Simulizi: Msegemnege

Simulizi: Msegemnege

Tupio la XXXV – Mzimuni

Ilipoishia…

Haooo, mama Rose, mama wawili na mama Junior wakaondoka kurudi Kihonda ambapo muda huo tayari alasiri ilikuwa imeshaingia mamana kulisikika kengele ya saa kumi kanisa la Kigurunyembe.

Mama Rose na Vai walipofika nyumbani waliwakuta watoto wao wakiwa mezani wanakula wali na maharage waliyopikiwa kabla wazazi wao hawajaondoka lakini pia walikuta wakila nyama ya kuku iliyochemshwa ambapo kulikuwa na paja na sehemu ya mgongo…

Sasa endelea…

Mama Junior: “Nyie mlikuwa bado hamjala tu hadi saa hizi?”

Onesmo: “Tulikuwa tunacheza”

Mama Rose: “He! Na hizo nyma za kuku mmepata wapi?!”

Rose: “Si mlituwekea, mie wakati napakuwa nimekuta mmetuwekea kwenye poti yetu…”

Mama Rose na mama Junior walipigwa na mshangao walipoona watoto wao wanakula nyma ya kuku ambayo hawakuachia. Wao waliandaliwa wali na maharage tu.

“Mama Rose, hebu njoo huku kwanza…” Vai alimwita mwenzake ili watete.

“Enhe, mwenzangu umejifunza nini?...” Vai amumuuliza mama Rose

“Nahisi hizo nyama wanazokula watoto ndio zile tulizoziweka kule mzimuni kwenye shuka jeupe ili mizimu wale….” Alijibu na kushangaa

“Sasa imekuwaje zifike huku na watoto ndio wale….” Vai alishangaa pia kwa kuuliza

“Mwenzangu, hata sijui, makubwa haya, lakini Junior alituambia tusiende sisi ndio tuling’ang’ania…”

“Sasa tufanyeje!?” Mama Junior aliuliza

“Mmh!, tusubiri hadi hiyo kesho mapema tupate majibu ya mganga kwanza kisha tutajuwa cha kufanya…”

“Ok, basi watoto tujifanye tuliwawekea wao ili wasipate wasiwasi…” Vai alisema

Saa kadhaa baadaye jua likazama, siku ikaisha. Asubuhi na mapema akina vai walipitiwa na yule muumini aliyewapeleka kwa mganga kisha wakawahi kwenda huko mzimuni. Ilikuwa mapema sana kabla ya jua kuchomoza. Walifika kwa mganga na wakapokelewa vizuri.

Baada ya maandalizi macheche yam ganga wote watano, yani mganga, msaidizi wake, na akina mama Rose walielekea mlimani chini pale mzimuni.

“Sadaka zimeliwa, sadaka zimepokelewa…” Mganga alisema maneno hayo baada ya kuona vile vipande vya nguo walizoaacha jana havipo na wala zile nyama hazimo na unga uliomwagwa pia ulikuwa umeliwa na kubakia sehemu chache tu.

Mganga akaanza kuongea kwa kubonga kwa muda mrefu kisha akatulia. Muda huo wote pale waliamriwa kukaketi chini na kufanya nusu duara ambapo mganga alikuwa mbele yao na msaidizi alikuwa pembeni ya mganga.

Mganga akwa anaongea kwa lugha isiyoeleweka na msaidizi akawa anatafsiri:-

Mganga: “******£$@####!!”

Msaidizi: “Mizimu imewapokea vizuri, mmepokelewa, mmekaribishwa na wamepokea sadaka zenu…”

Mganga: “£%^&”****~@!!”

Msaidizi: “Mnasumbuliwa na ‘malaika’ wa mama yenu, lakini nia yake ni ulinzi tu…”

Mganaga:” %%%%%$$£””(“)””&^%”

Msaidizi: “Mjukuu wa mama yenu alichaguliwa kuwa kiongozi, hivyo alipatiwa ulinzi maalumu kwa ajili yake na mama yake…”

Mganga: “~@:><%£$£&*()!”£!!”

Msaidizi: “Hivyo msiwe na wasiwasi, lakini mnatakiwa mlete maadao ya sadaka ya kinywaji na mnyama kwa ajili ya usumbufu wa kutuita kutokea mbali..”

Maelezo yaliendelea pale mengi hatimaye mganga akarudi katika hali ya kawaida kisha akamuuliza yule msaidizi wake…

Mganga: “Wamesema nini?!”

Msaidizi akaeleza kama nilivyojaribu kueleza hapo juu na mganga akatingisha kichwa eti ameelewa.

Mganga: “Mizimu wanataka sadaka ya mbuzi kwa usumbufu pamoja na vifaa vya kutengenezea pombe.

Mama Vain a wenzake wakaangaliana kisha wote wakainamisha vichwa chini na kubinua midomo ile kana kwamba kusema mmh, shughuli ipo!

Baada ya hapo waliondoka na kurudi kilingeni kwa mganga na kuagana kwa ajili ya kusubiri hiyo sadaka ya mbuzi na maandalizi ya pombe ambapo waliambiwa na mganga walete, ufuta kidogo, uwele kidogo, ulezi kidogo, mtama kidogo na mahindi kidogo bila kusahau ‘sukari guru’ kidogo.

Waliondoka kurudi Kihonda, lakini kabla hawajaagana na yule muumini mshauri, waliazimia kusitisha lile zoezi la kwa mganga…

“Naona kama tumegeuzwa wateja tena, kila siku mahitaji…” Mama Junior alisema

“Kweli mwenzangu, tuliyo yajuwa yanatosha, tuachane naye”…” Muumini mshauri alichangia

“Mmh, sasa hakutokuwa na madhara kama tusipoeenda?!” Aliuliza mama Rose

“Junior alishatuambia tusiende, sidhani kama tutadhurika, si wamesema wenyewe kuwa tuna ulinzi?!” Mama Junior alijibu na kuuliza

“Mmh, huo ulinzi labda kwa Junior, sisi je tusio na ulinzi!?” Alidakia muumini mshauri

“Yesu si yupo, tumekengeuka tu kwenda kwa mganga, mlinzi wetu Yesu, na kwa jina lake hatutodhurika..” Mama Rose alisema

Walibadilishana maneno pale ya kushaurina lakini hatimaye walihitimisha kutokwenda tena kwa yule mganga.

Mama Rose na Vai walipokuwa nyumbani wakawa wanajadili peke yao…

“Mwenzangu, lakini kama mganga amesema kweli…” Mama Rose alisema

“Ni kweli wanganga wapo ila matapeli wengi siku hizi, mimi kinachonifanya niamini ni vile vipande vya kuku tulivyo vicha mzimuni na kuvikuta nyumbani…” Vai alisema.
---

Majibu ya darasa la saba yalikuwa yameshatoka na Onesmo alifauli daraja “A” na siku chache baadaye yakabandikwa matokeo ya uchaguzi sehemu za watoto kwenda kusoma.

Onesmo yeye alichaguliwa kwenda shule ya Ilboru Arusha. Lakini kwa kufuata ushauri wa ile sauti iliyomtokea usiku hawakushughulika na maandalizi ya shule hiyo bali walianza kuhangaika kutafuta shule za Seminari.

Kwa msaada wa shule aliyosoma Junior, hatimaye alipata Seminari iliyopo Mbulu iitwayo ‘The Sacred Heart Prepaeudetical’.

Jumapili panapo majaaliwa nitatupia ndefu ndefu.
Jamani mkuu vipi mbona hivyo,jumapili imepita kimya
 
Tupio la XXXVI – Mwanzo mpya

Ilipoishia…

“Zai, kwangu siyo mbali kutoka hapa, nimeona ni vyema nikabe nafasi mapema maana siku kama leo magari hujaa sana hapa kiasi cha kufanya mtu uweze kukosa nafasi nzuri ya kuegesha gari…”

Tukawa sasa tunaelekea usawa wa nyumbani kwangu uswahilini.

Sasa endelea…

“Lakini tusikae muda mrefu muda umeenda sana halafu nyumbani sijwataarifu kuwa nitachelewa…”

Zai alitahadharisha pale wakati tumeshakaribia kabisa kuingia ghettoni.

“Karibu sana Zai, hapa ndipo ninapojifichaga usiku…” Nilimkaribisha.

Nilikuwa naishi kwenye chumba na sebule, lakini kilikuwa chumba kilichosheheni kila aina ya samani vyenye thamani ambavyo kijana wa kisasa angependa kuweka kwenye chumba chake cha ukubwa ule. Sebule na chumba vilikuwa na ukubwa sawa tu wa futi tisa kwa kumi.

“Pazuri jamani…” Alipasifia huku akifanya ukaguzi ule wa kike kuangalia kama kuna dalili ya uwepo wa mtu wa jinsia yake anayeishi hapo. Nilimuachia nafasi nikaingia ndani mara moja na kutoa shati ililovaa na nikavaa fulana nyepesi nikarudi sebuleni.

“Enhe Zai, naona umeanzisha bifu na Emmy!” Nilianza uchokozi

“Emmy naye kazidi, kila bwana mwenye hela anamtaka yeye, atakufa kwa maradhi asipojiangalia…” Zai alisema.

Hapo kwangu kulikuwa na makochi mawili ya mtu mmoja mmoja, lakini yalikuwa mazuri maana niliyarithi kutoka kwa wazazi. Hivyo tulikaa kwa kuangaliana, runginga ilikuwa inaendelea na vipindi vya miziki.

“Zai, jisikie upo nyumbani, unakaribishwa muda wowote, hii ndio ‘sapraiz’ niliyokuambia…” Nilimuambia huku nikiinuka na kueleke kwenye jokofu kuangalia vinywaji…

“Najuwa muda huu tumbo limejaa, lakini kinywaji hiki hakitokosa nafasi tumboni mwako…” Nilisema huku nikimmiminia kiasi tu mchanganyiko wa juisi ya nanasi na machunywa (ya dukani) kwenye glasi nami nikijimiminia pia.

“Na tunywe kwa ajili ya mwanzo mpya!” nilichagiza kisha nikainua glass ili tugonganishe (cheers)

“Kwa mwanzo mpya…!” Kisha naye akainua glass yake tukagonganisha kwa kusogeleana tukiwa mkabala (opposite).

Nilipiga funda moja kisha nikachukuwa remote control na kuizima tv lakini nikawasha music system, nayo hii nilirithi nyumbani, ilikuwa ni sony music system yenye 5.1 speakers. Nilifungulia kwa sauti ya chini mziki heavy country ya Don Williams “I don’t wanna love you”

“Aaaaah kumbe na wewe unapenda Country, hata Hemedi alikuwa anapenda…” Zai alidakia alivyosikia melody za wimbo huo wa taratiibu wenye kubembeleza.

Mimi sasa nikawa naufuatisha maneno ya ule wimbo nikasimama na kumfuata Zai nikampelekea mikono yangu yote miwili kuashiria nataka asimame, naye akanyoosha mkono mmoja nikaushika kama namvuta hivi, akasimama kisha wote tukaanza kurindika kwa mdundo wa ule mziki huku tukiwa tumesogeleana kabisa.

Zai kama nilivyosema awali alikuwa ni mtu wa kuvaa nguo za kujihifadhi, muda wote ana ushungi na nguo zinazoficha maungo yake, hivyo hadi muda huo ilikuwa sikuwahi kubahatika kumuona vizuri zaidi ya uso wake, sehemu kidogo ya mikono na miguu.

Wakati tunabembea kwa wimbo ule tulizidi kusogeleana kiasi cha miili kuanza kugusana na mapigo yangu ya moyo yakaanza kuongezeka kasi, nilijitahidi tusogee hadi kwenye switch ya kuzimia taa kisha nikazima taa yenye mwanga mkali nikawasha taa nyeusi (black fluorescent lamp) ambapo kwa macho ya kawaida huonekana kama rangi ya zambarau hususani inapoaikisi vitu vyenye rangi yeupe.

Mkono mmoja tukiwa tumeshikana, mkono wangu mwingine ukaanza utalii wa ndani sehemu za nyuma ya mwili wake kuanzia shingoni kushuka hadi kwenye milima ya Malkia wa Sheba. Hapo ndipo nilipogundua kuwa mawingu huziba nisione vizuri vilele vya milima hiyo, si wa shepu ile. Mnara ukaanza kusoma taratiibu na wakati huo wimbo ulikuwa tayari umeshabadilika, ‘Especially for you’ ndio ulikuwa unacheza…

Ilipofika kwenye ayah ii tulijikuta wote tunayafuatisha yale maneno huku tukiangaliana…

“I touch the texture of the state,
I felt for the good and I felft for the best,
But I never new what touch coul do, Until I was touched by you!”

Wimbo huo ulikuwa wa mwisho katika orodha hiyo na sikuweka auto replay, basi wimbo ulivyoisha kukawa na ukimya mle ndani, tukiwa bado tumesimama zero distance tukajikuta midomo yetu inagusana…

Tukawa tunafanya dry kiss pale yeye akiwa amenishika mkono mmoja begani na mwingine nyuma ya shingo yangu nami mikono yango yote mwili nilikuwa nimeshika vilele vya milima ya sheba na kuiminya minya kwa mahaba.

“Wait” Mara Zai akili ikarudi…

“Ngoja niwajulishe nyumbani kuwa sirudi, muda umeshaenda sana wasije wakaacha wazi..” Zai alisema huku akifuata mkoba wake ili achukue simu.

Kweli muda ulikuwa umeshaenda, saa tano na nusu ilikuwa inakaribia.

“Wajulishe kuwa uko na mpenzi mpya Alex kama ulivyomjulisha Emmy!” Nilimtania wakati ameanza kubonyeza simu ili apige.

“Hallo!, Aunt, sijafika nyumbani, nipo kwa Alex yule aliye nileta huko, nyumbani nitaenda kesho muda umeshaenda sana…” Waliongea mawili matatu kisha akakata simu.

Kumbe alianza kupiga simu kwa shangazi yake Kigamboni, du. Moyoni nikawa nashangilia, kutaraji kupata ladha ya aina yake. Sijawahi kuyafunua majuba!

“Halo, msiache mlango wazi, nipo Kigamboni kwa Aunt, nitakuja kesho…” sikusikia ya upande wa pili, Zai alikata simu. Muda wote mimi ilikuwa kimya huku nikitafakari cha kuanza kufanya.

“Umefanya jambo jema sana Zai, muda umeenda, nafasi ya kulala ipo, karibu sana.” Nilimshukuru kwa maamuzi yake.

“Zai, maisha ya ushwahilini haya, ngoja nikuandalie maji ukajimwagie, bafu lipo nje na muda huu wala hakuna foleni…” Nilisema huku nikichemsha maji kwenye jagi ili nichangaje na mengine apate kuoga maji ya uvuguvugu.

Nikaenda chumbani kumuandalia taulo, nikalitoa kabatini na kuliweka kwenye kitanda kisha nikatoka chumbani na kumuambia akajiandae kwa ajili ya kwenda kujimwagia maji.

Nilimsindikiza hadi bafuni nikiwa nimembebe kasha maalumu ambalo huwekea sabuni, dawa ya meno, mswaki ambapo nilimuwekea mswaki mpya ambao haujafunguliwa, wavu maalumu wa kujisugulia mgongoni na mazaga mengine yahusuyo maliwato kisha nikamwacha na kurudi chumbani.

Mara txt msg igaingia kwenye simu yangu ambayo niliweka katika hali ya mitetemo. Nilipoifungua nikakuta msg ya Mourine…

“I miss you handsome boy, Kesho jiandae kwa sebene lingine, G9t”

Ile text msg ikanifanya niyakumbuke mautundu yake, na muda huu nipo na Zaituni, nitalala naye hadi asubuhi, ilikuwa mara yangu ya kwanza kwa mimi kwa miaka mitano tangia nihamie nyumba ile kulala na mwanamke mle ndani, siku zote shida zangu namaliziaGa huko natoka Dar naenda Dar.

Wakati natafakari nimjibu nini Mourine text msg ikaingia tena…

“Alex, naomba niletee maji mengine…”

Nikawaza, ina maana lita 18 zote hazijamtosha hadi nimuongezee maji mengine! Oooh nikakumbuka huenda amefanya safari kubwa labda, basi nikachemsha fasta maji mengine kisha nikachanganya kwenye kindoo cha lita 10 nikampelekea.

Nilivyofika nikamwita kisha nikamwambia maji haya hapa ile nimenyanyua ndoo kwa mkono mmoja kumpatia naye akafungua mlango akiwa amejifunga taulo kisha akaniambia…

“Ingia Alex…”

Sikusita, nikaingia.

Nilipoangalia maji kwenye ile ndoo ya lita 20 yalikuwemo ya kutosha tu mtu mzima kuoga, ni kama alitumia kidogo sana na wala hakuwa amejimwagia maji mwilini.

“Kumbe bado hujaanza kuoga muda wote ule…” Nilishangaa kwa kuuliza

“Nilikuwa nataka nijisaidie lakini sikupata choo, nimekuita ili unisugua mgongoni...” akasema na kuanza kujichekesha pale…

Ilikuwa ni giza, choo cha nyumba ile juu palikuwa wazi hivyo hapakuwa na taa. Ni mwanga tu wa nyumba za jirani unaofanya eneo lile lionekane na mwanga hafifu wa usiku. Hata hivyo sikuacha kuona uzuri wa maumbile ya Zai. Hakika majuba yanaficha mambo. Alikuwa amejifunga lile taulo juu ya matiti, na kwa mara ya kwanza niliziona nywele za Zai, zilikuwa ndefu ba bado alikuwa amezibana na kibanio kwa nyuma kufuzifunga (kama mchicha).

Fasta nikatoa ile suruali niliyokuwa nimevaa, na ile tshirt nyepesi, nikabakia na boxer. Mara paap, akaitoa ile taulo na kuitundika kwenye moja ya misumari iliyopo jirani na mlango, Zai akabakiwa kama alivyozaliwa…

Tuliogeshana, kisha tukafua nguo zetu za ndani, halafu akaniambia nitangulie ndani yeye anakuja, kwenye ndoo alibakiwa na maji kiasi mimi nikaondoka na ile ndoo kubwa. Kitendo cha kuogeshana kilifanya mnara usome full netwaork, hadi natoka mle hali ya mti nyama ilikuwa ya maumivu. Mazingira ya bafuni mle yalikuwa siyo rafiki kufanya lolote zaidi pia nilikuwa na wasiwasi juu ya uslama wa chumba changu maana mlango niliacha wazi.

Saa tatu asubuhi ndio tuliamka, tulichelewa sana kulala. Shughuli ilikuwa pevu. Hongereni wanawake wa Tanga kwa usafi na mahaba.
---

Jioni ya siku hiyo nikiwa na Mourine, mafundi walinikabidhi nyumba yangu ikiwa imesamaniwa ipasavyo, ilikuwa na muonekano mpya kabisa ingawaje jengo kwa nje lipo vile vile. Sote tulifurahia madhari yam le ndani. Ingawaje upepo mwanana kutoka baharini ulikuwa unaingia moja kwa moja ndani ya nyumba bila kizuizi lakini pia katika mabadiliko hayo kuliongezwa viyoyozi kadhaa ili kila eneo mle ndani liwe lenye hali ya joto itakiwayo. Niseme tu nyumba ilipendeza kuliko nilivyo tarajia. Pongezi nyingi ziende kwa wafanyao kazi za kuboresha mionekano ya nyumba za watu.

“Vipi tuizindue leo au?!” Yalikuwa maneno ya Mourine, alikuwa akisema kwa mahaba huku akiniangalia usoni…

“Hapana, tusiizindue leo, tumsubiri dada arudi ndio tuizindue, italeta maana zaidi” Nilimjibu kukwepa chombezo lake maana nilishaelewa anataka izinduliweje…

“Mmh, dada yako harudi hivi karibuni, labda baada ya miezi sita au tisa hivi, alinitumia txt msg pia akasema hatokuwa anapatikana hewani hadi atutafute yeye kwanza…” Mourine alisema

Nilipigwa na butwaa pale kusikia habari za miezi kadhaa mbele, nikaanza kuhisi kuna vitu sielewi, mbona dada hajaniambia mimi hivyo na tangia aondoke hajawasiliana nami.

“Hebu niione hiyo txt msg aliyokutumia…” nikawa naomba simu yake

“Nimeshaifuta….” Akajitetea

Hapo tulikuwa tumekaa sebuleni ghorofani kwenye sofa maridadi kabisa…

Nikang’ang’ania kuitaka simu yake, akawa mgumu kupita kiasi, lakini nikatumia nguvu za uanaume wangu nikafanikiwa kuipata smartphone yake.

Nikajaribu kuifungua lakini ilikuwa na nywila.

“Nitajie PIN nifungue…” Niliamrisha

Mourine akiwa anathema kwa kasi alikataa kwa kuinua mabega juu huku akijifanya kununa.

“Pls Mourine, nifungulie niione hiyio msg aliyokutumia…” Niliamua kumbembeleza huku nikimkabidhi simu yake.

Akaipokea lakini akakataa kunirudishia tena. Basi nami nikapata sababu ya kusitisha maongezi yale na kumruhusu aende ili nipate kutafakari mambo.

Kwa ugumu sana Mourine aliinuka, nikamsindikiza kushuka ngazi hadi parking za magari akachukua gari aliyokuja nayo (ya da Queen) na kuondoka, mimi nikarudi ndani ili kutafakari mambo.

Wakati napandisha ngazi nikasikia mlio wa simu wa ujumbe wa maandishi…

“I’m sorry Alex, simu yangu ina vimeo sana ndio maana sikutaka kukupatia, ungenichukia…” Ilikuwa ni txt msg ya Mourine

Sikuijibu na wakati nafikiria nini cha kufanya msg ya whatsapp ikaingia…

“Hi Alex, bila shaka uko poa, niko mbali na Tz, pls uniangalizie nyumba yangu na mali zingine vizuri, nikirudi nitakupa habari njema. Uwe makini na Mourine asije akakukomaza huyo Malaya, lakini ishi naye vizuri. ..” ilikuwa namba ya Queen

Nilipojaribu kuipigia kawaida haikuita, nikajaribu kuipigia kwa whatsapp call, ikaita tuu bila kupokelewa. Nikaitumia txt msg haikwenda. Mwisho nikaamua kuachana nayo. Nikajilaza kwenye sofa nikendelea kutafakari mambo.

Usingizi ulipotaka kunipitia mara simu ikaita…

Mimi: “Halo”
Upande wa pili: “Hi Alex, uko poa?” Kumbe alikuwa na Zaituni

Mimi: “Aaa Zai, mimi niko poa, nina la surprise nyingine kama ya jana, Ijumaa hii utaipata...”

Hapo hapo nikapata wazo la kumualika Zaituni kwenye nyumba hii ili tuizindue, lakini kikawaza, hivi hii si ndio itakuwa fursa nzuri ya kumtamanisha Emmy kisha kutangaza kubuti mbele ya watu kama alivyonifanyia! Nikajikuta natabasamu.

Wiki hiyo nikafanya mpango wa kuwaalika wote wale walioshuhudia kupigwa kibuti na Emmy siku ile kule kwenye viwanja vya Hotel, alikosekana Hemedi tu aliyekuwa bwanaake Zai. Wote niliwatumia location including Emmy mwenyewe.

Nilipata ‘reply’ nyingi za kukubali na kufurahi kufanya ‘party’ fupi, lakini reply iliyokuwa interesting Ilikuwa ya Emmy…

“Weee Alex, hapo si kwenu kwa zamani!?, Umerudi tena hapo?!!!” Emmy alishangaa kwa kuuliza

Niliona ni vyema tu nimjibu ili asipoteze ‘interest’ ya kuja…

“Yes, ndio hapo, karibu sana siku hiyo, tena wewe jirani yangu inabidi uwe na kiherehere kwenye party!” Nilimjibu

Nilimjulisha pia Mourine juu ya ile party na nilitaka ushiriki wake pia dada Queen nilimuandikia ujumbe kwenye whatsapp ili akiingia basi akutane nao, na niliazimia kumrushia picha za nyumba siku ya part ikiisha.

Siku sasa zikawa haziendi, lakini mipango thabiti iliandaliwa nikishirikiana na rafiki yangu Bony ambaye muda wote alikuwa anashangaa jinsi maisha yalivyobadilika kuwa mazuri upande wangu…
---

Nilibahatika kumpata yule mlinzi mkuu aliyekuwa tukiishi naye, house maid wa awali sikumpata maana alikuwa ameajiriwa sehemu nyingine lakini kupitia wakala wale wale nilipatiwa house maid mwingine wa kutoka huko huko Malawi. Pia niliingia mkataba na Suma JKT wakawa ndio walizi hapo kwangu saa 24 ingawaje yule mlizi wa zamani pia alikuwepo, yeye alisaidia zaidi kazi nyingine za bustani nk. Ni muhimu sana kuwa na watu unao waamini ama unao wafahamu vizuri.

“Mshakaji, unauza unga nini!? Au tuseme ndio kubeti! Maana si kwa maendeleo haya!…” Bony alinidodosa akidhani mimi ni mmoja wa wauza unga…

“Hapana Bony, sijakuambia tu maisha yangu kabla ya kuamua kuishi Manzese…” Nilianza

Bony: “Enhe, nidokeze!”

Siku hiyo ilikuwa alhamisi jioni baada ya kutoka darasani tulienda na Bony hadi Masaki pale home.

Mimi: “Hapa ni kwetu, nimekulia nyumba hii, hapa ni kwa baba na mama, ni nyumba yetu ambayo sasa nimerudishiwa na bandari baada ya kukamilisha utaratibu wao…”

Nilimuelezea Bony kwa ufupi bila kufafanua mambo na akaonekana kuanza kuelewa

Bony: “Anhaaa, sasa nimeelewa, nyumba nzuri sana”

Mimi: “Na kutoka hapa hadi kwa akina Emmy ni jirani sana, hata nikiishiwa chumvi naweza kupaza sauti akanisikia…”

Mimi: “Tulifahamiana na akina Emmy na familia yao nikiwa hapa, ndio maana nilikuambia kuwa Emmy ananifahamu vizuri tu nami namfahamu lakini mwenzangu alinibadilikia, na sasa ni zamu yake…”

Bony: “Alex, unataka kufanya nini!, usije ukaua tu mtoto wa watu!”

Mimi: “Hafi, amekubuhu yule, juzi juzi tu hapa tumekutana sehemu akiwa na jamaa yake mwingine msanii akawa anajishaua…, safari hii maumivu yatahamia kwake”

Bony: “Hahahaaa, itakuwa njema sana hiyo, ninaona kama kesho haifiki”

Tulikuwa tunapiga stori huku tukikamilisha baadhi ya maandalizi na nikimpanga Bony jinsi atakavyo endesha uDj na mpangilio mzima wa mziki siku hiyo.

Tulivyoridhika na maandalizi kwa ajili ya kesho jioni tukatoka na Bony, tukapitia sehemu tukala kisha nikamrudisha hostel nami nikarudi kulala Manzese.
---

Itaendelea Alhamisi jioni, in shaa Allah
 
Asante, japo inachelewa sana hadi mtu unasahau iliishia wapi, ukianza kusoma inabidi uunganishe dot kwanza ndio ujue uelekeo ni wapi[emoji23][emoji23][emoji23]
Pole, mazingira yananinyima muda wa kuandika, muda mwingi nipo mbio mbio barabarani. Imagine juzi nilikuwa Mbeya, leo nipo kwingine kabisa!
 
Tupio la XXXVII – The Party

Endelea…

Nilivyorudi nyumbani Manzese wakati natafuta usingizi, whatsapp msg kutoka kwa Mourine iliingia…

“Hi Handsome, nimekumiss ujue, halafu nisamehe kwa kukukatalia kuangalia msg kwenye simu yangu, lakini ipo siku utajuwa kwanini, muda bado, naisubiri kwa hamu hiyo party ya kesho. Umesema umewaalika na marafiki zako?!”

Mimi: “Okay, ndiyo nimewaalika washkaji wa chuo, sio wengi lakini nataka tufurahi pamoja.”

Tulisogoa mawili matatu kisha tukaagana, mimi nikaendelea kuutafuta usingizi.

Kule Masaki nyumba yetu (yangu) na nyumba ya akina Emilia ni mjengo wa aina moja, yani kila kitu kilijengwa sawa, Wazazi wa Emmy wote wawili walikuwa wanafanyia Mamlaka ya Bandari pia.

Kwa upande wa Zai tangia siku ile tuamke wote nyumbani pale Manzese, ni kama alikuwa ananionea aibu hivi, muda mwingi alikuwa ananikwepa kukutanisha macho ingawaje msg zake zilikuwa hazikatiki kwenye simu yangu.

“Ahsante, umeufungua moyo wangu upya…”

“Ulinikamua vizuri siku ile, upwiru wote umeisha, niliinjoi sana…”

“Nimesha-msahau sasa Hemedi, apotelee huko huko…”

Yani kwa siku nilipokea msg zake za namna hiyo zaidi ya 17.
---

Usingizi ulinichukua, nilizinduka alfajiri kwa ajili ya kwenda haja ndogo, baada ya hapo nikaanza maandalizi madogo kwa ajili ya chuo na kuweka utaratibu vizuri kwenye karatasi kwa ajili ya party ya jioni.

Kabla sijaenda chuo nilipitia kwanza kule Masaki kuangalia maandalizi, nilikuta Mlinzi na house maid wapo vizuri kama nilivyo waelekeza, nyumba kwa nje ilipambwa vizuri eneo ambalo ndilo nilitarajia tungeanzia kufanya party yetu na kisha kungekuwa na kipande cha kuizindua nyumba ambapo tungeingia ndani.

Waliandaa alama ya tambala la tangazo lililoandikwa kuashiria part iko nyumba ile. Nilifurahia sana ubunifu ambao baadaye nilijuwa kuwa ulitoka kwa vijana walinzi wa SumaJkt.

Tulimtumia mwanachuo mwenzetu mmoja kuchukuwa kazi ya kutuandalia chakula, maana dada yake huwa ana shughulika na kazi hizo za catering, kwa uzoefu wake tulijuwa kuwa hakuto haribika kitu na tenda hii ilikuwa tofauti kabisa na alivyozoea kwenye maharusi nk.

Ilihitajika uchomaji wa nyama za mbuzi, ng’ombe na kuku wa kienyeji kwenye viwanja ya nyumba (ndani ya uzio. Nyumba ilikuwa na uzio mkubwa sana wa ukuta wa matofali. Kulihitajika viazi mbatata vya kuchoma na pia chips zake na vikorombwezo vingine.

Baada ya muda wa chuo, kukawa na msafara usio rasmi kwa baadhi ya waalikwa wakinifuata kuelekea Masaki, wengine walipitia sehemu wajuazo kwanza kisha wakaungana nasi kwa kutumia gps location, kwenye hili la kukaribisha wageni, Emmy alinisaidia sana.

Saa kumi na mbili jioni tayari magari ya walikwa yalikuwa yamejaa sehemu za kuegeshea ndani ya uzio nan je ya uzio, wote niliowaalika walikuja pamoja na wazamiaji wachache (partners), watu walianza kunywa, kula nyama na kuburudika na miziki mbali mbali kabla hata shughuli yenyewe haijafunguliwa rasmi.

Mourine naye akafika kwa kuchelewa lakini aliwahi kabla ya tamko la kufunguliwa kwa party, Emmy alikuwepo tangia mwanzo na alijipa kitengo cha ukaribishaji, ajabu siku hiyo sikumwona yule msanii wake.

Niliifungua party rasmi kwa kutangaza kwamba imefunguliwa, baada ya kuwashukuru waalikwa wote walifika, na kwamba madhumuni ya party ile ilikuwa kuizindua nyumba ambayo tuliitelekeza kwa miaka kadhaa na sasa tumerudi tena. Nilitumia wingi ili kuonesha siko peke yangu mle ndani.

“Kwa wazazi wake hapa, nyumba za Bandari hizi…” alisikika jamaa mmoja akimwambia mwenzake

“Nyumba zimeshauzwa hizi, itakuwa wameinunua…” alimjibu mwingine kurekebisha

“Pazuri sana, hewa safi, upepo mzuri kutoka baharini, na bustani umeandaliwa vizuri…” mdada mwingine alichangia

Ilikuwa furaha sana, huku Emmy akijisogeza sogeza kuonesha tupo jirani…

Baadaye kidogo nilimuashiria Dj Bony asitishe mziki ili nitoe utambulisho, maana kuna watu kadhaa mule ndani walikuwa hawajuani…

“Eeee napenda kuwatambulisha kwenu dada yangu mpenzi Mourine, (nikamshika bega), yeye ni mjasiri-amali yupo hapa hapa Dar na anaishi maeneo haya haya ya Masaki…”

Waalikwa tayari walikuwa na vinywaji kichwani, walipiga makofi…

“Pia yule pale ni house keeper wetu anaitwa Alice, yule kule mzee wetu anaitwa Nchumari bila kuwasahau walinzi wetu kama mnavyo waona na timu ile kule ya catering ni ya dada Neema…”

“Tuendelee kuburudika na baada ya muda mfupi tutaizindua nyumba kwa kuitembelea angalau sehemu chache…, Dj!”

Mziki ukaweka na watu wakaendelea kufurahia. Hapakuwa na ratiba ya kula lakini kila mtu akihitaji chochote yeye mwenyewe alikuwa anaenda kule upande wachomapo nyama na kuchukuwa sehemu anayoridhika kwa aina ya nyma aitakayo na kuendelea kuparty .

Ingawaje kulikuwa na viti vya kukaa, lakini muda mwingi watu walikuwa wamesimama huku wakinywa vinywaji vyao pendwa.

Baada ya muda ikafika wakati wa kuitembelea nyumba kwa sehemu nilizochaguwa watu wafike, tukaanza kuingia ndani na kufika sebuleni ambapo tulisimama, palikuwa pamependeza sana, yani sana hadi Emmy alishindwa kujizuia…

“Hongera Alex, umebadilisha kabisa muonekano wa ndani, sio kama kule kwetu…” alisema hivyo huku ‘akinipalatia’, Mourine alikuwa mtulivu sana, Zai wala hakuonesha lolote ila uso wake ulikuwa na furaha.

Tulivyomaliza ziara ya mle ndani tukashuka chini na kurudi kuendelea na kuburudika kwa nyama na vyakula vingine na vinywaji vilikuwa havikauki. Wengine walianza kuchukuliwa na ulevi ikanibidi nimuombe Dj Bony asitishe mziki ili nitoe tangazo…

“…Pamoja na kuwashukuru kwa kuitikia wito wa kujumuika nasi hapa, kuzindua nyumba, kula na kunywa na kufurahi lakini pia nina tangazo rasmi leo…”

Pakawa na ukimya kila mmoja akijiuliza ni tangazo gani…

Dj Bony kama nilivyompanga aliweka wimbo wa kuchombeza taratibu wakati naanza kuongea…

“…Tangazo lenyewe ni kwamba leo rasmi nawatangazia mpenzi wangu ….”

Utulivu ukazidi

“Tangia nimeanza uhusiano naye, moyo wangu umetulia, yeye ni mpole, mnyenyeku na ana sifa zote za kuwa mke bora…”

Watu wakawa wanaangaliana kisha macho yote yakawa yanamuelekea Mourine ambaye ndiye wanachuo walikuwa hawamjui lakini hapo alionesha ukaribu sana nami ingawaje nilimtambulisha kuwa ni dada.

“…Kwa sababu hiyo basi, napenda wote humu na dunia yote ifahamu kuwa….”

Wafukunyuku wakawa wanarikodi lile tukio kwa simu zao, kumbe wengine walikuwa wapo live tiktok na youtube wakirusha baadhi ya matukio…

“….napenda mfahamu kuwa kuanzia sasa Zaituni Nassoro Ahmed ndiye mpenzi wangu mpya!....”

Watu wengine walishangaaa, wengine walifurahia na nderemo na vifijo vikasikika…

Nikamsogelea Zaituni ambaye muda wote wala hakutaka kuonesha kama yupo karibu nami kimahusiano isipokuwa Emmy tu ndio ambaye angeweza kuhisi kutokana na siku ile tulivyokutana kule Rombo Green view Hotel…

Emmy alikuwa ameduaa kama ameloweshwa maji, akiwa amesimama huku mikono yake yote miwili akishika mdomo wake kwa kufanya kama anauziba…

Nikazidi kumsogelea Zai ambaye sasa alikuwa anaona aibu huku akitabasamu, kichwa ameinamisha chini huku akinema nema!

Nikapiga goti moja…

Watu wote mle ndani walilipuka kwa shangwe hata kabla sijasema neno…

“Zai…” nilisema na watuwakitikia weweeeeeeee!

“Zai, will you marry me!?”

Nikatoa kasha ya pete uchumba kisha nikaifunua lile kasha na ile pete kuonekana… nikishikilia kusubira response ya Zai.

Badala ya kujibu akawa anaruka ruka kwa furaha huku akiwa anafunika macho kwa aibu na furaha…

Waalikwa wakawa wanasema..

“Say yes, say yes!”

Bado nikiwa katika hali ile ya kupiga goti, Zai alinisogelea huku akirusharusha miguu kwa furaha kama anapiga maktaim na kunyoosha mkono wake huku akisemaa…

“Yes Alex, I will” Nikamvalisha pete maridadi kabisa ya uchumba

DJ naye hakuwa mbanizi wa kufuata maelekezo, ilipigwa bonge la blues ambapo nilisimama na kumkumbatia Zai huku tukishangiliwa na waalikwa…

“Jamani, Emmy ameanguka!” tulikatishwa ghafla na sauti ya Laula, rafiki yake Emmy

Mourine fasta akamsogelea Emmy na kuanza kumkagua…

Mziki ukazimwa na wote tukawa tunamwangalia Emmy

“Anapumua, mlazeni ubavu wa kulia…” Mourine aliamrisha

Mara Emmy akainuka mwenyewe akawa amekaa na akaanza kulia….

Akainuka na kuchukuwa mkoba wake kisha akatoka nje ya geti na kutokomea…

“Mfuateni, asije akaenda kujigongesha barabarani…” Mourine alisema kuwaambia wenzake ambapo Laura na Rachel walimfuata, Mlinzi mmoja akaongozana nao, Emmy alionekana akitembea harakaharaka akielekea numbani kwao huku akilia.

“We Alex, ungeua mtoto wa watu!” Mourine alisema huku akiwa amekasirika…

“Dada, hujui tu huyo alichonifanyiaga, leo hii ni zamu yake. Hata hivyo yeye alishaniacha siku nyingi na ameshabadilisha mabwana wawili sasa hivi yupo na msanii (nikamtaja), hivyo hana sababu ya kuumia wala kuhuzunika, Emmy siyo mpenzi wangu…” Nilimjibu Mourine

“Kama siyo mpenzi wako mbona kazimia!, nyie mna yenu!” Mourine alikazia

“Hakuna lolote dada, muulize Zai, ni yeye Emmy alitutambulisha pia kwa mpenzi wake mpya huyo msanii na Zai ni shahidi…” Nilimjibu

Tuliobaki mule ndani tukapata wasaa wa kukaa kwenye viti na stori zikawa za Emmy na tabia zake na jinsi nilivyolipiza kisasi kimtindo.

Zai kuanzia hapo muda wote alikuwa hakai mbali nami, alikuwa mwenye furaha sana na uso ulikunjuka kisawasawa!

Tuliendelea kunywa na kula huku waalikwa wakitupongeza…

“Halafu nyie watu mna siri, kumbe mna date halafu wadau hatujui…!” Margareth alisema kiushabiki

Itaendelea…
 
Mambo hayoo.
Lunch time hii wacha niserereke nayoo.
Thanks Mzee Jason.
 
Back
Top Bottom