi muda umeshakwenda sana" Nilimuamsha Amina ambae alionekana bado kuwa na usingizi sana

“Mmmh unasema? Kwani usiku umeshafika Giih!!” Amina aliniuliza

“Hapana, amka ukaoge, ili twende tukale mapema tuna mambo mengi ya kufanya baadae” Nilimweleza

Amina kusikia vile aliamka, akaenda kuoga bafuni na baada ya muda akarudi chumbani na kubadilisha nguo kisha tukatoka pamoja nje, huko tulikwenda na kutafuta chakula tukala kisha tukaanza kupiga stori za hapa na pale. Amina aliniuliza kuhusu wazazi nyumbani na mimi nilimuulizia habari za masomo shuleni, hatukuongelea kabisa habari za mahusiano, ni kama tulichora mstari wa mazungumzo yetu.

“Nadhani turudi Lodge sasa" Nilimueleza Amina ambae nilimuona ameshaanza kunywea, nadhani woga ulikuwa umeshaanza kumuingia. Hata mie nilikuwa na hofu lakini sikutaka kuionesha kwa Amina, nilihitaji kuwa jasiri ili kumfanya Amina awe na amani.

Tulifika lodge, tukaingia ndani ya chumba chetu kisha nikatoa mashuka yote kitandani yaliyokuwa yametandikwa kisha nikatandika shuka langu nililokuwa nimekwenda nalo.

“Chukua hizi nguo ukavae huko chooni" Nilimpatia vitenge Amina ili akajifunge kwani alipaswa kubadilisha kabisa zile nguo alizokuwa amezivaa ili asije kuzichafua na damu wakati mimba inapotoka.

Amina alikwenda bafuni kubadilisha nguo, baada ya muda akarudi akiwa tayari. Nilimtazama kwa kumtamani sana, vazi lile la kitenge lilinipagawisha lakini sikutaka kuziruhusu hisia zile zinichanganye,kwani nilijua fika tukio lililokuwa mbele yetu halikuwa tukio la kuzihitaji hisia hizo.

“Naomba uketi kitandani, Kuna vidonge hapa nahitaji kukuwekea huko chini" Nilimueleza Amina ambae hakunielewa ninachokimaanisha,

“Vidonge? Vidonge gani hivyo unahitaji kuniwekea?” Amina aliniuliza

“Hivi hapa, nimeelekezwa nikuwekee huko chini kati kati ya mapaja yako na vingine utakaa navyo mdomoni" Nilimueleza

“Hapana, siwezi kukubali, hata mimi mwenyewe naweza kujiwekea naviomba nikajiwekee mwenywe kikubwa wewe nielekeze namna ya kufanya" Amina alionekana kumaanisha alichokiongea, sikutaka kubishana nae, nikampatia vile vidonge ili nianze kumuelekeza namna ya kuvitumia.

Amina alivipokea lakini kabla sijaanza kumuelekeza chochote kile simu yangu ilianza kuita, ikabidi niitazame. Elias alikuwa ananipigia, Amina naye aliliona hilo kwani alilisoma jina la mpigaji kwenye kioo cha simu yangu hivyo tukabaki tunatazamana, kichwani niliwaza nisiipokee simu ile lakini vidole vya mikono yangu vilinisaliti, nikajikuta naipokea ile simu,

“Oya Giih Amina ametoroka shule na anatafutwa kinoma, vipi labda anaweza kuwa amerudi nyumbani?" Elias aliniuliza

“Amina ametoroka?!! Kwa sababu gani?” Nilijifanya kama sijui kinachoendelea

“Acha tu Giih najuta kiukweli najuta sana kwa niliyomfanyia Amina"

“Unajuta?! Mbona sikuelewi, kwani umemfanya nini Amina eenh!!”

“Ni mambo yetu binafsi lakini kama utamuona Amina mwambie anisamehe sana yalikuwa ni masihala tu sikutegemea kama atachukua maamuzi haya" Elias aliongea. Amina muda wote huo alikua anatusikiliza tu, na alionekana kama kutaka kuongea jambo lakini alishindwa.

“Sawa nitamueleza kila kitu kama atakuja nyumbani maana hata sie bado hatujapewa taarifa kama Amina ametoroka shule"

“Ok sawa mwanangu naomba unisaidie sana kwa hilo najuta sana hapa nilipo"

“Sawa usiwaze nitafikisha ujumbe wako" Elias akakata simu, Amina akasimama kutoka pale kitandani alipokuwa ameketi kisha akaanza kuzunguka mule chumbani kama mtu aliyechanganyikiwa hivi, akawa anakaa mara anasimama bila kuzungumza chochote,

“Vipi Amina mbona sikuelewi?” Nilimuuliza

“Nadhani sikupaswa kuwa hapa Gift"

“Unamaanisha nini kusema hivyo Amina mbona sikuelewi"

“Kila kitu tunachokifanya hapa tunakosea sana Gift, Hauoni kama nitakuwa namkosea baba wa hiki kiumbe nachotaka kukitoa?” Amina aliniuliza

“Unamkosea vipi? Hebu nieleweshe”

“Gift usichokielewa nini hapa? Hauoni kama Elias bado anamuhitaji mtoto wake, alafu mimi nipo hapa nataka kumtoa?.......... Aaaanh!!! Kweli mimi ni mjinga sana" Amina aliongea maneno ambayo yalinichanganya kidogo

“Amina..... Hebu tulia kwanza, mbona nakuwa kama sikuelewi, inamaana unataka kusema unataka kuhairisha kuitoa hiyo mimba ama!!!”

“Ndio, Gift siwezi kuitoa mimba hii hali ya kuwa baba yake hajaniruhusu" Amina alinijibu kwa ujasiri, macho yake yalionesha alichokuwa anakiongea alikuwa amekimaanisha, nguvu ziliniisha kwani sikujua ninapaswa kufanya nini kwa muda ule.

ITAENDELEA

WhatsApp Number:0625000557

#KAKAMKUBWA
 
MPENZI WANGU AMINA........(10)

Imeandikwa Na SALUM KALASE

Mawasiliano: 0625000557

SEHEMU YA KUMI.

Naikumbuka vizuri sana ile mechi yangu ya kwanza kucheza na Koleta, mechi ambayo ilihitaji vipindi vitatu vyenye heka heka za kutosha, nakiri kusema Koleta alikuwa amenipania sana siku ile kwani hakuniachia hata sekunde moja ya kupumzika, muda wote alitaka nimpelekee mashambulizi kwa kumpigia pasi ndefu tu tena za haraka haraka, hakutaka kabisa mambo ya pasi fupi fupi kwani alidai zinaupozesha mchezo na kufanya mechi iboe. Kiukweli naweza sema kwenye mechi zangu bora kuwahi kucheza siwezi itoa mechi ile mimi na Koleta tulipocheza kwa mara ya kwanza.

“Baby naomba usiende kunisaliti basi huko shuleni kwenu" Koleta alinieleza baada ya mechi yetu kuisha. Sikutaka kumjibu chochote kile kwani nilihofia kumpatia ahadi ambayo nilijua fika nisingeweza kuilinda.

Kesho yake asubuhi sana niliamka na kuanza safari ya kurudi shule. Nakumbuka nilifika shule mida ya saa nane mchana, nikapokelewa vizuri na mwalimu aliyenieleza niende darasani kwani wanafunzi wenzangu walikuwa bado hawajamaliza masomo yao ya siku ile, nikamtii na nikaianza safari yangu ya kuelekea darasani.

Nilifika darasani kwetu na kubisha hodi, mwalimu aliyekuwamo darasani alinipokea na kunitaka niende nikakae kwenye siti yangu. Nilielekea hadi kwenye siti yangu na kumkuta Elias akiwa amekaa pale, nilifika na kumtazama, sikutaka kumsemesha chochote kile. Elias alielewa nilichokuwa nakihitaji hivyo alinyanyuka na kunipisha kwenye kiti changu, nikakaa.

Nilimtazama Amina aliyekuwa pembeni yangu kama sijamuona kwani sikumsalimia, na hadi kipindi kinaisha hatukuwa tumezungumza chochote kile mimi na Amina ambae aliamua kuondoka tu mara baada ya kipindi kile kuisha. Nikamuona Elias anamkimbilia Amina, kisha akamshika mkono na wakaamua kuondoka pamoja. Kitendo kile kwa kiasi fulani kikanitia wivu kiasi moyoni mwangu japo nilijitahidi kuupotezea wivu ule.

Maisha yangu shuleni tangu nimerudi hayakuwa sawa tena kama mwanzoni kwani watu wawili wa muhimu sana, Amina na Elias wote kwa pamoja nilikuwa sisemezani nao. Amina aliamua kukata mawasiliano na mimi kabisa kwani aliamua kubadili hata siti ya darasani aliyokuwa anakaa mwanzoni ilimradi tu awe mbali na mimi.

Elias pia hakutaka mazoea na mimi, kwani alianza kwa kuhama bweni tulilokuwa tunaishi pamoja na kuhamia bweni jingine, kisha akamshawishi Amina atoke pale alipokuwa anaketi na mimi darasani na badala yake ahamie kwake na kweli Amina alifanya hivyo kama nilivyosema hapo mwanzo.

Suala la mimi kutozungumza nao halikuniumiza hata kidogo, ila kilichokuwa kinanitesa nafsi yangu ni ule ukaribu waliokuwa nao, ni kama nilikuwa najitazama mimi kwa Elias nilivyokuwa na Amina kabla hatujaachana, yaani Elias alijua fika kuuvaa uhalisia wangu kwa Amina kwani alikuwa anafanya vile vile nilivyokuwa nafanya mimi na Amina kipindi tupo pamoja. Kiukweli hali ile ilikuwa inanitesa sana kiasi cha kufanya nishindwe kuielekeza akili yangu kwenye masomo kwani muda wote nilikuwa najikuta namuwaza tu Amina bila kutaka.

Mitihani iliwadia tukafanya, sijui wenzangu waliifanyaje lakini kwa upande wangu mitihani ile niliifanya kutimiza wajibu tu, kwani mambo mengi nilikuwa sijasoma na hata nilipotaka kusoma akili yangu ilishindwa kwa sababu ya mawazo juu ya Amina wangu kuwa na Elias.

Tulimaliza kufanya mitihani yetu ya kidato cha nne, tukaruhusiwa kurudi nyumbani, ilikuwa ni shangwe sana kwa watu wengi ikiwemo na mimi ambae nilifurahia kwa mambo makuu mawili. Moja, kumaliza kidato cha nne kwa upande wangu haikuwa rahisi kwa sababu ya heka heka nyingi nilizozipitia lakini Mungu alisimama na kuniwezesha nimalize. Mbili, nadhani hii sababu ya pili ndiyo iliyonipatia furaha zaidi kwani Amina na mimi tulikuwa tunarudi nyumbani Kahama na Elias alikuwa anakwenda kwao Kagera, yaani kwa maana hiyo ni kama kusema Amina na Elias walikuwa wanaachana bila kuambiana kuwa wameachana.

Mimi na Amina tulirudi nyumbani, tukafikia kwetu ambapo ndipo baba yangu na mama yake Amina walipoelewana kuwa tutakuwa tunaishi hapo. Tofauti na mimi niliyeonekana kuwa na furaha ya kurudi nyumbani, Amina yeye alionekana kuwa ni mtu wa mawazo sana na alipenda kujitenga peke yake muda wote. Amina hakuwa tena mtu aliyependa kuongea na hakuwa mtu wa kucheka ama kufurahia hata kama litokee jambo gani la kufurahusha, yeye hakufurahia.

Hali ile kwa namna fulani ilikuwa inanitesa hata mimi ambae nilikuwa namshuhudia mara nyingi. Baba na mama wao muda mwingi walikuwa wanautumia makazini kwao, Lakini sikutaka kumuuliza kwani ni kama nilikuwa nimeshajipatia majibu yangu tayari.

Kwanza nilihisi Amina anaweza kuwa na mawazo juu ya ujauzito alionao ya kuwa ataanza vipi kuwaeleza wazazi wetu. Pia niliwaza huenda Amina akawa ana mawazo juu ya mpenzi wake Elias ambae yupo mbali nae kwa muda ule, hivyo niliamua kumuacha adili na mambo yake mwenyewe hadi pale atakapotaka kunieleza yeye mwenyewe changamoto inayomkabili tushauriane.

Mie nilianza kuwa bize na biashara ya mchele ambayo nilikuwa nafundishwa kuifanya kwa ukaribu sana na Koleta ambae aliniahidi kunielekeza biashara hiyo jinsi inavyofanywa. Koleta alinielekeza kila hatua aliyoifahamu, kwani alihitaji niifahamu vyema biashara ile ambayo nilionesha nia ya kutaka kuijua.

“Mume wangu, una kichwa cha kuelewa sana mambo haraka" Koleta alinieleza, nikabaki namtazama tu bila kuongea chochote kile. Ni kama sikuwa nataka Koleta aniite vile lakini nilikuwa nashindwa kumueleza ukweli kwani alionekana kunipenda sana. Kwa upande wangu Koleta nilimuona kama mshkaji wangu tu hata ile kulala nae kwangu niliona kama bahati mbaya na sikutaka kurudia tena kufanya nae jambo hilo.

“Giih, leo naomba twende ukalale kwangu basi nimekumisi sana mpenzi wangu" Koleta aliniomba

“Mmmmh!!! Sidhani kama leo itawezekana Koleta" Nilimjibu

“Kwanini sasa isiwezekane, au ushapata mwanamke mwingine huko nje"

“Hapana sio hivyo, ni kwamba nyumbani leo nipo mwenyewe, wazazi wangu ameenda safari itabidi niilinde nyumba haiwezi kubaki peke yake" Ilibidi nimdanganye Koleta kwani sikutaka kwenda nae kwake, kwa kuhofia kitakachokwenda kutokea huko baada ya kwenda.

Kishingo upande Koleta alinikubalia, tukaagana nikarudi nyumbani. Kufika nyumbani nilipitiliza chumbani kwangu nikaoga na kubadili nguo kabla ya kurudi sebuleni kwa ajili ya kula chakula cha usiku.

Nilivyofika sebuleni sikukuta chakula mezani, ikabidi nielekee jikoni kutazama huko nako sikukuta chakula wala dalili za chakula kuwa kilipikwa mahali pale. Nikawaza kwanini Amina hajapika na wakati hiyo haikuwa kawaida yake kabisa, ni kweli hatukuwa na stori sana lakini Amina hakuwahi hata mara moja kuacha kunipikia hivyo nikawaza niende chumbani kwake nikamtazame kujua ni nini kinachomsibu hadi ashindwe kunipikia chakula.

“We Amina" Nilibisha hodi huku nikiwa naliita jina la Amina ambae hakuwa akiniitikia lakini sikuacha kwani nilihisi huenda yakawa ni mapozi yake tu ya kutokutaka kuzungumza na mimi.

Nilijikuta nabisha hodi kwa zaidi ya dakika tano bila majibu hivyo nikaamua najaribu kuufungua mlango kuona kama upo wazi, mlango ukafunguka nilipoujaribu kuufungua, hivyo nikausukuma na kuingia ndani ya chumba cha Amina.

Sikutaka kuamini nilichokishuhudia mule ndani, Amina alikuwa amelala chini sakafuni na alikuwa anatokwa na mapovu mengi mdomoni mwake.

“Oooh Mungu wangu!!!” Nilijikuta najisemea kwa nguvu kisha nikamfuata Amina pale alipokuwa amejilaza.

Sikutaka kupoteza hata sekunde moja tena, akili yangu ilikuwa inawaza kumsaidia Amina ambae nilijua fika alikuwa na shida. Nilimbeba mikononi mwangu na kuanza kutoka nae nje ambako nilifika na kuita boda haraka ambae Nilimweleza atupeleke kituo cha afya kilichokuwa karibu na pale tulipokuwa tunaishi.

Tulifika kwenye Dispensary moja ya karibu na nyumbani ambapo tulipokelewa haraka,

“Ana shida gani huyu?” daktari aliniuliza kabla ya kuanza huduma, nikamweleza

“Nadhani amekunywa hivi vidonge( huku nikimuonesha yule daktari vile vidonge nilivyokuwa navyo) kwani nimevikuta chumbani kwake pale chini alipokuwa amelala”

“Ok sawa, tusubiri hapo tukamsaidie ndugu yako" Yule daktari alinieleza, ikabidi nielekee kwenye benchi lililokuwa pale Dispensary kisha nikaketi.

Siti haikukalika hata kidogo kwani muda wote nilikuwa na mawazo juu ya uhai wa Amina ambae nilikuwa nahisi huenda alikuwa anataka kujiua. Nikiwa ni mwingi wa mawazo bado ndipo nikakumbuka kuwa kulikuwa na kikaratasi nilichokichukua kutoka kwenye mikono ya Amina wakati namchukua chumbani kwake hivyo nikakitoa na kukifunua kwa lengo la kukisoma.

“Najua unaweza kunichukua kwa haya nitakayokueleza lakini huu ndio uhalisia wenyewe. Mimi bado ni kijana mdogo sana kuwa baba, na nina ndoto nyingi za kutimiza ambazo naona ninaweza shindwa kuzitimiza kwa kujifanya baba bora kwa kiumbe nisichokihitaji kwa sasa. Ni hivi Amina, hutonisikia nikikutafuta tena katika maisha yako kwahiyo fanya namna utoe hiyo mimba, na uendelee na maisha yako kama kawaida kuliko kung'ang'ania uhalisia wa mambo usiokuwepo.
Kuwa na maisha mema”

Nilimaliza kusoma barua ile iliyonitia hasira kwani nilijua fika ni barua iliyokuwa imetoka kwa Elias.

ITAENDELEA

#KAKAMKUBWA.
 
Back
Top Bottom