NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA TISA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA NANE: Taa nyekundu ikawa ndani ya ndege, wote wakapeleka macho kwenye langao la nyuma kabisa ya ndege ambako walikuwa wamegeukia, wakauona mlango unafunguka taratibu kama mlango wa pantone la kigamboni, ambao ulishuka taratibu mpaka ulipogota, baada ya hapo safari hii ikasikika sauti toka kwenye speeker za ndege, “landing position,” askari bado walikuwa wametulia hapo ikasikika sauti ikihesabu, 1….2….3, ikawaka taa ya kijani.....…….ENDELEA…
Sijui ni ujasiri gani ulioveshwa kwenye mioyo ya askari hawa, maana kama vile mtu anatumbukia kwenye swimming poor la nyumbani peace hotel, mmoja baada ya mwingine akasogea mlangoni na kujirusha huku kile kikamba chenye kipachiko kikifuata kitambaa fulani toka ndani ya begi kubwa la mgongoni, na mwisho kukatika na huku kile kitambaa kikijaa upepo na kuonyesha sura halisi ya mwamvuri wa kijeshi, ndani ya dakika mbili tayari askari ishirini walikuwa wamesha toka ndani ya ndege na kuwaacha askari wawili tu na lango la ndege likajifunga.******
Naaam Cheleji ambae alikuwa anasubiri kusikia taarifa za askari wake waliowakimbiza wakina Songoro, mara anaona simu yake inaanza kuita, anaitazama na kuona kuwa ni simu toka kwa Ulenje, anaipokea mara moja na kuiweka sikioni, “vipi mmesha maliza kazi” anauliza Ulenje kwa sauti ya chini, “ndio afande, ila kasoro watu wawili hatuja watambua kwa sura, ila tunawashughurikia, alisema Cheleji kwa kujiamini, “ok! Sawa hebu fanyeni haraka, fagieni ushahidi wote, tupo njiani tunakuja na vikosi vyote” alisema Ulenje kwa sauti yenye msisitizo, “sawa mkuu, lakini inakuwaje kuhusu sisi, tuondoke au?” aliuliza Cheleji, “hapana musiondoke, taarifa zilizopo ni kwamba nyie mlienda huko kwenye doria, mutasema mumekutana na kikundi ambacho kimewashambulia na nyie mkakishambulia, cha msingi hakikisheni munachukuwa simu ya Songoro, maana nimewasiliana nae mara nyingi sana” alisisitiza Ulenje, “sawa mkuu itatekelezwa” alisema Cheleji kabla Ulenje hajakata simu.
Kisha akatoa amri ya kwamba, askari waanze kukagua miili ya wale jamaa, ilikutambua kama kuna Songoro, na pia wahakikishe kuwa, wanachukua simu za wale jamaa.*******
Yaaap! taarifa zinazidi kusambaa, iwe kwenye maredio TV na mitandao ya kijamii, saa tisa za usiku ikiwa inaelekea saa kumi, lakini watu walionekana wakitoa maoni yao kwenye kurasa mbali mbali za mitandao, wapo waliochukulia kuwa ni taarifa za kutisha na kuhuzunisha, hasa kwa waasi ambao wanataka kuiharibu nchi nzuri inayotamaniwa na karibu kila raia wanchi nyingine, iwe kwa maisha mazuri wanayoishi wa #mbogo_land, au kwa uroho na urafi wa mali za nchi hiyo, kama ilivyo kwa nchi kubwa kubwa zenye kuhitaji kila kitu kiwe chao.
Wapo waliochukulia kama matukio yenye mzaha, kama ambavyo mtu asiejua maana ya machafuko anavyo chukulia habari za vita za mashariki na kati ya afrika, au vile ambavyo waliopo Kinshasa wanavyo chukulia vita vya mashariki mwa congo, hawakujua kuwa kuna watu wapo porini wanakosa usingizi, hawakujali kama ni kweli kuna watu wanauwawa huko porini, hawakuifikiria kazi ngumu wanayo ifanya polisi, huku ndani yao kukiwa na watu wasaliti, hawakujali hatari waliyonayo polisi wao wanao watafutia Amani na utulivu ndani ya nchi yao, wao walikuwa wamejilaza kama sio wanasoma habari za machafuko hayo, basi wanajiandaa kwenda makazini, hasa kwa wale wanaoishi mbali na mjini, wakichelea kukutwa na foleni za barabarani, wapo waliokuwa wanarudi toka kwenye starehe zao, na wapo ambao bado walikuwa kwenye starehe zao.
Makamanda wa vikosi vya polisi na majeshi ya ulinzi, walikuwa macho kusubiri amri ya kwenda kuongeza nguvu huko porini, wakuu wa idara za usalama wa taifa nao walikuwa macho wakiendelea kupokea taarifa na kuzifanyia kazi ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, na sasa macho na masikio yao yalikuwa ni kwa kikosi cha marine special force ambacho kinaenda kuungana na kikosi cha AR cha MLA, pamoja na section mbili za jeshi la miguu lililotoka kwenye kikundi cha ulinzi cha pale airport ili kuhakikisha Deus na mschana Veronica wanapatikana salama.
Wakati hayo yanatokea, huku marine commando nao wakiwa na magari yao nane, wanapasua mbuga kuelekea upande wakisarawe, na sasa wanakaribia relini, huku wakipanga kuwa wakifika karibu na sehemu ya makutano wachukue maficho ili Deus Nyati asijue kuwa, sheria yake ya hakuna majeshi rafiki tayari imeshavunjwa, na sasa anaenda kukamatwa.********
Naaam Songoro akiwa haamini macho yake kwa kile alichokiona kwa macho yake, kwamba vijana wake wakiuwawa kama siafu ndani ya kikaango juu ya moto, alikimbia mbio zisizo na mfano, sambamba na kijana wake mmoja, kuifuata njia ile ambayo ni wazi kuna watumiaji wa kila siku huwa wanaitumia kila siku, ni kama bado walikuwa wanaisikia mivumo ya risasi masikioni mwao, moyoni mwake Uled Songoro alikuwa anamlaani Ulenje kwa kumtumia askari wamuuwe, “huyu mshenzi ni yeye pekee ndie aliekuwa anajua sisi tupo hapa, kwanini amenifanyia hivi?” alijiuliza Songoro, huku anakimbia mbele ya kijana wake wote wakiwa na bunduki zao.
Wakiwa wanaendelea kukimbia mara wakasikia vishindo vya watu nyuma yao, nadhani kutokana na giza ndio maana hawakuweza kuwaona mapema wanao wafukuza, “mkuu ongeza mwendo wanatufuata” alisema kijana yule, ambae baada ya kumsikia sauti ndio akamtambua kuwa ni Side, yule kijana wa mzee mfupi Eze, mpenzi wa Emmy au mama P, “hebu tuwaonyeshe kazi” alisema Songoro, huku anachepuka kuingia kichakani, na Side akamfuata, ile wanaingia tu kichakani hawakwenda mbali wakalala na kugeuzia mitutu barabarani, ambako vilikuwa vinasikika sidhindo vikiwasogelea kwa kasi, niwazi waliokuwa wanawafuata nao walikuwa wanawakimbiza.
Ni kweli bwana, sekunde chache baadae wakaweza kuona taswira ya watu wakiwa wanakuja upande wao mbio mbio, “haooooo! Sasa hawa ndio watalipia walicho kifanya wenzao” alinong’ona Songoro akimweleza Side aliekuwa jirani yake kabisa, “tena ni polisi kabisa hao, sasa kwanini wametufanyia hivi?” aliuliza Side huku wakiwatazama wale jamaa wanne ambao sasa walikuwa wamekaribia kabisa usawa wa sehemu ambayo wao walikuwa wamejificha, “acha kuuliza maswali shambuliaaa” alisema Songoro na hapo wote wawili, waliminya trigger za bunduki zao kuruhusu nyundo kugonga pini ya kuwashia, iliyoenda kukandamiza kwenye kitako cha risasi na kuruhusu prime ikaminye baruti ndani ya risasi ambayo inakosa uvumilivu inalipuka na kusukuma kichwa cha risasi ile kilichotengenezwa kwa madini ya shaba, nacho kinachomoka kwa kasi ya ajabu, kasi ambayo inatumia kilomita moja yani mita 1000 kwa sekunde moja, kama hujui huo ndio umbali pekee ambao mtu anaweza kukwepa risasi baada ya kutoka kwenye mtutu.
Mitambo inarudi na kuchota risasi nyingine, kisha inapelaka chemba, kwa kuwa Songoro na Side walikuwa wameng’ang’ania kifyetulio huku kifungo cha usalama wa bunduki ile kikiwa katikati, pini inagonga kitako na risasi zinaendelea kuchomoka kwa muisho wa risasi thelathini kwa sekunde mbili, vichwa vya risasi vinakita kwenye miili ya askari wanne wa jeshi la polisi, nao wanajibwaga chini kama vile wanacheza au wanalala chini kutafuta maficho, lakini tayari walikuwa wamesha achanisha roho na miili yao, “tuondoke haraka hawa washenzi wasitukute hapa” alisema Songoro huku wanainuka na kuingia tena barabarani, kisha wakaanza kutimua mbio kuelekea upande ule ule ambao walikuwa wanaelekea mwanzo, safari hii hakukuwa na mtu anae wafuata.********
Yaaap! msafara wa magari matatu, unaonekana ukiyoyoma kaskazini ya mbali ya #mbogo_land, yakiwa tayari yameshavuka mpaka wa Tanzania, mbele kulikuwa na gari aina land rover mia na kumi lenye askari wa tano, mmoja amesimama nyuma ya bunduki kubwa aina ya anty air 12 mm, yenye mkanda mrefu wa risasi kama lilivyokuwa gari la nyuma, ambalo pia lilikuwa hivyo hivyo, tofauti ni kwamba, lile la mbele silaha ilitazama mbele na hili la nyuma ilitazama nyuma, katikati lilionekana gari dogo jeusi la bwana Chitopelah aliekuwa anaendesha gari lake mwenyewe, huku anaongea na simu, “nimesha wakataa, mpaka saa mbili ndio watashtuka kuwa sipo, ni baada ya kuona kuwa sitokei kwenye kikao chao cha mtego” alisema Chitopelah huku akiendelea kuendesha gari kulifuata lile gari la mbele, “sawa mkuu, na sisi ndio tuna pambana tupate fedha zetu kisha tuanze safari ya kurudi huko” alisema mtu wa upande wa pili, ambae sasa tunagundua kuwa ni Kadumya, “jitahidini, maana sasa ni lazima tufanye kila linalowezekana ili tuichukue nchi, hatuwezi kurudi nchini mpaka siku tumeshakuwa wenye nchi” alisisitiza Chitopelah kabla ya kukata simu.
Naam wanatembea muda kilomita mbili mbele, wanaibukia kwenye lango lililotengenezwa kwa miti, ambapo wanawakuta askari wawili, waliokuwa katika zamu ya ulinzi, ambao wanafungua geti huku wanapiga salut, wakati magari yale yanapita ambayo yalielekea moja kwa moja kwenye hema moja kubwa na zuri, hema ambalo mara zote anakaa mkuu kabisa wa kambi hilo ambalo kwa hapa ni Major Kwanguru.
Akiwa ndani ya gari Chitopela anakagua kambi kwa macho anaona lipo kimya sana tofauti na siku za nyuma alizowahi kutembelea kambi ili la pekee mara kadhaa, hapakuwa na askari waliokuwa wanacheza karata huku wanakunywa pombe na kuvuta bangi, hapakuwa na askari waliokuwa wanapeana dudu na askari wa kike au wanawake walio wateka kijijini, yani kambi lilikuwa kimya isivyo kawaida, “au pengine ni kwaajili ya wenzao walioenda dar es salaam” alijipa jibu Chitopela, maana alimini kuwa kama kungekuwa na tatizo basi hawa askari waliokuja wangempa taarifa, na kama ingetokea kabla basi angepata taarifa kwa wale askari waliokuwa kwenye lango la kuingilia.
Naaam gari linaenda kusimama mbele ya lile hema zuri na kubwa, ambapo mbele yake anaonekana bwana Kwanguru, akiwa amesimama na wanawake wanne waliovalia nusu utupu pasipo kujali baridi kali iiliyokuwa inachamanda kule porini, pia askari wanne wenye bunduki zao mkononi wakiwa wamesimama pembeni ya hema lile wakiimarisha ulinzi, huku macho yao yakionekana wazi kuwa yamelemewa na kitu kama usingizi uliosababishwa na matumizi ya bangi kupita kiasi kwajinsi yalivyo lembuka, “karibu mkuu, karibu sana, karibu ndani upunguzwe uchovu na awa warembo wanne” alisema kwanguru, ambae alionekana wazi kuwa alikuwa amelewa sana.
Chitopela anawatazama wale wanawake, kwa awamu na wao kama vile walijua wanakaguliwa, maana waligeuka kwa kuzunguka wakionyesha makalio yao, hapo Chitopela anakubali kwa kichwa, kisha anaonyesha ishara ya kuongoza ndani na wale wanawake wanatangulia ndani huku yeye akifuatia, sijui n iaina gani ya utendaji, maana alikaribishwa wanawake pasipo kupeana taarifa za kiutendaji kwanza, “naona leo vijana wamelala mapema, unawachosha sana kwa mazoezi” alisema Chitopela, ambae sio tu uchovu wa usingizi, ila pia alikuwa na uchovu wa pombe, “nashangaa leo wamelala mapema, ila muda mfupi uliopita walikuwa wanasikika hapa nje wakifanya fujo zao” alijibu kwanguru, ambae alikuwa amesimama nje akimpisha Chitopela aliekuwa anaingia ndani.
Na baada ya Chitopela kuzama ndani, Kwanguru nae akaingia kwenye mlango mwingine wa pembeni, ambako tunawaona wanawake wawili wakiwa juu ya kitanda wamepitiwa na usingizi mzito.********
Naaam tukirudi kule porini kwa Side na Songoro, ambao baada ya kukimbia kwa umbali wa mita kama mia tatu wakizidi kusonga mbele, Songoro na Side wanaiona nyumba fulani mbele yao umbali kama wa mita mia moja hivi, “kumbe kuna watu wanaishi huku, anasema Songoro, ambae sasa anaanza kutembea, anaonekana amechoka kweli kweli lakini mbona kama naiona ipo moja tu?” anauliza Side, huku na yeye anatembea, “unaweza kukuta ni nyumba ambayo bado haijakamilika, sidhani kama kuna mtu anaweza kuishi huku” alisema Songoro huku anageuka kutazama nyuma kama kuna mtu anawafuata, lakini haonekani mtu yoyote, songoro anageuka na kutoa simu mfukoni huku wanazidi kuisogelea ile nyumba.
Songoro alibofya namba za Ulenje na kuipiga ile simu ambayo iliita kwa muda kidogo, kiasi cha Songoro kutaka kukata tamaa, maana mpaka wanalifikia lile jengo ambalo kiukweli lilikuwa halijaisha ujenzi wake, na ndipo simu ikapokelewa, “hallow nani Songoro?” ilisikika sauti ya ulenje ikiuliza kwa tahadhari, “inamaana namba yangu hujaisave au ndio ulidhania nimesha uwawa Ulenje?” aliuliza Songoro kwa sauti yenye jazba, huku anaingia ndani ya jengo lile kuu kuu na kwenda kujibanza kwenye moja kati ya madirisha ya pale sebuleni, ambayo yalitazama upande waliotokea, “kivipi songoro mbona sikuele….” Kabla Ulenje hajamaliza kuongea, tayari Songoro akadakia, “hulewi nini Ulenje, kwa hili utalilipia, huwezi kunifanyia ushenzi kama huu, nimesha washusha askari wako wanne na sasa nawasubiri hawa wengine niwapukutishe kisha niitafute familia yako kwa gharama yoyote lazima niiangamize” alisema Songoro kwa sauti yenye hasira kali, “lakini Songoro tunaweza kuliongea hili, labda niambie upo wapi sasa hivi?” aliuliza Ulenje kwa sauti ambayo tayari ilikuwa imesha onyesha wasi wasi, nadhani baada ya kusikia kuwa familia yake itahusishwa.
Lakini kabla hajajibu lolote, mara Songoro akasikia kishindo cha kitu kama silaha kikianguka chini mita chache pembeni yake, akageuka haraka na kutazama upande ule, na kwa macho yake akamuona Side akiwa ameachia bunduki ianguke chini, huku yeye akiwa amesimama kwa kuganda, mikononi ipo shingoni, viganja vimefunika koo vinavuja damu nyingi sana, mdomo upo wazi unavuja damu nyingi pia, kama ilivyokuwa puani mwake, nikama Side anajaribu kumueleza Songoro jambo fulani lakini anashindwa.
Songoro anamtazama Side kwa mshangao na uoga kama vile ameona mzimu, maana hajaelewa amekutwa na nini, hapati jibu lolote zaidi hali ya Side inazidi kuwa mbaya, anamuona Side anakosa nguvu anashindwa kuendelea kushikilia koo lake, anachia na kuruhusu macho ya Songoro, yaweze kuona jeraha kubwa shingoni kwa Side, ni jeraha kubwa kiasi kwamba, ungesema ni mbuzi au ng'ombe amechinjwa, damu zinatoka kwa wingi kama bomba la maji lililopasuka, Side anaenda chini kama furushi la pumba.
“mzee umeamua kufuata kifo chako mwenyewe” ilisikika sauti nyuma ya songoro, ambae bado alikuwa anajiuliza maswali bila majibu, Songoro anageuka kwa haraka na kutazama ilikotokea sauti, hapo anakutana uso kwa macho na sura ya upole ya kijana ambae mpaka leo hajaelewa kama ni kweli sura yake au kuna kinyago anakivaa ili kuficha sura yake halisi, “dereva” anatamka Songoro kwa kuhamaki, huku anainua bunduki yake ambapo inashikwa haraka na kupapaswa juu ya kava ya mitambo na sehemu ya magazine, Songoro anawahi kuminya trigger lakini anashangaa kuona inaenda bure kwa maana ya kwamba, inakosa kizuwizi chochote, huku spring ya mitambo inafyetuka, kitengo hicho kinamaanisha kuwa tayari kifuniko cha mitambo yani recever cover ilisha tolewa. Weweee hatariiii ...ENDELEA
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWA MATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THELATHINI NA TISA: ambae bado alikuwa anajiuliza maswali bila majibu, Songoro anageuka kwa haraka na kutazama ilikotokea sauti, hapo anakutana uso kwa macho na sura ya upole ya kijana ambae mpaka leo hajaelewa kama ni kweli sura yake au kuna kinyago anakivaa ili kuficha sura yake halisi, “dereva” anatamka Songoro kwa kuhamaki huku anainua bunduki yake, ambapo inashikwa haraka na kupapaswa juu ya kava ya mitambo na sehemu ya magazine, Songoro anawahi kuminya trigger lakini anashangaa kuona inaenda bure, kwa maana ya kwamba inakosa kizuwizi chochote, huku spring ya mitambo inafyetuka, kitengo hicho kina maanisha kuwa tayari kifuniko cha mitambo yani recever cover ilisha tolewa. .....…….ENDELEA…
Kwa macho ya mshangao, Songoro anatazama kwenye mkono wa kushoto wa kijana huyu mpole, aliekuwa amesimama mbele yake, anamuona ameshika mkebe wa risasi, huku mkono wa kulia ukiwa hewani unakuja shingoni mwake, na kabla hajafanya lolote kwa kasi ya ajabu na nguvu ya nyati unakita ubavuni mwashingo hilo, kiasi cha kupenya nusu nzima ya kifaa hicho chenye urefu wa centimeta ishilini, “de…de…dereva” alihangaika kuongea Songoro huku anarudi nyuma kwa kupepesuka kama mlevi aliezidisha kipimo, kisha akaenda kujikwaa kwenye mwili wa Side aliekuwa amelala chini, kitendo ambacho kinasababisha bwana Uledi Songoro ajibwage chini kama mzigo.*******
Yap! Chitopela sasa yupo ndani ya hema kubwa, zuri lenye mwanga hafifu, amesimama mbele ya kioo kidogo huku wanawake wote wanne wakiwa wanamvua nguo kila mmoja cha kwake, mmoja akiwa anamvua kiatu mmoja anamfungua mkanda, huku mwingine anamfungua vishikizo vya koti, hayo yote yaliambatana na matendo ya kimahaba, kama vile kumtomasa tomasa sehemu mbali mbali za mwili bila kusahau sehemu ya kiume, huku mmoja wao akiwa ameshilia grass ya pombe kali, ambayo alikuwa anamnywesha taratibu, waliyafanya hayo kwa kuamini kuwa wanae mfanyia hivyo anaenda kuwa kiongozi wa nchi ya #mbogo_land.
Wakati hayo yanaendelea mara kikasikika kishindo kama cha paka au jibwa toka nje ya hema, hapo Chitopela akatulia kidogo kisikilizia kama ni kweli kishindo cha mnyama aliemfikilia au kuna kitu kingine ambacho hajakisikia vyema, lakini kikapita kimya, akajua kuwa ilikuwa ni michato ya paka au jibwa kama alivyofikiria, hivyo hata wale wanawake ambao walitulia kama alivyotulia waziri Chitopela nao wakaendealea kufanya walichokuwa wanakifanya.
Sekunde chache baadae, tayari waziri alikuwa amesha pembuliwa nguo zote, akakaa kwenye kitanda na sasa wanawake wale wanne ambao sasa walikuwa wamepembua nguo zao, walikuwa wanacheza na viungo vya uzazi vya Waziri, ambae alikuwa amesha valishwa joho la kulalia, mwanamke mmoja aliekuwa anamkanda mkanda mabega wazir Chitopela, mwingine alikuwa anachezea tuchuchu twa kiume kifuani kwa mzee huyu, wakati mwingine akipapasa tumbo la mwanaume huyu mtu mzima alie acha mke wake amelala kitandani huko TT City, yeye akiwa ametulia anasikilizia mdomo wenye joto katika msitu huu wenye baridi ukiwa umemeza dudu yake na kuimung’unya kama vile anakula ice crem ya cony.*********
Naaaaam, tayari askari walikuwa wamesha maliza kuwakagua wale vijana wa Songoro, lakini licha ya kusikia milipuko ya risasi mita chache mbele yao, bado hawaoni wakirejea, “oya watu wote wanakuja huku, hebu Othman bakia hapa na askari watano, ngoja sisi tuwafuate hao, wasije wakawa wameenda mbele zaidi” alisema Cheleji, huku anaingia kwenye gari na askari nao wakaingia kwenye magari mawili wakibakiza gari moja tu na askari watano pamoja na kiongozi wao Othman, kisha safari inaanza kuelekea kule ambako wenzao walikuwa wameenda kuwakimbiza wakina Songoro.
Sasa basi msafara ule wa bwana Cheleji haukufika mbali, kabla haujakutana na miili ya askari wao wanne waliokuwa wamelala barabarani, wanashuka kwenye gari kwenda kuona kilichowakuta wenzao, macho yanawatoka kwa mshangao wa kuto kuamini walicho kiona, roho zinawauma, wengine wanatoa machozi ya uchungu ungesema leo hii ndio mara yao ya kwanza kuona watu waliouwawa, wakati muda mfupi uliopita walihusika kuuwa watu wanane, pengine hii ni kwasababu ya ukaribu wao, hawakuangalia uharifu wao, “kumbe zile risasi walikuwa wanashambuliwa wenzetu” alisema Cheleji, huku anatoa simu yake na kupiga kwa Ulenje ili kumpa hii taarifa mbaya sana, lakini alipopiga simu ile akakutana na sauti ya kike, ikimueleza kuwa “mtumiaji wa simu ile anaongea na simu nyingine, tafari subiri au jaribu tena baadae” Cheleji anakata simu na kuiweka mfukoni, kisha kwa hasira anaongoza kupanda kwenye gari, “hawa washenzi lazima wapatikane na wauwawe” anasema Cheleji, huku wenzake wanaingia kwenye magari na kuondoka kwa speed kuelekea mbele hawa kujua kuwa huko wanakoenda ndio kugumu zaidi.*********
Yaaap! msafara wa magari mengi ya polisi, unaonekana ukifika pale makutano ya barabara ya kisarawe na kibaha na kushika njia ya kuelekea upande wa kibaha, yakiwa katika mwendo wa kasi sana, gari la kumi na moja ni gari la kamanda polisi wa mkoa wa kipolisi wa ilala, ASP Ulenje, ambae anaonekana akiwa ametulia simu ikiwa sikioni anasikiliza jambo linaloendelea upande wapili wa simu, kiukweli sasa alikuwa katika wakati mgumu sana, ukiachilia kugundua kuwa aliekuwa hai ni songoro mwenyewe, ambae sasa tayari alishauwawa ila kilicho mshtua ni kile ambacho kimemtokea Songoro, muuwaji wake akiwa ni dereva, “hallow najua bado upo hewani na unanisikia vyema bwana Ulenje” ilisikika sauti toka upande wapili wa simu.
Ulenje anashtuka sana kwa kusikia jina lake likitajwa na mtu ambae alijuwa wazi kuwa ni Dereva.*******
Naaam wakati hayo yanaendelea huko porini, kisarawe kazimzumbwi, na kwenye kambi ya UMD, kitu ambacho Chitopela na major Kwanguru hawakuwa wanakifahamu, kuna watu walikuwa kilomita sabini mbali na wao, ndani ya jiji la Treanch Town, ndani ya chumba fulani chenye mwanga hafifu ulioletwa na TV kadhaa kubwa zilizopachikwa kwenye ukuta mmoja wa mbele wa chumba kile, wakiwa wanatazama matukio ya kibabe na kinyama yaliyokuwa yanaendelea ndani ya kambi lile, huku vitu kama heard phone zikiwa masikioni mwao.
“upande A kupo safi” ilisikika sauti toka kwenye zile speeker za masikioni, huku ikionyesha kipande katika TV moja kubwa, yenye alama A, pembeni, ambayo ilionyesha eneo la kambi ya mafunzo ya UMD, ambayo ilionyesha vijumba hafifu vya nyasi na miili mingi ya askari waliokuwa wamelala chini damu zikiwavuja sehemu mbali mbali za miili yao, “upande B safi” ilidakia nyingine, ambayo kama mwanzo nayo ilionyesha mazingira ya kambi lile, lakini sasa ungeweza kuona pamoja na askari wa MLA wenye kuvalia mavazi meusi wakiwa wanasonga mbele, pembezoni mwa vibanda dhaifu vya nyasi, kwa umakini wa hali ya juu, kambi lilikuwa kimya chini askari wametapakaa, kwa kulala kwenye vidimbwi vya damu.
“Ok! sasa hakikisheni kwa kutumia akili nyingi sana, mnawakamata hao wawili, hellcopter ipo njiani sambamba na askari na magari ambayo yatawasafirisha mateka na wafungwa wao” ilisikika sauti mmoja kati ya watu waliokuwepo ndani ya chumba kile, ambae sasa tuna mtambua kuwa ni major General Sixmund, “ndiyo mkuu” ilisikika hiyo sauti toka kwenye hear phone, huku video namba A, inaonekana ikisogelea taratibu na kwa tahadhari kwenye hema zuri, na wakati huo huo wanaonekana askari MLA, mbele ya camera ile alama A, wakijitokeza na kugawana njia kulizunguka lile hema na visu vyao mkononi, hatua chache mbele tunamuona askari mmoja wa UMD, akiwa amelala chini tayari alisha shugulikiwa, askari wa MLA anamruka bila kumjari anasonga mbele.
Wakati huo camera C, inawaonyesha askari wawili mbele ya camera za miwani, wanaonekana wakisogele mlango mkuu wakuingilia pale kambini, ambapo tuliweza kuowaona askari wa eneo lile wakiwa wametulia wanasinzia hawana habari yoyote, askari wanawasogelea kwa mwendo wa chui mwindaji, mpaka wanapowafikia kisha kimya kimya wanawakaba na kamba kutokea nyuma na kukita visu vyao kwenye vifua vyao usawa wa titi la kushoto.
Kama vile kunywa chai kwa mkate, askari wanatulia na wale askari wa MLA wanawalaza chini, “upande C, safi” inasikika ile sauti na kabla Sixmund hajasema chochote, ghafla unaonekana mwanga wa gari kama mita mia tano hivi kwenye barabara ya kujia kambini, “tunaingia” inasikika sauti kwenye visikio vya masikioni, huku yale magari yakianza kuja mbio mbio.
Naaam wakati huo huo tukirudi kwenye camera A, tunaweza kumuona askari mmoja MLA, anamvizia askari mlinzi mmoja wa UMD, pembeni ya hema zuri na safi, ambalo ndani yake alikuwemo wazir Chitopela, aliekuwa anaamini kuwa amesha kimbia kukamatwa na serikali ya kifalme ya #mbogo_land.
Askari mwenye mavazi meusi wa MLA, anazidi kumsogelea yule askari wa UMD, aliekuwa amesimama anajivutia bangi yake pasi na kuwa na habari ya kuwa kuna mtu anasogelea, yeye alikuwa busy na kile kivuto chake haramu, ambacho kule kusini mwa Africa wanaita Kangonya.
Kufumba na kufumbua anastuka kuna mtu yupo karibu yake ile anageuka kujihami, tayari kisu kimesha penya kwenye chemba ya moyo wake, na kabla hajaanguka chini yule askari anamdaka, na kumlaza chini taratibu, kisha askari anatazama upande wa camera yetu, ambayo kumbuka ipo usoni kwa mtu, imevaliwa kama miwani, anaonyesha ishala ya kwamba mmoja apite, hapo mmoja anaonekana akipita kwa mwendo wa tahadhari, akifuatiwa na camera na kuibukia upande wa mbele wa hema, ambako wanakutana na askari mwingine MLA, yule aliepitia upande wa pili, hapo wakaonyeshana ishara ya kuingia ndani ya hema. .....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapahapa
jamii forums