Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Good Story
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Much thanks S.JrNILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA .
MTUNZI SINGANOJR.
Mono no aware
SEHEMU YA 754.
Roma aliishia kukunja sura akiwa ndani ya Kizimba(Cage) amekunja ngumi kwa hasira huku akiwa kimya wakati vipele vikienelea kuota katika mwili wake na kunyauka kwa kasi.
Wakati Roma akionekana kama vile amejikatia tamaa kabisa majini wale walishangilia na kuridhika kabisa.
“Haha..ulikuwa na maringo sana lakini sasa hivi umekuwa mpole kama mbwa , unaonaje ukipiga magoti na kuomba msamaha?”Aliongea Menyu mkuu wa miliki ya Kekexil huku akicheka kicheko cha furaha.
“Nadhani anaogopa sana hapo kiasi cha kushindwa kuongea chochote , ndani ya lisaa limoja na nusu huyu shetani atakuwa amekwisha kufa”Aliongea Gefu akiwa katika hali ya kutabasamu
“Uhai wa raia wa Panas zaidi ya elfu moja umepotea katika mikono yako hivyo ni damu yako inakwenda kulipia deni”Aliendelea kuongea.
“Haina haja ya kupoteza maneno yetu , tumuueni kwa nguvu zetu zote ili kusitokee tatizo kabisa”Aliongea Anjiu.
Majini hao hatimae walikaa kimya lakini hakuna ambaye alijali kwani asilimia mia moja wote walikuwa wakitaka kuona kifo cha Roma.
Dhana ya fuvu la misumari tisa ya mfupa wa Dragon iliendana na jina lake , majini hao katika vitabu vyao walisoma na kuelewa kwamba ambao washawahi kutumia Dhana hio wengi wao wamekwisha kufa kutokana na kunyonywa damu.
Ukweli ni kwamba hata kwa Shozi ambaye alikuwa mdhibiti wa Dhana hio, kama akifanikiwa kumkamata Roma katika kizimba hicho cha damu baada ya hapo kuna uwezekano mdogo sana wa kuendelea kuishi muda mrefu , hio Dhana athari yake kubwa ni kupunguza urefu wa maisha kutokana na kwamba inanyonya uhai kupitia damu.
Roma alikuwa amesimama katikati ya boksi hilo , chungu chake cha maafa kilikuwa pia kipo ndani kikielea katika kichwa chake, ule ukali wa chungu hicho ulionekana kupungua kabisa.
Dakika iliofuata baada ya Roma kunyanyua kichwa chake uso wake haukuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi lakini viashiria vya kukata tamaa vilionekana kwa mbali.
“Inanishangaza kuona bado unao uwezo wa kutumia huo mkono…”
Majini hao waliokuwa wamezunguka kizimba hicho cha gereza la damu hawakumwelewa Roma anachomaanisha na walioamini anaongea ujinga.
Roma mara baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa palepale aliweka kila alichokuwa amekishikilia katika hifadhi ya pete na kisha mkono wake mmoja wa kulia alibadilisiha nishati za mbingu na ardhi kwa kutengeneza moto wa rangi ya zambaranu na mwingine akatengeneza moto wa rangi ya bluu na madonge yale ya moto yalizidi kuongezeka ukubwa kadri sekunde zilivyokuwa zikisonga.
“Dogo bado tu unahangaika , unachokitafanya ndio kitakuua mapema”Aliongea Umini.
Roma alimpotezea kabisa na wakati moto ule ukiwa unawaka katikam mikono yake alifanya kitu kama vile anapiga makofi ili kuunganisha ule moto kwa pamoja.
“BOOM!!
Moto wa rangi ya Zambarau na wa bluu uligongana na kusababisha kishindo cha aina yake , ilikuwa ni kama vile aina hizo mbili za nishati zilikuwa zikiumana na kujaribu kumezana kwa wakati mmoja.
Ilichukua sekunde kadhaa tu kama vile kemikali zimeungana hatimae kulitokea matokeo mengine kabisa ambayo ni ya kimaajabu mno.
Roma mikono yake ilikuwa ikitetemeka kwa nguvu kama vile inaungua na alitumia nguvu ambayo sio ya kawaida kujaribu kuhakikisha nguvu hizo mbili za moto zinaungana ili kutengeneza kitu kingine.
“Buzz. Buzzz, Buzzz!!!!”
Ilikuwa ni cheche za umeme ambazo zilitoa sauti flani hivi kama ile ambayo inasikika wakati wa mafundi wakichomelea chuma na umeme lakini yenye sauti kubwa mno.
Mwanga wa ajabu uliweza kutokea pia katikati ya viganja vya mikono ya Roma na kuna kitu ambacho ni kama vile kinafutuka kana kwamba muda wowote kinakwenda kulipuka.
“Hicho ... hicho ni……!!!!!”
Anjiu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki mara baada ya kuhisi kitu cha ajabu , macho yake yalikuwa yamepanuka kiasi kwamba yanataka kumchomoka.
Wucheni na wenzake pia walianza kuhisi nguvu ya ajabu ikitoka katika eneo ambalo amesimama Roma , ilikuwa ni nguvu ambayo hawakuwahi kuihisia katika maisha yao yote na ilionekana nguvu ile ilikuwa ikianza kula ukuta wa kizimba cha damu.
Mwanga uliokuwa ukionekana katikati ya mikono ya Roma ulizidi kuongezeka na kuzidi kuwa na nguvu sekunde hadi sekunde.
“Hehe.. hahaha simaanishi ,,, kila kitu kilichopo chini ya nguvu ya radi ya mapigo mengi , moto wa mbingu na maji ya kiroho hayana nguvu.. dah .. ninashauku .. kama nguvu ya radi ya mapigo tisa athari zake zilivyo”
Roma alikuwa akibwabwaja mwenyewe maneno ambayo hayakuwa yakieleweka ilionekana ni kama vile kuna ufunuo anaupata.
Palepale aliinua sura yake juu kama vile anaangalia anga huku akitunisha kifua na ghafla tu mikono yake ilijiachia.
“Hey!!”
Ghafla tu shoti ya radi ya mwanga wa bluu na zambarau ilitoka katika mikono yake na kutengeneza umbo kama la mkuki uliopinda pinda huku ukitoa cheche.
Mwanga wake ulikuwa ni mkali mno na ndani ya sekunde tu Roma alikuwa amefunikwa na mwanga ule na sehemu aliosimama ilionekana kama vile ni jua la rangi ya bluu zambarau na ngurumo kubwa ilianza kugonga na mwanga ulikuwa ukizidi kuongezeka na kuwa mkubwa sekunde hadi sekunde.
Upande wa Roma alikuwa akiendelea kuzalisha moto wa bluu na wa zambarau katika mikono yake na kuunganisha kwa spidi kubwa na kadri alivyokuwa akifanya hivyo ni kama yeye mwenyewe anageuka na kuwa nishati ya ajabu vile.
Ndani ya sekunde chache tu kile kizimba cha damu kilibadilika rangi na kufunikwa na mwanga na ngurumo za radi zilizidi kuongezeka na shoti za rangi ya urujuani zilianza kutoka.
“Haiwezekani … radi ya Zambarau!!!?”
Gefu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki , huku majini wengine wakiwa ni kama hawaamini kile ambacho wanakiona mbele yao.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba moto wa bluu unatokana na mapigo tisa ya radi yaani kwa lugha nyepesi ile nguvu ambayo unaipata baada ya kupitia mapigo tisa ya radi ndio inakufanya kuweza kudhibiti moto wa bluu , upande mwingine mapito tisini na tisa yanakupa uwezo wa kutengeneza moto wa zambarau.
Sasa kwa haraka haraka Roma ni kama ameunganisha nguvu ya radi ya mapigo tisini na tisa na nguvu ya radi ya mapigo tisa na kufanikiwa kudhibiti radi ya rangi ya urujuani(Violet).
Sasa majini walishangaa mara baada ya kuona Roma amegeuza moto wa bluu na wa zambarau kutengeneza radi ya zambarau.
Shozi ambaye ndio alikuwa akidhibiti kizimba cha misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa Dragoni alianza kutetemeka kwa maumivu ,ilikuwa ni kama vile mwili wake unakwenda kupasuka kutokana na presha kubwa iliokuwa ikimwingia.
“Haraka ongezeeni nguvu ya nishati za mbingu kuimalisha ulinzi , anataka kujinasua!”Aliongea Shozi kwa kubweka.
Haikujalisha aliongea kwa sauti kubwa namna gani lakini majini hao mioyo yao ilikuwa imetingishika kabisa na kukosa ujasiri.
Moja ya udhaifu wa majini ni radi(Wenyewe wanaita moto wa mbingu) , wanaiogopa radi kuliko kitu chochote kile na ndio adhabu yao kubwa ambayo ukiipita wanakupa heshima.
Kile kizimba kilishindwa kumnyonya Roma damu tena na sekunde baada ya sekunde kilikuwa kikipoteza nguvu.
Anjiu macho yake yalionyesha hali ya kusita kulikokithiri , alikuwa pia ni jini ambaye amepitia mapigo ya radi hivyo swali liliibuka kwanini Roma kuwa na mwili wenye utimamu wa namna hio mpaka kufanikiwa kuidhibiti radi , alishakuwa katika mshangao kwa uwezo wake wa kudhibiti moto wa bluu , Wa zambarau na maji ya kiroho lakini wakati huo amefanikiwa pia kuidhibiti radi ya rangi ya urujuani.
Alijiambia hapana haiwezekani sio ujuzi pekee wa Roma katika kung’amua siri za mafunzo ya mbingu za ardhi na mbingu tu , pengine ametawaliwa na nguvu ya roho ya andiko la Urejesho.
Kadri alivyokuwa akiwaza ndio namna ambavyo alizidi kuwa na hasira , alijiambia kwanini sio yeye mwenye kumiliki mbinu hio ya andiko la urejesho wa azimio, kwanini ashindwe na binadamu ambaye amejifunza utamaduni wao.
Yeye ni jini kikamilifu kwanini ashindwe na binadamu ambaye hana damu ya kijini.
Pengine Roma angeangua kicheko kama angejua kile ambacho Anjiu alikuwa akiwaza , mbinu hio ya mafunzo ilikuwa amepatiwa ndio lakini hakuwa akiwaza watu wanavyoichukulia wala kuamini uwezo wake.
“Kama nilivyotarajjia , ijapokuwa hichi kizimba chenu kinaweza kuwa kama gereza kwa jini mwenye kuipita radi lakini ni ngumu kuhimili shambulizi la radi ya Urujuani ambayo hata jini ambaye amepitia mapigo elfu moja anaogopa”Aliongea Roma.
Aliangalia kizimba hicho ambacho tayari kilikuwa kikitetema na alijitingisha kidogo tu radi ile ya Zambarau ilitoka kama vile ni mshale na mara baada ya kugusana na kingo za kizimba kile kilipasuka na kuharibu kabisa ile Dhana.
Roma ni kama vile hakuwa na uwezo wa kudhibiti uwezo wake na kama angejua nguvu ya radi hio ilikuwa na nguvu namna hio asingetumia kiharibu Dhana hio kwani angeipata huenda ingekuwa na matumizi kwake hapo baadae.
Lawama alizipeleka kwa jini Shozi kwa kutokuwa na nguvu za kutosha za nishati ya mbingu na ardhi ndio maana shambulizi lake moja limeharibu Dhana hio.
Shozi mara baada ya Dhana yake kuharibiwa ilikuwa ni kama moyo wake ndani umepasuka na alitema damu nyingi sana na uso wake ulikuwa mweupe kama vile ni karatasi kutokana na kukosa damu na hakuendelea hata kusalia katika anga kwani alidondoka chini kama kifusi akiwa katika hali ya kukata tamaa kabisa.
Dhana ya misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa dragoni ndio uikuwa ni kiini cha uhai wake na kitendo cha kuharibiwa na pigo la radi ya bluu zambarau haikuwa tu nguvu zake za kijini kumpotea lakini pia kifo kilimpata .
Hatimae Roma alikuwa amechoropoka kwa mara nyingine katika mtego wao wa kizimba cha damu na sasa alirudi na kusimama katikati ya mbingu na ardhi, kwa jinsi mwili wake ulivokuwa ukipumua ni kama kila sehemu ya mwili wake kulikuwa na moyo unaosukuma damu.
Roma sasa alikuwa ameijua siri ya radi ya zambarau , yaani alikuwa kama ule mnara wa kuingia katika ulimwengu wa majini pepo , radi na Roma ilikuwa ni kitu kimoja.
Anjiu na majini wenzake wote walionyesha hali ya hofu katika macho yao , walikuwa wamemzingira kwa umbali mrefu sana na hakuna ambaye aliweza kuthubutu kusogea karibu hata kwa nchi moja , wote walikuwa wakiogopa nguvu ya radi iliokuwa ikimtoka Roma.
Radi ilikuwa na uwezo wa kuharibu sio mwili tu bali mpaka roho na nafsi na kupotea katika anga.
“Inaonekana tayari umekwisha kufanikiwa kubobea katika kuidhibiti radi ya Zambarau ?”Aliongea Anjiu , ijapokuwa alikuwa kwa mbali lakini sauti yake ilikuwa ikisikika kwa ukaribu.
Roma alinyanyua mkono wake mmoja na ile anafungua kiganja ilikuwa ni kama vile kuna mnyororo wa radi unamtoka na kwenda angani na kutengneza kitu kama upinde.
“Kama ilivyokuwa siku ile nilivyoficha kete yangu ya ushindi leo pia ni hivyo hivyo , kama ningekuambia nimeweza kugundua siri ya kuidibiti radi ya zambarau ungenichokoza?”Aliongea Roma akiwa katika hali ya utani.
Ukweli ni kwamba ile siku mara baada ya kufanikiwa kuinyonya nguvu ambayo Chaos alikuwa ameificha aliweza kugundua mambo mawili matatu namna ya kudbiti radi , alichokuwa amekosa tu ni changamoto ya kufungua mawazo yake.
Ili kupanda levo Roma alikuwa akihitaji changamoto na ndio maana aikuwa akizitafuta sana , wakati majini wakiwaza kumuua Roma yeye alikuwa akichukulia changamoto hizo kama mbinu ya kufungua mawazo yake na hio ndio siri kubwa ambayo ipo katika nguvu ya andiko la Urejesho.
Andiko la Urejesho ni kama njia ya kupokea maono na ili iweze kukupatia maono lazima ukidhi vigezo vya kimazingira ambavyo ni kuwa katika changamoto , pale linapotokea giza kubwa la changamoto mbele yako ndio maono yanapotokea.
Yaani utofauti wa mbinu nyingi za majini wanazojifunza katika kupanda levo na kuvuna zaidi na zaidi nishati ya mbingu na ardhi ni kufanya mazoezi kila siku na kutamka maneno maalumu lakini kuhusu andiko la urejesho ni kama vile ni ahadi ambayo Mungu amemuwekea binadamu kwamba pale ambapo utakuwa katika changamoto atamletea maono ya kutatua changamoto hio.
Unapaswa kuelewa andiko la urejesho wa azimio jina hilo sio jina lake bali ni jina ambalo Roma aliamua kuliita , mwalimu wake ambaye alimfundisha kuhusu mbinu hio alimwambia aipatie jina analotaka yeye na ndio jina la Andiko la urejesho wa Azimio lilipozaliwa.
Sasa siku ambayo Anjiu alipitia dhiki ya Radi upaande wa Roma iikuwa ni kama vile maono yalimjia na kuona radi ambayo alikuwa akipitia Anjiu ilikuwa na rangi mbili yaani rangi ya bluu na Zambarau hivyo moja kwa moja Roma aliamini pengine ni muunganiko wa elementi za moto wa bluu na elementi za moto wa zambarau na matokeo yake yalikuwa ni kama vile alivyokuwa amewaza.
Roma hatimae alikuja kuelewa pengine kinachomtokea katika maisha yake ni mambo yaliopangwa na Mungu tokea mbali , hakuwahi kuamini sana katika Mungu lakini kila kinachomtokea kilikuwa katika fumbo la namna yake na njia ambazo anapitia ni kama vile zimekwisha kuandaliwa.
Ukweli ni kwamba katika sheria za kikanuni za matokeo ya radi katika rangi tofauti tofauti ukizungumzia radi ya urujuani ni matokeo ya muunganiko wa elementi zinazozalisha mwanga wa bluu na zambarau ki ufupi ni kanuni zilezle za kisayansi .
Bila shaka haikuwa kama vile unafanya majaribio ya kikemikali kwamba lazima kutokee makosa kwanza mpaka unapofikia mafanikio.
Mbinu za mbingu na ardhi zilikuwa ni za tofauti kidogo , ufunuo ukishakutokea na ukaufahamu basi ukiufanyia kazi matokeo yake ni sahihi na namna ya kupata maono ni kujua asili ya dunia ilivyo , kila kitu kipo kwa sababu kiwe na uhai kisiwe na uhai , kila tukio la asili linatokea kwa sababu na hio ndio njia rahisi ambayo ilimuwezesha kupata ufunuo.
Sasa Roma kutokana na uzoefu wake wa kijamii ulimwambia kwamba asili ya moyo wa kiumbe chenye utashi siku zote ni Dhambi kwanza kabla ya kupitia utakaso na ndio maana hakutaka kuambia mtu yoyote kwamba ameweza kufanikiwa kujua siri iliopo katika kuidhibiti radi.
SEHEMU YA 755.
Roma sasa alikuwa na hali ya kujiamini na alijiambia akishaingia katika levo ya mapigo ya radi elfu moja atakuwa na uwezo wa kutumia moto wa bluu na elementi za moto mweusi na kufanikiwa kutengeneza radi ya mapigo elfu moja.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba Roma ameweza kudhibiti radi ya mapigo tisini na tisa , hii haikumaanisha kwamba Roma anaweza kutengeneza mapigo tisini na tisa lakini katika kanuni za nguvu za mbingu na ardhi inamaanisha kwamba anao uwezo wa kutengeneza radi yenye nguvu mara 9 katika awamu 11 na ndio hutokea hesabu ya 99.
Nishati za nguvu ya radi zinaenda katika kanuni hii tatu mara tatu , tisa mara kumi na moja , tisa mara mia na kumi na moja na kuendelea.
Maana yake ni kwamba unaweza ukapigwa na awamu tatu za radi yenye nguvu sawa ya mapigo matatu ambapo moja kwa moja utakuwa umepitia mapigo tisa , au unaweza kupigwa na mapigo kumi na moja yenye ujazo wa nguvu ya mapigo tisa hivyo kimahesabu utakuwa umepigwa na mapigo tisini na tisa au mapigo mia moja kumi na moja hapo utakuwa na uwezo wa kupigwa na mapigo mia tisa tisini na tisa , kanuni hii inabadilika lakini majawabu yanakuwa yanafanana, inategemea sana namna anga lilivyokasirika na mbinu yako ya mafunzo kwa mfano Anjiu na Rozu wao walipitia mapigo matatu tu ambayo ni sawa na mapigo tisa lakini kwa Roma alipitia awau tisa na awamu tisini na tisa katika mnara
Kila pigo lina rangi yake , asilimia kubwa ya mapigo tisa rangi yao ni bluu , tisini na tisa ni zambarau na kuendelea.
Roma sasa mara baada ya kuangalia majini waliokuwa mbele yake , aliona kabisa hana cha kuogopa licha ya kwamba walihesabika kama wabobevu wa nguvu za mbingu na ardhi katika ulimwengu huo.
“Nilikuwa nikipasha mwili joto na nishamaliza sasa , ni muda wa kuanza kazi..”
Mara baada ya kuongea kauli hio alitengeneza wimbi kubwa la radi ambazo shoti zake ziligawanyika na kuwa kama mishale midogo na kuwarushia wale majini.
Ngurumo iliosikika ni kama vile dunia imegongana na sayari nyingine na kabla hata majini hao wa Hongmeng na miliki nyingine masikio yao hayajatafsiri sauti hio walikwisha kufikitwa tayari na boriti za radi na kuwayeyusha.
Kwa Roma lilikuwa pigo la kawaida tu lakini athari zake hazikuwa za kawaida kwani majini waliokuwa katika levo za maji ya kawaida wote walipotea.
Majini wote ambao wamekwisha kuijua nguvu ya radi ya zambarau walijua namna ilivyokuwa ni hatari kuguswa na radi hio ukiwa hujajiandaa , hata Anjiu mwenyewe ambaye alikuwa na uwezo wa juu alitumia chungu cha Roma kuweza kuipita radi.
“Kimbieni!”
Sauti ilisikika kusikojulikana kama vile ni ya binadamu , meza ilikuwa imepinduliwa kibabe na kitu pekee ambacho majini hao waliona ni aidha kukwepa au kukimbia na sio kufanya mashambulizi.
Majini wa levo za chini waliosalimika walikimbia kwa kutawanyika lakini Anjiu , Gefu, Wucheni walikuwa wamebakia.
“Mnataka kukimbia , kukimbia kwenda wapi?”Aliwaza Roma akiwaangalia majini hao wa levo ya majji ya kiroho.
“Nyie vipi mbona hamkimbii kama wenzenu?, nimetoa kionjo tu show yenyewe haijaanza”
“Mh Tukimbie! ,unataka tukimbie kwenda wapi , unataka turudi katika miliki zetu ili utufuate huko huko ukaondoe mizizi ya vizazi vyetu kama ulivyofanya hapa Panas”Aliongea Menyu katika uchungu mkubwa na Roma hakukataa kwani ndio alichokuwa akiwaza.
“Hujakosea , isitoshe kama mnataka nianze kuwatafuta mmoja baada ya mwingine ni usumbufu ni kheri kama kutakuwa na mmoja wenu ambaye atakuwa ananielekeza njia”
“Ni kweli unataka kuua majini wote? , Roma kwa nguvu zako unaweza kutawala dunia nzima wewe mwenyewe na hatutanii katika hili… hatuwezi kukuchokoza tena kama utatuacha tuondoke leo hii .. au kama huridhiki na hivyo sisi kama miliki ya Panas tupo tayari kuwa chini yako , itakuwa ni kutuambia tu unachokitaka na sisi tutakutimizia”Aliongea Gefu akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake.
“Ndio bro Roma , tunaomba msamaha kwa kukuchokoza , Mungu anatutaka kuishi maisha mazuri na nia yako ya kimauaji ni kubwa mno na inaenda kinyume na sheria za ulimwengu , sasa hakuna haja ya kuuana sisi kwa sisi kwanini unataka kwenda mbali namna hio?”Aliongea Umini.
“Sio wewe ambaye ulikuwa ukitaka kuniua muda huu , sasa nipo katika nafasi ya kukuua ndio unaniambia huo ujinga , kwasababu mmeamua kubakia na kufa basi sina haja ya kuwachelewesha”Aliongea Roma na palepale radi ya zambarau ilianza kumzingira katika mwili wake kwa namna ya ajabu kabisa na haikuwashambulia moja kwa moja bali ilichomoza na kwenda kugongana na wingu.
Wakati huo wingu kubwa juu angani lilikuwa likizunguka kwa kasi mno katika usawa aliosimama Roma na cheche za moto kugongana zilikuwa zikionekana.
Anga kati ya mbingu na ardhi lilikuwa giza tupu likiwa limefunikwa na ngurumo za radi sauti ilikuwa kubwa kana kwamba Mungu amaemua kuharibu sayari nzima.
Katika mabadiliko ya spidi ambayo ilikuwa ikionekana kwa macho ya kibinadamu , mawingu ya ngurumo yalitengeneza kizingia kikubwa ambacho kilizngira mzingo wa maili mia moja , katika maeneo mengi mbali na miliki hio kulikuwa na Dhoruba kubwa ya upepo.
Sasa katikati ya kizingia hicho ndio mahali ambapo Roma alikuwa amesimama , ilionekana alikuwa akiivuta radi kutoka juu kuja chini , haikuwa uwezo wakudhibiti radi tu lakini alikuwa na uwezo wa kuyasuguanisha mawingu kwa moto wa bluu na zambarau kutengeneza radi.
“Hivi bado tunaweza kusema huyu ni binadamu kweli…!”’Majini waliokuwa wakitetemeka kwa hofu wakiwa hawaaini kile wanachokiona waliongea , kilichokuwa mbele yao ilikuwa ni zaidi ya uhalisia wa kiumbe binadamu.
“Kulingana na vitabu vyetu, majini wa enzi hizo walikuwa na uwezo zaidi ya huo, hivyo nguvu hio ni nusu ya nguvu zao”Aliongea Shombeli.
Ubaridi wa maji ya mvua uligonga uso wa Anjiu na aliishia kukunja ngumi tu huku macho yake yakiwa yamejaa husda.
“Andiko la urejesho wa Azimio …hii ni mbinu ya namna gani, kuna siri gani iliopo nyuma yake?”
Anjiu ambaye alikuwa na tamaa kubwa ya kupanda levo mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu iliokuwa ikiongezeka kila sekunde na namna ambavyo Roma analizungusha wingu na kufanya linavyotaka alijikuta akishindwa hata kujua ni hisia gani anazipata.
Roma alikuwa katika levo za juu kabisa na kwa wakati huo hakuwafikiria majini hao kama washindani wake , moyo wake ulikuwa ukiimba wimbo wa; ‘Athena njoo nikushikishe adabu’.
Roma alijiua pengine hisia anazozipata hata Athena alikuwa amezipata kwa muda mrefu sana , pengine Athena hakuwa akiigiza kuwa na ukiburi na ukauzu , vile vitu ambavyo watu wengi walikuwa wakiviona vya thamani kwake havikuwa vya thamani na hisia hizo ndio alizokuwa nazo Roma.
Ni kama vile mtu mzima kutokuvutiwa na midoli ya kuchezea watoto basi ilikuwa ni kama yeye vile kutokuvutiwa na vitu kama vile pesa na madaraka , Roma hakuwa hata na tamaa tena ya kuua viumbe dhaifu tena.
Roma alikuwa na uwelewa na hisia hizo mwanzoni lakini katika nguvu ya namna hio aliweza kufikiria kama vile alivyokuwa akifikiria Athena,
Mabadiliko ya kimtazamo na kiakili ilikuwa ni hatua ya ukuaji kwake ambao ulimpa hali ya kujiamini , Roma sasa alijiambia hawezi tena kuogopa yule mkuu wa umoja wa majini aliekutana nae Dodoma tena.
Mambo mengi alikuwa akiyafikiria katika kichwa chake na alikuwa ameshasahau kuna kundi la majini chini yake ambao linasubiria hukumu yake.
Katika wakati huo Roma sasa alikuwa katika hali ya utulivu kabisa na macho yake hayakuonekana kama yale ya fujo tena kama alvyoweza kuingia katika ulimwengu huo , ilikuwa ni kama vile amebatizwa na kuwa kiumbe kipya.
Roma alikiwa amesimama juu angani alinyanyua mkono wake na kunyoosha kidole upande wa aliposimama Menyu na wenzake.
“Boom!!”
Kitendo cha kunyossha kidole ni kama ishara ya kuruhusu pigo kwani wingu lililokuwa likizunguka juu yake lilishusha radi na kwenda kupiga katika eneo lile alilonyooshea kidole.
Ijapokuwa radi hio haikuwa kubwa kama ya mapigo tisa lakini ilikuwa na nguvu kubwa mno ya kugeuza majini wa nne wa levo ya maji ya kiroho kuwa majivu.
Anjiu na wenzake waliweza kukwepa shambulizi lile lakini ile wanakuja kumgeukia Menyu na baadhi ya majini walikuwa wamebadlika na kuwa moto wa rangi ya bluu na roho zao na nafsi zao ziliunguzwa .
Ijapokuwa walijua hawakuwa saizi ya Roma tena lakini walishangazwa na uwezo wake wa kuua majini wa levo ya kati ya maji kwa pigo moja tu.
BOOM!!
Radi nyingine ilishuka bila hata ya tahadhari , na awamu hio wazee wakuu wa miliki ya Xia walishambuliwa na kuuliwa palepale.
Roma alihisi ni kama vile ameanza kutumia radi miaka mingi iliopita namna ilivyokuwa rahisi kushambulia, moto huo wa mbingu aliweza kuita kama vile akili yake imetawaliwa na mdudu ambaye anawezesha hayo yote.
Gefu na wenzake waliona kabisa hali sio nzuri kwao kabisa na alipanga kuchukua baadhi ya watu wake kukimbia , hata kama angeamua kucheza kamari lakini ni kheri kuishi kwa muda mrefu kidogo kuliko asili yao kufutwa.
“Tawanyikeni , jiokoeni”Aliongea na baadhi ya wazee wa miliki ya Panas mara baada ya kusikia kauli hio walianza kukimbia kuelekea pande tofauti tofauti.
Roma hakuwaangalia kabisa na palepale aliita moto wa mbingu na kisha kunyoosha vidole upande wao na palepale walishukiwa na mashambulizi na kumezwa ndani ya sekunde ikiwemo Gefu mwenyewe.
Majini wote wa miliki ya Panas walipotea na kilichoweza kubakia ni Dhana ya kiuungu ya mkuki peke yake , ilikuwa ni dhana ya kilijendi hivyo haikuharibika kirahisi.
Ikawa Roma amekwisha kuua mkuu wa miliki ya Panas na mkuu wamiliki ya Kekexil.
Katika kifo cha Gefu hakuna jini ambaye alikuwa hata na habari ni wapi Dhana yake ya kiuungu ilipokuwa imedondikea.
Anjiu aliishia kung’ata meno yake na katika hali kama hio aliamua kuita pepo lake la ndani la kijeshi na mwili wake wote ulifunikwa na nguvu ya moto wa ndege wa dhahabu wa miguu mitatu.
“Msikimbie ni vizuri kupigana nae kuliko kushambuliwa wakati wa kukimbia , sidhani kama anao uwezo wa kuhimili uharibifu wake mwenyewe kwa kutuua wengi namna hii’
“Anjiu upo huru kufa mwenyewe , wewe ndio umetuleta katika hali hatarishi namna hii”Umini alitoa alimwangushia lawama kwa hasira , huyu kijana wa miaka mia mbili hatimae alijua kwamba tayari kifo kinamuita.
Kinyume chake Wucheni na Shombeli na wenzake wote walikuwa katika muoenekano wa utulivu kabisa , ni kama wamejiandaa kufa kimya kimya.
Roma aliweza kuoneysha kejeli katika macho yake na wakati kama huo alichopata kuona kati ya majini hao ni Anju peke yake ambaye alikuwa na muonekano wa kishujaa.
Mbele ya israeli mtoa roho Anjiu alikuwa bado akionyesha hali ya kujiamnni , ni kama hakutaka kufa kama muoga bali alitaka kufa kama mwanajeshi.
Pengine hio ndio sababu ya kumfanya Anjiu kuwa maarufu katika ulimwengu wa majini , Roma alijiambia kama sio Anjiu mwenyewe kutaka kumchokoza pengine angeweza kumfanya kuwa rafiki yake kwani kuna vitu vingi wanafanana.
Ni dakika kadhaa wakati Roma akijiandaa kumalizana na Wucheni hatimae aliweza kuhisi nguvu za majini zikisogea katika eneo hilo huku akisikia sauti ikimwita.
“Master Roma naomba usimuue mjomba tafadhari ,, usimuue”
Roma aliweza kuijua sauti hio kutokea mbali , ni kama vile alishawahi kuisikia na kufumba na kufumbua aliweza kuona wanawake wawili pamoja na mwanaume mmoja wakisogea katika eneo hilo.
“Bi Zenzhei!!”
Roma alishangaa mara baada ya kumuona ni Zenzhei , ijapokuwa Zenzhei alikuwa amebadilika na kuwa msichana lakini Roma alikuwa akimtambua kwani alionana nae wakati akiwa anaondoka.
Lakini alishangaa Zenzhei kusema mjomba wake asiuliwe
SEHEMU YA 756.
Roma mara baada ya kumjua Zenzhei alionyesha hali ya kuwa na furaha , ukweli licha ya kwamba alikuwa ni msichana lakini hakujizuia kumuita bibi.
Watu aliokuwa ameambata nao ni Nefi pamoja na Yiyu ambao ni watoto wa Wucheni.
Zenzhei mara baada ya kusikia Roma akimuita Bibi , Zenzhei alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi ya furaha neno bibi lilikuwa na maana kubwa kwake , ilimaanisha Roma alikuwa akimheshimu.
“Master Roma siamini kama kukutana kwetu kutakuwa kwa namna hii , mambo yanaendaje nyumbani Tanzania?”Aliuliza Zenzhei.
“Mambo kwanini yasiwe shwari wakati nipo , nina vitu vizuri kwa ajili ya yule mzee na umri wake kwasasa sio tatizo, usiwe na wasiwasi kabisa”Aliongea Roma akiwa katika tabasamu la furaha kumuona Zenzhei kwa mara nyingine.
“Ndio , nimesahau kama tayari unao uwezo wa kutengeza vidonge”
Baada ya kumuona Zenzhei anamsogelea Roma , Nefi na Yiyu walienda kwa baba yao wakiwa katika hali ya wasiwasi.
“Zenzhei usimsogelee atakuuwa huyo”Wucheni alibweka lakini Zenzhei aligeuza sura yake na kumtingisha kichwa mjomba ake na kisha akamgeukia Roma.
“Mr Roma Zenzhei anajua kwamba Hongmeng wamefanya makosa , nilipofika nilipata kujua ukweli wa mambo menginyuma ya vifo vya wazazi wangu kutoka kwa mjomba Wucheni na nimejua ni maamuzi gani ambayo nilipaswa kufanya muda mrefu juu ya kisasi changu , Mjomba ana makosa ndo lakini bado ana majukumu makubwa , najua nakosa aibu kukuomba hili kulingana tulivyokubaliana lakini naomba unikubalie hili ombi moja , muache aondoke ..nimeweza kusikia kutoka kwa baadhi ya wenzetu waliokimbia hapa kwamba tayari unao uwezo wa kudhibiti radi , hata kama Hongmeng wanatamani kukuchokoza hawatothubutu kwani wanajua unao uwezo mkubwa tayari”
Majini wa Hongmeng wote walikuwa kimya na walikuwa na taarifa ya Zenzhei kuishi katika taifa la Tanzania tokea akiwa mdogo hivyo ni kama ni raia wa Tanzania.
Lakini hawakuwa wakijua kama wakati Roma anaingia katika levo ya nafsi mara baada ya kukamilisha mzunguko wa Andiko la urejesho msaada mkubwa aliupata kutoka kwa Zenzhei.
Kutokana na kujua hayo Shombeli , Umini na wengne walijua pengine kuna tumaini la kubakia hai kwa kumtegemea Zenzhei.
“Acha kumbembeleza , hata kama watoto wangu na mabinti zangu watakufa hawawezi kukupigia magoti , mimi Wucheni ijapokuwa siwezi kujiita shujaa lakini sio mjinga ambae ninaweza kuishi kwa kuchekwa na kuomba kuhurumiwa”Aliongea Wucheni akionyesha hali ya kujisikia vibaya kwa Zenzhei kumuombea msamaha kwa Roma.
“Bi Zenzhei huna haja ya kunibembeleza , kama unataka nimuachie mjomba wao nitamuacha , sitaki kukuona ukinibembeleza”Aliongea Roma akimwangalia Zenzhei ambaye alikuwa na muonekano wa kinyeyekevu.
Majini wote ambao walikuwa hawampendi Roma walishangaa mara baada ya kuona Roma kweli alikuwa akijali maneno ya Zenzhei.
“Usishangae sana , wewe kwangu ni mwanafamilia na umekuwa mkarimu kwangu kwa muda mrefu sana na bado sijalipa yale yote ambayo umeyafanya kwa familia yetu , ijapokuwa mjomba wako alitaka kuniua lakini bila shaka nitamuacha aende lakini hii itakuwa ni mara yake ya mwisho kumpa nafasi nyingine , awamu nyingine akinichokoza ajue kwamba ndio mwisho wa uvumiivu wangu”
“Binadamu ulielaaniwa wewe acha kunibebesha uovu , hata kama nitakufa mimi na uzee wangu huu huwezi kunisingizia vitu ambavyo sijafanya , ni lini nikataka kukuua?”Aliongea Wuchen.
“Kwahio unataka kusema sio wewe uliekuja Australia katika nyika ya Arnhem na kutaka kuniua?”
“Australia!!. , unaongea nini?, Lini nikaja Australia na kutaka kukuua miii?”Aliongea Wucheni akiwa katika hali ya kushangaa.
“Roma! Baba yangu siku zote ni mtu mwema asie tayari kuvunja sheria , kama kweli alitaka kukuua unadhani ungeweza kumshinda wakati huo?”Aliongea Nefi.
“Nilishambuliwa na mtu aliekuwa amevalia Mask ya chuma na kutaka mbinu yangu ya mafunzo , mtu huyo alikuwa na uwezo wa kutumia kinga ya boma la barafu na kuita pepo wa kikaskazini , vipepeo wa kufikirika na mbingu nyingine , mtu huyo uwezo wake wa kijini ulikuwa mkubwa mno , kama sio Wucheni je ni nani kama sio mmoja wenu ndani ya miliki yenu?”
Mara baada ya kuongea kauli hio wazee hao wa Hongmeng walijikuta wakishangaa , ilikuwa haiwezekani Roma kumsingizia mtu kwasababu alikuwa na uwezo wa kumuua mtu yoyote ambae hakuwa akimfurahisha.
Dakika ileile macho yao yote yaliokuwa katika hali ya hasira yalimgeukia Anjiu.
“Anjiu unathubutu vipi kutumia mbinu ya familia yangu kujifanyisha ni mimi katika kufanya uovu wa namna hio , una moyo uliojaa hila, je ulikuwa ukinitafutia matatizo kati ya Roma na miliki yetu?”
“Nini , Anjiu!?, kwanini Anjiu aweze kutumia mbinu yenu?”
“Mr Roma mjomba hajahusika kabisa na kinachoendeea ni kama kilichoitokea familia yangu , kuna baadhi ya majini wa jamii yetu walijua siri ya mbinu yetu ya mafunzo lakini walikufa wote na mpaka sasa aliebakia katika ulimwengu wetu ni Anjiu pekee , alijua mbinu yetu kwa njia ya kumhadaa kimapenzi binamu yangu Yiyu ndio maana mpake leo hii kuna ugomvi mkubwa baina yao”
“Ushachelewa kufahamu hili, vyovyote vile lazima unapaswa kujiona mwenye bahati , nilitumia hii mbinu kwa ajili ya kukugombanisha na Hongmeng lakinni inasikitisha kwamba hukuchukua hatua na badala yake ukaja katika miliki yangu na kuanzisha vurugu, nadhani nilikosea mahesabu yangu”
“Kama ni hivyo wakati nilipokuwa kwenye Dhehebu la Tang , mtu ambaye alikuwa akiwatala kiakili wale wazee jr wewe pia?, je ambaye alijaribu kumtumia Tang luyi kwa kumleta binti wewe pia unahusika?”
“Ndio ni mimi, usisahau ilikuwa rahisi sana mimi kukuua wakati ule na usione inaweza kuwa rahisi kuniua leo hii”
“Kama ni hivyo basi utakuwa unamjua binti wa damu wa Tang Luyi, hivyo sema binti yake yupo wapi?”
Tang Luyi ni Master yake na Magdalena kutokea milima ya Shushan katika ngome ya Tang sasa siku ile Roma alivyoenda katika ile ngome alikuta wazee wote wakiwa katika kutawaliwa kimawazo na kutaka kumshambulia.
“Kwanini nikuambie?”Hali ya muonekano ya Anjiu ilibadilika.
“Haijalishi kama hutaki kujibu, hivyo nitakuuliza tena swali lingine, Je umejuaje nilikuwa nikitumia mbinu ya Andiko la Urejesho , je swala hili linahusiana na mtu ambaye alikuwa akimfukuza Master wangu Tang Chi na kutaka kumuua?”Aliuliza Roma.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa akijiuliza swali la namna hio kwa muda mrefu na kukosa majibu na hio yote ni kukosa mtu wa kumuuliza , hata alivyokutana na Tang Chi kwenye ulimwengu wa majini pepo hakumpa habari juu ya ubini wa adui ambaye alikuwa akimfukuza.
Kitu kingine ni kwamba asilimia ya majini wote ambao wapo katika ulimwengu wa majini watu hawakuwa na uelewa na mbinu hio aliokuwa akitumia , jambo ambalo lilimfahamisha kwamba hawakuwa wakijua mbinu ya andiko la Urejesho ni mara baada ya kukuta karatasi lenye andiko linalofanana na kwake japo majina tofauti.
Hivyo moja kwa moja lazima kuna mtu ambaye aliwaambia majini kwamba Roma anatumia mbinu ya Andiko , mbinu ya kijini ambayo hawaiujui ndio maana miliki zote zilikuwa zikihitaji kupata mbinu hio.
“Kama nikijibu maswali yako je utaniacha hai?”
“Huna jinsi zaidi ya kujibu maswali yangu au ufe , usifikiri pepo lako la ndani linaweza kudili na mimi awamu hii , ninao uwezo wa kukuua na radi kabla hata hajafanya shambulizi”
Anjiu mara baada ya kusikia maneno hayo aling’ata meno kwa hasira na kisha alimwangalia Roma na sura iliokuwa ikicheza cheza kwa hasira.
“Kama ni hivyo basi jibu langu ni kwamba sijui chochote, nasema hivi kwasababu mtu ambaye aliniambia kuhusu mbinu yako alikuwa ni wa ajabu sana haieleweki alikuwa ni mwanamke au mwanaume lakini nilichoweza kukuta ni barua katika meza yangu nyakati za usiku ambayo imeachwa na mtu huyo , sikujua hata kama kuna mtu aliingia katika ofisi yangu , kutokea siku hio huyo mtu alionekana sio wa kawaida hivyo sikumuwazia sana … kuhusu swala la kumfukuza Master wako na kutaka kumuua sijui hata kama una master wa jina hilo , hivyo sina majibu unayotaka na unaweza kuamini unachotaka”
Haikujalisha Roma alisikiaje jibu hilo lakini alihisi ni kama vile ni ujinga lakini kwa kumwangalia Anjiu haikuonekana alikuwa akidanganya
Mara baada ya kuona Roma yupo kwenye mawazo kila mmoja aliona hakuwa na nia tena ya kuendelea kuua na hatimae waliweza kupata ahueni ya kupumua.
Shombeli na Umini waliangaliana na kisha walipeana ishara ya maelewano na kwa haraka sana waliondoka na kundi la majini wa miliki ya Hongmeng.
Roma hakujali hata kuwafukuzia , mpaka wakati huo alikuwa na uwezo wa kuua jini yoyote kwa muda wowote anao taka laikini aliona kabisa kuua majini hao hakuna faida kubwa kwake
Iwe ni kwa kuua sana au kuua kidogo kwake hakukuwa na utofauti wa aina yoyote zaidi ya kujisumbua tu.
“Hakuna siku niliodhalilika kama leo , sijawahi kupitia huu uzoefu , umeniumiza na kisha ukachukua Dhana yangu , nipo tayari kufa nikipigana kuliko kukimbia ninakataa kushindwa lakini mimi Wucheni nachagua kuishi leo hii kwa ajili ya familia yangu .. mimi Wucheni nina deni la uhai kutoka kwako na kwanzia leo hii natangaza Hongmeng haitokuja kuwa na uadui na wewe kama ili mradi nitaendeea kuwa hai”Roma mara baada ya kusikia maneno hayo almwangalia Wucheni na palepale alijikuta akiangua kicheko.
“Sawa mzee , ndio uondoke wakati huu ambao nimekuruhusu na sitaki uchukulie mimi kukuacha hai ni kama deni , kama nilivyosema mwanzo nimekusamehe wewe na watu wako kwa ajili ya Bi Zenzhei , viumbe kama nyie ni swala la mimi kujiuliza kama niwaue au niwaache hai hivyo usijifanyishe kama utakuja kuwa na manufaa kwangu , kwangu muwe maadui msiwe maadui kwangu haibadilishi kitu kwanni mtabakia kuwa viumbe dhaifu mbele yangu”
Maneno yale ya Roma yalitaka kumfanya Wucheni kubadilika na kuonyesha hasira zake lakini mtoto wake Nefi na Yiyu walikuwa na hofu mno ya Roma kuwachukulia hatua.
“Zenzhei alimwangalia Roma na kisha akamwangalia Anjiu lakini kwa jinsi alivyokuwa akimwangalia Roma hakuonyesha aina yoyote ya hofu.
“Mr Roma nadhani sina haja ya kuwa na wasiwasi tena kwa mafanikio yako naamini yule mtu alifanya chaguzi sahihi , kwa mara nyingine niseme asante sana kwa ukarimu wako wa leo”
“Bibi kama upo tayari unaweza kurudi Tanzania na nitahakikisha hakuna anaeweza kukurudisha katika huu uimwengu wakifanya hivyo naua wote”
Zenzhei alifurahishwa na maneno yake , alikuwa na muonekano wa kijana na kwa Roma ni kama vile alikuwa akilinganga nae umri licha ya kwamba alikuwa akimwita bibi na aliishia kutingisha kichwa tu na palepale aliondoka kwa kupotea.
Sasa aliebaki alikuwa ni Anjiu peke yake , sio kwamba hakutaka kuondoka lakini alijua Roma anaweza kuwaacha wote waondoke lakini yeye asimruhusu
“Kusema ukweli sina uhakika kama ulichoongea ni ukweli kwasababu ya hilo najikuta nakuona wa hatari sana , kama unachochote unachotaka kuongea ongea kabla ya kifo chako”
“Nishajua unakwenda kuniua muda mrefu hivyo sogea tupambane , ijapokuwa nafasi yangu ya kushinda ni ndogo lakini siwezi kufa”
Mara baada ya kuongea hivyo aliita pepo lake la ndani na palepale ni kama vile kivuli cha mtu kinamtoka na kusimama mbele yake , kilikuwa ni kivuli kinacholingana kila kitu na yeye na kufumba na kufumbua kivuli kile kilimsogelea Roma kwa kasi.
Roma alikuwa tayari amekwisha kujindaa na aliita chungu cha maaafa na kwenda kugongana na kwa ana na lile pepo.
Lakini kwa nguvu ya Chaos ilivyokuwa kubwa ilikuwa ni mchezo wa kitoto sana kwa pepo wa namna hio kuweza kushindana na chaos kwani palepale mara baada ya kukaribiana na mdomo wa chungu lilipuka. Kama bomu.
Roma aliishia kupiga yowe kwenye moyo wake , ilionekana Anjiu hakuwa na nia ya kutumia pepo hilo kushambulia bali alilitoa kafara na kulitumia kama bomu la moshi.
Pepo la namna hio hata kama lilipuke ilikuwa ni swala la muda tu kwa Anjiu kulirudisha licha ya kwamba inaweza kumgharimu nguvu nyingi za mbingu na ardhi.
Sasa mara baada ya mlipuko ule wa pepo ambao ulitengeneza wingu Anjiu alitumia nafasi hio kukimbia lakini Roma ni kama alitegemea anachotaka kufanya na hakuwa na mpango wa kumuacha akimbie kizemba namna hio.
Uelekeo aliochukua Anjiu ilikuwa ni kuelekea katika miliki ya Xia na ilionekana alikuwa akitaka kuita wasaidizi wake
Ijapokuwa Roma alikuwa na spidi kubwa lakini spidi ya majini haikuwa ya kawaida hawakuwa wakipotea bali walikuwa wakisafiri kwa kasi mno kiasi kwaba wanaonekana kama wanapotea na ndani ya sekunde tu Anjiu alikuwa maili nyingi sana akiwa amemuacha Roma na hio ilimfanya Roma kutokuweza kuita radi kumshambulia tena.
Kilichomshangaza Roma ni uwezo wa Anjiu kukimbia huku akiacha kinga nyuma za barafu kama maboma
Ilimchukua Roma dakika kama tano kuweza kumfikia Anjiu lakini ile anataka kumzuia kwa mbele na kumshambulia na pigo la radi ghafla tu alihisi msisimko wa nguvu za kijini ukiongezeka kwa kuwasogelea na kufumba na kufumbua walitokeza majini waliokuwa katika kundi kutoka katika miliki ya Xia wakiongozwa na msichana mdogo Xiao .
“Mnafanya nini hapa?”Anjiu alikuwa amekasirika mno mara baada ya kumuona binti yake Xiao.
Roma alitaka kutumia ile nafasi kuwashambulia na pigo moja la radi na kuwaua lakini mara baada ya kumuona Xiao alisita.
Msichana huyo nusu jini nusu binadamu alimpa Roma ugumu wa kumshabulia , pengine ni kutokana na kwamba Rufi alikuwa na deni nae na yeye pia alikuwa amemshuku zaidi ya mara mbili.
“Baba wewe unaweza kuondoka , mimi binti yako nitamzuia huyu mtu mbaya”Aliongea Xiao na kisauti chake cha kuumiza masikio na palepale alisogea mbele ya Roma na kumkinga baba yake.
“Wewe mhalifu mkubwa niue sasa kama uwezo huo unao , hujatosheka kunichokoza mara kibao lakini na sasa hivi unataka kumuua baba yangu, dhamiri haikusuti?”
Roma aliguswa na maneno ya Xiao , yalikuwa ni kama vile ni shambulizi la radi , ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kuua majini kwa kufikiria tu lakini alijikuta akiwa mzito sana kumuuiza huyo mrembo.
“Sogea pembeni , Mimi na Rufi tuna deni kwako ndio , lakini kinachotokea hapa ni kati yangu na baba yako , kama nisipomuua leo hii ataniua mimi”
“Unaongea ujinga, kama kweli una deni kwangu kwanini unataka kumua baba yangu , hii ndio namna ya kulipa hilo deni?”
“Hili ni tofauti..”
“Ni tofauti kivipi?”
Anjiu macho yake yaliongezeka ukubwa , palepale aligundua Roma alikuwa akimjali sana binti yake.
Kama ingekuwa ni zamani angemtumia Xiao kama mateka ili kumzuia Roma asimuue lakini tokea siku ambayo alirudi kutoka katika ulimwengu wa kawaida alianza kumchukulia kama binti yake kipenzi.
Siku hio ndio Anjiu aliweza kumjua Roma vizuri , alikuwa ni katili ambaye anao uwezo wa kuua miliki karibia zote hivyo alijua mtu wa aina hio anaweza kumuua hata kama atakubali kutokumuua kwa ajili ya binti yake
Anjiu hakutaka kumuona binti yake akijihatarisha kwa ajii ya kumuokoa.
Kuna vitu nadhani alisahau kuvijua kuhusu Roma , ukweli ni kwamba alijua kama Roma hakuwa akimjali Xiao basi mpaka wakati huo angekuwa ashawaua yeye na binti yake na kuwageuza majivu.
Roma hakuwa bado amefanya maamuzi , alikuwa akiwaza namna ya kutokumdhuru Xiao lakini amuue Anjiu kwani ni tishio kwa usalama wake na watu wake.
Mara baada ya kuona Roma anawaza wale majini wengine walianza kumbembeleza Anjiu kuondoka lakini yeye aliwafaokea kwa kumruhusu Xiao kuja nao.
“Mkuu tulikuwa na wasiwasi juu yako , taarifa za vita imesambaa katika miliki zote za majini , mkuu aliepita bado hajapona tutafanya nini kama na wewe tutakupoteza”
“Baba ondoka , nitamzuia asikudhuru , huyu nanamdai fadhila hivyo siwezi kumruhusu kukudhuru”
Xiao aliacha kumwangalia baba yange na alikuwa akijaribu kumsukuma Roma kurudi nyuma bila ya hofu yoyote , pengine ni hisia zake za kimapenzi ndio zinamfanya kutokumuogopa Roma.
Anjiu alitaka kumzuia Xiao lakini wazo lilimwingia , alijiambia kama ataendelea kumshikilia si nitangia katika mtego wa Roma labda anapanga kumtumia kama mateka ili kunikamata.
Kutokana na mawazo hayo alishindwa kuchukua maamuzi ya kukikimbia.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa hata na mpango wa kumtega Anjiu,alikuwa na uwezo wa kutokumdhuru Xiao na kisha kumuua Anjiu lakini matendo ya Xiao yalimfanya kutokuchukua hatua yoyote.
Xiao alienda mbali na kumshikilia Roma kiuno kwa kupitisha mikono kwa mbele ili kumzuia asisogee , vitendo hivyo vilimfanya Roma kushangaa na kuishia kucheka kwani vilikuwa vya kitoto sana
Licha ya kwamba uwezo wake ulishafikia levo ya nafsi lakini bado matendo yake yalikuwa kama ya msichana mdogo.
Upande wa Anjiu alikuwa na wasiwasi mno kwa kuogopa Roma kumuua binti yake.
“Baba kimbia basi”
Aliongea Xiao akiamini kwa namna alimvyomshikilia Roma hawezi kuchoropoka.
“Haka kajinga kanadhani Roma hawezi kuniua kwa kufanya vile”Aliwaza Anjiu.
Roma palepae alitoa tabasamu la kifedhuli na alimgeuza Xiao kama karatasi na kumshikilia na kwapa la mkono na kabla hata hajaleta ukinzani alikuwa tayari ashamzimisha.
Roma mpango wake ulikuwa ni mwepesi , alijua kama ataondoka na kurudi nae anaweza kumjua vizuri Xiao ni nani na kama ni mtoto wa Tang Luyi angempeleka kwa mama yake lakini pia asingekuwa na wasiwasi kuivamia Xia na kuisambaratisha.
Anjiu hakuweza kumuokoa binti yake na aliamua kukimbia huku akiamini Roma hawezi kumdhuru.
Upande wa Roma alikuwa mzito mno kumuacha Anjiu akimbie na alijaribu kumshambulia kwa kumrushia shoti za radi na mkono mmoja lakini kwasababu alikuwa amembeba Xiao alishindwa kubomoa ngao yake ya kijini ya barafu.
Roma aliweza kukiri ngao ya barafu ya pepo wa kaskazini ilikuwa sio ya kawaida kabisa , ilikuwa na nguvu mno kwani iliweza kumsaidia Anjiu kutoroka.
Lakini licha ya kwamba Roma hakuweza kumpata Anjiu na shambulizi lake lakini wale majini waliofika hapo waliweza kupatwa na mashambulizi hayo na kupoteza maisha.
Roma hakutaka kumwangalia tu akipotea katika macho ake na aliamua kumfukuzia kwa nyuma kwa kasi kubwa huku akiwa bado amembeba Xiao.
Anjiu alichukua uelekeo wa Kaskazini mashariki na alikuwa na spidi ya kasi mno lakini Roma licha ya kumfukuzia kwa kasi hakuwa na wasiwasi wa kumpata.
Roma alijiambbia hata kama asipomkata Anjiu miliki yake anaifahamu hivyo angeenda Xia na kuilipua na aone kama hatojitokeza.
Wakati Roma akiwa nyuma anaendelea kumfukuzia Anjiu alihisi kitu kisichokuwa cha kawaida kimeamka , ilikuwa ni kama vile kuna kitu kinataka kumtoka katika mwili wake , Roma mara baada ya kujichunguza alikuja kugundua ni kitu ambacho kilikuwa ndani ya hifadhi yake ya pete na jambo lile lilimshangaza sana.
Kabla hata hajagundua ni kitu gani hicho baada ya kufungua hifadhi hio kivuli cheusi kilitoka kwa kasi na kumvaa , kivuli hicho kilikuwa na nguvu ya giza , na kimejaa roho ya ukichaa , kifo na baadhi ya hisia hasi ambazo hazikuwa zikielezeka.
“Ni ile Hazina ya majini pepo!!!”
Roma alishangaa mno kwani ilikuwa ndio mara ya kwanza hazina hio ikawa hai na kutoka katika hifadhi bila ya ridhaa yake.
Kubwa zaidi ni kwamba hajawahi kujua kazi ya hazina hio ni nini na tokea mwanzo hakuweza kuhisi kama ilikuwa na nguvu zozote zile.
“Kwanini ghafla tu imeamua kuzalisha nguvu ya ajabu ya namna hii ya giza?”
Roma alijiuliza na kabla hata hajapata majibu kivuli kile kilichokuwa kimemzingita kiligeuka na kuwa kama vile ni kizingia au kimbunga na kuanza kumzunguka kwa kasi mno huku kikielekea juu angani zaidi na zaidi huku ncha yake juu kabisa kukiwa na ile hazina nyeusi.
Msuguano wa nisahti za mbingu na ardhi na nishati za hazina ile ziliongezeka kwa kiasi kikubwa na kuanza kumsukuma Roma kwenda juu angani , ilikuwa ni kama vile alikuwa amefungwa kamba kiunoni na kulazimishwa kwenda juu kwa kuvutwa.
Nguvu ilikuwa ni kubwa mno na Roma hakuweza kujinasua kwa kadri alivyokuwa akijitahidi , alijaribu kutumia chungu cha maafa kuweza kumeza nguvu inayotokaana ile hazina lakini alishindwa kabisa , alijaribu uwezo wake wote wa nguvu za kijini katika levo ya radi lakini pia ilishindikana na alijikuta akitoa macho.
“Hii nguvu ya hazina mbona kama inanyonya nguvu zangu?”
Roma aligeuza macho yake juu angani na palepale aliona katika anga ni kama vile kuna shimo kubwa jeusi ambalo anga yake ilikuwa ikichemka kana kwamba ni mafuta meusi yanayochemswa na moto mkali.
Roma kutokana na uwezo wake wa kuelewa kanuni za anga aligundua kilichokuwa juu yake ni Lango(Portal) la shimo ambalo ndio lilikuwa likimvuta.
Ilikuwa ni ndani ya sekunde tu ilikuwa ni kama alivyowaza kwani akiwa amemshikilia Xiao aliweza kutumbukia katika lile shimo refu na hakujua hata kinachomtokea ni kitu gani , kila kitu kwake kilikuwa cha maajabu.
Roma alijiuliza au pengne Hazina hio haikuwa na uwezo wa kuzalisha nguvu yoyote bali kazi yake ilikuwa ni kuamsha malango ya anga.
Kilichokuwa kimemtokea ni kama vile alivyovutwa na mnara na kupelekwa katika ulimwengu wa majini pepo na ndio kitu cha namna hio hio ndio kilichokuwa kikimtokea tofauti tu ni kwamba alijihisi ni kama vile anatumbukia kwenye shimo lefu la giza huku akishindwa kujizuia.
Roma mara baada ya kutumbukia mzima mzima katika shimo hilo ndio sasa anakumbuka kwenye mikono yake alikuwa memshikilia Xiao.
“Ni kitu gani hichi kinanitokea , kwanini nina bahati mbaya namna hii , au majini pepo waliniwekea mtego , au hii hazina yao ilikuwa ni ufunguo wa kuteleport kwenda ulimwengu mwingine , kama ningejua ningerudisha hazina yao mara moja”
Roma alianza kujilaumu wakati akiwa ndani ya giza totoro asijue ni wapi anaelekea , alichokuwa akijua tu ni kwamba nguvu inayomvuta ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi kufanya lolote.
Anjiu ambaye alikuwa akikimbia kwa kasi kuokoa maisha yake hakujua ni kipi ambacho kinamtokea Roma na mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu alijiuliza au kuna mbinu nyingine Roma anajaribu kufanya ili kumuua.
Kitendo cha kugeuka nyuma aliona kitu kama duara nyeusi ambalo linapungua ukubwa kwa namna ya kusinyaa na ilikuwa ni kwa haraka sana kidoti kile cheusi kilipotea na hakuhisi tena msisimko wa nguvu za Roma wala za binti yake Xiao.
Ilikuwa ni kama vile Roma na Xiao walikuwa wamepotea katika anga jembamba , aliishia kukunja ndita na alirudi kwa kasi nyuma na kujaribu kumtafuta Roma , alijaribu kutumia nguvu zake za kijini za utambuzi ili kumuona binti yake lakini hakukuwa na dalili yoyote.
Roma kapotelea wapi au ndio mpango wa Athena kumpoteza Roma kukamilisha mambo yake.
Hatima ya Lekcha na Aoiline ni nini.
[emoji1635]NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.
MTUNZI: SINGANOJR.
Mono no aware
SEHEMU YA 728.
Tabasamu la uovu ambalo alikuwa akionyesha ‘Roma’ liliwafanya wale majini kujihisi ubaridi usiokuwa wa kawaida.
“Uwezo wake sio wa kawaida”Aliongea Jini Anjiu kwa hamaki mara baada ya kuona Roma amebadilika.
Senjii na Sena wote walionyesha nyuso za wasiwasi na kweli waliweza kuona uwezo wa Roma ulikuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na dakika kadhaa zilizopita.
Ijapokuwa hawakuweza kukadiria uwezo wake ulikuwa mkubwa kiasi gani lakini mkandamizo wa nguvu za kijini aliokuwa akitoa ulikuwa ni wa levo nyingine kabisa kuliko mwanzo.
Chaos hakutaka kujisumbua kabisa na namna majini hao walivuokuwa wakimwangalia badala yake alionyesha furaha kwa namna ya kupumua kwa nguvu.
“Tamuuu…. Pumzi yenu inatamanisha sana”Chaos aliekuwa katika sura ya Roma aliongea na kumfanya Senji kuzidi kuwa na wasiwasi.
“Anajaribu kututania huyu… msiwe na wasiwasi , lazima atakuwa ametumia mbinu ya hadaa kujaribu kutuaminisha uwezo wake umeongezeka , hakuna jini au binadamu mwenye uwezo wa kupandisha uwezo wake ndani ya dakika kadhaa tu”
“Upo sahihi hakuna kumuachia aondoke hapa”Aliunga mkono Senji na palepale alitoa Dhana yake ya alama ya kiganja cha mkono na kurushia hewani na palepale maandishi ya njano yaliweza kuonekana.
“Mkondo nyota , kupasuka kwa anga!!”.
Ndani sekunde tu kulikuwa na wingu kubwa la nguvu za mbingu na ardhi ambazo zilikuwa zimejikusanya juu ya Chaos na ziliongezeka na kutengeneza nguzo kubwa ya kinishati ni shambulizi ambalo lilitolewa na Senji.
“Boom!!!”
Nguzo ile kubwa ya kinishati ilidondoka kutoka juu kwenda chini na kusambaza mionzi ambayo ilisambaa karibia eneo lote la chini yake , ilikuwa ni kama vile anga linaharibika.
Lakini hata hivyo Chaos hakuonyesha kujali kabisa na shambulizi hilo na aliruhusu kushambuliwa na palepale aligeuza nguvu zote hizo na kuzisharabu kwa kuzigeuza nishati za mbingu na ardhi.
Katika spidi ya kupepesa macho mashambulizi hayo yalionekana kuwa ya kawaida mbele ya Chaos.
Takribaki miaka elfu nne iliopita majini wa enzi hizo waliweza kumiliki nguvu ya Radi , ni sanaa ambayo waliweza kuistadi kwa kuweza kuvuna nishati za mbingu na ardhi lakini licha ya hivyo iliwachukua miaka kumi katika kumfungia Chaos katika gereza la Cauldron.
Kitendo cha Chaos kuweza kumiliki mwili wa Roma alihamisha nguvu zote ambazo zilikuwa kwenye Cauldron na kuziingiza katika mwili wa Roma ndio maana alionekana kuwa na uwezo wa juu sana tofauti na mwanzo.
Kwasababu Chaos alikuwa tayari ashamiliki mwili huo hakutaka kuficha uhusika wake kamili na iliamua kufanya mashambulizi kwa kasi kubwa.
Siku zote Chaos alitaka kupata mwili wenye nguvu ambao utamuwezesha kurudisha utukufu wake kuliko kuendelea kukaa katika gereza la chungu.
Yaani njia pekee ya Chaos kuweza kutoka katika gereza ni kuweza kuvamia mwili wa Roma
“Hayo ndio mashambulizi yenu , nyie majini hamna kitu kizuri zaidi cha kunipiga nacho tofauti na hii mitekenyo yenu?”Chaos alitoa tabasamu la kejeli na baada ya kauli yake hio ilimrushia Rufi ndani ya kile chungu ili kuendelea kumpatia ulinzi.
Rufi alishajua mtu ambaye yupo mbele yake sio Roma bali ni Chaos na Roho ya Roma ilikuwa imefungiwa , alikuwa kwenye hali ya wasiwasi lakini alishindwa kutoa hata sauti kutokana na hali ya woga aliokuwa nao.
Anjiu alionekana kufikria jambo na kugundua kitu na palepale akapaza sauti kubwa.
“Wewe sio Roma Ramoni , wewe ni mnyama wa kishetani wa machafuko , The Chaos!”
“Nini?”Kauli ya Anjiu ilishitua wale wengine lakini Chaos alitoa cheko kubwa la kishetani.
“Haijalishi mimi ni nani , muhimu ni kwamba nyie wote mnakwenda kuwa chakula changu”
“Unajiona ni nani wakati ndio mwisho wako leo ,Ewe Joka sanaa ya wino tokaa… Hasira ya Joka kuu!!”Aliongea Sena kwa nguvu na hakuonyesha kuogopa kabisa.
Dakika ileile wino ulifyatuka kutoka kwenye mwili wake na kutengeneza kizingia ambacho ndani ya dakika tu kilibadilika na kuwa Joka kubwa mno ambalo lina meno marefu na kuanza kushambuliana na Chaos.
Chaos hakuweza kukwepa shambulizi lake na alikutana nalo ana kwa ana lakini kabla hajaguswa palepale ule wino uliyeyuka na kugeuzwa nishati ya mbingu na ardhi na ukamezwa palepale , shambulizi hilo linaweza kuonekana la kimaajabu lakini mbele ya Chaos lilikuwa ni la kitoto sana.
“Bi Sena kuwa makini”Anjiu aliongea kwa nguvu lakini alionekana kuchelewa kumtahadharisha.
Chaos tayari alikuwa akimsogelea Bi Sena kwa spidi na Sena alionekana hakutegemea Chaos angeweza kumsogelea kwa kasi na muda huo kitu pekee alichokumbuka kutoa kama siraha yake ni Dhana ya Kilio cha pepo.
“Cling , Clng , Cling!!!”
Dhana ya kawaida kama hio mbele ya macho ya Chaos ilikuwa ni kama kijiti na ilivunjwa vunjwa palepale.
“Arghhhh…!!!”
Sena aliishia kutoa kilio kikali mno ambacho kilisambaa na kutengeneza mwangwi mara baada ya kukamatwa na Chaos na kupigwa kibao cha kichwani.
Kichwa cha Bi Sena kilipasuliwa palepale kama vile ni tikiti lililopigwa na nyundo na damu zilifyatuka kama vile ni Fountain.
Tabasamu la Chaos lilikuwa la ukichaa kabisa mara baada ya shambulizi hilo lakini kwa majini wengine walaikuwa katika hali ya mshituko kwa kile ambacho kimetokea.
Roma ambaye sasa ndio Chaos mwenyewe mara baada ya kumpasua Sena kichwa chake ilichomoa mishipa mikubwa ya damu iliokuwa shingoni na kuanza kuinyonya damu yake kwa starehe zote kama vile alikuwa na kiu ya damu ya muda mrefu sana.
Baada ya damu kukauka ilirarua mwili wake palepale na kisha kuanza kutafuna nyama yake , ijapokuwa kwa nje alikuwa akionekana kama Roma lakini matendo aliokuwa akiyafanya ni ya kimnyama kabisa hasa wakati alivyokuwa akitafuna nyama ya jini Sena.
“Arghhhh…!!!”
Rufi alishindwa kuvumilia na kuishia kutoa kilio mara baada ya kuona mpenzi wake akitafuna nyama mbichi , ijapokuwa alikuwa akijua anaemwangalia sio Roma ni Chaos lakini bado hakuamini macho yake.
Majini wengine wa miliki hio ambao walikuwa kwa mbali waliishia kushikwa na bumbuazi huku miguu yao ikilainika na nyuso zao kupauka, hawakuelewa ni kwa namna gani meza imegeuzwa.
Jini ambaye alikuwa amefikia mwishoni mwa levo ya maji ya kiroho alikuwa ameuliwa kwa kuraruliwa namna hio na mtu kama mnyama ambaye yupo katika sura ya Roma.
Machafuko aliangalia juu mara baada ya kumaliza kutafuna na sura yake yote ilikuwa imefunikwa na damu na vipande pande vya nyama , ilikuwa ni kama vile imeibukia kutoka kwenye dimbwi la damu , ijapokuwa alikuwa amefunikwa na damu mwili mzima lakini alikuwa akitoa tabasamu kama vile alikuwa akiufurahia muonekano wake.
“Utamu ambao nilikuwa nikiuota mara kwa mara hatamae nimeweza kuuonja katika uhalisia .. Daah …!!”Aliongea huku akilamba midomo.
Kama kuna yoyote ambaye angeweza kusikia kauli yake , na kuona tukio hilo na pia kama usingeweza kuamini maneno ya Anjiu alioongea basi hakika mtu huyo angesema Roma ni kichaa tena zaidi ya neno lenyewe la ukichaa.
Machafuko au Maafa ndio jina lake halisi , alikuwa ni mnyama aliepewa jina hilo kutokana na matendo yake, alikuwa ni mnyama wa Ghasia, mnyama wa kigaidi ambaye wakati huo alikuwa akimiliki mwili wa Roma na kuonyesha uhalisia wake.
Dakika chache zilizopita walikuwa wana uhakika wa kumshinda Roma lakini sasa hivi mashambulizi yao yalikuwa ni kama vile wanarusha mayai kwenye jiwe na hatimae wanakuja kuelewa sababu ni nini.
“Kimbieni , Kimbieini wote katika uelekeo tofauti tofauti!!”
Anjiu mara baada ya kuona hali sio hali palepale aliona sulushisho ni kukimbia kwa majini hao katika kila pande , maana aliona hakuna namna wanaweza kushinda pambano hilo mbele ya Machafuko kwa tukio lile la kuweza kumuua Sena kwa shambulizi moja tu.
Anjiu hata yeye hakutaka kubakia tena katika eno hilo na alitimua nduki kuelekea upande wa kusini magharibi, wakati huo akipaza sauti kuwaamrisha majini wengine kukimbia bila kufuatana.
Uelekeo ambao alichukua nni kuelekea upande wa miliki ya Panas , Anjiu alijiua kama Chaos ataamua kumfukuzia basi ni vizuri kuelekea upande ambao kuna wajuzi wa mbinu za kijini za juu ili kuweza kusaidiana katika kumdhibiti.
Lakini sasa wakati Anjiu yeye akifanikiwa kushituka kwa dakika na kuanza kutimua jini ambaye alifika hapo pamoja na Senji yeye alichelewa kidogo licha ya kwamba alijua kabisa hana uwezo wa kushinda na alipaswa kukimbia hata kabla ya kauli ya Anjiu.
Kitendo cha Anjiu kutoa agizo la majini kukimbia, Machafuko alionekana kukasirika sana na kujiambia hawa kunguni wanathubutu vipi kukimbia , haileti tofauti yoyote kwani tayari yupo katika mwili wa Roma hivyo ingekuwa ni swala la muda tu kuwararua wote na kuwatafuna.
Lakini sasa kitendo cha majini hao kukimbia katika uelekeo tofauti ilimuia vigumu kuwakamata wote kwa wakati mmoja na alibakiwa na chaguo moja tu la kuchagua upande wa kufukuzia na hapo ndio iliona jini mzee ambaye yupo katikati mwa levo ya maji ya kiroho ambaye alizubaa.
“Arghh…!!!, tafadhari usinitafunee”
Jini yule mzee mara baada ya kuona Machafuko amemuungia spidi alipiga makelele huku akiwa na wasiwasi namna ambavyo anakwenda kuraruriwa , hakuamini miaka yake mia moja aliotumia kuvuna nishati za mbingu na ardhi itaishia katika mdomo wa Chaos.
Licha ya kujitahidi kukimbia huku akipiga yowe Chaos alikuwa na spidi kuliko yeye na ndani ya dakika tu alishikiliwa mkono na kuvutwa kwa nguvu na kukamatwa shingo ambayo ilivunjwa palepale na kuanza kunyonya damu na nishari yake yote ya mbingu na ardhi na kisha kugeuzwa majivu.
Majini wote wa miliki ya Xia walikuwa wametoweka katika makao hayo kwa kukimbia pande tofauti tofauti na Chaos hakutaka kujisumbua kuwafukuzia.
Chaos aliona hana haja ya kujisumbua ili hali ana uelewa juu ya Roma alichoona mara baada ya kufika katika miliki ya Kekexil , kama ni kutaka kwenda kuendelea kujipatia vitoweo basi tofauti na kufukuzia majini waliosambaa itakuwa vizuri kuelekea Kekexil kula nyama ya majini na baada ya hapo angeenda na Hongmeng na kisha Panas kumalizia na hatimae utukufu wake ungeonekana.
Kutokana na Chaos kuwa mnyama ambaye hana mwisho , mnyama ambaye hafi na wa kishetani uwezo wake wa kiakili ulikuwa mkubwa mno lakini licha ya hivyo kitu kimoja ambacho hakuwa na uwezo wa kujizuia ni tamaa ya kunyonya kila aina ya nguvu ambayo ipo katika ulimwengu huo na kisha kuhamia katika ulimwengu wa kawaida na kula kila kiumbe kinachovuta pumzi.
Ilikuwa ni kwasababu hio hio ya tamaa ya mnyama huyo ndio maana aliishia kwenye mtego wa chungu na kufungiwa kwani kama sio hivyo angeweza kufuta jamii ya kibinadamu na majini mara moja.
Hayakuwa maamuzi ya mnyama huyo bali ilikuwa ni hatima yake , ni swala ambalo ili kuendelea kuishi asingeweza kuepuka kufanya hivyo.
“Mh wapo vizuri kwenye mikimbio…”Aliongea huku akimalizia utamu wa mwisho mwisho wa nyama mbichi na mara baada ya kukamilisha iligeuza macho yake kwa Rufi ambaye alikuwa amemhifadhi kwenye chungu.
Rufi mara baada ya kukutanisha macho na Chaos alihisi kutetemeka kusikokuwa kwa kawaida.
“Umemfanyia nini mume wangu?”Aliongea Rufi kwa kujikaza.
“Bado tu unapata ujasiri wa kuniongelesha wewe msichana… mwanaume wako tayari hayupo hapa na kuanzia leo na kuendelea huu mwili ni mali yangu na si vinginevyo”
“Wewe ni muongo , mpenzi wangu hawezi kukupatia mwili wake kirahisi hivyo”Aliongea Rufi huku machozi mengi yakimtoka akiwa na tumaini hafifu kwenye moyo wake na kujiambia Roma ataweza kuishinda nafsi hio.
“Hahahaha…. Hahahaha.. sina muda wa kupoteza na binadamu usie na thamani kama wewe.. Roma alileta ujuaji na kuniambia oh eti nilindie mpenzi wangu mpuuzi yule , nilimkubalia ndio lakini haikuwa nia yangu ya dhati kukulinda, nilitaka akubaliane na matakwa yangu tu, ili kurudisha uwezo wangu katika viwango ninatakiwa kuendelea kunywa damu ya
majini na sina muda wa kujibishana na binadamu mimi”
Chaos muda huo alikuwa akiendeshwa na roho ya kisasi kwa kile majini walichomfanyia mpaka kumfukia katika chungu na alitaka kulipa kisasi kwa kuwatafuna.
“Roma anadharau sana ameshiindwaje kuniheshimu wakati nilipokuwa dhaifu na kunifanya mbwa wake, sasa ili kulipiza machungu ya kunidharau nitaanza na wewe mwanamke wake na baada ya hapo nikimalizana na kunywa damu ya majini nitaenda kisiwani kwake na kula wengine ili kutuliza chuki yangu, lakini kwasasa ninachotamani ni kuona wewe mrembo ukiomba huruma yangu hahahaha… nitakusamehe kama utanifurahisha pengine unaweza kuwa mpenzi wangu”
“Wewe ni mnyama tu unaesikitisha na kutia huruma na utabakia kuwa hivyo , niue kama unataka unafikiri nitaomba uniache hai , mwanamke dhaifu kama mimi bado tu pia ninao uwezo wa kukudharau”Aliongea Rufi kwa hasira na kumfanya
Chaos kutoa tabasamu la kifedhuli na hasira kuongezeka maradufu huku macho yake yakizidi kuwaka taa nyekundu.
“Kwasababu unaleta ujeuri mbele yangu nitararua mwili wako vipande vipande na kukutafuna , sipati picha Roma atakavyojiskia mara baada ya kujua amemtafuna mpenzi wake”
Baada ya kumaliza kauli hio Chaos alimsogelea Rufi kwa spidi kwa kulenga kifua chake akidhamiria kunyofoa moyo wake nje.
Lakini kadri alivyokuwa akijitahidi kunyoosha mkono wake kumfikia Rufi alishindwa kabisa kumfikia na aliishia kufurukuta na kutetemeka kaa vile anaishiwa na nguvu.
“Nini… imewezakenaje… pumbavu.. noo!!”
Chaos alijikuta akizidi kupagawa huku mwili wake ukitetemeka , kiini cha macho yake ambacho kilikuwa ni cha rangi nyekundu kilianza kufifia na nguvu yake ya giza ilianza kupungua pia.
Rufi ambaye alikuwa amefumba macho yake na
masikio yake akiwa tayari kufa ghafla tu alihisi jambo ambalo halikuwa la kawaida na kujikuta akiingiwa na tumaini na wasiwasi kwa wakati mmoja.
Wakati huo kulikuwa na vita kali vya kifahamu kati ya Chaos na Roma, ufahamu wa Roma ulikuwa ni kama unaibukia ulikolala na kumfaya Chaos kuzidi kupambana lakini alionekana kushindwa vita.
“Wewe mwanaharamu nilijua tu huwezi kutii ahadi yako ulidanganya kwa kuniahidi kulinda wanawake wangu , lakini je unaona mimi ni mtoto mdogo mpaka kukuamini sio?”
Fahamu mbili zilikuwa zikishindana Roma alikuwa akiongea akionekana alikuwa na ngauvu zaidi ya fahamu ya Chaos.
“Huu uwezo wako umetokana na kuimarika kwa uungu wako!!?”Chaos hatimae alielewa nini kinacheondela , alichokuwa akipambana nacho sio
Roma bali ni uungu wa Hades ambao Roma aliurithi.
Lakini sasa kwa namna isioelezeka uungu huo ulionekana kuimarika sana kuliko ilivyokuwa mwanzo na hakutarajia hilo wala kugundua.
Roma alitoa tabasamu huku macho yake yakionyesha hali ya msisimko kuendelza vita hivyo ya kifahamu.
“Unaonaje, nadhani hukutegemea nilikuwa na mpango wangu kichwani , ijapokuwa umeweza kurejesha sehemu ya uwezo wako lakini Caulrdon imefungia kiini cha nafsi yako ndio maana unao uwezo wa kutumia mwili wangu lakini Roho yako halisi ya ndani kama sikosei haina nguvu ya kutosha kumeza nafsi yangu vinginevyo ungekuwa ushannimeza muda mrefu na usingeanza kunibembeleza bembeleza kukuruhusu kutumia mwili wangu”
Kauli hio ilifanya nafsi ya Roho ya Chaos kuchanganyikiwa na kuwa na hasira kwa wakati mmoja , ilikuwa ni kweli roho yake ilikuwa imefungiwa katika Cauldron na hakuna njia rahisi ya kutoka huko kutokana na vizuizi.
Kutokana na athari ya Chungu ilikuwa pia ni ngumu kupata uwezo wake wote na kukimbia au kujitoa na kitu pekee kupata nguvu zake ni kujiambatanisha katika nafsi ya Roma.
Kama nafsi yake halisi ilikuwa na nguvu zake za kutosha roho hio ingekuwa ishammeza Roma muda tu tena bila hata ya kumbembeleza mbeleza.
Sasa muda huo mara baada ya kuona Roma yupo kwenye majanga iliona hio ndio nafasi adhimu ya kumfanya Roma kumwachia mwili wake kihalali na kujikusanyia nguvu kwa haraka na kuizima Roho ya Roma moja kwa moja kumbe alikuwa akitegwa.
Nafsi hio iliamini haijalishi uwezo wa Roma upoje ili mradi Roma atatoa mwili wake kwa hiari yake hatokuwa na uwezo wa kulera ukinzani katika kurudisha nafsi yake , sasa yote hayo yalikuwa ni makisio tu na ilionekana mpango wake haukwenda kama alivyokuwa amepanga kutokana na kutokutegemea uwezo wa akili wa Roma ugekuwa na nguvu kubwa namna hio.
“Imekuwaje , imekuwaje utimamu wako wa akili ukaongezeka kiasi hicho?”Roho Chaos aliongea.
“Kitu pekee ambacho unaweza kuona katika akili yangu ni tabia yangu lakini huwezi kujua mawazo yangu ya ndani , siku chache zilizopita tokea kuanza kwa kufufuka kwa moyo wa Gaia uwezo wangu wa kiuungu wa akili umeongezeka kwa kiasi kikubwa mno , haikuwa kwangu tu hata kwa miungu uwezo wao wa akili pia ulikuwa ukiimarika , usingeweza kujua hili kwasababu mimi situmii kanuni za anga mara kwa mara hivyo ulishindwa kujua kama uwezo wangu wa akili umeongezeka au lah , kitendo cha kuanza kufufuliwa kwa moyo wa Gaia nafsi yangu iliimarika licha ya kwamba uwezo wangu wa
nishati za mbingu na ardhi ulibakia vilevile , hivi unadhani utimamu wangu wa akili unaweza kulingana na huo wa kwako dhaifu , ki ufupi ni kwamba nishakupita muda mrefu na hakuna namna unaweza kunifikia na ukatawala akili yangu labda nikuruhusu”
Maneno ya Roma yalishusha hali ya majigambo ya roho ya Chaos , haijalishi roho hio ilijitahidi vipi lakini haikuweza kufanikiwa hata kutingisha ufahamu wa Roma.
Ki ufupi ni kwamba Chaos aliingia kwenye mtego wa Roma kwa kuamini Roma wa kule Korea aliemeza moyo wa Kibudha ni huyo huyo mara baada ya moyo wa Gaia kuanza kufufuka.
“Hapana , siwezi kupoteza kwako kizembe hivi , hii sio sawa,, arghhh..”
Chaos alijikuta akipambana lakini ilikuwa haina maana tena kwasababu ufufuo wa Moyo wa Gaia ulikuwa ukiimarisha nafsi za miungu hii ni kwasabau nafsi zao zimeungana na Gaia.
Mpango wa Athena ulikuwa ni kufufua ndugu zake ambao nafsi zao zilimezwa na binadamu hivyo njia pekee ya kufanikisha hilo ni kufanya moyo wa Gaia kuwa na nguvu zaidi ambayo itawezesha zile Roho ambazo zilimezwa kuamka, sasa kwasababu na Roma alikuwa na uungu ndani yake moja kwa moja ni kwamba anakuwa na Koneksheni na moyo wa Gaia hivyo kadri moyo huo unavyofufuka ndio ambavyo uwezo wake wa akili pia huimarika.
“Nilishakuambia kwangu wewe huna tofauti na mbwa tu , unatoa wapi ujasiri wa kutaka kummiliki anaekufuga , nina madaraka kamili zidi yako na kitendo chako cha kuonyesha uwezo ambao ulikuwa umeficha muda si mrefu nitaweza kutawala Radi kama siraha , kama unataka kuendelea kula keki yangu basi hakikisha unaendelea kuwa mbwa mtiifu” “Binadamu fisadi sana wewe… hapana.. kafiri wewe”
Nguvu ya Chaos katika fahamu za Roma iliendelea kufifia na mwishowe ikapotea kabisa katika ufahamu wake na kurudi katika Cauldron.
SEHEMU YA 729.
Sasa mara baada ya Roma kuweza kumiliki mwili wake kikamilifu kwa kumfukuza Chaos katika ufahamu wake na kwenda kwenye Chungu macho yake yalirudi katika muonekano wa kawaida , ukiachana na damu ambazo zilikuwa zimemchafua lakini kila kitu kilikuwa sawa.
Kitendo cha Chaos kutumia mwili wa Roma ilimfanya kutoa uwezo wake wa kijini ambao alikuwa ameficha na hilo lilikuwa kosa kwake kwani Roma aliweza kumiliki uwezo huo , ukijumlisha na mapigo matatu ya awamu za radi alijihisi kujiamini maradufu zaidi na kuamini anao uwezo wa kuwashinda Anjiu na wengine.
Baada ya kumtoa Rufi kwenye Chungu na kumkumbaita palepale Roma alikificha, ki ufupi ni kwamba Roho ya mnyama huyo milele itakuwa chini ya Roma na kuwa kama mbwa tu wa kumsaidia kushambulia maadui.
Roma mara sasa baada ya kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha hatimae aligeuza macho yake na kumwangalia Rufi na kutoa tabasamu.
“Rufi wewe kilaza unalia nini sasa hebu kaone ? Si nipo sawa?”Aliongea Roma mara baada ya Rufi kuanza kulia kilio cha Kwikwi kama kafiwa vile.
“Hubby…nili ,,,nilijua umesha..”Mwili ulimsisimka kila akikumbuka tukio ambalo limetokea dakika kadha zilizopita.
“Nilikuambia pale kwamba ninabetia uwezo wa Cauldron na sio kwamba nilisema ninakipa mwili wangu , inamaana hukuniamini na ulijua nitamezwa?”
“Mimi ningejua vipi unachomaanisha … hukuniambia nikaelewa”
“Kaone sasa kalivyo kajinga … kama ningekuambia kila ninachowaza Chaos angenishtukia na mpango ungefeli”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kutoa kicheko kilichoambatana na aibu.
“Roho ya Chaos imeingia cha kike , Babe wewe ni mjanja sana unajua”
“Hehe sikuwa na jinsi muda ule , hawa majini walikuwa wamenipania si mchezo na kabla ya kuanza pambano nilijua ninaweza kuingia katika hatari hivyo niliiandaa ‘ escape plan’ mapema … nimefaidika sana hata hivyo kwasasa uwezo wangu umeongezeka maradufu na ninaweza kuwaua muda wowote nitakaotaka”Aliongea Roma huku akikumbuka Lahani na baba yake walivyotoroka lakini hata hivyo alikuwa ashaua majini zaidi ya wa nne wa levo za maji ya kiroho katika miliki hio.
Kama utafananisha na hasara waliopata kati ya Kekexil na Xia basi miliki ya Xia imepoteza zaidi majini wenye nguvu kuliko ilivyokuwa kwa Kekexil ambao walipoteza kwa kiasi kikubwa madawa hivyo hasara ni ya kawadai kwani ni rahisi kutafuta madawa na vidonge kuliko kupandisha uwezo wa kijini.
Rufi sasa alipatwa na msisimko na furaha mara baada ya kutoka katika hali ya hatari.
“Hubby kwahio muda si mrefu utakuwa na uwezo wa kudhibiti Radi , nadhani kwa msaada wa Cauldron haitokuwa ngumu kupita dhiki ya radi ya mapigo mengi , ukijumlisha na utimamu wako wa mwili kila kitu kinafaida kwako”
“Upo sahihi kwasasa nguvu zangu ni za kutosha na busara pia zimeimarika lakini bado nitahitajika kuwa na muda sahihi kabla ya kupita , nataka kupata fursa ya kuelewa kanuni za mbingu zinavyofanya kazi , ni kama Anjiu tu ambaye alisubiri muda mrefu ili kuja kuelewa fumbo la kaunni za mbingu
zilivyo”Aliongea Roma na Rufi alitingisha kichwa na furaha ilikuwa imemtawala na alishindwa kuyazuia mahaba yake na kumkumbaita Roma na kumbusu shavuni licha ya kwamba alikuwa amechafuka na damu.
“Hey embu acha kunibusu huoni namna ambavyo Chaos amechafua mwili wangu , Babe Rufi ninafuraha hatujapata majeraha na pia tumeweza kupata faida kubwa , nitakupeleka sasa visiwani , nikishakamilisha maswala yangu huko duniani nitarudi tena na kuwaua wote”
Rufi alitingisha kichwa kwa mchecheto huku akiwa na hamu kubwa ya kukutana na mlezi wake Sui.
Roma bila ya kuchelewa alimshikilia vizuri na kumuwekewa kinga ili aweze kupumua na kisha alianza safari ya kuelekea kusini magharibi, ilikuwa ndio ulelekeo ambao Anjiu alikimbilia lakini Roma hakuwa na mpango wa kumfukuzia tena, mpango wake ilikuwa ni kurudi Visiwa vya wafu mapema kadri iwezekanavyo kwani misheni ya kumuokoa Rufi ilikuwa imekamilika.
Wakiwa njiani Roma alimuuliza Rufi namna ambavyo alilelewa kwani aliletwa katika ulimwengu huo akiwa mdogo sana na ilionekana Rufi aliweza kuwa mkubwa kutokana na kunyonyshwa maziwa ya kopo ambayo yalitokea katika ulimwengu wa kawaida.
Ukweli ni kwmaba majini kwao hawakuwa wakipika chakula kama binadamu kwao wale wasile haina madhara kwao vyakula vyao vimekaa kama madawa madawa , wanatafuna mizizi na majani si mchezo.
Hatimae bila ya kukutana na jini mwingine njiani waliweza kufanikiwa na kutokea katika ulimwengu wa kawaida kupitia baharini.
Baada ya safari ndefu ya nusu dunia hatimae waliweza kufika Mediterranian muda wa jioni kabla ya machweo na kukaribishwa na upepo wa bahari.
Uwezo wa utambuzi wa Roma ulikuwa mkubwa mno hivyo aliweza kuchunguza eneo ambalo Sui alipo na ndani ya muda tu aliweza kugundua Sui yupo na Bi Wema na wengine wamekaa nje ya kijumba kilchotengenezwa kwa miti pembezoni mwa fukwe mita kadhaa kutoka ngome ilip.
Roma kabla ya kufika katika visiwa hivyo alikuwa ashabadili mavazi na kujisafisha kabisa ili asije kutisha watu hivyo moja kwa moja alienda mpaka walipo.
Ilikuwa ni nyumba ya miti ambayo ilikuwa ikitumiwa na Ron kwa mapumziko na ndani yake alikuwa sio Bi Wema tu walikuwepo Neema Luwazo , Nasra na Doris.
Wakati huo huo Edna na Lanlan walikuwa wakicheza kwenye bembea katika bustani ambayo imezungukwa na maua ya kuvutia katika eneo hilohilo.
Ijapokuwa Lanlan alikuwa na uwezo wakuharibbu bembea hio ya chuma kwa uwezo wake lakini alijitahidi kujifanyisha mtoto wa kawaida.
Mara baada ya Roma kutua kutoka angani akiwa na Rufi kila mmoja aligeuza shingo yake na kuwaangalia kwa mshituko na furaha pamoja na shukrani ya kuona wote walikuwa wazima wa afya.
“Hubby !, Rufiii..!!!””Nasra ndio aliekuwa wa kwanza kutoka kwenye mshituko na kupiga kelele za shangwe.
“Omg,,, naona mnatufanyia surprise si mtoe hata taarifa jamani kabla ya kuja”Aliongea Neema kwa utani.
Lanlan ambaye hakuwa mbali na eneo hilo alitoka kwenye bembea na kutimua mbio kwenda kumlaki baba yake, huku Edna ambaye bado alikuwa amekalia bembea aliishia kutoa tabasamu hafifu huku akitingisha kichwa chake kwa namna ya kusikitika kutokana na spidi ya Lanlan.
Bi Wema upande wake palepale aliangua kilio mara baada ya kuwaona na mara baada ya kujihakikisha hakuwa akiota alikimbia na kwenda kumkumbatia Rufi.
“Mwanangnu …. jamani binti yangu mimi…. umejua kunitia wasiwasi”Rufi alianza kuchunguzwa kwanzia nywele mpaka vidole ili kuona kama kuna sehemu iliokuwa na jeraha.
Laiti angemuona Rufi na yale makovu pengine angepoteza fahamu hapo hapo na ilikuwa afahdali Roma alikuwa amechukua hatua ya kumponyesha kabla ya kumrudisha.
Rufi aliishia kumkumbatia mama yake huku machozi yakimtoka na aliishia kuangaliana na Sui na wote kwa pamoja waliishia kutokwa na machozi na aliishia kuita jina la mlezi wake’ nanny’ ijapokuwa alitaja kwa sauti ya chini lakini Sui alisihindwa kujizuia na yeye kwenda kuungana nao katika kukumbatiana.
Onesho la wanawake watatu wakiwa wamekumbatiana huku wakilia ilimfanya Roma kuguswa , ilikua hivyo lakini kwa namna moja alihisi kutojisikia vizuri na aliishia kukumbaitia na Lanlan na kisha alimwangalia Edna wa kwanza na kumpa tabasamu la ushindi na kisha akageuza macho yake kwa wengine na kuwapa ishara zinazofanana.
“Hehe… mnaonaje ushujaa wa mume wenu katika misheni za ki uokozi”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la kihuni huku akiangaliwa na warembo wake.
Hakuna ambaye alikwepesha macho na wote walikuwa na sura za kutaka kujua kile kilichojiri katika ulimwengu huo wa majini.
“Punguzeni munkari …. nitawaambia stori yote baadae, ukiachana na hivyo huyu mzee Ron yuko wapi?”Aliongea Roma na dakika ileile aliweza kuhisi uwepo wa Ron kwenye msitu uliokuwa nyuma ya kibanda hicho.
“Wewe Ron hebu leta uzee wako hapa”
Kiongozi wa kundi la kimafia Ron alikuwa bize kupunua bustani yake ya miti na mua kwenye msitu huo na mara baada ya kusikia sauti ya Roma aliacha kila alichokuwa akifanya na kukimbia.
“You have returned , your Majesty Pluto”Aliongea Ron huku akitoa tabasamu la kiaina hivi , alikuwa amevalia mavazi ya kishamba na kofia aina ya hat huku akiwa ameshikilia koleo.
“Una maagizo yoyote mfalme?”
“Mzee hayo mavazi naona yamekupendeza sana… ninataka kusherehekea kuungana kwa Rufi , Bi Wema na Sui , nataka uandae mvinyo mzuri kutoka kwenye Cellar”
“Does the 1982 Margarita sound good, Your majesty Pluto?”Aliuliza Ron.
“Ndio itafaa , kwanza sijui ni mvinyo upi umebakia kule chini lakini nikipata chupa kadhaa za aina hio itakuwa bomba”Aliongea Roma na Ron alitingisha kichwa lakini Edna alimkodolea macho Roma .
“Ron ni mbunifu wa kimataifa lakini pia mzee wa kuheshimika kwanini unamfanya kama vile ni kijakazi wako , huo ni ukorofi huoni Lanlan anakuangalia?”
“Ohoo.. Wife hapo sasa ndio unakosea , kama nitakuwa mpole mbele ya hawa watu wataona labda napanga kuwaua lakini nikiwa mkorofi mbele yao kwao ndio wananiona mkarimu”Aliongea Roma huku akicheka na kumfinya Lanlan shavu lake , alijisikia amani sana mara baada ya kurudi nyumbani.
Bi Wema, Rufi na Sui hatimae walipoa na kisha kurudi na kukaa kwenye banda hilo la mapumziko
Sui na Bi Wema walitaka hata kumpigia Roma magoti kuonyesha shukrani zao lakini Roma aliwazuia na palepale alimshusha Lanlan chini.
“Kwanini ndio nyie tu , Yezi , Rose na wengine wapo wapi?”
“Hao wadada wameenda mbali kule kisiwani kwa ajili ya kuendelea kujifunza kwani hawakutaka kusumbua watu wakati wakipambana wao kwa wao”Alijibu Dorisi.
“Mage na Yezi pia wameenda? , unamaanisha washaingia..”
“Ndio wamefanikiwa .. Mage aliingia levo ya nafsi masaa kadhaa baada ya wewe kuondoka , sijajua nini lilikuwa tatizo lake lakini kitendo cha Amina kufanikiwa ilimfanya kuwa na wasiwasi lakini wasiwasi huo ndiio uliomsaidia kuingia levo ya nasi , kwa Yezi inaonekana ana kipaji na alifuatia mara baada ya Mage na sasa wanalingana”Aliongea Neema.
Roma alishangaa na hakutegemea kama Yezi ambaye alianza kwa kuchelewa kuweza kufikia levo ya nafsi ndani ya muda mfupi hivyo.
Ijapokuwa walikuwa wakitumia vidonge lakini kupata uelewa na ufumbuzi ilikuwa ni kitu kingine kabisa.
Inaonekana maisha ambayo Yezi amekulia ndio ambayo yamempa uzoefu ambao umemsaidia kupata ufunuo kwa haraka..
Ni Edna , Dorisi , Neema , Nasra na Najma ndio ambao hawakuwa wamefikia levo ya nafsi ,Rufi yeye hakuwa akihesabika kwani hakuwa na uwezo wa kujifunza.
“Wenzenu wamefanikiwa kupita nyie hamna wasiwasi?”
“Ndio tulichokuwa tukijadiliana hapa , na kujiuliza au ni kwasababu ya umri , wenye umri mdogo wanaonekana kupanda levo kwa haraka kuliko sisi ambao umri umeenda kidogo”Aliongea Dorisi na kumfanya Roma kutoa tabasamu na kumwagalia Edna.
“Honey , huoni kuna kitu hakipo sawa katika maneno ya Dorisi , ninachojua unalingana na Mage na Magdalena au nimekosea?”
Upande mwingine Edna hakuonyesha wasiwasi na alikuwa na muonekano wa maringo na alichukua juisi yake ya matunda nakunywa kidogo na kisha akamwnagalia Roma.
“Sina haraka”
Jibu hilo la kawaida lilimfanya Roma kukosa usemi lakini hata hivyo aliishia kutoa tabsamu bila ya kuongea chochote.
“Ukiachana na hayo , Hubby, Mage akirudi hebu angalia ufunuo ambao amepata ni wa ajabu mno”
“Kwanini ni wa ajabu?”
Muda huo wakati wakiongea ndio Ron aliweza kufika akiwa na chupa za mvinyo mwekundu wa Margarita , mvinyo huo gharama yake haina kiwango maalumu sokoni , Margarita ya kawaida ambayo haijazeeshwa kwa muda mrefu inagharimu zaidi ya dola elfu moja sasa hizo ambazo zina umri mkubwa thamani yake ilikuwa ngumu kueleweka.
Lakini Roma kutokana na kuwa na koneksheni dunia nzima marafiki zake walimletea kama zawadi na aliishia kuzihifadhi katika chumba cha ardhi katika Cellar.
Roma mara baada ya kufungua chupa baadhi alimwambia Ron kubakia hapo na kuungana nao kwani alikuwa na maswali anataka kumuuliza lakini pia ilikuwa siku nzuri kwa Roma.
Roma alikuwa na hamu kubwa ya kuwasubiria Rose kurudi pia.
Harufu nzuri ya mvinyo huo iligusa pua za warembo huo na Edna ndio aliekuwa wa kwanza kuomba na yeye apatiwe lakini sasa mara baada ya kuonja aliitema chini akisema mvinyo huo mwekundu ulikuwa hata ukizidiwa utamu na maziwa na juisi ya matnda.
Muda huo huo Roma pia alianza kuelezea kile ambacho kilitokea katika ulimwengu wa majini watu na namna ambavyo Rufi alitoa ushirikiano kwa kutokuwa na hofu kubwa katika kupitia hali hio ya kuogofya.
Mara baada ya kuona Roma alikuwa amepanda zaidi kilevo walishangaa na kuwa na furaha kwa ajili yake.
Kwa upande wa Roma alijua kabisa bado hakuwa juu zaidi ya sehemu ambayo anataka , bado hakuwa na uwezo wa kupambana na jini yule ambaye alikutana nae Dodoma yaani Master namba moja.
Ron hakuelewa chocho te ambacho walikuwa wakiongea kwani kiswahili ndio kilichokuwa kikitumika zaidi na kingereza mara chache.
“Mfalme Pluto , kwasababu ndio umerudi nina taarifa ya kukupatia”Aliongea Ron mara baada ya maongezi kukauka.
“Oh , ni taarifa gani hio?”
“Ni kuhusu Princess Clark , amepanga kugeuza makazi yake hapa kisiwani kuwa maabara , tayari ashasafirisha vifaa vya kimaabara kuja na baadhi ya nyaraka na malighafi kutoka London, muda ambao vitu hivyo vinakaridiwa kufika ni usiku na atafika wakati huo”
“Yale ni makazi yake hivyo muache afanye anachotaka , pia inamuokolea muda kwenda na kurudi kwa ajili ya majaribio ana ukichaa na maswala ya kitafiti ni kama vile hawezi ishi bila ya kuwa na maabara”Aliongea Roma akiwa hana mshangao.
Tokea siku ambayo Roma aliweza kupatiwa hatimiliki ya visiwa hivyo Catherine na Clark walikuwa wakipenda sana kuja kutembelea na walikuwa na ardhi yao kabisa na ilikuwa kubwa mno saizi ya kisiwa na walijenga majengo kama hoteli kwa ajili ya mapumziko.
Zamani Clark alikuwa akija kisiwani hapo mara chache sana lakini furaha ya kuja kisiwani hapo kuungana na wavuna nishati wenzake ilikuwa kubwa ndio maana alitaka kufanya makazi yake kuwa katika eneo hilo ili kuwa rahisi kuendeleza kazi yake na kupata uzoefu katika mafunzo kwa kupambana na wenzake.
Lisaa limoja mbele hatimae wanawake waliokuwa na muonekano wa kimaringo waliweza kufika kutokea kusini , alikuwa ni Rose na wengine na mara baada ya kumuona Roma na Rufi iliwafanya kuwa na furaha isiokuwa na kifani , awamu nyingine ya vicheko na maelezo ilihitajika.
Roma kwa kuwachunguza Rose , Magdalena na Amina walikuwa washaanza kuingia katika mwisho mwa levo ya nafsi , uwezo wa Amina ulikuwa umeongezeka kwa spidi kubwa nje ya matarajio na kuwakaribia Rose na Magdalena na kitu kingine kilichomfanya Roma kushangazwa na Amina kiini cha macho yake ni kama kimebalika na kuwa na ukijani ndani yake na alikuwa akikumbuka aina ya macho hayo kuna mahali aliyaona ila hakuwa akikumbuka vizuri.
Upande wa Yezi na Magdalena walikuwa wamepiga hatua na Roma alijua kutokana na uwepo wa vidonge basi muda si mrefu watafikia mwishoni mwa levo hio.
“Babe otea nilichoweza kufanikisha?”Mage hakutaka hata kuulizwa na alikuwa na hamu ya kumuonyesha Roma.
“Nitajuaje sasa wakati kila mmoja anasema ni kitu cha kushangaza?”
SEHEMU YA 730.
Mage alikuwa na hamu ya kumuonyesha Roma ufunuo ambao amepata kwa kugeuza nguvu za mbingu na ardhi na kuwa siraha na ndani ya sekunde tu aliweza kubadilisha nguvu zile na kutengeneza moto mweupe kama wingu kwenye mkono wake.
Roma alishangazwa na kitu kile na hakujua moto ule ni wa aina gani kwani hakuwahi kuuona.
“Huo utakuwa ni moto wa maajabu!!”Aliongea Roma aliekuwa katika hali ya mshangao.
“Hubby kumbe unaujua ?, Aunt Sui amesema inawezekana ikawa ni Heart flame sehemu ya moto wa kimaajabu”
“Heart flame!!!?”
Roma alishangazwa na kauli ile na kugeuza macho yake kwa Sui na palepale alielezea.
Heart flame maana yake moto wa moyo , ilikuwa ni kweli ni sehemu ya moto wa kimaajabu , ambao mara nyingi huweza kutengenezwa kwa kugeuza nguvu za mbingu na ardhi na majini ambao wana hasira za haraka, sasa kutokana na tabia zao zilivyo majini wa namna hio hawanaga muda wa kukaa chini na kuvuna nishati hivyo moto wa namna hio kuona unatumika kama siraha ni mara chache sana.
Isitoshe hata hivyo kuwa na hasira za haraka haitoshi kugeuza nishati za mbingu na ardhi kwenda kuwa moto huo bali lazima kwanza mtu kuwa na moyo wa barafu ikimaanisha kwamba tofauti na kuwa na hasira za haraka lazima uwe na kiasi walau kidogo katika kutuliza hasria zako.
Sasa Afande Mage tabia yake ilikuwa ikijulikana kabisa , alikuwa ni mwanamke ambaye ana hasira za karibu na ni hasira hizo hizo ambazo zilimkutanisha na Roma. Hivyo kutokana na tabia yake hio alijikuta akibatatika kupata moto wa namna hio.
Roma alimwambia Mage kujaribu kumshambulia na huo moto na alikuja kugundua sio moto ambao ulikuwa ukiunguza bali ni moto ambao ulikuwa ukifanya akili yako kupatwa na ukichaa ni kama vile shambulizi la kichawi hivi.
Ilikuwa ni kwasababu uwezo wa Roma ulikuwa juu sana ndio maana athari zake zilikuwa kidogo lakini kama Mage atakutana na mshindani ambaye ni wa levo yake akigusana na huo moto kuna uwezekano wa kumfanya kuwa kichaa.
Upande wa yezi licha ya kuingai levo ya nafsi lakini bado ufunuo wa kisiraha hajapata bado, lakini hata hivyo haikuwa na maana kwamba kila ukiingia katika levo ya nafsi ndio moja kwa moja unapata ufunuo wa kisiraha.
“Hii ni kwa ajili yako , upanga wa daraja la kati huu,
ninaona unakufaa sana hivyo usiwe na huzuni”aliongea Roma akimkabidhi Yezi upanga kwasababu bado hakuwa na uwezo wa kisiraha.
Wote walijikuta wakishangazwa na uzuri wa upanga huo ambao katikati ulikuwa umeandikwa jina la Manjushage.
“Manjushage? Hii ni Dhana ya daraja la kati ambayo ni maarufu ndani ya ulimwengu wa kijini , hubby umeipata mara baada ya kuua jini wa miliki ya Xia?”Aliuliza Rufi.
“Ndio nimeaua majini wengi na kuangalia siraha zao lakini ni huu upanga tu ambao mashambulizi yake yamenifurahisha na nimeona unafaa kabisa kutumiwa na Yezi , kwanini unasema ni maarufu sana?”
“Hii ni Dhana ambayo ni mbili kwa moja kadri uwezo wako unavyoongezeka neno manjushage linagawanyika mara mbili na kuwa Manju na Shage, ukishajigawanya mmoja unaweza kutumia kama siraha ya mashambulizi na nyingine unaweza kutumia kama kinga, faida nyingine ni kwamba ukitumia unakuongezea spidi wenywe katika mshambulizi , kama una msingi mzuri wa mashambulizi ya upanga basi inageuka kuwa Dhana ya hatari sana ambayo inaweza kuua hata jini wa nafasi ya maji ya barafu, lakini kama uwezo wako ni wa chini basi inaweza kutokuwa na maana kubwa na inaweza kuwa hatari kwani wenyewe unanyonya nguvu za kijin”
Licha ya Yezi kutokuwa na msingi mzuri wa kutumia panga lakini hakutaka kupokonywa na alificha upanga wake..
“Haijalishi ili mradi nimepewa basi ni zawadi yangu , nitajifunza namna ya kutumia na naahidi kutoitumia kabla sijaelewa namna ya kuitumia”
Uzuri wa upanga huo wa kioo ulimfanya Amina kuwa na wivu na kumwangalia Roma kwa macho ya kurembua na kutia huruma.
“Hubby kwanini unakuwa na upendeleo kwa kumpa
Yezi zawadi peke yake?”
“Sister Amina aisee huna aibu na umri wako huo bado tu unafanya hivyo?”Aliongea Yezi na kumfanya Amina kuona aibu na kujiweka sawa
Roma mara baada ya kuona kila mmoja alitegemea zawadi aliamua kutoa kila Dhana aliopata , Magdalena alipatiwa ule mkanda wa ngurumo radi , upande wa Rose alipewa siraha ya Sanyua na Mage akapewa kisu cha mfupa wa Dragon.
Kila mmoja alipata Dhana kasoro Edna tu ambaye yeye alikuwa na bangiri kwenye mkono wake.
Ukweli ni kwamba licha ya Roma kuwa na uwezo mkubwa sana wa nguvu za kijini lakini mpaka wakati huo alishindwa kujua nguvu halisi ya bangiri hio ambayo amevaa Edna ikoje.
Kwa namna moja ama nyingine ni kama bangiri hio ilikuwa na muunganiko wa moja kwa moja na mvaaji.
Roma hakumsahau kipenzi chake Lanlan pia kwani na yeye alimpa siuraha za daraja la chini kwa ajili ya kuchezea.
Ikiwa giza limeingia kabisa hatimae Roma alihisi ongezeko la mtu mwenye uwezo wa nafsi na alipotumia uwezo wake wa utambuzi alikuja kugundua ni Clark
Kwasababu hawakuwa na chakufanya Roma na warembo wake walianza kutemba kandokando ya fukwe hio na ndio wakati ambao waliweza kuona meli kubwa ya mizigo ya Uingereza iliokuwa na chata la ‘British Royal Cargo’ ikielea taratibu kuelekea kwenye gati.
Ilikuwa na bendera ya jumba la kifalme la Wales kama utambulisho ambayo ilikuwa ikipeperushwa na upepo.
Ni kama nusu saa mbele wanajeshi wa jeshi la majini wa Uingereza ambao wamevalia kombati za kijeshi walionekana kuwa bize kushusha maboksi kadhaa na baadae makontena na kupandishwa kwenye gari na kunza kusafirisha kuelekea makazi ya Clark , sehemu ambayo ndio anapanga kufungua rasmi maabara ya ki utafiti.
Dakika chache mbele helicopter ilionekana kushuka tataribu upande wa mbali kidogo na kushusha baadhi ya watu.
Alionekana mwanamke alievalia shati la kola lenye vifungo kutoka chini mpaka juu ambalo limemkaa vizuri rangi nyeupe , huku akiwa na suruali yenye michirizi miwili ya rangi nyeupe pande zote , nywele zake za kahawia ziliuwa zimechanguka kutokana na upepo uliokuwa ukizipeprusha, ni umaridadi na hadhi ya utukufu ndio vilionekana kutoka kwake..
Clark alitembea kwa kuwasogelea Roma akiwa na tabasamu huku nyuma yake akifatiwa na wanawake wawili wote wakiwa ni wazungu , mmoja alikuwa na muonekano wa kitajiri na mwingine alikuwa ni mwenye wasiwasi na kutokuwa na hali ya kujiamini kidogo.
Mwanamke mrembo mwenye muonekano wa ki utu uzima alikuwa akifanana na Clark kwa vitu vingi , alikuwa ni Catherine mama yake , alikuwa ni ‘hot’ na ‘sexy’ hususani na mavazi yake aliokuwa amevalia.
“Oh my , Clark walk slower , wait fo mama..”
Catherine alikuwa akimpigia makelele Clark akimwambia atembee taratibu lakini Clark ni kama vile hajamsikia na alitembea kuelekea kwenye kundi la watu waliokuwa mbele yake.
Edna na Roma pamoja na wengine wote walisalimiana na Clark huku Roma akimkumbatia kawaida.
“Mama yako anafanya nini hapa?”Aliuliza Roma huku akiwa na wasiwasi kidogo na muonekano wa Catherine.
“Alikuwa akijua mara baada ya kuanza harakati za kuhamisha vitu vyangu na alilazimisha kuja na mimi huku kwa kuogopa namkimbia na kumuacha mwenyewe”
Roma aliishia kutingisha kichwa kwa maneno hayo, yalienda sawa na haiba ya Catherine.
Muda huo huo mara baada ya Catherine kumfikia Roma alishindwa kuzuia furaha yake na kumsogelea akiwa amchanua mikono yake na kumkumbatia.
“Oh my Dear Roma Ramoni , it has been a while don’t you mis me? Mwaaaahh.”
Catherine alimpiga busu shavuni kiasi cha kuacha alama na muda huo Roma alijihisi ubaridi mgongoni na kuishia kugeuka na kuangalia warembo wake ambao walikuwa wakimwangalia kwa macho ya kutisha.
Roma alijihisi kuogopa ,ijapokuwa mabusu hayo kwa wazungu ni kitu cha kawaida na yeye na Catherine ni marafiki lakini ukweli ni kwamba urafiki wao ni wa faida kwani walikuwa wakinyanduana.
Isitoshe kwa wakati huo Clark alikuwa tayari ni mpenzi wake hivyo ni kama Roma anakula kuku na mayai yake.
“Hello , your majesty Pluto”
Sauti ya wasiwasi ilitoka kwa mwanadada ambaye alikuwa ameongozana nao.
Roma alikuwa bize wakati huo na hakuwa amesalimiana nae na palepale alimkumbuka na kutoa tabasamu.
“You must be Grace , the student Clark
Accepted?”Aliuliza Roma akimaanisha kwamba huyo atakuwa ni Grace mwanafunzi ambaye alikubaliwa na Clark.
“Ndio Mfalme Pluto bado unanikumbuka?”
“Bila shaka , ndio ulieokoa maisha ya Rufi lazima nikukumbuke”Aliongea Roma na kisha alisalimiana nae kwa kumpatia mkono,
“Ni Profesa ndio ambaye alimponya Rufi mimi nilifanya wajibu wangu tu”
Wanawake hao hawakuelewa kwanini maongezi yako hivyo lakini Clark aliwaelezea kile kilichomkuta Rufi kule kwenye msitu wa Australia mpaka kumpeleka hospitali ya London kwa ajili ya matibabu na Grace akaonyesha ujasiri wa kutaka kumsaidia Rufi licha ya kuwa nesi asiwe na cheo chochote.
“Kwanini umekuja nae?”Aliuliza Roma mara baada ya kuona Grace alikuwa akijua jina kamili la Roma.
“Ni mwepesi kujifunza na ana kipaji , na zaidi ya yote ana mtazamo chanya na mkarimu , nadhani kipaji chake kilikuwa kimejificha tu kutokana na mazingira pamoja na kutopata elimu sahihi , nipo katika hatua za kumfunza ili kuwa msaidizi wangu namba moja ili baadae aje kutidhi tafiti zangu , hivyo nimekuja nae kwa ajili ya kuona mahali ambapo masomo yake yataanzia”
Grace aliishia kuona aibu huku akifurahia kwa wakati mmoja namna bosi wake anavyomsifia.
Roma aliishia kumchokoza Clark kwa kumgonga kwenye paji la uso, ilikuwa ni Roma na Catherine tu ambao walikuwa wakiruhusiwa kumfanyia hivyo Clark kutokana na cheo chake cha uprincess.
“Hivi tayari ndio ushazeeka mpaka kutaka mrithi , jifanyishe mbele ya wanafunzi wengine lakini sio mble yangu ,… haya waachieni wanajeshi hio mizigo na tutarudi ngomeni kwa ajili ya chakula cha usiku .. oh ?yeah Grace na wewe ungana na sisi”Aliongea Roma akiona amkaribishe na Clark aliishia kutabasamu akimwangalia namna Grace ambavyo alikuwa na wasiwasi.
Kwa kutembea wote walirudi ngomeni huku stori zikiendelea kimakundi makundi na ziliendelea hata wakati wa chakula cha usiku na ilikuwa ni lugha ya kisawahi na kingereza ndio iliokuwa ikisikika hapo ndani ,
Roma alimuuliza Clark kama alikuwa na uhitaji wa Dhana lakini alikataa na sababu ni kwamba Dhana hizo aliona ni dhaifu sana.
Upande wa Catherine alitaka na yeye vidonge vya kuendeleza urembo wake na Roma alimpatia mpaka mbinu za kufanya ili kuendelea kudumisha ujana wake asizeeke haraka na kuhusu kufanikiwa Roma hakutaka kujisumbua sana.
Ki ufupi kila mmoja alionekana kuwa na furaha ndani ya eneo hilo , upande wa Lanlan Roma Ramoni alikuwa amekaa kwenye kiti chake maalumu cha kitoto akiendelea kufurahia nyama yake.
“Hubby unapanga kukaa hapa kwa muda gani , nimesikia kutoka kwa Rufi unapanga kurudi kwenda kuua wanafamilia wa miliki ya Xia?”Aliuliza Afande Mage huku akioneysha hali ya msisimko sana na kumfanya Roma atabasamu kwani ni kama vile anajua anachofikiria.
“Mage najua unachofikiria lakini lazima nikuambie ijapokuwa unamiliki moto huo wa kimaajabu lakini uwezo wako upo chini , Anjiu yule mshenzi anao uwezo wakuua watu wa levo yako elfu moja kwa shambulizi moja tu la moto wake wa ndege wa Dhahabu, hivyo usifikirie kabisa mimi kukupeleka”
“Acha hizo basi , wewe si utakuwepo na utatulinda ?”Mage alibembeleza , kwa haiba ya Mage kwake ilikuwa ni mateso kuvuna nishati bila ya kupambana katika mapigao ya uhalisia , alikuwa ni polisi
mpenda haki na alikuwa na hamu ya kuua jini hata moja ambaye amemsababishia Rufi mateso.
“Mage inatosha bwana ukienda nae utamuongezea tu mzigo , atakuwa mwepesi akiwa peke yake lakini na sisi itakuwa ni udhaifu kwake”Aliongea Magdalena.
“Dada unaongea kama vile hutaki kwenda , mimi shauku yangu ni kuona ulimwengu wa majini ulivyo tu”
“Hakuna kikubwa cha kushangaza , ulimwengu wa majini ni ardhi ya kimisitu na barafu tu kama Antarctica pamoja na nyumba za kimaajabu ajabu”Aliongea Roma huku akicheka.
“Kwahio ukirudi huko kumuua baba na mtoto si itakuwa kazi rahisi?”Aliuliza Rose,
“Nataka kwanza kuacha kufikiria kuhusu hili na kufanya mazingatio mengi lakini kwasababu nina uhakika ninao uwezo wa kuwaua sina haraka , ninachotaka ni kupata uwezo wa juu zaidi kupitia uzoefu wa kule hasa katika kudhibiti radi , pia natamani wao ndio waje huku niwapigie huku huku na kujaribisha na kanuni za anga lakini sidhani kama watakuja kutokana na hofu ya kukutana na miungu , ila kwa siku hizi chache kwanza nataka kukaa na nyie huku nikiangalia ukuaji wa Lanlan, sio kwamba napenda sana kuua majini ila nafanya yote kwa ajili ya maisha yetu kuwa salama yasiokuwa na misuko suko”
Kila mmoja alikuwa kimya wakati Roma akiongea na walimwangalia Roma kwa macho ya shukrani.
“Kama sio wewe vile wa kuongea maneno ya namna hio ukiwa na muonekano wa usiriasi hivyo?”
Edna ambaye alikuwa pembeni ya Roma aliongea huku akimwangalia Roma kwa macho ya kuibia ibia.
“Haha … mwanaume ambaye amekwisha oa mara nyingi hupevuka haraka , tumeona kwa miaka inaenda mitatu sasa na yote hayo ni kutokana na juhudi zako boss wangu”
“Acha kuwa chawa basi”Aliongea huku akimzodoa kichwa chake kwenda pembeni na kumfanya Roma kucheka.
“Nataka kusubiri subiri pia kwani Kule Bagamoyo nimemuacha Tannya ambaye anejifanyisha kuwa Maimuna , nataka nipate taarifa ya nguvu ambayo ipo nyuma ya familia ya Sharif kuchukua hatua, hilo ni jambo ambalo napaswa kushughulika nalo pia , ukiachana na hayo nasubiria uwezo wenu kuwa mkubwa ili niwe na amani hata kama hao washenzi wakitoka huko na kuvamia muweze kudili nao”
“Unaongea kama vile upo vizuri sanaa na hatuwezi kupambana pia lakini jua kama kitu kibaya kitakupata na sisi tutapotea hivyo uelewe kwamba katika hili haupo peke yako”Aliongea Nasra.
Maneno yake yalipeleka wimbi la usiriasi katia sura za wanawake hao na kuanzia muda huo walijua wanapaswa kujiandaa kwa lolote lile baya ambalo linaweza kutokea.
Malkia Catherine kutokana na usriasi wa maongezi hayo alishindwa kuvumilia na akaweza uma na vijiko vyake chini.
“I say since Roma has returned and everyone is here , staying on the island may be too monotonous ,what about going to London to see a football game? Its all on me”
(“Nasema kwasababu Roma amesharudi na kila mmoja yupo hapa , kuendelea kubakia hapa kisiwani kunakuwa kunachosha sana vipi kama tukienda London kuangalia mechi ya mpira miguu , gharama zitakuwa juu yangu”
Alishauri Catherine na mtu wa kwanza kukunja sura alikuwa Clark kama vile hajaridhika na pendekezo hilo.
“Mama kwanini mpira ghafla hivyo na tangu lini tukapenda maswala ya mipira sisi?”
“Hicho sio nilichomaanisha , Clark unachojua ni utafiti tu na hujali nini kinatokea katika mazingira ya kukuzunguka tarehe nane ya mwezi ujao fainali ya UEFA Champion leagued inaenda kuchezwa katika uwanja wa Wembley”.
“Kama ni UEFA inahusiana nini na sisi?”
“Bila shaka lina wahusu , nadhani hamjapata taarifa Sophia msanii kutoka Tanzania amealikwa kutumbuiza, hivi unajua ni wasanii wangapi wameweza kupata nafasi ya kutumbuiza laivu katika mashindano makubwa kama hayo , hii ni mara ya kwanza kwa msani chipukizi kupewa nafasi hio “Kila mmoja alishangazwa na habari hizo kwani hakuna aliekuwa akijua.
“Pumbavu kabisa yaani Sophia ameshindwa kuniambia kuhusu hili , ni hatua kubwa mno amepiga halafu kutoka hapa kwenda Uingereza sio mbali”
“Wewe kama mwenyekiti wa Multinational Campany
unafikiri unao muda wa kujisumbua na kinachoendelea ndani ya kijikampuni kidogo cha habari na utamaduni? Nina uhakika Sophia yupo bize kujiandaa na kakosa muda wa kukupa taarifa”Aliongea Roma kwa kutania.
Kutokana na ukaribu uliopo kati ya hapo na Uingereza kila mmoja aliona hakuna haja ya kukataa kutokwenda kuona mechi hio isitoshe hata kama hawapendi mpira wachukulie kama kitendo cha kumsapoti Sophia.
Kutokana na kurudi kwa Roma hawakuona haja ya kuwa na wasiwasi na waliona kwasababu pesa wanayo sio mbaya kama watembelee taifa hilo kwenda kujifanyia manunuzi na kushangaa shangaa staarabu zingine.
*****
Upande mwingine katika ulimwengu wa majini katika miliki ya Panas kulikuwa na kikao kilichokuwa kikiendelea , Gefu hakuonyesha kuwa katika hali nzuri katika kusikia ripoti iliowafikia kutoka kwa shushu ambaye yupo ndani ya miliki ya Xia,
“Okey inatosha”Aliongea kwa kuonyesha ishara ya mkono na yule shushu alitoka katika chumba hicho cha mikutano.
Baada ya kutoka Gefu aligeuza macho yake na kuangalia ndugu zake na wazee wa ukoo huku akiweka tabasamu la uchungu usoni mwake.
“Huyu Roma Ramoni hakika ni binadamu mwenye bahati sana , ameweza kupona”
“Cha kuogopesha ni kwamba kama alichosema
Shushu ni sahihi basi hata Anjiu na Senji pamoja na wazee wengine waliopo levo ya maji ya kiroho ni kwamba wamemshindwa na kusambaratika kwa kukimbia , hili linamaanisha vitu viwili mosi Roma anaweza akawa tayari ashapitia mapigo zaidi ya mia moja…..”Aliongea Gefu.
“God damn it… huyu nwanaharamu imewezekanaje akawa na uwezo mkubwa hivi kuliko hata sisi majini wenyewe hakuwa ni wa kutsha sana mara ya mwisho nilivyomuona… uwezo huo ni wa majini wa karne zilizopita ambao ni wachache sana na ni levo ambayo ni ngumu kufikiwa katika kipindi hichi”Master namba nne aliongea.
“Kuweza kumiliki Dhana ya kihistoria kama Chaos Cauldron inamaanisha kwamba Roma sio binadamu wa kawaida , Mkuu hata kama miliki yetu haina uhusiano wa karibu na Roma hatupaswi kuwa na uadui nae vinginevyo hata kama wazee wetu wa miliki kuja kupambana bado tunaweza kumshindwa”Mwanaume mweupe ambaye alikuwa amevalia nguo za rangi ya majivu aliongea.
“Namba nne nadhani uende ulimwengu wa kawaida na kumpatia taarifa Jeremy kuwasiliana na binti yake , kupitia yeye nina imani Roma atakubali kukutana na sisi kwa siri”
“Nini , Kaka mkubwa ,,, hio ni hatari sana , huyu binadamu ni muuaji”Maneno yalimtoka Master namba nne akiwa na wasiwasi.
“Bila hatari bila faida”Aliongea
SEHEMU YA 731.
Siku mbili mbele wanajeshi wa majini wa Uingereza waliondoka kisiwani mara baada ya kukamilisha utengenezaji wa maabara katika ukamilifu uliohitajika.
Roma alikuwa akiinjoi maisha bila mawazo kabisa katika siku mbili zote usiku na mchana , alikuwa akicheza na warembo wake kila wakati aliojisikia.
Hakujali mazingira ni kwenye mchanga wa fukwe au kwenye meli au chumbani kwao yeye aliendeleza kazi.
Viashiria vya kufanya mapenzi na wanawake hao viikuwa vikonekana kila mahali , Stamina yake isiokuwa kawaida ilidhihirika kwa mara nyingine.
Hajawahi kuwa mtakatufu hata hivyo hivyo hakuweza kuona aibu kuzungukwa na wanawake wengi namna hio , zaidi sana ni kwamba kila mwanamke wake alitaka kupata mimba yake hivyo hakuna ambaye alikataa kutoa utamu kwa Roma labda pale ambapo wanajishi kuwa wachomvu sana.
Roma hata pale anapofumwa na mwanamke mwingine asingeona aibu na kumwambia na yeye na ajiunge , ki fupi alijihisi ni kama yupo mbingu ya saba , maisha kwake yalikuwa ya burudani kiasi kwamba hakujua hata muda unavyoenda.
Upande mwingine wanawake ambao hakuwa nao karibu zaidi ni Clark na Yezi , sio kwamba hakuwahitaji lakini ni kama hakujisikia huru mbele ya Yezi na kuhusu Clark ni kwamba muda wote yupo bize na maswala yake ya kisayansi , alikuwa akifanya kazi bila ya kupumzika na msaidizi wake Grace.
Roma alilewa na marafiki zake wanajeshi ambao walifika kisiwani hapo kwa ajili ya kumtembelea , siku ya tatu wakati akirudi ngomeni moja kwa moja alienda hadi chumba cha Master ambacho analala Edna na alimkuta Edna akiwa bize kusoma nyaraka ambazo zimetumwa na Recho.
Alikuwa amevalia Lace blouse kama gauni hivi fupi la kulalia , na alikuwa ameupa mlango mgongo.
Roma aliekuwa amesismama nyuma yake aliweza kumwangalia mrembo huyo kuanzia chini mpaka juu na namna ambavo shepu ilivyojiachia kwenye kiti.
Roma aliishia kumeza mate mengi huku akimsogelea na kisha akamkumbatia kwa nyuma huku mkono wake ukitambaa kwenye mlima wa manyonyo yake.
Edna aliishia kutoa nywele zake ndefu ambazo zimemfunika uso na kumwangalia usoni.
“Nenda kalale kwenye chumba kingine , Lanlan anataka kulala na mimi”
“Aa.. Honey acha hizo basi , Lanlan anaweza kuja muda wowote tu kwani sio kwamba kuna utundu nitakufanyia , si itakuwa vizuri kama sisi wote watatu tukilala kitanda kimoja”Aliongea Roma huku akiminya minya na kufurahia manukato ya mke wake.
Edna alionekana kushindana na msisimko aliokuwa akisikia na aliishia kufumba macho na kulamba lipsi na hatimae alijitahidi na kuondoa mkono wa Roma kwenye nyonyo lake.
“Inatosha bwana , nina jambo muhimu nataka kuongea na wewe”
Roma alishangaa kidogo na aliishia kuweka tabasamu la kihuni kwenye uso wake.
“Jambo gani la usiriasi , ni kweli Mama alikupigia simu tena ? ,kuna kitu ameongea ambacho hakijakufurahisha , usiwe na wasiwasi siku zote lazima kuwe na migogoro na mama mkwe na mke ,
nadhani ni sahihi kwake kuwa na wasiwasi kwasababu tumeamua kukaa nje ya nchi , kesho nitaenda kumtembelea na Lanlan”
“Sio kuhusu mama …”Aliongea huku akionyesha ishara ya wasiwasi kwenye macho yake na aliishia kung’ata lipsi zake huku akionekana kama mwanamke ambaye anatafuta ujasiri.
“Ni kuhusu mheshimiwa Jeremy?”
Roma mara baada ya kusikia kauli hio tabasamu na hali ya utani ilimpotea palepale.
“Nini kuhusu Jeremy amekuambia nini awamu hii?”
Edna mara baada ya kuona muonekano wa Roma alijua kabisa hakuwa katika hali ya matani tena.
“Alitaka nikuambie kwamba mkuu wa miliki ya
Panas… anataka mkutane kwa siri . sasa nawaza kama unaweza kufanya hivyo kwa ajili yangu , wewe mwenyewe ndio utachagua mahali na muda”
Roma alishangazwa na jambo hilo mkuu wa miliki ya Panas anataka kukutana na yeye , ilikuwa sio kawaida kwa wakuu wa majini kutaka kuonana nae katika ulimwengu wa kawaida.
“Edna umesema nifanye hivyo kwa ajili yako , hilo limekuja katika moyo wako mwenyewe au amekulazimisha uongee hivyo mbele yangu?”
“Kauli yangu italeta utofauti wowote hata nikibaadilisha?”
“Ndio , kama wewe ndio umeamua hivyo kwa utashi wako nitaenda kukutana nae kwasababu siwezi kukataa ombi la mke wangu lakini kama ni Jeremy ambaye anajaribu kuchukulia kwa faida uhusiano wetu ili nikutane na nao sitoenda sitaki kuonana na mtu ambaye hawezi kuwa rafiki yangu , ni aidha nisiwe kabisa na uhusiano nae au nimuue kabisa , maana majini sio wa kuaminika kabisa siku zote wana ajenda zao za siri”
Edna aliishia kumwangalia mwanaume wake huku akiwa amezuia pumzi , sekunde kadhaa mbele alitoa tabasamu kana kwamba kuna mzigo ametua.
“Kama ni hivyo basi usiende , nitampatia jibu ake na usisumbuke kwa ajili yangu”
“Kwani kuna haja ya kuendelea kuwasiliana nae .. kwanini usiache kabisa kudili nae tena?”
“Kwasasa naona ni sawa tu .. siwezi fanya kitu cha kijinga ninao uwezo wa kufanya maamuzi”
“Yule mwanaume Jeremy sio mtu wa kuaminika kabisa , ni mtu ambaye haoni tatizo kuitelekeza damu yake… wasiwasi wangu ni baadae kukuumiza”Aliongea Roma hakuacha kufikiria namna mwisho wa Kizwe na Desmond ulivyowafika.
Edna aliishia kuinamisha kichwa chini bila ya kuongea chochote na Roma kwa wakati huo alijua hata kumshauri hakuna maana na ambacho anapaswa kufanya ni kumlinda pekee.
Kwasababu ya jambo hilo Roma alikosa mudi kabisa na baada ya Lanlan kufika na nguo zake za vidoti doti kwa ajili ya kulala alimlaza kitandani na kisha aliondoka.
Roma mara baada ya kutoka nje alienda kusimama juu kabisa ya ngome hio akiangalia mwezi angani , alikuwa na wasiwasi pengine kuna mtego Jeremy na familia yake ya majini wana kitu wanamwandalia.
Wakati akiangalia mandhari ya kisiwa hicho macho yake yalitua upande wa kilomita moja kutoka alipo na kuona mwanga na kumfanya kutoa tabasamu , ilikuwa ni maabara ya Clark ilioanzisha hapo rasmi ilikuwa ikitoa mwanga ikionyesha Clark hakuwa amelala bado.
Palepale alikumbuka alikuwa na maswali kwa Jiniasi huyo hivyo alielekea moja kwa moja upande huo , mara baada ya kuona hakuna mtu nje ya jengo hilo anaeangalia palepale alikwenda kutua katika floor ya kwanza na kuanza kutembea kupandisha juu
Jengo hilo lilikuwa ni la Ghorofa saba kwenda juu na mbili kwenda chini ya ardhi na ni floor moja tu ambao ndio hutumika kama makazi na floor zote ni maabara na maktaba.
Yaani kila floor ilikuwa ikihusiannisha tafiti zake , kulikuwa na vifaa vingi vya ajabu ndani ya eneo hilo ambavyo Roma aliamini hata wanasayansi wanaweza wasijue namna ya kuviendesha kutokana na ukisasa wake.
Hio ilikuwa ni Hazina ya Clark , wasichana wa umri wake wanapenda kuwa na mapochi ya brand kubwa au kumiliki vito lakini mapenzi ya princess huyo ni tofauti kabisa.
Kwa namna ambavyo jengo hilo lilivyo ilionyesha Clark alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kuhamishia maabara hapo lilikuwa ni jengo ambalo hata madirisha yake hayakuw aya kawaida na ambayo yamefunwa kwa nje lilionekana kama boksi la kioo.
“Teacher the accelerator has reached the critical point of the force field..”
“What is the conversion efficency?”
“99.99% and above “
“Cordinates checked , start the countdown ..”
“Yes 5,4,3,1!”
Roma ambaye alikuwa ndio anafika floor ya juu kabisa ya jengo hilo ndio maneno ambayo alikuwa akisikia na alijiuliza ni nini hicho wanafanya au wanataka kurusha roketi kwenda angani.
Kidogo tu adondoke mara baada ya kuona hicho ambacho walikuwa wakifanya .
Katikati ya maabara hio kulikuwa na Silinda ya rangi
nyeupe kama darubini kubwa hivi ambayo inaangaliana na anga.
Boriti ya mwanga hafifu kama wa Laser ulitoka katika silinda ile na kuelekea angani.
Roma alishangazwa na jambo lile ijapokuwa hakujua ni nini lakini uwezo wake ulihisi mwanga huo haukuwa wa kawaida kabisa kutokana na nguvu yake ya kutisha.
Baada ya mwanga ule kufifia maabara hio ulirudi katika mwanga wake wa kawaida na ndio sasa Roma aliweza kumuona Clark na Grace wote wakiwa wamevalia mamiwani makubwa ya kujikinga na mwanga.
“Mwalimu kulingana na taarifa , ni kiasi cha 0.1 Attometer nje ya Accuracy ya tageti ,tumefikia malengo”Aliongea Grace huku akionyesha furaha.
Clark ambaye alikuwa upande mwingine kwenye mavazi ya kimaabara alivua miwani yake ile kubwa na kionyesha tabasamu usoni na ndio muda ambao aligeuzia macho yake na kumwangalia Roma.
“Grace umefanya kazi nzuri leo , unaweza kwenda kupumzika sasa nitamalizia palipobakia”
Grace pia alikuwa ashamuona Roma na kwa hali ya aibu kidogo alipita na kuanza kushuka kuelekea chini mara baada ya kuwatakia usiku mwema.
“Inaonyesha ulichagua mwanafunzi sahihi , anaonyesha kuridhika kabisa na utafiti mnaofanya”Aliongea Roma sasa akitembea kuelekea katikati ya maabara hio.
“Grace alikuwa akipenda maswala ya kitabibu mwanzoni lakini nilikuja kugundua ana kipaji cha kuwa mtafiti ..”Aliongea huku akivua gloves na kuzitupia kwenye dustbin na kisha akamsogelea Roma.
“Honey kujitokeza kwako usiku usiku kwenye muda kama huu sio kama wewe vile”
“Hebu tusiende huko kwanza , niambie kwanza mlichokua mkifanya hapa ni nini , mbona
inaonekana kama siraha yenye nguvu hivi?”Aliongea
Roma na Clark alianza kushika ile silinda kana kwamba anaparaza kwa kuoneysha ni kitu cha thamani.
“Huu ni utafiti ambao nilikuwa nikifanya kwa nusu mwaka mpaka sasa ni teknolojia ambayo nimeipatia jina la Cumberbatch Particle lightbeam Cannon’ unaiuonaje si inapendeza kwa kuangalia tu”
“Kupendeza tena?”
Mara baada ya kuelewa anachotaka kuongea Roma aliishia kutingisha kichwa huku akitabasamu.
“Inaonekana kupendeza sana”
Mara baada ya kupewa sifa na Roma macho yake yalionyesha furaha na kuanza kumuelezea Roma kuanzia Wazo la kimuundo , fizikia , mekanikia na nadharia za kimahesabu.
Roma alishangazwa na maneno ya Clark na mara baada ya kuona Clark anaenda mbele katika kuelezea vitu ambavyo vinamuumiza kichwa alimzuia asiendelee.
“Clark kuhusu hiki kifaa…. Kwanini usiende moja kwa moja na kuniambia inahusiana na nini na kazi yake ni nini au ni siraha ya kuua watu?”
“Kuu watu tena?”
“Unaweza kuwa sahihi kwani inaweza kuua lakini nimeitengeneza kwa ajili ya kuzuia vimondo na
Magimba kwa ajili ya spaceships hapo baadae”.
“Hebu rudia”
Roma alikuwa katika mshangao na kujiuliza kwanini maswala ya Spaceship tena.
“Alichosema Hawking ni sahihi , kuna mamilioni ya sayari angani , katika mtazamo wa kitakwimu uwepo wa viumbe tofauti na sisi binadamu ambavyo vipo vinaishi katika Cosmos havihesabiki bila hata ya kwamba hakuna viumbe kutoka sayari nyingine ambao wamegundulika mpaka sasa ukiachana na the gods , hiyo kama Alien wakitupata sisi kabla ya sisi kuwapata inamaanisha sisi bindamu ambao hatuna hata uwezo wa kupeleka kiumbe kwenye sayari ya Mars tutakuwa hatarini , kama mwanasayansi mchango mkubwa ambao anaweza kutoa ni kuwezesha binadamu kutoka duniani na kwenda kuishi katika sayari nyingine ili kulinda jamii yetu , imethibitishwa kwamba binadamu atafikia katika nyakati za Galactic kipindi ambacho tutakuwa na uwezo wa kusafiri kutoka sayari moja kwenda nyingine kwa urahisi tofaut na kusafiri bara moja kwenda bara lingine, sasa kama ni hivyo tunaweza kukutana na vitu kama Magimba , vimondo na mambo mengi hatarishi , sasa ndio wakati ambao kifaa hichi kitaingia katika matumizi , pili binadamu hawezi kusafiri kwenda sayari nyingine akiwa na mizigo mingi , hivyo niliona itakuwa sawa kama nitetengeneza siraha ambayo msingi wake ni
particle light beams, ni sawa na siraha ambazo
unaona kwenye muvi za sayansi fikirishi. Ofcoz hapa nimefanya mjaribio tu haimaanishi kwamba nimeshakamilisha , kama tutataka kutumia katika spaceship tutahitajika kujenga particle accelarotor kubwaa na ongezeko la sayansi itakayofiti muda huo , kukuelezea kwa kifupi ni kwamba sio ngumu kutengeneza siraha kwa kutumia hii Prototype, ninachojaribu kugundua ni kwamba ni namna ipi naweza kupata nishati yenye usanifu wa hali ya ambayo itatumika katika anga za mbali , lakini hilo sio tatizo kwasasa kwani naamini nikiendeleza juhudi nitapata majibu hata miaka mitatu ijayo?”
Roma mara baada ya kusikia maelezo hayo macho yake yalionyesha kutokuamini na kujiuliza hiko kitu kina uwezo wa kuharibu kimondo au magimba , kwahio inamaana kama nguvu yake itaongezeka ni kwamba risasi yake moja itaweza kusabaratisha mji,
“Bora tu mimi ndio mwanaume wako vinginevyo dunia itakuwa katika hatari kama dunia itakuibia tafiti zako hizi za hatari”
“Usiwe na wasiwasi mpenzi , najua mwisho wangu, katika kila vifaa hatarishi nilivyotengeneza nimeweka itifaki za ki usalama ngumu sana kuzijua , ukilazmisha tu inamaanisha unaharbu kabis kifaa hicho , hivyo hata kama mtu akiiba tafiti zangu itakuwa ni bure kabisa , hakuna mtu ambaye anaweza kuiba tafiti yangu na ikawa na maana kwake au kudukua mifumo yangu , ukweli ni kwamba hajawahi kutokea mtu wa aina hio ambaye anaweza kushindana na mimi ni Profesa Shelukindo na Yan Buwen pekee ndio waliokuwa wakinifikia, nimemkumbuka Yan Buwen sana alikuwa ni mwanasansi mwenye akili sana kuwahi kuwepo” “Sitaki hata ujaribu kumkumbuka , mwanaume pekee ambaye anatakiwa kutokea katika mawazo yako ni mimi tu”
Aliongea Roma huku akikaa katika kiti kilichokuwa wazi na kisha akamruhusu Clark kumkalia kwenye mapaja.
“Clark nina kitu ambacho siku zote nilitaka kukuuliza”Aliongea kwa namna ya kumnong’oneza sikioni na msisimko alioupata Clark ulimfanya kujihisi aibu na kuwa mwekundu kama yai.
“Niulize”
“Miezi kadhaa iliopita nilipokuwa Korea mara baada ya kukutana na Athena alisema sielewi msingi halisi wa nadharia ya kanuni za anga ni nini ,na pia alisema katika Anga hakuna ‘force’ kauli yake hii imenifanya kutokumuelewa kabisa , sasa kwasababu wewe ni mtaalamu wa maswala ya fizikia na unajimu kwanini usinielezee ni nini amemanisha kusema Angani hakuna ‘force’”
mimi nilijua ndo inaisha baada ya roma kupata nguvu0688151346 WATSAPP ONLY ITAENDELEA JPILI
OkNILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

Tafadhari bro sikiliza sisi wanaume wenzako wa jf ndo tutakupa heshima za mwisho.Umesema wewe Madam , mimi ni nani hata nisikutii
nimekuwa nikiona silaha nyingi sana ila ya utupu wa mzimu wa nebula nimecheka sana![]()
Tulia basi![]()
Ila nimecheka sana pale mage alipoambiwa na yeye ana uasili wa majini mbweha akauliza sasa na yeye anaenda kuota mkia na masikio?????[emoji23][emoji23][emoji23]Tulia basi
Nimecheka sanaNi Amina sio Mage
Umesema wewe Madam , mimi ni nani hata nisikutii
Mkuu ebu acha basi ujue me mwanamke[emoji1787][emoji1787]Tafadhari bro sikiliza sisi wanaume wenzako wa jf ndo tutakupa heshima za mwisho.
achana na wamama.shusha vipande vingine kama vitatu
DuhMkuu ebu acha basi ujue me mwanamke[emoji1787][emoji1787]