Simulizi: Umalaya na Ukahaba wa Kishua

Kwa tafsiri kutoka katika kamusi ya kiswahili sanifu, Malaya ni mtu asiye na msimamo awe mwanume au mwanamke ,Nyerere alishawahi kumuita Oscar Kambona ni malaya.
 
mwanamme kuwa na uwezo wa kulala na wanawake wengi ni sifa na anaitwa rijali.
mwanaume kuwa na wanawake wengi ni umalaya. Rijali ni kuridhisha na si kutembea na wanawake wengi.
Unaweza tembea na wanawake wengi sababu ya tamaa na pesa zako zinakuwasha na usiwaridhishe hao wanawake.
 
It is so interesting kuona watu wanapenda sana story zinazohamasisha uzinzi, story zisizookoa kabisa ila zinapoteza. Mungu anatupenda lakini, Mungu anapenda malaya wabadilike au makahaba unavyowaita. nakumbuka siku Yesu alipowakuta washika dini wakiwa tayari kuanza kumpiga mwanamke aliyekamatwa uzinzi,akawaambie asiye na dhambi awe wa kwanza, wote wakakimbia kwasababu walijiona wana dhambi. Rehema za Mungu zipo kwa kila mmoja wetu kwa dhambi zozote tulizozifanya, anatuhitaji tutubu na kubadilika.

Biblia katika Warumi 2:4 imeandikwa, Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?

maana yake, kila siku kila saa ukiona u mzima, jua Mungu amekuweka mzima ili utengeneze maisha naye, uokoke, uache dhambi ili ustahili uzima wa milele. ni neema kwasababu kuna wengine wamekatika tu ghafla kwa ajali ila wewe upo hapa u mzima unapiga story za uzinzi. Mungu anakuita, anataka utubu na uugeukie Wokovu kwa Yesu Kristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…