Simulizi: Nusu ya Uhai

Simulizi: Nusu ya Uhai

Akaliza

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2022
Posts
227
Reaction score
239
Simulizi: Nusu Ya Uhai
Mwandishi: Akaliza


Tuanze.


2017, KASANGA-KIGOMA.

Majira ya usiku shughuli za uvuvi zilikuwa zikiendelea kama kawaida, boti nyingi na mitumbwi zilikuwa na idadi kubwa ya wavuvi waliokuwa wakielekea katika sehemu ambako waliamini kungelikuwa na samaki. Sehemu ya Kasanga inayopatikana Mkoani Rukwa ilikuwa na watu wengi mno, ila kutokana na ukaribu wa eneo ilo na Ziwa Tanganyika watu wengi walijikuta wakipambana na kazi ya uvuvi. Watu wachache walikuwa wakifanya shughuli za kusafirisha samaki na dagaa kwenda kwenye mikoa mingine. Hali ya hewa ya usiku huo ilikuwa shwari mno, upepo kiasi ilikuwa ukivuma kwa kasi ndogo. Hali ya hewa katika ziwa Tanganyika ilikuwa nzuri mno, miale ya mwanga katika boti mbalimbali za kisasa ilimulika sehemu mbalimbali za maji.


Mawimbi ya ziwani hapo yalikuwa yakipanda juu na kushuka kwa kasi ndogo na hii iliwapa morali ya kufanya kazi wavuvi wote waliokuwa mahali hapo. Amani Hafidhi alikuwa ndani ya mtumbwi wake uliokuwa na jumla ya watu watano, ndani ya mtumbwi kulikuwa na nyavu, ndoo moja ndogo ya maji iliyokuwa tupu na vikorombwenzo vingine vingi. Amani akiwa anaendelea kuandaa nyavu yake alikuwa akikaza macho yake kuangalia sehemu ya mbali kidogo ambayo ilikuwa imekumbwa na kiza kiasi, mwanga wa mwezi haukutosha kuangazia mahali ambapo Amani alikuwa anaangalia.

" Amani hatuna muda hapa, shusha hiyo nyavu mapema " aliongea Abdul aliyekuwa ameegama akiuruhusu mgongo wake kupumzika kwa muda kidogo. Amani aliishusha ile nyavu na umakini wake akauweka kwenye nyavu aliyoizamisha kwenye maji, kwa kutumia mikono yake yote miwili Amani alishikilia sehemu ya nyavu ambayo ilikuwa imebakia ndani ya mtumbwi.

" Abdul, vipi unapumzika ? " Amani aliuliza akiwa anageuza shingo yake kumtazama Abdul ambaye hakuwa hata na tone la aibu kwani alikuwa akianza kusinzia.

" Ndio, kwani kuna tatizo ? " Abdul alijibu akiwa anajaribu kuinuka.

" Lipo tena kubwa tu. Hii nyavu nitashikilia peke yangu hadi saa ngapi ? " Amani aliongea akiwa amebadilisha hata namna yake ya kuongea, sauti ya Amani muda huu ilitoka ikiwa na jazba.

" Haya nakuja, naona unadhani siku ya leo ni kama jana. Watu wanotumia motaboti wameshindwa kupata samaki, sisi ni akina nani mpaka tupate samaki muda huu ? " Abdul aliongea kwa utulivu akiwa anasogeza mikono yake na kuishika nyavu. Kwa muda huu Abdul na Amani waliamua kukaa kimya, hakuna mtu hata mmoja baina yao aliyeona kulikuwa na ulazima wa wao kuingia kwenye maongezi.


Ukimya ukiwa umetawala vijana wengine watatu walikuwa wakiandaa mahali pakuwekea samaki. Hali ya ukimya iliendelea, si Amani wala Abdul aliyefungua mdomo wake kuongea jambo lolote lile. Wale vijana wengine watatu nao walikuwa kimya mno. Hali ya ukimya ilivamiwa na kutikisika kwa mtumbwi.

" Kuna nini? " Abdul aliuliza

" nini nini ?, mbona sikuelewi wewe " Amani alijibu kwa ghadhabu akiwa anamtazama Abdul, kwa wakati huu Amani alishindwa kabisa kuzuia hasira zilizokuwa zinamsongasonga mno.
" kwani hujaona mtumbwi umeyumba ? " Abdul alijibu akiendelea kukazia macho yake juu ya uso wa ziwa Tanganyika. Baada ya muda mchache nyavu ilianza kuvutwa kuelekea majini, Abdul na Amani wakakaza mikono na kutumia nguvu zao kuivuta ile nyavu kwa nguvu.

" vuta kama mwanaume wewe, acha kulegea hovyo hovyo " Amani aliongea kwa jazba akiwa anamtazama Abdul. Abdul hakuona kama kulikuwa na umuhimu wakutoa majibu yake muda huo. Baada ya kukuru kakara za muda mrefu hatimaye nyavu ikapandishwa juu, Abdul alitoa tusi kubwa la nguoni baada ya kuona kitu kilichonasa kwebye nyavu.

" Aisee huu mkosi aisee " Abdul aling'aka akiwa anamuangalia Amani aliyekuwa akishirikiana na vijana wale watatu kukitoa kile kitu kilichonasa kwenye nyavu. Amani aliachia nyavu na kukunja lipsi zake akiziruhusu zijikusanye kwenye upande mmoja wa mdomo. Baada ya kumaliza kukitoa kitu kilichonasa kwenye nyavu Amani alichukua tochi kubwa na kumulika. Alichokiona Amani kilimtia mashaka mno ila akaona ni kheri kama angeangalia kwa umakini. Nguo nyeusi tii ikiyotota maji ilikuwa imeviringishwa katika hali ya ajabu sana na ndani yake kulionekana kuweko kitu ambacho hakikuwa na umbo la kueleweka.
" Tupa hicho kitu, usipoteze muda " Abdul aliongea kwa jazba akiwa anamtazama Amani.

" sasa nitupe nini ?, kwani umeona kilichomo ndani yake au unaongea tu kwakuwa unaongea ? " Amani alijibu akiwa anaendelea kufungua kile kitambaa cheusi.




SIMBO, IGUNGA- TABORA.

Majira ya usiku Mr. Morgan alikuwa ndani ya jumba lake la kifahari lililokuwa linapatikana sehemu ya Simbo. Mr. Morgan alikuwa raia wa Uingereza ambaye alikuwa akifanya biashara za mazao, mara nyingi Mr. Morgan alikuwa akisafiri kuelekea mikoa ya kusini mwa Tanzania kuenda kununua mazao kutoka kwa wakulima. Baada ya kununua mazao alikuwa akiyasafirisha mpaka jiji la Dar Es Salaam ambako huko angeyauza kwa faida na baada ya hapo angerejea jijini Tabora ambako alikuwa na makazi yake. Baada ya kuona biashara ilikuwa inamlipa Mr. Morgan aliamua kuchukua na uraia wa Tanzania kabisa. Kwakuwa sheria za Tanzania haziruhusu uraia pacha, Morgan aliukana Uingereza na kuukubali U-Tanzania.


" Nadhani utakuwa nyumbani kwako siku ya kesho ? " Mr. Morgan aliongea akiwa anamtazama Deus aliyekuwa amekaa kwenye kochi lililotazamana na kochi la Mr. Morgan.

" Ndio nitakuwepo, kwani kuna jambo unalotaka kusema ? " Deus aliongea akiwa anamtazama Mr.Morgan.

" Halipo kabisa. " alijibu Mr.Morgan

Baada ya maongezi hayo kuisha Deus alimuaga Mr.Morgan akawa anaendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake. Deus alikuwa kijana wa miaka 33, mwili wa Deus ulijengeka kimazoezi na alikuwa ana muonekano wakiume. Deus alikuwa na sura nyembamba na rangi ya ngozi yake ilikuwa ni maji ya kunde. Akiwa anatembea kuelekea nyumbani kwake ambako hakukuwa mbali kutoka kwa Mr.Morgan, Deus alijikuta akiingia kwenye mawazo mazito. Licha ya kuwa mfanyabiashara wa mazao Mr. Morgan alijihusisha na biashara ya kuwauza mabinti wadogo kwa wazungu wenzie ambao walitaka kufanya ngono na watoto wabichi wa miaka 16,17 hadi 20 na ushee. Deus alijuana na Mr. Morgan alipokuwa anaenda kuuza mazao yake kwa Mr. Morgan miaka miwili iliyopita. Kwakuwa Deus alikuwa na uwezo wa kuongea Kiingereza ilikuwa rahisi kuongea na Mr. Morgan. Ukaribu wao ulikuwa siku hadi siku. Siku moja Mr. Morgan alimtaka Deus afike kwake kwa ajili ya mazungumzo anbayo aliyaita mazungumzo ya maana mno. Siku hiyo Deus alifika nyumbani kwa Mr. Morgan na kukaribishwa ndani.

" Karibu " Mr. Morgan aliongea

" Ahsante " Deus alijibu akiwa anatembeza macho yake kuthaminisha vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo.

" Unaweza kujimiminia hiyo kahawa wakati tunaendelea na maongezi " Mr Morgan aliongea akiwa anasogeza birika lililokuwa na kahawa. Baada ya hapo maongezi yakaendelea, Deus aliombwa na Mr. Morgan kumtafutia binti mdogo w miaka 18 ambaye alitaka ampeleke pale nyumbani kwake. Na kuanzia siku hiyo Deus alikuwa akilipwa hela ili atafute mabinti ambao Mr. Morgan angefanya nao mapenzi. Baada ya siku nyingi kupita Mr.Morgan alikuwa akipokea marafiki zake wengi waliotokea Uingereza, Mr. Morgan aliwapatia rafiki hao mabinti wadogo waliofanya nao mapenzi. Mambo yakaendelea na Mr. Morgan akaendelea kufanya shughuli yake hiyo, kazi hii ya kununua mabinti wadogo na kuwafanyisha ngono ilikuwa inamlipa sana kwani wenzie walikuwa wakilipia huduma hiyo.

" Mume wangu, una nini ? " sauti ya Careen aliyekuwa mke wa Deus ilisikika akiwa anamtazama mumewe.

" Deus! Deus! " Careen aliita akiwa anamsogelea Deus ambaye alikuwa amezubaa tu nje ya geti la nyumba yake ambalo baada ya kulifungua alibaki akiwa ametulia tuli.

" aahh... " Deus alishtuka na akamtazama mke wake aliyekuja anaelekea alipokuwepo Deus. Deus aliona hakukuwa na faida yoyote kuendelea kukaa mahali pale aliingia ndani na kujitupa kwenye kochi. Careen ambaye muda huo alikuwa amevaa kanga na kiblauzi chembamba alisimama na kuntazama mumewe kwa huruma. Baada ya sekunde chache Careen alimfuata Deus na kukaa karibu yake. Akiwa anamshika shingoni akiwa kama anapima joto la mwili Careen aliamua kuvunja ukimya.

" Unaumwa ?, Deus mbona unakaa kimya unepatwa na nini? " Careen aliongea kwa huruma akiwa anamtazama Deus usoni

" Hamna shida yoyote, naomba niache nikalale" Deus alijibu na kuondoka mahali hapo.





ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom