Simulizi: Umalaya na Ukahaba wa Kishua

Simulizi: Umalaya na Ukahaba wa Kishua

Siyo sawa kusema kwamba

👇👇
*"Malaya ni mtu anaependa ngono, awe ni mwanamke au mwanamme, mradi anapenda ngono basi huyo ni malaya. Kwa asilimia kubwa umalaya unahusishwa kwa wanawake tu, lakini ukweli ni kua hata wanaume baadhi yao huwa ni malaya tu."

Siyo sahihi neno malaya kutumika kwa mwanaume.

Malaya ni mwanamke mwenye wanaume wengi, asiyetulia na mwanaume mmoja kwa wakati mmoja.

Kwa upande wa mwaume asiyetulia na mwanamke mmoja kwa wakati mmoja linatumika neno muhuni
Kwa tafsiri kutoka katika kamusi ya kiswahili sanifu, Malaya ni mtu asiye na msimamo awe mwanume au mwanamke ,Nyerere alishawahi kumuita Oscar Kambona ni malaya.
 
mwanamme kuwa na uwezo wa kulala na wanawake wengi ni sifa na anaitwa rijali.
mwanaume kuwa na wanawake wengi ni umalaya. Rijali ni kuridhisha na si kutembea na wanawake wengi.
Unaweza tembea na wanawake wengi sababu ya tamaa na pesa zako zinakuwasha na usiwaridhishe hao wanawake.
 
Episode 1: Introduction.

Hii episode ya mwanzo itakua zaidi ni utangulizi (introduction) ya kujua watu na maana ya maneno yalivyotumika. Tutajitahidi ziwe ni posts fupi fupi ili isiwe tabu kwa wasomaji.

Hivi ni visa vinavyotokana na matukio ya ukweli kwa kiwango kikubwa. Tutatiriririka navyo hapa, visa na mikasa vya umalaya na ukahaba unaofanyika kwenye nyumba za kishua zinazojulikana kama geti kali, kwa njia ya episodes zitazotokana na muhusika anaeongelewa. Kwenye hii episode ya kwanza tutaanza na familia ya kishua kabisa, ya Mama na Baba Nisha, kwa kiwango kikubwa episode hii itawahusu familia ya Mama na Baba Nisha na ndugu, jamaa, marafiki na watu wao wanaowazunguka kwa karibu kabisa.

Visa na mikasa mingi ya umalaya na ukahaba, huhusisha familia za walala hoi, lakini visa hivi vitavyofatia, vitajikita katika familia zinazojiweza kimali na kifedha, au kwa ufupi "familia za kishua" pia zinajulikana kama geti kali.

Kwanza kabisa tuelewe maana ya neno "malaya" na maana ya neno "kahaba".


Malaya
Malaya ni mtu anaependa ngono, awe ni mwanamke au mwanamme, mradi anapenda ngono basi huyo ni malaya. Kwa asilimia kubwa umalaya unahusishwa kwa wanawake tu, lakini ukweli ni kua hata wanaume; baadhi yao huwa ni malaya tu.

Umalaya hutokana na mengi, lakini zaidi hutokana na maisha zinavyoishi familia ndizo huchochea umalaya

Malaya huwa hajiuzi kufanya au ngono kwa ajili ya pesa au kipato. Yeye ni mpenda ngono, ambae hatosheki kwa ngono, yupo tayari kufanya ngono na yeyote, awe ndani ya familia au nje ya familia, awe wa jinsia yake au nyingine, mradi yeye akidhi kiu yake ya ngono tu.

Kahaba
Kahaba ni mtu anaejiuza mwili wake ili ajiingizie kipato au apate anachokitaka, si lazima awe na shida ya pesa, pengine anashida ya kutaka kitu fulani kifanyike, basi atafanya ulaghai kutumia maumbile yake ili afanikishe lake. Hajali kabisa kujiuza ili yake yaende.

Hizo ndio maana za malaya, umalaya na kahaba au ukahaba zilivyotumika kwenye visa hivi.

Kwa maana hizo kwenye kisa hiki tutaona kua, malaya na makhaba si lazima wawe hawajiwezi. Binafsi naamini, Umalaya na Ukahaba mkubwa zaidi hufanyika kwenye familia za kishua kuliko familia za kawaida, za walala hoi.

SOMA:
Sehemu inayofuata
Sehemu inayoendelea
Sehemu inayofuata
It is so interesting kuona watu wanapenda sana story zinazohamasisha uzinzi, story zisizookoa kabisa ila zinapoteza. Mungu anatupenda lakini, Mungu anapenda malaya wabadilike au makahaba unavyowaita. nakumbuka siku Yesu alipowakuta washika dini wakiwa tayari kuanza kumpiga mwanamke aliyekamatwa uzinzi,akawaambie asiye na dhambi awe wa kwanza, wote wakakimbia kwasababu walijiona wana dhambi. Rehema za Mungu zipo kwa kila mmoja wetu kwa dhambi zozote tulizozifanya, anatuhitaji tutubu na kubadilika.

Biblia katika Warumi 2:4 imeandikwa, Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?

maana yake, kila siku kila saa ukiona u mzima, jua Mungu amekuweka mzima ili utengeneze maisha naye, uokoke, uache dhambi ili ustahili uzima wa milele. ni neema kwasababu kuna wengine wamekatika tu ghafla kwa ajali ila wewe upo hapa u mzima unapiga story za uzinzi. Mungu anakuita, anataka utubu na uugeukie Wokovu kwa Yesu Kristo.
 
Back
Top Bottom