Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani kiongoziHADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
"Mbona kama taarifa haijakamilika?"
"Ndiyo haipo kamili"
"Kivipi?"
"Kwa sababu kuna mkanganyiko mkubwa wa habari juu ya uhalisia wa maisha ya mtu huyu"
"Unamaanisha nini?"
"Kwanza jina ambalo analitumia linaonekana kuwa sio lake kwa sababu msaidizi wangu amefuatilia kwenye mahospitali yote lakini hakuna mtu ambaye amewahi kuzaliwa akawa na jina kama hili hivyo ni wazi ametengeneza jina ambalo sio lake"
"Sasa kwanini afanye hivyo?"
"Kwa sababu inaonekana kwamba kuna watu ambao yeye anawatafuta watakuwa ndani ya lile gereza la DOMINIC"
"Unataka kuniambia hata jela ambako alipelekwa mara ya kwanza ameua watu makusudi ili aende kwenye lile gereza?"
"Ndiyo mheshimiwa"
"Why?"
"Huenda hao watu ana historia nao kubwa kwenye maisha yake ndiyo maana ameamua kurisk kila kitu chake ili tu aende kule"
"Kwahiyo unataka kuniambia hata kukamatwa pia ulikuwa ni mpango wake?"
"Sina uhakika ila tunahisi hivyo mheshimiwa"
"Ohhhh shit!"
"Msaidizi wangu anatuma mtu kwenye lile gereza ili aanze kumchunguza taratibu kila ambacho anakifanya kule nadhani ndiyo itakuwa njia bora zaidi ya sisi kuanza kujua mambo ambayo anaonekana kutuficha na kwanini anatumia jina ambalo sio lake maana yake lazima kuna mambo magumu na mazito sana nyuma yake"
"Hizo taarifa nahitaji kuzipata haraka sana na ikiwezekana inatakiwa niende mimi mwenyewe kukutana na huyo mfungwa"
"Mheshimiwa huwezi kwenda kwenye gereza lile"
"Mimi ni raisi wa nchi, naenda sehemu yoyote ile ambayo naitaka mimi, sasa kwanini unahisi kwamba sitakiwi kwenda kule?"
"Nisamehe mheshimiwa"
"Sawa unaweza kwenda nataka nitulie mwenyewe kwanza kwa muda" raisi habari zile zilimshtua sana kuona mtu anajiingiza kwenye hatari kubwa namna ile ili afanikiwe kuingia gerezani tu? huenda kulikuwa na mambo magumu na mazito sana nyuma yake.
"Sawa mheshimiwa, uwe na usiku mwema" mwanamama huyo aliaga na kuanza kutoka humo ndani ila hakujibiwa maana ni kama raisi huyo alikuwa amezama kwenye mawazo lakini wakati anashika mlango ili aufungue na kutoka humo ndani aliitwa na mheshimiwa hivyo ikamlazimu kurudi tena kukaa chini ili kumsikiliza mkubwa wa nchi.
"Una kumbukumbu zozote zile juu ya DOMINIC SAWA SAWA?"
"Unamaanisha yule ambaye lile gereza liliitwa jina lake?"
“Huyo huyo”
"Ndiyo mheshimiwa, yule familia yake yote iliuawa akiwepo yeye mwenyewe hivyo hakuna ambacho kilibakia kuhusu yeye"
"Sawa, waweza kwenda" kauli za mheshimiwa hata mwanamama huyo zilimpa wasiwasi na mashaka sana maana tangu ampatie raisi huyo hizo taarifa alionekana kubadilika kabisa tofauti na alivyokuwa amemkuta mwanzo kabla ya kumpatia taarifa hizo ila hakuwa na namna zaidi ya kutoweka ndani ya ofisi hiyo.
GEREZANI
Ndani ya gereza, kutokana na hali ambayo alikuwa nayo Remy, waliogopa kwamba anaweza kufa bila msaada pekeyake hivyo walimchanganya kwenye selo ambayo ilikuwa na watu wengine watano. Watu hao walionekana kujikatia tamaa kabisa ya maisha kwani sura zao hazikuwa na nuru kabisa. Wanaume wawili walikuwa wamekondeana sana huku wakionekana wazi kwamba walikuwa wamekaa ndani ya gereza hilo kwa muda mrefu. Remy ambaye alikuwa kwenye maumivu makali alibaki anawashangaa watu hao maana walipauka mpaka wakawa wanatoka kwenye ubinadamu ukijumlisha na harufu kali ambayo ilikuwepo humo ndani basi ilimfanya kuona namna baadhi ya watu walivyokuwa wanayaishi maisha magumu.
Watatu miili yao ilikuwa bado imeshiba na walionekana waliingia gerezani humo muda sio mrefu sana maana wao hawakuwa wamefubaa kama wenzao. Wanaume hao walikuwa wamelala lakini baada ya mtu huyo kuletwa na kutupwa humo kama mzigo walishtuka kutokana kwanza na hali ambayo alikuwa nayo kwenye mwili wake. Alikuwa na kisu mwilini pamoja na nondo kwenye paja lake huku mapaja yake yakiwa yamebeba risasi ndani yake. Wakati wanaendelea kumshangaa mwanaume huyo ambaye naye kwa mbali alikuwa anayashangaa mazingira ya humo ndani walisikia sauti ya kejeli ambayo ilichanganyika na matusi kutoka kwa moja ya maaskari ambao walikuwa wamemleta sehemu hiyo Remy.
"Ole wenu hata mmoja wenu ajaribu kumsaidia kwa lolote huyo mbwa hapo tutanyooka naye" ilikuwa ni sauti ya mamlaka haswa ambayo walipaswa kuitii kwa nguvu zote kisha askari huyo akalifunga geti la chuma la chumba hicho kidogo ambacho walihifadhiwa jumla wanaume sita.
Chumba kilikuwa kidogo sana huku kikiwa kinafukuta joto ambalo lilifanya kila mmoja humo ndani kutoa jasho sana isipokuwa wale wawili ambao walikuwa wamefubaa sana, sura zao hazikuwa hata zinaonyesha kama walikuwa wanavuja jasho sana huenda kwa sababu walionekana kuwa wazoefu ndani ya hilo eneo ukilinganisha na wenzao.
Harufu kali ambayo ilikuwa inapatikana ndani ya chumba hicho ni kwa sababu ya uchafu na kinyesi ambacho kilikuwa kinapatikakana humo humo, yaani hicho chumba ndicho kilikuwa choo na sehemu ya kulala hivyo kufanya hali kuwa mbaya sana hususani kwa afya ya mwanadamu ambaye bado yupo hai. Mmoja kati ya wale wanaume ambao walikuwa wamefubaa alionekana kuchoka sana kiasi kwamba alikuwa kwenye hali mbaya kama sio kiafya basi ni kwa sababu ya kukosa lishe lakini hakuna ambaye alikuwa na muda naye kabisa maana kila mtu alitakiwa kujiwazia yeye kwanza kabla ya kumuwazia mwenzie.
Watu hao ni kama walikuwa wana maswali mengi kwa huyo mgeni ambaye alifanyiwa kitu kibaya lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa na muda naye. Kutokana na hali kuwa mbaya humo ndani Remy hakufanikiwa hata kupata japo lepe wala tone la usingizi hali ambayo ilimfanya usiku mzima ateseke na vitu vitatu. Kwanza yalikuwa ni maumivu makali ambayo yalikuwa kwenye mwili wake, pili harufu kali na mbaya ambayo alikuwa anaipata humo ndani japo hakufanikiwa kuona kila kitu kwani kulikuwa na mwanga mdogo tu wa taa ya nje ndio ambao ulimfanya kuona baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa karibu yake usiku huo ila vingine hakufanikiwa kuvitia machoni kabisa. Lakini jambo la tatu lilikuwa ni joto kali ambalo alilipata sehemu kama hiyo halikumfanya kuwa na nafasi ya kupata usingizi hata kidogo hivyo mpaka asubuhi alikuwa yupo macho na ndipo alifanikiwa kuuona mwanga na mijongeo ya askari ambao wengi alikuja kugundua kwamba hawakuwa askari wa kawaida kama alivyokuwa anadhani mwanzo bali walikuwa ni wanajeshi kabisa na wengi walikuwa kwenye magwanda yao huku idadi ya askari ikiwa ndogo zaidi ya wanajeshi ambao walifurika kila sehemu.
Akiwa anaangalia mazingira ya nje, aliona wanajeshi wakija pale na kupitisha vibakuli vya supu ambayo haikujulikana ilikuwa ya nini maana ndani yake hakukuwa na nyama hata moja zaidi ya mchuzi tu, vilikuwa vibakuli vitano vya wale wafungwa watano ambao Remy aliwakuta mle ndani. Kila mtu alikikimbilia kibakuli kimoja kana kwamba walihofia aliye vileta asije kuvitoa tena kama wangechelewa kuvipokea. Hiyo ilikuwa ishara mbaya sana kwa Remy na kugundua kwamba watu hao hilo eneo walikuwa wakiteseka kwa njaa kali isivyokuwa kawaida ndiyo maana kwao chakula walikuwa wanakipa thamani ya hali ya juu tofauti na watu wa maisha ya nje walivyokuwa wanaishi kwa kuchagua vyakula huku wengine hata vile vyakula vya thamani wakivitupa jalalani, hiyo hali ilimpa moja kati ya masomo bora sana ya kuweza kuthamini kitu ambacho unakuwa unacho hata kama ni kidogo kwa wakati huo.
11 sina la ziada.
Febiani Babuya.
Namalizana na JIJI LA KAMARI Leo hivyo hii tunaanza nayo kesho au Leo usiku.Hadi leo kimya!!
Makini sana, vipi documents 72 part 2 Bado haijatoka?Namalizana na JIJI LA KAMARI Leo hivyo hii tunaanza nayo kesho au Leo usiku.
Niliamua niwe na moja moja.
DOCUMENT NUMBER 72/ NYARAKA NAMBA 72 ndiyo part 2 mkuu. Mpangilio uko hiviMakini sana, vipi documents 72 part 2 Bado haijatoka?
Nikuelewa kaka mkubwaDOCUMENT NUMBER 72/ NYARAKA NAMBA 72 ndiyo part 2 mkuu. Mpangilio uko hivi
1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA. Part one
2. NYARAKA NAMBA 72. Part 2.
Kwa sasa inayo subiriwa ni THE CONCLUSION (CHAPTER 3) ambayo ndiyo itakuwa mwisho wa hizo collection. Jina lake ni👇
3. KALAMU ILIYO-TUMWA KUNIUA....... Hii ndiyo ambayo itamkutanisha baba mtu na mtoto wake. Yaani Calvin Jackson wa kwenye ULIMWENGU WA WATU WABAYA pamoja na mwanae Calvinjr ambaye tumemsoma kwenye DOCUMENT NUMBER 72.
Kukujibu swali lako ni kwamba bado haijatoka.
Hii story inauzwa kama arosto ikizidi Sio mbaya kununua ili kumtia moyo mwandishi 🤔Hii story vipi ,mbona kimya sana au majukumu yamekubana?