Simulizi: Msegemnege

Simulizi: Msegemnege

Tupio la XXXIV – Pasport & Visa

Ilipoishia...

Mpango wangu ulikuwa zile hela niziweke benki na kubakisha kiasi kama cha milioni tatu cash ili ndio niende nazo nyumbani. Mwenge pake nikaenda kwa wakala wa huduma za kifedha na kudeposit milioni mbili kwa wakala wa kwanza na milioni mbili zingine kwa wakala mwingine kisha nikaelekea kupanda daladala za kwenda Kawe.

Nilikuwa mwenye furaha sana na mawazo sasa yakawa kwenye utaratibu wa kupata hati ya kusafiria.

Sasa endelea...

Niliwashirikisha wazazi wangu, wakafurahi sana, nyumbani nilienda na milioni tatu kasoro hivi sawa na dola 1,200 kama nilivyo andika kwenye mapendekezo ambayo nyumbani waliyaona.

Walifurahi sana hususani afande Baba ambaye alikuwa kama haamini hivi.

Mama alifurahi lakini kama alikuwa na wasiwasi hivi...

"Wiki ijayo sisi tutaondoka kuelekea Monduli Arusha, halafu ndio tutapanda ndege kuelekea huko masomoni ughaibuni..." Afande Juma alianza kutoa wasia kiaina...

"Usisahau kuwasiliana nami kwa njia ya whatsapp, siku nikiingia online nitaona salamu zako..."

"Sasa kazana upate hiyo hati ya kusafiria mapema na kama nikiondoka kabla hujapata utakuwa unanipa update kwa whatsapp..."

Mama naye akachangia maongezi...

"Mpaka hapa mwanagu sasa naamini kweli utasafiri, nilidhani ni masihara tu lakini kwa kutumiwa hela hizo bila shaka jambo hili ni la uhakika..."

"Lakini mwanangu nina wasiwasi na usalama wako ukiwa huko Uarabuni, lakini nakuombea Mwenyezi Mungu akuepushe na kila aina ya mabalaa, nawe ukawe mwaminifu huenda ukaja kuwa msaada mkubwa sana kwetu..."

Wazazi walikuwa wanatoa mawaidha kana kwamba tayari ninasafiri wakati hata hiyo passport sijaanza kuifuatilia.

"Lakini mama, bado safari haijawa tayari, pili msiwe na wasiwasi, kama nikiondoka na siku ikapita bila kuwasiliana nanyi basi ndio muwe na wasiwasi, hata hivyo nitatafuta namna ya kujilinda kisirisiri.
---

Kesho yake nikamtafuta yule nusu teja anipe ‘abc’ za kupata passport, sikumpata kwenye simu. Nikajaribu kutumia msg kwa whatsapp ndio akajibu...

"Mwanaa, hongera kwa kukomaa hadi umepata hela ya kitabu (passport)

Sasa sikia mwana, nenda kule kurasini uhamiaji, kuna maduka ya jirani hapo opoziti na jengo lao, ingia kwenye steshenari yoyote muulilize mshkaji mmoja anaitwa Hemed, utaoneshwa anapokaaga kisha utamweleza shida yako, fasta tu mwana, ila utamtoa kiasi fulani atakuambia yeye..."

Nusu teja: "Utanijulisha basi maendeleo kwa whatsapp maana sipo Bongo, niko zangu Brazil lakini siku si nyingi nitarudi..."

Nusu teja alimaliza hivyo.

Hemedi, kijana wa Kipemba, (Mwenyezi Mungu amwie radhi) alishafariki kwa ajali ya gari; alikuwa ni kishoka mzoefu na mambo yake yalikuwa ya uhakika. Alikuwa mwaminifu sana maana niliendelea kufanya naye kazi za aina nyingine maana alikuwa ana connection kubwa.

Basi nikaenda hadi kule makao makuu ya uhamiaji kirasini na kufanya kama nilivyoelekezwa...

Kwa bahati mbaya siku hiyo hakuwepo maeneo yale lakini nikapewa namba yake ya simu....

"Andika namba hii 0789 xxxx08, hiyo lazima apokee ila pia ana namba nyingine atakupa mwenyewe..." Dada mmoja wa stationery aliniambia.

Nilirudi nyumbani na kuanza kupanga namna nitakavyofanya shopping.

Bajeti ilikuwa ya kutosha sana kwa hizo milioni tatu kasoro, lakini pia nilikuwa na akiba benki ya milioni 4.

-Nguo za ndani dazani 1...
  • Fulana za ndani nusu dazani...
  • Trucksuit jozi tatu..
  • Raba pea moja...
  • Viatu vya kuvalia suti pea moja...
  • Sendoz (sandals) pea mbili
  • Suti spesho tatu na kaunda suti 1
  • Jeans tatu
  • Mshati ya mikono mirefu 6 na ya mikono mifupi 6
  • Tshirts form six sita
  • Kanzu mbili moja nyeupe na nyingene ya rangi tofauti
  • kofia ya mkono 1 na ya kudarizi moja
  • Begi la safri 1
  • Misuli miwili

Yani niliorodhesha mahitaji kisha nikaenda kufanya ‘windows shopping’ kesho yake.

Pamoja kuorodhesha msululu wa mahitaji lakini haikuzidi 2.7m

Basi nikasema ngoja nipate passport kwanza na kisha ndio nifanye shopping.

Nilipata nguvu ya kuorodhesha mahitaji mengi nilipokumbuka kuwa kuhusu nauli wao watanitumia tiket.
---

Niliwasiliana na Hemedi (R.I.P) kwa simu na tukapanga ahadi ya kuonana kesho yake Temeke.

Kesho yake sasa Temeke!...

"Cheti cha kuzaliwa unacho?" Hemedi aliniuliza

"Ndiyo" nilijibu

Hemedi: "Hebu nikione"

Nikamtolea

Hemedi: "Da, hiki orijino mdogo wangu halafu ni vya kisasa siyo yale mavyeti marefu hata kwenye bahasha hayaingii.."

Hemedi: "Enhe, una kadi ya NIDA?

Mimi: "Ndiyo"

Hemedi: "Hebu niiione..."

Nikampatia

Hemedi: "Una Nida ya baba au mama?"

Mimi: Ndiyo, baba na mama wote wana NIDA na baba pia ana passport ila hapa sina nakala zao..."

Hemedi: "Safi sana, yani hii itakuwa kama kumsukuma mlevi..."

Hemedi: "Mambo mengine madogo madogo nitayamaliza mwenyewe..."

Hemedi alinitia moyo pale hadi nikaona passport hii hapa ilhali hata fomu sijajaza.

"Sasa dogo, niachie laki moja kwanza nianze nayo nipe siku 3 unicheki.." Hemedi alihitimisha kwa kuomba kianzio ambapo nami sikuwa na hiyana nikampatia kwa njia ya simu na ya kutolea.

Baada ya siku tatu tulikutana Mwenge ambapo nilimpatia nakala za nyaraka muhimu kwa ajili ya maandalizi ya passport...

"Ile juzi pale nilikuwa na safari ya kwenda Unguja ndio maana nilikuomba unisaidie kilo moja, nimerudi leo na kuja moja kwa moja hapa nili nianze kazi yako..." Hemedi alifunguka

"Gaharama ya passport ni kilo na nusu tu, na mie utanitoa kilo na ishirini kwa mambo yote, hivyo nakudai elfu ishirini nikishamaliza kazi..."

Alinipatia fomu nikaijaza vizuri na picha zangu passport size nikampatia.

Hemedi aliendelea kunipa somo pale nikaelewa na aliniambia haifiki wiki mambo yatakuwa mazuri.
---

Baba aliondoka kwenda Jeshini kwao Monduli na alinipa ushirikiano kabla ya kuondoka kuhusu nakala za kitambulisho chake cha Taifa na nakala ya sehemu muhimu za Passport yake.

Siku nne baada ya baba kuondoka Hemedi alinipigia kuwa tukutane Uhamiaji ya pale posta mpya.

"Mdogo wangu, passport ipo tayari, chukuwa hii risiti orijino niliyolipia utaingia nayo humo ndani nenda kwenye dirisha la kupokelea passport, watakuomba hii risiti lakini watakurudishia kisha utasaini kwenye kitabu chao na sehemu watakazo kuelekeza kisha watakupa passport yako. Mimi utanikuta hapahapa nakusubiri...."

Hemedi alinipa maelekezo ya mwisho mwisho tulipo kutana pale jengo la wizara ya mambo ya ndani. Dakika ishirini baadaye nilitoka mle mjengoni nikiwa na passport yangu, nilimkuta Hemedi ananisubiri, akaniambia nihakiki majina na taarifa zingine kama zina kasoro niirudishe warekebishe, lakini kwa bahati nzuri haikuwa na kasoro yoyote.

Nilikuwa mwenye furaha sana siku hiyo na nilimpatia Hemedi elfu hamsini badala ya elfu ishirini aliyokuwa ananidai.
---

Angalizo:

Mifumo ya kupata passport siku hizi ipo vizuri, kama una nyaraka zote muhimu jaza fomu online na fuata maelekezo itaipata ndani ya muda mfupi, haina haja ya kutumia vishoka.
---

Tuliagana na Hemedi, kila mmoja akashika njia yake, lakini yeye pia alinishauri siku ya kwenda kupata yellow card, niende moja kwa moja bila kutumia wale ‘wapiga winga’.

Ijumaa nikaenda Hospitali ya mnazi mmoja na kuchanjwa chanjo mbili, moja walisema ya homa ya manjano na nyingine wala siikumbuki ilikuwa ya nini. Nilishauriwa pia kupima homa ya ini lakini sikuweza kupima siku hiyo maana muda ulikuwa umeenda. Waliniambia kama nitakuwa sijaambukizwa homa ya ini basi pia nichanje maana ni ugonjwa hatari sana usio na tiba lakini una kinga hiyo ya chanjo.

Wakati tunapewa elimu hiyo ya ugonjwa wa ini walisema unaambukizwa kwa njia ya kujamiiana (ngono zembe) na watu wengi huambukizwa bila kujuwa. Pia waliniambia nisubiri angalau siku kumi kabla ya kusafiri. Bahati nzuri safari yangu bado ilikuwa haijapangwa tarehe.

Wakati wote wa mchakato wa kupata passport nilikuwa nawasiliana na Nasreen kumpa maendeleo, alifurahi sana kusikia nimesha chanjwa homa ya manjano lakini pia akanishauri na hiyo homa ya ini nifanye utaratibu nichanjwe.

Kwakuwa pale mnazi mmoja siku za chanjo ni mbili tu kwa wiki, yaani Juma nne na Ijumaa, ilibidi nisubiri hadi Jumaane inayofuata niwahi mapema nipime na kuchanjwa.

Kwa bahati nzuri sikuwa nimeambukizwa virusi vya homa ya ini, hiyo siku hiyo ya Jumanne nilichanjwa baada ya kupata majibu, nikaambiwa baada ya mwezi mmoja nirudi tena kupata sindano ya pili na ya tatu miezi sita baada ya sindano ya pili. Lakini kwakuwa nilikuwa na safari sikujuwa sindano ya pili nitachomewa wapi.

Baba baada ya siku tatu tangia afike Arusha walituaga nyumbani kwa video call alipokuwa uwanja wa ndege wa KIA, alituambia kuwa wataenda Nairobi (ratiba ya ndege) kisha wataenda Ethiopita kisha ndio watapotelea ughaibuni.

Siku hiyo usiku Nasreen pia alinipigia video call kwa whatsapp…

Nasreen: “Hi Omari”

Mimi: “Helo, how are you today?”

Nasreen, “I’m doing well”

Nasreen: “So Omari, as now you have passport, and passport size photo, I need to arrange visa for you before I send you a ticket…”

Nasreen: “Send me copy of your passport so that I use the datails for your visa…”

Omari: “Okay Nasreen, will send you as soon as we hang up the phone.

Nasreen: “Don’t forget to grant me access to your email address to facilitate the process…”

Tuliongea mambo mengine ya kawaida tu, ni kama vile alikuwa ananipima uelewa wangu maana katika mazungumzo ya nyuma nilimuambia kuwa niliishia darasa la saba. Tulivyoridhika na maongezi ya siku hiyo tulikata simu.

“Hongera mwanangu, naona unapiga ung’eng’e kwa sana siku hizi…” Mama huyu alinisifia..

“Kiingreza chenyewe ‘mwayangu mwayangu’ tu ili mradi tunaelewana inatosha…” Nilimuambia kuwa naongea ‘broken English…’

“Hicho hicho mwanagu cha kuombea maji kitakufaa kwenye safari yako, utazidi kujuwa zaidi ukuenda huko in shaa Allah…” Mama alinitia moyo.

Mama: “Enhe, amesemaje leo!?”

Mimi: “Leo amesema nimtumie nakala za kurasa maalum za passport yangu ili aniandalie visa, visa ikiwa tayari ndio atanitumia tiketi…”

Mama: “Sawa mwanangu, sasa umeshamtumia?!”

Mimi: “Bado, nitamtumia baada ya kuvipiga picha kabla sijalala”

Mama: “Vizuri, sasa basi kesho uende kufanya ile shopping uliyosema, lakini usinunue nguo nyingi, wala begi kubwa, hela yenyewe ‘mkia wa mbuzi’…”

Mama alikuwa hajui uwepo wa milioni nne benki mbali na zile hela nilizokuwa nazo nyumbani ambapo hadi muda huo zilikuwa zimetumika kiasi. Nilitumia kama laki tano hivi, laki tatu hivi kwa maandalizi ya passport na chini ya laki kwa ajili ya yellow card, na matumizi mengine madogo madogo.

Baba wakati anaondoka alimuachia mama kadi yake ya benki ambapo angekuwa anachukuwa sehemu ya hela kama walivyokubaliana wenyewe.

Kuhusu orodha ya manunuzi nitakayofanya wala sikumshirikisha mama, nilijuwa tu angepiga kelele. Kesho yake nilienda Kariakoo na kuanza kufanya manunuzi, mzunguko ulihusu pia maeneo ya Posta mtaa wa Samora, na pia Mlimani City. Hadi narudi jioni nilikuwa nimetumia shilingi milioni mbili kasoro hivi. Nilipunguza idadi ya baadhi ya mahitaji ili nipate chenji ya kutosha, na kweli nilibakiwa na zaidi ya laki tano katika ile bajeti.

Jioni nilimuonesha mama manunuzi yangu, alifurahi lakini nilimdanganya pesa niliyotumia maana angepiga kelele. Alifurahi sana alipoona nimekumbuka kununua kanzu na kofia zake na kuniasa kuwa sasa niwe nafanya ibada kila kipindi badala ya Ijumaa hadi Ijumaa.
---

Wiki moja baadaye Nasreen alinitumia ticket kwa njia ya mtandao, nilitakiwa ku confirm tu tarehe ya safari. Na siku tatu baadaye Nasreen alinitumia ujumbe kuwa nipeleke passport yangu Ubalozi wa Sudani.

Nikaulizia nikaambia uko maeneo ya upanda bara bara ya Ali Hassan Mwinyi jirani na kituo cha utamaduni cha Ujerumani. Nikapeleka passport yangu, baada ya kujitambulisha kumbe tayari walikuwa wana taarifa zangu, hivyo nikawachia passport nami nikarudi nyumbani. Hakika sikujali kama passport ndio itapotea wala nini ilimradi maelekezo nilipata kutoka kwa Nasreen wala sikuwa na wasiwasi.

“We will send your passport to Khartoum, You come wedenesday next week at 9am…” ilikuwa sauti ya mhudumu wa pale ubalozini. Wala sikuwauliza kwanini waipeleke passport yangu huko Khartoum.

Usiku wake tuliwasiliana tena na Nasreen akaniambia kuwa nikishapata visa basi nitakuwa huru kuthibitisha tarehe ya safari. Alinitumia tiketi ya Emirates.

Tangia mama aniusie kuhusu kufanya ibada, nikawa muumini mzuri msikiti wa Kawe maarufu kama Masjid Wastwa. Nikawa najiendeleza kwa masomo ya dini mida ya magharibi hadi isha pale msikitini. Ile chenji iliyobakia kwenye manunuzi yote nilimpatima mama ili aongezee kwenye mtaji wa genge lake pamoja na matumizi yake mengine na ya nyumbani.

Tupio lingine Alhamisi hii panapo uhai na afya…
 
Safi sana....mambo ni moto sana...kiasi kwamba Alhamis inakuwa mbali mnooo.
 
Asante sana, imewahi mpaka rahaaa.
 
Asante sana, imewahi mpaka rahaaa.
Nilipata muda leo nikaona niandike.

Katika kuandika simulizi hii nilisahau kusema kuwa wahusika wakuu wakina Alex, wakina Omari na akina Junior matukio yao hayapo sanjari.

Kila wahusika wana muda wao wa matukio miaka tofauti, lakini huko mbele watakutana na kurindima katika muda mmoja yaani mwaka, mwezi, siku na matukio.
 
Nilipata muda leo nikaona niandike.

Katika kuandika simulizi hii nilisahau kisema kuwa wahusika wakuu wakina Alex, wakina Omari na akina Junior matukio yao hayapo sanjari.

Kila wahusika wana muda wao wa matukio miaka tofauti, lakini huko mbele watakutana na kurindima katika muda mmoja yaani mwaka, mwezi, siku na matukio.
Sawa sawa, hilo tutazingatia barabara!!
 
Shukrani JB
 
Ahsanteni nyote mnaofuatilia simulizi hii, ingawaje nimeandika "ni ya kubuni"
Hata kama .nimefurah sana kwanz fiction stories ndio rasnia yenye pesa ulaya. Huko kina dan brown wanaaandika wanakua matajir vitu vya kweli katika settings unazotaka wewe fanani.big up, manama napakubal sana anko wang yupo huko.
 
Tupio la XXXV – Mzimuni

Ilipoishia…

Haooo, mama Rose, mama wawili na mama Junior wakaondoka kurudi Kihonda ambapo muda huo tayari alasiri ilikuwa imeshaingia mamana kulisikika kengele ya saa kumi kanisa la Kigurunyembe.

Mama Rose na Vai walipofika nyumbani waliwakuta watoto wao wakiwa mezani wanakula wali na maharage waliyopikiwa kabla wazazi wao hawajaondoka lakini pia walikuta wakila nyama ya kuku iliyochemshwa ambapo kulikuwa na paja na sehemu ya mgongo…

Sasa endelea…

Mama Junior: “Nyie mlikuwa bado hamjala tu hadi saa hizi?”

Onesmo: “Tulikuwa tunacheza”

Mama Rose: “He! Na hizo nyma za kuku mmepata wapi?!”

Rose: “Si mlituwekea, mie wakati napakuwa nimekuta mmetuwekea kwenye poti yetu…”

Mama Rose na mama Junior walipigwa na mshangao walipoona watoto wao wanakula nyma ya kuku ambayo hawakuachia. Wao waliandaliwa wali na maharage tu.

“Mama Rose, hebu njoo huku kwanza…” Vai alimwita mwenzake ili watete.

“Enhe, mwenzangu umejifunza nini?...” Vai amumuuliza mama Rose

“Nahisi hizo nyama wanazokula watoto ndio zile tulizoziweka kule mzimuni kwenye shuka jeupe ili mizimu wale….” Alijibu na kushangaa

“Sasa imekuwaje zifike huku na watoto ndio wale….” Vai alishangaa pia kwa kuuliza

“Mwenzangu, hata sijui, makubwa haya, lakini Junior alituambia tusiende sisi ndio tuling’ang’ania…”

“Sasa tufanyeje!?” Mama Junior aliuliza

“Mmh!, tusubiri hadi hiyo kesho mapema tupate majibu ya mganga kwanza kisha tutajuwa cha kufanya…”

“Ok, basi watoto tujifanye tuliwawekea wao ili wasipate wasiwasi…” Vai alisema

Saa kadhaa baadaye jua likazama, siku ikaisha. Asubuhi na mapema akina vai walipitiwa na yule muumini aliyewapeleka kwa mganga kisha wakawahi kwenda huko mzimuni. Ilikuwa mapema sana kabla ya jua kuchomoza. Walifika kwa mganga na wakapokelewa vizuri.

Baada ya maandalizi macheche yam ganga wote watano, yani mganga, msaidizi wake, na akina mama Rose walielekea mlimani chini pale mzimuni.

“Sadaka zimeliwa, sadaka zimepokelewa…” Mganga alisema maneno hayo baada ya kuona vile vipande vya nguo walizoaacha jana havipo na wala zile nyama hazimo na unga uliomwagwa pia ulikuwa umeliwa na kubakia sehemu chache tu.

Mganga akaanza kuongea kwa kubonga kwa muda mrefu kisha akatulia. Muda huo wote pale waliamriwa kukaketi chini na kufanya nusu duara ambapo mganga alikuwa mbele yao na msaidizi alikuwa pembeni ya mganga.

Mganga akwa anaongea kwa lugha isiyoeleweka na msaidizi akawa anatafsiri:-

Mganga: “******£$@####!!”

Msaidizi: “Mizimu imewapokea vizuri, mmepokelewa, mmekaribishwa na wamepokea sadaka zenu…”

Mganga: “£%^&”****~@!!”

Msaidizi: “Mnasumbuliwa na ‘malaika’ wa mama yenu, lakini nia yake ni ulinzi tu…”

Mganaga:” %%%%%$$£””(“)””&^%”

Msaidizi: “Mjukuu wa mama yenu alichaguliwa kuwa kiongozi, hivyo alipatiwa ulinzi maalumu kwa ajili yake na mama yake…”

Mganga: “~@:><%£$£&*()!”£!!”

Msaidizi: “Hivyo msiwe na wasiwasi, lakini mnatakiwa mlete maadao ya sadaka ya kinywaji na mnyama kwa ajili ya usumbufu wa kutuita kutokea mbali..”

Maelezo yaliendelea pale mengi hatimaye mganga akarudi katika hali ya kawaida kisha akamuuliza yule msaidizi wake…

Mganga: “Wamesema nini?!”

Msaidizi akaeleza kama nilivyojaribu kueleza hapo juu na mganga akatingisha kichwa eti ameelewa.

Mganga: “Mizimu wanataka sadaka ya mbuzi kwa usumbufu pamoja na vifaa vya kutengenezea pombe.

Mama Vain a wenzake wakaangaliana kisha wote wakainamisha vichwa chini na kubinua midomo ile kana kwamba kusema mmh, shughuli ipo!

Baada ya hapo waliondoka na kurudi kilingeni kwa mganga na kuagana kwa ajili ya kusubiri hiyo sadaka ya mbuzi na maandalizi ya pombe ambapo waliambiwa na mganga walete, ufuta kidogo, uwele kidogo, ulezi kidogo, mtama kidogo na mahindi kidogo bila kusahau ‘sukari guru’ kidogo.

Waliondoka kurudi Kihonda, lakini kabla hawajaagana na yule muumini mshauri, waliazimia kusitisha lile zoezi la kwa mganga…

“Naona kama tumegeuzwa wateja tena, kila siku mahitaji…” Mama Junior alisema

“Kweli mwenzangu, tuliyo yajuwa yanatosha, tuachane naye”…” Muumini mshauri alichangia

“Mmh, sasa hakutokuwa na madhara kama tusipoeenda?!” Aliuliza mama Rose

“Junior alishatuambia tusiende, sidhani kama tutadhurika, si wamesema wenyewe kuwa tuna ulinzi?!” Mama Junior alijibu na kuuliza

“Mmh, huo ulinzi labda kwa Junior, sisi je tusio na ulinzi!?” Alidakia muumini mshauri

“Yesu si yupo, tumekengeuka tu kwenda kwa mganga, mlinzi wetu Yesu, na kwa jina lake hatutodhurika..” Mama Rose alisema

Walibadilishana maneno pale ya kushaurina lakini hatimaye walihitimisha kutokwenda tena kwa yule mganga.

Mama Rose na Vai walipokuwa nyumbani wakawa wanajadili peke yao…

“Mwenzangu, lakini kama mganga amesema kweli…” Mama Rose alisema

“Ni kweli wanganga wapo ila matapeli wengi siku hizi, mimi kinachonifanya niamini ni vile vipande vya kuku tulivyo vicha mzimuni na kuvikuta nyumbani…” Vai alisema.
---

Majibu ya darasa la saba yalikuwa yameshatoka na Onesmo alifauli daraja “A” na siku chache baadaye yakabandikwa matokeo ya uchaguzi sehemu za watoto kwenda kusoma.

Onesmo yeye alichaguliwa kwenda shule ya Ilboru Arusha. Lakini kwa kufuata ushauri wa ile sauti iliyomtokea usiku hawakushughulika na maandalizi ya shule hiyo bali walianza kuhangaika kutafuta shule za Seminari.

Kwa msaada wa shule aliyosoma Junior, hatimaye alipata Seminari iliyopo Mbulu iitwayo ‘The Sacred Heart Prepaeudetical’.

Jumapili panapo majaaliwa nitatupia ndefu ndefu.
 
Ngoja nishuke nayoo
 
Dah utamu unakata
 
Mganga: “~@:>

Asante sana JB
 
Back
Top Bottom