singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
- #3,881
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware
SEHEMU YA 767.
Haikuwa na ubishi kabisa Roma aliweza kuona namna ambavyo Lekcha uwezo wake ulivyokuwa umeongezeka , kwa mahesabu ya haraka haraka ilikuwa tayari ni mwaka na Roma alishangazwa kwa namna ambavyo Lekcha ameimarika na ukweli ni kwamba hakuwa binadamu , alionekana kama kiumbe ambacho kipo katika umbo la nishati.
Aoiline upande wake alikuwa amechanguka na alionekana alikuwa akihangaika sana kujilinda na ngao ya kijini , yaani ilionekana uwezo wa kushambulia hakuwa nao zaidi ya kujilinda.
Nywele zake zilizokuwa za kirembo zilikuwa zimejikunja kunja kunja huku gauni lake likiwa limechanika chanika, mikia yake yote tisa ilikuwa ikionekana na kuwa kama kinga kwake.
Kama sio kwa uzuri wake wa uso ingekuwa ngumu kudhania mwanamke huyo alikuwa na hadhi kubwa kati ya majini wa jamii ya Mbweha.
Wawili hao pia walionekana kuhisia uwepo wa Roma na mara baada ya kumuona akishuka kutoka juu haikuwa kwa Aoiline tu lakini hata kwa Lekcha mwenyewe alikuwa katika hali ya mshangao.
“Ni wewe!, Wewe mjinga hukuweza kufanikiwa kutoka wakati ule?”Aliongea Aoiline akipandisha sauti na ni wakati uleule alifanya uchunguzi wa haraka haraka wa kumkagua Roma na uso wake ulikunja ndita.
“Embu subiri kwanza… naona uwezo wako umeimarika sana!?”Aliongea akiwa katika hali ya hamaki.
Roma nae alikuwa kwenye mshangao baada ya kugundua watu hao walikuwa katika floor hio kwa mwaka mzima wakiendelea kupigana.
“Hahaha…Hades wewe mpuuzi muoga muoga umekuja wakati muafaka, usije ukakimbia awamu hii wakati ukijiona unataka kufanya hivyo”
Lekcha alionekana kufurahi mno kama vile ameokota hela na ari yake ya kutaka kupigana ilipanda maradufu , nguvu ya Ant- matter ambayo ilikuwa ni kama mlima iliweza kuongezeka zaidi na zaidi.
Roma alijua wakati huo sio wa kujielezea na aliruka na kwenda kutua upande aliopo Aoiline huku akijilinda na Chaos Cauldron.
“Nitajielezea baadae , kwasasa rekebisha hali yako ya kimwili na niachie nidili na hili”Aliongea Roma.
Aoiline hakuwa msichana mdogo ambaye uwezo wake wa kufikiria ni mdogo , ijapokuwa uwezo wake ulikuwa ukizuiwa na kanuni za kifizikia za ulimwengu huo lakini uono wake haukuwa mdogo.
Hivyo alipanga kumpatia Roma nafasi kudili na maswala yao , isitoshe Lekcha alifika katika ulimwengu huo kwasababu ya ugomvi wake na Roma na yeye ni kama alinunua vita hio.
“Kijana, mimi Master wako nimeweza kushindana na huyu mshenzi kwa zaidi ya mwaka sasa hivyo usiniangushe”Aliongea.
Aoline alimwangalia Roma kwanzia chini na hali isiokuwa ikielezeka ilionekana katika uso wake na aliishia kutoa tabasamu hafifu sana na kisha alisogea pembeni kuangalia pambano.
“Sijawahi kuwaza juu ya uwezo wako lakini ushaanza kuniwazia vibaya , ngoja nikuonyeshe kwamba nilichokuwa nikifanya huko nje hakikuwa kitu cha kupuuzwa”Aliwaza Roma.
Kutoka kuwa chokoraa anaelala chini ya daraja mpaka kuwa mtu mwenye nguvu wa kuweza kushindana na Aoiline kwa zaidi ya mwaka mzima si jambo dogo na Roma alijikuta akimkubali Lekcha bila ya wasiwasi , maana uwezo wake sio wa kawaida.
Wakati Roma akiingia ulimwengu wa majini pepo na kukutana na Aoiline kwa mara ya kwanza alishindwa kabisa kushindana nae , lakini Lekcha aliishi katika ulimwengu huo kwa muda mfupi sana lakini alikuwa ameweza kupandisha uwezo wake kwa viwango vya juu hivyo kwake aliona kabisa hakuwa mtu wa kawaida lakini hata hivyo Roma wakati huo uwezo wake sio wa kawaida na alitaka kumuonyesha Lekcha maana ya nguvu halisi.
Unaweza kusema kwamba Lekcha alifika katika uwezo huo kwasababu ya Roma kumsukumia Kizwe kwake.
Yaani kama Roma asingempa adhabu Kizwe ya kubakwa na machokoraa basi ni hakika Lekcha asingeweza kukutana na Kizwe na hatimae kumuua Yan Buwen na kurithi uwezo wake.
Roma hakutarajia athari ya kile alichokifanya ingemfikisha katika hatua hio, wanasema kila unachokifanya leo kina athari mbeleni na ndio ambacho Roma aliweza kushuhudia na kwa namna yoyote ile kwasababu yalikuwa maamuzi yake wakati ule hakuwa na budi ya kuyakabili matokeo.
“Kwa vyovyote vile kwasababu Mungu amenileta na kukutana nae hapa ,, basi ni wakati wa kuhitimisha huu uhusiano mbaya kwa mikono yangu miwili”Aliwaza tena Roma.
“Inaonekana umekula vitu vingi ndani ya huu mnara”Aliongea Roma akiwa na tbaasamu.
“Kuna haja ya kuuliza , au ndio ushaanza kuniogopa , hivi unadhani mwaka wote niliokuwa ndani ya huu mnara nilikuwa napoteza muda , ijapokuwa nimeshindwa kumuua huyo mbweha lakini ilikuwa ni swala la muda tu .. majani ya kiroho na matunda yaliopo ndani ya huu mnara yamenifanya kuwa wa tofauti kabisa”Aliongea Lekcha akiwa katika hali ya kujiamini kabisa.
“Basi tuchukulie hii ni bahati maana hata mimi nimekuwa wa tofauti kuliko mwanzo , ngoja tuone nani alikuwa akipoteza muda”
Mara baada ya Roma kuongea tu mazingira yaliokuwa yakimzunguka ni kama vile yanaganda na kusababisha msuguano mkali wa elementi za hewa na kufumba na kufumbua radi ya Zambarau ilianza kujitengeneza kama vile ni transfoma la umeme linapiga shoti ambazo ziliruka kwa kunyongorota kama umbo la nyoka.
“Radi ya zambarau!!!”
Aoline ambaye alikuwa akiangalia kwa mbali alimaka huku akiingia katika tafakari nzito, ni kitu ambacho hakutegemea kukiona kwa Roma.
Roma licha ya kuonyesha karata yake hio kwa Lekcha hakubadilika hata kidogo na aliishia kutoa tabasamu la dharau katika uso wake na mkono wake ulibadilika na kuwa kama mkono wa chuma uliotengenezwa na nishati ya Ant- Matter, Shoti za nguvu ile zilikuwa zikitisha mno na ziiongezeka kila sekunde na kutaka kummeza Roma.
Ilikuwa ni sawa kusema mwili wa Lekcha kwa wakati huo ulikuwa ni nguvu ya Ant Matter na ilionekana ni kama vile alikuwa ashapata ufuno wa namna ya kuendeleza kuziongeza maradufu.
Kama sio kwa mnara huo kutokuwa wa kawaida , nguvu ambayo alikuwa akidhalisha Lekcha mnara huo ungekuwa umedondoka muda mrefu sana.
Roma ili kupambana na nguvu ile ya nishati isio maada palepale alibadilisha radi ile na kuwa kama mkuki na kisha alimrushia Lekcha ule mkuki kumchoma.
Nguvu ya radi haikuwa ya kawaida kabisa pia , ijapokuwa nishati ya Lekcha kila ilipokutana na radi ambayo huundwa na maada kulitokea ‘annihilation’ yenye nguvu kubwa kiasi kwamba uwiano ulikosekana.
BOOM, BOOM, BOOM!
Mlipuko mkubwa wa nishati zote mbili kukataana ulikuwa mkubwa mno na ulilipuka katika mfululizo na shambulizi la Lekcha likawa limesabaratishwa namna hio
Lekcha macho yake yalionyesha hali ya kukasirika , hakuamini shambulizi lake hilo ambalo alikuwa ameliongezea nguvu kwa muda mrefu lingeweza kusambaratishwa na nguvu ya radi.
Roma alikuwa mjanja mara baada ya kusambaratisha pigo la Lekcha alikuwa ameongezea nguvu kubwa mno shambulizi lake na mara baada ya mlipuko kutokea mshale mwingine uliweza kutoka na kumpata Lekcha katika kifua na kutengeneza shimo lakini hakukuwa na damu yoyote ilioweza kutokea zaidi ya nishati ambayo iliziba shimo lile haraka sana .
“Hey ..hahaha…Good .. what a powerfull move”Lekcha aliongea kwa kingereza huku akitingisha kichwa chake na kushika eneo la kifua chake ambacho kilitobolewa.
“Inasikisha kwamba huwezi kuniua kizembe namna hii na viradi vyako”
Roma aliishia kukunja sura , aliamini pengine shambulizi la radi lingeweza kumyeyusha lakini ilionekana nguvu ya Ant Matter ilikuwa kubwa mno na kufanya mwili wa Lekcha kuwa na kinga ilio imara.
Lekcha mara baada ya kupona palepale macho yake yalibadilika na aligeuka na kuwa kama lichuma lililotengenzwa kwa uji uji na ilikuwa ni kama mwili wake unaungua kwa shoti na kuzisambaza katika eneo lote.
Roma hakutaka nishati zile kumpata na alijikinga kwa kutumia Chaos Cauldron , chungu kile ni kama kilikuwa kikisubiria fursa hio kwani ile roho ya mnyama iliokuwa ndani yake iliweza kujitokeza kuonyesha ukali wake na kani kubwa ya mvutano ilidhalishwa na kutaka kummeza Lekcha.
“Aaah..ni yale yale , unadhani nitakuogopa kwa kutumia hilo lijichungu lako?”
Lekcha alitoa kicheko kama mwehu na bila ya kukwepa chungu kile alikisogelea na kukivaa na mara baada ya kufikiana na mwili wa Lekcha alilipuka kama bomu la nyuklia.
“Bang!!
“Hoooo…!!!
Ile nafsi ya Chaos ilinguruma kwa sauti kubwa mara baada ya kufunikwa na mlipuko wa nishati ile isiokuwa ya kawaida na kisha kiliachiwa na Lekcha alirudi katika umbo lake la kawaida.
Roma alijikuta akishangazwa na kitu kile , Dhana hio ya Cauldron ilikuwa imeunganishwa na nguvu zake na kama kikipigwa na kuathirika na yeye alikuwa akiumia.
Kilichomshangaa Roma ni mara baada ya roho ile ya mnyama kujificha mara baada ya kuachiliwa na nguvu ya nishati ya ant- matter na hii ilimaanisha kwamba Lekcha alikuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba Dhana hio imekuwa sio tishio kwake tena.
“Unashangaa nini wewe ndio unaefuatia baada ya kuharibi chungu chako”Aliongea Lekcha.
Ilikuwa ni muda uleule Lekcha alitengeneza ngome ya nishati ya Ant- Matter na kuifanya iwe ni kama gunia na kutaka kumfunika nalo Roma.
Roma alishangazwa, nishati ile nyingi haikumtoka Lekcha bali ilikuwa ni kama vile ameitengeneza katika mazingira , yaani likuwa ni kama vile yeye alivyokuwa na uwezo wa kukusanya nishati za mbingu na ardhi ndio alichokifanya Lekcha.
“Nenda kuzimu mshenzi wewe”
Lekcha aliongea kwa sauti na palepale lile boma la nishati alilotengeza lilipuka na kuwa kama vile ni fataki na zile cheche zote kumvaa Roma huku zikiwa zimechanganyika na nguvu nyingine ambayo Roma hakuweza kuitambua lakini ambayo ni hatarishi.
Lekcha alikuwa akibweka kama vile alikuwa kwenye maumivu , chuki yake yote ya zaidi ya miaka aliokuwa nayo zidi ya Roma alionekana aliiwekeza katika ngurumo aliokuwa akitoa
Muonekano wake ulikuwa umebadilika kabisa na kuwa kama mtu mwingine na alionekana kabisa alikuwa akipambana kwa ajili ya kulipa kisasi.
Yaani ile hamasa aliokuwa nayo wakati akipambana na Aoiline ilikuwa ni tofauti wakati huo alivyokuwa akipambana na Roma.
Roma hakutaka kuwa mzembe , aliamua kukiongezea nguvu chungu chake na kisha akakipa kazi ya kunyonya nishati ile ya Ant Matter ili kuipunguza nguvu isimdhuru kwa kiasi kikubwa.
Lakini hata hivyo hakikuweza kuimeza yote na pale ilipomwangukia ilimfanya kujihisi ni kama vile anashambuliwa na nyuki.
Maumivu aliokuwa akihisi hapo yalikuwa ni mara mbili na yale ambayo aliyahisi wakati akiwa ndani ya kizimba cha Dhana ya mafuvu na misumari tisa ya Joka.
Katika hali hio ya kupambana na nguvu kubwa hata ule ugonjwa wake ni kama vile umeshituka kiasi cha kufanya macho yake kuanza kubadilika rangi na kuwa ya kijani..
“Arghh…!!”
Roma alitoa mguno mkubwa mno huku mishipa yake ya damu ni kaa vile inataka kumpasuka na mwili wake ulionyesha hali ya kutaka kupitia mabadiliko , ilionyesha ni dhahiri virusi ambavyo vilikuwa vimelala kwenye mwili wake viilitaka kuamka na kumfanya kuwa jitu.
Lakiini hata hivyo lilikuwa shambulizi dogo sana la kuweza kummaliza Roma kwani maumivu yale ni kama vile yalimfungua ubongo na kujikuta akiingiwa na utashi wa kutaka kufanya shambulizi kubwa zaidi.
“Radiii…!!
Roma alibweka na palepale kimbuka cha nishati ya nguvu ya mbingu na ardhi kilijikusanya juu na kugeuka kuwa moto wa zambarau na wa bluu na mara baada ya kuunganika tu radi ilimshukia Lekcha kutoka pande zote na kuanza kupambana na ile nishati ya Ant- Matter.
Roma nguo hakuwa nazo tena kwenye mwili wake na alikuwa yupo uchi kabisa na mwili wake ni kama vile unapigwa na shoti ya radi kwani ulikuwa ukitetema sio mchezo.
Wakati radi ikishambuliana na nishati ile ya nguvu isiokuwa maada Roma alishuka chini kama vile ni kimondo na mara baada ya kujipigiza chini aliweza kutengenza wimbi kubwa mno la nishati ya nguvu za kijini liloambanta na nguvu ya radi na kumshambulia Lekcha kwa chini.
Roma hakuishia palepale alifyatuka kama mshale huku akiwa amekunja ngumi na kumsogelea Lekcha kwa kasi na kumchapa ngumi ya kichwa iliokuwa na uzito wa tani nyingi mno.
“Pfff!!”
Lekcha alijikuta akipokea mashambulizi matatu kwa wakati mmoja na kufanya nguvu yake ya nishati ya anti-matter kusambaratika lakini wakati uleule ikiyeyushwa na shoti za radi.
Roma mpango wake ulikuwa mwepesi , alijua nishati ya Lekcha ilikuwa na kikomo na kwasababu dunia ki asili ni maada basi uwezo wa Lekcha kuidhibiti nguvu hio ilimhitaji uwezo mkubwa hivyo alimshambulia Lekcha kwa kasi kusambaratisha nguvu zake huku akitumia shoti za umeme wa radi kuziyeyusha ili zismrudie.
Mashambulizi yale ya haraka yalimfanya Aoiline aliekuwa akiangalia kwa mbali kuwa katika hali ya kutokuamini kile alichokuwa akiona.
Alikuwa ni jini wa uwezo wa juu sana ambaye alishawahi kuwepo na alikuwa ameona vitu vingi na mbinu nyingi ambazo majini wanazotumia lakini havikumshangaza , lakini upande wa Roma kila alichokuwa akifanya kilikuwa kipya kwake na kumfanya kushangaa.
Unachopaswa kuelewa hata ukiwa ndani ya mnara huo bado sheria za ulimwengu wa mapeppo zilikuwa zikitumika hapo hivyo kufanya uwezo wake kuwa wa chini , lakini sasa kama kwa nusu ya uwezo wake aliweza kupigana na Lekcha kwa mwaka mzima lakini hakufanya shambulizi kubwa kama ambalo Roma amefanya bali alimuona ameimarika nje ya matarajio yake.
Hivyo kimahesabu ni kwamba Roma na yeye alikuwa akitumia nusu ya uwezo wake na moja kwa moja aliona lazima Roma atakuwa amemuacha mbali sana hata kama akitoka katika ulimwengu wa kawaida na kurudiwa na uwezo wake wote.
Mbaya zaidi alichoona ni kwamba Roma anaonekana uwezo wake huongezeka kila ndani ya dakika.
“Huyu kijana ubora na utimamu wa kimwili unafaida kubwa kwake, kautoa wapi huo mwili?”Alijiwazia.
Aoiline aliamini mwili wa Roma ndio chanzo cha kuweza kufunikiwa kwa muda mfupi na alimfananisha na ukoo wa majini joka wa zama zile.
Kadri ambavyo Roma hakuwa akimpa nafasi Lekcha kujikusanya ndio ambavyo alikuwa akizidi kupoteza nishati yake ya Ant- Matter na ilichukua muda mfupi ilionekana Lekcha alibakiwa na nguvu kidogo sana.
Nishati ya Ant matter inaweza kuwa na nguvu lakini ni ghali sana , hii inamaanisha kwamba ni muda mwingi sana unahitajika kwa ajili ya kuikusanya tofauti na nishati ya mbingu na ardhi ambayo mara nyingi haina kikomo ili mradi tu ubongo wako unafanya kazi vizuri, hasara kubwa ya nishati hio ni kwamba asili yake sio ya kidunia hivyo huharibika kwa kasi.
Lakini sasa wakati Roma akiwa na mawazo kwamba amemzimisha Lekcha mpaka kuwa dhaifu Lekcha alirudi katika umbo la kawaida na kumfanya Roma amuone ni kama ndoto ambayo hawezi kuifuta.
Lekcha mara baada ya kurudi katika umbo la mfanano wa kibinadamu alianza kukunja shingo yake kama vile anaweka mwili sawa kana kwamba anamwambia Roma pigo zako ni za kitoto.
“Vipi tena bwana mdogo Roma Ramoni A.k. a Hades dhaifu, hicho ndio ambacho unaweza kujivunia , hii radi yako inaonekana kuwa na nguvu kweli lakini athari zake kwangu ni ndogo”Aliongea Lekcha huku akitoa tabasamu la uovu.
Roma moyo wake ulisinyaa , alidhania akitumia mahesabu ya kikanuni ya nishati ya nguvu hio anaweza kummaliza Lekcha kwa kumshambulia bila kukoma kwa kasi lakini ilionekana kuna kitu ambacho hakukitambua kutoka kwa Lekcha.
“Roma usichokijua na wasichokijua wanasayansi ni kwamba wakati wa nishati ya matter na anti matter zinapogongana hakutokei kitu kinachoitwa Annihilation kama wanavyoamini bali asilimia mia moja kunatokea nishati nyingine yenye tabia tofauti , nishati hii ndio ilionifanya uwezo wangu kuimarika maradufu kadri nilivyokuwa nikipambana na yule Mbweha , bomu la nyuklia ambalo hutengenezwa kwa kurutubisha viini vya atomu ni sawa na asilimia moja tu ya nishati inayotokea wakati wa kugongana kwa nishati hizi mbili , hivyo ninao uwezo wa kuharibu kisiwa kwa kukadiria tu uwezo nishati ninayotaka itokee , sasa hebu jiulize gunduzi yangu hii ndio nataka kuiajaribisha kwako”
Aliongea Lekcha na palepale alitengeneza kitenesi cha nguvu ya nishati ya Ant-Matter na kukirusha aliposimama Roma kwa kasi.
Roma alitaka kutumia Chaos Cauldron kuweza kukijikinga na shambulizi lile lakini Chaos alionyesha hali ya kunywea kutokana na ukubwa wa shambulizi lile.
Roma alijikuta akikosa chaguo lingine na kung’ata meno yake kwa hasira na kisha palepale kwa spidi ya haraka sana alichoropoa lile Shoka kutoka katika hifadhi yake ya pete.
Inasemekana katika ulimwengu wa majini kulikuwa na Dhana kumi na saba ambazo zilikuwa na nguvu sana enzi hizo na kati ya Dhana hizo ni Shoka hilo la Pangea ambalo halikueleweka namna linavyofanya kazi , kuna tetesi kwamba linaweza kuingia katika shimo jeusi la anga na kutoka.
Kitu kingine ni kwamba nguvu yake pia ni kama ilivyokuwa kwa Cauldron, shoka hilo linaonyesha uwezo wake kulingana na uwezo wa mtumiaji. Lakini kitu cha uhakika ni kwamba Shoka hilo lilikuwa na uwezo wa kuchana anga na kwenda kinyume na kanuni za anga.
Katika kanuni za kifizikia kutoka kwa mgunduzi Einstein anasema anga ni kama kitambaa, ijapokuwa hakumaanisha kitambaa kama kitambaa lakini ndio namna rahisi ya kuelewa kwamba anga linaweza kuharibika kikanuni.
Sasa Shoka hilo lilikuwa na uwezo wakuchana hiko kitambaa ambacho ni kama anga sasa kwa kukiuka sheria za anga.
Unaweza kushangaa hizi Dhana zinafanyake kazi lakini teknolojia ambayo ipo nyuma yake ni nje ya uelewa wa fahamu za kibinadamu na hata viumbe wenye akili sana kama majini na hata miungu hawakuwa wakijua siri iliopo nyuma ya uhunzi wa Dhana hizo..
Chukulia mfano safu ya ulinzi ya gereza la Roho katika miliki ya Hongmeng mpaka wakati huo sio Athena wala kiumbe chochote aliweza kujua teknojia ya safu hizo za ulinzi zinafanyaje kazi.
Hivyo hata kwa Roma mwenyewe hakuwa akijua namna Dhana hizo zilivyotengenezwa alichokuwa akijua ni namna ya kutumia tu.
Sasa Roma aliamini kwasababu kanuni za anga hazikufanya kazi vizuri katika ulimwengu huo kutumia Shoka hilo ambalo linaenda kinyume na kila sheria ya asili ndio tumaini pekee la kuhimili nguvu ya Ant- matter.
Kitendo cha Shoka lile kutua katika mkono wa Roma na kuliingizia nguvu za kijini lilibadilika palepale muonekano wake na zile herufi ambazo zilikuwa zimechorwa katika Shoka hilo ziling’aa.
Ijapokuwa lilionekana kama shoka la kawaida lakini uzito wake haukuwa wa kawaida na pengine hata Rose ambaye yupo mwishoni mwa levo ya Nafsi asingeweza kulishika mkononi.
Kwa namna ambavyo liliamshwa na nguvu za mbingu na ardhi za Roma ilikuwa ni kama vile shoka hilo lilikuwa likitawaliwa na nafsi lakini ukweli ni kwamba hakukuwa na nafsi yoyote , ilikuwa ni kama kifaa tu ambacho kimelala na muda huo kimepata nishati na kuingia katika matumizi.
Roma hata yeye ndio inakuwa mara yake ya kwanza kujaribisha shoka hilo na kitendo cha kuamka kwake ile sehemu aliosimama ni kama vile upepo unakimbia , msisimko ulioweza kutoka ilikuwa ni kama vile kiumbe mwenye nguvu sizizokuwa za kawaida anawavamia.
“Arghh…!!!”
Roma alipiga yowe na kwa kutumia nguvu zake zote za kijini aliinua lile shoka juu na kisha akalipigiza chini ndani ya sekunde.
BOOM
Wimbi la nguvu iliotokana na shoka hilo ilikuwa ni kama vile inakwenda kutenganisha mlima wa gereza la nafsi za giza na kuziachia.
Shambulizi lile la Lekcha mara baada ya kugongana na msisimko wa nguvu ya lile shoka mwanga wake ulibadilika katika rangi zisizokuwa zikihesabika na shambulizi lake nikama vile limetumbukia kwenye shimo.
Aoiline ambaye alikuwa mbali aliweza kuhisi msisimko usiokuwa kawaida kutoka kwa nguvu ya nishati ya Ant-matter iliotengenezwa na Lekcha , aliamini kama Lekcha angetumia shambulizi hilo kumshambulia basi angepatwa na majeraha makubwa mno, lakini sasa alishangaa pale Roma akitoa kitu kilichomwacha mdomo wazi.
Licha ya kwamba aliishi miaka mingi hakutegemea kuona Roma angeweza kumiliki kitu cha ajabu kama hicho , alikuwa akisikia kuhusu shoka hilo lakini hakuwahi kuona katika uhalisia.
Unajua bwana majini wengi wana historia kama ilivyokwa binadamu lakini utofauti wa majini na binadamu ni kwamba majini wa zamani walikuwa na akili nyingi sana na kufanya vitu vya ajabu kuliko hawa wa sasa lakini kwa sisi binadamu uwezo wetu wa akili unaongezeka kulingana na muda.
Yaani wakati binadamu akiendeea kutafuta siri za dunia kwa kupanua uwezo wa kufikiria upande wa majini wao wanataka kufikia levo za kufikiria za watangulizi wao.
Sasa katika vitabu vya kihistoria vya majini walikuwa wakisoma uwepo wa Dhana kumi na saba na kati ya Dhana hizo ni Chaos Cauldron , Shoka la kipangea , kioo cha nafsi, Fimbo ya muujiza na zinginezo lakini licha ya kuishi miaka mingi sana hakuwahi kushuhudia hizo Dhana.
Sasa alijjiuliza Roma amewezaje kumiliki Dhana mbili kati ya Dhana kumi na saba za kihistoria. Alijiambia huyu mtoto katoa wapi vitu hivyo.
Lakini licha ya kuwa kwenye mshangao hakuonyesha hali ya kufurahi mara baada ya kuona nguvu halisi ya shoka hilo , hakujali nguvu yake itauathiri vipi mnara lakini alitaka kuona matokeo tu.
Ile sehemu ambayo amesimama Roma kulionekana hali ambayo haikuwa ikielezeka ilikuwa ni kama vile kataratasi ya nailoni linaungua katikati na kutengeneza ufa katikati.
Roma mwenyewe alishangazwa na kitu kile na palepale wazo lilimwingia na kuhamaki na kujiambia kwahio kuchanika kwa anga ndio kupo hivi.
Roma alishangazwa na jambo hio radi yake ilikuwa ikileta machafuko lakini shoka hilo ilionekana ni kweli ilikuwa ikiharibu anga na kumfanya yeye kuwa kati , yaani ni kama lile shoka linaharibu anga na wakati huo huo kunatengenezeka anga lingine jipya ambalo ndio anaonekana yupo yeye sasa.
Roma alijua kabisa anga la ulimwengu huo sio ‘Parallel dimension’ kama ilivyokuwa kwa ulimwengu wa majini watu, bali ni tofauti kabisa ndio maana ukiwa katika huo ulimwengu huwezi kufanya mawasiliano kwa namna yoyote ile na ulimwengu wa kawaida, pili kanuni zake za anga hufanya kazi kitofauti.
Kama anga la uimwengu huo lilikuwa la kawaida basi majini hao wasingeweza kufungiwa kirahisi hivyo.
Moja kwa mmoja ilimaanisha kwamba Shoka hilo lilikuwa na sheria zake za ufanyaji kazi.
Kuna kitu kilikuwa kikimwambia kuna uwezekano wa Roma kubadilisha utendaji kazi wa ulimwengu huo kwa kutumia hilo shoka , ikimaanisha kwamba ameshikilia ufunguo ambao unaweza kuruhusu njia ya kutokea.
Yaani ni kama ilivyokuwa kwa mfalme Wuja mkuu wa majoka kutengeneza Dhana ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza njia ya kutokea ulimwengu wa kawaida ndio ambavyo Roma alihisi uwezo wa shoka lake ulivyo.
Shambulizi ambalo Lekcha aliamini kwamba linaweza kuharibu kisiwa lilisambatatishwa na Sururu la Roma na moja kwa moja alijihisi kukasirika mno kwani hakutegemea hilo.
“Haiwezekani… Hadae nasema haiwezekani ukapangua shambulizi langu namna nyepesi hivyo”
Lekcha aling’aa meno yake kwa hasira, nguvu yake ya nishati ambayo ilikuwa kama dhoruba baharini ilijikusanya upya katika mkono wake na kwa mara nyingine alijaribu kumshambulia Roma.
Roma baada ya kuona utukufu wa shoka lake hali ya kujiamini iliongezeka na kujiambia yes ni muda wa majaribio na palepale alifyeka anga na shoka lake kutengenza wimbi lingine la mchaniko uelekeo wa shambulizi la Lekcha.
Shambulizi la Lekcha lilikuwa kubwa kweli lakini shoka lile liliteneneza hali ya kuyumba kwa anga hivyo kufanya shambulizi lake kusambaratika , kwa bahati nzuri ni kwamba anga lina nguvu ya kinishati kubwa sana hivyo hata kama shoka hilo lilikuwa na uwezo wa kubadilisha utedaji kazi wa kawaida wa anga ilikuwa ni eneo dogo tu hivyo athari zake zilikuwa katika mzingo mdogo na pia ile sehemu ambayo huonekana kuharibika inarudi upya kwa kasi.
Lekcha alikasirika mno mara baada ya kuona ana mashambulizi yenye nguvu lakini bado hakuweza kumfanya chochote Roma kutokana na shoka lake na aliamua kupotezea kila kitu na kuanza kukusanya kiwango kikubwa cha nishati ya ant matter.
Roma alijua Lekcha yupo katika hali ambayo ni ngumu kumuua , alikuwa ni kama nishati na ili kumaliza lazima kuyeyusha nishati yake hivyo alitumia Chungu , radi na shoka kushambulia kwa wakati mmoja.
Wakati huo ni kama Cauldron imeweza kutambua uwepo wa shoka na hali ya roho ile ya mnyama kujiamini ilirudi.
Wakati huo sasa katika floor hio ukiangalia kwa juu ni kama vile kuna nishati mbili ambazo zilikuwa zikivamiana huku watu waliokuwa wakidhalisha nishati hizo hawaonekani.
Aoiline aliekuwa akiangalia pambano hilo uwezo wake ulikuwa umerudi lakini hata hivyo hakutaka kuingilia.
Sio kwamba hakutaka lakini nguvu ya kimauaji iliokuwa ikimtoka Roma ilimfanya kuona kabisa hana haja ya kuingilia.
Lakini hata hivyo Roma asingependa maana katika maisha yake hakupenda kumtumia mwanamke kama chombo cha mafanikio yake ndio maana tokea amuache Aoiline ndani ya mnara huo roho iikuwa ikimsuta.
Kadri Roma alivyokuwa akishindana na nguvu ile ya Ant-Matter ni kama vile kichwa chake kinakuwa kizito mno kiasi kwamba ule ugonjwa uliokuwa umempotea ulianza kurudi kwa kasi na kufanya macho yake kuwaka taa nyekundu.
Ilikuwa ni kama vile ile nishati ya Ant- matter inashitua hali flani ya utendaji wa mwili wake.
SEHEMU YA 768.
Wakati huo huo vita hio ikiendela katika ngome ya makao makuu ya kambi ya kitafiti ya Zeros organisation alionekana Madam Dyana akiwa na tabasamu la aina yake usoni huku akiangaia kitu kwenye skrini , ilikuwa ni kama vile alitamani kuona kitu cha namna hio kwa muda mrefu.
Dyana ni mwanamama ambae ni Chief wa kitengo cha usimamizi wa maendeleo ya mpango LADO yaani idara ya PLMC.
Kitengo hicho kwa muda mrefu sana kilikuwa kimya sana na hakukuwa na dalili yoyote ya taarifa kutoka kwa ajent wao na hata wale wanasayansi ambao walikuwa wakihusika walikuwa wakilala tu muda mwingi lakini siku hio ilionekana kuwa tofauti katika miezi mingi.
Licha ya kwamba ulimwengu ulikuwa katika hali ya sinfofahamu lakini kazi zilikuwa zikiendelea kawaida ndani ya kambi hio na ukweli ni kwamba ubize ulikuwa umeongezeka kwa kiwango kikubwa sana.
Sasa ni miezi kadhaa tokea Dyana kupokea maagizo kutoka kwa mheshimiwa Barack Mabo.
Unajua katika jumuia yoyote ambayo inahusisha viumbe binadamu lazima kuna wale ambao wana mtazamo tofauti na hio ilionekana ndani ya umoja wa Zeros organisation.
Inaaminika kwamba Barack Mambo ndio moja ya wanachma wa vyeo vikubwa ndani ya jumuia hio ya siri tena akiwa mkuu chini ya The First Black lakini ndio mtu pekee ambaye alikuwa na mawazo tofauti na malengo ya Zeros.
Mpango LADO ni mpango ambao una sahihi yake na sio kwake tu karibia kwa maraisi wote waliopitia katika nyumba nyeupe mpango huo hujumuishwa katika viapo vyao ili kuulinda na kuudumisha.
Ki uhalisia haukuwa mpango mbaya kwani malengo yake yalikuwa wazi , malengo ya mpango LADO hayakuwa kwa ajili ya kumtengeneza ajent mwenye nguvu pekee lakini ukweli ni kwamba ni mpango ambao uliundwa kwa ajili ya kupata binadamu mwenye DNA tofauti, yaani kwa lugha nyepesi kilichokuwa kikilengwa ni kutengeneza kizazi kipya.
Illuminat ndio jamii ambayo ‘ideology’ yake imepewa kipaumbele katika zeros organisation kuliko jamii yoyote ile , waliamini ili dunia izidi kuwa salama kuelimika kwa binadamu lazima kuendane na kasi ya muda na ili hilo kufanikiwa lazima kuwepo binadamu wenye uwezo tofauti wa kufikiria na huo ndio utakuwa mwanzo wa gunduzi mpya tofauti na mwendelezo wa teknolojia zilizopo.
Upande wa Ant-Illuminat wao umoja wao ulianzishwa kupinga ‘ideology’ za Illuminat kwamba ii dunia iendelee kuwa salama maendeleo ya teknolojia yanatakiwa kuendelea katika spidi sawa na ukuaji wa kifikra wa kibinadamu , yaani kusiwe na ‘hacking’ ya aina yoyote ile ya kujaribu kuharakisha ukuaji wa kufikiria kwa binadamu.
Sasa Barack Mabo katika mawazo hayo mawili yeye ni vuguvugu, ikimaanisha kwamba nusu anakubali ajenda za illuminat na nusu anakubali ajenda za Ant-Illuminat na hili ndio ilimfanya kujikuta kuwa na mawazo tofauti.
Kati ya watu ambao anafanana nao kimawazo ni Dyana mwanamama ambaye ndio aliepewa jukumu la usimamizi wa maendeleo ya mpango LADO.
Sasa ni miezi kadhaa tokea yatokee mabadiliko ya hali ya hewa duniani , moja ya watu ambao hawakuwa na utulivu na kile kilichokuwa kikiendelea alikuwa ni yeye.
Na wasiwasi ulimfanya kufanya vikao vingi sana na wadau wengi kuzungumzia kile kinachoendelea na nia halisi ya viumbe hao kutoka sayari nyingne zidi ya binadamu.
Ijapokuwa ni kweli Athena aliwahakikishia kwamba ili kuibadilisha dunia kutoka katika hali ya sasa ya Dystopia na kwenda kuwa ulimwengu wa Utopia kuna kafara itahitajika lakini bado haikutosha kumuamini moja kwa moja na kutokufanya chochote au kutokuchukua tahadhari.
Ieleweke kwamba Athena licha ya kuanzisha umoja huo hakuwahi kujionyesha hadharani na hata pale alipokuwa akijionyesha ni katika hali ya kuogofya pengine hii iliwafanya watu kuwa na imani dhaifu juu ya mipango yake.
Ukweli ni kwamba hakuanzisha Zeros kwa njia ya moja kwa moja bali ni binadamu wenyewe ambao walitoa pendekezo na yeye akaingiza ushawishi wake na mwisho wa siku ikaonekana ni kama yeye alieanzisha.
Sasa Barack Mabo na wanachama wengine walikuwa katika vikao vya kila siku na ajenda kubwa iliokuwa ikizungumziwa katika vikao hivyo ni kufumbua fumbo gumu ambalo Athena amelitega.
Fumbo lenyewe ni kwamba kama Athena alikuwa na nguvu kubwa kwanini akataka mpango LADO kufanikiwa kwa silimia mia moja na kumfanya Roma kuendelea kuwa na nguvu kila uchao.
Yaani viongozi hao na wanasayansi hao waliona kabisa hakukuwa na uhusiano wowote uliopo kati ya mipango ya Athena na kupanda madaraja ya ki uwezo kwa ajent Thirteen.
Athena aliwaambia kufanikiwa kwa Roma ni kwa ajili ya kutengeneza uzao mpya , binadamu ambaye atakuwa na uwezo wa kufikiria tofauti lakini kwanini inaonekana ni kama vile Athena anataka kuua binadamu wote.
Yamkini ni kwamba binadamu hao ambao wanajiita ndio watu waliokuwa karibu na mwishoni mwa piramidi la uongozi wa dunia walikosa majibu , walikosa majibu kutokana na kwamba waliekuwa wakimuuliza maswali hakuwepo na hakujisumbua hata kujitokeza kwao.
Walijikuta kama vile ni viumbe ambavvyo vimetelekezwa kwani hali ya dunia ilizidi kuwa mbaya lakini hakukuwa na majibu kwamba hali hio ingedumu kwa muda gani na matokeo yake ni nini ,walijuliza je hali hio ndio dunia ambayo Athena anataka kutengeneza lakini kimahesabu wanaonna hakuna namna Athena akawa na nia nzuri kwa binadamu.
Mwisho wa maamuzi ya vikao ndio wengine wanashauri kujengwa kwa Safina kuokoa binadamu asipotee , huku kundi la watu wakipinga pendekezo hilo na kutaka kushindana na miungu.
Moja ya watu ambao waliona kujenga Safina sio suruhu ni mstaafu Barack Mabo na kutokana na kuwa na mawazo ya tofauti aliamini mtu mmoja pekee ambaye anaweza kutatua kitendawili kilichokuwa kikiwasumbua wengi ni Hades pekee kwani alikuwa ni nusu binadamu na nusu viumbe hao.
Sasa ule wakati ambao walikuwa wakitamani Roma aingilie kati ndio wakati ambao Roma ametoweka ghafla tu na asijiulikane alipo.
Ni muda wa mchana usiokuwa na jua nchini Marekani , licha ya kwamba dunia ilikuwa katika hali ya baridi kali lakini baadhi ya raia waliokuwa wakijiweza kiuchumi hawakuwa na hali mbaya.
“Dyana nipe ripoti , naamini simu hii sio ya bure kuna matokeo chanya?”Aliongea Raisi Barack Mabo akiwa nyumbani kwake na hio ni mara baada ya simu yake kuita na kupokea kwa haraka haraka.
“Ndio mheshimiwa tumeweza kupata dalili ya mabadiliko ya kimwili ya Ajent 13 na taarifa zimeingia katika mfumo wetu dakika chache zilizopita”
“Nini! Dyana unamaanisha mmepata Hades?”
“Mheshimiwa tokea tuanze kutafuta taarifa za Hades alikopotelea ni leo tu mifumo yetu imeonyesha uhai , vijana walikuwa macho kutokokosa hata viashiria kidogo ndani ya mfumo na juhudi zao za kuwa macho leo hii zimezaa matunda, inaonekana Hades yupo katika hali ya mapambano makali na signal za sayansi ya Devine light zimetuma taarifa hatujui kwa uhakika ni nini kinaendeea na katika lango lipi la anga lakini ni dalili nzuri”Aliongea Dyana na Mheshiimiwa Barack Mabo alionekana kuonyesha hali ya mabadiliko kidogo katika wasiwasi wake.
“Dyana nataka kujua kama Hades anaweza kurudi?”
“Mheshimiwa ili mradi yupo hai naamini atarudi , ndio tegemeo letu kwasasa kujibu maswali ya kinachoendelea, Barrack mpaka sasa umeshindwa kuwaamini watu wa Vatican?”
“Sio kama siwaamini lakini wamekuwa ni watu wa njama sana na mitego , wanasema kuna unabii unaopaswa kutimia ndio maana hawachukui hatua yoyote lakini mpaka leo hii hawatupi maelezo”Aliongea na kumfanya Dyana kutulia.
“China na Japani msimamo wao upoje , nasikia hawakushiriki katika vkao vyote vya kimataifa vya dharula lakini walikuhitaji kama mjumbe wao”Aliongea na kumfanya Barrack Mabo kukumbuka namna alivyofuatilia kikao cha viongozi wa China.
*****
Wiki kadhaa ndani ya Zhongnahai Beijing kulikuwa na kikao kizito ambacho kilihusisha viongozi wote wa juu wa taifa hilo na wale wastaafu waandamizi(Country senior’s).
Kiongozi mkuu namba moja mwandamizi ndio ambaye alikuwa akiongoza kikao hicho , pembeni yake kulikuwa na viongozi akiwemo Li Moshen waziri wa ulinzi , YangChen mkuu wa majeshi , Cai Yuncheng mkuu wa kikosi cha wachawi na Ning Guanyao ambaye ni waziri mkuu hao ni baadhi tu.
Katika watu waliokuwa na wasiwasi ndani ya kikao hicho ni Cain Yuncheng huyu ndie ambaye ni kama anahusika na utendaji wa Hongmeng katika ulimwengu wa kawaida na wasiwasi wake ni kwamba Hongmeng inaweza kukosa nguvu kutokana na kwamba Anjiu mkuu wa miliki ya Xia alikuwa akiwashambulia.
Ijapokuwa baridi ilikuwa kali sana ndani ya taifa hilo lakini China ni moja ya nchi ambazo zina hakiba kubwa ya chakula lakini pia limeeendelea katika urahisishaji wa social service delivery kwa raia wake.
Yaani haikuwa na haja kwa raia kutoka nje kwa ajili ya kwenda sokoni wala dukani bali teknolojia ilirahisisha kazi hio hivyo kufanya nchi hio yenye watu wengi zaidi duniani kwa mara ya kwanza kuonekana kama vile haina watu.
Bila shaka sio kwamba watu wote hawakutoka , kuna wafanyakazi walitoka lakini ilikuwa kwa tahadhari maalumu na hata wale wenye vipato kidogo walikuwa wakisaidiwa.
Baada ya kimya kirefu cha mkuu wa nchi hio hatimae alianza kuongea.
“Hatuwezi kuendelea kukalia mikono yetu zaidi , kwanzia sasa tutajitegemea sisi wenyewe na sio wengine”Aliongea lakini hakuna ambaye aliongea kwani wote walikuwa kimya wakimwangalia , licha ya kwamba dunia ilikuwa katika hali isiokuwa ya kawaida lakini tabasamu halikumtoka.
“Kutokana na janga hili linaloendelea nchi yetu yote na hata kwa binadamu tunapitia changamoto , kama unachochote cha kuongea waziri Ning tafadhari sema, kwanini upo kimya sana siku hizi?”
“Mheshimiwa ulimwengu wa majini sasa hivi upo kwenye machafuko kutokana na vita inayoendelea , miliki ya Xia kwa kutumia watu wao ambao wamefikia levo ya radi wanajaribu kuvamia miliki nyingine , ikumbukwe Xia ipo ndani ya bara la Asia na kwa muda mwingi wamekuwa na wivu na Hongmeng , je uhakika tunao kama wakiiteka Hongmeng hawatotaka kuchukua nafasi yao na kuingilia maswala yetu?”
“Usiwe na wasiwasi , hawawezi”Alijibu Raisi na kisha akaendelea.
“Ijapokuwa miliki ya Xia imepanda na kuwa na nguvu ndani ya ulimwengu wa majini kuliko miliki zote , kutumia nguvu zao kutaka kuingilia maswala ya ulimwengu wa kawaida hakutowasaidia chochote , zaidi ya kujiingiza hatarini kwa kuwachokoza wajumbe wa muungano wa ulinzi wa dunia na ulimwengu wao,sidhani wanaweza kuwa wajinga hivyo”
Mara baada ya kutajwa wajumbe wa ulinzi wa umoja kila mmoja alionyesha hali ya msisimko.
Haikuwa kwa majini tu ambao walikuwa wakijua uwepo wa umoja wa ulinzi wa dunia , ukweli ni kwamba historia hio haijawahi kufutika katika uso wa dunia tokea siku ambayo viumbe kutoka sayari nyingine kutua duniani.
Ni wajumbe hao hao wa umoja ndio waliohusika na ambao waliendelea kushikilia ulinzi wa usalama wa dunia.
Katika hali kama hio ya dunia kuwa hatarini na vilevile kupotea kwa Roma kitu pekee ambacho binadamu wenye kuelewa siri ya uwepo wa wajumbe hao waliomba waingilie kati.
Walinzi wa dunia au The Guardians jukumu lao kubwa ni kuhakikisha dunia inaendelea kuwa salama na wajumbe hao wa ki’umoja hawakujali maswala ya nchi na nchi , ukweli ni kwamba hawakujihangaisha na maswala ya kiserikali ya kibinadamu wala majini.
Hawajali Israeli kumvamia Mpalestina wala Mchina kumvatia Mtaiwani au Mrusi kumvamia Ukraine , ajenda yao kuu ni kulinda uwiano wa usalama wa kidunia hii ikimaanisha katika malango yote ya dunia , iwe ni ulimwengu wa kawaida ama ulimwengu wa ajini pepo au ulimwengu wa majini watu lakini vilevile kuzuia jamii moja ya viumbe kushambulia viumbe wengine.
Majini wa Panas , walitakiwa kubakia Panas na majini wa Xia walitakiwa kubakia Xia na kama wataamua kushambuliana wao kwa wao hakuna tatizo lakini kama watashambulia binadamu na kutaka kuteka nchi ndio tatizo hutokea ambalo lilipaswa wajumbe hao kuingilia.
Lakini kilichokuwa kikiwasumbua sio serikali ya China tu bali serikali zote ambazo ziikuwa zikijua historia ya uwepo wa watu hao ambao haikueleweka ni majini , binadamu au malaika ni kwamba hawajui walikuwa na ajenda gani na pili hawafahamika kwa sura ni wakina nani na wanatokea nchi gani au wanaishi nchi gani.
Inasemekana ni matiafa makubwa duniani tu ambao wameweza kukutana na mmoja ya wajumbe hao yaani Mkuu namba moja na mara nyingi alijitokeza kwao kwa ajili ya kutoa onyo tu na haikuwa vinginevyo.
Nchi pekee ambayo ni ndogo na mkuu namba moja alijitokeza kwa kiongozi wake ni Rwanda tu na hio yote ni kutokana na Jeremy kushikirikiana na miliki ya Panas kutaka kuingilia maswala ya kibinadamu,
Mtu binafsi tu ambaye aliweza kukutana na mkuu namba moja ambaye huunda baraza la usalama wa ulimwengu ni Roma pekee.
Ki ufupi ni kwamba Master Namba moja mwenyewe alikuwa na nguvu sana kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kukutana na raisi wa Urusi kwa kutumia sura ya Singanojr na vilevile akakutana na raisi wa Korea Kaskazini kwa sura ya mtu mwingine , ili mradi amefikisha ujumbe haikujalisha ni sura ya nani inatumika.
Sasa Raisi wa China na baadhi ya watu tofauti tofauti ndio walijua siri hio ya uwepo wa hivyo viumbe lakini hawakujua ni wakati gani watachukua hatua hivyo tofauti na kusubiri waendelee kuteseka ni bora kujitegemea wao kwa wao.
Wakati kikao hicho kikiendelea upande mwingine Raisi Barack Mabo alikuwa akifatilia kila kitu, ni kama alipewa ruhusa ya kuangalia namna kikao hicho kinavyoendelea.
Ukweli ni kwamba Raisi Barak Mabo alikuwa akiamini kwamba wajumbe hao wa ulinzi wa dunia walikuwa na mawasiiano na taifa la China na hio yote ni kutokana na uwepo wa Hongmeng lakini matokeo yake ni kwamba hata raisi mwenyewe wa China hakuwa na mawasiliano nao lakini licha ya hivyo Barack Mabo hakumuamini na ndio maana mheshimiwa alimpa nafasi ya kuangalia kikao chake na vongozi wake waandamizi ili aweze kuamini maneno yake.
“Mheshimiwa dunia nzima ipo katika hili janga la baridi na miungu wanaendelea kutukandamiza , Hongmeng ambao ni tegemeo letu wenyewe wapo na matatizo , je hakuna uwezekano wowote wa hawa walinzi kutusaidia ?”Aliuiza mkuu wa kikosi cha uchawi.
“Bado hamjanielewa tu nilichojaribu kuwaelezea..?”Aliongea na kisha akawaangalia mmoja mmoja na kisha alivuta pumzi na kuendelea.
“Sio mimi tu ambaye nimejaribu lakini wenzangu wengi wamejaribu lakini hakuna uwezekano wowote ambao nimeweza kuwasiliana nao”
“Kwaho hii inamaanisha hawana mpango wa kusaidia binadamu?”Aliuliza Ning.
“Hilo sijui lakini na wenyewe wana falsafa yao mpaka kuamua kuingilia maswala ya kibinadamu, pengine wanaona dunia haipo hatarini”
“Hawana lolote hao nina uhakika wanawaogopa miungu”Aliongea waziri mkuu Ning kwa hasira.
“Waziri chunga mdomo wako”Aliofokewa na mheshimiwa Raisi
“Kila kitu kinatokea kwasababu maalumu mheshimiwa waziri , mzunguko wa kimaisha unatafsiriwa kutoka kuzaliwa mpaka kufa , uwezekano wa hawa watu kuwepo ni kweli lakini haijalishi kama wapo au hawapo , hatua ambayo binadamu tumefikia haijatokana na wao , ni kwa maarifa yetu na upumbavu wetu wenyewe , dunia ilipofikia sio kwa msaada wa kiumbe chochote bali ni sisi binadamu wenyewe na ndio sisi ambao tunapaswa kuipambania kurudi katika hali yake ya kawaida”Aliongea mkuu wa majeshi.
“Mr Yang upo sahihi katika hali kama kila taifa linataka kujitegemea hatuna budi na sisi kujua namna ya kujilinda”
Kwa mheshimiwa Barack Mabo ilikuwa ni kama vile anaangalia filamu , alichokuwa akitarajia hakukipata ijapokuwa kwa namna flani alijua ni kweli kuna uwepo wa hao viumbe lakini bado hakuamini.
Na swali hata yeye kwake lilibakia je ni kweli kama inavyosadikika kwamba kuna viumbe wasiofahamika wanaojiita walinzi wa dunia kama wapo ni lini watajitokeza na ni viumbe wa namna gani.
Mpaka mwisho hakuwa na majibu na alijikuta akirudi nchini kwake akiwa mnyonge.
SEHEMU YA 768.
Ilikuwa ni vita ya wanaume wawili na ingekamilika vizuri kama mmoja kati wao angeshinda bila kuongezewa nguvu ndio maana Aoiline hakutaka kuingilia.
Vita hio ya Roma na Lekcha ilikuwa sio ya kawaida kabisa iliojaa mizungusho , kurushiana makombora ya nishati na kuoteana.
Radi ya zambarau na bluu ndani ya mnara huo ilikuwa ikipiga mara kwa mara lakini katika floor hio ya kwanza haikufika
Roma alizidi kuwa jasiri kila sekunde ilivyokuwa ikisonga na alijiua licha ya kwamba akili yake ni kama vile imetawaliwa na mdudu na kufanya macho yake kubadilika rangi mara kwa mara lakini uungu wake ulikuwa imara mno na haikuwa kama kipindi cha nyuma ambapo hakuweza kujitawala kiakili.
Roma aliweza kuhisi mwili wake ukipitia maumivu mara baada ya kupigwa na mlipuko wa nishati ya ant-matter na kuhisi kupoteza kiasi flani cha nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi lakini hata hivyo alijiponyesha kwa haraka sana.
Kwa jinsi mwili wake ulivyokuwa ukifanya kazi , illikuwa ni kama vile alikuwa na mawasiliano na kila kiungo cha mwili , hata pale seli ambazo zilikufa na kujitengeneza zingine ni kama vile alikuwa akijua kinachofanyika.
Hisia za namna hio katika wakati huo zilikuwa ni za kipekee sana na ilimfanya kuhisi ulimwengu uliokuwa mbele yake ulikuwa sio , ilikuwa ni kama vile yupo katika lango jipya la anga.
Kila kitu ambacho kilionekana kuwa halisi katika macho yake ni tofauti..
“Hahaha…”
Roma wakati akiwa anahangaika ni kama vile alipata utashi flani hivi uliomfanya kucheka na hakujua hata ni kwa namna gani alisogea na hakujali ni shambulizi gani ambalo Lekcha atampiga nalo.
Kwa wakati huo upande wa Roma vita hio haikuwa ya kifo na uhai bali furaha mpya ili ujaza moyo wake, ni kama vile alikuwa akifurahia kinachoendelea katika wakati huo.
“Mvulana mjinga huyu … anacheka nini sasa”
Hata kama uwezo wa kufikiria wa Aoiline ni mkubwa kuliko wa Roma lakini hakuweza kuelewa ni kitu cha namna gani Roma alikuwa akipitia , hakuelewa hisia zake zilikuwa zikimaanisha nini.
Baada ya muda mfupi Aoiline alikunja ndita na aliangalia juu katika sehemu walipokuwa wakipambana Lekcha na Roma.
Kipande cha anga katika eneo waliopo ni kilikuwa kikiharibika kwa kasi , kwa macho ya kawaida unaweza usione kinachoendelea lakini kwa macho ya kijini au ya kiuungu lazima uone kinachotokea na kufanya nishati ya Ant-Matter aliokuwa akizalisha Lekcha kuwa na mawasliano na ulimwengu wa nje ya mnara hhuo.
Ilikuwa ni mnara huo umetengeneza ufa ambao ulikuwa ukipitisha hewa kwa juu.
“Hii nii…”
Aoiline aliwaza lakini macho yake yalichanua kama vile alikuwa ametegemea kitu ambacho kinakwenda kutokea.
Roma ambaye alikuwa akipambana na Lekcha alikuwa akicheka kama vile ni kichaa na uso wake ulikuwa umejaa hali ya kujiamini, hali flani ya utambuzi na ukuu kama vile ni mtawala mbele ya watawaliwa.
Lekcha ambaye alikuwa akipambana na Roma alijikuta akikasirika sana mara baada ya kutumia njia zote kujaribu kumfikia Roma kimashambulizi na kushidwa , kilichompa kero zaidi moyoni ni namna ambavyo Roma hakumchukulia siriasi.
“Siwezi kushindwa , siwezi kushindwa nimetoka mbali kufika hapa siwezi kushindwa leo , lazima nikumalize leo Hades”
Lekcha alibwatuka kama vile ni kichaa lakini sauti yake ilimezwa na ngurumo ya radi kubwa sana ambayo ilisikika kutoka nje ya mnara.
BOOM!!
Ilikuwa ni sauti kubwa ya kuumiza masikio ambayo ni kama vile mnyama ananguruma katika lindi la ukiwa wa milele au kama vile ni Mungu anafungua makufuli ya mateso k wa viumbe wake binadamu.
Ilikuwa ni ngurumo ambayo haikuwa ya kawaida , ambayo kwa haraka haraka haikuwa na asili ya mnara huo na kufanya waliokuwa wamesikia ni kama vile masikio yao yanasikia Kengele ya tahadhari .
Na ile sehemu ambayo walikuwa wamesimama Roma na Lekcha palikuwa na tundu ambalo limejitokeza kwa juu kupitia kwenye ule ufa ambalo lilikuwa na mawasiliano na ulimwengu wa nje.
“Hio ngurumo ya Dhiki ya mapigo elfu moja ya radi!! , Aisee huyu mtoto hazuiliki , kijana umefanikiwa vipi kuelewa haraka hivi tamaduni zetu na kupanda levo kila unapokuwa kwenye changamoto?”
Ailione ambaye alikuwa tayari amekwisha kupitia adhabu ya mapigo mengi ya radi alikuwa akijua kani ya radi ya mapigo mengi , alikuwa amepitia adhabu ya mapigo zaidi ya elfu moja hivyo asingeweza kushindwa kujua kinachoendelea.
Lakini sasa umri wa Roma ni miaka ishirini kwenda therathini kitu ambacho sio cha kawaida kwa umri huo kuweza kusababisha radi ya mapigo mengi.
Alijiambia mtoto huyo ambaye alionekana kuwa na tamaa ya pesa na maisha ya anasa haijalishi nini amefanya au wapi ametokea uwezo wake wa kutambua siri za mbingu na ardhi ni mkubwa mno kiasi kwamba unamfanya yeye mwenyewe kuona wivu.
Lekcha alijikuta akihamaki kwani hakutgemea mabadiliko ya namna hio.
Alikuwa akielewa kuhusu radi na mateso yake tokea siku ambayo aliweza kuuvaa mwili wa mkuu wa majoka mfalme Wuja , ijapokuwa alikuwa akijiamini kutokana na nguvu yake ya nishati ya Ant -matter lakini hakuwa na uhakika kama anaweza kupona kama atapigwa na radi ya mapigo elfu moja.
“Muda wowote radi itafika ndani ya hili eneo , je bado unataka kuendelea kushindana na mimi?”Aliuliza Roma huku akiona ishara ya wasiwasi kutoka kwa Lekcha
Lekcha alijikuta akiona ni kama vile anadhalilishwa na aliishia kutoa tabasamu la kejeli akionekana hataki kushindwa.
“Inaonekana umekasirisha anga na muda wowote radi inakuja kukupa adhabu yako ,hivi wewe mwenyewe unao uwezo wa kupona kabla ya kuniuliza , nina ngungu ya ant-matter ambayo inawea kulinda mwili wangu , unadhani radi hio itaweza kunifanya nini?”Aliongea Lekcha kwa kujiamini.
Roma hakuwa akipanga kumkasirisha Lekcha ukweli ni kwamba alijua kumdhibiti Lekcha lilikuwa ni swali la muda tu.
Hata kama hatomuua Lekcha Roma bado alikuwa na uwezo wa kutumia shoka lake na kumfungia katika space crack au kumpoteza mazima katika malango ya anga.
Lakini kwasababu Lekcha alionekana kuwa na hamu ya kupitia uzoefu wa nguvu ya radi akiwa na yeye hakuona haja ya kumjali
Mara baada ya kusita kidogo palepale alikiita chungu chake cha maafa kwa mara nyingine lakini hakutumia kwa ajili ya kujikinga na radi ambayo inatarajia kushuka alisimama na kisha alikizibia na mwili wake
Yaani alichokifanya Roma ni tofauti kabisa na mwanzo , kwani ili kupita dhiki hio ya mapigo mengi alitakiwa kukiweka chungu hicho juu ake kama kinga lakini awamu hio ni kama anakilinda chungu hicho na radi.
Kitendo kile kilimfanya Aoiline kuwa katika hali ya mshangao na alitaka kumuuliza Roma anajitafutia kifo lakini mara baada ya kufikiri kwa haraka alioneakna kupata wazo ambalo Roma anajaribu kufanya na macho yake yalijaa mshituko na kuamua kukaa kimya akitarajia namna Roma anavyokwenda kupita dhiki hio.
Upande wa nje mnara wote ulifunikwa na dhoruba ya wingu zito mno kiasi kwamba ni hakika wale ambao wapo karibu na mnara huo wasingewea hata kuuona kwani ulifunikwa mpaka kwenye maji na ni cheche tu na ngurumo ambazo zilikuwa zikisikika.
Katika ile floor ambao walikuwepo Roma ile ufa ambao umejitengeneza ulionekana muda wowote unakwenda kuporomoka kutokana na presha ambayo inajiandaa kuingia ndani.
Hali ya giza ilizidi kuongezeka ndani ya mnara na hakukuwa na mwanga tena kama mwanzo.
Roma upande wake hakuwa na muda tena wa kumfirikia Lekcha , ukweli ni kwamba aliacha kabisa kupambana nae.
Kulikuwa na nafasi ndogo sana kwa Lekcha kuweza kukwepa radi ile kwani alikuwa amekaribiana sana na Roma.
Ilionekana ni dhahiri baada ya Dhiki hio ambaye atafanikiwa kutoka hapo wa kuipita hio dhiki basi moja wa moja anaweza kuwa mshindi.
Boom!!
Palepale mwanga ulionekana ndani ya eneo lile mara baada ya shoti ya radi iliokuwa katika mwanga wa rangi ya fedha(silver), yaani ni mwanga ambao haukuwa mweupe sana wala mweusi sana.
Shoti ile ilianza kidogo kidogo na kwa nje ilikuwa ni kama vile anga linashambulia ule mnara na radi na kutaka kuangusha kwani wingu lilikuwa likizunguka kwa kasi kubwa mno , ni kama vile kuna panya yupo shimoni na paka anatafuta namna ya kupita ndo ilivyokuwa kwa namna wingu hilo lilivyokuwa likizunguka kupata upenyo wa kumpa Roma anachostahili.
Kitendo kile kilifanya mnara wote kuwa na hali flani ya umeme ambao ulikuwa endelevu , yaani ni radi ambayo haikukoma ni kama vile umeme umewashwa kutoka mawinguni na kuingia ndani ya mnara huo.
Upande wa Roma na Lekcha walikuwa wamefunikwa na shoti za radi ambazo ni kama hazina mpango wa wa kuwaachia na kuwafanya hata miili yao isionekane.
Zile nguvu za nishati ya Ant-Matter ambazo zilikuwa zimesambaa zote ziliyeyushwa na shoti za radi na kupotea mara moja , ikionekana kabisa hakuna uwezekano wa kuhimili nguvu yake.
“Arghhhh…uwiii!!”
Lekcha alipiga yowe kubwa mno la kilio cha kusaga meno na hio yote ni kutokana na kuyeyuka kwa kasi kwa nishati yake ya Ant Matter na kugeuka mvuke ambao ulipotelea angani. Alikuwa akibabuka kama vile ni magamba ya mti.
Upande wa Roma hakuonyesha ishara yoyote kama alikuwa akipitia maumivu .
Ukweli ni kwamba ile radi ilikuwa imemfunika Roma sio kwamba ilikuwa ikimshambulia lakini ni kama vile ilikuwa ikimzingira na kushidwa kupita katika mwili wake hivyo kutokumsambabishia maumivu yoyote.
Ilikuwa ni kama vile inamuogopa Roma kumshambulia kabisa tofauti na ilivyo kwa Lekcha.
Katika mkono wa kulia wa Roma alikuwa akibadilisha kwa kiwango kikubwa nishati za mbingu na ardhi na kutengeneza moto wa rangi nyeusi huku mkono wa kulia alikuwa ametengeneza kiwango kikubwa cha moto wa rangi ya bluu.
Moto ule ulikuwa ukimzingira na kutengeneza kitu kama gamba la radi ya rangi ileile ambayo ilikuwa ikisukumana na ile ya radi ya Dhiki.
Yaani ilikuwa ni kama vile nguvu ambayo Roma anadhalisha ilikuwa ikikataana na dhiki ile ya radi ndio maana ilitengeneza ‘magnetic field’ ambayo ilifanya radi ile kumzunguka Roma na kutokumgusa.
Ushawahi kuona filamu ambayo binadamu yupo msituni na anakutana na Dubu na yupo katika hali ya kutoweza kukimbia na anafumba macho kusubiria kuraruliwa na lile Dubu lakini ajabu mnyama yule aina ya Dubu anapiga magoti na kukusujudia basi hali hio ilikuwa ni kama vile kwa radi ile ya mapigo mengi.
Kitendo cha Roma kudhalisha moto mweusi na bluu na kisha kuunganisha kulimfanya kuweza kutengeneza radi yenye tabia sawa na ile ya Dhiki na kumfanya isihindwe kumsogelea.
Kifizikia kilichokuwa kikitokea ni sheria ya Ki’Electrostatic , sheria ambayo inaelezea kwamba kunapotekea chaji mbili zinazofanana ziwe aidha ni chanya au hasi ili mradi ziwe zimefanana basi zitakataana na kama zikitofautiana zitavutana.
Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema hakuna mvutano wowote kati ya mwanaume na mwanaume bali kuna mvutano mkali ambao huleta madhara pale mwanamke na mwanaume wanapokutana sasa chukulia radi aliotengeneza Roma ni radi dume na iliotaka kumuadhibu ni radi dume pia hivyo ki asili zitakataana.
Sasa ni kwamba kabla ya radi hio kushuka Roma alishajua kwamba akiunganisha elementi za moto mweusi na moto wa bluu atatengeneza shoti ya radi ya rangi ya fedha ambayo ndio rangi hio hio ya Dhiki.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba radi ya mapigo tisini na tisa ilikuwa na rangi yake na radi ya mapigo tisa ilikuwa na rangi yake vilevile na radi ya mapigo mia tisa tisini na tisa ilikuwa na rangi yake vilevile.
Utofauti huu wa rangi inamaanisha namna inavyotokea kuna utofauti mkubwa wa elementi za chaji.
Roma hakuhitaji chungu kujilinda na radi tena hio yote ni kwamba anao uwezo tayari wa kutengeneza radi ya rangi ya silver kwa kuunganisha moto wa rangi nyeusi na moto wa rangi ya bluu na matokeo yake ni kwamba akawa anafanana na radi ya mapigo mia tisa tisini na tisa na kama sheria kifizikia ya asili inavyosema radi ile ilimtambua Roma kama mwenzake kutokana na kudhalisha nguvu inayolingana na kwake na matokeo yake ilishindwa kumdhuru.
Upande wa Lekcha yeye ni kama vile alikuwa Chanya na radi ilikuwa hasi na sheria ya asili inaelezea kwamba ikitokea nguvu mbili hazifanani basi zitavutana na ikitokea hizo nguvu mbili moja ni dhaifu basi itamezwa na ile iliokuwa na nguvu.
Hivyo ant Matter ilikuwa ni dhiafu na radi ilikuwa na nguvu hivyo moja kwa moja nishati ile ilifunikwa.
Radi ile ilikuwa ni endelevu , pengine ni aina ya radi ambayo binadamu wa kawaida hajawahi kuishuhudia na kadri ilivyokua ikiendelea kushambulia upande wa Roma alikuwa akipitia steji mbili muhimu sana ambayo ya kwanza ni Soul Evolution(Kukua kwa nafsi) na pili ni Soul Cleansing(Usafi wa nafsi) ambazo steji hizi zote mbili ukiziunganisha majini wanaita Ubatizo wa moto wa mbingu(heavenly fire baptism) ama ubatizo wa radi katika lugha ya kibinadamu.
Ukumbuke majini hawaiti radi kama radi bali kwao radi ni sawa na moto wa mbingu au moto wa Mungu na wao wanaamini kwamba moto wa mbingu ndio huwatengeneza au ni kama chanzo cha kukua kwao.
Katika hatua za juu kabisa za uwezo wao au unaweza kusema levo ambazo majini wa viwango vya juu sana ambao walipitia ni katika hatua ya ubatizo wa moto wa mbingu.
Lakini sasa tokea enzi zile hakuna jini ambaye ashafanikisha kupitia hatua ya ubatizo wa moto.
Roma hakupata faida ya kusafishwa kwa nafsi au kukua kwa nafsi pekee bali pia alipata usafisho wa mwili , yaani ni kama vile mwili wake uliondolewa kitu ambacho kilikuwa kikimsumbua kwa muda mrefu na kumfanya kuzidi kuwa imara.
“Hatimae imetokea… huyu mtoto amekwisha kupata ufunuo wa radi ya mapigo mengi na namna unavyotokea , hii radi ya kimungu haina tena madhara kwake zaidi ya kuwa ndugu aisee sijatarajia baada ya maisha yangu marefu kushuhudia kitu cha namna hii”Aliongea Aoiline mwenyewe .
Huku hisia mbalimbali zikipita katika moyo wake , ilionekana kwamba ukiachana na Roma kuweza kujua siri ambayo ipo katika adhabu ya mapigo tisini na tisa ya radi lakini pia alikuwa amefahamu siri iliopo nyuma ya mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi.
Kwa mtu wa kawaida anaweza kusema kwanini majini waogope radi ilihali Roma anaweza kuwaambia siri ya radi hizo lakini ukweli ni kwamba ili waweze kufanikisha hilo lazima wakaanze moja katika hatua za uvunaji wa nishati za anga kwa kutumia mbinu ya andiko la urejehso.
Roma aliweza kudhibiti siri ya radi hizo kutokana na kwamba alikuwa amepitia njia ndefu ya mafunzo hayo ambayo ndio kama msingi na hii ilimpelekea kuwa na uwezo wa kutengeneza moto adimu sana ambayo una elementi zote za kutengeneza radi , mfano wa moto wa bluu , maji ya kiroho na moto mweupe.
Siraha za namna hio ni majini wachache sana ambao wanaweza kutengeneza au hakuna kabisa ndio maana tokea mwanzo miliki zote za majini watu zilikuwa zikimuwekea Roma njama ya kutaka kumpa siri hio.
Ikumbukwe kwamba katika hatua za andiko la urejesho mbinu ya hatari zaidi ni ile ya kufa na kufufufuka , yaani steji ya kifo na uhai.
Kwahio basi mpaka muda huo Roma aliweza kupitia hatua muhimu ambayo ya kwanza ni mapigo tisa ya radi ambayo steji hii alitumia uwezo wa mwii wake kujiponyesha kwa haraka na andiko la urejesho , hatua ya pili ya dhiki ni mapigo tisini na tisa ambayo aliyapata katika mnara huo wakati wa kutoka kwa msaada wa Cauldron na hatua ya tatu ni mara baada ya kumshuhudia Anjiu akipitia levo ya mapigo ya radi alikuja kufahamu siri ya kutengeneza radi ya zanbarau na hatua nyingine ni hio ya sasa ya kupitia mapigo mia tisa tisini na tisa lakini awamu hio hakuumia zaidi ya kwamba aliidhibiti ile radi kwa kujifananisha nayo ili sheria ya asili(law of nature) ifanye kazi.
Wakati Roma akifurahia namna ambavyo radi ya mapigo mengi ilivyokuwa ikimzunguka na kuendelea kunyonya nishati yake Lekcha yeye alikuwa katika kilio cha kusaga meno.
Ilikuwa ni ngumu sana kwake kujiokoa katika hali ambayo alikuwepo , iapokuwa radi ya Zambarau ilikuwa na uwezo wa kuharibu mwili wake lakini ukubwa wa nguvu ya ant matter iliuwa na uwezo wa kumrejesha lakini awamu hio radi ya rangi ya fedha haikuwa mchezo kabisa , sio tu kuharibu mwili lakini pia ilianza kuharibu na nafsi yake.
Haikujalisha nishati ya Ant Matter ilikuwa na nguvu namna gani lakini hakuweza kulinda kitu muhimu sana ambacho ni roho au nafsi , ilimaanisha kwamba Lekcha alianza kukosa ufahamu wa kujiendesha na kuwa kichaa na kadri sekunde zilivyokuwa zikisonga angepotea moja kwa moja.
Alijitahidi kukusanya kiwango kikubwa cha nishati kulinda roho yake lakini hakufua dafu kwani nishati yake ilikuwa na kikomo lakini kwa mapigo elfu moja ya radi hakukuwa na kikomo cha ukubwa wake.
Aliweza kuona kabisa nguvu ya radi hio ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi kuvumilia tena na kifo kilikuwa kikimsogelea kwa kasi ya 5G.
BOOM
Awamu ya pili kubwa zaidi ya pigo la radi ilishuka , haikueleweka pigo moja lina uzito wa nguvu kiasi gani kukamilisha hesabu ya 999 lakini ni dhahiri mapigo yasingekuwa moja moja.
Roma alikuwa katika hali ya furaha ya ubatizo wa radi hio na mabadiliko ya kiakili aliokuwa akipitia ilimfanya kumpotezea kabisa Lekcha aliekuwa akilia kama mtoto.
Ajabu ni kwamba ni nje ya mahesabu ambayo Roma alitarajia kwani alipitia mapigo matatu tu ambapo kila pigo moja lilidumu kwa dakika kumi na tano.
Haikueleweka ni kwa namna gani majini waliweza kutoka na hesabu ya mapigo tisini na tisa katika awamu tatu lakini kutokana na ukubwa wa radi hio na nguvu yake Roma aliamini inawezekana awamu tatu kukamilisha mapigo yote mia tisa tisini na tisa.
Mara baada ya dakika kumi na tano kumalizika za pigo la mwisho hali ya hewa ilirudi katika hali yake ya kawaida kwa kasi sana.
Na hata ule mwanga wa rangi ya silver ambao ulidumu ndani ya mnara huo kwa dakika arobaini na tano ulirudi katika hali ya kawaida.
Hali ya hewa ndani ya mnara huo ilikuwa ni harufu flani hivi kama ya baruti iliochanganyika na kuungua kwa mimea na kuyeyuka kwa baadhi ya dhana zilizopo ndani humo.
Roma alivuta pumzi nzito na kisha alishuka taratibu na kukanyaga floor hio ambayo ilikuwa imepata moto , chungu cha machafuko kilimzhuguka Roma kwa namna flani hivi ya kumlaki kikimuelezea kwamba licha ya kumkinga na radi lakini pia kimefaidika .
Roma palepale aliamua kuficha Shoka lake la kimaajabu na chungu kile kwani hakuwa na uhitaji navyo kwa muda huo.
Mwili wake ulikuwa ukitoa harufu flani hivi isiokuwa ikielezeka lakini kwa mbali ni kama vile kuna cheche za shoti zilizokuwa zikionekana katika mwili wake uliokuwa umetuna kwa mazoezi.
Hakuwa na nguo hata moja wakati huo alikuwa uchi wa mnyama na kwanzia vidoleni mpaka chini alikuwa akitoa shoti za umeme na ilikuwa ni kama vile mwili wake unapo kwani shoti zile zilikuwa zikififia.
Roma alishangazwa na nguvu ya radi hio lakini alijua kabisa hapo sio mwisho , inasemekana majini wa enzi hizo walipitia mpaka hatua ya mwisho kabisa ya mapigo 9999 , sasa alijiuliza kama ni hivyo waliwezaje kupita hatua hio au na wao walikuwa kama yeye tu walijifananisha na radi hio na matokeo yake radi ilifuata kanuni ya asili.
Roma mara baada ya kuwaza kwa muda hatimae sasa akili yake iliwaza kuna Lekcha na aligeuka palepale na alipoangalia sehemu Lekcha alipo aliona vijicheche kwa mbali ambavyo vilikuwa vikipotelea.
Kama ilivyo kwa Roma mwili wake kupoa upande wa Lekcha alikuwa amerudi kawaida na mwili wake ulikuwa umepoa kabisa kwa kupoteza nishati yote ya Ant-Matter.
Ilionekana radi yote ilikuwa imekula nishati yake na kumbakisha mweupe na kuwa kama binadamu wa kawaida tu.
“Hukutakiwa kuwa na kiburi…. Vinginevyo ungeweza kupata nafasi ya pili , isitoshe mwili wako unaonekana kutokuwa wa kawaida”
Roma aliongea huku akitembea kumsogelea Lekcha aliekuwa akitetemeka kama vile mgonjwa wa Malaria kali.
Lekcha aliepiga goti alijikuta akivuta pumzi nyingi na kisha kwa unyonge aliinua kichwa chake , alikuwa amefubaa kama karatasi lakini hata hivyo hakupoteza ile hali ya ukejeli kwenye uso wake , ilikuwa ni kama vile hakujali tena kifo.
“Acha kunionyesha hio tabia yako ya kujiona unajua kila kitu , hivi unajua kinachonifanya kukuchikia zaidi ni nini , kinachonifanya ni kuchukie sana ni tabia yako ya majigambo”
“Inaonekana una chuki binafsi zidi yangu lakini niwe tu mkweli sijawahi kukuchukulia kama tishio kwangu lakini hata hivyo umenishangaza , sijui kuhusu mengine lakini kitu ninachojua ni kwamba sijali namna yoyote ile unavyonifikiria”
“Hahahaha… , kwaio ndio unajigamba , naona mwishoni nimekushindwa kama alivyoshindwa yule mjinga Yan Buwen na mjinga wake Denisi , mpaka mwishoni inaonekana hakuna ambaye anakuweza na yamkini hapo mwenyewe unajihisi sio wa kawaida lakini Roma ngoja nikuambie kitu , mimi Lekcha a.k.a Joseph Bikindi hujanishawishi juu ya uwezo wako wala siwezi kukubali, hata kama nikifa siwezi kukuruhusu ujione shujaa au kukufanya ufikirie umeniweza .. kitu pekee ambacho kimenifanya kuwa katika hali ya kushindwa ni bahati basi , najiuliza kwanini sikuwa na bahati ya kupata fursa ya kukutana na master ambaye ni mzuri kwangu , kwanini niligeuzwa na kuwa mtumwa , kwanini kuna watu nyuma yako ambao wapo tayari kukusaidia ,, Hades umefanikiwa hayo yote kwasababu bahati ilikuangukia na ukawa upande mzuri , tokea ulivyozaliwa Mungu alishakuandikia utafanikiwa kwa kutuchukulia sisi kama ngazi , lakini hebu jiangalie sasa hivi unavyojiona mwenyewe, sio juhudi zako pekee zilizokufikisha hapo mwanaharamu wewe”
Lekcha alitumia kadri ya uwezo wake wote kuongea kwa sauti lakini hata hivyo sauti yake ilionekana kunyongea sekunde hadi sekunde.
Roma aliishia kucheka kivivu kama vile ashajichokea hata kumgusa Lekcha lakini hata hivyo hali flani ilionekana katika macho yake mara moja.
“Huu ni muda wa wewe kuacha kuwa mpumbavu , najua haina maana kukuelewesha tena lakini nikuambie tu wewe ni moja kati ya maadui zangu ambae umechukua muda mrefu , ukweli sio kwamba nakuchukia kihiivyo , kabla roho yako haijauacha mwili wako nataka nikuambie kitu ,, pengine ulichosema ni kweli kwamba ni neema za Mugnu zilizonifikisha leo hii lakini unaweza kushangaa kwamba wakati wewe ukiwa mwanafunzi mzuri na kinara shuleni kwenu, unaependwa na walimu kwangu mimi sikuwa hata na uhuru wa kuitwa chokoraa .. hivi unadhani umeshindwa na mtu ambae alikuwa na kila kitu , ngoja nikuambie umeshindwa na mtu ambaye hakuwahi hata kujua alikuwa na familia wala ni wapi alizaliwa , mtu ambaye alitegemea nyama ya binadamu kuishi , mtu ambaye alikuwa ni sehemu ya majaribio ya kisayansi ambayo maumivu yake sio ya kawaida , kwasababu tu ya kupoteza ndugu na kuwa kilema ndio useme Mungu amenipendelea , ninachomshukuru Mungu leo hii kunipa nafasi ya kuendelea kuishi mpaka leo hii licha ya changaoto zote nilizopita na hii ndio tofauti yako na yangu , unaamini Mungu kanipendelea lakini mimi namshukuru kwa kunipa nafasi ya kuishi”
Machozi ndio dalili pekee ya uhai iliomtoka Lekcha na mara baada ya kuvuta pumzi ndefu palepale nywele zake zilianza kubadilika rangi na kuwa nyeupe na hatimae rangi ya kijivu na ngozi yake ikakauka na kujikunja na hatimae kukosa sifa ya ubinadamu na uhai wake ulionekana ndio unafikia mwisho taratibbu taratibu.
Katika uso wake huo ambao ulikuwa ni kama udongo hali ya furaha, huzuni na makasiriko iliweza kuonekana na alionekana kuwa wa tofauti sana kuliko mwanzo , hakuna neno ambalo liliweza kutoka katika kinywa chake kana kwamba alikuwa akisubiria wakati wake wa mwisho.
Roma aliendelea kumwangalia Lekcha jinsi alivyokuwa akibadilika rataribu kadri nishati ya ant-matter ilivyokuwa ikipotea hewani na palepale alivuta pakiti ya sigara kutoka katika hifadhi yake ya anga na kuchomoa moja.
“Vipi nikupatie moja?”Aliuliza Roma, ndio kitu pekee ambacho alikuwa na uwezo wa kumpatia Lekcha muda huo katika hatua zake za mwisho.
“Pengine hujawahi kuvuta sigara ghali kama hii maisha yako yote”Aliongea Roma na kisha alichuchumaa na kumshikisha Lekcha ile sigara na alisita kidogo na hatimae Lekcha alionekana kuishikilia japo kwa taabu na kisha akaitumbukiza katika mdomo wake, mara baada ya Roma kuiwasha Lekcha alivuta moshi kidogo tu na kushikwa na kikohozi kilichomfanya sifara kudondoka.
“Naona unanikejeli , nimepokea hii sigara kwasababu inaonekana ya thamani sana na ingesikitisha nikifa kabla ya kuonja moshi wake … usijione wewe ndio mtu pekee ambaye umepitia mengi na una uzoefu wa kuishi maisha ya kifahari”
Roma alivuta kwanza moshi na kuupuliza hewani na kisha alitoa tabasamu huku akiona kiwango cha mwisho mwisho cha nishati ya Ant-Matter kikipotea katika mwili wa Lekcha.
“Kama ningekuwa mtu mkarimu pengine ningekupatia bia ya ya thamani kubwa lakini nimekupa sigara kwani ndio kitu pekee cha thamani ndogo nilichokuwa nacho”Aliongea Roma na kumfanya Lekcha kutoa tabasamu la dhati lisilo na unafiki kwa mara ya kwanza mbele ya Roma.
Muda huo ndio aliweza kufika Aoiline kwani alijitenga mbali sana na eneo hilo na mara baada ya kutua alimwangalia Roma kwa namna ya kushangazwa nae.
Alimwangalia namna ambavyo Roma alikuwa akiwasha sigara moja baada ya nyingine huku akiangalia namna ambavyo Lekcha anavyochukuliwa na Israeli mtoa roho.
Roma baada ya kuona hakuna tumaini lolote kwa Lekcha alisimama na kisha alimsogelea Aoline na ni muda uleule aliruhusu radi kumpiga Lekcha na akageuka kuwa majivu na huo ndio ukawa mwisho wake.
“Inaonekana angalau mwishoni chuki yake zidi yako imempotea”Aliongea Aoiline.
“Labda , kumalizana nae ni kama kuagana na kipindi kingine cha maisha yangu , Ni nani ajuaye kinachonisubiri mbele”
Aliongea Roma huku akitoa tabasamu hafifu kana kwamba ashaona nini kinamngojea huko duniani.
ITAENDELEA.