Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Unaweza kusema hii ni story tu lakini ina asilimia kubwa za uhalisia wa Maisha ya binadam na Viumbe wengine (Creatures of universe).

Kwa asilimia kubwa matukio yanayotokea kwenye simulizi hii yanatokea pia kwenye dunia yetu hii ya Leo. Hapa unasikia habari za kupanda Level kwa Majini, hii Scenarial ina apply pia kwa binadama kwa asilimia nyingi. Mwili wa binadamu ukiwa msafi kimwili na kiroho huwa kuna ufunuo unakujia wa uelewa na uwezo fulani wa kufanya mambo katika Maisha.

Mfano:
1) Mtoto mdogo anapo balehe huwa anapata ufunuo(anapanda level) wa kujitambua (Biologicaly) na napata uwezo mkubwa wa kiakili.

2) Kijana aliyebalehe akitoa bikra(kufanya tendo kwa Mara ya kwanza) huwa anapata ufunuo(Anapandanda Level)

3) Kijana huyo akifikia umri fulani anapata ufunuo mwingine (Anapanda levo) na kupata uwezo wa kubeba majukumu fulani na hata kuanzisha familia.

4) Pia unapofikia hatua ya mtu mzima/ mzee huwa napata ufunuo (kupanda level ) unajawa na busara na Maono.

Sasa kinachotokea ni kwamba tuna vitu vingi mno vinatutoa kwenye reli (Distractions) na kushindwa kupata ufunuo mkubwa zaidi na kuwa na uwezo wa kufanya mambo makubwa hapa duniani Mfano: Ngono zembe(Uchafu wa kiroho) ,Pombe, Vyakula vibovu, matumizi yaliyopitiliza ya Teknologia, kukosa Mwongozo wa Misingi ya Maisha ya Mwanadamu na Mengine Mengi.

Binadamu Tuna uwezo wa kimaajabu ila wajanja wanaojua hizi siri wamezificha na wanatuwekea vizuizi tusijitambue kwa Wingi.

"The greatest Potential, Strength and Powers of Human being are hiden within us, Within our Mind"
The greatest Potential, Strength and Powers of Human being are hiden within us, Within our Mind"
 
Kama vitabu gani mkuu unaweza kuweka list hapa?
Vitabu ni vingi, we angalia au fiatilia vitabu vinavyoelezea stories za ancient world toka China, Greece Egypt and the Ancient civilization hizi hadith zote utazikuta huko. Haya wewe ukipendezwa na moja unaweza ukatafsiri na kuleta hapa.
Anza na www.allnoveljr.com utaikuta hii inaitwa UNDERSTATED DOMINANCE by Marina Vitolli au you just Google it utamkuta jamaa anaitwa Justin mambo kama ya Roma Ila yeye hana sifa😃😃
 
Achana na hizo porojo, eti dunia tambarare. Sasa singanoJr anao uwezo gani wa kuthibitisha hilo zaidi ya astronomical evidence zilizopo?
Sina maana aelezee kwa kuthibitisha.. ila aweke kisa kinachoendana na Imani ya wale wanaoamini Dunia tambarare! By the way ni maoni tuu! Unaweza kukosoa pia! Maana napenda kujifunz
 
Nashukuru kwa Elimu hii kiongozi
Unaweza kusema hii ni story tu lakini ina asilimia kubwa za uhalisia wa Maisha ya binadam na Viumbe wengine (Creatures of universe).

Kwa asilimia kubwa matukio yanayotokea kwenye simulizi hii yanatokea pia kwenye dunia yetu hii ya Leo. Hapa unasikia habari za kupanda Level kwa Majini, hii Scenarial ina apply pia kwa binadama kwa asilimia nyingi. Mwili wa binadamu ukiwa msafi kimwili na kiroho huwa kuna ufunuo unakujia wa uelewa na uwezo fulani wa kufanya mambo katika Maisha.

Mfano:
1) Mtoto mdogo anapo balehe huwa anapata ufunuo(anapanda level) wa kujitambua (Biologicaly) na napata uwezo mkubwa wa kiakili.

2) Kijana aliyebalehe akitoa bikra(kufanya tendo kwa Mara ya kwanza) huwa anapata ufunuo(Anapandanda Level)

3) Kijana huyo akifikia umri fulani anapata ufunuo mwingine (Anapanda levo) na kupata uwezo wa kubeba majukumu fulani na hata kuanzisha familia.

4) Pia unapofikia hatua ya mtu mzima/ mzee huwa napata ufunuo (kupanda level ) unajawa na busara na Maono.

Sasa kinachotokea ni kwamba tuna vitu vingi mno vinatutoa kwenye reli (Distractions) na kushindwa kupata ufunuo mkubwa zaidi na kuwa na uwezo wa kufanya mambo makubwa hapa duniani Mfano: Ngono zembe(Uchafu wa kiroho) ,Pombe, Vyakula vibovu, matumizi yaliyopitiliza ya Teknologia, kukosa Mwongozo wa Misingi ya Maisha ya Mwanadamu na Mengine Mengi.

Binadamu Tuna uwezo wa kimaajabu ila wajanja wanaojua hizi siri wamezificha na wanatuwekea vizuizi tusijitambue kwa Wingi.

"The greatest Potential, Strength and Powers of Human being are hiden within us, Within our Mind"
 
Sina maana aelezee kwa kuthibitisha.. ila aweke kisa kinachoendana na Imani ya wale wanaoamini Dunia tambarare! By the way ni maoni tuu! Unaweza kukosoa pia! Maana napenda kujifunz
Ok nimekuelewa, sorry for misconception
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZ: SINGANOJR

Mono no aware ILIPOISHIA:
Roma alivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha aliinama chini na kumkumbatia Lanlan na kumbusu shavuni na kisha akasimama na kumwnagalia Edna. “Mpenzi ni….”
“Usije ukathubutu ”
Kabla hata hajamaliza sentensi Edna ashabwatuka na kumnyooshea Roma kidole huku akionyesha mabadiliko.
Uso wake ulikuwa siriasi mno na alionekana kuwa kauzu isivyokuwa kawaida , alikuwa ni barafu.
Mabadiliko yake na namna alivyofoka iliwaogopesha kila mtu ndani ya hilo eneo lakini palepale waliweza kuona kitu katika macho ya Roma.
Roma muonekano wake ulibadilika mno wakati akiwa anamwangalia mke wake , ilionyesha alikuwa na majonzi na hali ya kuomboleza kwa namna alivyokuwa akimwangalia Edna.
Ni sawa na pale unapomwangalia mpendwa wako akiwa hospitalini huku ukijua hana muda mrefu wa kuishi ndio namna Roma alivyokuwa lakini haikueleweka muonekano wake unahisia za namna gani.
“Lakini sijaongea chochote mke wangu…”Roma aliongea kwa kusita.
“Najua unachopanga kufanya hata usiponiambia , nakukataza kwenda kupigana na miungu Roma”Aliongea tena na kutaja jina la Roma kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu sana kuonyesha namna gani alikuwa akisisitiza , kwa jinsi alivyokuwa akiongea ni kama swala hilo halina mjadala.
Roma aliishia kukunja ndita , ijapokuwa siku zote alikuwa akiwasikiliza wnawake wake lakini akiamua lake hakuna wa kumzuia.
“Edna I have made a decision , take care of Lanlan , I’ ll came back as soon as possible”Aliongea Roma akimaanisha Edna mwangalie Lanlan kwani ashafanya maamuzi na atarudi mapema iwezekanavyo.
Edna alionekana kutetemeka na kauli hio na haikujulikana kutokana na woga wa Roma kuwa hatarini au hasira , ghalfa tu alisogea mbele na kumshika Roma mkono.
“Roma mume wangu naomba tafadhari usiende , Please don’t go , kwa ajili yangu na mtoto naomba usiende”
Edna alibembeleza na alikuwa amebadilika akiwa ameinamisha kichwa chake chini na ilikuwa ni kama vile anaogopa kukutanisha macho na Roma.
Lanlan aliekuwa akiangalia alikuwa aking’ata lips zake kwa wasiwasi kwani aliona muda wowote mama yake na baba yake watagombana hivyo hakuweza kuongea chochote, upande wa Roma aliishia kutoa kicheko cha kivivu mno.
“Nilikuwa na chembe ya kusita dakika chache zilizopita lakini sasa nadhani napaswa kwenda , kuna vitu napaswa kukabiliana navyo mapema au baadae..”
Edna mkono wake ulitetemeka na kinyonge sana alimwachia Roma na kupiga hatua moja kurudi nyuma.
“Naomba umwangalie Lanlan , napaswa kwenda Edna”Aliongea Roma na kisha alimshika Edna mkono kwa sekunde na kisha akauchia na akapotea palepale.
Upande wa Edna alikuwa ni kama mwanamke ambaye haamini kilichokuwa mbele yake , aliishia kukosa nguvu na kidogo tu angekaa chini , ilikuwa ni kama vile kitendo cha kumwachia Roma mkono ni kama vile alikuwa yupo tayari kwenye maisha yake kuacha kila kitu lakini sio kumwachia Roma lakni mwisho wa siku alikuwa amemuacha.
Wakati warembo wengine wakiwa na wasiwasi juu ya usalama wa Roma Edna yeye alionyesha hali ya huzuni kama vile hatomuona tena.

SEHEMU YA 780.
Ni katika ulimwengu wa majini watu ndani ya miliki ya Hongmeng , hali iliokuwa ikiendelea katoka miliki hio ilikuwa ni ya kutisha.
Yale majengo mazuri na makubwa ambayo yalikuwa fahari ya miliki hio yalikuwa yamebakia vifusi.
Eneo lote lilikuwa ni vumbi na michanga iliochanganyika damu na viungo vya miili , kilichokuwa kikionekana ilikuwa ni maana halisi ya eneo la vita.
Licha ya hali hio ya kusikitisha katikati ya eneo hilo upande wa angani kulikuwa na jengo ambalo limezungukwa na miale ya mwanga ambao mwezi sio mwezi ni kama mwanga wa platinumu ule ambao haujakolea .
Naam eneo hilo ndio linapatikana Gereza la Roho na majini pepo, ndio.sehemu pekee ambayo miungu wameshindwa kuiangusha kutokana na uimara wake.
Sasa katika safu hio ya ki ulinzi ya mwanga wa dhahabu wanaonekana watu wa tatu wakiwa wamesimama , ilikuwa ni kama vile wamefanya kazi kubwa sana na ishara flani za kukata tamaa zilikuwa zimegubika nyuso zao .
“Hepheastus una uhakika hii mbinu itafanya kazi??”Mwanamke mrembo Rozu kwa jina la kijini na Hera kwa jina la viumbe kutoka sayari nyingine aligeuka na kumwangalia Monk aliekuwa pembeni yake na kumuuliza.swahi hilo.
Mwanaume ambaye alikuwa na kipara alievalia Kissaya mavazi maalumu ya kimonk alikuwa ndio Master Yanyuni ambae mwili wake inaishi nafsi ya Hephaestus, nafsi kiumbe kutoka sayari nyingine ambae wasifu wake ni mungu wa moto.
Kwenye mikono yake alikuwa ameshikilia gurudumu la kuwaka waka ambalo lilionekana ni Dhana yenye maandishi ya herufi ambazo hazikutafsirika.
Lakini kama Sharif na Aoiline wangeona herufi hizo wangezitambua mara moja ni lugha ya wajumbe wa Mkuu wa Enzi, lugha ambayo ilitumika miaka mingi iliopita wakati wa wajumbe hao kufika duniani kwa misheni maalumu.
“Numekuwa katika hiki kisiwa kwa muda wa miaka mia tatu na niliishi kwa kufanya utafiti wa namna ya kuvunja hili gereza kila siku, Busara na hekima iliotumika kujenga sio ya kawaida na ni ngumu mno na hatuwezi kutumia nguvu kulivunja, hata kama tukiweza kutengeneza upenyo msukumo wa presha ndani yake utalifunga ndani ya sekunde tu, ukweli ni kwamba tukifanya hivyo kutatokea misukosuko ambayo itafanya ulinzi wake kuimarika zaidi, lakini nilikuja kugundua njia pekee ya kufanikisha hili ni wakati wa presha ya safu yenyewe kuwa chini na hii ni kwasababu ni kama herufi zilizowekwa ndani yake ni kama programu maalumu.Kwahio nilitumia miaka yangu mingi kukusanya vitabu vya kale ambavyo vina tafsiri mbalimbali ya maandishi hayo na nilipo fanikiwa ndio nikatumia miaka mia moja mingineyo kutengeneza hii Dhana nilioipa jina la Reverse Dhamachakra, Hii Dhana haiwezi kufungua hii safu ya ulinzi mara moja lakini inao uwezo wa kupunguza kasi ya ufanyaji kazi mpaka kwenye hatua dhaifu na hapo ndipo presha ya nishati iliopo ndani ya gereza itapungua na kumfanya Zeus kutoka”
“Hehe..mbona ni maajabu hivyo Hephaestus, kama umefanikiwa kwanini unaendelea kusimama? “
“Hatuwezi kuharakisha, nishaona kwamba muda muhimu wa kugeuka ni mchana na safu hii inakuwa haipo imara wakati huo kutokana na kujaa kwa wingi wa nishati chanya, itakuwa ni salama zaidi nikiingiza mfumo wangu wa Reverse Dhamachakra kwani tutakuwa salama muda huo”
“I don’t care about anything that you said as long as Zeus can come out soon. Humph. I don’t want that b*tch to be so arrogant”Aliongea Hera akisema hajali chochote ambacho amesema ilimradi Zeus aweze kutoka mapema... Anasema hataki yule mal*ya(Athena) kuwa na kiburi.
“Muone unavyoongea Hera, hata kama Zeus mpenzi wako wa zama akitoka hawezi kukufanya wa kwanza kabla ya Athena, siku zote nguvu inatawala, haina maana kuendelea kumuonea wivu, Kila kitu kipo usawa wa kiganja chake, ashakushinda muda mrefu tu”Aliongea Hermes na kumfanya Hera kumwangalia kwa ukauzu na wakati anataka kusema jambo mara alikunja sura baada y kuhisi kitu.
"Nilikuwa nimeboreka lakini kwa bahati nzuri kuna wapuuzi wamejileta hapa kujitafutia kifo" Aliongea Hera.
"Nitawaacha mshughukike nao maana ni ngumu mimi kupigana" Aliongea Hephaestus , mawazo yake yote yalikuwa kwenye Gereza hilo la Roho kwa ajili ya kumruhusu Zeus kutoka hivyo hakufikiria sana kuhusu binadamu.
"Hehe... hutopata nafasi hata hivyo hawa viumbe dhaifu hivi kuwachangia wote ni kupoteza muda"
Palepale Hermes mabawa yake yalichanua kwa kujitokeza kusiko julikana huku mkono wake ilionekana siraha ya Caduceus.
Waliofika hapo ni Anjiu na kundi lake la majini , walikuja hapo haraka sana wakiwa zaidi ya majini mia moja huku wengi wao wakiwa katika levo ya Maji ya Barafu.
"Sikuwahi kufikiria viumbe dhaifu kama nyie mtajileta kwenye uwanja wa kifo badala ya kukimbia" Aliongea Hermes
.Majini hao pamoja na baadhi ya binadamu wenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi walikuwa wamekasirika mno na kwa jinsi walivyokuwa wakionekana ilidhihirisha ni namna gani wapo kwa ajili ya kupigana kufa na kupona.
Macho ya Anjiu yalitua katika uso wa Monk Yanyu hususani katika kifaa alichokuwa ameshikiria mkononi na uso wake ulizidi kukunjamana.
"Ile Dhana ni Dhamachakra na imetengenezwa kwa kufanana na maelekezo ya herufi za safu ya ulinzi , hofu yangu kuna uwezekano wa Dhana hio kudhoofisha mfumo wa safu ya ulinzi , hatupaswi kuruhusu hilo litokee" Aliongea Anjiu akiwaambia wenzake, master Shagoni na majini wengine.
"Umeeleweka kwahio tinachopaswa kufanya ni kumshambulia huyo mzee na para lake"
"Yanyu wewe mshenzi mwanaharamu kabisa , siamini kama umepotoka kiasi cha kusaliti sisi marafiki zako wa zaidi ya miaka mia moja, leo ndio mwisho wa uhai wako"
Wale wa miliki ya Hongmeng ndio waliongea hivyo na waling’aka huku wakitoa Dhana zao kwa ajili ya kushambulia.
"Mnaongea ujinga"
Kabla ya Shombeli na kundi lake hawajashambulia , Hermes alikuawa tayari ashajitokeza mbele yao kufumba na kufumbua tu.
Dhana yake ya Cadeceus ilikuwa ikifanana na nyoka , ni kama alama flani hivi zinazotumiwa sana sana katika kutambulisha hospitali lakini muda huo zana hio ikikuwa ni Dhana kwani ilikuwa hai na macho ya nyoka yalikuwa yaking’aa kama rubi.
Dakika hio wale majini walijikuta wakinywea kama vile walikuwa wamegeuka na kuwa barafu , na kitu pekee walichoweza kufanya ni kuzungusha macho yao kama vile wanajichunguza kitu kilichowashikilia.
Lakini ilikuwa ni dakika hio hio waligeukana wao kwa wao na kuanza kushambuliana.
"Shit wameshalogwa na yale macho ya nyoka na kuchukuliana kama maadui"Aliongea Anjiu na palepale bila ya kuchelewa nguvu nyingi za nishati ya mbingu na ardhi zilimtoka na kugeuka moto wa radi ya zambarau huku ukiungana na moto wa kijini wa Ndege wa dhahabu wa miguu mitatu, hakuishia hapo tu aliita pepo lake la ndani la kijeshi na kuliruhusu kwenda kumvaa Hermes.
"Hehe... naona unapaniki wakati bado hata sijaanza "Aliongea Hermes na palepale alizungusha ile fimbo yenye nyoka wa kimaajabu juu hewani na kumtupia Anjiu ndoto ya ukichaa.
Anjiu alionekana alikwisha kujiandaa tayari kwani aliruhusu pepo lake kumlipukia Hermes mbele yake.
Boom!!
Ikiambatana na sauti ya kuumiza masikio mlipuko ule wa pepo la kijeshi ulitengeneza wingu flani kama vile ni milipuko wa fataki unaotoa moshi mweusi.
Ilitokea ndani ya sekunde tu palepale mlipuko ule ulijikusanya na kugeuka tena na kuwa kama kivuli cha moshi kinachofanama na jini Anjiu.
Lakini sasa ilionekana alichofanya Anjiu kilileta faida kwani Shombeli na wenzake ufahamu wao ulirudi na kuacha kushambuliana na kumwangalia Hermes kwa macho makali, lakinj wakati huo huo wakiwa na hofu mara baada ya kugundua walikuwa wametupiwa uchawi wa uchizi.
Uchawi wa Hermes pengine usingekuwa na madhara kwao zamani lakini mara baada ya kuamka kwa Moyo wa Gaia nguvu zake zilizidi nguvu ya kiroho ya nishati za mbingu na ardhi ndio maana aliweza kuwachanganya.
"Tsk..Tsk..Huwa sipendi mtu kuharibu mipango yangu"
Bila kutarajia Hermes alitokeza nyuma ya Anjiu akiwa na sura iliokunjamana kwa hasira ile nyoka iliokuwa kwenye Dhana yake ya Cadeceus ilikuwa ni kama imepata uhai na ilipanua mdomo wake kama Cobra na kumlenga Anjiu kichwani.
Ni muda huo huo wale majini walipata kuelewa Hermes waliekuwa wakimuona mbele yao hakuwa uhalisia bali macho yao yalikuwa yakiwadanganya.
Hali hio ilikuwa ni uthibitisho kwamba uwezo wake ulikuwa mkubwa kuliko majini wote waliokuwa hapo.
Anjiu uso ulimfubaa kwani adui yake spidi yake ilikuwa ya juu sana kiasi cha kushindwa kumkwepa mapema.
Dakika ileile nguvu za kijini zilitoka na Aura ya siraha iliokuwa katika rangi ya bluu ilijitokeza kutoka kusikojulikana , ilikuwa kama vile ni wimbi la sauti kwani siraha ile ilikusanya nguvu kubwa na kumshambulia yulq1e nyoka.
"Madaraja 27 ya nafsi ya upanga ,Mpasuko wa kibuli!!"
Ilikuwa ni bahati kwa Anjiu kwani Shagoni alikuwa makini kuangalia kilichokuwa kikiendelea nyuma ya Anjiu na kumzuia Hermes na shambulizi lake.
Hermes mara baada ya kuona nyoka wake alikuwa amefyekwa na kusambaratishwa kwa kugeuzwa poda alionyesha namna gani hajapendezwa na jambo hilo , ijapokuwa nyoka wake alipona haraka na kujitokeza katika Dhana yake lakini bado ilimkasirisha kwani shambulizi lile lilikuwa ni kummaliza Anjiu moja kwa moja lakini likafeli.
"Una spidi kali ya kushituka"
Aliongea Hermes lakini pale umbo lake ni kama linagawanyika kutengeneza mazingara ya sura yake danganyifu kila mahali , ilikuwa ni ngumu kujua ni yupi ni uhalisia.
Shagoni na siraha yake ya kimaajabu ilizunguka hewani na kutengeneza Aura ya bluu katika mzunguko mkubwa na kushambulia yale mazingara ya sura ya Hermes kwa spidi kubwa.
Majini wengine pia hawakubakia kuangalia kizembe kwani walitumia uwezo wao wote kudili na yale mazingara ya sura.
Hatimae Hermes halisi aliweza kutokeza tena .
"Hivi mnadhani mnaweza kunishinda kwa kunichangia kimashambulizi?"Aliongea Hermes aliekuwa juu zaidi hewani akiwaangalia majini hao kwa chini na tabasamu la Dhihaka. "Madaraja 32 upinde wa Aura ya mchomoo!!!" Bila ya kusita Shagoni alirusha siraha yake ambayo iliweza kutoa mng'ao wa rangi nyekundu , alikuwa ameunganisha Aura ya siraha ile pamoja na nishati za mbingu na ardhi na kufanya itengeneze joto kali kama la kuchomelea chuma .
Siraha ile iliokuwa kama upinde ilimsogelea Hermes kwa kasi na kumchoma kwa kutoboa mwili wake ndani ya sekunde tu.
Alitema damu nyingi huku akishangaa ameshindwa vipi kukwepa shambulizi hilo.
Mara baada ya pigo hilo kwenda kwa Hermes morali ya majini iliamka palepale na wengine walienda mbali hata kuanza kupiga makofi wakionyesha kwamba safari yao ya mapambano sio ya bure.
Lakini sasa kilichotokea ndani ya sekunde kilisinyaza mioyo yao.
Hermes aliinua kichwa chake haraka na kisha aliwaangalia kwa tabasamu ka kifedhili, na damu iliokuwa mwenye midomo yake ilipotea kimaajabu.
"Samahanini , lakini hii damu pia na yenyewe ni feki"
Kwa Shagoni aliona alikuwa amemshambulia Hermes na kufanikiwa lakini ukweli ni kwamba alikuwa ni kama yupo kwenye usingizi wa pono na anaota.
Haikuwa kwake tu majini wote walikuwa wakiona maluweluwe ya ubalisia wa Hermes , kila kitu kilikuwa ni udanganyifu.
Hawakuamini kama Hermes alikuwa na uwezo huo wa kutengeneza udanganyifu na kuwaotesha ndoto kila mmoja.
Hera ambae muda wote alikuwa akiangalia pambano alionekana kuboreka na alitaka na yeye kuingia vitani.
"Vizuri , Mercury inatosha sasa kuwachezea akili waue wote"
"Hehe Hera lakini bado sijamaliza kucheza , haifurahishi kuwaua wote kwa haraka" Aliongea Hermes.
"Kama hutofanya hivyo nitawaua mwenyewe"
Tabasamu la kishetani lilijichezesha kwenye lipsi zake na palepale ghafla tu ulionekana upinde mkubwa wa dhahabu kwenye mikono yake.
Ulikuwa ni upinde ambao haukuwa na kamba kama ilivyo kwa upinde bali kulikuwa na kitu kama uzi wa moto uliokuwa umejifunga katika ncha zote za upinde na kutengeneza kitu kama kamba na kutoa msisimko ambao haukuwa wa kawaida , kwa haraka haraka kwa majini ambao wana elimu kubwa wangeweza kugundua ni Dahana ya Wajumbe wa mkuu wa enzi .
"Oh! Hapana , huo si upinde wa Dhana ya machweo!!?"Moja ya jini mzee levo ya maji ya kiroho aling'aka .
"Siamini macho yangu Panas kutoa hio hazina kwa msaliti"
"Hakuna aliejua nafsi ya miungu inaishi ndani yake , ni udhalimu wa namna gani huu!?"
Dhana hio inaitwa upinde wa Uungu wa Machweo , inasemekana ilipewa jina hilo na majini kutokana na uwepo wa malaika(mjumbe wa mkuu wa enzi) wa zama hizo ambae alitumia upinde huo kuzamisha jua kwa kulishambulia na mshale unaotoka katika upinde huo..
Majini wa jamii ya Panas wanaamini Hoyi Malaika mkuu ndie aliekuwa akihusika kuleta machweo yaani kuzama kwa jua.
Sasa hizo ni imani tu kama imani nyingine kwa majini , sasa Dhana hio ilikuwa ni kama urithi kwa majini wa jumba la kifalme huko miliki ya Panas , ijapokuwa kwao ni Dhana ya kiimani wanaamini nguvu yake imeshuka kutokana na kuharibika lakini hata hivyo ni Hazina ambayo mrithi aliefuatia ni Rozu.
Sasa Dhana hio ilikuwa na nguvu kubwa mno licha ya kwamba nguvu yake imeshuka.
Moja ya tabia yake kubwa Dhana hio ni kwamba inao uwezo wa kufanya mashambulizi yasiokuwa na kikomo ya kiroho .
Kama ilivyo kwa maji ya upako kuathiri roho ndio tabia ya upinde huo na nguvu yake ni mara mbili ya levo nishati za mbingu na rdhi kwa mtumiaji na kwa anaeshambuliwa.
Kwahio ni kama.Dhana hio ilikuwa na uwezo wa kuharibu kila kitu.
"Natumia Dhana ya majini kushambulia majini , nadhani utakuwa mwisho wenu mzuri"Aliongea Hera huku akitoa tabasamu la dhihaka na mikono yake ilishikilia ule uzi wa upinde na kuvuta.
Dakika ileile ule upinde ulianza kukusanya kiasi kikubwa cha nishati ya mbingu na ardhi na hali ya joto ndani ya eneo hilo ilizidi kuongezeka na ghafla tu mshale wa moto rangi ya Dhahabu ulionekana na kuanza kutishia kuunguza anga kwani ile sehemu ilicheza cheza kama vile ni gesi inayosamba angani.
Tukio hilo linaweza kuonekana la kitaratibu sana lakini lilitokea ndani ya sekunde tu na kufanya majini wote kuwa na wasiwasi.
Swoosh !!!.
Sauti ya mkato ya kitu iliweza kusikika na palepale mshale ule ulishatoka katika ule upinde ukimlenga jini mzee aliekuwa katika levo ya maji ya upako.
Mzee yule wa kijini alionekana kujiamini kupambana na ule mshale kwani alikusanya kiasi kikubwa cha mbingu na ardhi na ilionekana alikuwa akipanga kukwepa kwa wakati mmoja.
Lakini sasa akiwa katika kiwewe aligundua hakuwa na uwezo wa kusogea kwa namna yoyote ile kila alipojaribu kufanya hivyo.
“Inawezekana vipi hii!!
Alijikuta akimaka ndani kwa ndani huku akiangalia mshale ule ukimsogelea na hatimae kumfikia na kumtoboa.
Mshale ule mara baada ya kumtoboa yule jini haukupita bali uligeuka kama moto na kuunguza kila kitu na ni ndani ya sekunde tu jini yule aligeuka cheche zilizosambaa angani.
Majini walioshuhudia tukio lile walikumbwa na hofu isio na kifani.
Ukweli ni kwamba licha ya mshale wa upinde huo kuwa na nguvu lakini kama utafanikiwa kukwepa huwezi pata madhara na ndio mbinu pekee ya kupambama na Dhana hio.
" Ni ujinga kiasi gani mnao , yaani unajiona jini wa levo ya maji ya upako unaweza kushindana na nguvu ya kanuni za anga??" Aliongea Hera kama vile yule jini hajafa.
Hermes aliishia kuchezesha ulimi wake tu huku akizungusha kichwa , kikawaida alikuwa ashajua Hera ametumia kanuni za anga kumshikilia yule jini asisogee ili mshale wake umshambulie.
Kwahio ilimaanisha Hera alikuwa akirusha mshale kulenga shabaha ambayo haisogei.
Mara baada ya kuona kazi yake ni njema alitoa tabasamu la kifedhuli huku akiwaangalia Shagoni na Anjiu.
"Umekuja hapa kwa ajili ya kuongoza watu wako
katika kifo , je unajiona unaweza , nawaonyesheni namna gani maisha yenu hayana thamani kwa kujitia ujasiri mbele ya sisi miungu"
Mwishoni mwa.sentensi yake alianza kucheka kama kichaa lakini hakutingishika hata kidogo.
Dakika ileile alianza kutengeneza mishale ya moto na kuendelea kuwashambulia Anjiu na wenzake .
Mishale hio ilikuwa ikitoa sauti kama ya makombora na kusambaratisha majini.
Ijapokuwa walikuwa katika levo ya maji ya barafu kupanda lakini mbele ya Dhana hio ya upinde wa machweo hakuna ambae alikuwa na kinga.
Hawakuweza hata kujitengenezea vizuizi kwani waliishia kuungua na moto lakini hata hivyo walikufa huku wakionyesha hawakuwa wakijutia maamuzi yao ya kuja kupambana.
Muonekano wa Anjiu na Shagoni ulikuwa katika hali ya kusawijika , ijapokuwa hawakutegemea kushinda udogo wa uwezo wao zidi ya miungu ulikuwa ni nje ya fikra zao.
Uwezo wa Hera pekee unaweza kukadiriwa kama utaufananisha na mbinu za mbingu na ardhi kufikia levo ya mapigo mengi ya radi au juu kidogo , alikuwa na nguvu kuliko majini watu wote.
Yaani miungu wengine hawakuhitaji hata kuingia kwenye mapambano Hera pekee anatosha kusambararisha jamii hizo zote.
"Ni kweli tupo hapa kwa ajili ya kifo . je hii ndio hatima ya jamii yetu kuwa na mwisho mbaya hivi??"
Mawazo mbalimbali yalipita katika akili zao , hata kwa Anjiu ambaye alikuwa amepitia uzoefu mwingi kwenye maisha yake hakuweza kusaidika zaidi ya kuwa mnyonge mbele ya hatari iliokuwa mbele yao.
Ndani ya dakika chache tu majini karibia wote walikwisha kuuliwa na kubakia wasiozidi kumi na mbili akiwemo Shombeli , Anjiua , Umini na baadhi ya waliokuwa na uwezo wa juu lakini hata hivyo hakuna aliethubutu kushambulia.
Madhaliliko na aibu haikutosha kuelezea hisia zao wakati huo , ilikuwa ni zaidi ya majonzi ni kwa namna gani walikuwa dhaifu.
"Ni kwa bahati mbaya show ndio inakaribia ukingoni , mmefurahi ?, Hehe.. naona mmebakia wachache sana na hamuwezi kuniondolea hamu yangu ya kuua”.
Baada ya kuongea hivyo upinde wake alieulekezea kwa Anjiu.
"Unaweza kuleta ukinzani lakini kwangu ni kama mtoto mdogo anaeanza kutambaa"Aliongea Hera.
Mwishoni mwa sentensi yake aliachia mshale ambao ulikuwa na nguvu kubwa kuliko yote aliokuwa amerusha mwanzo.
"Whoosh!!
Anjiu alifumba macho yake kana kwamba alikuwa akijaribu kuvuta kumbukumbu nzuri za maisha yake yote wakati huo akisubiria kifo.
Lakini sasa palepale ulisikika mngurumo kama wa radi huku upepo wa ajabu ukifyeka lile eneo na ajabu kwao ni kwamba Anjiu alionekana mzima.
Moto ule wa mshale ulipotawanyika ndipo walipoweza kuona kuna mtu amesimama mita kadhaa alipo Anjiu "Romaa..!!!" Majini walimaka
"Hades" Miungu ilimaka.

END OF SEASON 26.

NILIEMDHANIA NI KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI : SINGANOJR

Mono no.Aware.

SEASON 27.

SEHEMU YA 781.
Miungu walikumbwa na hali ya mshangao mara baada ya kujua mgeni aliefika hapo alikuwa ni Roma Ramoni Au Hades.
Ni muda huo huo waliweza kumuona akishusha mkono chini , ilionekana alitumia mkono wa kulia kuzuia shambulizi hilo.
"Seriously ? Nimechelewa kwasababu nilikuwa nikifikiria kuhusu maisha lakini naona kuna majini wachache sana waliobakia , ni nini hiki , kwanini nyie watu mnaua fasta fasta namna hii , ni tofauti kabisa na kwenye filamu za mapigano ,
au ndio tuseme mmejifunza kutoka kwangu?"Aliongea Roma katika mawazo yake.
Isitoshe athari za kujitokeza kwake haukuwa mkamilifu.
Lakini kwa bahati nzuri wale wakubwa walikuwepo na Roma aliona kama Hera atawaua kutoka wa hadhi ya chini kwenda juu basi atakosa mahali pa kulilia.
“Hades, what is the meaning of this?”Aliuliza Hera akimaanisha hio ni maana gani lakini kwa muonekano wake ni kama hana nia ya kukaa chini na kuongea na Roma yaani alikuwa kishari zaidi.
"Wewe ndio Hera? ,Tsk , Tsk siamini ni nafsi nyingine ya miungu inayoishi ndani ya jini yenye kubeba chuki ya wazi , sio mbaya angalau wewe kuliko huyo popo mwenzako Hermes .... U’mrembo kupindukia , naona ulichagua mtu mzuri kwa ajili ya kuuvaa mwili wake ,kama sio nafsi yako kuishi ndani ya huo mwili pengine miliki ya Panas ingejipatia mkwe wa matawi ya juu"
"Unaongea nini wewe?" Aliuliza Hera ambaye alionekana kukasirika.
Alijiuliza huyu mtu katokea wapi na kuanza kuongea ujinga.
"Relax. I’m just joking to lighten up the mood. It’s too tense here.”Aliongea Roma akisema anachangamsha hali.
"Hehe..Hades acha kumtania Hera , uwezo wake unalingana na wa Poseidon ,hivyo nakusihi kufikiria kwanza ni kiwango gani cha uwezo Poseidon amepona , umekuja kufanya nini hapa , weka wazi??"Aliongea Hermes.
"Sio swala kubwa lililonileta , nimeona tu nyie watu mmesababisha matatizo ya kutosha na hakuna haja ya kuendelea kwenda mbali"
"Oh , kwahio unapanga kufanya nini??"Aliuliza Hera.
"Nilikuwa nikisubiri sana uongee hivyo , nilikuwa nikiwaza kuwakusanya wote kwa pamoja na itakuwa vizuri zaidi na Athena akiwepo ili tujadiliane namna ya kurudisha hali kawaida katika meza ya mazungumzo , kwanza tutapaswa kuzingatia namna ya kuzuia joto kutoshuka zaidi na zaidi , kwasababu watu wengi watapotea na isitoshe kuwa na dunia ya barafu haifurahishi na muhimu zaidi nitatoa wapi nyama kwa ajili ya binti yangu kama wanyama wote watapotea?, pia hatupaswi kuhusisha binadamu wa kawaida katika hili , hebu tukaeni chini sisi kwa sisi na tuone ni kwa namna gani tutapata suluhu , mimi nitabakia neutral ili mradi nitaona kila upande umepata haki, sitaki kumsaidia yeyote , mnaonaje je mpango wangu ni wa akili ??"
Maneno ya Roma yalionekana kusababisha miungu hao kuwa na muonekano usioelezeka , tofauti na kuita mpango huo ni wa akili wao waliona ni wa kijinga.
"Hades kama upo hapa kucheza , tafadhari rudi kisiwani kwako na ukaendelee na maisha yako ,
vinginevyo tutaamini wewe ni msaliti wa sisi miungu kwa kuamua kuungana na binadamu"Aliongea Hera.
"Hey hii ni mara yetu ya kwanza kukutana , kwanini kuongea maneno ya kuudhi hivyo, ,si nishawaelezeni hakuna haja ya kwenda mbali kama haifaidishi pande zote" Aliongea Roma akiwa na tabasamu.
"Acha kuongea ujinga , una chaguzi mbili , kwanza kaa pembeni na angalia bila kuingilia , pili tusaidie kuua hili kundi la viumbe wenye sura mbaya".
Muda uleule presha ya mwanamke huyo iliotokana na nguvu za kanuni za anga ilimtoka na kuzingira eneo lote , Anjiu na wenzale walijikua wakiwa katika mshangao mara baada ya kugundua hawakuwa na uwezo hata wa kutingisha vidole.
Hio ndio ilikuwa nguvu hlisi ya kanuni za anga ambayo miungu walikuwa na uwezo kuitoa kwa kutumia ufahamu wao wa kiroho.
Hermes na Hephaestus wote walionyesha nyuso za majigambo kana kwamba walikuwa wakiamini uwezo wa Hera unatosha.
Ilikuwa ni kwasababu ukiachana na Zeus na Athena , Poseidon na Hera ndio miungu waliokuwa na uwezo wa juu zaidi kuliko wengine wote.
Hata Hades wa zamani hakuwa na uwezo wa kumshinda Hera , sasa kwa Roma ambae alirithi nusu ya uungu wa Hades alikuwa hatoshi kabisa kushindana na Hera.
Kuhusu uwezo wa Hera wa nishati za mbingu na Ardhi hawakufikiri sana kwani Hera ni kama anaunganisha uwezo huo pamoja na uwezo wa kanuni za anga kitu ambacho kinamfanya moja kwa moja kuwa juu ya Roma hata kama amepitia mapigo mengi ya Radi.
Gepu dogo tu katika uwezo huo ni kubwa mno na haliwezi kuzibwa kirahisi.
Roma alipata kuonyesha muonekano wa kusumbuka na aliishia kulamba lips zake mara mbili , wakati kila.mmoja akionesha hali ya wasiwasi yeye alivuta pakiti ya sigara kutoka hifadhi ya pete na kuiwasha.
Mara baada ya kuiwasha aliweka taratibu mdomomi , ilimchukua sekunde chache tu kutoa sigara na kiberiti, ilimpa.shida kidogo kuwasha sigara kutokana na upepo na baridi lakini alifanikiwa.
Roma palepale alipiga pafu la moshi na kisha akalimeza na kulitoa puani .
Majini wale ambao walikuwa katika hali ya kujikatia tamaa walijiuliza huyu mtu amekuwa addicted kiasi gani na sigara mpaka kuwaza kuvuta muda huo wa hatari bila ya wasiwasi. "Haha.. msinifikirie vibaya , sio kwamba nipo addicted na sigara bali ni kwamba nina wasiwasi sana nyakati hizi , hivyo navuta ganja kidogo kujituliza"
[emoji769]Hades achana na maswala yako ya kujitakia umaarufu, umefanya vya kutosha na ni muda wako wa kurudi" Aliongea Hermes.
Roma aliishia kulamba lipsi zake kidogo na kisha alivuta pafu mbili za moshi na akatupa ile sigara huku akitoa moshi mwingi puani kama gari moshi na kuwaangalia kwa muonekano uliosawijika.
"Kama nilivyosema mwanzo mnapaswa kuacha mambo yenu ya kutesa binadamu mara moja"
"Do you truly believe I won’t attack you, Hades? The Gods’ revival is unstoppable, and no one is allowed to stand in its path!”
"Unadhani siwezi kukushambulia Hades? ,Ufufuo wa miungu hauzuiliki na hakuna wakusimama katika njia yake".Aliongea Hera.
Roma uso wake ulibadilika palepale na kuzidi kuwa mweusi na mara ileile msisimko wa kimauaji ulimvaa na alianza kuogopesha na hakukuwa na tone la utani katika macho yake , alikuwa amebadilika tofauti sana na mwanzo.
"Wewe Ajuza , nimekuita Hera kwasababu nilikuwa nikijaribh kuonyesha heshima , hupaswi kutokunielewa ilihali hatujawahi kuonana , jina langu ni Hades lakini ukiachana na hilo naitwa Roma Ramoni , Naongea tena ni aidha muache mara moja na tuongee au niwaue wote tuone kama hata mtaweza kuhamia katika miili mingine ,nadhani huelewi jambo moja , sijaja hapa kwa ajili ya mazungumzo wala kubembeleza mtu...Maneno yangu ni sheria ya mbingu na kama hutaki kutii kufa .."Miungu wote walijikuta wakipauka kutokana na hasira anazoonesha Roma.
"Ukaidi huu , unathubtu vipi kuongea na mimi namna hio ilihali ni binadamu mdhaifu uliepata nusu ya uungu wetu, hakuna wa kukuokoa leo hii , na nakwenda kukuonyesha ni kwa namna gani huna umuhimu wowote kwetu"Aliongea Hera kwa hasira.
Anga kumzunguka Roma ghafla tu lilibebeshwa kurasa za anga zaidi ya elfu moja huku Hera akijaribu kufanya shambulizi kwa kutaka kumfunga funga Roma.
Wakati huo huo ile Dhana ya upinde wa machweo katika mikono yake ulikuwa umeshikia mshale wa moto kumlenga na ulikuwa na nguvu mara nne ya alivyokuwa akishambulia majini.
"Nenda!!"
Mshale ule uliomlenga Roma eneo la moyo uliachiliwa na kuwa kama vule ni boriti ya mwanga wa laser inamsogelea kwa kasi.
Kutokea mwanzo mpaka mwisho Roma hakuwa amesogea hata inchi na akiwa na macho yake angavu aliangalia namna mshale ule unavyotoka katika upinde ule kumsogelea.
Lakini sasa sekunde tu ambayo mshale ule ulionekana kuufikia mwili wake radi ya rangi ya silver ilionekana kulipuka kutoka katika mwili wake kama shoti.
Boom!!
Nguvu ya mshale ule wa upinde wa Dhana ya machweo ulinywea mara baada ya kukutana na nguvu halisi ya radi yenye nguvu mara elfu moja kasoro moja na kusambaratishwa kabisa.
Unachopaswa kuelewa hata radi ya zambarau tu ni hatari sana mbele ya miungu sembuse nguvu ya radi hio ya silver , radi ambayo ni adimu sana kuonekana duniani imetoka katika mwili wa Roma kwa namna ya ajabu hivyo.
"Ni radi ya rangi ya Silver !!! ..Haiwezekani, umewezaje lujua siri ya radi ya aina hio?" Hera alionekana kuhamaki asiamini anachokiona,ule utukufu wa neema yake ya ki uwezo ilimpotea palepale.
Ilikuwa ni kama vile hakutarajia Roma anaweza kupanda levo haraka namna hio.
Walikuwa na mbinu za kupambana na radi ya zambarau lakini nguvu ya radi ya mapigo mengi ni kama hawakuwahi kuifikiria, hata kama uwezo wao unaweza kufikia ule wa Zeus au Athena.
Roma alipiga hatua moja mbele.,.muonekano wake ni wa kiutawala zaidi , kana kwamba alikuwa akimiliki ulimwengu wote na anao wezo wa kudhibiti kinachotokea kati ya mbingu na ardhi.
Ni dakika hio hio ni kama wingu juu angani limeitikia wito na lilijikusanya kwa kasi na kuanza kuzunguka huku mingurumo ikiwa ni ya juu sana.

Zile kurasa elfu moja za vizuizi vya anga ziliungua kama vile karatasi inavyoungua na kusambaratika.
Radi ya mapigo mengi ilianza kuomyesha mbwembwe zake juu mawinguni na wingu lilianza kushuka chini kwa kasi kama kimbunga na kutishia kuharibu kila kiumbe kilichopo chini yake.
Hera hali ya wasiwasi na ya kusita ilimvaa na hakuweza kufikiria tena kupambana na Roma ambae uwezo wake ni kama vile anatawala viumbe wote.
"Hephaestus usisubri tena fanya sasa hivi na kwa haraka"Aliongea Hara.
Hephaestus mungu wa moto alielewa amri na palepale alisogelea safu ya gereza ile sehemu dhaifu na kuchomeka Dhana yake ya Reverse Dhamachakra kwa ajili ya kumsaidia Zeus kutoka.
Shombeli na wenzake walikumbwa na wasiwasi mara baada ya kuona Yanyu anachotaka kufanya na kuanza kumpigia makelele Roma.
"Mzuie .., Mzuie haraka anaharibu safu ya ulinzi huyo"
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI : SINGANOJR

Mono no aware
ILIPOISHIA

SEHEMU YA 782.
Roma hakuwa ameweka umakini wake katika safu ya ulinzi wa Gereza la Roho na alikuja kushangaa mara baada ya kugundua Hephaestus alikuwa na mpango wake.
Bila ya kusita tena aliruhusu boriti ya shoti ya radi ilioshuka kutoka juu na kwenda kumvamia Hephaestus na Dhana yake ya Reverse Dhamachakra.
Kama miungu hao watatu wataamua kulinda Dhana hio wangeweza kupigwa na radi hivyo alijua hawatasogea mbele karibu na uelekeo wa pigo la radi lakini ilionekana hakuwa sahihi.
Hera alikuwa amesogea na kuzuia ile radi kwa kusimama mbele yake
"Haogopi kufa??" Roma alijikuta akishangazwa na kitendo kile cha Hera. na kujiuliza ni kweli Hera anachagua kifo kwa ajili tu ya kumuokoa Zeus kutoka katika Gereza hilo la roho , maana kama radi hio itamuua wakati hajachagua mwili ni ngumu tena kuhamisha nafsi yake.
Lakini sasa sekunde iliofuata ilimshangaza Roma.
Ni mwanga wa Dhahabu uliotokea katika eneo ambalo amesimama Hera , ilikuwa ni kama vile kuna mtu ameibukia mbele ya Hera wa rangi ya Dhahabu na kupokea mapigo yale ya radi.
Hera mwenyewe ambae alikuwa na muonekano wa kiwewe alionekana kupona katika radi ile na kwenda kuibukia nyuma ya Hephaestus.
Roma palepale aliweza kuona kilichosababisha mwanga ule wa miale ya Dhahabu ni kutoka katika kitu kilichokuwa kikifanana na sanamu lenye kufanana kabisa na Hera ndio dakika ambayo Roma alipata kufikiria kitu na kupata ufumbuzi wa tukio lile.
"Golden Apple!? You used the Golden Apple!?” Aliongea Roma akimaanisha Je Hera katumia Golden Apple.
Katika hadithi za miungu wa kigiriki inasemekana Mother of Earth yaani Titani au Gaia alimpatia Hera Tunda la Rangi ya Dhahabu la Shufaa(Golden apple) kama zawadi ya ndoa yake na Zeus.
Sasa katika hazina ambazo zimetajwa kuwa na umuhimu mkubwa katika hadithi za kigiriki moja wapo ni hazina hio ya tunda la.dhahabu la shufaa , inasemakana ni tunda ambalo linatokea kila baada ya miaka elfu moja.
Lakini sasa unachopaswa kuelewa stori hizi zilipandikizwa na hawa viumbe kutoka sayari nyingine kuonekana kama ni za dunia lakini katika uhalisia ni vitu ambavyo vilitokea katika sayari yao , mara baada ya kufika duniani ili utamaduni wao kutokusahaulika ndipo walipopandikiza stori hizi kwa wagiriki na kuzisambaza.
Sasa tunda hilo halikuwa tunda kama tunda bali ni kitu kama Dhana ya moyo ambayo inao uwezo wa kuokoa mtu maisha yake.
Sasa haikueleweka je ni kweli Hera alikuwa na Hayo ma'golden apple mangapi lakini ukweli ni kwamba kama utataka kumuua kabisa na kuizimisha nafsi yake huwezi kufanikiwa kirahisi labda tu umuue mara elfu moja , ushawahi kusikia Paka ana roho zaidi ya moja basi ni sawa na kwa Hera, hilo tunda hudumisha Roho yake mara mia zaidi.
Sasa kitendo cha Roma kutofanikiwa kumuua Hera ilifanikisha ile Dhana ya Reverse Dhamachakra kuingia kwa kufanikiwa katika eneo Dhaifu kwenye safu hio ya ulinzi, ki ufupi ni kwamba Roma kachelewa kwani mpango wa Hephaestus kutumia Dhana hio umefanikiwa na kazi ni Zeus mwenyewe kutoka.
Saa hio hio safu ile ilianza kufanya kazi isivyokawaida , ilikuwa ni kama vile umeme wake unaosababisha mwanga ni hafifu hivyo kufanya miale kuwaka na kufifia kwa wakati mmoja.
Majini walijikuta wakishikwa na hali isioelezeka lakini hata hivyo hawakuwa na chochote ambacho wanaweza kufanya na waliishia kuangalia Safu ya ulinzi wa gereza hilo ikiyumba kwa huzuni.
"Safiii, Mfumo wa uendeshaji wa safu unaanza kupoteza nguvu , kwa nguvu alizokuwa nazo Zeus ataweza kutengeneza upenyo na kutoka mapema tu" Aliongea Hephaestus.
" Hehe ni kwa bahati nzuri nilihifadhi kete ya dharula"Aliongea Hera na kisha akamgeukia Roma na kumwangalia na muonekano usioelezeka na kisha akaendelea kuongea.
"Hades, although your strength caught us off guard, you still can’t stop us! Once Zeus is out, he’ll surely defeat you!”(Hades ijapokuwa uwezo wako umetuzubaisha lakini bado huwezi kutuzuia , baada ya Zeus kutoka ni uhakika atakushinda).
Roma alikuwa akifikiria kitu kingine kabisa , wakati alipokuwa katika ulimwengu wa majini pepo master Chi alisema mtu ambae alikuwa akimuwinda ni mwanamke mtaalamu wa hali ya juu na wakati alipokuwa akitaka kumezwa na mnara alitoa kitu cha Dhahabu ambacho ni kama kilimuokoa.
"Ilikuwa ni wewe uliemuwinda mkufunzi wangu master Chi na kujaribu kuiba mbinu ya Andiko la urejesho wa azimio??'
Roma alikodoa macho mara baada ya kuona alichowaza kina ukweli asilimia kubwa , kwa maana hio ni kama Hera alikuwa ashatengeneza uadui na yeye muda mrefu.
Kama ilipangwa kwake kuweza kuingia katika levo ya nafsi basi pengine alikuwa na deni kubwa kwa Bi Zenzhei lakini likija swala la Master Chi deni lake lilikuwa kubwa zaidi kwani ni kama ndio alimfikisha alipo wakati huo.
Ijapokuwa Roma hakuwa mwanafunzi rasmi wa Master Chi lakini alimchukulia kama mtu muhimu zaidi katika maisha yake.
Hivyo hakuwa tayari kukubali kuona huyo mwanamke ndio alietaka kumuua Master Chi.
"Oh! Naona umekwisha fahamu , je inamaanisha tayari ushakutana na yule binadamu maskini ,Haha kwahio vipi sasa kama ni mimi , kama asingeweza kutoroka kwa bahati tayari ningeweza kupata mbinu ya andiko la urejesho usio na kikomo na usingeweza kuleta ubabe wako leo hii"
"Nani alikuambia kuhusu mbinu ya andiko la urejesho ?"Aliuliza Roma
Mwanzoni Anjiu alisema kuna mtu wa maajabu ambae alimtumia ujumbe kwa siri juu ya mbinu ya andiko la urejesho lakini mpaka.siku hio hakuweza kumjua alikuwa ni nani , sasa alijiuliza je ni hata kwa Hera imetokea hivyo hivyo.
"Sioni haja ya kukuambia lakini kwa jinsi ulivyomjinga sijali kukuonea huruma , Sio mtu mwingine bali ni Athena"Aliongea Hera
"Nini??"Roma alijikuta akishangaa.
Unachopaswa kujua ni kwamba mbinu ya andiko la urejesho tokea mwanzo ilikuwa ni siri na hakuna hata majini walioifahamu.
Mbinu hio inakuwa siri kwasababu Roma yeye mwenyewe ndio aliipatia jina kwa kuiita Andiko la urejesho wa Azimio mara baada ya Master Chi kumwambja aiite atakavyo kipindi walipokuwa mafunzoni katika jangwa la Gobi..
Hivyo ni sawa na kusema hakukuwa na majini wowote waliojua mbinu hio iliitwa Andiko la.urejesho wa Azimio , kama ni hivyo ilimaanisha mtu aliekuwa akimjua nje ndani alivujisha siri
"Haha.. usishangae .."Hera alicheka kwa kebehi na akaendelea.
"Mbinu ya Andiko la urejesho unayotumia ni mbinu iliokuwa ikitumiwa na binadamu wa maajabu mtaalamu wa hali ya juu ambae ndie aliewatega Athena na Zeus kuingia katika Gereza la roho miaka elfu ishirini iliopita , ni mbinu ambayo tulikuwa tukiitafuta kwa zaidi ya miaka elfu ishirini.Tuliamini njia pekee ya kumshinda yule mtu ni kufungua code juu ya mbinu hio ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi , ijapokuwa Athena ana nguvu ya unabii , kadri mtu anavyokuwa na nguvu ndio inavyokuwa changamoto kwake kumtabiria kesho yake kwa usahihi , hatimae mara baada ya kugundua juu ya mbinu hio alikuja kwangu na kuniambia mimi kama.jini juu ya taarifa hio , ijapokuwa ilikuwa ngumu kwangu kupokea kitu kutoka kwa Athena kama zawadi sikuwa na sababu ya kuona fursa hio inapita , Master Chi alionekana shabaha nyepesi wakati huo kuliko wewe , hivyo angalau shukuru sikukufuata wewe"
Roma alijikuta akikunja ngumi kwa hasira,ijapokuwa alikuwa ashaotea muda mrefu lakini alikasirika zaidi na zaidi mara baada ya kujua Athena alikuwa nyuma ya kila kitu.
"Kama unataka kulipiza kisasi kwangu fanya hivyo , vinginevyo sisi tunaondoka "
Aliongea Hera kwa Kiburi na kuwapa ishara Hephaestus na Hermes kuondoka.
Hawakuwa na haja ya kumsubiri Zeus kutoka kwani angetoka kwa wakati wake.
Pembeni Shombeli na wengine walimkemea Roma katika sauti zenye wasiwasi.
"Roma hatuwezi kuwaruhusu waende , Gereza ndio linakaribia kupoteza nguvu na uwezo wetu hautoshi kurekebisha , kama tutasubiri Safu ya ulinzi kudondoka na Zeus kutoka pamoja na maelfu ya majini pepo wabaya waliofungiwa ndani hatutokuwa tena na uwezo"
"Acha watoke wote nitawaua mmoja baada ya mwingine"Aliongea Roma akiwa na tabasamu la.kimauaji na.mara baada ya kuongea hivyo aliwaangalia wale miungu kwa kebehi.
"Kwasababu mnakuwa wakaidi kunisikiliza ilihali na waongelesha kwa amani , basi msijelaumu nikiondoa mizizi yenu katika huu ulimwengu"
Bila ya kusubiri miungu hao kuelewa alichokuwa akimaanisha na Roma aligeuka na kuwa radi ya rangi ya silver na kupotea kama flash kuelekea upande wa Kaskazini.
"Sh*t! Is he going to the Mother Tree!?”Hermes alimaka akisema. je anaenda ncha ya kaskazini ulipo mti mama.
" Hatuwezi kumruhusu aharibu mti mama tuondokeni" Aliongea Hera kwa kupaniki.
Miungu hao hawakujali kitakachotokea katika ulimwengu huo wa majini watu na kufumba na kufumba walipotea kuelekea Ncha ya kaskazini.
Majini waliangaliana kwa sekunde kadhaa na mwishowe na wao walisaga meno yao , katika hali kama hio hawakutaka kukimbia tena kwa namna yoyote ile hivyo waliamua kufuata nyuma.
Mara baada ya kila.mtu kuondoka hali ya ukimya ililereja katika kisiwa hicho cha anga.
Lakini sasa dakika hio hio kivuli cha mtu kiliweza kuonekana kikiibukia hewani ,alikuwa mtu alievalia joho la rangi nyeusi na mask ya chuma.
Mtu huyo hakuwa mwingine bali ni mtu mwenye mask wa maajabu ambae alikuwa ni mshirika wa karibu wa Athena ambae alikuwa akitii kila maagizo , mtu ambae alikuwa ndio mlinzi wa hatua za mwanzo za ufufuo wa Moyo wa Gaia.
Mara baada ya miungu kufika ncha ya Kaskazini kwa ajili ya kulinda yeye alipotea lakini kwa hali hio ilionekana alikuwa amejificha katika ulimwengu huo wa majini watu.
Mtu yule mwenye mask alitoa kicheko kikubwa cha kuumiza masikio chenye uovu ndani yake huku akiangalia safu ya ulinzi ikikaribia kuzima kabisa na presha yake kupungua.
" His Majesty, in no time, you will lead tens of thousands of my people to return to the human world. My mission is finally about to be accomplished…”
"Mfalme muda wowote ,utaongoza makumi elfu ya watu wangu kurudi katika ulimwengu wa binadamu ,misheni yangu hatimae inatimia .."Aliongea yule mtu mwenye mask isieleweke anamaanisha nini.
*****
Katika Ncha ya Kaskazini sehemu ambayo iliaminika kwa kuwa na barafu na Theluji inayosambaa , kilichokuwa kikionekana ni kama ndoto nyeupe.
Mti mkubwa wa Dhahabu ulioitwa Mother tree ni kama.vile ni nguzo ilioshikilia anga.
Ukubwa wa mti huo uliziba anga na matawi yalioenda mbali ni kama yamegusana na wingu.
Saa ambayo Roma alipata kufika alijikuta akishindwa kupumua vizuri kwa kiwewe cha mshangao , hakukuwa na vitu vya kumshangaza hapa duniani lakini ukubwa wa mti huo ulimwacha ndomo wazi.
Kawaida ujio wake haukuwa ule wa kujificha , wingu na ngurumo za kutisha zilizokuwa zikimsindikiza zilimeza eneo lote la ncha hio , hali ya hatari ilikuwa kama uvimbe wa jipu lililoiva na kitu kidogo cha ncha kinaweza kubadilisha kila kitu.
Radi ya rangi ya bluu na silver ilikuwa ni kama inamlaki Roma kwa kucheza cheza kuzunguka mwili wake ikisubiria wito wa kuharibu kila kitu.
Pengine kama ni kiumbe chenye imani dhaifu kingesujudu kwa kumuona Roma ndio muumba.
Hali ya kitisho aliokuwa akiitoa Roma pengine ni uthibitisho kamili wa uwepo wa Mungu mwenye nguvu isiokuwa na kikomo.
Kwa kiumbe yoyote wa kawaida kuona radi iliokuw aikicheza cheza kumlaki Roma ikishuka inamaanisha kifo.
Mapema tu baadhi ya watu walijitokeza umbali kidogo mbele yake.
Kulikuwepo na sura tano ambazo alizifahamu , mungu wa jua ,mungu wa mahaba, mungu wa mwezi , mungu wa bahari na mungu wa vita .
Wakati huo hali zao za kihisia katika macho yao ilidhihirisha ni kwa kiasi gani walikosa utulivu.
Nyuma ya Roma alisimama Hera , Hephaestus na Hermes ambao walikuwa wakimfukuzia.
Ukimjumlisha na Roma mwenyewe hatimae miungu yote tisa ilikuwa imejikusanya mahali pamoja chini ya Mti mama.
Anjiu na wenzake waliweza kufika pia lakini hawakuthubutu kusogea karibu na walichoweza kufanya ni kuangalia kwa mbali miungu hio na mti huo wa kushangaza.
Roma alikuwa ni kama bomu kubwa sana la nyuklia wakati huo na hakuna aliethubutu kumsogelea na wote walikaa mbali wakimwangalia kwa wasiwasi.
Roma hatimae macho yake yalitua katika sura ya mwanamke mrembo Christine na kumwangalia kwa macho yaliojaa uchungu.
"The thing you were hiding from me before was this tree? The decrease in temperature and the recovery and growth of divinity all happened because of this tree?”
"Kitu ulichokuwa ukinificha tokea mwanzo ni huu mti , Kushuka kwa joto la dunia na kupona na kukua kwa uungu yote yametokea kwasababu ya huu mti?" Aliongea Roma.
Venus(Aphrodite) uso wake ulikakamaa kidogo , ule urembo wake na mitego yake mbele ya Roma ilipotea kana kwamba anajua kinachokwenda kutokea.
"Hades, this is the Gaia’s Heart’s original appearance. This is the mother of us Gods, our origin—Mother Tree.”.
"Hades ,huu ndio muonekano halisi wa Moyo wa Gaia, huu ni mti wa uzao(mama) wa sisi miungu , asili yetu ...Mti Mama"
Roma alikunja ndita na kisha palepale.akasambaza uungu wake na ghafla tu aliweza kuhisi kitu na kufumba na kufumbua aliibukia katika eneo hilo juu ya tawi la mti huo .
Miungu wote nane walifuata nyuma huku wakimwangalia Roma kwa wasiwasi na tahadhari wakionekana kuogopa anaweza kufanya kitu .
Walijua fika hakuna yeyote mwenye uwezo wa kuhimili radi ya mapigo mengi anayotoa , hata kama watakuwa sawa hakuna uhakika kama Mti mama hautaathirika.
Roma macho yake yalitua juu ya tawi hilo na yalionekana maua ya rangi ya dhahabu yaliochanua kwa namna ya kuvutia macho.
Katikati ya moja ya ua lililokauka kulikuwa na kitu kama tunda ambalo lilikuwa likitoa mng'ao usiokera na nishati yenye kutuliza akili.
Tunda hilo lilikuwa dogo mno la mviringo , ijapokuwa udogo wake ni kama kidole gumba lakini kumesheheni nguvu kubwa ya uhai na nishati flani hivi ya kiroho.
"Huu ndio uungu?? "
Hatimae Roma alitambua tunda lile ndio uungu halisi wa miungu
Ijapokuwa nguvu yake sio kubwa kama ilivyo kwa uungu wao lakini hakukuwa na mashaka juu ya kitu hicho kuwa uungu halisi , zaidi ya yote ulionekana kuongezeka taratibu .
"Upo sahihi tunachukulia Mti mama kama Mungu mzazi na Gaia mama yetu kwasababu tulizaliwa kupitia ukuaji wa Mti mama , sisi ndio tulikuwa wa kwanza kuzaliwa kutoka mtini , uungu kumi na mbili kutoka kilele cha mti , tulipata kuwa miungu watawala kutokana na uwezo wetu kuwa na nguvu kubwa kuliko kizazi chote kilichozaliwa mbeleni , unachoona leo hii na kuhisi ni mwanzo mdogo kabisa mwa uungu , katika miezi sita ijayo au zaidi, uungu utakomaa na hatua za mabadiliko zitatokea na ndio mwanzo wa kuzaliwa kwa kabila la miungu pamoja na kuamka kwa makumi elfu ya nafsi zilizopotea "
Aphrodite alijua haina maana tena kumficha Roma hivyo aliamua kumwelezea kila kitu.
Ijapokuwa Roma alijua Moyo wa Gaia una umuhimu mkubwa kwao lakini sio kwa kiasi hicho.
Ilionekana alichokuwa akipambania Athena kufufua miungu ilikuwa ndio kama hivyo .
Kupitia mti huo wataanza.kuzaa miungu katika miili yao halisi mmoja baada ya mwingine na ndani ya muda mfupi dunia yote itajaa miungu.
Na ikifika wakati huo binadamu wasingeweza kabisa kukabiliana na kundi hilo la viumbe wenye uwezo wa ajabu wa kutumia kanuni za anga.

SEHEMU YA 783.
Roma alijikuta akiona alikuwa na chaguzi mbili pekee mbele yake , ya kwanza ni aidha awaache miungu watawale dunia au aharibu mti huo na kurudisha dunia katika hali ya kawaida kama mwanzo.
Yale maneno yake ya mazungumzo ya amani kwake aliona ni kama ndoto kufikia wakati huo.
Kwanini miungu hawakuweka juhudi kutafuta Moyo wa Gaia mapema iwezekanavyo tokea mwanzo kama mti mama ulikuwa na uwezo wa kuendeleza kizazi chao , zaidi kwamba Astreus sehemu ya viumbe hao alionekana kutumia Dhana ya Selene kwa ajili ya kuuhifadhi na kisha ukatoweka kusikojulikana.
Kama kweli uwezekano huo ulikuwepo basi haikuwa na sababu yoyote ya ku u'freeze' kwa kutumia Selene tokea mwanzo na hakukuwa na sababu ya miungu kupoteza miili yao , pengine wangevamia tu dunia na kisha kuuotesha na pale dunia ingeonekana kuwa salama.wangeshuka , Roma alijiuliza je kulikuwa na sababu ya Astreus kumuua mama yake na kutumia moyo wake wa barafu pamoja na Selene kuuhifadhi moyo wa Gaia , je kuna kitu alichokuwa akihofia.
Pengine walijua tokea mwanzo athari za mti huo ndio manaa walihofia kuufufua mapema.
"Tumekuwa tukikuchukulia siku zote kama mwenzetu Hades , ikiwa sasa tupo njia panda katika historia ya uzao wetu , tunaamini utakuwa upande wetu , si ndio?"Akiwa na muonekano wenye nia ya wazi Aphrodite aliongea.
Miungu hao walikuwa na aibu aidha kidogo au sana hususani Apollo na Artemis ambao walikuwa na ukaribu mzuri na Hades.
Upande wa Roma alionekana katika tafakari na aliishia kuzungusha kichwa chake kuwaangalia viumbe hao.
"Mimi ni wenzenu?.. haha..Hivi ni kweli mnanichukulia kama mwenzenu ilihali Moyo wa Gaia na huu mti wenye nguvu kiasi hichi ndio nauona leo??"
"Hades unapaswa kufikiria katika mtazamo wetu , hatukutaka kukuficha yote haya , tulitaka kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri"Artemis aliongea.
"Bullshit ,hivi mnadhani mimi ni mjinga?, sababu ya moyo huu kutoonekana kwa muda mrefu na kuhifadhiwa katika barafu na Astreus kwa zaidi ya miaka 20000 iliopita kiasi cha kuwafanya msiupate haraka ni kwasababu huu mti una haribu kila kitu , si ndio??"
Sura za miungu hio zilibadilika na kuwa mbaya huku wengi wao wakiwa na sura mpauko.
Mara baada ya kuona muonekano wao alizidi kuwa wazi juu ya mashaka yake.
"Kama nipo sahihi huu mti sio tu kwamba unanyonya nishati ya jua pekee lakini vilevile unafvyonza kiasi kukubwa cha elementi za madini katika kiini cha dunia , kulingana na hali ilivyo sasa ya kasi ya kushuka kwa joto ndani ya mwaka mmoja au zaidi itakuwa haiwezekani binadamu kuishi ndani ya dunia"
"Hata kama miungu mtaendelea kuishi ndani ya hii dunia , nishati za kidunia na nguvu ya uhai wa dunia itaendelea kunyonywa kwa kiwango kikubwa na huu mti na haitochukua muda mrefu dunia kuwa sayari ya Mars nyingine.
Nina uhakika mlikuja duniani miaka elfu ishirini iliopita kwasababu ya mti huu uliowazaa na kuwalea uligeuka na kuwa Janga la sayari yenu "
Kauli za Roma.ziliwafanya miungu sura zao kukunjamana , ilionekana makisio yake yote yalikuwa sahihi.
Mti huo wa Uzao hakika ulikuwa ndio janga la sayari yao.
Haikueleweka ilikuwaje mti huo ukachipuka katika sayari yao wala wao wenyewe hawakuelewa historia ya chimbuko la mti huo ila walizaliwa kutoka katika huo mti na kuishi chini ya kivuli chake na ndio mti huo huo waliamini uliwapatia uungu wa ufahamu mkubwa sana wa kuamini ni viumbe wa kipekee na wenye nguvu kuliko viumbe wote.
Lakini mwisho wa siku ni mti huo huo ulitoa uhai na kisha ukatwaa uhai.
Ilikuwa ni hali kama ya mama kutumia nguvu nyingi sana kufanya watoto wake wawe na nguvu lakini nguvu hizo zilijengwa juu ya uharibifu wa sayari.
Kwa lugha nyingine kadri miungu hao walivyokuwa na nguvu kubwa ya ufahamu kutokana na mti mama ndio namna ambavyo sayari yao ilivyoingia matatizoni.
Mara baada ya kuona hakuna neno lolote litokalo katika vinywa vyao Roma aliendelea kusemezana nao.
"Lazima mtakuwa mmekwisha kujua haya yote ndio maana mlisita kuufufua , nakumbuka kwa mara ya kwanza mlipoongea kuhusu Moyo.wa Gaia kuna wengi kati yenu mlioona Athena ni kichaa na mlikuwa na hofu kwasababu mlijua kama utafufuliwa Dunia itakuwa kama.Sayari yenu"
Wakati wa kuongea Roma aliwatazama Apollo na Dada yake na palepale.alikumbuka.muonekano wao mara baada ya kuuona Moyo wa Gaia katika mikono ya Athena kule Korea Kusini , sasa muda huo anakumbuka aliona ni rahisi kuelewa.
"Upo sahihi Hades ." Hera aliongea kwa kiburi
"Hades makisio yako yote ni sahihi hata hivyo unapaswa kufikiria kwanini bado tukaamua kufufua Moyo wa Gaia licha ya kujua nguvu ya uhai itaendelea kushuka kwasababu ya huu mti"
Roma alikunja sura hata yeye hakutaka kuamini kama ni kweli lakini kukiri kwa Hera ilimshangaza na kujiuliza kwahio bado wanataka kupoteza uhai kama ilivyokuwa kwa sayari yao .
"Hades ngoja nikuelezee kwanini , ni kwasababu kila sayari ndani ya Cosmos ina sapoti maisha kwa namna yake hivyo urefu wa uhai wake kutofautiana, uhai wa dunia unaweza kuwa mrefu katika mikono ya binadamu lakini hata kwa nyota kama jua itakuja kuzima mara baada ya kufika mwisho wake kama ilivyokuwa kwa mti wetu ,Dunia ikiwa katika mikono yetu miungu ni kweli uhai wake utapungua na kufikia nusu lakini je unadhani tunajali?"
"Binadamu ni toleo la mwisho la viumbe wenye ufahamu wasio na umuhimu wowote na hawastahili hii sayari ,dunia ni kama kito cha thamani sana cha kung'aa katika galaksi ambacho kinapaswa kumilikiwa na wenye nguvu ambao ni sisi miungu , ni sisi pekee ambao tuna uwezo wa kuibadilisha hii dunia kitu ambacho binadamu hawajui zaidi kwamba hata thamani ya sayari yao hawaijui."Aliongea Hera kwa kejeli na kiburi kikubwa mno zidi ya binadamu na akaendelea.
"Unlike the stupid humans who are still going through this elementary barbaric social system, developing this lowly and backward civilization, while at the same time, constantly polluting and wasting the resources of this planet… To put it bluntly, a bunch of bugs are not qualified to occupy a beautiful palace, do you understand?”
"Sisi sio kama binadamu wajinga wajinga ambao ndio kwanza wapo chekechea katika mfumo wa kijamii wa kishenzi, kuendelea taratiibu na kustaarabika kinyume kinyume wakati huo huo wakichafua na kupoteza rasilimali za sayari hii.. kwa ufupi ni kwamba kundi la kunguni halikidhi vigezo vya kuishikilia sayari hii nzuri, Unanielewa ??
Aliongea Hera na kumfanya Roma kushangaa kwani hakuamini mwanamke huyo angeongea matusi ya namna hio kwa binadamu.
Ingawa miungu mingine kwa namna flani hawajapendezwa na maneno ya Hera lakini hakuna aliempinga.
Waliamini tofauti na wao , binadamu ustaarabu wao ulikuwa nyuma sana na kama wao wangetawala dunia , ustaarabu wake utapiga hatua kubwa sana l.
Kurahisiha maneno hata baada ya miaka 20000 miungu hawakuwahi kujichukulia sawa na binadamu na maisha yao hapa duniani ni kama mchezo tu wa kuendana na mazingira.
Mwanzoni hawakusumbuka kuutafuta moyo wa Gaia kutokana na kwamba walikuwa katika maumivu makubwa ya kuooteza sayari yao na walikuwa na wasiwasi wa kuipelekea dunia kuoata janga kama la.kwao.
Bila.shaka pia wataalamu wa Dunia enzi hizo waliwaogopesha .
Wale majini waliokuwa wakiisikia maneno ya Hera kwa mbali walishikwa na hali isioelezeka.
Kwa wakati huo hawakujichukulia kama. majini wanaoishi ulimwengu unaojitenga lakini walijichukulia kama wawakilishi wa binadamu kwasababu hapo mwanzo walishaishi pamoja na dunia ni ya kwao pia.
Dharau za miungu zidi ya binadamu ziliwafanya kukasirika lakini hawakuwa na cha kufanya.
"Hades, Hera ameenda mbali sana na maneno yake lakin wewe ni mtu mwenye busara , unapaswa kuelewa kila kitu huamuliwa na sheria ya msituni , kama kweli binadamu hawastahili kufa tusingeweza kuwashikilia na vidole vyetu baada ya miaka elfu ishrini kupita
Binadamu ni dhaifu sana na hawawezi kutufanya chochote na haya yote yalishamauliwa na hatima yao ,hivyo unapaswa kuacha kufanya mambo kuwa magumu kwetu na wewe kama mmoja wetu tutakushirikisha katika utukufu wa ufufuo wa koo yetu"
Aphrodite alimsogelea Roma na kujaribu kumgusa gusa mgongoni kumtuliza.
Roma aliekuwa ameinamisha kichwa chake chini alifyatuka na kwenda kutua katika moja ya tawi akimkwepa Aphrodite.
"Inatosha sasa"
Aliinua kichwa chake na kisha kuwakagua mmoja baada ya mwingine , sauti yake ilikuwa nzito na isiokuwa na utani.
"I’m not interested in listening to all of your grand strategies to change the world, nor am I interested in listening to all of your laws of life that rely on eliminating the weak. I don’t want to say anything on behalf of humans, nor do I want to do something for them. I just want you to understand one thing…”
"Sivutiwi kusikiliza mikakati yenu mikubwa ya kuibadilisha dunia , wala.sivutiwi kusikiliza sheria zenu za maisha zinazotegemea kuwaondosha wanyonge , sitaki kusema chochote kwa niaba ya binadamu , wala sitaki kufanya chochote kwa ajili yao , ninachotaka ni ninyi kuelewa jambo moja .."
Muda huo Roma.mwili wake ulishaanza kutoa kiasi kikubwa cha nishati ya mbingu na ardhi iliobadilika kuwa radi ya Silver .
Radi hio ya mapigo mengi ilikuwa ni kama.mnyama mkubwa ambae muda wowote ataonyesha ukali wake mbele ya kitoweo.
"Mmefanya la maana sana kunificha juu ya hili kwasababu nina uharibu mti wenu sasa hivi ..."
Palepale radi nyingi sana ilijikusanya kumzunguka kana kwamba ni bomu la.nyuklia linajiandaa kushambulia mti wote katikati ya shina lake.
"Noo...!! "Miungu ilipiga makelele
Hata kwa mti huo kuwa na uwezo wake wa ki ulinzi ,ukali wa nguvu hio ya radi ungesababisha athari kubwa sana , bila.kusahau kulikuwa na miungu wengi ambao walikuwa katika harakati za kuzaliwa.
Kwa spidi kubwa sana miungu wote nane walisogea mbele kujaribu kumzuia Roma na kanuni zao za anga lakini radi ya mapigo mengi ilikuwa na hatari kubwa kiasi kwamba hakuna hata mmoja aliekuwa na uwezo wa kuizuia na mtego wao wa anga waliojaribu kumuwekea Roma ulisambaratishwa .
Miungu walikuwa wamemkaribia Roma lakini hakuna aliekuwa na ujasiri wa kumsogelea kwa hofu ya kufa.
Lakini sasa katika wakati huo wakiwa na sura za kukata tamaa na kutokuamini kinachokwenda kukumba mti mama lilitokea pazia kubwa la mwanga kutoka juu angani , ijapokuwa lilishuka taratibu lilifanikiwa kufunika eneo ambalo Roma yupo kwa nguvu kubwa sana.
Ilikuwa ni kama maputo ya hewa ya rangi ya silver yalioungana yamegongana na shoti za radi ile lakini ajabu ni kwamba hayakupasuka na kuendelea kung'ang'ania kwa muda mrefu mpaka pale rangi yake ilipofifia.
Roma alijikuta kikunja ndita mara baada ya kugundua radi yake ya mapigo mengi ilikuwa ikipungua ukali wake na radi yake ni kama inaakisiwa kurudi kwake.
Ijapokuwa isingemdhuru lakini ilikuwa ni wazi aliweza kujua radi yake.haina uwezo wa kufanya chochote juu ya kizuizi cha rangi ya silver kilichokuwa mbele yake, zaidi kwamba hakuwa mgeni wa ngao za namna hio.
"Aegis shield ..."Apollo na miungu wengine walionyesha ishara ya furaha katika.sura zao mara baada ya kuona mti mama ulikuwa salama.
"That was close! Did this b*tch have to show up so late!?” Hera kama kawaida yake alianza kumlaumu Athena kwa kuchelewa kufika huku macho yake makali yakianglia juu.
Athena alievalia gauni refu kama joho kitambaa cha hariri alionekana ,.alikuwa hajavaa chochote miguuni na nywele zake nyeusi zilipeperushwa na upepo..
Kama kawaida yake mambo yake ylikuwa ni ya kimya kimya., lakini licha ya kusimama hewani bila kufanya chochote iliwafanya watu kuhisi mkandamizo wa hewa wa kiwango cha juu kabisa huku akili zao ni kama zimeingiwa na mdudu.
Roma aliinua uso wake na kumwangalia , kama alivyotegemea Athena uwezo wake kwa kupitia Moyo wa Gaia ulikuwa umepanda juu sana kwa hali ya kuogopesha.
Kupitia presha ya nguvu za kanuni za anga , Roma alimkadiria ni uwezo uliokuwa mkubwa zaidi ya jini aliefikia mwishoni mwa Levo ya mapigo mengi ya radi , kwa makadirio ya haraka haraka aliamini pengine ni mwanzo wa levo ya mapigo elfu kumi ya radi kasoro moja.
Vinginevyo isingewezekana radi yake kuzuiwa kirahisi hivyo kwa Dhana yake ya Aegis.
Kilichokasirisha zaidi ilionekana bado hakufikia juu kabisa ya uwezo wake na kama.Moyo wa Gaia utakavyoendelea kufufuka atafika levo ya juu zaidi na zaidi pengine kuvuka levo zaidi ya mapigo elfu kumi ya radi.
Kama miungu wangekuwa katika uwezo wao wa juu kabisa mikaa elfu ishrini iliopita , matokeo yangekuwa tofauti leo hii.
Lakini hata hivyo Roma hakuona anaweza kusbindwa mapema hivyo , ni kweli uwezo wa Athena ulikuwa juu zaidi lakini alikuwa na kete zake mbili ambazo hajacheza.
Athena taratibu alishuka chini na kwenda kusimama mbele.ya Roma kwa mbali .
Wakati huo upande mwingine wa mbali Anjiu na kundi lake walikuwa wakitetemeka mno,mshituko waliopewa na Athena ulikuwa ni nje ya fikra zao.
"Hades, you shouldn’t obstruct the revival of our clan. It’s foolish to go against the natural law of the jungle"Aliongea Athena kikauzu akimaanisha Hades hapaswi kuzuia kufufuliwa kwa kabila lao na ni ujinga kwenda kinyume na sheria ya msitu.
Roma alimwangalia mwanamke huyo ambae sura yake na mwili wake vilitawaliwa na udanganyifu wa kimwonekano na hakuweza kuona sura yake halisi.
"Wewe ndio ulimwambia Anjiu na Hera kuhusu master na mimi kumiliki mbinu ya Andiko la urejesho wa azimio ?"
Miungu walijikuta wakishangaa mara baada ya kuona Roma ana muda wa kuuliza swali la namna hio ambalo halina umuhimu na hata kuonekana kutokuwa na hofu yoyote.
Haikujulikana kama Athena atamuacha aondoke kirahisi kwani bado alikuwa amezingirwa na pazia la.mwanga ambao ulitokea katika Dhana ya Aegis.
Athena aligeuza kichwa chake taratibu na kumwnagalia Hera.
Hera uso wake ulibadilika kidogo lakini aliishia kubetua midomo na kuangalia pembeni kwa jeuri na kumfanya Athena kutoa pumzi ya masikitiko na kumgeukia Roma.
"Haina maana tena , haijalishi ni mimi nilomwambia Hera au lah , kila kitu kilikuwa kikienda ndani ya matarajio yangu nipo tayari kukubali matokeo"
Ijapokuwa aliongea hivyo , kila aliekuwepo aliweza kuelewa ni Hera aliemchoma Athena kwa ajili ya kuibua ugomvi kati ya Roma na Athena.
Ushindani wa wanawake hao wawili haukua na tofauti na wanawake wa kibinadamu wawili wanaogombania mwanaume.
Isitoshe miungu walijua nguvu ya utabiri ya Hera ilikuwa ndogo sana hivyo kukosea kila wakati.
Ilikuwa ni sahihi kama alivyosema Athena haikuwa na maana tena na hakuwa akivutiwa na jambo dogo namna hio au kujitetea yeye mwenyewe.
Upande wa Roma na yeye alionekana kutokuwa na makasiriko na aligeuza macho yake kuangalia pazia lililomzunguka.
"Utaendelea mpaka lini kujaribu kunizuia kwa namna hii , kama.unabii wako ni sahihi , si angalau unapaswa kujua uwezo wangu wote?"Roma aliongea.
Miungu walikuwa katika mshangao washindwe kuamini kama Roma hajatumia uwezo wake wote na walijiuliza au uwezo wake ni juu ya mapigo mengi ya radi?.
Athena hatimae aliinua mkono wake na kwa maringo kabisa alichezesha vidole vyake na lile pazia la mwanga lilipotea na mwanga wa rangi ya silver ulimrudia katika.mwili wake na kwenda kuungana na ngao yake ya Aegis ambayo ilionekana kuongezeka nguvu yake kwa kukamilika na umbo la mwanga ule mbele ya Ngao ile ni kama umbo la nusu mtu.
Ilikuwa ni ngao kama.zile za ma'crusaders' wa zama zile kwa uzito wake , ilikuwa ni ngao ya rangi ya silver ambayo ina mchoro wa jani la mzeituni ambalo lilikuwa likitoa mng'ao wa mchanganyiko wa rangi ya bluu na majivu.
Kama utaangalia katika ngao hio kwa umakini ungeweza kuona mchoro wa kichwa cha Medusa , kiumbe wa enzi hizo ambae alikuwa na vichwa vya nyoka , mchoro huo ulikuwa katikati kabisa ya ngao hio na kufanya kuogofya.
"Naelewa kwamba kama utaamua kwa uwezo wako wote kuharibu Mti mama ninaweza nisikuzuie, na itakuwa nimepoteza muda wangu wote niliokuangalia uwezo wako ukiongezeka taratibu taratibu mpaka kufikia leo hii una uwezo wa kushindana na mimi , lakini jua ya kwamba kama utatumia uwezo wako wote kupigana basi mmoja kati yetu atakufa na kupotea, nipo tayati kutumia uungu wangu wote kulinda heshima ya Moyo wa Gaia na Mti mama "Ilishangaza, Athena alionekana kukubali uwezo mkubwa aliofikia Roma.
Miungu hawakuelewa kwanini Athena ambae uwezo wake ni mkubwa kuliko wa Roma.kutamka kauli hio.
Mkandamizo wa nguvu zake za anga ulipanda tena na matawi ya mti mama yalianza kutingishika kwa nguvu.
Dakika ileile moto wa rangi ya bluu ulishuka kutoka juu angani na kwenda kutua katika mikono yake na siraha kama mkuki wa ajabu wenye urefu wa futi tano uliotengenezwa kwa madini ya ajabu ambayo yalikuwa yakitoa mng'ao hafifu uliopinda pinda kama nyoka mkubwa ulionekana..
Kichwa cha mkuki huo ni kama vile kinaungua na moto wa maajabu na kufanya kionekane kama umbo lake linabadilika badilika , ilikuwa ni kama kichwa cha Cobra ambacho kinajiandaa kummeza mtu.
Hio ilikuwa ni siraha nyingine isioharibika milele inayomilikiwa na Athena ifahamikayo kama Pallas.
Kwa muda mrefu sana hakuwahi kukutana na mshindani ambae angehitaji kutumia hio Dhana kama siraha pamoja na ngao yake kwa ajili ya kupigana.
Inasemekana siraha hio iliitwa Pallas mara baada ya Athena kukosea na kumuua Pallas ,kiumbe jamii yao ambae alikuwa ni mungu wa bahari wakati akiwa mdogo.
Hata hivyo mtu aliehusika katika kutengeneza siraha hio ni Hephaestus mungu wa moto lakini kichwa cha mkuki huo ni kweli kiliunganishwa na kiumbe kichaa wa baharini huko Mars.
Kwa uwezo wa kanuni za anga aliokuwa nao Athena siraha hio inaweza kuwa hatari sana katika mapigano.
Miungu wote walikuwa katika muonekano usioelezeka mara baada ya kuona Athena ameshikilia siraha hio ya mkuki kwa mkono wake wa kulia na ngao kushoto.
Ni muda mrefu sana kumuona akichukulia mapigano siriasi namna hio na walijiuliza ni kipi Hades anacho mpaka kumfanya Athena kuwa siriasi namna hio.
Lakini.sasa kitu kisichokuwa cha kawaida kilikuwa kikionekana katika macho yao kana kwamba walihisi kuna kitu zaidi ya vita wanayotaka kuanzisha.
Roma aliweza kuhisi namna mshindani wake alivyokuwa na nguvu lakini wakati huo akili yake ilikuwa katika utulivu .
Kwa kuonyesha tabasamu hafifu macho yake yalionyesha hali ya utayari kana kwamba alishafanya maamuzi na alitoa pumzi nyingi na kuzishusha.
"It seems like a choice has to be made…” Aliongea Roma .
Lakini muda uleule wakati akijiandaa kutumia uwezo wake wote Athena alitoa sauti ya kumzuia.
"Subiri kwanza dakika moja"Sauti yake ilionekana kubadilika haikuwa ya kikauzu na ya kiadui kama.mwanzo.
"Nini tatizo , hautaki tena kupigana??"
Athena alionekana kuwa kimya kwa.muda , kwa kile kinachoweza kuelezeka kama hali ya kusita.
"Kama nilivyosema kama utatumia uwezo wako wote inamaanisha mmoja wetu atakufa lakini je upo tayari kuniona nikifa mbele ya macho yako?"Aliuliza Athena.
"Haha.. unamaanisha nini??"
Roma alihangaika kukwepesha macho yake na Athena , alikuwa akionyesha kumdhihaki lakini hakuweza kuishinda nguvu ya kutaka kuzidi kumwangalia uso wake ambao ni kama umefunikwa na kiwingu muda wote lakini licha ya hivyo ilifanya mtu yoyote kuhisi Athena ni mrembo bila ya kumuona.
Lakini palepale ili kumjibu Roma swali lake Athena aliamua kuonyesha muonekano wake.
Roma aliangalia uso wake kidogo tu tena kwa mbali na hakuona macho yake yalikuwa yakimdanganya , ilikuwa ni sura ya mwanamke mrembo ambae alikuwa akimjua kiasi kilichopelekea mshituko katika moyo wake.
Kwa miungu waliokuwepo ambao walikuwa wakiujua ukweli tokea mwanzo waliishia kukumbwa na huzuni juu ya Roma.
Lakini Hera na Hermes ni kama vile wanataka kumwambia Roma msemo wa 'kiko wapi' , yaani walikuwa na sura zenye tabasamu la dhihaka.
"Heh..haha..haha..ah""
Roma mwili wake ulitingishika , mabega yake yalishuka na kichwa chake alikishusha chini huku akitoa kicheko kwa namna ya kujicheka mwenyewe pengine kujidharau , kicheko ambacho unaweza kukitafsiri kama kilio , ilikuwa ni kama vile amekuwa chizi na aliishia kutingisha kichwa kama mtu asiekubaliana na ukweli.
Mwishowe macho yake yaligeuka mekundu na haikuchukua muda machozi yalianza kujitengeneza katika mboni zake.
Roma alikuwa akishindana na kilio cha kwikwi kwa kukizuia na kumfanya kuonekana kama kuna kitu kimemkaba kooni , alijitahidi kujizuia lakini alionekana kushindwa.
Hali ile ya huzuni , majonzi na maumivu kwenye macho yake iliwafanya baadhi ya miungu kama vile Aphrodite na Artemis kushindwa kuzuia machozi.
Hakukuwa na ishara ya huzuni wala furaha katika sura ya Athena na alichokifanya ni kupaa na kwenda kutua mbele ya Roma akiwa katika hali ya utulivu .
Muda huo Aegis na Pallas alikuwa ashavirudisha katika hifadhi na hio ni kwasababu alijua ameshinda vita.
Kma alivyotabiri tokea mwanzo haijalishi mwanaume huyo atapanda levo kiasi gani na kuwa na nguvu lakini mwisho wa siku hataweza kumshambulia.
Athena katika hali ya utulivu alimwangalia Roma ambae alikuwa ameficha kichwa chake kwa kuangalia chini akiwa katika hali ya maumivu yasioelezeka na palepale alichanua mikono yake na kuizungusha katika kiuno cha Roma huku mwili wake ukimwegamia.
“I knew it. I know you couldn’t bring yourself to hurt me, am I right?”
"Nilijua tu , nilijua hutoweza kuniumiza , si kwel ??"
Alinusa harufu ya marashi anayoyajua na kumfanya kuhisi kitu kimemkaba kooni na ghafla tu alimsukuma Athena mbali na mwili wake kwa mkono mmoja na kisha mkono huo huo ukashilia kidevu cha mwanamke huyo na kuzungusha kichwa chake kwa kumkagua.
Macho yao yaligongana , wakati ya Roma yakiwa ya hasira ya kwake ni kama maji ya barafu kwenye friji, ni sawa na kusema moto na barafu vimekutana.
Ilikuwa ni ngumu mno kuelezea hali aliokuwa nayo Roma.wakati huo, alijiona ni kama vile amegeuka kichaa lakini kwa wakati mmoja hakuweza kuendelea kuwa kichaa.
Athena hakuleta ukinzani wowote na alimuacha mwanaume huyo kumfanya atakacho.
Ukauzu wake , urembo wake ulikuwa ukitisha usiohimilika kwasababu ya mkandamizo aliokuwa akitoa lakini pia hadhi ya jina lake.
"E... Edna kwanini unanifanyia hivi , si nilikuomba ...ukae nyumbani na kumwangalia mtoto , Kwanini .. kwanini unafanya hivi.."Roma alijitahidi kumeza mate huku mkono uliomshikilia Edna ukitetemeka.
Ishara ya huzuni ilionekana hatimae kwa mbaali katika uso ambao ni kama haiwezekani , uso wa mrembo Edna , kope zake zilicheza huku mboni ya macho yake ikiwa katika eneo moja.
"Na mimi nilikusihi ..nilikuomba sana ..nilikubembeleza Roma usije ila hukutaka kunisikia"Aliongea Edna mara baada ya kung'ata lipsi zake.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR

Mono no Aware.

SEHEMU YA 784.
Roma hakuwahi kutamani maisha yake yawe ya udanganyifu au kwamba pengine asingekuwa wa ulimwengu huu hapa Duniani. Hata kama utoto wake ulikuwa mgumu zaidi, utu wake ulimhimiza kutotelekeza uhai.
Lakini katika wakati huo ishara hafifu ya kifo ilijionyesha katika macho yake , ni ishara iliokuwa katika muundo wa uchomvu wa mwili na akili , uchomvu uliokithiri na wasiwasi ulioanza kula mizizi ya vyanzo vya uhai katika mwili wake.
Udanganyifu , uongo na unafiki . Maisha yake ni kama yamepoteza muelekeo na maana sekunde ambayo mwanamke Athena alipoonyesha sura yake.
Roma alijikuta akimwachia Athena na kurudi hatua mbili nyuma kwa kujikongoja halafu akamwangalia mwanamke huyyo kwa uso kama wa mtu mjinga. Wote waliangaliana bila ya kusemezana neno.
Umbali mchache Aphrodite ambaye alikuwa akitoa tayari machozi alijikuta akimgeukia Artemis.
“Hades , he … he seems to have known all along?”Aliuliza mbona ni kama Hades alikuwa akijua muda mrefu.
“Nafikiri hivyo pia , kwa nilichowasikia , inaonekana Athena alikuwa akijua Hades alikuwa akifahamu kila kitu wakati ambao tulikuwa tukidhania tumemficha kisawasawa”Alijibu Artemis .
“Nyie Hera na Hermes ndio mliomwambia sio?”Aliuliza Poseidon huku akiwaangalia kwa macho ya ukali.
“Ni mimi , nilimwambia muda mrefu tu lakini kipindi kile sikujua kama aliweza kuniamini”Aliongea Hermes huku akitoa kicheko.
“Kwaniin ulifanya hivyo?”Aliuliza Aphrodite.
“Si kila kitu kipo wazi , hata kama Hades alijua angeendelea kufuata ramani aliowekewa na Athena kupita kwasababu nyepesi tu hakuamini ukweli niliomwambia , kama angemuacha Athena mara baada ya kujua hili ingemaanisha kwamba mipango yake yote imefeli tokea mwanzo, nyie hamuoni hili swala linasisimua , kumfanya kuwa na wasiwasi huku akiamini anachokiwaza hakiwezi kutokea hatimae kimetokea…”
“Hermes ulienda mbali sana?”Apollo aliongea akiwa amekunja sura.
“Huh! Mbali kivipi? ,nilichofanya ni kuongeza tamthilia kidogo tu na chumvi chumvi kwa mhusika mkuu , nyie wanafiki kama kweli mngekuwa mnamjali Hades kwanini mlimficha ,nikijilinganisha na nyie bora hata mimi nina nafuu”Mara baada ya kuumbuliwa na Hermes wote walifunga midomo yao.
Ni kweli kabisa kila kitu kilikuwa kishajulikana muda mrefu sana, labda tu kama Roma asingekuja kuwa na hisia za kweli za kimapenzi kwa Edna asingeweza kufika hatua hio bila ya kujali uhusiano wa Edna na Athena upo vipi.
Kila hatua aliopiga Athena ilikuwa ni kumfikisha mahali alipofikia siku hio.
Kuchukua uwezekano wa mwanaume ambae alikuwa ametabiriwa kuwa na nguvu ya kubadili mpango mkubwa wa ufufuaji wa kabila la miungu kwa kumfanya mmoja wao.

Bila shaka mtu wa kawaida angejua juu ya hilo pengine angesema Athena ana fanya vitu visivyo na maana kwasababu tu kwa uwezo wake pamoja na wa miungu kama wataungana ingekuwa rahisi kumuua Roma.
Lakini kwa miungu hao walikuwa wakifikiria tofauti na watu wa kawaida , walikuwa wamejaaliwa akili kubwa ndio maana hawakumhukumu Athena kwa maamuzi yake tokea mwanzo.
Waliamini hakuna kitu ambacho Athena alifanya na kikawa hakina msingi kwasababu kwao alikuwa ni mwanamke aaeona mbali kuliko wengine wote.
Lazima tu kutakuwa na taarifa ambayo hakufunuliwa kwa asilimia mia moja katika unabii aliopata kitu kilichomfanya kukaa chini na kuandaa ramani ndefu ya miaka mingi iliomhusisha Roma ili kumfikisha katika hatua hio.
Kwa lugha nyepesi ni kama unaweza kusema Athena alikuwa akishindana na unabii.
Miungu waliweka imani zao kwa asilimia mia moja kwa Athena na katika uhalisia alikuwa ameishi katika matarajio yao.
Roma alionekana hakuwa na hamu tena ya kupigana na ufufuo wa miungu umebakia kidogo tu kukamilika.
Mara baada ya Roma kumwangalia Athena kwa muda mrefu , muonekano wake ulibakia tunduwaza(Daze), kama kwamba alikuwa amepoteza nafsi yake.
“Kabla sijaondoka naomba nikuulize swali moja?”Aliongea Roma kinyonge.
Athena alionekana kama ametarajia nini angeuliza , kwa kuchezesha vidole vyake tu kifaa kilichofanana na taji rangi ya majivu ,kiinachong’aa kama kioo kilionekana katika mikono yake , lakini bado ajabu ule ukijivu wake ulijaa msisimko wa kifo.

“Unataka kujua nimewezaje kujificha kwako bila ya kuonyesha ishara yoyote ?, hili ndio jibu langu”Aliongea huku akimnyooshea Roma kile kifaa kama taji kuangalia kisha akaendelea kuongea.
“Hades wa zamani alinikubalia ombi langu nusu kufuata mipango yangu na ili kuonyesha dhati yake ndipo aliponitunuku ‘Helmet of invisibility’ na kisha kukutunuku wewe nusu ya uungu wake kama nilivyohitaji … hiki kitu unaweza kukiita kama Dhana iliowahi kuwepo yenye uwezo wa kificha kila kitu , labda tu nitake mtu kuona , ila kama sio hakuna mtu yoyote ambae anaweza kuniona wala kuhisi uwepo wangu na kuona sura yangu halisi”
Miungu walihuzunika mara baada ya kuona Helmeti hilo , waliamini Hades wa Zamani alijitoa kafara kwa ajili tu ya kufufua miungu.
Ukweli ni kwamba tokea mwanzo Hades hakuonyesha waziwazi alikuwa akikataa mpango wa kufufua ndugu zake , alichokuwa na wasiwasi nacho ni athari zitokanazo na mpango huo na alifuata yote akiamini katika unabii.
“Ndio maana haishangazi ..nakumbuka ulipoondoa uungu kutoka katika Hollygrail , kile kitabu cha teknolojia ya Thanatos na Jiwe la Kimungu ..sikuweza kuhisi kitu chochote ambacho hakikuwa sawa , kumbe kilichokuwa kikikulinda ni hio Siraha ya maajabu. Haha..”
Roma alijikuta akikumbuka nyakati zile ambazo Athena aliweza kunyakua Hollygrail mara baada ya mnada kuvuruugika , lakini vilevile alikumbuka namna ambavyo alipoteza kile kitabu cha Thanatos kule Ufaransa lakini pia jiwe la Kimungu nchini Tanzania.
Matukio yote hayo yalitokea katika kipindi ambacho hakuwa karibu na Edna , wakati ananyakua Hollygrail kutoka katika mikono ya vampire Moses, Edna alimuacha Mlimani City , wakati anapokonywa kitabu cha Thanatos, Edna alimuacha katika gari , wakati anapokonywa jiwe la Kimungu Edna alikuwa kazini.

Roma aliishia kutoa tabasamu lililojaa uchungu na kinyonge alijikuta akigeuka na kisha palepale akatoweka , akipotezea macho ya kila mmoja yaliokuwa yakimwangalia.
Kwa wale waliokuwa na macho ya kijini na yasiokuwa ya kawaida waliweza kumuona namna anavyopotea katika upeo wake na ilikuwa ni kama mgongo wake muda wowote utapeperushwa na upepo.
Athena nae aliangalia na kuishia kukunja ndita kidogo ashindwe kuongea neno lakini Aphrodite upande wake hakuweza kujizuia kutokuongea.
“Athena , aren’t you worried abour Hades?”Aliuliza akimwambia je hana wasiwasi juu ya Hades.
Athena alifumba macho yake na kuvuta pumzi nyingi kama kwamba anatafuta harufu mbaya na kisha akaongea:
“Anapaswa kuwa peke yake kwa sasa , hawezi kwenda kinyume na sisi tena”
“Hilo sio tatizo , ninachomaanisha je humjali tena?”Aliongea Aphrodite mwenye mawazo.
“Nani!!?”Alifungua macho yake.
“Kila kitu nilichofanya katika miaka elfu ishirini yote ni kufanikisha kufufua roho za wenzetu zilizopotea na kurudisha uzao wetu , huyu ndio mimi iwe anakubali au kukataa hakuna kitakachobadilika iwe leo au kesho”Aliongea kikauzu akiwa hana ishara ya hisia zozote juu ya aliomfanyia Roma.
“Wewe…”Aphrodite alitaka kuongea lakini alijikuta akipaliwa kutokana na hasira na aliishia kusema:
“Sitaki kupoteza pumzi zangu kwako”
Athena upande wake alionekana hakuwa na chochote cha kumwambia na macho yake yote yalikuwa yakiangalia uungu ambao unazaliwa juu ya Mti Mama, alionekana akiwa amepotelea katika mawazo na hakuna ambae alijua anafikiria nini.
Majini wale wa miliki za Hongmeng na Xia haraka sana na wao walikimbia mara baada ya kumuona Roma akiondoka.
Ukweli walioweza kushuhudia uliwayumbisha na wao na hawakutuhubutu kukaa hapo hata kwa sekunde , hawakutaka kufa kusiko kwa maana.
Kama majini ambao nyumbani kwao ni ulimwengu wa majini walikuwa na mawazo pia , hakuna aliewahi kutarajia miungu kumzidi nguvu Roma , tumaini la binadamu na wao lilikuwa katika kiganja cha mkono wa Athena.
Hakuna mtu jasiri duniani ambaye anaweza kufanya maamuzi ya haraka ya kuua mke wake au watoto wake hivyo ni kama walielewa kile Roma anachopitia.
Hatima ya binadamu ni kama ilionekana imejulikana na kifuatacho ni mwisho wake.
*****
Katika eneo la kujitegemea la anga lenye mandhari nzuri na ya kushangaza kulikuwa na kundi la watu pia waliokuwa wakiangalia kila kitu kilichokuwa kikitokea ncha ya kaskazini katika kitu kama kioo kilichokuwa mbele yao.
Pengine katika akili za kawaida mtu akikuambia kuna akhera au mbinguni usingeweza kumuelewa kutokana na kukosa uthibitisho lakini uwepo wa eneo hilo kama mtu angeingizwa hapo pengine angeweza kuamini.
Clark ambae alikuwa amekaa katika kiti cha jiwe alijikuta akiinuka kwa kurupuka mara baada ya kuona Athena alikuwa ni Edna.
Wakati huo alipoweza kuona namna hali aliokuwa nayo Roma mpenzi wake alijikuta akishindwa kujizuia na kuanza kulia kilio cha kwikwi huku akiwa ameficha uso wake.
Alikuwa akijua fika umuhimu wa Edna katika maisha ya Roma na uzito wake katika moyo wake .
Katika ulimwengu huu maumivu makali sana yanayoweza kumpata mtu ni pale unapoumizwa na mtu uliempenda sana.
Ilikuwa ni kama Clark anahisi maumivu anayopitia Roma ndani ya moyo wake , ilikuwa ikiuma sana kwake na hakupata picha alichokuwa akipitia mpenzi wake.
Mara baada ya kumpiga macho Athena Chuki kali iliibuka katika macho yake.
Upande mwingine Sharif na wenzake walionekana walikuwa wakiujua ukweli muda mrefu sana na Aoiline ambae ni kama ndio kwanza anafahamu alionekana kutoshangaa,.
“Huyu kijana ni mjinga kukimbia”Aliongea Sharif asieleweke hisia zake zipoje kwani hakuonyesha ishara yoyote.
“Unadhani kila mtu ni kama wewe ambae unajikuta mkatili kwa unao wapenda? , watu wote sio kama wewe kuweza kuondoa hisia na mawazo kwa haraka yawe mazuri au mabaya”Aliongea Aoiline huku akimwangalia Sharif kwa macho ya dhihaka na Sharif hakujali dhihaka zake.
“Nilitarajia hili hata hivyo tokea mwanzo. Kuipita changamoto ya namna hii sio lelemama na niliweza kujua haya yote kutoka kwa barua walioacha Wajumbe wa mkuu wa Enzi katika mnara ndio nikaelewa kila kitu , hata hivyo usijali , nitamfuata mwenyewe , matumaini yangu ni kutokukuharibu nguvu zake kubwa”Aliongea Sharif.
“Master , awamu hii Hephaestus amefanikiwa kuzima nguvu ya safu ya ulinzi hivyo haitochukua muda mrefu Zeus kutoka pamoja na kundi la roho za majini wabaya , kama Roma ataendelea kusita sita kama hivi kuwashughulikia miungu , kwanini tusianze kuimarisha hali ili majini wasije kugeuza dunia kuwa kuzimu?”Aliongea Mzee Yasu.
“Kama Roma hatarudiwa na akili zake inamaanisha kwamba ni kudra za Mkuu wa enzi juu ya binadamu kutofanikiwa kuepuka hili janga , haileti tofauti iwe ni sasa au baadae , au ni majeruhi wachache au wengi, lakini kama unataka kuingilia unaweza kwenda , majini pepo wabaya wa zamani sio kama wanyama wakali tena , ni mizimu yao tu iliobakia katika nguvu kidogo, wanaweza kuwadhuru binadamu lakini sio majini watu”Aliongea Sharif.
Yasu na Xumei walijikuta wakishangaa , Sharif hakuwepo katika kundi la wanafunzi hao na haikueleweka alienda wapi.
Licha ya kujua Master wao hakuwahi kujali uhai wa binadamu lakini hawakuwahi kuwaza angeonekana kutojali kabisa.
Lakinni hata hivyo haikumaanisha Sharif alikuwa mtu mbaya , ilikuwa ni kwamba katika ulimwengu huu hakuna kitu kama Uovu na wema , kila kiumbe kilichopo katika uso wa dunia kina maana na sababu juu ya uwepo wake na isitoshe alikuwa ni kama ishara ya muunganiko wake na binadamu lakini vilevile alikuwa ishara ya muunganiko wake na Wajumbe wa Mkuu wa enzi.
“Sharif naona unawaogopesha wanafuzi wako , hehe.. wamekuwa pamoja na wewe kwa miaka elfu mbili lakini bado hawakufahamu vizuri, hawatokuwa na uvumilivu zaidi kama utaendelea kuongea maneno mengi ambayo ni kinyume na ulimwengu”Aliongea Aoilie huku akicheka kishambenga.
Sharif na yeye alicheka lakini hakuwa na nia ya kuelezea zaidi na kilichowapata ni upepo tu kwani alipotea palepale.

SEHEMU YA 785.
Kitendo cha Sharif kupotea katika eneo hilo kioo kilichokuwa mbele yao kilichokuwa kikionyesha kiachoendelea katika ncha ya Kaskazini kilipotea pia kana kwamba hakikuwepo kabla.
Clark ambae alikuwa kimya muda wote ghafla tu alimpigia magoti Aoiline huku macho yake yakiwa mekundu.
Aoiline macho yake yalimsinyaa kutokana na kitendo cha Clark na alimwangalia kwa tabasamu lililojaa uchokozi.
“Msichana unafanya nini?”Aliuliza.
“Najua unao uwezo wa kunitoa hapa na kunipeleka katika ulimwengu wa kawaida …”Clark alisaga meno , chuki aliokuwa nayo wakati huo ilikuwa ni ngumu kujificha.
Aoiline mrembo huyo wa kimaajabu alishika unywele wake na kuuzungusha kwa aina isioelezeka huku akiwa na tabasamu pana la kutojali chochote.
“Je ni kweli unao uwezo wa kubadilisha hali yote inayoendelea huko nje na uwezo wako?”
“Mimi sijui, lakini sijawahi kumuona akiwa katika majonzi namna ile tokea nimjue , nashindwa hata kudhania ni kiasi gani cha maumivu anachopitia , anatia sana huruma nashindwa kujizuia kulia kwa ajili yake”
“Uwezo wa kukutoa hapa ninao lakini sitofanya hivyo..”
“Kwanini?, Haupo upande wa Roma?”Aliuliza Clark kwa mshangao maana aliamini Aoiline na Roma ni marafiki na angemjali kwa kile anachopitia.

“Napendeea kuamini mpenzi wako ataweza kukabiliana na hatima yake yeye mwenyewe tokea nilipokubaliana na mipango yote ya Sharif, hivyo sitofanya mambo kinyume , hii ni imani niliokuwa nayo zidi yangu mwenyewe na ambayo ninayo zidi ya Roma”Aliongea Aoiline mara baada ya kutingisha kichwa.
Anaweza kuwa katika upande wa Roma lakini anataka apate ufumbuzi wa matatizo yake mwenyewe bila ya msaada wa nje.
Mara baada ya kuona usiriasi aliokuwa nao machoni kwake alijikuta akinywea na kuinamisha kichwa chake chini na kukaa kimya.
****
Upande mwingine ni masaa machache tokea kikao kizito kumalizika nchini Tanzania , kikao hiki kilikuwa kimeongozwa na Shekhe Idris kiongozi wa hadhi wa Ant- Illuminat..
Ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni juu ya mchoro wa unabii , kila mmoja ambae alihudhuria kikao hicho alikuwa katika hali ya kuhamanika pengine yote hayo yametokana na juu ya ukweli waliokuwa wameusubiria kwa muda mrefu sana.
Haikuwa hivyo tu kwa wanachama hao wa umoja huo bali vilevile kikao kingine kilifanyika jijini Nairobi kilichowakutanisha wanachama wote wa Hadhi ya juu wa Zeros Organisation , kikao hicho kilifuatana na kile cha umoja wa kimataifa kitakachoongozwa na Katibu mkuu wake Clelia Allisanto.
Katika kikao cha Zeros wanachama wote wa ngazi za juu kutoka jamii nyingi za siri na viongozi wakubwa wa mataifa yalioendelea walionekana kuwa na sura zilizokuwa zikifanana na zile za waachama wa Umoja wa Ant-Illuminat.
Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema wanachama wa umoja wa Illuminat walikuwa sawa kimuonekano na wanachama walewale wanaoenda kinyume na wao yaani Ant- Illuminat.
Swali ni moja tu je ni Ajenda zinazofanana zimejadiliwa katika vikao hivyo , swali hilo lilikuwa gumu kujibika mara moja kutokana na usiri uliokuwepo kati ya kikao cha Dar es salaam na kikao cha Nairobi.
Lakini kitu kimoja ambacho pengine kilionekana kuwa cha tofauti baina ya sura za watu hio ni kama kulikuwa na hali ya tumaini katika nyuso zao.
Ni dakika chache katika kuhitimika kwa kikao hicho , yaani wakati wa kikao cha Umoja wa mataifa kikianza moja ya tukio kubwa ambalo lilikuwa likitarajiwa ni juu ya kiongozi mkuu wa The Holly See kuongea kupitia Vidio call katika mwanzo wa kikao hicho.
Jambo hili pengine ni la kawaida kwani licha ya kiongozi huyo kukosa haki ya sheria ya kura katika baraza la Umoja lakini alikuwa na cheo cha uangalizi na maoni yake yalikuwa yakisikilizwa.
Tokea dunia ianze kuingia katika hali ya hatari ya kupotea kwa kiumbe binadamu Kiongozi huyo hakutoa msisimamo wake juu ya kile kinachoendelea wala maoni yoyote , ki ufupi ni kwamba hakujitokeza hadharani licha ya kwamba kwa siri sana , taarifa ambazo hazikuwa wazi baadhi ya wanajaeshi wake walikuwa wakishiriki katika ujenzi wa Safina huko nchini Ethiopia.
Sasa kwa mara ya kwanza Kiongozi huyo anajitokeza na mara hio ya kwanza ni katika kikao cha cha umoja ambacho ni cha mwisho kufanyika kitakachohusiana na namna ya kuokoa binadamu.
Kati ya watu ambao hawakuwa na shauku ya kujua kinachokwenda kuzunguzwa na kiongozi huyo ni Mheshimiwa Barack Mabo , hakuwa na shauku kwasababu alikuwa akitarajia kile ambacho kitasemwa.
Wakati mengi yakiendelea yeye pia alikuwa jijini Nairobi huku akijinasibu ni wa asili ya nchi hio lakini kwa siri na yeye alikuwa na mipango yake.
Na hakuwa na siku moja wala mbili alizokuwepo nchini hapo , ukweli ni kwamba ilijulikana kwa wengi alikuwa Nchini Narobi na familia yake lakini mara nyingi na kwa siri alionekana nchini Tanzania huku akijitahidi kuweka ukaribu na familia ya Kweka , yaani familia anayotokea Roma ilikuwa ni kama vile alikuwa akitaka kujua kinachoendelea mara baada ya kurudi kwa Roma.
Alikuwa na taarifa hizo lakini hakuwa na mwendelezo wa taarifa ya kila siku ya juu ya kile anachokifanya Roma kwa ajili ya kuokoa binadamu, haikuwa kwake tu pengine kwa viongozi wote walipata taarifa za kile kinachoendelea katika maisha ya Roma.
Akiwa ndani ya Hoteli kubwa simu yake ya mkononi iliita na kwa papara sana alipokea mara baada ya kuona namba ya mpigaji.
“Mheshimiwa nilikuwa nikisubiria simu yako kwa hamu kubwa”Aliongea yeye kabla wa upande wa pili hajaongea lakini licha ya hivyo upande wa pili ni kama alikuwa akisikia pumzi ya mtu pasipo neno.
“Barack wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na sipendi kukuficha , taarifa zilizonifikia si nzuri hata kidogo juu ya hatima ya kila mtu, nimepokea taarifa nzuri na mbaya ndani ya mpishano wa dakika sabini”.
Mara baada ya kauli hio Mheshimiwa Barack licha ya kuonyesha hamaniko lakini bado hamu yake ya kujua anacholenga mpiga simu haikumtoka.
“Nakusikiliza Shii..”Aliongea kwa sauti hio ikionekana kutaja jina lenye kusikika Kimandari.
“Roma alierejesha tumaini letu ndani ya dakika themannini zilizopita amegeuka na kuturudisha mwanzo mwa mioyo yenye wasiwasi mara baada ya kuona sura ya Adui yake mkubwa”Aliongea upande wa pili kwa kingereza kilichosikika sio cha kuzaliwa bali cha kujifunza kutokana na rafudhi.
“Naamini kashafanikiwa kuona sura ya Athena , lakini swala hili linaingiliana vipi na Adui”Aliuliza Barrack lakini licha ya swali lake alionekaa kuwa katika hali ya kawaida.
“Ni kama ilivyotarajiwa Barrack, hii ni taarifa yangu ya mwisho ya kuwa chanzo cha taarifa za kile kinachoendelea kwako”Mara baada ya kauli hio simu ile ilikatwa.
Barrack aliangalia jina la Xi likipotea katika simu yake na tofauti na kuwa na wasiwasi alionekana kuwa mwenye kufikiria na hazikuchukua dakika hata moja alifungua app ya simu na kisha alionekana kuingiza namba flani na ndani ya sekunde ileile aliweka sikioni.
“Diana nadhani una majibu juu ya kazi niliokupatia?”Aliongea Barrack.
“Amesema kuna utofauti katika muonekano wa picha mheshimiwa”Aliongea kwa lugha ya kingereza.
“Unataka kumaanisha nini kusema hivyo?”
“Ni mjuzi wa hali ya juu katika kukumbuka taarifa ndogo ndogo alizoziona mara moja tu na kuziweka katika mchoro , nimekutumia faili mheshimiwa Mstaafu”Sauti ya mwanamke aliefahamika kwa jina la Diana aliongea na hata hakuongea neno zaidi, Mheshimiwa alizama upande wa eneo la ishara ya taarifa zilizoingia katika app hio hio iliotengeezwa kwa teknolojia ya ‘BlockChain’ kwa ajili ya maswala ya ki ulinzi.
Dakika ileile kioo cha simu yake kilijaa faili ambalo lipo katika mfumo wa picha na alikodoa macho kusoma kila taarifa inayoonekana katika picha hio.
Picha ile ni ileile ambayo alionekana Athena akimuonyesha msichana mdogo Naira alietokana na Proiect Pro Human katika bara la barafu ncha ya Kusini mwa dunia.
Picha ya unabii unaweza kuiita hivyo , ni picha ambayo humuonyesha mwanamke aliekalia kiti cha kimalkia huku akionyesha tabasamu na chini yake kuna wenye kumuonyeshea heshima kwa namna ya kumsujudia.
“Kila ninachofanya ni kuhakikisha tabasamu la huyu mwanamke halikauki”Pengine ndio kitu cha pili yake kukumbuka kabla hata ya kuanza kuchora picha hio.
Naam kwasababu ni mtu mmoja tu alieonyeshwa picha hio basi moja kwa moja tunamjua ni Naira na hii inatuongezea kuamini kutokana na mwanamke Diana aliekuwa kwenye simu na Mheshimiwa Barrack Mabo.
Mheshimiwa huyo alionekana kuongea mwenyewe katika nafsi yake lakini simu mbili zilizoingia mfululizo zilimfanya aache kuyakiminika katika faili hilo na kugeuza sura yake kwa simu zinazoingia.
Moja ilikuwa ni ya Shekh Idriss na nyingine ilikuwa ni kutoka kwa Clellia na ilimfanya Mheshimiwa kuonyesha tabasamu .
“Katika nyakati kama hizi ndio umuhimu wangu huonekana baada ya kuwa mstaafu”Alijiwazia na akapokea kwanza ya Clelia.
“Ni Tofauti na mchoro wa Unabii Clellia, maelezo yako yanafanana na ya Naira wote mmedanganywa na Athena”Aliongea Mheshimiwa na upande wa pili haukuongea sana na simu ilikatwa na palepale aligeukia mtu mwingine aliekuwa akimpigia.
“Idriss nadhani haina haja ya kunipigia ilihali Ajenda katika vikao vyote zilikuwa sawa”Aliongea Mheshimiwa huku akivuta glass ya mvinyo na kuketi kwenye sofa.
“Sijataka kujua taarifa ya kikao cha jumii yenu , katika nyakati hizi ni rahisi kupata taarifa katika kipindi cha utulivu”
“Kama ni hivyo ni taarifa ipi unataka kutoka kwangu, nje ya mkataba wetu?”
“Uthibitisho wa unabii”
“Unabii wa picha alioonyesha Athena ni tofauti na Unabii uliowakilishwa kwetu leo na Vatican, maelezo ya Clellia Allisanto na Naira yanafanana”Aliongea , ilionekana hakuwa na haja ya kumficha tena Idriss.
Ukweli ni kwamba licha ya kuwa na nia nzuri ya kujiingiza katika jamii zote mbili na kuwa mwanachama alifanya yote hayo kwa ajili ya kujitengenezea thamani.
Kiongozi huyo alikuwa tofauti na maraisi wengine wastaafu , wakati wao wakijilimbikizia mali yeye hakupenda uthamani wake kutafsiriwa na kiasi cha pesa bali siri anazobeba ndio maana alijitahidi kujijengea Koneksheni na watu wenye kumweleza taarifa na sio wenye kumpa utajiri, moja ya watu hao ni Raisi wa China ambae alikuwa na muunganniko mkubwa na majini kutokana na kwamba alitawala nyuma yake wakiwepo jamii ya Hongmeng.
Sasa taarifa za Roma kukimbia uwanja wa mapambano ndio alizoweza kusikia kutoka kwa mtu alieitwa Shii yaani Xi ambae alionekana ni rafiki yake kulingana na namna walivyoongea.
Raisi huyo mstaafu ni moja ya wanachama wa Hadhi waliohudhuria kikao cha Zeros ambapo moja kwa moja ungesema ni kikao cha Illuminat kutokana na jamii hio kuwa na nguvu katika umoja huo.
Mheshimiwa alimuelezea namna mchoro ulivyokuwa na kwa maelezo yake ilionekana tofauti ya mchoro huo haikuwa kubwa picha waliopewa mwanamke hana tabasamu na mbele yake hakukuwa na wenye kumsujudia , alikuwa ni kama Malkia asie na taifa la kutawala lakini licha ya hivyo alionekana hajanuna bali alikuwa ameridhika huku macho yake yakimwangalia mwanaume aliekuwa mita kadhaa kulia kwake , ndio mtu pekee alieonekana katika mchoro.
Haikuwa rahisi kutafsiri mchoro huo kama unavyosemekana ni wa kinabii lakini pengine watu wenye maarifa wangeweza kuuelezea.
Picha nyingine ambayo ni kulingana na maelezo ya Clelia na Naira, picha ilionekana mwanamke akitabasamu lakini mwanaume aliemfanya mwanamke kuridhika katika picha ya mwanzo hakuonekana katika picha hio.
“Idriss leo nimekuwa mtiifu kwako tokea nilipofahamu wewe ni moja wapo ya walinzi wa dunia”Aliongea Barrack.
“Haibadilishi kitu juu ya wasifu wangu , hii ni simu yangu ya mwisho kwako” na simu palepale ilikatwa lakini Barack Mabo hakuonyesha kubadilika.
“Ni muda wa kujiongezea ushawishi juu ya jambo hili , ni muda wa kurejea nchini kwangu kueneza maneno ya ujasiri”Aliwaza na kisha palepale aliwasha runinga.
Kwa namna moja alionekana kufurahishwa na matokeo , picha mbili za unabii zinazotofautiana ni kama zilimpa furaha.
“Hii ndio ilikuwa sababu tokea mwanzo nilishindwa kumuua huyu msichana licha ya kuwa ndani ya taifa dogo kama Tanzania, alikuwa ni kila kitu ya kila kinachoendelea”Aliongea mwenyewe na ni kama alionekana kukumbuka nyakati zake za uongozi alivyotoa maelekezo ya Edna kufa kwa ajili ya kulinda siri ya Mpango LADO.

*******
DAR ES SALAAM SIKU SABA MBELE.(Seven days later in Dar es Saalam)
Hali ya hewa ndani ya jiji la Dar es salaam haikuwa mbaya sana , joto bado lilikuwa la kawaida na halikuwa limevuka nyuzi joto sifuri lakini lilikuwa la chini sana kuvunja rekodi..
Serikali ya Tanzania ilikuwa imetuliza ghasia zote ambazo zilitokea ndani ya jiji hilo na sasa hali ya amani ilikuwa imerejea lakini hata hivyo haikuwa kama siku za kawaida kwani wanajeshi wengi pamoja na polisi walikuwa kila mtaa kuhakikisha hakuna uhalifu wowote.
Kitu pekee ambacho raia waliongeza umakini nacho ni kuingia katika nyumba za ibada , haikuwa kwa waislamu wala wakristo kila mwananchi alionyesha jitihada za kuhudhuria ibada kulingana na ratiba za dini yake , hata wale ambao hawakujua milango ya nyumba za ibada walikuwa watiifu kuhudhuria kwa wakati pengine kuzidi hata wale ambao walikuwa ni wahudhuriaji wazuri.
Kila mtu aliekuwa na nia yake , wengine ilikuwa ni hofu ya kile kinachoendelea wengine waliamini katika unyakuo.
Ijapokuwa jiji hili halikuwa na baridi kali kama maeneo mengine lakini ukweli ni kwamba kulikuwa na baridi ambayo ilifanya watu wajifungie ndani, yaani kitu pekee ambacho hakikuonekana baadhi ya jiji hilo ni kama mvua ya theluji tu ambayo ilipatikana katika maeneo ya nyanda za juu.
Sasa moja ya sehemu ambazo zilikuwa hazina watu ni ndani ya hoteli ya JR mita kadhaa inapopatikana Club B.
Ilikuwa ni kama vile wenye hoteli yao walikuwa wamfukuza wagenni ndani ya hoteli hio kwani hakuonekana mtu ndani ya eneo la Bar kama ilivyozoeleka.
Katika kona ya eneo hilo alionekana mwanaume ambaye alikuwa na mavazi ambayo hayakuwa katika mkao mzuri , ilikuwa ngumu kusema mtu huyo alikuwa ni masikini kutokana na muonekano wake lakini ni rahisi kusema mtu huyo hakuwa katika hali nzuri ya kimawazo yaani kama kichaa kwa namna anavyogugumia chupa za bia huku mbele yake zikitawanyika chupa tupu.
Alikunywa kimimiika chote kilichokuwa kwenye chupa kwa pupa kama mtu anaelazimisha kulewa na mpaka aliposhusha chupa ile aliishia kucheua na muda huo alikuwa ni kama mtu wa kawaida tena mbele ya macho ya mtu anaemfahamu.
Alikuwa ni Roma ambae amerudi Dar mara baada ya kuzurula kwa siku mbili mfululizo katika maeneo ambayo hayakufahamika , alikuwa amechafuka mno.
Eneo alilokaa lilikuwa ni lile lile ambalo aliweza kukutana na mwanamke mrembo Edna kwa mara ya kwanza akimdhania ni kahaba.
Muda ulikuwa umeenda na mazingira yalikuwa yamebadilika lakini kumbukumbu za eneo hilo kwao hazikuweza kubadilika , zilikuwa kumbukumbu za kupuuza lakini tamu kwa wakati mmoja.
Lakini wakati huo kwa Roma eneo hilo alilichukulia kama sehemu ambayo ndio mwanzo mwa udanganyifu.
Roma alikuwa ametumia Dhana ya jani la upofu kubadili sura yake ili aonekane tofauti pamoja na kuficha uwezo wake , kwani hakutaka usumbufu wa mtu yoyote wala kuonana na mtu yoyoyote.
Yeye mwenyewe ndio alikuwa mhudumu na vinywaji kwani aliinuka na kuchukua vinywaji na kurudi navyo na kisha kuendeleza kazi , ilikuwa ni kama alitaka kukaa kama mlevi maisha yake yote.
Eneo hili ukweli ni kwamba halikuwa na watu sio kwasababu ya kukosa wateja bali hoteli hio ilifungwa kutokana na hali ya ki usalama wa jengo lenyewe kwani kulitokea mtitio wa ardhi mita kadhaa kutoka ulipo msingi wa jengo na ishara za ufa wa hoteli hio ndio ulifanya hoteli hio ifungwe kwa muda.
Roma muda huo alitamani angekuwa binadamu wa kawaida ili alewe kiasi kwamba asielewe hata kinachomtokea katika mazingira ya kawaida pengine kufa kabisa maumivu yampotee.
Lakini kila mara sura ya Lanlan na familia yake ilipokuja katika fahamu zake alitaka kuishi lakini bado aliona kuishi ni kubaya zaidi ya kifo.
Eneo hilo lilikuwa kimya mno na hakuna mtu ambae anaweza kumuona Roma aliejikalia kwenye kona kama angeingia ndani ya eneo hilo kutokana na giza na alikaa hapo kwa muda mrefu sana kama binadamu aliekosa tumaini kabisa.
Ikiwa ni katikati ya mchana siku ya saba tokea kupatwa na Janga la moyo na siku tao tokea aingie ndani ya jengo hilo kivuli cha mtu alievalia kanzu kilionekana ndani ya eneo hilo akitembea kwa hatua hafifu kumsogelea Roma.
Roma aliekuwa amelala kwenye Sofa ilikuwa ni kama vile hajamuona mtu huyo , ki ufupi ni kwamba hakujali ni mtu au ni mzimu wa mtu.
Mtu yule alisogea mpaka kwenye Sofa alilolala Roma na alisimama bila ya kuongea neno kwa dakika kadhaa na mara baada ya kuona Roma hakuwa na nia ya kuamka aliishia kutoa tabasamu lililojaa wasiwasi.
“Mbona unakuwa mjinga , umekutana na yule mwanamke kwa muda mchache sana kama ilivyo kwa kumbukumbu zako juu yake , haina haja ya kung’ang’ania juu ya swala dogo namna hii”Aliongea Sharif kama vile ni baba anaejaribu kumfokea mtoto.
Roma alijigeuza kwenye sofa lile na kugeukia upande mwingine huku akijjikunyata.
“Potea mbele yangu”Roma aliongea na hakuonekana kutaka kuongea neno lingine zaidi.
Sharif au Master namba moja hakufanya chochote zaidi ya kutabasamu , ilionekana Roma hakuwa amelewa licha ya kwamba alionekana kama mlevi , hivyo hata kama hajajitambulisha yeye ni nani ilionekana Roma ashamtambua tayari.
Ki uhaisia haikuwa ngumu hata kujua uwezo wa Sharif kwani Roma alikuwa ametumia Dhana ya jani la upofu na kama Sharif angekuwa na uwezo mdogo asingeweza kumpata Roma kirahisi.
Sharif hakujali ujeuri wa Roma , ukweli ni kwamba hakujali kabisa namna watu wanavyomchukulia na aliishia kutingisha kichwa na kisha aliketi kwenye sofa kando ya Roma.
“Kama methali zinavyosema, mtu na asivutiwe na sura tu bali aone ukweli ndani ya moyo , vilevile mtu asifungwe na ukweli wa moyo na hata aikatae sura”Aliongea Sharif.
“Nimesema Ondoka”Roma aliongea huku akionyesha hali ya kukereka , hakujali Sharif alikuwa na nguvu kiasi gani na alikuwa na nani bali hakutaka kuonana na mtu yoyote yule.
ITAENDELEA
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.
MTUNZI: SINGANOJR .
Mono no Aware

SEHEMU YA 786.
Roma sauti yake ilionekana kubadilika na kuonyesha zaidi hali ya kukasirika mara baada ya kuona anasumbuliwa na Sharif.
Alijiambia anaongea nini huyo na methali zake, muonekano ?, ukweli wa moyo?, Kama angekuwa mtu wa dini na angeambiwa aelezee upendo na chuki na yeye angejiuliza swali kama vyote hivyo vipo kweli kwanini ana mahusiano mengi na mikwamo mingi.
Sharif alijikuta akibakia mdomo wazi na aliona ni kama ujinga kwani kijana mdogo kama huyo ndio kwanza yupo kwenye miaka ishirini kuelekea therathini na licha ya kuwa na uwezo usio na mipaka bado ni mtoto tu na kama ataongea kwa namna anavyongea na Aoiline basi anaweza asimsikilize.
Kuhusu Roma kumwambia aondoke wala hakujali sana na mara baada ya kuwaza kwa akika kadhaa alionekana kuwaza kitu na kutingisha kichwa chake kwa mara nyingine.
“Kulingana na utafiti wa kibinadamu juu ya dunia ya kale , Kimondo chenye uzito wa zaidi ya tani trilioni moja kilidondoka duniani miaka milioni sitini na tano iliopita , spidi ya kimondo hiki inakadiriwa kuwa zaidi ya kilomita elfu themanini na tano kwa saa na nguvu yake ni sawa na kulipua vichwa milioni therathini vya mabomu ya nyuklia kwa wakati mmoja, Binadamu wanaweza wasielewe hili lakini kuna uwezekano wa aina ya kimondo cha namna hio kuigonga dunia kila baada ya miaka milionni kumi na kuharibu kabisa sayari ya Dunia , vilevile vimondo vya ukubwa wa wastani upande vinaweza pia kudondoka duniani muda wowote.
Ni miaka elfu hamsini tu iliopita wakati dunia iliopoingia katika vita kali ya majini na binadamu mpaka Wajumbe wa Mkuu wa Enzi kuingilia kati, kipindi hiki ndio wakati ambao Kimondo kilidondoka eneo la jangwa eneo ambalo sasa ni sehemu ya taifa la Marekani , jimbo la Arizona , baada ya kimondo hiki kufika ardhini kilirusha mawe tani milioni mia saba sabini na tano kwenda angani na kutengeneza shimo kubwa ambalo lilikuwa na upanda wa takribani kilomita saba na mita zaidi ya mia kwenda chini , sehemu hii ndio leo hii hufahamika kwa jina la Bariger Crater.
Wakati huo hiki kimondo kilikuwa na ukubwa futi mia tatu therathii ambazo ni sawa na ndege za sasa , baada ya kudondoka kilisababisha joto zaidi ya nyuzi 1600 , joto ambalo liliyeyusha mawe , mchanga na takataka zilisafiri kwa umbali maili sita kwa spidi mara tatu ya risasi , na kwa spidi hio watu wote wlaiokuwa karibu pamoja na wanyama miili yao ilitobolewa na kuvunjika mifupa hata pasipo ya kujua”
Sharif aliongea muda mrefu na haikueleweka alikuwa akielekea wapi katika mazungumzo yake lakini habari hizo zilimfanya Roma asimwambie andoke.
Roma taratibu sana alijinyanya na kukaa kitando na kisha akamwangalia Sharif ambaye alikuwa na uso uliopambwa na tabasamu.
“Ni kitu gani lakini ambacho unakusudia kusema kwa stori yako hii?”\Aliuliza Roma.
“Naona hatimae umevutiwa na kile ambacho nakusudia kuongea, si ndio?”Aliuliza Sharif.
“Kama sio kwasababu ya wewe kuwahi kuniokoa , ningepigana na wewe hata kama ilimaanisha sikuwezi”Aliongea Roma huku sauti yake ikiwa na hali ya mikwaruzo huku akimwangalia Sharif kwa macho makali kama vile ni mbwa mwitu.
“Oh!Umejuaje niliwahi kukuokoa?”Aliuliza Sharif.
“Wakati Yan Buwen alipofanikiwa kuunganisha nishati ya Ant Matter na mwili wake na kupambana nae, ilikuwa ni wewe ambae ulitawala mwili wangu na kutengeneza radi ya Zambarau na haikuwa mara moja , ijapokuwa sauti yako imebadilika lakini siwezi kusahau namna nilivyokuwa nikisikia sauti yako katika akili yangu , kama sijakosea ni wewe pia uliemfana yule mzee kumteka Clark , Wewe ndio Master namba moja”Aliongea Roma na kumfanya Sharif kutingisha kichwa.
“Naona hujalewa na hii inamaanisha hujakata tamaa bado”
“Ninaweza kuwa ziadi ya unavyowaza”Aliongea Roma na palepale alitawanyisha chupa za bia ambazo zilikuwa kwenye meza na mara baada ya kupata iliokuwa na kinywaji aligida yote kiasi kwamba ilimfanya hata kumwagikia kwenye kifua chake lakini hakujali.
“Haha..nini kingine ambacho unajua kuhusu mimi , kwanini usiongee nikakusikiliza?”Aliongea Sharif huku akimwangalia Roma na matarajio.
Roma alicheua kwanza kinywaji alichokunywa kwa pupa na kisha macho yake yalisinyaa kana kwamba alikuwa amelewa.
“Kama nipo sahihi , wewe utakuwa mtu ambae Aoiline alikuwa akizungumzia , wakati nilipokuwa katika ulimwengu wa majini pepo alisema nilikuwa nikifanana kwa kiasi flani na mtu mmoja na alimfikiria huyo mtu mara baada ya mimi kutumbia mbinu ya Andiko la urejesho wa Azimio , hii inamaanisha ni mtu anaetumia mbinu kama yangu”
“Mtaalamu ambae anaweza kumfanya Aoiline kumfikiria lazima atakuwa na nguvu kuliko mii na kwako wewe kuweza kudhibiti mwili wangu kwa kuuazima na kisha kuita radi ya mapigo tisini na tisa bila ridhaa yangu , huyo mtu lazima atakuwa ni wewe.
Aoiline ni jini mtaalamu wa kihistoria ambae aliingia katika ulimwengu wa majini pepo miaka elfu hamsini iliopita , kwa umri wako lazima angalau utakuwa unalinfana nae au umemzidi kidogo , kama wewe ni mtu ambae unaweza kupambana nae au kumshinda kabisa basi lazima utakuwa angalau katika levo ya mapigo elfu tisa tisini na tisa ya radi , zaidi ya yote na uelewa wako wa mbinu ya Andiko la urejesho wa azimio basi kuna uwezekano mkubwa wewe ndio mtu wa kwanza kutumia mbinu hii kama sio kuigundua na kama ni hivyo basi isingewezekana kwa namna yoyote kumshindwa Zeus na Athena miaka elfu ishirini iliopita wakati wanafika duniani , kuna uwezekano wa aina mbili , mosi kuna uwezekano hukushiriki vita ya miungu na majini , pili uliwaacha moiungu wote kumi na mbili makusudi kabisa licha ya kwamba ulkikuwa na uwezo wa kuwaua wote..”
Macho ya Sharif yalichanua kadri ambavyo Roma alikuwa akiongea na aliishia kutingisha kichwa hapa na pale huku akiwa na tabasamu la ajabu usoni mwake.
“Ndani ya ulimwengu wa majini watu niliweza kupata kopi ya andiko la urejesho wa Azimio lakini jina lilikuwa tofauti , kama mawazo yangu yapo sahihi basi kuna uwezekano hii mbinu ilisambazwa kwa viumbe wote wa dunia wanao onekana na wasio onekana kwasababu maalumu ya kumtafuta mtu ambae anaweza kujua siri yake”
“Mtu alietengeneza Andiko hili alijua vizuri nguvu yake ,lakini licha ya hivyo kauonyesha kujali kama watu au viumbe wabaya kujifunza na hili linanipa jibu kwamba mgunduzi alikuwa akijua vizuri kabisa ni ngumu mo kwa viumbe kujifunza mbinu hii kutokana na ugumu wake lakini aliishi katika tumaini siku moja itatokea mtu ambae ataweza kujifunza na kupita levo zote”Roma aliendelea kuongea na akaendelea.
“Na hili ndio ambalo lilifanya mbinu hii kujulikana kwa majina tofauti tofauti kati ya binadamu na viumbe wasioonekana na haya yote ni kwa ajili ya kupata mrithi ambae atafikia juu kabisa mwa levo zote ili kutimiza lengo flani , kama nilichootea kipo sahihi basi sababu inayokufanya kuwa mbele yangu saa hii ni kwasababu mimi ndio kiumbe pekee niliefanikiwa kuzijua siri zote za andiko la urejesho na kuyafkia mafannikio , binadamu ambae unapanga kumchagua …”
“Paah ! Paah!!”Sharif alijitkuta akipiga makofi kwa nguvu mara mbili huku akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake.
“Sio mbaya , katika sehemu zote ulizoongea umepatia , hii mbinu licha ya kwamba sijaigundua mimi lakini imechukua nguvu zangu nyingi kuielewa juu ya siri zake na hata kuirahisisha jina ambalo uliipatia mbinu hii ndio jiina hilo hilo ambalo mbinu hii inafahamika, Andiko la Urejesho waAzimio”
“Tofauti kubwa kati ya mbinu zote za kuvuna nishati za mbingu na ardhi na nyingine zote zinazotumiwa na viumbe wa aina zote wenye nguvu ni kwamba mbinu nyingine zinamtengenezea mvunaji njia ya kupita na hatimae kufikia mwisho na kupata ufunuo mpana , lakini mbinu ya Andiko la urejesho wa Azimio inamuonesha Mvunaji kwanza mwisho wa safari ulivyo kabal ya kuianza safari na njia ambayo mtu atatumia kupita mpaka kufikia huo mwisho alioona ni juu yake yeye mwenyewe kuitafuta , ki ufupi ni kwamba ni aidha kupata mafanikio katika hatua ya kwanza au kutumia maisha yao yote kujaribu kusiku kwa faida”
“Katika kipindi cha miaka elfu kumi yote kulikuwa na baadhi ya watu wachache sana tena binadamu ambao waliweza kufanikiwa kujua maana ya Andiko hili ni nini lakini nikiwalinganisha na wewe umewaacha mbali mno , Mastar wako Tang Chi alipata mafanikio ya juu juu ila huwezi kumlinganisha na wewe”Aliongea Sharif lakini Roma hakuonyesha ishara ya furaha wala huzuni.
“Hebu acha kuzunguka zunguka , ni ipi nia yako kamili kwa kufanya na kuongea haya yote?”Aliuliza Roma akiwa siriasi.
“Je unajua ni vimondo na magimba mangapi yanatosha kuharibu uhai wa dunia ambayo yameweza kuikaribia dunia katika miaka elfu hamsini iliopita?”Aliuliza.
“Wewe si umesema mwenye ni kila baada ya miaka milioni kumi”
“Hio ni nadharia tu , ni kama hesabu za Probability na uwezekano huo ni mdogo , lakini haiondoi uwezekano wa magimba na vimondo kuipiga dunia katika kipindi cha muda mfupi tu , kati ya miaka elfu hamsini iliopita na sasa , kimondo kilichosababisha Barringer Crater kuna kubwa zaidi angalau mara ishirini ya kimondo kile na kama kikipiga hapa duniani , inatosha kabisa kuibaribu dunia yote na kufuta uhai”
“Kama ni hivyo si ingekuwa miaka elfu hamsini iliopita ndio maisha yageanza?”Aliuliza Roma.
“Sababu ya Magimba hayo ya anga za juu hayaifikia dunia ni kwasababu ya mimi kama Mjumbe wa mkuu wa Enzi”Aliongea.
“Wewe…!!!”Roma alionekana kufikiria kitu lakini aliona ni nguvu kuvuta taswira.
“Kwahio unataka kusema kwmaba unao uwezo wa kupindisha muelekeao wa vimondo visifikie dunia , hebu acha kunitania , kama ni hivyo si utakuwa na uwezo wa kuupoteza hata mwezi?”
“Unaonekana kushangaa na hii inamaanisha huna imani yoyote nje yako tofauti na uwezo wako pekee , ukweli ni kwamba Wajumbe wa mkuu wa Enzi ambao waliacha dunia na kwenda nje galaksi nyingine wanao uwezo hata wa kuharibu sayari”
Roma alikuwa ni kama anaona muonekano wake mwenyewe , ilikuwa ni dhahiri alikuwa katika bumbuwazi lakini ilionekana ni kama vile Sharif hakuwa akitaniana nae.
Roma alijiuliza maswali mengi juu ya Wajumbe wa mkuu wa Enzi, Galaksi nyingine , alijiambia kwahio hao wakuu wa enzi tuseme wameenda nje ya anga la kawaida , yaani katika mbingu nyingine.
Mara baada ya kumuonaRoma akiwa katika hali ya Bumbuwazi aliona lazima atakuwa ameenda mbali katika maneno yake hivyo alimpa ishara Roma kutosisimkwa na mwili sana na kumsikiliza taratibu taratibu.
Sharif alijiweka sawa kama mtu ambae anakusanya mawazo yake na mara baada ya muonekano wake wa kawaida kurudi alianza kumwelezea kila kitu kuhusu Wajumbe wa mkuu wa Enzi , stori ambayo inaanzia juu ya yeye mwenyewe ni nani haswa.
****
Miaka elfu hamsini iliopita Sharif alikuwa ni mtoto wa kiume aliezaliwa nje ya ndoa ambae alikuwa amechanganya damu , akizaliwa na mama ambae ni binadamu wa kawaida na jini jamii ya mapepo , kutokana na kuzaliwa nje ya ndoa na binadamu ilimfanya kutohesabika kama mtoto mwenye umuhimu ndani ya familia ya baba yake Sharif.
Ikumbukwe kipindi hichi ni wakati ambao binadamu , majini pepo na majini watu walikuwa wakiishi pamoja , yaani kabla ya vita na utenganisho wa jamii hizo na hii ilifanya hata kwa majini pepo kuwa na koo zenye majina ya kufanana na za binadamu leo hii , hivyo Sharif alitokea katika ukoo wa Sharif kutokea bara la Asia yaani Uarabuni.
Ndani ya familia ya Majini Sharif , Sharif uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi ulikuwa mdogo sana zaidi ya kichekesho , mdogo zaidi hata kwa wadogo zake ambao walikuwa ni majini kamili.
Kitu ambacho familia ya Majini Sharif hawakukifahamu ni kwamba Sharif kilichosababisha uwezo wake kuonekana mdogo sio kama alikosa kipaji au elimu bali ni kwamba uwezo wake wa akili ulikuwa mkubwa zaidi kuliko familia nzima , kipindi hichi alikuwa ni kama mtoto ambae alipata maono tayari hivyo mbinu yake ya mafunzo ilikuwa ni tofauti kabisa na ndugu zake.
Mara baada ya kutengwa sana na familia kwa kuonekana mzigo alijifanyisha kufa wakati wa vita ya viumbe wa dunia na hapo ndipo alipoweza kujitenga na familia yake kwasababu ilijua alifariki walimsahau.
Haikueleweka alikuwa na elimu gani wala ufunuo wa namna gani , kwake ilikuwa ni kama Mungu akujie ndotoni na akuonyesha Akhera au Mbinguni kulivyo lakini akuambie shika hili andiko na elewa maana yake ili kuijua njia ya kufika Uzimani yaani Akhera au Mbinguni , hiki ndio kilichomtokea Sharif.
Sharif ambae alikuwa kama binadamu wa kawaida alikuwa tayari ashaingia katika kituo cha juu kabisa cha levo ya mapigo elfu kumi ya radi wakati ambao Aoiline Jini jamii ya Mbweha alipoanza kuupata umaarufu miaka elfu hamsini iliopita.
Ukweli ni kwamba licha ya Sharif mweyewe kutoweza kukutaa ana kwa ana na Wajumbe wa mkuu wa Enzi lakini alikuwa ashawafikia ki uwezo au pengine kuwapita kabisa na alifikia katika levo ambayo ilimuwezesha kufungua malango ya kwenda kwenye Galaksi nyingine ambako Mkuu wa Enzi na wajumbe wake huishi.

Wakati Sharf anafikia levo ya juu kabisa akiwa amejitenga alijikuta akipata uwezo wa kuweza kusafiri katika eneo lolote juu ya dunia , ikiwemo kuingia katika gereza la roho na kutoka ambalo lilitengenezwa na Wajumbe wa mkuu wa enzi , pamoja na kuingia ulimwengu wa kimaajabu wa majini pepo , pamoja na ulimwengu wa jicho la Anga kipindi hicho bado ulimwengu huo haujafahamika bado .
Katika matembezi yake hayo alikuja kujifunza ulimwengu wote wa aina tano umeungana katika sayari moja ya dunia kwa nama ya kipekee.
Mkuu wa Enzi pamoja na wajumbe wake ilionekana walitumia uwezo mkubwa sana wa akili kutengeneza kitu kama hicho.
Na wakati wa utenganisho kuanza kulikuwa na majini wengi wabaya ambao walikuwa wamefungiwa katika gereza la roho lakini kutokana na nguvu kubwa za giza walifanya ulimwengu wa majini wwatu kulemewa
Hivyo ndipo Wajumbe wa mkuu wa enzi walipotengeneza malango ya anga ambayo huunganisha ulimwengu wa jicho la anga na Gereza la roho na kuanza kunyonya nguvu za giza kuzijaza katika ulimwengu huo.
Kwa bahati nzuri ni kwamba nishari hasi inao uwezo wa kunyumbulishwa na kutengeneza radi ya zambarau hivyo walitumia nguvu zilezile za kwao za giza kutengeneza radi katika mnara ili kuzuia majini hao wasitoroke
Mambo haya yote yalifanyika kwa ajili ya usalama wa binadamu kwani kipindi hicho ndio wakati wao uliwadia wa kuondoka duniani na kurudi walikotoka
Walikuwa na uwezo wa ajabu mno zaidi ya nguvu za nishati ya mbingu na ardhi hivyo kuwa na uwezo wa kusafiri kwenda katika mbingu nyingine kabisa ya kushangaza.
Lilikuwa ni jukumu lao kulinda dunia kwa wakati huo lakini haikuwa kazi yao kulinda dunia milele hivyo mara baada ya kumaliza misheni yao walipaswa kurudi.
Misheni yao kubwa ilikuwa ni kwa ajili ya kuendeleza kizazi cha binadamu hivyo walipaswa kuhakikisha dunia sehemu ambapo ni nyumbani kwao panakuwa salama.
Hivyo majini wale wabaya walifungiwa gerezani na wale ambao walionekana kuwa wajanga wakawekewa mtego wa mnara ili kuwavuta kwenda kwenye ulimwengu mwingine
Sasa haya yote yalijulikana kwasababu waliacha maandiko juu kabisa ya mnara wa maajabu.
Ijapokuwa ulimwengu hizo zilionekana kama gereza lakini nia kubwa ya Mkuu wa Enzi kupitia wajumbe wake ni kutenganisha viumbe hatari na binadamu wa kawaida.
Viumbe wa dunia walikuwa ni majini watu , Majini pepo na binadamu na Mkuu wa enzi kupitia wajumbe wake alipanga kuacha mtu ambae anapaswa kuwa mwangalizi wa dunia na mtu ambae alichaguliwa kwa wakati huo ni Sharif lakini hata hivyo hakumpa misheni hio moja kwa moja.
Katika mnara wa Anga kuliwachwa nyaraka za lugha ilioandikwa na wajumbe , naraka hizo zilikuwa zikielezea mtu yeyote ambae ataweza kupitia mapigo tisini na tisa ya radi ya Zambarau na kufika kileleni mwa mnara , iwe ni binadamu , iwe ni jini mtu , iwe ni jini pepo kutoka ulimwengu wa majini pepo ilimaanisha nguvu yake ni kubwa ya kukidhi kigezo cha kurithi cheo cha Uangalizi kwa niaba ya Mkuu wa Enzi.
Ukweli ni kwamba Roma yeye ni Special case kutokana na uwezo wake mkubwa mno , kwanza kabisa mwili wake ulikuwa timamu mno kwa kwa kufanyiwa sayansi nyingi na kupata mabadiliko , pili aliweza kubahatika kumiliki Dhana ya Cauldron ambayo iitumiwa na Wakuu wa Enzi kumfungia mnyama Chaos.
Sababu ya Mkuu wa Enzi kupitia wajumbe wake kuacha nyaraka ya maelekezo juu ya mnara wa anga ilikuwa ni kama misheni ya kukidhi vigezo kwa mtu ambae anapaswa kuwa Mwangalizi kwa niaba.
Mkuu wa enzi aliamini mtu yoyote ambae ataweza kufika katika mnara huo na kuvuka Dhiki ya mapigo ya radi basi moja kwa moja inamaanisha anakaribiana ki uwezo na wajumbe wake hivyo anatosha kuwa mwangalizi.
Hivyo kwa lugha nyepesi ni kwamba wajumbe walikaribiana ki uwezo na mtu yoyote atakaefanikiwa kuingia katika mnara na kufika kileleni na hii ipo hata kwa Aoiline pia.
Wote ambao hufanikiwa kufika katika mnara huo kwa maelekezo ya nyaraka hizo wanapaswa kufanya chaguzi, mosi ni kuchukua Dhana ya Ngoma ya kinaoni na kuondoa radi inayowazuia majini pepo kutotoka katika ulimwengu wa majini pepo , pili ni kuiacha ngoma hio ili kuendelea kutenganisha binadamu na Viumbe hao hatari.
Ilikuwa ni kwa ajili ya kuwapa viumbe wote nafasi sawa , iwe ni majini watu , iwe ni binadamu wenye uwezo wa kuvuna nishati za mbingu na ardhi au majini.
Kama angetokea kiumbe chochote kikawa na nguvu na kuua binadamu basi ilimaanisha hio ndio hatima yao , hivyo hivyo kwa majini pepo.
Sasa Sharif ndio wa kwanza kabisa kuingia katika ulimwengu wa majini pepo kupitia mnara na hio yote ilikuwa ni kutokana na shauku yake tu.
Wakati huo mnara huo ulikuwa wazi masaa yote na miaka yote na haikuwa kila baada ya miaka sitini.
Mara baada ya kudhurula ndani ya ulimwengu huo wa majini pepo kwa muda hatimae aliamua kuondoka kwa kuingia katika floor ya kwanza ya mnara wa mbingu na kupanda juu hatua kwa hatua akipitia mapigo ya radi mpaka kileleni, alikuwa na uwezo mkubwa hivyo ilikuwa rahisi kwake.
Sasa mara baada ya kufika katika kilele cha mnara huo ndipo alipokutana na nyaraka zilizoachwa hapo kwa makusudi maalumu na palepale alijua yeye ndio wa kwanza kama kiumbe wa dunia kufika hapo.
Na ndipo alipokuja kupta ufahamu juu ya uwepo wa viumbe hai kabla ya binadamu katika uso wa dunia ambao walipotea mara baada ya Dunia kupigwa na kimondo , alipata kujua pia ni Mkuu wa Enzi na wajumbe wake waliokuwa wakihakikisha dunia inakuwa salama kwa kupindisha magimba makubwa kutoka angani ili yasiingie katika mzingo wa dunnia.
Haikueleweka kwanini Mkuu wa Enzi alikuwa akijali sana viumbe wa Dunia , haikueleweka kwanini alikuwa akiwalinda lakini mara baada ya Sharif kusoma barua hio alijua kwanzia siku hio amekuwa Mwangalizi wa usalama wa dunia, yaani amekuwa kama Mjumbe wa Mkuu wa Enzi licha ya kwamba ni nusu binadamu nusu jini.
Kila yoyote ambae angeweza kufika kilele cha mnara huo ilimaanisha alikuwa na uwezo wa kuibeba misheni na sio hivyo tu anao uwezo pia wa kuchukua nguvu ya Ngomba kama uwezo huo wanao.
Mwanzoni Sharif mara baada ya kupata misheni mpya alitaka kupotezea , lakini badala yake aliona lazima dhamiri ingemfunga milele hivyo moja kwa moja aliamua kukubali misheni yake na kwanzia hapo ndipo alipoitwa Master namba moja.
Alikuwa na uwezo hata wa kuondoka ndani ya hii syaari lakini hakufanya hivyo na aliamua kuishi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini kwa ajili ya kutii maagizo ya mkuu wa enzi.
Lakini Sharif hakuwa na mpango wa kuwa Master namba moja milele , hakuwa akiataka kuwa muangalizi milele na alipaswa kuondoka na kuwafuata Wajumbe wa mkuu wa enzi na ili kuondoka misheni ilikuwa ni kutafuta mrithi wake ambae angeendeleza alipoishia
Kwa lugha nyepesi ilikuwa ni kwamba misheni yake ilipaswa kuisha mara tu baada ya kupata mrithi.
Sasa siku hio hio ambayo aliingia katika mnara huo tayari alikuwa ashaandaa mpango wa kutafuta mrithi , yaani siku ambayo anapata isheni ndio siku ambayo alianza kuanza juu ya kupata mrithi wake.
Sharif alichukua ufunguo wa ulimwengu wa jicho la anga , yaani ile hazina inayofanana na kokoto ya umbo la mviringo na kisha ndipo alipotoka na kurudi ulimwengu wa binadamu.
Wakati anatoka tayari vita baina ya viumbe wa dunia ilikuwa ikiendelea bado na kutokana na uwezo wake aliamua kuzamia katika miliki ya majini chotara yaani Panas na kujiita jina linalofanana na jamii hio lakini licha ya kuwa na uwezo mkubwa hakujionyesha kabisa.
Ilikuwa ndio kipindi hiko hiko aliweza kukutana kwa mara ya kwanza na mrembo Aoiline ambae ndio yupo juu ki uwezo na kuzoeana lakini kwa bahati mbaya wakati huo tayari alikuwa na misheni hivyo ilikuwa ngumu kuwa nae kimapenzi , ijapokuwa mwanamke huyo alikuwa mrembo na alionyesha kila dalili ya kupendwa lakini alimkataa.
Aoiline alikuwa ni jini mwenye akili sana na alikuwa na uwezo wa kukisia mambo mengi hata yale ambayo Sharif hakumweleza na ili kutokuwa kikwazo kwa Sharif aliamua kutorokea kwa hiari yake katika ulimwengu wa majini pepo.
Aoiline hakuvutwa a mnara kama ilivyokuwa kwa majini wengine bali yeye mwenyew kwa hiari yake aliacha ndugu na kupotelea kwenye ulimwengu wa majini pepo.
Sharif hakutaka kumzuia Aoiline kutokana na kwamba alikuwa na vitu vingi vya kufanya.
Sharif ili kumaliza vita aliamua kuwavuta majini pepo wengi kuingia katika ulimwengu wa jicho la anga na mara baada ya kufika huko alijilipua kimaigizo huku akiwaua wote na ndipo walipogeuka mizimu baadae.
Kitendo alichokifanya Sharif katika ulimwengu huo wa jicho la Anga ulifanya kutengeneza upenyo kupitia ulimwengu wa ajini watu kwa kila baada ya miaka mia moja.
Kwasababu alichukua Hazina iliokuwa ni ufunguo unaounganisha ulimwengu wa jicho la anga na mnara geti lilijifunga na kupelekea nguvu hasi ya kutosha kutoingia katika mnara na hatimae kwenye Dhana ya ngoma kirahisi pamoja na kushikiria geti la mnara kwa upande wa majini pepo hivyo kusababisha mnra huo kufunguka kila baada ya miaka sitini kipindi maalumu ambacho Ngoma hio imekusanya nishati za kutosha kushikilia geti la mnara kuwa wazi.
Mara baada ya kutoa hazina hio alirudi katika asili yake sasa ambayo ni familia ya Sharif na kuacha hazina hio pamoja na ujumbe kwa kuwaeleza ili kurudisha wenzao ambao wamepotea yaani wale aliolipua katika jiccho la Anga na ambao wamemezwa na mnara basi Hazina hio ndio njia na hakueleza ni kwa namna gani ni njia na alifanya hivyo kutokana na kwamba aliamini hatima ndio itaamua.

Sharif yeye liacha hazina hio katika mikono ya ndugu zake akichukulia kama zawadi kwao lakini wakati huo akikisia kwamba kama itaokea majini pepo wataiteka miliki ya majini watu hivyo kuna uwezekano wa hazina hio ikafanya kazi kwa kufungua lango , kitu kama kilichomtokea Roma wakati ule , ilikuwa ni kama kitu kilichopangwa ambacho hakiwezi kubadilishika.
Sasa miaka elfu therathini ilipita ya Sharif kuendelea kufanyia kazi misheni aliopewa na kimya kimya aliendelea kuangalia ndugu ake wakati huo huo akiisaidia dunia katika kudili na mambo hatarishi.
Lakini kadiri alivyokuwa akiishi alikuja kugundua alikuwa akizidi kuongezeka ki uwezo maradufu huku binadamu , majini pepo na majini watu wakizidi kupoteza uwezo .
Majini pepo ambao walibakia katika ulimwengu wa kibinadamu ili kuepuka kushambuliwa na majini watu walienda kujichimbia katika ulimwengu wa jangwa tenganifu huku wakiaha Hazina katika ulimwengu wa binadamu wakiamini hio ndio sehemu waliopotea ndugu zao na kama walivyoambiwa ndio njia ya kuwarudisha basi tokea hapo waliifanya kama Dhana ya imani yao.
Upande wa majini watu Sharif pia aliona ni upuuzi mtupu kwani hakukuwa na wapanda levo zaidi ya udanganyifu tu.
Kitendo cha majini kupoteza uwezo kila kukicha ilimfanya kuwa na wasiwasi kama itakuja siku kupata mrithi na kujiuliza kama kuna hata haja ya viumbe hao kubakia katika dunia.
Alijjiuliza maswali mengi na wakati huo moja ya maswali hayo ni je kuwaacha binadamu kuwa watawala wakuu wa dunia kama ilivyoamuliwa na Mkuu wa enzi na kuwatenganisha na majini pepo.
Kadri ambavyo alikuwa akipanda levo ni kama alikuwa akijiweka mbali zaidi na viumbe wa binadamu , alichojali ni usalama wa dunia tu na sio usalama wa binadamu au majini.
Lakini kabla hata hajajua majibu ya maswali yake ikiwa imepita miaka elfu therathini ndipo viumbe kutoka sayari nyingine walitua duniani.

SEHEMU YA 787.
Sharif kwa muda mrefu alikuwa ashajua juu ya kabila la viumbe hao licha ya kwamba hakuwahi kufika katika sayari ya Mars.
Tofauti na kuwa na wasiwasi juu ya ujio wa hawa viumbe alijikuta akifurahi.
Likija swala la nguvu na uwezo miungu walikuwa na nafasi kubwa hapo kutokana na kwamba walizaliwa wakiwa na uungu ambao unawawezesha kuzitambua kanuni za anga.
Uwezo wa namna hio ni kama zawadi kutokana na kuwa na nguvu kubwa mno.
Kitu kingine kilichowapatia faida miungu ni uwezo wao wa kuhamisha nafsi zao kutoka mwili mmoja kwenda mwingine , hivyo walikuwa wakiishi muda mrefu kuliko binadamu.
Ijapokuwa miungu walikuwa na uwezo wa chini kuliko wajumbe walikuwa na uwezo wa kutegemea miili yao tu kusafiri kutoka katika sayari moja kwenda nyingine lakini ilikuwa ngumu kwa majini pamoja na binadamu kusafiri kutoka sayari moja kwenda nyingine na kuweza kupona na adha ya anga labda tu mtu awe levo ya mapigo elfu kumi ya radi.
Kitu kingine ambacho kilionekana kuwa faida kwa miungu ilikuwa ni kwamba wameungana pamoja kifikra yaani miungu yote kumi na mbili na walikuwa na mama mmoja wa kiuungu hili liliwapelekea kupunguza mingongano ya ndani licha ya kwamba kuna kutoridhika kati yao.
Ustaarabu katika sayari ya Mars chini ya miungu ulikuwa umeendelea mno kuliko hata wa dunia ya sasa.
Kama ugefananisha ustaarabu wa miungu na wa sasa wa kibinadamu ni kama vile ndio kwanza tupo katika zama za mawe, miungu walikuwa wa moja na hakukuwa na utofauti wa kidini wala kimsimamo ni kama wote walikuwa na mawazo sawa, ilikuwa ni sahihi kuita ulimwengu wao ni wa kiutopia.
Sasa mara baada ya sayari yao kushindwa kusapoti maisha na mti Mama kunyauka mahai sahihi walipoona ni pakukimbilia ni sayari ya Dunia lakini walijua fika miili yao haiendani na mazingira ya dunia kwa muda mrefu na hapo ndipo maauzi yalipofanyika kuhamisha nafsi zao na uungu wao kwenda kwa nafsi za binadamu.
Miungu kumi na mbili kutokana na kwamba walikuwa ndio uzao wa kwanza wa mti walikuwa na nguvu kubwa na walifanikiwa kuziteka nafsi za binadamu na kutawala miili yao , lakini ndugu zao ambao hawakuwa na nguvu kubwa kama wao waliishia kumezwa na nafsi za binadamu.
Sasa mara baada ya vita kuanza kati ya majini watu na miungu upande wa Sharif yeye alikaa pembeni kuangalia kinachoendelea na hakusaidia upande wowote.
Ijapokuwa Sharif alikuwa na uwezo wa kuua miungu hao kirahisi tu ikiwemo Athena na Zeus lakini hakuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Na hio ni kwasababu tokea zamanni alikuwa ashaacha kuingalia dunia kwa mtazamo wa kawaida , binadamu na miungu wote waliishi katika anga na mhimili wao ni sayari zao , ni rahisi kusema wote wana haki ya kuishi katika anga hivyo Sharif aliona hata wao wana haki ya uhai ndani ya mhimili wa sayari ya dunia na hakutaka kutofautisha viumbe kwa kuwaita Alliens.
Kipindi hicho ndio ambapo Sharif wazo lilimwingia na kuona kama dunia itatawaliwa na miungu basi moja kwa moja misheni yake inaweza kufikia mwisho.
Aliona kabisa miungu walikuwa na uwezo wa kulinda dunia na isipotee kwa kugongana na magimba au vimondo na wakati huo huo ustaarabu wao ulikuwa umekuwa sana kuliko hata ilivyokuwa binadamu.
Ukumbuke kipindi hichi miungu wakati wanashuka binadamu hawakuwa hata wakijua gari ni nini na walitegemea miguu yao kusafiri.
Sharif katika misheni yake ilikuwa ni kulinda viumbe wa dunia wasipatwe na majanga ya nje ya dunia lakini sio kuwafanya binadamu kuwa juu ya viumbe wegine au kuwa chini ya viumbe wengine , alijua kama miungu watakuwa ndio viumbe wenye nguvu zaidi ya binadamu kutokana na maendeleo yao basi wasingepoteza rasilimali za dunia katika kupambana wao kwa wao bali wangefikiria namna ya kuendeleza dunia jambo ambalo si baya.
Wajumbe wa mkuu wa enzi walikuwa tayari wamekisha andaa kila kitu , kulikuwa na safu ya ulinzi wa gereza la roho kwa ajili ya mashetani , mapepo na mazimwi kutokana na kwamba hawakutaka kuwaua wote na kutokana na hilo Sharif aliona hata kabila la waliostaarabika la miungu Mkiuu wa enzi na wajumbe wake wataweza kuwavumilia , isitoshe ndio walikuwa wakitafuta mahali pa kuishi.,
Ukweli ni kwamba Sharifi wakati huo alikuwa katika kujiluliza kwingi kama angeweza kufanya maamuzi hayo angeenda kinyume na mipango ya mkuu wa enzi lakini kwasababu hayakuwa maamuzi rahisi basi aliamua kuangalia kwanza kitakahotokea.
Katika miaka iliofuata ya miungu kufanikiwa kutawala baadhi ya miili ya kibinadamu , Sharif aliweza kugundua ni miungu wamepoteza miili yao na hawawezi kuendeleza kizazi chao.
Kitendo cha miungu kutelekeza miili yao ilimfanya Sharif kuingia katika uchunguzi na alichokuja kugudua kilimshangaza sana , ilionekana miungu hawakutegemea jua moja kwa moja kwa ajili ya kuishi na miili yao kusapoti maisha bali walitegemea jua kwa njia isiokuwa ya moja kwa moja.
Sharif alifungua miungu waliishi chini ya mti na huo mti kazi yake ilikuwa ni kubadilisha nishati ya jua kuwa nishati tofauti ambayo husapoti miili yao na kuwapelekea kuzaliana na mti kuwatunuku uungu.
Mara baada ya sayari yao kukubwa na janga lililowafanywa wakimbie Astreus moja ya viumbe hao aliamua kuficha moyo wa Gaia katika teknolojia ya kipekee na kuja nayo duniani , moyo wa Gaia ilikuwa ni kama mbegu ya mti huo.
Sasa Sharif mara baada ya kufanya utafiti wake wa chini chini alikuja kugundua mengi , alishangaa mara baada ya kugundua ni kweli mti maa ndio ulikuwa chanzo cha nguvu za miungu lakini nguvu zao walizipata kwa gharama ya nishati ya sayari yao kiasi cha kuipelekea kupoteza sifa ya uhai kwa spidi kubwa sana.
Ufumbbuzi wa jambo hilo ulimfanya kusita na mpango wake wa kuwafanya miungu kuwa juu ya binadamu
Alijua kama miungu wangepatia dunia kuitawala ni swwala la muda tu kuupata moyo wa Gaia na kisha kuufufua na kupanda Mti Mama tena ili kuarudisha uzao wao.
Misheni yake ilikuwa ni kulinda dunia na kama jambo hilo angeruhusu ilikuw ani kama anaangalia dunia ikiangamia.
Sharif ambae alikuwa na cheo cha uangalizi kutoka kwa Mkuu wa Enzi alijikuta akishindwa kufanya maamuzi ya moja kwa moja aidha kuwapa ukuu miungu kuitawala dunia au kuendelea kulinda ustaarabu uliopo wa kiumbe binadamu.
Wakati huo huo aliikuwa akiataka kuungana na wajumbe kwa Mkuu wa enzi haraka iwezekanavyo lakini hakuwa na uwezo wa kuondoka duniani kabla misheni yake haijaisha baada ya kupata mrithi.
Hivyo ilimpelekea Sharif kuchukua hatua kama Mwangalizi na kisha kuwaza maswala mengine baadae.
Alijifanyisha ni jini mtu kutokea Hongmneng kwa kubadili muonekano wake pamoja na uwezo wake kuushusha kidogo na hivyo kumfanya awe moja ya kiumbe jini mtu mwenye nguvu kubwa.
Baada ya kujifanyisha anapigana na Zeus alimtega na kumwingiza katika ulimwengu wa majini watu na kisha akamfungia katika gereza la roho huku Athena akimwahia huru makusudi.
Kufungiwa kwa Zeus ilimaanisha miungu kukosa nguvu ya kivita kwa asilimia hamsini na kushindwa kutamba mbele ya majini watu hivyo wakaona waache vita na hapo ndipo ulipotokea mkataba wa The Gods Treaty .
Maongezi hayo kati ya Roma na Master namba moja yalidumu kwa muda mrefu sana tokea mhana mpaka usiku.
Roma kadri alivyokuwa akimsikiliza Sharif akielezea historia hio ya miaka mingi alijikuta akkishindwa kujizuia na kutoa tabasamu hafifu.
“Dogo hivi unadhani kwa yote ambayo nimefikiria na kufanya ilikuwa ni kupoteza muda?”
“Sidhani kama ilikuwa ni kupoteza muda , kwako wewe haikujalisha ni binadamu , majini au miungu walikuwa ni kama kunguni tu ambao hupambana wao kwa wao na wewe ulikuwa ukiifurahia vita yao , haikujalisha maamuzi yako yalikuwaje lakini mwisho wa siku kila kitu ni juu yako”Aliongea Roma na kumfanya Sharif kuoekana ni kama vile ametegemea jibu la aina hio.
“Kama kweli hicho ndio unachofikiria , kwanini ukamuacha Athena ili hali ulikuwa na uwezo wa kufanya hivyo , kama hutaki kumua unafanya nini hapa peke yako?, unazo nguvu za kufanya maamuzi yoyote yale lakini bado upo hapa kujisahaulisha , vitu nilivyofanya vinaweza kuwa nikupoteza juhudi zangu lakini ni angalau kuliko chaguzi uliofanya
Mara baada ya neno Athena kutamkwa macho ya Roma yalicheza huku akikunja ngumi yake na kihisia alikosa mhimili lakini mara baada ya kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa alionekana kutulia , kwani bado alikuwa katika bumbuwazi juu ya maneno ya Sharif.
Roma alijiuliza hata kama ni kweli anao uwezo wa kufanya maamuzi yoyote je ni maamuzi ambayo anaweza kufanya kirahisi.
“Muunganiko wangu na hii sayari pamoja na viumbe vyote hai ni kama muunganiko wako na Athena , ijapokuwa ni toafuti lakini kuna uhusiano , umeshindwa kufanya maamuzi kwa sababu ya mwanamke mmoja , je unadhanni ilikuwa rahisi kwangu kufanya maamuzi kwa niaba ya viumbe wote?”
Awamu hio Roma hakuonyesha kumcheka ni kama kwa namna flani alikuwa akizielewa hisia zake , lakini kwa wakati mmoja alikuwa amekasirika kwasababu alijua nia yake kwake.
“Umefanya mambo mengi na bado ukasubiri kwa miaka elfu ishirini je ni kwasababu ulishindwa kufanya maamuzi wewe mwenyewe , ndio maana unataka mimi ndio niamue ni nani anapaswa kuitawala dunia?”Aliuliza Roma na Sharif aliishia kutingisha kichwa asikatae.
“Ndio , unaweza chukulia hivyo , lakini haya sio maamuzi yangu ni hatima yako kama unabii ulivyotabiriwa , wewe ndio mtu pekee ambae utaathiri matokeo”Aliongea Sharif.
“Nini kilichopo nyuma ya huu unabii ambao Athena ameshikilia , je atakuwa alikujua tokea mwanzo na uwezo wako na misheni yako, lazima utakuwa unajua kila kitu kuhusu Athena alichokifanya lakini ukamuacha tu makusudi , je ni kweli?”Aliuliza Roma huku akisaga meno yake.
“Dogo haina haja ya kuwa na hasira ,najua kila kitu unachotaka kufahamu na nisikilize nitakuambia taratibu , nimekuja kwako kuondoa hali ya kuchangayikiwa kwenye moyo wako …”Alionekana kuvuta pumzi na akaendelea.
“Kinachosemekana kama unabii pengine mtu ambae anaweza kukielewa ni Athena mwenyewe, lakini ninaweza kufanya makisio kwa kuangalia tu uungu wake , inasemekana karama ya unabii ndio upekee wa uungu wake , kwa kutegemea tu kanuni za anga anao uwezo wa kujua nini kitatokea baadae , inaweza kuwa ni sekunde ijayo ,dakika , siku , miaka na hata zaidi ya milenia ya wakati ujao …”
Njia pekee ambayo humfanya hupta huo unabii ni kitu ambacho anakifahamu yeye mwenyewe na hakuna mtu anaeweza kuelewa , ni kama sisi tu tunavyopata ufunuo , hata hivyo ukubwa wa athari za mtu , eneo au elementi nyingine za unabii wake katika anga ndio nguvu yake ya kiroho inavyotumika sana , isitoshe mbinu hio ya unabii mkubwa unatokana na kanuni za anga”
Kwa maneno mengine kama Athena atataka kutabiri kesho ya mtu wa kawaida basi ni sawa na kutumia chembe ya nguvu yake ya kiroho lakini kama atata kutabiri kesho yangu haiwezekani.. hii ni kwasababu nimepanda na kuwa juu ya kanuni za anga ambazo anazifahamu , sipo kwenye dimension sawa na yeye
Hatas kama atataka kukutabiria wewe Roma Ramoni itakuwa ngumu mno kwake , hio ni kwasababu wewe Roma wa sasa umebadilika sana tofauti na zamani , unabii wake ulikuwa sahihi tu kabla ya wewe kuingia levo ya mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi , unabii wake ni kama unafamna kujua unafikiria nini na unataka kufanya nini katika sekunde inayofuata hivyo kama utapigana nae atashindwa kuyatabiria mashambulizi yako hivyo hatojisumbua kutumia uwezo wake wa kutabiri na atashindana na wewe bila ya hira yoyote”
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Athena anaonekana kuwa na nguvu kutokana na kwamba anao uwezo mkubwa wa kutabiri tukio litakalotokea ndani ya sekunde moja kuendelea na hii inamfanya kuweza kukudhibiti kabla hata hujafanya shambulizi lakini kama mtu ana uwezo wa juu na yupo juu ya kanuni zake za anga basi moja kwa moja unabii wake unakuwa sio sahihi, alikuwa akimuweza Roma kutokana na kwamba alikuwa na uwezo wa kumtabiria na kujua kila kitu atakachofanya lakini hio yote ilikuwa ni kipindi kabla hajapitia mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi.
“Kwahio Athena hajui kabisa wewe ni nani?”Aliuliza Roma.
“Hapana , ijapokuwa hawezi kutumia unabii wake kukadiria uwezo wangu pamoja na wasifu wangu lazima atakuwa anajua uwezo wangu kupitia njia zingine , ukweli ni kwamba ashajua muda mrefu nitakubali kila kitu anachofanya hivyo hakuwa na haja ya kunitaja kwa yoyote , ni kama tu alivyoweza kuupata moyo wa Gaia , ijapokuwa alishindwa kutabiri eneo husika utakapotokea lakini alikuwa na uelewa ulikuwa ndani ya Taifa la Korea na wewe ndio utakuwa kama ramani kwake”
“Kama mimi wa sasa nitajiweka katika levo ambayo atakuwa na uwezo wa kufanya unabii sahihi , je atakuwa anajua kama unabii huo ni sahihi?”Aliuuliza Roma na kumfanya Sharif kuangau kicheko.
“Ukweli ni kwamba mbingu yake ya utabiri mkuu ishathibitishwa muda mrefu sio sahihi”
“Unamaanisha nini kusema hivyo?”Aliuliza Roma akiwa katika mshangao.
“Umenisikia vizuri , unabii wake mkuu wa Athena sio sahihi kwa asilimia mia moja , kuna mbinu za moja kwa moja za kuharibu utabiri wake kuliko kwenda mbali kwa kujiweka katika levo anayoweza kutabiri”Aliongea na kumfanya Roma kuonekana kuchanganyikiw .
“Ili kufanikisha hilo ni kumhusisha yeye mwenyewe kama kipengele cha unabii”Aliongea Sharif na kumfanya Roma kuwa na ufahamu unaokuja kwa mbaali.
“Athena ndio wa kwanza , mtu anawez akusema ni yeye pekee anaejua kila kitu anachotabiri kwa ukamilifu , hii inamaanisha kwamba ikiwa anataka kuathiri mustakabali wa jambo , anachohitajika kufanya ni kurekebisa tu baadhi ya hatua alizokuwa amepanga kuchukua na historia itabadilika yenyewe na mustakabali utafuatia”
“Kama ni hivyo , uliposema unabii wake haupo sahihi miaka kadhaa iliopita , je ni kwasababu alifanya kitu ambaho hakupwaswa kufanya?”Aliuliza Roma.
“Upo sahihi , ni kipindi kilichopita ambacho kinakuhusisha wewe zaidi, Athena hakutarajia atakuzalia mtoto na kumfanya ahame mwili mapema”Aliongea Sharif na ilikuwa ni kama ameshusha bomu.
“Unasema nini!!”Roma alijikuta akishindwa kuedelea kukaa na kujikuta akisimama huku macho yake yakimtoka wakati akuongea.

“Lanlan ?! , unamaanisha Seventeen alikuwa…”Aliuliza Roma kwa kuchanganyikiwa lakini Sharif alikunja nne kwa pozi murua.
“Hivi bado hujawahi kuwaza , hakukuwa na hali isiokuwa kawaida wakati ulipokuwa nae ?,Seventeen ni mwanamke ambae Athena alitawala mwili wake wakati akiwa hatua za mwisho za uhai wake , yote haya alikuwa ni sehemu ya unabii wake wa mwanzo”
Roma alijikuta akipata picha ya Lanlan kulazimisha Edna kuwa mama yake mzazi kila muda na Roma kukumbuka wakati ambao Edna alikuwa akitamka maneno ya Seventeen aliowahi kuongea.
Roma alikuwa na hisia za namna hio lakini mara baada ya kuthibitisha kwa masikio yake ilifmanya ajione ni kama amepigwa na radi.
“Sina uhakika unabii wa Athena wa mwanzo ulikuwaje lakini nilikuwa nikimwangalia hatua kwa hatua , ni wazi kabisa mara baada ya kuhamia katika mwili wa Seventeen hakutaka kabisa kuwa karibu na wewe lakini alishindwa kutabiri wakati atakapoamka katika mwili wa Seventeen tayari ana hisia za kimapenzi kwako na kubeba mimba yako”
“Unapaswa kuelewa kanuni za anga hazina athari yoyote mbele ya mapenzi ya kibinadamu ambayo huvuka nafasi na muda , upendo ni hisia nyeti ambazi hata miungu na akili zao zote wameshindwa kuelewa , ndio nguvu ya ajabu ambayo binadamu anayo ambayo haipo chini sana na uungu wa miungu”
Athena anaweza kutabiria kila kitu isipokuwa tu upendo anaokaribia kukutana nao , kwani mapenzi ya kibinadamu kadri yanavyosababisha hisia kali ndivyo unavyokosa maana na mantiki , Wakati Athena nafsi yake inaamka katika mwili wa Seventeen tayari alikuwa ni mjamzito na mtoto wako na ni wakati alipokuwa amezama baharini , labda unaweza kujiuliza kwanini aliamua kujificha kwa kutumia helmeti , kuzaa mtoto na kisha kumkabidhi kwa Tang Chi , lakini hayo yote yalibadilisha historia nzima , mapenzi ya kweli na mtoto ambae hakupaswa kuwepo kwenye maisha yake ilimfanya kufanya chaguzi nyingine ili kurekebisha makosa ya unabii wake wa mwanzo”
“Hembu subiri”
Roma alionekana kuingialia maneno ya Sharif huku akiwa na muonekano ambao una wasiwasi.
“Kama uyasemayo ni kweli , si inamaanisha Edna tokea mwanzo hakuwa ni Athena na hata Seventeen hakuwa Athena wakati tulipoanza kupendana pia?”Roma aliuliza na kumfanya Sharif kutingisha kichwa kukubaliana nae na palepale kumfanya Roma kupambwa na tabasamu la ahueni.
“Asante kwa kuniambia haya .. tafadhari endelea ..nataka kujua kila kitu”
Muda huo alonekana kuwa na furaha kana kwamba amezaliwa upa , miale ya mwanga ilipiga katika maisha yae na kufukuza kiza chote.
Iwe ni kwa Edna na pacha wake Seventeen hao wanawake wote wlaikuwa ni halisi , hawakuwa udanganyifu uliotengenezwa na Athena.
Ukweli ni kwamba hakuwa na chuki na Athena kwasababu yalikuwa ni maamuzi yake ammbayo yaliwezesha Lanlan kuzaliwa.
Kwa sababu zozote zile Roma hakutaka kuvuta taswira ni kwa namna gani Seventeen angejisikia kama angepoteza uhai akiwa na mtoto tumboni kama Athena asingeamua kumzaa.
Kwa ufupi ni kwamba Athena ili kuhakikisha anachotaka kitokee ni sahihi atafanya vitu ambavyo vinachangia mustakabali wa tukio husika , udhaifu mkubwa wa unabii wake ni pale tu anaposhindwa kujitabiria yeye mwenyewe , kitendo cha kushindwa kujitabiria mwenyewe ilimtokea kufanya kitu ambacho hakupaswa kufanya ambacho ni kumzaa Lanlan ambae ni mtoto wa Roma.
Yaani Athena alipanga kuutawala mwili wa Seventeen kwa kuhamisha nafsi yake na uungu wake lakini ikumbukwe kuhamisha nafsi kutoka kwenye mwili mmoja kwenda kwa mwingine sio kitu kinachotokea mara moja , nafsi inapohama hulala kwa kipindi cha muda flani na kisha ndipo huamka , kuwahi au kuchelewa inategemeana sana na uwezo wa uungu wao.
Sasa Athena mara baada ya kuhamisha nafsi yake kwenda kwa Seventeen kutokana na kushindwa kujitabiria wakati anaamka katika mwili wa Seventeen tayari alikuwa mjamzito wa Roma na ndio kipindi ambacho Seventeen anakaribia kupoteza uhai mara baada ya kuzama baharini wakati wa kulipuliwa na bomu na kundi laTakamagahara
Hivyo ni kama Athena alivaa mwili ambao ulikuwa ni mjamzito tayari a tofauti na kuua kiumbe kilichokuwa tumboni aliaamua kulea ujauzito kwa siku kadhaa na kisha akajifungua na baada ya hapo ndipo alipoenda kumkabidhi Lanlan kwa Tang Chi ili kumpelekea Roma , hivyo ni sawa kusema Seventeen na Athena walishikiana kumzaa Lanlan , Seventeen kama Seventeen alimpenda Roma na kubeba ujauzito wake , huku Athena yeye akarithi ujauzito wa Seventeen na kumzaa Lanlan.
Sasa ili kurekebisha unabii ambao Athena alitaka utokee alifanya maamuzi mengine na pengine ndio maamuzi yalioacha akaamua kuuvaa mwili wa Edna pacha wake Seventeen, Roma anafurahi kwa kuona kwamba tokea mwanzo Edna na Seventeen walikuwa halisi na kama walimpenda walimpenda kweli kabla ya kupoteza nafsi zao kwa Athena.
“Nadhani sasa unaweza kudhania ni kipi Athena alifanya ili tu kusahihisha makosa ili apate matokeo ya unabii wa mwanzo kuliko mustakabali ambao huamuiwa na hatima , ingawa kuhamisha nafsi inahitaji nguvu nyingi mno za kiroho lakini mwili wa Seventeen ulikuwa ukipoteza uhai taratibu na hata kama angekurudia ingekuwa tayari amekwisha chelewa kubadilidha unabii na katika maamuzi ya mwisho nipo Athena alipojikuta hana jinsi na kumtumia mtu ambae anaweza kuirudisha hitimisho la unabii wake wa mwanzo na mtu huyo ni Edna na alihama punde tu mara baada ya kuuachia mwili wa Seventeen , aliona kwasababu Edna na Seventeen ni mapacha wa kufanana basi anakuwa mtu sahihi kabisa wa kutengeneza mustakabali wa kesho ambao utakuwa sawa na unabii wake , hivyo maamuzi hayo alifanya mara baada ya kosa la mwanzo
Unapaswa kuelewa ugumu uliopo kuhamisha nafsi kwenda kwa mtoto ni tofauti na kwenda kwa mtot , bila kusahau anahamisha nafsi yake akiwa na asilimia ishirini tu ya nguvu zake zote
Ijapokuwa alikuwa na helmet la kumfanya asionekane na kuhama kimya kimya lakini ilikuwa haiwezekani kuamka mara moja na kwa kukamilika hivyo alichoweza kufanya ni kuufufua uungu wake tu katika mwili wa Edna huku akiitumia nafsi yake kumdhibiti Edna kila muda akihitaji
Wakati Edna anakuja katika hii hoteli sio yeye bali alikuwa ni Athena ambae alicheza na akili ya Edna , alitaka kuwakutanisha na kusababisha kilichotokea baadae , lakini hata hivyo kila kilichowatokea ilikuwa ni wewe na Edna katika uhalisia na sio Athena”
“Athena hakutaka kuhatarisha mpango wake kwa kumgundua mapema ndio maana hakutaka kuupandisha uungu wake wote katika mwili wa Edna ili kumtawala kikamilifu kwa muda mrefu , hivyo kuna muda aliuteka ufahamu wa Edna na mwili wake na kukutana na washirika wake akiwemo Yan Buwen , Athena hakumtawala sana Edna na mara zote aliibadilisha sura yake na kuonekana kama Mzungu mwanadada maarufu ambae ana historia nae nadhani unamjua”Aliongea.
“Clelia Allisanto”Aliongea Roma na hapo sasa ni kama akili yake inakaa sawa vizuri lakini kidogo akionekana kuchanganyikiwa Dorisi alisema alikutana na mwanamke alieitwa Clelia Allisanto wakati huo huo Edna alikutaa na mwanamke alieitwa Clelia Allisanto wakati Athena alikuwa akiishi ndani ya mwili wa Edna wakati huo
“Bila shaka kila kitu kilihotokea kati yako na Eda kilikuwa katika mipango ya Athena kutimiza unabii wake na ndio hizo hatua mlizokuwa mkipiga pamoja ndio zilizomuwezesha kufanikisha kurudisha hitimisho la unabii wake , lakini awamu hii hakutaka kuzembea kama alivyozembea kwa Seventeen baada ya kuchelewa kuamsha ufahamu wake bali aliamua kuwa macho wakati akiwa amejificha ili asifanye kosa tena , lakini hata hivyo kwasababu ya haraka kipindi cha muda wa kujihamisha ulikuwa mfupi sana na kwasababu hakutaka kulala tena kufuta kumbukumbu za Seventeen ndio maana ni kama Edna amekuwa na kumbukumbu zake ndio maana ilitosha kwa binti yako kuamini Edna ni mama yake mzazi , kwa maana hio nafsi ya Edna ina sehemu ya nafsi ya Seventeen ambayo imetokana na haraka za Athena”
Maneno yake yalimfanya Roma mapigo yake kwenda mbio mno kwasabu alikuwa amejua kitu amabcho hakutaka kukifikiria mwanzo.
“Kwahio unamaanisha Athena wa sasa .. ah namaanisha Edna licha ya nafsi yake kutawaliwa na Athena yeye pamoja na Seventeen hawajapotea , si ndio unachomaanisha?”Aliuliza Roma.
“Sahihi , ukweli ni kwamba kipindi ambacho Edna ameweza kutawala nafsi yake lazima kuna wakati alijihisi ana tatizo la akili lakini hakuweza kuongea chochote kutokana na nafsi ya Athena kumzuia , licha ya kwamba alikuwa akijua nafsi yake ilikuwa imetekwa ni kama kuna mtu mwingine katika akili yake lakini asingeweza kuongea chochote kwani Athena anamlinda, lakini sasa hivi ni tofauti kutokana na kufufuka kwa Moyo wa Gaia basi nguvu zake zote zitamrudia na atakuwa na uwezo wa kuzizima nafsi zote mbili za mapacha hao na kumiliki mwili wake kikamilifu na kwa kile ninachojua , miungu wote wakuu kumi na mbili hawawezi kupoteza kumbukummbu kila wanapohamisha nafsi zao lakini wanapoteza kwanza nafsi ya mwili uliopita kabla ya kuamka ambayo ni ya mmiliki wa mwili na ndio maana huchelewa kuamka hata kwa zaidi ya miaka ishirini kulingana na nguvu ya nafsi husika , lakini kwasbabau Athena alikuwa na haraka aliamua kulazimisha kuamsha nafsi yake kwa haraka katika mwili wa Edna na hakuwa na muda tena wa kufuta nafsi ya Seventeen , ndio maana utaona kuna muda mkeo ni kama anaropoka kitu alichofanya Seventeen lakini ni mara moja moja kutokana na kwamba ufahamu wake umekwisha kupotea hivyo nafsi yake inakuwa kama mtu ambae yupo ndotoni , haijalishi atakuwa makini namna gani lakini kuna muda atakuwa anatamka maneno kama vile anaota “
Roma sasa alielewa na ndio maana Edna kuna muda alikuwa kama Seventeen mtupu , iijapokuwa walikuwa mapacha lakini haikumaanisha walikuwa wakifanana , lakini hata hivyo Roma ni kama tumaini lilimwingia.
“Kwa maneno mengine kama nitaweza kufuta nafsi ya Athena nitaweza kufufua nafsi za wote wawili Edna na Seventeen”
“Haha.. aisee wewe ni mjinga”Sharif alijikuta akicheka huku akiatgisha kihwa chake , ni kama alikuwa akijua Roma anawaza nini.
“Unafikiri itakuwa rahisi , Athena ashatarajia utafikiria hivyo , alifanya makusudi kutozima nafsi zote mbili ili kuungana nazo , sasa hivi ni mtu katika nafsi tatu ndani yake, kwa maneno mengine labda tu Athena yeye mwenyewe aisalimishe nafsi yake na kufa , lakini chochote ambacho unapanga kuifanyia nafsi yake basi hivyo hivyo utaimiza nafsi ya Edna na Seventeen , Athena kafanya yote haya makusudi kabisa ili tu usije ukamgusa mpaka mipango yake itimie”
Maelezo hayo yalikuwa ni kama boriti ya radi ya bluu kwa kumfanya Roma matumaini yake yote kupot3ea.
Nini kitafuta usikose
ITAENDELEA.
 
Shukhran

Moja kati ya Riwaya za HOVYO na Kipumbavu kuwahi kusoma ni hii...Riwaya ndefuu haina kichwa wala miguu,,mtunzi anajaza matukio mengii mradi iwe ndefu isio na tija

Elfu 10 yangu nililopa bora ningenunua Malaya tu nipunguze uzito
 
Back
Top Bottom