Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

133.
“Ni Mmarekani, na kuhusu swali la pili, ndio nilikuwa nakuja huko.” Akajibu kifupi Rais na kuendelea. “Kwanza kabisa, ni mwanajeshi ambaye aliwahi kufa. Na baada ya kufa, ndipo Dokta mmoja ambaye naye ni marehemu, aliweza kumfufua kwa kumuingizia kemikali za C.O.D.EX.” Akakatishwa maelezo yake na Agent.

“Hizo kemikali si ndizo zile zilifungiwa miaka kumi iliyopita kwa sababu ya kuwaathiri sana Alex na Alex Junior ambao walikuwa wanajeshi tishio sana duniani.” Akaongea Agent.

“Wewe hayo umeyajuaje wakati yalikuwa ni ya siri kubwa?” Akauliza Rais.

“Kuna vitabu, kaviandika Tariq Haji na kaviita C.O.D.EX, vipo vitatu. Vinaelezea kinagha ubagha yote hayo. Ni kama riwaya, lakini nilipofuatilia, haya mambo ni kweli yalitokea.” Akajibu Agent.

“Okay. Ni kweli ulichoongea. Lakini CIA na FBI pamoja na serikali nzima ya Marekani, walifungua tena ile maabara na safari hii walikuwa wanachukua watu waliokwisha kufa hasa wanajeshi wa Kimarekani ambao walifia vitani au wananchi wenye IQ kubwa ili wawasaidie katika kutengeneza silaha.”

“Kwa hiyo huyo mwanajeshi yupo vipi?” Rais akavuta bahasha fulani na kutupa mezani ambapo Agent aliifungua na kuanza kuangalia baadhi ya picha ambazo zilionesha wanajeshi wa C.O.D.EX wakiwa katika mazoezi yao. Walikuwa wanatisha sana kwa wanachokifanya lakini walionekana kutojali wala kuhisi maumivu.

Baada ya picha hizo, Rais pia akampa kijana anayemuamini simu matata sana na kumchezeshea video ambayo ilionesha wale wanajeshi wakiungua na baadae kurudi katika hali yao ya kawaida. Na picha kadhaa za video zile, zilionesha ukatili na silaha zao hatari wanazotumia. Mwili ukamsisimka Agent.

“Hapa kuna kazi kubwa Mkuu.” Akaongea Agent huku anarudisha vile vitu alivyopewa.

“Ndio maana wanajeshi wetu hawawezi. Anahitajika mtu mjanja na mwenye uelewa wa kuwazuia hata kwa sayansi zake. Naye ni wewe.” Rais akatoa jukumu zito.

“Nahitaji kusoma kwanza na sehemu ambapo nitatengeneza baadhi ya silaha zangu.” Akaongea Agent na Rais akamuelekeza kwenye maabara fulani iliyopo ndani ya Ikulu yake. Kisha akamtolea mafaili baadhi ambayo alitumiwa na CIA kwa ajili ya kumtambulisha mtu wanayetakiwa kukamata. Baada ya hapo, akaanza kumuelekeza mambo mengine mengi ambayo alipewa na CIA. Hadi nusu saa inakatika, Agent alikuwa kashiba maneno mengi ambayo yangemuongoza kwenye msako wake.

****

Ndani ya maabara ambayo ilikuwa ndani ya Ikulu, Agent alikuwa kavaa mawani kubwa myeusi na alikuwa anachanganya vitu kadhaa kwenye chungu cha chuma na ambacho kilikuwa kimepata joto kali na kuwa chekundu sana. Kila alipotupia baadhi ya vitu alivyovijua yeye, moto mkali ulifumuaka na kuzidisha joto ndani ya maabara ile ya Kisayansi.

Baada ya kuridhika, alimwagia mchanganyiko ule kwenye sahani moja kubwa na ya bati. Pini ndo go ndogo nyingi sana zikaonekana ndani ya sahani, naye Agent akatabasamu baada ya kufanikisha zoezi lake la kwanza lakini hakuishia hapo, alizimwagia kemikali fulani ambazo zilifanya pini zile zisimame kwenye sahani na kuchongoka zaidi.

Akabofya kiparaza cha kompyuta yake ambayo alikuwa anatembea nayo, na ile sahani ikaanza kuzunguka taratibu kisha kuhama na kwenda sehemu moja ambayo kulikuwa na kijumba kidogo alichokibuni Agent kwa ajili ya shughuli zake za Kisayansi. Kijumba hicho yeye mwenyewe alikiita UHAI. Akimaanisha ni kijumba kinachoweza kuvipa uhai vitu ambavyo havina uhai.

****

Asubuhi iliyofuata, Agent alionana na Rais na kumuelezea kazi yake ilivyokwenda na alimwambia yupo tayari kwa kazi ambayo kamtuma.

“Sawa kijana wangu. Nakuamini.” Rais aliongea kwa tabasamu na kisha akampa simu yake ambayo safari hii, alimtaka aende kuitazamia chumbani kwake kwa sababu yeye hakai tena ofisi sababu ziara ya siku hiyo ya kwenda Tabora kufungua miradi ya treni za angani. “Humo utaona ni wapi mtuhumiwa wako unatakiwa kumpata. Fanya yako leo hii, apatikane. Nishawaambia kuwa kazi ni leo.” Akaongea Rais baada ya kumkabidhi ile simu.

“Sawa Mkuu.” Agent alikubali na kusimama tayari kwa kuondoka ofisini.

“Agent Zero.” Kijana wa Rais akageuka na kumtazama Rais wake. “Kuna zawadi pia kwa ajili yako ukifanikisha hilo, Dola Milioni Moja inakusubiri na yawezekana ikapanda hadi hamsini.” Akampa taarifa mwanana kijana wake na kumfanya Agent atabasamu na kupiga saluti ya kikakamavu. “Nikutakie kheri katika kazi yako.” Akamaliza na Agent Zero kama alivyomuita, akatoka nje ya ofisi.

****

Furaha kubwa ilikuwa imemtawala Idris ambaye kila wakati alijiona mwenye bahati kukutana na Limasi ambaye kama mapenzi alimpa yote mwanaume yule aliyeficha siri nyingi juu yake. Idris akiwa anarudi nyumbani na zawadi kadhaa alizomnunulia mke wake, alisimama njia panda moja ambayo ilikuwa ina mataa ya usalama barabarani. Ilikuwa yapata saa tatu na robo usiku wakati mataa hayo ya usalama yaliposimamisha gari lake.

Aliamua kutumia muda ule mdogo kupekua zawadi kadhaa alizokuwa amemnunulia mpenzi wake. Wakati anafanya hayo akiwa ndani ya gari lake lingine la gharama, kuna gari moja kubwa aina ya scania lilikuwa linatokea upande wa kushoto kwa kasi ya ajabu na ghafla lilikumba gari la Idris na kulipasua katikati kisha ile sehemu inapokaa injini, ililipuka na kusababisha taflani eneo zima la barabara.





Furaha kubwa ilikuwa imemtawala Idris ambaye kila wakati alijiona mwenye bahati kukutana na Limasi ambaye kama mapenzi, alimpa yote, mwanaume yule aliyeficha siri nyingi juu yake. Idris akiwa anarudi nyumbani na zawadi kadhaa alizomnunulia mke wake, alisimama njia panda moja ambayo ilikuwa ina mataa ya usalama barabarani. Ilikuwa yapata saa tatu na robo usiku wakati mataa hayo ya usalama yaliposimamisha gari lake.
 
134.
Aliamua kutumia muda ule mdogo kupekua zawadi kadhaa alizokuwa amemnunulia mpenzi wake. Wakati anafanya hayo akiwa ndani ya gari lake lingine la gharama, kuna gari moja kubwa aina ya scania lilikuwa linatokea upande wa kushoto kwa kasi ya ajabu na ghafla lilikumba gari la Idris na kulipasua katikati kisha ile sehemu inapokaa injini, ililipuka na kusababisha taflani eneo zima la barabara.

ENDELEA.

Scania liligonga gari la Idris, lilienda kusimama hatua zipatazo ishirini tokea pale ambapo mlipuko umetokea. Kisha ikasikika sauti ya injini kupumua na mlango wa dereva kufunguka. Akashuka yuleyule kijana aliyetumwa na Rais wa Tanzania, wenyewe wanamuita Agent Zero ambaye usiku ule alikuwa kavaa suruali ya jeshi la Tanzania na kwa juu kavaa koti la leiza nyeusi, lililomkamata vema na ndani yake kavalia fulana iliyokuwa imeandikwa Hadithi App.

Upande wa Idris ambapo baada ya gari lake kugongwa vibaya, yeye alibakia kwenye kipande cha injini ambacho kililipuka na baada ya sekunde kama arobaini, mwanaume yule alionekana akitokea kwenye moto ule mkubwa na ngozi yake ilianza kujitengeneza taratibu na baadae kukaa vema huku akitokea kavaa nguo zake zilezile alizokuwa kavaa mwanzo.

“Karibu Tanzania mwanajeshi.” Agent Zero ndiye aliongea baada ya kumuona Idris kamaliza kujiunga mwili wake. Mikono yake aliiweka kwa nyuma na kila mara alikuwa akiitingisha kwa mbwembwe.

Idris akiwa na hasira baada ya vamizi lile la kushtukiza alichomoka ghafla pale alipo na kuanza kumkimbilia Agent na kitendo bila kusita, kutokea kwenye mkono wa koti lake, vile visindano alivyovitengeza Agent, vilishuka hadi kwenye kiganja chake cha mkono na kujaa kisha Agent alivinyanga vyote kwa pamoja na kuvirusha kumuendea Idris.

Vilikuwa vinatoa mlio wa fulani kama wa nzi wa chooni, na pia mlio wa vyuma vidogo kugongana ulisikika ndani yake. Vilipofika karibu na Idris, Agent ambaye alikuwa amesimama palepale aliposhukia na gari lake, alifunua mkono wa koti lake na saa moja matata sana ilionekana. Akaibonyeza kitufe kimoja kilichopo pembeni na sindano zile ndogondogo zilijitenga na kisha vimamvamia Idris shingoni na kuzunguka shingo ile na kumfanya akabwe.

Idris alipiga goti chini na kuanza kuhangaika kuvinasua vile visindano ambavyo vilianza kumchoma shingo yake na kusababisha damu kuanza kutoka kidogo kidogo.

“Hapa sio Marekani Mwanajeshi. Hapa ni Tanzania. Nchi yenye amani na yenye wingi wa wataalamu.” Agent aliongea huku taratibu akianza kusogea eneo ambalo alikuwa kapiga goti moja, Idris.

“Unataka nini?” Idris aliuliza akiwa wazi analazimisha kutafuta pumzi.

“Rahisi tu! Waliokutengeneza wanakutaka urudi nyumbani, Tanzania si kwako.” Akajibu Agent na jibu hilo likamfanya Idris amuangalie aliemwambia hayo.

“Unafanya kosa kubwa kijana. Watakuua na wewe tu.”

“Hapana Mwanajeshi, mimi kwanza nimeahidiwa donge nono nikikukamata. Na hapa navyokwambia, wapo njiani kuja kukuchukua. Kwa hiyo chaguzi ni lako.”

“Nooo.” Idris aling’aka kwa sauti na kushika zile pini zilizojiunga shingoni kwake na kuzivuta kwa nguvu nyingi sana. Nazo zikaachia shingo yake na Idris akazitupa kwenda kumuelea Agent ambaye hakuamini kama silaha yake itaweza kuzuiliwa kirahisi namna ile.

Idris alichomoka kwa teke matata sana ambalo lilimkuta Agent kifuani na kumrusha mbali kana kwamba kapigwa na shoti ya umeme.

Akiwa haamini kama kapigwa au kakagongwa na gari moshi. Agent alianza kugaa gaa chini kwa maumivu na bila kutegemea, Idris alikuwa karibu yake na alimnyanyua kwa mkono wake mmoja na kumbamiza kwenye kioo cha scania na kukifanya kioo kile kitengeneze nyufa.

Taratibu Agent alishuka chini huku damu zikimtoka mdomoni lakini hiyo haikuwa sababu ya kuachwa kutembezewa kipondo na Idris ambaye hasira zilimjaa kupita maelezo.

Agent alipokea ngumi kali toka kwa Idris iliyomfanya aingie hadi chini ya uvungu wa scania alilolitumia kuharibu gari la gharama la Idris.

Idris alipomchungulia Agent, aliweza kumuona akitambaa kwa haraka akijaribu kutaka kukimbilia upande mwingine wa lile Scania. Idris kwa nguvu zake nyingi, alisogea ubavuni mwa scania lile na kuanza kulisukuma kwa lengo la kulipindua na hali hiyo ilizidi kumtisha Agent ambaye alimua kutulia bila kutambaa hadi aliposikia kishindo cha gari lake kupinduliwa. Akajigeuza na kulala kifudifudi na hapo alimuona Idris akinyanyua ngumi yake na kutaka kumgonga nayo usoni ila Agent alibiringitia pembeni na ngumi ile ilikita kwenye rami na kuitoboa kabisa. Hapo ndipo Agent aligundua kamchokoza nguruwe pori kwa kumuibia vitoto vyake. Ikabidi naye aanze kujibu mapigo ya Idris ambaye alikuwa anataka kumkanyaga kwa viatu vyake.

Agent akabiringita tena kidogo na kiatu kile kikamkosa kwa mbali sana na kwa haraka, alirudi pale alipotoka wa kubiringita na kukamata mguu wa Idris na kuubana vema kama anataka kuuvunja. Idris akashindwa kustahimili, akakosa balansi na kujikuta akikubali kudondoka aridhini na uso kwa uso alikutana na ngumi matata ya pua kutoka kwa Agent Zero. Akahisi pua kuvunjika lakini hakuhisi maumivu na alipomtazama Agent, alishuhudia kiatu chake kikimfuata na kutua palepale kwenye pua. Akagugumia kwa maumivu machache aliyoyapata.

Agent akajibetua kiustadi na kusimama kisha kwa haraka, alikimbia kumfuata Idris ambaye alikuwa kalala kifudifudi. Sarakasi ya mtupu, ilimtoka Agent lakini aliweza kutulia miguu ambayo ilikanyaga juu ya kifua cha Idris ambaye alikohoa vibaya kwa pigo lile toka kwa Mtanzania mwenye mapenzi na nchi yake. Agent kwa ukakasi wa raha, alijibetua tena sarakasi ya mbele na kutua kwenye rami, na kisha kwa utamu wa raha zake, akajibetua sarakasi ya kurudi nyuma na kwa mara nyingine alitua juu ya kifua cha Idris lakini safari hii, magoti yake yakiwa yamekita juu kifua hicho. Idris akazidi kukohoa na kujitutumua kwa kumsukuma Agent pembeni ambaye naye hakuwa haba katika kujitetea.

Akabiringita kwa chini na kwa ustadi wa aina yake, akajibetua kwa sarakasi na hapo akatulia huku mkono wake mmoja upo chini na miguu yake miwili imechukua balansi. Ukimuoa waweza sema labda mwanariadha ambaye anataka kuanza mbio zake. Idris naye alisimama na kutazama kiumbe anachopambana nacho.
 
135.
Kwanza kina kasi ya ajabu, pili kina mapigo ya kushtukiza, na tatu kina roho ngumu licha ya kuwa binadamu halisi. Kwa nini asikiulize kile kiumbe.

“Wewe ni nani?” Idris akajikuta anaropoka swali.

“The Undercover Agent.” Akajibu Agent Zero.

“Huna jina mbwa wewe?” Akabwata tena kwa sauti ya hasira.

“Niite Agent Zero. Agent wa kujitegemea, sinaga haja ya kushirikiana na mtu.” Akajibiwa tena kwa sauti ya utulivu. Lakini jibu lile likampa hasira zaidi Idris na kujikuta akianza kumfuata kwa kasi pale Agent alipoweka pozi la kiuana riadha.

Alipofika, alirusha teke lake kama anayebutua mpira lakini Agent aliliona na kupiga sarakasi ndogo ya kusogea upande mmoja na kisha kwa kasi ya ajabu, alinyanyuka kwa mateke matatu ya haraka ambapo moja lilimpata kwenye mguu, lingine likapanda hadi kiunoni na la mwisho likampandia kisogoni. Idris akajikuta anapepesuka kama mlevi anayeelekea kutumbukia shimoni na wakati huo Agent alitua chini na kusimama wima akiwa nyuma ya Idris, kisha kwa kasi alikwenda kumrukia kwa nyuma na kumkaba huku miguu yake ikibana tumbo la Idris.

Idris akaanza kuhaha kuchomoa kabali nzito aliyokuwa anaipitia kwa muda ule. Alihangaika bila kufanikiwa na kujikuta akipiga goti moja chini kwani tayari pumzi zilianza kumuisha. Kila alipotaka kuondoka kabali ile, alijikuta akizidi kukabwa.

Mara uso wake ukaanza kuona picha za ajabu ajabu. Mara alimuona mtoto akiwa anapelewa keki ya siku ya kuzaliwa. Na mara akamuona mwanamke akiwa anambusu kwenye paji lake la uso huku anamtakia heri ya kuzaliwa. Picha zilikuwa zinakuja kwa kuchanganyika sana na hakuweza kutambua zile picha zinatokea kwa sababu gani. Na wakati picha hizo ambazo zilikuwa kama video zinazidi kutokea, ndipo alipoweza kushuhudia mwanamke aliyembusu kwenye paji la uso akikatwa vibaya shingo yake. Na picha hiyo aliweza kuiona moja kwa moja kwenye kichwa chake. Na hapo ndipo akashuhudia mtu mwenye suti akiingia chumbani ambapo mwanamke yule alikatwa shingo yake kwa panga kali. Uso wa tabasamu ukawa umepambwa kwenye paji la mwenye suti.

Mara picha hiyo ikaanza kufutika na kumrudisha hadi eneo la tukio ambapo bado Agent alikuwa kang’ang’ania shingo yake. Idris akafungua macho yake na kusimama kwa nguvu na kusababisha uoga mkubwa kwa Agent Zero ambaye hakutegemea kuona yule bwana anasimama kirahisi namna ile. Idris akaaanza kuzunguka kwa kasi ya feni na kumfanya Agent ajihisi kizunguzungu na kujikuta akimuachia mwenyewe mwanajeshi yule ambaye alikuwa kama mbwa mwitu aliyejeruhiwa. Picha za kile alichokiona zikamrudia na kujikuta akiikumbuka sura la yule mwenye tabasamu.

“Uzo.” Akaongea kwa sauti ya chini huku akiwa kasimama na kuacha kuzunguka. Agent yeye alikuwa anagaa gaa chini huku akihisi kutapika lakini aliposikia Idris anataja jina la mtu aisyemjua, akili ikarudi na kumtazama yule mwanajeshi. Wakakutanisha macho, na Idris ndiye alikuwa wa kwanza kutaka kumfuata Agent pale alipolala lakini wakati anaelekea pale, mara alisikia milio ya nzi wa chooni na kwa haraka akaweka mikono yake shingoni na zilezile pini zikambana mikono yake kwenye shingo.

Agent akajibetua haraka kwenda nyuma na kutuma pini zingine ambazo zilienda kunasa kwenye mguu wa kushoto na zingine mguu wa kulia. Haikujulikana idadi ya pini alizozibeba lakini alikuwa anazitoa kwa wingi sana. Zile za miguuni, zikajiunga kwa pamoja na kufanya miguu ile iiunganike na kugandana kama sumaku. Idris kila akijipapatua, hamna kilichokubali kumuachia na viliendelea kujikaza eneo husika kila alipotaka kuvitoa.

“Hivi vinini wewe mbwa?” Akauliza kwa tusi lakini Agent hakujibu chochote zaidi ya kutuma tena pini zingine zilizoenda kuziba mdomo wake.

“Wewe si Mtanzania. Acha maneno mengi hapa.” Akaongea Agent na kurusha pini zingine ambazo zikaenda kumfunga kiuno chake na zingine kikaenda kunasa kwenye scania lililokuwa limepinduka. Pini zile zilizoenda garini, zikawasiliana na pini za kiunoni na kutengeneza kitu kama kamba. Napo kwa pamoja vikaanza kumvutia Idris kwenye lile scania. Idris akawa haamini kama kirahisi vile kashindwa hasa baada ya kubanwa kwenye gari na kunatia hapo.

‘Subiri wenzako waje wakuchukue.” Agent akaongea huku anafuta damu iliyokuwa inamtoka upande mmoja wa mdomo wake.
 
136.






“Hivi vinini wewe mbwa?” Akauliza kwa tusi lakini Agent hakujibu chochote zaidi ya kutuma tena pini zingine zilizoenda kuziba mdomo wake.

“Wewe si Mtanzania. Acha maneno mengi hapa.” Akaongea Agent na kurusha pini zingine ambazo zikaenda kumfunga kiuno chake na zingine zikaenda kunasa kwenye scania lililokuwa limepinduka. Pini zile zilizoenda garini, zikawasiliana na pini za kiunoni na kutengeneza kitu kama kamba, napo kwa pamoja zikaanza kumvutia Idris kwenye lile scania. Idris akawa haamini kama kirahisi vile kashindwa hasa baada ya kubanwa kwenye gari na kunatia hapo.

“Subiri wenzako waje wakuchukue.” Agent akaongea huku anafuta damu iliyokuwa inamtoka upande mmoja wa mdomo wake.

ENDELEA.

Dakika kumi mbele, gari moja mfano wa daladala lakini yenyewe inavioo vyeusi na imekaa kipelelezi zaidi, iliingia eneo la tukio na milango ilifunguka. Akashuka Uzo akiwa na wanajeshi wawili wamekamata bunduki kubwa. Mmoja wa wanajeshi hao alikuwa ni Merice, mtoto wa Dokta Ice na Simeria.

Idris akaanza kupapatuka pale alipo kwa kutaka afunguliwe lakini hamna aliyemuelewa maana yake, kwa sababu ya kuzibwa mdomo.

“Ohoo! Ni wewe kumbe. Best?” Akaongea Uzo baada ya kwenda mbele ya Idris. “Au huku unatumia jina gani eti.” Akauliza tena kwa nyodo nyingi na hakutaka jibu na badala yake alienda hadi kwa Agent ambaye alikuwa amekaa juu ya jiwe moja lililopo pembeni ya barabara ile huku anachimbachimba chini.

Uzo akamtazama Agent na kisha macho yake yakarudi kwa Idris. “Yaani mtu akisema umelifunga domo lile jitu, hawezi kuamini kabisa. Hauendani na mambo yako kabisa.” Akaongea Uzo huku ametabasamu lakini Agent hakuwa na la kuongea. “ Unaitwa nani wewe?” Ikabidi ajibaraguze kwa kuuliza.

“The Undercover Agent.” Akajibiwa kifupi.

“Agent Zero.” Akaongeza Uzo. “Unayeaminika na Rais wako wa nchi. Kazi nzuri umefanya, nimekubali sana na nimeshawishika kukubali kwa nini Rais wako anakuamini.” Akatoa pongezi ambazo zilikuwa kama kelele masikioni mwa Agent.

“Nimemaliza kazi yenu. Nakumbuka nina dola kadhaa kwenu. Nazihitaji mapema sana.” Agent aliongea huku anatoa rimoti ndogo na kumpa Uzo. “Hapa ukitaka kumfungua. Mfano nataka kufungua mdomo wake, nabofya hapa.” Akabonyeza na zile pini zikaanza kumtoka mdomoni Idris. Akaelekeza pote ambapo wanataka kumfungua. Na Uzo alionekana kuelewa vema.

“Okay Agent Zero, The Undercover Agent, ahsante kwa msaada wako. Na hii ni zawadi yako.” Uzo akatoa bastola na kumuwekea kichwani Agent.

“Nilikwambia dogo, watakuua na wewe tu.” Maneno yalimtoka Idris kwa sababu tayari alikuwa kafunguliwa mdomo. Maneno hayo yakamfanya Uzo ageuke haraka na kumpiga Idris risasi ya mguu lakini likawa kosa kubwa sana kumuachia Agent kwani aliruka kwa pembeni na kwa kasi yake ya ajabu, akarusha pini zake.

Uzo alipogeeuka amuangalie Agent, alisikia sauti za nzi na vichuma vikigongana na hapohapo bastola yake ikavamiwa na pini za Agent. Akaitupa bastola ile chini na alishuhudia ikiliwa na zile pini huku pini hizohizo zikiongezeka na kuwa nyingi sana.

“Umevunja uaminifu mzee. Kosa kubwa sana umefanya.” Akaongea Agent huku yupo pembeni akimtazama kwa macho ya ghadhabu Uzo.

“Utakufa tu hapahapa, mbwa we.” Uzo akabwata na kisha akawaamuru wanajeshi wake wawili wamvamie Agent nao bila kusita walianza kumwagia risasi Agent ambaye alikuwa akizikwepa kwa sarakasi za haraka na waliposhtuka, risasi zao zilikuwa zimekwisha na ni sauti za nzi ndizo zilisikika kwenye masikio yao. Bunduki zao zikawa mali ya pini za Agent.

Agent akasimama wima na kuwatazama wale watu.

“Tatizo hamnijui, na wala siwajui. Ila hapa mmeingia sehemu mbaya.” Agent aliongea. “Tena mbaya sana.” Akasisitizia kauli yake. “Mmeona hii?” Akafunua mkono wake na kuonesha saa aliyoivaa. Saa hiyo ndio ilikuwa inakontroo zile pini. “Hiyo rimoti si kitu kama una hii. Hii inaweza kufanya yote unayoyafanya kwenye hiyo rimoti. Kwa mfano,” Agent akabofya saa yake na mara Idris akaanza kufunguka kimoja baada ya kingine huku pini zile zikimkimbilia Agent na kuingia kwenye mifuko ya nguo zake.

Wale wanajeshi waliokuja na Uzo, kuona hivyo, wakaanza kumkimbilia Idris lakini walikwishachelewa kwani tayari jamaa alikuwa huru. Ngumi za hatari zikamtoka Idris kwenda kwa wale wanajeshi ambao walipaishwa angani na kudondokea migongo.

“Mmenisaliti mimi, na mmemsaliti Rais wangu. Sivyo tulivyokubaliana. Mkamateni wenyewe, huyo hapo.” Idris alikuwa kama mbogo kwani alikamata kichwa cha mwanajeshi mmoja wa kiume na kuvunja shingo yake na wakati huo Merice naye alinyanyuka na kukaa vema tayari kwa kukabiliana na Idris aliyeonekana hana huruma mbele ya wale wanajeshi wenzake. Uzo akawa hana la kusema na macho yamemtoka kwa wahka pamoja na uoga.

Idris akamsogelea Merice na kumrushia ngumi lakini mwanadada yule aliikataa kwa kumzunguka Idris na kutokea nyuma yake ambapo alimtwanga ngumi nzito ya kisogo.

“Ouuch.” Agent alipiga kelele kwa ngumi ile ya kisogo lakini aliweza kumshudia Idris naye akirusha teke la kinyume nyume na kumtwanga Merice tumboni na kwa pamoja wakawa wanaachiana mmoja akienda mbele na mwingine akirudi kinyumenyume. Ilikuwa ni picha ya kusisimua.

Walipotulia, wakawa wanaangalia kwa macho ya uchu.

“Merice kamata huyo.” Uzo alibwata.

“Kumbe wewe ni Merice? Mwana wa Dokta Ice na Simeria.” Akaongea Idris na kutikisa kichwa chake. Picha zikaanza kumrudia tena kichwani mwake kwa haraka. “Inasemekana ulikufa na mama yako, kumbe upo?” Maneno hayo yakamfanya Idris ashushe mikono yake aliyoiweka kimpambano. Merice akawa katika mshangao. “ Uzo ni mtu mbaya sana, kaua familia yangu yote na baba yako ndio alinileta huku ili anifiche. Baba yako alitulea mimi na wewe kama wanawe. Tafadhali Merice, achana na hii kazi.” Idris akaendelea,

“Muue huyo.” Uzo akabwata tena lakini alipotaka kuongea akafumbwa na mdomo wake na pini za Agent. Akabaki kama bubu anayeomba chakula kingine.

“Acha watu waongee.” Agent aliongea kwa mbwembwe na kukaa juu ya jiwe lake alilokutwa kakaa mwanzoni.

“Dokta Ice alikufa siku mbili mbele ulipotoroshwa. Alijinyonga mwenyewe.” Merice alijikuta akiongea hayo na kumfanya Idris alie sana baada ya kugundua kuwa mtu aliyemlea alikufa kwa sababu yake.

Akamuendea Uzo na kumuinua kwa nguvu zake zote kisha akamrusha na kujibamiza kwenye bodi la scania alilokuja nalo Agent. Na wakati huohuo, ving’ora vya polisi vilianza kusikika kwa mbali vikija eneo lile.

“Ondokeni haraka. Polisi wameruhusiwa kuja hapa, msije mkaleta madhara kwa polisi wetu, nitawaua wote.” Agent aliwaambia Merice na Idris na macho ya Idris yalimuangalia kwa uchu Uzo lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda kwenye daladala ya kipelelezi aliyokuja nayo Uzo, na kisha kuondoka eneo lile akiwa na Merice ndani yake.

Polisi walifika na kumkuta Uzo akijizoa zoa na wakati huo yule mwanajeshi aliyevunjwa shingo alijirekebisha katika hali yake na kusimama tena. Uzo akapata ahueni baada ya kuona ulinzi wake umerudi.

Baada ya polisi kufika, gari nyingine nyeusi ilifika eneo lile na Rais alishuka na moja kwa moja alimuendea Uzo.

“Umemsaliti mwanajeshi wangu. Umetaka kumuua, unataka nini sasa?” Rais alimfokea Uzo na Uzo akatabasamu kisha kwa mbwembwe nyingi akajitapa.

“Mbwa wako hawezi kazi, ilipaswa afe kama wewe.” Akaongea hayo na kujaribu kutaka kumkwida Rais lakini ghafla alisikia sauti za nzi na mara mikono yake ikafungwa kwa pini za Agent.

“Unadhani hii ni nchi yako na unaweza kufanya lolote utakalo?” Sauti ya Agent akiwa palepale kwenye jiwe lake ilisikika na kisha akaviruhusu vile vipini vimuachie.

“Washenzi nyie, hamjui sisi ni wa Marekani eeh’” Maneno hayo yakaenda sambamba na kumuamuru yule mwanajeshi aliyebaki kumteka haraka Rais ambaye alikuwa kasimama mbele yake bila uoga wowote.

Lakini kabla mwanajeshi yule hajasogea hata hatua moja, alijikuta akipokea risasi ya kichwa na risasi ilipofika ndani ya kichwa, ikapasuka na kufanya kichwa cha mwanajeshi yule kivurugike kama tikiti maji lililopigwa ngumi na roboti.

“Hujui kuwa hapa haupo Marekani?” Rais akamuuliza. “Vizuri sana Lisa.” Akampa sifa mtu aliyemtwanga risasi yule mwanajeshi. Anaitwa Lisa, mwanamke mjanja kwenye shirika la siri la kipelelezi la Tanzania.

“Ahsante Mr. President. Msalimie Agent Zero. Nimemaliza kazi yangu.” Sauti ilisikika kwenye simu ya upepo aliyokamata Rais wa nchi.

“Sawa binti yangu.” Akaitikia Rais na kumgeukia Uzo ambaye alikuwa haamini kama mwanajeshi wake kafa kizembe tena kwa silaha za Kitanzania. “Sikiliza nikwambie kijana.” Safari hii aliongea huku yeye ndiye anamfuata Uzo. “Umemsaliti mtu wangu kijinga sana. Tulikubaliana tufike hapa kwa pamoja, lakini wewe ukajidai mjuaji na kufika kabla yetu ili umuue kijana wetu. Unajua tumegharimu kiasi gani kumtengeneza huyu Agent? Unajua wakati tunamtengeneza ni wangapi walifeli na wangapi walifaulu? Unajua watu kama hawa wapo wangapi duniani? Wewe unataka kumuu kirahisi tu!” Uzo alikuwa kimya na mpole kama asomewaye mashitaka. “Sikuhitaji nchini kwangu, ondoka haraka sana. Huyo mwanajeshi unayemtaka, ni Mtanzania.” Rais akamaliza na kugeuka tayari kwa kuondoka.

“Ameondoka na mwanajeshi mmoja niliyekuja naye.” Uzo akaongea na kumfanya Rais ageuke na kumtazama.

“Kwa hiyo.” Akamuuliza.

“Nataka kuondoka na mwanajeshi wangu.” Akatoa wazo Uzo.

“Ruhusa. Kamchukue. Ukitaka beba wote lakini sitaki uwadhuru wananchi wangu wala miundo mbinu yangu na kitu chochote kile cha hapa nchini.” Akaongea Rais.

“Hamna shida. Nitaingiza wanajeshi kadhaa leo hii kwa huu msako.” Uzo akakubaliana na Rais.

“Ukiharibu chochote, nchi yako italipa. Nitawasiliana na Rais wako kuhusu hili.” Uzo akakubali na Rais akaanza kuelekea lilipo gari lake huku nyuma pia, Agent Zero alinyanyuka na kuelekea kwenye lilelile gari.

Uzo akabaki kuwatazama na kiburi chote kikamuisha hasa wanaume wale walivyokuwa wanaondoka na magari waliokuja nayo.

“Kumbe ndio Tanzania hii. Duh! Nimeingia kichwa kichwa hapa.” Akajiwazia.

*****

Idris aliegesha gari lake eneo moja lenye miti mingi na kumwambia Merice ashuke ili waelekee nyumbani kwake. Mwanajeshi yule wa kike, alikubaliana na hilo na moja kwa moja wakaanza kuelekea nyumbani kwa Idris ambapo palikuwa na umbali wa Kilometa zipatazo kumi na tano toka pale walipolitelekeza gari la kipelelezi.

Uzuri walikuwa ni wanajeshi imara ambao hawawezi kuchoka kizembe. Hilo liliwasaidia kufika nyumbani kwa Idris baada ya dakika kumi toka pale walipoliacha gari lao.
 
137.


“Wao kipenzi. Ulikuwa wanipa mashaka sana kwa kimya chako, nini kimekukuta?” Limasi aliongea huku akiwa kamkumbatia Idris ambaye naye alikuwa kamkumbatia.
“Ni historia ndefu, lakini leo utajua kila kitu.” Idris alijibu na kumuita Merice ambaye yeye hakusogea eneo lile hadi pale alipoamuriwa. “Huyu anaitwa Merice. Ni mwenzangu wa kitambo sana. Tutakuhadithia mengi sana leo hii kabla ya kuondoka hapa.” Akaongeza Idris baada ya utambulisho.
“Unaondoka unaenda wapi Honey? Halafu nina habari nzuri kwako.” Limasi aliongea kwa kudeka bila kujali hisia alizokuwa nazo Idris wakati huo.
“Tuingine ndani kwanza.” Idris akapendekeza na wote wakaingia ndani.
ENDELEA.
Habari kubwa iliyozungumzwa humo ndani, ilikuwa ni tukio lililomkuta Idris. Alieleza kitu kama kilivyo. Hakusita kumwambia hali yake iliyosababisha yeye kupona ndani ya ajali ile kubwa na ya kupagawisha yeyote yule.
“Idris. Mbona mimi sikuelewi unachoniambia?” Swali likamtoka Limasi kwa sababu hakuamini lolote lile. Alimuona mume wake yupo sawa na salama kabisa. Hadithi anayompa ilikuwa kama inajambo ndani yake. “Au ndio njia ya kuniacha ili uwe na huyu mzungu wako?” Hatimaye mwanamke wa Kitanzania, alitabainisha hisia zake.
“Hapana Limasi. Embu ngoja nije ili unielewe nachomaanisha.” Idris alisimama na kwenda moja ya chumba kilichiomo mle ndani.
“We are soldiers. Dangerous soldiers. You have to believe your husband. (Sisi ni wanajeshi. Wanajeshi hatari. Unatakiwa kumuamini mumeo)” Aliongea Merice lakini Limasi aliona mapicha picha tu. Akakaa kimya akimsubiri Idris arudi. Na baada ya dakika moja, Idris alirudi akiwa kakamata kisu kirefu na kikali.
Alichofanya baada ya kufika na kisu chake, alivua shati lake na kuanza kujichana kutoka upande wa kushoto wa kifua chake hadi chini ya tumbo upande wa kulia. Pia akajichana upande wa kulia juu, hadi chini upande wa kushoto. Akawa kama kajichora X kwenye mwili wake. Damu zilikuwa zinamchuruzika na Limasi alikuwa anapiga kelele baada ya kuangalia picha ile. Alikuwa amejiziba usoni ili asiendelee kuangalia ile picha ambayo Idris alikuwa anaifanya mbele yake.
“Tazama Lim.” Idris alimwambia Limasi ambaye alitoa mwanya mdogo katikati ya vidole vyake na kuangalia jeraha la Idris. Aliona damu zinaanza kurudi ndani ya kidonda alichojichana na mara ngozi yake ikajifunga vema.
“How this happen? (Inawezaje kutokea hii?)”Akauliza kwa mshangao Limasi huku akiwa ametoa mikono yake usoni.
“Hili ndilo nilikuwa najaribu kukueleza Lim. Tafadhali nielewe sasa. Tupo hatarini, mimi na wewe na huyu dada yangu.” Akaongeza Idris kujibu swali la Limasi.
“Ndio maana siku zile club hukudhurika.” Akaendelea kujiuliza na kujijibu mwenyewe, Limasi.
“Lim. Embu tuachane na hayo, huu si muda wake. Tupo hatarini mke wangu, muda wowote tunavamiwa hapa.” Idris akawa anajaribu kumleta kwenye mada husika Limasi.
“Wakina nani waje kutuvamia?” Limasi akauliza kwa mshangao.
“Kuna wanajeshi zaidi ya mia moja kama sisi. Ni hatari na hawana huruma hata kidogo. Wakiingia humu, hamna atakayesalimika.” Idris akamuwelewesha kwa kifupi.
“Kwa hiyo unataka tufanyaje sasa?” Akauliza Limasi akiwa na kitete.
“Nataka nikuchukue, nikupeleke kwa dada yako sasa hivi halafu tuache sisi tupambane nao.” Idris akajibu.
“Hapana, nitapambana nikiwa na wewe. Ndiyo ahadi niliyoapa.” Akaonesha uanamke wake.
“Hawa hupaswi kupambana nao. Tafadhali Lim. Nielewe, tupo katika hatari kubwa.” Idris akazidi kumuelewesha mke wake ambaye alikuwa anaogopa lakini bado anataka kuwepo.
“Soldier. Go and discuss this on your bedroom. (Mwanajeshi. Nenda na mkajadili hili chumbani kwenu)” Merice ambaye alikuwa hana sura ya kutabasamu, muda wote alikuwa kanuna, alitoa wazo kwa sauti ya kikatili.
Idris akamchukua Limasi na kwenda naye chumbani. Ambacho kiliendelea huko ni kujaribu kumsihi Limasi akubali kuondoka pale haraka sana.
Saa sita usiku. Limasi alikuwa kaelewa alichoelezwa na Idris alitoa mkoba mmoja aliokuwa amehifadhi baadhi ya nyaraka zake za siri zikiwemo nyaraka alizopewa na Dokta Ice, akamkabidhi Limasi.
“Nenda kasome haya. Vyote vilivyomo humo nakukabidhi wewe. Ni muhimu sana. Usije ukavipoteza, sawa mama?” Hakutaka mwanamke yule ajibu, akamvuta na kumchapa busu zito la mahaba. Pia akampa na kompyuta yenye maelezo mengi kuhusu yeye. “Hii pia itakusaidia pale ambapo hujaelewa. Acha sisi tupambane kuwazuia hawa wajinga,” Idris alimaliza na kumpa kompyuta. Akaanza kumvuta Limasi ili warudi sebuleni na kisha kuondoka naye.
“Id.” Limasi akagoma kwenda na kumvuta Idris. Idris akawa anamuangalia kwa lengo la kumsikiliza sababu ya yeye kumvuta. “Nina mimba yako.” Limasi akaongea na Idris akatabasamu na kumkumbatia kwa nguvu Limasi.
“Ahsante kwa hilo mke wangu. Ila hatuna muda. Twende nikupeleke kwa dada yako.” Akaongea Idris na kisha kwenda hadi sebuleni ambapo walimkuta Merice amesimama dirishani huku taa zote zimezimwa.
“Tumechelewa mwanajeshi.” Merice aliongea kwa lugha ya Kiingereza. “Tayari wapo mtaani na wanaingia nyumba hadi nyumba.” Akaongeza na kumfanya Idris aende hadi pale dirishani na kushuhudia wananchi wakitolewa nje na kutishiwa mitutu ya bunduki na wanajeshi wa C.O.D.EX ambao walikuwa wametapakaa kila kona ya mtaa.
“Tunafanyaje sasa?” Akauliza Idris huku akimuhofia zaidi Limasi.
“Huna silaha zozote?” Akauliza Merice kwa lugha ileile ya Kiingereza.
“Twende huku.” Akamchukua Merice na Limasi na kwenda nao hadi katika stoo yake na kisha akasukuma pembeni mashine moja ya kukatia majani, akafunua sehemu moja iliyokuuwa sakafuni. Hapo kulikuwa na uwazi wa pembe nne, na akashauri waingie humo kwani ni handaki. Wote wakaingia na kisha wakafunga kwa kifuniko walichofungulia.
Ndani ya handaki hilo lililopo ndani ya nyumba kubwa na a kifahari, kuliwashwa taa na hapo macho ya Merice na Limasi yakashuhudia mali mbalimbali anazomiliki Idris. Magari ya kifahari pamoja na silaha mbalimbali za kivita, vilionekana ndani ya handaki lile. Kwa kifupi lilikamilika.
“Hapa tunaweza kupambana.” Merice aliongea lakini bila tabasamu kuonesha kuwa kakubali yale anayoyaona.
Idris akaenda hadi chumba kimojawapo na kuwasha runinga za mle ndani ambazo zilionesha nyumba yake nzima kuanzia nje hadi ndani. Pia aliweza kuuona mtaa mzima.
“Wapo karibu kufika hapa. Sitaki kuwalipua kwa sababu ni kazi bure tu. Na hapo unapoona hamna silaha za kuwasimamisha hawa wajinga. Hivyo dawa ni kuwachelewesha kwa mapigo yetu.” Idris aliongea na baada ya hapo. Akaenda kwenye sehemu zilipo silaha na kuanza kuzipanda ndani ya mabegi yaliyopo humo.
Bunduki, mabomu pamoja na visu, vilipangwa humo kwenye mabegi. Naye Merice alikuwa anajichagulia silaha zake na kuzipanga kwenye begi lake. Limasi akawa mtu wa kuangalia tu akiwa haamini anatazama filamu ya Rambo au anaona kitu mubashara bila chenga.
Baada ya kupanga silaha zao za kutosha, wakavaa mavazi mengine ya kijeshi na kisha kwenye mavazi hayo, wakaweka silaha zingine za moto. Kwa kifupi walikuwa wamedhamiria kupambana na jeshi la Uzo ambalo lilishuka usiku huo kwa ajili ya kuwasaka wao.
“Lim. Hawa ndio sisi. Tafadhali, usiwe na wasiwasi, upo salama na utafika salama popote pale.” Aliongea Idris.
“Na kitu ambacho kitakuwa kibaya kwake hata hapo baadae, ni sisi kwenda naye kwa dada yake. Huko kuna polisi na kama hawa majamaa watajaribu kutufuata, hiyo inamaanisha kuwa, tunawaingiza wote matatani.” Merice aliongea mawazo yake.
“Tunafanyaje sasa?” Akauliza Idris.
“Twende sehemu nyingine ili kuwapoteza hawa wajinga. Huko ndipo tutajua la kufanya. Bado na uchungu sana na baba yangu. Licha ya kutokuwa na kumbukumbu, lakini moyo wangu uliniuma sana kwa kile nilichokiona. Damu ilinisisimka kuliko kawaida. Kuna sauti iliniita kabla Dokta hajafa. Na mama yangu ndiye aliyemuua, anatakiwa alipe haya kabla sijafa.” Merice aliongea kwa kisirani na Idris alimfuata pale alipo.
“Nitakuwa nawe katika hili kwa sababu ya Dokta Ice.” Aliungana na Merice nao kwa pamoja wakaunga mikono kuonesha umoja usiokuwa na jina.
“Nina nyumba ipo Moshi. Nadhani Limasi tutamuacha huko, halafu sisi tutapambana na hawa wenzetu kwa njia ya vita.” Akaongeza Idris na kwenda hadi sehemu yenye uzio mkubwa uliopambwa kwa magari ya kifahari. Akachagua jeep moja nyeusi na yenye tairi kubwa. “Nadhani hili litatufaa kwa vita. Ni imara na haliingizi risasi. Twende kuwaonesha kazi wajinga hawa.” Wote wakakwea garini huku Idris akishika usukani na Merice akikaa upande wake wa kushoto na Limasi akikaa nyuma na kufunga mkanda vema tayari kwa kupelekwa Moshi.
Mwanaume akawasha gari na kubonyeza kiruninga kidogo kilichopo kwenye gari lile. Kikaonesha ramani ya wanapokwenda na pia kikaonesha watu waliopo nje. Akaanza kuliendesha gari lake kwa tararibu na alipofika umbali fulani, aliongeza kasi na kubonyeza rimoti moja hivi, mbele yake kukafunguka mlango fulani ambao ulishuka chini na kutengeneza mpandisho ambao Idris aliupanda kwa kasi. Katika hali ya kustaajabisha, alitokea mbele ya geti la nyumba yake. Akawasha taa ‘full’ na kuweza kushuhudia baadhi ya wanajeshi wakiwa mbele yake na mitutu yao kuisimamisha.
Idris bila uoga, akagonga wanajeshi waliokuwa barabarani na kusababisha taharuki kubwa kwa wananchi ambao walikuwa nje wakishangaa ule msako ambao hauna jina. Wanajeshi waliyosalia kwenye ajali ile, walianza kulishambulia gari la Idris lakini hamna walichoambulia kwani lilikuwa haliingizi risasi.
“Twendeni tuwakimbize hawa wajinga. Wanatutoroka.” Uzo alibwata akiwa na nguo za kjeshi la Marekani na wanajeshi wake hata wale waliopamiwa na gari la Idris, walianza kukimbia magari yao na kuyapanda tayari kwa kumfukuzia Idris, ikiwa imetimu saa saba kasoro usiku.
****
Taarifa za wanajeshi wa C.O.D.EX kuvamia makazi ya watu huko Arusha, zikafika hadi kituo kikubwa cha Polisi cha Arusha. Mkuu wa kituo akaamuru haraka polisi wake waende eneo la tukio kwa ajili ya kufanya mahojiano na wananchi waliokumbwa na msala huo.
Polisi walifika nyakati ambazo tayari wale wanajeshi wamekwishaondoka hivyo mahojiano yalikuwa ni kuhusu kile walichofanyiwa na walichokiona. Polisi macho yakawatoka baada ya kuambiwa kuwa kuna wanajeshi ambao hata wakigongwa na magari hawafi. Taarifa hizo za mahojiano, zikafikishwa kwa mkuu na mkuu akawasiliana na Jeshi la Polisi La Tanzania, nalo likapeleka taarifa hizo kwa Amiri Jeshi mkuu ambaye alishangazwa sana tabia aliyofanya Uzo.
“Huyu mbwa nilimkataza huu ujinga. Hanijui eeh, ngoja kwanza.” Akatwaa simu yake ikiwa ni usiku wa mnene. “Wewe unafanya nini eti.” Rais akabwata kwa hasira.
“Nawataka watu wangu.” Akajibu Uzo kwenye simu.
“Nilikwambiaje kuhusu usalama wa watu wangu?”
“Nchi yangu itakulipa.”
“Pumbavu wewe, unaweza kulipa maisha ya watu?”
“Hilo halinihusu. Fanya unaloweza.” Uzo akata simu na kumfanya Rais aitazame ile simu kwa dakika kadhaa akiwa haamini kama kuna watu wanakiburi vile.
“Mshenzi ananikatia simu huyu?’ Akajiuliza akiwa na hasira. “Yaani anaifanya hii nchi kama yake, si ndio eeh. Halafu hajui kuwa anacheza na maisha ya watanzania. Na huyo mwanajeshi kamuoa Mtanzania. Kama wanaye humo wanapotoroka? Si atakufa mwananchi wangu?” Rais akawa anawaza huku anaongea mwenyewe. “Ngoja nimuoneshe.” Akawasha tena simu yake na kuingia sehemu ya majina yaliyomo humo, akabonyeza kitufe cha kupigia. “Haloo Agent. Naona anakiburi yule mtu. Nenda kasaidie kumkomboa Mtanzania mmoja.” Rais akaongea kisha akasikiliza upande wa pili. “Nakutumia sasa hivi muelekeo wao.” Akamaliza maongezi na kukata simu. “Sitakagi ujinga mimi.” Akaongea huku anaelekea chumbani kwake.
****
 
138.


“Hilo halinihusu. Fanya unaloweza.” Uzo akakata simu na kumfanya Rais aitazame ile simu kwa dakika kadhaa akiwa haamini kama kuna watu wanakiburi vile.
“Mshenzi ananikatia simu huyu?’ Akajiuliza akiwa na hasira. “Yaani anaifanya hii nchi kama yake, si ndio eeh. Halafu hajui kuwa anacheza na maisha ya watanzania. Na huyo mwanajeshi kamuoa Mtanzania. Kama wanaye humo wanapotoroka? Si atakufa mwananchi wangu?” Rais akawa anawaza huku anaongea mwenyewe. “Ngoja nimuoneshe.” Akawasha tena simu yake na kuingia sehemu ya majina yaliyomo humo, akabonyeza kitufe cha kupigia. “Haloo Agent. Naona anakiburi yule mtu. Nenda kasaidie kumkomboa Mtanzania mmoja.” Rais akaongea kisha akasikiliza upande wa pili. “Nautumia sasa hivi muelekeo wao.” Akamaliza maongezi na kukata simu. “Sitakagi ujinga mimi.” Akaongea huku anaelekea chumbai kwake.
****
ENDELEA.
Barabara ndefu na ya rami, ilikuwa inakiona cha moto kwa kuandamwa na magari yapatayo kumi ambayo tisa yalikuwa yanalikimbiza gari la Idris, na lingine moja ni Idris mwenyewe. Hali ilichafuka. Mapambano ya kurushiana risasi ndio yalichukua nafasi na yaliendelea kupamba moto muda huo wa saa tisa hadi saa kumi na moja ambapo tayari jua lilionekana likichomoza.
Merice akiwa anatokeza mara kwa mara dirishani kujibu mashambulizi, alionekana kuzidiwa kwa sababu ya wale wanajeshi kutupa vitu vyao mara kwa mara na kwa mbinu za kijeshi.
“Soldier, hapa ni pagumu sana. Wanaweza kutukamata hawa.” Merice aliongea baada ya gari lao kuwekwa katikati kwa kubanwa kushoto na kulia, huku nyuma pia Uzo akiwa anafanya vema kumzuia.
“Hapana. Hawana jipya hawa. Hizi mbinu ni za kizamani sana.” Idris alimpa moyo Merice. “Shika usukani mara moja.” Akamuamuaru Merice na kitendo bila kuchelewa, Merice akakamata usukani na Idris naye akawa anataka kubadilishana nafasi na mwanamke yule wa shoka.
Wakafanikiwa. Dereva akawa Merice na wakati huo Limasi alikuwa anatetemeka kama mwizi aliyeshtukiwa.
Idris akafunga mkanda vema na maajabu ya gari lile, mikanda ipo minne. Mmoja ukafunga kawaida, yaani toka begani hadi upande mwingine wa kiunoni. Mkanda mwingine ukafunga miguu, mwingine kiuno na mwingine kifua. Baada ya kuhakikisha kajifunga vema, akabofya kitufe kimoja kilichopo pembeni ya kiti chake. Ghafka kiti chake kikajipetua kwa kuzunguka. Kule alipokaa Idris kukaenda chini, na chini kukawa juu.
“Idris.” Limasi akapiga kelele kubwa baada ya kushuhudia hali ile lakini hamna alichojibiwa toka kwa Idris ambaye alipotea pale alipokuwepo, na Merice pia hakuongea lolote.
Huko chini, Idris alikuwa anaishuhudia rami lakini hakuigusa kwa sababu ile mikanda aliyojifunga ilimzuia vema na hivyo kuonekana kama aliyelala au mtu anayepaa huku miguu yake kainyoosha na mikono yake kaitanua.
Idris akatazama kushoto na kulia. Akaziona vema tairi za maadui wake. Kwa uangalifu mkubwa aliweza kutoa mabomu ya kisasa kwenye sehemu alizohifadhi. Kisha mabomu hayo akayapachika mbele ya bunduki maalumu kwa ajili ya kufyatulia mabomu hayo ambayo yalionekana kama kifuniko kidogo cha kopo la mafuta ya kupaka. Lakini mabomu hayo, yalikuwa meusi na yalinakishiwa na utepe wa siliva kwa pembeni.
Baada ya kuyapachika mabomu mawili kwenye bunduki ya kufyatulia (Launcher Gun), Idris alianza kulenga tairi la adui wake wa kwanza, alipofanikisha shabaha yake, akafyatua bunduki yake, nalo bomu lile dogo likaenda kunasa kwenye sehemu ambazo wanafunga boliti. Alipofyatua bomu la pili, lilienda kunasa chini ya tanki la mafuta.
Akapachika tena mabomu mengine mawili na kuligeukia gari la upande mwingine. Akafanya tendo lilelile na baada ya kufanikiwa, akabonyeza kitufe kilekile, nacho kikamgeuza haraka na kumleta ndani ya gari na kumkuta mke wake analia.
“Idris, unataka kufanya nini?” Aliongea huku anafuta kamasi, mwanadada Limasi ambaye ghafla tabasamu lilikuja huku bado machozi yanamtoka.
“Nimerudi mamaa, ona kitakachowatokea mbwa hawa.” Idris alijibu huku anamfuta Limasi machozi yake. Limasi akashika mkono wa Idris na kuubusu kwa nguvu. Hakika mapenzi yalikuwa yamemkamata mtoto wa kike.
“Umefanya nini huko chini?” Merice akauliza.
“Nimewategea, ‘magnetic power bombs’” Idris alimjibu Merice kuwa yale mabomu aliyoyatega yanaitwa Mabomu ya Nguvu za Sumaku na ndio maana alipoyatuma, yalikimbilia kunasa kwenye sehemu zenye asili ya chuma.
“Vema.” Merice akajibu na kutazama yale magari yalivyokuwa yanazidi kumbana ili apunguze mwendo. Na kuna nyakati, wanajeshi wa C.O.D.EX walikuwa wakipiga risasi nyingi sana kioo cha gari lao lakini hawakufanikiwa walau kumuona mtu wa ndani kwa sababu ya vioo vile kuwa vyeusi vyote.
“Muda wao wa ngebe umekwisha. Nadhani walio nje, wataona filamu nzuri ya vita kuliko sisi.” Idris aliongea huku akitoa kitu kama peni ya kubonyeza, na kisha akabonyeza sehemu ya juu ya peni ile. Bomo la kwanza kupandwa ndilo lilianza kulipuka, likapasua vibaya tairi la mbele na kusababisha gari lile lipoteze muelekeo. Bomu la pili ambalo lilipandwa kwenye tanki la mafuta, nalo likaitika. Hapo gari lilinyanyuliwa juu na kuzunguka kama mjiti uliyorushwa angani kwa nguvu nyingi sana.
“Hoolly! Shit.” Uzo alifoka ndani ya gari baada ya kuona gari la wanajeshi wake likiranda angani na kisha kutulia pua. Baada ya hapo, ukasikika mlipuko mkubwa toka kwenye gari lile.
Sekunde kadhaa mbele, gari la upande mwingine, nalo lilikumbwa na dhahama ileile. Ambayo imelikumba gari la kwanza. Merice akacheka kwa furaha kwa mara ya kwanza na kumsifu Idris kuwa ni mwanaume wa shoka huku akimsihi Limasi amlinde sana yule mwanaume.
Uzo kuona lile tukio, aliamua kupunguza mwendo wa gari lake na kumfanya Merice alichanganye la kwake na kumuacha umbali mkubwa sana.
“Wajinga hawa, wanatufanya sivyo. Sasa dawa yao ni kufa tu.” Uzo akaongea na wenzake kwenye magari mengine na kisha kwa mtindo wa kipekee, magari matatu yakampita Uzo na kukaa mbele yake, kisha yote matatu yikajitanua yikiwa mwendo sawa lakini mbele kidogo, lile la katikati likaongeza mwendo kiasi na kuwa mbele zaidi. Ikatengenzwa pembe tatu toka kwenye yale magari. Gari la Uzo nalo likasogea mbele kidogo, likiwa usawa wa lile la katikati. Napo kukatengenezwa alama ya pembe nne na wakati huo magari matatu ya nyuma nayo yakajitengeneza kama yale ya mbele lakini ile iliyokuwa katikati, yenyewe ikawa nyuma zaidi. Hivyo gari la Uzo likaonekana lipo katikati na yale mengine yakawa kama yanamlinda.
“Shenzi hawa. Wanatumia ‘Knife style’ kuchinjia kitu kimoja.” Idris aliongea baada ya kuona ule mtindo wa magari alioufanya Uzo ambao ulionekana kama karata ya kisu, na wakati huo tayari ilikwishatimu saa kumi na mbili asubuhi. Jua lilikuwa linaangaza kwa asilimia kubwa.
Uzo na mtindo wake wa karata ya kisu, kwa pamoja wakaongeza kasi ya magari yao ambayo nayo si haba, yalikuwa ni mitindo mipya ya magari ya kijeshi ambayo yaliongezwa vitu vingi sana vya kijeshi. Mwendo wa magari ya Uzo, ulikuwa mkubwa kulikoni ule wa gari la Idris hivyo hawakuchukua muda sana, tayari walikuwa wanalipumulia kwa nyuma Jeep la Idris.
Lile gari la mbele, kwa ustadi mkubwa wa dereva wake, likafunga breki ya mkono (Hand Brake) na kujigeuza, yaani nyuma kukatamazama mbele, na mbele kukatazama walipokuwa wakina Uzo. Na likawa linaenda vivyo hivyo kinyume nyume na wakati huo Mwanajeshi wa C.O.D.EX alifungua mlango wa nyuma na kutoka na silaha ambayo kwa kitaalamu wanaiita RPG.
Kwa huku Watanzania tumezoea kuita silaha ile Kombora. Mwanajeshi kwa haraka, akafyatua kombora lile ambalo mara nyingi hutumia kutungulia ndege au magari magumu ya kivita kama vifaru. Gari la Idris lilinyanyuliwa kwa nyuma kulipuliwa lakini uimara wake, likarudi tena chini huku humo ndani si Limasi wala Merice ambao hawakutoa sauti kali za mshtuko.
“Idris, tukilemaa tunamalizwa sasa.” Merice aliona hali inapotaka kuelekea na Idris akamuangalia mke wake kwa imani, akaona kuwa mwanamke yule atapotea kizembe kwa sababu yake.
“Hapana. Mimi ni mwanajeshi. Hamna atakayekufa.” Idris akawatoa hofu wanawake wale ambao walikwishaanza kukata tamaa.
“Nakupa nafasi wanajeshi. Punguzeni mwendo wa gari lenu, ama la, tunatuma RPG lingine.” Sauti ya Uzo ilisikika toka kwenye spika za gari la Idris lakini hamna hata mmoja aliyejibu.
Kwa haraka Idris akapachika mabomu yake ya sumaku kwenye ile bunduki na kisha akajibetua na huko chini aliweza kuliona gari ambalo lilijigeuza lakini safari hii, likiwa tayari linatembea katika hali ya kawaida. Akatupa mabomu mawili na yote yakaenda kunasa sehemu ya mbele ya gari au boneti kwa lugha inayoeleweka.
Dereva wa gari aliyaona mabomu yale na kwa haraka akabonyeza kitufe fulani kilichokuwa karibu na redio ya gari. Boneti ile ikawa ya plastiki na kufanya mabomu yale yatereze na kudondoka.
“Huwezi fanikiwa hilo soldier. Mabomu yake hayajanasa safari hii.” Sauti ilisikika baada ya Idris kurudi ndani na aliponyeza ile peni, yale mabomu hayakulipuka kwa sababu yalikuwa hayajanasa kwenye chuma chochote.
“Hali ni tete Merice, bomu linalofuata nadhani linatuzungusha hewani.” Idris kwa mara ya kwanza alionesha kukata tamaa.
“Nakupa dakika moja ya kusimamisha gari lenu wanajeshi,” Uzo akasikika tena na si Merice wala Idris ambaye hakuwa akitokwa na jasho ukiachana na Limasi ambaye alikuwa analia kama mtoto mdogo. “Bado sekunde thelathini.” Uzo akaongea tena na hilo likawafanya Merice na Idris kuangalia wakitaka kufanya shauri la mwisho.
Idris alivyoona kama anaweza kuzidiwa, haraka alifungua mikanda ya siti za kiti na kujitupia siti ya nyuma ambapo alikuwepo Limasi. Akachomoa bunduki yake ambayo ilikuwa na uwezo wa kutoa risasi kwa juu na chini yake mabomu, wanaziita M-16 bunduki hizo. Akaiweka kwenye usawa kioo cha nyuma ya gari lile.
“Fungua mlango wa nyuma Merice. “Alibwata Idris na wakati huo gari la mbele la maadui zake, lilifanya tendo lilelile na mlango wa nyuma ulifunguliwa na yule bwana mwenye kombora alionekana kalikamata tayari kwa kuliachia lakini kwa bahati mbaya alichelewa kuliachia kwani Idris alikwishaachia lake mapema na kumkuta kifuani yule bwana. Likamrudisha ndani na kwa bahati mbaya bwana yule akadondokea mgongo na kombora alilokamata, likafyatuka na kumpiga dereva wa gari lile na kumtolea dirishani huku lile bomu alilopigwa kifuani, nalo likilipuka na kupoteza kabisa muelekeo wa gari.
“Mmekosea sana.” Uzo aliongea na lile gari la nyuma likatoka lilipo na kuchukua nafasi ya lile lililopoteza muelekeo. Idris akawa hana jinsi, mbinu zake zote zilikuwa zimetumika na sasa alikuwa anasubiri litakalotokea tu!
Akamuangalia mpenzi wake na kumkumbatia kwa nguvu na wakati huohuo, lile gari lililochukua nafasi ya lile lililopoteza muelekeo, lilikuwa linajigeuza na watu wawili wenye makombora walijitokeza tayari kwa kufyatua makombora yao.
Lakini kabla hawajafanikiwa kufanya hivyo, masikioni mwao walisikia sauti zinazofanana na nzi na vyumavyuma fulani ambavyo kama vilikuwa vinagongana. Hawakujua ni vitu gani, lakini mambo yalibadilika ndani ya sekunde chache baada ya kusikika sauti hiyo.
ITAENDELEA.
 
139.


“Mmekosea sana.” Uzo aliongea na lile gari la nyuma likatoka lilipo na kuchukua nafasi ya lile lililopoteza muelekeo. Idris akawa hana jinsi, mbinu zake zote zilikuwa zimetumika na sasa alikuwa anasubiri litakalotokea tu! Akamuangalia mpenzi wake na kumkumbatia kwa nuvu na wakati huohuo, lile gari lililochukua nafasi ya lile lililopoteza muelekeo, lilikuwa linajigeuza na watu wawili wenye kombora walijitokeza tayari kwa kufyatua makombora yao.
Lakini kabla hawajafanikiwa kufanya hivyo, masikioni mwao walisikia sauti zinazofanana na nzi na vyumavyuma fulani ambavyo kama vilikuwa vinagongana. Hawakujua ni vitu gani, lakini mambo yalibadilika ndani ya sekunde chache ya kusikika sauti hiyo.
ENDELEA.
Kwa hali ya kushangaza, wale wanajeshi walijikuta wanafungwa mikono yao iliyokamata makombora. Hawakuweza kufyatua wala kufanya lolote. Mikono yao ilikuwa migumu kufanya tendo hilo. Pini za Agent ambaye bado alikuwa hajaonekana, ziliwabana vilivyo kwenye vidole vyao pamoja na sehemu ya kuvalia saa. Na kibaya zaidi, pini zile zikaanza kuwavuta waingie ndani na makombora yao. Hawakuamini kinachowatokea katika maswala yao.
“Mbona sioni matokeo?” Alibwata Uzo.
“Kuna vichuma vimetukamata mikononi.” Alijibu mwanajeshi mmoja huku akijaribu kukataza mikono yake isizunguke na kuelekea upande wa dereva lakini haikuwa hivyo. Mwisho wake ulikuwa ni kumlenga dereva upande wa mgongoni na kisha pini zile zikalazimisha kubonyeza kifyatulio. Kombora likachomoka na kumtoa dereva kupitia kioo ambacho kilipasuka vibaya. Uzo akashuhudia dereva wa gari lililokuwa mbele yake akija na kutua kwenye boneti. Akiwa haelewi kinachoendelea, mara yule mwanajeshi mwingine naye alianza kulenga gari la uzo na kufyatua kombora ambalo kwa haraka, Uzo alipindisha gari lake na kombora lile likapita pembeni huku gari la wahusika wenye makombora, likipoteza njia na kwenda kupindukia pembeni ya barabara na kulipuka vibaya kwa sababu lilikuwa kwenye mwendo wa kasi.
“Nini kinatokea tena? Mbona wanapoteza muelekeo wenyewe?” Akauliza Merice na swali hilo likamfanya Idris amuachie Limasi na kutazama kilichotokea. Hata yeye hakuamini hali ile. Akajikuta anatabasamu peke yake.
“Sijui ni nini kinatokea lakini ni afadhali maana haya magari mawili yaliyopinduka ndio silaha kubwa ya mtindo ule wa kisu, kwa hiyo kwa sasa, tunaweza kupambana na hawa wengine.” Idris aliongea kwa furaha.
Wakati hayo yanajiri ndani ya gari la Idris, Uzo alikuwa mwenye kiwewe kikubwa akiwa hafahamu ni nini ambachoo kinatokea kwenye nyakati zile ambazo alikuwa karibu sana kuwakamata wanajeshi wake.
Akiwa katika hali hiyo ya taharuki, mara vumbi zito likaanza kuonekana pembeni ya barabara ile ya rami. Uzo akatazama vema. Na vumbi lilipotulia, aliweza kuona ndege kubwa ya kivita, pembeni imeandikwa Jet P112 FISSA, na kisha mlango wake wa nyuma ulifunguka na katika hali ya kupendeza, pikipiki kubwa ilichomoka ndani ya ndege ile na kutua ardhini hadi cheche kuonekana japo jua tayari lilikuwa limechukua nafasi yake kwa kiasi kikubwa.
Ndege iliondoka kwa kasi na kuacha pikipiki ile ambayo ilikuwa inaendeshwa na mtu aliyekuwa katika mavazi meusi na kichwani kwake kavaa kofia ya pikipiki, ikiwa rangi hiyohiyo nyeusi, ikiingia barabarani kwa mbwembwe nyingi sana.
Mtu yule alisogeza pikipiki yake hadi mbele ya gari la Uzo ambaye kwa wakati huo alikuwa mbele kuliko wale wenzake. Na mbele kabisa alikuwepo Idris na kundi lake, hivyo bwana mwenye pikipiki yeye alikuwa katikati ya Uzo na Idris.
Mwenye pikipiki akageuka nyuma na kulitazama gari la Uzo, kisha akafungua kioo cha kofia ya pikipiki. Macho yake yakakutana na Uzo ambaye alirudisha haraka mgongo wake kwenye kiti alichokalia.
“Agent Zero.” Maneno yakamtoka na ni kama yalisikika kwa Agent Zero, kijana tegemezi wa Rais wa Tanzania. Akafunga kioo cha kofia yake baada ya maneno ya Uzo, na kisha akanyoosha mkono wake kuelekea gari la Uzo. Uzo alipotazama mkono wa Agent Zero, aliona kidole kikubwa kikimtazama. Akachoka zaidi.
****
“Ni The Undercover Agent huyu.” Aliongea Idris baada ya kuona pikipiki ile. Japo hakuona sura, ila alikuwa kalikariri vema umbo la Agent Zerio.
“Ndiye nani huyo?” Aliuliza Merice.
“Ni yule jamaa aliyenikamata kule barabarani.” Idris akajibu. “Jamaa kama si mtu aisee, sijawahi kupambana na binadamu mbishi kama huyu.” Akaongeza.
“Ahaa! Ni yule mshenzi?” Akauliza tena kwa nyodo, Merice.
“Naona safari hii kaja kutusaidia maana ndiye aliyewasambaratisha hawa wajinga. Anasayansi za ajabu sana. Sijamuelewa hadi sasa hivi.” Akasifia Idris na wakati huo Agent Zero alichanganyia pikipiki yake hadi upande wa kushoto wa gari la Idris na kisha akafungua kioo cha kofia yake na kugonga kioo cha sehemu aliyokaa Idris. Idris akafungua kioo hicho.
“Nasikia kuna Mtanzania humu kwenye gari lenu.” Ndilo swali la kwanza ambalo aliuliza Agent Zero kwa sauti ya juu ili asikike sababu upepo ulikuwa mkali.
“Ndio. Ni mke wangu.” Akajibu Idris.
“Shukuruni MUNGU amewaokoa.” Agent Zero akafunga kioo cha kofia yake na kupunguza mwendo ambapo gari la Idris likatangulia na Agent Zero akageuza haraka pikipiki yake na sasa akawa anawatazama Uzo na jeshi lake ambapo gari tano ndizo zilibakia.
Mtindo wake uleule wa kutupa pini, ndio alioutumia na pini zile zikaenda kwenye vioo vya magari matatu na kunata hapo. Agent kwa haraka akageuza pikipiki yake na kisha akabofya saa yake ambayo ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuendesha zile pini, vioo vyao vya mbele vikapasuka vibaya mno. Na wakati huohuo, alirusha pini zingine nazo zikaenda kunasa kwenye mikono ya madereva. Akabofya saa yake kama kawaida, na pini zile zikalazimisha kupindisha usukani wa magari yao. Yakagongana gongana na kuwa mtafaruku mwingine mkubwa sana.
Idris ambaye alikuwa anachungulia shughuli ya Agent Zero, aliweza kuona mtafaruku ule na kwa kusaidia tu, alimrushia Agent Zero mabomu ya sumaku pamoja na bunduki yake ambavyo vilikuwa vinaelekea pembeni kabisa, yaani vilikuwa haviendi kwa Agent Zero lakini Agent yule, alituma pini zake na vifaa vile vikavutwa hadi mkononi kwake.
Akatupa mabomu yale mawili na Idris naye akabofya peni yake. Mlipuko mzito ukatokea eneo lile ukiacha magari ya wanajeshi wa Uzo yakipaishwa angani kama ndege inayopaa.
“Simamisha magari.” Uzo alifoka kwa kiwewe baada ya kushuhudia hali ile. Magari yakasimama likiwepo na la kwake. Kutahamaki, yalikuwa yamebaki mawili tu. Lake na la wanajeshi ambao walikuwa watano kati ya wengi aliowaagiza waje Tanzania. “Watatumaliza hawa. Huyu Agent wao si mzui. Anahitajika kupotezwa au tumsikilize Rais wao anataka nini.” Akaongea Uzo.
Pikipiki ya Agent Zero ikaendelea na safari ikiwa inatoa ulinzi mkubwa wa gari la Idris ambalo lilikuwa linaelekea Moshi kwenye nyumba yake nyingine.
****
“Samahani mkuu, nimekukosea sana. Mtu wako kaja kutuharibia kazi ambayo tulianza kufanikiwa.” Uzo aliongea kwenye simu.
“Nilikwambia sitaki uwadhuru Watanzania wangu, lakini ukakjidai nunda. Unajua kwenye gari kuna Mtanzania mle? Mke wa Idris?” Rais akafoka.
“Sikujua mkuu. Naomba unisamehe.” Akaongea Uzo kwa huruma.
“Sikutaki nchini kwangu. Ukijidai mjuaji tu, namtuma huyo mwanaume aje akufanyie uchafu. Huwa hakosei kazi.” Akatishia Rais.
“Tutaondoka lakini ukiniahidi kitu kimoja.” Akatoa pendekezo Uzo na Rais akawa tayari kumsikiliza.
“Nataka utuletee hawa wanajeshi wetu Marekani. Vinginevyo, tutashusha C.O.D.EX wote nchini kwako, tuone kama huyo Agent atapambana mikoa yote.” Bado kiburi alikuwa nacho Uzo.
“Usinitishe. Nina jeshi lenye roho mbaya kama simba mwenye njaa. Lakini sitaki tu! Ondoka nchini kwangu na wanajeshi wako utakutana nao huko kwenu.” Rais akakata simu baada ya maneno hayo. Uzo akashusha pumzi ya nguvu.
****
Gari la Idris lilifika Moshi mapema na hawakupata tena vikwazo vya wale wanajeshi wa Uzo ambao walionekana wazoefu kwenye kazi zao za kupambana. Agent Zero ambaye naye alikuwepo kwenye msafara ule, aliingiza pikipiki yake ndani ya geti la nyumba ya Idris na kisha kushuka kumuangalia Limasi ambaye ndiye Mtanzania aliyemfanya aingilie ule ugomvi kwa mara ya pili.
“Upo sawa dada?” Akauliza Agent Zero.
“Nipo vema. Ahsante kwa msaada wako.” Limasi alishukuru.
“Ni kazi yangu. Yatupasa tuondoke hapa haraka sana kabla ya wanajeshi wa yule bwana kuja tena.” Aliongea Agent Zero.
“Hapana.” Limasi aliongea kwa sauti ya juu kidogo na kumfanya Idris naye asogee eneo la tukio. “Siwezi kuondoka bila kujua usalama wa mume wangu.” Akaongeza.
“Hawa ni wanajeshi hatari kupata tokea duniani. Wanaweza kuungua na kujirudi vilevile. Wanaakili nyingi na uwezo mkubwa wa kupambana na kitu chochote. Huna haja ya kuwa na wasiwasi hivyo.” Agent Zero alimuweka sawa kiakili, Limasi.
“Hata kama. Lakini mume wangu si mmoja wa wanajeshi hao hatari. Ni mpole na muelewa. Hana hizo sifa unazozitaja.” Limasi alimuambia Agent Zero huku Idris akiwa makini kupata hili na lile.
“Unakosea sana mwanadada.” Akaongea Merice huku naye anasogea eneo la tukio. “Mmeo si kama unavyodhani. Kaundwa kwa njia za tofauti sana na sisi. Sisi uwezo wetu si kama wa mumeo. Huyu ni hatari kuliko sisi. Sisi ni jeshi lingine la maangamizi lakini huyu, ni jeshi moja la kipekee. La ukombozi na pia maangamizi. Baba yangu alimuunda kitaalamu sana. Kuna wanajeshi wengine ambao hata mmoja hajaja huku, hao ndio wanaoweza kupambana na huyu mumeo.” Merice akaongeza.
“Embu twendeni ndani kwanza maana hapa naona mnaanza kunichanganya.” Idris aliweka wazi hasa baada ya yale maongezi ambayo yalikuwa yanamuhusu yeye kwa asilimia kubwa. Wote wakaingia ndani na kuanza kuongea mengi juu ya wao.
****
“Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa nina uwezo mkubwa kuliko nyie?” Baada ya maongezi marefu, Idris aliuliza swali hilo kwenda kwa Merice.
“Ndio.” Akakubali lile swali. Kuna video iliachwa na Baba yangu, nadhani kuwatisha wakina Uzo, inaonesha uwezo wako. Na nilishangaa sana kukutwa umekamatwa na huyu kijinga vile.” Merice aliongea.
“Huyo hawamuwezi wanajeshi wenu tu! Hapa kwangu ni mchuzi.” Agent Zero akaongea kwa dharau.
“Umekosea. Idris angekuwa anajitambua yeye ni nani, wewe ungekuwa maiti.” Merice akajibu nyodo za Zero.
“Unataka kusema kuwa jamaa hajitambui?” Agent akauliza huku ametabasamu. Idris naye akamuangalia Merice kuonesha kuwa naye anataka jibu la swali hilo.
“Hajitambui uwezo wake. Labda tumuulize tu, tangu aje Tanzania, kafanya jitihada gani kujua nguvu zake na uwezo wake? Huyu kapachikwa hadi chipu ya kuweza kubadilisha lugha, kawekewa chipu ya kujua mapigo ya mapambano, anachipu ya kujilinda mwenyewe, anachipu ya kuruhusu mabomu ya nyuklia kulipuka na anachipu ya kumbukumbu na huruma. Mimi nina chipu ya lugha, mapigo na ukatili pekee.” Merice akawatazama wenzake ambao walikuwa kimya.
“Ni kweli asemacho. Sijawahi kufanya majaribio yoyote juu ya nilichonacho mwilini. Ila nakumbuka, niliweza kujua haraka kucheza muziki wa kileo, kufanya mapenzi kwa mitindo tofauti tofauti, na mambo mengine ya kidunia. Nilijua haraka sana.” Kauli hiyo ikamfanya Agent Zero acheke kidogo.
“Unacheka nini?” Akauliza Limasi.
“Hamna dada yangu. Ila kaniacha hoi hapo kwenye kufanya mapenzi kwa mitindo mbalimbali. Kwa hiyo hata ile staili ya…..” Hakumaliza kauli yake, Limasi akampiga ngumi ya mbavu. “Auwuu!” Sauti ya kuumia ikamtoka Agent Zero. “Vipi mbona wanipiga lingumi?” Badala ya Limasi kujibu, akaweka kidole chake kwenye midomo yake akimaanisha akae kimya.
 
140.


“Ni kweli asemacho. Sijawahi kufanya majaribio yoyote juu ya nilichonacho mwilini. Ila nakumbuka, niliweza kujua haraka kucheza muziki wa kileo, kufanya mapenzi kwa mitindo tofauti tofauti, na mambo mengine ya kidunia. Nilijua haraka sana.” Kauli hiyo ikamfanya Agent Zero acheke kidogo.
“Unacheka nini?” Akauliza Limasi.
“Hamna dada yangu. Ila kaniacha hoi hapo kwenye kufanya mapenzi kwa mitindo mbalimbali. Kwa hiyo hata ile staili ya…..” Hakumaliza kauli yake, Limasi akampiga ngumi ya mbavu. “Auwuu!” Sauti ya kuumia ikamtoka Agent Zero. “Vipi mbona wanipiga lingumi?” Badala ya Limasi kujibu, akaweka kidole chake kwenye midomo yake akimaanisha akae kimya.
ENDELEA.
“Sikilizeni.” Merice akawatoa wale Watanzania kwenye hali yao na wote wakawa tayari kumsikiliza. “Dada hapo, utaondoka na kaka yako. Tuache sisi tupambane. Huo ndio usalama wako. Leo hii hii yakupasa uondoke.” Merice akaweka wazo lake mezani.
“Upo sahihi mwanadada. Huyu naondoka naye sasa hivi. Mi’ nawaacha na majitu yenu.” Akaongeza Agent Zero.
“Kweli Lim. Usalama ni mdogo sana kwako. Naomba uende penye usalama. Ila hayo niliyokupa, kayafanyie kazi.” Idris naye akaongeza na mara simu ya Agent Zero ikaita. Akaichomoa na kuanza kuongea na upande wa pili.
“Yupo salama, mkuu.” Akajibu na kusikiliza upande wa pili wa mpiga simu. “Ndio, nipo nao hapa.” Akaongeza tena na kisha akampa simu Limasi.
“Sawa mkuu. Tumekubaliana kuwa nirudi.” Akaongea Limasi na kusikia upande wa pili utakachomwambia. Na baada ya majibizano hayo, akampa simu Idris.
“Sawa Mkuu. Tutafanya hivyo.” Ndilo jibu alilolitoa Idris baada ya dakika zipatazo tatu za kuisikiliza simu ile upande wa pili unachoongea. Simu ikakatwa na Idris akamtazama Limasi na kisha Merice. “Uzo na jeshi lake wametaka sisi turudishwe Marekani. Na Rais kakubaliana na hilo kwa sababu hapa tunawaletea matatizo wananchi wake.” Idris akaanza kuweka bayana aliyoongea na Mkuu wa Nchi.
“Yupo sahihi. Lakini huko tunapoenda, hawawezi kutukamata kirahisi?” Merice akauliza.
“Kasema atatusaidia kuingia Marekani bila Uzo kujua. Najua ananjia nyingi, atafanya hivyo na hawezi kutusaliti. Na kasema baada ya sisi kuingia Marekani tumtaarifu ili awape taarifa wakina Uzo kuwa tumeingia. Anataka watutafute wenyewe na si kutupeleka kirahisi rahisi tu.” Idris akamfanya Merice ameze mate kwa maneno hayo. Ahueni ikamkumba.
“Hapo sawa. Tutapanga cha kufanya tukiingia huko.” Merice aliongeza na wakati huo Agent aliinuka na kuanza kuitamaza ile nyumba kwa makini. Hakuna ambaye alimtilia maanani kwa sababu akili za wote mle zilikuwa zipo katika mawazo ya kurudi Marekani.
Agent akiwa anatazama huku na huko na kushindwa kuelewa muundo wa nyumba ile, alienda hadi sehemu ambapo kuna kabati kubwa la vitabu. Akalitazama kwa muda huku anasoma kitabu kimoja baada ya kingine. Mara macho yake yakatua kwenye kitabu kimoja ambacho kilifanya macho yake yakitazame kwa muda mrefu kabla hajawageukia wenzake.
“We’ Idris, umesema unaitwa nani jina lako lote?” Akauliza kwa wahka Agent Zero.
“Idris Iris. Kuna nini?” Idris akajibu huku wote wakiinuka na kwenda pale ambapo Agent kasimama.
“Hii ni nyumba ya nani?” Akauliza tena Agent baada ya wote kufika pale alipo.
“Ni ya Dokta Ice. Anayo hii na ile ya Arusha.” Akajibu na Agent Zero akamuonesha kile kitabu kilichomfanya aulize jina lote la Idris.
Idris naye akasogea akiwa kama haamini kile akionacho. Kitabu alichokuwa anakitazama, kilikuwa kinamaandishi makubwa yanayosomeka ‘IDRIS IRIS’.
“Ni nini hii?” Akauliza huku anasogea kwenye kabati na kutaka kukichomoa kile kitabu na hapo ndipo maajabu ya nyumba ile yakaonekana.
Nyumba yote ikafungwa vioo vyake na kuwa giza totoro. Na baada ya hali hiyo, wakaanza kusikia sauti za vitu kujivuta na baadaye kwenye kuta za nyumba zile, zikatokea kompyuta nne na kwa chini yake kulikuwa na majokofu manne. Yaani kila jokofu moja lilikuwa na kompyuta moja. Na vyote vilikuwa vinatoa mwanga mkali kiasi.
Baada ya majokofu na kompyuta zile kusogea na kutulia, kwenye ukuta mwingine, ikatokea runinga kubwa na kujiwasha yenyewe na kisha Dojta Ice alionekana na kuanza kuongea mambo ambayo hapo mwanzo Idris hakuwa na taarifa nayo.
“Idris. Huyu ni wewe. Nimekutengeza kwa lengo jema na si kwa malengo mabaya kama wale wa mwanzo niliyowatengeneza. Sikukupa taarifa za jinsi ya kuutumia uwezo wako lakini hapa, ndipo utaanza kujua uwezo wako ambao si rahisi wewe kuujua.” Alianza hivyo Dokta Ice na wakati huo, wote walikuwa kimya kumsikiliza. “Hayo majokofu unayoyaona, ndio uwezo wako na nguvu zako. Utakapoingia humo, tayari utakuwa unachaji nguvu zako na tayari kuzitumia dhidi ya wabadhilifu wa dunia hii. Naamini wewe ni mwanajeshi imara, na haya majokofu nimeyaunda kwa ajili yako wewe tu! Nilijua ipo siku utafika huku. Naomba utumie nguvu utakazozipata katika jema.” Dokta Ice aliongea hayo machache na kisha runinga ile ikaanza kuonesha jinsi majokofu yale yanavyoweza kufanya kazi ili kumpa Idris nguvu alizoumbwa nazo. Baada ya dakika kadhaa, video ikaisha na taa nyeupe zikawaka na mle ndani pakawa mfano wa Maabara kubwa sana ya kufanyia sayansi.
“Nimepapenda humu.” Agent Zero aliongea huku katabasamu.
“Patakuwa pako kama utatusaidia mambo tunayoyataka.” Agent Zero akatoa macho baada ya kauli ya Idris. Agent anamapenzi makubwa sana na ya Sayansi. Hivyo kwa muonekano ule wa ile nyumba, tayari moyo wake uliingia tamaa ya kutaka kumiliki mambo kama yale.
“Ni ndoto zangu kumiliki kitu kama hichi. Nipo tayari kuwasaidia kama kitakuwa ndani ya uwezo wangu.” Agent Zero akajibu kwa furaha.
“Utaweza tu. Nimeona silaha zako za Kisayansi. Najua utafanya vema kuweza kututengenezea zetu zitakazo tusaidia huko.” Idris hakukwepesha kumpa alichokiwaza.
“Hilo tu! Halina shida. Nitafanya kazi yako kwa sababu nina kila kitu hapa.” Agent aliongea kwa furaha.
“Kazi ianze mara moja. Zima na simu yako. Nataka haya yafanyike ndani ya siku hizi na yawe yamekamilika.” Idris aliongea na Agent Zero akakubali kufanya alichoambiwa.
Cha kwanza alichukua damu za Merice na Idris, kisha akawaruhusu watoke ndani ya maabara ile ili afanye kazi yake bila bugudha. Wakatoka mle ndani na cha kushangaza, badala ya kutokea chumba kingine, wakajikuta kwenye sebule ambalo waliingia mwanzo na kujadiliana mambo kadhaa na lile kabati waliliona lakini bila kitabu kilichoandikwa IDRIS IRIS.
“Dokta hakuwa mtu wa mchezo mchezo.” Idris akaongea huku ametabasamu.
“Ni baba yangu.” Merice naye akajibu akilazimisha tabasamu limtokee. Limasi akaamua umvute Idris na kumuacha Merice peke yake. Wivu ulimuingia ghafla. Wakaenda chumba kingine na kuanza kuongea mambo kadha wa kadha na wakati huo, Merice alitoka nje na kuanza kuikagua nyumba ile kuona kama kutakuwa na jipya lolote kwa sababu baba yake, alikuwa ni mtaalamu si kitoto. Yawezekana akagundua lolote lakini haikuwa rahisi kwake kung’amua hilo.
Usiku uliingia. Agent Zero aliweza kutoka na kupata chakula na kuwapa matokeo kidogo huku akiwaahidi kuwa atafanikiwa japo kazi yake ilikuwa ngumu sana.
Idris na Limasi, walienda kulala kwa pamoja huku Merice akilala chumba kingine na wakati huo, Agent Zero, Kijana ambaye yupo ladhi kukesha kwa sababu ya Sayansi, aliingia maabara na kuendelea kufanya kazi ambayo kapewa.
*****
Ndani ya siku tatu, Rais hakupata mawasiliano yoyote toka kwa kijana wake. Wasiwasi ulimuingia na wakati huohuo, CIA na Uzo, walikuwa wanamuulizia kuhusu wanajeshi wao. Rais alikuwa hana jibu la uhakika na wakati huo alikuwa makini sana kutowapa taarifa kuwa kijana wake kapotea kwani wakina Uzo wangekuja na kufanya vurugu.
“Huyu kijana wamemteka nini? Maana hawa wanajeshi siwaelewi hata kidogo. Simu yake haipatikani na wala haoekani kwenye satelaiti yetu. Nini kimempata?.” Akajiuliza Rais huku akikaa kwenye kiti cha ofisini kwake. Mawazo tele yakamjaa. Amekwishatuma wapelelezi kibao waende Moshi kumtafuta lakini hamna aliyemuona yeye na hata wale wanajeshi wa C.O.D.EX. “Asije akanifanya nikamuita The Last.” Akajionya.
Wakati Rais anawaza hayo, Agent Zero alikuwa amejawa na furaha baada ya kukamilisha kazi aliyoombwa na Idris. Aliwaita kwenye maabara na wote walifika akiwemo Limasi. Wote kwa pamoja walishangaa kukuta ambacho Agent Zero kakifanya.
Waliweza kuziona nguo zikiwa kwenye chumba cha kioo na nguo hizo zilikuwa ni za kike na za kiume. Pia mezani kulikuwa na bunduki pamoja na risasi zilizokuwa na kimiminika ndani yake. Waliona mabadiliko makubwa ndani ya maabara ile. Walikuwa hawaamini kama kazi ile kaifanya mtu mmoja.
“Sasa wazee, hizi ni silaha zenu.” Akawaonesha bunduki mbili pamoja na risasi zake. Vilikuwa mezani. “Risasi hii moja, inaweza kukuua wewe, na kukuharibu kabisa. Hunyanyuki. Ni mchanganyiko wa kemikali zilizowatengeneza na kemikali zingine ambazo ukizichanganya kwa pamoja, unatengeneza kifo. Yaani kemikali zenu, zikichanganywa na kemikali fulani, zinatengeneza mlipuko mkubwa sana. Ndicho nilichoweka humo.” Akaeleza kwa kifupi na kuchukua risasi moja ambayo ilikuwa inaonekana kama inamaji ndani yake. Akaitikisa na maji yale yakabadilika na kuwa mekundu. “Hapa ukimtungua mwanajeshi mmoja, akinyanyuka, njoo uchukue nyumba yako.” Akaongea na kuitikisa tena, ikawa ya blue. “Hapa anaweza kunyanyuka, lakini anakuwa hana uwezo wa CODEX tena. Itategemea umempiga wapi. Hayo ndio matumizi yake.” Akamaliza kwenye upande wa risasi. Akabonyeza kiparaza cha kompyuta iliyokuwepo mezani, na meza ile ikafunguka mitoto (droo) yake ambayo ilikuwa kumi. Kila mtoto wa meza ile, ulikuwa unaboksi la risasi nyingi sana pamoja na mabomu ambayo nayo alielezea madhara yake kwa watu wanaoenda kupambana nao.
Pia kulikuwa na visu na silaha nyingi za kivita ambazo wakina Idris, walikubali kuwa kazi yao itaenda kuwa rahisi.
“Hapa ndipo napopataka sasa.” Akaongea Agent huku anaelekea kwenye kabati moja la kioo ambalo lilikuwa na nguo alizoziunda. “Hizi ni nguo ziwezazo kuwasaidia sana katika mapambano yenu. Haziingizi moto, risasi wala haudhuriki kwa njia yoyote labda kwa hizo risasi ambapo napo, ni lazima mpigaji wa risasi akumendee.” Akaelezea kidogo na kubonyeza vitufe vya kompyuta iliyombele ya nguo mojawapo. Suti ile ikasogea mbele.
“Hii inauwezo wa kuhisi hatari inayokufuata na kuizuia. Yaani kama kuna risasi, basi yenyewe inageuka kuwa chuma na kuzia risasi hiyo. Pia kama kuna moto unakuwakia, inaweza kuuizima bila shida. Inaulinzi madhubuti na inaweza kugeuka parachuti kwa wale wa angani. Yaani unaweza kuifanya itokee mabawa na hiyo kukusaidia kushuka hadi sehemu unayoitaka. Kwa kifupi, inavitu vingi ambavyo vinaongozwa na hii saa.”Akawaonesha saa ambayo ilikuwa kwenye ya suti ile rangi nyeusi.” Si Idris wala Merice ambao hawakufurahia uwezo wa Agent Zero.
“Baada ya hili, naomba niwashe simu ili kumtaarifu Rais wangu uzima wangu.” Akaongea Agent na kuwasha simu na kuanza kuongea na Rais ambaye alishukuru kwa kijana wake kuwa salama na wakati huo, alimpa maelekezo kuwa anatakiwa kuiandaaa ndege maalumu kwa ajili ya kuingia Marekani na si ndege ya abiria. Hilo likapita na Rais akamwambia Jet P112 itakuja kuwabeba hapo Moshi na kuwapeleka hadi Dar es Salaam kabla ya Limasi kupelekwa Arusha kwa dada yake. Wote wakakubali.
 
141.


“Hapa ndipo napopataka sasa.” Akaongea Agent huku anaelekea kwenye kabati moja la kioo ambalo lilikuwa na nguo alizoziunda. “Hizi ni nguo ziwezazo kuwasaidia sana katika mapambano yenu. Haziingizi moto, risasi wala haudhuriki kwa njia yoyote labda kwa hizo risasi ambapo napo, ni lazima mpigaji wa risasi akumendee.” Akaelezea kidogo na kubonyeza vitufe vya kompyuta iliyombele ya nguo mojawapo. Suti ile ikasogea mbele. “Hii inauwezo wa kuhisi hatari inayokufuata na kuizuia. Yaani kama kuna risasi, basi yenyewe inageuka kuwa chuma na kuzia risasi hiyo. Pia kama kuna moto unakuwakia, inaweza kuuizima bila shida. Inaulinzi madhubuti na inaweza kugeuka parachuti kwa wale wa angani. Yaani unaweza kuifanya itokee mabawa na hiyo kukusaidia kushuka hadi sehemu unayoitaka. Kwa kifupi, inavitu vingi ambavyo vinaongozwa na hii saa.”Akawaonesha saa ambayo ilikuwa kwenye ya suti ile rangi nyeusi.” Si Idris wala Merice ambao hawakufurahia uwezo wa Agent Zero.
“Baada ya hili, naomba niwashe simu ili kumtaarifu Rais wangu uzima wangu.” Akaongea Agent na kuwasha simu na kuanza kuongea na Rais ambaye alishukuru kwa kijana wake kuwa salama na wakati huo, alimpa maelekezo kuwa anatakiwa kuiandaaa ndege maalumu kwa ajili ya kuingia Marekani na si ndege ya abiria. Hilo likapita na Rais akamwambia Jet P112 itakuja kuwabeba hapo Moshi na kuwapeleka hadi Dar es Salaam kabla ya Limasi kupelekwa Arusha kwa dada yake. Wote wakakubali.
ENDELEA.
Makubaliano hayo, yalikuwa ndio mwanzo mpya wa Idris kuanza kutaka kujua nguvu zake siku hiyohiyo kabla ya kuanza safari hiyo. Aliingia kwenye jokofu la kwanza, na Agent kupitia maelezo ya Dokta Ice, aliweza kufanya kazi mwanana ya kumjaza nguvu ambazo Dokta Ice alisema kuwa zipo. Ndani ya jokofu, Idris aliweza kuona picha nyingi wakati anajazwa nguvu hizo muhimu kwenye mapambano yake.
Kumbukumbu za akiwa mtoto na picha ya Uzo, iliendelea kuandama. Na kwa kuwa nguvu zile zilikuwa zinaingilia kwenye mishipa ambayo kemikali za C.O.D.EX ndimo zilipandikizwa, Idris alijikuta akiumia sana lakini hakuwa na uwezo wa kutoka hadi kompyuta ya jokofu lile ilipoandika ‘finish 100%’.
Hamna aliyejua maumivu yaliyompata Idris ndani ya jokofu lile kwa sababu kelele zake zilikuwa hazitoki nje. Na yeye hakutaka kuonesha kuwa ameumia, akaingia jokofu lingine na Agent Zero alifanya yaleyale. Hali ikawa ileile kwa Idris hadi alipoingia jokofu la tatu na baadae la mwisho.
Humo kulikuwa na ubaridi wa raha. Misuli yake ilipoozwa na kumpa amani tele. Alitamani akae humo daima. Alifungua macho yake na kutabasamu kwa sababu ya raha azipatazo humo. Akiwa katika tabasamu, kioo cha jokofu hilo kikafunguka runinga ndogo na kuanza kuonesha nguvu ambazo anazo Idris baada ya kuingia kwenye majokofu yote manne. Aliweza kushuhudia uwezo wake na akili yake ikaanza kunakili haraka sana yale ambayo anaweza kuyafanya. Yalikuwa mambo mengi ya kufurahisha na kumpa ujasiri na alitokea kufurahia sana uwezo ambao kaumbwa nao kwa kutumia video ile.
“Download Complete.” Sauti ilisikika na jokofu la mwisho likafunguka na kutoa moshi wa baridi kisha Idris alitokeza akiwa na mwili mpya, mwili ambao safari hii ulijaa kidogo na kuwa mzuri zaidi kuliko wa mwanzo.
“Nipo tayari sasa. Nipo tayari kupambana hata na wewe Agent Zero.” Idris aliongea kwa utulivu akiwa kavaa ‘boxer’ pekee. Agent akatabasamu kwa kauli Ile na kwa kasi ya ajabu na ya kushtukiza, alichomoa visu vidogo viwili na kuvirusha kwa pamoja. Idris akawa anaviona kwa uzuri na kwa jicho la tatu zaidi, yaani hadi kasi ya visu vile alivisoma kupitia akili yake. Vilivyofika karibu yake, Idris akakinga mkono wake na ile sehemu ambapo palitakiwa kuchomwa na visu vile, pakawa chuma, visu vikadunda na kudondoka chini. Akamtazama Agent na wakati huo, ikabidi Merice na Limasi watoke nje ya maabara ili wawaache wababe wale wapambane.
Agent akatoka nyuma ya meza ya kompyuta na kitendo kingine cha kushtukiza, akakifanya yule kijana. Safari hii alirusha visu vitatu. Na wakati visu vile vinamuelekea Idris, vikajitengua na kuzaa visu vingine vitatu na kumfanya hesabu za Idris kuvurugika kwa sababu yeye aliona vitatu. Akajaribu kuvikwepa kwa sarakasi mwanana, lakini kimoja kiliweza kumpata mkononi.
“Hivyo visu pia ni silaha hatari sana katika kuwaua wanajeshi. Hapo kimekuchoma, nikibonyeza saa yangu hapa, vinatoa kemikali ambayo inaweza kukudhuru. Endelea kufanya mazoezi kuhusu kuzuia na suti hii, ni muhimu kwako kwa sababu yakupasa kwenda kupambana sasa.” Agent aliongea na wakati huo Idris alivimba kidogo na kisu kile kikachomoka bila kuguswa. Jeraha lake likajifunga.
“Hapana, hapo nimetumia silaha ya kwanza kati ya kumi na tano nilizonazo. Nataka kukuonesha kazi Agent.” Aliongea Idris.
“Karibu kwenye mpambano.” Agent Zero bila uoga aliongea na kitendo bila kupoteza muda, alichomoka kwa kasi kwenda kwa Idris na wakati huo alikuwa anarusha visu vyake na kuvitengua tengua na kuwa vingi lakini safari hii Idris aliviona vema yeye akawa anamfuta Agent huku anarusha vichuma ambavyo viligongwa visu vile na kuvipotezea lengo la kumdhuru. Wakakutana katikati na Agent akawa wa kwanza kurusha ngumi lakini Idris aliidaka na kumrusha juu Agent aliyebamiza vibaya mgongo wake.
Idris hakuishia hapo, akatumia silaha nyingine ya mwili wake. Akapotea ghafla, na alipoibuka, alikuwa mbele ya Agent. Akamnyanyua kwa mkono mmoja na kumtupa tena ukutani. Agent akawa anagaa gaa kwa karaha na maumivu lakini hilo halikumshutua sana Idris ambaye alidhamiria kumfundisha adabu Agent Zero. Akamkamata shingo kwa mkono mmoja na kunmyanyua juu, Agent akawa kama anaelea angani. Na mara akajipapasa kiunoni na kuchomoa bastola kuanza kuifyatua kwenye mkono wa Idris. Haraka Idris akamuacha na mkono ule ukabadilika na kuwa na rangi nyekundu na kisha ukaanza kuwaka moto. Moto ulipozima, hali yake ikarudi vilevile.
Lakini wakati anakaa sawa, masikioni mwake akaanza kusikia sauti kama ya nzi wa chooni. Kwa haraka, akageuza mwili wake na kuwa chuma. Pini za Agent Zero zikashika shingo yake na ghafla vikalipuka na kumrudisha Idris katika hali yake huku akiwa katika maumivu makali.
“Nimeviongezea vikorombwezo aisee. Bado hii suti unaihitaji sana tu.” Agent aliongea huku akijaribu kuinuka baada ya kupata kichapo kizito toka kwa Idris.
“Hapana. Wewe huwezi kunishinda kirahisi namna hii. Ngoja nikufundishe adabu sasa.” Idris aliongea na kichwani mwake, akiruhusu kutumia chipu mbili, ya kupigana na kuzuia. Hapo ndipo Agent aligundua kitu kingine cha hatari toka kwa Idris.
Hakupewa nafasi ya kurusha ngumi wala kurusha silaha zake. Kipigo alichokipokea kilikuwa ni cha mbwa mwizi. Idris alikuwa anapotea, na kurudi akiwa karibu na Agent na aliweza kumsoma Agent haraka kwa kitendo ambacho anataka kukifanya. Kuna muda alimsoma anataka kuchomoa bastola, alimuwahi kumkamata mkono na kisha kuuzungusha kama anataka kuuvunja. Alimzidi vitu vingi vya kijanja.
Agent ni wazi alikuwa kazidiwa lakini naye hakutaka kukubali kirahisi kama kawaida ya Watanzania wengi, huwa hawakubali kushindwa hadi wapoteze kiungo kimoja au kufa kabisa. Mikono ya Agent ikatokeza ‘groves’ fulani ambazo ziliacha vidole nje. Mara nyingi huvaa wanamieleka au wapigana judo na karate. Tendo hilo alilifanya alipobonyeza saa yake. Na grovu zile zikaanza kumsaidia katika kurusha ngumi zenye nguvu kwa sababu nazo zilitengenezwa Kisayansi.
Ngumi za nguvu alizirusha na kuna muda alitoa hadi moto kwenye grovu hizo lakini kwa Idris hazikuwa kitu. Idris akawa anawaka na kuzima, yaani aliweza kupotea na kutokea ghafla mbele ya Agent ambaye naye kwa kasi hiyohiyo aliweza kuchomoka kwa kutumia sayansi yake aliyoibuni.
Idris akapotea tena na alipoibuka, akamkamta Agent shingo yake na kumrusha kwenye ukuta. Agent akagugumia kwa maumivu na wakati huo Idris alipaa juu na kukita kwenye tumbo lake na kisha akaanza kumtwanga makonde ya nguvu usoni. Uso wa Agent haukuwa wake tena kwa sababu kuna kinyago cha uso ‘Mask’ kilijifunga usoni kwake wakati Idris anafanya makeke yake. Kila Agent akijitahidi kumtoa Idris mwilini mwake, hakuweza na makonde yaliendelea kumuandama kwa kasi.
Ni simu ya Agent ndio ilimfanya Idris amuache Agent ambaye alipoachwa alianza kugaa gaa kwa maumivu makali sana.
“Mbwa wewe unataka kuniua?” Akauliza kwa maumivu makali Agent Zero.
“Yule wa kule barabarani si huyu tena. Nitakuua mimi. Pokea simu yako.” Agent akafunguka kinyago chake na kwenda iliposimu yake.
“Nyie mnakuja saa ngapi huku?” Rais alifoka baada ya Agent kupokea simu.
“Tunasubiri ndege mkuu. Hatuioni.” Ikabidi aongee kana kwamba yupo tayari. Rais akakata simu. Agent akavua shati lake na kubaki kavaa suti kama ile aliyowatengenezea wakina Idris. “Bila hii, ningekuwa marehemu leo. Imenisaidia sana. Nashauri nanyi kuwa nazo.” Alimwambia Idris akimuonesha ile suti yake. Idris akacheka na kutoamini ujanja wa Agent yule. Yeye alidhani ni ukomavu wake, na kumbe alivaa kitu cha kumsaidia.
Agent akiwa anachechemea huku kakamata kiuno chake, alianza kutoka ndani ya maabara ile huku maumivu yakiandama mwili wake kwa asilimia kubwa.
“Kusanyeni silaha zenu. Mimi za kwangu ninazo.” Alipofika mlangoni alimwambia hayo Idris na kisha akafungua mlango na kutoka.
****
Jet P112 ilifika walipokuwepo wakina Idris na kuwachukua ambapo baada ya kuwachukua ilienda hadi makao makuu ya FISSA. Huko walielekezwa watakapoachwa ambapo palikuwa porini nao iliwapasa waende hadi mjini kuwatafuta wanajeshi wenzao.
Limasi aliweza kuagana na Idris na kuachwa mikononi mwa maafisa usalama wa FISSA.
“Sawa mkuu, ahsante kwa msaada wako.” Idris alimshukuru mkuu wa FISSA,
“Niite Malocha Malingumu. Huna haja ya kuniita mkuu.” Malocha alimwambia Idris na Idris alitabasamu.
“Huyo Agent Zero yeye alikataa kujitambulisha.” Akamnyooshea kidole Agent Zero ambaye alikuwa nyuma ya Malocha.
“Ahaa! Huyu ni Agent Zero. Ni The Under Cover Agent wetu. Huwa tunamuita kwa kazi maalumu kama hizi. Yeye anaitwa Prince Mubarak au Mubah. Ni kijana wetu lakini anamkuu wake ambaye yeye ni chaguo la pili kama huyu atashindwa. Huyo naye ni The Under Cover Agent na ndio jicho letu hapa. Kama mlimshindwa huyu, basi yule sidhani kama mngemuweza.” Aliongea Malocha huku katabasamu.
“Huyu hajatushinda. Muulize.” Akaongea Idris huku katabasamu. “Na huyo Under Cover mwingine yupo wapi?” Akauliza.
“Yupo. Lakini hatujui yupo wapi. Huwa hatakagi kujulikana alipo. Yeye huwa na kazi maalumu tu. Kama huyu lakini huyu ukija humu utamkuta.” Akajibu Malocha.
“Anaitwa nani huyo mwingine?” Akauliza Idris.
“Huyo anajiita Man’Sai. Au The Last, yaani yeye ni Agent asiye na namba na ndio maana yupo huru na hata hapa hayupo.” Akajibu Malocha na mara mlango wa ofisi ulifunguliwa na aliingia mwanamama mmoja wa makamo na mwenye kupendeza.
“Samahani jamani. Nimewakatiza.” Aliongea yule mwanamama na kisha aliinama na kumnong’oneza jambo Malocha. Malocha akatikisa kichwa kukubali alichoambiwa sikioni. Mwanamama yule akasimama wima na kuomba tena msamaha kwa kuwaingilia,
“Huyu anaitwa Lisa Lindsay. Pia ni askari wetu. Mume wake ndiye The UnderCover Man’Sai. Naye ni muhimu sana kwetu.Alikuwepo siku ile Agent Zero alipokukamata. Yeye alikuwa mdunguaji na alimpiga mwanajeshi wenu mmoja risasi. Msimuulize mume wake yupo wapi tafadhali.” Malocha akamtambulisha Lisa ambaye utamuona kwenye riwaya kali ya Jina na Duka la Roho ambazo kaziandika mwandishi wa watu, Frank Masai.
Idris. Limasi na Merice wakashukuru kuwafahamu baadhi ya wapelelezi wa shirika la kijasusi la siri la nchini Tanzania, FISSA (Federal Interigency Secret Services Agency).
 
142.


“Samahani jamani. Nimewakatiza.” Aliongea yule mwanamama na kisha aliinama na kumnong’oneza jambo Malocha. Malocha akatikisa kichwa kukubali alichoambiwa sikioni. Mwanamama yule akasimama wima na kuomba tena msamaha kwa kuwaingilia,
“Huyu anaitwa Lisa Lindsay. Pia ni askari wetu. Mume wake ndiye The UnderCover Man’Sai. Naye ni muhimu sana kwetu. Alikuwepo siku ile Agent Zero alipokukamata. Yeye alikuwa mdunguaji na alimpiga mwanajeshi wenu mmoja risasi. Msimuulize mume wake yupo wapi tafadhali.” Malocha akamtambulisha Lisa ambaye utamuona kwenye riwaya kali ya Jina na Duka la Roho ambazo kaziandika mwandishi wa watu, Frank Masai.
Idris. Limasi na Merice wakashukuru kuwafahamu baadhi ya wapelelezi wa shirika la kijasusi la siri la nchini Tanzania, FISSA (Federal Interigency Secret Services Agency).
ENDELEA.
Wakatembezwa ndani ya Shirika lile la kijasusi na kutambulishwa maeneo mbalimbali na mwisho wa yote, ilikuwa ni kwa wao kuondoka Tanzania na kurudi Marekani huku Idris akimuahidi mke wake, Limasi kufanyia kazi vitu alivyompa na zaidi, akimuahidi kuwa atarudi Tanzania kumchukua ili wakaishi wote huko Marekani.
Limasi alikuwa ni mtu wa huzuni pale aliposhuhudia mume wake akipanda ndege aina ya Jet P112 ambayo imeelezewa vizuri sana uwezo wake kwenye riwaya kabambe ya Duka la Roho. Ila kwa kifupi, Jet P112 ni ndege mojawapo yenye kasi kubwa sana. Ni ndege inayoweza kuhama nchi hadi hadi ndani ya dakika kadhaa. Mwendo wake ni sawa na ndege zinazokwenda kwenye sayari zingine. Hujichochea na baadae huchomoka kwa kasi na kupotea. Huja kuonekana baada ya kufika eneo la tukio.
Naam. Merice na Idris walikwea ndani ya ndege hiyo wakiwa na silaha zao ambazo zIlitengenezwa na mtundu Prince Mubarak, au Agent Zero. Wakaaga ardhi ya Afrika rasmi baada ya Jet P112 kuondoka ndani ya FISSA.
“Watakuwa salama tu! Usihofie sana.” Aliongea Malocha huku akiondoka na kumuacha Limasi bado kasimama mbele ya kioo ambacho kilikuwa kinazuia moshi na kelele za Jet P112 pale inapoondoka.
“Nakusubiri Id. Nenda katafute haki zako.” Limasi aliongea peke yake na kuondoka eneo lile tayari kwa kupanga safari ya kurudi kwao.
****
CALIFORNIA, MAREKANI.
Kwa mbali anaonekana Idris na Merice wakishuka toka angani huku wamevaa suti ambazo walitengenezewa na Agent Zero. Kwenye makwapa ya suti ile, kuliwa na kitambaa ambacho kilizuia upepo na kuwafanya waweze kuhimili kushuka chini bila kudhurika. Katika mashamba makubwa ya mahindi yaliyopo hapo California, Idris na Merice wanaweza kutua salama na kisha wanaangalia huku na huko na kuanza kuvaa mavazi ya kiraia juu ya zile suti zilizotengenezwa na Agent.
Wanaweka vema silaha zao zilizokuwepo kwenye mabegi na kisha wanaanza kukimbia katikati ya mashamba yale ambapo kulikuwa na mahindi marefu na yamekauka. Yalikuwa ni mashamba makubwa na walitumia muda mwingi kukimbia bila kutokea sehemu yenye uwazi.
Ndani ya lisaa limoja, ndipo walitokea sehemu moja na kuona gari la kizamani likiwa limepakia mabua ya mahindi. Gari hilo aina ya Pageuot lilikuwa imesimama peke yake na injini yake kuunguruma. Idris na Merice walitazama huku na huko kuona kama kuna mmiliki, lakini hawakuona lolote. Wakaamua kulivamia na kuiondoa eneo lile kwa kasi huku wakiacha mabua yakidondoka huku na kule.
Muda kidogo, waliweza kuingia barabara moja ya vumbi na kwa kasi ileile, waliikanyaga barabara ile na kusababisha vumbi kubwa sana. Idris akiwa kashikilia usukani, alikuwa anaongeza mwendo kila alipopata wasaha wa kufanya hivyo, hilo ndilo likawa nyenzo kubwa ya yeye kufika anapotakambapo ilikuwa ni barabara ya rami, na kwa kasi ileile waliingia na kuanza kuisakama rami ile kwa mwendo wa kushangaza.
Katika masaa mawili, walikuwa wameweza kukata kilometa nyingi sana huku lengo likiwa kufika Los Angeles kabla ya usiku, na baadaye kupata usafiri utakaowapeleka hadi New York, yalipokuwa makao makuu ya C.O.D.EX. Walisimama vituo kadhaa na kujaza mafuta na kisha kwa mwendo uleule, waliweza kuondoka.
Saa kumi na moja ya jioni, ndipo walipofanya kosa dogo la kupita kwa kasi sehemu ambayo kuna askari wa barabarani.
“Code One Six, One Six.” Askari mmoja wa kikosi cha barabarani aliongea kwenye simu ya upepo iliyokuwepo kwenye gari lake ili kuwasiliana na wenzake wa mbele waweze kulisimamisha gari hilo lililompita kwa kasi ya mshale. Wenzake wakakubali na kwa haraka, na yeye alikwea ndani ya gari yake ya kazi na kuanza kuifukuzia ile ya Idris na Merice huku zile kelele za kipolisi, nazo zikiongezwa.
“Idris tunafukuzwa na polisi.” Merice aliongea baada ya kusikia ving’ora vya gari la polisi kwa mbali vikija.
“Unajua la kufanya. Hawa hawawezi kutusimamisha lengo letu kwa muda kama huu.” Idris aliweka msimamo wake na Merice alitoa bunduki moja kubwa kiasi na kupachika mabomu mawili na kuikoki bunduki ile tayari kwa mashambulizi.
Gari la polisi lilizidi kusogelea gari alilokuwa anaendesha Idris ambalo sasa lilikuwa halina yale mabua ya mahindi kwa sababu yalimwagika kwa ule mtikisiko wa kurukaruka kwa gari.
Polisi yule wa Los Angeles akiwa kabakiza hatua chache kulifikia gari la akina Idris, aliweza kumshuhudia Merice akiibuka toka kwenye kioo cha gari lao akiwa na bunduki na kisha akafyatua bomu moja lilienda kunasa kwenye bonet ya gari la polisi yule.
“Shit. Magnetic Boom.” Aliongea yule askari huku akili yake ikihama katika kuwafukuzia wakina Idris na kuliangalia lile bomu ambalo lililipuka pale kwenye boneti na kuifanya gari ile ipae juu na kutua chini kama mzigo. Kisha injini yake ilianza kuungua na wakati huo polisi aliweza kutoka na kuanza kukimbia akiacha gari yake ikilipuka na kusababisha mtafaruku mkubwa eneo lile.
“Safi. Hapo nadhani ujumbe utawafikia wahusika na wataanza kutufuatilia.” Idris aliongea na wakati huo aliangalia pembeni baada ya kuona kituo cha mafuta na watu kadhaa wakikimbilia kule ambapo mlipuko umetokea. Akapiga kona ya ghafla na kwenda hadi kituo kile kisha kwa haraka akashuka pamoja na begi lake na silaha, huku Merice naye akifanya vivyo hivyo.
Waliona Range Rover Sport nyeusi ikiwa imesimama hapo na mpira wa kujazia mafuta ukiwa bado kwenye tundu la kuwekea mafuta. Idris akafungua gari lile na kutupia begi lake la silaha na kisha kujaza mafuta ya kutosha. Ilionekana wazi muhusika wa gari lile alikuwa amekimbilia kule kwenye mlipuko au amekimbia mbali kutoka eneo lile kwa sababu ya vitisho vya kigaidi vilivyokuwa vinaendelea nchini Marekani.
Baada ya kufanikiwa kujaza mafuta, Idris na Merice walikwea ndani ya Range ile na kuitoa kwa kasi yao ya mwanzo na wakati huo muuza mafuta wa eneo lile akianza kulalamika kuwa wanaondoka bila kufanya malipo. Alichofanya muuzaji yule ni kunakiri namba za gari haraka na kupiga simu polisi, kisha akatoa taarifa. Naye alikuwa anashangaa mlipuko ule hivyo hakuona wakati wakina Idris wanafanya yao.
“Umesema wapo wangapi?” Akauliza Askari wa usalama baada ya simu ya yule mhudumu.
“Sijajua, ila nahisi wawili. Tena naona gari lao wameliacha hapa na wameiba hili la Range.” Yule bwana aliongea huku akiliangalia lile gari walilokuwa wameliacha wakina Idris.
“Gari aina gani na namba zake ni zipi?” Akaulizwa tena.
“Ni Peugeot ……” Akajibu na kutaja namba za usajili wa gari lile na plate namba zake. “Old Model” Akaongeza.
“Okay. Sasa kuwa makini na usiguse gari hilo. Hao ndio wamesababisha huo mlipuko na taarifa zao tunazo kwani askari aliyelipuliwa gari lake, katuambia. Hivyo kaa mbali na gari hilo, hao ni wavamizi hatari na wanasilaha za hatari sana.” Akaonya mwanausalama.
Muhudumu wa sheli ile ambayo iliunganika na supa maketi moja ndogo, akasogea mbali kabisa na gari ile huku akiwasubiri wanausalama waje.
Rage Rover Sport, ilikuwa imekamata barabara ya kuelekea mjini Los Angeles na ilikuwa inayapita magari kadhaa makubwa kwa madogo kwa kasi ya ajabu. Kasi ambayo iliwashangaza madereva wengine.
Wakiwa katika mwendo huo, helikopta mbili zilijitokeza angani na kuanza kutangaza kwa kipaza sauti kuwa gari ile isimame yenyewe kabla ya polisi hawajaivamia. Idris akatabasamu na kwa makusudi alimwambia Merice achomoe uso wake kwenye kioo cha dirisha ambapo kwa wakati huo lilikuwa limefungwa kwa vioo vyeusi.
Merice akafungua kioo kimoja na alijua nia na sababu ya Idris kufanya hivyo. Akaangalia helikopta moja kwa dakika moja na kisha akarudisha uso wake ndani. Polisi waliokuwepo kwenye ile helikopta, waliweza kuinasa sura yake kwa haraka na kuiingiza kwenye kompyuta yao tayari kutaka kujua wale ni wakina nani lakini kulikuwa hamna taarifa zozote kuhusu Merice, hivyo picha zile zilitumwa hadi makao makuu ya CIA. Huko zikatazamwa kwa muda na baadaye kutumwa hadi makao makuu ya C.O.D.EX. Macho yakamtoka Uzo baada ya kushuhudia uso wa Merice.
“Wajinga wapo mjini.” Uzo aliongea huku akibonyeza kompyuta yake na kumuangalia vema Merice. “Karibuni nyumbani wanajeshi wangu.”Akaongeza Uzo na kisha akatoka eneo lile na kwenda hadi maabara ambapo aliamuru wafanye kazi yao.
“Simeria.” Akamuita kimada wake. Naye yule mwanamama ambaye alikuwa mzazi halisi wa Merice, aligeuka na kumuangalia mwanaume wake kama ishara ya kuitikia wito. “Merice amefika lakini hayupo upande wetu.” Akampa taarifa lakini mwanamama yule hakuonekana kushtuka.
“Kwa hiyo nini kinachofuata?” Akauliza.
“Unajua kinachofuata. Ni muda wa kuona uwezo wa wanajeshi wako.” Uzo akamwambia na mwanamama yule alitabasamu na kuelekea hadi ilipo maabara kuu. Akaanza kubofya viparaza vya kompyuta yake, nayo ikakubali kubonyezeka. Majokofu yapatayo kumi na tano yalianza kuchemka maji yake na baadae ilisikika sauti ya kike ikisema ‘upload complete’ ikimaanisha kuna vitu vilikuwa vinaingizwa kwenye miili ya wanajeshi waliokuwepo kwenye yale majokofu kukamilika.
Baada ya hapo, yakafunguliwa na wanajeshi imara wakajitokeza wakiwa hawana vazi lolote miilini mwao na sura zao zilikuwa za kazi tu. Simeria akawataka waende chumba fulani ambapo huko walikuta mavazi na silaha zao, wakavaa kwa pamoja haraka haraka na kumaliza sawa sawa na kisha wakapanga mstari.
Uzo akatokea na kuwapa majukumu ya kwenda kufanya huku akiwataka kuwa makini kwa sababu ya watu wanaoenda kupambana nao.
“Kutakuwa hamna kiongozi, ni nyie wenyewe ndio mnatakiwa cha kufanya. Sisi tutakuwa tunaongea nanyi kwa kutumia hizo simu za sikioni. Sawa?” Akauliza na wanajeshi wale wakajibu kiukakamavu kuwa wameelewa.
Wakaruhusiwa kutoka ndani ya chumba kile na walitoka huku wanakimbia hadi nje na kisha wakapanda helikopta moja kubwa ya kivita ambayo nayo si haba kwa kasi yake kwani ndani ya dakika kadhaa, ilikuwa ipo barabara kuu.
Gari alilokuwa anaendesha Idris, lilikuwa linakuja kwa kasi na mbele yao kulikuwa na magari mengi ya polisi yaliyozuia barabara huku polisi hao wakiwa wamelenga kule gari ya Idris inapotokea kwa kutumia bastola zao ndogo.
Idris akiwa kadhamiria kwenda kukatisha katikati ya magari ya polisi wale, kwa kutumia macho yake ambayo yalikuwa yanadarubini ya kujitegemea, darubini ambayo ilikuwa inaweza kuona hadi kasi ya silaha, safari hii aliweza kuona wanajeshi wa C.O.D.EX wakiwa wanashuka kwa kutumia kamba nyuma ya polisi wale wa Los Angeles.
“C.O.D.EX advanced wameagizwa.” Alimwambia Merice ambaye alisogea karibu na kuweza kushuhudia wale wanajeshi wakianza kusogea mbele lakini Idris hakupunguiza mwendo.
Zikiwa zimebaki mita zipatazo mia mbili ili gari la Idris ifike kwenye gari za polisi, wanajeshi wa C.O.D.EX walisogea mbele ya gari zile za polisi wakiwa na mitutu yao na kuanza kushambulia kwa risasi nyingi gari la Idris na Merice.
 
143.


Idris akiwa kadhamiria kwenda kukatisha katikati ya magari ya polisi wale, kwa kutumia macho yake ambayo yalikuwa yanadarubini ya kujitegemea, darubini ambayo ilikuwa inaweza kuona hadi kasi ya silaha, safari hii aliweza kuona wanajeshi wa C.O.D.EX wakiwa wanashuka kwa kutimia kamba nyuma ya polisi wale wa Los Angeles.
“C.O.D.EX advanced wameagizwa.” Alimwambia Merice ambaye alisogea karibu na kuweza kushuhudia wale wanajeshi wakianza kusogea mbele lakini Idris hakupunguiza mwendo. Zikiwa zimebaki mita zipatazo mia mbili ili gari ya Idris ifike kwenye gari za polisi, wanajeshi wa C.O.D.EX walisogea mbele ya gari zile za polisi wakiwa na mitutu yao na kuanza kushambulia kwa risasi nyingi gari la Idris na Merice.
ENDELEA
Gari la Idris hadi linafika pale walipo wanajeshi wa C.O.D.EX, lilikuwa limechakaa kwa risasi na kioo cha mbele kupasuka vibaya sana. Endapo kungekuwa na binadamu wa kawaida, basi ni damu pekee ndiyo ingekuwa imetapakaa barabara nzima.
Gari la Idris likasimama mbele ya wale wanajeshi likiwa hatua kama kumi toka pale walipo. Polisi walikuwa hawana la kufanya na walikuwa hawaelewi ni nini kinaendelea kwani ni tukio la haraka sana limetokea.
“Nendeni watatu mkaangalie watuhumiwa wetu.” Sauti ilisikika sikioni mwa wanajeshi wale na wao wakaitii na kusogea haraka pale gari liliposimama. Idris alikuwa katanua mikono yake kama aliyekufa na wakati huo Merice naye alikuwa katulia tuli huku kichwa chake amekilaza nyuma ya kiti alichokalia.
Macho ya wale Wanajeshi yakaanza kuwaskani Idris na Merice bila kuwagusa ili kuona kama wapo hai au ni wafu.
“Wanaonesha hawana mapigo ya moyo hawa.” Mmoja wa wanajeshi wale waliokwenda kuwatambua Idris na Merice, aliongea kupitia kipaza kilichoungana na kisikilizo cha sikioni.
“Angalieni vizuri. Sii rahisi hivyo.” Uzo akaongea na yule mwanajeshi akaanza kuskani tena kuanzia kiunoni kwa Idris, akaja tumboni, akafika kifuani ambapo ndipo penye moyo. Bado kulikuwa hamna mapigo ya moyo. Ikabidi apande hadi shingoni na baadae akatua usoni ambapo alikutana na kitu asichokiamini katika macho yake.
****
Nchini Tanzania, mwanadada Limasi, anafanikiwa kurudishwa hadi kwa dada yake Timasi ambaye alipomuona tu! Alimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu huku akimpa pole kwa yote yaliyomkumbuka.
“Ahsante Dada, nipo salama mdogo wako.” Limasi aliongea wakati kapewa pole na Dada yake, Timasi.
“Karibu tena nyumbani dada yangu.” Timasi akamfariji na wote wakaingia ndani wakiwa na baadhi ya mizigo, huku wakiliacha gari toka ikulu, likiondoka eneo lile.
Ndani ya nyumba anayoishi, walikutana na mume wa Timasi ambaye alijulikana kwa jina la Bwana Sema au Shelanga Sema, lakini hakutaka sana kujitambulisha jina lake halisi bali ubini wake ndio ulinakiriwa katika vinywa vya wengi.
“Karibu shemeji,” Alimkaribisha Limasi, Bwana Sema. Na mwanadada yule alishukuru huku akitua baadhi ya mizigo midogo aliyoingia nayo ndani. “Pole sana kwa matatizo.” Akaongeza Bwana Sema.
“Ahsante sana Shemeji. Nashukuru MUNGU kwa upande wangu nipo salama. Ila sifahamu kitakachoendelea kwa mume wangu.” Aliongea Limasi kwa huzuni.
“Naaminii atakuwa salama. Tuzidi kumuomba Mola, amfikishe huko alipo na atimize jukumu lake.” Sema, akampa moyo shemeji yake wa pekee.
“Amen.” Timasi akaongeza maneno ya kusindikizia sala ndogo ya mumewe. Na kimya kikafuata kabla ya Limasi ajaanza kuhadithia mengi ambayo hawayajui Timasi na Mumewe.
“Ujue kama sijakuelewa Shem,” Sema, mume wa Timasi alikaa kitako baada ya hadithi nzima kuisha. “Yaani jamaa yeye aliuawa. Kisha akaingizwa hayo makemikali, akafufuka.” Akarudia yale aliyoelezwa. Limasi akajibu ndio.
“Hiyo inamaanisha kuwa jamaa si yeye. Yaani si binadamu. Ni kama roboti au wale watu wa kwenye muvi za kufikirika.” Akaongeza mawazo yake. “Halafu cha kushangaza, akakupenda, akakuthamini mpaka akakuoa….”
“Na nina mimba yake. Ya miezi miwili.” Akaweka taarifa mpya aliyokuja nayo.
“Eheee! Na kakupa mimba tena?” Akazidi kushangaa Bwana Sema.
“Ila hata mimi nashangaa Lim. How this happens?” Akaweka bayana Timasi.
“Ni kwamba hamniamini?” Akauliza Limasi kwa mshangao.
“Ni ngumu sana Shemeji. Yaani ni ngumu kukubali kuwa mtu aliyefufuliwa, akaingizwa madawa mwilini mwake. Ni kama zombie au labda ni vamp…” Maneno hayo hayakumuisha Sema, yakamfanya Limasi avute begi mojawapo lililokuwepo mahali pale ambapo bado mizigo ile haikuwa imeingizwa chumbani.
Akatoa kompyuta ambayo aliachiwa na Idris. Akaifungua na kuingiza neno siri. Kompyuta ikafunguka na bila kuchelewa, alifungua faili moja. Video kadhaa zikaonekana, akacheza moja na kuwawekea mbele wale ndugu zake muhimu.
“Naitwa Idris. Ndivyo navyojulikana japo jina langu halisi ni Best Bouncher. Mtoto wa Hayati Bouncher. Mmarekani aliyeshiriki kutengeza tena kanuni mpya ya kemikali hatari ya C.O.D.EX” Video ikaanza kwa utambulisho. Hapo ikawaweka kitako Timasi na Sema. “Ni mmoja wa waliyopandikizwa kemikali zile ambazo zinatupa uwezo wa ajabu.” Mara video ikaanza kuwaonesha wanajeshi wa C.O.D.EX wanavyopambana. Wakipigwa risasi, wanalala dakika kadhaa, kasha wanainuka wakiwa hawana jeraha hata moja. Wanaendelea kupambana.
Macho yakawatoka Timasi na Sema lakini wakakaa kimya kuona nini kitafuata. “Na mimi nipo hivyo unavyoona.” Video ile ikamuonesha Idris akisimama na kuchukua kidumu cha lita tano na kukifungua ambamo ndani yake kulikuwa na kimiminika. “Hii ni petrol.” Akaonesha huku anajimiminia kichwani. Kisha akachukua kiberiti cha gesi na kuanza kukiwasha. Zile cheche pekee, zikatosha kumuwasha Idris na kuanza kuungua.
“MUNGU wangu weee.” Timasi akapiga ukulele mkubwa huku akijificha asiweze kuona ile video. Sema alikuwa anaangalia lakini akiwa haamini kama mtu yule atapona. Ila alichokuwa anashangaa, Idris alikuwa hapapariki wala kuonesha kuwa anaumia au kujali kuhusu ule moto mkubwa uliomkumba.
Baada ya dakika tano, Idris alikuwa mweusi kama mti uliokuwa unachomwa ili kwanza ufe matawi yake au labda wadudu wakali waondoke kwenye mti ule. Kimya kikatanda kwenye video ile. Timasi akajaribu kuangalia ni nini kinaendelea, lakini bado picha ile ikamtisha. Akaendelea kujificha na wakati huo, Limasi alikuwa kimya akisubiri waone majibu.
Ghafla mwili wa Idris ukaanza kujirudi katika hali yake. Ngozi ikaanza kujitandika kwenye mwili wake kama vile mtu avaliswaye nguo zake.
“Shit. This is impossible.” Alihamaki Sema akimaanisha kuwa ile ilikuwa haiwezekani. Maneno hayo yakamfanya Timasi naye aangalie. Na aliona jinsi kichwa cha Idris kinavyojitengeneza hadi akarudi katika hali yake na kuchanua tabasamu mwanana. Sema akaifata kompyuta na kuirudisha nyuma kidogo hasa pale wakati anajiunga. Limasi akaacha afanye anachotaka kufanya.
“Shit. No editing. It’s real.” Akabwatuka baada ya kuiangalia video ile kwa umakini zaidi. Alikubali kuwa ile video hamna kilichohujumiwa, vyote vilikuwa ni kweli. “Ina maana haya mambo yapo kweli dunia hii?” Akajiuliza lakini hamna aliyejibu.
“Si kuungua tu. Ningeamua ningejizima mwenyewe. Lakini hii niliyowaonyesha, nilitaka muone ni kiasi gani tunauwezo wa kufanya mambo haya ambayo wengi wenu ni ngumu kuamini.” Video ile ikawatoa kwenye mawazo mengine. “Nataka muijue siri ya wanajeshi hawa, na ninataka mfanyie kazi siri hii.” Kabla video ile haijaendelea, Sema akaingilia kati.
“Ngoja, ngoja, ngoja.” Akamfanya Limasi asimamishe ile video. “Ngoja kwanza.” Akazidi kuwamakinisha Limasi na Timasi. “Anataka wakina nani wajue hapo?” Akauliza. Limasi akamtazama.
“Anataka dunia ijue.” Akajibu Limasi kwa kifupi.
“Kivipi sasa? Tukapeleke habari na video hii kwenye vituo vikubwa vya habari? Au wajue vipi?” Akauliza tena.
“Vyovyote vile. Na ni kheri tupo hapa.” Akaongea Limasi.
“Kwa Marekani hii. Na Wamarekani hawa. Na wakijua tu kuwa sisi ndio tumesambaza, mbona tutakiona?” Akaweka hisia zake Bwana Sema.
“Shem!” Limasi akashangaa kwa yale maneno.
“Kweli nakwambia Shemeji. Tutapotezwa mapema. Na sitamuona mwanangu wa tumboni mwako.” Akazidi kutabainisha.
“Kwa hiyo kutomuona Id kwako ni sawa tu?” Limasi akaja juu kidogo.
“No. I didn’t mean that, Shem….” Akataka kujitetea kuwa hakumaanisha vile alivyofikiria Shemejiye lakini Limasi akamkata.
“So, what do you mean?” Limasi akamuuliza kuwa anamaanisha nini sasa. Sema akabaki na kigugumizi asijue alikuwa anamaanisha nini. “Mbona unauoga wa ajabu sana Shemeji?” Akauliza kwa kukata tamaa, Limasi.
“Lim.” Timasi akamuita pacha wake kwa upole. “Sivyo unavyochukulia haya mambo. Ni magumu kupindukia. A time utakapoweka hadharani haya mambo, eidha utachekwa kwa kupeleka filamu na kisha baada ya kuchekwa,itafikia zamu ya kutafutwa na kuangamizwa ukidhaniwa kuwa unajua mengi sana kuhusu hiyo Protex.
“Siyo Protex na wewe.” Akamkatisha dada yake.
“Eee! Hiyo hiyo sijui phonex au sijui mwatex,” Akawafanya wengine wacheke kwa sababu ya kuchanganya majina.
“Ni C.O.D.EX bwana Dada. Hahahaa.” Limasi aliongea huku hana mbavu.
“Ni hatari hiyo kwako. Heri umuache Id apambane huko alipo. Akirudi, yeye atajua afanyaje.” Akaongeza baada ya kurekebishwa.
“Yaani umenifanya nicheke hadi utumbo kudunda dunda.” Limasi akiwa ndani ya kicheko, sijui kama alisikia ule ushauri wa Timasi. “Hata hivyo nimewaelewa lakini. Nahitaji kufanya jambo ambalo litamsaidia mume wangu.” Akaongeza baada ya kicheko kupoa.
“Jambo gani Limasi. Embu achana na hayo. Ama la! Basi peleka hayo mambo kwa Rais wan chi. Labda hapo kidogo nitakuunga mkono.” Sema akaongea kwa hisia.
“Najua unanijali Shem. Ila huyu ni mume wangu. Yupo vitani sasa. Sijui kama atatoka salama, ila namuombea heri tu. Kitakachotokea, nitamshukuru maulana. Ila sitakaa hivi hivi, kuna jambo nahitaji kulifanya na ninaomba kutopingwa kwa hili.” Limasi akaacha nafasi ya kupokelewa maneno ya familia yake.
“Mi’ kama hayana mashiko kwangu, kwa kweli nitaweka doubt (kikwazo) tu.” Akaongea Bwana Sema.
“Najua ni lazima uogope haya mambo Shem. We’ siyo wale hata kidogo. Japo unatengeneza filamu kama zile, lakini naona wazi, hutaki yatokee kiukweli ukweli.” Limasi aliongea huku akiunganisha na kazi ambayo Shemeji yake anaifanya. Kazi ya kutengeneza filamu za kisasa.
Bwana Sema, akaafiki maneno yale kwa kichwa, lakini Limasi akaendelea. “Ila huyu ni mume wangu. Nampenda mno na anakiumbe chake kwangu. I can’t wait for him to return wakati nina uwezo wa kufanya jambo litakalo muweka pazuri hata pale atakaporudi. Anaweza akashinda vita ambayo anahangaika nayo huko, lakini je? Atamaliza maadui zake wote?” Akauliza lakini swali lake ni kama alikuwa anajiuliza mwenyewe. Kila mmoja aliyekuwepo mle, alikuwa anataka kusikia ni nini hasa anataka kufanya. “Hawezi hata kidogo. Ila mimi nina uwezo wa kuwapunguza baadhi.” Akaongea maneno ambayo yakazidi kuwashangaza wenzake.
“Lim. How can you…” Timasi akabaki anazungusha mkono akiwa anashindwa atumie neno gani zuri kumaanisha anachotaka kukisema. “I mean, unawezaje kupambana na hao watu?” Akauliza. Hakutaka jibu hata hivyo. “Ni wagumu hao. Kwanza hawafi na wala hawana mpango wa kufa. Wanawezana wao tu. Lim, tafadhali embu ongea mambo ya kujenga akili kuhusu suala hili na si kutaka kupambana. Kumbuka ni wewe ndiye nakuona kama baba na mama leo hii, nikikupoteza je? Hapana Lim, hapana kabisa.” Timasi, dada wa Limasi. Akaonesha kutokubaliana na akili ya mdogo wake. Limasi akatikisa kichwa kwa masikitiko.
 
144.



“The problem is….” Akasita kidogo, kisha akaendelea. “Mnadhani kuwa kila kitu ‘kinasoviwa’ kwa kumwaga damu….” Hakumaliza kauli yake, Timasi akawa kamdakia.

“Kumbe..” Timasi akauliza huku anamtazama dada yake ambaye hakupata nafasi ya kuongea. “Unadhani kuna njia gani ya ‘kuyasovu’ haya mambo kwa kutumia mashairi au nyimbo?” Akauliza huku bado kamtazama dada yake.

“Hamna.” Mumewe akajibu. Kisha akaendelea, “No way. Hamna njia yaani, ni lazima ushike mtutu wa maana na kupigana nao. Limasi, you can’t.” Bwana Sema akakataa kabisa kwa shemijiye kuingia vitani na watu wale wa hatari.

“Ujue mnanishangaza,” Limasi akaongea huku anamtazama mmoja baada ya mwingine. “Yaani ni watu wasomi lakini nashindwa hata kutumia elimu zenu,” Wote wakawa kimya wanamtazama kwa makini. “Wewe ni mtu wa kutengeneza ‘mavideo’, umesomea huko Marekani kwa miaka zaidi ya mitano...” Aliongea hayo huku anamtazama Sema, mume wa Timasi. Kisha akamgeukia Timasi. “Na wewe umesomea mambo ya usalama na uhamiaji. Miaka karibu sita. Na wote mnatumia elimu yenu sehemu stahiki. How about me?” Akabakiza swali akiuliza vipi kuhusu yeye na elimu yake?

“Unataka kusema kuwa, utafungua mashitaka juu ya haya mambo?” Akauliza dada yake baada ya kung’amua maana ya dada yake.

“Hilo si swali tena. Linahitaji baraka zenu tu hapa.” Akajibu Limasi na kumfanya Timasi atikise kichwa kwa masikitiko huku anainamisha kichwa chake na tafakari zito likaanza kutembea katika ubongo wake.

“Lim,” Timasi akamuita dada yake baada ya kimya kifupi. Dada yake hakuitika bali kumuangalia akiwa tayari kusikia kauli yake. “Sawa wewe pia ni msomi wa Sheria. Lakini hapo unapotaka kuanzia kuonesha elimu yako, ni pagumu na pabaya pia.” Akaongea kwa upole dada yake, kuliko safari ya kwanza.

“There’s no easy way when you are starting sis. (Hamna njia rahisi kwenye kuanza Dada)” Limasi alishuka toka kwenye kochi lake na kupiga magoti mbele ya dada yake na kuikamata mikono yake. Uso wake akiuweka kwenye bembelezo mbele ya macho ya dada yake. “Hivi ndivyo nitavyoanza dada. Just give me a chance...” Akasisitiza. Timasi akabaki anakigugumizi. “Najua wanipenda na hutaki kusikia baya likinifika, lakini, I have no choice.” Akaongea hayo akimaanisha kuwa hana chaguzi zaidi ya kufanya kile alichokusudia. Timasi akapumua pumzi ndefu na mikono ya dada yake akiwa bado kaikamata.

“Nashindwa Limasi. Nashindwa kukuzuia lakini bado nakupenda na nakuhitaji sana Lim, please.” Timasi aliongea kwa huzuni na wakati huohuo, mume wake akamshika bega na kumfinyanga kidogo kwa kumfariji.

“Tim mke wangu. Wewe unampenda dada yako. Naye anakupenda sana. Lakini tayari anatakiwa kuanzisha familia yake. Awe na watoto na mume. Ingekuwa anaenda vitani na bunduki na mabomu, hata mimi ningekataa. Lakini anaenda kufuata sheria ili amuokoe mumewe, waje walee familia. Upendo wake kwako, upo daima, lakini anatakiwa kumpenda zaidi mumewe na familia yake atakayoanzisha. Ni sawa na wewe, leo hii nikipatwa na la kupatwa, hutomsikiliza Dada yako, lazima upigane ili niwe sawa.” Sema, mume wa Timasi akaongea kwa kubembeleza. Timasi akamuangalia mumewe na kisha akamuangalia Limasi.

“Dada.” Timasi akaita.

“Abee.” Naye Limasi akaitika.

“Unataka nini kumuokoa Idris wako?” Akauliza Timasi. Badala ya Limasi kujibu, akainuka na kumkumbatia kwa nguvu dada yake na machozi ya furaha yakimbubujika. Sema akawa anawatazama na kutabasamu bila kupanga kufanya hivyo.

“Ushauri wako pekee, unatosha sana dada yangu. Nitawasiliana na marafiki zangu wa huko nje, tutaifumua hii kesi. Nadhani hawatakataa kwa sababu watapata umaarufu mkubwa sana baada ya kufanikiwa kuwatia mbaroni hawa wajinga na mume wangu kuwa huru.” Limasi aliongea huku bado akiwa kamkumbatia dada yake.

“Fanya hivyo dada. Kwa lolote, usisite kunieleza.” Timasi akampa rasmi uhuru dada yake ili afaniikishe kumuokoa mumewe.
Baada ya hapo. Limasi aliamua kuwapa mkakati wake na kisha akawaonesha video zote ambazo aliachiwa na Idris Iris. Walizitizama kwa pamoja na kunukuu baadhi ya mambo ambayo yatasaidia sana ile kesi. Wakasoma pia nyaraka zilizokuwepo na kujipa moyo kuwa watafanikiwa kuliko hapo mwanzo walivyokuwa wanafikiria.

“Lini utaanza kazi hii Limasi.” Mume wa Timasi aliongea baada ya masaa karibu manne ya kutazama zile video na kusoma makaratasi yaliyoachwa na Idris.

“Kesho nitawasiliana na marafiki zangu popote walipo. Nadhani watakuja Tanzania kwa sababu wanajua sana ubora wangu na wanatamani sana kufanya kazi na mimi.” Akajibu Limasi.

“Okay. Pia na mimi nitawasiliana na kampuni moja ya Uwakili na Sheria za makosa ya jinai iliyopo Afrika Kusini, nadhani itawasaidia sana.” Akaongeza mume wa Timasi.

“Hapo utakuwa umecheza vema sana Shem maana vikampuni vyetu vya hapa, hamna kitu. Ila tukianzia South, itakuwa poa sana.” Limasi akaongezea kuhusu hilo.

“Nitakupa website yao ili uone utendaji kazi wao na kama utaridhika, nitakuunga nao ili ukapambane. Najua utafanikiwa tu.” Sema, akampa moyo zaidi na Limasi akapokea ujumbe ule kama habari njema kwake. Akamshukuru shemeji yake.
****
Mwanajeshi aliyekuwa anamkagua Idris, alijikuta amekutana na macho makali sana ya Idris. Macho ambayo kwa yeyote mwenye roho ndogo, anaweza kukimbia au kutoa hewa chafu.

“Oh! Oh!.” Mwanajeshi yule alijikuta akishangaa wakati Idris alipotoa bunduki yake ghafla na kulenga kichwa chake. Mlipuko mkubwa ukasikika ukifuatiwa na mwanajeshi yule mwenye sura mbaya kurushwa mbali akiwa hana kichwa ambacho kilichobongonyolewa vibaya kwa bunduki ya kisasa aliyoiunda Agent Zero.

Kazi ikaanza tena kwa wale wanajeshi wengine kufyatua risasi zao na mabomu kwa ujumla. Hali ikawa tete lakini Idris na Merice hawakuthubutu kujibu mapigo yale.

Baada ya dakika mbili, ukimya mkubwa ukatanda tena na macho ya Uzo yakawa kwenye runinga za mle ofisini mwake ambapo zilikuwa zinaonyesha vema gari la Idris lililokuwa limetobolewa vibaya na wakati huo moto mkubwa ukiwa unawaka kwenye injini ya gari hilo.

Polisi walikuwa mbali na eneo lile na hawakuthubutu kusogea bali kutazama kwa mbali jinsi wanajeshi wale walivyokuwa wanafanya kazi waliyoagizwa.

Sekunde kadhaa mbele, mlipuko mkubwa ukasikika toka kwenye lile gari. Gari likarushwa juu kwa sababu ya mlipuko huo. Na wakati lipo juu, huku chini, mwanadada Merice alibiringita kwa pembeni na kusogea mbali kidogo na eneo lile na hamna aliyemuona kwa sababu ya moshi mkubwa uliyokuwa umetanda muda ule.

Wakati gari lao linashambuliwa kwa risasi, Merice alichomoa bunduki ndogo yenye gesi na kuanza kutoboa kwa gesi sehemu ya kuwekea miguu ya gari alilopanda. Pale lilipoanza kushika moto, yeye alipita kwenye tundu hilo na kulala kwenye rami, kisha akapandikiza bomu moja la kulifanya gari lile lipae angani wakati linalipuka. Na alifanikiwa hilo.
Pale alipoona ni muda wa kulipuka gari lao, alibonyeza kifyatulio cha bomu lile, na bomu likarusha juu zaidi gari na kumpa nafasi yeye ya kuchomoka pale chini na kwenda pembeni ambapo hapatamdhuru kama gari litadondokea hapo.

Mshindo mkuu ukasikika wakati gari lile lilipotua chini likiwa linawaka moto kama nyumba ya nyasi iliyomwagiwa petroli na kurushiwa njiti ya kiberiti iliyowashwa.
Moto ule mkubwa uliendelea kuwaka lakini mara ukaanza kupungua taratibu kama vile mwanga mkali, halafu ghafla ukaanza kufifia labda kwa sababu ya kuishiwa nguvu ya umeme.
Ndani ya dakika mbili, tayari moto ule ulikuwa umepungua kabisa na alionekana Idris akiwa kapiga goti kwa mguu mmoja, mkono wake wa kushoto kakamata bunduki yake ya kisasa, M-16 202 Advance Grade ambayo aliifanya kama fimbo ya kutembelea jinsi alivyoikita kwenye rami na wakati huo, mkono wake wa kulia alikuwa kakunja ngumi nayo ikiwa imekita ardhini.

Wanajeshi wa Uzo wakakoki silaha zao na kujipanga vema kimakabiliano. Nyama za mwili wa Idris zikaanza kujirudi kwa haraka wakati bado kaweka pozi lake la mapigano na mwili wake ukiwa mwekundu sana kama kijinga cha moto. Ngoma iliwaduwaza wote waliokuwa wanaitazama.

“Bidhaa bora ya Dokta Ice.” Uzo alijikuta akiropoka maneno hayo bila kutegemea akiwa kakubali kile ambacho alikiunda Dokta Ice.

Idris akajiunga na kurudi akiwa katika hali yake ya mwanzo ndani ya nguo za kijeshi na zilizokuwa zimependeza sana. Taratibu akiwa kainamisha kichwa chake, akaanza kukinyanyua na kuwaelekea wale wanajeshi wa Uzo ambao walikuwa wamemuweka ‘tageti’ kwa bunduki zao za hatari kwa binadamu wa kawaida.

Kichwani mwa Idris, akaziseti chipu zote za mapambano, kujilinda, ukatili, na yote ambayo alikuwa anaweza kuyafanya. Akatabasamu pale alipoona wanajeshi wamemuelekezea silaha bila kujua wanapambana na kiumbe wa aina gani.

Katika hali ya kushtukiza, Idris akapotea eneo lile na alipoibuka, alikuwa mbele ya mwanajeshi mmoja huku M-16 yake toleo bora iliyoongezewa ubora na Agent Zero, ikiwa kichwani kwa bwana yule ambaye hakuamini kama kuna binadamu kama Idris kwa dunia ambayo amekuja kuishi.

Mlipuko mkubwa ulisikika na wakati huo damu zikiruka kwa nyuma na tobo kubwa likionekana kwenye paji la uso la yule mwanajeshi. Wenzake wakashtuka na kumtazama na walikutana na risasi nyingi za Idris ambaye alikuwa anazimwaga huku anajirusha upande mwingine wa barabara ile. Alipotua chini, akarusha bomu fulani dogo ambalo ndani yake lilikuwa linagesi hatari sana inayoweza kuteketeza wanajeshi wengi wa C.O.D.EX na binadamu wa kawaida.

CARBO-NITRO. EX, ni bomu dogo aliloliunda Agent Zero. Limechanganywa baadhi ya hewa ambazo zinaweza kuwanyong’onyeza maadui ndani ya sekunde kadhaa. Bomu hilo dogo, mfano wa yai la kisasa, hudondoka na kupasuka lenyewe kisha moshi mzito hutokea na uvutapwo na uliyemdhamiria auvute, basi kifo ni halali yake.

Idris akadondokea mbali kidogo na wanajeshi wale ambao walikuwa wamepigwa risasi za hatari za kifuanii na walikuwa wanagaa gaa kama wachawi waliokuwa wamepata maombi ya kichungaji.
Bomu dogo nalo likafunguka na kuanza kutoa moshi ambao wanajeshi wale waliuvuta na taratibu wakaanza kujifinya finya ngozi zao na baadae kukauka kabisa. Ngozi ikashikilia mifupa ya miili yao huku macho yakigeuka na kuwa meusi.

Moshi ulipotulia, Idris alisogea hadi kwa mwanajeshi mmoja na kutoa kifaa kilichokuwa jichoni kwake. Kifaa hicho ndicho kilikuwa kinapeleka mawasiliano ya picha hadi kwa Uzo. Idris akakitazama kifaa hicho na wakati huo Uzo alikuwa anamtazama pia. Hivyo picha ilivyokuwa imejengeka baina yao, ilikuwa kama wanaangaliana kwa uchu.

Baada ya kitendo hicho, Idris bila kusema neno, alikidondosha kile kifaa mfano wa kamera ndogo inayokaa jichoni. Akakikanyaga kwa nguvu na kukivunja. Kule kwa Uzo, runinga aliyokuwa anaiangalia, ikakumbwa na chenga nyingi sana. Uzo akasonya kwa kiburi.
 
145.



Baada ya Idris kukanyaga kamera ile, aliangalia huku na huko kuona kama kuna tatizo au kizuizi chochote, lakini hakuona kibaya cha kumzuia zaidi ya polisi kadhaa ambao bado walikuwa wamepigwa butwaa na hawaamini kile walichokishuhudia muda mdogo uliopita.

Idris kwa kutumia macho yake, aliweza kuwaona polisi wale walivyokuwa wanaogopa. Na yeye akaamua kutumia mwanya huohuo kwenda kuchukua moja ya magari yao. Wakati anaelekea huko, mwanadada Merice naye alitokea pembeni na kuungana naye kufuata usafiri mpya, tayari kwa kuendeleza kazi ambayo wameianza.
****
“Anajidai tayari ameshinda hii mechi,” Uzo aliongea wakati huo mwanamama Simeria alikuwa amesimama nyuma yake. “Anajiona ninja na kumbe ni katuni tu.” Akaongeza na msonyo mrefu uliomfanya Simeria agune. “Na wewe unaguna nini sasa?” Akauliza baada ya mguno huo wa hawara yake.

“Unajua umeonesha tabia za Kiafrika kabisa?” Uzo ambaye alikuwa ni mzungu halisi kabisa. Akamtazama mwanamke anayempa raha ikifika mida ya raha. “Tena tabia zenyewe ni za Kitanzania.” Akaongeza.

“Usinitajie hiyo nchi hata kidogo. Bora utaje hata habari za mimi kutafuna na kunywa damu za watu.” Akaongeza kwa kisirani Uzo.

“Kisa nini? Halafu huijui Tanzania tu. Ni wakarimu, waelewa na wapenda amani.” Mwanamama Simeria, aliongea huku akiwa anamtazama bwana wake.

“Yote hayo unayajua kwa sababu ya mumeo Ice ambaye sasa ni mifupa chini ya mchanga wa moto.” Akaongea Uzo.

“Upande mwingine naweza sema hilo ni jibu, ila kwa upande mwingine, hata Jografia inalitambua hilo.” Simeria alimuelimisha Uzo kuhusu nchi yenye amani na upendo ya Tanzania. “Labda uwachokoze ndio utawaona ubaya wao.” Wakati anamaliza maneno hayo, alikuwa anaondoka eneo lile.

“Sasa unaelekea wapi?” Uzo akauliza.

“Naona unanichanganyia mafaili tu hapo.” Simeria akajibu baada ya kugeuka na kumtazama mwanababa wa kizungu, mwenye mamlaka na jeshi la C.O.D.EX.

“Hatujamaliza hapa, kuhusu huyu mbuzi.” Sauti ya Uzo iliambatana na kumuonyesha kioo cha runinga mle ndani, akimaanisha mbuzi ni Idris.

“Ndio useme sasa na si kuanza porojo za mimi na Ice. Am done with him.” Hasira zilijionyesha wazi kwenye uso wa Simeria.

“Waandae Pro Soldiers.” Ndiyo maneno ya Uzo ammbayo yalimfanya mama yule aondoke eneo lile bila kusema chochote.
****
Huko Tanzania, Limasi na familia yake, hawakulala kabisa siku hiyo. Usiku kucha wakawa wanatuma barua pepe kwenda kwa watu ambao waliamini kuwa watakuwa msaada mkubwa sana kwao. Barua zilienda kwa Wanasheria wakubwa duniani na makampuni ambayo yanaaminika katika kufanya kazi za kisheria.
Limasi kwa upande wake, aliweza kuwaandaa Wanasheria watano aliomaliza nao huko India. Kazi waliyoipanga, walihitaji kuifanya haraka kabla hata mambo hayajawa mabaya kwa Idris Iris ambaye kwa wakati huo alikuwa ameanza kuuwasha moto wake ndani ya nchi kubwa na babe duniani, Marekani.

Hadi inafika siku nyingine, tayari Limasi alikuwa anauhakika wa watu aliowataka kuja kumsaidia katika kesi ya kuwatuhumu watengenezaji wa kemikali walizozipa jina la C.O.D.EX. Alifurahi zaidi alipoahidiwa na watu hao kuwa watafika Tanzania siku mbili mbele baada ya kukamilisha masuala yote ya kusafiri nje ya nchi.

Na wakati huohuo, mume wa Timasi, Bwana Sema alikuwa bado hajajibiwa maombi ya kampuni kubwa za kisheria alizozihitaji katika kusimamia kesi ambayo Limasi anaenda kuifufua. Hilo halikuwa lina shida sana kwa sababu ilikuwa mapema sana kwa wao kupata majibu. Ilikuwa ni uhakika kupata kampuni ya kisheria nzuri kwa sababu kesi yenyewe inagusa nchi kubwa na endapo watashinda, watapata umaarufu mkubwa sana. Hiyo ni kutokana na wanasheria wengine kushindwa kuitetea kesi ile hasa kwa sababu ya vitisho mbalimbali walivyokumbana navyo, ikiwemo mauaji makubwa.
****
Ndani ya nchi ya Marekani, gari la polisi alilokuwa analiendesha Idris, lilikuwa linachoma mafuta yake kuelekea katika Jiji la New York ambalo lilisifika kwa kuwa ulinzi mkali, labda kuliko jiji lingine pale Marekani. Lilikuwa na ulinzi huo kwa sababu ya biashara kubwa nyingi kufanyika eneo hilo pamoja na kubarikiwa watu maarufu duniani. Lakini hiyo, haikuwa sababu ya Idris kuacha kuchoma mafuta ya gari alilokwapua. Aliendelea kubadilisha gia kila alipokuwa anapata nafasi ya kufanya hivyo. Gari lilikuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi kupita maelezo.

Asubuhi na mapema, jua linachomoza, bado gari la wababe wale lilikuwa halijafika katika Jiji la New York na mara kwa mara walitazama ramani ya kwenye gari lao ili kuona wamebakiza umbali gani kuweza kufika katika jiji hilo.

“Saa moja pekee, inaweza kutufikisha tunapotaka.” Idris aliongea na maneno hayo yalimuingia vema mwanadada Merice ambaye naye kuonesha alikuwa kadhamiria, aliikoki bunduki yake na Idris akazidi kuichakaza rami kwa kukanyaga mafuta.

Upande wa Uzo, alikuwa kasimama mbele ya wanajeshi watano ambao wao walikuwa ni wa aina tofauti na wale walio pita. Hawa walikuwa wamevaa nguo maalumu kutokana na kile wanachokifanya. Wanaitwa Pro. Soldiers ama kwa kirefu Professional Soldiers yaani kwa lugha rahisi, ni wale wanajeshi wenye taaluma binafsi.

Katika hao wanajeshi watano, mmoja alikuwa kavaa nguo za mpira wa miguu na alikamata mpira huo mikononi mwake. Mwingine yeye alikuwa kavaa nguo nyeupe na mkononi kakamata rungu pamoja na kitenesi kilichotengenezwa kwa marumaru, huku kichwani kwake akiwa kavali kofia kama ile ya pikipiki lakini mbele ikiwa na nyavu. Ukimuona katika mavazi hayo, utajua wazi anacheza mchezo maarufu huko India au Australia, wanauita Cricket.

Mwanajeshi mwingine, yeye alikuwa anamwili mkubwa na alivaa mavazi makubwa kama yeye. Alikuwa pia kavalia kofia kama ya pikipiki, lakini yeye alikuwa anampira wenye umbo kama la yai. Huyu alionekana wazi kuwa anacheza mchezo wa kutumia nguvu sana wa Rugby. Katika wanajeshi hao watano, pia kulikuwa na mwanadada mwenye nywele ndefu na alikamata kitenesi cha kawaida pamoja na fimbo moja ambayo ilikuwa ina nyavu kwa mbele. Ilikuwa ni fimbo maalumu kwa ajili ya kucheza mchezo wa Tennis. Na wa mwisho yeye alikuwa kavaa koti lenye rangirangi nyingi, na miguuni alivaa viatu ambavyo chini vilikuwa na matairi. Mkononi alikamata fimbo ya chuma ambayo kwa chini ilikuwa bapa. Na mwanajeshi huyu alikuwa anakirusha kitu fulani cha chuma ambacho kilikuwa cha duara lakini kipo kama kifuniko cha kopo la mafuta ya kupaka.

“Nimewaita hapa kwa kazi moja tu. Kazi ya kuua au kumleta mbwa mmoja akiwa hai.” Alianza kuongea Uzo baada ya kimya kifupi kilichotawala tangu wanajeshi wale waletwe na Simeria. “Ni mwanajeshi ambaye tayari amehangamiza baadhi ya wanajeshi wetu. Na nawatuma nyie kama chaguo langu la mwisho. Na najua, mtafanya kile ambacho nakiota.” Akaongeza. Wanajeshi wale ambao walionekana wana uchu wa kufanya kazi yao, walifarijika kwa maneno ya Uzo ambaye alizidi kuwajaza maneno yake. “Si mwanajeshi rahisi kama mnavyodhani, ila nina uhakika kuwa, atakuwa rahisi sana kama mkifanya kazi hii kama timu moja. Nyie ni wanamichezo, lakini mnacheza michezo tofauti. Mkiiweka michezo kwa pamoja, mnaweza kufanya makubwa sana.” Akaendelea kusifia kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo. Na wale wanajeshi ambao walikuwa hawana tabasamu, waliendelea kusikiliza kila ambacho mkubwa wao alikisema.

“Tumekuelewa mkuu. Tunaanzia kazi wapi?” Akauliza mwanajeshi mmoja ambaye alikuwa anamwili mkubwa kuliko wenzake. Ni yule mcheza rugby.

“Wapo njiani wanakuja New York. Hivyo tutawaweka nyie mahali ambapo wataanza kuingilia. Tumewakataza polisi wote kuwazuia. Hii ni nzuri sana kwenu kwa sababu hamtaingiliwa na yeyote kwenye suala hili. Hivyo mkipata nafasi ya kuua hawa paka, ueni tu.” Akajibu Uzo.

“Wapo wangapi?” Akauliza mwanadada mcheza tennis.

“Wapo wawili. Na mmoja ni mwanamke lakini hana sumu kabisa. Ni huyu wa toleo la kwanza la C.O.D.EX. Ila huyu mmwanaume, hatujui katengenezwa kwa njia gani. Ndio maana tunamtaka sana yeye kuliko huyu mwanamama. Huyu wa kiume akija maiti au mzima, tutamchunguza ili tuwaunde wengi kama yeye. Anaonekana kaundwa kitaalamu sana.” Uzo alijibu na kuwasha video ambayo ilionyesha jinsi Idris anavyopambana na wale wanajeshi wengine huku akiwapiga mapigo ya kuzima na kuwaka. Yaani anajitokeza na akijitokeza, basi ni balaa.

“Yupo vema.” Mwanadada alisifu jinsi alivyoona ile video ya Idris anavyoweza kuwapiga na kuwagalaza vibaya wanajeshi wa Uzo.

“Lakini hawezi kuwa vema zaidi ya hii.” Mwanajeshi mwenye mwili mkubwa, ambaye alikuwa na taaluma ya kucheza mchezo wa kutumia nguvu, rugby, aliongea huku na kuukamata mpira wake wa rugby na kuubonyeza hadi kuupasua.

“Safi sana jemedari,” Uzo alisifia kitendo cha mwanajeshi mcheza rugby na kisha kwenda hadi kwenye kabati moja lililokuwa limefungwa kwa namba maalumu na kubonyeza namba hizo. “Na ndio maana nimewaita hapa ili mfanye kile nachotaka,” Alizidi kuongea huku akibofya namba moja baada ya nyingine. Kisha akabonyeza ‘ok’ na kabati hilo likafunguka. “Na kwa sababu nataka mshinde vita, nimewatengenezea silaha maalumu kwa ajili ya kushinda vita hiyo.” Vifaa vya michezo vikaonekana ndani ya kabati hilo na kuwafanya wale wanajeshi kila mmoja aendee silaha yake kutokana na mchezo anaocheza.

“Hii ni kubwa kuliko tulivyotegemea bosi.” Mwanajeshi mmoja aliongea baada ya kuchukua mavazi na kuyavaa, kisha kukamata silaha inayomuhusu.

“Kila kitu kipo hapa kuhusu silaha hizo. Utazitumia kama unavyoweza kuzitumia ukiwa uwanjani au kwenye mchezo wako.” Sauti hiyo ilienda sambamba na Uzo kuwasha video ambayo ilitoa maelezo jinsi ya kutumia silaha hizo za kimichezo. Zilikuwa ni silaha hatari kuliko wanajeshi wale walivyotegemea. Na kila mmoja aliahidi kuzitumia kwa jinsi alivyoelekezwa. “Chochote ambacho kitakuwa kikwazo kwenu, kivurugeni. Iwe wananchi au wana usalama. No mercy.” Uzo alitamka hayo akimaanisha wanajeshi wale wasiwe na huruma katika kazi yao. “Nendeni kazini, kila kitu nitakiona kupitia hivyo mlivyovivaa. Na kumbukeni, mavazi mliyoyavaa, naweza kuyafanya yakawaongezea nguvu pale nitakapopaswa kufanya hivyo. Na ninaweza kuwaua kama mkionekana kuleta huruma au kutaka kusaliti.” Wanajeshi wote wakakubaliana na hilo bila kuonyesha tabasamu. “Tawanyikeni. Nendeni eneo la tukio.” Akatoa amri na wanajeshi wale walitoka ndani ya maabara hiyo kwa mstari.

Nje ya jengo la kutengenezea wanajeshi wa C.O.D.EX, walionekana wanajeshi wale wakipanda helikopta maalumu kwa ajili yao tayari kwa kwenda kupambana na Merice akiwa na Idris. Helkopta ilikuwa juu ya ghorofa refu ambalo lilijengwa pembeni kidogo mwa Jiji la New York. Baada ya wote kupanda, helikopta ikakata mawingu.

Idris aliliingiza New York gari alilochukua toka kwa polisi kwa kasi ya hatari kabisa na kusababisha kimuhe muhe na taflani ndani ya jiji lile. Kila mwananchi alishangaa kasi ya ajabu ambayo Idris aliingia nayo katikati ya jiji lile.

Akiwa katika kasi hiyo, alijikuta ghafla akikanyaga breki na macho yake kutazama mbele huku akiwa kayakodoa na kushindwa kufanya lolote zaidi ya kuacha injini ya gari lile kunguruma pekee.

“C.O.D.EX Proffesinals.”Alisikika Merice huku naye macho yake yakiwa yanawatazama wanamichezo watano waliyosimama katikati ya barabara kubwa ndani ya jiji lile kongwe.
 
146.


“Mjinga kaamua kutuma jeshi lake la mwisho.” Idris aliongea huku macho yake yakimanika zaidi na wale wanajeshi. Kompyuta aliyopandikizwa kwenye kichwa chake, tayari ilikwisha wasoma wanajeshi wale na walionekana kuwa ndio jeshi la mwisho kuundwa na C.O.D.EX.

“Nilisikia hilo. Na mama ndiye aliwaunda hawa baada ya wale advanced. Ila hawa, ni hatari kwa sababu hufanya mazoezi kwa pamoja kutokana na michezo yao. Wana ubovu mmoja tu, ambao ukiudhibiti, unakuwa umewashinda.” Merice alitabainisha kidogo anachokijua.

“Ubovu wao ni nini?” Idris aliuliza na kuendelea. “Naona pia wamevaa mavazi kama silaha. Na kila kitu mwilini mwao ni silaha.”

“Ubovu wao ni huyo mcheza mpira wa miguu. Wao wamembatiza jina la Maradona. Ni hatari sana huyo. Ukimdhibiti, unakuwa umefanikiwa. Ila ni hadi uwadhibiti hawa wengine.” Merice akajibu bila kuongeza neno.

“Si mimi peke yangu wa kuwadhibiti hawa. Naamini kwa pamoja, tunaweza kwa kutumia silaha hizi za Agent Zero.” Idris aliongea na kukoki bunduki yake na kuchukua silaha zingine na kuziweka kwenye mavazi yake tayari kwa mapambano. Naye Merice hakuwa nyuma kufanya vile mwenzake alivyofanya.

Raia wengi walisimama pembeni wakiwashangaa wale wanajeshi jinsi walivyojipanga kwa kuvutia mbele ya gari la Idris. Waliyoweza kuwapiga picha, walifanya hivyo, na waliyoweza kuwachukua video, pia walibahatika kufanya hivyo. Lakini zaidi, ilikuwa ni hatari kubwa sana kwao.

Maghorofa marefu yaliyotapakaa katikati ya jiji lile, yaliendelea kuonesha matangazo ambayo yaliwekwa kwenye runinga kubwa za maghorofa hayo. Wananchi waliendelea kutizama kile ambacho kinataka kutokea katikati ya jiji la New York.

Dakika tano mbele, Idris alichomoza toka kwenye mlango wa gari alilolichukua. Na upande mwingine, Merice naye alichomoza huku akiwa kakamata vema mtutu wake tayari kwa mapambano ya kivita ambayo hayakuwa na jina.

Raia waoga walianza kujikusanya wao pamoja na watoto wao, na kukimbia mbali kabisa na eneo lile ili kunusuru roho walizopendelewa na MUNGU.

“Muda wa Vita vya Tatu vya Dunia. Ni vita kati ya mashine na mashine. Ni vita kati ya vilivyoumbwa na binadamu mwenyewe, na vile vya MUNGU.” Uzo aliongea akiwa ofisini kwake akitizama vema tukio lililokuwa linaendelea kuchukua nafasi katikati ya New York.

Idris na Merice wakasogea mbele ya gari walilokuja nalo na kuweka mitutu yao ya bunduki sawia kuwaelekea wale wanajeshi wanamichezo.
Risasi kadhaa zikachomoka kwenye bunduki za Merice na Idris na kuzidisha mkimbizano mkubwa ndani ya jiji lile. Risasi hizo ziliwaelekea wale wanajeshi na wao wala hawakuwa na wasiwasi zaidi ya kupinda huku na huko na risasi hizo kupitiliza bila kuwadhuru. Walizikwepa vema sana bila miguu yao kuondoka pale waliposimama.

Idris na Merice walipoona hivyo, tayari akilini mwao walikwishajua kuwa watapoteza risasi nyingi sana kama watapambana kwa kusimama eneo moja. Mawazo hayo yalikatiza vichwani mwao haraka, na walipoamua kufanyia kazi mpango wa pili wa mapambano, ndipo hapo jiji la New York lilipoanza kuchafuka.
****
Katika Jiji lingine kabisa, mbali na New York na mpakani mwa Mexico, nazungumzia Jiji la Texas. Jiji ambalo linasifika kwa ufugaji wa farasi pamoja na kuwa na polisi wakongwe waitwao Rangers. Bwana mmoja aliyekuwa anaangalia runinga yake, alijikuta akitabasamu baada ya kushuhudia kile ambacho alikuwa anakitazama kwa muda mrefu kwenye ile runinga.

Bwana yule akainuka na kwenda hadi kwenye jokofu lake na kulifungua, kisha akatoa kinywaji kimoja kikali kilichokuwa kwenye chupa ndefu. Bila kumimina kwenye gilasi, akaanza kuigida vivyo hivyo kwenye chupa yake.
Baada ya kuridhika, akairudisha chupa ile kwenye jokofu na kabla hajafunga jokofu lake, akapekua nyuma ya chupa kadhaa. Huko nyuma ya chupa hizo, akakukatana na kidubuwasha kimoja ambacho kimetuna kwa mbele na kina rangi nyekundu. Akakibofya, nacho kikaingia kwa ndani na hapohapo, mlango mkubwa wa ukuta uliokuwa nyuma ya jokofu, ukaanza kufunguka.

Baada ya kumalizika kufunguka, bwana yule ambaye alikuwa ana asili ya Kiafrika, na kavalia jinzi nyeusi pamoja na fulana nyekundu iliyombana sana, aliingia kwenye chumba kile kilichokuwa nyuma ya jokofu. Na mlango wa ukuta ulijifunga ukimuacha jamaa akiwa ndani yake akiangaza huku na huko.

“Muda wa kazi umewadia.” Alijisemea jamaa yule na kishja akaenda kwenye meza kubwa ya kioo na kubonyeza namba fulani, na kioo kile kikajitoa rangi nyeusi (tinted) iliyokuwa inaziba usione kilichokuwa ndani. Na baada ya kujitoa rangi ile, kioo kile kilijifungua na zikaonekana silaha mpya na za kisasa za kivita.
Jamaa akashusha pumzi ndefu na kisha akaanza kuchagua silaha ambazo alizihitaji kwa ajili ya kazi ambayo hadi muda huo ilikuwa haijulikani ni kazi gani na anaenda kuifanyia wapi.

Silaha kadhaa zilikuwa zimechaguliwa na yule jamaa baada ya kufungua makabati mbalimbali ambayo yalikuwa yamezagaa ndani ya chumba kile kilichoonekana ni maalumu kwa ajili ya silaha.

“Haloo makao makuu.” Jamaa aliongea kwa simu baada ya kuchukua baadhi ya silaha na kuweka kwenye begi maalumu la kubebea. “Agent Unknown, 000 Unknown.” Akajitambulisha kodi zake na upande wa pili ukamuitikia. “Watahiniwa niliyokuwa nawasubiri, wamejitokeza leo hii huko New York.” Akawapa taarifa kwa kile alichokuwa anakifahamu.

“Na sisi tumewaona” Ikajibu sauti ya kike upande wa pili wa lugha ya Kiingereza. “Tayari tumemuagiza mia na tano kwenda kukusaidia kupandikiza chipu ya kuwafuatilia popote watakapokwenda.” Akaongeza mwanadada.

“Muhase asifanye lolote. Asiingilie ule ugomvi.” Agent Unknown, aliongea kwenye simu.

“Hilo analijua. Akipandikiza hiyo chipu, taarifa za wanapokwenda itakuja kwenye simu yako haraka.” Akajibu mwanadada na kutoa maelezo mengine mafupi.

“Vema. Safari hii lazima wateketee.” Akaomgea jamaa aliyejiita kwa kodi ya Agent Unknown.

“Nikuitakie kheri Agent. Ukimaliza kazi hii, nadhani utachukua likizo ya mwaka mzima.” Akaongea dada huyo maongezi mengine binafsi.

“Nitafanya hiivyo kwanza. Kisha nitakuja China kukuchukua mrembo.” Akatania Agent Unknown.

“Wewe, acha hayo maneno, bado upo hewani na maongezi yako yanarekodiwa.” Akaonya dada yule ambaye hata kama hujamuona, ni wazi alikuwa katabasamu kwa yale maneno.

“Tatizo nini sasa? Au vibaya kwa mtoto wa Kichina kuchukuliwa na mweusi kama mimi?” Agent akauliza na hakumpa nafasi ya kujibu yule mwanadada, akapandishia maongezi yale. “Au labda sina mvuto wa kuja kwenye familia yako na kujitambulisha kuwa mimi ndiye mwanaume wa pekee katika hii dunia, ambaye naweza kukulinda kwa lolote baya na kukupa kile ambacho wengi sa……” Hakumaliza kauli yake, akawa kakatishwa na sauti nzito.

“Acha ujinga Agent, nenda kazini. Kamalize hiyo misheni kisha njoo China kuchukua barua yako.” Simu ikakatwa baada ya maneno hayo ya kijeshi.

“Shit. Sasa nimefanyaje hadi akate simu yangu? Kwani kapiga yeye au mimi? Huyu bosi boya sana. Wakisema nimuue, nitamuua kwa sababu ya kunibania kumchukua mwanaye.” Akajiongelea mwenyewe Agent Unknown huku anatoka kwenye chumba kile na begi la silaha mkono wa kulia.

Akabonyeza namba kadhaa kwenye ukuta ule, na makabati yote yakajifunga na ukuta ule aliyoingilia, ukaanza kufunguka na kumpa nafasi ya yeye kutoka na moja kwa moja akaenda kwenye runinga ambayo alikuwa anaitazama kabla hajaenda kwenye kile chumba.

Hapo alimuona mwanajeshi mmoja mweusi pamoja na mwanadada (Idris na Merice) wakiwa wamezungukwa na wachezaji wa michezo mbalimbali na wachezaji wale wakiwa wanawavuta kwa nyaya nyembamba zilizojichimbia kwenye miiili yao. Hali ilikuwa tete kwa wale wanajeshi wawili na kituo kimoja cha habari nchini Marekani, kilikuwa kinaonesha tukio lile moja kwa moja kutoka Jiji la New York.
*****
Uso wa Idris ulikuwa unawatazama wale wanajeshi wa jeshi la CODEX kwa uchu wa ajabu na pale walipoanza kuwavamia, yeye pamoja na Merice, hali ikazidi kuwa mbaya sana hasa kwa raia wa kawaida ambao walikuwa bado wanahisi wanaangalia filamu ya kusisimua moja kwa moja kupitia macho yao.

Idris alikuwa anamimina risasi nyingi za kawaida bila kutumia zile alizotengenezewa na Agent Zero. Na risasi hizo wakati anazitema, alikuwa anasogea mbele kwa kasi huku anapishana pishana na Merice ambaye naye hakuwa nyuma kuwashambulia wale wanajeshi kwa silaha zake za kawaida.

Wanajeshi wenye taaluma, walikuwa kwenye kazi ya ziada kukwepa risasi za Idris na Merice na wakati huohuo, wakiwa makini pia kumuangalia Idris asipotee kimazingara na kuwatokea kwa nyuma. Hivyo walichofanya, ni kuseti nguo zao ziweze kuzuia risasi na vilevile, kuweka duara ambalo liliwasaidia kuona pande zote ambazo kama Idris atatoweka ghafla na kutokea upande mwingine, basi wangeweza kupambana naye. Lakini haikutokea hivyo bali Idris na Merice kufika hadi pale walipo na kuanza kupambana nao uso kwa uso bila silaha.

Bunduki iliyokwisha risasi, aliirusha kwa nguvu Idris kumuendea bwana mwenye mwili mkubwa na bunduki ile yule mcheza Rugby, aliikwepa na kwa haraka kabla hajageuka, Idris aklikuwa kafika na kumshushia ngumi nzito ya uso iliyompaisha hatua tano nyuma toka pale aliposimama. Wenzake wakiwa hawana hili wala lile kwa pigo lile la kushtukiza, walijikuta nao wakiambulia ngumi nyingi za haraka zilizowatupa umbali uleule ambao alitupwa mcheza Rugby.

“Mmeingia pabaya madogo, bora mngeenda kucheza michezo yenu huko porini na si kwangu.” Idris aliongea wakati wale mabwana wakiwa chini wanajizoa zoa ili kunyanyuka.

“Hapana Soldier, wewe ndiye umekosea kuja mjini.” Aliongea mcheza mpira au Maradona na saa hiyohiyo akachanganya mikono yake, mpira wa miguu ukatokea na kuuweka chini kisha akaupiga shuti zito sana. Idris aliuona jinsi unavyokuja na kwa mkono wake mmoja akaudaka mpira ule. Lakini kabla hajafanya maamuzi, mcheza mpira wa miguu alibofya rimoti yake na mpira ukalipuka na kumrusha vibaya Idris bila kutegemea huku mkono wake ukiwa unawaka moto sababu ya mlipuko.

Merice kuona hivyo, akaanza kumkimbilia Iris lakini mwanajeshi mwenye viatu vya matairi, alichomoka kwa kasi akisaidiwa na viatu vyake na huku kakamata fimbo ya mchezo wake, akamfikia Merice na kumchapa ngwara nzito kwa kutumia fimbo ile.

Wakati huo Idris alikuwa anajaribu kujiinua pale kwa mkono mmoja, ndipo alishuhudia kichapo kizito kikimkuta mshirika wake Merice.

“Yaaah.” Idris alilia kwa uchungu na kusimama wima kisha akawaangalia wale wanajeshi wakiwa wamejitayarisha kupambana naye na kabla hajafanya lolote, alishuhudia mpira wa Rugby ukimuijia. Akawaza nao kuwa akiudaka, basi utalipuka hivyo aliamua kutaka kuukwepa. Lakini kabla haujamfikia, mpira ule ulilipuka na kutoa sindano nyingi sana ndogo ndogo zilizomchoma kila mahali kwenye mwili wake.

Na wakati akiwa katika kimuhemuhe hicho cha kujiokoa kwenye zile sindano, kishindo kikubwa cha kukimbia, kilisikika mbele yake. Alipoangalia, alikuwa ni mwanajeshi mcheza Rugby ambaye alimkumba kwa bega lake sehemu ya kiunoni na kumtupa Idris mbali kama mzigo. Japo Idris si mtu wa kuhisi maumivu, lakini baada ya kudondoka, zile sindano zikazidi kujikita ndani ya mwili wake, na uchungu ulimuingia kwa sababu sindano zile zilikuwa na sumu maalumu ya kumnyonya nguvu zake.
 
147.


Kijana yule mwenye asili ya weusi, ambaye alichukua uraia wa Tanzania na ambaye aliumbwa tena baada ya kufa, akawa mwanajeshi mwenye kemikali hatari za C.O.D.EX, aligalagala pale chini kwa sababu ya zile sindano zilizotoka kwenye mpira wa rugby. Wakati huo naye Merice alikuwa yupo chini kakamatika vema na yule mcheza mchezo wa fimbo. Mwenye viatu vya matairi.

Idris baada ya kugaa gaa pale chini, aliamua kulala chali, akawa analitazama anga ambalo halikuwa na jua kali, na wala jua hilo halikuwa katikati ya dunia kwa muda ule.

“Idris fanya kitu.” Aliisikia sauti ya Merice kwa mbali ikiongea maneno hayo. Macho ya Idris yakaingiwa na mwanga fulani machoni mwake, picha za mwanamke akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa, ikamuijia. Na picha za bwana mmoja wa makamo aliyekamata keki ya siku hiyo ya kuzaliwa, nayo ilimuijia huku sura za watu wengi wakimuimbia kijana mdogo wimbo wa siku ya kuzaliwa.

“Happy Birthday mwanangu.” Mwanamke aliyekuwa pembeni ya kijana yule mdogo, ilimuingia masikioni vema. Mtoto yule alitabasamu na mama yake akamkumbatia na wakati huo keki ilitua mezani na bwana aliyeileta, naye alimuita mtoto yule mwanangu.

Mishumaa saba juu ya keki ile ilizimwa na mtoto. Keki ilianza kukatwa tayari kwa mtoto yule kuwalisha watu wachache waliyoalikwa kwenye tafrija ile ndogo. Wakati tendo lile linaendelea, mara aliingia bwana mwingine mwenye suti nyeusi na kutoa samahani kwa kuchelewa kwenye sherehe ile. Wote walimuelewa na moja kwa moja bwana yule alimuendea mtoto yule,

“Happ Birthday, Best.” Alimtakia heri ya kuzaliwa na kumkabidhi kibox kidogo kilichofungwa na karatasi la zawadi. Mtoto yule akatabasamu na kumkumbatia yule bwana.

“Ahsante Dokta Ice.” Mtoto Best alimshukuru yule bwana aliyemkabidhi kiox kidogo cha zawadi. Alikuwa ni Dokta Ice, baba wa Merice na mume wa zamani wa Simeria. Alikuja kwenye tafrija ndogo ya familia ya Dokta Bouncher ambaye ni mwanzake waliyeunda upya kanuni (formula) ya C.O.D.EX.

“Happy Birthday Best.” Mtoto mdogo wa kike naye alimpa saa ya mkononi Best huku anamtakia heri ya kuzaliwa. Dokta Ice akamnyanyua mtoto yule wa kike na kumbusu kwa upendo.

“Na wewe yako ikifika, atakuja kukuletea gari, sawa Merice eeh.” Dokta Ice alimuambia binti yake na mtoto yule alicheka kwa furaha na kumkumbatia zaidi baba yake.

Baada ya dakika kadhaa, Dokta Ice na Dokta Boucher, walitoka nje na kuanza kuongea peke yao. Nyumba ambayo alikuwa anaishi Best na familia yake, ilikuwa na vioo kwa asilimia kubwa. Hivyo baada ya Best kuona baba yake anachelewa kurudi, alikwenda sehemu ya kutokea nje, na akiwa mlangoni, aliweza kumuona baba yake akiwa anazunguka huku na huko kama kachanganyikiwa na Dokta Ice alionekana kuzidi kumchanganya kwa maongezi yake. Dokta Boucher alikuwa kakamata kichwa chake kwa mikono miwili na kwenda huku na huko lakini Ice hakuacha kumwambia.

Ndipo mtoto Best alipotoka na kwenda hadi pale alipo baba yake na kumuulizia ni nini kinaendelea. Baba yake badala ya kumjibu, alimyanyua na kumpa tabasamu la ahueni, kisha akampooza kwa kumwambia hamna kibaya kinachoendelea.

Maneno hayo ya faraja, yakamuingia mtoto mdogo Best. Wakarudi ndani na baba yake na kuendelea kusherehekea siku ya mtoto wao kuzaliwa.
Usiku huohuo, Best aliweza kuwasikia wazazi wakifokeana huku mwanamama akitaka waondoke na baba akikataa kuondoka kwa sababu pale ndipo maisha yake yalipo. Hali ilikuwa tete usiku huo. Na si usiku huo pekee, mwezi mzima kulikuwa hamna maelewano mazuri ya baba na mama Best. Lakini mwisho wa yote, walikubali kubaki kwa msemo wa liwalo na liwe. Na ndipo usiku mmoja wenye mvua kubwa, waliingia wale mabwana ambao sasa hivi kesi yao inataka kufufuliwa upya na Limasi.

Ndani ya maono hayo, Idris aliweza kujitambua kuwa zile ni kumbukumbu zake za utotoni. Na wakati zinaendelea kujirudia, ndipo ikafika ile sehemu ya mama yake kuchinjwa kama ng’ombe wa mnadani.

“Amka Idris. Watakuua hawa mabwana. Amka.” Sauti ilisikika masikioni mwa Idris akiwa kalala pale chini na wale wanajeshi wanamichezo, kila mmoja akimpiga kwa mateke mazito na ya nguvu nyingi. Kwenye maono yake, aliweza kuona mama yake aliyekatwa shingo, akiongea maneno hayo angali damu zinaendelea kumtoka. “Inuka pambana Idris.” Maneno yalimtoka mama yake na ghafla picha ikabadilika na kuja ya Dokta Ice.

“Wewe ni mwanajeshi bora kupata kutokea kwenye uzao wetu. Hamna ambaye anaweza kusimama na wewe uso kwa uso. Utamuondoa duniani.” Dokta Ice aliongea akiwa katika mavazi meupe.

“Amka mwanangu, pambana.” Baba yake naye alitokea pembeni na kumsihi kuamka ili apigane na wale wanajeshi ambao sasa walikuwa wametulia kumpiga na kuhema kwa nguvu huku wakisubiri amri nyingine toka kwa mkuu wao.

“Amka Idris.” Sauti kali ya mama yake ilipenya masikioni mwake na ghafla alifungua macho yake kwa pamoja. Akawa karudi duniani baada ya muda kidogo kutoweka kwa sababu ya sumu iliyokuwa inasambaa mwilini mwake kwa kutumia zile sindano zilizomuingia.

Idris akatoa yowe zito baada ya kufumbua macho. Yowe ambalo alilitoa, halikukata kwa dakika moja nzima. Mwili wake ukaanza kubadilika na kuwa mwekundu kama moto. Sindano zilizokuwa zimemuingia, zikaanza kujichomoa na kusababisha wale wanajeshi wanamichezo kuanza kurudi nyuma kwa hadhari kubwa.

Idris akaamka kama mzuka huku macho yake yakiwaka kama taa zinazofungwa kwenye viwanja vya mpira. Merice akiwa chini naye hajiwezi baada ya kupigwa sana, alitabasamu baada ya kuona mwanaume yule karudi duniani. Ni sauti yake ndiyo ilikuwa inamuhasa Idris aamke na si mama yake wala baba zake, ila kichwani mwa Idris, aliona ni watu hao.

Kwa nguvu za ajabu, Idris alianza kuwakimbilia wale wanajeshi ambao walichomoa silaha zao tayari kwa kumdhibiti.

“Unatakiwa kumdhibiti mcheza mpira. Yule ndiye kila kitu.” Alikumbuka Merice aliyomwambia kama anataka kuwashinda wale wanajeshi. Na wazo hilo alimua kulifanyia kazi.

Maradona, yule mcheza mpira wa miguu. Alifanya manjonjo yake na mpira ukajitokeza mikononi mwake na kisha akaurusha kidogo juu ili aupige shuti kumuelekea Idris. Lakini ghafla Idris alipotea na sekunde hiyohiyo, akatokea mbele ya Maradona huku kaukamata mpira ambao haukufika mguuni kwa mwanajeshi yule. Akatumia mpira ule kama ngumi kwa kumpiga nao kifuani na kumuacha nao akiwa kaushikilia pale kifuani huku karushwa mbali kwa sababu ya ngumi mpira aliyokumbana nayo.

Mpira ule, Idris aliupandikiza bomu dogo sana ambalo lililipuka baada ya Maradona kutua chini. Mpira nao bila hiyana ukamlipukia Maradona na kumfanya apoteze uwezo wake wa kupigana japo hakufa. Wakati hayo yakiwashangaza wale wanajeshi wengine, Idris yeye alikuwa anapotea na kutokea tena mbele ya wale wengine na kuwapa kipigo cha mbwa mwizi. Hali iakabadilika ghafla. Idris ndiye akawa kaukamata mchezo.

Akiwa kama kapagawa, akiwapa kichapo wale wanajeshi wa Uzo, mara ilihisi kitu kikiingia shingoni kwake. Na haraka akakishika na kukitoa. Ilikuwa ni sindano na alipotazama ilipotokea, aliona sura ya Uzo ikiwa juu ya gari ambalo lilifunuka kwenye dari lake na kuacha upenyo wa mtu kutokeza. Idris akajikuta anapata hasira hasa baada ya kukumbuka kuwa yule ndiye hasa aliyeimaliza familia yake hadi leo hii mambo ya dunia yanampita.

Akataka kujitikisa kidogo, sindano nyingine ikaingia kwenye paja lake. Nguvu taratibu zikaanza kumuishia, wekundu ambao ulikuwa umejitengeneza, ukaanza kupotea taratibu. Alipojaribu kupotea, alijikuta akitokea mbele ya gari la Uzo, na saa hiyohiyo akapokea sindano nyingine ya kifuani kwa kutumia bunduki maalumu aliyokuwa kakamata Uzo.

Hali ikawa tete kwa mwanajeshi yule. Na wakati huohuo, wanajeshi wanamichezo walisimama wima na kutoa dhana zao za kimichezo. Mwenye kitenesi cha tenis, alikitoa na kukipiga kwa fimbo yake yenye nyavu. Kitenesi kile kikiwa bado hakijamfikia Idris, kikachoka sindano nyingi ambazo zilikwenda na kujikita ndani ya mwili wa Idris na kabla hajageuka, sindano kadhaa zikatoka kwenye kile kitenesi kilichonatia kwenye mwili wa Iwake na kwenda moja kwa moja kwenye nyavu ya fimbo ya tenisi. Mwanadada mcheza tenisi, akabonyeza kitufe fulani kwenye fimbo ile na zile sindano zilizonata kwenye nyavu, zikatengeneza umeme ambao ulimuingia Idris kupitia mawasiliano ya kitenesi.

Idris Iris akajikuta anapata kitetemeshi kikubwa cha mwili baada ya shoti kali ya umeme. Alipiga goti moja na kung’ata meno yake kwa maumivu makali ambayo alikuwa anayapitia kwa wakati ule. Pale alipotaka kunyanyuka, mwanajeshi mwenye viatu vya matairi alitoa kichuma chake mfano wa kifuniko kidogo cha mafuta na kukiweka chini kisha kukipiga kichuma kile. Nacho kikaenda kunasa shingoni kwa Idris kisha kikatuma waya mwembamba sana uliyokuja kunasa kwenye fimbo ya mwanajeshi mwenye viatu vya matairi. Naye bila huruma, akabonyeza fimbo yake ambayo ilipeleka umeme kwenye mwili wa Idris. Ikawa tatizo zaidi kwa Idris ambaye alikosa msaada hata toka kwa Merice ambaye alikwishapigwa pingu za shoti ya umeme muda mrefu sana.

Idris kila alipotaka kunyanyuka, wanajeshi wanamichezo walituma vifaa vyao ambavyo vilinasa kwenye mwili na kusababisha maumivu makali yatokanayo na umeme unaomwingia. Mwanajeshi mcheza rugby, yeye ndiye alikuwa kwenye pigo la mwisho. Akiwa anaurusha mpira wake juu na kuudaka kiustadi, alionekana yupo tayari kumuangamiza mwanajeshi aliyemchakaza vibaya Maradona.

Mcheza rugby aliurusha mpira wake kwa nguvu kumuelekea Idris na wakati huohuo, alikuwa kama anaukimbilia mpira wake. Mpira ule ukatua mgongoni kwa Idris na kulipuka mlipuko wa kawaida lakini ukitoa upepo mkali na kumfanya Idris achomoke mwenye zile shoti za wachezaji na wakati yupo angani, mcheza rugby alimkumba vibaya sana na kutua naye chini hadi sehemu ile ya rami, ikatengeneza shimo lililotokana na ule mshindo wa wale watu wawili. Idris macho yakamuingia giza, na kujikuta yanafunga yenyewe. Sindano za Uzo, shoti za wanajeshi na pigo la mcheza rugby, zilitosha kumtoa mchezoni Idris na wakati huo sauti ya kusikitika toka kwa Merice, ilisikika.

“Mleteni kwenye gari.” Uzo aliongea huku anaingiza mwili wake kwenye gari toka pale ambapo alichomoza nusu ya mwili wake.
Wanajeshi wanamichezo wakaenda hadi pale alipodondokea Idris na mcheza rugby, wakampongeza mwenzao na kisha kumchukua Idris kwa kumburuza hadi ndani ya gari alilokuja nalo bosi wao.

“Umekwisha mwanajeshi.” Uzo aliongea baada ya mwili kuingizwa ndani ya gari na yeye kumpiga pingu za kisayansi kwenye mikono na miguu yake. Baada ya dakika mbili, aliingizwa Merice naye akiwa hoi kwa kipigo. “Na wewe nawe unaenda kufa.”Aliongea Uzo na kufunga mlango wa gari baada ya wale wanajeshi wengine kukwea ndani ya gari hilo mfano wa Noah. Dereva akalizungusha vema na kuanza kuelekea alipotoka.

Walati wanaondoka eneo lile, pikipiki moja ilikuwa inakuja kasi mbele yao na kuwafanya wale wanajeshi kumakinika zaidi na mtu wanayemuangalia. Alikuwa kavaa nguo nyeusi, pamoja na kofia ya rangi hiyohiyo lakini pikipiki ikiwa nyekundu. Mtu yule alikuja kwa kasi na kuzidi kuleta taharuki ndani ya gari la Uzo.
 
148.


Dereva wa gari hakuonekana kusita kwenda mbele na alikuwa tayari kumkumba mtu mwenye pikipiki kwa gharama yoyote na hakuna ambaye angekataa hali ile kwa sababu mwenye pikipiki alikuwa anapita eneo siyo lake.

Pikipiki iliendelea kuja kwa kasi na ilipofika karibu, hatua kama tano ili kufikiana, pikipiki ile ilipinda upande wa kushoto nakupita kwa kasi ubavuni mwa gari iliyombeba Idris huku hata koti la leiza alilovaa mwendesha pikipiki, likigusa ubavu ule.

Uzo alichomoa kichwa chake dirishani na alishuhudia yule bwana akititia toka eneo lile na yeye kujikuta akishusha pumzi ndefu ya ahueni kwa sababu hali ilikuwa tete kwake hasa alipofikiria uwepo wa baadhi ya watu kwenye ile vita.

“Nilidhani ni The Lens kafufuka.” Aliongea huku akikaa vema kwenye kiti chake.

“Yule si kitu, tulikwishamuondoa muda sana mchezoni.” Maradona ambaye alikuwa tayari kapatiwa matibabu, aliongea kwa tambo ndani ya gari lile na wengine wakacheka kwa kumuunga mkono kauli yake.

“Hapana. Mshukuru MUNGU mmefanya kazi bila yeye kutokea.”Uzo aliongea. “Nina taarifa kuwa yupo duniani, lakini sijui yupo wapi.” Akaendelea na wakati huohuo, alifungua mkoba (dashboard) au droo ya gari ile na kutoa bahasha moja kubwa. “Hizo picha zimepigwa wiki iliyopita. Alionekana maeneo ya Los Angeles, kwenye supermarket fulani huko.”Aliwakabidhi baadhi ya picha wanajeshi wale toka kwenye bahasha, nao wakaanza kuzipitia zile picha moja baada ya nyingine.

The Lens, kama Uzo alivyomuita, alikuwa ndiye yule bwana aliyeitwa Agent Unknown wa Jijini Texas. Bwana ambaye nyumba yake inamlango wa ajabu nyuma ya jokofu lake la vinywaji.
“Bosi mbona hukutuambia hili?” Mcheza tenisi, mwanadada aliongea kwa sauti ya jazba na kumfanya Uzo amuangalie kwa macho makali. Mwanadada yule alijikuta anarudisha mgongo wake nyuma na kutulia kama mwanzo.

“Kama ningewaambia uwepo wa huyu mbwa, basi msingeweza kupambana na huyu pumbavu. Akili zenu zingekuwa zinamuwaza The Lens. Mngeshindwa kazi mapema sana. Huyu naye si mwanajeshi wa kubeza, si mnaona alivyotaka kuwazimisha pale?” Uzo aliongea huku akimtazama Idris ambaye hakuwa na chembe ya uhai wala fikra za kuwepo duniani.
Wanajeshi wanamichezo wakaamua kukaa kimya huku nyuso zao zikisononeka baada ya kugundua uwepo wa mtu ambaye wanamuita The Lens.

MIEZI MITANO NYUMA.

Vita ya maneno kati ya nchi za Ujamaa na nchi za Ukabaila, bado ilikuwa zinachukua nafasi kubwa sana duniani. Nchi kama China, Korea, Urusi, Cuba na zingine, zilikuwa ni nchi zinazojiendesha kiujamaa kwenye mwamvuli wa Udikiteta na Ukabaila. Na wakati huohuo, nchi nyingi za Ulaya kama vile Uingereza, Hispania, Ubelgiji zilikuwa zinaendesha nchi zao kwa sera za Ukabaila na huku nchi yenye nguvu duniani, Marekani, ikiwapa mkono wanaotawala kwa Ukabaila.

Katika vita hiyo baridi, ndipo kila nchi ilianza kuonyesha uwezo wake wa kijeshi kwa kubuni silaha mbalimbali za maangamizi na kuzijaribu maeneo mbalimbali duniani na kurusha video kadhaa kwenye mitandao ili kuwatisha wapinzani.

Marekani na washirika wake, ndio walikuwa kichecheo klikubwa cha utengenezaji wa silaha ambazo zilikuwa zinatishia sana amani ya nchi ambazo ziliingia naye kwenye vita baridi.
Dokta Simeria, alipewa kazi ya kutengeneza silaha mpya za C.O.D.EX na ndipo alikuja na mpango wake wa muda mrefu wa kuwaunda Pro. C.O.D.EX. Mpango ambao ulikwishaandikwa zamani sana na mwanamama huyu na alishawahi kuuzungumza lakini alipewa muda wa kuwabuni zaidi ili wawe imara, na hilo likafanyiwa kazi na kufanikiwa kwa asilimia tisini na nane.

Baada ya kuwaunda wanajeshi wanamichezo, ndipo wakataka kwenda kuwafanyia majaribio ili kuona kama watafanya kazi ambayo wanatakiwa kuifanya mbele yao. Ndipo walipopata habari ya majaribio ya silaha zingine za Kisayansi katika bara la Antarctica, bara ambalo linasifika kwa kuwa na baridi kuliko bara lingine lolote duniani. Ni bara ambalo hamna binadamu wanaoishi kwa sababu ya msimu mzima wa mwaka kuwa barafu pekee.

China iliamua kwenda kufanya majaribio ya silaha zake huko na ilipeleka silaha zake mpya mbili ambazo wao waliamini kuwa ndizo uzao mpya wa silaha za maangamizi. Marekani nao wakaamua kupeleka wanajeshi wao huko wakiwa wamewajaza hali ya kutokuwa na ubinadamu bali uwezo wa kuhimili hali yoyote ya hewa pamoja ugumu wa vita watakayokutana nayo.

Silaha mbili za maangamizi kutoka China, ziliundwa kama mavazi ambapo binadamu waliweza kuyavaa na kuyatumia katika shughuli walizoagizwa. The Lens, ni silaha ambayo ilibuniwa na kupewa jina hilo na Wachina wenyewe kutokana na uwezo wa silaha hiyo ya mavazi, kuwa na uwezo wa nguvu za jua huku zikiundwa kwa vioo aina ya lens.

Silaha ya pili waliita The Storm. Ni silaha ambayo ilikuwa inaweza kumfanya mvaaji ageuke na kuwa kimbunga na wakati huohuo, kubadili hali ya hewa na kuwa mawingu magumu kana kwamba kuna mvua kubwa ya mawe inataka kuchukua nafasi eneo hilo.

Mwanadada wa Kirwanda pamoja na mwanakaka mmoja mweusi lakini hajulikani anauraia wa nchi gani duniani, ndio walipewa jukumu la kuvaa mavazi hayo ya silaha na kwenda kujaribu huko kwenye bara la barafu na baridi kali, Antarctica.

Agent Unknown na Agent R huku herefu ya R ikiwakilisha Rwanda, ndio majina waliyopewa watu hawa katika shirika la kipelelezi la kujitegemea China. Wakiwa Barani Antarctica, walikuwa wanafanya majaribio hayo ya silaha kwa kubomoa vitu kadhaa ambavyo vilikuwa vimewekwa kwa lengo hilo la majaribio.

Wakiwa wanafanya majaribio hayo, kwa mbali waliweza kuona ndege kubwa ya kivita ikija maeneo yao na kwa kasi sana, ikawapita na kwenda kutua mita kama mia tano toka pale walipo The Storm na The Lens.

“Tumeona badala ya kufanya mazoezi peke yenu, basi tufanye kwa pamoja ili tuone nani anajeshi imara na zuri.” Sauti ilisikika kwenye ndege ile na ilipenya moja kwa moja hadi kwa wanajeshi wa China ambapo sauti hiyo iliingia kwenye vichwa vyao na kusafiri hadi makao makuu.

“Hatuhitaji hitaji lako, tupo vema kwa hapa tulipo.” The Lens aliongea maneno ambayo aliambiwa haijibu ile sauti toka kwenye ndege kubwa ya kivita.

“Mnadhani hayo mnayoyawaza, na hawa hapa wanayawaza?” Mlango wa ndege ile ulifunguka na kisha wanamichezo sita walitokeza, huku mwanajeshi mmoja pekee akiwa kaongezeka kati ya wale watano waliopambana na Idris na Merice.
Mmoja huyu aliyeongezeka alikuwa mwanadada mwenye mwili mdogo kiasi, na alifunga nywele nyuma na kuvaa mavazi meupe, na mkanda mweusi kiunoni, yakiwa ni mavazi maalumu kwa ajili ya mchezo wa kung fu na kareti.

“Hatuhitaji vita Uzo.” Sauti ilisikika tena toka kwa The Lens, ambaye mavazi yake yalikuwa kama vyuma lakini yaliyopendeza hasa kwa rangi yake nyeusi. The Lens alikuwa na mwili mkubwa kuliko wale wanajeshi kutokana na yale mavazi. Viganja vyake vya mikono vilitapakaa lens kali sana inayoweza kutandaza mionzi mikali ya nyuklia inayojitengeneza mwilini mwa vazi lile huku likishindwa kumdhuru mvaaji

“Najua hamuhitaji vita, ila hawa wapo majaribio.” Maneno hayo yalienda sambamba na wale wanajeshi sita wanamichezo, kujipanga mstari na kuweka silaha zao za kimichezo tayari kwa kuwavamia.

“Sawa, ngoja tuone mlichobarikiwa.” The Lens aliongea kwa sauti ya chini lakini ilimfikia vema The Storm ambaye naye alikuwa kavaa mavazi mepesi mithili ya yale ya Kihindi lakini yamebarikiwa kuwa na Sayansi ya aina yake endapo yakihisi hatari. Usoni kwake huyu mwanadada, alikuwa kavaa kinyago cheusi kinachomuwezesha kuona na kuvuta hewa kwa ufasaha bila kudhurika.

Alikuwa ni Maradona, yule mcheza mpira aliyeanzisha vurumai baada ya ndege iliyowaleta kuondoka. Aliupiga mpira wake kwa nguvu kumuelekea The Lens lakini Lens hakufurukuta bali kusogeza kidogo mwili wake na mpira ule kupita.

“Hapo ndio mwisho wako dogo?” Akauliza Lens baada ya mpira ule kutokuwa na madhara. Lakini kabla hajajibiwa swali lake, mpira ule ulimrudia toka nyuma lakini suti yake aliyoivaa, iliweza kuhisi ujio huo, hivyo mikono yake ikatoa muhale mkali uliyoteketeza mpira ule kabla hujamfikia. “Nadhani hilo ndilo ulilokuwa unalitegemea.” Akamwambia baada ya mpira ule kugeuka moto.

Wanajeshi wachezaji wakaangaliana, na kisha kwa pamoja walianza kufanya mavamizi yao ya kimichezo lakini The Lens pamoja na The Storm, waliweza kuwadhibiti vema bila wao kutumia silaha. Kila wanamichezo walipojaribu kupambana, waliambulia kupigwa vibaya sana.

“Mimi nashauri muite ndege yenu, muondoke hapa kabla hatujaanza kufanya yetu.” The Storm alifunguka uso wake na kuongea hayo huku akiwa anawaangalia wale mabwana wanavyotweta kwa nguvu baada ya kuchoka.

“Tumekuja kufa huku, hatujaja kufukuzwa na nyie mbwa.” Aliongea mcheza rugby kwa hasira.

“Ohoo! Basi sawa.”The Lens alitabasamu na kukubaliana na wale mabwana. “Storm, waonyeshe.” The Storm alifunga uso wake na kisha akiwa palepale, akanza kuzunguka kwa kasi na kuanza kutengeneza kimbunga kikali sana.

Baada ya dakika kadhaa, kimbunga kilikuwa kikubwa na kilikusanya asilimia kubwa ya Barufu. The Lens akiwa mbali na The Storm, suti yake yote ilibadilika na kuwa ya kioo na kisha kutengeneza miale mikali ya nyuklia au jua ambao ulitoka mwilini mwake na kuingia ndani ya kimbunga kile ambacho nacho kilichukua miale ile ya jua toka kwenye mwili wa The Lens, na kutengeneza moto mkali wa kimbunga.

Kimbunga kile cha moto, kikaanza kuwafuata wanajeshi wa C.O.D.EX kwa kasi na kila kilipozidi kutembea, ndivyo kilizidi kuwa kikubwa. Wanajeshi wanamichezo, walikumbwa na uoga mkubwa sana. Na kabla kimbunga kile hakijawafikia, ndege iliyowaleta ilitokea na kurusha bomu kubwa sana kwenda kwenye kile kimbunga.

“Hapanaaaa…” The Lens alipiga ukelele mzito baada ya bomu lile ambapo lilipotulia, The Storm alikuwa chini kalala huku damu zikimtoka kila mahali. The Lens alikimbia hadi pale na kumuangalia na kisha kuangalia ndege ile ilipo. Akajikusanya nguvu, na kurusha miale mingi ya nyuklia toka mwilini mwake lakini ndege ile ya kijeshi ilikwepa.

Ndipo alipoamua kuwageukia wale wanajeshi wachezaji, lakini kwa bahati mbaya, miale yake ilikuwa imekwisha na inatumia dakika zipazo kumi ili kujikusanya tena. Ikabidi achomoke toka kwenye ile suti na kushuka chini yeye mwenyewe kwa ajili ya kupambana nao wale wanajeshi uso kwa uso.

Alikimbia kwa kasi kuwaelekea wanajeshi wa C.O.D.EX na wakati huohuo, mwanajeshi mwenye viatu vya matairi na vyenye uwezo wa kutereza kwenye barafu, naye alikuwa anamfuata kwa kasi ileile akiwa kakamata fimbo yake ya michezo. Walipokaribiana, The Lens alichana msamba mkali na kuacha nguo zake zimsaidie kutereza na wakati huohuo, akaachia ngumi kali sana iliyomkuta mwanajeshi kwenye ubavu wake, huku yeye fimbo yake ikipiga hewa.
 
149.



Mwanajeshi yule alijikunja tumboni na kuruka hewani kama njiwa aliyepigwa risasi, na kisha kutulia mgongo. Wale wenzake walipoona hivyo, ikabidi wajipange kumshambulia The Lens lakini, walikuwa wamekwishachelewa.
Mcheza Rugby, ambaye yeye alikuwa tayari kuurusha mpira wake kwa nguvu nyingi sana, alikutana na upinzani mkubwa wa mkono mmoja wa The Lens ambaye aliuzuia mkono ule ukiwa angani tayari kwa kuurusha mpira. The Lens alimtazama Mcheza Rugby kwa macho makali na wakati huo yule mwanajeshi akiwa analazimisha kuukandamiza mpira wake kwenye mkono wa The Lens.
“Nakuua leo. Na baada ya wewe, nawaua na wenzako kisha namuua na baba yako aliyekutengeneza mbwa wewe.” The Lens aliongea kwa kisirani na yule mwanajeshi aliacha kuhangaika kujipapatua kuukandamiza mpira wake ambao ni kama alikuwa anashindana nguvu na mkono mmoja wa The Lens ambaye aliuzuia mpira ule pale mkononi kwa Mcheza Rugby ukiwa angani.
Mwanajeshi alimtazama The Lens usoni na aliona kuna sura ya mauaji pekee na kabla hajafikiri afanye nini, The Lens aliuvutia mpira kwake na kuukamata mkononi na kumfanya Mcheza Rugby aduwae kwa tukio lile. Na kabla hajaduwaa zaidi ya pale, The Lens alimpiga vibaya sana kwa mpira ule eneo la sikio lake.
Pigo lile lilikuwa kama ‘ngumi mpira’, yaani The Lens alimpiga na mpira ule sikioni bila kuuachia mpira. Mcheza Rugby akaona maruwe ruwe, akajihisi kama anataka kudondokea upande wa pili wa sikio ambao haukupigwa ngumi mpira, lakini alijikuta anarudi alipokuwepo kwa kupigwa ngumi nyingine nzito ya sikio la upande mwingine, akapofuka masikio.
Na wakati huo The Lens alimuachia karate matata sana kwa kumpiga kwa vidole vyake shingoni. Akawa kamziba hewa na mwanajeshi yule akawa anarudi nyuma huku kakamata shingo yake. Na hakurudi nyuma pekee, alisindikizwa kwa mpira wake wa kasi kutoka kwa The Lens ambao mpira ule ulitua tumboni kwake na kumrusha hadi kwa wenzake ambao walikuwa hawaamini kama jitu kubwa kama lile, linazuiliwa na mtu mwenye mwili mdogo tu.
Kwa hasira, mwanadada aliyekuwa kavalia mavazi ya kuchezea mchezo wa kung fu na karate, aliruka sarakasi kadhaa kumwendea The Lens na wakati huo The Lens alikuwa anarudi kidogo kidogo. Mwanadada mcheza karate, alifika karibu na The Lens na kutua kwa miguu miwili kisha akarusha mateke kadhaa ambayo The Lens aliyetolea nje kiustadi. Mateke yalipoanza kuisha, mwanadada yule akaanza kurusha ngumi.
Wakati ngumi hizo zinarushwa, saa ya The Lens ikaonesha kuwa zile nguo zake zimejaa nguvu. Akaibofya saa yake na mara kiganja cha mkono toka kwenye ile suti kilienda hadi mkononi na kujivaa. Yule mwanadada mrusha ngumi, alishangaa anadakwa mkono wake kwa mkono wa chuma na baadae chuma kile kilitoa muale mkali wa jua na kumkata kabisa mkono yule dada.
Mwanadada alipiga yowe la uchungu lakini haikuwa sababu ya The Lens kumuacha. Alimgeuza haraka na kuwa kama amemkaba kwa nyuma, kisha kwa mkono uleule uliyovaa chuma, akamuwekea shingoni na kwa nguvu sana, akalivuta koromeo la yule dada na kulitupia pembeni. Na kabla yule mwanamichezo hajadondoka, mkono ule ukawa kioo ambacho kilitumika kukata kabisa shingo ya yule mwanadada. The Lens akabaki kashika nywele za kichwa cha mwadada huku kichwa chenyewe kikining’inia na kiwiliwili kikidondokea tumbo.
“Pumbavu.” Maradona, yule mcheza mpira alijikuta akitukana na kuanza kusogea mbele lakini alisita baada ya kuona nguo za The Lens zikianza kujivaa mwilini. Kwa haraka, wale wanamichezo walijipanga mstari mmoja na kushikana mikono. Kisha nguvu nyingi sana zilianza kuwatoka mwilini na kusababisha tetemeko ambalo lilianza kubomoa ardhi ya barafu. Na ghafla nguvu zile ziligeuka na kuwa mlipuko mkubwa ambao ulifanya eneo lile kugeuka kuwa maporomoko ya barafu.
Ndege iliyowaleta, ilifika haraka walipokuwepo wale mabwana na kutua juu yao kama vile inawavaa, na ilipoinuka, kulikuwa hamna wanajeshi. Ngege ikapotea huku The Lens akijitahidi kuogelea kutoka mle chini ya barafu alipotumbukia baada ya mlipuko ule. Lakini hakuweza kujiokoa na hata nguo zake za mapigano, hazikuweza kumsaidia kwa sababu zilikuwa zimeundwa kwa mtindo wa jua na kitu chochote chenye asili ya jua/moto, hakipatani na maji. The Lens taratibu akaanza kuzama ndani Zaidi ya eneo lile huku kanyoosha mkono wake angani kama mwenye kutaka msaada ili mtu amuokoe. Na wakati huo, The Storm naye alikuwa anazama baada ya kifo chake kuchukua nafasi mapema sana.
Wale waliyokuwa ndani ya ndege, walishuhudia hali ile. Walisikitika hasa pale walipokumbuka kisanga kilichompata mwanajeshi wao mcheza karate. Walimuona naye akizama ndani ya maji akiwa hana kichwa.
“Mashujaa hufa kifo kibaya kuliko watu wowote wale.” Aliongea Mcheza Rugby baada ya kuona miili ile ikizama. Alikubali kuwa wale walikuwa mashujaa ambao walijitokeza kwenye maisha yake.
****
Gari lililokuwa limewapakiza Uzo na wanajeshi wake pamoja na Idris na Merice, lilifika makao makuu ya C.O.D.EX na kwa haraka, wanajeshi wale walishuka na kisha kumtoa Idris ambaye alikuwa kafungwa pingu kwa nyuma na pingu hizo, zimeunganika na pingu zingine miguuni kwake na kufanya Idris kuwa kama mnyama mkubwa wa porini aliyeuawa na kisha kuning’inizwa mwenye fimbo kubwa, kisha kubebwa na wawindaji hao mabegani.
Idris ambaye alikuwa hana fahamu, alitolewa ndani ya gari na kuanza kuburuzwa kama kitu kizito kilichochokwa kubebwa na wahusika. Merice naye ambaye alikuwa anafahamu zake, alitolewa ndani ya gari lile na kuanza kupelekwa ndani ya maabara ile kubwa kwa kusukumwa.
“Karibu mwanangu.” Simeria, mama wa Merice aliongea huku katabasamu na kumfuata Merice ambaye alikuwa hana chembe ya furaha usoni kwake.
“Nimeletwa nikuue tu, mbwa mkubwa we.” Merice aliongea kwa hasira na kumfanya mama yake azidi kutabasamu.
“Usijali mwanangu, najua umejazwa ujinga na huyu paka shume,” Aliongea huku anamtazama Idris aliyekuwa anatolewa nguo zake baada ya kufunguliwa pingu. “Hapa utarudi kwenye hali yako ya zamani, na utakuwa mwanajeshi ambaye utasikia amri zetu tu!” Akaongeza Simeria.
“Hutonipata tena.” Merice naye alijibu kwa uhakika bila kuogopa.
“Sawa. Ngoja tuone,” Akaongea Simeria. “Mpelekeni kwenye jokofu lake.” Akatoa amri, na madaktari kadhaa wakiongozana na wanajeshi wenye silaha, walikuja kumchukua Merice na kwenda naye hadi eneo ambalo Idris alikuwa anaandaliwa tayari kwa kuingizwa kwenye vifaa maalumu kwa ajili yake.
****
Huko Texas, bwana ambaye aliitwa Agent Unknown, aliweza kupata taarifa ya gari la Uzo lilipokwenda baada ya pikipiki nyeusi iliyokuwa inaendeshwa kwa kasi na mtu ambaye hakuonekana uso wake, kupishana na gari hilo. Bwana ambaye alikuwa juu ya pikipiki, aliweza kupandikiza kitu kidogo sana kwenye gari lile. Kitu hicho ilikuwa ni ngumu sana kuonekana na mtu mwingine au mitambo yoyote ile.
Baada ya kitu kile kupandikizwa, saa ya Agent Unknown iliwaka mwanga mwekundu na kisha kuonesha dira na kialama cheupe ambacho kilisimama kama gari la Uzo.
“Baada ya siku tatu nitakuwa hapo wazee. Mjiandae tu.” Aliongea Agent Unknown baada ya kushuhudia mwisho wa alama ile ambapo ilikuwa ni pale makao makuu ya C.O.D.EX
Nchini Tanzania, Limasi na kundi lake walikwishaanza mchakato wa kupitia video na nyaraka mbalimbali alizokuwa ameacha Idris. Walikuwa katika hali ya kufanya kazi kuliko kipindi kingine chochote. Nyumba ya Idris ambayo ipo Arusha, na ambayo Limasi na Idris walikuwa wanaishi, ndio ilikuwa kambi maalumu ya wanasheria wale kukaa kwa pamoja na kuijadili ile kazi ambayo waliitiwa toka kwenye nchi zao.
“Hii kesi ni lazima tuipeleke Kimataifa.” Mwanadada mmoja abaye alikuwa anaasili ya Kihindi, aliwaambia wenzake huku kakamata karatasi ambayo ilikuwa inamaelezo mengi sana juu ya Idris.
“Umeona eeh, Chameli, hapo lazima ifike hadi mahakama za kimataifa ili wakione cha moto hawa.” mwanadada mwingine, aliitwa Brighita, anaasili ya Brazil, alimuunga mkono mwanadada wa Kihindi. Chameli.
“Tujitahidi tu wapendwa. Hapa lazima tutapata sana msaada.” Faruq Omary, kijana wa kiume toka Iran, naye hakuwa nyuma kuungana na wenzake aliosoma nao huko India masomo ya sheria.
“Na tukifanikiwa kushinda hii kesi, nadhani dunia kwa ujumla itakuwa inatutazama sisi kwa macho ya tisa.”Buja Bujiku, Mnaijeria mwenye ucheshi mwingi aliongeza.
“Macho ya tisa?” Akauliza mwanadada mwingine, yeye aliitwa Theresa Tyrese, Muingereza mwenye asili ya weusi. Alikuwa anacheka sana baada ya kusikia macho ya tisa. “Yaani wewe nilikumiss hapo tu kwenye ucheshi wako.” Akaongeza na wakati huo wote walikuwa wanacheka.
“Mmenikumbusha sana shule jamani. Yaani najihisi kama bado nipo chuoni, kila napowatazama.” Limasi aliongea huku anawatazama mmoja baada ya mwingine. “Ahsanteni sana kwa kuja kufanikisha hii kazi.” Akawashukuru.
Watu hawa sita ndio walikuwa kundi bora la wanachuo katika mwaka waliomaliza chuo huko India. Kundi hili la kujisomea, liliundwa kwa kuunganisha mataifa sita tofauti, yaani India, Uingereza, Naijeria, Tanzania, Iran na Brazil. Na ndilo kundi lililokuwa linawatu toka mataifa mbalimbali bila kuchagua dini na rangi zao. Walishinda kundi bora la chuo katika masomo ya Sheria, na sasa, wapo pamoja tena katika kutimiza ndoto na malengo yao ya kimaisha. Wapo tayari kupigania kesi ngumu ya Idris.
”Limasi, kila wakati tunajaliana. Hiyo ndio kauli mbiu yetu. Au umesahau?” Mbrazil, Brighita, alimwambia hayo Limasi huku anampigapiga begani kwake.
 
150.


Baada ya kukusanya kila kitu vema, Agent Unknown, alikwenda haraka nyuma huku kaiweka bunduki yake aliyoikunja upande wa kushoto. Kisha baada ya kufika usawa anaoutaka, akaanza kukimbia kwenda mbele kwa kasi zaidi na kisha kupita kwenye dirisha lililokuwa wazi, na ambapo alikuwa anachungulia kila kitu kinachoendelea kule kwenye maabara ya C.O.D.EX. Aliruka toka kwenye ghorofa lile ambalo lilikuwa lina ghorofa thelathini na tano. Yeye, Agent Unknown, alikuwa ghorofa ya thelathini na tatu.
Alipojirusha, akatua kwenye ghorofa linalofuata lakini kwenye chumba cha watu ambapo alipitia dirishani na kuvunja kioo cha chumba kile. Ndani ya chumba hicho, alikuta watoto wawili wanacheza kwa pamoja na midoli yao.
“Hamjambo watoto?” Unknown aliwasalimia na watoto wale wakajikuta wanafurahia hasa baada ya kuona mavazi ya Kikomando ya Agent pamoja na bunduki ambayo ilikuwa bado inaning’inia.
“Hatujambo shikamoo kamanda.” Wakasalimia nao watoto huku wakiwa wanatabasamu.
“Oooh! Nimelipenda hilo jina.” Unknown aliongea na kujipekua mifukoni na kutoa boksi dogo la bazuka na kuwapatia. “Mama na baba wapo wapi?” Akawauliza tena.
“Wametoka.” Wakajibu kwa pamoja.
“Wakija mtawapa hii hapa ili watengeneze dirisha. Sawa eeh. Na nyie msicheze tena humu, nendeni sebuleni.” Akaongea huku anawakusanya na kuwapa noti tano za dola mia moja kila moja.
Watoto wakatoka mle chumbani na midoli yao pamoja na bazuka. Unknown akachomoa ufunguo wa chumba kile na kufunga kwa nje. Kisha akabomoa kitasa kile ili wale watoto wasiweze kufungua hata kama wataupata ufunguo.
Baada ya kuhakikisha usalama wa wale watoto upo, akachomoka na kuingia hadi sebuleni kwao. Huko aliwakuta wakifurahia bazuka na mchezo wao wa kupiganisha midoli.
“Natokea hapa watoto eeh.’ Akawaambia na wakati huo anafungua dirisha kubwa la sebuleni hapo.
“Sawa Kamanda.” Unknown alichomoka mwili wake kwenye dirisha lile na kisha alilifungua kwa nje. Watoto wakawa hawaamini wanachokiona. Agent unknown akatizama chini. Ulikuwa ni umbali mrefu sana kuruka. Lakini yeye hakutazama chini kwa sababu ya umbali, alitazama chini kuona kama mali yake ipo salama.
Akaona kuwa ipo vema. Akajirusha na wakati huo watoto walitoka kwa kasi na kwenda kuchungulia. Hapo walimuona Agent akiwa kafungua parachuti na moja kwa moja akenda kutua kwenye gari moja la gharama sana, na ambayo ilikuwa wazi. Na wakati huohuo, akiliondoa parachuti lake mwilini.
“Woow. Kamanda ni hatari sana” Wale watoto walifurahi walichokiona na wakati huo, Unknown aligeuka na kuangalia alipotoka. Kulikuwa ni mbali sana, alakini alihisi kuwa wale watoto wanamuangalia, akawaonyeshea dole gumba. Japo wale watoto nao walikuwa hawana uhakika kwa kile kitendo, walimpungia mkono Kamanda wao.
“Muda wa kazi.” Akawasha gari lake la gharama na kwa kasi sana akaanza kuliondoa pale na kuzidi kusababisha mshangao mkubwa kwa watu waliokuwa wanamuona tangu anafika pale chini kutoka juu ya ghorofa la thelathini.
Safari yake alionekana anaelekea yalipo makao makuu ya C.O.D.EX hivyo ulinzi wa eneo lile ukaongezwa kwa kufungwa mageti yake na wanajeshi kadhaa kujiweka sawa na mitutu yao yao ya bunduki.
Unknown alipoona kuwa ulinzi umewekwa zaidi kwenye geti la makao makuu ya C.O.D.EX akatabasamu na kisha akabonyeza vitufe fulani kwenye sehemu ya usukani wa gari lake. Mbele ya gari lile kukatokea ngao kubwa sana. Naye Agent akaongeza kasi ya gari lake na alipofika getini, alilikumba geti lile kubwa na gumu na kulivunjilia mbali. Akaingia ndani kwa ubabe mkubwa na wakati huo risasi zilikuwa zinamiminika toka kwenye bunduki za walinzi. Hakujali kwa sanabu gari lile lilikwisha jifunga juu na halikuweza kuingiza risasi.
Msele mkubwa ukapigwa eneo la ndani ya makao makuu ya C.O.D.EX na Unknown alitazama juu ambapo anatakiwa kwenda. Walinzi wa eneo lile waliendelea kupoteza risasi huku Agent akiwa wala hana fikra juu yao, yeye alikuwa anawaza ni vipi atafika walipokuwepo wakina Uzo.
Katika hali ambayo hamna aliyeitegemea, Agent Unknown, alibonyeza vitufe kadhaa kwenye sehemu ambapo mara nyingi hukaa redio ya gari au tv (dashboard), na mara gari lile likaanza kujifungua fungua na baadaye likawa kama roboti.
“Hee! Transformer?” Mlinzi mmoja alishangaa kwa sauti wakati gari lile likibadilika na kuwa roboti. Alifananisha badiliko lile na yale anayoyaona kwenye filamu za Transformers.
“Hapana. Huyu ni The Lens.” Unknown ambaye alikuwa ndani ya roboti lile, aliongea huku anamuinamia hadi usoni yule askari ambaye alihisi haja ndogo inataka kumchomoka.
The Lens, aliangalia juu ambapo anataka kwenda. Ghorofa ya thelathini na mbili ndipo wakina Uzo walipokuwepo. Kuna umbali mrefu sana toka pale alipo. Alichofanya ni kubonyeza tena vitufe kadhaa, na The Lens akageuka na kuwa roketi, ndege yenye kasi kubwa sana. Wale walinzi ambao waliacha kushambulia lile gari, wakawa hawaamini hasa pale roketi ile ilipochomoka ghafla na kwenda juu.
*****
Ndani ya maabara ya C.O.D.EX, tendo la kuhamisha damu kutoka kwenye mwili wa Idris kwenda kwenye wanajeshi wengine watano, lilikuwa linaendelea kwenye asilimia sabini. Na ndio wakati ambao Unknown alikuwa amechomoka toka kwenye jengo alilokuwa anaaangalia kila kitu kinachoendelea kwenye maabara ile.
“Nadhani tunaelekea kufanikiwa.” Uzo aliwaambia watu kadhaa aliokuwa nao na wote walitulia wakisubiri mafanikio hayo wajionee kwa macho na si kwa midomo ya Uzo.
Asilimia mia ilifika lakini kimya kilikuwa kikubwa. Hamna ile sauti ambayo ilitegemewa kuwa itasikika ya kuwa tendo la kuhamisha damu limekamilika. Na badala ya kusikia sauti hiyo, mstari uliyokuwa unahesabu asilimia hizo, ukaanza kushuka kwa kasi kwa wale wanajeshi wanne, kasoro Merice.
Na wakati tendo hilo linatokea, Uzo alipokea taarifa kuwa wamevamiwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la The Lens, na alibadilika na kuwa roketi.
“Mungu wangu. Tayari tumekwisha.” Uzo aliongea huku macho yamemtumbuka kama mgonjwa wa kwashakoo.
“Nini tena Uzo?” Akauliza Jenero.
“The Lens tupo naye mjengoni. Na sasa kaimarisha silaha yake.” Akajibu na akafanya akili ya haraka kwa kuwafungulia wanajeshi wake wa michezo. Nao kwa haraka wakafika kwenye eneo husika na kujipanga mstari na vifaa vyao huku macho yao yakiwa sehemu ambayo waliamini kuwa The Lens atatokeza.
Roketi ya Unknown ilipita kwa kasi nje ya dirisha ambalo wanajeshi wanamichezo walikuwa wanalitazama. Nao hawakujua wafanye nini kwa sababu hawakujua The Lens alifanya tendo lile kwa sababu ipi.
Kimya kikiwa kimetawala na akili zao wote zikihamia kwa The Lens, mara sauti toka ndani ya maabara ile ilisikika. Ilikuwa ni sauti ya kike toka kwenye kompyuta ikisema ‘Upload Complete’, yaani kile kitendo cha kuingiza damu kwenye miili ya wanajeshi kilikuwa kimekamilika.
Simeria akatazama yale majokofu yote matano na alijikuta akipiga ukelele mkubwa sana wa kero. Majokofu yalionyesha kuwa, ni Merice pekee ndiye alifanikishiwa kuingiziwa damu ya Idris. Wale wengine wanne, baada ya kuingiziwa ile damu ya Idris, wakaanza kunyonywa tena kwa mwili wa Idris kuichukua damu yake pamoja na ile ambayo wanayo. Simeria aligundua hilo na ndio maana akapiga ukelele wa kero.
“Nini Simeria?” Uzo akabonyeza kitufe cha kusafirisha sauti toka alipokuwepo kwenda ndani ya maabara.
“Tumefeli Uzo. Tumefeli…” Simeria aliongea huku kajikamata kichwa chake na wakati huo madaktari wengine walikuwa wanahangaika kufanya jitahada za kufanya yale matokeo yasiwe yenyewe.
“Nini kimetokea?” Uzo akauliza tena kwa hamaki.
“Hamna kama Dokta Ice. Atabaki kuwa yeye kama yeye. Ni namba moja daima.” Badala ya kujibu swali, akamsifia Dokta Ice ambaye alikuwa ni mume wake wa zamani.
“Simeria. Nini kimetokea?” Uzo akauliza tena na safari hii kwa kufoka.
“Hamna kilichofanyika zaidi ya kuwapa nguvu Idris na Merice.” Akajibu kifupi.
“Nilitaka kuwaambia, mkanikatisha hapa. Nilijua kuna kitu mmekisahau kwenye uchunguzi wenu.” Dokta Boss, Mkemia wa nchi, alibwabwaja na Uzo akamtazama kwa macho ya udadisi.
“Una maana gani?” Ikabidi amuulize yule bwana.
“Ni kwamba, huu ni mpango wa huyo mwanajeshi wa Dokta Ice kumbadilisha huyo mwanajeshi wenu wa kike ili awe kama yeye. Na kukubali kuingia ndani ya maabara hii, ni kwa sababu anajua anachokifanya. Huyo mwanajeshi wa Dokta Ice, hata wangekuja wanajeshi wenu wanaocheza mipira na rugby mia tano, wasingemuweza huyo. Na ndicho kitu kilikuwa kinanishangaza, kwa nini akubali kirahisi?” Maneno yakamtoka Mkemia Mkuu.
“Tunafanyaje sasa?” Uzo akauliza kama mjinga vile.
“Tusubiri waamke na watuue tu.” Akajibu Dokta Boss na mara risasi ikatua kwenye paji lake la uso.
“Pumbavu wewe. Hamna anayekufa leo, zaidi yako.” Jenero aliongea huku akirudisha bastola yake sehemu husika na kisha mlinzi wake alimletea simu ambayo ilikuwa kwenye mkoba kama ule wa Hayati Dokta Boss. Mkoba ukafunguliwa na simu ile ikaonekana ikiwa imezungukwa na mitambo kadhaa kama mixer za studio za muziki.
Jenero akanyanyua simu yake na kubonyeza vitufe kadhaa.
“Tuletee F.O.F hapa makao makuu ya C.O.D.EX” Baada ya maneno hayo, akakata simu. Uzo akabaki mdomo wazi asielewe alichoongea Jenero.
“F.O.F?” Akajiuliza Uzo.
“Future Of Forever.” Jenero akamtajia Uzo kirefu cha F.O.F yaani kizazi kijacho cha milele.
“Ni nini hiyo?” Akauliza
“Wanajeshi wapya toka kwenye maabara mpya.” Akajibiwa.
“Sijaelewa. Maabara mpya, ipi na ya tangu lini?”
“Living Lab. Ipo tangu miezi mitatu iliyopita.”
“Mbona hamkuwahi kuniambia kuhusu hili?”
“Kwa sababu hatutumii kemikali wala maiti kuunda silaha zetu. Tunatumia kama hiyo ya Wachina kuunda silaha zetu.”
“Hata kama, ndio…..” Hakumaliza Uzo, kishindo kikubwa kikaanza kusikika juu ya paa ya ghorofa lao. “The Lens huyo.” Akajikuta anabwatuka na kitete kikimzonga usoni pake.
Baada ya roketi ya Unknown kupita kwa kasi kwenda juu, ilianza kutoboa ghorofa lile toka juu ya paa ambapo kulikuwa ni ghorofa ya hamsini. Na sasa roketi ile ikawa inaelekea ilipo maabara ya C.O.D.EX.
“Wote, sogeeni hapa.” Uzo alibwabwaja na wachezaji wake wakakimbilia hadi kule walipo na kuweka uzio ambao usingeruhusu Uzo na wenzako kudhurika kwa lolote litakalotokea.
Pindi macho yao yote yapo kwenye paa la maabara ile, huku ndani ya majokofu kulianza kulipuka na cheche zilonekana kutokea mle ndani. Hali ikawa tete kwa Simeria na wale madaktari wengine waliyokuwepo.
“Vita imeanza.” Uzo alinong’ona peke yake.
 
151.



Dakika moja pekee ilitosha ndani ya maabara ile kutulia milipuko yake na kuacha moshi mkubwa ambao ulipotulia, yakaonekana majokofu ya Merice na Idris yakiwa wazi lakini, wao hawakuwepo.

Simeria akiwa anashangaa huku na huko, mara madaktari aliyokuwa nao, wakaanza kutupwa kwenye kuta ngumu za maabara ile na kupasuliwa vibaya matumbo pamoja na vichwa vyao. Damu zilijitengeneza kwenye kuta na vioo ambavyo viliizunguka maabara ile. Lakini hamna kilichoonekana kinafanya vile hadi pale madaktari wote walipo poteza uhai.

Merice akajitokeza akiwa kama anawaka moto lakini baadae alirudi katika hali yake na kuvaa mavazi ya kijeshi. Na wakati huohuo, Idris naye alijitokeza kwa njia kama ya Merice. Simeria macho yakamtoka hasa mwanaye alipoanza kumfuata pale alipo.

“Nilikwambia mama yangu, huwezi kunipata kirahisi hivyo. Umefanya kosa kubwa sana ambalo…” Merice alikuwa amefika pale kwa mama yake na kumkaba. “….. Halistahili msamaha, zaidi ya ……” Akanyoosha mkono wake kisu kirefu kikajitokeza mkononi mwake.

“Mwanangu. Unajua nakupenda sana. Nakupenda kuliko chochote kile maishani mwangu.” Simeria akaanza kujitetea.

“Najua. Na ndio maana uliniua, na kisha kunitengeza mwanajeshi nisiye na huruma. Na ukamuua baba kwa sababu ya umalaya wako, na tamaa ya kumiliki kila kitu. Lakini baba, bado akili yake hukuiweza.” Merice akamwambia mama yake huku macho yake kuna muda yakiwa yanabadilika na kuwa kama vijinga vya moto.

“Nisamehe mwanangu.” Ndilo neno aliloongea Simeria kwa shida sana kwa sababu ya roba kali aliyokuwa kakamatwa.

“Adhabu yako ni…” Merice aliingiza kile kisu kirefu nyuma kidogo ya kidevu cha Simeria, na kisu kile kikatokea kwenye utosi wa mwanamke yule. “Kifo…” Akamalizia kauli yake baada ya kumuua Simeria.

Dakika iliyofuata, kishindo kikubwa kilisikika kwenye paa la maabara ile na ile roketi ya Unknown ilijitokeza kwa kushtukiza na wakati huohuo, ikijigawa gawa vipande kadhaa. Bawa la kushoto la roketi likachomoka, na la kulia pia. Na katikati ya roketi napo kukaenda mahali pake na yale matairi yake, nayo yakachomoka kwa kasi na kwenda kugonga kioo kikubwa ambacho kilitenganisha maabara ile. Kioo kikavunjika na matairi yale mawili, moja likamfuata Merice na lingine Idris.

Merice na Idris wakajiweka mkao wa mapambano na matairi yale yalipofika karibu yao, waliyakata kwa mapanga fulani yaliyojitokeza kwenye mikono yao. Lakini walifanya kosa kubwa sana kwa sababu matairi yale yalilipuka na kuwarushia mbali na vibaya sana, huku mlipuko ule ukizidi kuvunjavunja chumba kile na kuzidi kusababisha mtafaruku mkubwa mle ndani.

Yale mabawa mawili, yalichomoka pale yalipokuwepo na kwenda moja kwa moja kwa wale wanajeshi ambao walikuwa wamewatinga wakuu wao, na kisha yaliwakumba vibaya sana kuwatupia kwa wakubwa wao. Kisha mabawa yale yalirudi eneo ambapo yalidondokea toka juu, na ile sehemu ya kati ya roketi, nayo ikajiunga na mabawa yale. Baada ya dakika ipatayo moja, roketi ilikuwa imejiunda lakini ilikuwa haina matairi. Sekunde hiyohiyo baada ya kurudi na kuwa roketi, ikajibadilisha kwa haraka na kuwa The Lens, yule roboti mkubwa ambaye walinzi walimfananisha na transformer.

Uzo akiwa chini baada ya wanajeshi wake kumkumba kutokana na msukumo wa mabawa ya roketi, aliweza kumshuhudia Agent Unknown akijitokea kwenye tobo lililotobolewa na roketi yake huku miguuni kavaa viatu ambavyo vilimsaidia kupaa au kutua chini bila kudhurika. Viatu hivyo vilikuwa vinatoa moto mdogo wa bluu (nitro) na ndio ulimfanya Agent aweze kupaa au kutua. Na moja kwa moja, sehemu ya kifuani ya The Lens, ilifunguka na yeye kuingia hapo tayari kwa kuchezesha mwili wa roboti yule.

“Nimerudi.” The Lens aliongea na wakati huohuo, wale wanajeshi wanamichezo wakamakinika zaidi na kukaa mkao wa mapambano.
The Lens akachomoka pale alipokuwepo na kuruka kuwaelekea kule walipo wanajeshi lakini alikutana na upinzani mkubwa wa bomu lililomtupa pembeni bila kuwafikia wale wanajeshi. Wote waliyokuwepo mle ndani, wakatazama ni wapi bomu lilipotokea, ndipo wakaona mkono wa Idris ukijirudi na kuwa mkono wake halisi baada ya kuwa RPG kwa sekunde kadhaa ili kumsambaratisha The Lens aliyekuja kama adui kwake.

“Pumbavu.” The Lens alibwata na kusimama tena wima kwa kutumia nguvu zaidi. Akamtazama Idris, kisha akamtazama Merice ambaye alijiunga naye sekunde kadhaa mbele. The Lens akajitoma kama anayejitoma kwenye bwawa la kuogelea. Na wakati yupo juu, akabadilika na kuwa roketi ya vita na kurusha mabomu kadhaa toka kwenye mbawa zake kuwaelekea Idris na Merice na kusababisha mlipuko mkubwa na wa haja.

“Tutokeni humu haraka sana.”Uzo aliongea na kuanza kujikusanya tayari kwa kutoka ndani ya maabara ambapo kulikuwa kumechafuka kwa mapambano aliyoyaanzisha Unknown. “Jenero, tutoke.” Akabwata baada ya kumuona Jenero akiwa anatizama ile filamu ya kumpendeza machoni mwake na wakati huo, ile roketi ilijibadili tena na kuwa roboti kisha kutua chini mbele ya Merice na Idris ambao walikuwa wameyapangua yale mabomu kwa kuyapiga pembeni na kulipuka huko. Lakini wakati wanaweka akili zao sawa, ndipo wakashtukia, The Lens yupo usoni mwao kujikuta wanapokea makofi mazito yaliyowatupa pembeni kabisa ya maabara ile.

“Hii ndio silaha ambayo nataka kuijenga. Inavutia sana tena sana. Hili wazo tungelipata sisi, tungetisha sana.” Jenero alijiongelea baada ya kuona mbwembwe za The Lens ambaye alikuwa anatoa mambo ya kushtukiza {surprise} kwa wakina Idris.

“Tutoke humu Jenero.” Uzo aliongea na kuanza kumvuta Jenero ili watoke nje.

“Unadhani nani atashinda hii vita?” Jenero akauliza wakati Uzo anamvutia kwenye mlango wa kutokea.

“Jenero twende zetu. Humu si pazuri tena.” Uzo akasisitiza na wakati huo wanajeshi wanamichezo walikuwa mlangoni wakisubiri wakuu wao wapite ndipo nao watoke.

“Hao makemikali wenu, hata waje mia, hawawezi kushinda hiyo zana hapo. Ina kila silaha na kila mbinu zinazohitajika kwenye mapambano.” Jenero akawa anazidi kuongea lakini safari hii tayari alikuwa ametolewa kwenye kile chumba na kubakiza mashine za vita zikipambana.

Idris akainuka tena kama mzimu na mkono wake ukageuka kuwa silaha nzito ambayo ilianza kumtupia The Lens mabomu lakini Unknown ambaye ndiye alikuwa anaendesha lile roboti, alikuwa anayekwepa na kuyapangua yale mabomu kwa ustadi mkubwa na Idris akajikuta anaacha kwanza kumaliza silaha zake bila sababu ya msingi.

“Ndicho ulichobarikiwa kuwa nacho we’ nguruwe mweusi?” The Lens, akamuuliza Idris.

“Hapana. Sina hiyo tu. Nina hii pia.” Idris akaongea na hapohapo akabadilika na kuwa mwekundu sana kama moto mkali unaowaka kwenye msitu mkubwa uliokauka miti yake. Idris akapiga chini kwa mikono yake miwili, mlipuko mkubwa ukatokea eneo lile huku The Lens akirushwa vibaya sana na kutolewa nje kupitia kule dirishani.

Kila alipotaka kujibadilisha na kuwa roketi, ilishindikana na alikuwa anashuka chini kwa kasi ya ajabu sana. Alijaribu tena na tena, lakini ilishindikana na tayari alibakiza sekunde ndogo sana kufika chini. Ndipo alifanya maamuzi ya kuacha mwili wa The Lens na yeye kwa kutumia viatu vyake, akachomoka mle ndani na kupaa juu alipotoka, huku mwili wa The Lens ukijibamiza chini na kusababisha mshindo mkuwa sana eneo lile.

Unknown akarudi kulekule alipotoka na alipoingia tu, akakutana uso kwa uso na Idris ambaye alirusha ngumi moja kali, lakini Unknown aliiona na kuegama kidogo upande mwingine, ngumi ikapitiliza na wakati huo naye Unknown akirusha ngumi yake na kumpiga kisogoni Idris ambaye badala ya kugugumia maumivu, akamtazama Agent kwa macho ya kumsikitikia.

“Usiniangalie kimahaba hapa. Mimi siyo hao wajinga wenzako.” Unknown aliongea kwa kujinadi huku akiingalia saa yake ambayo ndio iliendesha mwili wa The Lens.
Ilionesha kuwa nguvu za roboti yule zilikwisha baada ya kukutana na nguvu zingine za jua kutoka kwenye mwili wa Idris. Na sasa, saa ile ilionyesha kuwa, nguvu imefikia asilimia ishirini ili ijirudi tena upya. “Nitakuua wewe, na kisha nitaenda kuwaua wanajeshi wenzako wanaojifanya wanajua sana kucheza na mipira.” Akaongezea kwenye kauli yake ya mwanzo lakini yote hiyo ilikuwa ni kupoteza muda ili roboti wake arudiwe na nguvu. Alijua wazi kumpiga Idris ni ndoto za kuota unakufa.

“Sina bosi. Na ninakuua leo.” Idris alimjibu Unknown na kuruhusu mkono wake kutoa bunduki ndogo aina ya uzi, na kuanza kumshambulia Unknown ambaye alikuwa anakimbia na wakati huo risasi zikiwa zinamkosa kosa kumpata.
Idris akabadilisha bunduki na kutoa bunduki ambayo ilikuwa na uwezo wa kutoa mabomu na risasi kwa pamoja kama utaruhusu.

Bunduki ile ilianza kutema risasi zake kwa wingi sana Agent alipoona hali imekuwa tete, akajificha nyuma ya jokofu moja ambalo lilikuwa limetupwa pembeni. Akiwa kajificha hapo, alijua hamna risasi ambayo itaweza kutoboa jokofu, ila kuna njia moja pekee ya kuweza kumfikia pale.
Akachomoa bunduki yake ambayo ilikuwa inaning’inia kwapani. Kisha akaifungua na kuiweka sawa tayari kwa uvamizi na wakati huohuo, alisikia bunduki ya Idris ikiwekwa sawa upande wa mabomu. Unknown akajilaza kitumbotumbo na bunduki yake akaielekezea upande mwingine kwa sababu upande wa mbele ulikuwa una jokofu.

Sauti ya kutoka bomu ikasikika kwenye bunduki ya Idris, na bomu hilo lilienda kutua kwenye jokofu, kisha likanyanyua lile jokofu kwenda juu, na kulitupia mbali kabisa na pale alipokuwa kalala Agent Unknown. Na wakati jokofu hilo likinyanyuliwa, Unknown yeye hakuwa na haja nalo na aliachana nalo kabisa. Alirudisha bunduki yake mbele toka kule pembeni na kuweka jicho lake kwenye lens. Akamuona vema Idris akiwa na bunduki yake tayari kwa kuanza tena mashambulizi.

Agent Unknown, akaachia risasi moja na kumkuta Idris kifuani. Akaikoki tena na kumpiga tena palepale na kumfanya Idris arudi nyuma kwa sababu ya misukumo ya risasi zile. Unknown akaikoki tena na kumlenga Idris kwenye kichwa chake lakini ghafla alijikuta akiiachia bunduki yake na kulia kwa maumivu sana. Kisu kidogo kilizama kwenye mkono wake na alipotazama ni nani kafanya yale, alimuona Merice ambaye alianza kujizoa zoa na kuinuka tangu muda ule alipozabwa kofi na The Lens.

Unknown akaanza kukimbilia mlangoni walipotokea Uzo na wenzake huku akivua kata mikono yake na kisha kukichomoa kile kisu na kukitupa pembeni. Akatumia ile fulana yake ya kata mikono kwa kufunga jeraha ambalo alilipata muda ule huku akiwa kajificha nyuma ya mlango. Akatazama saa inayoonyesha nguvu za The Lens, ikawa imeandika asilimia tisini na tano na inaelekea kuwa tisini na sita. Kisha akachungulia kule walipo maadui zake. Akashuhudia Idris akijiminya na kuchomoa zile risasi mbili na matobo yaliyopita risasi zile, yakijifunga na kurudi katika hali ya kawaida.

“Pumbavu hawa. Sijui wanatengeneza majitu ya hivi ya nini,” Agent alijiuliza huku akiwa kaacha kumchungulia Idris. “Zile risasi zilitakiwa zimpige na kumtokea mgongoni. Ila zilibaki mwilini mwake. Sasa kumbe ni liroboti tu nalo hili.” Akamaliza kwa tusi.
Akachomoza uso wake tena na kuchungulia na alishuhudia macho ya Idris yanatoa mwanga wa kijani ambao ulikuwa unapanda na kushuka toka kwenye chumba kile.
 
Back
Top Bottom