Man Middo tz
Senior Member
- Sep 9, 2020
- 182
- 279
- Thread starter
- #21
SIMULIZI: SABABU NI KIFO CHAKO BABA! (Kisa cha kweli cha kusisimua)
SEHEMU YA TISA (09)
MTUNZI: Man Middo Tz
WHATSAPP: +255 655 969 973
Damu zikawa zinatoka nyingi harafu ziwezi hata kuusukuma ule mzigo kwa pembeni, nikaa kama dakika 5 bila kupata msaada ndipo baadhi ya wanafunzi waliokua wamepanga karibu wakanikuta.
“HE! Jaman pole Hesha, hujaumia?”
Nikajibu kwa kutikisa kichwa, sikuweza hata kuongea, mwingine akasema
“Lakini huu mzigo mbona mzito sana harafu kuni zenyewe mbichi na usiku unaingia kwani hakuna watu wengine wakupeleka mpaka wewe au kwasababu wewe ni bonge”
Waliendea kuongea pale huku wakinionea huruma, basi baadhi yao wakachukua zile kuni na kuzipeleka bustanini na mimi wakanirudisha nyumbani.
Sasa kufika nyumbani mama Frida kuniona tu akasema
“Khee! Kumetokea nini tena na kuni zangu zimefika?” Wale vijana wakamjibu
“Tumemkuta kadondoka chini na kuni zimemlalia anaonekana anaumwa ila kuni tumezipeleka ila..”
“Haya hongereni”
Kabla hajamaliza yule mama akamkata kauli, alikua ni mmoja kati ya wale vijana walionisaidia, wakashangaa kisha wakaondoka.
Basi nikafikiria huenda nitapelekwa hospitali kwa hali yangu lakini wapi. Sasa maumivu yakawa makubwa mnoo, nikajiuliza
“Inamaana huyu mama haoni kuwa hali yangu, hata kama mimi sio binti yake ila anakosa hata ubinadamu je nikimfia hapa hatalaumiwa kweli?” Niliwaza sana lakini sikupata jibu.
Sasa usiku kwenda kulala maumivu niliyosikia sio ya mchezo, ule mzigo ulikua umeniumiza sana, pia ukizingatia nilikua naumwa kwa kweli nilijua nitakufa siku hiyo.
Kwenye kulala nililala kifudi fudi, yani huwezi kuamini nikilala chali au kulalia ubavu nikua nahisi maumivu makubwa mnoo mwilini ikawa kupiga yotwe tu.
Sasa jambo lililokuja kunishangaza ni asubuhi nilivyoamka nikajikuta NIMEJIKOJOLEA hapo hapo kitandani, sasa Frida akagundua
“Wewe Hesha Tabia gani hii, yani unajikojolea msichana mzima khaah!”
Kilikua kitendo cha aibu sana kwangu na ukizingatia nipo kwa watu, harafu hata huko mtaani na shuleni naonekana mchafu.
Hapo nikaona nipo kwenye wakati mgumu ila kwasababu ni bahati mbaya nikamuomba Frida kuwa
“Frida naomba usimwambie Mama Kwasababu nikutokana naumwa na sijwahi kufanya kitendo hiki”
Nikashukuru Mungu akanielewa, sasa maajabu ikwa ni tabia endelevu yani nakojoa hata bila kubanwa mkojo. Maisha sasa yakabadilika nikawa najichukia mnoo! Nikakosa amani, sina furaha aibu kama yote, Nikawa najiuliza mengi sababu ni nini? Msichana kama mimi kidato cha kwanza najikojolea, je ikijulikana itakuaje!?
Nikawa namuomba Frida asimwambie mama yake kila siku lakini mwishoe akagundua aisee daah!.
“Khee! Mwanamke mzima unakojoa kitandani, haya chumba kinanuka mikojo ya mtu na maziwa yake huna hata aibu looh! Sasa hakuna sabuni ya kufulia ukikojoa utajua mwenyewe”
Ooh my God!!! Huyu mama alivyokua na kiherehere akaenda kuwambia wale wa kaka, ambao mmoja ni mtoto wa yule mwanaume wa mama yangu na rafiki yake. Mungu wangu! Wakawa wananitania sasa
“Kikojozi kikojozi”
Hapo kila muda nililia yani, nikajichukia mnoo na ukizingatia sina nguo ndio nikawa rafu kama nimeokotwa.
Kipindi chote hicho bado naumwa sijapona na hali ni hiyo, harafu pia mama yangu mzazi bado hajui kitu....... ITAENDELEA.
Unadhani kipi kitatokea, Aisee mengi yanakuja. Kumbuka ni Kisa Cha kweli.