Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Ninaona sasa dhahiri kwa nini JR alikabidhiwa kwa Edina kiulaiiniii[emoji23][emoji23][emoji23]

singanojr tupe udambwiudambwi mwingine aisee
 
Ninaona sasa dhahiri kwa nini JR alikabidhiwa kwa Edina kiulaiiniii[emoji23][emoji23][emoji23]

singanojr tupe udambwiudambwi mwingine aisee
Baharia katuacha sehemu mbaya Asee yaani utamu umekuja then umekata........... Napredict huu mchezo umepangwa na mwana mfalme cha pombe anamzunguka baba yake pia kuna Mkono wa kina Abuu , yule mjeshi anayemfukuzia CEO atapigwa na bustwaa atakapoonana ana kwa ana na mkufunzi wao mpya Pluto huko kambini
 
Umepatia robo tu ,Elvi e mjeda atajichanganya huyo na Roma atamuua mbele ya Edna[emoji3][emoji3]
 
SEHEMU YA 43.

DAR ES SALAAM .
Askari waliopewa kazi ya kumlinda mke wa mwamba Roma walikuwa wakiendelea na majukumu yao kwa weledi mkubwa Sana, huku wakitumia mafunzo yote waliyoyapata kutoka kwa eagles.
Siku ya jumatano majira ya saa kumi jioni walimuona mrembo huyu akiwa katika viti maalum vilivyojengwa na kupambwa vizuri mno katika bustani iliyopo nyumbani kwake.wakati wakiendelea kufuatilia ndipo wanagundua Jambo la hatari mno kutoka katika simu ya mlinzi wa nyumbani kwa edna.
"Bro hatukukosea kudukua mawasiliano ya huyu mlinzi"alisema mmoja ya askari wa roma wakati akimuonesha ujumbe ulioingia kwenye simu ya mlinzi huyo."haraka Sana wahi Serena hotel kabla chambo hakijamezwa." "Ukiwa huko usisahau kuwaweka tayari tayari makomando,mie nitabaki hapa kuchunga lindo"alieleza.
Aisee mtunzi njoo uposti hii stori ni nzuri Sana. Tujue mkata was Japan una nini
 
Sas mkuu unatuonjesha tu
 
umetisha sana ,naweka muendelezo baada ya nusu saa
 
SEHEMU YA 43

Dorisi alimuuliza Roma wanatokaje baada ya kutulia, Roma alimwambia amfuate na Dorisi hakubisha alfuatisha nyuma nyuma mpaka wakatokea eneo la mbele sehemu ambayo kwa kushoto kulikuwa na magari yaliokuwa yameegeshwa, na uzuri ni kwamba eneo hili, taa mwanga wake ulikuwa ni mdogo san ana wa rangi ya kijani kiasi kwamba hawakuwwa wakionekana , kwani watu wote ndani ya hili jumba walikuwa wapo upande mmoja.

“Sasa tumekuja kufanya nini kwenye haya magari?” Aliuliza Dorisi kwamshangao.

“Inabidi tuondoke na gari moja”

“Tutawezaje kuondoka bila kushitukiwa nadhani umesikia mwenyewejambazi lilisema linaona kila kinachoendelea hapa ndani tukiwasha gari atajua” Aliongea kwa wasiwasi na Roma alimwangalia na kisha akatabasamu.

“Sikia Dorisi tutatoka na gari bila kuliwasha” Aliongea Roma na kumfanya Dorisi ajiulize inawezekana vipi.

“Roma hakutaka kuendelea kupoteza muda alizunguka upande wa kulia na kuchagua gari ya bei rahisi na akaipata na Roma alijua tu huenda hio gari itakuwa ni ya moja ya wafanyakazi kazi hapa ndani kwani ilikuwa ndio gari ya kawaida, na ilikuwa bahati kwake kwani kioo cha upande wa kulia kilikuwa hakijafungwa vizuri mpaka kufiti juu , na uwazi ulioachwa ulikuwa ukiingiza vidole viwili na Roma hapa alitabasamu na kisha aliingiza vidole viwili kwenye ile sehemu na kuminya kwa nguvu kwenda chini na kioo kile kilianza kushuka kwa mbinde na ndani ya dakika moja tu Roma alikuwa ashafanikisha zoezi hilo la kwanza , na Dorisi alishangzwa na uwezo wa nguvu za Roma.

Roma aliingiza mkono na kufungua mlango kwa ndani na kumwambia Dorisi aingie.

“Utaendesha mimi nitalisukuma mpaka tutoke eneo la nje sawa”

Dorisi alizidi kushangaa , na kujiuliza mtu mmoja anawezaje Kusuma gari , lakini hakutaka kuuliza sana aliingia ndani ya gari na kushika usukani na Roma akaanza kulisikuma kwa nyuma na kweli gari lile lilianza kusogea taratibu na Dorisi alizungusha usukukani na gari ikakaa sawa kwenye barabara na Roma alizidi kusukuma kwenye barabara hio ya Tambarare na gari ilikuwa ikijongea utadhani imewaka na Dorisi licha ya kuwa makini na usukukani kwani kulikuwa na giza na taa hawakuwa wamewasha kutokana na gari kuwa imezima. Aliendelea kuwaza na kujiuliza Roma ananguvu za aina gani.

Baada ya dakika kama tano hivi kupita wlaikuwa washatoka kabisa nje ya uzio na kuingiza gari barabarani na Roma aliacha kusukuma na kuingia kwenye gari , lakini wakati wote Dorisi akiwa anamshangaaa , alikuwa akishangazwa na uwezo wa Roma kusukumba gari peke yake .

Roma alivuta nyaya chini ya usukani na kisha akachomoa nyaya tatu , nyekundu ,Blu una nyeusi , aliunganisha ule mweusi na wa blue na kisha akagusanisha na wa rangi nyekundu gari ikawaka , kitendo ambacho kilimfanya Dorisi aone kama anaangalia muvi kwani mambo kama hayo hakuwahi kuyashuhudia , lakini pia hakuwahi kuwaza kama atakuja kuona mambo hayo yakitendeka laivu.

“Umejifunzia wapi haya Roma?”Aliuliza Dorisi na Roma alitabasamu pasipo kuongea lolote

Baada ya kwenda mita kadhaa mbele Roma alikunja kushoto na kuchukua barabara ya Rami lakini iliokuwa nyembamba kiliko waliokuwa wametoka .

“”Tunaelekewa wapi?”.

“Tunamfuata Tikayi”

“Unajua alikoelekea?”

“Ndio maana naendesha wewe tulia lazima tuwafikie” Aliongea Roma huku akiendesha gari kama mwehu na alionekana haya maeneo kwake ni kama chochocho za mbagala Rangi Tatu , kwani hakuwa na wasiwasi kabisa na Dorisi alikuwa akimshangaa sana na kujiuliza huenda hamfahamu Roma vizuri , inawezekanae mtu kafika leo kwa mara ya kwanza Japani ila anaonekana kama kaishi Japani miaka mingi , ila hakutaka kuuliza Zaidi alitaka kujua mwisho wake.

Baada ya Roma kukata kulia na kushoto hatimae waliingia kwenye kajimsitu na kupita baadhi ya nyumba chache ndani ya eneo lililokuwa likifahamika kwa jina la JPN na kisha akasimamaisha gari na akashuka na hata Dorisi pia.

“Hapa tutatembea , si umali mrefu kutoka hapa na majambazi yalipo?”

“Wewe umejuaje au unafamiana na majambazi”

“Ningejuana nayo nisingekuja huku Dorisi hilo swali ni la kijinga”

Roma aliongoza njia kuelekea mbele , hakutaka kuendelea na gari kwani aliamini lingepiga makelele na kuwashitua maadui.

Baada ya kutembea kwa dakika kadhaa hatimae walikuwa mbele ya jengo kama kiwanda na Roma alimwambia Dorisi kuwa ni hapo na akae nyuma yake amfuate , na ni kweli ile wanasogea mbele waliweza kuonga gari ambayo Roma aliamini kabisa itakuwa ni gari la Tikayi lakini pia kukiwa na magari matatu kampuni tofauti tofauti maawili yakiwa Rangi yeusi yote na moja Rangi nyeupe.

“Vua viatu halafu tembea na vidole”Aliongea Roma akimwamlisha hivyo Dorisi , ili wasipige makele na Dorisi hakutaka kubisha na pia hakuwa muoga , aliamini alikuwa na mwanaume hivyo hapaswi kuogopa kabisa.

Hapa ndani upande wa kulia kulikuwa na manguo nguo yaliokuwa yamerundikwa upande mmoja kwa mbele kulikuwa na dude kama tanki hivi , na kushoto kulikuwa na nyumba ambayo mlango wake ulikuwa ukionekana kwa mbele , taa za mwanga zilikuwa hafifu kidogo , ila zenye mwanga , palikuwa pametulia kimya kiasi kwamba usingedhania hapo ndani kuna watu.

Roma alimwangalia Dorisi nyuma yake na kuanza kumpa ishara za kijeshi lakini mwanamke akawa haelewi , ilibidi Roma aongee nae kwa kuinua mdomo ili Dorisi aweze kusoma lipsi zake na alielewa na Roma alikuwa akimwambia kwamba watumie vidole na watakimbia haraka na kujibanza kwenye ukuta wa kushoto karibu na mlango , baada ya kuhesabu mpaka tatu.

Dorisi alimwangalia Roma na kujikuta akitabasamu na haikueleweka alikuwa akitabasamu nini , ila alijiona kama mwanajeshi wakati huo na hapo wapo kwenye misheni ya kijeshi(Rescue Mission) ya kiuokozi , alijihisi shujaa na kapata kitu cha kwenda kupiga nacho umbea, alipanga kuwaambia marafiki zake namna ambavyo yeye na mpenzi wake Roma Ramoni walivyamua kufanya misheni ya kiokozi kwa ai kumuokoa mtoto wa Tajiri mkubwa ndani ya jiji la Japani… Dorisi alimwangalia Roma na kujiona anafikiria ujinga.

Baada ya kwenda kujibanza kwenye ukuta kushoto , hatimae walikuwa hatua chache kutoka ulipo mlango na hapo Roma alimpa ishara Dorisi na kumwambia atembee usawa wake kwa nyuma na Dorisi alionyesha kidole gumba kuonesha kuwa wako pamoja.

Kitendo cha kuzama ndani tu walikutana na watu waliokuwa wamenyoosheana Bastola lakini jambo ambalo Lilimshangaza ni baada ya kumuona Abuu pia ndani ya eneo hilo na hata kwa Dorisi pia alishangaa…..
 
SEHEMU YA 44

Dorisi na Roma walizidi kushangaa kwa hali iliokuwa hapa ndani , kilichowafanya washangae zaidi ni uwepo wa Tikayeshi na Abuu.

Wakati huuTikayeshi hakuwa tena yule toto jinga aliekuwa akililia mapenzi kama alivyokuwa dakika kadhaa nyuma ,pia hakuonekana kama mpumbavu kama baba yake Yamamoto alivyokuwa ana muita , Dorisi na Roma walimuona Tikayeshi kama mtu anaejiamini.

Upande wa kulia alikuwepo Tikayi akiwa na begi lake vilevile kama alivyotoka Twillght Villa huku upande wa Tikayeshi alikuwa amesimama na Abuu ,Yoshida yule mlinzi ambae Roma alimtambua kwa uwezo wake wa kimapigano kwa kumuangalia tu , lakini pia walikuwepo baadhi ya walinzi wa Mzee Yamamoto ambao wote walionekana wapo tayari kupambana kwa ajili ya Tikayeshi..

Kwa hii hali ya hapa ndan Roma na Dorisi waligundua Abuu yuko upande wa Tikayeshi ,lakini swala walilojiuliza ni vipi akawa upande wa Tikayeshi na ni sababu gani kaamua kufanya hivyo kwani Abuu alikuwa na kiasi kikubwa cha pesa tu hivyo hawezi kutega mabomu ndani ha Twillight Villa kwa ajili ya kupata kiasi cha Yen Bilioni kumi.

"Tikayi umekuwa wa kujifanya mjanja sana na leo ndio utakuwa mwisho wako"Aliongea Tikayeshi huku akiwapotezea Dorisi na Roma kama vile hajawona , walionekana kujiamini kutokana na Sitaha walizokuwa nazo ,lakini pia walionekana kujiamini kutokana na wingi wao na pia waligundua kuwa Dorisi Na Roma wako peke yao baada ga Mlinzi mmoja kutoka na kukagua eneo la nje kujihakikishia kama kuna watu wengine waliokuja nao.

"Tikayeshi nimekufanya nini mpaka unichukie namna hii ya kunipangia njama kwa ajili ya kunidhuru mimi mdogo wako wa damu"

"Tulia acha kuongea unafiki Tikayi , unajua sana nini umefanya kwenye Maisha yangu mpaka ukanifanya kuchukua haya maamuzi magumu , siku zote baba alikuwa ni mwenye kukupendelea na kukuona una akili sana kuliko mimi na akaniita mtoto mjinga bila ya kuutafuta ukweli wote,umekuwa ukinizunguka kwa kila kazi ambayo baba alikuwa akinipatia na kuhakikisha inafeli , ili tu nionekane mjinga na uchukue nafasi yangu ndani ya urithi katika famlia"

Tikayeshi aliongea kwa uchungu sana na jambo ambalo alikuwa akiongea lilionekana kuwa kweli na kwa jinsi hali ilivyo, ilionesha Tikayeshi hakuwa mjinga kama Baba yake alivyokuwa akimuona , ila ilionekana pale ambapo Tikayeshi alikuwa akipewa Jukumu ndani ya kampuni ,Tikayi alikuwa akihakikisha jukumu hilo linafeli , alifanya hivyo ili Tikayeshi aonekane hana akili na hayuco ‘competent’ katika kuongoza kampuni.

Dorisi na Roma walionekana kushangaa , ila walikaa kimya kuangalia Drama hio ya kifamilia waone nini muisho wake ,Katika mapambano hayo ya kugombea urithi.

Kwa Roma hakuonekana kushangaa sana , alionekana kuzoea kuona mambo hayo yakitokea mara kwa mara ndani ya familia za kitajiri ,watoto kugombana mpaka kuana kisa tu kupata urithi , kwake ni mambo ambayo hayakuanza leo wala juzi ni , ni mambo ambayo yalikuwepo tokea enzi za kale na yataendelea kuwepo.

"Hahahahaha.... Tikayeshi wewe ni mjinga na siku zote utakuwa mjinga .. na nikuambie tu mimi mdogo wako nimekuzidi kila kitu"

"Acha kuongea ujinga Tikayi , leo ndio mwisho wako na kauli zako za majigambo nakuua hapa na kampuni itakuwa yangu"

"Huna uwezo huo Tikayeshi .. hauko smart kichwani kama mimi na haitokuja siku ukanizidi akili .. masikini kaka yangu , jaribu kuniua kama una uwezo huo"

Roma na Dorisi walishangaa namna Tikayi alivyoanza kujiamini , lakini pia hata kwa Tikayeshi alishangaa na kupandwa na jaziba maradufu na kupandwa na hasira, yeye alitaka amuone Tikayi akipiga magoti na aombe asimuue lakini hali imekuwa tofauti , kwanini asishangae.

"Mpigeni risasi acheni kuzubaa muda unaenda"

Aliongea Tokayeshi lakini ajabu ni kwamba vijana wake hawakuonekana kusogea wala kunyanyua siraha zao na alishangaa na wakati akiendelea kuwa katika hali yake ya mshangao Yoshida , Abuu na vijana wake wakatoka upande waliokuwa wamesimama na Tikayeshi na kusimama upande wa Tikayi na jambo hilo likawashangaza Dorisi na Tikayeshi lakini Roma akatabasamu.

"Hahaha.. brazaaa.. umejiona sasa ulivyokuwa mjinga , siku zote nimekuwa wakukuambia kuwa hauwezi kunishinda kiakili , angalia sasa ulivyoanguka kwenye mtego wangu .. hahahaha"

Tikayi alicheka kifedhuli na hapa hakuonekana mpole kama baba yake alivyokuwa akimtambua bali alionekana kama muuaji na mtu mwenye roho mbaya sana .

"Yoshida wewe sio wa kunisaliti mimi , Abuu hapana .. hii haiwezekani "

Aliongea Tikayeshi huku akionekana kuchanganyikiwa , alijikuta akiwa peke yake wale ambao alikuwa akiwaamini kama wako upande mmoja walikuwa wamemgeuka ,tena wamemgeuka kwenye wakati ambao alikuwa akiwahitaji sana , alijiona kama mtoto alieachwa katikati ya msitu mnene peke yake ,Bwana Tikayeshi chozi lilimtoka.

"Usijali sana broo .. leo nitakuondoa duniani ili kumpunguzia baba kichwa kuuma mara kwa mara ,maana siku zote umekuwa mzigo kwake"

"Hapana Tikayi naomba usiniue .. tafadhari mdogo wangu naomba usiniue .. nimekosa kuanzia sasa nitaendelea kuwa mjinga naomba usiniue"Aliongea Tikayi akiwa amepiga magoti na kupasha viganja vyake baada ya kuona hali ya hewa imebadilika na chaguo pekee ambalo aliona kwa muda huo ni kupiga magoti na kuomba kusamehewa , ungemuona usingedhania ni yule aliekuwa akiongea kwa kujigamba dakika chache zilizopita , Tikayi alionekana kumzidi mbinu na akili.

"Broo pole sana kwa kuzaliwa mjinga , unawaona hawa wote walikuwa wangu kabla ya kuja kwako na nilichokifanya nikuwapa maneno ambayo yatakurubuni na hata huu mpango niliupanga mwenyewe na nikamtumia Yoshida akuambie huu mpango na ulivyokuwa mjinga ukaufuata alichokuwa anakuambia ,huo ndio ujinga wako na usinilaumu mimi kwa kukuua ,familia yetu haiwezi kuwa na mjinga kama wewe"

Baada ya kuongea hivyo, Tikayi bila ya kumsikiliza kaka yake aliekuwa akiomba msamaha kwa kumkosea, wala kumhurumia alivuta upanga uliokuwa kwenye kiuno cha Yoshida na kisha akamsogelea kaka yake huku akiwa na macho yaliojaa roho ya kinyama na akamfyeka kaka yake kwenye shingo na damu pekee ndio zilizosambaa kwa kuruka na kutapakaa mahali hapa na kila mmoja alishangazwa na roho ya kikatili ya Tikayi.

"PAAA...PAAA ... PAPAPA .."

Roma alinyanyuka kutoka alipoketi na kuanza kupiga makofi huku akisogelea upande waliokuwa wamesimama Tikayi , Abuu na Yoshida na Tikayi aligeuza shingo na kumwangalia huku akionekana hakuwa na hatia hata kidogo ya kumuua kaka yake kifo cha kikatili .

Dorisi alijikuta akijuta kuja na Roma ndani ya hili eneo kwani alikuwa akitetemeka mno , kwa mara yake ya kwanza alikuwa akishuhudia laivu mtu akikatwa kichwa kikatili kwa namna hio , kwake alijiambia tukio hilo ndio la kwanza na ambalo halitakuja kufutuka katika akili yake ,alishindwa hata kuendelea kuangalia maiti ya Tikayeshi na kugeuzia shingo yake pembeni .

"Nishamalizana na Tikayeshi na sasa nimalizane na nyie wawili ,licha ya kwamba sikutaka yafikie hapa yalipofikia lakini sina budi , kutokana na umbea wenu wa kufatilia mambo yasio wahusu leo mmeweza kushudia jambo ambalo hakumpaswa kushuhudia na hio ni tiketi yenu ya kunifanya nisiwaache hai , mngebaki kule Twillght Villa kesho tungesaini mkataba na kumalizana"

“Hongera bwana Tikayi kwa kumuua ndugu yako , sio watu wote wanaweza kufanya hivi”Aliongea Roma na kama kawaida yake hakuwa akitishika na meneno ya Tikati , alifika aliposimama na kisha akampita na kuchuchutama huku akiangalia maiti ya Tikayeshi , aliingiza kidole sehemu ambayo panga lilipita na kama kawaida yake alitoa kidole na kukipeleka puani na kumfanya Abuu na wengine kushangazwa na ujasiri wa Roma.

Baada ua Roma kufanya kitendo chake kiilichowashangaza hawa watu , alinyanyuka na kumuangalia Tikayi lakini ghafla tu Yoshida aliekuwa mita kadhaa kutoka aliposimama Tikayi kwa spidi ya hali ya juu alikuwa ashafika aliposimama Roma na kumzibia Tikayi kwa mbele , huku bwana huyu akionekana kuwa tayari kimapigano.

****

Ni ndani ya mji wa kigamboni saa tatu kamili za usiku Edna leo hii alionekana kusimama nje ya Balconi akiwa ni kisweta chake cha Rangi nyekudu pamoja na pensi huku mkononi akiwa ameshikilia glasi ya kinywaji cha Wine.

Wakati Edna akifurahia upepo wa baharini , upande wa nje ya ukuta ilisimama gari aina ya Noah mita kadhaa kutoka lilipokuwa geti la Nyumba hii anayoishi mrembo Edna , baada ya gari hio kusimama , walishuka watu wanne waliokuwa wamevalia kofia nyeusi aina ya boshori ambazo zilikuwa zimewaziba uso mzima na kubakiza uso tu , watu hawa wanne pia walikuwa na siraha kwenye mikono yao.

Mmoja ya wale watu aliwapa ishara kwa kuwaonyeshea ishara ya Vidole viwili na kuonyesha upande wa kushoto , akimaanisha kuwa wawili wazunguke nyuma ya ukuta upande wa kushoto , eneo hili lilikuwa limetulia kama ilivyokuwa kawaida ya utulivu wa hili eneo , basi mabwana hawa walionekana kutumia nafasi hio vyema.

Wawili waliobaki wakazunguka upande wa kulia mita chache kutoka lilipokuwa geti na kisha walirusha kifaa flani ambacho hakikuonekana vizuri mfano wa chuma kinene na kutua kwenye nyaya za juu za ukuta na kuning`inia na baada ya kufanya hivyo jamaa alimpa ishara mwenzake na wote kwa pamoja wakaruka juu na kutua kwa ndani bila ya kupigisha kelele ya aina yoyote ile na walionekana kuwa wataalamu.

Edna wakati akiendelea kuangalia mandhari ya usiku ya bahari , alijikuta akigeuza shingo na kuangalia upande wa getini na hapo ndipo alipoona watu wakiruka ukuta na moyo wake kupiga paa.

Wakati akiendelea kuwa katika hali yake ya mshangao , majambazi yale yaliinama kwa ustadi mkubwa na kunyata kuelekea upande ilipokuwa nyumba ya walinzi na kwa eneo ambalo Edna alikuwa amesimama , alikuwa akiona vyema kilichokuwa kikiendelea licha ya kwamba taa za eneo la getini zilikuwa zikitoa mwanga hafifu, walinzi waliokuwa eneo la getini ni kama walikuwa wamezubaa kwani ile wanataka kufanya shambulizi walikuwa washafikiwa kitaalamu kabisa na kugongwa shingoni na kulazwa chini na yote hayo yalikuwa yamefanyika kwa wakati mmoja kati ya mabwana wale wawili waliozunguka upande wa kulia na wale waliokuwa wamezunguka upande wa kushoto na wote wakawa wamekutana getini na walikuwa washakamilisha kuwaweka chini walinzi wote wanne waliokuwa wakilinda nyumba ya Edna.

Upande wa Edna ni kama sasa akili yake imerudi na kuanza kufanya kazi kwani alijikuka akijisema.

“Majambazi!!!”Aliongea Edna kwa mshituko
 
SEHEMU YA 45.

Edna ile anataka kugeuka kukimbilia ndani kufuata simu ili apigie polisi mara muda huohuo, bila ya kueleweka imetokeaje , waliingia wazungu wawili mmoja mwanamke na mmoja mwanaume walitokea hewani na wakatua kitaalamu kabisa ndani ya eneo hili la ndani , wale majambazi yaliokuwa yamevalia maski yaligeuka na kushangaa uwepo wa watu waliongia ghafla na kujiandaa kwa mapigano , lakini mabwana hawa walionekana kukosa spidi , kwani ile wananyanyua bastora zao zilizokuwa mikonni walifikiwa kwa spidi ya hali ya juu kabisa na siraha zile zikaenda pembeni na haikuishia hapo tu, walipigwa kitaalamu tumboni na shingoni kwa mapigo ambayo hayakueleweka ni Karate au ni Kungfu kwani walijikuta wote wakiona nyotanyota na kudondoka chini.

Kwa namna walivyodhibitiwa na wazungu hawa ilikuwa ni ya kushngaza kwani spidi iliotumika haikuwa ya kawaida kabisa maana wazungu walikuwa ni wawili lakini wao walikuwa ni wanne na licha ya wingi wao walidhibitiwa ndani ya sekunde mbili tu.

Baada ya wazungu wale kuona wamefanikiwa kuwadhibiti majambazi walibeba wale majambazi mmoja mmoja na kufunfua geti na kutoka nayo nje na hali ikawa imetulia kama kawaida kama hakuna kilichokuwa kimetokea Zaidi ya Derick na walinzi wenzake kuwa katika hali ya kuzimia.

Lakini sasa wakati yote hayo yanatendeka Edna aliekuwa juu ya Balconi aliweza kushuhudia kila kitu , kilichokuwa kimetokea , hakuelewa ni nini kilichokuwa kikiendelea kwa wakati mmoja , alichokifanya ni kukimbilia ndani na kuchukua simu yake na kupigia polisi.

Na wakati huo huo akashuka mpaka sebuleni na kumkuta Bi Wema ambaye hakujua hata nini kilitokea getini kwani alionekana kunogewa na tamthilia ya kimexico ilikuwa ikonyeshwa ITV.

“Miss kuna nini?”Aliuliza baada ya kumuona Edna anashuka mbio mbio.

“Bi Wema kuna majambazi yameingia ila nimeshindwa kuelewa kilichotokea”

“Yako wapi hayo majambazi?” Aliongea kwa kupaniki lakini Edna alishindwa kuongea , woga ulikuwa umemvaa na muda huo huo gari ya polisi iliingia , na ilikuwa imewahi kweli kuliko ilivyokuwa mategemeo ya Edna, baada ya Edna kuona polisi wamefika alijikuta akivuta pumzi ya ahueni.

“Nini kimetokea hapa?”Aliuliza afande aliejitambulisha kama Koplo Juma aliekuwa ameambatana na polisi wenzake watano na Edna alielezea kilichotokea na polisi hawa walishangaa lakini pia waliweza kuamini kwani Derick na wenzake bado walikuwa ndio wanaanza kurejewa na fahamu baada ya kupulizwa na maji ya ubaridi huku wakionekana kuwa na maumivu shingoni.

Kitendo cha Edna kumaliza kuongea namna ya tukio lenyewe lilivyotokea Bi Wema alipata kujua sasa tukio zima na akili yake ikasimama kwenye neno ‘Mzungu’.

Polisi wale baada ya kuona hawakuwa na cha ziada hapo ndani na hakuta uharibifu wowote uliotokea waliaga na kuondoka huku wakiahidi wataendelea kulifanyia kazi swala hilo na kuwatoa hofu.

“Itakuwa ni walinzi wa Roma”Aliongea Bi wema na kumfanya Edna kushangaa.

“Walinzi gani Bi wema Roma kaleta?”

“Jana wakati anaenda kazini aliniambia kama kuna wazungu watakuja hapa niwaruhusu kufanya mambo yao kwani ni maswala ya kiulinzi na akaniambia hakuna haja ya kukuambia lakini nilisahau na pia hawakutokea kama alivyosema”

Aliongea bi wema na kumfanya Edna ashangae Zaidi na kutoka tena nje na kumfuata Derick na kumuuliza kama Roma jana aliacha maagizo yoyote kuhusu kuja kwa wazungu na Derick alisema ndio alitoa maagizo hayo na hapo ndipo sasa akili ya Edna ilianza kufunguka na alijua sasa wale waliowadhibiti majambazi huenda ni Wazungu ambao Roma alileta , lakini swali likabaki kwenye kichwa chake , Roma kawezaje kuleta wazungu.

****

Yoshida alionekana kuwa tayari kupigana na Roma na alichokuwa akisikiliza ni oda ya bosi wake tu , lakini licha ya kuonesha kutaka kupigana kwa Roma hakuonesha mabadilio yoyote na aliishia kutabasamu baada ya kuangalia mwili wa kimazoezi wa Yoshida.

Tikayi hakuwa na wasiwasi na Roma kabisa ,alijua kabisa ataweza kumdhibiti na ndio maana alimpa ishara Abu waondoke na kazi wataimaliza vijana wake.

“Nani kasema mnaweza kuondok?a”Aliongea Roma kwa sauti na kumfanya Tikayi pamoja na Abu wasimame huku Tikayi hakuwa hata na wasiwasi lakini kwa Abu alionekana kuwa na wasiwasi , licha ya kwamba alishawahi kukutana na mziki w a Roma lakini hakuwa akijua uwezo wake halisi.

“Unaonekana kujiamini sana Bwana Roma , lakini ni bahati mbaya kwamba leo hauwezi kutoka mahali hapa pamoja na huyu mwanamke , mmeona mambo ambayo hamkupaswa kuona”

Aliongea Tikayi na ile anamaliza kuongea haikueleweka Roma alimpita vipi Yoshida , kwani tayari alikuwa mbele ya Tikayi , lakini tofauti ni kwamba leo hii macho yake yalikuwa kawaida tu.

“Umekosea sana kutujumlisha kwenye mpango wako , kwanza kabisa nikwambie tu nilikuwa nishafahamu kuna drama iliokuwa ikiendlea kati yako na kaka yako , lakini jambo lililoniuzi ni kuagiza watu waje kutudhuru”

Aliongea Roma huku akiwa siriasi na Tikayi alishangazwa utambuzi wa Roma mapema , lakini muda huo huo kabla hajaongea chochote Yoshida huyu hapa na panga lake linalowakawaka likiwa hewani kama vile kwenye muvi za wakorea akiwa na dhamira ya kumdhuru.

“Romaa.. angalia”

Ilikuwa ni sauti ya Doris akiongea kwa kupaniki baada ya kuona Yoshida anataka kumfyeka Roma na panga lake , lakini ile panga linamkaribia Roma karibu na Tumbo alilishika kwa mkono wa kulia bila ya kujali kama ameshika upande ambao ulikuwa na makali na kisha akalipindisha kwa nguvu kwa spidi ya hali ya juu na palepale panga likakatika vipande viwiwili na kumfanya Yoshida ashangae huku damu zikiwa zinatoka kwenye mikono ya Roma , lakini pia Yoshida hakuwa mzembe kwa kutumia kipande kilichobaki kwa spidi kabisa alizungusha na kupeleka usawa wa shingo ya Roma huku akiwa hewani na ile anafikisha sentimita kama kumi na tano kutoka kwenye shingo ya Roma alijikuta kile kipande kingine kikizama kwenye koo lake na kutokezea upande mwingine , jambo ambalo lilimfanya Dorisi mwili kuwa wabaridi na huo ukawa mwisho wa Yoshida.

Baada ya wale walinzi wengine waliokuwa wamesimama mita kadhaa kutoka mlangoni kuona Yoshida mkuu wao kashakufa waliinua bastoa zao na kuanza kumlenga Roma na hapa ndipo kila mmoja alijikuta akipatwa na kiwewe kwani Roma ni kama alikuwa akijua ni nani anavuta triga na kuachia risasi kwani alikwepa risasi nne kwa ustadi mkubwa sana kiasi kwamba Tikayi hakuamini.

“Nachukia sana bunduki”Aliongea Roma kwa sauti nzito sana kama Roboti huku akiwa ameinamisha uso wake chini na hio ni mara baada ya kukwepa risasi ya tano , lakini sasa sauti yake ya awamu hii haikuwa ya kawaida na kumfanya Dorisi atoe mshangao na kumwangalia Roma , na haikuwa kwake tu hata Abu na wengine wote walikuwa kwenye mshangao.

Roma bado alikuwa ameinama chini vilevile huku mwili wake ukianza kutingishika kama mtu anaepandisha mashetani na hakuna aliekuwa akielewa Roma alikuwa akifanya nini na walianza kushangaa Nguo alizovaa Roma zikianza kuloana huku mwili wake ukitoa mvuke mwingi kama sufuria iliokuwa ipo jikoni.

“Mnashangaa nini mpigeni Risasi”Aliongea Tikayi kwa kijapani huku akianza kupiga hatua kuelekea mlangoni baada ya kuona hapa ndani hapakaliki , lakini kitendo cha kufumba na kufumbua Roma kama jini vile alipotea na kuibukia mlangoni.

“Nani kasema unaweza kuondoka”

Ilikuwa ni sauti nzito sana ambayo ilisababisha mwangwi , yaani Roma aliongea mara moja lakini sauti ilisikika mara mbili katika masikio ya watu wote waliokuwa hapa ndani ,Tikayi ile anainua macho na kumwangalia Roma alijikuta akidondosha begi la hela alilokuwa ameshikilia na hakuelewa mkojo ulitokea wapi kwani alihisi majimaji ya moto yakishuka kwenye mapaja yake na hio ni mara baada ya kushuhudia macho ya Roma yaliokuwa ya kijani huku yakiwa na michirizi ya damu iliokuwa ikionekana kabisa na sio kwa Roma , kila mtu alianza kutetemeka huku mwili wa Roma ukiendelea kutoa mvuke ambao ulisababisha aina flani hivi ya Harufu kama nailoni inachomwa jikoni kwenye moto.

“Paaa.. paaa , khaaa...”

Ilikuwa ni milio ya risasi zilizokuwa zikirushwa kuelekea alipokuwa amesimama Roma , lakini ni kama walikuwa wakipiga hewa kwani hakukuwa na risasi hata moja iliompata Roma zikaishia kwenye mlango na ni kama walikuwa wamepandisha mashetani ya Roma kwani palepale ni kama muvi iliokuwa ikipelekwa mbele Roma alionekana akiwaadhibu wale walinzi kwa spidi sana huku akiwavunja shingo na alitumia sekunde therathini tu walinzi wote walikuwa wapo chini wakiwa hawana uhai.

Dorisi hakuwa akiamini kama mtu aliekuwa mbele yake ni Roma aliekuwa akimjua , mwanaume ambaye alimsababishia hata kudiriki kufanya nae mapenzi ndani ya ofisi , alionekana hakuwa ni mwenye kuamini kile alichokuwa akikiona mbele yake na haikuwa kwake tu Abu na Tikayi walikuwa wamebaki na Bumbuwazi huku suruali zao zikiwa zimeloa kwa mbele walikuwa kwenye woga usiokuwa na kifani na kuzidiwa hat ana Dorisi ambaye hakuonesha woga mwingi ila alikuwa na wasiwasi huku machozi yakiwa yanatiririka kwenye mboni za macho yake.

Roma aligeuka kama Roboti baada ya kumaliza kudili na walinzi na sasa alisogea taratibu kumuendea Tikayi , Roma alikuwa akipiga hatua moja mbele na Tikayi alikuwa akipiga hatua mbili kinyume nyume na ile Roma anaongeza hatua Tikayi aligeuka na kuanza kukimbia , lakini sasa ni kama alikuwa amesahau mlango kwani kule alikokimbia ndio ukuta ulipokuwepo na kufika ukingoni.

Kwa upande wa Abu ni kama alipata upenyo kwani alichomoka kama mshale kuelekea nje na Roma aligeuka na kumwangalia akitokomea lakini hakuwa na habari nae.

“Romaaa…!!”Ni sauti ya Dorisi iliojirudia rudia kama mwangwi kwenye masikio ya Roma na kumfanya ageuke na Dorisi alimwangalia kwa woga na kutingisha kichwa akimuoneshea ishara ya kwamba asifanye anachotaka kufanya na Roma aliongekana kumuelewa na hapohapo mwili wake ulipoa ghafla na mvuke kukauka lakini kiini cha macho yake kilikuwa hakijabadilika.

Roma alimwangalia Tikayi aliekuwa amedondoka chini akitetemeka miguu kwa woga.

“Naomba unisamehe?”

“Ulifikiri ni rahisi hivyo mimi kusamehe”.

“Hapana naomba unisamehe , nitafanya chochote unachotaka”Aliongea kwa pupa huku akipiga magoti kama ilivyokuwa kwa kaka yake.

Roma sasa alionekana kurejewa na fahamu zake za kawainda ,kwani licha ya kwamba rangi ya macho yake ilionekana kuwa ya kijani bado , lakini ilikuwa imefubaa.

“Siwezi kukusamehe kirahisi hivyo , napaswa kukuua hapahapa kwa kuvuka mipaka , sipendi kutishiwa kwenye Maisha yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…