Simulizi ya Kijasusi: Bado Ninaishi

Simulizi ya Kijasusi: Bado Ninaishi

FEBIANI BABUYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2022
Posts
1,916
Reaction score
3,850
Hi! once again fellas, mimi ndiye yule mwandishi wa simulizi za kijasusi kama ULIMWENGU WA WATU WABAYA, I WANT TO DIE JUDGE, GEREZA LA HAZWA, NYARAKA NAMBA 72, JIJI LA KAMARI, NAFSI ZILIZO TELEKEZWA na zingine.

Leo kwa mara nyingine nadondosha wino wangu ndani ya huu mzigo mzito na mkali wa kusisimua vilivyo. Mzigo ni simulizi ya kijasusi ama wengine wanapenda kuita ya KIPELELEZI, ni wewe tu utakavyo.

Bila shaka ni moja kati ya simulizi bora sana ambazo utazisoma sio tu kutoka kwangu bali katika maisha yako yote. Kama umeyasoma maandiko yangu kadhaa basi utakuwa unaelewa wazi kwamba sibahatishi kwenye huu ulimwengu.

Simulizi hii itakuwa inaletwa episode moja kila siku na kama ikitokea siku sijaileta basi siku ambayo nitakuwa online nitafidia vipande vya siku ambazo sikuwepo.

Sanjari na hilo ni kwamba simulizi hii ipo yote mwanzo mpaka mwisho kabisa, italetwa hapa lakini kwa wale ambao wanahitaji kuisoma yote kwa pamoja wanakaribishwa sana inbox kwangu kwa maelekezo ambayo yanakuja hapo chini kwenye introduction yetu ili ili ujue unaenda kusoma nini ndani na utamsoma nani. Baada ya introduction naachia na episode ya kwanza.

See you [emoji872]

CIAO

IMG-20240614-WA0002.jpg
FB_IMG_1713700409446.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240614-WA0002.jpg
    IMG-20240614-WA0002.jpg
    116 KB · Views: 54
BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)

Intro.....

Inamhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa ni kiongozi wa genge la kihalifu ambalo lilikuwa linaitwa SARAFU KUMI NA TANO.

Mwanaume huyo alikuwa anasakamwa na mamlaka za usalama ndani ya taifa la TANZANIA kwa miaka kumi bila mafanikio. Ndipo alitumika mwanamke mrembo ANELIA BATON ambaye alimwingiza mwanaume huyo kwenye HONEY TRAP kwa kupitia kikosi hatari kutoka ndani ya shirika la kijasusi kiitwacho HOLY TRINITY, walifanikiwa kumpata na kumkamata.

Alihukumiwa kifungo cha miaka sitini gerezani na baada ya hapo angenyongwa. Alipelekwa ndani ya gereza hatari la DOMINIC, huko alikutana na tajiri mmoja ambaye alikuwa amejificha ili kuyalinda maisha ya mwanae ambaye alitekwa.

Tajiri huyo alikutana na mwanaume huyo aliye itwa REMMY CLAUDE na kumuomba akamuokoe mwanae yeye angemsaidia kumtorosha gerezani. Walifikia makubaliano mwanaume akatoroshwa gerezani.

Huko uraiani alienda kumtafuta mtoto wa kiongozi huyo lakini wakati anafanikisha hilo tajiri huyo alikuja kupata habari kwamba mfungwa huyo aliye mtorosha gerezani hakufungwa kwa bahati mbaya bali ilikuwa ni mipango yake yeye ili akutane na tajiri huyo.

Alishangaa sana inakuwaje mtu ajitoe kafara kufungwa gerezani kwa sababu yake? Ndipo akaja kugundua kwamba Remmy alikuwa anautafuta umoja wa watu ambao hawakuwa wakifahamika na tajiri huyo ndiye mtu pekee ambaye angemsaidia kuwajua wote ndani ya umoja huo.

Anakuja kushtuka akiwa amechelewa, mwanaume huyo alikuwa amempata mwanae tayari na kupotea naye hali ambayo ilileta maafa makubwa sana Tanzania na kulilazimu shirika la kijasusi kuanza na moja kumtafuta.

SARAFU KUMI NA TANO halikuwa pambo bali ilikuwa idadi ya wanafamilia ambao waliuawa kikatili takribani miaka ishirini iliyokuwa imepita ila kwa bahati mbaya mtu mmoja alifanikiwa kuishi.

Sitaki nikumalizie uhondo. Unataka kujua huyo Remy ni nani? Kwanini alijitoa sadaka kwenda gerezani? Huo umoja una nini hasa ndani yake na unaongozwa na nani?

Nini hatima ya maisha ya Remy Claude?

Hili ni moja kati ya andiko ambalo litakufanya ujivunie sana kuyasoma maandishi.

Sasa RASMI IMEACHIWA NA UNAWEZA KUIPATA KWA PESA ZA KITANZANIA SHILINGI 5000 TU.

5000 yako unapewa andiko lote mpaka mwisho kwa softcopy safi kabisa ukae nayo.

Unaweza kufanya malipo kwa namba hizi hapa [emoji116]

0621567672 (WhatsApp).... HALO-PESA

0745982347..... M-PESA

0714581046..... TIGO-PESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Ni wakati sasa..... KARIBU INBOX.

ASHRAFU NDILO JINA LANGU

Wasalaam,
FB_IMG_1713700409446.jpg
 
Asante kwa kutuletea simulizi
Utaimaliza hadi mwisho au tukutane whatsApp?
Simulizi hapa itafika mpaka mwisho, ukisoma vizuri maelekezo hapo juu nimeelekeza vyema. Ni kwamba kila siku lazima tusoma ila WhatsApp ni kwa wale ambao hawataki kulaza damu, yaani wale ambao wanataka kusoma full kwa mkupuo.

Nadhani nimeeleweka madame.
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672

SEHEMU YA KWANZA

GEREZA LA DOMINIC
Kiza totoro kilizalisha nyota za kuvutia angani ikiwa ni usiku sana. Dunia ilikuwa imetulia hususani yale maeneo ambayo watu walikuwa wanautegemea mwanga wa jua kufanya mijongeo ambayo haikuwa na mwisho bali mwanzo ambapo ungeona watu wanatoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya utafutaji na mahitaji mengine ya kibinadamu.

Hali ilikuwa ni tofauti sana kwa usiku huo wa manane ambao ulikuwa umezongwa zongwa na kiza kinene, shukrani kwa taa za umeme ambazo ziliufanya mji uendelee kuvutia na kupendeza huku mvua zikiwa zinashuka kwa wingi na kufanya mijongeo ya watu kuwa michache sana.

Usiku huo ndio wakati ambao msafara wa gari tano za jeshi ulikuwa barabarani kwa spidi huku madereva wakionekana kuwa makini kuhakikisha kwamba wanafika salama mahali ambapo walitakiwa kuwepo usiku huo. Gari hizo za jeshi zilikuwa zinalilinda gari moja la wafungwa ambalo lilikuwa katikati ya gari zingine na kuufanya msafara huo kuwa na jumla ya gari sita ambazo zilikuwa kwenye mwendo wakati huo.

Msafara huo ulikuwa unaelekea nje ya mji, sehemu ambayo kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo kiza kilivyokuwa kinazidi kuwa kingi kwani nje ya mji hakukuwa na taa za kusema kwamba zingemlika kila sehemu hususani zile ambazo hazikuwa makazi ya watu.

Gari hiyo ya wafungwa ndani yake ilikuwa na cage (kizimba) ndogo ya chuma ambayo ndani yake alikuwa amehifadhiwa mfungwa huku kwenye mwili wake akiwa amefungwa minyororo kila sehemu. Hakuonekana kuwa mtu mwema sana wala kuwa mtu wa kawaida sana ndiyo maana licha ya uwepo wa makamanda wa jeshi wa kuaminika bado hawakumpa mtu huyo nafasi ya kuweza kuwa huru hata kidogo zaidi ya kumfunga minyororo karibia sehemu yake kubwa ya mwili.

Ndani ya hiyo cage ndogo kwenye hiyo gari ya wafungwa, alionekana mwanaume mmoja kwa mbali kutokana na uhaba wa mwanga ambao ulikuwepo usiku huo. Kipara kilichokuwa kinang'aa sana kilionekana kwa usahihi kabisa, mwili wake ambao ulikuwa umegawanyika vipande vipande ulijichora vyema ndani ya gari hiyo huku akionekana wazi kwamba aliyafumba macho yake kama sio kulala usingizi.

Haikujulikana mwanaume huyo alikuwa amefanya kitu gani hasa kwenye maisha yake mpaka kuwekewa ulinzi mkali sana namna hiyo huku makamanda wa jeshi wapatao sita wakiwa ndani ya gari hiyo na silaha zao walizielekezea kwa mwanaume huyo kiasi kwamba kama angefanya jambo lolote baya basi risasi zilitakiwa kumhusu moja kwa moja.

Baada ya safari ya muda mrefu gari hizo zilisimama ghafla sana hali ambayo ilimfanya mwanaume huyo kuyafumbua macho yake. Macho yalikuwa yanawaka moto kwa kumtazama mwanaume huyo kwa mbali, ni macho ambayo yalionekana kuongea lugha nyingi sana za hisia zenye maumivu makali ambayo hayakujulikana nini kilikuwa chanzo chake hasa mpaka akaishia kwenye hiyo minyororo.

Mbele ya sehemu ambayo gari hizo za jeshi zilisimama kulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa ambao ulionekana wazi ulikuwa umejengwa kwa uimara mkubwa kwa muda mrefu sana. katikati ya kuta hizo kulikuwa na lango kubwa la vyuma ambalo baada ya msafara huo kufika hapo lilifunguliwa taratibu na ndipo wanaume hao wakaingia na gari zao.

Juu kabisa ya hilo lango kubwa kulikuwa na maandishi makubwa ambayo yalikuwa yameandikwa GEREZA LA DOMINIC. Lilikuwa ni gereza la kuogopeka zaidi ndani ya nchi ya Tanzania, gereza ambalo hakuna mfungwa aliwahi kutamani kuingia huko hata kama angekuwa na kosa gani kubwa. Yote ni kwa sababu ya taarifa ambazo zilikuwepo zikidai kwamba lilikuwa kinyume kabisa na haki za wanadamu na wananchi wengi sana walikuwa wakilipigia kampeni gereza hilo liweze kufungwa kwani hakuna mtu aliwahi kupelekwa huko halafu akafanikiwa kutoka akiwa hai na mzima wa afya. Huko ndiko ambako mwanaume huyo aliweza kupelekwa usiku huo na msafara wa kijeshi.

Kwenye moja kati ya vyumba vikubwa na bora zaidi ambavyo vilikuwepo ndani ya jengo hilo, alikuwa ameketi mwanaume mmoja ambaye gwanda lake lilikuwa na nyota za kutosha akiwa anapata chai taratibu huku kwenye mkono wake akiwa ameshika kishikwambi na kuendelea kusoma habari ya mtu ambaye muda mchache ujao alitakiwa kumpokea kwenye mikono yake.

Huyo ndiye alikuwa mkuu wa hilo gereza la Dominic, Luka Gambino ndilo lilikuwa jina lake. Mwanaume huyo aliwahi kuwa kanali wa jeshi kabla ya kuja kuipata nafasi hiyo na historia yake ya nyuma haikuwa nzuri sana. Akiwa hapo anapitia pitia taarifa za mwanaume huyo, mlango wa ofisi yake ulikuwa unagongwa ambapo alitoa ruhusa mgongaji aweze kuingia na wakati huo huo aliingia msaidizi wake.

"Mkuu mtuhumiwa amefika tayari, inasubiriwa amri yako tu" ndiyo kauli ambayo aliitamka iliyo mfanya kiongozi huyo kutoa tabasamu hafifu kwenye uso wake.
"Hii ndiyo habari kubwa zaidi ambayo mimi nilikuwa naisubiri kwenye maisha yangu. Kufanikiwa kumhifadhi mtu kama huyu eneo hili kutanipa sifa kubwa sana nchini na kila mtu atatamani kuhitaji kunifahamu mimi kwa undani kwamba ni nani hasa na hapa ndipo nitamuonyesha huyo bwana mdogo kwamba dunia sio sehemu salama sana hususani kwa watu wa aina yake. Naapa huu utakuwa mwisho wake mbaya, atatamani ni bora angefanikiwa kujiua kabla hajaingia ndani ya jengo hili. Nipeleke huko waliko sasa hivi" aliongea kwa msisitizo huku akiwa anachora alama ya X kwenye picha ya mwanaume huyo ambaye haikujulikana alikuwa amefanya kosa lipi mpaka watu waweze kumpania sana kiasi hicho.

Mwanaume ambaye alikuwa amefungwa ndani ya gari hiyo ya wafungwa alionekana kuwa kwenye mawazo makali mno baada ya kugundua kwamba alikuwa ameingia ndani ya kuta za gereza hilo.

Maumivu yalionekana kuutafuna sana moyo wake kiasi kwamba chozi lilikuwa linashuka kwenye mashavu yake huku likikosa mfutaji au mtu wa kuweza kulipa sehemu ya kuelekea. Haikuonekana kuwa sehemu njema kwenye maisha yake ndiyo maana alikuwa anatoa machozi, hiyo sehemu alionekana kuwa na historia nayo kubwa sana kiasi kwamba nafsi yake ilikuwa inamuenda mbio baada ya kuifikia.

Aliyafumba macho yake kwa hisia na alipokuja kuyafumbua tena machozi hayakuwepo kwenye macho yake na gari zilikuwa zinasimama kwa kasi kiasi kwamba aliyumba kidogo na kujigongesha kwenye nondo moja ya chuma ila hakuonyesha mshtuko wa aina yoyote ile kana kwamba kwake lilikuwa jambo la kawaida tu. Walishuka wanajeshi wengi na kuisogelea ile gari ambayo yeye alikuwepo na baada ya hapo wanaume sita ambao walikuwa wanamlinda walifungua milango mikubwa ya gari hiyo na kuitoa cage ambayo alikuwepo mfungwa huyo nje.

Wakati huo wote walitoa heshima kwa kiongozi mkuu wa gereza hilo ambaye alikuwa anafika wakati huo ndani ya hilo eneo. Mtu mzima wa miaka karibia sitini ndiye ambaye alikuwa anakuja kumpokea mfungwa huyo akiwa ndiye kiongozi mkuu wa gereza hilo. Alisogea mpaka walipokuwepo makamanda hao ambapo mmoja wao aliyekuwa kiongozi alimsogelea na kumpa heshima kisha akampa maelekezo ambayo alitakiwa kuyapata kabla ya kumpokea mfungwa wake.

"Mkuu kazi yetu ilikuwa ni kumfikisha hapa salama na kwa sasa kuanzia hapa itakuwa ni kazi yako. Wakubwa watakupa maelezo zaidi juu ya mtu huyu na kile ambacho unatakiwa kukifanya ila kuanzia sasa sisi tunageuza makao makuu. Usije ukafanya kosa la kumpa hata nafasi ndogo ya kuwa huru kwa sababu unaweza kuleta madhara makubwa sana ndani ya hili gereza ndiyo maana anatakiwa kuishi kwenye minyororo hivyo hivyo mpaka pale ambapo utakuwa na uhakika kwamba hatakuwa hatari tena kwa ajili ya maisha ya watu wengine ndani ya eneo hili"

"Hauna haja ya kuongea sana, najua aina ya mtu ambaye nimeletewa na nina uhakika pia hata wewe unajua aina ya eneo ambalo ameletwa hivyo yeye ndiye anatakiwa kuyahofia maisha yake kwani hii sehemu sio salama kabisa kwa mtu kama huyu na huenda akawa na maisha mafupi sana"

"Fanya yote ila usije ukamuua kwa sababu huenda akawa na matumizi kwa hapo baadae, ni mtu mhimu na anadaiwa kwamba huenda kuna taarifa za siri ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa hili ambazo anazo"

"Waambie hatakufa ila atatamani ni bora angekufa huko mliko mtoa, kwanza mmefanya kosa kubwa kumnyoa nywele zake akiwa huko, mlitakiwa kumleta hapa nimnyoe mwenyewe kwa chupa, mpuuzi mmoja kama huyu hatakiwi kuishi kwa starehe sana namna hii"

"Tusamehe kwa hilo mkuu, sisi tunaondoka na tunakutakia bahati njema" mheshimiwa hakujibu kauli ya kamanda mkuu wa kikosi bali alitabasamu tu huku akitoa ishara kwa vijana wake kwenda kumtoa mwanaume huyo kwenye cage ambayo alikuwepo huku makamanda wakiwa wanaondoka na gari zao kwa kasi ndani ya hilo eneo kwa sababu kazi yao ilikuwa imekamilika na kuanzia hapo maamuzi hayakuwa yao tena juu ya nini cha kukifanya kwa mwanaume huyo.

Baada ya kutolewa kwenye chuma ambacho alihifadhiwa, akiwa na minyororo mkononi na miguuni ambayo iliunganishwa mpaka shingoni, mwanaume alikuwa anasukumwa kuelekea ule upande ambao alikuwepo Luka Gambino ambaye alikuwa kiongozi mkuu wa eneo hilo. Mwanaume mmoja ambaye hakuwahi kuujua ustaarabu wala kuelewa maana halisi ya neno huruma kwenye maisha yake, alikuwa ni mtu mkatili sana ambaye alikuwa anaogopwa na kila mfungwa au mtu ambaye alipata kumjua japo kwa uchache tu kwenye maisha yake.

Mjongeo wake wa lazima, uliweza kumsogeza zaidi sehemu ambayo ilikuwa na mwanga wa kutosha hivyo ukasaidia kuweza kumuonyesha vizuri. Mwanaume wa miaka isiyo pungua thelathini na mitano alikuwa anaonekana vyema, macho yake yakiwa makali na mekundu sana. Hakuonekana kuwa sawa kwenye mwili wake kwa sababu alikuwa anavuja damu.

Kwenye mbavu yake ya kulia damu ilikuwa inatoka kwa wingi sana huku kisu kikiwa kimenasa eneo hilo kuonyesha kwamba kuna mtu alikizamisha na hakukitoa hivyo kikawa kinaendelea kumletea maumivu makali lakini hakuwa na muda nacho maana alivyokuwa amefungwa asingeweza kabisa kukichomoa. Miguuni alikuwa peku huku kila alipokuwa anakanyaga alikuwa anaacha damu, miguu ilitobolewa na misumari na nguo zake zilichakaa damu, paja lake la kulia likiwa na damu ya kutosha na nondo moja ambayo ilikatikia eneo hilo ikiwa bado haijatolewa. Ilionekana muda mfupi tu uliokuwa umepita mwanaume huyo alitoka kuchezea kipigo kizito sana kutoka kwa hao watu ambao walikuwa wamempeleka eneo hilo.

Ndo kwanzaaaaa tunaufungua ukurasa wa kwanza wa andiko hili.

Sitaki niongee sana, karibu kwa wakati mwingine tena tuweze kucheza na huu wino pamoja...


Bux it'sa ma neim.

CIAO
 
Wakisema Yesu anarudi sasa hivi, mwenye hela zaidi ya shillingi 100 anaenda Mbinguni, mimi mtaniacha Sembuse 5k
Haina shida, kwan yesu akirud na kuondoka we si unaendelea na ishu zako tu. Sio lazima akirud na wewe uondoke nae
 
Katika ubora wako mkuu, kongole sana kwa kutuliza kichwa na kuandika mambo ya kuamsha bongo zetu. You have my respect
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA PILI
Mkuu wa gereza alimsogelea mwanaume huyo huku akiwa anatabasamu sana lakini baada ya kufika na kumkagua mtu huyo aliikunja sura yake vibaya kwa ghadhabu kubwa.

"Wewe ndiye mpuuzi mmoja ambaye umenifanya mpaka usiku huu nishindwe kulala na mwanamke wangu nikae nikikusubiri hapa? Siwezi kuacha hili lipite, nakuhakikishia lazima ukalipe kwa hili mpuuzi mkubwa wewe. Niliwahi kuapa kwamba watu ambao walikuwa kwenye gereza hili walikuwa wanatosha na sikuwahi kuhitaji kuletewa mtu mwingine ila wewe umefanya kosa la aina ile ile ambalo sikuwa nahitaji litokee na hatimaye umeletwa huku sehemu ambayo hatakiwi kuhifadhiwa mwanadamu wa kawaida, je unajua ni kipi kitakupata kwenye maisha yako bwana mdogo? Niamini mimi ni bora wakati wa kiangazi ungeenda kuishi jangwani sehemu ambako hakuna hata maji ila sio kuletwa sehemu kama hii" aliongea akiwa anamzunguka mwanaume huyo ambapo alimtwisha rungu la chuma mgongoni lakini mwanaume huyo alibaki ameganda tu hivyo hivyo bila kutamka neno lolote lile wala kutikisika.

"Una familia?" kwa mara ya kwanza mwanaume huyo aliitoa sauti yake ambayo ilikuwa nzito sana na ya kukwaruza kwa mbali akionekana wazi kwamba alikuwa anamlenga ni kiongozi huyo wa hilo gereza. Alihisi aliisikia vibaya kiasi kwamba akawageukia vijana wake lakini aligundua kwamba mwanaume huyo alikuwa amemlenga ni yeye mwenyewe. Alishikwa na hasira kali mno kitu ambacho kilimfanya atoe bastola yake na kumpiga risasi mbili za kwenye mapaja mwanaume huyo mpaka akashindwa kusimama na kuishia kupiga magoti huku akiwa anauma meno kwa maumivu makali sana ambayo alikuwa anayapata wakati huo.

"Mpuuzi mkubwa wewe kijana, wewe hapo ndiye mtu ambaye unathubutu kuliingiza jina la familia yangu kwenye huu upuuzi wako? ulitakiwa kuisoma historia ya maisha yangu ya nyuma. Nina historia mbaya sana ya haya maisha mpaka leo kuwa kiongozi kwenye gereza kama hili ni bahati nasibu kwa sababu mimi nilitakiwa kuwa miongoni mwa wafungwa ambao wangekuwa wanayaishi maisha magumu ila mimi ndiye kiongozi kwenye sehemu kama hii. Ukajifunze maana ya jina langu la pili la Gambino nililipataje, kaisome familia yenye historia ya jina hilo huko Marekani kisha utagundua kwamba umefanya kosa kunijibu nikiwa naongea" aliongea kwa hasira huku akiwa anairudisha silaha yake kwenye mfuko wake ambao uliunganishwa na ganda lake kisha akawageukia vijana wake.

"Hatakiwi kulala kwa masaa arobaini na nane, apitie mateso makali ila hakikisheni hafi na hizo risasi atakaa nazo kwa muda mwilini akili imkae ndipo ataelewa kwamba huku sio kwa ajili ya watoto wa mama ambao wakiguswa tu wanataka kuwalilia mama zao na kuhitaji kunyonya. Akimaliza hiyo adhabu ndipo aanze kupatiwa matibabu kidogo kidogo" alitamka huku akiwa anageuka na kuelekea kwenye ofisi yake, muda ulikuwa umeenda sana hivyo alihitaji kurudi ili akajiandae kupumzika maana kazi ya kumpokea mfungwa huyo ilikuwa imekamilika tayari.

Mwanaume huyo akiwa ndani ya maumivu makali kwenye mwili wake, aliunyanyua uso wake ambao haukuwa na nuru hata kidogo kuangalia juu ya ukuta wa kuingilia kwenye vyumba ambavyo walikuwa wanahifadhiwa wafungwa mbali mbali, huko aliona maandishi makubwa tena yakiwa yameandikwa GEREZA LA DOMINIC. Baada ya kuliona jina hilo, kuna picha nyingi zilikuwa zinapita kwenye kichwa chake kwa kasi sana kiasi kwamba zilianza kumuumiza mpaka akayafumba macho yake, alipokuja kushtuka wanaume walikuwa wapo nyuma yake wakimnyanyua kwa nguvu huku wakimpiga na vitako vya bunduki zao kumtaka aelekee sehemu ambayo yangekuwa makazi yake mapya kwa wakati huo.

Luka Gambino baada ya kufika kwenye ofisi yake alisogea mpaka kabatini ambako alitoa chupa ya pombe na kuanza kuinywa kwa pupa akionyesha kutoridhika na kauli ya mwanaume ambaye muda mfupi uliokuwa umepita alitoka kumpokea kwa makamanda wa jeshi. Akiwa anainywa hiyo pombe yake aliingia msaidizi wake akiwa na bahasha mkononi mwake.

"Kuna kingine umesahau?"
"Ndiyo bosi"
"Sikio langu ni lako" alimaanisha anamsikiliza.

"Kuna hizi taarifa za mtu huyu zimefika muda sio mrefu, kuna mtu amezileta inaonekana zilisahaulika, pia kuna frashi ndogo inasemekana kwamba kuna taarifa zote za mtu huyo hivyo itakuwa ni jambo la busara kama tutafanikiwa kuweza kuzipitia na kuweza kumjua kiundani ukiachana na zile taarifa fupi ambazo zilikuja mwanzo" mheshimiwa baada ya kumsikia kijana wake anaongea hayo maneno, alisogea kwenye kiti na kumpa ishara kijana huyo kuelekea ukutani ambako kulikuwa na skrini kubwa ili aweze kumchambulia taarifa hizo na maelekezo yake yaliyokuwepo ndani.

"Remy Claude ndilo jina lake linalo daiwa kuwa la kuzaliwa lakini jina lake ambalo linafahamika sana kwa watu wake ni Menace likiwa na maana ya muuaji wa hatari. Mwaka huu anaingia mwaka wa thelathini na sita tangu azaliwe, hakuna alama yoyote ambayo inaonyesha kwamba alizaliwa wapi na lini ila taarifa zilizopo ni kwamba ni mtoto wa mtaani ambaye maisha yake hayana mwanzo bali mwisho wake utakuwepo."

"Ni kiongozi wa genge la hatari sana la kihalifu ambalo linajulikana kwa jina la SARAFU KUMI NA TANO (FIFTEEN COINS). Hizo sarafu kwa mujibu wake ni kwamba zilishapotea hivyo anazitafuta na haijulikani kwamba hizo sarafu zina maana gani kwa sababu jina la genge hilo linaonekana lilibadilika baada tu ya yeye kuanza kuliongoza"

"Watu ambao alikuwa anawaongoza kwenye genge hilo wanadaiwa kwamba kwa sasa wote wamekufa kwa kuuawa na mtu pekee ambaye amefanikiwa kuishi ni yeye ambaye ndiye alikuwa kiongozi. Ni genge la kimafia ambalo limesababisha athari kubwa sana kwa taifa yakiwepo mauaji ya kutisha, kuliyumbisha taifa kiuchumi lakini ilidaiwa kwamba pia genge hilo lilikuwa likisambaza madawa ya kulevya mitaani na kuwatumikisha vijana wengi kwa kuwaachisha masomo na kuwaingiza kwenye biashara hiyo huku wote ambao walikuwa wanapingana na genge hilo walikuwa wanaishia kuuawa na wanawake kubakwa hovyo hovyo" msaidizi wa mkuu wa gereza aliacha kwanza kuichambua na kuisoma taarifa hiyo huku jasho likiwa linamtoka kwenye uso wake. Yalikuwa ni maelezo ya juu tu lakini yalikuwa ni maelezo mazito sana ambayo hayakuwa na usalama mkubwa kwa walikokuwa wanaelekea. Alikunywa maji na kuikuza picha kubwa ya mwanaume ambaye walikuwa wanamuongelea hapo akiwa ndani ya suti safi na begi lake huku kwenye kichwa chake akiwa na nywele nyingi za kutosha kisha akaendelea tena.

"Baada ya jambo hili kutokea na kuwa kubwa mtaani ndipo serikali ilitengeneza mazingira ya kuweza kumkamata mtu huyu. Kumkamata haikuwa kazi rahisi kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye pesa na jina hivyo ulikuwa unahitajika ushahidi wa kutosha ili kumpata kwani kazi yake alikuwa anaifanya kwa usahihi na umakini sana. Hali hiyo ilipelekea maafisa wengi kupoteza maisha kwa wale ambao walikuwa wanaingia kwenye njia zake ili kuweza kumtafutia ufumbuzi mtu huyo na ndipo shirika la usalama la nchi lilipo amua kumvalia njuga kisawa sawa baada ya kukerwa na kupotea kwa maofisa wengi ambao walikuwa wanapewa kazi ya kuweza kumfuatilia mtu huyu"

"Sentinel Nexus Intelligence Agency (SNIA), shirika letu la usalama wa taifa chini ya mkurugenzi Cleopatra Gambo lilimteua mwanamke mrembo Anelia Baton kuweza kuifanya kazi ya kufanikiwa kumuweka karibu mwanaume huyo ili kujua njia zake zote ambazo alikuwa anazitumia kwenye biashara yake kwa ujumla lakini bila kusahau kuweza kuuangamiza mtandao wake wote ili ikiwezekana akamatwe ama kuuawa japo serikali ilikuwa ikimhitaji zaidi awe hai kwani angekuja kuwa na msaada mkubwa sana kwa taifa hapo baadae"

Sehemu ya pili inafika mwisho.

Wasalaam,
 
Back
Top Bottom