Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Safi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kadu boy ananiangusha kweli,General wenu Kadumya mwenyewe mchumba tu anaongeleshwa Kwa sauti ya church boy anaigopoa ila anajipa moya kishingo upande.😂
Hapo sasa ndpo huwaga nafeli🙏🙏🙏🙏,mhanuzi wangu mzee wa UMD mbona hujanishtua,ona saa saba hii ndo naamka kusoma.
jaman ngumi tena😅😅 Hiyo ngumi kwa mbali halaf kuna moja hiyo eeeh nikiileta humu nitatukanwa mpka nikimbie maan sio kwa arosto yake.
Mambo yetu hayo,jaman ngumi tena
😂😂😂 Me sio UMD me team Ezze mtu mfupi anae miliki mizigo mizito.Du, mambo yanazidi kukolea.
Shukrani sana mkuu
Abou Shaymaa. UMD mwenzangu😂😂😂😅😂😂😂😂
Bahati umenikuta online sasa,😂😂😂 Me sio UMD me team Ezze mtu mfupi anae miliki mizigo mizito.
Mkuu ntumie location ya huko kwenye vichaka vya Kizimzwumbi,😂😂😂 Me sio UMD me team Ezze mtu mfupi anae miliki mizigo mizito.
"MWISHOOOOOOOOOOOOOOO AHSANTENI KWA KUWA NAMI MWANZO MWISHO SHUKRAN SANA KWENU NA KWA UONGOZI WA JamiiForums TAYARI VERO KAENDA KWA BABA YAKE NA CHITOPELAH ANANDA KUKAMATWA, TUKUTANE SEHEMU YA THELATHINI NA SITA TUJUE NINI KIMEENDELEA KULE KWA SONGORO NA WALE UMD, MUSIJALI HII MPKA KIELEWEKE ESPSODI YA MWISHO KABISA,KUNA WATU TAYARI TUMBO JOTO... TUNAENDELEA"NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA TANO
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA NNE: Mpaka hapo nikama jopo zima lilikuwa limeshaelewa, Chitopela amesimama upande gani katika matukio yale, japo hawakutaka kukatiza maelezo ya bwana Ashraf, “opration iliendelea huku nikiamini kuwa mimi tu ndio nilikuwa sijui kinachoendelea, lakini wakati operation ile ikiwa imesha malizika ndipo nikagundua kuwa, ile operation kwa kiasi kikubwa ilifanywa na UMD, ikisimamiwa na Kadumya ambae wakati huo tayari alikuwa amesha hesabika kama mtoro kazini” alieleza Ashraf....…….ENDELEA…
Na wakati ule wa mwisho wa operation katika mwaka wa 1993 kwenda 94, ndio yakaanza matukio ya ajabu kwa askari walioshiriki operation, chitopela alituma watu wake kuja kukushawishi kuachana na jeshi na kujiunga na UMD, endapo utakataa basi wewe na familia yako wote munauwawa, hilo liliwafanya askari wengi kukubali kujiunga na UMD, wakiwepo wakina Zaidi Tambwe na wengine waliokuwepo kwenye operation ile, na wachache waliokataa, waliuwawa pamoja na familia zao, na pia kama ulionekana kugundua kitu na haupo ndani ya UMD, basi napo ungeuwawa” alieleza Ashraf, ambae hakujua kama kuna watu wazito katika nchi wanamsikiliza.
“ilipofikia zamu yangu, ukweli sikutamani yanikute yaliyowakuta mwenzangu, moja niliamini kuwa kujiunga na UMD ni sawa na kujichimbia shimo mimi mwenyewe, na pili niliona wazi jinsi walivyokuwa ni wepesi wa kuuwa watu wasio na hatia, hivyo niliona kuwa wasingesita kuniuwa endapo nitaonyesha dalili ya kukubaliana nao kishingo upande, hivyo nikachukua familia yangu na kukimbilia mkunya huko newala nchin tanzania ambako nilikaa kwa muda mrefu nikijishughulisha na kazi za uvuvi na kilimo pembezoni mwa mto Ruvuma, mpaka mwaka juzi nilipoamua kurudi nyumbani kutokana na maisha magumu niliyokuwa naishi kule newala, huku nikiamini kuwa tayari UMD na bwana Chitopela, wamesha shindwa kufanikisha mapinduzi yao haramu” alieleza Ashraf huku tayari wakina Elvis wakiwa wameshapata jibu la nani kiungo wa UMD na watu waliopo serikalini.
Hapo ni kama swali walilokuwa nalo wakina Elvis, pia alikuwa nalo luten Elia Enock, “sajent taji Ashraf, kwa vyovyote katika kipindi ambacho ulikuwa karibu na Chitopela ulipata kumfahamu kiongozi wa UMD, je ni nani huyo?” aliuliza luten Elia, hapo wote mpaka wakina Elvis wakatega masikio kusikiliza jibu la Ashraf, mwanzo nilidhania kuna kiongozi anaesimamia kundi na shughuli zote za UMD, ambae pengine ni tajiri mkubwa kutoka kwenye nchi kubwa, lakini ukweli ni kwamba, hakuna mwingine zaidi ya Dickson Chitopela mwenyewe, ambae alitumia biashara isiyo halali ya madini yanayopatikana nchini, kujitafutia fedha za kuendesha kikundi chake kinachosimamiwa na Kadumya” alijibu Ashraf.
Hakika ndani ya chumba alichokuwepo mfalme, kila mmoja alimtazama mfalme kuona ni kiasi gani atakuwa ameshtuka, lakini baada yake, mfalme aliachia tabasamu laini huku anamtazama mke wake, “ndio maana nakuambia sikukosea kufunga safari mpaka Tanzania kukutafuta we Malkia wangu, nikama ulivyosema, na sasa alitaka kutufanyia kama alivyowafanyia babu zetu, mwaka ule wa 1992” alisema kingElvis kwa sauti yenye dalili za furaha ya ushindi.
Wakati mfalme anaongea hayo, wakamsikia Luten Enock anahoji swali moja muhimu sana, “kwanini hukutoa taarifa kwa mfalme kama alivyofanya Frank Nyati, baada yake ukakimbia na kuiacha nchi katika maandalizi ya kuipindua?” aliuliza Luten Elia, “nilikuwa askari wa kawaida sana, ujue wapo hata mabrigedia ambao hawawezi kuonana na mfalme pasipo kuweka miadi week kadhaa au mwezi kabla, zaidi ya wale wachache walioaminiwa na mfalme mwenywe, na kama ujuavyo simu ya mfalme ya kawaida ambayo sisiwote tunaifahamu nilazima isikilizwe na watu zaidi ya kumi, ndipo yeye asikilize na kukujibu, sasa kwa wakati ule sikuwa na fahamu nani UMD na nani sio UMD, hivyo nilihofia kujikuta nimeingia matatizoni mimi na familia yangu, na kubwa kuliko yote ni Imani ambayo mfalme Eugen alikuwa ameiweka kwa Chitopela, kila mmoja anafahamu hilo, maana yeye ndie mtu wa kwanza kumueleza kuwa kuna uwepo wa waasi ndani ya serikali, kama mfalme hakuweza kumuelewa Frank Nyati, asingeweza kunielewa mimi ambae sikuwa nafahamika popote” alieleza Ashraf, ambae kiukweli alikuwa amefunua akili za Elvis na mke wake na viongozi waliokuwepo pale.
Mpaka hapo hakukuwa na maelezo ya ziada waliyo kuwa wanayahitaji wakina Elvis, “General, unashauri nini?” aliuliza Elvis, huku anamgeukia Sixmund, “mtukufu mfalme tunasubiri amri yako, nivile utakavyoona inafaa, ila ni muhimu Chitopela awekwe chini ya ulinzi mara moja” alisema Sixmund, ikiwa ndiyo ushauri wake kwa mfalme Elvis, “sawa, mara moja Chitopela akamatwe na avuliwe hadhi ya kuwa waziri na aondolewe kuwa katika orodha ya VIP, huku akinyimwa haki yakuwa waziri mstaafu, alisema Elvis kwa maana ya kwamba, hapo tayari alishafanya maamuzi, na kilichobakia ni taarifa kuanza kupelekwa sehemu husika, mtukufu mfalme kabla ya yote, kwanza kabisa tunaomba tumkamate Chitopela kabla hajagundua kama kuna lolote linaendelea” alisema Sixmund na hapo Malikia Vaselisa akaunga mkono, “tena itafaa kama utamuita Golden House, kisha utangaze kumvua uwaziri na kisha awekwe chini ya ulinzi, vinginevyo ataweka mpango ya kutoroka mapema na kwenda kujipanga kivingine kwaajili ya kurudi na mapinduzi yake” alisema malkia Vaselisa na Elvis kaonyesha kukubaliana na hilo.
“Six hakikisha Ashlaf anapata sehemu nzuri ya kuishi wakati tunaweka sawa makazi yake kule phumbu za Kwala, na apate huduma zote za kiutawala, mavazi chakula na kila kitu, ila musimuweke wazi mpaka operation itakapoisha” alisema Elvis wakati anaondoka na mke wake.********
Naaam wakati huko nchini #mbogo_land mambo yakiwa yanaendelea kuwa hadharani, huku Tanzania nje ya jiji la dar, tunazungumzia kwenye msitu wa Kazimzumbwi, ambako msako mkali ulikuwa unaendelea huku mipango mbali ikipangwa ndani ya msako huo huo baina ya polisi wao kwa wao, pasipo polisi wengine kujua kinachoendelea.
Akiwa anamaliza kuongea na Ulenje Kadumya akashtuliwa na captain Kobwe aliekuwa amejificha pamoja nae kwenye ficho moja, kwamba atazame upande wa kusini, ambako kuna njia ya kuingilia pale kwenye machimbo ya kokoto, kwa mbali wanaona mianga ya tochi za simu, “haooo! Wameshajileta” alisema Kadumya, kwa sauti ya chini, “sasa mkuu tunafanyaje maana lazima watayao magari hapo chini” aliuliza Kobwe ambae kama alivyokuwa Kadumya, alikuwa na bunduki yake aina ya SMG, huku Kadumya akiwa na bunduki aina ya H&K G95 ASSAULT RFLE 5.56 MM, “lakini Ulenje amesema kuna tukio litatokea na hawa watarudi walikotoka, na kuwahi hilo tukio, maana tukiwasha…” kabla Kadumya hajamaliza kuongea, tayari ikasikika risasi toka kichakani, “tumepigwaaaaaaa” ilisikika sauti ya toka kwa wale watu wenye vitochi.
Hapo ikawa kama wamefungulia mbwa, zilisikika risasi nyingi mfululizo, zikiandama lile eneo ambalo wale wenye vitochi walikuwepo, yani askari wa jeshi la polisi ambao walionekana wakijaribu kukimbia huku na huko kutafuta maficho lakini walikutana na risasi zilizowapeleka chini, wakati huo huo unaonekana mwanga wa wa magari mawili yaliyoibukia kwenye bonde toka upande wa barabarani.
Kitendo bila kuchelewa, nayo yanakutana na risasi nyingi sana, kiasi cha kuanza kurudi nyuma, huku nawao wakijaribu kujibu mashambulizi, wakati huo hakuna hata polisi mmoja pale chini, alieonekana akijaribu kujiokoa, maana tayari wote walikuwa wamelala chini, idadi yao japo hawakuonekana vyema walikuwa kama watano hivi, pale chini ilionekana mianga ya tochi za simu zao zikiwa zimelala chini.
Yale magari ya polisi yana fanikiwa kutoka eneo lile, nao wakatoa taarifa kwa wenzao, ambao bila hata kuambiwa tayari walikuwa wameshajua kilichotokea kupitia milindimo ya risasi, “kabwe madereva waingie kwenye magari haraka watoke na karudi na ile barabara mliyotoka, gari la nyuma kabisa wakae watu wanne na RPG mbili, najua lazima wataamua kuwa fuata na watakapo fanya hivyo, walipue gari moja, lazima watapunguza mwendo na kuwa tayari mumesha watoa hapa na sisi tutapata nafasi ya kuondoka eneo hili” alisema Kadumya huku anajitoa kwenye kichaka, na askari wengine wakafanya hivyo na mara moja Kabwe akaanza kuwapanga, huku luten Enock Kafulu, alitazama sehemu njia za kuondokea, “nivyema mkuu akalijua hili” alisema Kadumya, huku anachukua simu yake toka mfukoni.*********
Naaam ndani ya nyumba ya James kule kinyerezi, ni watu wachache sana waliokuwa macho, ukiachilia askari waliokuwa nje ya nyumba, pia ni kamanda Amos Makey na yule luten wa jeshi la ulinzi, sajent Girbart Ngasa, koplo Side Nyeza, na mzee James mwenyewe ndio waliomudu kufumbua macho mpaka mida hii ya saa tisa za usiku, lakini askari wengine wa MLA na mke wa James, pamoja na binti yake, walikuwa wamesinzia kwenye makochi, kwa wanajeshi hii inaitwa pumzisha mwili kabla ya tukio, yani unapopata nafasi ya kupumzika pumzika, ili likija jukumu usikumbuke muda uliopoteza nyuma.
Katika misinzio yote, mlalo wa mama na binti yake Carolona ndiyo iliyovutia pale sebuleni, maana mama alikuwa amekaa kwenye kochi, Carlona amejilaza kwenye kochi huku kichwa na kifua vikiwa mapajani kwa mama yake, kiuno kimebinuka na kuacha msambwanda juu, huku mama mtu akiwa ameweka mikono juu ya mabega ya binti yake na kulaza kuchwa chake, hii ilimsaidia hata koplo Side kutokupata usingizi,
Sura za kukata tamaa zikiwa zimewatawala, hakuna aliekuwa ana uhakika na lengo la Deus Nyati juu ya Veronica, japo sauti ya Veronica ilimjia kichwani, “jamani mchoraji wangu, si umkubalie mteja wako” ilimfanya ahisi kuwa binti yake alikuwa salama huko aliko, “jamani nasikia kama kuna simu inaita” alisema sajent Ngasa, na wote wakatazamana, “ni hii ya kwangu” alisema James huku anaingiza mkono mfukoni na kuibuka na simu, ni kweli ilikuwa inaita, akatazama jina la mpigaji ilikuwa ni namba ngeni, “huyooooo Dereva anapiga” alisema mzee James kwa pupa na mshtuko kiasi cha kuwaamsha wote waliolala.
Mzee James ambae aliipokea haraka ile simu akaiweka katika mtindo wa sauti ya wazi, ili kila mmoja asikilize maongezi yao, “hallow dereva habari za saa hizi” alisamia mzee James, huku anajaribu kudhibiti kihoro chake, “naomba kuongea na captain Amos Makey wa MLA ilisikika sauti tulivu ya kiume toka upande wa pili wa simu, wote wakamtazama Amos Makey, ambae ni kama na yeye alishangazwa na ombi la Dereva, “zingatia sheria asijekukata simu” alinong’ona mzee James huku anampatia simu Amos Makey, “captain Amos Makey, troop kamanda, naamini wewe ni Private Deus Nyati” alisema captain Amos Makey kwa sauti tulivu yenye tahadhari kubwa, huku mzee James, akiwa anajaribu kumkonyeza Amos makey kufuata sheria za kijana huyu mwenye misimamo isio ya kawaida katika sheria zake, “ndiyo afande captain, nahitaji kukukabidhi Veronica James, je unaniahidi usalama kwake na kwa familia yake mpaka watakapofika mbogo land?” ilisikika ile sauti tulivu ya Deus Nyati.
Hapo captain Makey akamtazama mzee James, ambae alimuonyesha ishara ya kukubali, kisha akamtazama sajent Ngasa, ambae pia alitoa ishara ya kukubali kwa kichwa, “yes nakuahidi, labda uniambie tunakutana wapi na saa ngapi” alisema Amos makey kwa kujiamini, “sawa uelekeo ni kisarawe, muda wowote kuanzia sasa, lakini na hali moja” alisema Deus Nyati kwa sauti ambayo wakina Amos, hawakuamini kama inaongelewa na mtu hatari waliowahi kumsikia kabla ya leo, “nakusikiliza Deus” alisema Amos, huku wote wakiwa makini wakisubiri kusikia utaratibu wa kijana Deus Nyati ambae leo alikuwa tofauti na vile wanavyo zifahamu sharia zake, “hakuna majeshi rafiki katika mpango huu” alisema Deus kwa sauti tulivu, ambayo hata kama ikikuambia kimbia unaweza kucheka na kukaa chini kabisa, hata kama ulikuwa unatembea.
Wote wakamtazama yule luten wa jeshi la ulinzi, ambae pia alikuwa anawatazama huku anakubaliana nao kwa kichwa, “sawa imekubalika, japo naona kunasheria zako leo umeamua kuzivunja kama vile hakuna kujuana majina au ile ya kutumia bunduki” alisema Amos Makey, huku anacheka kidogo, “najua munahitaji kujilinda ndio maana siwezi kuzuia mwanajeshi kuwa na bunduki, pia siwezi kuficha jina au kuleta sheria za malipo na ulinzi wa mzigo kwasababu hii sio biashara” ilisikika sauti ya Deus na mwisho simu ikakatika.
Hapo Amos Makey akamtazama luten wa jeshi la ulinzi, “unasemaje kaka, umesikia sheria ya Deus Nyati” alisema Amos Makey, na mzee James akadakia, “na yule bwana ukivunja sharia yake moja tu tayari umeharibu kila kitu” alisema mzee James akionyesha msisitizo, “nafahamu lakini sasa hatuwezi kuwaacha peke yenu, maana ukiachilia UMD ambao wanawawinda wakina Deus, pia kuna askari wachache wa jeshi la polisi ambao pia wanawasaidia UMD kama mlivyo msikia Veronica akieleza"..... MWISHOOOOOOOOOOOOOOO AHSANTENI KWA KUWA NAMI MWANZO MWISHO SHUKRAN SANA KWENU NA KWA UONGOZI WA JamiiForums TAYARI VERO KAENDA KWA BABA YAKE NA CHITOPELAH ANANDA KUKAMATWA, TUKUTANE SEHEMU YA THELATHINI NA SITA TUJUE NINI KIMEENDELEA KULE KWA SONGORO NA WALE UMD, MUSIJALI HII MPKA KIELEWEKE ESPSODI YA MWISHO KABISA,KUNA WATU TAYARI TUMBO JOTO... TUNAENDELEA...
Umetisha saana mkuu,NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA THELATHINI NA SABA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA SITA: “watambuzi wa Tanzania walifanikiwa kitambua watu wao ambao idadi hawa kuzidi saba, wengi wao ni watu ambao walishahusishwa na makosa mbali mbali ya kiharifu, mengi yakiwa ujambazi n awao kutoweka katika hali ya kukimbia kesi zao, na mwisho wamepatikana wakiwa wameuwawa” alieleza msemaji wa mfalme, ambae pia alisema kuwa, “miili ya watu iliyobakia ambayo ni kumi na moja, tumetumiwa picha zao kwaajili ya kuwatambua na tumesha watambua ni wanausalama watoro wa MLSA na askari wa MLA wakiwemo wakina Tambwe Zaid na Ramadhan Mbwambo na wengine wengi ambao orodha yao itakufikia mapema kesho ofisini” alisema msemaji wa mfalme. ....…….ENDELEA…
Japo haikuwa ajabu kwa mfalme kusikia tena kuwa askari wake wa zamani kukutwa kwenye ushirika wa UMD, ila kuna jambo ambalo alitaka kujua, “hao watu wameuwawa vipi na nani muuwaji wao?” aliuliza Mfalme Elvis, “mtukufu mfalme, inasemakana kuwa waliuwawa katika mapambano na askari wa zamani wa jeshi la ulinzi la Tanzania, Deus Frank Nyati ambae pia ni mtoto wa kanali Frank Nyati, wakati wa mapambano ya kumuokoa mschana Veronica, toka kwa hawa UMD” alisema msemaji wa mfalme na likamtoka neno King Elvis, “safi sana, nahitaji kukutana na Deus Nyati” alisema king Elvis, ambae mara baada ya kukata simu akapiga simu kwa Six mund na kumueleza lengo lake la kuwa awaeleze askari wa kikundi cha AR wafikishe salamu zake mara watakapo kutana na Deus Nyati, “tena mtukufu mfalme nimepokea taarifa toka Tanzania, Deus Nyati sasa anaenda kukutana na askari wetu ili awakabidhi Veronica” alieleza Sixmund, “sawa nadhani mpaka asubuhi nitakuwa nimepata taarifa muhimu zote, ila kwasasa tuma askari wa kumfuatilia Chitopelah kwa kila anachokifanya, nina wasi wasi kwa jinsi mambo yanavyoenda anaweza akashtuka kuwa tayari tumeshagundua kuwa yeye ni muhusika mkuu wa UMD” alisisitiza Elvis, na kama ujuavyo neno la mkubwa kiserikali ni amri, hata akitanguliza neno naomba lakini huwezi kulijadili.********
Naaam kule kazimzumbwi, mambo yalikuwa mchaka mchaka, upande wa Deus kijana wetu anapomaliza kuongea na captain Amos Makey anamtoa Veronica kwenye mapaja yake, kisha anaingia chumbani nakuanza maandalizi, ya safari, alivaa suruali ya kaki tishert jeusi, viatu vya ngozi vyenye shingo ndefu, kwamaana ya buti za rangi nyeusi, pia alifunga kihifadhio cha kisu kwenye mguu wake wa kulia karibu kabisa na kilipoishia kiatu, akachukua kila alicho kiona kinafaa usiku ule, kuanzia tochi, kamba ndogo ya chuma, na kifuko kidogo cha kubebea maji, water bag wanavyoita wazungu, ambacho hubebwa mgongoni, baada ya hapo akaandaa nguo na viatu kwaajili ya Veronica, japo ilikuwa kazi ngumu kidogo kutokana na umbo la mwanadada huyu kutokuendana na nguo nyingi za kijana wetu Deus.
Deus alipoona amesha maliza maandalizi, akarudi sebuleni, ambako Veronica alikuwa amelala fofofo, akamuamsha taratibu, “mchoraji jamani huoni kama usiku sana, unaniamsha kwanini au unataka tena” alisema Veronica kwa sauti ya kulala mika, “hapana Veronica, inabidi twende kwa baba yako, maana hajaacha kuwa na wasi wasi toka muda ule” alisema Deus huku anaanza kumpembua nguo mwanadada huyu kwaajili ya kumvalisha nguo nyingine, “jamani si tungesubiri kesho, alisema Veronica kwa sauti yenye kulalama lakini kwa kudeka, “mchana ni hatari kwetu, ni vyema tukiutumia usiku huu kupunguza hatari ya kuonekana na maadui zetu” alisema Deus huku anaendelea kumpembua nguo Veronica na sasa alikuwa anamalizia kumtoa nguo ya chini.
Hakika ilikuwa inahitaji moyo kutenda vile, maana hata yeye Deus alisha hamasikika kula kitumbua, lakini hakuweza kufanya hivyo kwasababu alikuwa anajukumu mbele yake, ni jukumu la kumfikisha Veronica kwa baba yake, “kwahiyo ndio hutaki kukaa na mimi tena?” aliuliza Veronica kwa sauti iliyonyongea, akionyesha kutopenda kabisa kuachana na Deus usiku ule, “hapana mpenzi wangu, haina maana ya kuwa hatuto kuwa pamoja, ila ni muhimu ukaungane na wazazi wako ambao wanatakiwa kwenda kukutana na mfalme” alisema Deus ambae sasa alianza kumvalisha tishert mwanadada huyu mrembo, “vipi kuhusu wewe, nitakupata vipi au ndio mwanzo wa kutokuonana tena na tukaishia kuwasiliana kwenye simu kama zamani?” aliuliza Veronica ambae kama una moyo mdogo ungegairi kumrudisha kwa wazazi wake, “haiwezi kutokea Vero, amini nakuambia, kuanzia leo na siku zote tutakuwa pamoja, sito ruhusu mtu atutenganishe” alisema Deus, akimaliza kwa kumkiss mdomoni huku anashusha tishert usawa wa tumbo.*******
Wakati hayo yanaendelea dar es salaam huko #mbogo land nako kulikuwa kunazidi kuwa kwa moto, maana wakati mfalme anajifunika shuka mara baada ya kutoka kuongea na msemaji wake, mara anasikia tena simu yake inaanza kuita, akaichukua na kuitazama kuona mpigaji alikuwa nani, “sixmund tena, sijui kuna habari mpya au zile zile” alijiuliza Elvis, huku anapokea simu ile, “sixmund tutafumba macho japo dakika moja kweli?” aliuliza Elvis kwa sauti ya kulalamika, “samahani mtukufu, kuna taarifa muhimu, nimeona itakuwa vyema ukizipata” alisikika general Sixmund, kwa sauti ya kumradhi, “taarifa zipi General au ni zile za dar es salaam, kuhusu UMD waliouliwa, mbona tulizasha ziongea?” aliuliza king Elvis kwa sauti ya kuonekana amekeleka kidogo, “hapana mtukufu, taarifa niliyo kuletea ni kuhusu Chitopela ni wazi hayupo nyumbani kwake na walinzi wake wanasema allionekana akitoka kuelekea kaskazini na baada ya kufuatilia camera za mji za barabara ya kaskazini tumeona gari lililotoka nyumbani kwake likiwa linatokomea nje kabisa ya mji wa TT, kama nusu saa iliyopita” alieleza General.
Naaam taarifa hii ilimshtua kidogo mfalme Elvis, “inamaanisha nini, ameshagundua kuwa tunazo taarifa zake, je kuna mmoja wetu anashirikiana nae?” aliuliza kwa sauti ya ukali King Elvis, “mtukufu kwa kweli imetushangaza hata sisi, ila inawezekana ameshagundua kitu kupitia watu wake wa Tanzania, hasa ukichikulia kuwa, ana watu wake kwenye jeshi la polisi la Tanzania, “lakini bado tulifanya siri kubwa ili asijue kuwa tumesha mbaini” alisema Elivs ambae kiukweli ni kama alianza kutilia mashaka juu ya watu anaoshirikiana nao, “ni kweli mtukufu mfalme, lakini bado haiwezi kumfanya asijue, kutokana na kwamba mpaka sasa vikundi vyake vimesha bainika huko Tanzania, pia tayari bwana James, tumempatia ulinzi na wanashindwa kumfikia, pia tumeshauthibiti mtandao wao wa habari za kichochezi, lazima atakuwa anachukua tahadhari za mapema, maana mpaka sasa vyanzo vyetu vya mipakani vinasema amaesha pokelewa na majeshi yake yaliyopo upande wa pili wa mpaka” alisema Sixmund, akionyesha kuwa na wasi wasi juu ya uzembe uliotokea.
Na hapo mfalme akazidi kuchanganyikiwa, “sasa tutafanyaje General, na huyu mpuuzi amesha ondoka?” aliuliza Elvis kwa sauti ambayo General Sixmund aliitambua kuwa Mfalme alikuwa amekasirika vibaya sana, “tunasubiri amri yako mfalme, maana mpaka sasa anadakika arobaini na tano mpaka lisaa kufika kambni, na kutoka kambi lilipo mpaka kufika barabara kuu ya songea tunduru ni kilomita mia mbili, mwendo wa masaa mawili kwa gari lenye mwendo mzuri, na hii nikutokana na hali ya barabara, kambi lake halina ndege wala helicopter, tunaweza kuwahi na kumzuia kabla hajaingia ndani zaidi ya miji ya kusini mwa Tanzania” alifafanua Sixmund, “ok! Sixmund hii nafasi yako ya kuweka sawa mambo, pengine ikawa na faida kubwa kwako au hasara kwako” alisema Elvis na kwa sauti kali ya kifalme, sauti ambayo mara ya mwisho iliwahi kusika mdomoni kwa mfalme Eugen, na sio Eric baba yake Elvis, “kama ulivyosema mtukufu, nasubiri kibali chako” alisema Sixmund kwa unyenyekevu, “kibali gani Six, tuma askari wakamrudishe huyo mshenzi na hakikisha wanaangamiza kabisa kikundi chote cha hao wajinga, tumia silaha yoyote ambayo utaona inafaa kutumiwa” alisema Elvis na hapo ikasaikika sauti toka upande wa pili, “kama ulivyosema mtukufu mfalme”.*******
Naaam wakati magari nane mchanganyiko yani ya kijeshi na yale ya kiraia, yaliyobeba askari wa jeshi la ulinzi na askari wa MLA, huku gari la tano, likiwa lema mbeba tajiri mfanya biashara James Kelvin, ambae muda wote alikuwa anapapasa kifua chake kama vile anatuliza mapigo yake ya moyo, ambae licha ya kukaa set ya kati kati, akizungukwa na makamanda kadhaa wa jeshi la MLA, lakini bado alijitahidi kutazama mbele ili kuona anakoelekea.
Wakati huo huo kule porini kwenye nyumba ya maficho kijana Deus sasa tunamuona Veronica akiwa amesha valia sruali nyeusi ya jinsi yenye asili ya mpira, tishert jeusi na koti jepesi, kichwani kofia nyeus na viatu vya michezo raba nyeusi yenye fito nyekundu, licha ya kwamba zilikuwa na kuunga unga lakini ungesema ni mavazi yaliyo nunuliwa maalumu kwaajili yake, ni kwa jinsi yalivyo mkaa vyema mwilini mwake na kumpendeza, “twende zetu” alisema Deus, baada ya kuridhika na muonekano wa mpenzi wake huyu, huku anachukua lile fuko la fedha ambalo ilikuwa ni lazima lirudishwe kwa wahusika, “hauna silaha yeyote kama ikitokea tukakutana nao?” aliuliza Veronica, ambae alikuwa bado amesimama, “hii hapa” alisema Deus akionyesha kisu kilichopo kwenye mguu wake wa kulia.
Veronica akatabasamu kwa kuonyesha kwamba Deus anafanya utani, “na maanisha bunduki hivi” alisema Veronica, ambae bado alikuwa anaamini kuwa maadui walikuwa wengi na watakuwa wanawasaka, “huwa sipendi bunduki Vero, mara nyingi nikikutana nazo huwa zinanisababishia matatizo” alisema Deus kwa sauti yake tulivu, “lakini tutawezaje kupita mbele ya watu kama wale wenye bunduki?” aliuliza Veronica huku anaonyesha kwenye kioo cha TV kubwa, yenye kuonyesha picha kwa mgawanyo wa vipande vinne na katika kipande chenye Cam 2, palionyesha jambo lisilo la kawaida, maana ukiachilia magari mawili na wale jamaa waliokuwepo toka mwanzo, ambao alisha watambua kuwa ni wakina Songoro, sasa yaliongezeka magari mengine matatu, japo kulikuwa na umbali kiasi fulani na kwa usiku huu, lakini aliweza kuyatambua kuwa ni magari ya polisi.
Hiyo haikuwa sababu ya mvuto wa video ile, ila ni namna ambayo walionekana watu fulani kwenye vichaka wakizunguka eneo lile, ambalo walikuwepo wakina Songoro, watu ambao ni wazi kabisa walikuwa ndio polisi waliokuja na magari yale matatu, “tena wanabunduki” alisema Deus, kwa sauti ya upole, hakika usingejuwa uzito wa maneno yale, na kile kilichojijenga akilini mwake, hata Veronica alishangaa kuona kijana huyu akiacha fuko la fedha, “zima hiyo tv hapo, kisha nenda kalale nisubiri” alisema Deus, huku anaufuata mlango wa kutokea sebuleni, “jamani sasa unataka kufanya nini?” aliuliza Veronica kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa hakutaka Deus aende nje ya jengo hili la chini ya ardhi, naenda kuongea nao kidogo, maana inaonyesha wameshafahamu sehemu tuliyopo, hii ni hatari kwetu” alisema Deus, huku anafungua mlango na kutoka nje ya jengo.
Naaam mara tu baada ya kijana Deus kutoka nje, Veronica anakimbilia kwenye kiti ambacho kipo mbele ya ile tv ya camera za ulinzi na kukaa kabisa huku macho yake yakiwa kwenye kamera namba mbili, ambapo kwa macho yake anawaona watu wakiwa katika makundi mawili, kama yalivyo magari yao, na sasa aliweza kuwaona watu wale ambao walionekana kama ni polisi, wakiwa wanawazunguka wale ambao walikuwepo pale toka mwanzo, waliokuwa wanajigawa huku wengine wakisogelea magari ya polisi ambayo bado yalikuwa yanawaka taa, ni kama walikuwa wanaenda kutazama mule kwenye gari kuna nani, lakini cha kushangaza Veronica anaweza kuona wale waliokuwa vichakani wanaanza kuwashambulia wale wengine, ambao wanaanza kutawanyika hovyo na kukimbia vichakani kutafuta maficho, waliokimbilia upande wa kulia wanakutana na risasi ambazo zina wapeleka chini.
Ndani ya sekunde chache wale walioshambuliwa wanaonekana wakiwa wamelala chini, huku wawili tu wakionekana wanakimbia kuelekea upande iliko camera, kwa maana hiyo ni wazi walikuwa wanakimbilia kule iliko nyumba ambayo wao wapo ndani yake, hapo wanachomoka polisi wanne kuwa kimbiza, huku wanawashambulia kwa kutumia bunduki zao, ni wazi hawakutaka achomoke mtu hata mmoja.*********
Yap! Upande mwingine wa msitu ambako kuna msitu wa Kazimzumbwi, kamanda Nyambibo, anatoa amri ya vikosi vyote kuelekea kule ambako milindimo imesikika, askari wanaingia kwenye magari mbio mbio, wengine wakiwa kwa mguu, wanakimbia haraka kuelekea upande ule huku silaha zao zikiwa mikononi, kila mmoja akiwa na hali tofauti, wapo waliovaa ujasiri wa asili, wapo walioshikwa na uoga na wapo waliosema kitakachotokea na kitokee tu, yani walimwachia mungu.
Lakini wakiwa wanakaribia njia ya kwenda kwenye machimbo ya kokoto, ambako waliowaona wenzao wa mkoa wa kipolisi wa konondoni wakiwa wamesimama eneo lile kwa tahadhari kubwa, mara wakashtuka kuona magar yanakuja kutokea upande wa machimbo, hapo Kamanda Nyambibo akapiga ukelele, “shambuliaaaaa” ile neno shambuliaaaa, halikuweza kumalizika, maana ulisika mpasuka kama wa radi kari toka upande ule unaotokea magari yale yenye muonekano wa kijeshi, ikifuatiwa na mbinja iliyosikika hewani ikija upande wao, ni sekunde mbili tu zilitumika kusika kwa mluzi ule kabla hawaja ona kitu kama muale wa moto ukishuka kati kati ya barabara upande wa kisarawe, mkito wa nguvu samamba na ngurumo kubwa ya kutisha wa kombora la RPG, vipande vya moto vinaonekana vikitawanyika eneo lote la karibu....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa JamiiForums
Karibu Sasa ujionee kwetu kulivo kuzuri,Nilikuwa mbali na dunia
Unanipa cheo niende kufa mkuu?Karibu Sasa ujionee kwetu kulivo kuzuri,
nakupatia na cheo kabisaa
uwe Captain wangu mpya wa UMD.😂😅😅😂😅😂😂
Wewe hutaki kuja kuwa waziri wa fedha baada ya mapinduzi? 😂🤣😂😂🤣🤣🤣Unanipa cheo niende kufa mkuu?