Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Vanity of vanities , all is vanity

SEHEMU YA 793.
“Zeus..!1”
Roma moyo ulimsinyaa , alijiuliza inamaana wimbi la sauti ambalo ni kama lilikuwa likitaka kuharibu anga lilitoka kwa Zeus?, ni palepale alipata kujua lazima sauti aliokuwa akiisikia kwenye akili yake ilipitia kwenye uungu wa Hades
Wakati huo mara baada ya kusikika kwa sauti, radi ya rangi ya dhahabu na bluu yenye urefu wa zaidi ya futi kumi ilipasua anga kama ilivyokokotwa kutoka kwenye kitu kisichoweza kuonekana na kwenda moja kwa moja kupasua radi na mawingu ambayo yalikuwa chini ya udhibiti wa Roma.
Mkono imara ulijitokea kutoka mawinguni na kunyakua shoti ya radi bila kujeruhi ule mkono kwa namna yoyote licha ya kwamba radi ile ilionekana kuushambulia ule mkono.
Ndani ya sekunde tu lile wingu lote lilitawanyika na hatimae mwili wa miraba minne ulionekana juu angani.
Alikuwa na ndevu ndefu nyeupe ambazo zilikuwa zikipeperushwa na upepo huku mashavu yake yakiwa na kingo kama za mawe pamoja na kona zake.
Macho yake yote mawili ni kama yametawaliwa na umeme na kufanya yatoe mng’ao wa ajabu ambao mweupe sio mweupe ni kama rangi ya majivu.
Mwili wake ulikuwa umesitiriwa na joho la rangi nyeupe lenye mikono mifupi ilioacha wazi mikono yake , huku misuli yake iliotuna ikionekana waziwazi na ilikuwa ni kama vile mwili wake wote umejaa kutu.
Roma aliishia kutoa macho yake tu asiweze kuamini , aliekuwa juu yake ni kama hakuwa amebadilika kabisa , kama alivyokuwa miaka elfu mbili iliopita.
Imewezekana vipi?
Miungu wote ambao walikuwa wamepoteza miili yao mara baada ya kuja duniani na kuvaa miiili ya binadamu, alishangaa mara baada ya kumuona Zeus akiwa na mwili wake wa awali.
Mara baada ya miungu kushuka hawakukaa hata siku moja wote waliamua kuivamia miili ya binadamu na kutelekeza ya kwao lakini kwa wale ambao walikuwa na uwezo wa juu ikiwemo miungu kumi na mbili waliweza kuishi nayo kwa muda mfupi kidogo kabla ya kuhamia katika miili ya binadamu.
Inasemekana Zeus ndio ambae alidumu katika mwili wake kwa muda mrefu na aliingia na mwili wake katika gereza la Roho.
Ndio maana muda huo Roma anashangaa ameweza vipi kutohamia katika mwili mwingine na kuishi na mwili wake licha ya kwamba katika mazingira ya dunia haiwezekani.
Alijiuliza je kulikuwa na sababu ya kipekee ndani ya gereza la Roho ambayo ilimfanya kuishi na mwili wake tofauti na mazingira ya dunia, maana kwa anavyoonekana ni kama haikuwa swali bali jibu.
“Kuwa na uungu wa Hades halafu kuwa adui wa miungu hustahili kabisa uungu wake na haustahili kabisa kuwa sehemu ya miungu , leo nitakuuwa na radi hii iliopo kwenye mikono yangu”Aliongea Zeus akimwangalia Roma kwa macho makali..
Na mara baada ya kauli hio aliinua mkono wake mkubwa juu na bila ya kuchezesha chezesha aliachia radi yote kutoka kwenye mikono yake kumshambulia Roma.
Mara baada ya miungu kuona tukio hilo wengine walikuwa katika hali ya heshima kwa Zeus na wengine walikuwa na furaha.
Ilionekana walikuwa wakijua fika kama Zeus ataamua kuingilia kati, Roma hana nafasi ya kushinda tena.
Roma spidi yake ilikuwa kubwa mno , hata kama ni radi ya Zeus haikuwa rahisi kutokuiona kwa macho yake na kabla radi ile haijamtoka Zeus alikuwa tayari ashajiandaa kukwepa.
Lakini sasa mara baada ya Roma kusogea upande mwingine kwenye hewa akijua kabisa amefanikiwa kukwepa shambulizi lile alipigwa na boriti tatu nyingine za radi na kusababisha mlipuko mkubwa wa shoti.
BOOM!
Roma alishindwa kuamini na hakujua ni nini kinaendelea , ilikuwa ni ile radi imetoka alipokuwa amesimama na kumfuata alipokuwa amehamia na kuvunja ukuta wake na kisha kumshambulia.
Ilikuwa ni kama vile radi ile ilikuwa na ufahamu kwamba atasogea hivyo ilibadilisha uelekeo bila ya taarifa.
Mwili wake wote ulionekana kuungua kwa kiwango cha juu cha joto, huku viungo vya ndani vikionyesha kuumia pia na kujinyonga nyonga, alishindwa kuzuia sauti zaidi ya kupiga yowe.
Maumivu hayo yalikuwa makubwa mno kuliko yale yaliosababishwa na siraha ya Athena wakati wa kumshambulia.
“Arghh..!!”
Roma macho yake ni kama yanapasuka na ni kama anajua sasa nama maumivu halisi ya radi yanavyokuwa
Mwili wake ni kama unaelekea kupalalaizi huku maumivu ni kama yameungana na mwili wake na kumfanya akitamani kifo kuliko kuendelea kuishi.
Uwezo wa Zeus ni sawa na kusema ulikuwa wajuu kiasi kuliko ule wa Athena , jambo ambalo lilimaanisha shoti ya radi yake ilikuwa na nguvu mara mbili na ya jini au mtu aliepitia mapigo elfu kumi ya radi.
Sasa Roma uwezo wake ulikuwa katika mapigo mengi ya radi na pengine ni sawa na kusema ni bahati kwake hajafa mara baada ya kupigwa na radi hio , ilimuwia vigumu kupona haraka kuliko mwanzo.
“Athena kwanini unasita sita, radi yangu itamfanya kuwa dhaifu , tumia mkuki wako kumchoma eneo la moyo na kisha tukiondoe kichwa chake”Aliongea Zeus.
Alikuwa akimwangalia Roma kwa madharau kutokana na kushindwa kwake kusogea huku akiongea na Athena.
“Huna haja ya kunifundisha cha kufanya”Aliongea Athena na palepale aliishikilia vyema siraha yake.
Roma alijikuta akipatwa na kiwewe mara baada ya kuona Zeus na Athena wanataka kumchangia kumshambulia .
“Sikutugemea kuishi lakini siwezi kufa bila ya kupambana”Aliwaza Roma.
“Ni mapema sasa kuniua”
Roma aliongea kwa nguvu akionyesha tabasam lake la ukichaa wakati akiwa anavumilia maumivu ya pigo la mwanzo.
Alikusanya mawingu kwa kasi ya ajabu ili kuanza kutengeneza radi na wakati huo huo alitoa Shoka lake na kumshambulia nalo Zeus.
Lakini sasa kumsogelea Zeus kwa ajili ya kumshambulia halikuwa swala jepesi hata kidogo kwani Athena ni kama alikuwa ashamtabiria ni njia gani Roma atapita na alitumia ngao yake ya Aegis kumzuia.
Bang!!!
Sauti kubwa ya kishindo ilisikika, radi pamoja na shoka lile viligongana na Ngao ya Aegis na ni ndani ya sekunde hio hio Athena alitoa ile ngao na kilichomkuta Roma ni pigo lingine la radi kutoka kwa Zeus.
BOOM!!
Shambulizi lingine la radi ya dhahabu lilimpata Roma na kufanya harufu ya kuungua kwa mwili kusambaa na Roma alijikuta akipiga yowe la maumivu huku akidondoka kutoka angani kama kimondo.
Radi ya Zeus kama ilivyosimuliwa na wagiriki inaweza kumshambulia adui na pasionekane mahali pa kujificha.
Radi hio ilikuwa na uwezo wa kumfuata adui eneo lolote hata kama ajaribu kukwepa vipi, hivyo ni sawa na kusema siku zote lazima ifikie shabaha, sasa ukijumlisha na uwezo wa Athena katika kutabili ilikuwa hatari kabisa kwa Roma.
Pengine dakika chache zilizopita alikuwa na uwezo wa kushambulia Mti Mama lakini muda huo ni kwamba hata uwezo wa kujilinda alikuwa hana na hata kama aamue kupokea mapigo ya Zeus kama alivyoamua kupokea ya Athena basi anaweza kuuliwa mara moja.
Haikushangaza kabisa kwani ki uwezo anaanza Zeus na kisha anaingia Athena lakini mara nyingi watu wanasema Zeus na Athena wapo levo sawa ila kinachomfanya Zeus kuwa juu zaidi ni kwamba Athena anao uwezo mkubwa wa kujilinda huku Zeus akiwa na uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi.
Kwa mfano kama ikatokea Zeus na Athena wakapambana inaweza asitokee mshindi kutokana na utofauti wao, Athena hatoweza kumshambbulia Zeus kutokana na kwamba hana mashambulizi imara na wakati huo huo Zeus kama atamshambulia Athena mashambulizi yake hayatopita kutokana na Athena kumiliki Aegis , ngao yenye uwezo mkubwa sana wa kukinga mashambulizi mengi.
Mpaka kufikia hatua hio ni kwmaba Roma hakuwa na uwezo wa kushambulia tena , kwani akishambulia Athena tayari ashatabilia mashambulizi yake na kuyakinga na ngao yake wakati huo huo Zeus radi yake ni kama ina ufahamu wakati wa kumshambuilia.
“Nadhani huu ni mwisho ambao hujautarajia?”Aliuliza Athena na sauti ya kikauzu huku akiwa na hali ya kihisia isiokuwa ikielezeka.
Roma ambae alikuwa akidondoka kutoka juu angani alijitahidi kutingisha kichwa chake kwa taabu.
Athena alikuwa na uwezo wa kumuongelesha Roma kutokana na kwamba alikuwa akishuka na Roma sambamba, tofauti ni kwamba Roma alishindwa kujizuia kudondoka wakati Athena ni kama anamfatilia Roma kwa karibu.
Sasa wakati alipomaliza kuuliza kwa kauli hio aliinua mkuki wake akinuia kumchoma nao Roma eneo la moyo.
“Sio kirahisi hivi , siwezi kufa kirahisi”Roma aliongea kwa sauti iliojaa maumivu.
“Kweli..?”
Muonekano wa Athena ulikuwa katika utulivu sana , yaani ni kama vile hana uadui na Roma lakini mikono yake ilikuwa tofauti.
“Pfff..!”
Mkuki wa Pallas uliokuwa ukitoa mng’ao wa rangi ya bluu ulikuwa tayari ushamchoma Roma eneo la kifuani kuingia kwenye moyo wake lakini hata hivyo haukuweza kupita kama ambavyo kila mmoja alitarajia .
Kabla Athena hajafanikiwa kumchoma kifuani , Roma alikuwa ashafanikiwa kuushikilia ule mkuki kwa nguvu usipite japo ya kwamba ulimchoma nchi kadhaa kuingia ndani lakini hakujali.
Damu ya moto ilimtoka Roma mkononi na kwenye kifua chake na kusambaa.
“Hatimae nimekukamata … Mkuki wako hatimae nimeushikilia na usione unaweza kuuchukua kutoka kwangu kirahisi”Aliongea Roma huku macho yake ni kama vile yanataka kumtoka pengine ni kutokana na maumivu.
“Kwel?”Athena aliuliza kana kwamba Roma alikuwa akiongea vitu visivyo na maana.
Sekunde iliofuata Athena alimbutua Roma na mguu wake kwa nguvu zote.
“Bang!!
Muda ambao Roma aliweza kusikia sauti ya kishindo alikuwa ni kama vile amegeuka kuwa satilaiti akiizunguka dunia huku yeye mwenyewe akijizungusha katika mhimili wake , kichwa chake kilipindishwa kwa angle mia na sitini na kwenda kuvaa mlima wa barafu.
Miungu wote waliweza kuona namna Roma alivyoenda kuvamia mlima wa barafu na kudidimia ndani asionekane kwa nje.
Athena alirudisha siraha yake iliokuwa imechafuliwa na damu na kuishia kuangalia sehemu ambayo Roma ametumbukia
“You… you can’t win against us”Athena alionekana kumung’unya maneno kwa lugha ya kingereza akimaanisha Roma hawezi kushinda zidi yao.
Zeus alieshikilia kitenesi cha shoti ya radi hatimae aliweza kufika juu ya barafu na alijikuta akikunja sura yake.
“Uungu wake unapotea kwa haraka sana!”Aliongea.
Miungu wengine na wao pia walifika kwenye barafu na waliweza kugundua pia uungu wa Hades unaisha kwa spidi kubwa mno
Ilikuwa ni kama kibatari ambacho kishaishiwa na mafuta na muda wowote kinakwenda kuzima na hio ndio namna uungu wa Hades ulivyokuwa ukipotea na palepale Christen machozi yalimjaa.
“Hades..!.ni kweli umeamua kumuua?”Aliongea Christen akimlaumu Athena akidhania amemuua Roma.
“Hapana, Aphrodite hebu tumia hisia zako kwa umakini, ijapokuwa uungu wake unapotea lakini mkandamizo wa nishati za mbingu na ardhi…”
“Uwezo wake unaongezeka … huyu mwanaharamu anatumia nafsi ya mnyama kuunyonya uungu wa Hades na kuubadilisha kuwa nishati za mbingu na ardhi”Aliongea Hera kwa kupaniki.
“Nini?!”Wengine wote sasa ni kama wanajua kinachotokea na kupiga kelele huku Zeus akiishia kumwangalia Athena.
“Hio ni mbinu yake nyingine?”Aliuliza Zeus lakini Athena hakukubali wala kukataa na wahenga wanasema kimya ni jibu hivyo moja kwa moja ilieleweka bila ya neno.
Dakika hio mlima wa barafu ambao ulikuwa katika hali ya utulivu ulianza kutingishika kwa nguvu kama vile unataka kuporomoka na ikafuatia wimbi ambalo lilikuwa likitoka chini yake.
Ni kitendo cha sekunde tu mlima wote wa barafu ulipasuka na kurusha mapande ya barafu juu angani kwa mita kadhaa na palepale Roma aliweza kuonekana tena ikiwa ni kama vile hakuwa ameumizwa eneo lolote.
Lakini muda huo miungu hao hawakuweza kabisa kumjua Roma kama mwenzao tena kwani uungu wa Hades ulikuwa ushamtoka kabisa.
Mtu ambae alikuwa mbele yao hakuwa tena Hades bali alikuwa ni binadamu mkamilifu mwenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Roma sio Hades tena kwani jina hilo lilitokana na nusu ya uungu wa Hades, hivyo ni sawa na kusema Roma amerudi kuwa Denisi binadamu kamili aliezaliwa duniani.
Uungu ndio mzizi wa miungu au unaweza kusema ndio asili yao ambao hubeba uwezo wao wa hali ya juu sana na kuwafanya kuwa na nguvu kubwa ya kiroho mpaka kuwawezesha kuhama kutoka katika mwili mmoja kwenda katika mwili mwingine.
Chaos ni mnyama wa machafuko ambae anao uwezo wa kumeza kila kila kitu ndani ya ulimwengu, hivyo hata kwa uungu ni kitu ambacho kinaweza kumezwa na Chaos kutokana na kwamba uungu hubeba nguvu ya kiroho ambayo chanzo chake sio ardhi bali ni ulimwengu(Universe).
Roma aliamua kufikiria nje ya boksi na akaamua kuitumia nafsi ya Chaos kuumeza uungu wa Hades ambao alikuwa akimiliki kwa ajili ya kupandisha uwezo wake kwa levo ya juu zaidi ndani ya muda mfupi.
Mara baada ya kufufuka kwa moyo wa Gaia uungu wa Hades na wenyewe ni kama ulikuwa unapona na kufikia uwezo ambao ni sawa na mapigo elfu moja ya radi.
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba Roma alikuwa na uwezo wa kutumia kanuni za anga na kama utamfananisha na mtu anaevuna nnishati za mbingu na ardhi basi ni katika levo ya mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi uwezo ambao ni wajuu sana.
Sasa unapaswa kuelewa mara baada ya Chaos kumeza uungu wa Hades aliugeuza kuwa nishati ya mbingu na ardhi ambayo moja kwa moja ilienda kwa Roma.
Sasa katika mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi Roma alikuwa levo ya mapigo mengi ya radi huku upande wa kanuni za anga ni hivyo hivyo , kwa lugha nyepesi ni kama Roma ameunganisha uwezo wake wote kuwa kitu kimoja yaani alichanganya uungu wa Hades na nishati ya mbingu na ardhi.
Zamani ilimpasa Roma kutumia kanuni za anga peke yake na vilevile nishati za mbingu na ardhi peke yake , lakini muda huo vyote vilikuwa pamoja mara baada ya kufanikiwa kuubadilisha uungu kuwa nishati ya mbingu na ardhi.
Ukweli ni kwamba hio ndio mbingu ya kipekee ambayo Roma alifanya na miungu hawakutarajia kabisa.
Maana kitendo cha kufanya hivyo ni kama Roma kaamua kuachana na amswala ya kanuni za anga kwa ajili tu ya kuongeza uwezo wake.
Bila hata ya maelezo kutoka kwa Athena miungu hao walijua ni namna gani uwezo wa Roma umeongezeka na kuwa wa kutisha.
“Mkandamizo wa nguvu zake ni mkubwa mno , nashindwa hata kuangalia ni levo gani kafikia, ukijumlisha na uwezo wake wa mwanzo naogopa kusema kwasasa kafikia levo ya mapigo elfu kumi ya radi”Aliongea Hera akiwa na wasiwasi .
Roma sasa ni kama amekidhi vigezo vya kupambana na Zeus na Athena kikamilifu..
******
Sharif , Aoiline na wengine wote walikuwa wakiangalia kilichokuwa kikitokea katika ncha ya kaskazini kwa kutumia kioo cha maajabu.
Clark mwanzoni alijua Roma ameshindwa vita na kumfanya aanze kulia lakini mara baada ya kumuona mpenzi wake akisimama tena akiwa na uwezo uliongezeka haraka hakuweza kujizuia na kushangilia kwa furaha.
“Hehe .. huyu mtoto hatimae amegundua kwanini Hades alimwachia nusu ya uungu wake bila fahamu , alipaswa kujua siri hii mapema kama angeacha kujali sana maswala ya wanawake…”Aliongea Sharif.
Moja ya sababu kubwa ya Athena kumuomba Hades kutii takwa lake na kumwachia Roma uungu ni kwasababu tu alitaka kuweza kumtabiria kirahisi hata kama apande levo za juu sana , ilikuwa rahisi kumtabiria Roma kupitia uungu kuliko akiwa binadamu kamili.
Yaani kwa lugha nyepesi uungu wa Hades katika mwili wa Roma ilikuwa ni njia ya mawasiliano ya kinabii kati ya Roma na Athena.
Kulingana na maelezo ya Sharif kitendo cha Roma kufikia levo ya mapigo elfu moja ya radi ilimaanisha Athena hana uwezo tena wa kumtabiria lakini ajabu ni kwamba Athena bado alikuwa na uwezo wa kumtambiria Roma hio yote ni kutokana na uungu wa Hades ambayo ni njia ya mawasiliano.
Sababu ya pili Athena kutaka Roma aachiwe uungu ni kwa ajili ya kumfanya kuwa sehemu yao.
Ikumbukwe mara baada ya Athena kufika duniani aliweza kuangalia nini kitakuja kutokea mbeleni na kupitia unabii wake aliweza kugundua ni binadamu Roma Ramoni atakaeweza kuzuia mipango yake ya kufufua ndugu zake.
Sasa kwanzia miaka elfu ishirini iliopita Athena alikuwa akipambana na unabii kwa kubadilisha historia.
Kitendo cha kutaka Hades kumpatia Roma uungu ukiachana na dhamira ya kutaka kumtabiria kwa urahisi lakini vilevile alitaka kumfanya mmoja kati yao.
Lakini kitu ambacho Athena hakukifahamu ni kwamba Hades alikubaliana nae kirahisi akiwa na ajenda nyingine kabisa, kwa Athena Roma alipewa uungu kwa ajili ya kurahisisha mipango yake kwa Hades wa Zamani alimwachia Roma uungu wake kwa ajili ya kukwamisha mipango ya Athena.
Hivyo Roma kutumia uungu kupandisha uwezo wake ndio kete ya mwisho ambayo Hades wa Zamani alitarajia Roma kuicheza ili kuja kumshinda Athena na wenzake lakini hata hivyo hakumwambia Roma juu ya siri hio, ni kama alimpa mtihani wa kugundua yeye mwenyewe.
Hayo yote Sharif aliyajua tokea mwanzo wa mpango LADO unaanzishwa na yeye pia hakutaka kumpatia Roma siri hio kama anao uwezo wa kupandisha mara mbili uwezo wake kupitia uungu wa Hades.
Sasa Roma alishindwa kugundua siri hio mapema kutokana na Christen mpenzi wake Hades wa zamani kuwa rafiki yake, pengine kama asingekuwa na mfungamano wa kirahifi na Christen angeweza kugundua siri hio mapema sana.
Sasa Sharif alikuwa kwenye mshangao mara baada ya kuona Roma anazidi kushambuliwa na Athena na Zeus bila ya kutumia uwezo wake wote, yaani uungu wa Hades, alijiuliza au bado hajajua siri hio.
Sharif hakuwa mjinga kumtaka Roma apambane licha ya kwamba kimahesabu levo aliokuwa amefikia kulinganisha na wapinzani wake ni ndogo lakini ukweli ni kwamba hakuwa akibahatisha , alikuwa akijua tokea mwanzo njia pekee ya Roma kushinda ni kutumia Chungu chake kuubadilisha uungu kuwa nishati za mbingu na ardhi na kupandisha uwezo wake kwa haraka.
Aoiline macho yake yalicheza na haikujulikana anafikiria nini na aliishia kuangalia kioo bila ya kuongea neno.
Xumei na Mzee Yasu walikuwa na furaha , ijapokuwa walikuwa wakiyaheshimu maamuzi ya mwalimu wao kwa kuwapa binadamu na miungu nafasi sawa , wao walikuwa bado ni binadamu na walitamani kuona Roma anawaua miungu wote na dunia kubakia salama.
Sharif alikuwa ni kama Hades wa zamani tu wote walikuwa Neutral , Sharif hakutaka kuwazuia miungu kutokuitawala dunia kama uwezo huo wanao lakini pia hakutaka kujisumbua kama binadamuw atashindwa kulinda dunia yao.
Kama miungu wangeshinda na Mkuu wa Enzi kutokuingilia basi moja kwa moja Dunia ingekuwa chini ya miungu , kama binadamu wangeshinda kwa kuilinda sayari yao basi pengine ndio mapenzi ya Mkuu wa enzi, na moja kwa moja uangalizi angemkabidhi Roma
Hakukuwa na haja ya kati y a miungu kuwa na muangalizi kwani alijua fika wanao uwezo wa kuilinda sayari lakini kwa binadamu wote waliwakilishwa na Roma hivyo kama Roma angeshinda ilimaanisha ndio yeye kati ya binadamu wote mwenye uwezo wa kuilinda dunia.
*****
Muda huo namna ambavyo miungu walimwangalia Roma haikuwa ikielezeka kama walikuwa wakihisi kitu cha namna gani kwenye mioyo yao.
Mara baada ya kupoteza uungu, Roma alikuwa sasa amekuwa adui yao kikamilifu , hata kwa Apollo na Poseidon ambao walikuwa na urafiki na Roma hawakuwa na huruma nae tena.
Walikuwa wakimchukulia kama mwenzao kwasababu ya uungu wake na sio kwasababu alikuwa binadamu.
Lakini kubwa zaidi kwa wakati huo ni kwamba Roma alikuwa tishio kubwa kwa ajili ya ufufuo wao.
“Inavutia sana kwa ulichofanya , ni kheri kuua binadamu aliekamilika kuliko kumuua kaka yangu Hades”Aliongea Zeus huku akitoa kicheko kizito.
Upande wa Roma ni kama vile hakuwa akimsikia Zeus anachoongea na alikuwa amefumba macho yake huku akichanua mikono yake kama vile anaomba baraka kutoka juu mawinguni.
Ni dakika hio hio waliweza kuhisi kitu cha ajabu , kutoka kila pande nguvu kubwa ya kiroho ilikuwa ikijikusanya kumsogelea Roma.
Roma alikuwa ni kama sumaku na kuanza kuvuta kila aina ya nguvu ya kiroho iliokuwa karibu yake
Nguvu hio ya kiroho ilimwingia Roma na kubadilika kuwa nishati ya mbingu na ardhi na kuzidi kufanya sehemu ambayyo Roma amesimama kuwa na upepo mkali unaomzunguka kama kimbunga.
Kitendo cha upepo mkali kumzunguka Roma ilifanya kuwa ni kama Dhoruba ya kimbunga kikali na kufanya hewa kusukumwa kwenda juu angani kwa spidi kubwa , hatimae sehemu ambayo Roma alikuwa amesimama hakukuwa na hewa ya aina yoyote ni sawa na kusema Roma alikuwa ndani ya Ombwe(vacuum)
“Hii ni hatua ya mwisho ya mapigo ya radi , levo elfu tisa mia tisa tisini na tisa ya radi, levo ya mwisho wa Dhiki na mwanzo mwa ufunuo mkuu”Aliongea Hera ambae ni kama sauti imempotea.
Hakuwahi kushuhudia radi ya levo hio na inakwenda kuwa mara yake ya kwanza , ukweli ni kwamba ni majini wachache sana ambao wameshuhudia radi ya mapigo elfu kumi na wengi wao waliamini ni ngano tu katika vitabu.
“Ukali wa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi kumzunguka ni kama chuma kigumu , hii ndio levo ya mwisho kabisa ya ufahamu wa mbingu..”Aliongea Hephaestus akiwa katika mshangao.
“Inaonekana hii levo ya dhiki ya mwisho haitokei kwa kukusanya mawingu , hicho kizingia cha nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi kinataka kufanya nini?”Aliuliza Apollo kwa mshangao.
“Mnashangaa nini sasa , tumieni nafasi hii kabla Dhiki haijaisha , muueni”Aliongea Hermes.
Zeus ni kama amekumbuka cha kufanya na palepale aliongezea nguvu ya radi iake na kuirusha katika eneo ambalo Roma amesimama.
“Chwiiiii….!!!”
Dakika ambayo radi ile inataka kumkaribia Roma ilizuiwa na kizuizi ambacho hakionekani na kusababisha msuguano kama vile ni wa breki a gari uliopelekea mlipuko.
“Ule ni ulinzi wa kiroho?!”Hera aliuliza akiwa katika hali ya mshangao mkubwa
“Hicho kizingia kimemzunguka tayari na inaonekana ni kama ulinzi”Aliendelea kuongea.
Miungu walikumbwa na mshangao mkubwa mara baada ya kuona radi ya mapigo elfu kumi ilikuwa na tabaka lake la kumlinda mpitia Dhiki.
Kizingia cha mkusanyiko mkubwa wa nguvu ya kiroho ilikuwa ni tabaka la ulinzi kwa mtu yoyote au jini anaepitia mapigo ya levo ya mwisho wa Dhiki ili asiwe na mawasiliano na ulimwengu wa nje na isitokee yoyote wa kufaidika.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba radi hio inampata yule tu ambae anapitia mapigo hayo na si vinginevyo na ombwe ambalo limetengezwa na kizingia hicho ni kama njia maalumu ambayo radi itapita.
Ukweli ni kwamba sio kama radi hio inataka kumlinda Roma au nini bali ili radi hio kuweza kutokea lazima kuwe na mkondo maalumu , ni kama mfereji au useme njia maalumu ya radi hio kupita.
Roma alikuwa amesimama kwenye ombwe hilo la kisingia akiwa ametulia kabisa huku macho yake akiwa ameyafumba , ni kama vile alikuwa amesahau kila kitu kinachoendelea ulimwengu wa nje.
“Uzio umeweza kuzuia radi kupita , inamaana huo ulinzi una nguvu kiasi hicho”Walishangaa.
Hata radi ya Zeus ambayo ilisifika kwa ukali haikuweza kupita au kusababisha mtingisho wa aina yoyote ile
Miungu hao hatimae washajua hawana uwezo wa kumshinda Roma akiwa ndani ya kizingia na waliishia kuangalia namna anavyopitia mapigo ya radi.
Zues uso wake ulikunjamana , macho yake yaliwaka mwanga na aliongea kwa sauti.
“Kwasababu mambo yamefikia hatua hii , basi na tuogeni utukufu wa Mama Gaia na turudi katika miili yetu ya Titani”Aliongea Zeus.
Miungu walimwangalia kwa mshangao mkubwa kutokana na maamuzi yake.
“Zeus ni lazima kufanya hivyo ..tutakula nguvu nyingi kutoka kwenye Mti Mama na uungu unaochipua utanyauka na kuzuia roho nyingine kuchelewa kufufuka”Aliongea Poseidon kwa uangalifu.
“Naunga mkono , hata kama atafanikiwa kupita levo ya mapigo elfu kui ya radi uwepo wako na Athena ukijumlisha na sisi haina haja ya kurudi katika miili yetu ya Titan”Aliongea Hera.
“Na tuanzeni , tunahitaji kurudi katika miili yetu ili kumaliza hii vita”Aliongea Athena ambae alikuwa kimya muda wote.
Miungu walijikuta wakishangaa na kwasababu alioengea ni Athena basi waliamini kuna sababu hivyo maamuzi ya Zeus kutokupingwa na wengine.
Ijapokuwa baadhi yao waliona haina haja ya kwenda mbali hivyo lakini kilichokuwa mbele yao ni vita ambayo hawapaswi kushindwa.
Mwishowe miungu wote walifanya maamuzi na kupaa mpaka kwenye kilele cha mti mama na kutengeneza duara.
Sekunde ileile miungu wote walianza kutoa miale ya mwanga na anga kuwazunguka lilianza kupinda pinda na kucheza huku eneo la katikati nguvu ya kiroho ikichemka kwa kasi kubwa.
Kadri walivyokuwa wakiendelea kiasi kingi cha nguvu ya kiroho kiliungana na Mti Mama na palepale mwanga wa dhahabu uliokuwa kama uji uliwafunika wote hata wasiweze kuonekana kwa nje.
Muda huo huo upande wa Roma ambaye alikuwa kwenye kisingia cha nguvu ya kiroho hakushituka hata kidogo licha ya kujua kila kitu kinachoendelea nje yake, alikuwa amezama kwenye utambuzi wa Adhabu ya mapigo ya radi.
Roma alikuwa akiitikia wito wa mapigo elfu kumi ya radi na kupanua ubongo wake kukwea katika mbingu za ufahamu , kujua asili ya vitu vyote na kutafuta uthibitisho.
Upande wa miungu walikuwa tayari washafanikuwa kuunganisha ufahamu wao na mti mama na miili yao ilizidi kufuka miale ya mwanga.
Katika anga hilo ndani ya ncha ya kaskazini hatimae sauti zilipaa angani na kugonga huku na huko mawinguni, zilikuwa ni sauti za wimbo ambazo lugha yake haikufahamika.
Hio ndio lugha ya miungu waliokuwa wakitumia.ilikuwa ni ushairi(Ode) ambao miungu pekee ndio wanaoweza kuelewa.
“Wakati wa kuyeyuka kwa barafu juu ya Olympos , ukuu wa mungu utatanda ulimwenguni kote, tutauvaa utukufu wa ardhi na kuzisikiliza sauti za ngurumo ya radi , mambo yote chini ya utawala wa kifalme wa miungu milele ivukayo kesho, Hiki ni kizazi cha Titani”
Waliimba kwa kurudia rudia maneno na kufanya dunia yote sauti zao kusambaa kwa kasi sana.
Na muda uleule mti ule ulianza kufuka mwanga wa rangi ya Dhahabu na kuvamia juu ya duara walilotengeneza miungu , huku mwanga ule ni kama vile unazama mwilini na kuungana.
Miili ya miungu ilikuwa ni mwanga kulingana na aina ya nishati na kufanya kila mtu kung’aa kwa namna ya kipekee , huku ming’ao yao ikiendelea kuongezeka na kupanuka na nguvu yao ya kiroho ilizidi kuongezeka maradufu na kufanya mkandamizo wa hewa kuwa mkubwa kuliko isivyokawaida.
Mwili wa rangi ya Dhahabu na bluu ulionekana kutoka kwa Zeus , mwili wa jitu kabila la Titani , Zeus ndio aliekuwa wa kwanza kubadilika na ndani ya sekunde tu alikuwa ni jitu likubwa mno.
Mara baada ya kunyanyua mguu wake na kukanyaga juu ya bahari barafu yote ilipasuka pasuka vipande vipande na wimbi alilosababisha lilitengeneza Tsunami.









SEHEMU YA 794.
Ili kurudiwa na uwezo wao asilimia mia ilikuwa ni lazima warudi katika miundo yao ya Kititani , ilikuwa ndio njia moja tu ya kujipandisha ki uwezo zaidi na zaidi.
Ndani ya dakika chache tu mti wote ulipoteza nishati ya kutosha kwa kuwavalisha miungu miili yao kupitia uungu.
Ijapokuwa walikuwa wamekosa damu ya Titani kama ilivyokuwa kwa miili yao ya awali Mti mama ulikuwa na uwezo wa kuwapatia nguvu ileile.
Kitendo hicho kingeweza kusababisha mti kuathirika na kusababisha uungu uliokuwa ukihipua kunyauka kwa kiasi kikubwa lakini hilo ni swala ambalo miungu hawakutaka kulifikiria kwa wakati huo.,
Walihitajji nguvu ya kutosha kwa ajili ya kumdhibiti Roma ambae anapitia levo ya mwisho ya mapigo ya radi.
Kilichokuwa kikiogofya ni kwamba ukijumlisha na mwili wa kititani wa Zeus , miungu wote wlaikuwa wamebadilika kutoka katika miili ya kibinadamu na kuwa katika maumbvo yenye nguvu kubwa.,
Kama ambavyo binanamu huitwa binadamu , jini kuitwa jini na malakka kuitwa malakika ndio ilivyokuwa kwa iungu hawakuwa binadamu tena walikuwa ni Watitani.
Walikuwa na maumbo marefu mno ni kama vile viuno vyao ndio vinatenganisha mbingu na ardhi
Kila dakika walivyopiga hatua walisababisha wimbi kubwa la upepo na kila dakika walivyochezesha mkono ilikuwa ni Dhoruba.
Mara baada ya miungu yote kuzunguka mti ,mti huo haukuwa mkubwa tena.
Kitu kingine cha ajabu zaidi ni kwamba Dhana zao walizokuwa wakimiliki na zenyewe zilikuwa zimeongezeka ukubwa , haikujalisha ni Athena ngao yake au upinde wa Apollo na Artemis kila kitu kiiongezeka ukubwa kulingana na miili yao.
Bila shaka kama hazikuongezeka basi zisingeweza kuitwa Dhana za kititani.
Kuwa katika miili ya kititani iliwapa uwezo wa juu sana wa kutengeneza mashambulizi , kitu kikubwa zaidi miungu hao walikuwa wakipata bado nishti kutoka kwenye mti mama.
Jua , bahari , madini na kila kitu kingine ni rasilimali za kulisha siraha zao na ngao zao pamoja na miili yao.
Miili yao ilikuwa ni nishati , haikuwa miili ya nyama kama ya kibinadamu , ilikuwa ni kama wamegeuka na kuwa mwanga lakini katika maumbo ya watu.
Lekcha na wao kulikuwa na tofauti kidogo tu , pengine Lekcha alikuwa na mwili wa nishati wa Ant matter lakini wao walikuwa na miili ya kinishati inayotokana na Mti mama , nishati ambayo ilionekana kabisa wanapaswa kuipata ili kuendelea kuishi.
Pengine siku mmoja nishati ya dunia itaisha lakini wasingejali , pengine wangeweza kutafuta sayari nyingine na kurudisha uhai wao kama waivyovamia dunia.
Sasa kitendo cha miungu hao kupata miili yao ya kinishati , miili ya Titani inawafanya kuwa katika muonekanno wao wa awali isipokuwa tu kwa Zeus ambae mwili wake alionekana kuudumisha hivyo kumfanya kuwa na mwili wa damu na sio wa nishati kama wenzake.
Hera alikuwa amevalia taji la shaba huku mwili wake wote ukitoa mwanga wa rangi ya Cyani, mkonno wake wa kulia mkubw aulikuwa umeshikilia Golden Apple huku vazi lake likifanana na mng’ao wa mwanga aliokuwa akitoa.
Viumbe hao kwa jinsi walivyokuwa wakitoa mwanga wa ajabu pengine unaweza kuwafananisha na malaika kwa jinsi walivyosimuliwa tofauti tu ni kwamba walikuwa na maumbo makubwa kuliko malaika lakini kwa jinsi wlaivyokuwa wakitoa mngao wa kuumiza macho inaweza kuwa moja ya sifa ya kufanana.
“Kwasababu aaendelea kupitia Dhiki , tutamshabulia kwa uwezo wetu wote na pengine tunaweza kuvunja kizuizi kinachomlinda”Aliongea Hera,
Mara baada ya kubadilika katika maumbo yao ya kititani sauti zao ni kama zinatoka juu angani na kufanya sauti kusambaa umbali mrefu sana kama sio dunia nzima.
“Hatuwezi kuvunja , ilishapangwa kufanikiwa kufikia katika levo hio ya mwisho wa dhiki ya radi”Sauti ya Athena iligonga ngoma zao a masikio
Athena yeye alikuwa akitoa mng’ao mtakatifu wa rangi ya fedha , nywele zake ndefu zilionekana kuwa laini kupita kiasi zilizojisokota kwa kutengeneza mawimbi , alidhihirisha ushujaa na kufanya sura yake isichoshe kuangalia.
Kama malaika alikuwa amevalia na yeye gauni la kitambaa cha hariri huku eneo la kifuani kukiwa na mchoro wa jani la mzeituni , alinyoosha mikono yake na kuinua ngao ya Aegis usawa wa kifua chake na Siraha ya Pallas upande wa kulia , chuma hicho kilitoa mngao na msisimko unaoendana na mwili wake.
“Unaweza kuona nani anakwenda kushinda ?”Aliuliza Poseidon ambae alikuwa ameshikilia Chusa kubwa ya meno matatu.,
Mfale huyo wa bahari alikuwa katika muonekano usiokuwa ukivutia m nywele zake zilikuwa zimetapakaa na alikuwa na mwili mkubwa unaotoa mng’ao wa rangi ya bluu , alikuwa na mgogo wenye ncha kali kama vile ni mnyama wa baharini , kuanzia kwenye kiwiliwili kwenda chini alikuwa na umbo kama la nyoka wa baharini.
“Mimi na Zeus katika miili yetu uwezo wetu ni sawa na kusema levo a mapigo elfu kumi ya radi , uwezo wa Roma mara baada ya kuipita Dhiki ni sawa na wa kwetu au uliongezeka kidogo , kwa adui wa uwezo huo pamoja na kutokuwa na uungu unabii wangu hauwezi kuwa sahihi”Aliongea Athena akimjibu Poseidon,
“Haiwezekani , haijalishi ni kwa spidi kiasi gani uwezo wake unaongezeka hawezi kufikia mwisho mwa levo mwa mapigo elfu kumi ya radi “Aliongea Hephaestus mungu wa moto.
Alikuwa na nywele ambazo ni kama vile zinawaka moto akiwa nusu mtupu na mwili wake wa rangi ya shaba , alikuwa na utimamu wa kutosha wa kimwili na misui yake imepinda pinda kama jiwe huku akiwa na makovu kama vile yamechongwa katika mwili wake makusudi , upande wa hini kabisa alikuwa amevalia suruali ambayo imeunganisha na vyuma kwa namna flani hivi kama magamba.
Ijapokuwa alikuwa jitu kubwa sana, muonekano wake ni kama ulikuwa ukiadilika badilika na kumfanya kuwa mwepesi kama mwewe.
“Wewe Hephaestus kwanini usijaribu na hilo nyundo lako kuvuruga Dhiki yake?”Aliongea Hermes huku akitoa kiheko.
Tofauti ya Hermes na wengine ni kwamba hakuwa na mwili mkiuubwa na alikuwa na muonekano kama wa binadamu lakini sura yake ikiwa imezidi uzuri kimuonekano , alikuwa na kiuno chembamba mno, alikuwa ni kama vile amevaa vazi la kutengenea ambalo limeunganishwa na mbawa.
Hakuwa mpana sana bali alikuwa mrefu kwenda juu na kumfanya kuonekana kuwa mwepesi zaidi.
“Unadhani nashindwa kufanya hivyo , kwanini uwezo wa sisi Titanni kuwa mdogo mbele ya binadamu?”Alliongea Hephaestus kwa jeuri na palepale aliinua lishoka lake juu ambalo liliweza kushika moto mara moja na kuanza kuyeyusha anga.,
Faida nyingine ya miili ya kititani ni kwamba miili yao imeunganishwa na namna kanuni za anga zinavyofanya kazi , mashambulizi yao hayakuhitaji kutumia kanuni za anga kwa nia maalumu bali anga lenyewe ndio huwapatia nguvu.
Ni kama Hephaestus alivyoinua tu nyondo yake palepale ilishika moto na kuana kuunguza anga,
“Nyundo ya moto mtakatifu”
Hephaestus aliruka huku akifyatua lile linyundo na kulifanya lionekane ni kama linadondoka mahali Roma alipo , nyundo hio ilienda moja kwa moja kuvamia kizingia kilichomfunika Roma.
BOOM!!!
Mshindo mkubwa wa sauati uliweza kusikika mara baada ya kizingia kutingishika , nguvu yake ilisambaa kila kona
Wimbi hilo lililoambatana na moto liliyeyusha barafu yote iliokuwa katika nha ya kaskazini na kuwa bahari kikamilifu,
Lakini bado tu licha ya kizingia hicho kupigwa na kanuni za anga kupitia nyundo hakikuharibika wala kusogea hata kidogo
Hephaestus aliishia kukunja sura na miungu wengine pia walikuwa katika hali ya mshangao.
“Ni tabia gani ya ki elementi imetumika kutengenezea nguvu ya kiroho mpaka kutfengeneza kizuizi chenye nguvu namna hio kiasi cha kutoarhirika na kanuni za anga?”Aliuliza Hera.
Upande wa Roma alikuwa akijua mabadiliko ambayo yametokea upande wa ncje na uwezo wa miungu ulikuwa umeongezeka katika levo nyingine kabisa na wanajarbu kuigilia Dhiki yake,
Lakini ujio wa radi ya mapigo elfu kumi ulimfanya kutojali sana kile kinachoendelea
Katika Ombwe la mfereji uliotengenezwa na nguvu za kiroho hali ya giza ilitanda huku msukumo wa mawimbi ya hewa yakiongezeka na msisimko wa nguvu ya ajabu ulivamia ndani yake.
Kadri msisimko wa nguvu ya kimaajabu kungezeka ndivyo namna uzio uivyoendelea kuimarika zaidi na zaidi , kisingia kilizidi kuzunguka kwa kasi kubwa mbo na kufanya mfereji wa ombwe kuzidi kwenda angani
Roma aliweza kuhisi mvutano wa hali ya juu mno wa nguvu ya ajabu na tabasamu la ahueni lilijjionyesha kwenye midomo yake
“Kwahio kumbe ipo hivi”Roma alijisemesha moyoni.
Dakika ileile ilikuwa ni kama vile nyoka mweusi anashuka kutoka juu angani kupitia lile ombwe la mfereji na kufanya iwe kitu cha ajabu mbo kwa miungu wote waliokuwa katika eneo hilo.
Ukiachana na Sharif na Aoiline wlaiokuwa katika ulimwengu unaojitegemea hakuna ambae alitarajia radi ya mapigo elfu kumi ni nyeusi.
Radi hio yenye rangi nyeusi ya kimaajabu ilionekana kama vile ni wino na urefu wake ulifanya kuwa kama kamba nyeusi ndefu inayoheza cheza kutoka juu mawinguni,
Kilichowashangaza zaidi ni kwamba , radi hio nyeusi ilishuka bila ya ngurumo , yaani hali ilikuwa tulivu mno na ilikuwa ni kama hakuna kilihokuwa kimetokea.
Mandhari yalikuwa ya kimaajabu kwa wote na walizidi kuona ni maajabu mara baada ya pigo la radi kumfikia Roma bila ya sauti kabisa.
Waliweza kumuona Roma ndani ya ombwe la mfereji akiwa amezingirwa na ile radi nyeusi.
Radi hio haikutoa mwanga kama radi nyingine , ki ufupi ni kwamba unaweza kusema sio radi ni kitu kingine kabisa
Ukichana na mfereji huo mazingira yanayozunguka eneo hilo yalikuwa hayajaaathirika hata kidogo hata bahari iliokuwa chini ya Roma ilionekana kuwa tulivu.
“Hii ndio radi ya mapigo elfu kumi kwanini ni nyeusi?”Aliuliza Hermes lakini ilikuwa wazi miungu wote waliokuwa ndani ya hilo eneo hawakuwa na majibu.
Roma ambae alikuwa amezingirwa na kiza cha radi nyeusi ni kama vile alikuwa kwenye ulimwengu mwigine kabisa.
Akiwa amefumba macho yake aliruhusu radi ile nyeusi kuungana na mwili wake kidogo kidogo.
Alizuia pumzi na kuindoa akili yake katika mazingira ya mbingu na ardhi , alikuwa pia amezuia nishati za mbingu na ardhi kutofanya kazi .
Katika macho yake alichoweza kuoa ni anga lisilokuwa na mwisho , Roma aliweza kugundua alikuwa katika kundi la nyota za galaksi ya Milk way.
Nyota alizokuwa akiona zilitoa mingao ya kucheza cheza kama vile ni madini ya thamani kubwa yaliokuwa gizani.
Ulimwengu ulikuwa katibu yake na kumpa hali flani ya ukawaida ambayo hakuwahi kuihisia hapo kabla , katika eneo ambalo akili yake ilikuwa mwili wake ni kama vile ulikuwa ukijongea bila shida yoyote na kumfanya kusafiri mamilioni ya maili ndani ya sekunde tu.
Alikuwa ni kama samaki anaeogelea katika maji mengi au ndege anaepaa angani , ulimwengu aliokuwa ulimshangaza sana.
Radi ile iliendelea kuwa endelevu ikimzunguka kana kwamba inamlaki Roma . haikumletea maumivu yoyote wala usumbufu.
Lakini sasa Roma kila alipojaribu kuishikilia na mkono wake alishindwa kabisa
“Nini nakosa , bado nashidwa kuidhibiti?”Roma alijiuliza.
Katika radi hio Roma alikuwa akiona kabisa nishati za aina tatu ambazo ni kama anazijua
Nishati ya moto wa Zambarau , moto wa rangi ya bluu na moto wa rangi ya samawati”
Ni radi au moto wa rangi tatu ambao umetokana na elementi za moto , maji na nishati ya hasi na chanya lakini ajabu ni kwamba nishaati zote tatu zilionekana kuungana pamoja na kutengeneza radi hio nyeusi.
Kuungana kwa moto wa zambarau na bluu kunatengeneza radi ya mapigo tisini na tisa , kuungana kwa moto wa bluu na samawati ilitengeneza radi ya mapigo elfu moja ya radi
Je kuna uwezekano wa radi ya mapigeo elfu kumi kutokea kwa kuunganishwa kwa elementi zote tatu za moto ? hapana…
Kwa akili zake za haraka aliwez akuhisi kuna kitu cha ziada kilihokuwa katika hio radi ya kimaajabu , ilikuwa na nguvu zaidi kuliko elementi zote tatu za rangi ya moto.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kutokea kwa radi hio nyeusi ni unganiko la nguvu za aina nne na kufanya radi hio kuvuka vizuizi vya kanuni ya nafasi na muda na nguvu yake ni kama ufunguo wa kuvunja vizuizi vyote vya mbingu na ardhi na kumfanya kuingia katika ulimwengu wa anga.
Roma alikumbuka swali la Clark akimuuliza je anao uwezo wa kupaa kwenda anga za mbali bila shida yoyote na alimjibu kwamba hawezi kwasababu hana nishati ya kutosha kuishi katika anga za mbali
Sasa radi ilikuwa mbele yake ilikuwa ni kama ufunguo wa kumuwezesha kwenda anga za mbali
Bila kujielewa Roma alikuwa ameingia katika mbingu nyingine yenye ufumbuzi tofauti na muda ulikuwa umesimama na kanuni za anga ni kama hazifanyi kazi katika mbingu hio.
Alikuwa ni yeye na ulimwengu ulikuwa wake, ilikuwa ni kama amefanaishwa na ulimwengu wa anga za mbali.
Taratibu kila kitu katika ulimwengu wake wa kawaida kilipotea , miungu waliokuwa wakimshambulia , Mti mama , bahari , hewa , dunia , anga na kila kitu kilipotea.
Hata zile nyota ambazo zlikuwa akiangalia zilianza kupotea tena katika ufahamu wake na hakuona tena , lakini sasa hata kama kila kitu kilikuwa kikipotea katika ufahamu wake hata muda kusimama lakini kila kitu kilikuwepo licha ya kuonekana kutokuwa na athari zozote,
Hio ndio ilikuwa ni asili ya anga tokea mwanzo , hio ndio ilikuwa ni nishati ya awali kabisa iliokuwa imefunika kila kitu ikiwemo dunia na sayari nyingine.
Roma kwa haraka sana alihisi ni kama alikuwa na macho manne ambayo mawili yametokea ndani kabisa katika nafsi yake, yaani ilikuwa ni kama vile kuna mtu anaemfunilia kila kitu kilichokuwa mbele yake.
Kila kitu alichofahamu kuhusu ulimwengu kilibadilika kabisa kutoka katika ujazo mpaka kuwa mtupu na tena kutoka kuwa mtupu mpaka ujazo.
Radi ya mapigo mengi ilikuwa imebadilika mara moja kutoka kutokushikika mpaka kushikika.
Kwa kutingishika tu hatimae aliweza kurudi kutoka uliwengu wa ufahamu mpaka katika uhalisia na kilichofuatia ni tabasamu la kutoka katika ujinga lililopamba uso wake na alianza kucheka kwa furaha kubwa kiasi cha kumfanya atingishike mwili na taratibu akayafumbbua macho yake.
Katika ombwe la mfereji ile nguvu ya kimaajabu ni kama ilihisi kitu na kuanza kujikusanya kwa kujitosheleza.
Kizingia kilichokuwa kikimzunguka kilianza kupotea taratibu na hatimae kabisa na kufanya iwe ni kama hakuna kilichotokea na amani ikarudi duniani.
Jambo hilo liliwashangaza miungu kwa mara nyingine , radi ya mapigo elfu kumi haikuwa kama matarajio yao kwani ilipiga mara moja tu na kisha kupotea.
“Hapo tunaweza kusema kafanikiwa ?”Aphrodite aliuliza akiwa na muonekano usioelezeka.
Kama alivyopewa utu wa jina la mapenzi na urembo hakika alikuwa na muonekano wa kuvutia mno , alitoa mng’ao wa rangi ya dhahabu , mtu anaweza kumsifia kwa kumfanya kielelezo cha ustadi safi , gauni lake la hariri nyeupe lilipambwa na udarizi wa maua yaliochanua na ndege wa dhahabu anaeruka , kiunoni alikuwa amefunga mkanda wa dhahabu ambao ulikuwa na utajiri wa mchoro wa kuvutia mno, mkanda huo ndio ulipewa jina la Magical Girdle.
“Nashindwa kuhisi mkandamizo wowote kutoka kwenye nguvu ya nishati na mbingu , hivyo ninaamini atakuwa amefanikiwa kupita Dhiki kwa asilimia mia moja”Aliongea Zeus akimjibu Aphrodite.
“Vyovyote vile , hii ndio vita yetu ya mwisho”Aliongea Ares.
Ares alikuwa ni kama vile ni mwanavita wa zama zile za kale , ukiachana na mkuki wake mrefu wa chuma alikuwa amevalishwa mwili mzima na cchuma kizito na kumfanya aonekane pua tu.
“Wote kaeni pembeni katika hili na mlinde mti mama , mimi pekee na Zeus ndio tupo na uwezo wa kupambana nae , kama tukipoteza nyie msipoteze muda wa kupambana nae”Aliongea Athena akimwangalia Roma,
Watitani hao wote hususani Hera na Poseidon walionekana kukasirishwa na maneno ya Athena , ijapokuwa uwezo wao haukulingana na wa Zeus na Athena lakini pengine walilingana na jini wa levo ya mapigo elfu kumi ya radi mara baada ya kujibadilisha kuwa mwili wa nishati , kubwa zaidi Hera alikuwa na mti wa matunda ya shufaa na kila tunda moja linaweza kumsaidia kufukuza aina yote ya mashambulizi.
“Acha kujiona unaweza kila kitu , umeshakiri wewe mwenyewe huna uwezo wa kumtabiria , nini kinakufanya uamini una uwezo wakushindana nae ukijumlisha na alivyo na akili , ukweli wa kwamba amefanikiwa kuigia katika levo ya mapigo elfu kumi ya radi na akapita moja kwa oja anatakuwa katikati mwa levo ya mwisho wa Dhiki, hebu achaneni na huyo malaya anachoongea na tumuueni huyu mwanaharamu na kuiharibu kabisa nafsi yake ili ajue ni kosa gani amelifanya kuua uungu wa Hade”Aliongea Hera.
Mara baada ya kutaja kuua uungu wa Hades , viumbe hao wote wa kititani waliharuka kwa hasira na kutupia pembeni wasiwasi wao na kumnyooshea Roma siraha zao.
Apollo alikuwa amekwisha kurudi katika umbo linalofanana na mngao wa madini ya almasi na bahari kumzunguka iliana kugeuka mvuke kutokaa na mngao wake kuwa na joto kali.
Artemis na yeye alikuwa katiak umbo la kititani na alitoa mngao mweupe kama wa mwezi , katika kiichwa chake amejifunga kibanio cha rangi ya dhahabu huku nywele zake ni kama vile zina umeme kwa namna inavyocheza cheza. amevalia gauni refu kama vile ni la harusi huku akimshambulia Roma kupitia Selene, bahari chini yake ilikuwa imeganda kutokana na nishati ya ubaridi aiokuwa akitoa.
Poseidon , Ares , Hephaestus na Hermes wote waliinua siraha zao wakipgana kummaliza Roa na pigo moja.
Nishati ya anga ilijikusanya karibu yao na kutengeneza umbo la chusa linalotoa mngao wa rangi ya bluu iliokolea , upande wa mungu wa vita Ares alikuwa ni kama vile anadidimiza anga katika eneo alilosimama Roma huku Caduceus ikiana kumtengenezea Roma ndoto na kuingilia usikivu wake.
Ukimtoa Aphrodite pekee , miungu wote ni kama wamepamba kutumuia uwezo wao wote kushambulia , hata hivyo hakuna wa kumlaumu kwani siraha yake ya magical girdle haikuwa kama siraha zao ambazo zinafanya mashambilizi ya moja kwa moja , hivyo kumfanya kuwa mnyonge kati yao.
Ares ambae alichujuliw akama mdhaifu sasa alikuwa na uwezo sawa na mwishoni wa mapigo mengi ya radi na kwa kuagalia tu miungu wote walionekana uwezo wao wakutumia kanuni za anga umeimarika maradufu.
Zaidi sana ni kwamba miungu wote walijua mashambulizi ya rasha rasha hayana maana hivyo walihitaji mbinu yakinifu ambayo inaweza kumzimisha Roma na kumtengenezea majeraha makubwa.
Mara baada ya kuona hakuna wa kumsikiliza Athena hakutaka kuongea lolote na aliinua siraha yake a kisha wakapenda ishara na Zeus na ghafla tu alimsogelea Roma kwa spidi kwa ajili ya kumshambulia.
 
NILIEMDHANIA NI KAHABA KUMBE BIKRA .

MTUNZI: SINGANOJR.

Mono no aware.

ILIPOISHIA
Poseidon , Ares , Hephaestus na Hermes wote waliinua siraha zao wakipanga kummaliza Roma na pigo moja.
Nishati ya anga ilijikusanya karibu yao na kutengeneza umbo la chusa linalotoa mng’ao wa rangi ya bluu iliokolea , upande wa mungu wa vita Ares alikuwa ni kama vile anadidimiza anga katika eneo alilosimama Roma huku Caduceus ikianza kumtengenezea Roma ndoto na kuingilia usikivu wake.
Ukimtoa Aphrodite pekee , miungu wote ni kama wamepanga kutumuia uwezo wao wote kushambulia , hata hivyo hakuna wa kumlaumu Aphrodite kwani siraha yake ya magical girdle haikuwa kama siraha zao ambazo zinafanya mashambilizi ya moja kwa moja , hivyo kumfanya kuwa mnyonge kati yao.
Ares ambae alichukuliwa kama mdhaifu sasa alikuwa na uwezo sawa na mwishoni wa mapigo mengi ya radi na kwa kuangalia tu miungu wote walionekana uwezo wao wakutumia kanuni za anga umeimarika maradufu.
Zaidi sana ni kwamba miungu wote walijua mashambulizi ya rasha rasha hayana maana hivyo walihitaji mbinu yakinifu ambayo inaweza kumzimisha Roma na kumtengenezea majeraha makubwa.
Mara baada ya kuona hakuna wa kumsikiliza Athena hakutaka kuongea lolote na aliinua siraha yake na kisha wakapeana ishara na Zeus na ghafla tu walimsogelea Roma kwa spidi kwa ajili ya kumshambulia.

SEHEMU YA 794.
Licha ya umbo la Athena kuongezeka ukubwa, spidi yake haikupungua na zaidi sana mwili wake mkubwa ni kama umempa faida ya kimashambulizi na hii ilimfanya kitendo cha kusogea tu bahari kuchafuka.
Siraha yake ya Pallas ilikusanya chembe chembe kama vile ni visu vya vioo , na vilizunguka kwa kuzingira eneo kubwa takribani mita elfu moja.
Muda huo Roma alikuwa ni kama punje juu ya mchanga kutokana na udogo wake zidi ya maadui zake walio na miili mikubwa , kwa namna ambavyo alikuwa amezingirwa na chembc chembe za elemnti za anga ilikuwa ngumu hata kumuona.
Mishale ya moto na ya barafu ilimshukia kutoka juu kama vile nyota zinamdondokea.
Zeus na yeye alikuwa tayari ashaandaa shoti kubwa ya radi kwa ajili ya kumshambulia nayo Roma.
Ijapokuwa mashambulizi ya miungu yalikuwa yakichukua eneo kubwa lakini hawaku hofia kuumiza mti mama kwani kulikuwa na uzio ambao mti huo umejitengenezea.
Roma ambae alikuwa amesimama angani aliishia kuangalia mashambulizi ya miungu hao yakimfikia na kuushambulia mwili wake na kummeza kabisa asipate kuonekana.
BOOM!!
Mshindo mkubwa wa mlipuko uliweza kusikika kiasi cha kumfanya Roma katika ile sehemu aliokuwa amesimama asiweze kuonekana kutokana na kumezwa na mlipuko ule.
Hali ya anga ya kuchafuka na nishati ilisababisha athari za uharibifu kuzunguka eneo lote la ncha ya kaskazini.
Eneo lote la ncha ya kaskazini lilikuwa limefunikwa na mwanga mkubwa mno , mlpuko huo ulisababisha maji ya bahari kuwa vipande vipande vya barafu.
Mwanga huo ulidumu kwa dakika tu na baadae moshi mzito sana ulitokea karibu na Mti mama , miungu waliishia kuangalia shimo kubwa lililojjitokeza kwa mshangao.
Lakini sasa ajabu Roma alikuwa vilevile , hakuwa ameumizwa na mashamblizi yao licha ya kwamba walikuwa na uhakika mashambulizi yao yalimfikia.
Kitendo cha Roma kutokuumia walijua lazima kuna namna mashambulizi yao hayakumfikia moja kwa moja.
Jambo lile la Roma kutoathirika hata kidogo kwa mashambulizi yao makubwa ya namna hio , iliwafanya kuwa na wasiwasi.
Hatimae wasiwasi wao ulithibitika kwa muonekano uliokuwa mbele yao.
Kitu walichoweza kuona ni mtu ambae amefunikwa na radi nyeusi iliokuwa ikicheza cheza bila kusogea mbali na mwili wake.
“Radi nyeusi?!, amefanikuwa kujua kutengeneza radi nyeusi ?”Hera alishindwa kujizuia mshangao wake akimwangalia Roma kwa macho ya wivu.
Ilikuwa ni nje ya fikra zake kama Roma ambae amepitia mapigo elfu kui ya radi kuweza kuielewa siri iliokuwa nyuma ya radi hio na hatimae kufanikiwa kuidhibiti.
Uelewa wa namna huo ulihitaji ujuzi mkubwa ambao miungu hawakuwa nao.
Ilikuwa ni kama vile ile nguvu ambayo majini walikuwa wakiitamani kuimiliki siku moja kwa zaidi ya miaka elfu kumi iliopita ilikuwa ni zawadi ambayo inakuja baada ya kupita dhiki ya mapigo elfu kumi ya radi.
Muda huo Roma aliondoa radi ile iliokuwa ikimzingira na macho yake yakatua kwa miungu akiwa na tabasamu pana usoni , tofauti na mwanzo wakati huo alikuwa katika hali ya utulivu mkubwa mno , hakukuwa na chembe yoyote ya waswasi katika macho yake.
“Bado tu mnataka kuendelea na hii vita? , mashambulizi yenu yanayotokana na sheria za anga inaonekana kabisa hayana athari zozote kwangu mbele ya radi nyeusi”Aliongea Roma.
Ares ndio aliekuwa wa kwanza kupandwa na jazba kwasababu sauti ya Roma ilisikika kidharau sana , kwa mara nyingine aliinua siraha yake na kuiruhisha kuelekea alipo Roma.
“Acha majigambo yako”
Siraha ile ambayo ni kama mkuki ilifunga nafasi zote karibu na aliposimama Roma na kuacha nafasi pekee ambayo siraha ile ingeweza kumpiga Roma.
Kitendo cha Roma kutoa radi ya mapigo elfu kumi, shambulizi la Ares lilisambaratishwa kirahisi sana na hata kitendo cha Ares kumfungia nafasi kumzunguka kama mtego, ulifyatuliwa mara moja na shambulizi lake likawa halina maana tena.
Lakini bado Ares alionekana kuwa na ukiburi na aliendelea kumshambulia Roma lakini spidi yake haikuwa kubwa hivyo hakuweza hata kumgusa Roma.
Sura za miungu baada ya kitendo kile cha Ares kutoweza kumfikia kabisa Roma zilijikunja kwa wasiwasi.
Kwa kujilazimisha sana kukubali , walijua kabisa mashambulizi yao hayakuwa yakifanya kazi mbele ya Radi nyeusi.
Mishale yao na radi zao zilizotokana na kanuni za anga zilikuwa ni kama upepo mbele ya Roma anaemiliki radi nyeusi.
Hata Nyoka wa Hermes alishindwa kumtengenezea Roma ndoto ya udanganyifu , jambo hilo lilimfanya Hermes kuhisi alikuwa akipatwa na ukichaa yeye mwenyewe.
Roma akiwa kama vile anakagua mzingira alipotezea mashambulizi ya miungu kabisa , ili mradi yalikuwa yakitokana na kanuni za anga alijua hayawezi kumuumiza kwa namna yoyote.
Mara baada ya kuona moto wake wa kiuungu hauwezi kumuunguza Roma , Hephaestus alifanya maamuzi ya haraka sana kubadilisha aina ya mshambulizi yake.
Aliinua nyundo yake na kujaribu kutumia kanuni za anga kumshambulia Roma.
Roma akiwa katika tabasamu la kifedhuli aliishia kumyooshea kidole Hephaeustus na palepale nyoka wa radi nyeusi ilitoka na kwenda kukumbana na lile nyundo la Hephaestus.
Kitu cha ajabu kiliweza kutokea mbele ya miungu wote na kuwaacha hoi.
Ilikuwa ni kufumba na kufumbua , Nyundo la Hephaestus lilipotea katika mikono yake na hakukuwa na hata chembe ilioweza kuonekana.
Hephaestus alijikuta akirudi nyuma , akijaribu kumkwepa Roma kwa mbali huku akimkodolea macho akiwa amepaniki , ilionekana kile alichokiona ni kama alikuwa akiota na sio uhalisia.
“Yaani ka shoti kadogo hivyo ka radi nyeusi kameweza kuwa na athari ya kutisha ya namna hio?”Hephaestus lazima ndio alichokuwa akiwaza muda huo.
“Bado mnataka kuendelea kupambana na mimi?”Roma aliuliza kwa mara nyingine , awamu hio alikuwa amemwangalia Athena ambae alionekana kukunja sura akifikiria.
Miungu pia walionekana kumwangalia Athena , isitoshe alisema yeye na Zeus ndio wenye uwezo wa kupambana na Roma na wengine haikuwa na haja ya kupambana.
Kwa kile ambacho walikiona ni kama walikuwa wameelewa alichomaanisha, maana muda huo Hephaestus na Ares walionyesha wasiwasi mkubwa wa kumshambulia Roma.
“Radi hio nyeusi naona ina nguvu ya kubatilisha kanuni za anga na kufanya mashabulizi yetu yasiwe na athari zozote kwako , kama sijakosea,hii radi inaleta uharibifu kwa kiumbe chenye uwezo wa chini kuliko wewe”Aliongea Athena akiwa amefumbua macho yake mazuri kwa ukubwa unaofanana na mkanganyiko(Bewildered).
“Upo sahihi , nguvu ya radi nyeusi imepita kanuni ya nafasi na muda , mbingu na ardhi na elementi zote za ulimwengu,Pengine mnaweza kuweka ukinzani kwa kutegemea mti mama lakini litakuwa ni swala la muda tu kuwaua wote na hakuna hata mmoja wenu atakuwa na uwezo wa kujilinda”Aliongea.
Roma hakutaka kuficha kitu tena , aliweka kila kitu wazi juu ya uwezo wa radi aliokuwa akiidhibiti , radi ya rangi nyeusi , radi ambayo ilikuwa tofauti kabisa kimwonekano na radi nyingine.
“Is it ‘Dark matter’?”Athena alionekana kuuliza ghafla tu akimaanisha je ni Maada Giza , swali lake hata yeye lilimshangaza kwanini ameuliza hivyo lakinin pia lilimshangaza Roma.
“As expected of the goddess of wisdom to guess it so quickly …”Roma aliongea akitabasamu akimaanisha kama alivyo kama mungu wa kike wa busara kuweza kuotea mapema juu ya radi yake.
“Upo sahihi , kwa namna nyingine mchanganyiko wa radi hii unaweza kuiita Dark Matter hilo ni jina ambalo binadamu wameamua kuipatia aina hii ya maada lakini ukweli hata mimi sijui ni nini , sio radi kama radi na jina lake silijui , lakini haijalishi kwani ni maada ambayo ipo mbele yako”
“Oh! hata mimi nilijua tokea mwanzo sio radi peke yake inayoweza kuwa na matokeo hayo, kabla ya kuja duniani tulikuwa kwenye utafiti juu ya uwepo wa maada hii ya kimaajabu iliofunika anga na kuathiri kanuni za anga ili kuthibitisha uwepo wake na tabia zake lakini mpaka sasa hivi na wakati ule hatukuweza kuthibtiisha kama kweli ‘Dark matter’ ipo, kwa bahati mbaya hatukupata muda wa kutosha kufanya utafiti..”Aliongea Athena.
Upande mwingine mara baada ya Clark kusikia kauli hizo aijikuta akilipukwa na furaha.
“Sir! , Je radi ya mapigo elfu kumi imeungana na Dark Matter ndio maana ni radi ya muonekano mweusi, je hii ndio namna ambavyo wajumbe wa mkuu wa enzi wanavyo safiri kutoka anga za mbali kuja duniani na kuondoka?”Clark alimuuliza Sharif.
Ilikuwa ikileta maana juu ya fumbo la wakuu wa enzi kusafiri kupita katika anga za mbali ambazo zimejaa mionzi ya hatari na mabalaa, hio yote ni kwasababu ya radi hio ya kimaada nyeusi.
Dark Matter ni tofauti na nishati ya mbingu na ardhi ambayo ingeisha mara tu baada ya kwenda umbali mrefu angani na vilevile si sawa na kuitafsiri kama Giza bali ni kitu ambacho kipo chenye tabia ya uzito(Mass) kisichokuwa na mwisho.
“Kama Roma alivyosema , ijapokuwa tunao uwezo wa kwenda anga za mbali bila shida yoyote kupitia mchanganyiko wa nishati ya radi na maada nyeusi , bado hatujui ni kitu gani na imetengenezwa vipi , ni kitu ambacho kimebeba siri kubwa sana ya ulimwengu , kuna uwezekano tusiweze kujua leo wala kesho , lakini kwa levo ya uelewa wetu hatuchukulii mambo haya kama kipaumbele , ni siri pekee za ulimwengu ambazo zitajifunua zenyewe mbele yetu”Aliongea Sharif na kauli yake ni kama vile anasema ni Mungu mwenyewe ndio anajua.
“Hakuna wa kuelewa siri hizo kirahisi , ukweli ni kwamba sio Dark Matter tu , haijulikani mpaka leo hii kwanini kuna Adhabu ya anga ya radi na kwanini radi hio ni kama ufunguo wa siri zote za ulimwengu, ukilinganisha na watangulizi wetu ambao washawahi kupanda levo kubwa zaidi sisi ni wadogo sana mbele yao likija swala la ufahamu wa kujua siri za anga”Aliongea Aoiline.
Clark aliishia kutingisha kichwa chake kwa kukubali , kwake yeye ilikuwa ni kitu kipya ambacho alikuwa na hamu zote kukifanyia utafiti.
Mata au maada nyeusi ni moja ya maajabu makubwa ya ulimwengu , ni aina ya muunganiko wa dutu nyeusi ambazo hutengeneza asilimia themanini na tano ya hali ya giza inayoonekana katika anga za mbali(Cosmos) ambayo huathiri nguvu ya uvutano kati ya maada zinazoonekana kama vile nyota na sayari.
Wanasayansi wa dunia wana makisio mbalimbali ambayo hawana uhakika nayo , kuna wale wanaosema weusi huo upo kwasababu ya nguvu ya mvutano kama ilivyokuwa kwa nyota na galaksi lakini mpaka leo hii hawajui weusi(giza) huo wa ajabu(Dark Matter) unaomeza mwanga umetokana na nini na kwanini ukawepo , kwa lugha nyepesi ni sawa na kujiuliza giza linatokana na nini, mpaka leo hatujui giza linatokana na nini na halitengenezeki katika maabara kama ilivyo kwa mwanga.
Mmoja wa watu ambao walikuwa wakijua hayo yote ni Profesa Clark na alijikuta akipatwa na hali ya furaha mara baada ya kumuona Roma akiwa na uwezo wa kudhibiti kitu cha ajabu namna hio.
Lakini sasa licha ya furaha yake kwa wakati huo alikuwa katika shangwe ya kujua kwamba mpaka hatua hio Roma ameshashinda vita kwani nguvu aliokuwa nayo ilikuwa imepita nguvu za kanuni za anga ambazo miungu hutumia.
Hata Sharif mwenyewe alionekana kuridhika kwa matokeo , ijapokuwa alimuona Roma bado hajavuka kufikia ule upepo lakini alijua mapema tu ataufikia kutokana na uwezo wake mkubwa wa ki uelewa, hivyo angeweza kuiacha dunia na kuondoka akiwa katika hali ya amani.
Juu ya bahari ya Arctic , miungu walishindwa kujizuia zaidi ya kushangaa mara baada ya kusikia mazungumzo kati ya Athena na Roma.
Walijiambia inamaana ameweza kuelewa nguvu ya kimaajabu ambayo haikuwa ikihamika , nguvu ya Dakr Matter , kwa hatua huo waliona kabisa hawakuwa na nafasi ya kushinda tena.
Ilikuwa ni kama vile kuchukua yai na kisha kulitupia kwene jiwe , hajalishi utalipiga jiwe hilo na mayai mangapi , jiwe hilo linaweza lisipate athari zozote na hivyo ndio ilivyokuwa kwa mashambulizi yao zidi ya Roma.
“Sasa uwezo wangu umebatilisha mbinu zenu zote za kanuni za anga , kuendelea kupigana itapelekea niwaue tu , hivyo huu mti achaneni nao na muwaache watu wa dunia waishi kwwa amani , na sitofanya mambo yawe magumu kwenu kutokana na ukaribu tuliokuwa nao mwanzo”Aliongea Roma.
Kulingana na maelezo ya Sharif , kulikuwa na matokeo mawili katika vita hivyo , kwanza ni aidha miungu waitawale dunia wakishashinda au Roma awaue na kisha ufufuo ukome.
Lakini sasa Roma hakutaka kufanya kile ambacho Sharif alitarajia kutokana na kwamba alihitaji na yeye pia kuwajibika kama binadamu kutokana kuwa baba , lakini vilevile kwasababu alikuwa mume kwa Edna hakutaka kumuua Athena.
Ndio maana alitamani Athena aache ukiburi wake na kisha amani irudi , hakujali kama atamruhusu Edna kurudi au ataendelea kuishi kama Athena katika mwili wa Edna ili mradi nafsi zote zitakuwa ndani yake.
Roma alikuwa akielewa nguvu ya nishati inayotokana na maada nyeusi kama ingemgusa Athena ni dhahiri kwamba angekufa mara moja na kusingekuwa na namna ya kumuokoa Edna.
Sasa hakutaka kuona ni kwa namna gani angejibu pale Lanlan atakapomuuliza huku akichezesha macho yake mzuri ni wapi mama yake alipo ilihali alimuahidi atarudi , asingeweza kumwambia amemuua mama yake kwa mikono yake miwili.
Isitoshe kwa namna moja ama nyingine iwe ni Seventeen ,Athena na Edna wote watatu walikuwa kama mama kwa Lanlan kwa njia tofauti tofauti , Seventeen alibeba mimba na Athena akakubali kujifungua na kumzaa Lanlan na Edna akakubali kumlea Lanlani kama mtoto wake wa kumzaa.
Roma alijiambia anapaswa kusamehe mambo yote licha ya kwamba anaweza kukiuka taratibu , lakini hata hivyo baadhi ya vitu vilikuwa na muunganiko na yeye na asingeweza kubadilisha ukweli, Athena anaweza kuwa adui wa binadamu lakini ndani yake kuna nafsi ya mke wake na Seventeen mpenzi wake.
Kwa upande wa Aoiline hapo ndipo alpoiona tofauti ya Sharif na Roma, Sharif kwa sababu tu ya misheni alimtelekeza yeye , lakini Roma licha ya kwamba alikuwa na misheni hakutaka kumtelekeza mke wake na kumuua.
Wakiwa wamesikia vyema maneno ya Roma , miungu hao walijikuta wakikaa kimya.
Haikuwa kwasababu hawakuwa tayari kukubali kushindwa lakini ilikuwa ni kwasbababu hawakuona namna yoyote ya kumshinda Roma.
Wakati huo Athena alikuwa ashaweka siraha yake chini na kisha akainua ngao yake juu.
“Hatuwezi kurudi tuliko toka tena , nimesubiria hii siku kwa miaka elfu ishirini, huu ni muda wa kupata majibu”Aliongea Athena.
Roma alijikuta akikunja sura , ukiburi wa mwanamke huyo ulikuwa ni nje ya matarajio yake , hata kama alijua ilikuwa ngumu kwake kushinda lakini bado tu alitaka kuendelea kupambana.
“Roma! , hata kama unamiliki radi nyenye nguvu ya maada nyeusi , ili mradi tu Mti Mama utaendelea kuwa hai , sisi ni wa milele na tusiokufa , kama unataka kupambana , basi itoe kafara nishati yote ya ulimwengu kwa ajili yetu”Aliogea Zeus.
Palepale aliwaamrisha wenzake kuimarisha ulinzi wa kizuizi kinacholinda Mti Mama huku yeye na Athena wakipanga kupambana nae.
Roma alijikuta akishindwa kujizuia na kuishia kutoa kicheko na aliishia kuongea kivivu.
“Kwannini mnataka kwenda mbali hivi , hivi hamjui mimi Roma Ramoni siwezi kukubali kushindwa kama uwezo wa kushinda ninao , siwezi kupoteza pambano kwa yoyote kati yenu hata kama itokee kubetia usalama wa dunia”
“Kama ni hivyo endelea na uone”
Zeus aliongea kwa sauti nzto na palepale bonge la radi lilijitokeza katika mkono wake huku likifuka shoti ya hali ya juu kwa kuendelea kuunganisha nguvu yake na Mti Mama , uwezo wake ulikuwa wa juu mo hivyo hivyo kwa radi yake ilikuwa na uwezo mkubwa wa kushambulia.
“Ghadhabu ya miungu !!”Alikemea kwa sauti kubwa.
Ndani ya dakika hio hio , ilikuwa ni kama vile anga linataka kudondoka kutokana na ukubwa wa ngurumo iliosikika.
Mara baada ya radi iliokuwa katika mkono wake kuiachia , ilisababisha msuguano wa juu sana katika nafasi ambayo alikuwepo na matokeo yake mionzi mikali ilidhalishwa.
Kutokana na mng’ao wa radi hio anga lote lilikuwa ni la rangi ya Dhahabu na njano , Roma alikuwa akionekana kama kidoti kidogo juu ya anga hilo na pengine ukipepesa macho huwezi kumuona tena.
Lakini sasa ndani ya nusu sekunde weusi uliokuwa kama nguzo ulionekana kwenda kushambuliana na ile radi iliokuwa na rangi ya dhahabu na bluu na kumezwa .
Macho ya Zeus yaliwaka kwa hasira na kwa haraka sana alitengeneza radi nyingine katika mkono wake.
Lakini kabla, cha ajabu ni kwamba radi alioweza kutengenea awamu hio ilikuwa na nguvu nusu na ile alioweza kutengeneza mwanzo.
“Radi yangu nyeusi sio tu kwamba inabatilisha sheria za anga lakini vilevile ina elementi za roho wa machafuko ndani yake hivyo inaweza kumeza kila kitu, ndio maana radi yako imepungua nguvu nusu yake”Aliongea Roma
“Unakasirisha sana”
Zeus alikuwa na hasira za viwango , tokea dakika ambayo alitoka katika gereza la roho mpango wake ulikuwa ni kufufua ndugu zake tu na kuitawala dunia.
Lakini sasa mara baada ya kuanza safari yake ya mafannikio anajikuta akipambana na Roma ambae anamzuia kutotimiza ndoto zake
Zeus alijiambia hapana , haweizi kumruhusu Roma kuzima ndoto zake alizokuwa nazo kwa miaka elfu ishirini iliopita , hawezi kupoteza muda ambao alivumilia akiwa ndani ya gereza la roho.
Mara baada ya kuwaza hivyo aliamua kutumia kila mbinu na kuanza kumshambulia Roma kwa spidi.
Zeus ngumi yake iliokuwa imebeba radi ilikuwa ikifuka mwanga wa rangi ya dhahabu , ijapokuwa uwezo wake haukulingana na wa Roma lakini Roma aliona haina haja hata ya kuumeza kwani uwezo wa kukwepa mashambulizi yake anao.
Roma aliona fika kwamba miungu hao hawatoelewa gepu ambalo lipo kati yake na wao ,. Hivyo aliona haina haja ya kumchelewesha Zeus muda mrefu.
Palepale radi nyeusi ilitokea katika mkono wa Roma , katikati ya ombwe iliungana na kutengeneza kitu kama mkuki wa urefu wa futi kumi.
Kama mwanga wa radi alimsogelea kwa spidi Zeus huku akimlenga eneo la kichwani.
Zeus mara baada ya kuona Roma anamsogelea kwa ajili ya kumshambulia , aliinua mkono wake mkubwa kwa ajili ya kumzuia lakini ile siraha ya Roma ya kinishati iliweza kupita katika mkono wa Zeus na kutoboa kama vile imepita kwene karatasi.
“Kuwa makini!”
Hera ambae alikwisha kujua kuna kitu hakipo sawa palepale alirusha tunda la shufaa la dhahabu kuelekewa kwa Zeus na kisha kumfunika kwa kutengeneza sanamu.
BOOM!!
Mwanga wa dhahabu uliweza kuwaka kutoka katika mwili wa Zeus na kuzuia shambulizi la Roma lisimfikie kichwani na Zeus kutumia nafasi hio kumkwepa Roma.
“Golden Apple..”Roma shambulizi lake lilifeli kutokana na tunda hilo na aliishia kumwangalia Hera huku sauti yake ikiwa imejikunja.
“Kwasababu unakuwa kimbelembele na kunichelewesha , nitaanza na wewe kwanza”Aliongea Roma.
Hera mara baada ya kumsikia Roma alijua kabisa hali sio nzuri kwake , na palepale alichukua tunda lingine na kumfanya apoteee kwa kujitengenezea sanamu.
Roma wala hakutaka kujali hila za Hera na palepale radi yeusi ilishuka kutoka angani na kilichosikika ni mshindo.
Ilikuwa ni kama joka ambalo linameza kila kitu kilichokuwa mbele yake kujitengenezea njia ndivyo ilivyo kuwa kwa radi hio nyeusi , kwani ilianza na sanamu na kulimaliza na kuendelea kukua kinguvu na hatimae kumvaa Hera.
Hera alijikuta akitoa kilio cha kusaga meno , Tunda la dhahabu ambalo lilikuwa kwenye mikono yake lilitaka kumsaidia lakini lilishindwa kuhimili nguvu ya radi nyeusi na ndani ya sekunde tu liligeuzwa na kuwa mvuke.
Hera alikuwa akitegemea zaidi matunda hayo ili kupunguza majeraha na kupitia nishati ya Mti mama hakuweza kufa lakini uungu wake ulikuwa umepungua nguvu mno na hali ile ilimpelekea kushindwa kuendelea kuwa katika mwili wa Titani na alirudi katika mwili wake wa mwanzo wa jini Rozu, uso wake ulikuwa umepauka mno na alijitahidi kadri awezavyo kujibakisha juu angani.
Shambulizi hilo moja tu kwenda kwaHera liliwaogopesha miungu wote , Hera alikuwa ameguswa na shambulizi kidogo tu la radi hio lakini madhara yake yalionekana kuwa makubwa mno huku siraha yake ikiharibiwa .
Ilifikia hatua mpaka wakaanza kufikiria kama Roma ataaamua kumshambulia tena Hera je ataweza kuhamisha mapema nafsi yake na kuzaliwa katika mwili mwingine.
Kilichowaogopesha sana ni juu ya spidi ya radi hio nyeusi kuwa nje ya fikra zao , bila kutokuwa na unabii kama wa Athena kukwepa shambulizi lake ni ngumu mno.
Wakati miungu bado wakiwa katika mawazo , Roma alikuwa tayari ashatengeneza radi nyingine akilenga moja kwa moja kwene kizuizi cha Mti mama.
“Msimruhusu kuvunja huo uzio , Ulindeni mti mama kwa uwezo wenu wote”Poseidon aliiongea kwa nguvu.
Miungu hawakutaka kuzubaa na kumuacha Roma avunje uzio wa mti mama , hivyo walijikuta wakisogea mbele pamoja na siraha zao na kutumia mbinu zao zote huku wakijitoa mhanga kupokea mashambulizi ya radi nyeusi.
Lakini hata hivyo radi hio ilikuwa ngumu kuvumilika sio tu kwa miungu hata kwa majini waliokuwa katika levo ya juu ya mapigo elfu kumii ya radi ingekuwa ngumu kwao , hivyo hawakutaka kudhania ni namna gani wanaweza kupita katika hio hali ya maumivu baada ya kuguswa na radi hio.
Mara baada ya radi ya Roma kuwafikia miungu na kuvunja ukinzani wao , ilikuwa ni kama kwa Hera tu , wote walivuliwa miili yao na kurudi katika ubinadamu kutokana na uungu wao kutokuwa na uwezo mkubwa.
Mpaka hatua hio ilikuwa ngumu kwao kupigana tena, kwa kuumia kwa uungu wao iliwahitaji muda mrefu kupona.
“Kama mnavyoona , hakuna wa kunizuia kuuharibu huu mti wenu”Aliongea Roma akiwaangalia Zeus na Athena.
Athena alionekana kukunja ndita na ilikuwa ni kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza.
Zeus na yeye alikuwa katika uso mkavu lakini ghafla tu aliangua kicheko cha furaha ikiwa ni kama ameona kitu cha kumshinda Roma.
“Kama ni hivyo basi hakuna namna , tutaendelea kupambana mpaka mwisho”aliongea Zeus.



SEHEMU YA 795.
“Naona una kete nyingine umeficha sio?”Roma alitabasamu.
Zeus alikuwa na tabasamu la ajabu na ghafla tu mwili wake wa kititani ulianza kutoa msisimkoo mkubwa wa nguvu ya giza yenye uovu ndani yake.
Mapepo , mizimu na roho chafu ziliuzingira mwili wake na ilikuwa ni kufumba na kufumbua tu mwili wake wote ulikuwa ukitoa sauti za vilio vya wafu na ming’ako ya ajabu kila kona , ilikuwa ni sauti ya kutisha mno na kushangaza kwa wakati mmoja.
Roma alijikuta akibunga’aa kwa kile alichokuwa akiiona , hata miungu wengine kasoro Athena walikuwa katika hali ya mshangao.
Roma macho yake yalisinyaa , kabla ya hapo alikuwa akijiuliza ni kwa namna gani Zues aliweza kudumisha mwili wake licha ya kuishi ndani ya gereza la roho kwa miaka mingi na kujiuliza kwanini hakuhamisha nafsi yake lakini swali lake ni kama sasa linapata jibu.
Sekunde iliofuata Zeus alikuwa ni kama vile anayeyuka kwa spidi kubwa sana, ilikuwa ni kama vile amegeuka na kuwa bwawa la uji mweusi mzito sana , uji ambao ulikuwa ukijikunja kunja na kumchemka huku ukitoa msisimko wa kighadhiba.
Dakika nyingine mbele kilichoonekana mbele yake ni jini pepo wa kutisha mno ambae hakuwahi kumuona hapo kabla hata katika ulimwengu wa majini pepo.
Jini pepo huyo alikuwa na rangi nyeusi na muonekano wake wote alikuwa ni kama mnyoo mkubwa mno mara mia moja ya ukubwa wa Chatu ,lilikuwa na urefu wa mita kama mia tano hivi na upana wa mita mia moja.
Mwili wake huo mnene pamoja na mkia wake ulikuwa tayari katika maji ya bahari na ilionekana linakwenda kuzama muda wowote.
Kichwa cha jini pepo kilikuwa tofauti na viungo vya kawaida , mdomo wake ulikuwa ukitoa uteute wa rangi nyeusi ambao ulikuwa na harufu kali mno , ilikuwa ni kama vile mwili wake wote umetengenezwa na uteute unaotoka mdomoni.
“What is this thing… Zeus how..”Apollo macho yake yalionyesha hali ya hofu.
“Inamaana alihamisha nafsi yake katika Gereza la roho ndani ya hili limnyoo”Aliongea Hephaestus akiwa katika hali ya kutopendezwa.
Kila mmoja aliekuwa hapo hakujua jambo hilo kasoro Athena tu ambae alionyesha kufahamu.
Mwili aliokuwa amehamishia nafsi yake Zeus ni wa jini aliewahi kuwepo aliepwa jina la Phantom Mother Cavern Worm aliewahi kuwepo dunia katika nyakati za kale, yaani kwa lugha ya kiswahili ni mnyoo wa kizimwi unaoishi pangoni.
Sifa kubwa ya jini huyu kupewa jina hilo kwanza kabisa alikuwa ni kama mnyoo ambae makazi yake makubwa yalikuwa ni ndani ya pango na ndio aliezaa minyoo yote mikubwa ya kijini ambayo yaliwahi kuwepo yalioishi katika mapango enzi za kale.
Inasemekana asili ya jini pepo wa namna hio hakuzaliwa akiwa na nguvu kabisa lakini alikuwa na tabia ambazo linaweza kumeza jini pepo mwingine ambae atakutana nae njjiani na kisha kujibadilisha katika umbo la jini huyo aliemmeza na kumfanya kuwa ngumu kumuua , kwani ndio namna ambavyo uwezo wake ulikuwa ukiongezeka.
Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba jini pepo huyu mwenye umbo la mnyoo mkubwa alizaliwa akiwa hana nguvu na hata uwezo wa akili ulikuwa mdogo lakini alikuwa akipandisha uwezo wake kwa kumeza majini wengine na hata binadamu.
Sasa mara baada ya Zeus kuuona huo mnyoo katika gereza la mepepo miaka elfu ishirini iliopita alilisaidia kukua kwa kumeza majini wenzake na mara baada ya kufikia katika levo kubwa ya ki uwezo alihamisha uungu wake na nafsi yake katika hilo Jongoo na kisha mara baada ya kupata ufahamu wake akiwa ndani ya mnyoo huo alimeza mwili wake wa awali hivyo moja kwa moja mnyoo huo ukapatwa uwezo wa kubadilika na kuwa katika umbo la mwili wa Zeus ule orijino.
Hio ndio sababu majini wote waliokuwa ndani ya Gereza walimwita Zeus mfalme wao , ijapokuwa alikuwa ni kiumbe tofauti lakini alikuwa na mwili wa jini pepo tayari hivyo majini waliokuwa ndani hawakuweza kumtofautisha wala kugundua kama alikuwa kiumbe mwingine hapa ndio maana jini Kivuli alimchukulia Zeus kama mfalme.
Sasa mara baada ya Zeus kutoka kama mfalme wa miungu asingeweza kuonyesha umbo hilo la mnyoo kwa miungu wenzake , kwani ingekuwa sio heshima na zaidi kwamba ingekuwa ni laana kuwa na mwili mbaya namna hio unaoshusha hadhi yake.
Lakini sasa katika hatua hio , Zeus hakuwa na namna tena zaidi ya kushindana na Roma mpaka akione kifo chake kwa kutumia mwili huo, yaani alitaka kummeza Roma kwa kutumia nishati ya mti mama.
Mdudu huo aina ya mnyoo ulipanua mdomo wake na kufanya ionekane ni kama shimo lisilokuwa na mwisho na upepo mwingi ulivutwa kuingia ndani , mwili wa mnyoo huo wa mita nyingi ulitengeneza kisingia cha upepo wenye kani mvutano kilichoelekea alipo Roma.
Kilikuwa ni Kisingia chenye kani kubwa ya kimvutano pengine mara mia tano ya kani mvutano ya injini ya ndege kubwa ya abiria.
Roma hakutaka kumezwa na limnyoo hilo , ijapokuwa alijua hata kama akimezwa hakuna kitakachomtokea lakini hakutaka kuingia kwenye kitu cha kutia kinyaa namna hio.
Lakini sasa wakati Roma akijiandaa kukwepa kisingia hicho cha kani mvutano alikuja kugundua yeye hakuwa shabaha .
“Hisss..!!!
Mnyoo huo uliongezeka mdomo mara mbili zaidi na palepale ukamlenga Athena kutaka kummeza.
Athena aliishia kukunja sura lakini ajabu ni kwamba hakujizuia kutokumezwa bali aliishia kufumba macho yake tu na kuruhusu upepo kumvuta mara baada ya kumpunguza umbo lake la mwili wa kititani na kisha akaingia mzima mzima.
Hatimae Athena akawa amemezwa katika mnyoo huo uishio pangoni na hakukuwa hata na dalili kama alikuwa amemezwa.
“Zeus umekuwa kichaa , kwanini umemmeza Athena?”Ares ndio aliekuwa kwa kwanza kupandwa na jazba na kumfokea Zeus.
Lakini Zeus hakujali kabisa macho ya miungu wenzake , ijapokuwa alikuwa katika mwili wa Mnyoo lakini alikuwa na uwezo wa kuongea kwa sauti nzito.
“Roma Ramoni, Athena yupo ndani ya tumbo langu , ninahitaji dakika moja tu kummeng’enya , nafsi za wanawake wawili unaowapenda pia zitapotea , ijapokuwa unataka kumshinda lakini unapaswa kufikira matokeo yake kwa umakini kabla hujapambana na mimi au kudhuru Mti Mama”
Sauti iliokuwa kama inatokea kwenye spika yenye besi kubwa ilisikika na kutengeeza hali flani hivi ya kuibua ukichaa.
Miungu hatimae waliweza kuelewa kwanini , Zeus alikuwa akitumia nafsi ya Seventeen na Edna kumfanya Roma asiendelee kushambulia
Athena ambae alikuwa na akili kubwa alikuwa ashawaza hilo pia na ndio maana hakuleta ukinzani wowote wakati Mnyoo huo wa Zeus ukimmeza.
Kwa ajili ya kufanikiwa kufufua miungu , Athena alikuwa tayari kufanya lolote hata kama lilikuwa halimpendezi , hata kama itafikia hatua ya Zeus kumuua.
Miungu walishindwa kujizuia na kuishia kujisikia vibaya na huzuni kwa wakati mmoja.
Miaka elfu ishirini ya kusubiri pengine ilikuwa ikimaannisha kitu kikubwa sana zaidi ya uhai wake ndio maana alikuwa tayari kujitoa kafara.
Roma pia alikuwa katika mshangao wa jambo hilo , alikuwa amesimama akiuangalia mwili huo wa mnyoo kwa macho makavu , kana kwamba alikuwa na uwezo wa kumuona Athena ndani ya tumbo .
Mishipa ya damu ilipanuka katika uso wake huku misuli yake ikicheza na alikuwa amekunja ngumi yake sana kiasi kwamba ilidhihirika alikuwa akijitahidi kuzuia hasira yake isimtawale.
Hakuamini Athena angekuwa na maamuzi ya namna hio ya utayari ili mradi tu kulinda ufufuo wa ndugu zake licha ya kwamba inaweza kumgharimu maisha yake ,hali hio ilimfanya Roma kuzidiwa na hisia za huzuni juu ya wale anao wapenda.
Muda huo Roma alikuwa ni kama amefungwa miguu , hakusogea na alishidnwa kuongea lolote na kumfanya Zeus kutoa cheko kubwa zito.
Upande mwingine wa eneo watu waliokuwa wakiangalia filamu hio ya kutisha kupitia kioo walijikuta wakisimama.
Mwanzoni Sharif alidhania hakuna kitu ambacho kitaenda kombo lakini ilionekana Roma hakuwa na uwezo wa kuchukua hatua , muonekano mgumu uliuvaa uso wake huku akionekana kukatishwa tamaa.
“Huyu mtoto bado hajaliona hili tu , nguvu ya radi nyeusi inao uwezo wakuua hilo linalojiita limnyoo la pango, lakini bado anasita sita”
“Lazima atakuwa anajua hilo , lakini kinachomfanya kusita sio kwamba hajui namna ya kumuua Zeus lakini Athena amejiandaa kufa pia..”Aliongea Aoiline huku akitingisha kichwa chake akimwangalia Sharif.
“Mh hafundishiki kabisa, kitendo cha kuendelea kujali sana kuhusu mapenzi na kusahau ulimwengu , sidhani kama anaweza kufanikiwa”
Clark macho yake yalifunikwa na machozi huku akimwangalia Zeus katika umbo la mnyoo kwa chuki kubwa sana lakini hakuwa na uwezo wa kufanya chochote.
Muda huo huo kwa Roma ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu , ghafla alikiinua kichwa chake huku akiuangalia mnyoo huo wa pango kwa macho makali sana , wakati huo huo akitoa msisimko wa kimauaji.
Zeus alihisi kabisa kuna kitu hakipo sawa , na sauti yake ilikuwa katika hali ya kitetemeshi.
“Roma umekwisha fanya maamuzi?”Aliuliza
“Pengine kuishi kwako gerezani kwa muda mrefu umekosa mtu wa kukuambia ni kitu gani nachukia zaidi”Aliiongea Roma huku akiwa na tabasamu lililojaa uovu.
“Nini..”Mwili huo wa Mnyoo wa Zimwi wa pango ulitingishika.
Nguvu kubwa sana ya nishati ya mbingu na ardhi iliibuka ikiambatana na ukali wa radi nyeusi na mwili wake wote ulibadilika na kuwa kama shimo jeusi kutokana na hali ya msisimko wa kimauaji aliokuwa akitoa.
“Nachukia kutishiwa amani kuliko kitu chochote”
Wakati aktoa kauli hio alikuwa ashatoka alipokuwa amesimama na kama mwanga alikuwa ashasogelea kichwa cha Zimwi mnyoo na kukishambulia.
“Pffff!!
Zeus alikosa hata muda wa kujitayarisha, Roma aliunganisha mkono wake na radi na kutifua kichwa chake mpaka kufikia mwanzoni mwa tumbo lake .
Kutokana na wingi wa kiza uliofunika eneo la kichwa cha Zeus miungu hawakuweza hata kuona kinachoendelea , walichoweza kuona ni kutingishika kwa kurudi nyuma na kwenda mbele kwa mkiwa wa limnyoo hilo kama vile linatapa tapa.
Zeus alitoa sauti ya’sii’ kama nyoka lakini ilikuwa bure , nguvu kubwa ya uharibifu ya radi nyeusi ilimfanya kuwa ngumu kudhibiti mwili wake ,sasa angewezaje kummeng’enya Athena aliekuwa ndani.
Mara baada ya Roma kujitokeza angani alikuwa ameshikilia kitu chenye ukubwa wa jicho la ng’ombe kilichokuwa kikitoa mwanga wa rangi ya dhahabu na bluu pamoja na uteute mweusi katika mkono wake wa kushoto.
Ilikuwa ni uungu wa Zeus.
Katika shammbulizi lake alidhamiria kuondoa uungu wa Zeus moja kwa moja kutoka katika mwili wa Zimwi mnyoo.
Ngurumo na kilio kiliweza kusikika kutoka kwa Zeus lakini haikuwa na maana tena , kitendo cha kuzimwa na Roma uungu wake asingekuwa hata na uwezo wa kuhamisha nafsi yake kwenda kwenye mwili mwingine.
Roma aliangalia mabaki ya mwili wa mnyoo huo unaotapatapa bila ya kutojali kabisa na hatimae ulianza kuyeyuka na kuwa kama majivu yaliosambaa hewani.
“Ungekuwa na nafasi ya kuishi kama usingenitishia , wewe mwenyewe ndio wa kulaumiwa , mimi Roma Ramoni nina weza kukubali kushindwa kwa muda mfupi lakini haimaanishi nitashindwa maisha yangu yote , ninao uwezo wa kujizuia kwa muda mfupi kutoshambulia lakini haimaanishi ninaweza kupokea vitisho…
Mara baada ya kauli hio radi nyeusi iliuvaa ule uungu wa Zeus na kuugeuza majivu na huo ndio kikawa kifo halisi cha Zeus.
Hakuna aliekuwa akiamini kifo cha Zeus kingekuwa cha namna hio , hakuna alieamini kama kutoka kwa Zeus gerezani anakuja kukutana na kifo chake.
Miungu hao walikuwa katika hali ya huzuni mno kwa kile ambacho kimetokea, Zeus alikuwa ndio mfalme wao , kiongozi wao, mtawala wa mbingu lakini ameuliwa namna hio.
Walijiambia pengine mipango yao ilikuwa ni kosa tokea mwanzo , Roma aliekuwa mbele yao alikuwa hawezekani tena, ni nje ya uwezo wao.
Miungu wote kumi na mbili ni kumi pekee waliobaki , na kwa uelewa huo walijikuta wakishindwa kujizuia kuonyesha majonzi yao.
Athena upande wake alikuwa asharudi katika mwili wa Edna baada ya kuachana na wa Kititani na kushusha siraha zake zote yaani ngao ya Aegis na mkuki wa pallas.
Roma mara baada ya kukutanisha macho na sura hio ya kirembo alijikuta akimmisi sana mke wake , alikuwa ndani ya ule mwili lakini ilikuwa ni kama vile yupo maili nyingi sana na yeye.
Macho yao yote mara baada ya kukutana kila mmoja alidhihirisha ni kwa namna gani alikuwa katika utulivu, hakukua na ishara yoyote ya hasira huzuni au furaha , badala yake waliishia kuangaliana tu kama hivyo yani.
Baada ya muda mchache Roma hatimae alionyesha tabasamu, tabasamu ambalo ni kama vile Edna alikuwa akiliona.
Upepo na moshi katika eneo hilo ulipotea ,ilionekana ni kama vile kila kitu kimerudi katiika hali ya amani kwa mara nyingine na kifuatacho ni furaha ya milele.
Tabasamu pia ambalo halikufahamika ni la hisia gani liliweza kuonekana pia katika uso wa Athena kwa kipindi kufupi.
Roma alionekana kulamba lipsi za midomo yake na kisha akavuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha akaongea:
“Kwahio inamaanisha unaacha kupigana kwa kuweka chini siraha zako?”Aliuliza Roma.
“Nipo katika levo sawa na Zeus au pengine nipo chini kidogo kuliko yeye kama sitotumia unabii wangu kwako , ukweli wa kwamba kitendo cha kuweza kumuua inamaaisha unao uwezo wa kuniua na mimi pia, kuendelea kupigana haina maana tena zaidi ya kujidhalilisha , sipigani na wewe tena .. lakini hili halijaisha” Aliongea Athena.
“Inaonekana hata kama niharibu Mti Mama na kumuua kila mtu hapa bado hutoachana na wazo lako la kufufua miungu si ndio?”
“Ndio”
“Kwanini?”Aliuliza Roma kwa huzuni.
“Unapaswa kunijua mimi vizuri , umekuja hapa na kutushambulia sio kwasababu unatuchukia sisi kama watitani au kwasababu unataka kuwalinda binadamu kama shujaa wao , hii ni hatima ambayo ulipaswa kukutana nayo , hakuna sababu juu ya hilo kabisa , hii ni hatima ambayo umeamua kuikubali kama binadamu , binadamu ambae atabadilisha mustakabali wa binadamu wote , kwako wewe umeshindwa kukaa chini na kupotezea maumivu ya binadamu , kwangu mimi , ni huu Mti mama , Huu mti ni mama yangu ,ni mama yetu , miungu ambao watazaliwa kupitia uungu ni watu wangu , yote nilioyafanya kwa kipindi chote cha miaka elfu ishirini ilikua ni kwasababu ya kufufua miungu leo hii , haijalishi kama nitafanikiwa au nitafeli , hio itakuwa ni hatima yangu ambayo napaswa kuikubali , siwezi kuacha na sihitaji sababu yoyote ya kujishauri”
Athena aliongea kwa utulivu kabisa , maneno yake alipowafikia miungu waliguswa kwa namna yake kiasi cha kuingia katika hali ya kimawazo.
“Haha.. upo sahihi , ndio , ni kweli kabisa huhitaji sababu juu ya mambo yote yaliotokea , ni jambo ambalo limekwisha kupangwa”Aliongea Roma akijicheka yeye mwenyewe na palepale hali ilirudi katika ukimya kwa mara nyingine na baadae Athena akaongea tena.
“Sasa maamuzi yapo katika mikono yako , kama hutaki miungu kufufuliwa chaguo lako litakuwa ni kuniua , vinginevyo hata kama ukoo wetu wote wa miungu kufa , hata kama mti Mama kunyauka , hata kama kuzimu yote ikawa wazi , siwezi kuacha , kama ukishindwa kuniua basi inamaanisha unabii wangu umefanikiwa mwishowe na itakuwa ni mwanzo wetu miungu tutakao utumainia , mustakabali juu ya mwanzo wa maisha yetu mapya katika dunia utaanza rasmi”
Roma alijikuta akikumbwa na hali ya kimawazo na kuishia kushika kidevu chake kwa kukiminya minya.
“Nimejitahidi sana kukulinda siku zote lakini mwishoni wewe ndio unakufa na mimi kuishi…”Aliongea Roma na maneno yake hayo ni kama alikuwa akimlenga Edna.
“Kama unao uwezo wa kuiondoa nafsi ya Edna na Seventeen katika nafsi yangu au kuharibu nafsi yangu pekee basi pengine kutakuwa na matokeo tofauti”Aliongea Athena akiwa katika hali tulivu.
“Acha kejeli , kama ninao uwezo wa kufanya hivyo ningekuwa nishafanya muda mrefu , ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kujua wewe ndio uliekuwa ukiendesha maisha yangu ukiwa gizani hivyo sikujiandaa vya kutosha”
Ukweli ni kwamba Athena alikuwa akimkejeli tu , hakukuwa na uwezekano wowote ule wa Roma kuiua nafsi yake alioifungamanisha na ya Edna na Seventeen, hata Sharif ambae ana uzoefu mkubwa hana uwezo huo , labda tu Athena mwenyewe kwa hiari yake awaachie Edna na Seventeen na kuondoka.
Isitoshe Athena hakuwa binadamu , nafsi yake ilikuwa ikilindwa na nguvu kubwa ya ajabu ya kiroho kutoka katika uungu wake hivyo ilikuwa ngumu zaidi ya jiwe
Kabla roho yake kutodolewa kwa nguvu katika mwili wa Edna atakuwa tayari ashaziaua nafsi hizo.
Roma hata yeye alijua jambo hilo haliwezekani kabisa na hakutaka hata kufikiria ni kitu gani afanye kumuondoa Athena kutoka katika nafsi ya Edna.
Aliishia kufumba macho yake na kuyafumbua baada ya muda mfupi , mara baada ya kumwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida alirudi katika hali yake ya ukauzu.
“Kama ndio hivyo , chukua siraha yako ya Pallass na hii iwe ni nafasi yako ya mwisho ya kimapigano kukitamka kifo chako”Aliongea.
Athena kope zake za macho zilitingishika kidogo mara baada ya kusikia maamuzi yake , hakuweza kujizuia zaidi ya kuonyesha rabasamu la utulivu na kisha alitingisha kichwa akikubaliana nae.
Mkuki ule wa bluu hatimae ulionekana kwa mara nyingine katika mikono ya Athena na akauinua kumnyooshea Roma.
Mara baada ya kuona tukio hilo miungu chini yao waliishia kuwa katika hali ya majonzi makubwa hata wale ambao hawakuwa na urafiki mzuri na Athena akiwemo Hera na Hermes.
Athena kupigana na Roma ambae uwezo wake ni wa kiwango cha juu walijua kabisa anaenda kujitoa kafara , lakini licha ya hivyo alikuwa tayari kupambana licha ya kujua kwamba hatokuwa hata nafasi ya kuhama katika mwili mwingine .
Upande mwingine Sharif aliekuwa akiangalia pambano hilo alijikuta akitoa tabasamu la furaha kwa kuridhika mara baada ya kuona Roma yupo tayari kupambana na Athena .
“Huyu mtukutu naona hatimae amefikia katika maamuzi sahihi , miaka yangu elfu hamsini ya kusubiri haijapotea bure”Aliongea.
“Huyu mwanamke wa kititani ni mgumu kweli , kwanini anataka kwenda mbali hivyo , hakuna tatizo kwa pande zote kukaa chini na kufikia makubaliano , anaumiza wengine na yeye mwenyewe kwa ukiburi wake , Hii ni kweli kabisa, wanawake warembo hatujawahi kuwa na maisha mazuri tokea kale zile”Aliongea Aoiline.
“Aoiline muda mwingine ili kukamilisha mambo makubwa na kupata ufunuo mkubwa lazima kuwe na kafara , ambacho Roma anakwenda kufanya leo hii kitamfanya kuwa karibu zaidi na ule upeo , ni jambo zuri kwake , huwezi kupata kila kitu hata kama uwe na uwezo mkubwa vipi , sio jambo la kuanza kujiumiza vichwa”Aliongea Sharif.
“Usidhani kila mtu ni mkatili kama wewe , najua una upeo mkubwa lakini sikupendi na tabia yako hio , Roma alikuwa yupo vizuri mwanzo lakini umemsababishia haya na kujikuta hana chaguao zaidi ya kumuua mwanamke anaempenda , umeridhika sasa?”
“Kama hutaki hilo limtokee nenda wewe kamuue yule mwanamke kumuepushia”Aliongea Sharif na kauli hio ilizidi kumkasirisha Aoline.
“Kama nikienda yule mwanamke wa kimiungu sio mwelewa ataniacha nimuue tu na kukosana na Roma”Aliongea.
Upande wa Clark alikuwa akiangalia kioo hicho na majonzi makubwa , ilikuwa ni ngumu kabisa kuelezea ni hali gani aliokuwa akijisikia
Upande wa Mzee Yasu na Xumei waliishia kutabasamu kiwasiwasi mara baada ya kuona Master wake na Ex wake kubwekeana.
Hatimae kila mmoja alitulia wakiangalia kwa hamu Roma akifanya shambulizi la kumuua Athena.
Roma tayari alikuwa ashaumba donge la radi nyeusi na kujibadilisha kuwa kama mkuki wa urefu futi sita.
Ijapokuwa ilionekana kama mwanga , lakini kila mtu alijua ni matokeo gani yatatokea kama Athena atashambuliwa nayo.
Roma taratibu sana alimsogelea Athena , kila hatua aliopiga ilisababisha mioyo mizito kwa miungu waliokuwepo na kufanya ukichaa wao kuwapanda.
Tembea yake kukisogelea kifo ilimaanisha pia ndio anguko la miungu .
Aphrodite na Artemis walikuwa wakilia kwa vilio vya kwikwi kabisa kwa kushindwa kuizuia huzuni yao juu ya kifo cha Athena.
Upande wa Athena alikuwa katika hali ya utulivu kabisa akimwangalia Roma namna ambavyo anamsogelea karibu na karibu tena , mkuki wake ulinyooka vilevile bila ya kutingishika ukimlenga mwanaume huyo , hakusogea hata kidogo.
Ikiwa ni mita chache tu wakiwa karibu Roma aliongeza spidi yake , kama simba aliekasirika zidi ya kitoweo chake , alitoa msisimko wa kimauaji , akiwa na siraha yake ya kinishati katika mkono wake alimlenga Athena uelekeo wa kichwa chake.
Athena aliweza kuhisi nguvu ya ajabu sana ikimsogelea na kufanya macho yake mazuri kuchanua , hakuna wa kuweza kuona namna ambavyo alikuwa akisugua meno kwa hofu na aliishia kufumba macho.
Lakini hatimae macho yake na lips zake zilipinda katika tabasamu la ahueni baada ya sekunde kadhaa kupita.
Damu nyingi ya moto ilifyatuka kutoka hewani na kudondokea baharini kama matone ya mvua.
Miungu mara baada ya kuangalia damu hio inayotitirika kwa chini walijikuta wakiacha mara moja kuomboleza , majonzi yao yalibadilika na kuwa mshituko huku akili zao zikikosa cha kuwaza.
Athena muda huo aliweza kuhisi ule msisimko wa nguvu ya ajabu umekwisha kupotea dakika ambayo ilikaribiana na uso wake.
Dakika hio hio mkono wa kiume wenye joto uliyashika mashavu yake kwa namna ya kuyapangusa upande wa kushoto.
Alijikuta akivuta pumzi nyingi na kufumbua macho yake mazuri , kwa sekunde kadhaa mwili wake ulikakamaa kama sanamu la barafu.
Bila kujua, mkuki wake ulikuwa tayari umekwisha kumchoma Roma , tena mbaya zaidi ulikuwa umemchoma katika eneo la moyo wake na haukuchoma juu juu bali ulienda ndani kabisa na kupita umbali ambao ulitosha kuharibu kabisa moyo wa Roma na kisha kuonekana mgongoni.
Kipande cha mkuki kilichoonekana kwa nyuma mgongoni kilikuwa na urefu wa mita mbili , kikifunikwa na madonge ya damu.
Lakini upande wa Roma ni kama hakuwa akijali juu ya kile kilichomtoboa zaidi ya kumwangalia mwanamke huyo kwa tabasamu na macho yaliojaa mapenzi mazito , alimwangalia Athena aliekuwa katika sura ya Edna kwa hisia kali mno , ni kama alikuwa akimwambia kama huna sababu ya kujishauri kuacha basi nakufa ili kukupatia hio sababu.
Mkono wake ambao ulikuwa umeshikilia kifo hatimae ulileta joto katika mashavu yake na kumfanya mwanamke huyo macho yake na pua yake vyote kwa pamoja kutetemeka.
*****
Upande mwingine katika ulimwengu unaojitegemea watu wote walijikuta wakisimama wasiamini macho yao .
Hata kwa Sharif na Aoiline wote walisimama kwa pupa wakimwangalia Roma akikiendea kifo kwa mshangao mkubwa na kutokuamini.
“What the hell is he thinking …”Sharif hakujua akasirike , achanganyikiwe au ni hisia gani nyingine ambazo zilimsababishia kukunja ngumi yake kama mwanamasumbwi anaetaka kuingia ulingoni., hisia zake alishindwa kuzitawala jambo ambalo ni nadra sana kwake.
Aoiline bila kutarajia na pengine kwa zaidi ya miaka mingi sana hakuwahi kutoa machozi lakini muda huo machozi yaliufunuka uso wake mzuri sana na kumzidi kupendeza na kusikitisha kwa wakati mmoja.
“Amefikiria nini huyu mtukutu… kwanini kafanya maamuzi ya kijinga namna hio?”Ndio kauli pekee alioweza kuongea huku akipaliwa na mate.
Upande wa Clark alikuwa ashajipigia magoti huku akitoa kilio cha kwikwi , uso wake wa kirembo ulifubaa kama vile umekosa virutubisho kwa muda mrefu , aliishia kufumba macho yake akiwa na majonzi makuu huku aking’ata lipsi zake kiasi cha kujitoa damu , alitingisha kichwa chake kwa majonzi makubwa ya kutokukubali.
“I Knew it .. I knew it ..”Aliongea akimaanisha alijua , alijua juu ya hilo lakini ilikuwa ameshachelewa kuongea neno hilo.
Maamuzi ya Roma yalikuwa ni nje ya matarajio ya kila mmoja .
“Wh.. Why..?!”
“Kwanini?”
Katika ubaridi huo wa upepo Athena alijikuta kwa kutetemeka midomo kama mgonjwa wa malaria alimuuliza Roma kwanini kafanya hivyo , macho yake yalikuwa makavu kama kioo akiwa bado ni mwenye kushindwa kuamini uhalisia uliokuwa mbele ya macho yake.
Unadhani kifo cha Roma kitamfanya Athena kuachana na mipango yake, Je unabii wa Athena unakwenda kutimia?.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR .

Mono no aware

ILIPOISHIA
Upande mwingine katika ulimwengu unaojitegemea watu wote walijikuta wakisimama wasiamini macho yao .
Hata kwa Sharif na Aoiline wote walisimama kwa pupa wakimwangalia Roma akikiendea kifo kwa mshangao mkubwa na kutokuamini.
“What the hell is he thinking …”Sharif hakujua akasirike , achanganyikiwe au ni hisia gani nyingine ambazo zilimsababishia kukunja ngumi yake kama mwanamasumbwi anaetaka kuingia ulingoni., hisia zake alishindwa kuzitawala jambo ambalo ni nadra sana kwake.
Aoiline bila kutarajia na pengine kwa zaidi ya miaka mingi sana hakuwahi kutoa machozi lakini muda huo machozi yaliufunuka uso wake mzuri sana na kumzidi kupendeza na kusikitisha kwa wakati mmoja.
“Amefikiria nini huyu mtukutu… kwanini kafanya maamuzi ya kijinga namna hio?”Ndio kauli pekee alioweza kuongea huku akipaliwa na mate.
Upande wa Clark alikuwa ashajipigia magoti huku akitoa kilio cha kwikwi , uso wake wa kirembo ulifubaa kama vile umekosa virutubisho kwa muda mrefu , aliishia kufumba macho yake akiwa na majonzi makuu huku aking’ata lipsi zake kiasi cha kujitoa damu , alitingisha kichwa chake kwa majonzi makubwa ya kutokukubali.
“I Knew it .. I knew it ..”Aliongea akimaanisha alijua , alijua juu ya hilo lakini ilikuwa ameshachelewa kuongea neno hilo.
Maamuzi ya Roma yalikuwa ni nje ya matarajio ya kila mmoja . “Wh.. Why..?!”
“Kwanini?”
Katika ubaridi huo wa upepo Athena alijikuta kwa kutetemeka midomo kama mgonjwa wa malaria alimuuliza Roma kwanini kafanya hivyo , macho yake yalikuwa makavu kama kioo akiwa bado ni mwenye kushindwa kuamini uhalisia uliokuwa mbele ya macho yake.

SEHEMU YA 796.
Athena alijihisi ni kama nguvu zake zote zinampotea kutoka katika mwili wake, ukiachana na kuongea kauli hio ya kuuliza akili yake haikuwa ikifanya kazi kisawasawa.
Wakati wa unabii wake kushindwa kutabiri kwa usahihi , hatimae pigo kubwa linampata , akili yake ilirudi katika uhalisia na kujua nini kimetokea.
Kwa sababu ambazo hazikujulikana alikwepesha macho yake na ya Roma na hakuweza hata kuangalia jeraha ambalo amemsababishia ,lakini vilevile hakuelewa kwanini katika wakati huo alikuwa akitaka kulia.
Mara baada ya tone la chozi kumdondoka na kuyafikia mashavu yake , kwa upole lilifutwa na vidole vya Roma.
“Nini tatizo ?, unalia..?”Aliuliza Roma akiwa ni mwenye tabasamu hafifu.
Licha ya damu nyingi kutoka katika eneo la moyo , bado alikuwa katika hali ya utulivu na hakuonyesha ishara yoyote ya maumivu , ni kope za macho tu ambazo ndio zilikuwa zikicheza cheza kwa haraka.
“Unaniuliza kwanini nimefanya hivi? , kwani sijakuambia kwamba ni jambo ambalo limekwisha kupangwa , kwasababu hutaki kuacha na siwezi kukuua vilevile basi mimi ndio nakufa , kama nikifa sitowajibika tena , sitomuangusha yoyote na ukweli sitokuwa na haja ya kujali sana haya mambo , pia
sitojihangaisha na mambo yako ambayo unafanya .. kwa maana kwamba utaweza kuishi vizuri mimi nikiwa mfu”
Athena alijaribu kukizungusha kichwa chake pembeni akijitahidi machozi yasimtoke lakini alikuwa akishindwa.
Mkono wake ambao ulikuwa umeshikilia mkuki
hatimae ulikosa nguvu zote na kuanza kutetemeka na alijikuta akiachia .
Roma alidondoka akiwa na mkuki ule kutoka angani na jambo lile lilimuogpesha zaidi na kwa kutumia kanuni za anga alimshikilia.
Athena mara baada ya kuangalia uso wa Roma ambao umepauka aliweza kugundua Roma alikuwa amezuia andiko la urejesho kutokumponyesha.
Ki ufupi ni kwamba Roma aliacha kila kitu ambacho kinausaidia mwili wake wakati wa majeraha kutofanya kazi , ilikuwa tayari ashaamua kufa, sio kwasababu Athena kamchoma kisu bali ni kwasababu yeye ndio kaamua kufa.
Ilikuwa ni swala la muda tu kupoteza damu yote na mwili wake kuacha kufanya kazi na hatimae kukikaribia kifo.
Ni miujiza tu kwa yeye kuweza kuongea mpaka wakati huo kulinganisha na ukubwa wa jeraha.
Roma ambae alikuwa amezuia uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi hakuwa pia na nia ya kuifanya nafsi yake kuendelea kuishi , bila msaada wa nishati za mbingu na ardhi nafsi yake taratibu ingetoka katika mwili wake wakati mwili wake na ubongo vitakapo kufa.
Kujiua sio kazi ngumu sana kwa mtu kama Roma ambae alikuwa amepata upeo mkubwa.
Hata kama mtu anamiliki andiko la urejesho , mbinu ambayo ina uwezo hata wa kurudisha maiti kuwa hai , hakuna wa kuweza kumuokoa Roma kama yeye ndio kaamua kufa.
“Ni kweli unataka kufa .. unadhani unastahili kufa kwa ajili yangu?”Athena alionekana kuwa na maneno mengi ya kuongea lakini kuna kitu kilikuwa kimemkaba kooni na kuishia kutingisha kichwa chake
“Haunichukii , Mimi sio Edna wala Seventeen… ni mipango yangu yote ya mimi kukutanisha na Edna na kwanzia wakati huo nilikuwa nikitumia hisia zako kwa Edna na Seventeen kukamilisha mipango yangu, kwanini umeamua kufanya hivi?”Aliuliza Athena.
“Hata kama wewe sio Edna au Seventeen , bado tu ulimlinda na kumzaa binti yangu … , haijalishi ulifanya hivyo kwa ajili yangu au lah , ninakushukuru sana …. , Siwezi kuona nafsi ya mwanamke yoyote ndani yako ikifa , nitaweza vipi kumuua mama wa mtoto wangu kwa mikono yangu miwili , kama nikikuruhusu wewe kuniua vilevile utakosa ujasiri wa kujitokeza mbele ya Lanlan na hilo sitaki litokee , hivyo chaguo sahihi ni mimi kujiua mwenyewe”
Mara baada ya kuhisi uhai wake unazidi kupotea , alijikuta akizidi kutetemeka na nafsi ambazo
zilikuwa zimejificha ndani yake zilianza kufurukuta kama kwamba zimekuwa zimefanikiwa kupita katika msukosuko.
Alikuwa katika hali ya mkanganyiko kutokana na hisia zilizokuwa zikiibuka ndani yake , hisia ambazo hakuwahi kuzielewa kabla , ilikuwa ngumu kwake kujidhibiti.
Huyu mwanaume, inakuwaje hajawahi kunichukia na bado ananishukuru vilevile?
Roma alimwangalia kwa macho ya ndani , macho yake yalianza kukuosa nguvu na muda wowote ni kama angepata usingizi.
Kitendo cha mwanamke huyo kulia mbele yake ni kama kilimpa hali ya kuridhika na kuishia kutoa tabasamu hafifu.
“Edna…”
Roma aliita kana kwamba alikuwa akimwangalia Edna akitabasamu mbele yake.
Muda huo kumbukumbu zilizopita zilirudi upya katika akili yake moja baada ya nyingine kama vile ni michoro ya kuvutia.
Mwili waAthena ulitikisika, uso wake ulijikunja kama vile ni mtu anaepitia maumivu, ilionekana ni kama vile alikuwa akihangaishwa na kitu.
“Ndio , mtu anaempenda ni Edna na Seventeen na sio mimi kwa hakika, hili halinihusu kabisa … kwanini niwe na huzuni kwasababu ya kifo
chake, kwanini nilie kwasababu yake , au ni kwasababu nilikuwa nyuma yake katika maisha yake yote kwa kujificha .. , huu si ndio mwisho ambao nilikuwa niki utumainia , si nimesubiri kwa miaka elfu ishirini kwa ajili ya hii siku .. lakini mbona moyo wangu unauma hivi…”Alikuwa akijiwazia ndani kwa ndani.
Roma hakuwa na uelewa kama nafsi ya Athena ilikuwa ikipitia hali ya mkanganyiko kwa muda huo.
Nafsi tatu zote zilianza kuwasiliana , kuungana, kuamka , kumezana , kugawanyika na kujitofautisha bila kukoma kwasababu ya kuzimwa mwanzoni na kufanya hisia zao kulala.
Ubini wa mwanamke aliekuwa mbele yake haukujalisha kabisa na aliishia kutoa tabasamu tu.
“Edna mke wangu .. uhai wangu umekaribia mwisho , lakini mambo mengi yametokea kati yetu , mengine ni mazuri na mengine ni mabaya na mengi zaidi siyakumbuki .. lakini nina uhakika wa nyakati nzuri tulizokuwa pamoja ..jambo moja ambalo sijutii na zuri katika maisha yangu , ni kukutana na wewe, Edna hata kama unataka kuniua sasa hivi utabakia kumbukumbu nzuri kwangu , kila kitu kilichotokea leo hii ni maamuzi yangu , ni chaguo langu na haihusiani kabisa na wewe .. usije kuishi maisha ya huzuni na yasio na furaha kwa sababu yangu , kwani itanifanya nijihisi vibaya zaidi nikiwa mfu kuliko nikiwa hai”
Athena kichwa chake kilikuwa kikimuuna sana , kila neno lilikuwa ni kama kisu kinachomkata na kumchoma katika kichwa chake , ilikuwa haiwezekani kujizuia zaidi na aliishia kujilazimisha kuzuia maumivu yake na kulia huku akiuliza;
“Kwanini hukunizuia .. ulijua tokea mwanzo nilichokuwa nikifanya ,, ulijua muda mrefu tu mimi ni nani ,kwanini? , hata kama ni sasa hivi ungeniambia maamuzi yako , pengine ningeacha , pengine nisingeenda mbali..”
Roma kwa mikono yake yote alishikilia mkuki katika eneo la moyo wake , damu nyingi iliokuwa ikimtoka ilimfanya kupoteza ufahamu na kukosa udhibiti wa mwili wake.
“Kwasababu siwezi ….”Macho yake yalikuwa nusu yamejifunga huku akicheka kicheko dhaifu.
“Kwasababu siwezi na wewe huwezi , si ulisema mwenyewe hakuna kitakachobadilika mbeleni , umeendeleza misheni yako kwa miaka elfu ishirini , unadhani ni kwa namna gani nitakufanya uache kwa sentensi moja tu , natumia maisha yangu ya miaka ishirini kwa kubadilishana na maisha yako ya miaka elfu ishirini .. hata hivyo haijalishi wewe ni nani , nipo tayari kufanya lolote , hiki ndio kitu pekee ninachoweza kufanya , kitu pekee ninachoweza kufanya kwa ajili yako..”
“No …!”
Mwanamke huyo alijikuta akishikiria kichwa chake kwa mikono yote miwiili na kukitingisha kwa nguvu, alionekana kukosa mhimili na kuangaua kilio.
Miungu wote walishindwa kujizuia na kuishia kuomboleza kimya kimya wakiangalia tukio hilo.
Roma sauti yake ilikuwa ikidhoofika zaidi na zaidi lakini bado tabasamu halikuwa limetoka usoni.
“Nikishandoka .. naomba usiwasumbue watakao omboleza kifo changu, waambie sina maana tena na wanisamehe .. na zaidi ya yote naomba usimfanye Lanlan kuishi bila mama … kabla ya kuja hapa nilishamwambia mama yake atarudi..” “Acha kuongea… Acha kuongea ..!!”
Mwanamke huyo alibembeleza akimtaka Roma asiendelee kuongea kwani ukichaa ulikuwa ukimvaa , aliishia kujipigia magoti kwenye hewa mbele yake huku mikono yake ikiwa imemshikilia Roma katika kiuno.
Roma hakuwa na uwezo tena wa kuinua mgongo wake na alijikuta akilegea taratibu , damu ilikuwa imemchafua mwanamke huyo lakini alionekana kutokujali na aliishia kulia kutokana na maumivu.
Hatimae alifumba macho yake na sauti yake haikusikika tena zaidi ya midomo kucheza cheza.
“Edna … unajua ..unajua , nilishawahi kuwaza mtu pekee anaeweza kuniua itakuwa ni mimi mwenyewe…. siwezi kushindwa na mtu yoyote wala hukunishinda , nimejishinda mimi mwenyewe kwasababu , Edna sikuweza.. sikuweza kukupenda…”
Roma sauti yake haikueleweka alitaka kumalizia kuongea nini lakini huo ndio ulikuwa mwisho wa sentensi isiokamilika , alikuwa ni kama Tiara iliokatika uzi na kupotea kusikojulikana kiasi cha kutokupatikana tena.
Wakati huo mwanamke huyo alijikuta akipumua pumzi ya barafu , alifumbua macho yake na kuinua kichwa chake juu , aliukumbatia vizuri mwili wake ambao tayari ushakuwa wa baridi.
Alimwangalia kwa macho yasio ya kawaida mwili wa mwanaume huyo ambao haukuwa na dalili yoyote ya uhai , alijikuta akiinamisha mdomo wake na kukutanisha na mdomo wa marehemu na kumbusu kwenye lipsi zilizokauka.
Wakati machozi yake ya moto yakiloanisha sura ya mwanaume huyo alijikuta akilazimisha tabasamu.
“Roma mume wangu si nilikuambia kipindi kile , nilikuambia kabisa ukiendelea kubakia na mimi utakufa , nilikuwa nikipata ndoto za kila siku kwa muda mrefu sana lakini bado ukakataa kuamini maneno yangu …. Now its too late , ndoto imekuwa uhalisia lakini bado unaniambia nisiwe mwenye hatia , Hubby kwanini unanifanyia hivi , kwanini unanifanyia matani ya namna hii , unaniogopesha mwenzio , tafadhari acha kuniogopesha , Amka sasa mume wangu , Mimi ni mkeo Edna..”
Kilio cha Edna hakikuwa kikielezeka ni upepo tu uliofanya asisikike , Aliita majina yote mazuri kwa ajili ya kumrudisha Roma hai lakini mwanaume huyo hakuamka kabisa.
*****
Upande wa visiwa vya wafu ndani ya ngome ya marehemu Hades,Lanlan alionekana akitoka katika chumba chake huku akichezesha lipsi zake , alikuwa akipiga miayo na kujinyoosha nyoosha huku akijiuliza kwanini mashangazi zake hawajamuamsha siku hio.
Kibonge nyanya huyo alikuwa amepitiliza kulala muda mrefu siku hio na kumfanya kuhisi njaa kali.
Lakini hata hivyo alijisiikia vizuri maana hakukuwa na wa kumlazimisha maswala ya kusafisha kinywa na kuosha uso wake , isitoshe alikuwa akichukia usumbufu huo mno , dawa ya meno yenyewe haikuwa tamu.
Akiwa amevalia kijiblauzi cha mikono mifupi na kisuruali cha rangi nyeupe , Lanlan aliangaza kulia na kushoto na kisha kutembea katika vyumba vya mashangazi zake na kila chumba alichopita hakikuwa na mtu.
Hali ya kujikatia tamaa na kutokufurahi ilijionyesha katika uso wake huku akijiambia inamaana kila mtu kaelekea kupata chakula bila kutaarifiwa, lakini mara baada ya kuacha pua zake za utambuzi kunusa hakuweza kupata harufu nzuri ya chakula hata kidogo.
Hatimae fahamu zake zilimwambia aende katika chumba kikubwa, mara baada ya kufika akashika komeo na kuanza kulizungusha lakini mlango ulionekana kufungwa kwa ndani.
Dakika hio hio kwa kutumia uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi aliweza kusikia sauti za pumzi zikisikika kutoka ndani ya chumba hicho na hazikuwa pumzi ya mtu mmoja bali ya wengi.
“They are all playing hide and seek and ignoring
me on purpose!”Aliongea mwenyewe akimaanisha wanacheza mchezo wa kutafutana makusudi tu huku wakimpotezea.
“Puuh!!!”
Nguvu za Lanlan hazikuwa za mchezo mchezo , alijirudisha nyuma kidogo tu na kupiga mlango huo wa chuma kikumbo na loki zake zote zilifyatuka na kuharibika kabisa na kwenda kudondoka kwenye sakafu ya chumba hicho.
“I’m hungry ! Aunties , what are you doing hiding here ?”
Mara baada ya kupiga makelele na kusimama alijua kuna kitu hakipo sawa.
Kitu cha kwanza ni kwamba mashangazi zake wote walikuwa uchi ,walikuwa wamelala bila nguo za kulalia huku kila mtu akilala staili yake katika kitanda hicho kikubwa .
Pili baba yake hakuwepo na kulikuwa na harufu isiokuwa ikielezeka.
Lakini hata hivyo harufu hio haikuwa mpya kwa Lanlan , kwani alishawahi kuinusa wakati baba yake na mama yake wakimaliza kuchukua mazoezi na shangazi zake pia.
Sasa kwasababu bibi yake alimwambia ni jitihada za baba yake kumpatia wadogo zake hakujisumbua sana kufikiria.
Mara baada ya kushika tumbo lake ambalo lilikuwa likinguruma , kama mpira alijirusha na kwenda kutua juu ya kitanda na kuanza kumtingisha mmoja mmoja kwa nguvu.
Hatimae wanawake wote waliamka wakiwa katika bumbuwazi kutokana na ukatili wanaofanyiwa na kashetani hako kadogo , maana hakuwa akichagua sehemu maalumu ya kutingisha.
Mara baada ya wote kuamka na akili zao kukaa sawa walijikuta wakitamani kuingia uvunguni kutokana na hali waliokuwa nayo , hususani baadhi yao ambao walikuwa na kimiminika kilichogandiana mwilini.
Waliishia kumwambia Lanlan kushuka chini sebuleni akaangalie TV na kisha wakakimbilia kwenye vyumba vyao kwa ajili ya kujisafisha
Kwa wakati huo hakuna ambae alijisumbua kufikiria kile ambacho kinaendelea juu ya Roma na hawakuwa wakikumbuka vizuri lakini walielewa alikuwa amewawekea kitu kilichowafanya kulala muda mrefu.
Wakati wanawake hao wakijishangaa na kujiuliza maswali mengi upande wa Blandina alikuwa akimsaidiaAfande Kweka kuzishuka ngazi kuja sebuleni na kisha alianza kuita jina la mwanae Roma.
Ilikuwa tayari ni mchana lakini hakuweza kuona mtu yoyote na hata pale walipojitokeza hakuna ambae alikuwa na ujasiri wa kuongea wapi Roma alipo licha ya kuwa na hisia juu ya kile kinachoendelea.
Kila mmoja aliamua kupotezea hali ya wasiwasi na kujiweka bize kuandaa chakula ili wasimfanye Lanlan kuzidi kutoa miayo.
Blandina alimjali sana Lanlan kuliko kitu chochote na alienda jikoni kumchemshia uji kwanza ili kupunguza njaa.
Crashhh !!!!
Sauti ya bakuli kupasuka ilisikika huku uji wote ukimwagika chini na vipande kusambaa.
Waliosikia mlio huo walishituka na kukimbia kuangalia kilichotokea na walishangaa kuona alikuwa ni mama mkwe wao aliedondosha bakuli la udongo.
Blandina moyo wake ulikuwa mzito mno ghafla tu na alilazimisha tabasamu na kuwaambia kwamba yupo sawa lakini licha ya hivyo mapigo ya moyo yalikuwa yakienda kasi mno kiasi cha kukishika kifua chake., kwasababu zisizoeleweka alikuwa akijihisi maumivu.
*****
Upande wa ncha ya kaskazini wingu kubwa jeusi lilikuwa limetanda na upepo ulikuwa mkali mno.
Mti Mama ambao ulikuwa umechukua nafasi kubwa ulikuwa ukipungua ukubwa wake kwa spidi ambayo inaonekana kwa macho.
Matawi na majani yake vilianza kugeuka chembechembe kama za madini ya dhahabu na
kupotelea angani , ule ulinzi uliokuwa umezingira mti huo uliweza kupotea pia .
Uuungu ambao ulikuwa katika hatua za ukuaji ulianza kupotea pia kwa kudondoka juu ya mti.
Mti huo mkubwa sana ambao ulkuwa umelitanda anga ulianza kurudi taratibu katika umbo la moyo wa Gaia.
“Its over .. Athena too has lost ..”Christen aliongea huku akiangalia namna Mti mama ulivyokuwa ukisinyaa akimaanisha imekwisha , Athena na yeye ameshindwa.
Miungu muda huo walikuwa wamesimama katika barafu wakiangalia tukio hilo
“Uungu wa Zeus umepotea , Athena amepoteza
udhibiti wa uungu wake na wa kwetu umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na majeraha , hata kama Mti mama usirudi katika umbo la moyo wa Gaia hatuna uwezo wa kuulinda sisi wenyewe , hatuna nguvu tena”Aliongea Hera akiwa ni mwenye masikitiko.
Kutokana na ufahamu wao kuungana na Mti mama , ilikuwa tayari ushahisi kushindwa kwa miungu ndio maana ukaamua kupotea wenyewe kwa kurudi katika umbo la Moyo wa Gaia ili kujificha.
Hio ni mmoja ya njia ya ulinzi binafsi ya mti mama , pale upatapo misukosuko chaguo la mwisho la kujilinda ni kurudi katika umbo la mbegu au moyo na kusubiri nafasi nyingine ya kuota tena.
Muda huo miungu hawakuonekana kuwa ni wenye furaha au huzuni.
Kushindwa ni kushindwa tu , hata kama Roma amepata ushindi huo kupitia kifo chake haikumaanisha kwamba miungu hao walikuwa wameshinda.
Asiwepo hata mmoja , wote waliangalia upande mwingine juu ya barafu kwa mbali.
Edna alikuwa amepiga magoti juu ya barafu , akiwa ameshikiria maiti ya Roma katika mikono yake huku akiwa halii bali mtu aliekuwa amepotelea kwenye mawazo.
Eneo la kifua chake kulikuwa kumebakia shimo kubwa mara baada ya mkuki ule waPalas kutolewa , damu ilishakauka na jeraha kuganda kwa barafu , kuhusu moyo wake ulikuwa ushaharibika na kuwa vipande vpande.
Mwanamke huyo mrembo machozi yalikwisha kumkauka na aliishia kuyaangalia mashavu yaliopauka ya marehemu mume wake bila ya kusema lolote.
Kwa jinsi upepo ulivyokuwa ukipeperusha nywele zake ilimfanya kuonyesha kuwa mpweke sana na kutia huruma na hakuna ambae alimsumbua.
Baada ya muda kidogo hatimae Christen alimsogelea Edna pale alipo na mara baada ya kuangalia sura ya Roma kwa huzuni alimgeukia Edna.
“Wewe ni Edna?”
Edna alikuwa ni kama hajamsikia kwani hakujisumbua hata kujibu swali lake , alichokuwa akifanya ni kumkumbatia Roma kana kwamba hataki mwili wake kugeuka barafu bila kuonyesha hisia zozote.
Hera na wengine wote walifika pia na kuiangalia maiti ya Roma huku wakiwa na hisia zisizoelezeka.
Chuki zao na majonzi yao hayakuwa na tofauti kubwa na kile alichokuwa akijisikia Edna..
Ufufuo wa miungu umeshindikana kiasi cha kuwafanya kuonekana kuchoka pia .
“Aphrodite acha kumsumbua atakuwa anajisikia vibaya sana hapo , naona uungu wa Athena bado upo lakini kwa hiari yake ameamua kuisalimisha nafsi yake kwa Edna”Aliongea Apollo.
“Imewezekanaje? , hata kama Athena hamuwezi Roma lakini haimaanishi hawezi kulnda nafsi yake zidi ya Seventeen na Edna”Aliongea Ares.
“Labda ni kwasababu jina la mwisho alilotamka Roma ni la mke wake Edna”Alijibu Artemis.
“Inaonekana si tu kipindi akiwa katika mwili wa Seventeen au wa Edna , Athena amekuwa na hisia za kimapenzi kwa Roma , inasikitisha kuona amekuja kulijua hilo sasa hivi na kitu ambacho ameona anaweza kufanya kwa ajili ya
Roma ni kuisalimisha nafsi yake kwa Edna”Aliongea Apollo
“Kwahio inamaana sasa hivi Edna ndio mtawala wa uungu wa Athena?!”Aliuliza Hermes akiwa amekunja sura.
“Haha.. una wasiwasi atatuaa sasa hivi , tuna bahati hata hivyo kuwa hai mpaka sasa hivi , kuna haja gani ya kuogopa kifo?”Artemis aliongea kwa kucheka.
Sura ya Hermes ilikakamaa ashindwe kutamka neno.
Lakini muda huo huo hali ya eneo hilo ilibadilika kwa haraka sana.
Anga lilionekana kuchemka na kutengeneza shimo kama ombwe na mwanamke na mwanaume waliweza kuonekana wakitoka , miungu hao hawakuweza hata kuelewa ni kwa namna gani watu hao wamefika hapo.
Watu hao walikuwa ni Aoiline na Sharif.
Mara baada ya Aoiline kuona maiti ya Roma aliishia kutingisha kichwa chake huku muonekano wake ukiwa ni wa kuomboleza , alionekana kuthibitisha ukweli juu ya Roma kupoteza maisha na hakuna uwezekano wowote wa kumponyesha kwasababu kaamua yeye mwenyewe kujiua.
Miungu hao mara baada ya kumwangalia vizuri Sharif , wote walikakamaa huku sura zikijikunja.
“Its you , the one from 20000 years ago!!?”
Miungu kwa haraka sana waliweza kujua mtu huyo ni jini aliehusika kumfungia Zeus katika gereza la roho miaka elfu ishirini iliopita pia mtu ambae alizuia miungu kutokuitawala dunia na kisha kuwasainisha The gods treaty.
Sharif upande wake hakuwa na mudi ya kuwaangalia kabisa na mara baada ya kuiangalia maiti ya Roma aliishia kuonyesha muonekano usioelezeka.
“Mtoto mjinga sana wewe , umeyakatisha maisha yako mwishoni mwa safari , kwanini hutaki kusikiliza maneno ya wakubwa zako?”
Edna hatimae aliinua uso wake kama vile ni mtu alieitambua sauti ya mtu huyo anaongea na hasira zilimvaa palepale.
“Umeridhika na mwisho wa haya matokeo?”Aliongea akiwa hana chembe ya woga hata kidogo.
Mara baada ya Athena kujjisalimisha kwa Edna , ilimaanisha pia kumbukumbu zote za kwake na za Seventeen alizisalimisha pia , hivyo kikawaida Sharif asingekuwa mgeni kwake.
Kama kuna mtu ambae kwa muda huo Edna alikuwa na chuki nae sana basi ni Sharif au Master namba moja , muangalizi wa dunia.
Kama sio kutengeneza mchezo huo wa kimtego , Roma kujitoa kafara kusingetokea.
Edna hata yeye alitamani asingefahamiana na Roma au kipindi kile angeachana nae moja kwa moja.
Lakini hakutaka kujimilikisha nguvu ya Athena ili kupigana na Sharif.
Alijua kabisa kulikuwa na gepu kubwa kati yake na Sharif , hata kama alikuwa akimchukia sana hakuwa na chakumfanya.
Maneno ya Roma kabla ya kifo chake yalikuwa yakigonga katika akili yake , bado alikuwa na mtoto wa kulea na mambo mengi ambayo alihitajika kuyafanya hivyo hakutaka kufa muda huo , alihitaji kuishi kwa ajili ya mambo hayo , kwa ajili ya Lanlan.
“Sikutarajia kama atachukua maamuzi haya …”Aliongea Sharif huku akionyesha namna gani alikuwa akijutia.
Ijapokuwa miungu wamepoteza pambano juu ya ufufuzi wa miungu wenzao , Roma pia amekufa.
Kwa matokeo hayo ni kama alijikuta akishindwa kufaidika kwa namna yoyote ile , hakumpata mtu wa kuchukua mikoba yake wala miungu kutawala dunia.
Sharif alitamani kama binadamu wangeshinda basi angemrithisha Roma mikoba yake na kuondoka , lakini vilevile kama miungu ingeshinda asingekuwa hata na haja ya kumtafuta mrithi angeondoka kwani alijua uwezo wa kujilinda wao wenyewe wanao, ki ufupi ni kwamba misheni yake imefeli pia.
“Mhmh , kwahio unasema kwamba mimi ndio nilipaswa kufa leo hii na sio mume wangu .. kama ni hivyo basi samahani kwa kukuangusha na tumaini lako kuyeyuka”Aliongea Edna katika hali ya dhihaka.
Sharif upande wake hakutaka kujisumbua na maneno ya dhihaka ya Edna , alichokifanya muda huo ni kuangalia maiti ya Roma kimya kimya akiwa katika hali ya kihisia isioelezeka.
Isitoshe matokeo ambayo aliyasubiria kwa zaidi ya miaka elfu ishirini yalikuwa ni ya kuvunja moyo.
Aoiline hakutaka kumuongelesha Sharif muda huo kwanamna ya kumchokoza , hivyo aliishia kuangalia miungu waliobakia katika hilo eneo kwa sura isiokuwa na utani.
“Mnapaswa kuacha kumkodolea macho huyu mtu , kwa uwezo wenu wa kanuni za anga hata muishi miaka mingine milioni moja hamtomuweza , nawashauri kuishi maisha yenu kwa amani hapa duniani , sehemu ambayo imeathirika na misheni zenu pamoja na mapepo mlioyaachia , kurudi katika hali yake ni jambo litakalochukua muda , kama mnahitaji amani ni kheri mkafanya kitu tofauti na kuendelea kuangalia watu , mmenielewa?”
Miungu hao walijua kabisa mtu ambae anaweza kuongozana na Sharif lazima uwezo wake hautakuwa wa kubezwa hata kidogo , hivyo hawakutaka kutotii maneno yake.
Ilikuwa ni kweli , kama wanataka kuishi hapa duniani vizuri wanapaswa kwenda kuisafisha dunia ambayo wameichafua , iwe wanataka au hawataki , kwa vyovyote vile dunia ni ya binadamu na wao watabakia kuwa wageni.
Mara baada ya kuongea kauli hio Aoiline alimsogelea Edna ambae alikuwa amejichokea na kumshika bega.
“Wewe kuishi vizuri ndio njia nzuri ya kulipia alichokifanya leo hii , naamini hataki kukuona katika hali ya ukiwa”Aliongea.
Edna hakuongea neno zaidi ya kuiinua maiti ya mume wake na kusimama.
Alimwangalia Sharif kwa macho makali mno kama kwamba alikuwa akimwambia inaweza isiwe leo ila siku nitakuua na kisha aligeuka na kuianza safari.
Alikuwa na mpango wa kumrudisha Roma visiwa vya wafu ili kuzikwa na aishi hapo hapo ili alione kaburi lake kila siku.
Mjane huyo alisababisha hali kuwa ya huzuni na ukimya usio wa kawaida , kwa namna alivyoupakata mwili wa Roma ilisikitisha sana kwa wale waliokuwa wakimwangalia.
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 797.
Ni muda huo huo wote wawili yaani Sharif na Aoiline ghafla tu walijikuta wakipatwa na hali ya hofu iliowasababishia kufubaa nyuso zao.
“Hebu subiri!!”Sharif aliongea kwa nguvu akimzuia Edna ambae alikuwa akijiandaa kutumia kanuni za anga kupotea na mwili wa Roma.
Hata Aoiline alikuwa katika hali ya mshangao , macho yake yote yalkuwa yakiangalia angani kupitia pete iliokuwa kidoleni katika mkono wa Roma.
Kati ya hali hio ya mshangao wa kila mmoja , miale saba ilimulika kutoka kutoka katika hifadhi ya pete ya Roma.
Kwa kuangalia kwa umakini utaweza kuona kitu kilichokuwa kikifanana na kioo kikubwa mno cha mviringo wa yai kilichotengenezwa kwa shaba kikifyatuka kutoka katika hifadhi hio.
Ilikuwa ni kama kipindi hazina ya Sharif ilivyokuwa ikichomoza katika hifadhi ya pete ndio kilichotokea.
Kioo hicho chenye muonekano wa kikale cha muudo wa yai , nyuma yake kilikuwa na mchoro kama wa Logo flani au Sigilisi uliochorwa katikati , huku upande wa kioo kilikuwa kikitoa miale saba ya mwanga kama vile ni TV ya kimaajabu.
Kadri miale ile ya mwanga ilivyozidi kuwaka ndio ukubwa wa kile kioo ulivyoongezeka na kufikia ukubwa wa futi kama sita hivi.
Kile kioo kilikuwa kikielea angani , lakini eneo ambalo kilikuwa kikielea ni kama vile kinavutana na mwili wa Roma.
Mara baada ya watu wote kuangalia kwa ukaribu zaidi ndani ya kile kioo, kitu pekee walichoweza kuona ni anga lenye nyota katika umbali uliochorwa kwa ramani, yaani ni kama kuna ramani ya kimstari kutoka nyota moja kwenda nyota nyingine ndani ya kioo hicho.
Katika anga hizo za mbali , nyota hao wa kutokuhesabika walionekana kuzunguka katika mzunguko wa milkway, Nebula zake ni kama vile zimepata uhai.
Katikati ya kundi hilo la nyota kulikuwa na mstari kama wa Ramani ambao kwa namna ilivyo ni kama vile nyota zote zilikuwa zikionyesha utukufu kwa nyota ya katikati, yaani kwa lugha nyepesi ilikuwa ni kama vile nyota hio ya katikati ilikuwa ni ya kipekee sana.
Ilonekana ni jambo la ajabu sana , kwani ilionekana kana kwamba haikuwa ni uchoraji bali ni mfano halisia wa eneo mahususi katika anga za mbali.
“Hii Dhana si ni moja ya Dhana zilizoachwa na Wajumbe wa mkuu wa enzi , Dhana ya kioo cha nafsi?!?”
Aoiline ndie aliekuwa wa kwanza kutambua Dhana hio , hakuitambua kwasaabu ashawahi kuiona bali ni kwasbabbu katika elimu yao Dhana hizo zilitajwa kwa muonekano wake na tabia zake , kama ilivyokuwa kwa Shoka la Pangea , Chaos Cauldron na Ngoma ya Naoni na zingine.
Ukweli ni kwamba hakuna jini au kiumbe chochote ambae ashawahi kuona Dhana hio ikitumika sio kwa Aoiline tu hata kwa Sharif mwenyewe.
Edna na yeye alikuwa kwenye mshituko , bila ya kuelewa alijikuta akiharakisha na kumlaza Roma kwenye sakafu ya barafu na akayainua macho yake kuangalia kioo hicho kwa wasiwasi , kulikuwa na hali ya tumaini katika macho yake.
Sharif upande wake aliishia kutingisha kichwa chake mara baada ya kudhibiti mshituko wake.
“Inawezekana vipi , Dhana hizi za wajumbe wa Enzi huwa zina nafsi zao wenyewe zenye nguvu kubwa , kama ikitokea mtu hana nguvu inayolingana na Wajumbe wa mkuu wa enzi au kufikia ule upeo , huwezi kutambuliwa na nafsi yake , hata kama mmoja kuupita ule upeo vilevile hawezi kutambuliwa na Dhana hizi , vinginevyo Dhana hizi za mkuu wa Enzi zisingewezekana kuwatambua wajumbe pekee .. kwahio inamaanisha huyu mtoto…”
Anachomaanisha Sharif kwa lugha nyepesi ni kwamba Dhana zote za wajumbe wa mkuu wa enzi walizoziacha hapa duniani zina ufahamu wao zenyewe na ufahamu huo ni wa kutambua wajumbe wa mkuu wa enzi pekee.
Hapa utofautishe kabisa na Chaos Cauldron ambapo ni roho ya mnyama wa maafa ndio ilimtambua Roma na kumkubali kama Master wake , kuhusu Dhana kama hio ya kioo cha nafsi ufahamu wake unaungana na ule ufahamu wa Wajumbe wa mkuu wa enzi , yaani ni kama aina vile Dhana hio hufanya kazi pale tu itakapopokea maelekezo maalumu ambayo ni wajumbe wa mkuu wa enzi wanayoyajua tu.
Sharif hata yeye mwenyewe hakuwa akijua juu ya namna ya kuziita ama kutumia Dhana hizo licha ya uwezo wake , Roma ni kweli alikuwa na uwezo wa kutumia Shoka la kipangea lakini ukweli ni kwamba aliweza kulitumia kwasababu tu lipo katika mikono yake lakini hakutambuliwa na shoka hilo.
Kama kweli Roma angetambuliwa na shoka hilo basi miungu wasingeweza hata kudumu katika shambulizi moja , yaani kwa lugha nyepesi Roma alitumia theruthi tu ya uwezo halisi wa Shoka la kipangea na hio yote ni kwamba hakuwa na uwezo wa kulipa maelekezo yeye kwani sio mjumbe au Mkuu wa Enzi.
Sasa kama mtumiaji wa Dhana hio asipopata kutambuliwa na Dhana kama Kioo cha nafsi , uwezekano wa kujua siri ya uwezo wake wote ni mdogo mno ndio maana Roma alibahatika kuwa na kioo hicho katika hifadhi yake ya pete bali hakuwa na uwezo wa kukitumia.
Katika Dhana ambazo Roma alizipata na kufanya siri wakati akiwa ulimwengu wa jicho la anga ni pamoja na kioo hicho , haikuwa Shoka tu na jambo hilo alifanya siri hata kwa Xiao ambae aliambatana nae.
Sasa kitendo cha kioo hicho kutoka katika hifadhi ya pete ya Roma na kuonyesha uwezo wake kwa kummulika Roma ilikuwa ni dalili tosha kwamba Roma ametambuliwa na koo hicho hivyo kwanzia muda huo anakuwa ndio Master.
Aoiline alikuwa pia akijua kuhusu mambo hayo hivyo aliishia kutoa kicheko tu cha masikitiko kama vile aliona ni kama kuna mchezo wanachezewa.
“Sharif umeona sasa , huyu mtoto nilishakuambia ashafikia ule upeo kama ilivyokuwa kwako , hakuchagua kukata tamaa lakini vilevile amefanikiwa kupita , amefanikiwa pia kupata utambuzi moja kwa moja kutoka kwa mkuu wa enzi kupitia kioo cha nafsi , Amekushinda ki upeo awamu hii”Aliongea Aoiline huku akinyooshea kioo kilichokuwa kikinesa nesa angani kama kwamba kuna mtu kakishikiria.
Sharif alikuwa na mawazo na hali ya mkanganyiko , hakuwa na furaha kabisa , hali ilikuwa nje ya uelewa wake aliokuwa nao kwa miaka elfu hamsini alioishi.
Wakati Aoiline na urembo wake akicheka , kitu cha ajabu kilionekana kutoka katika kile kioo kwa awamu nyingine.
Ni kitu katika umbo la binadamu hali ya kinishati ya mwanga ambalo ni kama vile umbo lile limeshikiliwa na ule mwanga wa rangi saba unaotoka katika kile kioo.
Mwanzoni umbo lile halikuonekana vizuri kiasi cha kufanya iwe ni kama kiumbe cha ajabu lakini kadri ambavyo mwanga ule ulivyokuwa ukiungana na lile umbo ndio muonekano wake ulivyozidi kudhihirika.
Hatimae waliokuwa wakiangalia waliweza kutambua ni nafsi ya Roma ilioshikiliwa na kile kioo.
Kila mtu alijua nafsi ya Roma imekwisha kupotea mara baada ya kuachana na mwili lakini maajabu yake ni kwamba ilionekana ilinasa katika hicho kioo kama sio kushikiliwa.
“Katika vitabu vyetu inasemekana kwamba kioo cha nafsi kina uwezo wa kusafiri kupita katika ombwe kwenda anga za mbali na kurudisha muda nyuma na nafasi , hivyo inaonekana
mara baada ya kumtambua Roma kama Master wake, kilizuia muda na nafasi kwa nafsi ya Roma isiondoke duniani”Aliongea Aoiline.
Maneno yake yalitokana na vile walivyojifunza , majini walikuwa na siri nyingi sana kuhusu ulimwengu wa anga za mbali na maajabu ya dunia , sasa kile ambacho amesoma ndio kilichokuwa kikitokea katika macho yake.
Dakika ileile ni kama vile ule mwanga wa rangi saba ulikuwa ni lift kwani uliishusha nafsi ya
Roma mpaka kwenye maiti yake taratibu sana.
Kitendo cha kuamka kwa nafsi katika mwili wake na Andiko la urejesho palepale lilianza kufanya kazi yake ya kimiujjiza.
Awamu hio kila kitu kilienda vizuri kwani Roma sio kwamba alikuwa akizuia Andiko la urejesho wa Azimio usifanye kazi.
Muda uleule upepo ulianza kuongezeka katika eneo ambalo Roma mwili wake umelala na nguvu ya kiroho ilitawala kwa kiasi kikubwa na damu ambayo imeshaganda ilipata moto kwa mara nyigine na nishati za mbingu na ardhi iliamka kwa kasi kubwa na kufanya senta ya mwili wake kutuna na kusinyaa kama vile ni jipu.
Dakika chache eneo la kifua chake paliziba kabisa huku ikionekana moyo wake kupona na kuanza kudunda kwa mara nyingine chini ya nguvu ya kimaajabu ya kutisha ya Andiko la Urejesho wa Azimio.
Edna aliishia kuduwaa akiangalia kile kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake , hakupepesa macho hata kidogo akiogopa alichokuwa akiangalia kitatoweka na kubakia kuwa ndoto.
Ukweli ni kwamba hakuthubutu hata kupiga kelele na aliishia kuziba mdomo wake na mkono , huku machozi yakiendelea kumtoka mfufulizo, huku uso wake wa kirembo ukiwa mwekundu kama yai , hakuthubutu kuonyesha furaha yake kwa makelele.
Wakati kila mmoja akiwa katika hali hio ya kushangaa hatimae Roma aliweza kupona kabisa na hakuonekana tena kama maiti bali kama mtu alielala usingizini.
Kifua chake na tumbo lake vilipanda na kushuka ikionyesha amerudiwa na pumzi na hatimae aliyafumbua macho yake.
Kana kwamba alikuwa katika hali ya furaha mara baada ya sura ya kwanza kuiona akifumbua macho ni Edna alinyanyua mkono wake na kumfuta Edna machozi.
“Hehe.. Babe wife , usiwe na hasira hivi , sio kama nilikuwa nikifanya utani kwa kujifanyisha kufa , kidogo tu nipoteze uhai moja kwa moja awamu hii”
Edna hatimae hakutaka kuzuia tena hisia zake na kwa haraka sana alimnyanyua Roma kwa nguvu zake zote na kumsimamisha na kisha alipitisha mikono yake katika shingo na kuanza kuangua kilio akijilaza kifuani.
Kwa wakati huo , akili yake haikufanya kazi , hakuweza kuelezea namna gani anajisikia zaidi ya kutoa kilio cha furaha.
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

ILIPOISHIA
Kila mtu alijua nafsi ya Roma imekwisha kupotea mara baada ya kuachana na mwili lakini maajabu yake ni kwamba ilionekana ilinasa katika hicho kioo kama sio kushikiliwa.
“Katika vitabu vyetu inasemekana kwamba kioo cha nafsi kina uwezo wa kusafiri kupita katika ombwe kwenda anga za mbali na kurudisha muda nyuma na nafasi , hivyo inaonekana mara baada ya kumtambua Roma kama Master wake, kilizuia muda na nafasi kwa nafsi ya Roma isiondoke duniani”Aliongea Aoiline.
Maneno yake yalitokana na vile walivyojifunza , majini walikuwa na siri nyingi sana kuhusu ulimwengu wa anga za mbali na maajabu ya dunia , sasa kile ambacho amesoma ndio kilichokuwa kikitokea katika macho yake.
Dakika ileile ni kama vile ule mwanga wa rangi saba ulikuwa ni lift kwani uliishusha nafsi ya
Roma mpaka kwenye maiti yake taratibu sana.
Kitendo cha kuamka kwa nafsi katika mwili wake na Andiko la urejesho palepale lilianza kufanya kazi yake ya kimiujjiza.
Awamu hio kila kitu kilienda vizuri kwani Roma sio kwamba alikuwa akizuia Andiko la urejesho wa Azimio usifanye kazi.
Muda uleule upepo ulianza kuongezeka katika eneo ambalo Roma mwili wake umelala na nguvu ya kiroho ilitawala kwa kiasi kikubwa na damu ambayo imeshaganda ilipata moto kwa mara nyigine na nishati za mbingu na ardhi iliamka kwa kasi kubwa na kufanya senta ya mwili wake kutuna na kusinyaa kama vile ni jipu.
Dakika chache eneo la kifua chake paliziba kabisa huku ikionekana moyo wake kupona na kuanza kudunda kwa mara nyingine chini ya nguvu ya kimaajabu ya kutisha ya Andiko la Urejesho wa Azimio.
Edna aliishia kuduwaa akiangalia kile kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake , hakupepesa macho hata kidogo akiogopa alichokuwa akiangalia kitatoweka na kubakia kuwa ndoto.
Ukweli ni kwamba hakuthubutu hata kupiga kelele na aliishia kuziba mdomo wake na mkono , huku machozi yakiendelea kumtoka mfufulizo, huku uso wake wa kirembo ukiwa mwekundu kama yai , hakuthubutu kuonyesha furaha yake kwa makelele.
Wakati kila mmoja akiwa katika hali hio ya kushangaa hatimae Roma aliweza kupona kabisa na hakuonekana tena kama maiti bali kama mtu alielala usingizini.
Kifua chake na tumbo lake vilipanda na kushuka ikionyesha amerudiwa na pumzi na hatimae aliyafumbua macho yake.
Kana kwamba alikuwa katika hali ya furaha mara baada ya sura ya kwanza kuiona akifumbua macho ni Edna alinyanyua mkono wake na kumfuta Edna machozi.
“Hehe.. Babe wife , usiwe na hasira hivi , sio kama nilikuwa nikifanya utani kwa kujifanyisha kufa , kidogo tu nipoteze uhai moja kwa moja awamu hii”
Edna hatimae hakutaka kuzuia tena hisia zake na kwa haraka sana alimnyanyua Roma kwa nguvu zake zote na kumsimamisha na kisha alipitisha mikono yake katika shingo na kuanza kuangua kilio akijilaza kifuani.
Kwa wakati huo , akili yake haikufanya kazi , hakuweza kuelezea namna gani anajisikia zaidi ya kutoa kilio cha furaha.

SEHEMU YA 798
Muonekano wa Roma kwa upande wake ulikuwa ni ule ulionekana kuwa na mawazo kidogo, aliishia kuinua mdomo wake juu kama mtu ambae amekosa pumzi.
“Okey , Okey … Edna Darling , najua unafuraha .. lakini imekuwaje ukawa na nguvu nyingi kiasi hichi ?Ouch .. nashindwa kupumua..”
Roma alikuwa hajui acheke ama alie kwani Edna alikuwa amemkaba mno shingo yake kama kwamba anataka kumnyonga , hivyo kumfanya kushindwa kupumua vizuri.
Kwa bahati nzuri hakuwa hatarini kiafya , alijiambia kama angerudi kuwa hai na kisha kunyongwa na mke wake kutokana na kumbatio angejisikia vibaya sana.
Edna hatimae alimuachia huku macho yake yakiwa na machozi , aliishia kupiga mapaja yake huku akiendelea kulia kwa kwikwi akikosa hata ujasiri wa kumgusa Roma tena.
“Bado tu unapenda kunichezea , kwanini unapenda kucheza na akili yangu , nani kakuambia ujiue , wewe ni mtu mbaya sana .. kwanini ulitaka kumtelekeza mtoto wetu na kuondoka mwenyewe….”
Edna alishindwa kabisa kujizuia kuacha kulia , ule ukauzu wake wote ulikuwa umeshampotea na kwa wakati huo alikuwa mwepesi kihisia kama ua ambalo litadondoka na kunyauka muda wowote.
Roma alichoweza kufanya ni kuishia kumkumbatia na kumpiga piga mgongo wake kwa namna ya kumtuliza , kulikuwa na dalili za kukosa cha kufanya muda huo kutuliza hali aliokuwa nayo mke wake lakini hata hivyo alikuwa na furaha kuona namna ambavyo mke wake alikuwa akimpenda.
Tukio hilo liliwafanya Aphrodite na Artemis kutoa machozi , ilikuwa ni kama vile jua limepotea milele na vilevile hakukuwa na baridi kwa wakati mmoja.
Hatimae Roma aliweza kumfanya Edna kuacha kulia na kukigeukia kioo ambacho bado tu kilikuwa kikielea Angani.
Kioo hicho na nafsi mara baada ya kupungiwa mkono na Roma kiliacha kuendelea kutoa ile miale ya rangi na kurudi katika ukubwa wa kawaida na kisha kilidondoka kutoka juu na kwenda kutua katika mikono ya Roma.
Kila mtu aliekuwa katika eneo hilo alimwangalia Roma akifanya mambo hayo yote , kwao kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni miujiza ,walikuwa wakijiuliza inakuwaje kioo cha namna hio kufanya miujiza kuurudisha uhai wa Roma.
Baada ya Edna kufuta machozi hatimae na yeye alikodolea macho kioo hicho ambacho kilikuwa katika mikono ya mume wake kwa macho ya shukrani.
Ni kama alikuwa akitaka kusema asante kioo kwa kumrudisha mume wangu hai.
“Hey ,Asante kwa msaada wako Lumiel, nadhani tutakuwa marafiki wazuri kuanzia sasa na baadae , umeyaokoa maisha yangu hivyo nitahakikisha unaishi maisha mazuri , sitokufanyia ubaya na urafiki wetu utadumu katika wema, sawa?”
“Lumiel?!”
Kila mtu aliekuwa hapo akiwemo Sharif walikuwa na muoneknao usio kuwa wa kawaida mara baada ya kusikia kioo hicho kikiitwa na Roma jina la Lumiel.
Kioo kile kilionekana kuelewa maneno ya Roma kwani kilitoa miale yote saba kwa namna ya kuitikia na kumfanya Roma kucheka.
“Haha.. jina linaweza kuwa sio zuri kimatamshi lakini libebeba maana kubwa , Nuru ya mkuu wa Enzi. Ila kwanzia sasa nitafupisha jina lako na kukuita Lumi, unaonaje juu ya jina hili?” Roma alikuwa akiongea na kile kioo na baada ya kuuliza hilo swali kilitoa mwangaza tena.
Watu wote walishikwa na butwaa kwa namna ambavyo Roma alikuwa akiwasiliana na kioo hicho , katika mazingira ya kawaida ilikuwa ni kama vile mtu anawasiliana na Roboti ambalo linatumia akili mnamba(AI) .
“Hubby inamaana hiki kioo kina kuelewa unachoongea ?”Aliuliza Edma ambae alikuwa na shauku kubwa , hata kama alikuwa tayari na maarifa yote ya Athena katika akili yake , hakuwa akijua kioo hicho kilikuwa ni nini.
Lilikuwa swali ambalo hata Sharif na Aoiline pia walikuwa nalo na waliishia kumwangalia Roma ili kusikia jibu lake.
“Dahh .. nimejikuta nikiwa bize na rafiki yangu Lumi na kusahau kilichotokea..”Aliongea Roma kwa kujipiga paji la uso kama vile kuna kitu amesahau na palepale ndipo alipoanza kuelezea kila kitu.
Kumbe hata kwa Roma mwenyewe alijua tayari amekwisha kufa lakini mara baada ya nafsi yake kutoka Roma alijihisi ni kama vile yupo ndotoni , kwani alijikuta akiwa katika ulimwengu mwingine ambao ni kama vile Kioo hicho cha nafsi ni mlango wa kuingilia na kutoka.
Ulimwengu huo aliokuwepo ni ule wa nafsi , yaani kwa lugha nyepesi ni kama vile alikuwa katika ulimwengu ambao nafsi huhifadhiwa baada ya kifo kwa kukusanywa na kioo hicho.
Sasa mara baada ya kufika katika ulimwengu huo ambao ni kama haukua na ardhi yaani chini ni anga na juu ni anga alisikia sauti ikisemezana nae na iligeuka ni nafsi hio ya Dhana hio ya mkuu wa Enzi ndio iliokuwa ikimuongelesha.
Nafsi hio ilimwambia kwamba imepata ruhusa kutoka kwa mmiliki wake wa awali kumtambua yeye kama Master wake na msaidizi mkuu kwanzia sekunde moja katika mazingira ya sayari ya dunia , yaani ulimwengu wa binadamu na hio ndio sababu ambayo kioo hicho cha nafsi kirudisha nafsi ya Roma na kuurejsha uhai wake kwa ajili ya kumtambua.
Sababu kuu ya kupata ruhusa ya kioo hicho kumtambua Roma ni kutokana na kwamba alifikia upeo mwingine ambao ndio kiumbe pekee kutoka duniani aliefikia upeo huo juu ya siri za ulimwengu.
Lakini hata hivyo kama Roma asingekuwa na kioo hicho tokea mwanzo kutoka katika Jicho la anga angekuwa amekufa kweli hata kama ameweza kufikia katika upeo huo .
Sasa kutokana na uwezo wa Roma kioo hicho ambacho kilikuwa katika mikono ya Roma kiliamua kuomba ruhusa kumtambua Roma kama Master wake na msaidizi.
Sasa ilionekana ni kama kulikuwa na maelezo mengi sana juu ya kioo hicho kwanzia kwa mtu alieomba ruhusa lakini kwa upande wa Roma hakuwa na kingine zaidi cha kuelezea kwani nafsi ya kioo hicho haijamwambia bado.
Sasa Roma aliona kila kitu kilichotokea mara baada ya kifo chake wakati akiwa katika miliki ya kioo cha nafsi , mwanzoni alitaka kutoka mapema na kurudi lakini nafsi ya kioo hicho ilikuwa na maelezo mengi ya kumwambia hususani uwezo halisi wa kioo hicho ukiachana na kushikilia nafsi.
Kila mmoja aliesikia alijikuta akishangazwa na jambo hilo , kwani kioo hicho kilionekana kuwa na uwezo wa maajabu mno.
“Nadhani sijakosea kabisa kuweka matumaini yangu makubwa kwako tokea mwanzo , hatimae umenifanya nijivunie , unaiisikiaje kufikia katika huo upeo?”Aliuliza Aoiline.
“Nimeelewa kwa namna flani tu hivi kwa msaada wa Dhiki ya mapigo Elfu kumi ya radi , vingineyo ingekuwa ni ngumu sana kuja kufikia katika huu ufunuo nilio nao sasa”
“Upeo na ufunuo gani , mbona mnaongea kimafumbo mafumbo?”Aliuliza Edna ambae alionekan kukunja sura , huku akionekana kutopenda namna ambavyo Aoiline alikuwa akimwangalia Roma kwa macho ya matamanio huku akiongea vitu ambavyo haelewi.
“Ninachomaanisha ni kwamba , ufunuo ambao mwanzoni nilikuwa nao kikomo chake ilikuwa ni katika mazingira ya dunnia pekee , upeo wako ukishatoka katika mazingira ya dunia au Parrallel Space ni kitu kingine kabisa , kwa mfano moja ya upeo ambao nimepata ni Maada giza(Dark Matter) kuwa asili halisi ya ulimwengu wote, uelewa huu umenileta karibu zaidi na ufunuo wa kihisia usioelezeka ambao ni wa ki-Cosmic zaidi , unaweza kuita ufunuo wa anga za mbali wa kinishati”
Roma aliongea kwa kutumia fasihi zaidi , ilikuwa ni kama kuna kitu anajaribu kuficha na kuwafanya waliokuwa wakimsikiliza wasielewe kabisa.
Lakini hata hivyo kuna kitu kimoja ambacho miungu waliweza kuelewa , ukweli wa kwamba Roma alikuwa na uwezo wa kubatilisha kanuni zote za anga kwa kuwa tu na uwezo wa kudhibiti radi nyeusi ambayo ilikuwa na mchanganyiko wa maada nyeusi , kwao lilikuwa jambo la kushangaza.
Radi nyeusi ilikuwa na nguvu ambayo yenyewe ilitokana na mchangyaiko wa radi kama radi na maada nyeusi , sasa ukija katika uhalisia wa Maada nyeusi , ni aina ya njia ambayo humfanya mtu kuona zaidi.
Yaani kwa lugha nyepsi ni sawa na watu wote mue katika chumba chenye giza lakini Roma peke yake ndio mwenye uwezo wa kuona kila mtu aliekuwa ndani katika chumba hicho bila kutumia mwanga , hio sio kwasasababu alikuwa na nguvu za kimaajabu lakini ni kwasababu alikuwa na uwelewa wa namna giza linavyokuwa na asili yake.
Sasa unachopaswa kuelewa kuvuna nishati ya mbingu na ardhi kupitia mbinu ya andiko la urejesho ni kama njia, ni sawa na muumini wa dini yoyote anaambiwa ukitenda mema na kushika sheria zote za dini utafikia uzimani au Akhera.
Sasa basi kama Radi ya mapigo elfu moja ndio mwisho kabisa wa safari ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi kinachofuata kuanzia hapo ni hatua ya kwanza ya ufunuo mkuu , sasa hapa ndio kina kuja kitu kama sehemu ya kwanza ya ufunuo , sehemu ya pili ya ufunuo mkuu na sehemu ya tatu ya ufunuo mkubwa.
Roma alikuwa katika sehemu ya pili ya ufunuo mkuu huku upande wa Sharifu yeye alikuwa katika sehemu ya kwanza ya ufunuo mkuu. “Inaonekana ni mimi ambae sikuweza kuiona nuru mapema , kuna ufunuo wa aina tofauti tofauti katika upeo wa kidunia na ufunuo huo wote humpeleka mtu katika mwisho mmoja ambao ni ufunuo wa Anga , ni kitu ambacho sikukukielewa mapema lakini huo ndio ukweli”Aliongea Sharif,
“Sasa hivi tayari Roma amekidhi vigezo na anaweza kushika majukumu yako kwanini usiwe na furaha , angalau unaweza kuondoka duniani na kuiendea njia nyingine”Aliongea Aoiline.

Sharif alijua mbweha huyo alikuwa akimtania lakini hata yeye pia alikuwa amefikiria mambo mengi , ukweli wa kwamba Roma alikuwa ameweza kufikia upeo huo kupitia njia ya upendo na kifo ilimfanya kuelewa mambo mengi , kitu ambacho ni kama alielimika.
“Umeshinda , sipo vizuri sana kama wewe lakini pia nataka kukushukuru , kwanzia sasa nadhani
ni muda wangu wa kuondoka kwa amani”Aliongea Sharif.
“Kama unataka kuondoka unaweza kuondoka lakini kabla ya yote hakikisha unarekebisha ulinzi wa gereza la roho na kusafisha hali ambayo umeisababisha mwenyewe , haya yote yametokana na mipango yako hivyo sitaki kukusaidia kurekebisha makosa uliofanya”
Sharif alijikuta akikosa cha kufanya na kujiambia huyu mtoto hakuwa tena akimuogopa kama mwanzo kwasababu muda huo ni kama wanalingana ki uwezo na ukiburi umeongezeka mara mbili kiasi kwamba anaanza kumpa maagizo.
“Nitarekebisha Gereza la Roho , sio kazi ngumu hata hivyo lakini hayo mapepo yanahitaji watu kuyakamata na kuyaharibu , hivyo siwezi kudili nayo moja baada ya lingine , kuhusu athari zilizopita dunia na joto kushuka sana ….”Aliwageukia miungu na kisha akatoa tabasamu.
“Nitamwalika mtu mmoja ambae anaweza kurudisha nguvu ya uhai wa dunia haraka iwezekanayo”.
Kauli hio ni kama iliwafumbua akili miungu na kujua alichokuwa akimaanisha.
“Dionysus!, Unafahamu Dionysus alipo ?”Aliuliza Hera ambae alikuwa na shauku ya kusikia jibu.
“Ni nani huyo sus’..”Aoiline aliuliza akishindwa kutamka jina.
“Ni Dionysus moja ya miungu kumi na mbili waliofanikiwa kuhamisha nafsi zao wakati ule , huyu mwenzao hapendi kabisa kupigana na anapendelea amani , hivyo siku zote alikuwa ni mwenye kujificha , lakini uungu wake una uwezo wa kipekee unaofahamika kama; ‘Uzao mpya’ , pia ana vitu viwili mno vya kuvutia , cha kwanza ni Ngozi ya Mbweha ambayo huvaa , ngozi ambayo ina uwezo wa kimaajabu wa kuotesha mimea na kingine ni Kikombe cha Divai ambacho kina uwezo wa kugeuza maji yote kuwa divai ya uhai na pale inapomwagikia mimea hukua kwa haraka sana , muda ambao atatoka , haitochukua muda mrefu kwa mimea yote kurudi katika hali ya kawaida na kutokana na dunia kuendelea kupata joto basi kila kitu kitarudi kama ilivyokuwa mwanzo”
“Sina haja sana na hicho kikombe cha Divai , lakini hio ngozi ya Mbweha, ikitokea nikiiona ninamuua”Aliongea Aoiline.
Miungu hao walijikuta wakipatwa na wasiwasi , lakini kwa Roma na Edna walijua fika Aoiline alikuwa mbweha hivyo lazima afurahiswe na kusikia ngozi ya mbweha.
“Wapi Dionysus amejificha ?, nimemtafuta kote bila ya mafanikio?”Aliuliza Edna ambae ni kama Athena anaeuliza.
“Roma na Aoiline mnamjua fik..”Aliongea Sharif.
“Sisi ?, nimeishi miaka elfu hamsini ndani ya ulimwengu wa majini pepo namjulia wapi mim..”
“Ndio kiongozi wa majini pepo mashetani wa anga katika miliki ya msitu wa mianzi Zambarau , jina lake ni Master Zao”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.
“Kumbe ni yeye , imekuwaje sijawahi kuona kitu cha tofauti kutoka kwake?”
“Uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi sio mdogo , hivyo haikuwa ngumu kwake kuficha uungu wake “Aliongea na kisha akamwangalia Edna.
“Kuhusu unabii wa Athena hawezi kufika katika ulimwengu wa majini pepo , lakini ukiachana na hivyo Zao aliamua kujificha yeye mwenyewe hivyo ingekuwa ngumu kumjua , hata mimi mwenyewe nisingempata kama nisingekuwa nawafatilia ninyi wote”
Roma aliona Master Zao alikuwa ni mwigizaji mzuri sana , alimfahamu fika kwani ndio aliekuwa rafiki wa Master wake Tang Chi na kulingana na wote kufanana tabia ndio maana wakawa marafiki wakubwa.
Hata kipindi kile cha shindano la kuingia mnarani mara baada ya kumuona Aoiline , alijifanyisha kuwa muoga kumbe yote ilikuwa ni maigizo tu ya kutotaka kugundulika ili mradi aendeee kujificha.
Lakini sasa kwa vyovyote vile vita imeshaisha na miungu walikuwa tayari kupotezea kila kitu na kuianza siku mpya wakiwa pamoja na binadamu.
Roma alikumbuka vyema Sharif alikuwa amemfcha Clark , hivyo alimwamrisha kumrudisha na kwa Sharif asingeendelea kumshikilia Clark hivyo aliahidi atarudishwa kisiwani.
Hatimae Roma aliridhika na matokeo yote na kisha alimshika mkono mke wake na kumkonyeza.
“Wife ni muda wa kruudi nyumbani sasa”Aliongea na kumfanya Edna atoe tabasamu lake tamu na kutingisha kichwa kukubali.
Dakika hio hio kama ilivyokuwa kwa Sharif na Aoiline walivyofika katika eneo hilo ndio namna ambavyo Roma na Edna walipotea mara baadaa ya anga kutengeneza shimo na kutumbukia.
Upande wa miungu waliuchukua Moyo wa Gaia na kuurudisha kama mwanzo ulivyokuwa chini ya miliki ya familia ya Yezi kule Korea na kisha wakampatia Poseidon kwa ajili ya kuuhifadhi.
Kisha wote kwa pamoja waliangaliana kwa kutabasamu kuoneysha hali za ahueni katika macho yao, ilikuwa ni wakati wa kufikiria upya maisha yao yajayo katika mazingira ya dunia.
Amani hatimae ikarudi.
Aoiline na Sharif walipaa mpaka juu angani zaidi na kuiangalia dunia kwa chini huku wakijaribu kuhisi joto la jua ambalo ni kama sasa limerudi katika ubora wake huku wakijaribu kuyawazia matendo yao yote na uzoefu wote waliopitia kwa miaka mingi ya hapa duniani.
“Aoiline , unadhani nini kimesababisha huyu mtoto kunipita na kushinda?”Aliuliza Sharif akionekana kama vile ni mwenye hali ya mkanganyiko ni kama hakuwa akiamini Roma ameweza kumpita ki upeo na kuwa chini yake.
“Au ni kwasababu sina elimu kubwa kuliko yeye
, haiwezekani anishinde ili hali ni mimi niliorahisisha mbinu ya Andiko la urejesho , au ni kwasababu ilipangwa , au ni kile kioo au nini , mbona nashindwa kuelewa?”
Aoiline alijikuta akimwangalia Sharif ambae alionekana kuchangayikiwa , kwa muda huo alimuona mwanaume huyo ni kama amerudi katika wakati ule ambao ndio kwanza anakutana nae.
“Ukweli ni kwamba kwa mtazamo wangu , ambae ameshinda sio Roma , sio hatiima yake au kioo cha nafsi au wewe..”
“Kama ni hivyo ni nani ameshinda?”Aliuliza kwa mshangao kidogo.
Alinyoosha mkono wake na kisha kuchukuwa wa Sharif na kisha kupitisha vidole vyao kwa namna ya kuunganisha.
“Its love!”
Alijibu akisema ni mapenzi au upendo ndio ambao ameshinda na kisha wawili hao wakiwa wameshikana mikono waliangaliana kwa tabasamu na kisha wakapotea pamoja.
******
TEN YEARS LATER (MIAKA KUMI BAADAE).
Ni katika ulimwengu wa majini pepo , ulimwengu ambao ki asili hujulikana kama ulimwengu wa majini pepo wa milenia.
Sasa katika miliki ya msitu wa mianzi zambarau upepo ulikuwa ukivuma na kutengeneza sauti kama ya wimbo na harufu yake kuvutia pua kwa wale waliokuwa wakiivuta.
Hali hio ya upepo ilichangayika na harufu nzuri ya mvinyo uliokuwa umejaa kilevi cha hali ya juu.
“Nimeshinda , Haha, Braza Chi , inaonekana hii
pombe ya kijani ni ya kwangu kwa ajili ya kunywa”
Wanaume wawili walionekana wakicheza mchezo wa Chess juu ya jiwe huku mshindi alikuwa akijipatia kikombe cha mvinyo wa kijani.
Watu hao walikuwa ni Master Chi na Master Zao ambae sasa jina lake lingine ni Dyonysus mungu wa divai.
Katika miezi kadhaa walikuwa na utaratibu wa kucheza michezo mbalimbali ile ambayo Zao alikuwa akiijua na ambayo Chi alimfundisha
Zao , katika mchezo ambao Zao hakuujua ni wa Chess na baada ya kufundishwa kwa muda alionekana kuelewa na hatimae kwa mara ya kwanza aliweza kumshinda Master Chi.
Sasa kwasababu ambazo hazikuwa zikielezeka , siku hio Master Chi alijikuta kila mchezo ambao alijaribu kucheza na Zao alifungwa na kunywa pombe yote iliokuwa na thamani kubwa.
Sasa kikombe cha mvinyo wa kijani ndio pekee ambacho kilikuwa kimebakia na mara baada ya kuona Zao anakaribia kukipeleka mdomoni alimzuia.
“Hey , hebu tulia kwanza”
“Ah , Braza Chi ndio kwamba hutaki kukubali kushindwa”Aliongea Zao ambae kwa wasiwasi alirudisha kile kikombe chini.
“Braza Zao huu mvinyo wa kijani ni zawadi nilioletewa na mjukuu wangu Lanlan alipokuja kunitembelea mwezi uliopita , ukinywa wote nitakuwa sijauonja hata kidogo , nakubali kushindwa lakini nikikuacha uumalizie nitaenda kinyume na nia yake nzuri kwangu , unaonaje kama nikikupatia aina nyingine ya pombe kufidia hii?”
“Unataka kunipa ile tuliozoea , kama naitaka si bora nitengeneze mwenyewe”
“Unatoa wapi ujasiri wa kunikumbusha hili swala , umekuwa ukinificha kwa muda mrefu kumbe muda wote ulikuwa mungu wa mvinyo , hapana huwezi kunywa huu mvinyo tena”Aliongea Master Chi kwa hasira.
“Acha zako hizo Braza basi , si miaka kumi imepita mpaka tumalize hili swala , inakuwaje bado una kinyongo tu ..”
Miaka kumi iliopita , Sharif alifika katika ulimwengu wa majini pepo na kumchukua Dyonysus kwa ajili ya kurudisha hali ya kimaisha katika sayari ya dunia na hapo ndipo Master Chi alifahamu rafiki yake ni sehemu ya miungu.
Sasa kilichomkasirisha Tang chi ni kwamba siku zote alijiona yeye ndio yupo vizuri kwenye kutengeneza mvinyo lakini matokeo yake Zao ndio alikuwa bingwa .
Kwa mwaka mzima Dyonyus alitumia Dhana zake katika kuifanya Biosphere ya dunia kurudi katika hali yake ya kawaida na baada ya hapo ndipo aliporudi ulimwengu huo wa majini pepo na kuendelea kunywa kujigalagaza na rafiki yake Master Chi.
Wote wawili walikuwa wakifanana tabia hawakutaka kufanya chochote zaidi ya kulewa.
Dakika hio hio wakati wakiendelea kulumbana juu ya kikombe cha pombe, kulikonekana kitu kikubwa umbo la koni cha rangi ya silver kikipaa kuja eneo hilo la msitu wa mianzi ya Zambarau kwa spidi kubwa sana.
Muoneknao wa kifaa hicho ilikuwa ni kama vile ni kisahani hasa kwa spidi yake na kufumba na kufumbua kilishafika katika mazingira ya wale wazee walipo na kilitoa mwanga mkali kutoka eneo la chini na kuanza kushuka taratibu katika mstari mnyoofu(Vertical line) na eneo la juu lilibadilika rangi kutoka silver na kuwa kama kioo na kisha mlango wake ukafunguka.
Msichana mmoja mrembo sana wa ajabu alishuka kutoka kwenye kifaa hicho na kukanyaga chini , alikuwa ni makadirio ya miaka kumi na moja au kumi na tatu hivi.
Alikuwa na mashavu yalionona , huku akiwa amevalia Tshirt ya bluu , Denim Short(Kaptura fupi hivi kama jeans) na Sneaker za rangi ya bluu , yalikuwa ni mavazi yalio jaa ujana ule wa kisasa zaidi na kilichomfanya kupendeza zaidi ni namna shepu yake ilivyokuwa ikianza kuchepua kwa kasi.
Sekunde ambayo Master Chi alimuona msichana huyo mrembo alimpotezea kabisa Zao na kutoa tabasamu la furaha huku akisimama.
“Are you here to visit me again , Lanlan?”Aliongea Master Chi huku akiwa ameipanua mikono yake.
Msichana huyo ambae alikuwa akivutia sana hakuwa mwingine ni Lanlan ambae alikuwa amekwisha kukua na kurithi uzuri wote wa mama yake na zaidi ya kumpita kabisa, jina lake kamili ni Lanlan Roma Ramoni Kweka.
Ukizungumzia uzuri wa Lanlan ni sawa na kusema amerithi kutoka kwa Edna au Seventeen lakini hata hivyo pengine ni mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi yamemfanya kuwa tofauti sana , alikuwa na nywele ndefu mno kama vile ni mzungu na uso wake ulituna kidogo na kumfanya kupendeza zaidi.
Ijapokuwa hakuwa m’cute kama alivyokuwa mdogo lakini alikuwa ni pisi kali na classic , shukrani zimwendee Edna kwa malezi mazuri.
“Grandpa!”
Lanlan alitabasamu huku akimkimbilia babu yake na kwenda kukumbatia kwa nguvu.
“Grandpa are you gambling with Mr Drunkard?”Aliuliza akimaanisha anacheza kamari na Mr mlevi.
“Hehe, ndio tena ninatia huruma maana nimekuwa nikipoteza sana kila mchezo , Lanlan , umekuja na mvinyo mwingine leo?”Aliuliza Master Chi kwa furaha.
“Naona nimeshakuwa chupa ya mvinyo katika macho yako siku hizi?”Aliongea Lanlan lakini licha ya kuongea hivyo alichezesha mkono wake na palepale alitoa chupa za mvinyo kutoka hifadhi ya pete na kumuwekea katika meza.
“Nimemuibia baba hizi chupa za Dalmore kutoka katika hifadhi yake , nimesikia kutoka kwa babu Ron ni ghali mno zaidi ya paundi elfu kumi kwa chupa moja , Babu hakikisha ukimaliza unaficha chupa Dady asije kuziona , akiona lazima atanisemea kwa mama tena”Aliongea huku akimtingisha Master Chi mkono wake.
Wanaume hao wawili waliitikia haraka haraka kama vile wanataka kunywa haraka kilevi hicho.
Baada ya kukagua chupa hizo huku wakimsifia Lanlan kwa kuleta zawadi hio nzuri hatimae walitaka kujua kilichomleta, kwani ni mwezi uliopita tu alikuwa amekuja kutembea hivyo ni lazima alikuwa na ujumbe.
“Lanlan kuna kingine umekuja nacho?”Aliuliza MasterChi.
“Mr Mlevi leo nimekuja hapa kwa ajili yako ,
Mommy ameniambia nikufikishie taarifa Auntie
Clark na Sis Naira wameshamaliza kujenga Spaceship kwa ajili yenu , iwe unataka kubaki duniani au kuondoka ni juu yako lakini unapaswa kukutana na wenzako kwanza”Aliongea Lanlan.
“Mbona mapema hivyo?, sitaki kuondoka hapa duniani mapema hivi , lakini nadhani napaswa kuwaaga , lini wanatarajia kuondoka”
“Tunaweza kuondoka wote sasa hivi , unachopaswa ni kumrukia Kibonge wangu na tuondoke”Aliongea akinyooshea kijindege chake alichokuja nacho.
Ndege hio ilikuwa ni teknolojia mpya ya Ant- Gravity ambayo ilivumbuliwa na Clark miaka saba iliopita , spidi yake ilikuwa ni kubwa mnno na ilikuwa na uwezo wa kusafiri kuingia katika ulimwengu wa majini pepo na wa binadamu.
Sasa kutokana na ulimwengu huo kutokuwa na anga la kawaida usafiri wa aina hio ulihitajika.
Sasa kindege hicho kilijengwa maalumu kwa mtu mmoja moja na spidi yake kutokana na ukubwa ilihitaji angalu nishati za mbingu na ardhi kukidhibiti.
Sasa kutokana na kwamba akiwa mdogo wengi walikuwa wakimwita kibonge aliamua kuiita kindege chake hicho Chubi yaani kibonge.
Master Zao hakuwa na pingamizi na alitaka rafiki yake Master Chi kumsindikiza , hivyo wote watatu walipanda katika ndege hio ya Lanlan na kisha wakaondoka kuelekea ulimwengu wa binadamu.
Miaka kumi iliopita Aoiline na Sharif waliondoka pamoja , safari yao ilikuwa ni kutaka kuzijua zaidi siri za anga za mbali na kwanzia hapo ni kama kila kitu katika dunia kilikuwa chini ya Roma,
Kitu cha kwanza alichofanya mara baada ya kuwa Mwangalizi ilikuwa ni kuondoa ngoma katika mnara wa anga na kuwaruhusu majini pepo ambao walikuwa wakiishi katika ulimwengu wa majini pepo kuwa na uwezo wa kusaifiri kutoka na kurudi katika ulimwengu huo.
Binadamu walikuwa washajua tayari hawakuwa peke yao kama watawala wa dunia bali kulikuwa na viumbe wengine kama vile majini wa jamii zote tatu hivyo hawakuwa na woga tena.
Roma aliwaambia pia kulikuwa na viumbe wegine kutoka sayari ya Mars waliwahi kupata kufika duiani ambao hujiita miungu kama walivyosimuliwa katika hadithi za wagiriki na kwa mara ya kwanza dunia ilijua kwanini kulikuwa na uwepo wa hadithi hizo kumbe yote hayakutokea duniani bali ni sayari nyingine.
Sababu ya Roma kuwafanya binadamu kujua juu ya uwepo wa viumbe wengine ilikuwa ni kuwaandaa kisaikolojia kwa kuwambia kama hawatochukua hatua basi wataishia kuwa chini ya viumbe wengine,waliopo na ambao wanaweza kufika.
Alijua kama wataelewa muda wowote wanaweza kukumbwa na janga kama ambalo lilitaka kuwatokea basi watapiga hatua ya kujua namna ya kujilinda.
Chini ya utawala wa dunia wa Roma hakuna jini wala kiumbe chochote kilichotuhubutu kuleta fujo katika ulimwengu wa binadamu na hio ni kutokana na kwamba kulikuwa na sheria maalumu katika kila mpaka kati ya ulimwengu na ulimwengu.
Majjini pepo walibakia katika miliki yao ya kijini pepo lakini walikuwa na uwezo wa kufika katika ulimwengu wa binadamu , hivyo hivyo kwa binadamu walikuwa na uwezo pia wa kufika katika ulimwengu wa majini pepo na ikawa hivyo kwa majini watu.
Miliki za Hongmeng , Xia , Panas na Kekexil zilijengwa upya, majini waliokuwa wakiishi katika ulimwengu wa jangwa tenganifu na wenyewe walipewa ruhusa ya kutembelea katika ulimwengu wa majini watu , na binadamu.
Ndani ya muda mfupi ulimwengu wa binadamu ulibadilika mno na hatua za kimaendeleo ziliongezeka kwa kasi mno kuliko ilivyokuwa mwanzo,majini walikuwa na siri nyingi na siri hizo walishirikiana na binadamu na kufanya uelewa wa binadamu kuongezeka kwa haraka.
Hakukuwa na siri tena juu ya uwepo wa ulimwengu wa majini watu , wa majini pepo , binadamu walijua yote hayo.
Kwa sheria maalumu iliwawezesha binadamu kuamua kujifunza kanuni za mbingu na ardhi na hata kuchagua aidha aombe uraia wa miliki flani au abakie katika ulimwengu unaonekana.
Ki ufupi ni kwamba hata baraza la umoja wa kimataifa ambalo lilikuwa chini ya Clellia Allisanto lilitambua rasmi jamii za viumbe wasionekana na walipewa siti yao.
Mashulenni somo la kuvuna nishati za mbingu na ardhi kwa ajili ya kujikinga na magonjwa na kuishi muda mrefu liliingizwa katika mitaala ya mataifa mengi na msisitizo kuwekwa.
“Lanlan maamuzi ambayo baba yako alifanya wakati ule yalikuwa sahihi mno na inaonekana faida zake sasa hivi”
Aliongea Master Chi mara baada ya ndege hio kuingia katika ulimwengu wa binadamu na kuona baadhi ya binadamu ambao walikuwa na uwezo wa kupaa.
Binadamu walijikuta wakijua haikuwa na maana sana kutengeneza makombora kwa ajili ya kuuana wao kwa wao , yote waliona ni mambo batili na kupoteza rasilimali za dunia tu, ki ufupi ni kwamba binadamu aliufikia upeo mwingine kabisa.
Wale waliokuwa wakiamini katika Dini waliimarika sana kwani walitumia dini zao kuvuna nguvu za kiroho kupitia mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi.
Ki ufupi ni kwamba ulimwengu ulikuwa ni nusu Utopia , ijapokuwa matatizo hayakuwa yakikosekana baina ya watu lakini angalau amani ilikuwa kubwa zaidi kuliko mwanzo.

“Ndio , baba yangu ni shujaa , tatizo Bichwa kubwa anamwita mjinga”Aliongea na kuwafanya watu hao kucheka.
Dakika chache mbele ndege hio ilikuja kutua katika Visiwa vya wafu miliki inayotambulika kama ya Roma, haikuwa visiwa vya wafu tena bali ilikuwa ni kama taifa ambalo lilipewa jina kama miliki ya Roma.
Roma alionekana alikuwa akisubiria tayari na alikuwa nje amevalia mavazi yake ya rangi nyeupe upande wa shati na sandals za ngozi , kwa alivyokuwa akionekana utadhani sio baba mzazi kwa Lanlan , alikuwa akionekana kijana zaidi kuliko mwanzo.
“Master naona umekuja na Mzee
Zao?”Aliongea Roma huku akipitisha mkono wake kwenye shingo ya Master Chi.
“Hebu kuwa na maadili, ndio maana mtoto wako wa kiume anakwita mjinga”Aliongea Master Chi akijitoa kwa Roma na kumfanya Roma kumwangalia Lanlan ambae alikuwa akijifanyisha hajasikia chochote.
“Chubi , naona ulikuwa ukinichoma bila ya kujua tena?”
Ijapokuwa Lanlan hakuwa kibonge tena , Roma hakuona haja ya kubadilisha namna alivyokuwa anamwita.
“Lakini ndio Bichwa kubwa anavyokwita , usinilaumu mimi?”Aliongea Lanlan
“Inaonekana nakudekeza sana kama mama yako anavyosema , unadhani sijui mama yako Seventeen alikupatia zile bangiri , haya rudisha hapa ,hutakiwi kucheza na moto”
“Hapana , Mama Seventeen amesema ninaweza
kucheza nazo nitakavyo, ukizuchukua nitamwambia siku nyingine”
Roma midomo yake ilicheza mara baada ya kukumbuka namna tabia za Seventeen zilivyo wakati akiamka katika nafsi ya Edna.
“Master nina uwezo wa kuwadhibiti watoto
wengine lakini huyu kanishinda”Aliongea Roma
.
Upande wa Lanlan ambae alikuwa akicheka alitoa zile bangiri mbili na kisha aliziingizia nishati ya mbingu na ardhi na palepale zilibadilika na kuwa kama magurudumu yaliomvaa kiunoni na alianza kupaa kwenda angani.
“Aisee , ni mdogo mno lakini tayari ashapita
mapigo tisini na tisa ya radi ya
Zambarau…”Aliongea Master Zao.
“Mafanikio yake yanaridhisha , kati ya watoto wangu wote Lanlan ndio ambae ameoneysha uwezo mkubwa , Rusi amefanya vizuri pia na sasa ameingia levo ya nafsi siku chache zilizopita”
“Rusi yupo levo ya nafsi , lakini si ana umri wa miaka saba tu!!?”Aliongea Master Chi , alikuwa akiwajua watoto wote wa Roma kwani walikuwa wakimwita babu.
Furaha ya Roma haikujificha kwenye uso wake , lilikuwa jambo la kujivunia kama mzazi .
“Hivi huyo Rusi ndio mtoto wa kiume wa Rose sio ?”Aliuliza Zao.
“Ndio tofauti na wenzake yeye anapenda kuwa mwanajeshi , ijapokuwa hayupo vizuri kama Lanlan kiakili lakini anajuhudi kubwa na laiti
Lanlan angekuwa na nusu ya juhudi alizonazo Rusi angekuwa amepiga hatua kubwa , Lanlan tabia yake ya kupenda kula na maisha ya bata yanamrudisha nyuma”.
“Inatosha sasa , hebu ongoza njia nimechoshwa na majigambo yako”Aliongea Master Chi na kumfanya Roma kucheka.
Ijapokuwa uwezo wake ulikuwa umefikia hatua ya juu sana lakini aliweza kufanikisha kupata watoto kupitia kwa Edna , Rose na Clark lakini ajabu pia Amina na yeye alikuwa mjamzito.
Upande wa Edna yeye alipata watoto mapacha ambao hawafanani yaani ikiwa ni wa kike na wa kiume , Roma siku ambayo Edna alijifungua salama alifurahi mno kiasi kwamba alienda kushangilia juu angani kidogo tu agongane na Space station.
Miaka saba iliopita Rose alijifungua mtoto wa kiume huku Clark yeye akijifungua mtoto wa kike , ndani ya muda mfupi tu Roma alikuwa na watoto wakike watatu na wa kiume wawili na alikuwa akitegemea mmoja kutoka kwa Amina ambae mimba yake ilikuwa changa.
Wanawake wengine licha ya kuwa na wivu lakini walijitahidi sana kufanikisha uwezo wao ili na wao wapate watoto.
Lakini hata hivyo Roma hakuwa na haraka kwani walikuwa na muda mrefu wa kuishi.
Waliongea huku wakitembea na ndani ya muda mchache tu waliweza kufika katika bandari iliokuwa upande wa Kaskazini magharibi ya ksiiwa hicho kikubwa.
Upande huo ndio mahali ambapo familia yake ilikuwepo wakifurahia maisha pamoja na miungu wote.
Mara baada ya kumuona Roma ameongozana na wageni hao walisalimiana nae kwa ishara ya kirafiki.
Upande wa baharinni kulikuwa na chombo kikubwa mno chenye muonekano wa kimaajabu kilichofanana na UFO.
“Master Chi karibuni”Aliongea Edna ambae alikuwa amevalia gauni la chiffoni na aliwakaribisha Master Chi kwa heshima.
Ule ukauzu wa Edna ulikuwa ushampotea mara baada ya kujifungua watoto mapacha na umbo lake liliongezeka mno , ki ufupi alikuwa amenenepa japo hakupoteza mpangilio.
“Haha.. Edna kwanini naona kila mtu tayari yupo hapa , au hii ndio sherehe ya kuagana na ndugu zetu hawa”Aliongea Master Chi akicheka.
Aliuliza hivyo kwasababu wanawake wa Roma hawakuwa wakiishi tena kisiwani , alikuwa ni Edna tu mara nyingi ndio anakuwa yupo kisiwani na mume wake na kama wataonekana kisiwani ni nyakati za wikiend tu.
Clark yeye alikuwa maarufu sana katika sayansi hivyo licha ya kuwa na maabara katika Kisiwa hicho mara kwa mara alikuwa katika mataifa tofauti tofauti akifundisha katika vyuo vikuu.
Lakini licha ya wanawake hao kuwa mbalimbali watoto wa Roma wote walikuwa wakiishi na baba yao chini ya uangalizi wa Edna.
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

MTUNZI: SINGANOJR .

Mono no aware

ILIPOISHIA
Miaka saba iliopita Rose alijifungua mtoto wa kiume huku Clark yeye akijifungua mtoto wa kike , ndani ya muda mfupi tu Roma alikuwa na watoto wakike watatu na wa kiume wawili na alikuwa akitegemea mmoja kutoka kwa Amina ambae mimba yake ilikuwa changa.
Wanawake wengine licha ya kuwa na wivu lakini walijitahidi sana kufanikisha uwezo wao ili na wao wapate watoto.
Lakini hata hivyo Roma hakuwa na haraka kwani walikuwa na muda mrefu wa kuishi.
Waliongea huku wakitembea na ndani ya muda mchache tu waliweza kufika katika bandari iliokuwa upande wa Kaskazini magharibi ya ksiiwa hicho kikubwa.
Upande huo ndio mahali ambapo familia yake ilikuwepo wakifurahia maisha pamoja na miungu wote.
Mara baada ya kumuona Roma ameongozana na wageni hao walisalimiana nae kwa ishara ya kirafiki.
Upande wa baharinni kulikuwa na chombo kikubwa mno chenye muonekano wa kimaajabu kilichofanana na UFO.
“Master Chi karibuni”Aliongea Edna ambae alikuwa amevalia gauni la chiffoni na aliwakaribisha Master Chi kwa heshima.
Ule ukauzu wa Edna ulikuwa ushampotea mara baada ya kujifungua watoto mapacha na umbo lake liliongezeka mno , ki ufupi alikuwa amenenepa japo hakupoteza mpangilio.
“Haha.. Edna kwanini naona kila mtu tayari yupo hapa , au hii ndio sherehe ya kuagana na ndugu zetu hawa”Aliongea Master Chi akicheka.
Aliuliza hivyo kwasababu wanawake wa Roma hawakuwa wakiishi tena kisiwani , alikuwa ni Edna tu mara nyingi ndio anakuwa yupo kisiwani na mume wake na kama wataonekana kisiwani ni nyakati za wikiend tu.
Clark yeye alikuwa maarufu sana katika sayansi hivyo licha ya kuwa na maabara katika Kisiwa hicho mara kwa mara alikuwa katika mataifa tofauti tofauti akifundisha katika vyuo vikuu.

SEHEMU YA 799.
“Kila mtu amekuja kwasababu sio muda wa kuagana , kama ingekuwa hivyo wasingefika maana inahuzunisha”Alijibu Edna.
“Haha.. upo sawa”Aliunga mkono Master Zao. “Hey , Dionysus! Mbona unapoteza muda tena , hebu tuletee mvinyo uliotengeneza , Roma ni mbahili mno anatumia pombe ya bei chee kwenye hii sherehe”Aliongea Ares ambae ni kama vile anafoka , ilionekana hakuwa ameridhishwa na aina ya vinywaji ambayo vimeandaliwa na Roma.
“Unaongea upuuzi , huo ni mvinyo mzuri tu , kwa uwezo wako wa kuhimili kilevi ni kuingia hasara tu kama nitakupatia mvinyo wangu wa gharama kubwa”Aliongea Roma.
“Seriously , yaani muda si mrefu tunaondoka lakini bado unakuwa mbahili hivyo , Tsk tsk”Ares hakutaka kujisumbua kujibishana na Roma hivyo aliendelea kumuomba Zao mvyinyo ambao ametengeneza.
Mapema tu sherehe ilianza na kila mmoja alianza kuongea huku wakifurahia vinywaji na chakula.
Habari kuu zilizokuwa zikiongelewa ni juu ya kuondoka kwa miungu kwenda sayari nyingine.
Dionysus hakuwa tayari kuondoka na Athena pia, hivyo ni miungu nane tu ambao walikuwa wakiondoka.
Miaka tisa iliopita Clark alitoa pendekezo la ujenzi wa Spaceship ili miungu kutafuta sayari ambayo ina mazingira mazuri ya kufufua moyo wa Gaia.
Miungu walikubaliana na wazo la Clark , haikujalisha sayari ya Dunia ilikuwa nzuri kiasi gani lakini bado haikuwa ni sayari yao.
Pendekezo la Clark juu ya ujenzi wa Spaceship hio ilitokana na kioo Cha nafsi.
Moja ya kazi kubwa ya Kioo cha Nafsi ni kuwa na taarfa zote za anga za mbali na sayari zake na nyota zake.
Inasemekana kwamba kioo hicho kilikuwa na uwezo wa kuangalia sayari za mbali ambazo zipo miaka zaidi ya elfu moja ya mwanga.
Sasa kwa msaada wa kioo cha Nafsi Roma aliweza kugundua uwepo wa sayari nyingi sana ambazo zilikuwa na muonekano wa kimazingira unaofanana na dunia na sayari kubwa mara mbili ya dunia, aliweza hata kugundua baadhi ya uwezo wa miezi ambayo inasapoti maisha.
Haikuwa hivyo tu Roma aliweza kugundua vitu vingi sana kwa muda mchache sana kuhusiana na anga za mbali , aliweza kugundua baadhi ya uwepo wa viumbe wengine waliopo nje ya galaksi.
Sasa katika sayari zote ambazo aligundua moja wapo ya sayari iliokuwa karibu zaidi ndio ambayo ilikuwa na mazingira ya kusapoti maisha na haikuwa imetawaliwa , kwa maana ya kwamba haikuwa na viumbe wenye akili zaidi ya wanyama.
Roma yote hayo hakuwa na haja hata ya kusafiri kwenda anga za mbali , kwake ilikuwa ni kama anaoteshwa tu juu ya mazingira hayo kupitia msaada wa kioo.
Sasa ili kufika katika sayari hio ambayo aliona inawafaa ilihitajika tu usafiri wa kuelekea huko ambao ni SpaceShip huku kioo kikitumika kama ramani na kisha angekirudisha kioo hicho duniani.
Miungu wangeweza kufika katika sayari hio na kwa kupitia uwezo wao wangeweza kufufua Mti Mama na kuzaliana.
Bila shaka mawazo hayo hayakumjia Roma yeye mwenywe , ilikuwa kwake ni kama wazo ambalo liliwasilishwa na Mkuu wa enzi kupitia kioo hicho ndio maana alifanya maamuzi.
Ijapokuwa Roma alikuwa na uwezo wa kwenda anga za mbali kusalimiana na marafiki zake lakini bado aliona aandae sherehe ya kuwaaga kabisa , isitoshe mahali wanakoelekea ni mamia ya miaka ya mwanga.
Mamia ya miaka ya mwanga sio umbali mdogo , kwa teknolojia ya Roketi pengine ni zaidi ya miaka elfu moja mpaka kufika mwisho wa safari lakini kupitia teknolojia mpya yote hayo yaliwezekana kwenda umbali mrefu kwa muda mchache.
Mara baada ya kunywa na kula Venus(Aphrodite) alimsogelea Roma na kumpiga busu la shavuni na lipsi zake zilizopakwa rangi.
“Roma , don’t you have anything to say to me now that I’m leaving?”Aliongea Christen akimwambia Roma kwamba hana cha kumwambia wakati huo anataka kuondoka.
Muda huo Roma alikuwa akihangaika na steki ya nyama kwenye sahani na aliinua uso wake kumwangalia mrembo huyo kwa hali ya kusita.
“Ni kipi ninachoweza kukuambia sasa, Uwe na safari njema “
“Unadhani nataka kusikia hio kauli , unaonaje ukija chumbani kwangu usiku wa leo kabla ya kuondoka?”Aliongea huku akiweka mapozi ya kumtega Roma.
Kitendo hicho kilimfanya Roma homoni zake kuanza kuongezeka kwa kasi na aliishia kumeza mate akisita kutoa jibu la ombi kwa mrembo huyo.
“Wapi unataka kwenda usiku?”
Dakika hio hio Edna alikuwa ashasogea , ni kama alijua nini kinataka kutokea lakini licha ya hivyo alikuwa na tabasamu usoni.
“Wife hamna ninapoenda , alikuwa akimaanisha usiku anga ni la bluu sana hivyo kama tunaweza kutembea?”Roma alijibaraguza.
“Oh!, ndio hivyo?”Edna aliongea huku akipiga pafu laChampagne iliokuwa kwenye glasi yake na kumwangalia Christen kwa macho yaliojaa ukali.
“Athena nakuonea sana wivu”Aliongea Christen mara baada ya kumsogelea Athena na kisha akampita baada ya kuona ombi lake haliwezi kutimia.
“Halafu wewe hebu niambie , umelala wapi usiku wa jana , Rose alianiambia uliondoka hotelini kwake mepema tu”
“Nilienda kumwangalia Sophia na maandalizi yake ya Show”
Baada ya hali ya dunia kutulia Sophia alirudi katika maswala yake ya usanii na alikuwa maarufu mno karibia dunia nzima na kambi yake kubwa ilikuwa ni nchini Tanzania.
“Kama ulienda kwa Sophia kwanini ulirudi nguo zako zikitoa harufu ya perfume ya
Recho?”Aliuliza Edna huku macho yake ni kama yalikuwa yakiiangalia akili ya Roma. “Babe , umejuaje ni marashi ya Recho?”
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa amebadilika sana , katika kipindi cha muda mfupi alikuwa na wanawake ambao hawakuwa wakifahamika mmoja wapo alikuwa ni Recho , Benadetha na Nadia.
Wanawake hao hawakuwa na haja kubwa ya kutambulika kama mahawala wa Roma na waliendelea kufanya kazi katika kampuni ya Vexto, kwa Recho ambae alishaolewa na kuachika hakupenda tena kuwa na mwanaume na alifurahia kuchepuka na Roma ambae alikuwa akimpatia vitu vingi ikiwemo vidonge na mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi , upande wa Benadetha ilikuwa hivyo , Nadia yeye japo hakuridhika na kuwa mchepuko wa siri lakini kutokana na mapenzi makubwa aliokuwa nayo kwa Roma aliona angalau inatosha , taasisi yake binafsi ya kisheria ilikuwa ikifanya kazi kubwa sana na alikuwa na mikataba na kampuni kubwa katika usimamizi wa maswala ya kisheria ikiwemo kampuni ya Vexto na Kanani.
“Unadhani nilimpatia zawadi ya marashi ambayo hakuna anaeyatumia bila sababu ?”Roma alijikuta sura ikimshituka kumbe ulikuwa mtego.
“Edna Darling , nimekukubali kuja na mbinu hio, I’m so impressed”
“Fanya mambo yako ukidhania sijui , najua unachokifanya na Mkurugenzi wa tawi langu nchini Japani Tannya , na juzi tu ulikuwa na Lilith ….”
Roma hakutaka kumsikiliza tena zaidi ya kumziba mdomo .
“Nakuomba mke wangu , tafadhari acha kuongea tena juu ya haya maswala , kwanini usinifungie kama adhabu , sitokudanganya tena, nimekosa mimi Babe”
“Najua tabia yako ya kuuchezea mwili wangu wakati Seventeen na Athena wakijitokeza wakati nikiwa nimepumzika , ijapokuwa hawawezi kukudhibiti lakini naona kila kitu katika fahamu zao”
“Nimeelewa , nimeelewa mke.. najua nafsi zote tatu ndani yako ni kitu kimoja”
Edna ndio aliekuwa mtawala kamili wa nafsi tatu lakini kuna muda mwingine akichoka ni kama nafsi hizo huamka kwa wakati wake, katika kipindi chote aligundua akili yake inapata utulivu kama atawaacha Seventeen na Athena kuutumia mwili wake hivyo ndio maana akitaka kupumzika anaizima nafsi yake.
Sasa upande wa Roma alikuwa akitumia fursa wakati nafsi hizo zikiwa zimeamka kufanya yale ambayo Edna hayapendi , sio kwamba hakupenda kufanya na Edna lakini ukweli ni kwamba Roma alikuwa akimhofia zaidi Edna kuliko hata Athena na Seventeen , pengine ni kutokana na upekee wake.
Roma alifurahia siku ambazo nafsi hizo zikuwa zinafanya kazi kwani maisha ni ya amani lakini hata hivyo kuna muda alipatwa na mawazo kwani tabia ya Seventeen ilikuwa tofauti kabisa na ya Edna.
Seventeen akiamka atampa Lanlan kila anachotaka , hata bangiri zile za ulinzi Lanlan alipewa na Seventeen , ki ufupi ni Seventeen aliemfanya Lanlan kupenda kula bata kuliko kitu chochote na hakujali matokeo ya tabia yake kwa Lanlan ili mradi impe furaha.
Upande wa Athena yeye nafsi yake iliongoza kwa kuwa na aibu na Roma akimuona mwanamke huyo ameamka anamtoa nje kwani wakati wa kale machezo akifika kileleni lazima kutokee tetemeko kiasi cha kumfanya Roma aogope nyumba yake itaporomoka.
Upande wa Edna alirudi kikamilifu kwenye biashara zake na alifufua ndoto yake ya kuifanya kampuni ya mavazi kuwa kubwa mno na swala hili liloimfanya kufanya biashara mpaka na miliki za majini ya Kibra na Panas.
Ki ufupi alipenda kufanya kazi sana na kumfanya kutokuwa karibu zaidi na Roma ndio maana ilimpa nafasi Roma ya kuwatembelea wanawake zake.
Lakini licha ya hivyo alikuwa na mbinu zake za kumfatilia kila mahali bila hata yeye mwenyewe kujua.
Muda huo wakati Edna anataka kumchimba
Roma juu ya tabia yake alibadilika palepale mara baada ya kuona msichana wa miaka saba alievalia gauni akisogea maeneo hayo huku akiwa ameshikilia boksi la vikeki.
“Nyromi wewe mtoto , kwanini unakula keki zangu , haya tema haraka , tema”
Nyromi , Naomi au Nyomi ni jina la kiebrania ambalo Roma alichagua kumpatia binti yake sababu kubwa ni kutokana na Naomi kufanana kila kitu na Edna haikuwa muonekano tu bali mpaka tabia na hisia alizokuwa akipata akimwangalia biti yake huyo ndio sababu ya kuja na jina hilo.
Kulingaa na Bi Wema ambae alishuhudia ukuaji wa Edna anasema kama Naomi angezaliwa miaka ishirini iliopita basi kusingekuwa na ubishi wa kuwa pacha wa Edna, ki ufupi ni kwamba Edna alijipiga kopi tu na kumleta Naomi Duniani.
Wote walifanana katika vyakula wanavyopenda na kufanya muda mwingi kugombana, kwani Edna akinunua keki zake anakuta zimeliwa zote.
Jambo hilo lilifanya watu wengi kucheka mno ugomvi unapotokea kutokana na tabia zao.
Dakika ambayo Naomi alijua tayari ameshakamatwa alichukua keki iliobakia kwenye kiboksi na kuibugia yote mdomoni bila ya kujali mdomo ulikuwa mdogo.
“Si nilikupatia za kwako , kwanini unakula na zangu , unatafuta kupigwa mbele ya wageni?”Licha ya kufoka kwake Naomi ambae ni kama sasa amefanya jambo la kujivunia alimwangalia mama yake kwa macho ya kijasiri.
“Mama.. mama anatia aibu kugombania chakula na mtoto..”
“Wewe..”Edna alikuwa na hasira na alimsogelea Naomi na kumfinya shavu.
“Haya tema , tema nakuzuia kumeza , tema..”Licha ya kushikilia shavu Naomi alionyesha ukiburi wake na kukataa kutema na kufanya wageni kucheka.
Tabia zao zilimfanya Blandina kama mama mkwe kuona aibu mbele ya mjukuu wake na mke mwana.
“Wifey .. usiwe na hasira hivyo , nitakununulia vingine , Nyromi ni mtoto ambae haelewi kitu lakini vilevile ni binti yako…”
“Kwahio akiwa binti yangu ndio anifanyie hivi?”
“Ndio kama mama yao ni wa kawaida”Roma aliwaza lakini hata hivyo aliamua kumaliza hali hio.
“Unaonaje kama nikimuadhibu na mazoezi ya masaa mawili , Wife punguza jazba ashazimaliza zote hata hivyo”
Wakati wakiendelea kuongea kumaliza hali hio mtoto mdogo wa kiumbe alievalia suti ya ugoro na tai nyekundu juu ya shati jeupe aliishia kutingisha kichwa huku akiendelea kula chakula kwa uma.
“Aunt Clark .. naona kabisa kama sisi wawili tusingekuwa sehemu ya hii familia , ukiunganisha IQ zao matokeo yatakuwa ni hasi .. Baba anafikiria na kichwa cha chini, mama na dada mbele ya vijikeki wanakuwa wajinga ..moyo wangu unauma nikiwaangalia na inanipa changamoto kuona namna nilivyo na majukumu makubwa”
Maneno aliokuwa akiongea huyo mtoto hayakulingana na umri wake,ijapokuwa alikuwa mzuri wa sura na mpole lakini alikuwa akiongea kama mtu mzima.
Alikuwa amevalia miwani kubwa ambayo haikuwa na kioo , yote hayo ilikuwa ni kwa ajili ya maonyesho tu.
Huyo alikuwa ni pacha wake Naomi afahamikae kwa jina la Rube au Rubchen jina la kijerumani ambalo lilimaanisha kichwa kikubwa.
Sababu za Roma kumwita Kichwa kikubwa ni kutokana na kwamba alionyesha dalili ya kuwa Jiniasi tokea akiwa na mwezi mmoja tu.
Tokea apate ufahamu wa kujitegemea Rube hajawahi kupenda kukaa karibu na Roma wala mama yake , muda wote alikuwa karibu na Clark ambae alipenda kujifunza vitu vingi kutoka kwake na hakuchagua cha kujifunza , iwe ni mambo ya anga , bailojia au Jiografia alijifunza kwa spidi kubwa mno.
Clark alikuwa akimpenda sana Rube kutokana na akili yake yenye uwezo wa ajabu na alimfundisha kwa moyo wote huku akitegemea makubwa kutoka kwake , lakini upande wa Roma ilimpa mawazo.
Rube ndio mtoto wake wa kwanza lakini licha ya hivyo hakuonyesha kumpenda kabisa na kumuona yeye hana akili na Clark pekee ndio ambae aliona ni mtu wa kufatishana nae.
Ijapokuwa Rube alijua baba yake ni mtu mwenye uwezo mkubwa na nguvu lakini hakukubali uwezo wake , yeye aliamini katika maswala ya sayansi pekee na mambo ya kuvuna nishati kwake hayakuwa kipaumbele na aliona ni ujinga.
Roma alijaribu kumtaka Rube kujifunza namna ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi lakini alikataa na mwishoni aliamua kumwacha afanya anavyotaka.
Katika ujenzi wa Spaceship Naira kutoka idara ya sayansi ya Zeros alitoa mchango wa teknolojia mpya ya injini lakini mara baada ya utafiti wake kufanyiwa uchambuzi na Rubeni kulionekana kuna mapungufu mengi na yote yalizibwa na mtoto huyo , hivyo kwa lugha nyepesi ni kama injini ya Spaceship ilitengenezwa kwa mchango wa Rube.
“Upo sahihi Rube , muda mwingine naona kama vile nimekuzaa mimi na kuna namna baba yako alifanya miujiza yake na ukazaliwa na Sister Edna”Aliongea Clark alievalia koti la maabara.
“Hata wewe umeona , mimi mwenyewe najiuliza kwanini kuna utofauti mkubwa wa IQ na Naomi?”Aliongea Rube.
Lakini muda huo msichana mdogo ambae alikuwa akila Ice Cream pembeni alionekana kutofurahiswa na Clark .
“Am I not your Daughter ?Do you not want me anymore?”Aliuliza msichana ambae alikuwa na muonekano kamili wa kizungu.
Alikuwa na nywele nyingi mno za rangi nyeusi na macho yake ya Bluu , alikuwa ndio mtoto mdogo zaidi wa kike ambae amezaliwa na Clark , kitu pekee ambacho pengine Roma aliona amerithi ni Komwe la Ashley, ki ufupi ni kwamba rangi na macho alirithi kwa Clark lakini sura yake alikuwa akifanana mno na Ashley mdogo wake Roma.
Binti huyo alifahamika kwa jina la Dami na hio ni kutokana na namna ambavyo alionekana wakati akiwa mdogo , Dami alikuwa na mashavu yaliotuna kama Andazi ndio maana Roma akaibuka na hilo jina.
Clark mara baada ya kuona binti yake anavyotia huruma aliishia kucheka na kumpakata huku akimchokoza kwa kufinya mashavu yake.
“Kwaninni nisikutake tena , wakati unaonekana mzuri hivi , unajua kuimba na kucheza na pia unaweza kunichora bila ya kunikosea , kaka yako Rube anajaribu kutania tu”Aliongea kwa kumbeleza na Rube alitingisha kichwa kukubaliana na Clark kumtuliza msichana huyo mdogo ambae alionekana kutaka kulia.
Dami licha ya kwamba mama yake alikuwa mwanasayansi mkubwa lakini yeye hakupenda kabisa maswala ya sayansi , alipenda mno sanaa kuliko kitu chochote kile.
Alipenda kuimba , kucheza na kuchora , alikuwa na uwezo wa kuchora kitu bila ya kukikosea kwa kuona mara moja tu na pia alikuwa na uwezo wa kuigiza namna ya kuimba na kucheza kwa kujifunza mara chache sana.
Dami ndio ambae alionekana kuwa mpole kuliko wote , ijapokuwa alionekana kama ana uwezo mdogo wa kuchanganua sentensi zenye zaidi ya maana lakini alionekana atakuja kuwa mwanasanaa mkubwa sana.
Clark hakutaka kumlazimisha binti yake kufanya kile anachokifanya , hata hivyo aliridhika na kile ambacho kinaonyeshwa na Rube.
Kinachofurahisha zaidi Dami ni namna ambavyo ana ukaribu mkubwa na Lanlan , walikuwa wanapendana mno pengine ni kutokan na wote wawili kupenda kula na maisha yao kutojali sana vitu vingi.
Dakika chache wakati stori zikiendeea Lanlan aliweza kufika huku akiita kwa nguvu jina la baba yake .
“Dad , Dad , Dad , I want to eat sashimi”
“Sister Lanlan!!”Dami furaha yake yote ilichipua mara baada ya kumuona Lanlan ambae ameshikilia Samaki mkubwa aina ya Tuna(Jodari).
“Dami hii ni zawadi yako”Aliongea Lanlan huku akitoa Kombe(conch) kutoka katika hifadhi yake ya pete na kumpatia mdogo wake, aina hio ya kombe huweza kutumika kutengenezea mziki kwa kupuliza.
“You are the best Sister Lanlan”Kaliongea kwa furaha huku kakiruka ruka wakati huo Edna ni kama ameamka sasa kwani muonekano wake ulibadilika, kitendo cha kumuona Lanlan akiwa na samaki wa aina hio alijua fika Lanlan anaendeleza tabia yake ya kuzama baharini kwenye kina kirefu cha maji.
“Lanlan mbona huchoki kusababisha matatizo , mara ya mwisho Rusi alikuambia umpitishe kwenye Dhiki ya radi ya zambarau kwa kumshambulia nayo na kweli ukafanya hivyo , kama isingekuwa kwa Dhana alizokuwa nazo , mdogo wako angekuwa ashafariki”Alifoka Edna.
“Sikufanya makusudi , na sitofanya tena”Lanlan aliishia kuinamisha kichwa chake chini.
Hakutaka habari hio izungumziwe kabisa , kwani mara baada ya tukio hilo alipatwa na hofu kubwa kwa namna ambavyo Rusi alikuwa ameunguzwa na radi hio.
Kitendo hicho kilimfanya Rose kufoka mno na Edna alimpiga Lanlan mpaka akalia , hata Roma ambae alikuwepo hakuingilia kabisa.
Ndio hivyo tu walikuwa ni familia na Rusi alijua sio makosa ya Lanlan peke yake , yeye ndio ambae alikuwa na shauku ya kuona namna Dhiki ya radi ilivyokuwa na Lanlan hakuona mbaya kumuonjesha mdogo wake.
“Inatosha sasa Edna , hilo swala lishapita na Rusi ashapona , haina haja ya kuendelea kumfokea nalo Lanlan”
“Sio kosa la Sister Lanlan , ni kwasababu sikumsikiliza baba na kuwa na wasiwasi juu ya kupanda levo ndio maana nikapata shauku”
Rose alimpatia mwanae jina la Rusi kama mbadala wa neno Utulivu , kutokana na changamoto alizopitia katika maisha yake kukutana na Roma ilikuwa mwanzo wa utulivu ndio maana kuweka kumbukumbu sawa akaamua kumwita mtoto wake Rusi yaani Utuliivu , Rusi ni msemo katika lugha ya Bengali huko Bangladesh.
Katika watoto wote wa Roma, Rusi ndio ambae alikuwa na ndoto za kumfikia baba yake katika mafunzo ya nishati ya mbingu na Ardhi , angefanya chochote kile ili mradi kiwe kinahusiana na maswala ya kuvuna nishati. Lakini licha ya ya umakinni wake mkubwa spidi yake ya kupanda levo haikuwa kama ya Lanlani na swala hilo lilimpa mawazo na hata kutamani kutafuta njia ya mkato.
“Inatosha sasa , leo ni siku ya furaha utamfunza vizuri muda mwigine , halafu Lanlan ni mtoto wetu wa kwanza kwanini unakuwa mkali sana kwake hivyo?”
“Ushasema ni mtoto wa kwanza ndio maana nakuwa mkali , nisipokuwa mkali utamharibu kwa kupenda kumdekeza “Aliongea Edna.
Roma aliishia kunyamaza na kisha alimkonyeza Lanlan na Dami kumfuata nyuma wakamtengeneze samaki na Lanlan alimpa ishara na Rusi na wote walimkimbhilia baba yao.
Baada ya kuona watoto hao wanamfatisha Roma Edna aliishia kuangaliana na Rose na kuishia kutabasamu.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kizazi cha Roma mara baada ya kuwa mwangalizi , ijapokuwa kwake alikuwa akichukulia familia yake kama familia nyingine lakini watoto wake walikuwa wakiangaliwa kwa jicho pekee mno , ni kama dunia ilikuwa ikisubiria kuona ni namna gani kizazi hicho kitabadilisha maendeleo ya binadamu kwa haraka.
Isitoshe Mpango LADO haukuwa kumfanya Roma kuwa na nguvu tu na kuweza kuwa na nguvu ya kuwashinda miungu bali pia kizazi chao ilikuwa ni sehemu ya mipango hio.
Na kama ilivyotarajjiwa , licha ya kwamba watoto hao walikuwa na hobi tofauti tofauti lakini mustakabali wa maisha yao ulikuwa ukisubiriwa na msisimko mkubwa na hasa hasa macho yalikuwa kwa Rubcheni ambae muda wote aliambatana na Clark na hata kuvumbua teknolojia mpya ya injini ya Spaceship.
Moja ya watu waliokuwa wakitamani kufanya kazi na watoto wa Roma ni Naira Mkurugenzi wa kitengo cha sayansi cha dunia cha Zeros.
Miaka kumi iliopita makao makuu ya kitafiti ya
Zeros yaliondolewa kutoka katika umoja wa Zeros organisation ambao ulivunjwa na kuingizwa kama kitengo maalumu cha maswala ya kitafiti kinachodhibitiwa na umoja wa Mataifa.
Naira ambae ndio aliekuwa mwanasayansi kinara wa taasisi hio alipewa ukurugenzi kamili wa kuendesha taasisi hio na makao hayo makuu hayakuwa siri tena, ijapokuwa hayo yote yalifanyika chini ya mapendekezo ya Roma kama njia ya kuboresha usalama wa dunia lakini hakutaka kuingilia moja kwa moja maswala ya kibinadamu.
Majukumu ya Roma kama mwangalizi hayakuwa kufuatilia binadamu wanafanya nini bali ni kuzuia majaribio yota hatari ambayo yanaweza kupelekea dunia kutokuwa salama, hivyo hata maswala ya jamii za siri hakujihusisha kabisa na aliacha ziendelee kama ilivyokuwa mwanzo.
Naira aliweza kukutana na Dorisi na ilikuwa ni furaha kwa wawili hao kukutana na kumfanya Dorisi sasa kujihisi amepata ndugu , ijapokuwa kukutana kwa Dorisi ndio ilikuwa mwanzo wa kujua sababu ya vifo vya wazazi wake lakini kwa namna moja ama nyingine alifurahi aliweza kufuta ule mkanganyiko aliokuwa nao muda mrefu.





SEHEMU YA 800.
Mwezi mmoja baadae hatimae miungu iliacha dunia na kuelekea sayari nyingine kupitia Spaceship , tukio ambalo lilishuhudiwa na dunia nzima huku pongezi zikienda kwa Clark , Naira na Rubeni wafanikishaji wa teknolojia hio.
Upande wa Roma hakuwa na majuto ya kuagana na marafiki zake , licha ya macho makali ya Edna ya kumfatilia , Roma alifanikisha kwenda kuweka kumbukumbu nzuri na Christen, lakini haikujalisha alikuwa makini namna gani lakini Edna aliweza kujua kupitia uungu wa Athena na kumfanya Roma wiki nzima kumbembeleza mke wake amsamehe kwa magoti.
Hatimae wanawake wote wa Roma walirudi katika majukumu yao ya kimaisha kwa kuondoka kisiwani wakimuacha Edna pekee katika Ngome.
Roma pekee ndio mtu ambae hakuwa na kazi rasmi ya kufanya lakini hio haikumaanisha kwamba alikuwa amekaa kizembezembe.
Ukiachana na kufuatilia kwa ukaribu ukuaji wa watoto wake na elimu zao lakini pia alisafiri kila kona ya dunia kuangalia maendeleo ya sayari yalivyo.
Ukweli kitendo cha kuwaruhusu binadamu kuvuna nishati za mbingu na ardhi ni kama ilimuongezea jukumu lingine la kuhakikisha hakuna ambao wanatumia mbinu hizo kufanya uharifu., hivyo akiona wale ambao wanataka kudhuru binadamu kwa namna yoyote ile alikuwa akiwaua.
Kuhusu kulinda anga na matishio ya mbali kioo ndio kilikuwa kama darubini yake angani ya kumjuza , ukweli ni kwamba kazi yake haikuwa ngumu sana kama ilivyokuwa kwa Sharif ambae hakuwa na Dhana hio.
Hakutafuta pia mrithi kama Sharif alivyofanya bali yeye aliona ana miaka mingi ya kuishi na bado ni kijana hivyo swala hilo atalifanya baadae.
Neema licha ya kuzidi kutajirika kwa kufanya biashara ya Vidonge lakini vilevile aliweza kuitwa bibi baada ya Donyi kujifungua mtoto na Kassimu , jambo hilo lilimfanya kuwa na mawazo, lakini hata hivyo alikuwa na furaha kwa ajili ya binti yake.
Magdalena alipandishwa cheo na kuwa
Kamanda mkuu wa kitengo cha Wachawi nchini Tanzania na alikuwa ndio msimamizi wa maswala yote yanayohusiana ulimwengu unaonekana na ule usioonekana.
Mage yeye aliingizwa katika kitengo cha usalama wa taifa kama mkuu wa idara ya sera za kigeni hivyo alifanya kazi karibu zaidi na raisi.
Upande wa Afande Tobwe alipandishwa cheo na kuwa katibu mkuu wa wizara ya ulinzi huku Afande Maeda yeye aliteuliwa na kuwa mkuu wa majeshi.
Najma ambae mwanzoni alitaka kuwa mwanasiasa aliachana na maswala hayo na alifanywa mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya kimisaada ya Blandina Foundation ambayo iliingia katika maswala ya ushirikiano na taasisi ya Edna Foundation iliokuwa chini ya Suzzane, hivyo ilimfanya Najma muda mwingi kusafiri akiwa na Blandina.
Janga ambalo lilitokea miaka iliopita lilifanya watoto yatima kuwa wengi hivyo ni kama kazi ya watoto waliohitaji misaada iliongezeka.
Athena kupitia mwili wa Edna aliweza kumpatia Dorisi robo ya kiasi cha hela zote alizokuwa nazo pamoja na Naira na kiasi kilichobakia kiliingizwa katika mfuko wa maendeleo ya jamii dunia nzima.
Nasra alijiunga na benki ya dunia kama makamu wa raisi Afrika ya mashariki na kusini na Dorisi aliendeleza biashara za wazazi wake kwa mtaji aliokuwa nao , biashara ya uchimbaji wa madini ,biashara hio ilimfanya Dorisi kusafiri mpaka katika ulimwengu wa majini kwa ajili ya kukusanya madini.
Rufi na Amina waliungana pamoja na kufungua kampunni ya mawasiliano, wakati huo Amina alikuwa akitambulika kama sehemu ya majini wa Mbweha katika miliki ya Braki na alifika na kutambulishwa kabisa, ijapokuwa haikuwa na umuhimu sana lakini ilifanyika hivyo ili wanamiliki hao kujiweka karibu na Roma.
Upande wa Rufi yeye licha ya kufanya kazi katika kampuni lakini kupitia mwili wake ulivyokuwa alifanikiwa kupanda levo kwa haraka sana na kuwapita Rose , Clark na wengine wote kasoro Edna tu ambae alikuwa na uungu wa Athena jambo ambalo lilimshangaza sana Roma.
Yezi alirudi Korea na kupewa urithi wake na kuanzisha vyuo binafsi vinavyofudisha namna ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi, ndani ya muda mchache tu kwa kuchanganya na urithi aliopata aliweza kuwa tajiri mwenye pesa nyingi mwanamke katika bara la Asia, aliweza hata kumpita Edna likija swala zima la utajiri.
Mataifa mengi ya Afrika yaliingia katika hatua nyingine kabisa ya kimaendeleo na moja ya mataifa yaliopiga hatua kwa haraka ni Tanzania, Raisi Senga kwa kupitia ushawishi wake aliweza kubadilisha katiba , ambayo ilimpa nafasi ya kugombea uraisi mara nne.
Kutokana na kukubalika kwake na sapoti kubwa kwa familia aliweza kushinda kila awamu hivyo kuwa raisi wa kwanza nchini Tanzania kutawala muda mrefu zaidi ya miaka kumi.
Raisi Jeremy upande wake kwa kushirikiana na majini wa Paasi waliofanikiwa kukimbia alianza kujenga upya miliki hio na miliki nyingine hazikumwingilia sana kutokana na kwamba walihofia Roma anaweza kuingilia kati kutokana na mke wake kuwa na uhusiano na Jeremy.
Upande wa Afande Kweka maisha yake yalikuwa ni yale ya kizee , kucheza na wajukuu , hakujutia kwa maamuzi yake yote alioyafanya miaka mingi iliopita kumhusisha Roma(Denisi) katika mpango LADO, aliona alifanya maamuzi sahihi kabisa hasa kwa kwa kuwa na vitukuu wengi namna hio wenye akili kubwa.
Upande wa Omari aliteuliwa kama raisi wa chama cha wavuna nishati za mbingu na ardhi duniani na hio yote ni kutokaa na kupata sapoti kubwa kwa Roma , wale ambao waliona hafai walinyamaza wakimhofia Roma.
Ukweli ni kwamba uwezo wake haukuwa mkubwa sana , Omari alikuwa amepitwa hata na Lanlan ki uwezo lakini licha ya hivyo Roma aliamini huko mbeleni atakuja kuimarika nakushawishi kila mmoja kuwa raisi wa ushirika wake.
Upande wa XioXiao alikuwa akifika mara kwa mara kisiwani kwa Roma , ijapokuwa mara zote alifika kwa kisingizio cha kutaka kucheza na Lanlan pamoja na kuvuna nishati pamoja lakini alikuwa akitafuta nafasi kumtega Roma , alijua fika Roma ni mwanaume tu na siku moja lazima ataingia kwenye mtego wake.
Lakini hata hivyo alikuwa na furaha , mama yake alikuwa akiishi na baba yake na walikuwa wameirudisha miliki yao kama ilivyokuwa mwanzo japo sio kwa asilimia mia moja.
Roma alijua fika mipango ya Xiao Xiao lakini kutokana na kumhofia mke wake hakufanya lolote.
Wale wanafunzi wa Sharif , yaani Mzee Yasu na
Xumei wenyewe walipotea kusikojulikana na Roma hakujisumbua kuwatafuta akijua lazima wameenda kujichimbia kwa ajili ya kuelewa namna ya kufikia levo ya mapigo elfu kumi ya radi, ni Shekhe Idriss tu ambae alikuwa ndio kiongozi wa umoja wa Ant-Iluminat mara baada ya kutawazwa rasmi na Edna ambae alikuwa akitegemewa kama kiongozi, ijapokuwa sera zilikuwa zimebadilika lakini walikuwa ndio wamiliki wakubwa wa Project Binamu Island.
Dunia ilirudi katika hali yake ya Amani kabisa na maisha yakaendelea na ilikuwa ni kama hakuna kilichotokea,
Umoja wa kimataifa ulitangaza Safina ambayo ilikuwa ikijengwa huko Ethiopia kukamilishwa na kisha kufungwa injini zilizotumika katika Spaceship ya miungu na kisha kutumwa anga za mbali kwa ajili ya utafiti na kupitia taasisi ya Zeros hilo lilifanikiwa kwa asilimia mia moja.
Serikali ya Tanzania ilimpatia Roma kisiwa cha Mbudya kama zawadi kwa ajili ya ujenzi wa makazi.
Edna kupitia kampuni yake ya ujenzi alijenga hekalu la kifahari la kutosha familia yote ya Roma na ilikuwa ni sehemu maalumu kwa ajili ya mapumziko yao ya mara kwa mara , japo hawakuishi hapo moja kwa moja.
Roma alihakikisha watoto wake wanasoma katika shule moja ili wasitengane kutokana na kuzaliwa na mama tofauti tofauti , lakini pia aliwaacha kusoma katika shule zenye mchangayiko wa wanafunzi wengine wa kawaida ili kushirikiana na jamii.
Maimuna aliweza kurudi na kusimamia biashara za ukoo wake baada ya Tannya kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Vexto tawi la Japani.
****
Ilikuwa ni siku ya tatu yaani tarehe nne baada ya Mwaka mpya, mwanga wa jua uliingia kupitia dirisha na kuyagusa mashavu ya Roma na kumfanya atoke usingizini.
Roma alinyoosha mkono wake bila ya kufumbua macho yake akijaribu kumtafuta Edna na aligundua ashaamka tayari na ilimfanya kuangalia saa na kuona ni saa kumi na mbili na nusu.
“Huyu mwanamke hajui kabisa kuinjoi maisha, ukute ashaenda kazini tayari”Aliwaza Roma.
Aliondoa blanketi na kushuka chini akiwa hana nguo yoyote mwilini , usiku wa jana alicheza na mke wake mpaka usiku wa manane na kuishia kulala akiwa amemkumbatiaa bila ya kuoga.
Roma alivaa boksa tu na kisha alitoka chumbani na kuegamia kwenye uzio akiangalia chini sebuleni.
“Lanlan kula hizi tambi , nimekutengenezea kwa ajili yako , ni tamu sana”Aliongea Bi Wema ambae alikuwa amevalia Apron.
Lanlan mara baada ya kuwekewa sahani hio yenye tambi hakutaka kupoteza muda maana alikuwa ashameza mate vya kutosha.
“Bi Wema unamdekeza sana Lanlan kwa kumpa kila anachotaka , halafu tena sasa hivi ni asubuhi”Bi Wema hakujali maneno ya Edna kabisa huku akiwaangalia watoto wakila chakula kwa furaha.
Edna aliishia kutoa pumzi na kumgeukia Rube ambae alikataa kula tambi alizowekewa na Bi
Wema.
“Rube is the best , he knows how to follow a balanced diet and only eat eggs and drink milk in the morning”Aliongea Edna akimshika kichwa Rube ambae ameshikilia kikombe cha maziwa.
“Ni kwasababu kama mtu akila na akashiba kabisa tena ikiwa ni asubuhi anasababisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuhitaji kiasi kikubwa cha damu hivyo kufanya ubongo kuchoka haraka , Mimi kama mwanasayansi mkubwa ambae dunia inanitegemea , siwezi kukifanya kichwa changu kiathiriwe na chakula”
“Also Mother, can yoo stop touching my head , I am not a kid anymore”Aliongea Rube huku akimwangalia Edna akimaanisha hataki kuguswa kichwa kwani sio mtoto.
Tabasamu ambalo lilikuwa katika uso wa Roma lilipotea na kujiambia huyu mtoto anamaanisha nini lakini hata hivyo aliondoa mkono wake kiabu aibu.
“Unaongea ujinga gani Rube , kwahio wewe ni mtu mzima kama sio mtoto?”Aliongea Edna lakini hata hivyo aliishia kugeuzia macho yake kwa pacha yake Rube yaani Nyromi na kumwangalia namna ambavyo alikuwa akinywa chai kimapozi kama vile ni Princess.
“Naomi! Why are still eating so slowly ? you will be late for school”Aliongea Edna lakini Naomi alitingisha kichwa.
“Mom , you told me to be a lady! A lady should not gobble down food or else I will look rude..”Aliongea kimapozi kwa jinsi alivyo ilionyesha atakuja kusumbua sana mbeleni kwa maringo.
“Mh , unajifanyisha mtiifu lakini mbona hukuwa hivyo wakati ukila keki zangu , hebu muone.. na ole wako nilete zigine uniibie”Aliongea lakini Naomi aliishia kumtolea Edna mdomo.
“Bi Wema hebu kaangalie haka katoto , kwanini kazaliwa kuwa adui yangu , kwanini ananifanyia hivyo asubuhi yote hii , akikua je , mimi nafanya nini?”
Bi Wema aliishia kutabasamu tu na aliishia kutingisha kichwa bila ya kumuunga mkono Edna.
Hata hivyo alikuwa ashazoea na tabia za hao wawili , Naomi yeye alikuwa tofauti kabisa na dada yake Lanlan ambae alikuwa akipenda kujali mambo yake lakini Naomi atahakikisha anafanya kila kitu kumkasirisha Edna.
“Haha…”
Roma ambae alikuwa amesimama floor ya juu akiangalia kinachoendelea alishindwa kujizuia na kucheka na kumfanya Edna ainue macho yake na kumwangalia kwa ukali.
“Unacheka nini , vaa nguo zako kama umeamka , unadhani unaonekana vizuri ukiwa na hio boksa tu?”
Roma aliishia kutingisha kichwa kwa haraka huku akimnyooshea kidole gumba Naomi .
Roma hakuwa na haraka , mara baada ya kurudi chumbani aliingia kwenye jakuzi na kufurahia maji ya moto na mpaka anakuja kutoka Bi
Wema alishaondoka kupeleka watoto shule.
Ukweli ni kwamba alikuwa akishinda huko huko maana Roma akili za watoto wake alikuwa akizijua hivyo hakutaka watoroke.
“Honey , hivi unadhani Naomi atasumbua sana akishangia katika ule umri .. kulea sio kazi rahisi , mwenyewe hapa nikimfikiria Rube kichwa kinauma .. yaani kila siku atakimbilia kwenye maabara ya Clark utadhani ndio mama yake ,mpaka najiuliza isije ikawa Clark anampa madawa , inakuwaje kuwa na mtoto aina yake ,,, Hey! unafanya nini?”Edna kabla hata hajamaliza kulalamika alijikuta akibebwa juu juu na Roma.
“Hubby naomba tuache..nataka kwenda kazini”
“Babe Edna wewe ndio umekosea, nani kakuambia uanze kulalamika kuhusu watoto asubuhi yote hii , mimi niliona namna ambavyo unafurahisha kama mama nakujikuta nikitamani mtoto mwingine”
“Ah … basi nitaacha , acha kwanza niende kazini
, unajua leo tunapaswa kwenda kuandaa mazingira kwa ajili ya harusi ya Ashley… napaswa kuandaa zawadi…”
“Ushachelewa.. zawadi tutafuta wote…”Edna alijitahidi kujitetea lakini haikuleta maana tena.
“Basi tufanye kwa nusu saa tu .. usizidishe baada ya hapo ?”
“Unaonaje dakika arobaini..”
“Hapana , nusu saa tu”
Roma aliishia kusugua mano yake na kujiambia vyovyote vile nitafanya tu , pengine anaweza kunogewa na kusahau muda.
Dakika arobaini baadae Edna ndio ambae alikuwa hataki Roma aondoke mapema , alikuwa akihema kama vile roho inataka kumtoka lakini licha ya hivyo alijihisi yupo ulimwengu mwingine.
Upande wa Roma alikuwa kama mnyama ambae hachoki na alipeleka moto kisawa sawa , walianzia kitandani mpaka sakafuni na hatimae masaa mawili yalipita.
Edna baada ya kumaliza hakutaka kuendelea kubakia hivyo , alijua amechelewa lakini alihitaji kwenda kazini.
“Umeona sasa nimechelewa , ni makosa yako”Alilalamika Edna huku akikwepesha macho kidogo na Roma huku akijitahidi kufunga vifungo vya shati lake.
“Unataka kufanya nini?”Aliuliza Edna akirudi nyuma mara baada ya Roma kushika shati lake tena huku akivifungu vile vifungo.
Roma hakuongea na Edna alikuja kugundua alikuwa amekosea kufunga vifungo hivyo kiasi cha kuvipishanisha, kitendo kile kilimfanya
Edna kumwagalia Roma kwa macho ya mahaba.
“Nenda sasa kafanye kazi ukiwa mpya ..”Aliongea Roma mara baada ya kumaliza kuweka nywele za mke wake vizuri pamoja na koti lake.
Edna alipepesa macho kidogo na kisha alipanua mikono yake na kumsogelea Roma na kisha akambusu kwenye lips.
“I love you so much Honey” Edna aliongea huku akitabasamu na macho yake yalivyokuwa ni kama vile anataka kulia lakini haikuwa hivyo.
“Nakupenda sana mke wangu , nina furaha sana kuwa na wewe,Na ibarikiwe ile siku niliokudhania…”Kabla Roma hajamalizia alifinywa , Edna hakutaka kabisa kusikia kauli ya kudhaniwa kahaba , hata hivyo kila kitu kilikuwa wazi siku ile akili yake ilikuwa na mdudu.
“Tutaelekea wote kwenye harusi ya Ashley, baadae unifuate tukaangalie nguo zetu”Aliongea Edna na Roma aliitikia kwa kutingisha kichwa akiwa na tabasamu lakini ni muda huo huo simu ya Edna iliita.
“Nimechelewa , Matilda anapiga simu , Bye Honey”Aliongea Edna akimaanisha Mkurugenzi wa kampuni ya JR anapiga simu, kampuni ya JR chini ya uongozi wa Matilda iliweza kufanya vizuri mno , yote hayo ni baada ya Matilda kufuata ushauri wa Edna.

MWISHO
ASANTENI KWA KUIFUATILIA MWANZO MWISHO , KWA AJILI YA REFERENCE NITAFUTE WATSAPP 0687151346


ALL APRECIATION TO MY MENTOR : Ron Timm -PATH OF DAO.(Ingia google search ' Path of Dao' ,nstagram@pathofdaoqiqong).

INSPIRED BY MY ALL TIME FRIEND: LUANG JIZI(A.k.a flatbread)

SPONSORED BY : VOLAR MEDIA
 
Ndugu Mtunzi Hii Riwaya hata ungeipeleka kwa Wahariri hakika wangekurudishia ukafikirie upyaa

Mimi ni mpenzi wa Riwaya za aina Zote,nimefanikiwa Kusoma Riwaya nyingi sana na katika simu yangu nina Soft copy ya Riwaya nyingi na zote huwa nasoma nukta kwa nukta ila hii yako nimesoma naona haishi matukio mengi yasiyo na maana ikabidi niende kusoma hitimisho tu na nikaona hitimisho ni lile lile nililoliwaza

Ili uwe bora lazima usome Kazi za wenzako kwa waandishi wa sasa hivi kuna bwana wa kuitwa GEORGE IRON MOSENYA jaribu kutafuta Riwaya zake mbili tatu mfano za kumuhusu GEZA ULOLE uone na Simulizi za kijasasi zinatakiwa kuwa na sio hii ujinga unayo hangaika nayo Inatakiwa Riwaya usome sio ikuchoshe ila ikuchangamshe zKo zinachosha tuu hadi unahisi Homa......


Badilikaaa mas

Watu wamezoea simulizi za kimalaya malaya zisizo na faida yoyote.

Hii simulizi ukiisoma vema utagundua mambo mengi sana yanayozunguka maisha ya binadamu katika picha isiyoonekana.

Bahati mbaya kuna watu mnasoma kama burudani na kina mini tunasoma kama kuongeza maarifa ya mambo fulani fulani na hii simulizi haina burudani yoyote kama sikosei tangu naanza kuisoma mimi nimecheka sehemu moja tu ya amina kuwa mbweha wa mikia.

Singano jifanye kiziwi na kipofu tupia mwendelezo atakayesoma asome atakayeacha aache.
Fact.
 
Watu wamezoea simulizi za kimalaya malaya zisizo na faida yoyote.

Hii simulizi ukiisoma vema utagundua mambo mengi sana yanayozunguka maisha ya binadamu katika picha isiyoonekana.

Bahati mbaya kuna watu mnasoma kama burudani na kina mini tunasoma kama kuongeza maarifa ya mambo fulani fulani na hii simulizi haina burudani yoyote kama sikosei tangu naanza kuisoma mimi nimecheka sehemu moja tu ya amina kuwa mbweha wa mikia.

Singano jifanye kiziwi na kipofu tupia mwendelezo atakayesoma asome atakayeacha aache.
Endelea kuongeza maarifa yakakufae maishani[emoji3]
 
Kama mnawapenda hawa waandishi wa namna hii washaurini wawe wanazipeleka kwa Wahariri kabla hawajazileta kwa wasomaji
 
Kama mnawapenda hawa waandishi wa namna hii washaurini wawe wanazipeleka kwa Wahariri kabla hawajazileta kwa wasomaji
Tatizo lako wewe ni old school na tabia yenu kubwa ni kukariri , unadhani simulizi ndefu haziwezi kuhaririwa , hebu tumia hio simu yako kuingia hata Amazon kindle kuna simulizi zina episode 5000 ujifunze funze acha kuishia kuangalia makalio ya malaya ununue kama ulivyojinadi.
Kwa taarifa yako hii simulizi ipo kwa mhariri tayari na ina ISBN number.
Sema wazee wengine bwana mnajifanya wajuaji ila Exposure ndogo mno[emoji706][emoji706]
 
Moja kati ya Riwaya za HOVYO na Kipumbavu kuwahi kusoma ni hii...Riwaya ndefuu haina kichwa wala miguu,,mtunzi anajaza matukio mengii mradi iwe ndefu isio na tija

Elfu 10 yangu nililopa bora ningenunua Malaya tu nipunguze uzito
Kwsni ulilazimishwa mkuu! Ulipoona anazingua ungeachana nae ukafanya mambo mengine
 
Tatizo lako wewe ni old school na tabia yenu kubwa ni kukariri , unadhani simulizi ndefu haziwezi kuhaririwa , hebu tumia hio simu yako kuingia hata Amazon kindle kuna simulizi zina episode 5000 ujifunze funze acha kuishia kuangalia makalio ya malaya ununue kama ulivyojinadi.
Kwa taarifa yako hii simulizi ipo kwa mhariri tayari na ina ISBN number.
Sema wazee wengine bwana mnajifanya wajuaji ila Exposure ndogo mno[emoji706][emoji706]
Huenda hata ni kipofu huyu mzee anasomewa ndio maana haelewi. Mambo yalivo
 
Nice story ever!
Nimeupenda sana mwisho wake
Kumbe Athena na ukauzu wake bado alikuwa anamkubali mwamba [emoji23][emoji119]
Kaka singanojr ...Mungu akuweke sana mkuu, unajua mpaka kesho kutwa [emoji110]
Sema kule kwa Hamza, tunaomba hata episode Moja kwa siku ili twende vzur [emoji120]
 
Singano jr ilikua story nzuri na mwisho wake umekua Bomba Sana uandishi ni karama sio kila mtu anayo na sio kila mtu ni targeted audience wako but for me nmekua your number one fan keep it up father
Kuna mmoja kashindwa kuuelewa uzi kaishia kulalamika ni mrefu sana kumbe kazoea simulizi za kimalaya malaya.

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom