Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Hii story jamani nimeipenda mnooo
Yan segments za mama Erica zilikua zinanichekeshaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna moja hiyo eti " Erica mwanangu rudi nyumbani nimekukumbuka sana, yani mjomba wako ameniuliza hivi tulisomesha mtu au paka[emoji28][emoji28].... daah asante mtunzi, nawe ulieileta JF!
Pamoja sana mkuu
 
Hii story jamani nimeipenda mnooo
Yan segments za mama Erica zilikua zinanichekeshaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna moja hiyo eti " Erica mwanangu rudi nyumbani nimekukumbuka sana, yani mjomba wako ameniuliza hivi tulisomesha mtu au paka[emoji28][emoji28].... daah asante mtunzi, nawe ulieileta JF!
Pamoja sana mkuu
simulizi bora ya mwaka huu Jf...2020🔥🔥🔥
 
SEHEMU YA 455 ................ MWISHO


Basi walicheza na kusherekea hadi muda chakula ambapo watu walikula na kusaza na muda wa zawadi ulivyofika watu walianza kupeleka zawadi zao ambapo Bahati alienda na kumkabidhi Erica hati ya shamba na kuongea kidogo,
“Napenda kutoa zawadi hii ya shamba kwa Erica maana ulikuwa ni mpango wangu wa muda mrefu sana, siwezi kuacha kwakweli. Shamba hili likawe faida kwa Angel, nampenda sana huyu mtoto na nilisema kuwa napenda sana kuwa baba yake sema mambo yaliingiliana ila bado sio kwamba ni mwisho wa kuwa familia, nampenda na ninatoa shamba hili kama zawadi kwake, naomba mpokee zawadi hii”
Bahati alijua kama akisema ni zawadi kwaajili ya Erica basi Erick anaweza kuigomea kwahiyo akasema ni zawadi ya Angel, muda kidogo Rahim nae alienda kutoa awadi yake ambayo pia aliielekeza kwa Angel, alikuwa na hundi ya milioni kumi na tano na kusema,
“Nakumbuka Erica uliwahi kuniomba pesa hii ili ufanyie biashara kwaajili ya kulea vyema mtoto wetu ila sikutaka kwani nilijua nakukomesha na lazima utanyenyekea sana kwangu, sikuwa na haja na wewe sababu nilikuwa na wanawake wengine ambao nilikuwa naona wananifaa kumbe sikuangalia ya mbeleni, natoa hundi hii ukaiweke kwenye akaunti ya Angel na ajue kwamba nimetubu na nitamjali”
Erica alipokea ile hundi kwa uzuri kabisa sema hawa watoa zawadi walikuwa wakiongea moja kwa moja na wahusika kwahiyo watu walikuwa wakisikia ni wale wa karibu tu.
Basi muda wa zawadi uliisha na walikuwa wakicheza tu, kisha ukawa muda wa kuaga wale maharusi ili wakapumzike, Mc akawataka wale mabibi harusi waeushe maua akiamini kuwa atakayedaka ndio harusi inayofatia.
Basi Erica alirusha ua lake na likadakwa na Bite, walifurahi sana na kuona kumbe harusi ya Bite inanukia, kisha Tumaini nae akarusha ua lake, likadakwa na bi.Aisha, watu walicheka sana kuona bi.Aisha kadaka lile ua maana walimuona ni mtu mzima, walicheka sana. Mzee Jimmy alimvuta pembeni bi.Aisha na kumuuliza,
“Na wewe unahitaji kuolewa?”
Bi.Aisha alicheka tu, kisha mzee Jimmy aliendelea kuongea,
“Niambie ukweli una mpango wa kuolewa? Maana hata mimi nahitaji kuoa ila nimeathirika”
“Na mimi ni muathirika pia”
Mzee Jimmy alimsogelea bi.Aisha na kumkumbatia kisha akamwambia,
“Wewe utakuwa mke wangu”
Watu waliowaona walicheka sana.
Kisha maharusi wakaruhusiwa kwenda kupumzika, ila kabla hawajaondoka walimuomba Yule mama wa maombi aseme neno moja nae alisema,
“Alichokiunganisha Mungu basi mwanadamu asikitenganishe”
Ukumbu wote ulisikika ukisema,
“Ameeeen”
Na vigelegele, nderemo na vifijo vilisikika kisha maharusi ndio wakaondoka kwa furaha.

Siku ya birthday ya Erick na Erica ni siku ambayo waliamua kwenda kupima ule ujauzito ambao Erica alikuwa nao kwa ultrasound, na furaha iliongezeka maradufu baada ya kuona kuwa mimba ya Erica ilibeba mapacha wa kike na kiume. Erick alifurahi sana na kumkumbatia Erica kwa furaha kwani aliona kuwa ile ni zawadi kubwa sana kwenye siku yao ile muhimu.

---------MWISHO---------

Safi sana... Bonge la story...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom