Simulizi: My family

Simulizi: My family

Kim hakika wewe ni mwandishi mzuri sana nimependa Kila kilichomo kwenye story✊🏿
Unaendelea saa ngapi😂
Ni juma tatu mkuu ila baada ya hapo nitakuwa naiweka Alhamisi na juma tatu. nataka nijipe muda wa kuandika kwa utulivu si unajuwa hii simulizi yenyewe nimeileta kwa mihemko ya mapenzi🤔
 
Kwanini hujui kiswahili
Kwa sababu ya mazingira ambayo nimekulia, nimekulia vijijini ambako kiswahili ni lugha ya dharura kuongeleka na hata kinapo ongelewa hutamkwa tofauti na kiswahili cha taifa (cha darisalama)

Hiyo ndiyo sababu ninashindwa kitamka vizuri baadhi ya matamshi ya kiswahili, japo siachi kujifunza kila ninapokosolewa.
 
Kwa sababu ya mazingira ambayo nimekulia, nimekulia vijijini ambako kiswahili ni lugha ya dharura kuongeleka na hata kinapo ongelewa hutamkwa tofauti na kiswahili cha taifa (cha darisalama)

Hiyo ndiyo sababu ninashindwa kitamka vizuri baadhi ya matamshi ya kiswahili, japo siachi kujifunza kila ninapokosolewa.
Safi sana
 
Simulizi: My family
Sehemu ya pili
Mtunzi: Kijana Masikini


ILIPOISHIA
"Daa Qashy nae akapanda bodaboda na kumpa ishara dereva aifate pikipiki aliyopanda yule mzee. Muda huo watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, mimi nikaenda sehemu aliyotupa simu Sista na kukuta imepasuka kama unavyo iona, baada ya hapo nikachukuwa simu yangu ili nikupigie lakini iligoma mtandao, nikaazima simu ya mshkaji hapo jirani nilipopiga namba yako ilijibiwa haipo"

Aliongea Mshamba huku akininesha simu iliyo kwenye kiti ambacho hukaa Qashy Lilith.

"Ooophwwwwwwww......"
Nilishusha pumzi huku ubongo wangu ukifanya mchakato utakaoamua ni swali lipi liwe la kwanza kumuuliza Mshamba, kwani hadithi aliyonipa imeniacha na maswali ambayo hata idadi yake tu siijui

ENDELEA

"Dah ni nini hiki au Qashy alikuwa sirias"
Niliongea huku nukikumbuka kama majuma mawili nyuma Qashy aliwahi kuniuliza ikitokea yeye amekufa nitaishije bila uwepo wake, nikamjibu sijuwi nitaishije kwasababu haijatokea.
Akaniambia kifo chake kwangu kipo karibu hivo anaomba siku tutoke nje ya mji sehemu ambayo itakuwa na utulivu mkubwa mno ili awe huru kufurahia penzi langu kwa masiku ya mwisho.

Nilimchukulia Qashy kama mtu ambae akili yake haipo sawa pengineni kwa sababu ya mambo ya biashara yake ama ni mambo mengine, nilijaribu kumuuliza maana ya maneno yake lakini alisema atanieleza vizuri siku tukiwa mbali, yaani tukiwa nje ya mji kama alivo taka. alikuwa amelaza kichwa chake kifuani pangu, nikamuitikia kila alichokiongea usiku ule huku nikimchezea nywele zake, nilimshushia mtanange mzito ndani ya usiku ule kuirudisha akili yake katika hali ya kawaida mrembo huyo mwenyewe asili ya kichaga ambae ni mrefu mwembamba na mweupe kiasi.

"Mshamba naomba tufunge hapa twende nyumbani hapa hatutaongea kwa uhuru"

"Sawa bro"
Tukafunga duka na kuchukuwa bajaji, Umbali kutoka soko kubwa dadi kufika nyumbani ninapoishi ni mdogo sana, kwa mwendo wa mguu ni kama dakika nane tu.
Ndani ya muda mfupi tu tukawa nyumbani.

"Halafu bro umesahau samaki kule dukani"
"Tuachane nao twende tudili na hili jambo la msingi"

Tukaingia ndani kisha nikaanza kumhoji Mshamba maswali mengi kuhusiana na utowekaji wa Qashy.

Japo Mshamba alieleza mengi lakini yote yalikuwa yanaendana na maelezo aliyonipa kule dukani hapakuwa na jambo ambalo ni ziada sana.

Ila kitu nilichokigundua mpaka sasa hivi ni kwamba watu wa karibu wa Qashy namba zao za simu zimefungiwa ama zimesitishiwa huduma.

"Mshamba. hapa sasa wewe nenda nyumbani mimi naenda kwa Qashy. Asubuhi kafungue goli kama kawaida ila kama utahisi unahitaji kupumzisha akili basi utabaki nyumbani tu"

"Poa bro nitaangalia hiyo asubuhi nitaamka vipi, ila kuwasiliana ingekuwa ni vizuri zaidi ili mimi pia nijuwe ni nini kitakacho endelea utapoenda kwa Daa Qashy"

"Ni kweli lakini sasa mimi sina muda wa kusajili laini zingine, hii ni saa kumi na dakika thelathini na moja natakiwa niwahi ili pengine tunaweza kupata mwanga wa hiki kinacho endelea"

"Poa bro ila mimi nitapita pale dukani kuchukuwa simu ya Daa Qashy na kuwatoa wale samaki maana hadi kesho wataharibika"

"Kachukuwe samaki tu simu iache humo humo kwa usalama zaidi"

Akaitikia Mshamba hachekwi na kutoka ndani ili kuelekea nyumbani kwao mtaa wa majengo anako ishi na wazazi wake.

Nikatoka ndani na kuingia barabarani kuianza safari ya kuelekea kwa Qashy Mtaa wa kiangu ambako amepanga.

Nikasimamisha pikipiki ambayo ilikuwa inakuja kutokea mbele yangu.

"Nipeleke nangwanda bro"

Dereva bodaboda akaigeuza pikipiki nikapanda.
Baada ya kama dakika mbili tu tukawa tumefika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona. Nikashuka na kumlipa, nikaanza kutembea kuelekea nyumbani kwa Qashy. Nikatembea taratibu mno huku nikiiona kwa mbali nyumba anayoishi Qashy lakini mazingira yalikuwa ni ya kawaida mno, niliwaona watoto wa kike Mama mwenye nyumba wakicheza mdako huku dada mmoja ambae ni mpangaji mwenzake Qashy alikaa kwenye kibaraza anachezea simu.

"Habari Evelyn"
Nilimsalimia Dada huyu anaeitwa Evelyn Salt baada ya kufika alipoketi

"Salama shemeji habari za masiku"
"Salama nashukuru, hivi Habibi wangu yupo ndani?"

"Hapana, alikwenda kazini tangu asubuhi hajarudi, yeye kama kawaida yake kurudi ni jioni sana vipi hujamtafuta kwenye simu?"

"Hapatikani kwenye simu"

"Ahaa ngoja nimjaribu mimi"
Aliongea huku akipangusa simu yake.

"Hii! hivi watu wa nyumba hii leo tuna nini"
Aliongea Evelyn baada ya kujibiwa namba anayopiga haipo

"Mmm vipi?"

"yaani mimi unaponiona hapa hii line nimetoka kusajili sasa hivi laini zangu zote zimezuiliwa huduma, na hata hivyo nimejaribu kurenew zote zime goma, Mama humo ndani nae hivyo hivyo laini pia hadi baba pia nae katoka kwenda kurenew, sasa nashangaa nampigia Qashy nae wanajibu namba haipo! Cha kushangaza zaidi watu wengine mtaani kote huko nilikopita hakuna mwenye hiyo shida"

'Hivi huyu Qashy alikuwa ni nani! Hivi kulikuwa na Qashy Lilith mwingine nyuma ya huyu ninaemfahamu? Halafu kwanini alimwambia Mshamba kwamba aliipenda pesa kabla yangu'

"Kim Babaangu habari"

Ilinitoa mawazoni sauti ya Mama Edina Mama mwenye nyumba hii, nikageuza kichwa na kumtazama mlangoni alipo simama.

"Aa.. Salama Mama Habari za tangu juzi"

"Salama namshukuru mungu. nakuomba tuongee kidogo"

Aliongea Mama Edina huku akizama ndani, nami nikamfata tukapitiliza hadi nyuma,
Mlango wa chumba cha Qashy ulikuwa umefungwa.

Mama Edina akaketi kwenye kiti cha plastiki nami nakaketi kwenye kiti cha pembeni yake.

"Kim.. wewe ni kama mwanangu, mwenzako Qashy nae ni mwanangu pia hivo kila nitakacho kuuliza naomba unipe majibu ya kweli ili nione namna ambavyo naweza kuwasaidia"

Taratibu moyo wangu ukaanza kuongeza kasi ya mapigo yake huku nikimtazama Mama Edina usoni kwani sijuwi anataka kuniambia nini.

"Kim katika siku za hivi karibuni mahusiano yenu yapo katika hali gani?"

"Tupo vizuri tu Mama, vipi kwani kuna tatizo"

"Ndiyo kuna tatizo ndiyo maana nikakwambia nataka unipe majibu ya kweli"

"Sisi tupo sawa tu si unaona hadi juzi nimekuja hapa na wote tulikuwa na furaha tu, tena hadi tukawa tunataniana kama kungalikuwa na shida kati yetu unadhani tungeweza kuwa katika hali ile! Kwani kuna nini Mama hadi uniulize hivo?"

"Unacho kisema kinalandana na ukweli lakini sitaki kuamini kwamba hamuna tatizo kabisa. hujawahi kulala na mwanamke mwingine labda au hata kutongoza mwanamke mwingine?"

"Hapana mamaangu sijawahi kwa hivi karibuni labda zamani kidogo wakati mapenzi yetu hayajafikia kuwa ya wazi"

"Ni kama muda gani na ulimtaka tu huyo mwanamke au ulilalanae kabisa?"

"Kipindi hiko penzi letu lilikuwa na kama mwezi tu, kama inazidi basi ni siku chache, na sikuwahi kulala nae huyo mwanamke, kiufupi ni kwamba tangu niwe na Qashy sijawahi kukutana kimwili na mwanamke mwingine"

"Ahaa nimekuuliza hivo kwa maana, ni kama mwezi huu hali ya Saikolojia ya Qashy haipo sawa, muda mwingi anakuwa ni mtu wa kujiudhi sana na hata uchangamfu wake kwa ujumla haupo kama zamani. mwili wake pia umepungua kiasi Qashy wa miezi mitatu nyuma sio huyu wa leo, sasa kile kitu alichokibeba na kuwa katika hali ile haifai kabisa, inatakiwa awe mtu wa furaha kama anavyoishi siku zote, tena ikibidi furaha yake iongezeke. Ndiyo maana nikakuuliza haya ili kama kuna mahali mnakwaruzana katika safari yenu nione ni kwa namna gani naweza kuwasaidia"

"Umesema kitu alicho kibeba haifai awe katika hali ile ni kitu gani kakibeba?"

Nilimuuliza huku nikimtazama usoni kwa umakini wa hali ya juu.

"Unamaanisha hujuwi kwamba Qashy ni mjamzito?"

"Mjamzito!"

"Eee kwani hajakwambia?"

"Hapana hajawahi kuniambia kwahiyo wewe umejuwaje au amekwambia mwenyewe"

"Hahahah.. eh nyie watoto wa kiume kwenye mambo haya mungu kawafumba pakubwa. kwahiyo mpaka mnalala kitanda kimoja na bado hujuwi tu kwamba ni mjamzito! Yale mapua yake nayo huyaoni kwamba yanazidi kutanuka? Una muda gani sasa hujawahi kumuona Qashy anakula samaki?"

Nikakaa kimya huku nikiyatafakari maneno ya Mama Edina ambayo yamekuja na mshangao mkubwa sana kwangu.
Ubongo wangu taratibu ukaanza kurudisha kumbukumbu za mara nyingi ambazo nimewahi kula chakula pamoja na Qashy na akawa anakwepa kabisa mchuzi wa samaki au kula samaki hata kama kakaangwa.
Kigezo chake kilikuwa ni kwamba amekula sana samaki tangu tumekuwa pamoja hivyo sasa wamemtosha.
Wajawazito wengi huwa na changamoto ya kutapika pindi wanapo kula samaki au kitu chochote chenye shombo kupindukia, hasa ujauzito unapokuwa na miezi michache.

"Vipi mbona upo kimya? Qashy ni mjamzito mimi sijampima wala hajaniambia ila ni mjamzito, tena haupungui miezi mitatu hivyo jiandae kuitwa baba kama hujawahi kuitwa"

"Mh sawa kwahiyo Qashy mwenyewe tangu atoke asubuhi ndiyo hajafika tena?"

"Eee kama alivokwambia Evelyn"

Nikawaza kwenda kufungua chumba cha Qashy lakini nikakumbuka funguo ya chumba chake sijaibeba nimeiacha nyumbani.

"Sawa Mama nitajitahidi kuona ni changamoto ipi inamsumbua ili tuweze kuitatua"

"Sawa ila usimwambie kuhusu suala la ujauzito kwa sababu atajuwa mimi ndiyo nimekwambia kwani nimeshamuona anatapika kama mara mbili hivi kila alipojaribu kula samaki, lakini katika hizo mara mbili zote alijitahidi kujifanya yupo sawa tu ni tumbo tu ndio linamsumbus ila mimi ni mtu mzima naelewa, na baada ya hizo mara mbili amebadilisha kabisa aina yake ya ulaji"

"Sawa Mama nashukuru kwa kunifumbua macho"

Nikamuaga Mama Edina na kutoka ndani huku nikitawaliwa na mawazo mengi.

'Mh mbona nashindwa kabisa kuelewa kabisa haya mambo, kama kweli Qashy ni mjamzito kwanini asiniambie? Kwanini pia aondoke katika mazingira ya namna hii, Inaamaana ndio kaondoka kweli? Lakini pia kwanini karibu kila namba ya mtu wa karibu imefungiwa mawasiliano, aaah haya mambo ni magumu. amesema anajuta kwanini aliipenda pesa kabla yangu , pia nisimtafute siwezi kumuona kwa jitihada zangu, Inaamaanisha ameondoka huku akijuwa kuwa ana mimba! Na hiyo mimba yang..?'

"Jamani shemeji unaondoka bila hata kuniaga?"

Ilinishutua sauti ya Evelyn Salt nikiwa katika msitu mkubwa wa mawazo, nikageuka nyuma na kimuaga kisha nikaondoka.

Nikatembea hadi karibu ya uwanja wa Nangwanda Sijaona, nikasimama chini ya mti uliopo nje ya uwanja huu huku mawazo bado yakiendelea kuniandama, muda huo ilikuwa ni kama saa kumi na moja na dakika kadhaa.

'Mh naanzia wapi kumtafuta huyu mtu, najuwa tu kwao ni moshi, sijuwi ni Mtaa gani kata wala wilaya, sijuwajui wazazi wake wala ndugu yake mmoja, isivyo bahati pia hana rafiki wa kudumu. mh nitaanzia wapi? nadhani teknolojia ndiyo inaweza kunisaidia kwenye hili, Ahaa ngoja nikamshirikishe Joanah pengine anaweza kunisaidia, ni mambo mengi huwa ananisaidia tena mengine huwa ananilaumu kwanini sikumwambia mapema. Joanah anaweza kuwa msaada kwenye hili sina cha kupoteza'

Mwili wangu ukapata nishati mpya baada ya kumkumbuka rafiki yangu Joanah ambae anafanya kazi TIFFANY DIAMOND HOTEL iliyopo karibu kabisa na soko kubwa la mtwara.
ITAENDELEA


Nakaribisha maoni, maswali, ukosoaji.
Nakini pia nakaibisha ushauri wa kiutunzi na kiuandishi.
 
Simulizi: My family
Sehemu ya tatu
Mtunzi: KIjana Masikini

ILIPOISHIA
'Mh naanzia wapi kumtafuta huyu mtu, najuwa tu kwao ni moshi, sijuwi ni Mtaa gani kata wala wilaya, sijuwajui wazazi wake wala ndugu yake mmoja, isivyo bahati pia hana rafiki wa kudumu. mh nitaanzia wapi? nadhani teknolojia ndiyo inaweza kunisaidia kwenye hili, Ahaa ngoja nikamshirikishe Joanah pengine anaweza kunisaidia, ni mambo mengi huwa ananisaidia tena mengine huwa ananilaumu kwanini sikumwambia mapema. Joanah anaweza kuwa msaada kwenye hili sina cha kupoteza'

Mwili wangu ukapata nishati mpya baada ya kumkumbuka rafiki yangu Joanah ambae anafanya kazi TIFFANY DIAMOND HOTEL iliyopo karibu kabisa na soko kubwa la mtwara.

ENDELEA
Nikaita pikipiki ambayo ilikuwa imepaki kwenye eneo la gereji.

"Nipeleke Tiffany bro"
Kijana huyu muendesha pikipiki akaitikia na kuindoa pikipiki kwa mwendo wa taratibu, tukaingia kwenye barabara ya lami inayoelekea bima mataa.
"Bro nakuuliza unashuka kwenye jengo lenyewe la Tiffany au unashuka pembeni yake"

sauti ya bodaboda huyu ikanitoa katika dimbwi la mawazo.

"Ni Tiffany penyewe mkuu, nilikuwa sijakusikia"

Baada ya muda mfupi tukawa nje ya jengo hili la Tiffany hotel.

Nikamlipa boda hela yake, nikaanza kupiga hatua kuelekea kwenye mlango wa jengo hili.

"Karibu bosi"
Aliongea jamaa mmoja ambae alikuwa anatoka nje, aina yake ya mavazi na usmart wake ulinijulisha kuwa ni miongoni mwa wafanya kazi wa hapa.

"Asante kaka habari yako"

"Salama tu karibu nikusaidie"

"Asante ninashida na dada mmoja anaitwa Joanah"

"Ahaa sawa, ingia hapo ndani kuna dada yupo atakusaidia hilo"

"Poa"

Nikaingia ndani ya jengo hili ambalo sio mara yangu ya kwanza kuingia.
Nikamkuta mdadaa anaeshughulika na kupokea wageni akiwa kwenye kiti ambacho mbelevyake kuna meza kubwa kiasi. Mdada huyu huwa namkuta mara kadhaa ninapofika hapa ila sijalifahamu jina lake.

"Habari za jioni"

"Salama habari yako kaka"

"Nzuri tu nina shida na Joanah"

"Hayupo amesafiri"

"Ameondoka lini na amekwenda wapi"
" No Ushiled mwambie nakuja hapo sasa hivi namkuta, dakika moja"

Niliisikia sauti ya Joanah ambayo nilijua tu kwamba imetoka katika kifaa kama simu au radio lakini sikujua kifaa hiko kipo wapi kwani Mdada huyu anaeitwa Ushiled hana kifaa chochote mkononi mwake.

"Sawa Dada"

Ushiled aliitikia kwa sauti ya juu kidogo, huku akigeukia upande wake wa kulia ikanifanya nigundue kuna kifaa cha mawasiliano katika ukuta.

"Kaa hapo kwenye kiti umsubiri"

Sikutaka kumuuliza Ushiled kwamba kwanini alinijibu Joanah kasafiri wakati inaonekana wazi kuwa yupo ndani ya hili hili jengo.
Nikakaa kwenye kiti ambacho nielekeza huku kila aina ya sauti nikiisikia kichwani mwangu kutokana na mgongano wa mawazo.

"Kaka unaoneksna una tatizo"

"Hapana, kwa nini umeniuliza hivyo?"

"No sio kwa ubaya lakini mara chache unapofika hapa naona unakuwaga mchangamfu sana"

"Ahaa kumbe unanifahamu vizuri tu, sasa kwa nini ulikuwa unanikazia kumuona Joanah"

"Ni maelekezo yake, ana mgeni leo ndio maana alihitaji muda mwingi wa kupumzika, ila pole nakuona unajitahidi sana uonekane upo sawa lakini mwili wako tu unakukataa"

"Ah haya tufanye ndiyo umeyajua matatizo yangu una nini cha kunisaidia?"

"Hahaha! Ninaweza kuwa na cha kukusaidia pengine umeachwa je"

Kauli hii ikanifanya nitabasamu kidogo huku nikimtazama mwanadada ambae chini amevalia sketi fupi nyeusi, juu amevaa shati jeupe lililomkaa vizuri huku kifuani pake pakiwa dede haswa.
Kwa kumtazama tu Ushiled umri wake haupungui miaka ishirini na miwili na wala hauzidi miaka ishirini na mitano.

"Yaani umeaminiwa kupewa ofisi kubwa hivi na bado muda wa kazi unawaza ngono"

"Ha! Mtu anawaza ngono wakati yupo kwenye sala itakuwa kwenye kazi, hivi mna mahusiano gani na Sister Nah nje ya kumuuzia samaki?"

"Kwanini unaniuliza hivyo?"

"Sister hapendi kabisa ukaribu na vijana wa mtaani nashangaa mmekuwa na mazowea sana"

"Kwahiyo mimi ni kijana wa mtaani siyo"

"No sijamaanisha hivyo ambavyo wewe unataka kutafsi.."

"Ila umemaanisha nini?"

"Hahaha.. Jamani, em niachie namba yako kwanza nataka siku tukae mahali tuongee"

"Sina simu hapa na siikumbuki kichwani"

"Ok ningekuandikia namba yangu ila Sister anakuja"

Nikatazama upande ambao Ushiled alitazama kwa jicho la kuibia, nikamuona Joanah akiwa amevalia gauni refu jekundu.

"Karibu Kim"

Alinisalimu Joanah huku akisogea nilipo.

"Asante mambo vipi?"

"Poa tu, nashukuru umekuja mwenyewe maana nimekutafuta kwenye simu sijakupata, nina mgeni wangu nataka nimpikie supu flani matata ya Samaki, ili akirudi kwao abaki kuikumbuka mtwara na pia kunikumbuka mimi. twende hivi basi tukaongee maana naona wewe pia kuna shida imekuleta"

Tukatoka na kuelekea kwenye chumba kidogo ambacho mara nyingi huwa naingia nikiwa na mazungumzo na Joanah.

" mh Kim vipi za masiku"

Aliongea Joanah huku tukikaa kwenye viti ambavyo katikati yake kuna meza ndogo ya kioo.

"Mimi namshujuru mungu naendelea kupumua, lakini kuna jambo linanitafuna mno na ndio maana nimekuja kwako"

"Jambo gani hilo"

Nikamsimulia Joanah kila kitu kilichotoke kuanzia kutoweka kwa Qashy Lilith dukani kwake, laini za watu wake wa karibu kufungiwa, hadi habari ya ujauzito ambayo amenipa Mama Edina
Mwisho nikamuomba anisaidie kumpata Qashy au kujwa alipo.
Haikuwa shida kumpa maelezo kumhusu Qashy maana anamjua kwa sura kwani nilishawahi kumtambulisha kwake.

"Mh huyo kijana anaefanya kazi dukani kwa Qashy yupo wapi sasa hivi"

Aliniuliza Joanah baada ya kumsimulia mkasa mzima.

"Amekwenda kwao"

"Ahaa huyu nitamuhitaji asubuhi ya saa mbili najuwa huyu nitaweza kumuuliza baadhi ya mambo ambayo yanaweza kunisaidia katika kujuwa Qashy alipo. Pia ngoja nikupe karatasi uandike namba za simu za Qashy"

"Sawa nitamleta hapa hiyo asubuhi"

"Hapana hupaswi kumleta wewe wala kwao hupaswi kwenda, kwakuwa umesema wote mmepoteza mawasiliano mtafute bodaboda anaepajuwa kwao ndiyo amfuate hiyo asubuhi na asimlete hapa kuna mahali nitamwambia ampeleke.

Pia yule bodaboda wako ambae nae amefungiwa laini usimtumie chochote kuanzia sasa hadi pale tutakapo pata majibu ya hili. Sidhani kama kuna jambo lolote la kutisha kwenye hili ila ni vizuri tukaweka kinga kwenye baadhi ya mambo pengine kukawa na mengine ambayo hatuyawazii"

"Sawa nitashukuru sana Joanah"

"Usiwaze Kim kitu kikubwa cha kuzingatia usitoke kwenye mfumo wako wa kawaida wa maisha hili umeshaliweka kwenye mikono yangu igiza kama limekwisha, japo najuwa ni ngumu lakini utalazimika kuishinda hii hali"

"Sawa swahiba, najua hujawahi kufeli Kwenye jambo langu. nitafosi niwe katika hali ya kawaida hapa itabidi niingie hapo sokoni kwanza ili nidake laini kwa ajili ya mawasiliano maana hapa kila kitu kitasimama bila ya mawasiliano"

"Sawa lakini hiyo laini utakayo sajili usiongelee taarifa yoyote ya ndani kumhusu Qash, pia nitakupa laini kwaajili ya kuongea na mimi tu hadi pale tutakapopata majibu ya kueleweka"

"Sawa"

Joanah akatoka na kuniacha, baada ya kama dakika mbili hivi akarudi akiwa ameshika peni, karatasi nyeupe pamoja na simu.
Nikamwachia namba ya Qashy nae akanikavmbidhi simu huku akisisitiza nisiwasiliane na mtu yoyote kupitia laini aliyonipa.
Tukaongea kidogo kisha tukaagana.

Nikatoka chumbani na kuanza kutembea kuelekea nje. Nikapita kwenye sebule ya jengo hili ila sikumkuta tena Ushiled kwenye kiti chake.

Nikatoka nje na kuelekea sokoni kwa miguu.
Nikafika ndani ya muda mfupi tu kwani ni jirani tu.
Kwa kutumia kitambulisho changu nikasajili laini mpya.
Nikasogea sehemu ambayo duka la Qashy lipo, nikamsogelea bodaboda ambae anapajuwa vizuri nyumbani kwa Mshamba hachekwi nikampa maelekezo na kuchukua namba zake za simu ili tufanye mawasiliano hiyo asubuhi nikampa hela aliyohitaji nikaanza kuondoka kuelekea nyumbani.

Wakati huo kiza ishaanza kuingia nikatazama saa kwenye simu aliyonipa Joanah na kukuta ni saa kumi na mbili na dakika ishirini na nane.

"Dah hapa sasa niende wapi kwa wazee? au kwa Edo kissy lakini ngoja niende kwa wazee Edo nitamwendea nikirudi"

Nilijiongelesha huku nikikaribia nyumbani nilifika nyumbani na kuwakita wapangaji wenzangu wakiwa na habari zao nikawasalimia na kuingia chumbani kwangu, nikaenda mbele ya kioo na kujitazama.

"Mh! Kweli wanaume tumeumbwa mateso"

Niliongea huku nikiutazama mkufu wa Qashy ambao upo kwenye nakshi ya uwa la mbao ya fremu iliyozunguka kioo.

"KIIM.."

Niliisikia sauti ya kenzi ikiniita ikabidi niongeze umakini ili kuhakiki kama ananiita kweli.

"KIIM.."

"naam kaka"

"Kuna mgeni wako"

"Poa nakuja"

Nikatoka chumbani na kuelekea sebuleni ambako nimesikia sauti ya KENZI ikitokea.

Nikamkuta Mallerina mdogo wangu wa kike mwenye miaka 19 akiwa kwenye sofa huku kenzi akiwa akipiga piga kisabufa chake ambacho kinakeroma tu badala ya kutoa sauti ya kueleweka.

"Habari dada"

"Nzuri kaka habari za tangu jana"

"Salama, vipi Bimkubwa ndiyo kakutuma uje unicheki?"

"Eee maana tume kutafuta kwenye simu wanasema namba haipo, lakinipia namba za Mama na Baba zote zimefungiwa, ndiyo maana Mama akasema nije kukutazama. vipi laini zako na wewe zimefungiwa?"

"Ndiyo zimefungiwa, nyumbani kuna mpya gani?"

"Sisi wala hatuna mpya tulikuwa na hofu na wewe tu, ila Baba aligomea mimi kuja kukuona hii jioni ila Mama ndiyo akalazimisha"

"Hahaha! Mzee nae mbele ya bimkubwa ni jimbwa koko tu halina makali, ila ana point za msingi usije ukaanza kuitwa singo maza wakati hata twenty hujafikisha"

"Hahahah! Ngoja niwahi kurudi, hapo nikimwambia nimekukuta na uko poa ataanza kujitutumua MIMI NIMEWAAMBIA KILE KIDUME CHANGU NAKIAMINI.. SIJUWI NINI NA NINI.."

Tukaangua kicheko kwa pamoja baada ya Mallerina kuigiza sauti ya Baba.

" Hahaha! mimi niko sawa tu, nilipanga kuja kwenu huu usiku lakini basi nitakuja kesho, mwambie bimkubwa aniandalie ugali wa muhogo na ng'onda nikirudi bichi mida ya saa tisa hivi au kumi sitakula popote breki ya kwanza itakuwa kwenu"

"Sawa mimi acha niende"

Nikazama mfukoni na kutoa vichench kadhaa na kumkabidhi Mallerina kwa ili akawapatie wazee.
Tukaagana kisha akatoka ndani.

"Mbona usiku Sister kwa Salama?"

Niliisikia sauti ya Edo kwa nje bila shaka nikajua anamuongelesha Mallerina kwani nae humwita Dada kama nimwitavyo mimi.

"Eee kwa Salama nilikuja kumwona kaka ila hapa"

"Ahaa yupo lakini?"

"Ndiyo"

"Sawa safari njema"

"Hodii"

"Karibu Edo"

"Poa mwanangu"

Tukatoka sebuleni na Edo tukaelekea chumbani kwangu.

"Dah mwanangu ishakuwa jau zile laini si hazifanyi kazi na ninejaribu kurenew hazikubali pia, nimesajili laini mpya"

Aliongea Edo huku akijitupa kwenye sofa ambalo nilimumuliwa na Qashy Lilith.

"Ah mwenyewe hivyo hivyo nina laini nyingine vipi chambo umekipata?"

"Eee nimekipata sema jamaa siku hizi wana tamaa, wanakutajia tu bei kubwa kisa tu wavuvi wanaohitaji chambo Kipindi hiki ni wengi"

"Ahaa sawa ila kesho tuondoke mapema zaidi kwa sababu maji kupwa ya mapema ndio yana nema, basi sijuwi utalala wapi leo!"

"Ah nilale wapi zaidi ya hom! Lile Toto nililobonganalo kule pwani linatimba huu usiku"

"Duh!"

"Eee wewe si unawachekea chekea tu wakina ephen_ wanakuchuna samaki kama zuzu halafu utamu wanaenda kula wajomba huko majuu"

"Sawa bhana nishakuzoea kila ukipata demu mpya lazima unichambe, ila shida ni kwamba hujuwi unachokitafuta kwa wanawake"

"Si utelezi nitafute nini? Au wewe huwa unatafuta nini kwa mwanawake"

"Hahaha! Sawa bhana tufanye umeshin.."

"Sio tufanye nimeshinda, ukweli ndiyo huo hakuna cha kukipata kwa dem zaidi ya ganda la ndizi"

"Hahaha! Sawa Edo"

"Eee mimi sikulazii damu kwenye mambo kama haya"

Tukaongea stori sana na Edo hadi ilipofika mida ya saa tatu Edo akaniaga na kuniambia anaenda kumpokea mgeni wake dada ambae alimuaprochi pwani mchana.

Nikabeba maji na kwenda bafuni kuoga
Nikarudi na kuvaa suruali kubwa nyeusi ya mpira ambayo huwa naivaa wakati wa kulala.
Nikajilaza chali kitandani huku nikiuwazia mchana wa leo jinsi ulivyokuja na vitendawili.
Nikahisi njaa inautafuna utumbo wangu, nikakumbuka nilinunua vitafunwa mchana wakati tunarudi baharini.
Nikaenda kuchukua mfuko ambao nili vihifadhi, nikafungua na kuchukuwa sambusa tano nikaziweka kwenye sahani ndogo ya plastiki, nikarudi kitandani na kuiweka sahani kwenye godoro, nikajilaza tena na kuanza kutafuna sambusa huku mawazo yakiwa yanaendelea kutalii kichwani.

"Jamani hivi Kim nimemkuta"

Niliisikia sauti ya Ephen kiasi cha kunifanya nistaajabu kwani Ephen hapajuwi ninapoishi na sina mawasiliano yake.

"Eee yupo itakuwa analala sasa hivi mgongee hako chumbani kwake"

Alijibu KENZI na sekunde chache nikasikia mlango wa chumba changu ukigongwa, nikainuka kwa bashasha na kwenda kufungua.

"EPHEN!"
Niliitaa kwa mshangao huku nikitumbua macho kwani sio tu namshangaa Ephen kuwepo hapa muda huu bali pia aina ya mavazi aliyovaa sikuwahi kumuona ameyavaa hata siku moja.

"Kim ni mimi, nimekuja kwa ajili yako naomba unipe muda wako mchache kabla sijakuaga na kurudi nyumbani"

Aliongea Ephen kwa sauti ya upole mno.
Umri wa Ephen ni kati ya miaka ishirini na minne hadi sita hivi kwa kumkadiria.
Umbo lake ni mnene kiasi cha kutosha kumuita bonge pia ana urefu wa wastani tu na rangi yake ni mweusi. sura yake ni yakawaida yaani ukimweka kwenye mashindano ya kutatuta wanawake wazuri hapa mkoani mtwara hawezi kushinda. lakini pia hata ukimweka kwenye mashindano ya kutafuta wanawake wabaya atapishana mbali mno na ushindi.
Kitu kinacho kikubali zaidi kutoka kwa Ephen ni Bakery yake iliyopo uwani ambayo ina mikate miwili tu lakini kama itatokea siku mikate hiyo ikahalalishwa kuliwa basi bila shaka kila mkate mmoja unaweza kuliwa na watu wazima kumi na wawili na wote wakashiba haswa.

"Karibu Ephen karibu ndani"

Niliongea huku nikimuonyesha ishara aingie chumbani.
Akaingia huku nikimsindikiza kwa macho akiotingisha mikate yake miwili kiasi cha kufanya mnara ulio ndani ya suruali yangu ueanze kupandisha mawimbi ya kimtandao hadi kufikia 5G.
Alikuwa amevaa kigauni cha rangi ya zambarau kifupi chepesi chenye asili ya mpira.
Nilimsindikiza kwa macho hadi alipokaa kwenye sofa, nilibaki nimesimama tu mlangoni huku akili yangu ikiiwazia hii neema iliyojileta bila kuitumilia mabavu.

Nikafunga mlango na kwenda kwenye sofa alilokaa nikachuchumaa huku nikimtazama machoni.
Alikwepesha macho kwa aibu kitendo kilichonipa mafasi kubwa zaidi ya kuutazama uso wake uliumbwa kwa mashavu manene kiasi na midomo minene iliyoficha meno yake membamba.

Nikamshika kichwa na kukisogeza kwangu kwa lengo la kunywa juisi isiyo na rangi wala sukari.

"Hapana Kim mimi nimekuj.."

Sikutaka kumpa nafasi ya kuongea, nikauleta tena mdomo wake kwangu na kuanza kunywa juisi yake tamu isiyopita kiwandani.
Mara hii alitulia kabisa yaani hakuleta upinzani.

Nikaona sina muda wa kupoteza nikambeba juu juu kwa kutumia nguvu ambazo sikujuwa zimetokea wapi.
Kabla dakika haijaisha wote tukawa kama vichanga.
Sikuona haja ya kuleta mbwembwe nyingi zaidi ya kumuuwa mende tu kwasababu rungu ninayo ya kutosha.
Ndani ya dakika sita tu za mtanange huu mzito nikahisi watoto wanaanza kiherehere cha kumdai Mama, sikuwa na uwezo wa kuwazuia tena kumwona Mama yao.
Nikafumba macho na nikuanza kufyatua hovyohovyo risasi katika bunduki yangu huku nikilita ja jina la Ephen kwa nguvu.
Mwana dada huyu hakuwa na la kufanya zaidi ya kulizingusha feni lake taratibu ili kunipulizia wakati naendelea kufyatua risasi.

Nikafumbua macho yangu taratibu ila cha kushangaza sikumuona tena Ephen kitandani, kulikuwa na sahani lenye sambusa tu nikastuka sana na kuinika kisha nikakaa.
Nikahisi ubaridi katika mapaja yangu.

"nini hiki"

Niliongea huku nikiingiza mkono ndani ya suruali yangu ambayo niliivaa kwa ajili ya kulalia.

"Ah ku** la m*mae Fatuma ndoto"

Niliachia matusi baada ya mkono wangu kukutana na utelezi ambao moja kwa moja nilijuwa tu ni Manii.
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom