Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Niko na chuma cha MY DREAM MY FAVOURITE
MTUNZI:Singanojr
 
Achia vitu mkuu umeifanya likizo yangu kuwa tulivu
 
NILIEMDHANIA NI KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI:SINGANOJR .
AGE:18+

UTANGULIZI.

NB:SIMULIZI HII NI YA KUTUNGA​

PROLOGUE../DIBAJI

Ilikuwa ni muda wa usiku saa tisa kamili ndani ya chumba kikubwa anacholala mheshimiwa Rais Senga , akiwa amepumzika na mke wake mara simu yake kubwa ya I phone 13 ilianza kuita mfuliulizo kiasi cha kumuamsha na kushangaa ni nani anampigia muda huo kwani sio kawaida yake , na mara nyingi akipokea simu usiku sana huwa ni za dharula na kuna tatizo kubwa ambalo wasaidizi wake wameshindwa kulitolea maamuzi, aliangalia jina la mpigaji na kujikuta usingizi ukimuishia, jina kwenye kioo lilionekana limeandikwa Senior(Mkubwa kazini).

“Senior kuna nini? , maana sio kawaida kunipigia muda huu”.

“Senga ulinihakikisha kuwa Edna atakuwa salama ndani ya taifa lako , lakini nini hiki kinaendelea ndani ya nchi yako”

“Naomba upunguze jazba Senior nini tatizo?”

“Vijana wangu wamenitumia ripoti kwamba Edna alitekwa”

“Nini..!! , unahakika na hio taarifa Senior?”

“Nina uhakika na vijana wangu wangu Senga , nimewapa kazi hio moja tu ya kumlinda Edna kwa siri”

“Vipi hali ya Edna kwa sasa??”.

“Ni bahati kwamba sasa hivi ana mume , kwa hilo namsifia sana , yule mtoto ana akili sana kachagua mume bora”

“Unamaanisha Roma ni mume bora kwa Edna?”.

“Ndio Senga mchunge sana huyo kijana sio mtu wa mchezo mchezo na ni mtu katili kuwahi kutokea katika huu ulimwengu, hakikisha unakuwa upande mzuri na yeye kukusaidia kwenye mpango wako, mimi yangu ni hayo tu na nikwambie Senga haupo makini kabisa Edna anatekwa huna habari , mimi niliopo ng`ambo ya pili ya nchi yako nimepata taarifa kabla yako , nimekasirishwa sana na jambo hili ,Usiku mwema nadhanni tutaongea Zaidi juu ya mipango yetu siku tukionana”Aliongea Senior na kisha kukata simu.

“Who is this Guy?”Alijiuliza mheshimiwa Senga huku akiwa ni mwenye kushangaa Senior anamfahamu vipi Roma.

“ My guess was right he is not normal , there is more hidden info about him , I have to dive deep to discover more details”.Aliwaza mheshimiwa.

Kabla haujaendelea jiulize haya maswali:

Roma ni nani katika hii simulizi , kwanini Senior anasema ni mtu katili kuwahi kutokea kwenye huu ulimwengu?.

Edna ni nani , kwanini Senior anamlinda kwa siri ?”

Senior ni nani na ni mipango gani anayo yeye pamoja na Senga Raisi wa Tanzania.

UTANGULIZI
Roma mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi Tatu anamdhania Edna Kama mwanamke anaejiuza ,baada ya mwanadada huyu kuwekewa dawa ya usingizi kwenye kinywaji na maadui zake katika ulimwengu wa Biashara akiwa ndani ya hoteli na Roma anambeba Edna na kumpeleka Geto kwake na afanya nae mapenzi.

Edna kwa Mara ya kwanza analala na Roma pasipokujitambua na kupoteza usichana wake ,baada ya tukio Hilo anaamua kuolewa na Roma kwa mkataba wa Miezi sita ili kuepuka kuolewa na mwanaume asiempenda ,baada ya Roma kufunga ndoa na Edna anakuja kugundua kuwa mke wake anamiliki kampuni kubwa Nchini huku akiwa na utajiri wa kutisha.

Edna anamuona Roma kama mtu asiyekuwa seriasi na maisha kutokana na aina ya mfumo wa maisha yake ,maisha ya kuwa na wanawake wengi swala linalomkasirisha Edna.

Edna anajitahidi kuweka ukaribu na Roma ili kujua sababu ya mume wake macho yake kubadilika Rangi anapokuwa na hasira na kuwa ya kijani huku akiwa na roho ya ukatili mno

Idara na mamlaka za kiusalama Nchini zinashangazwa na uwezo wa Roma wa kuzungumza Lugha zaidi ya ishirini na mbili na wanaanza kutafuta taarifa zinazomuhusu Roma lakini licha ya kupata taarifa inayoonyesha Roma kusomea ndani ya chuo kikubwa Duniani Cha Harvard wanakosa taarifa zingine zinazomuhusu Roma na kuishia kujiuliza Roma ni Nani haswa

SEHEMU YA KWANZA

Ni muda wa saa moja za jioni ndani ya soko la Mbagala Rangi tatu pilika pilika zilionekana kuwa nyingi sana kwa wafanya biashara , kwani muda huu kwa wafanya biashara wengi ndani ya soko hili ndio muda ambao walikuwa wakifunga biashara zao na kurudi majumbani , hususani wale waliokuwa wakifanya biashara za nguo na vyakula.

Kikawaida ndani ya hili soko wafanyabiashara wengi walikuwa wakihifadhi mizigo yao sehemu salama kwa wale ambao walikuwa na mizigo mikubwa ambayo hawakuwa na uwezo wa kurudi nayo nyumbani , ambao pia hawakuwa na maduka maalumu ya kufanyia biashara , hivyo mara nyingi hulazimika kuhamisha mizigo yao kutoka eneo wanalo fanyia biashara mpaka sehemu ya kuhifadhia.

Kazi hii ya uhamishaji wa mizigo ni kubwa kwa wafanyabiashara hivyo huomba msaada kwa waendesha mikokoteni na wabeba mizigo kuwasaidia kuhamisha huku wakiwalipa kwa kiasi cha mizigo wanayobeba.

“Roma njoo leo unisaidie kubeba mizigo yangu basi nikahifadhi muda umeenda sana” aliongea mwanamama mmoja hivi mweupe wa wastani mnene aliekuwa akifanya biashara ya kuuza madela , vijoli pamoja na viatu vya kike ndani ya soko hili la Rangi tatu.

“Mama Nasra wala hata usiwaze , nitakuhamishia haraka haraka maana nina kazi pia ya kuhamisha na mzee Saidi”.

“Haya mwanangu nashukuru sana”Aliongea mwananamama huyu huku akimuonesha Roma mizigo ya kuingiza kwenye mkokoteni wake kwa ajili ya kwenda kuhifadhi sehemu husika.

Ndani ya dakiika kadhaa tu Roma alikuwa ameshamaliza kazi ya kuhamisha mizigo yote ya kibiashara ya Mama Nasra na kulipwa buku lake na sasa alikuwa bize na kuhamisha mizigo ya Mzee Saidi , ambaye alikuwa ni muuza Viatu vya mtumba.

Uchapakazi na uaminifu wa Roma ulikuwa ukiwafurahisha sana wafanya biashara wengi sana wa soko hili kiasi cha kupelekea mara nyingi kumtaka Roma awasaidie kila linapokuja swala la kubeba mizigo kuitoa sehemu moja kwenda nyingine , alikuwa akifanya kazi kwa haraka sana , kiasi ambacho hata wenzake abao aliokuwa akifanya nao kazi hio hio walikuwa wakimshangaa kwa uwezo na nguvu alizokuwa nazo Roma .

“Kijana Asante sana kwa kuhamisha kwa haraka haraka maana nina dharula”

“Usijali mzee wangu” Aliongea Roma kwa kuweka tabasamu usoni mwake na kisha alipokea noti yake ya shilingi elfu mbili na kisha kuingiza mfukoni.

Mpaka kufikia muda wa saa nne za usiku Roma alikuwa amesomba bidhaa nyingi za wafanya biashara na kwenda kuzihifadhi na sasa alikuwa amekaa kwenye moja ya meza tupu iliokuwa haina kitu akihesabu hela zake.

“Hatimae nimeingiza Elfu kumi na tano , ni kiasi kikubwa sana hiki kwa leo , ngoja nikale ugali na nyama ya Mbuzi kwa mama Joshua nisepe home nikalale”Alijiongelesha Roma huku akinyanyuka mahali alipkuwa ameketi na kusogelea mkokoteni wake na kuuweka pembeni sehemu ambayo mara nyingi anauhifadhi yeye pamoja na wenzake mpaka siku inayofuata .

“Oy mwanaa , leo umepiga kazi sio poa”.

“Kawaida tu Juma , japo ni kweli siku ya leo haikuwa kama jana”Aliongea Roma akiongozana na rafiki yake Juma wakielekea uelekeo mmoja . Juma ni rafiki yake Roma wa muda na walikuwa wakifanya kazi pamoja , utofauti wa Juma na Roma ni kwamba Juma yeye alikuwa ni mwenyeji wa jiji hili la Dar es salaam , akiwa amezaliwa ndani ya jiji hili na Roma alikuwa na muda wa miezi sita tu tokea aingie ndani ya jiji hili la Dar es salaam kutokea mikoani na alikuja ndani ya jiji la Dar kama moja ya vijana wengi wanaokuja kwa kisingizio cha kutafuta maisha.

Roma alikuwa ni mrefu wa wastani , mwenye mwili uliokuwa umejengeka vyema kimazoezi , hakuwa handsome sana wala hakuwa mwenye sura mbaya , alikuwa ni wale wanaume ambao walikuwa wakionekana kawaida sana katika macho ya wengi na moja ya sababu kubwa iliompa Roma umaarufu ni kutokana na uchapaji kazi wake ndani ya soko hili la Rangi tatu.

Baada ya marafiki hawa kuvuka upande wa pili wa barabara hatimae walikuwa ndani ya mgahawa wa Mama Joshua kwa ajili ya kupata chakula cha usiku , waliungana na wenzao wengi waliokuwa ndani ya eneo hilo na kuagiza chakula huku wakiendelea kupiga stori za hapa na pale ili mradi kunogesha maongezi yao.

“Oya Wadau leo Club B kuna bonge la Party , leo ni full bia nusu bei”Aliongea jamaa mmoja mbeba mizigo aliekuwa maarufu sana ndani ye eneo hili la Rangi tatu aliekuwa akifahamika kwa jina la Yusuph.

“Tukitoka hapa lazima tukatembelee eneo hilo, ila hio parti inahusu nini?” aliuliza jamaaa mmoja mwembamba hivi.

“Mrembo Rose leo ni siku yake ya kuzaliwa na kuna bosi anaetoka nae hapa town ndio kaamua kumfanyia bonge la sherehe”.

“Kama ni hivyo hapo ni sawa kwa sisi kwenda kutembelea , au unaonaje Roma “ aliongea Juma akionekana ni mwenye kufurahia tukio hilo linalokwenda kutokea kwani alikuwa ni mwenye kupenda sana kunywa bia hasa zile za ofa.

“Nyie mtatangulia mimi nitarudi Getto kwanza nikaoge then nitaungana na ninyi”

“Ahaaa.. mzee unazingua , hapa hata sisi tutaenda kuoga kwanza ndio turudi kwenye Parti”aliongea Juma na kuwafanya wengine wote wamsapoti.

Naam ni muda wa lisaa limoja tu Juma akiwa ameongozana na Roma walikuwa mbele ya nyumba iliokuwa na geti jekundu Mbagala Biasi pembezoni kabisa na kilipokuwepo kituo cha Tanesko , taa kubwa za kituo hiki ziliwamulika na kufanya waonekane vyema kwa wapiti njia , kwani licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda sana , lakini bado pilikapilika za watu wa eneo hili zilikuwa zikiendelea.

Baada ya kusimama kwa madakika kadhaa hatimae mlango mdogo wa geti hilo ulifunguliwa na mwanadada mmoja mrembo aliekuwa amevalia shungi na kuwakaribisha ndani.

“Najma vipi , ulikuwa umelala mbona umechelewa kfungua mlango?”.

“Hapana nilikuwa chumbani na hata sikusikia” aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake iliokuwa ikisikika vyama na kisha alimwangalia Roma na kumsalimia.

“Roma mambo”

“Poa Naj , habari za siku nzima”.

“Safi tu”

“Oya Roma kajiandae chap tuondoke muda unakwenda wenzetu watatangulia kufika” aliongea Juma ilimradi tu akatishe maongezi yaliokuwa yakiendelea kati ya Roma na Najma .

Najma alikuwa ni mdogo wake Juma , alikuwa akiishi ndani ya nyumba hio ambayo ilikuwa ni yakwao walioachiwa ya urithi , ilikuwa ni nyumba kubwa tu ambayo ilikuwa wameigawa nusu wapangaji na nusu walikuwa wakiishi yeye pamoja na kaka yake.

Najma alikuwa akifundisha shule ya chekechea eneo moja lililokuwa likifahamika kwa jina la Kiramba, licha ya kwamba alikuwa akilipwa ujira mdogo , lakini alikuwa pia akionekana kuipenda kazi yake hio ya ufundishaji.

Tokea siku ambayo Roma anafika ndani ya nyumba yao na kupanga , Najma alitokea kumpenda Roma, Najma alikuwa si mwenye furaha asipomuona Roma , na kutokana na shughuli za kaka yake na Roma kuwa ni za kuwaruhusu kurudi usiku na kudamka asubuhi asubuhi , hivyo mara nyingi alikosa muda wa kuonana na Roma , hali ambayo ilimfanya kuhakikisha kila siku yeye ndio anaewafungulia mlango kila wanaporudi kutoka kazini.

Licha ya Najma kumpenda Roma kwa kaka yake ilikuwa ni tofauti , hakupenda kabisa Najma kujihusisha kimapenzi na Roma kabisa na hii yote ilisababishwa na hali ya kimaisha aliokuwa nayo Roma ,Juma alimuona Roma kama mtu ambaye hakuwa na malengo na maisha yake , hivyo aliona kitendo cha dada yake kuingia katika mapenzi na Roma dada yake asingefika mbali kimaisha na angeendelea kuishi katika hali ya maisha duni jambo ambalo hakuwa akitaka litokee kwani aliamini kwa uzuri aliokuwa nao dada yake , kama ni kupata mwanume mwenye pesa na kumuoa lisingekuwa jambo gumu , lakini asiliolijua Juma ni kwamba ni wanaume wengi sana walikuwa wakikataliwa na Najma licha ya kutaka kumhonga pesa nyingi na hata kumuahidi kumuoa ,mlimbwende huyu alikuwa amekufa na kuoza kwa mwanaume ambaye hakuwa na chochote cha kutishia jamii , mwanaume wa kawaida sana na maskinini mpangaji wao anaenda kwa jina la Roma.

Katika akili ya mwanadada huyu mrembo Najma aliamini siku moja Roma atamtamkia tu kuwa anampenda na yeye pia atamkubali na watayaanza maisha yao pamoja , hio ndio Imani aliokuwa nayo Najma juu ya Roma.

Kwa upande wa Roma alikuwa akijua fika kuwa Najma alikuwa akimpenda sana kimapenzi , lakini pia alikuwa akijua sana kwamba Juma hakuwa akitaka dada yake kutoka na yeye kimapanzi kutokana na hali yake ya kimaisha , hivyo licha ya yeye kumuona Najma kama mwanamke mrembo ambayey yeye kama mwanaume rijali anapaswa kuwa naye katika mahusiano , lakini alijitahidi sana kujizuia kumuonyeshea mapenzi mwanadada huyo , kwani hakuwa ni mtu mwenye kutaka ugomzi na rafiki yake Juma , kifupi alikuwa amependa sana chumba alichopanga ndani ya nyumba hii ya Roma na dada yake.

Basi baada ya Roma na Juma kujiandaa na kubadilisha nguo hatimae walitoka kwa kupitia geti dogo na kisha kutoka ndani ya nyumba hio na kuelekea uelekeo wa Club B , kutoka Bias mpaka ilipokuwa ikipatikana Club B hapakuwa mbali sana , Club hii ilikuwa ikipatikana Chalambe nyuma kidogo kabla haujafika sehemu iliokuwa ikifahamika kama Maji Matitu , ilikuwa ni moja ya Club kubwa sana na ya kuvutia iliokuwa ikipatikana ndani ya eneo hili , lakini pia ilikuwa maarufu sana kiasi kwamba ilikuwa ikitembelewa na watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huu pamoa ambao waliokuwa wakiishi nje ya eneo hili , ikiwemo Chamazi , Temeke , Kisemvule na baadhi ya meneo ya karibu.

“Wadau mmechelewa sana tena Sanaa yaaniii ….. bia ya tatu hii”Aliongea Yusph huku akigida bia yake kwa mbwembwe iliokuwa na chapa la Safari Lager .

“Usijali Yusuph tutakufikia tu “Aliongea Juma huku akiangaza macho huku na kule akikagua mandhari ya hapa ndani na hata kwa upande wa Roma hivyo hivyo.

“Siku hii ya leo watu walionekana kuwa wengi , kwani makelele yalikuwa mengi , huku harufu ya Pombe ikiwa imetapakaa kwa hali ya juu ndani ya eneo hili.

“Handsome Boys karibuni niwahudumie”Ilikuwa ni sauti moja nyororo iliosikika kwa vijana hawa na kuwafanya wamuangalie aliekuwa akiongea na hapo kila mmoa alitoa macho ya uchu baada ya kumuona mwanamke wa haja. Mrembo alievalia suruali ya kitambaa iliomchora vyema umbo lake namba nane , mwanamke huyu alikuwa ni mzuri kweli , si kujaliwa tu shepu lakini pia alikuwa amejaliwa sura nzuri yenye urembo wa asili ambao huwafanya wapenda ngono wengi kummezea mate.

“Aaaaa..hhh Sister Rose sjijatarajia kukuona leo ukihudumia bhana”Aliongea Juma kwa mshangao na kumfanya Rose kutabasamu huku macho yake yote akiwa ameyaelekeza kwa Roma ambaye alionekana kama mtu ambaye hakuwa na habari na mtu aliekuwa mbele yake kwani alikuwa ni mwenye kukagua kila mtu aliekuwepo ndani ye neo hilo kama jasusi anaetafuta adui.

“Mimi nipe Safari kama Broo wangu yusuph hapo , nipe ya baridiii”Aliongea Juma huku akikaa vizuri kwenye viti hivyo virefu huku akiwa amechia tabasamu pana usoni mwake.

“Na wewe Roma vipi leo” Aliongea huku akimwangalia Roma kwa madaha kiasi kwamba wenzake wote walikuwa wakimuonea wivu kwa kuangalia na mwanamke mrembo kama Rose kwa staili hio.

“Nataka ofa leo , nipe Heinken gharama ni juu yako”Aliongea Roma pasipo kupepesa macho na kumfanya Rose atabasamu na kisha kumwambia asijali anamletea na atalipia kwa kila kinywajia atakachokunywa kwa siko hio , jamboa mbalo liliwafanya marafiki zake waone ni upendeleo , lakini wala Rose hakuwajali.

“Oya mwanangu Roma huyu Manzi anakukubali sana kitambo tu , nashangaa mzee huchangamki , au unaogopa ni vya wakubwa”Aliongea jamaa mmoja aliekuwa pembenni ya yuspuh ,jamaa huyu alikuwa akifahamika kwa jina la Samia.

“Kweli kabisa Samia , Manzi anamkubali sana Mwamba hapa , lakini jamaa anazembea zembea , ningekuwa mimi ningekuwa nisharekebisha tayari na hapa ningekuwa nakunywa bia fulu fulu bureeee”Aliongeezea Yusuph na muda huo huo alikuja Rose na kuweka vinywaji huku akimpatia kinywaji Roma.

“ Bebi kuna ,mbuzi choma nikuleteee” wote waliangaliana kwa macho ya kimshangao na ya kutamani kile kilichosemwa , lakini hawakuambiwa wao , mtu aliekuwa amepewa ofa hio alikuwa ni Roma.

“Kweli mama leo umezaliwa upya , kama ni ofa mimi sina tatizo na nipo tayari kwa kila ofa inayopatikana”Alionea Roma .

“Ofa nyingine hautaweza , siku zote umekuwa ni wa kunikimbia” aliongea Rose kwa kumnong`oneza Roma na kumfanya atabasamu , kwani alikuwa akijua alichokuwa akimaanisha Mrembo huyu.

Huu usiku kama walivyotegemea vijana hawa ndio kile walichopata , kwani walilewa chakalii kwa bia za ofa ambazo zilikuwa zimetolewa na kibosile ambaye ilikuwa ikiaminika alikuwa akitoka kimapenzi na mwanadada Rose.

Baada ya masaa matatu baada ya ya keki kukatwa na sherehe kukaribia kumalizika , huku waliokuwa wakiendelea kula mziki na kunywa bia wakiendelea , alikuja jamaa mmoja aliekuwa mhudumu wa hii Club na kumpa kijimemo Roma, ambaye licha ya kunywa bia nyingi alionekana kuwa ngangari kuliko wenzake wote , baada ya kufungua kimemo hiki , alitabasamu na kisha alinyanyuka na kuoelekea nje , na kukata kushoto na ndani ya dakika chache alikuwa nje ya chumba na kugonga , na mlango ulifunguliwa na mrembo Rose aliekuwa amevaa khanga moja tu, alionekana alikuwa ametoka kuoga.

“Karibu Mpenzi”Aliongea Rose kwa namna ya kudeka huku akimvuta Roma ndani na kuzama mzima mzima .
iNAENDELEA HIVI PUNDE .
View attachment 2319976
Shusha nondo mtaalam!
 
SEHEMU YA 40

Roma aliendelea kumshangaa Mage mpaka pale alipowafikia, huku akiendelea kujiuliza maswali ni jambo gani limemleta Mage makao makuu ya jeshi , baada ya Mage kuwafiikia , alisimama wima kama mwanajeshi na kisha akakakamaa mwili maarufu kama kubana ta*ko.

“Jambo Afande , jambo afande ,Ajenti Flamingo kutoka kikosi cha wachawi naripoti”

“Karibu tena Tanzania Ajenti Flamingo”

“Asante sana Afande” Huku akilegeza , huku upande wa Roma akishangazwa na kitendo hiko inakuwaje Mage akawa mwanajeshi ghafla tena ndani ya kikosi cha wachawi.

“Meja naomba niulize kwanza”Aliongea Roma na kuwafanya maafande hawa wamwangalie na kumpa ruhusa .

“Huyu si Mage , polisi namba moja kwa kunichukia hapa Tanzania , mbona ni mwanajeshi?”Aliuliza Roma na Afande Maeda alitabasamu baada ya kuona Mage na Roma washakutana na kisha akamwangalia Afande Tobwe.

“Magreth ni polisi ndio , huyu ni pacha wake anaitwa Magdalena Tobwe ni Special Ajenti kutoka kitengo maalumu cha kupambana na maadui wanaotumia nguvu za giza na alikuwa nchini China kwa miaka minne akisomea mafunzo ya uchawi wa kachina na kijapan”.

“Kwa hio Afande Meada Mage na huyu Magadalena baba yao ni Kanali Tobo?”

“Kijana kuwa na Adabu nishakwambia naitwa afande Tobwe sio Tobo “Kitendo kile cha Roma kumuita baba yake Magdalena Tobo kilimuuzi.

Roma alimwangalia mwanadada huyu ambaye alikuwa akifanana kwa kila kitu na Mage na kisha akatabasamu na kisha akaagana na maafande na kuingia kwenye gari yake kuondoka.

Baada ya Roma kuondoka Afande Maeda alimwangalia Ajenti Flamingo na kisha akamgeukia kanali.

“Ajenti Flamingo wewe ni invicible Solder na kwanzia sasa utakuwa unafanya kazi kwa ukaribu na Pluto”.

“Afande unamzungumzia Pluto gani?”Aliongea Flamingo kwa mshangao na Afande Maeda alitabasamu

“Unaonakena kuwa na habari za kutosha kuhusu Pluto ulipokuwa kwenye mafunzo si ndio?”

“Ndio Afande , nimesikia sana habari zinazomuhusu Mrithi wa Mfalme Pluto Hades , hakuna mwanajeshi yoyote wa kitengo cha uchawi ndani ya China asiemfahamu Hades”Aliongea Ajenti Flamingo huku wakiwa wanaingia ndani ya ofisi.

Na baada ya mkuu wa Afande Maeda kukaa kwenye kiti chake , huku kanali Tobwe alikuwa asharudi kwenye ofisi yake kuendelea na majukumu.

“Okey Ajenti Flamingo , ninachokuambia hapa ni siri za jeshi na wewe kama mwanaeshi unapaswa kutotoa siri hii , hata Raisi amiri mkuu wa jeshi hajui hili ninalokuambia niswala linalojulikana na watu wachache sana ndani jeshi”Alitulia kidogo na kuvuta pumzi.

“Kijana tuliekuwa tumesimama nae hapo nje ni Pluto mwenyewe , ambaye umezisikia sana habari zake”Ajenti flamingo alijikuta akishangaa mno na alionekana kutokuamini maneno ya Mkuu wake.

Naona umeshangaa , lakini pia utakuwa unajiuliza kwanini na kuambia siri hii , nimekuambia kutokana na kujua uwezo wako wa kimapigano , wewe ni komandoo , lakini pia unajua mbinu zote za kichawi na uwezo wako unakufanya kuwa mtu sahihi wa kufanya kazi na Pluto”Ajenti Flamingo alizidi kushangaa .

Ukweli ni kwamba tokea aende kwenye mafunzo kichawi (Cultivation training) nchini china alikuwa akiskia habari nyingi zilizokuwa zinamuhusu Hades au pluto kama moja ya macultivator wakubwa waliovuka steji za juu kabisa za kucultivate.

Pluto na Hades ni majina sawa , Pluto ni jina ambalo miaka ya nyuma mtoto Venetia Burney aliekuwa mpenzi wa kusoma hadithi za Ugiriki alipenda kumuita Hades kama Pluto na kuanzia kipindi hiko jina la Pluto likawa maarufu Zaidi kuliko hades.

Licha ya mshangao wa Ajenti Flamingo na kukubali kazi hio , hakuwa akiamini kwamba mtu aliekuwa akisifika kwa ulozi wa kachina na Japani Mfalme Pluto kutoka jeshi la The Eagles ndio Yule mwanaume aliekuwa hapo nje , akili yake ilikataa kabisa , lakini akajiambia kwenye nafsi yake kwamba ataendelea kulithibitisha hilo kwa kumfatilia Roma kwa kila atakachokuwa anafanya

Ni muda wa saa nane nane hivi , wakati Roma akiwa ameshusha kiti cha gari yake na kuuchapa usingizi ufukweni kilomita chache kutoka lilipokuwa Daraja kubwa la Tanzanite , simu yake ilitoa mlio na aliinua na kuangalia na kujikuta akitabasamu.

“Hehe.. kwa mata ya kwanza Edna kanipigia” aliiongelesha Roma huku akipokea simu baada ya kuona jina la ‘My Wife’ kwenye kioo.

“Ndio wife , usiniambie umenimiss mume wako?”.

“Uko wapi?”

“Ufukweni bebi”.

“Njoo tukutane My World Fashion Mall pale”Na simu ikakatwa, Roma alitabasamu huku akifikiria ubabe wa mke wake , ila hakujali sana aliwasha gari na kisha alielekea lilipo jengo refu sana ndani ya Posta lililokuwa likifahamika kwa jina la My World Fashion Mall

Roma ndani ya madakika kadhaa tu alikuwa ashafika na nikama walikuwa wameambizana , kwani wakati Edna anaegesha gari na Roma alikuwa akiingiza gari maegeshoni, alisimamisha na kufungua mlango na kisha akamrushia ufunguo Valet(mtu uanaehusika na kupaki magari) na kumsogelea Edna.

“Bebi hapa tumekuja kufanya nini?”Edna hakujibu Zaidi ya kutangulia na Roma alimsogelea na wakaingia kwa pamoja na kama kawaida watu wengi wlaikuwa wakimshangaa Edna kwa uzuri aliokuwa nao , kuna waliokuwa wakimjua kama mfanyabiashara mkubwa , lakini pia kuna ambao hawakuwa wakimjua.

Edna hakuwa mtu wa kupenda sana kunyionyesha kwenye mitandano na vyombo vya habari , hakuwa hata na akaunti yoyote katika mtandao wa kijamii na ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu na hata mara nyingi kama tu atasaini mkataba ambao utahusisha waandishi wa habari mara nyingi Dorisi ndie aliekuwa akimuwakilisha , hivyo ndani ya Tanzania imemfanya kutotambulika sana licha ya kuwa mwanamke ndani ya taifa mwenye pesa nyingi kuliko mtu yoyote.

Baada ya kuingia kwenye duka moja kubwa ambalo lilikuwa limesheheni nguo za kiume , Edna alianza kupita taratibu upande wa suti na alionekana alikuwa akichagua , huku wafanyakazi hapa ndani wakionekana kutoa heshima kubwa kwa Edna.

Aliangalia baadhi ya suti karibia zote za Brand tofauti tofauti za ndani ya nchi na nje ya nchi na kila aliokuwa akivutiwa nayo aliinyoshea kidole na mfanyakazi wa hapa ndani alichomoa na kuishika mkononi.

Wakati huo Roma hakuwa na habari kwani alikuwa amekaa kwenye masofa , akimwangalia mke wake na kutabasamu , baada ya dakika kadhaa Edna alikuja akiwa amebeba suti na mashati mpaka alipokaa Roma.

“Kajaribu hizi nione zinakaaje kwenye mwili wako”Aliongea Edna kama kawaida na sura yake ya usiriasi.

“Bebi kwakua umezichagua wewe zitanipendeza haina haja ya kujaribu”

“Nimekuambia kajaribu”

Roma aliinuka huku akiangalia baadhi ya watu waliokuwa na wapenzi wao wakiwaangalia , na Roma alijua tu kuwa walikuwa wakimwangalia mke wake alivyokuwa mzuri.

“Kaka una mke mzuri , ukimsaliti utaonekana kichaa kaka , mchunge sana”Aliongea jamaa mmoja ambaye na yeye alikuwa akibadilisha.

“Jua mambo yako braza”Aliongea Roma huku akimpita na kwenda kubadilisha.

Walitumia takribani nusu saa ya kununua nguo viatu na saa .

“Bebi hivi vyote vya nini sasa?”

“Ni vya kwako na kesho utavaa hii na hii nyingine tukienda kwenye kusanyiko la wafanya biashara”Alionyesha moja moja.

“Kusanyiko la wafanyabiashara , mbona sijui kama tuna ratiba ya kwenda kwenye kusanyiko la wafanya biashara”

“Ndio nakuambia , ukisharudi inabidi nikakutambulishe kwa wafanyabiashara wenzangu”

Lakini wakati wakiwa wanaendelea kuongea , mara aliingia mwanadada mwingine hapo ndani akiwa ameongozana na mabaunsa kama manne hivi na kufanya hali ya hewa kubadilika kwani watu wote waliwakodolea macho.

“Donyi Donyi”Aliita Roma mara baada ya kumuona mwanamke aliekuwa mbele yake ni yule aliekutana nae siku kadhaa nyuma ufukwen, sasa Roma alimwita huyu mwanadada lakini huyu mwanadada ni kama hakuwa amemuona vizuri Roma na ile anageuka vizuri kumwangalia Roma alijikuta akipatwa na mshangao na kumkimbilia Roma na kumvaa mzima mzima mwilini na kumkumbatia , kitendo ambacho kilimfanya Edna na baadhi ya watu waliokuwa hapa ndani washangae , ikiwemo yule bwana aliempa ushauri Roma dakika chache nyuma.

Roma mwenywe ni kama tukio hilo kwake lilikuwa ghafla sana kwani alishindw akulizuia na aliona Donyi kaharibu Zaidi alivyoanza kumbusu mashavuni.,Roma alimwangalia mke wakena kumuona akianza kukunja sura kwa hasira na Edna alichukua mkoba wake na kupiga hatua kuelekea nje , huku akiona aibu , kwani aliona kitendo kile kimemdharirisha mbele ya watea waliopo hapo ndani kwani ni dakika chache nyuma tu walionekana kama mume na mke kweli lakini dakika kadhaa mbele kila kitu kimebadilika na mchepuko kwa Roma amemvaa.

“Sema wanaume hawajahi kuridhika , kwa jinsi yule mrembo alivyomkumbatia yule kaka ni lazima ni wapenzi”Aliongea mwanadada mmoja aliekuwa pembeni akilipia nguo alizonunua

“Tokea tulivyoachana nilishindwa kulala , kabisa nimekuwa nikikufikiria kila dakika kila sekunde kila saa , niliilaumu sana kwa kusahau kuchukua namba yako”Aliongea Donyi na kuzidi kumchangaynya Roma , alimtoa kwenye kifua chake na kisha akamwangalia.

“Donyi naomba nimuwahi mke wangu kwanza na naomba Mungu asije kutukutanisha tena”Aliongea Roma na kujitoa kwenye mwili wa mrembo huyu na kisha akachukua nguo walizonunua na kuwahi nje , lakini alikuwa amechelewa kwani ile anatoka aliona gari ya Edna ikitokomea nje kabisa ikiingia barabara kuu.

****

NEW YORK

Ni ndani ya chumba cha hoteli katika floor inayohudumia VVIP alionekana The First Black akiwa ameketi kwenye masofa ndani ya chumba hiki , huku mbele yake kukiwa na mwanaume mwingiene wa kizungu mwenye umri kimakadirio kama miaka arobaini hivi , aliekuwa amevalia suti na shati la blue na tai nyeupe .

Bwana huyu alifungua mkoba wake mweusi aliokuwa ameuweka pembeni na kisha akatoa picha na kumpatia mheshimiwa Mstaafu na Mheshimiwa alizipokea zile picha na kuanza kuangalia moja moja pasipo kubadili muonekanao wake , baada ya kuridhika na picha zile aliziweka kwenye meza ya kioo na kuinua macho nyake kumwangalia huyu bwana.

“Futeni Ushahidi wote , ambao unaweza kumfanya akafahamu ukweli , hakikisheni anajua kile ambacho tunataka sisi akijue na sio Zaidi ya hapo”Aliongea The first black huku akiangalia picha iliopo mezani , ni picha ambazo zilikuwa zikimuonesha Roma akiwa na Edna na picha hizi kwa haraka haraka zilionekana zilipigwa siku ambayo Roma na Edna walienda kusajili ndoa yao Bomani.

“Sawa mheshimiwa ila Mr President anataka nyaraka zote ambazo zinahusiana na Project LADO , maana kwa taarifa tulizonazo mpaka sasa inaonesha Urusi inataka imshawishi Agent !3 kujiunga nao , jambo ambalo kama litafanikiwa itakuwa hatari kwa upande wetu”.

“Kuhusu mikataba ile , nitakaa nayo , naelewa ni mali ya taifa , lakini mpaka sasa sina ninaemuamini nitaongea na Mr President mimi mwenyewe na kumuelewesha juu ya hilo , kuhusu Agent 13 acheni shaka kabisa , hawezi kujiunga na upande wowote, kabla ya kwenda Tanzania alisaini ‘The Gods Treaty’ na huu mkataba unamtaka kuwa Neutral , ninachowaasa ninyi kama CIA hakikisheni hamfanyi jambo lolote la kijinga na akafahamu kama mnafuatilia , itakuwa hatari kwenu na kwa taifa”Yule mzee alishangaa kidogo , lakini hakuweza kuongea chochote.

“Rogani Project LADO ilitugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa na mpaka sasa mimi ndio mkuu wa Project hio , hivyo Raisi kusema kuwa anataka nyaraka ni swala ambalo haliwezekani , licha ya kwamba nchi yetu iliwekeza sehemu kubwa kuliko taifa lolote , lakini bado Project LADO ni ya kimuungano”

“Nimeelewa mheshimiwa na sisi kama CIA tutakaa mbali na Hades”The First Black alitabasamu na kisha alinyanyua glass ya wine na kunywa kidogo.

“Itakuwa vyema sana kama utawaweka vijana wako under Control , labda nikudokezee tu Project LADO inaendelea na sasa tupo kwenye Testing Phase(Hatua ya majaribio)

Rogani alionekana kumuelewa vizuri mheshimiwa na hakutaka kuongea neno lolote kumpinga The First Black.
 
SEHEMU YA 41

Ni siku nyingine kabisa , siku ambayo Roma alikuwa akielekea nchini Japani kwa ajili ya kumuwakilisha mke wake katika dili nono kati ya kampuni ya Yamakuza , Vexto na JR , ni muda wa asubuhi kabisa saa mbili kamili Roma alikuwa ashajiandaa kwa kila kitu na kilichobaki ilikuwa ni kuelekea nchini Japan.

Edna alishuka kutoka kwenye chumba chake akiwa tayari ashajiandaa kwa ajili ya kumsindikiza Roma mpaka uwanja wa ndege, baada ya wawili hao kuungana huku Edna akionesha ukauzu wake kama kawaida mbele ya Roma ,alitangulia na kuingia kwenye gari yake ya Mercedenz aliokuwa akipendelea,na Roma na yeye akaingia na Edna kama dereva alitoa gari hio taratibu na wakatoka nje ya Geti na kuingia barabarani.

Muda mchache tu walikuwa washafika ndani ya uwanja huu wa ndege wa JNIA ,Doris alionekana kuwahi , kwani alikuwa ashafika tayari na alionekana alikuwa akiwasubiria , alikuwa amependeza kama kawaida kuzidi wanawake karibia wote walikuwa ndani ya uwanja huu wa ndege na kufanya baadhi ya wanaume wamkodolee macho.

Wakati wanaendelea kuongea , mara walisogelewa na watu wawili , mmoja akiwa ni mwanaume na mwingine alikuwa ni msichana mrembo hivi alievaaa akapendeza na hata kwa mwanaume alikuwa amependeza pia.

“Naitwa Isack Bathomayo ,Assistant CEO kutoka JR Group na huyu ni Sasha sekretari wangu na mpenzi wangu ”Aliongea bwana huyu kwa kujitambulisha na kuwafanya Dorisi , Edna na Roma kushangaa na Roma alijikuta akitukana matusi ndani kwa ndani Abuu , alikumbuka ile siku ambavyo Abuu alivyokuwa aking`ang`ania Edna aende huku akisema ni masharti kutoka kwa Yamakuza , lakini leo hii alikuwa ametuma muwakilishi alijua yote yale yalikuwa ni mipango yao na anashukuru aliifahamu mapema .

Edna alimwangalia Roma kwa kuibiaibia na Dorisi pia alimwangalia Roma na hawakutaka kuongea mengi ,Edna aliwapa maelekezo ya kuwa makinni katika kusaini mkataba huo na kisha wakaagana na ndani ya madakika kadhaa tu ndege ya Emirates iliapaa kuelekea Japan.

Kwenye ndege hakukuwa na maongezi mengi sana , kwani Dorisi alilala mapema sana , aliekuwa macho alikuwa ni Roma ambaye alikuwa akiwakagua wahudumu wa ndege kila aliekuwa akija kumhudumia ndani ya daraja la Kwanza la wafanyabiashara.

****

KANSAI -INTERNATIONAL AIRPORT,JAPAN

Saa kumi na moja kamili za Asubuhi Ndege ya shirika la Fly Emirates iligusisha taili zake ndani ya uwanja wa kimataifa wa Kansai ndani ya jiji hili la Osaka.

Osaka ni moja ya miji mikubwa sana ndani ya Japani ni mji ambao ni mzuri sana kutokana na uwepo wa safu za milima ndani ya jimbo lote la Honshu, na ni sehemu pekee ambayo watu wengi wanaosafiri kwa ajili ya kutalii hupendelea sana kufika.

Osaka ni maarufu sana kwa raia wake kuishi watakayo , lakini pia upatikanaji wa aina nyingi ya vyakula na hili lilivutia sana watu na kwa kwa kiasi Fulani unaweza kuufananisha mji huu na Los Angels Marekani. Kutokana na mazingira yake na pia namna watu wanavyokula bata ndani ya hili jiji.

Muda huu wa Saa kumi na moja Roma , Dorisi pamoja na wafanyakazi wawili wa JR Grupu walikuwa washakamilisha taratibu zote na sasa walikuwa wakitoka nje ya jengo hili la kufikia wageni , baada ya kutembea na kufika nje sehemu maalumu kwa ajili ya kupokelea wageni , hatimae waliweza kumpata mwenyeji wao ambao alikuwa amekuja kwa ajili ya kuwapokea baada ya kuona bango la JR na Vexto likiwa limeshikiliwa na kijana mmoja wa Kijapani ambaye alikuwa amesimama na bwana mmoja ambaye alionekana kibosibosi kutokana na aina ya mavazi yake, alikuwa amevalia Navyblack suti ambayo ilionekana kuwa ya bei kubwa , pamoja na saa kampuni ya Brand ya Radeon.

“We’ve been expecting you, friends of Vexto and JR Group . I’m Yamakuza Corporation’s Vice-CEO, Tikayi . My father, Yamamoto was unable to make the trip down due to sickness, so I am welcoming you on his behalf, and also express his apologies.”

“Tulikuwa tukiwasubiria ndugu zetu kutoka Vexto grupu na JR grupu , mimi ni CEO msaidizi wa Kampuni ya Yamakuza naitwa Tikayi , baba yangu ameshindwa kuja kuwapokea kutokana na maradhi yake na nipo hapa kuwakaribisha kwa niaba yake , na niombe Radhi kwa kutokuwepo kwake”:Aliongea Tikayi kwa kingereza safi.

“I never expected to be received so warmly, sorry to make you wait”(Sikutarajia mapokezi haya ya kikarimu tusamehe kwa kukufanya usubiri kwa muda mrefu” aliongea Doris .

“Tunafurahi kukufahamu bwana Tikayi , Niite Roma ni mkalimani kutoka kampuni ya Vexto”Aliongea Roma na kumpa mkono Tikayi na bwana huyu akatabasamu

“Nilikuwa nikisikia taarifa Tanzania kuna wanawake warembo nadhani leo ninaamini fununu hizo ni za kweli”Aliongea na Dorisi alitabasamu , ila Roma hakupendezwa na namna ambavyo Tikayi alikuwa akimwangalia Doris.

“Ni kweli kabisa bwana Tikayi ,Tanzania imebarikiwa na kuwa na wanawake warembo ila wanapendelea wanaume wenye mashine kubwa sio kama wajapani na vipenseli vyenu”Aliongea Roma kwa Kijapani na kumfanya Tikayi akunje sura , kwa dakika na kisha akatabasamu , huku Dorisi na wenzake wakishangaa ni nini Roma alimwambia mkaka wa watu mpaka akakunja sura.

Basi waliongozana na kuingia kwenye magari mawili yote yakiwa ni Caddillac limousine ambayo yalikuwa yameandaliwa kwa ajili yao na kisha wakatoka nje kabisa ya uwanja huu wa Ndege.

Jiji lilionekana kuwavutia sana Doris na wafanyakazi wa JR kweli , kwani walikuwa wakishangaa miundombinu na kujikuta kutabasamu bila kupenda, majengo ya Japani hayakuwa yameenda hewani sana , lakini yalikuwa yakipendezesha mji kutokana na mpangilio.

Ndani ya dakika chache walifika ndani ya eneo moja lililokuwa likifahamika kwa jina la Ashiya , hii ni sehemu ambayo inaishi matajiri wengi ndani ya Osaka na ni sehemu ghari sana kupata nyumba ya kuishi ndani ya eneo hilo ni kama hapa Tanzania useme Osterbay ndio ilivyokuwa kwa Ashiya.

Sehemu hii ilikuwa katikati ya Kobe na Osaka , na upande wa kushoto kulikuwa na fukwe ambayo ilizidi kupendezesha eneo hili.

Doris alionekana kupenda sana hili eneo na alishindwa kuzuia furaha yake na kumwangalia Roma aliekuwa pembeni yake na kutabasamu.

Upande wa Roma hakuonekana kushangaa sana , ila alionekana kama ni mtu ambaye alikuwa akikumbuka mambo mengi sana ya nyuma akiangalia maeneo haya.

Dakika chache mbele gari zote mbili zilikuja kuingia ndani ya kizuizi kilichokuwa kikipakana na barabara upande wa kushoto.

“Imekuwa heshima kwetu sana kufanya kazi na Kampuni kutoka Tanzania na kwasababu ya hilo tumeona ni vyema mkiishi kwa muda wote mtakaokuwepo hapa japani ndani ya Twillight Villa ya kifamilia”Aliongea Tikayi kwa kingereza na Dorisi alitabasamu na kisha akasema ‘Thank you’.

Hii sehemu ilikuwa nzuri mno na ilikuwa ikiendana na sifa ya eneo hili kuitwa sehemu wanayoishi matajiri , licha ya ukubwa wa eneo hili lakini pia unadhifu wake ulifanya kuvutia sana , bustani zilikuwa zimejengewa kwa ustadi mkubwa na miti yake mirefu ya wastani aina ya Italian Cypress Tree ilizidi kupendezesha macho.

“Karibuni Sana”

“Asante” Alijibu Doris huku akivuta pumzi ya hewa iliokuwa ikinukia ndani ya eneo hili , na mbele yao kulikuwa na jengo ambalo lilikuwa limejengwa kwa muundo wa Nyota , lilikuwa ni jengo kubwa na la kuvutia sana , kwa mbele kulikuwa sanamu la Samurai lililokuwa limejengwa na kunakishiwa kwa madini ya Dhahabu na kufanya sehemu hii kupendeza Zaidi.

Wakati wakiendelea kushangaa , uzuri wa hili eneo ziliingia gari mbili za kifahari MBW 7 na kwenda kusimama mita kadhaa kutoka walipokuwa wamesimama na akashuka mzee mmoja hivi makadirio ya miaka sabini hivi akiwa na fimbo ya kutembelea na akawasogelea huku akiwa ameweka tabasamu pana usoni.

Aliwasalimia kwa ukarimu sana na kuwakaribisha Japani ,Mzee alikuwa akiongea vizuri kingereza kwa rafudhi nzuri tofauti na Tikayi , huyu mzee ndio anafahamika kwa jina la maarufu la Yamamoto na ndio alikuwa mmiliki wa kampuni ya Yamakuza na pia alikuwa Tajiri mkubwa ndani ya jiji hili.

“Mr Vice ni muda gani mazungumzo yetu ya kibiashara yataanza?”Aliuliza Doris na alionekana alikuwa akitaka mazungumzo ya kibiashara yaanze wamalize ili wajue mambo mengine

“Miss Doris , please rest assured, you’re all fatigued from the flight today, so please rest at our Villa for hours My father and the others would also relax, and we will only begin the talks Tomorrow. Then, there will be two days of visits to the research facility, and exchanges with the researchers. Then, we will draft up a collaboration document.”

Hapo akimaanisha kwamba wapumzike kwanza ndani ya nyumba hio kwa masaa kadhaa kuondoa uchomvu unaotokana na safari na kesho wataanza maongezi ya kibiashara halafu baada ya hapo watatembelea taasisi ambazo zinahusika na utafiti wa Material hayo mapya na pia mabadilishano ya watafiti halafu watakaa mezani kwa ajili ya kujadiliana juu ya makubaliano ya pande zote .

Kwa mtiririko mzima wa kikazi itawachuku jumla ya siku tatu kukaa ndani ya nchi hii ya Japani na Doris alitabasamu , aliona atapata wasaa mwingi wa kukaa na Roma na kufurahia Maisha.

“Roma ushawahi kufika Japan?” Aliuliza mzee Yamakuza na Roma alimwangalia na kutabasamu na kisha akasema hakuwahi kufika , ila ukweli Roma kwenye moyo wake alikuwa amekuja ndani ya Japani mara kibao na mara zote alizoingia ndani ya hili taifa ilikuwa ni kwa kazi maalumu.

“Waheshimiwa mnaonaje kwanza tukiachana na maongezi na mkafanya mpango wa chakula maana nahisi njaa sio ya kawaida” Aliongea Roma mara baada ya kuona mzee huyu alikuwa bize kuongea na Dorisi juu ya umaarufu wa Japani na mambo yake ya kipekee yanayopatikana na Roma mambo hayo yalimchosha maana kwake hayakuwa na maana.

Msosi uliandaliwa baada ya mzee huyu kuwapa ishara wafanyakazi wa hapa ndani na ndani ya madakika kadhaa tu Meza ilichafuka kwa aina mbalimbali ya mapishi . jambo ambalo lilimfurahisha sana Roma.

Baada ya kupata chakula ambacho haikueleweka ni chakula cha asubuhii au cha mchana , Roma na Doris na wale wapenzi kutoka JR grupu walionyeshwa sehemu zao za mapumziko.

Dorisi na Roma kama kawaida walipewa chumba kila mmoja cha kwake , lakini waliishia kuwa ndani ya chumba kimoja na kuanzia asubuhi mpaka muda wa jioni ilikuwa ni kukiamsha na hata chakula cha mchana walikula humohumo.

Saa mbili kamili za jioni Roma , Dorisi na wale wapenzi kutoka JR walitoka kwenye vyumba vyao mara baada ya kuitwa na wahudumu kwa ajili nya chakula cha usiku , na walijikuta wakishanngaa mara baada ya kukuta watu wengi waliokuwa kwenye meza tofauti na ilivyokuwa asubuhi.

Baada ya kuketi kwenye nafasi ambazo walionyeshwa na wahudumu , Mzee Yamamoto alianza kuwatambulisha kwa wageni hao waliokuwa wanaonekana kuvaa mavazi ya suti na hapo Roma na Dorisi ndipo walipowatambua kuwa hao ni moja ya wafanyakazi wakubwa wa kampuni ya Yamakuza na wamealikwa kwa ajili ya chakula cha jioni kama sehemu ya kujipongeza katika mafanikio ya kuelekea kusaini mkataba kati ya Yamakuza na Kampuni mbili kutoka Afrika.

Msosi wa nguvu uliandaliwa , jambo ambalo lilimfurahisha sana Roma kiasi cha kutoa tabasamu, wageni hawa walitoa mshangao mara baada ya Roma kuanza kula bila habari , kwani wote walikuwa hawajaanza na ni kama walikuwa wakisubiria kukaribishwa na mzee Yamamoto , ila wakati wao wanasubiria Roma yeye alikuwa tayari ashaanza yake na hata Dorisi alimshangaa Roma ila aliishia kutabasamu na hata kwa mzee Yamamoto aliishia kutabasamu na ilibidi wote waanze kula.

Wakati wanaendelea kula mara aliingia bwana mmoja ambaye alikuwa amevaa suti lakini kwenye mfuko wa suti yake kukiwa na kibango kidogo kilivhokuwa kikionesha nafasi yake ya kazi ndani ya nyumba hii yaani ‘House’ Meneja na kumsogelea mzee Yamamoto na kumnong`oneza jambo na mzee huyu aliweka vijiti(chopstick) vyake alivyokuwa anatumia kula.

“Huu ni ujinga” Aliongea kwa sauti na kwa hasira na kufanya waliopo hapa ndani washangae.
 
SEHEMU YA 42

Kila mmoja alishangaa kwanini mzee huyu alipandwa na jaza ghafla namna hio mara baada ya kunong`onezwa jambo na muhudumu wa nyumba.

Tikayi aliekuwa amekaa pembeni na baba yake alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa ni kama mtu ambaye alikuwa akijua ni taarifa gani baba yake ameambiwa.

Na wakati wakiendelea kujiuliza ni kwanini mzee Yamamoto kapandwa na Jazba mara aliingia bwana mmoja mkumkukuku , bwana ambaye alikuwa amevalia shati lake rangi ya maua maua na suruali ya Jeans.

Bwana huyu ukimwangalia mara moja tu utagundua kuwa Tikayi na huyu bwana ni ndugu kimuonekano, jamaa huyu baada ya kuingia alijikokota na kudondoka kwenye miguu ya Yamammoto na kisha akaanza kulia kwa sauti na alionekana kulewa pia , jambo ambalo lilifanya hali ya hewa kuwa mbaya.

“Wu.. baba .. ninafanya nini mimi.. aaaaaah Dina kaniacha baba ..iiii .. Dina..weeee… aaaa”

Jamaa alikuwa akilia mpaka anatema mate kitendo kilichozidi kumkasiriasha mzee Yamamoto na alichokifanya ni kumpiga teke na akadondokea upande mwingine , lakini huyu bwana aliamka tena na kukamata mguu wa baba yake na kuanza kulia tena huku akiwa anamtaja mwanamkie anaeitwa Dina akilalamika ameachwa , na kila mmoja aliekuwa hapa ndani alikuwa ashajua ni nini kinaendelea kwa huyu bwana, walijua yote hayo ni sababu ya kimapenzi. Na bwana huyo alikuwa ameachwa.

“Jamani naomba mniwie radhi kwa jambo hili , huyu ni mwanangu mkubwa Tikayeshi , lakini licha ya kuwa mkubwa katika familia , ndio mpumbavu kuliko wanangu wote”Aliongea mzee huyu wa kijapani huku macho yake yakiwa mekundu kwa hasira.

“Hakuna shida mzee ni jambo la kawaida kwa vijana” Aliongea moja ya wafanya kazi wa kampuni na mzee huyu aliwapa ishara walinzi wamtoe eneo hilo na bwana huyu alikokotwa na kutolewa huku akiendelea kulia kwa sauti kama toto jinga , na kwa kumuangalia tu ungejua kuwa ni sahihi kwa mzee Yamamoto kumuitwa Tikayeshi mtoto mpumbavu kuliko Watoto wake wote.

Tikayi alionekana kutabasamu na kufurahishwaa na tukio hilo , ali mwangalia baba yake alivyokuwa na hasira na kuridhishwa na hali hio.

Basi baada ya chakula wageni wale walitawanyika na hata kwa Mzee Yamamoto waliagana na Roma na kuwatakia usiku mwema huku wakiwaahidi kuonana keshi kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara.

Roma aliingia kwenye chumba chake na hata kwa Dorisi hivyo na wale wawakilishi wa JR pia kila mmoja aliingia kwenye chumba chake .

Roma baada ya kuingia alipunguza nguo na kisha akajilaza kitandani kuutafuta usingizi kwani muda hio ilikuwa yapata saa nne usiku.

Roma alitumia nusu saa tu kujipumzisha mara mlango uligongwa na kujikuta akishangaa nani anagonga, kwani walikuwa washaagana na hata na Dorisi pia , akiwa na singlendi yake pamoa na pensi , alisogelea mlango na kufungua na mbele yake alikuwa mhudumu wa kiume ambaye alikuwa ameshikilia sahani ambayo ilikuwa imefunikwa na kitambaa cheupe na Roma akamwagalia huyu mhudumu pasipo kumsemesha chaohcaote na kushangaa ameleta nini kwani hakuwa amegiza aina yoyote ya huduma , lakini ghafla tu muhudumu huyu wa alievalia sare za hili jumba alitoa kile kitambaa kwa kasi na kwenye ile sahani kulikuwa na kisu na alikishika haraka sana kwa ustadi na kumrushia Roma kwa madhumuni ya kumdhuru , lakini Roma ni kama vile alitegemea , kwani ile kisu kinarushwa alihepa kushoto na kisu kikapita nusu inch na umbali wa kidevu chake kiasi kwamba hata ndevu ziliguswa kiana na Roma hapo hapo akajua huyu ni mhudumu feki na ametumwa kwa ajili ya kuua.

Baada ya mhudumu huyu feki kuona Jaribio lake limefeli , alirusha ngumi lakini kwa Roma alimuona kama mtoto anaejifunza kurusha ngumi kwani aliushika mkono na kuuzungusha na kilichosikika ni mlio wa mifupa kukatika , na Mhudumu feki akaachia mguno wa maumivu , lakini Roma hakuishia hapo tu , alimpiga kwenye koo kwa mkono , kama vile alikuwa akimchinja , kwnai pigo hilo lilikuwa ni la Karate na mhudumu feki aliregea na kudondoka chini.

“Shi*t watakuwa wengi hawa ,Dorisi atakuwa kwenye matatizo”

Aliongea Roma na kuchomoka kwa spidi kuwahi kwenye chumba cha Dorisi na ile anafika tu alimuona mhudumu akiingia ndani ya chumba cha Dorisi huku akiwa na sahani kama ile ile ya mhudumu aliemuua ikiwa imefunikwa na kitambaa cheupe.

Roma alikimbia kwa kasi na kuzama na ile anafika mhhudumu alikuwa tayari ashashika kisu na kumlenga nacho Dorisi kooni na Dorisi aliishia kufumba macho huku akiwa anatetemeka mwili mzima akisubiria kifo , lakini mhudumu baada ya kufikisha sentimita mbili karibu na koo la Dorisi alidakwa mkono na kuzungushwa kwa nguvu ambayo hakuwa ameitegemea , na baada ya kugeuka tu, aliopigwa na mikono miwili kwa wakati mmoja na Roma kwenye mbavu na mhudumu yule wa kijapani aliishia kuachama na kukosa pumzi na kisha akadondoka chini kwani mbavu zilikuwa zishakatika.

Dorisi alihikuta akimkimnbilia Roma na kumkumbatia huku akianza kulia kama mtoto na Roma alimtuliza na walati huo huo aliingia ndani ya chumba cha Dorisi Tikayi.

“Mko salama?” ndio swali la kwanza kutoka kwa Tikayi huku akimwangalia Roma kwa macho ya kumsanifu.

“Naona mmetuleta Japani kwa ajili ya kutua”Aliongea Roma kwa hasira na Tikayi alianza kuomba msamaha kwa tukio hilo na wakasema kwamba hawahusiki nalo.

“Mr Roma hili swala halituhusu hata kidogo na tutahakikisha tunawakamata wahusika , kwani tunaamini ni watu ambao wametumwa”:

Aliongea Tikayi na muda huo huo aliingia bwana mmoja alievalia Robes za kitamaduni za Japani huku akiwa ameshika upanga kwenye mkono wake na Roma kwa kumuangalia tu aliuona huyo jamaa anajua mapigano.

“Yoshida hakikisheni mnamkamata aliehusika na hili jambo haraka , naamini ana watu wake humu ndani na bado wapo, kagua wahudumu wote mmoa mmoja” aliongea Tikayi na bwana huyu aliamrisha walinzi waliokuwa wamevalia mavazi ya majoho meusi kama yeye na kuanza kutawanyika kumtafuta muhalifu.

Dorisi na Roma walitolewa na kupelekwa kwenye chumba maalumu cha usalama Zaidi na wakati huo huo mzee Yamamoto na yeye aliingia kwa spidi na kuanza kuasihi Roma, Dorisi na wawakilishi wa JR grupu watulie mpaka pale mtuhudumiwa atakapo kamatwa huku akiomba msamaha kw akujitetea jambo hilo hawakuwa wakihusika nalo.

Wote walikusanyika na kukaa kwenye masofa haya , akiwemo Tikayi ,Yamamoto Roma ,Dorisi pamoja na wawakilishi wa JR Group , wakati wakiendelea kuongea juu ya tukio hilo ambalo halijawahi kutokea ndani ya hii nyumba kutokana na ulinzi wake , mara aliingia meneja wa nyumba , yule ambaye alimnong`oneza Yamamloto kuhusu ujio wa kilevi wa Tikayeshi.

“Kuna nini meneja?”

“Boss kuna simu yako hapa kutoka kwa mtu ambaye hatumjui na anadai humu ndani ametegesha mabomu”

“Mabomu!”Aliongea kwa kupaniki huku akichukua ile simu na kusikiliza.

“Mr Yamamoto , nyumba yako yote imejaa mabomu ambayo yataripuka baada ya nusu saa , na hata ujifanye kuyatafuta hautoweza” ilisikika sauti hio ya kijapani kwenye simu na Roma aliisikia vyema kwani na yeye alikuwa akijua kijapani.

“Unataka nini katika familia yangu”Aliongea Yamamoto kwa hasira kwa kijapani.

“Kwanza kabisa nikwambie tu kwamba mabomu yatalipuka baada ya nusu saa na hata kama ulete wataalamu wa uwezo wa juu hatoweza kufanikisha hilo ndani ya nusu saa , na mabomu hayo ni ya sumu kwa maana hio nikibonyeza kitufe ambacho nimeshikilia hapa , itawachukua dakika tano kwa kila kiumbe ndani ya nyumba kufariki”

“Sema unataka nini acha maneno mengi”

“Ni jambo rahisti tu nahitaji Yen Bilioni kumi zinifikie mahali ambapo nitawaambia na nataka Cash….” Aliongea bwana huyo , lakini muda huo huo aliingia Tikayeshi huku akilia.

“Baba .. mabomu … mabomu baba… tunakufa .. Mama wee.. babab niokoe sitaki kufa sitomuaona tena Dina mimi ,,,,aaaaaa” Alilia bwana huyu kama chizi kiasi kwamba Yamamoto alikasirishwa Zaidi na kujisemea moyoni boar ahata abadilishane na mt una gunia la Pumba heanda akapunguza hasara ya kuwa na toto jinga.

“Mtoeni huyu mpuuzi hapa” Aliongea Yamamoto na Tikayeshi alitolewa huku akiendelea kulia kwa sauti akitaja mabom na baada ya Tikayeshi kuondoka Yamamoto aliendele akusikiliza simu.

“Endelea na masharti yako nakusikiliza”

“Nishasema mzee kiasi ninachotaka , shariti la pili mtu atakae leta hizo pesa lazima awe wewe au Tikayi” mzee alitoa macho.

“Kwanini mimi au Tikayi , shida yako ni pesa na tutakupatia haina haja ya mimi kuja au Tikayi kuja”.

“Mzee nadhani haulewi nishasema nahitaj wewe uje ulete pesa hizo au Tikayi ndio alete na niwaambie tu naona kila kitu mnachokifanya hapo ndani na ikitokea mtu atatoka ama kuingia ndani ya hio nyumba bila ruhusa yangu nabonyeza kitufe na Maisha yenu yatakuwa yamefika mwisho na kama haumini mlangoni hapo kuna mtu aliesimama kama kaegeshwa” Wote waliangalia mlangoni na kuona kweli kulikuwa na mtu ambaye alikuwa ni mlinzi wa Yamamoto na wakaini ni kweli bwana huyu alikuwa akiwaona.

Mzee yamamoto jasho lilianza kumtoka , licha ya kwamba kulikuwa na baridi kali lakini jasho lilionekana kwenye uso wake , hakuwa tayari kumuachia Tikayi aende kwani alikuwa ndio mrithi pekee na ndio mtoto ambaye alikuwa na akili , kwani kaka yake alikuwa ni kama chizi.

“Okey tupe dakika kumi na tano tukuandalie Cash”

“Dakika kumi zinatosha hakuna maongezi na narudia , naona kila kitu kinachoendelea hapo ndani mpaka panya wanaoingia na kutoka, hivyo nikiona mtu anatoka ambaye sio wewe au Tikayi nabonyeza kutufe na kuwalipua”.

“Sawa tupe dakika kumi tukuandalie Cash”

“Nitapiga baada ya dakika kumi , muwe na Cash na ndipo nitawapa eneo mnalotakiwa kuja”

Baada ya simu kukatwa Yamamoto alimuuliza Tikayi kama wanashilingi ngapi hapa ndani na Tikayi alisema wana Yen bilioni kumi na nusu, mzee baada ya jibu hilo alipata ahueni na kumuagiza Tikayi akaziweke kwenye begi na baada ya dakika kama saba hivi Tikayi alirudi akiwa ameshikilia begi zito likiwa na vibunda vya hela .

“Nitaenda mimi baba”Aliongea Tikayi na kufanya watu wote hapo ndani washangae.

“Hapana Tikayi , hao majambazi siwaamini kabisa wanaweza wakakufanya kitu , kibaya na wewe ndio mrithi pekee ambaye napanga kukuachia kuiongoza Yamakuza , hapana siwezi kukuruhusu kwenda”

Aliongea Yamamoto lakini Tikayi aling`ang`ania kwenda na baada ya malumbanio ya dakika mbili Mzee huyu alikubali Tikayi aende lakini akimsihi kuwa makini.

Baada ya dakika kumi Jambazi lilipiga simu na kutoa maelekezo ya sehemu ambayo alitakiwa kwenda , ni sehemu moja iliokuw aikifahamika kwa JPN.

Jambazi aliendelea kuwapiga mkwara kwamba hakuna mtu kutoka Zaidi ya Tikayi, na mzee Yamamoto licha ya kwamba alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa , alikubaliana na Jambazi , kwani hakuwa akitaka kuona watu wote waliokuwa humu ndani wanakufa kisa pesa,

Baada ya Tikayi kutoka akielekea mahali ambapo majambazi hayo ndio walisema wapo , Roma hakubaki hapo kwenye chumba cha usalama , alitoka na kuelekea kwenye chumba chake na baada tu ya kufika , aliangalia nje kwa kutumia dirishani kwa sekunde kadhaa na kisha akatabasamu na kufungua dirisha , alirudi na kuvaa shati na suruali na kisha akarudia dirisha na alionekana alikuwa akijiandaa kuruka.

“Unataka kuniacha sio?, ndani ya hii nyumba unajiokoa mwenywe ”Ilikuwa ni sauti ya Dorisi iliomfanya Roma aliekuwa amepandisha mguu kwenye dirisha ageuke na kumwangalia Doris.

“Doris narudi ,baki hapa naamini hakuna kitakacho kutokea” Aliongea Roma

“Hapana tunaenda wote na sipo tayari kubaki”Aliongea huku akionekana yupo siriasi na Roma alifikiria kwa sekunde na kisha akamgeukia.

“Utaweza kuruka hapa?”

“Hapana”

“Sasa utaendaje na mimi kama hapa huuezi kuruka” Dorisi hakuwa na jibu na Roma alifkiria jambo na kisha akamwangalia.

“ Natangulia kwenda chini , utajirusha na mimi nitakudaka”Aliongea lakini Dorisi alitoa mshangao , kwani alipochungulia umbali kutoka walipo mpaka chini aliogopa.

“Kama huwezi mimi nitaondoka mwenyewe”

“Okey nitajirusha kama kweli utanidaka”.

“Usijali nitakudaka”Aliongea Roma na kumwnaglaia tena Dorisi.

“Nitahesabu mpaka nne usipojirusha naondoka”.

Baada ya kuongea Roma alijirusha chini na kwenda kutua kwenye bustani bila ya kupiga kelele ya aina yoyote ile , alionekana kuwa mtaalamu kweli na baada ya kutua aligeuka na kuangalia juu huku akimpa ishara Dorisi ajirushe , ila Dorisi alikuwa akitetemeka ,Roma baada ya kuona Dorisi anatetemeka na hayuko tayari kujirusha , alimuonesha vidole kwa ishara na kuanza kuhesabu , na ile anafika tatu Dorisi alimpa ishara ya kujirusha na hakuwa na jinsi alikuwa akiogopa kufa mabomu na hakutaka kubaki mwenyewe hapo ndani na ndio maana alitaka kuondoka na Roma , alifumba macho na kujiachia kwa ujasiri na ile anafika chini alikuwa kwenye mikono ya Roma , huku akihema kwa kasi sana na Roma alimtuliza na kumwambia apunguze presha.
UNAJUA NINI KIMETOKEA ..TUKUTANE WIKIEND
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 60 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346

demu.png
 
Mpka ijumaaa duuuh balaaa ilo

View attachment 2340933
 
Dah mambo ni motoooooo[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4] Mkuutupe mamboooo
 
Back
Top Bottom