Simulizi ya Fred Vunjabei na Frank Knows

Simulizi ya Fred Vunjabei na Frank Knows

Encryption

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
997
Reaction score
1,348
Mfanyabiashara Fred Vunjabei ameandika hadithi fupi kuhusu maisha yake ya kibiashara na rafiki yake Frank Knows.

Ameandika hivi:-

[emoji117]Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa na duka moja dogo sana Kariakoo (Goli), baada ya kujikusanya tulikubaliana na rafiki yangu Frank Knows twende kujaribu kununua mzigo China, tulisubiri kipindi cha tiketi za offer na tukapata Ethiopian Airways, tulifanikiwa kufanya utafiti wa maana sana China na tukajilaumu tulikuwa wapi siku zote, Ndoto zangu nlianza kuziona zikikamilika licha ya kuwa China ilitakiwa uwe na hela nyingi na wote tulisafiri na pesa kidogo sana hazikutosha kununua mzigo.

Nilitafakari nifanye nini? hesabu zetu zilionesha kununua mzigo mdogo China ni kazi bure na hela itapotea, mwisho wa siku niliamka asubuhi nkamuita Frank nikamwambia “Nimeamua kukupa hela yangu yote ukifanikiwa utanishika mkono ukifeli tutakuwa tumejifunza kitu” alinishangaa sana, Alipojumlisha na yake jumla ikawa million kumi na mbili (12mil), Nlifanya hivyo kwa sababu zifuatazo;

Moja, Nilijua lazima mmoja wetu akubali kuwa na subira na mwingine atangulie (urafiki wetu hatukuwahi kuweka wivu na ubinafsi mbele)

Pili, Frank alikuwa na wateja wengi kuliko mm hivyo angezungusha hela haraka zaidi. (Ni vema kukubali ukweli)

Nilimuacha Frank akazungusha hela kwa muda kama wa miezi 6 na alikuwa akisafiri mara kwa mara, nlifurahi kumuona akifanikiwa na nilimsaidia sana kutafuta wateja na kumshauri, baada ya hapo alikuja akanipa 20,000,000/= (Cash) na tukaondoka wote tukaenda China kufunga mzigo. Nilifunga mzigo mzuri sana sababu Frank alipata experience kubwa na alikuwa ananionesha masoko mazuri bila kuona wivu.

Moral of the story: Urafiki wenye wivu na ubinafsi hauna tofauti na kufuga ng’ombe dume wawili then utegemee kupata maziwa.

Screenshot_20210127-132226.jpg
 
Porojo tu

Huyu bwana kuna interview nimewahi msikia alikuwa serikalini na alishafanya pia mashirika na taasisi binafsi huku akifanya biashara.

Alipoona amepata mtaji akaamua kuacha ajiajiri. Leo anasema alikuwa na mtaji mdg, porojo tupu.
 
porojo tu

huyu bwana kuna interview nimewahi msikia alikuwa serikalini na alisha fanya pia mashirika na taasisi binafsi huku akifanya biashara

alipoona amepata mtaji akaamua kuacha ajiajiri leo anasema alikuwa na mtaji mdg porojo tupu
Sasa enzi anazosimulia ni baada ya kuacha kazi Serikali kuu, kumbuka mtaji mdogo anaoongelea ni Milioni kadhaa
 
Sasa enzi anazosimulia ni baada ya kuacha kazi Serikali kuu, kumbuka mtaji mdogo anaoongelea ni Milioni kadhaa
Mkuu kabla ya kuanza tripu za china kwa maelezo yake alisema alikuwa kasha pata mtaji wa kutosha akaona ateme kazi leo anasema hazikutosha kule china
 
Back
Top Bottom