NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.
MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware.
SEHEMU YA 735
Callum waziri mkuu wa Uingereza alikuwa akimjua Roma na uhusiano wake na Edna pamoja na Raisi Jeremy , idara ya usalama ya Uingereza haikuwa kwa ajili ya maonyesho tu walikuwa wakijua mambo mengi.
Lakini hata hivyo hakuwa akijua nia halisi ya Raisi Jeremy kuja mpaka hapo lakini kwasababu ni swala ambalo lilikuwa linahusiana na Roma hakutaka kuvuka mipaka yake hiyo alijitahidi kuwa makini.
“Hakika una ushawishi mkubwa Raisi Jeremy , kuja London tu umeweza kutupata mara moja?”Aliongea Catherine akionekana kumtania raisi Jeremy, licha ya kwamba hawajawahi kukutana lakini bado alionyesha hali ya kumdharau pengine ni kutokana na kutokea taifa dogo.
“Nimesikia habari za kutosha kuhusu malkia wa Wales lakini sikutegemea kukuona hapa ,nipo hapa kwa ajili ya kikao cha umoja wa mataifa kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa dunia nzima na mara baada ya kusikia habari za binti yangu na mume wake wapo hapa nikaona sio mbaya kuwatembelea”Aliongea huku akiwa na uso uliopambwa na tabasamu.
Maelezo yake yalikuwa kamilifu na ilimfanya kuonekana kama vile alikuwa na ukaribu sana na Roma pamoja na Edna.
Baada ya salamu wengine wote walitoka nje na kumuacha Roma na familia yake ndani ya chumba hicho cha VIP.
“Kama upo hapa kwa ajili ya kunifanya nikutane na mkuu wako wa miliki basi sahau maana sina mpango wa kuonana nae kabisa , kama anataka sana kuonana na mimi basi mwambie aje huku yeye mwenyewe”Aliongea Roma na kufanya tabasamu la raisi Jeremy kupotea mara moja.
“Roma kuna haja ya kuwa hivyo mbele yangu , ninaweza nikawa nilifanya makosa lakini yaliopita si ndwele na isitoshe hatuna vinyongo kati yetu , nilifanya mambo yale kwasababu ya kutaka wewe na Edna kuishi kwa furaha”
Wakati wa kuongea alikuwa akimwangalia Edna kwa sura ya kumwambia amsadie kumuomba mume wake lakini Edna alionekana kumpotezea.
“Usingekuwa hai mpaka sasa kama sio kwa uhusiano uliopo kati yako na Edna , hiyyo acha kuzunguka zunguka na sema kilichokuleta”
“Sawa nitaenda moja kwa moja , mkuu wa miliki ya Panas anataka kuongea na wewe , kama utakataa kwenda katika miliki au kwenda Rwanda yupo tayari kuongea na wewe kwa njjia ya vidio Call , ukikataa kusikiliza utakuja kujutia baadae”
Ijapokuwa ulimwengu wa kijini ulikuwa ukijitegemea lakini majini waliokuwa wakiishi huko walikuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano na ulimwengu wa nje bila shida yoyote kutokana na teknolojia ya ajabu ambayo iliasisiwa na mababu wa miliki hizo.
Kuhusu Roma hakushangazwa na maneno yake kwani alikuwa ashajua kiasi kuhusu miliki hizo za kijini hiyo aliamini ilikuwa ikiwezekana.
“Kama ni hiyo niunganishe nitaongea nae"
Raisi Jeremy alijisikia furaha na kujivunia huku akijiambia pengine Roma alikuwa akiogopa miliki ya Panas.
“Nifuate nje tutafute sehemu nzuri kama ni hiyo , kuna watu wengi hapa”
“Hakuna haja , hawa wote ni marafiki zangu na familia yangu hiyyo sio lazima kuficha kitu kwao, labda kama mheshimiwa Jeremy anaogopa kugundulika ana uhusiano na majini?”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchokozi.
Baada ya kusikia maneno hayo hakutaka kusita tena na alitoa kishikwambi cha aina yake na alianza kukipangusa na ilionekana Panas walikuwa washajiandaa muda mrefu kupokea simu hio.
Sura ya jini Gefu iliweza kuonekana katika kioo cha kishikwambi hicho na alikuwa ndani ya ofisi yake.
“Sir, Mr Roma Ramoni yupo hapa tayari kwa kuongea na wewe”Aliongea Jeremy kwa sauti ya unyenyekevu huku akiwa amepamba uso wake na tabasamu.
“Sikutegemea kukutana kwetu kwa mara ya kwanza kutakuwa kwa namna hii , Roma hakika ni ngumu sana kukupata”Aliongea Gefu akiwa na tabasamu.
“Oh! Kumbe mkuu wa miliki ya Panas ndio upo hiyyo ..”Aliongea Roma lakini upande wa pili Gefu hakuelewa Roma anachomaanisha.
“Nilikuwa na haja ya kuonana na wewe kwa haraka kwasababu nina jambo muhimu napaswa kukuambia linahusiana na usalama wako na wanaokuzunguka”
“Unajaribu kumaanisha kuna kundi la majini ambao wanataka kuniua muda si mrefu?”
“Ndio , kwasasa ni kama unatembea juu ya barafu nyembamba, lakini sio tu kwmaba najua maadui zako wote lakini pia nipo tayari kukusaidia”
“Haina haja , sijakubaliana kuongea na wewe ili kusikia unaongea upumbavu”
“Nini!!. Roma unamaanisha nini kuongea hivyo au huamini maneno yangu?”
“Sio maswala ya kuaminiana, mimi nilitaka tu kujua mkuu wa miliki ya Panas anaonekana ipi ili nikiivamia miliki yenu nisipate shida ya kukutafuta na kukuua”
Ishara ya hasira iliweza kuonekana katika uso wa Gefu mkuu wa miliki ya Panas lakini fasta sana alirudi katika hali yake.
“Kijana mdogo chunga kauli zako naamini haipaswi kuwa na ugomvi kati yetu”
“Nyie ndio mliovujisha taarifa ya Rufi kuishi Tanzania kwenda kwa miliki ya Xia , hio ni sababu tosha ya mimi kutaka kuivamia miliki yenu na kulipa kisasi kwa umbea wenu”Aliongea Roma bila ya ishara ya utani.
Maneno yake ya kibabe yalimshitua Master Namba nne huku akijiuliza Roma alijuaje yeye ndio alivujisha taarifa.
“Kwa muonekano wenu inaonyesha nilikuwa sahihi , kama ifahamikavyo ukuu wa miliki ya Panas katika kujua kinachoendelea kwenye ulimwengu wa kawaida”
Upande wa Gefu alijua Roma hakuwa na ushihidi hivyo hakutaka kukamatika kizembe na alijua pengine Roma anamjaribu.
“Unathubutu ipi kunijaribu wewe bindamu?”
“Kwahio unatakaje?”
“Unafikiri tunakuogopa , tunakupatia nafasi ya mwisho ya kuungana na Panas, kwasasa umekuwa adui wa miliki ya Xia ,Kekexil na Braki , unadhani kujificha huko nje ya nchi kunaweza kukufanya ukawa salama na miungu wenzako dhaifu kukusaidia?”Aliongea kwa kufoka.
“Braki!!!”
Roma sura ilijikunja mara baada ya kusikia anahusishwa na Braki na kujiuliza Braki ndio kitu gani lakini Gefu alionekana kujua kinachoendelea kupitia sura ya Roma.
“Unajisikiaje kutokujua baadhi ya maadui zako?”
Roma hakujibu swali na badala yake palepale alipiga chini kile kishikwambi na kupasuka pasuka vipande vipande.
“Siogopi kiumbe chochote mimi , kama kuna adui anajiona mbabe anitafute tumalizane”Aliongea Roma na palepale macho yake yalisinyaa wakati wa kmwangalia Jeremy.
“I am not in a good mood , so get lost now when I still give a damn about your relationship with my wife”Aliongea akimaanisha aondoke wakati anajali uhusiano uliopo kati yake na mke wake.
“You .. you are Vexing … kwa ajili ya Edna!?, Roma nataka nikupatie ushauri … sisi binadamu tunao wajibu wa kufuata sheria za hii dunia , kila mtu yupo chini ya sheria na kila mtu atakushambulia kama utazivunja kutokana na ukiburi wako na wakati hayo yanatokea hakuna ambaye atakusaidia”
Baada ya kuongea kauli hio palepale licha ya kuwa na hasira zake aliondoka ndani ya eneo hilo , kwani alijihisi kutamani kumuua Roma ni hivyo tu uwezo huo hakuwa nao.
Mara baada ya kuondoka Roma alisimama na kusogelea dirisha na kuangalia upande wa uwanjani ambako mechi ilikuwa mapumziko , huku hali ya hewa ikiwa sio ya kawaida ndani ya eneo hilo kwani watu wake wa karibu wote walionekana kuwa na wasiwasi.
Bila kujua Roma alikuwa amejiongezea adui mwingine ambaye hamfahamu anaefahamika kwa jina la Braki.
Ukweli ni kwamba alikuwa na maadui wengi ambao hakuwa akiwajua na baadhi yao walitokana na wanawake wake na wengine walikuwa wakimchukulia kama adui kutokana na kuwa na uwezo mkubwa.
“Rufi unajua chochote kuhusu miliki ya Braki?”Aliuliza Roma mara baada ya kujituliza.
“Sijawahi kuisikia , Nanny ushawahi kuisikia?” Rufi alionekana kutokukujua na alimtupia swali Sui lakini hata yeye alionyesha kutokujua chochote.
Ijapokuwa ilikuwa ikihusiana na ulimwengu wa majini lakini kutokana na ukawaida wao hawakuwa wakiijua.
“Mimi nadhani Braki inahusiana na familia ya Mzee Sharif , si ulisema walishawahi kuleta majini wengi kupambana na wewe , nadhani tufikirie hivyo kwa sasa?”Aliongea Rose na Roma alitingisha kichwa baada ya kuona alikuwa na pointi .
“Hubby unataka kweli kwenda kuivamia miliki ya Panas?”Aliuliza Edna ambaye alikuwa amekunja sura.
“Hautaki niende?”
“Nili…”
“Edna siwezi kukusikiliza awamu hii , kila kitu kingekuwa sawa lakini katika vitu ambavyo vinahusisha uhai wa wengine sitokuruhusu ubadilishe mawazo yangu”
Edna mara baada ya kuona usiriasi uliopo katika macho yake alishia kuvuta pumzi na kuzishusha.
“Sijasema nataka kukuzuia , nikwamba naona itakuwa hatari sana”
“Tatizo hata kama niseme nisiende kuwavamia na kuwasambaratisha najua hawawezi kutulia na watatafuta tu namna ya kutaka kuniua … Hili ni daraja ambalo napaswa kuvuka na nikishapita kila kitu kitakuwa kimekwisha”Aliongea.
“Roma sidhani kama itakuwa ni rahisi, tayari tuna uadui na miliki tatu za kijini kubwa na tuna maadui maelfu na maelfu , unadhani ni sawa kuua na kuendelea kutengeneza maadui? , mimi naona labda hakuna haja ya kuua na tunaweza kutatua haya matatizo kwa njia nyingine , wao wanasheria zao pia na pale wanapojihakikishia kwamba huwezi zivunja hawawezi kukufanyia chochote”Aliongea Sophia.
“Sophia unaongea ujinga , hivi unajua tafsiri ya sheria mbele ya watu wenye nguvu ni tofauti na inavyotafsirika mbele ya watu dhaifu?”
Aliongea Roma na kisha alinyoosha kidole kuelekea uwanjani wakati wachezaji wakitoka katika vyumba ya mapumziko kwa ajili ya kuanza kwa kipindi cha pili.
“Hivi unajua ni kwasababu gani mpira wa miguu ni maarufu sana duniani na kwanini watu wengi kama hivi wanaupenda?”
Wanawake hao wote waliishia kushangaa tu wasiweze kuelewa swali lake,walijiambia wanaongea topiki ya hatari hiyo kuna haja gani ya kuhusisha mpira wa miguu lakini Roma alionekana kutojali mawazo yao.
“Ni kwasababu katika mechi ya mpira haijalishi timu ni bora kiasi gani au ni dhaifu kiasi gani lakini siku zote matokeo yanaanza sifuri kwa sifuri na mpira unachezwa kwa sheria, hii inamaanisha kwamba haijalishi timu ni dhiafu lakini kama watakuwa tayari kupambana katika kukaba kukimbia na kufunga hata wao pia wanaweza kuwa mabingwa , kwa maneno mengine hapo ndio wakati watu ambao sio wachezaji ndio wanajipatia riziki , sehemu ambayo uvumiliu wao huonekana , katika uwanja mshindi ndio bingwa hata kama ni dhaifu au alipendelewa kwa namna yoyote ile ili mradi tu ameifunga timu bora na yenye nguvu hata kama ni mara moja katika historia yake , hii inamaanisha kwamba wao pia wanayo nafasi ya kuwa nyota na hii ndio maana mpira wa miguu ni wa kuvutia sana”Aliongea na kisha akavuta pumzi na kuendelea.
“Lakini unadhani hio ni sawa kati ya wachezaji na wamiliki wa timu au wasimamizi wa mashindano? , ingawa mechi inaanzia sifuri kwa sifuri lakini kwa matajiri na wasimamizi wa UEFA mambo ni tofauti , kwao haijalishi nani anashinda bado watapiga pesa na kupata faida na ipo hivyo siku zote , kwa mfano mchezaji katika timu kama akishindwa kutoa ushirikiano wa maelekezo viongozi wanaweza kuto kumjumuisha katika mechi na kutoa sababu kama vile ni majeruhi au haendani na mfumo na mengineyo .. ,kwa lugha nyepesi ni kwamba wanaoendesha michezo na timu ndio wenye maamuzi ni taarifa gani iwafikie mashabiki na kuamua mchezo uwe vipi , unaweza kuona mechi kabisa hii mshindi ni wa kupangwa lakini wewe kama shabiki utafanya nini tofauti na kuongea ongea na kugoma, hakuna cha ziada ambacho unaweza kufanya kwasababu kwa nje wewe unaburudika na wachezaji wakicheza mpira lakini kwa ndani kuna mfumo ambao umetengenezwa kwa ajili ya kurahisisha maswala mengi aidha yawe ni ya kifedha au Ajenda zao za kijamii labda tu kama watu waache kuangalia mpira .. na huu ni mfumo endelevu na utaendelea hivi labda siku tu watu dunia nzima waseme hawaangalii mpira tena , sasa hili halipo kwenye mpira tu kila michezo maarufu yote wewe kama shabiki utaona ni burudani lakini nyuma ya pazia kuna mfumo..”
“Ndio inaweza kuonekana yanayofanyika ni uchafu lakini maisha ya kibinadamu tokea mwanzo yalianzia katika uchafu , sasa tuseme mimi ni kama mchezaji , Kocha au tuseme timu nyenye nguvu ambayo imepata umaarufu hivi karibuni, viongozi waandamizi na matajiri wote macho yao yatakuwa kwangu kwasababu mbili tu; mosi nifanye kazi kwao na niwasaidie kupata pesa au kutimiza ajenda zao , pili hawataki niwasaidie wengine kupata pesa, kwa maneno mengine ili nipate faida lazima na wao wapate faida na sasa hapa hizi ndio sheria ambazo wameweka ambazo hawataki mchezaji kuzivunja kwasababu zinaathiri utajiri wao pamoja na ushawishi wao”
“Kama nitafanya kazi nzuri kama mchezaji wataniacha niendelee kuishi kama mchezaji na kunifanya niendelee kuwa maarufu na watanipatia Ballon d‘or au Kiatu cha Dhahabu au watafanya hata timu yangu ya taifa kuwa bingwa wa dunia au club yangu kuwa bingwa wa UEFA na kama sitofanya vizuri au nikikataa matakwa yao watahakikisha wananizimisha aidha kwa kuniundia mchezaji uwanjanni ambaye atanijeruhi au kuanza kunitengenezea Zengwe nyingi tu ili kunitoa mchezoni hizi ndio sheria ambazo wameweka .. wakati nikiwa chini hawakuwa na habari na mimi na hawakuwahi kunichukulia siriasi lakini sasa nimekuwa tishio kwao hawataki kuzembea, hii haipo kwenye mpira tu kwa kila nyanja kuna huu mfumo na ambao wanasuka mipango hii ya kimfumo hawatojionyesha kamwe mpaka sekunde ya mwisho , isitoshe lazima wahakikishe mchezo ulikuwa ni wa haki”
Kila mmoja alijikuta akiwa kimya na kuangalia uwanjwani ambako mechi ilikuwa ikiendelea.
Maneno ya Roma yanaweza kuonekana kama yamebase upande mmoja lakini yalikuwa yamejaa ukweli mgumu(Harsh truth).
“Ijapokuwa hatuwezi kushiriki katika vita yako lakini kama mtu ambaye unapambania maisha ninaelewa hisia zako”Aliongea mmoja wapo na kumfanya Roma kuonyesha shukrani na palepale alimbeba Lanlan na kumpakata.
“Sina chaguo nyingine , kwasababu mpaka sasa hawaniangalii kama mtu Dhaifu , kama ninataka kuendelea kuishi ni aidha nishirikiane nao au kama sitaki kushirikiana nao niwaweke chini yangu kwa kuwapiga na kisha kuweka sheria zangu mimi”Aliongea na kisha aligeuza macho yake na kuangalia warembo wake waliokuwa wakimwangalia kwa macho ya matamanio na kisha akageuzia macho kwa Lanlan.
“Sio mimi tu lakini ni kwenu pia na kwa mtoto wangu”Aliongea Roma kwa sauti hafifu akionekana kama vile ni mtu ambaye anakumbukia maisha yake yaliopita na kitendo kile kilimfanya Blandina kukosa ujasiri wa kuendeea kusikiliza na machozi yalimtoka na kwenda kumkumbatia Roma na Lanlan na kuanza kulia.
Kila mmoja alijua hisia za Blandina zinatokea wapi , ilionekana alikuwa na hatia kama mzazi na kumfanya mwanae kupitia magumu mengi lakini kwa wakati huo machozi yake hayakuwakilisha huzuni tu lakini bali kujivunia kwa mafanikio ya mtoto wake.
Ukumbuke hapa ni ndani ya Chumba cha VIP ndani ya uwanja wa Wembley hivyo ni kama wamejitenga na mashabiki wengine.
Unadhani Roma yupo sahihi , ni kweli kuna mifumo ambayo imewekwa kwa ajili ya kushikiria mafanikio ya watu??
SEHEMU YA 736.
Ni upande wa Tanzania jijini Iringa muda wa mchana katika makazi ya Afande Kweka kulikuwa na kikao cha siri kilichokuwa kikiendelea.
Kikao hichi kilikuwa kikijumuisha watu kama saba hivi ambao ni Paster Cohen, Mellisa , Phill Knight , Nadia Alphonso , Suzzane , Linda na mwanamama mrembo kutoka Hungury afahamikae kwa jina la Zoe Kovacic.
Nadia ndio ambaye alikuwa akionekana kusoma ripoti licha ya kwamba kila mmoja ambaye alikuwa hapo ndani alikuwa ameshikilia kishikwambi, ilionekana ni kama vile walikuwa wakirudia kile ambacho Nadia alikuwa akisoma.
“Mzee kama mwanachama mkongwe wa jamii yetu, viongozi wameniagiza nikuelezee kuhusu ubini wa kiongozi wetu”Aliongea Mellisa kwa lugha ya kingereza.
“Kiongozi amekwisha kupatikana?”
“Ndio Komredi katika kikao cha mwisho kilichofanyika Saudi Arabia tumeweza kupata mawasiliano na Kiongozi kwa mara ya pili”Aliongea Pastor Cohen na kumfanya Nadia kuangaliana na Suzzane.
“Kulingana na Kalenda ya jamii yetu kiongozi alipaswa kufanya mawasiliano na viongozi wa juu ndani ya tarehe husika , ijapokuwa ilikuwa ni hatua ya pili ya kumthibitisha kama kiongozi, umoja umefurahi kwamba mpango A wa kalenda ulitimia na kwanzia tarehe hio Edna Adebayo anatambulika kama kiongozi wa Umoja wa Ant-Illuminat”Aliongea Mellisa na kumfanya Linda kuonyesha mshangao huku Afande Kweka yeye macho yake ya kizee yakichanua.
“Komredi ni kama tulivyotarajia”Aliongea Pastor Cohen.
“Kuna maswali mengi juu ya hili Komredi nilijua kiongozi ni Seenteen kulingana na maelezo yako Komred”
“Wote tulidhania kiongozi anakwenda kuwa Seenteen, kuna maswali mengi juu ya hili lakini kulingana na maelekezo ya mwasisi wa umoja wetu anasema Kalenda inakwenda kujibu maswali yote lakini ni Aidha kama Binadamu tutafanikiwa kuishinda vita na Miungu”.
“Viongozi wengi pia hawakuamini kama siku ya kikalenda Edna angefanya mawasiliano na sisi lakini ajabu alifanya hiyo na kila mmoja alishangaa lakini imeondolea umoja harakati za kuona mchoro wa Unabii?”
“Huu mchoro wa Unabii unaonyesha kitu gani , kwanini imekuwa kitu muhimu kwa pande zote mbili Mellisa?”
“Hatuwezi kujua kwa uhakika mchoro huu unamaanisha nini na nani anaonekana katika picha lakini makisio yetu ni kwamba mchoro huu unahusiana na kiongozi wa umoja wetu”
“Kwa taarifa za Shekh Assad ni kwamba mchoro huu pia una umuhimu kwa Illuminat na ndio kiongozi ambaye wanamsubiria, kama usemayo ni sahihi Edna ana uhusiano na huu mchoro wa unabii lakini si inamaanisha kwamba pia ndio kiongozi wao ambaye wanamtarajia kulingana na unabii?”
“Upo sahihi Zoe lakini kwasasa hata Illuminat wenyewe bado hawajaweza kuona mchoro huu wa Unabii kwani upo chini ya Vatican”Alijibu Mellisa.
“Madam kuna uwezekano wa Edna kuwa Seventeen?”Aliuliza Nadia.
“Kulingana na mpango ulivyokuwa , Seventeen ni zao la mpango LADO kama alivyo Roma Ramoni lakini majukumu yao tokea mwanzo yalikuwa ni tofauti , ijapokuwa mpaka sasa hivi hatujui Seventeen yupo hai chini ya Zeros lakini tokea mwanzo Seventeen ndio alikuwa ni msingi wa kufanikiwa kwa Ant-Illuminat”
“Kama ni hivyo kwanini Edna ndio awe kiongozi , sijawahi kuona ishara yoyote ya Edna kujua chochote kuhusu Ant- Illuminat?”Aliongea Suzzane.
“Ukweli ni kwamba tunaamini Seventeen amekwisha kufariki mpaka sasa chini ya maagizo ya Athena na kwa maelezo ya Chriss ili mchoro wa unabii kukidhi vigezo vya ki’unabii hakupaswi kuwa na uwepo wa watu wawili wenye sura zinazofanana”Aliongea Mellisa.
“Melllisa hili linajibu kilichopo kwenye mchoro huo wa Unabii , kama kweli maneno ya Chriss ni sahihi basi kuna uwezekano Mchoro wa Unabii unaonyesha sura ya Edna au Seventeen lakini kwasababu ni unabii wa mtu mmoja basi moja kwa moja mmoja wapo lazima atoweke”
“Naunga hoja ya Komredi lakini kwangu bado swali linaibuka Athena ni nani na kwanini mchoro wa Unabii kuwa na sura ya Edna , wote kati yetu tunajua mpango wa Athena ni nini zidi ya binadamu na hatari ya mipango yake kufanikiwa?”
“Afande mpaka sasa hatuwezi kujibu maswali lakini pia hatuwezi kufanya makisio kwani ipo kalenda ambayo inatuongoza ambayo haijawahi kufeli na hata pale ilipofeli kulikuwa na mpango B, nadhani wote tuamini katika Kalenda”
“Naunga hoja ya Mellisa akini je wakuu wanasemaje kuhusu hali inayoendelea kwa sasa?”Aliuliza Phill.
“Unazungumzia kushuka kwa joto la dunia?”Aliuliza Zoe na kufanya kila mmoja kumwangalia mwenzake kwa shauku kubwa ya kusikia jibu.
“Kulingana na Kalenda tukio muhimu ambalo ndio ishara kubwa ya hatua muhimu ya Athena kuchukua lakini vilevile hatua ambayo Umoja wetu unapaswa kuchukua ni kuona majira ya theluji katika bara la Afrika, nadhani hali hii ya hewa tunaelekea kuona ishara hii hivi karibuni hivyo tunaweza kusema mpaka sasa tunaingia katika hatua muhimu sana katika umoja wetu na kwa dunia kwa ujumla , hiki ndio ambacho viongozi waeniusia nikiseme katika kikao hichi na sio hapa tu dunia nzima vikao vya ajenda hii kwa wenzetu vinaendelea”Aliongea Mellisa.
“Mellisa yupo sahihi kushuka kwa joto la Dunia sio nchi moja bali ni dunia nzima lakini ni Afrika pekee ambayo inaonyesha joto kupungua taratibu sana , hii inamaanisha mpaka nyakati za theluji zikitufikia kuna uwezekano baadhi ya maeneo ya Dunia joto kushuka sana kiasi cha kuathiri maisha ya binadamu”
“Nadhani ndio maana Wanachama wengi wa Freemason na Illuminat wamenunua maneo mengi ndani ya Afrika kwa kipindi cha hivi karibuni huku wakifosi sheria nyingi za kimataifa kupitishwa , hii inaonyesha walikuwa wakiandaa mazingira rafiki kwa ajili ya kuishi wakiwa huru”Aliongea Zoe.
“Hii ni kweli na ni swala ambalo tulikuwa tukipambana nalo kama umoja,kuna baadhi ya mataifa ambayo tumeyachagua kama nguzo muhimu ya Umoja kwa ajili ya kulinda tamaduni zake ikiwemo Tanzania lakini kuna maeneo ambayo pia ndani ya Afrika yapo chini ya Illuminat na ushawishi wao ni wa juu na hili hatuwezi kulifanyia kazi kwani litaibua migororo”
“Nadhani naona unachojaribu kumaanisha Miss Mellisa , ni miezi kadhaa iliopita mataifa zaidi ya kumi ya Kiafrika yamepitisha sheria ya Ushoga kuwa huru hili ni swala ambalo linahusiana na ulichosema”
“Upo sahihi Linda , Tanzania ilikuwa ni nchi ambayo ingekuwa ya kumi na moja kutangaza hii sheria kama sio sisi kuingilia , shukrani kwa Suzzane na Nadia wameweza kutiisha misheni yao vizuri na sasa Tanzania imekuwa Neutral kwa sisi pamoja na wao”
“Urusi wanazungumziaje hili?”Aliuliza Afande Kweka.
“Wapo ndani ya mfumo , wanaweza kupinga wazi lakini ni taifa ambalo limegawanyika katika pande mbili”.
*******
Pumbavu zako Roma Ramoni , nitakuua tu siku moja”Aliongea Gefu kwa sauti kubwa na kwa hasira zake alipelekea kuharibu kila kitu kilichokuwa ndani ya ofisi yake lakini bado haikuwa ikitosha kutuliza hasira zake.
Mbele yake alikuwa ni Master Namba nne na mwingine mmoja ambao wote walikuwa katika hali ya wasiwasi kutokana na hasira za kiongozi wao mara baada ya kumaliza maongezi yake na Roma Ramoni.
Ilikuwa ni mara chache sana kwa Gefu kuwa katika hasira kama hizo , kitendo cha Roma kumdharau waziwazi mara nyingi mfululizo kilimfanya chuki yake kuongezeka maradufu.
“Kaka punguza jazba, ni sawa tu kama amekataa kuungana na sisi na kwasababu maadui zake ni pamoja na Braki lazima atakufa na sisi ndio tutachukua fursa hio ya kummalizia akiwa chini kabisa”
“Hawa majini kutoka Braki hawajawahi kuwepo katika uso wa dunia kwa zaidi ya milenia moja , nimesikia kutoka kwa wazee wanasema hawajui kabisa uwepo wa binadamu mwenye uwezo mkubwa kama Roma , Roma huyu mjinga amejitengenezea uadui na hawa mashetani ambao walikuwa wameshasahaulika”
“Namba nne fanya mawasiliano na Jeremy kusitisha mipango yetu yote ya kimsaada na Tanzania hususani familia ya Raisi Senga na kisha atasubiria maelekezo yangu ya mpango wa pili unaofuatia , pia tuma barua kwenda katika miliki zote zenye uadui na Roma hususani katika miliki ya Xia na Kekexil na waambie kupitia mashushusu wetu waliopo katika kila pande ya dunia ya kawaida watasaidia kujua nchi ambayo Roma anaishi na familia yake na kama wanahitaji msaada watuambie”
“Sawa kaka”Aliongea Master namba nne.
“Gegu chukua baadhi ya wazee kuelekea mlima Yoshe na mrudishe yule mtu kurudi Panas”
“Kaka namba moja sio kwamba ni mapema sana kumrudisha?”
“Fanya kama nilivyosema , vipi kama Roma akitushambulia unadhani nitaweza kuilinda miliki mwenyewe?”
“Umeeleweka bro”
Lakini sasa muda huo huo sura zao zilibadiika mara baada ya kuhisi kitu ambacho sio cha kawaida na Gefu ndio aliekuwa wa kwanza kupotea ndani ya ofisi hio na kuja kuibukia nje na kufuatiwa na wengine.
Wingu jeusi lilikuwa limejikusanya katika upande wa Kusini mwa eneo la miliki ya Panas , ngurumo na mwanga wa Radi vilikuwa vikisikika na kuonekana.
Sauti za ngurumo za radi zilikuwa kubwa kama vile anga linataka kuondoka chini.
Majini wengi wa miliki hio walikuwa nje wakiangalia hali hio ya kustaajabisha ambayo ni adimu sana kuonekana katika miliki za majini.
“Hii nii…”Jini mmoja ambaye alikuwa katike levo ya maji ya barafu aliongea.
“Hahaha…. tayari amekwisha kuipita levo ya maji ya kiroho , hii ni radi ya mapigo tisa ya adhabu ya anga”Aliongea mkuu wa miliki ya Panas kwa furaha.
“Hakika inashangaza ni juzi tu hapa Anjiu wa Xia ameweza kupita levo hii na leo ni zamu ya Rozu”
“Huu ni wakati wa kuwa na majini wa levo za juu katika ulimwengu wetu,ni heshima kwetu kuangalia kitu kama hichi kikubwa”Aliongea na kufanya wazee pamoja na majini wa miliki hio kuonyesha furaha zao.
“Kimya!!, huu ni mwanzo tu lakini hatuna uhakika kama ataweza kuvumilia mapigo hata matatu ya radi ya rangi ya Zambarau”
Baada ya kusikia kauli hio kila mmoja alipiga kimya kwani ni kweli radi hio haikuwa imeshuka bado na walikuwa na wasiwasi kwamba wanaweza kumpoteza mtu wao.
Majini wanaweza kupitia radi lakini sio wote ambao wanaweza kuihimili kwani ilikuwa na nguvu kubwa kwani dhumuni la kushuka kwake sio kwa ajili ya kunufaisha jini bali ni kwa ajili ya kutoa Adhabu kwa kukiuka sheria za anga.
Dakika chache mbele radi hio ilianza kuonyesha ghadhabu yake na boriti ya radi iliokuwa katika rangi ya Zambarau na bluu ilionekana ikishuka kama vile ni nyoka na kwenda kupiga katika sehemu ambayo yupo jini aliefahamika kwa jina la Rozu.
Ilikuwa ni sauti ya kuumiza masikio ya mwangwi ndio iliweza kusikika na kuwafanya majini kuogopa na kuwafanya wengine kukimbia
“Hii inatisha , sidhani kama Rozu ana Dhana ambayo inaweza kumkinga,atakuwa na uwezo wa kupita hii Adhabu bila kifo kweli?”
“Ni ngumu kusema na hatuwezi hata kusogelea eneo alipo kwasasa bila ya kupoteza nafsi zetu , hata mimi sijui kama ataweza kweli kuhimili?”.
Kila mmoja alikuwa akijiuliza swali linalofanana na kuna ambao walikuwa wakijutia kwa Rozu kukasirisha anga mpaka kupatwa na radi hio.
Dakika chache mbele radi ya pili ilipiga na ilikuwa kubwa kuliko ya mwanzo kiasi cha kutengeneza shimo na ndani ya dakika chache mara baada ya kufifia kitu kinachofanana na Dhahabu kilionekana katka lile eneo.
Kuna ambao waliweza kuona kitu hicho lakini hawakuweza kujua ni kitu gani lakini wakuu wa miliki hio walikuwa na uwezo wa kuhisia Rozu alikuwa hai bado kutokana na msisimko aliokuwa akidhalisha.
Hali hio iliwafanya wazee kujiuliza amewezaje kutoathirika katika mapigo hayo ya radi.
Radi ya tatu iliweza kupiga kwa awau nyingine na ilikuwa na nguvu kubwa zaidi lakini hata hivyo kile kitu ambacho kilikuwa katika muonekano wa Dhahabu bado kilikuwa kikionekana katika eneo lile.
Radi ile ilionekana haikuwa na mpango wa kuendeleza mapigo kwani mara baada ya mapigo matatu wingu lilianza kutawanyika na palepale shimo kubwa lilionekana kwa macho.
“Rozuu..!!!”
Mkuu wa miliki ndio aliekuwa wa kwanza kuita jina hilo lakini kufumba na kufumbua palepale alionekana mwanamke jini ambaye ameshikilia upinde wa Dhahabu akisogelea mbele ya kila mmoja akitokea eneo lile
Nywele zake ndefu zilikuwa hazijafungwa na zilisambaa kulingana na upepo ulivyokuwa ukivuma lakini licha ya hivyo hazikuweza kuficha uzuri wake wa ajabu na macho yake angavu , alikuwa mrembo haswa kwanzia ngozi , umbo la uso na kila kitu.
Alikuwa na muonekano wa ajabu kidogo mzungu sio mzungu , alikuwa ni kama vile ni mfilipino.
Ijapokuwa hakuwa na mavazi ya kirembo kama wanawake wa kidunia lakini upole wake pamoja na uwezo wake ulimfanya kuzidi kupendeza na kuwa ni mwenye kutamanika.
Huyu mwanamke alikuwa akifanana kwa kila kitu na mrembo ambae Hermes mjumbe wa miungu alikuwa akiongea nae katika kilele cha mlima kilimanjaro muda kadhaa mara baada ya Roma kumuokoa Edna katika mikono ya Vampire waliokuwa wakitafuta mshipi feki.
Ki ufupi ni kwamba ni huyu mwanamke bila shaka na haikueleweka ilikuwaje akawa katika jamii ya majini wa miliki ya Panas lakini ndio hivyo alionekana kupitia levo ya mapigo matatu ya radi ya mbingu na jina lake alikuwa akifahamika kwa jina la Rozu.
Ijapokwa Rozu hakuwa ameonyesha uwezo wake wote lakini kwa majini hao walijua alikuwa ni wa levo za juu sana , pengine alikuwa akilingaina ki uwezo na Jini Anjiu wa miliki ya Panas au kumpita.
“Hongera sana , kwasasa upo na uwezo mkubwa wa nguvu za kijini na hakuna ambaye anaweza kukushinda katika ulimwengu wa majini watu”Aliongea Master namba nne huku ile hofu yake ya kumhofia Roma na Anjiu ikiwa imetoweka kabisa , alijua kwa uwezo aliokuwa nao Rozu anapaswa kuwa na amani.
“Hongera sana , nilikuwa na wasiwasi muda si mrefu lakini kwa bahati nzuri umeweza kufanikiwa kupitia mapigo ya radi”Aliongea Mkuu wa miliki hio huku akijiuliza kimoyo moyo.
“Imekuwaje akapitia mapigo hayo ya dhiki ya radi kirahisi hivyo , anaonekana hajapatwa na majeraha ya aina yoyote yale”Aliwaza.
Ukweli ni kwamba kuna namna majini hao walikuwa wakimjua Rozu kama Rozu jini mwenzao lakini hawakumjua Rozu kama sehemu ya miungu , kitendo cha Rozu kuongea na Hermes juu ya mlima kilimanjaro ilimaanisha kwamba ni sehemu ya miungu lakini jina lake halifahamiki ni lipi katika miungu yote iliobaki ambayo hatujawaona wahusika wake.
“Kama hizi ni pongezi za dhati basi sina budi ya kuzipokea”Aliongea mwanadada mrembo Rozu huku akimwangalia Gefu kwa macho makali kidogo kiasi cha kumfanya Mkuu wa miliki hio kuwa na wasiwasi lakini alijitahidi kuonyesha tabasamu.
“Unapenda sana utani , sina haja ya kumuonea wivu mdogo wangu wa kike mafanikio yake , leo ni siku ya kusherehekea, uwepo wako unatufanya tusimhofie tena jini Anjiu”Aliongea.
Ukweli ni kwamba Rozu na Anjiu kidogo walikuwa na tofauti , wakati wa Anjiu anapokea mapigo ya radi chungu cha Roma ndio ambacho kilimkinga lakini kwa jini Rozu yeye ilikuwa tofauti kwa maana kwamba mapigo yote ya radi yalimfikia.
Majini wote walikuwa kwenye shangwe wakimzunguka Rozu na kumpa pongezi za dhati kabisa kwa kupigi hatua hio Adhimu.
Kuipita Dhiki ya radi ni hatua kubwa sana katika ulimwengu wa majini ndio maana.
Rozu mara baada ya kuweka upinde wake wa Dhahabu katika hifadhi ya pete alivuta pumzi nyingi na kisha kutoa tabasamu.
“Anjiu huna uwezo tena wa kunizidi, Hades namsapoti Athena na mipango yake na nataka nione ikifanikiwa”Aliwaza.
Haya sasa kuna kiumbe kingine katika miliki ya Panas , unadhani huyu jina lake halisi ni lipi kati ya miungu kumi na mbili ya mlima Olympus kutoka sayari ya Mars.
Hades A.k. a Roma Ramoni atamuweza kweli?.
SEHEMU YA 737.
Upande wa Roma mara baada ya mechi kumalizika hakuna ambaye alitamani kuangalia ugawaji wa makombe na medali hivyo walirudi moja kwa moja kwenye boti yao ya kifahari.
Upande wa Raisi Jeremy hakuwasumbua tena kwani alikuwa ndani ya Uingereza kwa ajili ya kikao cha Umoja wa mataifa kinachohusu mabadiliko ya hali ya hewa na hata Raisi Senga alikuwa ni moja ya viongozi ambao walihudhuria kikao hicho muhimu.
Kilikuwa ni kikao muhimu kutokana na mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa ya joto la dunia kuporomoka na kusababisha baridi kali licha ya kwamba katika maeneo mbalimbali ya dunia ilipaswa kuwa majira ya joto.
Ukiachana na wakuu wa mataifa lakini pia wanasayansi wengi na watu wa maswala ya kimazingira walikuwa wakihudhuria kikao hicho ili kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo mara baada ya kujua chanzo.
Clark ni moja ya wanasayansi muhimu kabisa ambao walialikwa katika kikao hicho muhimu lakini licha ya hivyo hakukuwa na maelezo ya moja kwa moja ambayo angeongea kwani ni swala ambalo bado hakuwa amelifanyia utafiti.
Roma mara baada ya kuingia katika boti ndio maandalizi ya kurudi katika visiwa vya wafu yalianza rasmi lakini ndio muda ambao aliweza kupokea simu kutoka kwa Afande Kweka.
“Wewe mtukutu hivi utaacha lini kuwa na huo ukiburi?”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Roma kuishia kushangaa.
“Ongea vizuri mzee basi”
“Kwanini umekataa kuongea na wajumbe wa Hongmeng ?, angalau hebu ongea nao maana kwasababu yako kila saa wapo ndani ya makazi yetu, unafikiri nadili nao vipi viumbe wa ajabu kama hawa?”
“Unamaanisha huyo Xuan Jizi yupo ndani ya makazi yako?”Aliuliza Roma huku hasira zikianza kumvaa maana aliona ni kama usumbufu.
“Anaonekana kuwa na hasira sana na amesema kama hutorudi mapema anaenda kutoa taarifa Hongmeng , hebu rudi udili na hii hali nishazeeka sitaki kuingizwa kwenye matatizo ya namna hii mimi”Aliongea na palepale alikata simu ikionyesha dhahiri alikuwa amekasirika.
Roma aliweka simu yake mfukoni na kisha aliwasogelea wanawake wake na kuwaambia juu ya hali inayoendelea nchini Tanzania hivyo anapanga kuondoka.
Kwasababu walikuwa ni waelewa hawakumzuia Roma na dakika hio hio alianza safari kurejea nchini Tanzania.
Ulaya na Tanzania masaa yalipishana kidogo sana hivyo Roma alifika wakati wa usiku pia ndani ya jiji la Iringa na wakati wa kutua tu aliweza kuona kuna wageni wamekaa katika sebule ya wageni ndani ya nyumba hio , walikuwa wawili na wote ni Wachina.
Moja kati yao alikuwa akimjua na mwingine hakuwa akimjua lakini alionekana kuwa handsome mno , ilikuwa ni kama vile sio mchina na alikuwa katike levo ya maji ya kawaida.
“Naona Mjumbe umeimarika kuliko mara ya mwisho tulivyoonana”Aliongea Roma akimlenga mjumbe wa Hongmeng mpenda rushwa.
“Haha… sipo hapa kwa ajili ya kukumbushia namna tulivyoonana mara ya mwisho nimemleta balozi”Aliongea na kisha alimpa ishara balozi Xuan Jizi.
“Wewe ndio Roma Ramoni ulietibua hali ya hewa katika miliki ya Kekexil na Xia?”Aliuliza yule bwana bila hata ya salamu , alionekana kuwa na hali ya ujeuri hivi.
“Ndio umekuja kote huku kwa ajili ya kuuliza ujinga?”
“Acha maneno yako makali , hivi unajua upo kwenye matatizo?”
“Nielimishe”
“Nikuelimishe nini? , unadhani kuna hata haja ya kufanya hivyo , unajua mwenyewe namna ambavyo umekasirisha majini kutoka miliki ya Xia na Kekexil , ukaenda mbali na kuchokoza miliki ya Braki , nguvu iliokuwa nyuma ya familia ya Sharif , unaonekana kabisa unaogopa ndio maana ukaikimbiza familia yako nje ya nchi”
“Umongea sana lakini sijui kilichokuleta ni nini?”
“Nipo hapa kwa ajili ya kupitisha maagizo niliopewa na wakuu wa miliki ya Hongmeng, wasimamizi wakuu wa sheria ya the gods treaty , ili kuongezea nguvu utulivu wa dunia na kukuzuia kupigana na miliki za kijini na kusumbua raia , Hongmeng kwasasa itakuwa ndio kimbilio lako licha ya kwamba kutakuwa na mashariti, ukikukubali hakuna miliki yoyote ambayo itakugusa”
“Roma usishangilie bado kuna masharti”Aliongea yule mjumbe na Xuan jizi aliendeea.
“Umekiuka sheria nyingi sana na kutumia uwezo wako vibaya na kuua wajumbe ambao waliagizwa kuja duniani kutimiza majukumu yao , lakini licha ya hivyo Hongmeng hawataki kulipiza kisasi na wameaua kukusamehe ili mradi tu kwa hiari yako utoe mbinu yako ya mafunzo , vidonge na Dhana ya Chaos cauldron na baada ya hapo sisi tutakupatia ulinzi”Aliongea akiwa siriasi na kumfanya Roma kuangua kicheko.
“Unacheka nini?”
“Wewe Mzee Jizi, lazima kwenye kwenye kichwa chako kuna nati zimechomoka au hao Hongmeng hawajui nini kinaendeea , nadhani napaswa kuwafafanulia kwa sentensi rahisi”
“Acha kunitukana … tunazo taarifa umeiba hazina yote ya Kekexil na Xia na unazo Dhana na vidonge kedekede , hivi unadhani vitu vya thamani kama hivyo utaweza kuvilinda peke yako, hivyo acha ukiburi na sikiliza tunachokuambia”
“Vipi kama nikikataa mtanifanya nin?”
“Roma acha kujifanyisha kijogoo , sekunde ambayo nitakuripoti katika miliki ya Hongmeng basi ndio utakuwa mwisho wako kwani utakuwa ni adui namba moja wa Hongmeng”
Roma aliwaza na kujiambia tokea siku anajua uwepo wa Hongmeng ndio uadui wao ulipoanzia hivyo hana mpango wa kuwasikiliza kwa chochote , kwanza kabisa alikuwa na deni kwa Zenzhei kumsaidia kulipa kisasi na tokea siku waagane ni kama Zenzhei katika ulimwengu huo wa kijini alikuwa akimsubiria.
Roma bila ya kujiuliza mara mbili mbili aliita nguvu ya Cauldon bila ya kukitoa nje na kuingiza katika mwili wa Xuan Jizi na kuanza kunyonya nguvu zake za kijini na nguvu ya Cauldron ilikuwa kubwa mno na ndani ya dakika chache tu alikuwa ashapoteza uwezo wake wote na kubakia binadamu wa kawaida.
Xuan Jizi hakuwa jini kama jini wa Hongmeng , alikuwa ni binadamu tu ambaye alikuwa na mafunzo ya kijini hivyo ilikuwa rahisi kwa Roma kudili nae kwani alikuwa ndio kwanza yupo katika levo ya maji ya kawaida.
Hakuna ambaye alitegemea Roma kuchukua maamuzi kama yale , lakini kwa Roma alitaka kuonekana kuwa siriasi na kutangaza vita vyake rasmi na Hongmeng kabisa na ili kuonekana yupo siriasi alitaka kwanza kumuadabisha balozi wao.
Mjumbe wa Hongmeng aliebakia ndio alipewa jukumu la kurudi Hongmeng na kutoa taarifa ya kile kilichotokea,
“Rudi ujinini na toa taarifa hizi , kama hao majini wanataka Dhana zangu , vidonge vyangu na mbinu yangu ya mafunzo basi waje huku nilipo wavichukue kwa nguvu kama nilivyofanya katika miliki ya Kekexil,likija swala la watu wenye nguvu kama haina haja ya kutii sheria za ulimwengu bali sheria ya msituni ndio itumike , atakae weza kuishi mpaka mwisho huyo ndio mtawala”
Baada ya kusema hivyo Roma alimbeba mzobemzobe yule Xuan Jizi na kisha kumtupia mbele ya walinzi akiwaagiza kwenda kumtupia mtaani huko kwani ashakua ni wa kawaida.
Alijua asingeweza tena kurudi Hongmeng kwani miliki hio haichukui majini wadhaifu kama yeye.
“Vipi kila kitu kimemalizika?”Aliuliza Afande Kweka mara baada ya Roma kuingia katika sebule ya kawaida na Roma aliishia kutingisha kichwa tu akiitikia amemaliza.
“Unajisababisha matatizo zaidi na zaidi juka uchao kulikuwa na haja gani ya kumuondolea nguvu zake za kijini?”Aliongea Afande Kweka bila ya kubadilisha muonekano wake , yaani hakuwa na furaha wala hakuwa na huzuni na hata usingizi hakuwa nao licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda.
“Babu hicho ndio kitu pekee ambacho unaweza kuongea”
“Unadhani ni kipi ambacho naweza kuongea , mwenyewe nipo najiuliza mambo ambayo yanaendelea katika hii dunia, nina hasira nyanya zangu zote zimekauka kutokana na baridi kali , hii baridi sijawahi kuiona na uzee wangu huu”Aliongea na kumfanya Roma amuone huyu mzee anaonekana kuficha mambo mengi na kila anachoongea ni kama anamwigizia lakini hakutaka kumhoji sana.
Huo ndio ulikuwa ukweli ugomvi wa Roma na majini ulikuwa ni wa kutisha lakini ulikuwa haukwepeki lakini kubwa zaidi ni kwamba Mzee huyo alitamani sana Roma kwenda kuwashambulia Hongmeng ili kulipa fadhila za Zenzhei kwa kumlinda kwa miaka mingi, ukiachana na hilo lakini pia Afande Kweka ni mwanachama wa umoja wa Ant- illuminat na ni juzi tu hapo alikuwa na kikao cha siri na baadhi ya wanachama na alikuwa akijua Edna ndio mkuu wake.
Yani kwa lugha nyepesi ni kwamba Edna ni mkuu mbele ya Afande Kweka lakinin mzee huyo licha ya kujua hayo yote hakuwa tayari kumwambia Roma kwani alijua itafikia siku yeye mwenyewe atakuja kujua ukweli na hata hivyo sheria za umoja huo hazikumpa ruhusa ya kuongea chochote kwani ingeharibu kabisa mipango inayoendelea.
“Babu nadhanni baada ya Hongmeng kupokea ujumbe wangu sitoweza kuendelea kuishi hapa Tanzania kwa muda , unaonaje na wewe ukielekea visiwani kwa muda , unaweza kuondoka na baadhi ya watu wako wa karibu pia”
“Unataka nitoke hapa Tanzania kwenda wapi na kwanini?”
“Si kila kitu kipo wazi mzee , sitaki waje wakukamate na kutaka kunitishia uhai wako kama chambo cha kunikamata”
“Mimi nipo nje ya maswala yote ambayo yanahusiana na maadui zako na sio kwangu tu hata kwa baba yako , kinachoendelea ni vita kati yako na majini na hayahusiani na ukoo wetu hivyo pambana kivyako”
“Unaongea tu lakini wanaweza wakapania sana na kutumia njia yoyote ile”
“Hata iweje nasema hapa siondoki “Aliongea kibishi.
“Kwannini sasa , huu sio muda wa kuonekana shujaa mzee”
“Mimi ni mzee wa taifa hili lakini pia mkuu wa familia ya Kweka , siwezi kuondoka na kwenda mahali pengine nje ya Tanzania, unaweza kutafuta chumba ulale , muda umeenda naenda kupumzika”Aliongea na kisha aligeuza na kuingia chumbani kwake.
Roma alikuwa na usingizi na wakati akiwaza kwenda katika chumba cha wageni kwa ajili ya kulala simu yake ilianza kuita mlio wa kuingia meseji na alipoangalia ilikuwa imetokea kwa Tannya.
“Master kuna kundi la majini wamefika na wanakuulizia hapa Bagamoyo”Ujumbe wa meseji ulisomeka hivyo.
“Naona hatimae wamejitokeza licha ya kwamba ni kwa kuchelewa kama nilivyotegemea lakini ni bora wamekuja kabla sijarejea katika ulimwengu wa majini watu”Aliwaza Roma
Sasa mara baada ya Roma kuona kwamba nguvu ambayo ipo nyuma ya familia ya mzee Sharif imejitokeza hakutaka kupoteza muda kabisa na shauku ya kutaka kujua Braki ni majini wa namna gani ilimvaa.
Roma mara baada ya kuondoka ndani ya eneo la Iringa dakika chache tu aliweza kufika mkoa wa Pwani katika makazi ya Sharif na aliweza kumuona Tannya akiwa amesima katikati ya ukumbi wa mikutano , ilikuwa ni eneo ambao hutumika kupokelea wageni mara nyingi.
Mbele yake kulikuwa na wanachama wa familia ya Sharif na mara baada ya kuwachunguza kwa umakini Roma aligundua hawakuwa wa kawaida wote walionekana kama waarabu hivi na hajawahi kuwaoana na walikuwa na nguvu za kijini.
Tannya tokea muda tu alikuwa amebadilisha wafanyakazi wote wa Sharif na kuweka wa kwake , ijapokuwa alikuwa mjapani lakini alikuwa mjuzi sana katika kuigiza na tokea siku ambayo amefika na kujifanyisha ni Maimuna hakuwahi kuonyesha dosari yoyote na hata ibada alikuwa akiongoza.
Roma kwa kutumia jani lake la upofu aliishia kujificha juu ya jengo hilo huku akihakikisha anasikia kinachoendelea kwa kutumia uwezo wake na majini hao hakuna hata mmoja ambaye aliweza kugundua uwepo wake.
Kulikuwa na majini jumla saba, wote walikuwa wamevalia kanzu kwa upande wa wanaume na wanawake wenyewe walikuwa wamevalia Abaya nyeusi , karibia wote walikuwa na muonekano wa ki utu uzima.
Kati yao mmoja tu ndio ambaye alikuwa na uwezo wa juu wa mafunzo ya kijini kwani alikuwa mwanzoni mwa maji ya kiroho. Na wengine wote walikuwa katika levo za maji ya barafu kushuka mpaka moto wa njano.
“Wewe ndio kiongozi wa familia ya Sharif katika ulimwengu huu unaefahamika kwa jina la Maimuna si ndio?”Mwanaume ambaye alikuwa na muonekano wa kizee alimuuliza Tannya , alikuwa na nywele nyeupe na ndevu nyeupe kama vile ni Nandra Modi waziri mkuu wa India na ndio ambaye alikuwa na uwezo wa juu wa kijini.
“Ndio , kwasasa mimi ndio nililazimika kuwa kiongozi , hivyo sina uhakika namna ya kuwaita kwani siwafahamu”Aliongea Tannya aliekuwa katika sura ya Maimuna.
“Hakuna shida kwani hata babu yako Sharif hana uwezo wa kututambua,kwa majina nafahamika kama Zando , nikiwa mwanachama kutoka makao makuu ya miliki , hapa kuna mzee Nuli na Yejini pamoja na majini wanne unao waona , tumekuja hapa kujua ni kipi kinachoendelea kwasababu hatukuweza kusikia habari zozote kuhusu mwizi alieiba hazina yetu , taarifa za kubadilika kwa kiongozi wa familia na imani ni zaidi ya matarajio yetu”
SEHEMU YA 739.
Katika moyo wake Tannya ukweli hakuwa akijua namna ya kujibu, ijapokuwa alikuwa akijua muda kama huo ungewadia lakini ndio mara yake ya kwanza kukutana na majini wa namna hio na angalau ni kwamba alikuwa tayari ashamtumia Roma ujumbe wa meseji.
Tannya simu yake ilitoa mnguruo mara baada ya kutaka kujibu na mara baada ya kuangalia aliona Roma alikuwa ametuma ujumbe kwa lugha ya kijapani.
“Tafuta njia yoyote upate taarifa zinazohusiana na wanakotokea na historia yao kwa ujumla”Aliongea Roma katika ujumbe huo.
Roma alitumia kijapani kwa kuamini ingekuwa ngumu kwao kuelewa kile alichokuwa ameandika.
Tannya mara baada ya kujua Roma ashafika hali ya kujiamini iliongezeka kidogo na palepale aliomba radhi
“Naombeni mniwie radhi wakubwa zangu, nilitamani pia kutoa taarifa kuja makao makuu lakini kwa bahati mbaya babu , walinzi na wengine walikufa vifo vya haraka sana na sikujua namna ya kuwasiliana na nyie hivyo…”
“Haina haja ya kujilaumu , hata sisi pia tunaelewa namna ilivyo ngumu kuwasiliana na sisi , umefanikisha kuongoza familia ndani ya muda mfupi na kuendeleza ibada taarifa hizi zikimfikia mkuu wetu atafurahi”Aliongea.
“Tafadhari naomba mniwie radhi kama nitavuka mpaka , lakini je mnaweza kunielezea historia yote ya familia pamoja na imani yake , ili mimi Maimuna niweze kuwa na uelewa mzuri na kufanya vizuri kwa ajili ya manufaa ya miliki kwa ujumla”
“Kwasababu umekuwa kiongozi pekee uliebakia basi ki asili umekidhi vigezo vya kujua historia yote ya Kibraki , Babu yako Sharif ana uelewa mdogo sana kuhusu jamii ya majini wa Braki pengine amewahi kusikia hili jina mara moja au mara mbili tu , lakini kutokana na mabadiliko ya hali na matukio ya kutotarajia hapa duniani makao makuu wameona ni sahihi familia za binadamu zinazotuwakilisha hapa duniani kujua uhalisia wa historia yetu na imani yote kwa ujumla, hivyo nitakuelezea kila kitu”
Roma ambaye alikuwa akipiga chabo alijikuta akifurahi mara baada ya kusikia kauli hio kwani hakutegemea jini aliefahamika kwa jina la Zando angeweka wazi kuhusu nguvu iliokuwa nyuma ya familia ya Sharif.
*****
Miaka elfu hamsini iliopita dunia iliingia katika hatua nyingine kubwa katika ustaarabu.
Wakati huu pia upande wa majini walikuwepo pia na wengi wao walikuwa katika levo za juu sana pengine levo ambayo haijawahi kufikiwa katika nyakati za sasa.
Kipindi hiki ni kabla ya miungu kufika katika sayari ya Dunia na ndio kipindi ambacho majini wengi walianza kupotea katika uso wa dunia na kuwaacha binadamu na baadhi ya majini watu.
Majini ni vumbe ambavyo vipo vya aina nyingi sana na tabia tofauti , ni kama ilivyo kwa makabila ya kibinadamu basi ndio ilivyo kwa majini hivyo hivyo.
Sasa kati ya majini wa enzi hizo ambao walikuwa na nguvu kubwa katika uso wa dunia ni majini pepo na hawa majini pepo wenyewe walikuwa wamegawanyika katika aina nyingi sana.
Inasemekana katika kipindi hichi majini walikuwa wengi kuliko hata idadi ya binadamu kutokana na spidi yao ya kuzaliana.
Kati ya majini pepo ambao waliweza kufahamika enzi hizo ni kama vile Mbweha na Majoka ambao ndio walikuwa na uwezo mkubwa sana .
Majinii jamii ya Mbweha walikuwa ndio wenye busara kubwa na mbinu nyingi za kimaajabu tofauti hata na majini Joka ambao walikuwa wamezaliwa na nguvu za kimwili sana sana.
Ukiachana na majini hao lakini pia majini watu hawakuwa nyuma pia kwani wengi wao walikuwa katika levo za juu kwa kuweza hata kudhibiti radi na ilikuwa ni kawaida kwa majini watu kuweza kumiliki Dhana za hali ya juu kabisa na shida ilikuwa tu kwamba licha ya uwezo wao hawakuweza kupata mbinu ambayo inaweza kuwainua zaidi na zaidi.
Hawa majini watu ndio ambao walipenda kuwa wa wazi kabisa na waliweza kuishi katikati ya binadamu wa kawaida tofauti na majini pepo ambao walikuwa ni hatari kabisa kwa binadamu.
Majini pepo waliishi katika maumbo yao ya kawaida pasipo ya kubadilika na ukweli ni kwamba walikuwa wakitisha sana na hali hio ki ufupi ni kwamba hawakuipenda na hii iliongeza chuki yao zidi ya binadamu na majini watu.
Lakini mwishowe walijitahidi kutafuta namna ya kuboresha muonekano wao ndipo walipokuja kugundua mbinu mbadala ambayo ilikuwa ni kuamsha pepo wao wa ndani tofauti na kuwazimisha au kuwakata kama ilivyokuwa kwa majiini watu ,hapo sasa ndio ikazaliwa majini halisi ambao walikuwa na nguvu za kijini, majini ambao walikuwa na uwezo wa kupaa.
Sasa kutokana na kuwa na maumbo yenye nguvu kubwa pamoja na kumiliki nguvu za kijini pamoja na kuwa wengi walikuja kuwa tishio kubwa kwa jamii nyingine za kijini na binadamu wa kawaida kiasi cha kupelekea kuibuka kwa vita ambayo majini watu waliungana na binadau kuwashambulia Majoka.
Sasa kati ya majini pepo wakaja kuibuka jamii nyingine kati ambao walijiita mashetani pepo wa anga , hawa ndio walikuwa wabaya zaidi kwani walikuwa na uwezo wa kumuingia binadamu na kumfanya afanye kila anachotaka huku wale majini pepo wengine wakichinja binadamu na kunywa damu yao.
Binadamu alionekana kuingia katika hatari na kuanza vita na viumbe hawa majini ,vita ambayo ilidumu kwa muda mrefu sana takribani miaka mia moja na siku moja tu ilitokea majini pepo wengi katika ulimwengu wa kawaida kuanza kupotea ikiwemo Mbweha na Majoka.
Kupotea kwao baadae ilikuja kujulikana walikuwa wakivutwa katika ulimwengu mwingine kwa kutumia aina ya mitego ambayo ilikuwa imewekwa mfano wa mnara ambao Roma aliingia.
Ni asilimia chache tu ya majini pepo ambao walibakia na kati yao hawakuwa hata na uwezo mkubwa na hapo ndipo majini watu wa enzi hizo walipoona hakuna haja ya kuwaua bali kwenda kuwafungia katika ulimwengu Tenganifu wa jangwa.
Kitendo cha mashetani pepo wa anga, Majoka na Mbweha kufungiwa katika ulimwengu wa Jangwa Tenganifu kwa muda mrefu iliwafanya kuchukulia hapo kama makazi yao rasmi.
Mara baada ya kuwasili kwa miungu katika uso wa dunia ndipo ilipoibuka vita kati ya majini watu yaani Hongmeng na jamii nyingine za kijini , vita ambayo ilidumu muda mrefu sana mpaka Zeus na Athena kushindwa vita na kuzaliwa kwa the Gods treaty.
Mpaka vita hio inakuja kufikia mwisho majini pepo ambao walikuwa katika ulimwengu wa jangwa tenganifu walikuja kugundua miliki za majini watu walikuwa wamepungukiwa nguvu sana kutokana na kupigana vita na miungu na wengi wao kuuliwa na hapo ndipo walipoona ni fursa adhimu ya kujiendeleza wao wenyewe kutokana na kipindi hicho majini watu kutokuwa nao makinu.
Mbinu pekee ambayo iliwafanikisha kujiendeleza ni kufanya ushirikiano wa kiimani na binadamu wa ulimwengu wa kawaida taratibu taratibu kwa namna ambayo waliweza wao na mwisho wa siku wakajikuta wanakuwa na nguvu kubwa kwani walijipatia mali asili nyingi kutoka Duniani na kuziingiza katika ulimwengu wao huku wakibadilishana na binadamu madini mengi ya thamani.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba majini pepo wengi ikiwemo majoka na Mbweha ambao walikuwa na uwezo mkubwa walimezwa katika ulimwengu wa majini pepo kwa njia ambazo mpaka siku hio hawakuelewa imetokeaje , huku upande wa majini watu , yaani majini wa kawaida ambao mbinu zao sio kuamsha mapepo wao walijitenga na binadamu wa kawaida mara baada ya kugundua Dimension nyingine na kuanzia hapo kila majini wakajitegemea na kukawa na ulimwengu wa majini watu , ulimwengu wa majini pepo na ulimwengu wa Jangwa Tenganifu sehemu ambayo hupatikana miliki moja tu ya kijini ambayo hufahamika kwa jina la Braki.
Kwa historia hio ilimaanisha kwamba hapo zama za kale majini na binadamu waliishi katika ulimwengu mmoja kabla ya vita kutokea, vita ambayo mpaka wakati huo majini wote wanajiuliza ilimalizwa na nani kwani sio wao ambao waliwafanya majini pepo wenye nguvu kuvutwa kwenye ulimwengu mwingine.
Sasa kati ya majini pepo hao ambao walivutwa ni kama vile Aoiline Mbweha wa mikia tisa , Majoka na mashetani pepo wa anga.
Roma mara baada ya kusikia habari hio aliishia kushangaa , katika ulimwengu wa majini pepo Zimo alisema ulimwengu wao ulikuwa ni wa miaka mingi kuliko hata Hongmeng na hio ilimaanisha kwamba kabla ya kumezwa ulimwengu huo ulikuwepo.
Sasa Roma mara baada ya historia hio anajua nguvu ambayo ipo nyuma ya familia ya Sharif ni majini pepo na ni sawa na kusema ni ndugu wa Aoiline.
Kulinganana msaada ambao Aoiline alimfanyia na wengine Roma aliona ni dhambi kama ataingamiza miliki hio ya Braki ambayo inapatikana katika Ulimwengu wa Jangwa na anachopaswa ni kujaribu kufanya urafiki nao lakini kabla ya yote lazima ajue hazina yao ilikuwa ikimaanisha nini.
“Asante sana kwa kunielezea haya”
“Hivyo licha ya familia ya Sharf kuumiza watu wengi katika ulimwengu huu wa kawaida lakini kwa upande wetu sio jambo kubwa sana na sio maagizo yetu , Sisi sio kama majini kutoka Hongmeng na miliki nyingine ambao wanachotaka ni umaarufu tu , sisi leo tumetoka kuja katika ulimwengu wa kawaida kwasababu ya muovu Roma Ramoni ambae ameiba hazina yetu”
“Je naweza kuuliza, Hazina hio ina matumizi gani , je kutakuwa na athari zozote kama isipokuwa kwenye mikono yetu?”Aliuliza Maiuna feki na hapo ndipo Roma alipokuwa akitaka kujua ile kokoto ina maana gani.
ITAENDELEA ,WATSAPP 0687151346