Simulizi ya kifantasia na kijasusi: The darkness of an angel

Nakukumbusha tu kwamba simulizi hii unaweza kuipata pale Fasihinet kwa link hii hapa chini 👇

Ipo yote mwanzo mpaka mwisho episode ya 122.

Kazi kwako
 
Attachments

  • Screenshot_20250819-152433.png
    Screenshot_20250819-152433.png
    390 KB · Views: 43
  • downloadfile-247.jpg
    downloadfile-247.jpg
    439.4 KB · Views: 48
HADITHI: THE DARKNESS OF AN ANGEL
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WhatsApp: +255621567672
Email: [email protected]
UMRI: 18+

SEHEMU YA KUMI

UWANJA WA FISI.
Ni moja ya maeneo maarufu ndani ya jiji la Dar es salaam, ni eneo ambalo hata ukimuulizia mtoto yeyote ambaye anaishi mitaa ya Manzese, Mburahati, Magomeni, Tandale na mitaa ya jirani anakupeleka. Umaarufu wake hauishii kwenye hayo maeneo tu bali kwa jiji zima la Dar es salaam ni maarufu.

Umaarufu wake unasababishwa hasa na shughuli ambazo zinaendelea ndani ya hilo eneo. Ni eneo maarufu na la kihistoria kwa sababu lipo miaka na miaka, umaarufu wake umekuja kutokana na aina ya maisha ambayo huwa yanapatikana ndani ya eneo hilo. Ni eneo ambalo zinazungukwa na watu wenye maisha ya chini sana, ni sehemu ambayo kwa zamani ilikuwa moja ya vituo vikubwa vya madawa ya kulevya na biashara ndogo ndogo hususani kwa wale watu ambao walikuwa wanatoka mikoani na kuja kujaribu bahati zao za kuweza kutafuta mlo ndani ya jiji kubwa la biashara.

Wengi walijikuta wakiishia kwenye mazingira magumu wakati wakiwa wanazipambania fursa ndogo ndogo zilizopo ambazo hata wazawa walikuwa wanazihitaji pia ndipo ikazuka biashara ya uuzaji wa miili kwa wanawake, biashara ya umalaya ikawa na umaarufu mkubwa mbapo imezidi kukua kila mwaka na kulifanya eneo hilo kuwa maarufu zaidi.

UWANJA WA FISI, ukitaja hilo jina kwa watu ambao wanasali ni eneo ambalo linaonekana kulaanika vilivyo lakini kwa wasaka tonge na kwa baadhi ya watafutaji ambao maisha yamewapiga parefu basi huona kama ni sehemu mhimu kwa ajili ya maisha yao. Usihukumu hautahukumiwa bwana! Wahenga wanasema hivyo kwa sababu kabla ya kumhukumu mtu ambaye anaponea eneo hilo basi kaa kwenye nafasi yake kwanza kisha uweze kuangalia kwamba kama ungekuwa wewe ungefanya nini kuweza kuikwepa hiyo hali? Ni eneo ambalo linalimiki danguro maarufu sana mjini, vijana kwa wazee ambao hawawezi kumiliki wanawake warembo wa mjini kutokana na gharama kubwa za maisha ambazo zinalivaa jiji la Dar huwa inawalazimu kwenda eneo hilo kwa ajili ya kuwatumia malaya hao kukidhi mahitaji yao ya kimwili.

Mbali na hilo imekuwa fursa kwa wajasiliamali pia ambao wengine wamefungua maduka na vibanda vya biashara eneo hilo. Aina ya maisha ambayo inaendelea kwenye hilo eneo ndiyo yanaifanya biashara hiyo kuwa maarufu zaidi huku ikifunguliwa miradi mbalimbali karibia na hilo eneo kwa sababu mzunguko wa watu unazidi kuwa mkubwa kila siku. Ni maeneo ya uswahilini haswa ambayo hayafai hata kwa ajili ya malezi ya watoto kwani kizazi ambacho kinapatikana eneo hilo sio kile kizazi ambacho kinaweza kutegemewa na taifa kwa ajili ya kuitengeneza kesho iliyo bora.

Ni kawaida eneo kama hilo hususani mida ya usiku mwanamke kuvaa chupi pekee na kutamba nayo akiwa anainadi biashara ya mwili wake, mabinti wengi ambao wamekosa kazi mjini, ambao wamekosa fursa za maisha na wengine ambao maisha yamekuwa magumu kwao wakajikuta hawana sehemu nyingine ya kukimbilia basi wamejikusanya ndani ya eneo hilo kuhakikisha nao wanaendana na kasi ya jiji.

Danguro hilo licha ya kupigwa marufuku na serikali lakini imekuwa ni ngumu kuweza kufungwa kutokana na kwamba serikali imekosa mbadala wa kuwatengenezea fursa za maisha na ajira ambazo zinaweza kuwakomboa watu wengi ambao wanalitegemea eneo hilo kwa ajili ya kuishi. Kushindwa kwa serikali kupata mbadala, ukosefu wa elimu thabiti, upungufu wa fursa za maisha umeifanya hata serikali mara kadhaa kuweza kufeli mpango wake wa kuifunga sehemu hiyo na kujikuta wanaimba SONG OF LAWINO mbele ya mbuzi ambao hawawezi kuelewa kwa sababu maisha duni ni KILIO CHAO hilo eneo hivyo wameacha waishi kwa namna watakavyo wao wenyewe.

Majira ya saa tano za usiku eneo hilo la UWANJA WA FISI, palikuwa pamewaka mno, shamra shamra kila sehemu zilikuwa zikisikika huku watu wakiwa wanayafurahia maisha ambayo walijiona kuwa wasindikizaji. Watu mbalimbali walikuwa wamejigawa, wengine walikuwa wakipata pombe, watoto walikuwa wamezagaa mtaani, wenye biashara zao muda ulikuwa unawaruhusu kutengeneza pesa kutokana na uwepo wa wanunuzi. Mabanda ya video nayo hayakuwa haba, vijana wengine walikuwa wanaendelea kujaribu bahati zao kwenye kamari lakini wote hao walikuwa wanakusanywa hapo na biashara moja kubwa ambayo ndiyo ilikuwa maarufu ndani ya eneo hilo kuliko jambo lolote lile.

UMALAYA, biashara ya uuzaji wa miili, yaani uwepo wa malaya ndani ya eneo hilo ndiyo ambao uliwafanya watu kupishana kila sehemu. Wadada na gauni zao za kubana na kutamanisha, sketi zao zilizo yachora maumbo yao vyema, suruali zao ambazo zilivigawa vipande vya miili ambavyo walibarikiwa na kuwafanye wale wanaume wakware kutokwa na mate, wengine wakiwa kwenye nguo za ndani tu, walijipanga pembezoni mwa vichochoro wakiwa wanainadi biashara yao. Wengine walikuwa wamesimama pembezoni mwa vyumba vyao kuruhusu biashara ya haraka haraka kuweza kufanyika.

Wanaume hawakuwa nyuma kuwa wateja wazuri, walihakikisha wanafanya kila waliwezalo kuhakikisha kwamba warembo hao walikuwa wanakula na kushiba. Kila wakati walikuwa wakiingia kwenye vyumba hivyo kwa kupokezana tena kwa uharaka mkubwa wakati ambao pembezoni mwa chumba kimoja, alikuwa ameketi binti mmoja juu ya kiti kidogo. Binti huyo alikuwa ni maji ya kunde yale ambayo yamekolea sana, alikuwa anavutia kumtazama na huenda hata kwa wanaume ambao walimuona eneo hilo iliwauma kwa sababu ya uzuri wake.

Huenda alitakiwa kuwa mke wa mtu ambaye wakati huo angekuwa ndani analea watoto na kutengeneza maisha bora lakini wanasema kwamba Usilo lijua ni sawa na usiku wa giza. Maisha hayakuwa sehemu yake, maisha yalikuwa tofauti na yale matarajio yake makubwa ambayo alikuwa nayo kiasi kwamba hakuwa na sehemu nyingine ya kuweza kuponea zaidi ya kwenda kupambana na ridhiki ngumu ndani ya hilo eneo. Alionekana kutumika sana siku hiyo kwa sababu hata sura yake ilionyesha uchovu wa hali ya juu na hata mwili wake uliongea kwa lugha ya picha lakini mwanaume gani alikuwa ana hiyo huruma ya kuweza kumuachilia mwanamke mrembo kama yule? Yaani Dar es salaam mtu akupe pesa bure kwa sababu tu una shida zako za kutoka huko kwenu? Hapana, jiji linaamini kwamba unatakiwa ufanye kazi ndipo ule, jua ni kali ila pesa unatakiwa kuitolea jasho kwanza ndipo uweze kuitia mfukoni.

Bibie yule ambaye alikuwa na uzuri wa pekee alionekana kuwa mbali kimawazo, alikuwa ameishika simu yake ya kidigitali mkononi lakini hata hakuonekana kuwa na muda nayo, kwa mbali mziki ulikuwa unasikika kumfariji mja wa Mungu ambaye maisha yalikuwa yanaonekana kumvuruga vilivyo. Akiwa amekaa pale amezama kwa mawazo mengi, alifika kijana mmoja mtanashati ambaye baada ya kuuona tu ule mwili hakujiuliza mara mbili zaidi ya kuingia ndani, yule mrembo ile biashara yake alikuwa akiielewa vyema hivyo naye aliingia na kuufunga mlango.

Lakini wakati anaingia ndani ndipo umbo lake halisi lilionekana, kama ungemkuta maeneo ya katikati ya jiji ungeomba awe mkeo na akuzalie watoto ukiamini kwamba ni mwanamke wa ndoto zako, haikuwa rahisi kutambua kwamba alikuwa anafanya biashara ya ngono. Mrembo yule alimaliza dakika tano akaufungua tena ule mlango huku yeye mwenyewe akionekana kuipandisha sketi yake fupi ambayo ilikuwa inauonyesha vyema mwili wake na ndani yake hakuwa amevaa kitu chochote, alikuwa kwenye biashara hivyo hakutaka kujipa kazi ngumu kwenye biashara yake hiyo.

Kuna jambo moja ambalo lilishangaza kabla hajatoka, alifunua godoro lake na kuzitoa bastola mbili akazipachika kiunoni wakati ambao alikuwa ameitoa sketi na kuvaa suruali kisha akatoka nje. Baada ya kutoka aliuvuta ule mlango ikiwa ni ishara ya biashara yake kusimamishwa kwa muda. Wenzake wa karibu walikuwa wameanza kupungua huku wengine wakija kuchukuliwa na bodaboda, alienda kukaa eneo lile lile ambalo alikaa mwanzo huku akionekana kwamba hakuwa sawa.

“Kila mtu ana simulizi yake ya maisha ambayo huwa hataki ulimwengu uifahamu, kila binadamu anayaishi maisha ambayo hakuna mtu anayajua vizuri, vivyo hivyo hata mimi nina maisha yangu ambayo ni wanadamu wa kuhesabika tu ndio wanayajua, naweza kusema wengi hakuwa wanalo lijua kuhusu maisha yangu” alimeza mate akiwa anaangalia hewani, kuna kijana alimsogelea na kumshika sehemu zake za nyuma pale ambapo alikuwa amekaa, alimkata jicho kali mpaka kijana yule akaondoka mwenyewe. Alikuwa anazitambua sheria za maeneo kama hayo kwamba huwa yanakuwa na ulinzi hivyo kama angeleta ujuaji angeweza kudhalilishwa ndiyo maana aliamua kuondoka mwenyewe kabla hajaingia kwenye majanga ikawa shida kwa upande wake.

“Mimi ni malaya, ni kweli hii ni kazi yangu ambayo siwezi kuikataa. Mimi ni malaya ambaye ninauza mwili wangu tena kwa pesa ambayo huenda hata haitoshi kununua nusu kilo ya nyama na ndiyo sababu inanilazimu kwa siku moja kulala na wanaume wengi ili niweze kupata hata pesa ya kutunza na ya kufanyia malengo. Sisemi hivi kwa sababu najivunia kwa kazi ambayo ninaifanya, lahasha! Bali kwa sababu sina namna na ndiyo kazi yangu ambayo imenitambulisha ndani ya hili jiji.

10 inafika mwisho.

Febiani Babuya.
 
HADITHI: THE DARKNESS OF AN ANGEL
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WhatsApp: +255621567672
Email: [email protected]
UMRI: 18+

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Kazi yangu imenifanya nikakosa heshima, imenifanya nikakosa thamani kwa sababu wengi kuniona hapa wanaona kama takataka isiyo na muokotaji, wananiona kama ni chombo cha starehe kwao ambacho wanatakiwa kukitumia watakavyo wao, lakini je ni uongo? Jibu ni hapana, kila ambalo wanalisema na kuliwaza ni sahihi kabisa. Umalaya sio kazi ya sifa wala kazi ambayo unapaswa kuiringia, ni moja ya kazi za laana hapa duniani, ni kazi ambayo inakufanya uwe mtumwa, ni kazi ambayo inanifanya nisemwe kwamba ni mtu ambaye nimepoteza mwelekeo wa maisha, naonekana kama nimezikimbia fursa nyingi mtaani nikaamua kupambana na kazi iliyo laanika kama hii.

Siwalaumu ambao wanaongea hivyo kwa sababu kwa upande wao wapo sahihi lakini sio kila mtu anakuja huku kwa sababu anaipenda hii kazi wala anatamani kuendelea kuwa sehemu ya maisha haya. Wengi ambao wapo ndani ya hili eneo ni mabinti ambao wametokea kwenye maisha magumu, maisha ambayo hayana mfano hata wa kuweza kusimuliwa. Hawakuwa na namna zaidi ya kujitoa wenyewe ili kutengeneza fursa ambazo serikali na familia zao zinaishia kuzihubiri tu ila hazijawahi kuzitengeneza hata siku moja na ndiyo maana hapa wamejazana kuweza kufanya biashara na sio kwa sababu hatuzioni fursa zingine au hatuoni kazi zingine, ukweli ni kwamba kazi zingine na hizo fursa hazipo na kama zipo basi haziwezi kuwatosha watu wote hawa.

Nakubali kwamba hii biashara ni ulevi mbaya, ni biashara ambayo ukiianza kutoka huku ni kazi ngumu na kubwa ndiyo maana hata baada ya kupata pesa, wengi wamejikuta bado wakiendelea kuhangaika kuifanya. Mimi sidhani kama ni mmoja wao, nasema hivi kwa sababu historia ya maisha yangu ina utofauti mkubwa na haya maisha yangu japo siwezi kuyakataa ndiyo maana tangu mwanzo nimeyakubali. Kila mwanadamu huwa ana utofauti ambao unamfanya kuwa tofauti na watu wengine na ndio ambao huwa unamfanya kuwa imara zaidi ya wengine, huo utofauti hautakiwi kujulikana kwa mtu mwingine yeyote zaidi ya mhusika mwenyewe kwa sababu huo ni uimara na udhaifu utofauti wake ni matumizi yake tu na namna wengine wanavyo uona. Acha nikurudishe nyuma unijue kwa undani kabla ya mimi kufanya moja ya matukio ya kutisha ambayo yataingia kwenye historia ya hili eneo hapa” binti huyo mrembo alitamka akiwa anauma ulimi wake, alihema na kuufungua vizuri mdomo wake tena ili kuweza kuileta hadithi ya maisha yake na sababu ambayo ilimfanya kuishia ndani ya hilo eneo lakini kufanya jambo ambalo yeye mwenyewe aliweza kutishia kwamba alikuwa anaenda kulifanya kwa wakati huo.

“Mimi ni mtu wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, nimezaliwa mkoani Kagera huko ambako tunatokea kabila maarufu hapa nchini, kabila ambalo sio kelele tu bali hata uwezo mkubwa tunao. Ni kabila ambalo limezalisha wasomi na matajiri wengi ndani ya taifa hili lakini pia hata ujivuni huwa ni sehemu kubwa ya maisha yetu ndiyo maana huwa tunaonekana kama ni watu ambao tuna maringo mengi. Mbali na kuzaliwa eneo la namna hiyo lakini mimi sijahabatika kuwa na hivyo vitu vyote.

Sidhani kama napaswa kuwalaumu wazazi wangu japo mara moja moja kuna muda huwa naona kama ni wao ambao walifeli kunitengenezea mimi maisha ya kunifanya niishi vizuri kwa amani na furaha lakini kuna nyakati baada ya kuyajua maisha huwa naona kama nilifanya kosa kuanza kuwalaumu wao. Jina langu naitwa Atusime Byarugaba, hili ni jina ambalo nilipewa na mwanamke ambaye alinizaa baada ya baba yangu kumkimbia alipokuwa na mimba lakini kwa hapa mjini wananijua kama Irene.

Maisha ya nyumbani hayakuwa mazuri, huenda ni kwa sababu sikuwa na baba ndiyo maana ila ukweli ni kwamba nimeishi maisha ya hovyo na magumu mno. Kama ambavyo ni kawaida ya kule nyumbani, mabinti wengi huwa wanaona fursa nzuri ni kuja ndani ya hili jiji la wajivuni wenzetu na wajuaji kwa ajili ya kujipatia fursa mbalimbali za maisha na biashara basi hata mimi niliamua kuwa moja ya sehemu ya watu wa namna hiyo ambapo baada ya ukata mkubwa wa maisha niliamua kukimbia kule nyumbani. Wakati ambao nakimbia nilikuwa nimejaribu kila aina ya maisha lakini yalishindikana.

Nilibarikiwa urembo na uzuri ambao haukuwa ukiisha kwenye mwili wangu, nilikuwa sehemu ya maisha ya mwanamke wa kupendwa na kila mtu lakini hata pale nilipo jaribu kuutumia uzuri wangu kwa ajili ya kujipatia maslahi yangu sikufanikiwa kuwa sehemu ya maisha mazuri. Niliishia kutumika tu na wanaume washenzi na baadae wakaamua kunitupa na kunifanya nikawa sina mwelekeo, nikawa naendelea kupata majuto tu. Nilifanikiwa kumpata bwana mmoja ambaye alinipatia mimba lakini mimi na yeye hatukuwa na mwisho mzuri kwa sababu aliikataa ile mimba na baadae nilikuwa mtu wa mawazo mengi mno kwani niliona kama maisha yangu yanaenda mwisho mpaka siku mimba yangu ikaja kutoka yenyewe.

Pale ndipo niligundua kwamba mshale wa masaa unasoma kuliko akili yangu ilivyokuwa inafikiria, kila nilipo muangalia mama yangu mzazi, nilimuona mwanamke jasiri ambaye alikuwa anaelekea kukata tamaa ya maisha jumla, niliumia na moyo wangu haukuwa tayari kuona jambo lile. Ningesema kwamba nitafute ajira nzuri lakini sikuwa msomi kwani niliishia kidato cha pili tu mpaka pale mama aliposhindwa kabisa kunilipia ada hivyo kazi zinazo hitaji wasomi hazikuwa sehemu ya maisha yangu.

Nilitamani nifanye biashara lakini sikuwa na mtaji wa kufanya hivyo, nikawa naishia kulia kila wakati mpaka siku ambayo nilikutana na moja ya marafiki zangu wa shule ya msingi, Koku. Koku alikuwa binti mashuhuri ambaye alikuwa amepotea kwa muda mrefu kule nyumbani, alikuwa binti mmoja ambaye alirudi akiwa amenona na kunawiri, sio siri niliyatamani yale maisha yake na kuwa sehemu kama aliyokuwepo yeye. Binti huyu alinitangulia mimi kwenda mjini ndiyo maana vitu vingi alivijua kabla yangu. Nilimkalisha kitako na kumtaka anipe njia za kuwa kama yeye, nilitamani kuwa sehemu yake na mimi niishi vizuri kama ambavyo nilikuwa naona yeye anaishi kwa wakati ule.

Akiwa bado binti mdogo alikuwa tayari amefanikiwa kumjengea mama yake nyumba, alikuwa tayari amemfungulia mama yake biashara japo haikuwa kubwa lakini iliwahakikishia kula kila siku na kuweza kubadilisha mavazi ndipo akasema kwamba kama nataka kuwa kama yeye basi wakati anaondoka kuja ndani ya jiji la Dar, nilitakiwa kuongozana naye. Alidai anaenda kunifundisha maisha ya mjini na namna watoto wa kike wanavyo zitafuta pesa kwa nguvu na jasho kuliko hata baadhi ya wanaume, nilimuona ni shujaa wangu mpaka pale ambapo nilifika jijini.

Kila maisha yana mwanzo wake, kila maisha yana ukurasa wake mpya, bila kuusoma huo ukurasa huwezi ukaelewa namna ya maisha yanavyokuwa na yanavyokwenda mpaka siku ukizigusa kurasa zake ndipo utayaelewa mambo kwa upana na urefu wake. Ile safari mama yangu aliipinga sana, alikuwa tayari kuyavumilia yale maisha lakini sio kuona mtoto wake wa pekee naenda mbali naye tena sehemu ambayo hakuwa na uhakika kabisa na usalama wangu. Mama yangu aliniambia nisije jijini kwa sababu aliamini nitatengeneza maisha ambayo huenda yanaweza kunifanikishia ndoto zangu au utakuwa mwanzo wa majuto makubwa kwenye maisha yangu lakini sikuwa tayari kuona ile hali nyumbani inaendelea kuwepo, ilikuwa ni kheri nikajaribu nifeli kuliko kukaa na kuangalia yeye anateseka kwenye maisha yale ambayo tulikuwa tunayaishi pale nyumbani.

Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nikafika ndani ya jiji ambalo lina sifa nyingi ukiwa nje ila ukiwa ndani yake kuna wakati zile sifa ambazo huwa linapewa hata hauzioni. Nikawa nimeingia rasmi Dar es salaam, rafiki yangu alikuwa anaishi Kinondoni, ndiko alikokuwa amepanga hivyo nilipofika kwake na kuona namna alivyokuwa anaishi kisasa, ni kweli kwamba nilimuonea wivu na kutamani mimi ningekuwa yeye, nilihisi ni mtu ambaye alikuwa na biashara zake nzuri tu mpaka mara ya kwanza alipohitaji kunifundisha kazi kwani sikuja mjini ili kulishwa, nilikuja kuangalia fursa za biashara, hiyo ndiyo ikawa mara yangu ya kwanza kuja hapa Uwanja wa Fisi ambapo mpaka dakika hii nimekaa pembezoni mwa hiki chumba ambacho wanaume wananitumia watakavyo wao na kuniona kama binadamu niliye takataka ama sijielewi ila hawajui tu kwamba nilikuja hapa kwa sababu sikuwa na chaguo lingine.

Nilishangazwa na aina ya maisha ya hapa ila sikuwa na nmna, baada ya kugundua kwamba rafiki yangu alikuwa ni malaya nilitambua kwamba nilikuwa na kazi ngumu na kubwa mbele yangu. Mara ya kwanza niliikataa kazi hii ila akaniambia kama sipo tayari basi natakiwa kurudi nyumbani ili nikaendelee kulima na kufubaa huku umaskini ukiwa unaniadhibu kila siku. Alinitaka siku hiyo nikae nishuhudie yeye akiifanya kazi hiyo na kweli nilifanya hivyo na mpaka anafunga alikuwa na pesa ya kutosha, pesa ambayo kama ungeihifadhi kwa mwezi basi ungejikuta una pesa nzuri tu. Pesa sabuni ya roho nikajisemea ni bora nirudi na ushindi nyumbani au irudi maiti lakini sio kuikimbia pesa hivyo nikaamua rasmi kujifunza biashara ya kuuza mwili wangu ili nipate pesa.

Rasmi na mimi nikawa sehemu ya jamii ya watu hawa ambapo nilikaa hapa kwa mwaka mzima nikiwa naifanya biashara hii, nilikuwa na uzuri wa kipekee, mvuto na umbo langu la kuvutia. Ukijumlisha na nilipo anza kujitunza na kutengeneza pesa nilianza kunawiri na uso joto la mjini likanikubali, kila mwanaume akawa anahitaji kulala na mimi hivyo nikajikuta natengeneza pesa nyingi mno ambazo zilinisaidia mimi kuanza kuyabadilisha maisha ya nyumbani taratibu. Kwenye hii biashara kuna wivu mkubwa, wivu ambao kwa huko nje huwa wanauita ushindani ila huku hakuna ushindani hivyo kama ukiwa unafanya biashara kuwazidi wengine basi wanaweza kukufitini au kukufanyia jambo lolote baya hivyo unaweza ukajikuta unaishia kupata matatizo au kurudi nyumbani kwenu mapema. Haya yote rafiki yangu alikuwa amenifunza vyema hivyo sikuwa fala hata kidogo, maisha yangu yakaanza kubadilika taratibu.

11 inafika mwisho.

Febiani Babuya.
 
Nakukumbusha tu kwamba simulizi hii unaweza kuipata pale Fasihinet kwa link hii hapa chini 👇

www.fasihinet.com www.fasihinet.com

Ipo yote mwanzo mpaka mwisho episode ya 122.

Kazi kwako
 
Attachments

  • downloadfile-53.png
    downloadfile-53.png
    390 KB · Views: 39
  • downloadfile-260.jpg
    downloadfile-260.jpg
    439.4 KB · Views: 38

Mambo ni moto
 
hivi vipande vya leo hata sijavielewa..sema mtunzi ufupishe hizi history za flash back ni ndefu hadi zinaboa
Mkuu kwanza pole sana kama hizi simulizi zinakuboa.......

Pili hii simulizi ni mwendelezo wa za kwanza hivyo flashbacks hazikwepeki unless achana nayo tu maana itazidi kukuboa...

Tatu: Mimi ni mwandishi wa simulizi ndefu hivyo kama zinakuboa sana sidhani kama mimi ni mwandishi sahihi kwako kumsoma....

NB
Kuwa na amani kwa sababu hiyo simulizi haitaletwa tena JF...

Wishing you a good day mkuu 🤝
 
Achana nae huyo
 
Kazi zuri sana hila mwendelezo umekawia sana.shambiki wako kutokea Nairobi Kenya.
 
MIAKA 15 NYUMA YA UKUTA WA GEREZA!!!!!

Alan, anatokea kwenye umaskini ulipo pitiliza, dunia inamfunza kuwa mshenzi ili aweze kuishi ndipo anaingia kwenye ulingo wa MAUAJI ili aweze kupata mkate wake.... Huko anaanza kuua watu kwa miaka mitano ambapo anafanikiwa kutengeneza pesa za kitanzania Bilioni 5....

Baadae unagundulika ulingo huo ulikuwa kinyume cha utaratibu hivyo wahusika wote wanakamatwa na kuporwa kila kitu yeye anafanikiwa kuachwa hai ila akiwa maskini kama zamani....

Baadae anapata kazi ya kwenda kumuokoa mtoto wa tajiri mmoja ndani ya jiji la ABUJA, NIGERIA ambaye alitekwa na magaidi kwa malipo ya shilingi bilioni 10 za kitanzania lakini kazi hiyo inaishia pabaya baada ya binti huyo kuuawa na yeye mwenyewe kudungwa sindano yenye sumu kali sana....

Alan anapotea namna hiyo lakini miezi miwili baadae anakuja kuonekana mtu ambaye anafanana naye kwenye kamera za shirika la kijasusi la Tanzania yaani (TIA) TANZANIA INTELLIGENCE AGENCY ndani ya jiji la Dar es salaam jambo ambalo linawashangaza kwa sababu walijua alikufa na walikuwa na uhakika na hilo ......

Wakiwa wanajiuliza na kuanza kufuatilia mkasa huo ndipo Tanzania inavamiwa na magaidi kwa ajili ya kesi ile ile baada ya miaka mitano kwa madai ya kwamba walihisi bwana huyo bado alikuwa hai tena aliwaibia kiasi cha shilingi bilioni 20 za kitanzania.

Nchi inaingia sehemu mbaya huku wakimtafuta bwana huyo bila mafanikio kwa miaka 15.....

Wanapata uvumi wa kwamba bwana huyo alipotea kwenye mazingira ya ajabu bila kuacha taarifa nyuma ila kwa taarifa za kudhania zilidai kwamba mwanaume huyo alienda kujificha kwenye GEREZA Moja la Siri ambako aliishi kwa miaka 15 ....

Sasa ni kipi kilimpeleka huko? Ni kweli kwamba alikuwa ni yeye hakufa kule Nigeria? Kama sio yeye ni nani alikuwa anatumia sura yake? Kwanini apotee miaka 15 tena kwenda gerezani?

KAMA ULIKUWA UNATAMANI KUKUTANA NA SIMULIZI YA KIJASUSI YENYE WATU WENYE NGUVU ZA AJABU (SUPERNATURAL POWERS) Upo sehemu sahihi..... Karibu sana.

Hii ni simulizi ambayo ina mapigano, upelelezi wa hatari, mapenzi, siasa, supernatural powers ( nguvu za ajabu) na story ambayo imeshiba haswa...... FANTASY

Unaweza ukaipata kwa shilingi 5000 tu za kitanzania kwa namba hizi hapa chini 👇

0621567672 (HALOPESA)..... WhatsApp

0745982347 (M-PESA)

0714581046 (TIGO-PESA)

0689440143 (AIRTEL MONEY)

36316279 (LIPA NAMBA (M-PESA) inapokea mitandao yote)

FEBIANI BABUYA
 
Attachments

  • Miaka 15.jpg
    Miaka 15.jpg
    379.1 KB · Views: 48
Back
Top Bottom