Tupio la XXXVI – Mwanzo mpya
Ilipoishia…
“Zai, kwangu siyo mbali kutoka hapa, nimeona ni vyema nikabe nafasi mapema maana siku kama leo magari hujaa sana hapa kiasi cha kufanya mtu uweze kukosa nafasi nzuri ya kuegesha gari…”
Tukawa sasa tunaelekea usawa wa nyumbani kwangu uswahilini.
Sasa endelea…
“Lakini tusikae muda mrefu muda umeenda sana halafu nyumbani sijwataarifu kuwa nitachelewa…”
Zai alitahadharisha pale wakati tumeshakaribia kabisa kuingia ghettoni.
“Karibu sana Zai, hapa ndipo ninapojifichaga usiku…” Nilimkaribisha.
Nilikuwa naishi kwenye chumba na sebule, lakini kilikuwa chumba kilichosheheni kila aina ya samani vyenye thamani ambavyo kijana wa kisasa angependa kuweka kwenye chumba chake cha ukubwa ule. Sebule na chumba vilikuwa na ukubwa sawa tu wa futi tisa kwa kumi.
“Pazuri jamani…” Alipasifia huku akifanya ukaguzi ule wa kike kuangalia kama kuna dalili ya uwepo wa mtu wa jinsia yake anayeishi hapo. Nilimuachia nafasi nikaingia ndani mara moja na kutoa shati ililovaa na nikavaa fulana nyepesi nikarudi sebuleni.
“Enhe Zai, naona umeanzisha bifu na Emmy!” Nilianza uchokozi
“Emmy naye kazidi, kila bwana mwenye hela anamtaka yeye, atakufa kwa maradhi asipojiangalia…” Zai alisema.
Hapo kwangu kulikuwa na makochi mawili ya mtu mmoja mmoja, lakini yalikuwa mazuri maana niliyarithi kutoka kwa wazazi. Hivyo tulikaa kwa kuangaliana, runginga ilikuwa inaendelea na vipindi vya miziki.
“Zai, jisikie upo nyumbani, unakaribishwa muda wowote, hii ndio ‘sapraiz’ niliyokuambia…” Nilimuambia huku nikiinuka na kueleke kwenye jokofu kuangalia vinywaji…
“Najuwa muda huu tumbo limejaa, lakini kinywaji hiki hakitokosa nafasi tumboni mwako…” Nilisema huku nikimmiminia kiasi tu mchanganyiko wa juisi ya nanasi na machunywa (ya dukani) kwenye glasi nami nikijimiminia pia.
“Na tunywe kwa ajili ya mwanzo mpya!” nilichagiza kisha nikainua glass ili tugonganishe (cheers)
“Kwa mwanzo mpya…!” Kisha naye akainua glass yake tukagonganisha kwa kusogeleana tukiwa mkabala (opposite).
Nilipiga funda moja kisha nikachukuwa remote control na kuizima tv lakini nikawasha music system, nayo hii nilirithi nyumbani, ilikuwa ni sony music system yenye 5.1 speakers. Nilifungulia kwa sauti ya chini mziki heavy country ya Don Williams “I don’t wanna love you”
“Aaaaah kumbe na wewe unapenda Country, hata Hemedi alikuwa anapenda…” Zai alidakia alivyosikia melody za wimbo huo wa taratiibu wenye kubembeleza.
Mimi sasa nikawa naufuatisha maneno ya ule wimbo nikasimama na kumfuata Zai nikampelekea mikono yangu yote miwili kuashiria nataka asimame, naye akanyoosha mkono mmoja nikaushika kama namvuta hivi, akasimama kisha wote tukaanza kurindika kwa mdundo wa ule mziki huku tukiwa tumesogeleana kabisa.
Zai kama nilivyosema awali alikuwa ni mtu wa kuvaa nguo za kujihifadhi, muda wote ana ushungi na nguo zinazoficha maungo yake, hivyo hadi muda huo ilikuwa sikuwahi kubahatika kumuona vizuri zaidi ya uso wake, sehemu kidogo ya mikono na miguu.
Wakati tunabembea kwa wimbo ule tulizidi kusogeleana kiasi cha miili kuanza kugusana na mapigo yangu ya moyo yakaanza kuongezeka kasi, nilijitahidi tusogee hadi kwenye switch ya kuzimia taa kisha nikazima taa yenye mwanga mkali nikawasha taa nyeusi (black fluorescent lamp) ambapo kwa macho ya kawaida huonekana kama rangi ya zambarau hususani inapoaikisi vitu vyenye rangi yeupe.
Mkono mmoja tukiwa tumeshikana, mkono wangu mwingine ukaanza utalii wa ndani sehemu za nyuma ya mwili wake kuanzia shingoni kushuka hadi kwenye milima ya Malkia wa Sheba. Hapo ndipo nilipogundua kuwa mawingu huziba nisione vizuri vilele vya milima hiyo, si wa shepu ile. Mnara ukaanza kusoma taratiibu na wakati huo wimbo ulikuwa tayari umeshabadilika, ‘Especially for you’ ndio ulikuwa unacheza…
Ilipofika kwenye ayah ii tulijikuta wote tunayafuatisha yale maneno huku tukiangaliana…
“I touch the texture of the state,
I felt for the good and I felft for the best,
But I never new what touch coul do, Until I was touched by you!”
Wimbo huo ulikuwa wa mwisho katika orodha hiyo na sikuweka auto replay, basi wimbo ulivyoisha kukawa na ukimya mle ndani, tukiwa bado tumesimama zero distance tukajikuta midomo yetu inagusana…
Tukawa tunafanya dry kiss pale yeye akiwa amenishika mkono mmoja begani na mwingine nyuma ya shingo yangu nami mikono yango yote mwili nilikuwa nimeshika vilele vya milima ya sheba na kuiminya minya kwa mahaba.
“Wait” Mara Zai akili ikarudi…
“Ngoja niwajulishe nyumbani kuwa sirudi, muda umeshaenda sana wasije wakaacha wazi..” Zai alisema huku akifuata mkoba wake ili achukue simu.
Kweli muda ulikuwa umeshaenda, saa tano na nusu ilikuwa inakaribia.
“Wajulishe kuwa uko na mpenzi mpya Alex kama ulivyomjulisha Emmy!” Nilimtania wakati ameanza kubonyeza simu ili apige.
“Hallo!, Aunt, sijafika nyumbani, nipo kwa Alex yule aliye nileta huko, nyumbani nitaenda kesho muda umeshaenda sana…” Waliongea mawili matatu kisha akakata simu.
Kumbe alianza kupiga simu kwa shangazi yake Kigamboni, du. Moyoni nikawa nashangilia, kutaraji kupata ladha ya aina yake. Sijawahi kuyafunua majuba!
“Halo, msiache mlango wazi, nipo Kigamboni kwa Aunt, nitakuja kesho…” sikusikia ya upande wa pili, Zai alikata simu. Muda wote mimi ilikuwa kimya huku nikitafakari cha kuanza kufanya.
“Umefanya jambo jema sana Zai, muda umeenda, nafasi ya kulala ipo, karibu sana.” Nilimshukuru kwa maamuzi yake.
“Zai, maisha ya ushwahilini haya, ngoja nikuandalie maji ukajimwagie, bafu lipo nje na muda huu wala hakuna foleni…” Nilisema huku nikichemsha maji kwenye jagi ili nichangaje na mengine apate kuoga maji ya uvuguvugu.
Nikaenda chumbani kumuandalia taulo, nikalitoa kabatini na kuliweka kwenye kitanda kisha nikatoka chumbani na kumuambia akajiandae kwa ajili ya kwenda kujimwagia maji.
Nilimsindikiza hadi bafuni nikiwa nimembebe kasha maalumu ambalo huwekea sabuni, dawa ya meno, mswaki ambapo nilimuwekea mswaki mpya ambao haujafunguliwa, wavu maalumu wa kujisugulia mgongoni na mazaga mengine yahusuyo maliwato kisha nikamwacha na kurudi chumbani.
Mara txt msg igaingia kwenye simu yangu ambayo niliweka katika hali ya mitetemo. Nilipoifungua nikakuta msg ya Mourine…
“I miss you handsome boy, Kesho jiandae kwa sebene lingine, G9t”
Ile text msg ikanifanya niyakumbuke mautundu yake, na muda huu nipo na Zaituni, nitalala naye hadi asubuhi, ilikuwa mara yangu ya kwanza kwa mimi kwa miaka mitano tangia nihamie nyumba ile kulala na mwanamke mle ndani, siku zote shida zangu namaliziaGa huko natoka Dar naenda Dar.
Wakati natafakari nimjibu nini Mourine text msg ikaingia tena…
“Alex, naomba niletee maji mengine…”
Nikawaza, ina maana lita 18 zote hazijamtosha hadi nimuongezee maji mengine! Oooh nikakumbuka huenda amefanya safari kubwa labda, basi nikachemsha fasta maji mengine kisha nikachanganya kwenye kindoo cha lita 10 nikampelekea.
Nilivyofika nikamwita kisha nikamwambia maji haya hapa ile nimenyanyua ndoo kwa mkono mmoja kumpatia naye akafungua mlango akiwa amejifunga taulo kisha akaniambia…
“Ingia Alex…”
Sikusita, nikaingia.
Nilipoangalia maji kwenye ile ndoo ya lita 20 yalikuwemo ya kutosha tu mtu mzima kuoga, ni kama alitumia kidogo sana na wala hakuwa amejimwagia maji mwilini.
“Kumbe bado hujaanza kuoga muda wote ule…” Nilishangaa kwa kuuliza
“Nilikuwa nataka nijisaidie lakini sikupata choo, nimekuita ili unisugua mgongoni...” akasema na kuanza kujichekesha pale…
Ilikuwa ni giza, choo cha nyumba ile juu palikuwa wazi hivyo hapakuwa na taa. Ni mwanga tu wa nyumba za jirani unaofanya eneo lile lionekane na mwanga hafifu wa usiku. Hata hivyo sikuacha kuona uzuri wa maumbile ya Zai. Hakika majuba yanaficha mambo. Alikuwa amejifunga lile taulo juu ya matiti, na kwa mara ya kwanza niliziona nywele za Zai, zilikuwa ndefu ba bado alikuwa amezibana na kibanio kwa nyuma kufuzifunga (kama mchicha).
Fasta nikatoa ile suruali niliyokuwa nimevaa, na ile tshirt nyepesi, nikabakia na boxer. Mara paap, akaitoa ile taulo na kuitundika kwenye moja ya misumari iliyopo jirani na mlango, Zai akabakiwa kama alivyozaliwa…
Tuliogeshana, kisha tukafua nguo zetu za ndani, halafu akaniambia nitangulie ndani yeye anakuja, kwenye ndoo alibakiwa na maji kiasi mimi nikaondoka na ile ndoo kubwa. Kitendo cha kuogeshana kilifanya mnara usome full netwaork, hadi natoka mle hali ya mti nyama ilikuwa ya maumivu. Mazingira ya bafuni mle yalikuwa siyo rafiki kufanya lolote zaidi pia nilikuwa na wasiwasi juu ya uslama wa chumba changu maana mlango niliacha wazi.
Saa tatu asubuhi ndio tuliamka, tulichelewa sana kulala. Shughuli ilikuwa pevu. Hongereni wanawake wa Tanga kwa usafi na mahaba.
---
Jioni ya siku hiyo nikiwa na Mourine, mafundi walinikabidhi nyumba yangu ikiwa imesamaniwa ipasavyo, ilikuwa na muonekano mpya kabisa ingawaje jengo kwa nje lipo vile vile. Sote tulifurahia madhari yam le ndani. Ingawaje upepo mwanana kutoka baharini ulikuwa unaingia moja kwa moja ndani ya nyumba bila kizuizi lakini pia katika mabadiliko hayo kuliongezwa viyoyozi kadhaa ili kila eneo mle ndani liwe lenye hali ya joto itakiwayo. Niseme tu nyumba ilipendeza kuliko nilivyo tarajia. Pongezi nyingi ziende kwa wafanyao kazi za kuboresha mionekano ya nyumba za watu.
“Vipi tuizindue leo au?!” Yalikuwa maneno ya Mourine, alikuwa akisema kwa mahaba huku akiniangalia usoni…
“Hapana, tusiizindue leo, tumsubiri dada arudi ndio tuizindue, italeta maana zaidi” Nilimjibu kukwepa chombezo lake maana nilishaelewa anataka izinduliweje…
“Mmh, dada yako harudi hivi karibuni, labda baada ya miezi sita au tisa hivi, alinitumia txt msg pia akasema hatokuwa anapatikana hewani hadi atutafute yeye kwanza…” Mourine alisema
Nilipigwa na butwaa pale kusikia habari za miezi kadhaa mbele, nikaanza kuhisi kuna vitu sielewi, mbona dada hajaniambia mimi hivyo na tangia aondoke hajawasiliana nami.
“Hebu niione hiyo txt msg aliyokutumia…” nikawa naomba simu yake
“Nimeshaifuta….” Akajitetea
Hapo tulikuwa tumekaa sebuleni ghorofani kwenye sofa maridadi kabisa…
Nikang’ang’ania kuitaka simu yake, akawa mgumu kupita kiasi, lakini nikatumia nguvu za uanaume wangu nikafanikiwa kuipata smartphone yake.
Nikajaribu kuifungua lakini ilikuwa na nywila.
“Nitajie PIN nifungue…” Niliamrisha
Mourine akiwa anathema kwa kasi alikataa kwa kuinua mabega juu huku akijifanya kununa.
“Pls Mourine, nifungulie niione hiyio msg aliyokutumia…” Niliamua kumbembeleza huku nikimkabidhi simu yake.
Akaipokea lakini akakataa kunirudishia tena. Basi nami nikapata sababu ya kusitisha maongezi yale na kumruhusu aende ili nipate kutafakari mambo.
Kwa ugumu sana Mourine aliinuka, nikamsindikiza kushuka ngazi hadi parking za magari akachukua gari aliyokuja nayo (ya da Queen) na kuondoka, mimi nikarudi ndani ili kutafakari mambo.
Wakati napandisha ngazi nikasikia mlio wa simu wa ujumbe wa maandishi…
“I’m sorry Alex, simu yangu ina vimeo sana ndio maana sikutaka kukupatia, ungenichukia…” Ilikuwa ni txt msg ya Mourine
Sikuijibu na wakati nafikiria nini cha kufanya msg ya whatsapp ikaingia…
“Hi Alex, bila shaka uko poa, niko mbali na Tz, pls uniangalizie nyumba yangu na mali zingine vizuri, nikirudi nitakupa habari njema. Uwe makini na Mourine asije akakukomaza huyo Malaya, lakini ishi naye vizuri. ..” ilikuwa namba ya Queen
Nilipojaribu kuipigia kawaida haikuita, nikajaribu kuipigia kwa whatsapp call, ikaita tuu bila kupokelewa. Nikaitumia txt msg haikwenda. Mwisho nikaamua kuachana nayo. Nikajilaza kwenye sofa nikendelea kutafakari mambo.
Usingizi ulipotaka kunipitia mara simu ikaita…
Mimi: “Halo”
Upande wa pili: “Hi Alex, uko poa?” Kumbe alikuwa na Zaituni
Mimi: “Aaa Zai, mimi niko poa, nina la surprise nyingine kama ya jana, Ijumaa hii utaipata...”
Hapo hapo nikapata wazo la kumualika Zaituni kwenye nyumba hii ili tuizindue, lakini kikawaza, hivi hii si ndio itakuwa fursa nzuri ya kumtamanisha Emmy kisha kutangaza kubuti mbele ya watu kama alivyonifanyia! Nikajikuta natabasamu.
Wiki hiyo nikafanya mpango wa kuwaalika wote wale walioshuhudia kupigwa kibuti na Emmy siku ile kule kwenye viwanja vya Hotel, alikosekana Hemedi tu aliyekuwa bwanaake Zai. Wote niliwatumia location including Emmy mwenyewe.
Nilipata ‘reply’ nyingi za kukubali na kufurahi kufanya ‘party’ fupi, lakini reply iliyokuwa interesting Ilikuwa ya Emmy…
“Weee Alex, hapo si kwenu kwa zamani!?, Umerudi tena hapo?!!!” Emmy alishangaa kwa kuuliza
Niliona ni vyema tu nimjibu ili asipoteze ‘interest’ ya kuja…
“Yes, ndio hapo, karibu sana siku hiyo, tena wewe jirani yangu inabidi uwe na kiherehere kwenye party!” Nilimjibu
Nilimjulisha pia Mourine juu ya ile party na nilitaka ushiriki wake pia dada Queen nilimuandikia ujumbe kwenye whatsapp ili akiingia basi akutane nao, na niliazimia kumrushia picha za nyumba siku ya part ikiisha.
Siku sasa zikawa haziendi, lakini mipango thabiti iliandaliwa nikishirikiana na rafiki yangu Bony ambaye muda wote alikuwa anashangaa jinsi maisha yalivyobadilika kuwa mazuri upande wangu…
---
Nilibahatika kumpata yule mlinzi mkuu aliyekuwa tukiishi naye, house maid wa awali sikumpata maana alikuwa ameajiriwa sehemu nyingine lakini kupitia wakala wale wale nilipatiwa house maid mwingine wa kutoka huko huko Malawi. Pia niliingia mkataba na Suma JKT wakawa ndio walizi hapo kwangu saa 24 ingawaje yule mlizi wa zamani pia alikuwepo, yeye alisaidia zaidi kazi nyingine za bustani nk. Ni muhimu sana kuwa na watu unao waamini ama unao wafahamu vizuri.
“Mshakaji, unauza unga nini!? Au tuseme ndio kubeti! Maana si kwa maendeleo haya!…” Bony alinidodosa akidhani mimi ni mmoja wa wauza unga…
“Hapana Bony, sijakuambia tu maisha yangu kabla ya kuamua kuishi Manzese…” Nilianza
Bony: “Enhe, nidokeze!”
Siku hiyo ilikuwa alhamisi jioni baada ya kutoka darasani tulienda na Bony hadi Masaki pale home.
Mimi: “Hapa ni kwetu, nimekulia nyumba hii, hapa ni kwa baba na mama, ni nyumba yetu ambayo sasa nimerudishiwa na bandari baada ya kukamilisha utaratibu wao…”
Nilimuelezea Bony kwa ufupi bila kufafanua mambo na akaonekana kuanza kuelewa
Bony: “Anhaaa, sasa nimeelewa, nyumba nzuri sana”
Mimi: “Na kutoka hapa hadi kwa akina Emmy ni jirani sana, hata nikiishiwa chumvi naweza kupaza sauti akanisikia…”
Mimi: “Tulifahamiana na akina Emmy na familia yao nikiwa hapa, ndio maana nilikuambia kuwa Emmy ananifahamu vizuri tu nami namfahamu lakini mwenzangu alinibadilikia, na sasa ni zamu yake…”
Bony: “Alex, unataka kufanya nini!, usije ukaua tu mtoto wa watu!”
Mimi: “Hafi, amekubuhu yule, juzi juzi tu hapa tumekutana sehemu akiwa na jamaa yake mwingine msanii akawa anajishaua…, safari hii maumivu yatahamia kwake”
Bony: “Hahahaaa, itakuwa njema sana hiyo, ninaona kama kesho haifiki”
Tulikuwa tunapiga stori huku tukikamilisha baadhi ya maandalizi na nikimpanga Bony jinsi atakavyo endesha uDj na mpangilio mzima wa mziki siku hiyo.
Tulivyoridhika na maandalizi kwa ajili ya kesho jioni tukatoka na Bony, tukapitia sehemu tukala kisha nikamrudisha hostel nami nikarudi kulala Manzese.
---
Itaendelea Alhamisi jioni, in shaa Allah