Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 120

“Wife ni wapi umesikia hilo jina?”Aliuliza Roma na kumfanya Edna afikirie kidogo , ukweli ni kwamba licha ya Mrembo huyu alikuwa akijiuliza wale wazungu wana uhusiano gani na Roma, Edna mwenyewe muda mwingine alikuwa akijishangaa ni kwanni licha ya mambo mengi kumtokea yanayohusiana na Roma alikuwa akiyapotezea.

“Ni wale wazungu wako”Aliongea Edna na kumfanya Roma atoe tabasamu la uchungu ,Roma aliona anapaswa kumpa Edna jibu la kueleweka.

“Wife nikitaka nikuelezee maana ya hio ya hilo jina , lazima nikueleze kwanza mimi ni nani na itachukua huenda takribani siku nzima ”Aliongea Roma na kumfanya Edna akose utulivu , huku akishindwa kujielewa, kwanini alikosa utulivu pamoja na wasiwasi.

“Wewe ni Roma ulielelewa Marekani, ulikuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta familia yako, ulifanya kazi ya kubeba mizigo mara baada ya kufika Tazania….,unataka kuniambia hayo yote yalikuwa ni uongo?”Aliongea Edna na kumfanya Roma asijue acheke au alie , maana hakuelewa kwanini mke wake ametoa ‘summarry’, lakini kwa Roma pia aliona hio ni fursa kwake kuingiza swala la Yan Buwen.

“Wife najua mpaka sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tokea tuanze kuishi pamoja, na ni mambo mengi ambayo yametokea kati yetu na yapo yale yanayohitaji maelezo na ambayo pia hayahitaji maelezo , Unaonaje leo tukitoka jioni na kutafuta sehemu tulivu nikuelezee kidogo ili ujue maana ya ‘Queen Peresephone’”,Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie Roma kwa sekunde kadhaa na alionekana kufikiria.

“Leo nina ‘Appointment ya kibiashara , labda tupange siku”Aliongea, na Edna ukweli katika moyo wake alikuwa na shauku sana ya kujua Roma ni nani haswa , mrembo huyu ukweli ni kwmaba hakuwa akiamini kabisa eti Roma alikuwa amelelewa Marekani na akarudi Tanzania kwa ajili ya kuitafuta familia yake , aliamini kabisa yote hayo ni uongo na swala ambalo lilimthibitishia Edna ni juu ya Sophia.

Ilikuwa ni siku kadhaa Edna akiwa kazini ndani ya ofisi yake na hii ni baada ya ujio wa Sophia, mlango wake ulifunguliwa na Monica.

“Boss Miss Suzzane anataka kuonana na wewe”Aliongea Monica na Edna alimpa ishara ya kwamba amruhusu.

“Karibu Suzzane”Aliongea Edna mara baada ya Suzzane kufika ndani ya ofisi ya Edna.

“Boss nishapata taarifa za Sophia”Aliongea Suzzane na kupangusa simu yake ya Sumsung S22 na kisha akampatia Edna ambaye alikuwa ana hamu ya kujua ni taarifa gani zinazomuhusu Sophia.

Siku ya jana yake alikuwa amempa kazi Suzzane kufuatilia taarifa za Sophia kwa njia ya simu.

“Ni kama nilivyodhania”Aliwaza Edna huku akiangalia simu hio , hakuonesha kushangaa sana.

“Asante Suzzane”Aliongea Edna na kisha akamrudishia Suzzane simu yake , hio ilikuwa ni siku kadhaa zilizopita baada ya Sophia kufika ndani ya familia yake , sasa siku ya Jumanne akiwa kazini asubuhi pia alipata ugeni.

“Madam kuna mgeni wako eneo la mapokezi , anafahamika kwa jina la Mrs Ramadhani, mke wa Balozi , anasema anataka kuongea na wewe”Ilikuwa ni taarifa iliotoka kwa Monica na kumfanya Edna ashangae kidogo , lakini aliishia kumwambia Monica awaambie watu wa mapokezi wamruhusu.

“Edna…!!!”Aliingia mama mmoja hivi Shombeshombe aliekuwa mnene mfupi huku akiliita jina la Edna kwa rafudhi yake ilioathiriwa na lugha ya kiarabu.

“Madam Rukaiyah!!,Karibu sana”Aliongea Edna akimkaribisha mwanamama huyu huku akimwita mke wa Balozi Ramadhani Rukaiyah , na kwa jinsi mwanamama huyu alivyokuwa akiongea na Edna ungefahamu tu kwamba sio mara yao ya kwanza kuonana.

“Edna nimekuja leo kazini kwako tuonane maana sikutaka Sophia afahamu nipo Tanzania”Aliongea Rukaiyah huku akiweka tabasamu usoni kwake,alionekana mchshi mno.

“Niambie Madam”

“Edna nilikuwa safarini nyumbani kwetu huko Abu dhabi kwa muda ,nilivyofika nyumbani sikumkuta Sophia na nikamuuliza baba Sophia kuhusu alipo mwanangu , ndio kaniambia yupo Tanzania anaishi kwako, niliuliza sababu ya Sophie ghafla tu kutaka kuja kuishi na wewe ukizingatia na namna familia zetu zilivyo , ndio balozi kaniambia eti Sophia anataka kuwa karibu na wewe , nilishangaa mwenzio , lakini kuna jambo ambalo lilinishangaza Zaidi”Aliongea Mama huyu na kumfanya Edna atake kujua Zaidi.

“Nini kilikushangaza Zaidi?”

“Kumbe mumeo ndio alimuokoa mwanangu wakati alivyotekwa,sikufahamu kama ushapata mume”Edna alishangaa.

“Nani alimteka Sophie!?”

“Edna kwani mumeo hajakuambia , unaonekana huna unachojua kabisa”Aliuliza mama huyu akishangaa Zaidi.

“Ndio sifahamu juu ya hilo?”Alijibu Edna kwa aibu na Mama Sophie alitabasamu.

“Sophie alitekwa pamoja na mtoto wa waziri mkuu wa Japani na watu wa Korea Kaskazini , nakuambia siku nilizimia hio nilivyopewa hio habari na nilipanga kabisa kuachana na Ramadhani kama Sophie asingerudi….,Edna najua familia zetu hazina ukaribu , lakini naomba Sophie akae nyumbani kwako , naogopa yasije yakamkuta tena, Yaani nakuambia Mwenzio sipendi kabisa kuishi Japani lakini Ramadhani hanielewei na sijui anafadika nini na ubalozi wake , mimi kwangu naona ni upuuzi tu na hauna faida ukilinganisha na biashara zetu”Aliongea mwanamama huyu mfululizo,lakini Edna hakuwa na taarifa za Roma kumuokoa mtoto wa waziri mkuu wa Japani na Sophia, hio ilikuwa ni siku ya jumatano mchana,

Edna hakutaa kumuuliza sana Roma kuhusu kumdanganya juu ya Sophia, Edna alijua Roma lazima atakuwa ameombwa na Balozi Ramadhani kwani mwanadada huyu alikuwa akikumbuka siku ya Kusanyiko ,Balozi Ramadhani alimuomba Roma kuongea nae na aliunganisha matukio na kuona huenda lilikuwa ni swala la Sophia , lakini pia mwanadada huyu aliweza kuona huenda pia sababu ya Roma kutomuambia juu ya Sophia ni kutokana na kutoelewana kwa familia ya Adebayo pamoja na Athumani.Hivyo Edna alimuona Sophie kama mdogo wake na Edna hakutaka kumwambie Roma , alijiambia kwasababu na yeye amemdanganya inapaswa alipize kisasi kwa kutomuambia yaani ,jino kwa jino’.

Roma alitabasamu baada ya kuona Edna kaingia kwenye topic ambayo alikuwa akiitaka , topic ya ‘Appointment’.

“Wife kama una appointment , basi tutapanga kwenda siku nyingine , lakini unaonaje leo nikikusindiza?”Aliongea Roma na kumfanya Edna afikirie na kuona hakuna ubaya kama atamsindikiza , kwanza miadi hio ilikuwa ni usiku na aliona na uwepo wa Roma atajiskia kuwa salama Zaidi, kabla ya Edna kumjibu Roma simu yake iliita na jina lilisomeka Monica.

“Kuna nini Monica?”

“Madam Mr Yan kabadilisha sehemu ambayo mnapaswa kuonana , anasema makutano yatafanyikia ndani ya Grape Hotel, anasema pia anayo miadi na mtu mwingine ndani ya hio hoteli ndio maana”Aliongea Monica

“Okey! Hakuna shida Monica “

“Boss !Unaonaje nikikusindikiza?”

“Nitaenda na mume wangu Monica , unaweza kwenda nyumbani ukapumzike , tutaonana kesho”Roma alisikia mazungumzo ya Edna na Miss Airport na kuona mpango wake umefanikiwa kwa asilimia mia moja na kilichobaki ni kwenda kuonana na huyu mtu anaeitwa Yan Buwen , alitaka kufahamu ni kwanini Yan Buwem alikuwa akimiliki Kadi ya kibenki inayotoa hela kutoka kwa akaunti ya Hegemeoni ,akaunti ambayo ilikuwa ikipokea miamala kutoka pande zote za dunia , lakini akaunti ambayo alikuwa akiamini mmiliki wake ni The Don,Licha ya kwamba Roma alikuwa na wasiwasi juu ya Dorisi pia , lakini aliamini jibu linaweza kupatikana kwa urahisi kupitia Yan Buwen.

Ni muda wa saa kumi na mbili kama na dakika aribaini na tano hivi , ndio muda ambao Roma alishuka kwenye gari aina ya Roll Royce akiwa ameambatana na Edna.

Edna leo hii alikuwa amevalia kiprofesheno kabisa ,kwani alikuwa amevalia Suti ya rangi ya Zambatau pamoja na viatu vya skuna , alikuwa amependeza na alionekana kujiamini kama kawaida yake , Roma kwa upande wake hakukuwa na jipya sana , alikuwa amevaa koti la suti na jeansi pamoja na miwani ya jua.

“Wife Naona leo umenifanya niwe bodigadi wako sio mume”Aliongea Roma aliekuwa amevalishwa miwani na Edna na alionekana kama jambazi.

Ukweli Edna hakutaka kumtambulisha Roma kama mume wake, walikuwa wamepatana, Roma atakuwa ni mlinzi na msaidizi wake wa karibu na ,Edna aliona angeonekana labda hakuwa akijiamini kama angemtambulisha Roma kama mume wake mbele ye Mgeni wake.

“Ndio uwe kama Bodigadi , kumbuka Bodigadi haongei ongei , ole wako upanua mdomo wako , kila nitakachoongea unatingisha kichwa na kusema Sawa Boss”Aliongea Edna wakati wakiwa kwenye Lift na kumfanya Roma afurahishwe na ubabe wa mke wake.

“Sawa Boss”Alijibu Roma na kumfanya Edna atabasamu na hata yeye alishangaa kwanini alishindwa kujizuia kutabasamu, labda ni namna Roma alivyoitikia

END OF SEASON 04
Upo vema kaka stori nzuri na muunganiko wa matukio congratulation
 
M
Huu mzigo hatari hii ni zaidi ya movie, hiki ni kitabu kinataupeleka kila nyanja ya dunia...china, japan,korea, marekani bingo, kenya Ruanda nk...ni ngumu sana kupredict nini kinafuata...hakika mwandishi umetutendea haki...Kongole kwako Singanojr big up...
Mwamba anajua mpaka anajua tena
 
Mwendelezo ni kila Jumatano na Jumamosi kila wiki. Naitwa Jay Alchemist mwandishi toka Afrika Mashariki. Uongozi wa taifa za Afrika ndio hutufanya waafrika tuwe nyuma. Tunaitwa The Dark Continent. Kisa? Viongozi wetu ni walafi na kama mwandishi wangu kipenzi BEN R MTOBWA alivyoandika: Hawa wanafakamia mali ya umma kwa njaa ile ya umaskini. Baada ya shibe, wanaendelea kufakamia mali ya jamii ili wailinde shibe hiyo. Jiunge nami katika hii safari ya wazalendo wa Afrika. Tusome hii simulizi iitwayo: Serikali ya Wezi, Taifa La Waliodanganywa. Simulizi hii ni sehemu Kijasusi kama ile series ya Joram Kiango ya Ben Mtobwa sehemu ya Kimaisha na sehemu kubwa riwaya kama zile za Ken Walibora

Kesho ni Jumatano: endelezo la simulizi yetu yenye utani na uandishi wenye kipaji kama waandishi wetu watukufu wa Afrika Mashariki. Katikati ya saa 6pm-8pm EAT. Tutamwona binti mwenye mini anavyomtesa fisi mtaani!
 

Attachments

  • Jamii.jpg
    Jamii.jpg
    783.9 KB · Views: 3
  • Serikali ya Wezi Article.png
    Serikali ya Wezi Article.png
    782 KB · Views: 5
Back
Top Bottom