Simulizi ya Kijasusi: Bado Ninaishi

Simulizi ya Kijasusi: Bado Ninaishi

HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA TANO
"Henry why?"
"Wakati tunaendelea na hii kesi nilikuwa nafuatilia kwenye kila hospitali hapa nchini na rekodi za majina ya watoto ambao wamezaliwa tangu uje utaratibu wa kuwasajili majina watoto ambao wanazaliwa kila siku. Hakuna mtoto yeyote ambaye amewahi kuzaliwa nchi hii anaitwa Remy Claude, ni mtoto mmoja tu ambaye jina lilikuwa linashabihiana na lake aliyekuwa akiitwa Claudia Remy lakini yeye alikuwa ni wa kike na alikufa miaka ishirini iliyopita kwa ajali ambayo alikuwa na familia yake. Ndiyo maana namtilia mashaka mtu huyu kwa kuhisi hata majina ambayo anayatumia sio yake na ndipo inakuja hii nadharia ya kwamba huenda huyu mtu anayaishi maisha ya mtu mwingine na maisha yake sisi hatuyajui kabisa"

"Whaaaaaat?" maelezo ya Henry Mawenzi yalimshangaza kila mtu na kumshtua mkurugenzi wa shirika la usalama la Tanzania. Habari ilikuwa mpya kwenye masikio yao kumhusu mwanaume ambaye dunia ilimtambua kama Remy Claude kiongozi wa genge la kihalifu la FIFTEEN COINS.

“Bosi najua hili jambo ni lazima limekushtua kwa sababu limekuwa ni ghafla mno lakini naomba unipe ruhusa yako niweze kulifanyia utafiti na muda sio mrefu nitakuja na majibu ambayo ni kamili na sahihi kuhusu uhalisia wa maisha ya huyu mtu"
"Unataka kufanya nini?"
"Nataka nimtume kijana mmoja huko gerezani akafanye utafiti juu ya hili jambo"
"Una uhakika na hiki unacho hitaji kukifanya?"
"Ndiyo bosi"
"Basi lifanye hili jambo kwa umakini, nitaihitaji ripoti yako. Kwa sasa naondoka inatakiwa nikutane na mheshimiwa raisi niweze kuiwasilisha hii ripoti kwake"
"Sawa bosi"

Mwanamama huyo alitoka ndani ya chumba ambacho walikuwa wanafanyia mkutano huku naye msaidizi wake akiwa anaelekea ndani ya ofisi yake kuweza kuanza kutekeleza jukumu ambalo lilikuwa mbele yake la kuanza kumchunguza Remy Claude mwanaume ambaye ilionekana kwamba maisha yake yalikuwa na utata mwingi"

Sehemu hiyo, kwenye vyumba vya chini kabisa ya ardhi, ndani ya chumba kimoja kizuri na cha siri alikuwa anaonekana mwanamke mmoja mrembo. Rangi yake ilikuwa sawia kabisa kuweza kuyavutia kila macho ambayo yangefika kwenye mwili wake, ngozi yake laini na rangi yake ilikuwa inamuongezea umaridadi na kumfanya aendelee kuonekana mrembo wa kufikirika vichwani mwa wanaume wengi.

Kwenye mwili wake alikuwa amevaa pajama la kulalia huku miguu yake ikiwa peku kwenye kapeti la manyoya ambalo lilikuwa linampa burudani kila akilikanyaga. Mwanamke huyo alikuwa ameketi karibu na kabati ya kioo ndogo ya kisasa ambayo ndani yake walifugwa samaki wa mapambo. Licha ya kuketi karibu kabisa na kabati hiyo lakini macho yake hayakuwa hapo.

Macho yake yalikuwa pembezoni mwa hiyo kabati ambapo palikuwa na picha kubwa ya watu ambao walionekana kuwa kwenye mahaba mazito. Mwanamke kwenye picha hiyo alikuwa ni yeye mwenyewe lakini picha ya mwanaume ilikuwa ni picha ya Remy Claude ambayo kwa wakati huo alikuwa ameyaanza maisha ya jela tayari. Kuna mambo mengi yalikuwa yanaendelea kwenye kichwa cha mrembo huyo, kila alipokuwa anaiangalia picha hiyo alijikuta anachukua pombe ambayo ilikuwa pembeni yake na kuanza kuigida kwa pupa kama anakimbizwa huku akionekana kuwa na hasira.

"Unampenda?" sauti ambayo hakuitarajia kwa wakati huo ilipenya kwenye masikio yake kwa usahihi. Haikuwa sauti ngeni kwake kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba alikuwa ni bosi wake jambo ambalo lilimshtua kwa sababu hakuhitaji bosi huyo aweze kujua kama yeye alikuwa anajisikia vibaya kwa sababu ya mtu huyo.
"Hapana bosi"
"Anelia nimekujua tangu ukiwa binti mdogo, acha kuniongopea. Unampenda?"

"Siwezi kusema ndiyo au hapana kwa sababu sina uhakika na jambo lolote lile. Yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuniangalia mimi machoni na kunisikiliza kile ambacho mimi nilikuwa nakitaka. Yeye ndiye mtu pekee ambaye alikuwepo wakati wote ambao mimi nilikuwa naihitaji faraja ila mwisho wa siku mimi ndiye nimeyateketeza maisha yake yote"
"Unajuta kufanya hivyo?"
"Hapana bosi"

"Hivyo ndivyo unavyo takiwa kuwa. Umefanya jambo jema sana ambalo linaenda kuyaokoa maisha ya maelfu ya watanzania. Huwa sio vibaya kufanya jambo sahihi kwa kutumia njia mbaya hususani ya kuyatoa sadaka maisha ya mtu mmoja ili kuokoa maisha ya wengi. Taifa linakupongeza kwa jitihada zako za kutusaidia kufanikiwa kumkamata mhalifu mkubwa kama yeye, kwa hili hata mheshimiwa raisi atahitaji kuonana na wewe"

"Raisi ahitaji kuonana na mimi kwa sababu zipi?"
"Umefanya jambo kubwa, unastahili kupongezwa hivyo mimi naenda kuonana naye na baada ya hapo nafikiri siku yoyote utaalikwa Ikulu"
"Mpaka lini nitaendelea kuishi hivi bosi?"

"Kwa sasa watu hawatakiwi kujua kama wewe upo hai kwa sababu kwenye kila taarifa tumeacha kiulizo juu ya jambo hili ili watu wasiwe na cha kuongea kuhusu wewe"
"Kwanini?"
"Kama wakijua upo hai inaweza kuwa hatari kwenye maisha yako kwa sababu hatujui ni nani na nani ambao huenda walikuwa na huyu mtu kwa siri hivyo kama habari zikija kuvuja kuhusu wewe basi unaweza kuwa kwenye mazingira hatarishi kitu ambacho mimi binafsi siwezi kuruhusu kiweze kufanyika nikiwa kama kiongozi wa usalama wa taifa"

"Asante sana kwa kujali uwepo wangu"
"Kwa sasa ukikutana na raisi utahitajika kwenda nje ya nchi kwa muda mpaka pale nitakapo kupatia taarifa ya kuweza kurejea tena nchini"

"Sawa bosi" mwanamama huyo baada ya kuongea na mwanamke Anelia Baton ambaye ndiye alifanikisha kwa ukubwa zoezi la kukamatwa kwa Remy Claude alitoka ndani ya hicho chumba na kuondoka huku akimuacha mwanamke huyo kwenye msongo mkubwa wa mawazo. Alificha ficha mbele ya bosi wake lakini ukweli macho yake yalikuwa yanazungumza na kumsuta kwamba alikuwa amempenda mwanaume huyo licha ya kumsababishia matatizo ambao huenda yangemfanya maisha yake yote aweze kuishia kwenye nondo za jela.

"Hivi haya ambayo yalikuwa yanaongelewa hapa yana uhalisia wowote ule?" Suzane ambaye alikuwa kiongozi wa kundi hilo hatari la TULIKUFA TUKIWA HAI aliuliza akiwa anawageukia wenzake kwa macho ya viulizo.
"Kazi yetu ilikuwa ni kuliteketeza genge la mtu yule na kumkamata yeye basi hayo mengine sisi sidhani kama yanatuhusu" alijibu mwanaume mmoja ambaye kwenye mkono wake alikuwa anamenya chungwa ila wenzake walimpotezea.

Sehemu ya tano inafika mwisho.

Febiani Babuya.
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA SITA
"Nikiwa ndani ya nchi ya Marekani kwa ajili ya kumalizia kozi yangu ya upelelezi, nilifanikiwa kuwa na rafiki yangu mmoja ambaye mpaka sasa anafanya kazi ndani ya FBI. Moja kati ya vitu vya mhimu ambavyo aliniambia ni kwamba; ni tatizo kubwa sana kwa nchi kama kuna wau wanaweza kulizidi taifa akili"
"Kai unamaanisha nini kusema hivyo?"
"Mimi nilitaka kuongea tangu mwanzo sema niliamua kukaa kimya kwa sababu nikielezea uhalisia wa mambo huwa mnasema naharibu kazi ambazo tunaenda kuzifanya. Kabla ya kuimaliza kazi hii kichwani mwangu nilipata ukakasi mkubwa sema kwa sababu amri ilikuwa imetoka kutoka juu basi sikuwa na cha kufanya"

"Unaongelea kuhusu nini wewe?"
"Kwanza iliwezekana vipi kiongozi wa genge la kihalifu ambalo limeisumbua nchi kwa muda mrefu kuwa na ulinzi dhaifu namna ile? pili yeye mwenyewe mbona kama hakuwa mtu ambaye alikuwa anajishughulisha kukimbia?"
"Kuhusu kukimbia huenda alikuwa anajiamini kwamba angeweza kutumudu"
"Sio rahisi hivyo Luqman. Kwa historia ya mtu yule nilivyo isoma japo kidogo ni kwamba tusingeweza kumkamata kirahisi sana namna ile na kuondoka naye"
"Kirahisi kivipi mtu ambaye tulimpiga vibaya?"
"Vipi kama yeye ndiye alitaka iwe hivyo?"
"Umechanganyikiwa?"
"Huenda wewe ndiye umechanganyikiwa Luqman kwa sababu hata haujaniruhusu nimalizie hiyo simulizi ya rafiki yangu wa FBI huenda ungeanza kuelewa kwanini nasema hivi" wote walibaki wameganda kumwangalia mwanaume huyo ambaye alikuwa ameishika kalamu ya wino kwenye mkono wake akiwa anaizungusha taratibu.

"Kwenye moja kati ya kesi kubwa sana ambazo waliwahi kukumbana na mambo mabaya ni baada ya muuzaji mmoja wa madawa ya kulevya ambaye alikuwa anatafutwa kwa miaka mingi kuwaingiza kwenye mtego na hatari kubwa. Mtu huyo ilikuja kusemekana kwamba yupo Chicago hivyo kwao wakaona kama ni nafasi ya dhahabu kuweza kumalizana naye mapema akiwa ndani ya mipaka yao kwa sababu kama angekuwa Mexico wasingeweza kumkamata"

"Kwa pupa bila kufanya mahesabu makali wakafanikiwa kujua alipo mtu huyo hivyo walimvamia na kuua baadhi ya vijana wake kisha yeye wamamkamata na kumtupia gerezani. Ni habari ambayo iliwapa umaarufu sana na wakaichapisha kwenye kila chombo kikubwa kama mafanikio ya kumkamata muuzaji huyo wa madawa ya kulevya ambaye alikuwa anatafutwa hadi na umoja wa mataifa"

"Lakini kwenye kutekeleza majukumu yao walisahau kujiuliza swali moja rahisi sana huenda ni kwa sababu kila mtu alikuwa ana hamu kubwa ya kuikamilisha kazi hiyo ili apate sifa kwa mabosi zake ndiyo maana hakuna hata mmoja ambaye alikumbuka kuhoji kuhusu hilo. Swali ambalo walishindwa kujiuliza kirahisi ni kwamba mtu yule alikuwa anaweza kuingia ndani ya Chicago bila wao kujua kwa sababu alikuwa na watu wengi kwenye mfumo wa serikali, sasa kwanini location ya yeye alipokuwepo ilipatikana kirahisi na wao waliipata kwenye mazingira gani? Furaha haikuwafanya wakumbuke hayo yote kwa sababu kama ni kazi ya kumkamata waliifanikisha vyema"

"Majuto yalianza baada ya mtu huyo kumaliza miezi sita akiwa anasubiria kesi yake iweze kurejewa upya mahakamani kama jaji alivyokuwa ameahidi na kuna nadharia zilikuwa zinadai kwamba hawakuwa na haja ya kumpeleka mtu huyo mahakamani kwani ushahidi ambao walikuwa nao juu yake ulikuwa unatosha kabisa kumfanya wanachotaka wao ili wasije kuwaamsha watu wake wakaleta maafa siku ya kusikiliza kesi yake mahakamani. Baada ya muda bwana yule alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha"

"Haikuwa kawaida kwenye gereza kubwa kama lile mfungwa kuweza kutoroka basi ikawalazimu kufanya uchunguzi mkali mno na ndipo walikuja kugundua mtandao mzito wa askari ambao walikuwa wanalipwa na mtu huyo kitu ambacho kilipelekea askari wengi kukosa kazi na wengine kufungwa kabisa. Wakati wanaanza kufanya uchunguzi wa kimya kimya kutaka kujua kwamba mwanaume yule alikuwa amekimbilia wapi ndipo walikuja kugundua mambo ya hatari na madhara ambayo walikuwa wameyasababisha kwa nchi yao ila walishtuka wakiwa wamechelewa"

"Mwanaume yule alikuja kugundulika kwamba alikuwa ni jasusi kutoka ndani ya kundi la KGB Urusi na tangu muda mrefu sana alikuwa anatafuta nafasi ya kupenya Marekani na sio Marekani tu bali gerezani. Sasa kama angeenda kama raia wa Urusi maana yake asingeweza kutekeleza lengo lake hata kama angefanya uhalifu asilimia nyingi asingefungwa Marekani bali angehukumiwa na kukabidhiwa kwa nchi yake kama mfungwa"

"Sasa kwanini alikuwa anahitaji kuingia jela ya Marekani? hapa ndipo palikuwa pabaya sana. Jamaa alikuwa anajua aina ya kosa ambalo unatakiwa kulifanya ili uweze kupenya ndani ya gereza ambalo alienda kufungwa ndiyo maana alianzia huko Mexico ambako alifanya mambo ya kutisha na kupata jina kubwa akiwa moja kati wa wafanya biashara wa dawa za kulevya ambao walikuwa wanaingia kwa kasi sokoni kiasi kwamba akawa ameingia kwenye rada za FBI. Sasa jamaa alijua kwamba kwa Mexico ilikuwa ni ngumu kukamatwa ndiyo maana akaamua kujipeleka mwenyewe Chicago halafu kupitia watu wake wakavujisha location ambayo atakuwepo huku FBI wakijua wamepata kete ya ushindi mkubwa kiasi kwamba wakakurupuka kwenda kumkamata na kuanza kujisifu kila sehemu"

"Ndani ya gereza ambalo alifungwa walikuwepo majasusi wa KGB ambao kwa muda mrefu walikuwa wakiishi ndani ya gereza hilo kwa kujihusisha na magenge ya Marekani ikiwemo uuzaji wa silaha, kwa vile walikuwa ni watu ambao walikuwa wamechukua mpaka uraia wa Marekani basi serikali haikuwashtukia kabisa. Watu hao kuna taarifa za mhimu ambazo walikuwa wamezikusanya kipindi chote ambacho walikuwepo Marekani na taarifa hizo zilitakiwa kufika makao makuu Moscow Urusi hivyo mwanaume huyo aliingia huko ili kuzipata taarifa hizo ambazo zilikuwa ni hatari kwa usalama wa taifa la Marekani. Kwahiyo baada ya kuingia gerezani, alifanikiwa kukutana na watu wake na kuchukua kile ambacho alikuwa anakitaka na kutoweka gerezani humo"

"Wakati wao wanashtuka alikuwa tayari amefanikiwa mpaka kurudi Urusi na baadae walikuja kugundua kwamba mtu huyo ni moja kati ya viongozi wakubwa ndani ya idara ya usalama ya nchi ya Urusi. Jambo hilo liliacha mtikisiko mkubwa ndani ya idara hiyo nyeti ya Marekani jambo ambalo hawakutaka kuutangazia ulimwengu maana wangejishushia heshima duniani ila walipata mtikisiko mkubwa mno kiasi kwamba mashirika yao yalianza kufumuliwa na kusukwa upya. Wale wafungwa ambao ndio walikuwa majasusi, walikutwa wamejiua wenyewe ndani ya gereza hivyo hawakupata nafasi hata ya kuweza kuwahoji lakini jambo hilo liliacha alama kubwa ambayo imewafanya kuwa makini mara kumi zaidi ya walivyokuwa wakati huo" mwanaume huyo ambaye alikuwa anaitwa Kai alitoa simulizi fupi ya kusisimua, simulizi ambayo ilionekana kama anasimulia jambo ambalo alilishuhudia kwenye movie za maigizo lakini ulikuwa ni uhalisia ambao alikuwa anawaambia wenzake.

"Mhhhhh hiyo ni moja kati ya stori bora ambazo nimewahi kuzisikia kwenye maisha yangu, kama ingesimuliwa kwa madairekta wa movie basi huenda ingetengenezwa moja kati ya movie bora za kijasusi za muda wote. Kama nchi kubwa zaidi duniani inafanyiwa jambo kama hilo na wana kila kitu basi hii ni hatari kubwa sana kwa nchi kama yetu ambayo hata nyenzo kubwa za kuendana na kasi ya sayansi na teknolojia hatuna" Venance alijibu akiwa anasikitishwa sana na jambo hilo.

Sehemu ya sita inafika tamati.

CIAO
 
NINI SIRI YA NAFSI ZILIZO TELEKEZWA?

Inahusu nini, inamhusu nani, kipi kipo nyuma yake? Ungana nami kwenye mtiririko huu uweze kuelewa NAFSI ZILIZO TELEKEZWA inahusu nini.

Mwaka 1991, ni mwaka ambao umoja wa nchi za Kisovieti ulidondoka baada ya kushindwa kwenye vita baridi dhidi ya watu wa Magharibi hususani Marekani. Baada ya vita hiyo kuisha kulikuwa na sababu nyingi sana zilizo wafanya washindwe ikiwemo utaifa na mchango wa nchi za magharibi.

Kwa madhara makubwa ambayo yalipatikana, nchi ya Urusi ilikaa chini kufanya tathmini ili kujua ni wapi walifanya makosa mpaka jambo hilo likatokea nchini mwao. Moja kati ya sababu kubwa ambazo walizipata ni kufeli kwa shirika lao la kijasusi la KGB kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kiusalama kwa asilimia miamoja, waliamini kwamba huenda kama shirika hilo lingekuwa imara mapema na kutekeleza majukumu yake kwa usahihi basi wangeishinda vita hiyo.

Sasa mjadala ukawekwa mezani, walishindwaje? Ndipo ikanukia harufu ya usaliti ndani yao, iligundulika kwamba ndani ya shirika lao kuna watu ambao walikuwa wasaliti na usaliti wao ndio ambao ulifanya shirika hilo kuyumba na kufeli. Sasa wasaliti walikuwa nani na nani? Jina ambalo lilitokezea kwenye makablasha yao ni jina la mwanamke wa miaka ishirini na mitano (IRINA ESPANOVICH). Sasa IRINA ni nani na alitokea vipi kwenye hiyo orodha ya wasaliti?

IRINA ESPANOVICH alikuwa ni jasusi mbobevu ndani ya shirika hilo, Moja kati ya wapelelezi ambao waliaminika mno kiasi kwamba akapata bahati ya kuolewa na moja kati ya maafisa wakubwa ndani ya shirika hilo la KGB. Kuolewa kwake na kiongozi mkubwa wa shirika hilo ikawa nafasi ya yeye kupata taarifa nyingi na za siri za shirika hilo kwa njia ya kawaida ama kuziiba kwa sababu huyo mwanaume alikuwa akiishi naye nyumba moja. Sasa kwenye ule mchakato wa kuwatafuta wasaliti, waligundua kwamba kuna akaunti ndani ya Urusi ilipokea mabilioni ya fedha kutoka ndani ya nchi ya Marekani na walipo jaribu kuichunguza akaunti hiyo ili wajue sababu ya msingi ya pesa nyingi kiasi hicho kutumwa kwa mtu ambaye taifa lake lilikuwa vitani na nchi hiyo ni ipi! Ndipo wakagundua kwamba akaunti hiyo ilikuwa inamilikiwa kwa siri na mwanamke huyo IRINA ESPANOVICH.

Baada ya kuunganisha doti, wakagundua kwamba hizo pesa zilitoka ndani ya shirika la kijasusi la Marekani CIA ambalo wengi huwa wanaamini kwamba ndilo shirika namba Moja kwa ubora zaidi duniani kutokana na kuwa na bajeti kubwa ya uendeshwaji wake. IRINA alipokea pesa nyingi ambazo hata angefanya kazi miaka mia-moja asingeweza kuzipata, CIA wamtumie pesa kama nani? Ikahitimishwa kwamba huyo ndiye msaliti ambaye alikuwa akiwauza kwa CIA ndiyo maana walifeli hivyo ikatolewa amri kwamba asakwe popote alipo, akamatwe, ateswe kisha auawe mrembo huyo.

Bahati ikawa upande wake, mlinzi mkuu wa mumewe akampatia taarifa kwa simu kwamba Maam you are to be killed (unatakiwa kuuawa) hawa watu wanajua kila kitu hivyo KIMBIA (RUN). Alikuwa hatarini hivyo hakuwa na muda wa kupoteza akapotea haraka, KGB hawakumpata mwanamke huyo hivyo ukaanza msako wa kimya kimya kwa sababu waliogopa kuziweka taarifa hizo wazi kwani zingewavua nguo kwa kuonekana ni wazembe mpaka yote hayo yanatokea na hawana taarifa! Hawakutaka aibu wakaamua kuifanya siri kumtafuta huyo DOUBLE AGENT IRINA ESPANOVICH.

Kupotea kwake Urusi mikononi mwa KGB ambao walimpachika jina la LUNATIC GIRL, ukawa mwanzo wake wa kuingia ndani ya nchi ya Tanzania. Kwanini iwe Tanzania? IRINA alipiga hesabu zake akagundua kwamba kama angeenda nchi kubwa hususani ambazo zina usambaaji wa taarifa haraka wangekuja kumpata tu siku moja hivyo alihitaji kuishi sehemu ambayo hata KGB wenyewe wasingeidhania kwamba anaweza kuwepo na ile amani ambayo imetawala Tanzania ikamvutia kuishi hapa kwani ingekuwa ni ngumu kuja kujulikana kwamba yupo hapa. Yes, mpango ulikuwa sahihi sasa Tanzania angeishije na angeweza vipi kujilinda? Ukawa mwanzo wa kuanzisha jamii ya Siri ambayo aliiita LUNATIC SOCIETY, jina ambalo alipewa na KGB kwa usaliti wake. Kumbuka alikuwa mgeni hivyo asingeweza kuianzisha jamii hiyo mwenyewe ikamlazimu kumtafuta mtu.

Macho yake yakadondokea kwa Novack Nyangasa, mdogo wa raisi wa Tanzania ambaye aliamini angekuwa na nguvu ya kumpeleka anapo pataka yeye. Alimshawishi mwanaume huyo kwa urembo wake na kumpa mpango mzima juu ya utajiri ambao wangeenda kuutengeza, Novack akatokwa na mate ya uchu, akakubali. Jamii hiyo ikaanzishwa kwa nguvu ya mdogo wa raisi ambapo waliwasajili watu wakubwa; wanasiasa wakubwa, maprofesa, wanafalsafa, madaktari bingwa, wafanya biashara wakubwa na kila ambaye walimuona anafaa. Baadae raisi akazipata habari, akachukia sana na kumuita mdogo wake IKULU.

Akamtaka aifute jamii hiyo kwa mwezi mmoja tu pekee, huo mwezi ukatumika kummaliza yeye, raisi akawekwa kati akatakiwa kufa ili jamii hiyo iwepo. Moja kati ya mipango mikakati ambayo waliiweka ili kujilinda ni kuanzisha chuo cha kuwatengeneza vijana hatari kwa ajili ya ulinzi na kufanya kazi yao kwa nguvu pale ambapo ingebidi, zoezi hilo likatua mikononi mwa jasusi wa zamani wa Tanzania ambaye aliachana na kazi hiyo baada ya kuhusika na mauaji ya watu wengi sana, NIKOLAI GIBSON. Mwanaume huyo kwenye moja ya mazao yake alifanikiwa kumtengeneza kijana wa kuitwa YOHANI MAWENGE, bwana mdogo ambaye alimuokota Tandale kwa Tumbo akililia mapenzi na kutaka kujiua kisa uchi wa mwanamke.

Alimfunza namna ya kuwa mwanaume akampa begi la pesa akale maisha kwa mwezi mzima, alale na wanawake warembo ambao aliishia kuwaona kwenye runinga ili ushamba umtoke kisha baada ya hapo alikuwa na kazi naye. Alitengenezwa kikawa kiumbe cha kutisha na Kazi yake ya kwanza ikawa kwenda kumuua mcheza KAMARI mmoja huko BAMBALI Senegal na alitakiwa kurudi na bilioni 30 zilizokuwa mkononi mwa bwana huyo..... Huyu tuna mengi ya kuyasoma kwake ni mhimu sana.

Ukawa mwanzo wa mwanamke huyo wa KGB kuitawala Tanzania kwa miaka takribani thelathini. Lakini baadae Moja kati ya makosa makubwa ambayo waliyafanya ni kumuua mwanasayansi aliyedaiwa kuwa binadamu mwenye akili zaidi nchini.

NAFSI ZILIZO TELEKEZWA ni zipi na za nani?
Kulikuwa na utata wa maisha ya mwanaume mmoja aitwaye Edison, bwana ambaye hakuwa na kumbukumbu na kwenye mfuko wake alikuwa anatembea na picha ambayo walidai ni ya mkewe, bwana huyu alikuwa akishangaa kwa sababu yeye binafsi hakuwa na kumbukumbu yeyote kama aliwahi kuwa na mke au familia. Kitu cha kushangaza kwa EDISON ni kwamba alikuwa anatafutwa ili auawe kuliko hata pesa inavyo tafutwa na maskini mpaka yeye mwenyewe akawa anashangaa.

Hali hiyo ilimlazimu kwenda kuishi maisha ya chini sana huko Kigogo Mwisho ili awe salama kwani hakuna ambaye angempata kirahisi akiwa kwenye maisha ya kifukara huko lakini usiku mmoja mvua ikiwa inanyesha akiwa ndani ya kijumba kibovu kwenye mkeka, anapokea simu ambayo ilimtaka atoweke eneo hilo kwa dakika kumi na tano vinginevyo angekufa. Aliduwaa ila hakuwa na namna aliondoka haraka ila kabla hajafika mbali akavamiwa na wanaume wa kutisha ambapo alimuua mmoja akafanikiwa kutoroka.

Safari yake ikawa ni kwenda kwa mlezi wake ambaye ndiye alimpa taarifa hiyo na ndiye alimtaka akaishi huko Kigogo mapaka mambo yakae sawa ili akampe ukweli wa kwanini anatafutwa sana? Kufika kwa huyo mlezi wake ambaye alikuwa ni mchungaji wa KKKT pale Mabibo Mwisho karibu na hosteli za wanafunzi wa NIT, alimkuta mtu huyo yupo kwenye hatua za mwisho za uhai wake. Hakumwambia kitu zaidi ya kumtaka aende nyumbani kwake kwenye banda la mbwa akachukue kitabu ambacho kingemfunulia ukweli kwamba yeye ni nani, kwanini hana kumbukumbu, maisha yake kabla yalikuwaje na kwanini anatafutwa sana na watu ambao yeye alidai hawajui!

EDISON alishangaa baada ya kuambiwa kwamba anatafutwa kwa kuhusika na mauaji ya makomando TISA wa kikosi maamulu cha KOM (KILL ON MISSION).akabaki ameduwaaaa!!!!!!!

Ilishawahi kukukuta kwenye maisha yako ukatakiwa kumuua mama yako mzazi kwa mkono wako mwenyewe? Hilo ni jambo baya na gumu lakini Yes, kuna mwanaume alitakiwa kumuua mama yake aliye mzaa ili nchi iwe salama. Je huyu naye hatima yake ilikuwaje?

Kuna uhusiano gani kati ya hizo NAFSI ZILIZO TELEKEZWA, IRINA ESPANOVICH na EDISON?

Unataka kumjua zaidi IRINA ESPANOVICH? Unataka kuijua kiundani LUNATIC SOCIETY? Unataka kujua uhalisia wa maisha ya EDISON kabla na baada ya hapo? Hizo nafsi ZILIZO TELEKEZWA ndizo hizo za makomando TISA (9) ambao alidaiwa kuwaua au kuna mengine nyuma ya mlango wa siri? Ungana nami kwenye simulizi yangu bora zaidi kuwahi kuiandika kwa mkono wangu.

1. Storyline yake ni kali sana
2. Dialogue (majibizano) yake ni kali sana.
3.Haitabiriki kabisa (huwezi kutabiri kinacho tokea baadae)
4.Lakini pia ina actions kali mno.

Simulizi hii imetoka tayari na unaweza kuipata kwa shilingi ELFU SITA (6000 tu za kitanzania). Unaweza ukalipia 6000 yako kwa namba hizi ili uipate muda huo huo. Inapatikana kwa Softcopy.

0621567672 (HALOPESA)..... WhatsApp.

0745982347 (M-PESA)

0714581046 (TIGO-PESA)

0689440143 (AIRTEL MONEY)

Zote jina FEBIANI BABUYA

Lipia muamala wako Kisha nicheki nikutumie yote, ama unaweza ukanicheki WhatsApp, ukatuma sms ama ukapiga cm kama utakuwa na swali lolote.

CIAO.
FB_IMG_1719138159383.jpg
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA SABA
"Kai are you sure about this story?" Suzane aliuliza akiwa anahema, maana ni stori ambayo iliibua jambo jipya kati yao.
"Ndiyo kiongozi"
"Kwanini unahisi hii stori inaendana moja kwa moja na huyu mtu?"
"Kwa sababu hata aina ya mazingira ambayo tulimkamatia yanatia mashaka. Anelia huenda alifanikiwa kukusanya taarifa nyingi za mtu huyu lakini asingejua kila kitu kwani ingembidi awe mtu wa kuuliza maswali mara kwa mara sababu watu kama hawa huwa hawaweki kila kitu chao hadharani. Sasa kuuliza kila kitu huoni kama inampa mashaka makubwa muulizwaji kuhitaji kujua kwamba ni kwanini unakuwa unahoji kila kitu?"

"Enhe endelea"
"Maana yake kama ni hivyo basi kuna uwezekano huyu mtu huu mchezo ni yeye anaucheza, alijiweka kirahisi tu na kupatikana kila ambapo Anelina alimhitaji ili aweze kuingia kwenye mikono ya serikali"

"Ni kitu gani ambacho unahisi kinakupa uhakika juu ya hilo?"
"Sina uhakika ila huyu mtu inaonekana kama kuna watu anawatafuta kwenye maisha yake"
"Whaaaaat?"

"Yaaa huenda naweza kuonekana kama kichaa kuongea hivi ila hisia zangu zinaniambia hivyo. Ukitaka kujua kwamba huyu mtu anajua anacho kifanya, kwanini alifungwa kwenye gereza la kwanza lakini alienda kusababisha mauaji mabaya na ya kutisha namna ile?"

"Kwamba aliua kwa makusudi?"
"Yes, kwa sababu alijua hawawezi kumuua hivyo ambacho kingefanyika ni kwamba angehamishwa gereza na kupelekwa kwenye gereza la DOMINIC ambalo wanapatikana watu wa aina yake"
"Na kwanini aende kule?"

"Hisia zangu zinaniambia kwamba mtu au watu ambao yeye anawatafuta wapo kwenye lile gereza"
"Oooohhhhh no, Kai kwa hapo utakuwa umekosea sina hakika na hilo jambo"

"Nakukumbusha tu wakati Venance anamzimisha yule mtu wakati tunamkamata alikuwa na nafasi ya kuniua mimi kabla hata Venance hajamfikia akiwa na kisu chake mkononi. Unadhani kwanini hakuniua akasubiri Venance amfikie kwanza?"

"Unataka kuniambia kwamba huyu mtu huu mchoro ni yeye aliuchora na sisi tumeicheza ngoma yake?"
"Kwa mtazamo wangu hilo ndilo jibu langu kwa sasa na msimamo wangu upo hapo"
"Oooooh f***k, kwanini afanye hivi kama ni kweli?"

"Bosi amesema historia yake tu ina utata mwingi, maana yake tukiijua historia ya maisha yake ndipo tunaweza kujua sababu ya mambo haya yote na kujua kwamba ana makusudi gani kwa hapo baadae? tunaweza kujisifu lakini kumbe tumeingia cha kike na baadae madhara makubwa yakitokea tunaweza kuwa miongoni mwa watu ambao tutalaumiwa sana"

"Sitaki kuamini kama kweli huyu mjinga anacheza huu mchezo hatari namna hii. Maana yake kama ni hivyo basi huyu mtu ni hatari kuliko hata taarifa zilivyokuja, anaweza asiwe binadamu ambaye sisi tunamfikiria machoni mwetu, tunatakiwa kulifanyia hili jambo kazi haraka sana iwezekanavyo" Suzane simulizi na mawazo ya Kai yalimfungua pakubwa, mwanaume huyo aliwaza mbali kuhusu mwanaume huyo ambaye yeye binafsi hakuwa akiamini kwamba alikamatwa kwa sababu walimzidi nguvu bali aliamini kwamba mtu huyo ulikuwa ni mpango wake mwenyewe kukamatwa.

"Unataka tufanye kazi bila ruhusa ya bosi?"
"Hao watatuchelewesha kutoa ruhusa hivyo hili tunatakiwa kulifanyia uchunguzi sisi wenyewe kwa kuanza na kuijua historia yake. Tunaweza kuwa tunasherehekea kumbe nchi ipo kwenye hatari kubwa"
"Suzane, are you sure about this?"
"Let's do it Kai, kama kuna jambo litatokea mzigo nitaubeba mimi" mazungumzo yao yaliishia hapo kila mtu akatawanyika akiwa na mawazo mengi kichwani.

UNGA LIMITED
Arusha, usiku majira ya saa tatu na nusu, ndani ya eneo ambalo vijana wengi huwa wanajihisi wamechanganyikiwa sana ama kushindikana kulingana na itikadi zao za maisha ya kila siku. Sehemu ambayo maisha ya uswahilini hayakwepeki hususani kwa vijana, pombe kali na bangi ikiwa sehemu yake ndiko ambako muda huo alionekana mwanaume mmoja.

Alikuwa mrefu sana wa miaka isiyo pungua hamsini lakini mwili wake ulikuwa bado unamchora kama kijana huku akionekana kabisa kwamba hakuwa mnyonge kwenye kuutengeneza mwili wake kuwa imara.

Alikuwa ndani ya buti la kimarekani na jeans nzito ya gharama huku nje akiwa amevalia koti kubwa kulingana na aina ya baridi kali ambayo ilikuwa inapatikana ndani ya mkoa huo wenye watalii wengi nchini. Juu ya kichwa chake alikuwa amevaa kofia ya kawaida ambayo ilikuwa inaendana rangi na buti lake chini. Alikuwa anatembea haraka haraka mpaka alipofika sehemu ambayo ilikuwa na jengo ambalo lilionekana kuwa la zamani kutokana na rangi yake kuonekana kuchubuka mno.

Lakini nje ya jengo hilo vijana wenye rika la miaka ishirini na walikuwa wanaendelea kunywa pombe kali huku wengine wakiwa wanaendelea kuvuta bangi na kuropoka. Hakuna ambaye alionekana kuwa na muda naye kabisa hivyo alipita moja kwa moja na kuingia ndani. Alitembea kidogo tu na kukutana na vijana wengine ambao walikuwa wanaifunga pombe ya kienyeji kwenye vichupa vidogo, hakuwa na habari nao akapitiliza mpaka akatokea nyuma ya mlango wa nyumba hiyo na kukutana na mlango mwingine upande huo ambao aligonga mara moja tu kisha ukafunguliwa.

Aliye fungua alikuwa kijana wa miaka ishirini na mitano tu
"Bosi karibu, mbona ghafla sana?"
"Kuna kazi ambayo nahitaji uifanye wakati huu haraka"
"Kuna tatizo bosi?"
"Kakae kwenye komputa yako sina muda wa kusubiri kwa sasa" hakuwa na swali lingine zaidi ya kutekeleza kile ambacho alikuwa ameambiwa. Kijana huyo alikuwa ni bingwa wa kucheza na mitandao, kwake komputa aliijua kama mlaji ambavyo hawezi kukosea kupeleka tonge mdomoni wakati wa usiku.

Sehemu ya 7 inafika mwisho.

Febiani Babuya.
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA NANE
Mwanaume huyo mtu mzima aliitoa simu yake na kumpa kijana huyo ambaye jina lake alikuwa anajikulikana kama Hezironi. Kwenye simu hiyo ilikuwa inaonekana picha ya mtu ambaye sura yake haikuwa inaonekana vizuri kwa sababu iliwekwa kivuli.
"Huyu nani?"
"Nahitaji ukitoe hicho kivuli ndiyo kazi yako hivyo nahitaji uifanye kwa uharaka mkubwa mimi niweze kuondoka hapa muda huu"

"Sawa bosi" kijana huyo hakuwa na maneno mengi zaidi ya kuiunganisha simu hiyo na kwenye komputa yake ambapo baada ya kucheza na tarakimu kwa dakika tano tu ilikuja picha yenyewe halisi kabisa ikiwa haina kivuli. Mwanaume ambaye alikuwa anaihitaji picha hiyo alihema kwa nguvu huku uso wake ukiwa na tabasamu kwa mbali.
"Mawazo yangu hayawezi kuwa yananidanganya huyu atakuwa ni yeye" aliongea kwa sauti ya tumaini kubwa ndani yake.
"Unamzungumzia nani?"

"Achana naye, nitolee picha moja kisha nipatie hiyo simu. Ila kabla ya kufanya hivyo unaweza kuingia ndani ya shirika la usalama wa nchi? kuna habari mhimu nataka tuzichukue"

"Haiwezekani kwa sasa, juzi nimejaribu komputa ilizima kwa siku nzima kama nikijaribu tena basi litakuwa ni suala la muda tu kutukamata bosi"
"Nipe hiyo picha kisha hakikisha haukatiki hewani hata kwa dakika moja" mwanaume huyo aliongea akionekana kuwa na haraka sana na baada ya kuipata picha hiyo ambayo iliprintiwa hakukaa tena sehemu hiyo akaamua kutoweka eneo hilo na kupotelea vichochoroni akiwa na furaha kwani alipata kile alikitaka.

Akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka huku akiwa anasindikizwa na manyunyu ya mvua ila alihisi kama kuna hatua za mtu mwingine zilikuwa zinaenda sawa na hatua zake yeye. Aligeuka haraka lakini hakumuona mtu yeyote yule ila mwili wake ulimsisimka sana. Aliishika picha hiyo na kuiweka kwenye mfuko wa koti kisha akajiweka sawa na kuanza kutembea kwa tahadhari kubwa.

Kila alivyokuwa anapiga hatua mwili ulikuwa unazidi kuwa mzito kiasi kwamba alihisi kama upepo unaanza kuvumia upande wake kitu ambacho kilimfanya ainame chini. Kuinama kwake kulimfanya apone na kufanikiwa kukikwepa kisu kizito ambacho kilikuwa kama cha buchani na kwa muda mrefu mhusika hakukitumia. Kilienda kukita kwenye kona moja ya nyumba ndogo ambayo ilikuwa pembeni na kulipasua tofali kisha kikadondoka chini.

Aligeuka haraka kuangalia nyuma yake kilipo tokea kisu hicho na ndipo alipo muona mwanaume mmoja akiwa kwenye mavazi ambayo yalionyesha wazi alikuwa hapo kwa kazi maalumu.

"Robert ni miaka mingi sana tangu tuonane kwa mara ya mwisho, wewe ni mtu mwenye bahati sana kwa sababu sikujua kama ulipata nafasi ya kuishi tena" mwanaume huyo aliongea huku akiwa anamsogelea Robert mwenyewe ambaye alishangaa kwa sura ambayo alikuwa anaiona.
"Justin!!?" aliita kwa mshangao akiwa haamini mtu ambaye anamuona mbele yake.

"Umeshangazwa kuniona mimi au mimi kujua kwamba unapatikana wapi?"
"Unahitaji nini?"
"Baada ya miaka yote hiyo hautaki hata kunipa salamu?"

"Acha kuigiza kuwa mtu mwema, unataka nini kwangu na umejuaje kwamba nipo hapa?"
"Nakujibu swali moja tu, nataka hiyo picha ambayo umetoka kuichukua kwa yule kijana pale na maelezo yake ya kutosha juu ya mtu huyo kwenye picha"

"Unamaanisha umeenda kwa yule bwana mdogo?"
"Usiogope bado sijamuua yule mtoto na sijaenda pale ila naenda baada ya kumalizana na wewe kwa sababu pale ningepata picha tu lakini kwako nitapata picha na maelezo ya kutosha"

"Nadhani umechanganyikiwa na leo nakuua mshenzi mkubwa wewe hata sijui inawezekanaje mpaka leo bado unaishi"
"Mhhhh unajua kabisa hilo haliwezekani Robert, naweza nikayaacha maisha yako niambie tu hiyo picha ni ya nani na je kuna mtu mwingine tena alifanikiwa kuishi kama wewe?"

"Go to hell Justin" Robert aliongea akiwa anamsogelea mwanaume huyo na kuupanga mkono wake lakini jitu hilo ambalo lilikuwa mbele yake halikuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya ujio wake.

"Nijibu nilicho kuuliza nitakuacha uende. Wote wanajua kwamba wewe ulishakufa hivyo usifanye hili jambo tulifikishe mbali zaidi ya hapa wakati tulikuwa tunaweza kulimaliza kwa amani tu Robert" licha ya jitu hilo la miraba minne kuongea kwa sauti yake kali na nzito ambayo ilipenya vyema kwenye masikio ya mwanaume ambaye alikuwa analisikiliza lakini haikutosha kumfanya aache msimamo wake ambao alikuwa ameudhamiria hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuweza kumshambulia mtu huyo.

Alimsogelea akiwa ameikaza mikono yake, alirusha ngumi sita za nguvu ambazo zote zilifika kwenye mwili wa mwanaume huyo na kumsogeza nyuma kwa hatua chache kutokana na jinsi alivyokuwa ameiva na kukomaa isivyo kawaida. Robert wakati anasogea tena ili kumbananisha mtu huyo alijikuta anapiga ukuta na kupasua tofali ambalo lilikuwa kwenye nyumba hiyo lakini wakati anageukia upande ambao mwanaume huyo alikuwa amekwepea ngumi hiyo alipokea ngumi mithili ya nyundo kwenye mbavu, alihema kwa nguvu huku akisogea nyuma kwa maumivu ili kujipanga upya.

Hakuwa na muda mrefu wa kuweza kujipanga vizuri kwani mwenzake alikuwa amemfikia, mwanaume huyo alijigeuza na teke zito mno ambalo lilimkosa na kukita kwenye nyumba moja ambayo matofali mawili yalidondokea ndani. Robert alijigeuza kwa sarakasi na wakati huo alikuwa anachomoa kisu kwenye kiuno chake ambacho kilimkosa Justin shingoni. Walikuwa na mpambano mkali sana lakini Robert alikuwa anatafuta namna ya kuweza kukimbia eneo hilo kwa sababu mtu huyo hakuwa wa kiwango chake na kama angezubaa basi alikuwa anapoteza maisha. Alidunda chini kwa mguu mmoja kisha akageuka kwa mguu mwingine na ngumi mbili ambazo zilitua kwenye kifua cha Justin lakini mguu wake ulidakwa.

Nane inafika tamati.

Febiani Babuya.

CIAO
 
Katik ubora wako mwamba, as usual you have my respect.
 
Hello fam,
Nilipotea siku mbili hizi but as usual, nikipotea nafidia hivyo leo tutakuwa na episodes 3, ya juzi, jana na leo.
 
Naam hayo ndo maneno sasa waiting ile kitu ya kuamsha bongo zetu
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA TISA
Alipigwa ngumi nzito tano na alipokuja kuachiwa alikuwa anatema damu huku kifua kikiwa kinawaka moto. Alikirusha kisu kwa nguvu na kumfuata mwanaume huyo lakini kisu hicho kilidakwa hata kabla hajafika hapo na wakati anakaribia kufika Justin alitishia kama anamfuata alipo kitu ambacho kilimpotezea mahesabu yake akajikuta anasita, hali hiyo ilifanya apigwe mtama mkali na kabla hajatua chini alikutanishwa na buti la tumbo ambalo lilimpeleka mbali mpaka ukutani na kuvunja vunja kijumba kidogo ambacho kilikuwepo eneo hilo.

Wakati anakwepa kuangukiwa na matofali alijikuta anapata maumivu makali mno isivyo kawaida basi ikamlazimu kuweza kuangalia tumboni, alishangaa kuona damu ikiwa inavuja kwa wingi. Baada ya kujikagua vizuri ndipo aligundua kwamba alikuwa amezamishiwa kisu ambacho kilitumwa kwa nguvu sana na mtu huyo, kuangalia kisu hicho kilimpotezeshea umakini mzuri alishangaa kivuli kinakuja alipo kwa kasi, alifanikiwa kukikwepa na buti hilo ambalo lilitua hapo lilipasua pasua tofali ambazo zilikuwa jirani vibaya.

Aliitumia nafasi hiyo kuweza kulivua koti lake mwilini na kulirushia kwa nguvu kwa Justin ambaye alikuwa anamsogelea kwa nguvu pale aliporukia huku mtu huyo akionyesha wazi kwamba alikuwa ni mtu ambaye alikuwa na usongo naye. koti lilimfunika Justin hivyo Robert akaitumia nafasi hiyo kuweza kujigeuza kwa nguvu kwa mkono mmoja na kumshambulia Justin kwa double kick moja ya nguvu ambayo ilimpeleka mbali. Wakati Justin anaangukia upande mwingine, yeye aliitumia nafasi hiyo kukimbia na ndiyo ilikuwa pona pona yake kwa sababu wakati Justin anafanikiwa kusimama na kulitupa koti hilo alikuwa amechelewa maana mtu huyo alikuwa amesha ondoka na hakujua ameingia upande gani hivyo akatakiwa kuwahi kurudi kwa Hezironi ambaye alijua kwamba lazima angekuwa na taarifa kamili za mtu huyo.

Robert alikimbia mpaka sehemu ambayo alikuwa ameipaki pikipiki yake akiwa anavuja damu kwenye tumbo lake na kwenye paji la uso ambapo tofali lilimpiga. Aliitoa simu yake mfukoni na kupiga akionekana kuwa na haraka sana, simu hiyo iliita kwa sekunde moja tu ikawa imepokelewa upande wa pili;
"Ondoka hilo eneo haraka sana tumesha gundulika tayari" aliongea na kuikata simu hiyo kisha akapanda pikipiki yake na kutoweka ndani ya eneo hilo haraka na kwa kasi ya ajabu.

Muda mfupi tu Justin alifanikiwa kufika kwenye lile jengo ambalo alikuwepo Heziron lakini alishangaa pakiwa kimya bila kuonyesha hata alama yoyote ya mjongeo wa watu ndani ya eneo hilo hali ambayo ilimshtua maana mara ya kwanza alikuta kuna vijana wengi. Alisogea karibu zaidi akiwa anaichomoa bastola yake ila hapakuwa na mtu hata mmoja. Alipitiliza mpaka mlango wa nyuma na kuingia kwenye chumba ambacho alikuwa anakitumia Hezironi, alikutana na kompyuta kubwa mbili ambazo zilikuwa zinamalizika kuungua kwa sababu mhusika alionekana kuzichoma muda mfupi tu ulio pita hivyo alikuwa amewakosa watu wake wote wawili. Alichukia sana mwanaume huyo na kuamua kutoweka kabisa kwenye hayo mazingira.

Robert alitembea kwa dakika sita tu akiwa na mwendo mkali sana juu ya pikipiki yake ya kazi. Safari yake ilienda kuishia Njiro sehemu ambayo walikuwa wanaishi watu wengi ambao maisha yao hayakuwa ya kubahatisha, walikuwa wana uhakika wa kuyaishi maisha mazuri. Kwenye moja kati ya jengo kubwa ambalo lilionekana kuwa la gharama ndipo yalipokuwa makazi yake mwanaume huyo wa miaka takribani hamsini.

Alifungua geti hilo kubwa kwa rimoti lakini wakati geti hilo linafunguka mlangoni kulikuwa na wanaume wawili ambao kwa mwonekano wao walionekana kuwa watu wa kazi haswa
"Bosi kuna nini mbona unavuja damu?" mmoja aliuliza wakati geti linajifunga na kiongozi wao huyo anaruka juu ya pikipiki ambayo ilienda kudondokea kwenye matairi ya magari ambayo yalikuwa karibu na bustani safi ya maua.

"Nimempata bosi"
"Whaaaat?"
"Yupo hai"
"Inawezekanaje wakati ulisema kwamba familia nzima iliuawa na wewe ndiye mtu pekee ambaye ulifanikiwa kuishi?"
"Twendeni ndani" aliongea akionekana kuwa mtu mwenye haraka huku akionekana kutokijali hata kidonda chake ambacho kilikuwa mwilini mwake.

Baada ya kufika ndani ya jumba hilo, waliingia mpaka ndani kabisa ambapo walikutana na ngazi ambazo zolikuwa zinashuka chini. Waliingia mpaka huko chini ambako kulikuwa na watu wengine watano, wanaume wanne na mwanamke mmoja ambaye alikuwa amekalia kiti kilichokuwa karibu na kompyuta kubwa zaidi ndani ya chumba hicho kilichokuwa kimebeba zaidi ya komputa kumi ukutani.

"Bosi kimekukuta nini?" aliuliza yule mwanamke huku akimwangalia mwanaume huyo akiwa anavuja damu na kisu kikiwa mwilini hata hivyo hakuwa na habari nao zaidi ya kumkabidhi binti huyo picha ambayo aliihitaji ikuzwe kwenye skrini kubwa maana alikuwa na maelezo mafupi ya kuweza kuwapa watu hao.

Baada ya dakika moja tu picha hiyo iliweza kusasishwa kwenye skrini zote ambazo zilikuwa ndani ya chumba hicho.
"Huyu ni mtu ambaye juzi hapa amehukumiwa miaka sitini jela kwa kosa la kuwa na genge la kihalifu na makosa mengi hususani ya mauaji na ubakaji" aliongea mwanamke yule akiwa anazitafuta taarifa za picha hiyo lakini hakuna kitu hata kimoja ambacho walikipata.

"Yeah upo sahihi. Licha ya picha zake kuwa adimu kupatikana lakini naona umefanya kazi ya ziada mpaka kufanikisha picha yake kuiona na kujua baadhi ya taarifa zake. Huyu ni mtu ambaye tunahitajika kumpata kwa gharama yoyote ile"
"Kwanini?"
"Huyu ndiye young master mwenyewe"
"Whaaaaat?"

"Huyu ndiye ambaye mimi nimemtafuta kwa miaka zaidi ya ishirini sasa na baadae nikawa nimeamua kujihakikishia kwamba alishakufa lakini yupo hai"
"Hili jambo linawezekanaje?"
"Huenda sikuwahi kumtilia maanani mtu huyu lakini baada ya hili vugu vugu kutokea nimegundua kwamba huenda ndiye ambaye mimi nilidhania kwamba alikuwa amepotea kwa wakati wote huu"
"Why?"

"Wazazi wake waliuawa akiwa na miaka kumi na tano kuingia wa kumi na sita na mimi nimeanza kufanya kazi na baba yake yeye akiwa na miaka kumi huku nikiwa nimepewa kazi ya kumlinda hivyo naweza kusema namjua sana kuliko mtu yeyote yule ukiacha wazazi wake. Siku ile nakumbuka nilikuwa nipo kwenye dakika za mwisho kabisa za kifo changu na nilishuhudia mtu akiwa anaenda kumuua chini alipokuwa amelala anavuja damu bila msaada wowote ule na baada ya pale hakuna kitu ambacho nilifanikiwa kukiona tena na nilipokuja kushtuka mwili wake haukuwepo lile eneo zaidi ya miili ya wazazi wake na mdogo wake wa kike ambayo ilikuwa imeuawa kikatili sana eneo lile"

"Hali ile ilinifanya nihangaike sana kumtafuta bila jitihada zozote zile mwisho nikaamua kuamini kwamba huenda alishakufa hivyo nikaamua kuanza kumtafuta mmoja mmoja ambaye nilihisi kwamba atakuwa amehusika katika hili na ndio mwanzo wa kuwatafuta nyie ili tufanye kazi kwa pamoja. Lakini kuna jambo moja ambalo lilikuwepo kwenye mwili wake, kwa taarifa kutoka kwa mama yake mzazi ni kwamba akiwa bado mdogo aliwahi kuangukiwa na mafuta ya moto upande wa nyuma wa sikio lake hivyo sehemu hiyo ilikuwa imetengeneza alama nyeusi ambayo isingeweza kuja kufutika kwenye maisha yake yote. Baada ya kuitazama picha hii kwa umakini nimeiona hiyo alama na sio rahisi alama kama hii kujitokeza kwa kila mtu ukilinganisha na sehemu ambayo yeye alikuwa ameumia miaka hiyo hivyo moja kwa moja atakuwa ni yeye"

9 naweka nukta hapa.

Febiani Babuya.
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA KUMI
"Sasa kwa hayo mazingira ambayo umeelezea kwamba alikuwepo mara ya mwisho na kwa umri wake mbona haionyeshi kama alikuwa na nafasi yoyote ile ya kuweza kupona, sasa unahisi labda alifanikiwaje kuishi? na miaka yote hii iliwezekana vipi ushindwe kujua kama yupo hai?"

"Kuhusu hilo bado ni mapema sana sina taarifa zozote zile ila natakiwa kumpata yeye ama kuyajua maisha yake yote ambayo mtu huyu ameyaishi kabla ya kufikia hapa ambapo amefikia leo na kuingia kwenye mikono ya jeshi la polisi"

"Una picha yake ya zamani bosi?" hakujibu lolote zaidi ya kuitoa simu yake na kuitoa picha ya huyo kijana ambaye alikuwa anahisi kwamba ni yeye. Mwanamke huyo ambaye alikuwa karibu na komputa aliinyonya picha hiyo na kuihamishia kwenye komputa yake ambapo aliiweka karibu na hiyo picha ya Remy Claude ili kuweza kuzilinganisha na kupata uhalisia wake.

"Ni picha tofauti kabisa hazina hata uhusiano japo asilimia moja tu hii inaonyesha kwamba ni watu wawili tofauti" mwanamke huyo alimjibu bosi wake huku akiwa anahakiki kwa mara nyingine tena kuona kama mtu huyo alikuwa anaendana na hiyo picha ya huyo mtoto wa miaka kumi na mitano.

"Dunia imeenda mbele sana ya muda, kuna uwezekano anaishi ndani ya mwili wa mtu mwingine hivyo sio rahisi sana kumpata namna hiyo"
"How?"

"Kama angekuwa kwenye sura yake halisi basi tungekuwa tulishamjua muda mrefu sana. Hili jambo siwezi kulipuuzia muda huu natakiwa kuwahi Dar es salaam, nitaenda na Hezironi tu na pale ambapo nitakuwa nawahitaji basi nitawapeni taarifa"
" Bosi una uhakika na hiki unacho taka kukifanya?"

"Niliapa mbele ya kaburi la baba yake mzazi kwamba ningemtafuta mwanae japo sikujua kama yupo hai, huenda hii ikawa nafasi yangu bora zaidi ya kuweza kulitimiza jambo hili hivyo sina namna ni lazima nilifanye hili"
"Bosi unaweza kutuambia leo kwamba ni mambo gani ambayo hatuyajui yalitokea miaka hiyo?"

"Hapana huu sio muda wake na wakati utakapo fika basi nitawaambia kila kitu mwenyewe" mwanaume huyo wa makamo alitoka humo ndani na wanaume wawili ambao walimpokea getini na kuelekea ndani ya chumba cha matibabu ili kuweza kumtibia kisha aingie ndani ya jiji la Dar es salaam ambako ndiko huyo mtoto aliyedai kwamba ni bosi wake alikuwa amefungwa ndani ya gereza la DOMINIC.


KIVUKONI DAR ES SALAAM
Ndani ya jengo kubwa la Ikulu ambamo kulikuwa na ofisi ya mheshimiwa raisi wa taifa la Tanzania, vyumba vya juu vya jengo hilo. Ndani ya ofisi moja ya kupumzikia walikuwa wamekaa watu wakubwa wawili ambao ndio walikuwa wanaiendesha nchi hasa kimaamuzi.

Mheshimiwa raisi Tobiasi Maalimu pamoja na katibu mkuu kiongozi Gofrey Likumbi walikuwa wameketi humo ndani wakiwa wanateta mambo ambayo walikuwa wanaona kwamba yalikuwa ni ya mhimu sana kwa ajili ya kuweza kulikuza taifa na kulifanya lizidi kwenda mbele zaidi.

"Yule kijana unahisi kwamba ni kweli amehusika na ambayo imedaiwa kwamba ameyafanya?"
"Wewe ndiye mtu mkubwa zaidi ndani ya hili taifa mheshimiwa hivyo taarifa ambayo inafika kwako inakuwa imenyooka sana sidhani kama inaweza kuwa ya uongo kwa sababu madhara yake ni makubwa"

"Lakini bado sijaletewa taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, taarifa ambayo huenda ilitakiwa kwanza ifike kwako kisha wewe ndiye uniletee lakini sioni haja ya hayo yote hiyo nahitaji tu aje kwangu moja kwa moja"
"Sawa mheshimiwa lakini sijaelewa kwamba ni kwanini una wasiwasi juu ya yule kijana"

"Kwa sababu ya aina ya watu ambao alikuwa anawaua, ni kama alikuwa anachagua kundi la watu fulani tu basi ndio anawateketeza na hainiingii akilini kwamba mtu huyu serikali imemtafuta kwa miaka kumi"

"Kla kitu kinawezekana chini ya jua mheshimiwa, wanadamu wengi kwenye macho ya kawaida ni wema na huwa wanatia huruma sana wanapokuwa wamefika kwenye mazingira ambayo wanakuwa hawana nafasi ya kuweza kujitetea ila ukiamua kuwakumbatia kwa sababu wanatia huruma baadae huwa wanageuka na kuwa nyoka ambao wanaweza kukudhuru mwenyewe"

"Mhhhhh hivi kwa upande wako wewe umewahi kutamani kuja kuwa raisi wa taifa hili? maana naona kama una maono ya mbali sana na hesabu kali"
"Hilo jambo siwezi na sijawahi kufikiria mheshimiwa"

"Kwanini? wakati huko nje watu wengi wanauana ili kuweza kuipata nafasi hii?"
"Wewe nakuheshimu sana hivyo siwezi kabisa kugusia suala hilo ukiwa hapo labda kwa baadae sana kama ukimaliza miaka yako na ukaamua kunibariki mwenyewe" raisi hakumjibu zaidi ya kutabasamu akionekana kumtathmini mtu wake huyo lakini akiwa anaendelea na tathmini zake simu yake ilikuwa inaita mezani.
"Mruhusu aingie" alijibu mara moja tu na kuikata simu hiyo. Muda mfupi mbeleni aliingia mkurugenzi wa usalama wa taifa Cleopatra Gambo na kuwapa heshima watu hao wawili ambao kicheo walikuwa ni wakubwa kwake na wote alikuwa na haki ya kuripoti kwao kwa ruhusa maalumu.

"Naomba utuache wawili tu Geofrey" mheshimiwa ni kama aliamua kumkataa katibu kiongozi wake na kuhitaji hayo mazungumzo ayafanye yeye mwenyewe na mwanamke huyo.
"Mheshimi...."
"Usijali kila kitu kitakuwa sawa, ni usiku sana saivi hivyo unaweza kwenda nyumbani tu tutaongea wakati mwingine" katibu mkuu kiongozi alitoka ndani humo lakini hakuonekana kuwa mtu ambaye alikuwa ameridhika na jambo hilo japo hakuwa na namna nyingine ya kuweza kufanya.

"Nipe ripoti Cleopatra" mwanamama huyo alimpatia raisi huyo ripoti kwenye bahasha ambayo ilisomwa kwa umakini sana na mheshimiwa kisha baada ya dakika tano akaishusha chini maana alikuwa ameyapata maelezo ya mhimu tayari.

10 inafika tamati.

Febiani Babuya.
 
HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
"Mbona kama taarifa haijakamilika?"
"Ndiyo haipo kamili"
"Kivipi?"
"Kwa sababu kuna mkanganyiko mkubwa wa habari juu ya uhalisia wa maisha ya mtu huyu"
"Unamaanisha nini?"

"Kwanza jina ambalo analitumia linaonekana kuwa sio lake kwa sababu msaidizi wangu amefuatilia kwenye mahospitali yote lakini hakuna mtu ambaye amewahi kuzaliwa akawa na jina kama hili hivyo ni wazi ametengeneza jina ambalo sio lake"
"Sasa kwanini afanye hivyo?"
"Kwa sababu inaonekana kwamba kuna watu ambao yeye anawatafuta watakuwa ndani ya lile gereza la DOMINIC"
"Unataka kuniambia hata jela ambako alipelekwa mara ya kwanza ameua watu makusudi ili aende kwenye lile gereza?"
"Ndiyo mheshimiwa"
"Why?"
"Huenda hao watu ana historia nao kubwa kwenye maisha yake ndiyo maana ameamua kurisk kila kitu chake ili tu aende kule"
"Kwahiyo unataka kuniambia hata kukamatwa pia ulikuwa ni mpango wake?"

"Sina uhakika ila tunahisi hivyo mheshimiwa"
"Ohhhh shit!"
"Msaidizi wangu anatuma mtu kwenye lile gereza ili aanze kumchunguza taratibu kila ambacho anakifanya kule nadhani ndiyo itakuwa njia bora zaidi ya sisi kuanza kujua mambo ambayo anaonekana kutuficha na kwanini anatumia jina ambalo sio lake maana yake lazima kuna mambo magumu na mazito sana nyuma yake"

"Hizo taarifa nahitaji kuzipata haraka sana na ikiwezekana inatakiwa niende mimi mwenyewe kukutana na huyo mfungwa"
"Mheshimiwa huwezi kwenda kwenye gereza lile"
"Mimi ni raisi wa nchi, naenda sehemu yoyote ile ambayo naitaka mimi, sasa kwanini unahisi kwamba sitakiwi kwenda kule?"
"Nisamehe mheshimiwa"
"Sawa unaweza kwenda nataka nitulie mwenyewe kwanza kwa muda" raisi habari zile zilimshtua sana kuona mtu anajiingiza kwenye hatari kubwa namna ile ili afanikiwe kuingia gerezani tu? huenda kulikuwa na mambo magumu na mazito sana nyuma yake.
"Sawa mheshimiwa, uwe na usiku mwema" mwanamama huyo aliaga na kuanza kutoka humo ndani ila hakujibiwa maana ni kama raisi huyo alikuwa amezama kwenye mawazo lakini wakati anashika mlango ili aufungue na kutoka humo ndani aliitwa na mheshimiwa hivyo ikamlazimu kurudi tena kukaa chini ili kumsikiliza mkubwa wa nchi.

"Una kumbukumbu zozote zile juu ya DOMINIC SAWA SAWA?"
"Unamaanisha yule ambaye lile gereza liliitwa jina lake?"
“Huyo huyo”
"Ndiyo mheshimiwa, yule familia yake yote iliuawa akiwepo yeye mwenyewe hivyo hakuna ambacho kilibakia kuhusu yeye"
"Sawa, waweza kwenda" kauli za mheshimiwa hata mwanamama huyo zilimpa wasiwasi na mashaka sana maana tangu ampatie raisi huyo hizo taarifa alionekana kubadilika kabisa tofauti na alivyokuwa amemkuta mwanzo kabla ya kumpatia taarifa hizo ila hakuwa na namna zaidi ya kutoweka ndani ya ofisi hiyo.


GEREZANI
Ndani ya gereza, kutokana na hali ambayo alikuwa nayo Remy, waliogopa kwamba anaweza kufa bila msaada pekeyake hivyo walimchanganya kwenye selo ambayo ilikuwa na watu wengine watano. Watu hao walionekana kujikatia tamaa kabisa ya maisha kwani sura zao hazikuwa na nuru kabisa. Wanaume wawili walikuwa wamekondeana sana huku wakionekana wazi kwamba walikuwa wamekaa ndani ya gereza hilo kwa muda mrefu. Remy ambaye alikuwa kwenye maumivu makali alibaki anawashangaa watu hao maana walipauka mpaka wakawa wanatoka kwenye ubinadamu ukijumlisha na harufu kali ambayo ilikuwepo humo ndani basi ilimfanya kuona namna baadhi ya watu walivyokuwa wanayaishi maisha magumu.

Watatu miili yao ilikuwa bado imeshiba na walionekana waliingia gerezani humo muda sio mrefu sana maana wao hawakuwa wamefubaa kama wenzao. Wanaume hao walikuwa wamelala lakini baada ya mtu huyo kuletwa na kutupwa humo kama mzigo walishtuka kutokana kwanza na hali ambayo alikuwa nayo kwenye mwili wake. Alikuwa na kisu mwilini pamoja na nondo kwenye paja lake huku mapaja yake yakiwa yamebeba risasi ndani yake. Wakati wanaendelea kumshangaa mwanaume huyo ambaye naye kwa mbali alikuwa anayashangaa mazingira ya humo ndani walisikia sauti ya kejeli ambayo ilichanganyika na matusi kutoka kwa moja ya maaskari ambao walikuwa wamemleta sehemu hiyo Remy.

"Ole wenu hata mmoja wenu ajaribu kumsaidia kwa lolote huyo mbwa hapo tutanyooka naye" ilikuwa ni sauti ya mamlaka haswa ambayo walipaswa kuitii kwa nguvu zote kisha askari huyo akalifunga geti la chuma la chumba hicho kidogo ambacho walihifadhiwa jumla wanaume sita.

Chumba kilikuwa kidogo sana huku kikiwa kinafukuta joto ambalo lilifanya kila mmoja humo ndani kutoa jasho sana isipokuwa wale wawili ambao walikuwa wamefubaa sana, sura zao hazikuwa hata zinaonyesha kama walikuwa wanavuja jasho sana huenda kwa sababu walionekana kuwa wazoefu ndani ya hilo eneo ukilinganisha na wenzao.

Harufu kali ambayo ilikuwa inapatikana ndani ya chumba hicho ni kwa sababu ya uchafu na kinyesi ambacho kilikuwa kinapatikakana humo humo, yaani hicho chumba ndicho kilikuwa choo na sehemu ya kulala hivyo kufanya hali kuwa mbaya sana hususani kwa afya ya mwanadamu ambaye bado yupo hai. Mmoja kati ya wale wanaume ambao walikuwa wamefubaa alionekana kuchoka sana kiasi kwamba alikuwa kwenye hali mbaya kama sio kiafya basi ni kwa sababu ya kukosa lishe lakini hakuna ambaye alikuwa na muda naye kabisa maana kila mtu alitakiwa kujiwazia yeye kwanza kabla ya kumuwazia mwenzie.

Watu hao ni kama walikuwa wana maswali mengi kwa huyo mgeni ambaye alifanyiwa kitu kibaya lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa na muda naye. Kutokana na hali kuwa mbaya humo ndani Remy hakufanikiwa hata kupata japo lepe wala tone la usingizi hali ambayo ilimfanya usiku mzima ateseke na vitu vitatu. Kwanza yalikuwa ni maumivu makali ambayo yalikuwa kwenye mwili wake, pili harufu kali na mbaya ambayo alikuwa anaipata humo ndani japo hakufanikiwa kuona kila kitu kwani kulikuwa na mwanga mdogo tu wa taa ya nje ndio ambao ulimfanya kuona baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa karibu yake usiku huo ila vingine hakufanikiwa kuvitia machoni kabisa. Lakini jambo la tatu lilikuwa ni joto kali ambalo alilipata sehemu kama hiyo halikumfanya kuwa na nafasi ya kupata usingizi hata kidogo hivyo mpaka asubuhi alikuwa yupo macho na ndipo alifanikiwa kuuona mwanga na mijongeo ya askari ambao wengi alikuja kugundua kwamba hawakuwa askari wa kawaida kama alivyokuwa anadhani mwanzo bali walikuwa ni wanajeshi kabisa na wengi walikuwa kwenye magwanda yao huku idadi ya askari ikiwa ndogo zaidi ya wanajeshi ambao walifurika kila sehemu.

Akiwa anaangalia mazingira ya nje, aliona wanajeshi wakija pale na kupitisha vibakuli vya supu ambayo haikujulikana ilikuwa ya nini maana ndani yake hakukuwa na nyama hata moja zaidi ya mchuzi tu, vilikuwa vibakuli vitano vya wale wafungwa watano ambao Remy aliwakuta mle ndani. Kila mtu alikikimbilia kibakuli kimoja kana kwamba walihofia aliye vileta asije kuvitoa tena kama wangechelewa kuvipokea. Hiyo ilikuwa ishara mbaya sana kwa Remy na kugundua kwamba watu hao hilo eneo walikuwa wakiteseka kwa njaa kali isivyokuwa kawaida ndiyo maana kwao chakula walikuwa wanakipa thamani ya hali ya juu tofauti na watu wa maisha ya nje walivyokuwa wanaishi kwa kuchagua vyakula huku wengine hata vile vyakula vya thamani wakivitupa jalalani, hiyo hali ilimpa moja kati ya masomo bora sana ya kuweza kuthamini kitu ambacho unakuwa unacho hata kama ni kidogo kwa wakati huo.

11 sina la ziada.

Febiani Babuya.
 
Back
Top Bottom