NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA .
MTUNZI SINGANOJR.
Mono no aware
SEHEMU YA 754.
Roma aliishia kukunja sura akiwa ndani ya Kizimba(Cage) amekunja ngumi kwa hasira huku akiwa kimya wakati vipele vikienelea kuota katika mwili wake na kunyauka kwa kasi.
Wakati Roma akionekana kama vile amejikatia tamaa kabisa majini wale walishangilia na kuridhika kabisa.
“Haha..ulikuwa na maringo sana lakini sasa hivi umekuwa mpole kama mbwa , unaonaje ukipiga magoti na kuomba msamaha?”Aliongea Menyu mkuu wa miliki ya Kekexil huku akicheka kicheko cha furaha.
“Nadhani anaogopa sana hapo kiasi cha kushindwa kuongea chochote , ndani ya lisaa limoja na nusu huyu shetani atakuwa amekwisha kufa”Aliongea Gefu akiwa katika hali ya kutabasamu
“Uhai wa raia wa Panas zaidi ya elfu moja umepotea katika mikono yako hivyo ni damu yako inakwenda kulipia deni”Aliendelea kuongea.
“Haina haja ya kupoteza maneno yetu , tumuueni kwa nguvu zetu zote ili kusitokee tatizo kabisa”Aliongea Anjiu.
Majini hao hatimae walikaa kimya lakini hakuna ambaye alijali kwani asilimia mia moja wote walikuwa wakitaka kuona kifo cha Roma.
Dhana ya fuvu la misumari tisa ya mfupa wa Dragon iliendana na jina lake , majini hao katika vitabu vyao walisoma na kuelewa kwamba ambao washawahi kutumia Dhana hio wengi wao wamekwisha kufa kutokana na kunyonywa damu.
Ukweli ni kwamba hata kwa Shozi ambaye alikuwa mdhibiti wa Dhana hio, kama akifanikiwa kumkamata Roma katika kizimba hicho cha damu baada ya hapo kuna uwezekano mdogo sana wa kuendelea kuishi muda mrefu , hio Dhana athari yake kubwa ni kupunguza urefu wa maisha kutokana na kwamba inanyonya uhai kupitia damu.
Roma alikuwa amesimama katikati ya boksi hilo , chungu chake cha maafa kilikuwa pia kipo ndani kikielea katika kichwa chake, ule ukali wa chungu hicho ulionekana kupungua kabisa.
Dakika iliofuata baada ya Roma kunyanyua kichwa chake uso wake haukuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi lakini viashiria vya kukata tamaa vilionekana kwa mbali.
“Inanishangaza kuona bado unao uwezo wa kutumia huo mkono…”
Majini hao waliokuwa wamezunguka kizimba hicho cha gereza la damu hawakumwelewa Roma anachomaanisha na walioamini anaongea ujinga.
Roma mara baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa palepale aliweka kila alichokuwa amekishikilia katika hifadhi ya pete na kisha mkono wake mmoja wa kulia alibadilisiha nishati za mbingu na ardhi kwa kutengeneza moto wa rangi ya zambaranu na mwingine akatengeneza moto wa rangi ya bluu na madonge yale ya moto yalizidi kuongezeka ukubwa kadri sekunde zilivyokuwa zikisonga.
“Dogo bado tu unahangaika , unachokitafanya ndio kitakuua mapema”Aliongea Umini.
Roma alimpotezea kabisa na wakati moto ule ukiwa unawaka katikam mikono yake alifanya kitu kama vile anapiga makofi ili kuunganisha ule moto kwa pamoja.
“BOOM!!
Moto wa rangi ya Zambarau na wa bluu uligongana na kusababisha kishindo cha aina yake , ilikuwa ni kama vile aina hizo mbili za nishati zilikuwa zikiumana na kujaribu kumezana kwa wakati mmoja.
Ilichukua sekunde kadhaa tu kama vile kemikali zimeungana hatimae kulitokea matokeo mengine kabisa ambayo ni ya kimaajabu mno.
Roma mikono yake ilikuwa ikitetemeka kwa nguvu kama vile inaungua na alitumia nguvu ambayo sio ya kawaida kujaribu kuhakikisha nguvu hizo mbili za moto zinaungana ili kutengeneza kitu kingine.
“Buzz. Buzzz, Buzzz!!!!”
Ilikuwa ni cheche za umeme ambazo zilitoa sauti flani hivi kama ile ambayo inasikika wakati wa mafundi wakichomelea chuma na umeme lakini yenye sauti kubwa mno.
Mwanga wa ajabu uliweza kutokea pia katikati ya viganja vya mikono ya Roma na kuna kitu ambacho ni kama vile kinafutuka kana kwamba muda wowote kinakwenda kulipuka.
“Hicho ... hicho ni……!!!!!”
Anjiu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki mara baada ya kuhisi kitu cha ajabu , macho yake yalikuwa yamepanuka kiasi kwamba yanataka kumchomoka.
Wucheni na wenzake pia walianza kuhisi nguvu ya ajabu ikitoka katika eneo ambalo amesimama Roma , ilikuwa ni nguvu ambayo hawakuwahi kuihisia katika maisha yao yote na ilionekana nguvu ile ilikuwa ikianza kula ukuta wa kizimba cha damu.
Mwanga uliokuwa ukionekana katikati ya mikono ya Roma ulizidi kuongezeka na kuzidi kuwa na nguvu sekunde hadi sekunde.
“Hehe.. hahaha simaanishi ,,, kila kitu kilichopo chini ya nguvu ya radi ya mapigo mengi , moto wa mbingu na maji ya kiroho hayana nguvu.. dah .. ninashauku .. kama nguvu ya radi ya mapigo tisa athari zake zilivyo”
Roma alikuwa akibwabwaja mwenyewe maneno ambayo hayakuwa yakieleweka ilionekana ni kama vile kuna ufunuo anaupata.
Palepale aliinua sura yake juu kama vile anaangalia anga huku akitunisha kifua na ghafla tu mikono yake ilijiachia.
“Hey!!”
Ghafla tu shoti ya radi ya mwanga wa bluu na zambarau ilitoka katika mikono yake na kutengeneza umbo kama la mkuki uliopinda pinda huku ukitoa cheche.
Mwanga wake ulikuwa ni mkali mno na ndani ya sekunde tu Roma alikuwa amefunikwa na mwanga ule na sehemu aliosimama ilionekana kama vile ni jua la rangi ya bluu zambarau na ngurumo kubwa ilianza kugonga na mwanga ulikuwa ukizidi kuongezeka na kuwa mkubwa sekunde hadi sekunde.
Upande wa Roma alikuwa akiendelea kuzalisha moto wa bluu na wa zambarau katika mikono yake na kuunganisha kwa spidi kubwa na kadri alivyokuwa akifanya hivyo ni kama yeye mwenyewe anageuka na kuwa nishati ya ajabu vile.
Ndani ya sekunde chache tu kile kizimba cha damu kilibadilika rangi na kufunikwa na mwanga na ngurumo za radi zilizidi kuongezeka na shoti za rangi ya urujuani zilianza kutoka.
“Haiwezekani … radi ya Zambarau!!!?”
Gefu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki , huku majini wengine wakiwa ni kama hawaamini kile ambacho wanakiona mbele yao.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba moto wa bluu unatokana na mapigo tisa ya radi yaani kwa lugha nyepesi ile nguvu ambayo unaipata baada ya kupitia mapigo tisa ya radi ndio inakufanya kuweza kudhibiti moto wa bluu , upande mwingine mapito tisini na tisa yanakupa uwezo wa kutengeneza moto wa zambarau.
Sasa kwa haraka haraka Roma ni kama ameunganisha nguvu ya radi ya mapigo tisini na tisa na nguvu ya radi ya mapigo tisa na kufanikiwa kudhibiti radi ya rangi ya urujuani(Violet).
Sasa majini walishangaa mara baada ya kuona Roma amegeuza moto wa bluu na wa zambarau kutengeneza radi ya zambarau.
Shozi ambaye ndio alikuwa akidhibiti kizimba cha misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa Dragoni alianza kutetemeka kwa maumivu ,ilikuwa ni kama vile mwili wake unakwenda kupasuka kutokana na presha kubwa iliokuwa ikimwingia.
“Haraka ongezeeni nguvu ya nishati za mbingu kuimalisha ulinzi , anataka kujinasua!”Aliongea Shozi kwa kubweka.
Haikujalisha aliongea kwa sauti kubwa namna gani lakini majini hao mioyo yao ilikuwa imetingishika kabisa na kukosa ujasiri.
Moja ya udhaifu wa majini ni radi(Wenyewe wanaita moto wa mbingu) , wanaiogopa radi kuliko kitu chochote kile na ndio adhabu yao kubwa ambayo ukiipita wanakupa heshima.
Kile kizimba kilishindwa kumnyonya Roma damu tena na sekunde baada ya sekunde kilikuwa kikipoteza nguvu.
Anjiu macho yake yalionyesha hali ya kusita kulikokithiri , alikuwa pia ni jini ambaye amepitia mapigo ya radi hivyo swali liliibuka kwanini Roma kuwa na mwili wenye utimamu wa namna hio mpaka kufanikiwa kuidhibiti radi , alishakuwa katika mshangao kwa uwezo wake wa kudhibiti moto wa bluu , Wa zambarau na maji ya kiroho lakini wakati huo amefanikiwa pia kuidhibiti radi ya rangi ya urujuani.
Alijiambia hapana haiwezekani sio ujuzi pekee wa Roma katika kung’amua siri za mafunzo ya mbingu za ardhi na mbingu tu , pengine ametawaliwa na nguvu ya roho ya andiko la Urejesho.
Kadri alivyokuwa akiwaza ndio namna ambavyo alizidi kuwa na hasira , alijiambia kwanini sio yeye mwenye kumiliki mbinu hio ya andiko la urejesho wa azimio, kwanini ashindwe na binadamu ambaye amejifunza utamaduni wao.
Yeye ni jini kikamilifu kwanini ashindwe na binadamu ambaye hana damu ya kijini.
Pengine Roma angeangua kicheko kama angejua kile ambacho Anjiu alikuwa akiwaza , mbinu hio ya mafunzo ilikuwa amepatiwa ndio lakini hakuwa akiwaza watu wanavyoichukulia wala kuamini uwezo wake.
“Kama nilivyotarajjia , ijapokuwa hichi kizimba chenu kinaweza kuwa kama gereza kwa jini mwenye kuipita radi lakini ni ngumu kuhimili shambulizi la radi ya Urujuani ambayo hata jini ambaye amepitia mapigo elfu moja anaogopa”Aliongea Roma.
Aliangalia kizimba hicho ambacho tayari kilikuwa kikitetema na alijitingisha kidogo tu radi ile ya Zambarau ilitoka kama vile ni mshale na mara baada ya kugusana na kingo za kizimba kile kilipasuka na kuharibu kabisa ile Dhana.
Roma ni kama vile hakuwa na uwezo wa kudhibiti uwezo wake na kama angejua nguvu ya radi hio ilikuwa na nguvu namna hio asingetumia kiharibu Dhana hio kwani angeipata huenda ingekuwa na matumizi kwake hapo baadae.
Lawama alizipeleka kwa jini Shozi kwa kutokuwa na nguvu za kutosha za nishati ya mbingu na ardhi ndio maana shambulizi lake moja limeharibu Dhana hio.
Shozi mara baada ya Dhana yake kuharibiwa ilikuwa ni kama moyo wake ndani umepasuka na alitema damu nyingi sana na uso wake ulikuwa mweupe kama vile ni karatasi kutokana na kukosa damu na hakuendelea hata kusalia katika anga kwani alidondoka chini kama kifusi akiwa katika hali ya kukata tamaa kabisa.
Dhana ya misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa dragoni ndio uikuwa ni kiini cha uhai wake na kitendo cha kuharibiwa na pigo la radi ya bluu zambarau haikuwa tu nguvu zake za kijini kumpotea lakini pia kifo kilimpata .
Hatimae Roma alikuwa amechoropoka kwa mara nyingine katika mtego wao wa kizimba cha damu na sasa alirudi na kusimama katikati ya mbingu na ardhi, kwa jinsi mwili wake ulivokuwa ukipumua ni kama kila sehemu ya mwili wake kulikuwa na moyo unaosukuma damu.
Roma sasa alikuwa ameijua siri ya radi ya zambarau , yaani alikuwa kama ule mnara wa kuingia katika ulimwengu wa majini pepo , radi na Roma ilikuwa ni kitu kimoja.
Anjiu na majini wenzake wote walionyesha hali ya hofu katika macho yao , walikuwa wamemzingira kwa umbali mrefu sana na hakuna ambaye aliweza kuthubutu kusogea karibu hata kwa nchi moja , wote walikuwa wakiogopa nguvu ya radi iliokuwa ikimtoka Roma.
Radi ilikuwa na uwezo wa kuharibu sio mwili tu bali mpaka roho na nafsi na kupotea katika anga.
“Inaonekana tayari umekwisha kufanikiwa kubobea katika kuidhibiti radi ya Zambarau ?”Aliongea Anjiu , ijapokuwa alikuwa kwa mbali lakini sauti yake ilikuwa ikisikika kwa ukaribu.
Roma alinyanyua mkono wake mmoja na ile anafungua kiganja ilikuwa ni kama vile kuna mnyororo wa radi unamtoka na kwenda angani na kutengneza kitu kama upinde.
“Kama ilivyokuwa siku ile nilivyoficha kete yangu ya ushindi leo pia ni hivyo hivyo , kama ningekuambia nimeweza kugundua siri ya kuidibiti radi ya zambarau ungenichokoza?”Aliongea Roma akiwa katika hali ya utani.
Ukweli ni kwamba ile siku mara baada ya kufanikiwa kuinyonya nguvu ambayo Chaos alikuwa ameificha aliweza kugundua mambo mawili matatu namna ya kudbiti radi , alichokuwa amekosa tu ni changamoto ya kufungua mawazo yake.
Ili kupanda levo Roma alikuwa akihitaji changamoto na ndio maana aikuwa akizitafuta sana , wakati majini wakiwaza kumuua Roma yeye alikuwa akichukulia changamoto hizo kama mbinu ya kufungua mawazo yake na hio ndio siri kubwa ambayo ipo katika nguvu ya andiko la Urejesho.
Andiko la Urejesho ni kama njia ya kupokea maono na ili iweze kukupatia maono lazima ukidhi vigezo vya kimazingira ambavyo ni kuwa katika changamoto , pale linapotokea giza kubwa la changamoto mbele yako ndio maono yanapotokea.
Yaani utofauti wa mbinu nyingi za majini wanazojifunza katika kupanda levo na kuvuna zaidi na zaidi nishati ya mbingu na ardhi ni kufanya mazoezi kila siku na kutamka maneno maalumu lakini kuhusu andiko la urejesho ni kama vile ni ahadi ambayo Mungu amemuwekea binadamu kwamba pale ambapo utakuwa katika changamoto atamletea maono ya kutatua changamoto hio.
Unapaswa kuelewa andiko la urejesho wa azimio jina hilo sio jina lake bali ni jina ambalo Roma aliamua kuliita , mwalimu wake ambaye alimfundisha kuhusu mbinu hio alimwambia aipatie jina analotaka yeye na ndio jina la Andiko la urejesho wa Azimio lilipozaliwa.
Sasa siku ambayo Anjiu alipitia dhiki ya Radi upaande wa Roma iikuwa ni kama vile maono yalimjia na kuona radi ambayo alikuwa akipitia Anjiu ilikuwa na rangi mbili yaani rangi ya bluu na Zambarau hivyo moja kwa moja Roma aliamini pengine ni muunganiko wa elementi za moto wa bluu na elementi za moto wa zambarau na matokeo yake yalikuwa ni kama vile alivyokuwa amewaza.
Roma hatimae alikuja kuelewa pengine kinachomtokea katika maisha yake ni mambo yaliopangwa na Mungu tokea mbali , hakuwahi kuamini sana katika Mungu lakini kila kinachomtokea kilikuwa katika fumbo la namna yake na njia ambazo anapitia ni kama vile zimekwisha kuandaliwa.
Ukweli ni kwamba katika sheria za kikanuni za matokeo ya radi katika rangi tofauti tofauti ukizungumzia radi ya urujuani ni matokeo ya muunganiko wa elementi zinazozalisha mwanga wa bluu na zambarau ki ufupi ni kanuni zilezle za kisayansi .
Bila shaka haikuwa kama vile unafanya majaribio ya kikemikali kwamba lazima kutokee makosa kwanza mpaka unapofikia mafanikio.
Mbinu za mbingu na ardhi zilikuwa ni za tofauti kidogo , ufunuo ukishakutokea na ukaufahamu basi ukiufanyia kazi matokeo yake ni sahihi na namna ya kupata maono ni kujua asili ya dunia ilivyo , kila kitu kipo kwa sababu kiwe na uhai kisiwe na uhai , kila tukio la asili linatokea kwa sababu na hio ndio njia rahisi ambayo ilimuwezesha kupata ufunuo.
Sasa Roma kutokana na uzoefu wake wa kijamii ulimwambia kwamba asili ya moyo wa kiumbe chenye utashi siku zote ni Dhambi kwanza kabla ya kupitia utakaso na ndio maana hakutaka kuambia mtu yoyote kwamba ameweza kufanikiwa kujua siri iliopo katika kuidhibiti radi.
SEHEMU YA 755.
Roma sasa alikuwa na hali ya kujiamini na alijiambia akishaingia katika levo ya mapigo ya radi elfu moja atakuwa na uwezo wa kutumia moto wa bluu na elementi za moto mweusi na kufanikiwa kutengeneza radi ya mapigo elfu moja.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba Roma ameweza kudhibiti radi ya mapigo tisini na tisa , hii haikumaanisha kwamba Roma anaweza kutengeneza mapigo tisini na tisa lakini katika kanuni za nguvu za mbingu na ardhi inamaanisha kwamba anao uwezo wa kutengeneza radi yenye nguvu mara 9 katika awamu 11 na ndio hutokea hesabu ya 99.
Nishati za nguvu ya radi zinaenda katika kanuni hii tatu mara tatu , tisa mara kumi na moja , tisa mara mia na kumi na moja na kuendelea.
Maana yake ni kwamba unaweza ukapigwa na awamu tatu za radi yenye nguvu sawa ya mapigo matatu ambapo moja kwa moja utakuwa umepitia mapigo tisa , au unaweza kupigwa na mapigo kumi na moja yenye ujazo wa nguvu ya mapigo tisa hivyo kimahesabu utakuwa umepigwa na mapigo tisini na tisa au mapigo mia moja kumi na moja hapo utakuwa na uwezo wa kupigwa na mapigo mia tisa tisini na tisa , kanuni hii inabadilika lakini majawabu yanakuwa yanafanana, inategemea sana namna anga lilivyokasirika na mbinu yako ya mafunzo kwa mfano Anjiu na Rozu wao walipitia mapigo matatu tu ambayo ni sawa na mapigo tisa lakini kwa Roma alipitia awau tisa na awamu tisini na tisa katika mnara
Kila pigo lina rangi yake , asilimia kubwa ya mapigo tisa rangi yao ni bluu , tisini na tisa ni zambarau na kuendelea.
Roma sasa mara baada ya kuangalia majini waliokuwa mbele yake , aliona kabisa hana cha kuogopa licha ya kwamba walihesabika kama wabobevu wa nguvu za mbingu na ardhi katika ulimwengu huo.
“Nilikuwa nikipasha mwili joto na nishamaliza sasa , ni muda wa kuanza kazi..”
Mara baada ya kuongea kauli hio alitengeneza wimbi kubwa la radi ambazo shoti zake ziligawanyika na kuwa kama mishale midogo na kuwarushia wale majini.
Ngurumo iliosikika ni kama vile dunia imegongana na sayari nyingine na kabla hata majini hao wa Hongmeng na miliki nyingine masikio yao hayajatafsiri sauti hio walikwisha kufikitwa tayari na boriti za radi na kuwayeyusha.
Kwa Roma lilikuwa pigo la kawaida tu lakini athari zake hazikuwa za kawaida kwani majini waliokuwa katika levo za maji ya kawaida wote walipotea.
Majini wote ambao wamekwisha kuijua nguvu ya radi ya zambarau walijua namna ilivyokuwa ni hatari kuguswa na radi hio ukiwa hujajiandaa , hata Anjiu mwenyewe ambaye alikuwa na uwezo wa juu alitumia chungu cha Roma kuweza kuipita radi.
“Kimbieni!”
Sauti ilisikika kusikojulikana kama vile ni ya binadamu , meza ilikuwa imepinduliwa kibabe na kitu pekee ambacho majini hao waliona ni aidha kukwepa au kukimbia na sio kufanya mashambulizi.
Majini wa levo za chini waliosalimika walikimbia kwa kutawanyika lakini Anjiu , Gefu, Wucheni walikuwa wamebakia.
“Mnataka kukimbia , kukimbia kwenda wapi?”Aliwaza Roma akiwaangalia majini hao wa levo ya majji ya kiroho.
“Nyie vipi mbona hamkimbii kama wenzenu?, nimetoa kionjo tu show yenyewe haijaanza”
“Mh Tukimbie! ,unataka tukimbie kwenda wapi , unataka turudi katika miliki zetu ili utufuate huko huko ukaondoe mizizi ya vizazi vyetu kama ulivyofanya hapa Panas”Aliongea Menyu katika uchungu mkubwa na Roma hakukataa kwani ndio alichokuwa akiwaza.
“Hujakosea , isitoshe kama mnataka nianze kuwatafuta mmoja baada ya mwingine ni usumbufu ni kheri kama kutakuwa na mmoja wenu ambaye atakuwa ananielekeza njia”
“Ni kweli unataka kuua majini wote? , Roma kwa nguvu zako unaweza kutawala dunia nzima wewe mwenyewe na hatutanii katika hili… hatuwezi kukuchokoza tena kama utatuacha tuondoke leo hii .. au kama huridhiki na hivyo sisi kama miliki ya Panas tupo tayari kuwa chini yako , itakuwa ni kutuambia tu unachokitaka na sisi tutakutimizia”Aliongea Gefu akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake.
“Ndio bro Roma , tunaomba msamaha kwa kukuchokoza , Mungu anatutaka kuishi maisha mazuri na nia yako ya kimauaji ni kubwa mno na inaenda kinyume na sheria za ulimwengu , sasa hakuna haja ya kuuana sisi kwa sisi kwanini unataka kwenda mbali namna hio?”Aliongea Umini.
“Sio wewe ambaye ulikuwa ukitaka kuniua muda huu , sasa nipo katika nafasi ya kukuua ndio unaniambia huo ujinga , kwasababu mmeamua kubakia na kufa basi sina haja ya kuwachelewesha”Aliongea Roma na palepale radi ya zambarau ilianza kumzingira katika mwili wake kwa namna ya ajabu kabisa na haikuwashambulia moja kwa moja bali ilichomoza na kwenda kugongana na wingu.
Wakati huo wingu kubwa juu angani lilikuwa likizunguka kwa kasi mno katika usawa aliosimama Roma na cheche za moto kugongana zilikuwa zikionekana.
Anga kati ya mbingu na ardhi lilikuwa giza tupu likiwa limefunikwa na ngurumo za radi sauti ilikuwa kubwa kana kwamba Mungu amaemua kuharibu sayari nzima.
Katika mabadiliko ya spidi ambayo ilikuwa ikionekana kwa macho ya kibinadamu , mawingu ya ngurumo yalitengeneza kizingia kikubwa ambacho kilizngira mzingo wa maili mia moja , katika maeneo mengi mbali na miliki hio kulikuwa na Dhoruba kubwa ya upepo.
Sasa katikati ya kizingia hicho ndio mahali ambapo Roma alikuwa amesimama , ilionekana alikuwa akiivuta radi kutoka juu kuja chini , haikuwa uwezo wakudhibiti radi tu lakini alikuwa na uwezo wa kuyasuguanisha mawingu kwa moto wa bluu na zambarau kutengeneza radi.
“Hivi bado tunaweza kusema huyu ni binadamu kweli…!”’Majini waliokuwa wakitetemeka kwa hofu wakiwa hawaaini kile wanachokiona waliongea , kilichokuwa mbele yao ilikuwa ni zaidi ya uhalisia wa kiumbe binadamu.
“Kulingana na vitabu vyetu, majini wa enzi hizo walikuwa na uwezo zaidi ya huo, hivyo nguvu hio ni nusu ya nguvu zao”Aliongea Shombeli.
Ubaridi wa maji ya mvua uligonga uso wa Anjiu na aliishia kukunja ngumi tu huku macho yake yakiwa yamejaa husda.
“Andiko la urejesho wa Azimio …hii ni mbinu ya namna gani, kuna siri gani iliopo nyuma yake?”
Anjiu ambaye alikuwa na tamaa kubwa ya kupanda levo mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu iliokuwa ikiongezeka kila sekunde na namna ambavyo Roma analizungusha wingu na kufanya linavyotaka alijikuta akishindwa hata kujua ni hisia gani anazipata.
Roma alikuwa katika levo za juu kabisa na kwa wakati huo hakuwafikiria majini hao kama washindani wake , moyo wake ulikuwa ukiimba wimbo wa; ‘Athena njoo nikushikishe adabu’.
Roma alijiua pengine hisia anazozipata hata Athena alikuwa amezipata kwa muda mrefu sana , pengine Athena hakuwa akiigiza kuwa na ukiburi na ukauzu , vile vitu ambavyo watu wengi walikuwa wakiviona vya thamani kwake havikuwa vya thamani na hisia hizo ndio alizokuwa nazo Roma.
Ni kama vile mtu mzima kutokuvutiwa na midoli ya kuchezea watoto basi ilikuwa ni kama yeye vile kutokuvutiwa na vitu kama vile pesa na madaraka , Roma hakuwa hata na tamaa tena ya kuua viumbe dhaifu tena.
Roma alikuwa na uwelewa na hisia hizo mwanzoni lakini katika nguvu ya namna hio aliweza kufikiria kama vile alivyokuwa akifikiria Athena,
Mabadiliko ya kimtazamo na kiakili ilikuwa ni hatua ya ukuaji kwake ambao ulimpa hali ya kujiamini , Roma sasa alijiambia hawezi tena kuogopa yule mkuu wa umoja wa majini aliekutana nae Dodoma tena.
Mambo mengi alikuwa akiyafikiria katika kichwa chake na alikuwa ameshasahau kuna kundi la majini chini yake ambao linasubiria hukumu yake.
Katika wakati huo Roma sasa alikuwa katika hali ya utulivu kabisa na macho yake hayakuonekana kama yale ya fujo tena kama alvyoweza kuingia katika ulimwengu huo , ilikuwa ni kama vile amebatizwa na kuwa kiumbe kipya.
Roma alikiwa amesimama juu angani alinyanyua mkono wake na kunyoosha kidole upande wa aliposimama Menyu na wenzake.
“Boom!!”
Kitendo cha kunyossha kidole ni kama ishara ya kuruhusu pigo kwani wingu lililokuwa likizunguka juu yake lilishusha radi na kwenda kupiga katika eneo lile alilonyooshea kidole.
Ijapokuwa radi hio haikuwa kubwa kama ya mapigo tisa lakini ilikuwa na nguvu kubwa mno ya kugeuza majini wa nne wa levo ya maji ya kiroho kuwa majivu.
Anjiu na wenzake waliweza kukwepa shambulizi lile lakini ile wanakuja kumgeukia Menyu na baadhi ya majini walikuwa wamebadlika na kuwa moto wa rangi ya bluu na roho zao na nafsi zao ziliunguzwa .
Ijapokuwa walijua hawakuwa saizi ya Roma tena lakini walishangazwa na uwezo wake wa kuua majini wa levo ya kati ya maji kwa pigo moja tu.
BOOM!!
Radi nyingine ilishuka bila hata ya tahadhari , na awamu hio wazee wakuu wa miliki ya Xia walishambuliwa na kuuliwa palepale.
Roma alihisi ni kama vile ameanza kutumia radi miaka mingi iliopita namna ilivyokuwa rahisi kushambulia, moto huo wa mbingu aliweza kuita kama vile akili yake imetawaliwa na mdudu ambaye anawezesha hayo yote.
Gefu na wenzake waliona kabisa hali sio nzuri kwao kabisa na alipanga kuchukua baadhi ya watu wake kukimbia , hata kama angeamua kucheza kamari lakini ni kheri kuishi kwa muda mrefu kidogo kuliko asili yao kufutwa.
“Tawanyikeni , jiokoeni”Aliongea na baadhi ya wazee wa miliki ya Panas mara baada ya kusikia kauli hio walianza kukimbia kuelekea pande tofauti tofauti.
Roma hakuwaangalia kabisa na palepale aliita moto wa mbingu na kisha kunyoosha vidole upande wao na palepale walishukiwa na mashambulizi na kumezwa ndani ya sekunde ikiwemo Gefu mwenyewe.
Majini wote wa miliki ya Panas walipotea na kilichoweza kubakia ni Dhana ya kiuungu ya mkuki peke yake , ilikuwa ni dhana ya kilijendi hivyo haikuharibika kirahisi.
Ikawa Roma amekwisha kuua mkuu wa miliki ya Panas na mkuu wamiliki ya Kekexil.
Katika kifo cha Gefu hakuna jini ambaye alikuwa hata na habari ni wapi Dhana yake ya kiuungu ilipokuwa imedondikea.
Anjiu aliishia kung’ata meno yake na katika hali kama hio aliamua kuita pepo lake la ndani la kijeshi na mwili wake wote ulifunikwa na nguvu ya moto wa ndege wa dhahabu wa miguu mitatu.
“Msikimbie ni vizuri kupigana nae kuliko kushambuliwa wakati wa kukimbia , sidhani kama anao uwezo wa kuhimili uharibifu wake mwenyewe kwa kutuua wengi namna hii’
“Anjiu upo huru kufa mwenyewe , wewe ndio umetuleta katika hali hatarishi namna hii”Umini alitoa alimwangushia lawama kwa hasira , huyu kijana wa miaka mia mbili hatimae alijua kwamba tayari kifo kinamuita.
Kinyume chake Wucheni na Shombeli na wenzake wote walikuwa katika muoenekano wa utulivu kabisa , ni kama wamejiandaa kufa kimya kimya.
Roma aliweza kuoneysha kejeli katika macho yake na wakati kama huo alichopata kuona kati ya majini hao ni Anju peke yake ambaye alikuwa na muonekano wa kishujaa.
Mbele ya israeli mtoa roho Anjiu alikuwa bado akionyesha hali ya kujiamnni , ni kama hakutaka kufa kama muoga bali alitaka kufa kama mwanajeshi.
Pengine hio ndio sababu ya kumfanya Anjiu kuwa maarufu katika ulimwengu wa majini , Roma alijiambia kama sio Anjiu mwenyewe kutaka kumchokoza pengine angeweza kumfanya kuwa rafiki yake kwani kuna vitu vingi wanafanana.
Ni dakika kadhaa wakati Roma akijiandaa kumalizana na Wucheni hatimae aliweza kuhisi nguvu za majini zikisogea katika eneo hilo huku akisikia sauti ikimwita.
“Master Roma naomba usimuue mjomba tafadhari ,, usimuue”
Roma aliweza kuijua sauti hio kutokea mbali , ni kama vile alishawahi kuisikia na kufumba na kufumbua aliweza kuona wanawake wawili pamoja na mwanaume mmoja wakisogea katika eneo hilo.
“Bi Zenzhei!!”
Roma alishangaa mara baada ya kumuona ni Zenzhei , ijapokuwa Zenzhei alikuwa amebadilika na kuwa msichana lakini Roma alikuwa akimtambua kwani alionana nae wakati akiwa anaondoka.
Lakini alishangaa Zenzhei kusema mjomba wake asiuliwe
SEHEMU YA 756.
Roma mara baada ya kumjua Zenzhei alionyesha hali ya kuwa na furaha , ukweli licha ya kwamba alikuwa ni msichana lakini hakujizuia kumuita bibi.
Watu aliokuwa ameambata nao ni Nefi pamoja na Yiyu ambao ni watoto wa Wucheni.
Zenzhei mara baada ya kusikia Roma akimuita Bibi , Zenzhei alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi ya furaha neno bibi lilikuwa na maana kubwa kwake , ilimaanisha Roma alikuwa akimheshimu.
“Master Roma siamini kama kukutana kwetu kutakuwa kwa namna hii , mambo yanaendaje nyumbani Tanzania?”Aliuliza Zenzhei.
“Mambo kwanini yasiwe shwari wakati nipo , nina vitu vizuri kwa ajili ya yule mzee na umri wake kwasasa sio tatizo, usiwe na wasiwasi kabisa”Aliongea Roma akiwa katika tabasamu la furaha kumuona Zenzhei kwa mara nyingine.
“Ndio , nimesahau kama tayari unao uwezo wa kutengeza vidonge”
Baada ya kumuona Zenzhei anamsogelea Roma , Nefi na Yiyu walienda kwa baba yao wakiwa katika hali ya wasiwasi.
“Zenzhei usimsogelee atakuuwa huyo”Wucheni alibweka lakini Zenzhei aligeuza sura yake na kumtingisha kichwa mjomba ake na kisha akamgeukia Roma.
“Mr Roma Zenzhei anajua kwamba Hongmeng wamefanya makosa , nilipofika nilipata kujua ukweli wa mambo menginyuma ya vifo vya wazazi wangu kutoka kwa mjomba Wucheni na nimejua ni maamuzi gani ambayo nilipaswa kufanya muda mrefu juu ya kisasi changu , Mjomba ana makosa ndo lakini bado ana majukumu makubwa , najua nakosa aibu kukuomba hili kulingana tulivyokubaliana lakini naomba unikubalie hili ombi moja , muache aondoke ..nimeweza kusikia kutoka kwa baadhi ya wenzetu waliokimbia hapa kwamba tayari unao uwezo wa kudhibiti radi , hata kama Hongmeng wanatamani kukuchokoza hawatothubutu kwani wanajua unao uwezo mkubwa tayari”
Majini wa Hongmeng wote walikuwa kimya na walikuwa na taarifa ya Zenzhei kuishi katika taifa la Tanzania tokea akiwa mdogo hivyo ni kama ni raia wa Tanzania.
Lakini hawakuwa wakijua kama wakati Roma anaingia katika levo ya nafsi mara baada ya kukamilisha mzunguko wa Andiko la urejesho msaada mkubwa aliupata kutoka kwa Zenzhei.
Kutokana na kujua hayo Shombeli , Umini na wengne walijua pengine kuna tumaini la kubakia hai kwa kumtegemea Zenzhei.
“Acha kumbembeleza , hata kama watoto wangu na mabinti zangu watakufa hawawezi kukupigia magoti , mimi Wucheni ijapokuwa siwezi kujiita shujaa lakini sio mjinga ambae ninaweza kuishi kwa kuchekwa na kuomba kuhurumiwa”Aliongea Wucheni akionyesha hali ya kujisikia vibaya kwa Zenzhei kumuombea msamaha kwa Roma.
“Bi Zenzhei huna haja ya kunibembeleza , kama unataka nimuachie mjomba wao nitamuacha , sitaki kukuona ukinibembeleza”Aliongea Roma akimwangalia Zenzhei ambaye alikuwa na muonekano wa kinyeyekevu.
Majini wote ambao walikuwa hawampendi Roma walishangaa mara baada ya kuona Roma kweli alikuwa akijali maneno ya Zenzhei.
“Usishangae sana , wewe kwangu ni mwanafamilia na umekuwa mkarimu kwangu kwa muda mrefu sana na bado sijalipa yale yote ambayo umeyafanya kwa familia yetu , ijapokuwa mjomba wako alitaka kuniua lakini bila shaka nitamuacha aende lakini hii itakuwa ni mara yake ya mwisho kumpa nafasi nyingine , awamu nyingine akinichokoza ajue kwamba ndio mwisho wa uvumiivu wangu”
“Binadamu ulielaaniwa wewe acha kunibebesha uovu , hata kama nitakufa mimi na uzee wangu huu huwezi kunisingizia vitu ambavyo sijafanya , ni lini nikataka kukuua?”Aliongea Wuchen.
“Kwahio unataka kusema sio wewe uliekuja Australia katika nyika ya Arnhem na kutaka kuniua?”
“Australia!!. , unaongea nini?, Lini nikaja Australia na kutaka kukuua miii?”Aliongea Wucheni akiwa katika hali ya kushangaa.
“Roma! Baba yangu siku zote ni mtu mwema asie tayari kuvunja sheria , kama kweli alitaka kukuua unadhani ungeweza kumshinda wakati huo?”Aliongea Nefi.
“Nilishambuliwa na mtu aliekuwa amevalia Mask ya chuma na kutaka mbinu yangu ya mafunzo , mtu huyo alikuwa na uwezo wa kutumia kinga ya boma la barafu na kuita pepo wa kikaskazini , vipepeo wa kufikirika na mbingu nyingine , mtu huyo uwezo wake wa kijini ulikuwa mkubwa mno , kama sio Wucheni je ni nani kama sio mmoja wenu ndani ya miliki yenu?”
Mara baada ya kuongea kauli hio wazee hao wa Hongmeng walijikuta wakishangaa , ilikuwa haiwezekani Roma kumsingizia mtu kwasababu alikuwa na uwezo wa kumuua mtu yoyote ambae hakuwa akimfurahisha.
Dakika ileile macho yao yote yaliokuwa katika hali ya hasira yalimgeukia Anjiu.
“Anjiu unathubutu vipi kutumia mbinu ya familia yangu kujifanyisha ni mimi katika kufanya uovu wa namna hio , una moyo uliojaa hila, je ulikuwa ukinitafutia matatizo kati ya Roma na miliki yetu?”
“Nini , Anjiu!?, kwanini Anjiu aweze kutumia mbinu yenu?”
“Mr Roma mjomba hajahusika kabisa na kinachoendeea ni kama kilichoitokea familia yangu , kuna baadhi ya majini wa jamii yetu walijua siri ya mbinu yetu ya mafunzo lakini walikufa wote na mpaka sasa aliebakia katika ulimwengu wetu ni Anjiu pekee , alijua mbinu yetu kwa njia ya kumhadaa kimapenzi binamu yangu Yiyu ndio maana mpake leo hii kuna ugomvi mkubwa baina yao”
“Ushachelewa kufahamu hili, vyovyote vile lazima unapaswa kujiona mwenye bahati , nilitumia hii mbinu kwa ajili ya kukugombanisha na Hongmeng lakinni inasikitisha kwamba hukuchukua hatua na badala yake ukaja katika miliki yangu na kuanzisha vurugu, nadhani nilikosea mahesabu yangu”
“Kama ni hivyo wakati nilipokuwa kwenye Dhehebu la Tang , mtu ambaye alikuwa akiwatala kiakili wale wazee jr wewe pia?, je ambaye alijaribu kumtumia Tang luyi kwa kumleta binti wewe pia unahusika?”
“Ndio ni mimi, usisahau ilikuwa rahisi sana mimi kukuua wakati ule na usione inaweza kuwa rahisi kuniua leo hii”
“Kama ni hivyo basi utakuwa unamjua binti wa damu wa Tang Luyi, hivyo sema binti yake yupo wapi?”
Tang Luyi ni Master yake na Magdalena kutokea milima ya Shushan katika ngome ya Tang sasa siku ile Roma alivyoenda katika ile ngome alikuta wazee wote wakiwa katika kutawaliwa kimawazo na kutaka kumshambulia.
“Kwanini nikuambie?”Hali ya muonekano ya Anjiu ilibadilika.
“Haijalishi kama hutaki kujibu, hivyo nitakuuliza tena swali lingine, Je umejuaje nilikuwa nikitumia mbinu ya Andiko la Urejesho , je swala hili linahusiana na mtu ambaye alikuwa akimfukuza Master wangu Tang Chi na kutaka kumuua?”Aliuliza Roma.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa akijiuliza swali la namna hio kwa muda mrefu na kukosa majibu na hio yote ni kukosa mtu wa kumuuliza , hata alivyokutana na Tang Chi kwenye ulimwengu wa majini pepo hakumpa habari juu ya ubini wa adui ambaye alikuwa akimfukuza.
Kitu kingine ni kwamba asilimia ya majini wote ambao wapo katika ulimwengu wa majini watu hawakuwa na uelewa na mbinu hio aliokuwa akitumia , jambo ambalo lilimfahamisha kwamba hawakuwa wakijua mbinu ya andiko la Urejesho ni mara baada ya kukuta karatasi lenye andiko linalofanana na kwake japo majina tofauti.
Hivyo moja kwa moja lazima kuna mtu ambaye aliwaambia majini kwamba Roma anatumia mbinu ya Andiko , mbinu ya kijini ambayo hawaiujui ndio maana miliki zote zilikuwa zikihitaji kupata mbinu hio.
“Kama nikijibu maswali yako je utaniacha hai?”
“Huna jinsi zaidi ya kujibu maswali yangu au ufe , usifikiri pepo lako la ndani linaweza kudili na mimi awamu hii , ninao uwezo wa kukuua na radi kabla hata hajafanya shambulizi”
Anjiu mara baada ya kusikia maneno hayo aling’ata meno kwa hasira na kisha alimwangalia Roma na sura iliokuwa ikicheza cheza kwa hasira.
“Kama ni hivyo basi jibu langu ni kwamba sijui chochote, nasema hivi kwasababu mtu ambaye aliniambia kuhusu mbinu yako alikuwa ni wa ajabu sana haieleweki alikuwa ni mwanamke au mwanaume lakini nilichoweza kukuta ni barua katika meza yangu nyakati za usiku ambayo imeachwa na mtu huyo , sikujua hata kama kuna mtu aliingia katika ofisi yangu , kutokea siku hio huyo mtu alionekana sio wa kawaida hivyo sikumuwazia sana … kuhusu swala la kumfukuza Master wako na kutaka kumuua sijui hata kama una master wa jina hilo , hivyo sina majibu unayotaka na unaweza kuamini unachotaka”
Haikujalisha Roma alisikiaje jibu hilo lakini alihisi ni kama vile ni ujinga lakini kwa kumwangalia Anjiu haikuonekana alikuwa akidanganya
Mara baada ya kuona Roma yupo kwenye mawazo kila mmoja aliona hakuwa na nia tena ya kuendelea kuua na hatimae waliweza kupata ahueni ya kupumua.
Shombeli na Umini waliangaliana na kisha walipeana ishara ya maelewano na kwa haraka sana waliondoka na kundi la majini wa miliki ya Hongmeng.
Roma hakujali hata kuwafukuzia , mpaka wakati huo alikuwa na uwezo wa kuua jini yoyote kwa muda wowote anao taka laikini aliona kabisa kuua majini hao hakuna faida kubwa kwake
Iwe ni kwa kuua sana au kuua kidogo kwake hakukuwa na utofauti wa aina yoyote zaidi ya kujisumbua tu.
“Hakuna siku niliodhalilika kama leo , sijawahi kupitia huu uzoefu , umeniumiza na kisha ukachukua Dhana yangu , nipo tayari kufa nikipigana kuliko kukimbia ninakataa kushindwa lakini mimi Wucheni nachagua kuishi leo hii kwa ajili ya familia yangu .. mimi Wucheni nina deni la uhai kutoka kwako na kwanzia leo hii natangaza Hongmeng haitokuja kuwa na uadui na wewe kama ili mradi nitaendeea kuwa hai”Roma mara baada ya kusikia maneno hayo almwangalia Wucheni na palepale alijikuta akiangua kicheko.
“Sawa mzee , ndio uondoke wakati huu ambao nimekuruhusu na sitaki uchukulie mimi kukuacha hai ni kama deni , kama nilivyosema mwanzo nimekusamehe wewe na watu wako kwa ajili ya Bi Zenzhei , viumbe kama nyie ni swala la mimi kujiuliza kama niwaue au niwaache hai hivyo usijifanyishe kama utakuja kuwa na manufaa kwangu , kwangu muwe maadui msiwe maadui kwangu haibadilishi kitu kwanni mtabakia kuwa viumbe dhaifu mbele yangu”
Maneno yale ya Roma yalitaka kumfanya Wucheni kubadilika na kuonyesha hasira zake lakini mtoto wake Nefi na Yiyu walikuwa na hofu mno ya Roma kuwachukulia hatua.
“Zenzhei alimwangalia Roma na kisha akamwangalia Anjiu lakini kwa jinsi alivyokuwa akimwangalia Roma hakuonyesha aina yoyote ya hofu.
“Mr Roma nadhani sina haja ya kuwa na wasiwasi tena kwa mafanikio yako naamini yule mtu alifanya chaguzi sahihi , kwa mara nyingine niseme asante sana kwa ukarimu wako wa leo”
“Bibi kama upo tayari unaweza kurudi Tanzania na nitahakikisha hakuna anaeweza kukurudisha katika huu uimwengu wakifanya hivyo naua wote”
Zenzhei alifurahishwa na maneno yake , alikuwa na muonekano wa kijana na kwa Roma ni kama vile alikuwa akilinganga nae umri licha ya kwamba alikuwa akimwita bibi na aliishia kutingisha kichwa tu na palepale aliondoka kwa kupotea.
Sasa aliebaki alikuwa ni Anjiu peke yake , sio kwamba hakutaka kuondoka lakini alijua Roma anaweza kuwaacha wote waondoke lakini yeye asimruhusu
“Kusema ukweli sina uhakika kama ulichoongea ni ukweli kwasababu ya hilo najikuta nakuona wa hatari sana , kama unachochote unachotaka kuongea ongea kabla ya kifo chako”
“Nishajua unakwenda kuniua muda mrefu hivyo sogea tupambane , ijapokuwa nafasi yangu ya kushinda ni ndogo lakini siwezi kufa”
Mara baada ya kuongea hivyo aliita pepo lake la ndani na palepale ni kama vile kivuli cha mtu kinamtoka na kusimama mbele yake , kilikuwa ni kivuli kinacholingana kila kitu na yeye na kufumba na kufumbua kivuli kile kilimsogelea Roma kwa kasi.
Roma alikuwa tayari amekwisha kujindaa na aliita chungu cha maaafa na kwenda kugongana na kwa ana na lile pepo.
Lakini kwa nguvu ya Chaos ilivyokuwa kubwa ilikuwa ni mchezo wa kitoto sana kwa pepo wa namna hio kuweza kushindana na chaos kwani palepale mara baada ya kukaribiana na mdomo wa chungu lilipuka. Kama bomu.
Roma aliishia kupiga yowe kwenye moyo wake , ilionekana Anjiu hakuwa na nia ya kutumia pepo hilo kushambulia bali alilitoa kafara na kulitumia kama bomu la moshi.
Pepo la namna hio hata kama lilipuke ilikuwa ni swala la muda tu kwa Anjiu kulirudisha licha ya kwamba inaweza kumgharimu nguvu nyingi za mbingu na ardhi.
Sasa mara baada ya mlipuko ule wa pepo ambao ulitengeneza wingu Anjiu alitumia nafasi hio kukimbia lakini Roma ni kama alitegemea anachotaka kufanya na hakuwa na mpango wa kumuacha akimbie kizemba namna hio.
Uelekeo aliochukua Anjiu ilikuwa ni kuelekea katika miliki ya Xia na ilionekana alikuwa akitaka kuita wasaidizi wake
Ijapokuwa Roma alikuwa na spidi kubwa lakini spidi ya majini haikuwa ya kawaida hawakuwa wakipotea bali walikuwa wakisafiri kwa kasi mno kiasi kwaba wanaonekana kama wanapotea na ndani ya sekunde tu Anjiu alikuwa maili nyingi sana akiwa amemuacha Roma na hio ilimfanya Roma kutokuweza kuita radi kumshambulia tena.
Kilichomshangaza Roma ni uwezo wa Anjiu kukimbia huku akiacha kinga nyuma za barafu kama maboma
Ilimchukua Roma dakika kama tano kuweza kumfikia Anjiu lakini ile anataka kumzuia kwa mbele na kumshambulia na pigo la radi ghafla tu alihisi msisimko wa nguvu za kijini ukiongezeka kwa kuwasogelea na kufumba na kufumbua walitokeza majini waliokuwa katika kundi kutoka katika miliki ya Xia wakiongozwa na msichana mdogo Xiao .
“Mnafanya nini hapa?”Anjiu alikuwa amekasirika mno mara baada ya kumuona binti yake Xiao.
Roma alitaka kutumia ile nafasi kuwashambulia na pigo moja la radi na kuwaua lakini mara baada ya kumuona Xiao alisita.
Msichana huyo nusu jini nusu binadamu alimpa Roma ugumu wa kumshabulia , pengine ni kutokana na kwamba Rufi alikuwa na deni nae na yeye pia alikuwa amemshuku zaidi ya mara mbili.
“Baba wewe unaweza kuondoka , mimi binti yako nitamzuia huyu mtu mbaya”Aliongea Xiao na kisauti chake cha kuumiza masikio na palepale alisogea mbele ya Roma na kumkinga baba yake.
“Wewe mhalifu mkubwa niue sasa kama uwezo huo unao , hujatosheka kunichokoza mara kibao lakini na sasa hivi unataka kumuua baba yangu, dhamiri haikusuti?”
Roma aliguswa na maneno ya Xiao , yalikuwa ni kama vile ni shambulizi la radi , ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kuua majini kwa kufikiria tu lakini alijikuta akiwa mzito sana kumuuiza huyo mrembo.
“Sogea pembeni , Mimi na Rufi tuna deni kwako ndio , lakini kinachotokea hapa ni kati yangu na baba yako , kama nisipomuua leo hii ataniua mimi”
“Unaongea ujinga, kama kweli una deni kwangu kwanini unataka kumua baba yangu , hii ndio namna ya kulipa hilo deni?”
“Hili ni tofauti..”
“Ni tofauti kivipi?”
Anjiu macho yake yaliongezeka ukubwa , palepale aligundua Roma alikuwa akimjali sana binti yake.
Kama ingekuwa ni zamani angemtumia Xiao kama mateka ili kumzuia Roma asimuue lakini tokea siku ambayo alirudi kutoka katika ulimwengu wa kawaida alianza kumchukulia kama binti yake kipenzi.
Siku hio ndio Anjiu aliweza kumjua Roma vizuri , alikuwa ni katili ambaye anao uwezo wa kuua miliki karibia zote hivyo alijua mtu wa aina hio anaweza kumuua hata kama atakubali kutokumuua kwa ajili ya binti yake
Anjiu hakutaka kumuona binti yake akijihatarisha kwa ajii ya kumuokoa.
Kuna vitu nadhani alisahau kuvijua kuhusu Roma , ukweli ni kwamba alijua kama Roma hakuwa akimjali Xiao basi mpaka wakati huo angekuwa ashawaua yeye na binti yake na kuwageuza majivu.
Roma hakuwa bado amefanya maamuzi , alikuwa akiwaza namna ya kutokumdhuru Xiao lakini amuue Anjiu kwani ni tishio kwa usalama wake na watu wake.
Mara baada ya kuona Roma anawaza wale majini wengine walianza kumbembeleza Anjiu kuondoka lakini yeye aliwafaokea kwa kumruhusu Xiao kuja nao.
“Mkuu tulikuwa na wasiwasi juu yako , taarifa za vita imesambaa katika miliki zote za majini , mkuu aliepita bado hajapona tutafanya nini kama na wewe tutakupoteza”
“Baba ondoka , nitamzuia asikudhuru , huyu nanamdai fadhila hivyo siwezi kumruhusu kukudhuru”
Xiao aliacha kumwangalia baba yange na alikuwa akijaribu kumsukuma Roma kurudi nyuma bila ya hofu yoyote , pengine ni hisia zake za kimapenzi ndio zinamfanya kutokumuogopa Roma.
Anjiu alitaka kumzuia Xiao lakini wazo lilimwingia , alijiambia kama ataendelea kumshikilia si nitangia katika mtego wa Roma labda anapanga kumtumia kama mateka ili kunikamata.
Kutokana na mawazo hayo alishindwa kuchukua maamuzi ya kukikimbia.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa hata na mpango wa kumtega Anjiu,alikuwa na uwezo wa kutokumdhuru Xiao na kisha kumuua Anjiu lakini matendo ya Xiao yalimfanya kutokuchukua hatua yoyote.
Xiao alienda mbali na kumshikilia Roma kiuno kwa kupitisha mikono kwa mbele ili kumzuia asisogee , vitendo hivyo vilimfanya Roma kushangaa na kuishia kucheka kwani vilikuwa vya kitoto sana
Licha ya kwamba uwezo wake ulishafikia levo ya nafsi lakini bado matendo yake yalikuwa kama ya msichana mdogo.
Upande wa Anjiu alikuwa na wasiwasi mno kwa kuogopa Roma kumuua binti yake.
“Baba kimbia basi”
Aliongea Xiao akiamini kwa namna alimvyomshikilia Roma hawezi kuchoropoka.
“Haka kajinga kanadhani Roma hawezi kuniua kwa kufanya vile”Aliwaza Anjiu.
Roma palepae alitoa tabasamu la kifedhuli na alimgeuza Xiao kama karatasi na kumshikilia na kwapa la mkono na kabla hata hajaleta ukinzani alikuwa tayari ashamzimisha.
Roma mpango wake ulikuwa ni mwepesi , alijua kama ataondoka na kurudi nae anaweza kumjua vizuri Xiao ni nani na kama ni mtoto wa Tang Luyi angempeleka kwa mama yake lakini pia asingekuwa na wasiwasi kuivamia Xia na kuisambaratisha.
Anjiu hakuweza kumuokoa binti yake na aliamua kukimbia huku akiamini Roma hawezi kumdhuru.
Upande wa Roma alikuwa mzito mno kumuacha Anjiu akimbie na alijaribu kumshambulia kwa kumrushia shoti za radi na mkono mmoja lakini kwasababu alikuwa amembeba Xiao alishindwa kubomoa ngao yake ya kijini ya barafu.
Roma aliweza kukiri ngao ya barafu ya pepo wa kaskazini ilikuwa sio ya kawaida kabisa , ilikuwa na nguvu mno kwani iliweza kumsaidia Anjiu kutoroka.
Lakini licha ya kwamba Roma hakuweza kumpata Anjiu na shambulizi lake lakini wale majini waliofika hapo waliweza kupatwa na mashambulizi hayo na kupoteza maisha.
Roma hakutaka kumwangalia tu akipotea katika macho ake na aliamua kumfukuzia kwa nyuma kwa kasi kubwa huku akiwa bado amembeba Xiao.
Anjiu alichukua uelekeo wa Kaskazini mashariki na alikuwa na spidi ya kasi mno lakini Roma licha ya kumfukuzia kwa kasi hakuwa na wasiwasi wa kumpata.
Roma alijiambbia hata kama asipomkata Anjiu miliki yake anaifahamu hivyo angeenda Xia na kuilipua na aone kama hatojitokeza.
Wakati Roma akiwa nyuma anaendelea kumfukuzia Anjiu alihisi kitu kisichokuwa cha kawaida kimeamka , ilikuwa ni kama vile kuna kitu kinataka kumtoka katika mwili wake , Roma mara baada ya kujichunguza alikuja kugundua ni kitu ambacho kilikuwa ndani ya hifadhi yake ya pete na jambo lile lilimshangaza sana.
Kabla hata hajagundua ni kitu gani hicho baada ya kufungua hifadhi hio kivuli cheusi kilitoka kwa kasi na kumvaa , kivuli hicho kilikuwa na nguvu ya giza , na kimejaa roho ya ukichaa , kifo na baadhi ya hisia hasi ambazo hazikuwa zikielezeka.
“Ni ile Hazina ya majini pepo!!!”
Roma alishangaa mno kwani ilikuwa ndio mara ya kwanza hazina hio ikawa hai na kutoka katika hifadhi bila ya ridhaa yake.
Kubwa zaidi ni kwamba hajawahi kujua kazi ya hazina hio ni nini na tokea mwanzo hakuweza kuhisi kama ilikuwa na nguvu zozote zile.
“Kwanini ghafla tu imeamua kuzalisha nguvu ya ajabu ya namna hii ya giza?”
Roma alijiuliza na kabla hata hajapata majibu kivuli kile kilichokuwa kimemzingita kiligeuka na kuwa kama vile ni kizingia au kimbunga na kuanza kumzunguka kwa kasi mno huku kikielekea juu angani zaidi na zaidi huku ncha yake juu kabisa kukiwa na ile hazina nyeusi.
Msuguano wa nisahti za mbingu na ardhi na nishati za hazina ile ziliongezeka kwa kiasi kikubwa na kuanza kumsukuma Roma kwenda juu angani , ilikuwa ni kama vile alikuwa amefungwa kamba kiunoni na kulazimishwa kwenda juu kwa kuvutwa.
Nguvu ilikuwa ni kubwa mno na Roma hakuweza kujinasua kwa kadri alivyokuwa akijitahidi , alijaribu kutumia chungu cha maafa kuweza kumeza nguvu inayotokaana ile hazina lakini alishindwa kabisa , alijaribu uwezo wake wote wa nguvu za kijini katika levo ya radi lakini pia ilishindikana na alijikuta akitoa macho.
“Hii nguvu ya hazina mbona kama inanyonya nguvu zangu?”
Roma aligeuza macho yake juu angani na palepale aliona katika anga ni kama vile kuna shimo kubwa jeusi ambalo anga yake ilikuwa ikichemka kana kwamba ni mafuta meusi yanayochemswa na moto mkali.
Roma kutokana na uwezo wake wa kuelewa kanuni za anga aligundua kilichokuwa juu yake ni Lango(Portal) la shimo ambalo ndio lilikuwa likimvuta.
Ilikuwa ni ndani ya sekunde tu ilikuwa ni kama alivyowaza kwani akiwa amemshikilia Xiao aliweza kutumbukia katika lile shimo refu na hakujua hata kinachomtokea ni kitu gani , kila kitu kwake kilikuwa cha maajabu.
Roma alijiuliza au pengne Hazina hio haikuwa na uwezo wa kuzalisha nguvu yoyote bali kazi yake ilikuwa ni kuamsha malango ya anga.
Kilichokuwa kimemtokea ni kama vile alivyovutwa na mnara na kupelekwa katika ulimwengu wa majini pepo na ndio kitu cha namna hio hio ndio kilichokuwa kikimtokea tofauti tu ni kwamba alijihisi ni kama vile anatumbukia kwenye shimo lefu la giza huku akishindwa kujizuia.
Roma mara baada ya kutumbukia mzima mzima katika shimo hilo ndio sasa anakumbuka kwenye mikono yake alikuwa memshikilia Xiao.
“Ni kitu gani hichi kinanitokea , kwanini nina bahati mbaya namna hii , au majini pepo waliniwekea mtego , au hii hazina yao ilikuwa ni ufunguo wa kuteleport kwenda ulimwengu mwingine , kama ningejua ningerudisha hazina yao mara moja”
Roma alianza kujilaumu wakati akiwa ndani ya giza totoro asijue ni wapi anaelekea , alichokuwa akijua tu ni kwamba nguvu inayomvuta ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi kufanya lolote.
Anjiu ambaye alikuwa akikimbia kwa kasi kuokoa maisha yake hakujua ni kipi ambacho kinamtokea Roma na mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu alijiuliza au kuna mbinu nyingine Roma anajaribu kufanya ili kumuua.
Kitendo cha kugeuka nyuma aliona kitu kama duara nyeusi ambalo linapungua ukubwa kwa namna ya kusinyaa na ilikuwa ni kwa haraka sana kidoti kile cheusi kilipotea na hakuhisi tena msisimko wa nguvu za Roma wala za binti yake Xiao.
Ilikuwa ni kama vile Roma na Xiao walikuwa wamepotea katika anga jembamba , aliishia kukunja ndita na alirudi kwa kasi nyuma na kujaribu kumtafuta Roma , alijaribu kutumia nguvu zake za kijini za utambuzi ili kumuona binti yake lakini hakukuwa na dalili yoyote.
Roma kapotelea wapi au ndio mpango wa Athena kumpoteza Roma kukamilisha mambo yake.
Hatima ya Lekcha na Aoiline ni nini.