Tupio la XXXVII – The Party
Endelea…
Nilivyorudi nyumbani Manzese wakati natafuta usingizi, whatsapp msg kutoka kwa Mourine iliingia…
“Hi Handsome, nimekumiss ujue, halafu nisamehe kwa kukukatalia kuangalia msg kwenye simu yangu, lakini ipo siku utajuwa kwanini, muda bado, naisubiri kwa hamu hiyo party ya kesho. Umesema umewaalika na marafiki zako?!”
Mimi: “Okay, ndiyo nimewaalika washkaji wa chuo, sio wengi lakini nataka tufurahi pamoja.”
Tulisogoa mawili matatu kisha tukaagana, mimi nikaendelea kuutafuta usingizi.
Kule Masaki nyumba yetu (yangu) na nyumba ya akina Emilia ni mjengo wa aina moja, yani kila kitu kilijengwa sawa, Wazazi wa Emmy wote wawili walikuwa wanafanyia Mamlaka ya Bandari pia.
Kwa upande wa Zai tangia siku ile tuamke wote nyumbani pale Manzese, ni kama alikuwa ananionea aibu hivi, muda mwingi alikuwa ananikwepa kukutanisha macho ingawaje msg zake zilikuwa hazikatiki kwenye simu yangu.
“Ahsante, umeufungua moyo wangu upya…”
“Ulinikamua vizuri siku ile, upwiru wote umeisha, niliinjoi sana…”
“Nimesha-msahau sasa Hemedi, apotelee huko huko…”
Yani kwa siku nilipokea msg zake za namna hiyo zaidi ya 17.
---
Usingizi ulinichukua, nilizinduka alfajiri kwa ajili ya kwenda haja ndogo, baada ya hapo nikaanza maandalizi madogo kwa ajili ya chuo na kuweka utaratibu vizuri kwenye karatasi kwa ajili ya party ya jioni.
Kabla sijaenda chuo nilipitia kwanza kule Masaki kuangalia maandalizi, nilikuta Mlinzi na house maid wapo vizuri kama nilivyo waelekeza, nyumba kwa nje ilipambwa vizuri eneo ambalo ndilo nilitarajia tungeanzia kufanya party yetu na kisha kungekuwa na kipande cha kuizindua nyumba ambapo tungeingia ndani.
Waliandaa alama ya tambala la tangazo lililoandikwa kuashiria part iko nyumba ile. Nilifurahia sana ubunifu ambao baadaye nilijuwa kuwa ulitoka kwa vijana walinzi wa SumaJkt.
Tulimtumia mwanachuo mwenzetu mmoja kuchukuwa kazi ya kutuandalia chakula, maana dada yake huwa ana shughulika na kazi hizo za catering, kwa uzoefu wake tulijuwa kuwa hakuto haribika kitu na tenda hii ilikuwa tofauti kabisa na alivyozoea kwenye maharusi nk.
Ilihitajika uchomaji wa nyama za mbuzi, ng’ombe na kuku wa kienyeji kwenye viwanja ya nyumba (ndani ya uzio. Nyumba ilikuwa na uzio mkubwa sana wa ukuta wa matofali. Kulihitajika viazi mbatata vya kuchoma na pia chips zake na vikorombwezo vingine.
Baada ya muda wa chuo, kukawa na msafara usio rasmi kwa baadhi ya waalikwa wakinifuata kuelekea Masaki, wengine walipitia sehemu wajuazo kwanza kisha wakaungana nasi kwa kutumia gps location, kwenye hili la kukaribisha wageni, Emmy alinisaidia sana.
Saa kumi na mbili jioni tayari magari ya walikwa yalikuwa yamejaa sehemu za kuegeshea ndani ya uzio nan je ya uzio, wote niliowaalika walikuja pamoja na wazamiaji wachache (partners), watu walianza kunywa, kula nyama na kuburudika na miziki mbali mbali kabla hata shughuli yenyewe haijafunguliwa rasmi.
Mourine naye akafika kwa kuchelewa lakini aliwahi kabla ya tamko la kufunguliwa kwa party, Emmy alikuwepo tangia mwanzo na alijipa kitengo cha ukaribishaji, ajabu siku hiyo sikumwona yule msanii wake.
Niliifungua party rasmi kwa kutangaza kwamba imefunguliwa, baada ya kuwashukuru waalikwa wote walifika, na kwamba madhumuni ya party ile ilikuwa kuizindua nyumba ambayo tuliitelekeza kwa miaka kadhaa na sasa tumerudi tena. Nilitumia wingi ili kuonesha siko peke yangu mle ndani.
“Kwa wazazi wake hapa, nyumba za Bandari hizi…” alisikika jamaa mmoja akimwambia mwenzake
“Nyumba zimeshauzwa hizi, itakuwa wameinunua…” alimjibu mwingine kurekebisha
“Pazuri sana, hewa safi, upepo mzuri kutoka baharini, na bustani umeandaliwa vizuri…” mdada mwingine alichangia
Ilikuwa furaha sana, huku Emmy akijisogeza sogeza kuonesha tupo jirani…
Baadaye kidogo nilimuashiria Dj Bony asitishe mziki ili nitoe utambulisho, maana kuna watu kadhaa mule ndani walikuwa hawajuani…
“Eeee napenda kuwatambulisha kwenu dada yangu mpenzi Mourine, (nikamshika bega), yeye ni mjasiri-amali yupo hapa hapa Dar na anaishi maeneo haya haya ya Masaki…”
Waalikwa tayari walikuwa na vinywaji kichwani, walipiga makofi…
“Pia yule pale ni house keeper wetu anaitwa Alice, yule kule mzee wetu anaitwa Nchumari bila kuwasahau walinzi wetu kama mnavyo waona na timu ile kule ya catering ni ya dada Neema…”
“Tuendelee kuburudika na baada ya muda mfupi tutaizindua nyumba kwa kuitembelea angalau sehemu chache…, Dj!”
Mziki ukaweka na watu wakaendelea kufurahia. Hapakuwa na ratiba ya kula lakini kila mtu akihitaji chochote yeye mwenyewe alikuwa anaenda kule upande wachomapo nyama na kuchukuwa sehemu anayoridhika kwa aina ya nyma aitakayo na kuendelea kuparty .
Ingawaje kulikuwa na viti vya kukaa, lakini muda mwingi watu walikuwa wamesimama huku wakinywa vinywaji vyao pendwa.
Baada ya muda ikafika wakati wa kuitembelea nyumba kwa sehemu nilizochaguwa watu wafike, tukaanza kuingia ndani na kufika sebuleni ambapo tulisimama, palikuwa pamependeza sana, yani sana hadi Emmy alishindwa kujizuia…
“Hongera Alex, umebadilisha kabisa muonekano wa ndani, sio kama kule kwetu…” alisema hivyo huku ‘akinipalatia’, Mourine alikuwa mtulivu sana, Zai wala hakuonesha lolote ila uso wake ulikuwa na furaha.
Tulivyomaliza ziara ya mle ndani tukashuka chini na kurudi kuendelea na kuburudika kwa nyama na vyakula vingine na vinywaji vilikuwa havikauki. Wengine walianza kuchukuliwa na ulevi ikanibidi nimuombe Dj Bony asitishe mziki ili nitoe tangazo…
“…Pamoja na kuwashukuru kwa kuitikia wito wa kujumuika nasi hapa, kuzindua nyumba, kula na kunywa na kufurahi lakini pia nina tangazo rasmi leo…”
Pakawa na ukimya kila mmoja akijiuliza ni tangazo gani…
Dj Bony kama nilivyompanga aliweka wimbo wa kuchombeza taratibu wakati naanza kuongea…
“…Tangazo lenyewe ni kwamba leo rasmi nawatangazia mpenzi wangu ….”
Utulivu ukazidi
“Tangia nimeanza uhusiano naye, moyo wangu umetulia, yeye ni mpole, mnyenyeku na ana sifa zote za kuwa mke bora…”
Watu wakawa wanaangaliana kisha macho yote yakawa yanamuelekea Mourine ambaye ndiye wanachuo walikuwa hawamjui lakini hapo alionesha ukaribu sana nami ingawaje nilimtambulisha kuwa ni dada.
“…Kwa sababu hiyo basi, napenda wote humu na dunia yote ifahamu kuwa….”
Wafukunyuku wakawa wanarikodi lile tukio kwa simu zao, kumbe wengine walikuwa wapo live tiktok na youtube wakirusha baadhi ya matukio…
“….napenda mfahamu kuwa kuanzia sasa Zaituni Nassoro Ahmed ndiye mpenzi wangu mpya!....”
Watu wengine walishangaaa, wengine walifurahia na nderemo na vifijo vikasikika…
Nikamsogelea Zaituni ambaye muda wote wala hakutaka kuonesha kama yupo karibu nami kimahusiano isipokuwa Emmy tu ndio ambaye angeweza kuhisi kutokana na siku ile tulivyokutana kule Rombo Green view Hotel…
Emmy alikuwa ameduaa kama ameloweshwa maji, akiwa amesimama huku mikono yake yote miwili akishika mdomo wake kwa kufanya kama anauziba…
Nikazidi kumsogelea Zai ambaye sasa alikuwa anaona aibu huku akitabasamu, kichwa ameinamisha chini huku akinema nema!
Nikapiga goti moja…
Watu wote mle ndani walilipuka kwa shangwe hata kabla sijasema neno…
“Zai…” nilisema na watuwakitikia weweeeeeeee!
“Zai, will you marry me!?”
Nikatoa kasha ya pete uchumba kisha nikaifunua lile kasha na ile pete kuonekana… nikishikilia kusubira response ya Zai.
Badala ya kujibu akawa anaruka ruka kwa furaha huku akiwa anafunika macho kwa aibu na furaha…
Waalikwa wakawa wanasema..
“Say yes, say yes!”
Bado nikiwa katika hali ile ya kupiga goti, Zai alinisogelea huku akirusharusha miguu kwa furaha kama anapiga maktaim na kunyoosha mkono wake huku akisemaa…
“Yes Alex, I will” Nikamvalisha pete maridadi kabisa ya uchumba
DJ naye hakuwa mbanizi wa kufuata maelekezo, ilipigwa bonge la blues ambapo nilisimama na kumkumbatia Zai huku tukishangiliwa na waalikwa…
“Jamani, Emmy ameanguka!” tulikatishwa ghafla na sauti ya Laula, rafiki yake Emmy
Mourine fasta akamsogelea Emmy na kuanza kumkagua…
Mziki ukazimwa na wote tukawa tunamwangalia Emmy
“Anapumua, mlazeni ubavu wa kulia…” Mourine aliamrisha
Mara Emmy akainuka mwenyewe akawa amekaa na akaanza kulia….
Akainuka na kuchukuwa mkoba wake kisha akatoka nje ya geti na kutokomea…
“Mfuateni, asije akaenda kujigongesha barabarani…” Mourine alisema kuwaambia wenzake ambapo Laura na Rachel walimfuata, Mlinzi mmoja akaongozana nao, Emmy alionekana akitembea harakaharaka akielekea numbani kwao huku akilia.
“We Alex, ungeua mtoto wa watu!” Mourine alisema huku akiwa amekasirika…
“Dada, hujui tu huyo alichonifanyiaga, leo hii ni zamu yake. Hata hivyo yeye alishaniacha siku nyingi na ameshabadilisha mabwana wawili sasa hivi yupo na msanii (nikamtaja), hivyo hana sababu ya kuumia wala kuhuzunika, Emmy siyo mpenzi wangu…” Nilimjibu Mourine
“Kama siyo mpenzi wako mbona kazimia!, nyie mna yenu!” Mourine alikazia
“Hakuna lolote dada, muulize Zai, ni yeye Emmy alitutambulisha pia kwa mpenzi wake mpya huyo msanii na Zai ni shahidi…” Nilimjibu
Tuliobaki mule ndani tukapata wasaa wa kukaa kwenye viti na stori zikawa za Emmy na tabia zake na jinsi nilivyolipiza kisasi kimtindo.
Zai kuanzia hapo muda wote alikuwa hakai mbali nami, alikuwa mwenye furaha sana na uso ulikunjuka kisawasawa!
Tuliendelea kunywa na kula huku waalikwa wakitupongeza…
“Halafu nyie watu mna siri, kumbe mna date halafu wadau hatujui…!” Margareth alisema kiushabiki
Itaendelea…