Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Tunashukuru kwa matusi yako.

Ubarikiwe.
Hapo hakuna Tusi nimeelezea uhalisia,Huyu mwandishi kazingua sana nimesoma mwezi mzima haiishi matukio mengi hayana maana ikabidi niende Episode ya mwisho kabisa kuona hitimisho la yote kwa kweli nilijuitia Elfu 10 yangu nilolipa Riwaya ilianza vizuri kwa kuwa na kichwa ila ikakosa miguu

Labda nyie mnaweza ona kawaida sababu ni aina ya riwaya mloanza zisoma ila kwa mimi mpenzi wa Riwaya nilosoma riwaya nyingi za toka zamani hizo hadi za miaka ya karibu niseme tu hakuna la maana aliloandika humo na ni moja ya Riwaya ya Hovyo zaidi nilowahi kusoma katika Maisha yangu...Kuna mwandishi wa Humu Jf anajiita FABIAN bakuya huyu jamaa niliamini ndo Mwandishi mbovu na niliwahi mwambia ila bora yule kuliko huyu
 
Zipo za Chombezo mkuu zimejaa kule fesibuku kakomae nazo
Ndugu Mtunzi Hii Riwaya hata ungeipeleka kwa Wahariri hakika wangekurudishia ukafikirie upyaa

Mimi ni mpenzi wa Riwaya za aina Zote,nimefanikiwa Kusoma Riwaya nyingi sana na katika simu yangu nina Soft copy ya Riwaya nyingi na zote huwa nasoma nukta kwa nukta ila hii yako nimesoma naona haishi matukio mengi yasiyo na maana ikabidi niende kusoma hitimisho tu na nikaona hitimisho ni lile lile nililoliwaza

Ili uwe bora lazima usome Kazi za wenzako kwa waandishi wa sasa hivi kuna bwana wa kuitwa GEORGE IRON MOSENYA jaribu kutafuta Riwaya zake mbili tatu mfano za kumuhusu GEZA ULOLE uone na Simulizi za kijasasi zinatakiwa kuwa na sio hii ujinga unayo hangaika nayo Inatakiwa Riwaya usome sio ikuchoshe ila ikuchangamshe zKo zinachosha tuu hadi unahisi Homa......


Badilikaaa masta
 
Ndugu Mtunzi Hii Riwaya hata ungeipeleka kwa Wahariri hakika wangekurudishia ukafikirie upyaa

Mimi ni mpenzi wa Riwaya za aina Zote,nimefanikiwa Kusoma Riwaya nyingi sana na katika simu yangu nina Soft copy ya Riwaya nyingi na zote huwa nasoma nukta kwa nukta ila hii yako nimesoma naona haishi matukio mengi yasiyo na maana ikabidi niende kusoma hitimisho tu na nikaona hitimisho ni lile lile nililoliwaza

Ili uwe bora lazima usome Kazi za wenzako kwa waandishi wa sasa hivi kuna bwana wa kuitwa GEORGE IRON MOSENYA jaribu kutafuta Riwaya zake mbili tatu mfano za kumuhusu GEZA ULOLE uone na Simulizi za kijasasi zinatakiwa kuwa na sio hii ujinga unayo hangaika nayo Inatakiwa Riwaya usome sio ikuchoshe ila ikuchangamshe zKo zinachosha tuu hadi unahisi Homa......


Badilikaaa masta
Sio lazima kusema ....
 
Moja kati ya Riwaya za HOVYO na Kipumbavu kuwahi kusoma ni hii...Riwaya ndefuu haina kichwa wala miguu,,mtunzi anajaza matukio mengii mradi iwe ndefu isio na tija

Elfu 10 yangu nililopa bora ningenunua Malaya tu nipunguze uzito
4 brave only bro👷
 
Ndugu Mtunzi Hii Riwaya hata ungeipeleka kwa Wahariri hakika wangekurudishia ukafikirie upyaa

Mimi ni mpenzi wa Riwaya za aina Zote,nimefanikiwa Kusoma Riwaya nyingi sana na katika simu yangu nina Soft copy ya Riwaya nyingi na zote huwa nasoma nukta kwa nukta ila hii yako nimesoma naona haishi matukio mengi yasiyo na maana ikabidi niende kusoma hitimisho tu na nikaona hitimisho ni lile lile nililoliwaza

Ili uwe bora lazima usome Kazi za wenzako kwa waandishi wa sasa hivi kuna bwana wa kuitwa GEORGE IRON MOSENYA jaribu kutafuta Riwaya zake mbili tatu mfano za kumuhusu GEZA ULOLE uone na Simulizi za kijasasi zinatakiwa kuwa na sio hii ujinga unayo hangaika nayo Inatakiwa Riwaya usome sio ikuchoshe ila ikuchangamshe zKo zinachosha tuu hadi unahisi Homa......


Badilikaaa masta
Umeongea kwa uchungu mkubwa sana pole mkuu na asante kwa maoni , wakati ukiendelea kutafuta simulizi au kitabu kitakachoendana na radha yako zingatia huushauri , upo kwa kingereza sijui hata unakijua.
Not liking novels doesn't mean one can't appreciate creativity in other forms. People have different tastes, and that's what makes art and literature diverse and interesting
 
Ndugu Mtunzi Hii Riwaya hata ungeipeleka kwa Wahariri hakika wangekurudishia ukafikirie upyaa

Mimi ni mpenzi wa Riwaya za aina Zote,nimefanikiwa Kusoma Riwaya nyingi sana na katika simu yangu nina Soft copy ya Riwaya nyingi na zote huwa nasoma nukta kwa nukta ila hii yako nimesoma naona haishi matukio mengi yasiyo na maana ikabidi niende kusoma hitimisho tu na nikaona hitimisho ni lile lile nililoliwaza

Ili uwe bora lazima usome Kazi za wenzako kwa waandishi wa sasa hivi kuna bwana wa kuitwa GEORGE IRON MOSENYA jaribu kutafuta Riwaya zake mbili tatu mfano za kumuhusu GEZA ULOLE uone na Simulizi za kijasasi zinatakiwa kuwa na sio hii ujinga unayo hangaika nayo Inatakiwa Riwaya usome sio ikuchoshe ila ikuchangamshe zKo zinachosha tuu hadi unahisi Homa......


Badilikaaa masta
Hii story uwez soma ukiwa umeachwa bro.
 
Na nimeanza nyingine ndefu tu zaidi ya hii tatizo ni moja tu you're not the targeted audience .
Kuliko kubishana na hadhira kwanini usingeweka muendelezo?!!! . singanojr uliahidi mpaka kwisha kwa mfungo wa ramadan ungeshamaliza, lakini mpaka Sasa bado. Hebu jaribu kuheshimu ahadi zako mwenyewe basi?!! 🤔
 
Watu wamezoea simulizi za kimalaya malaya zisizo na faida yoyote.

Hii simulizi ukiisoma vema utagundua mambo mengi sana yanayozunguka maisha ya binadamu katika picha isiyoonekana.

Bahati mbaya kuna watu mnasoma kama burudani na kina mini tunasoma kama kuongeza maarifa ya mambo fulani fulani na hii simulizi haina burudani yoyote kama sikosei tangu naanza kuisoma mimi nimecheka sehemu moja tu ya amina kuwa mbweha wa mikia.

Singano jifanye kiziwi na kipofu tupia mwendelezo atakayesoma asome atakayeacha aache.
 
Watu wamezoea simulizi za kimalaya malaya zisizo na faida yoyote.

Hii simulizi ukiisoma vema utagundua mambo mengi sana yanayozunguka maisha ya binadamu katika picha isiyoonekana.

Bahati mbaya kuna watu mnasoma kama burudani na kina mini tunasoma kama kuongeza maarifa ya mambo fulani fulani na hii simulizi haina burudani yoyote kama sikosei tangu naanza kuisoma mimi nimecheka sehemu moja tu ya amina kuwa mbweha wa mikia.

Singano jifanye kiziwi na kipofu tupia mwendelezo atakayesoma asome atakayeacha aache.
haswa
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

MTUNZI: SINGANOJR

WATSAPP: 0687151346

Mono no aware

SEHEMU YA 788.
Roma alijikuta akiweka tabasamu kama vile alikuwa amekula kitu kichachu , ilikuwa ni kama vile alikuwa amepoteza uwezo wake wote.
Kila kitu kilirudi mwanzo , asingeweza kumgusa Athena ambae alikuwa ameshikilia mwili wa Edna kwasababu alishajua Athena alikuwa ni Edna na Seventeen.
Wakati akiona furaha kuona nafsi zote mbili yaani Edna na Seventeena wanaishi , wanawake ambao walikuwa na umuhimu mkubwa kwake lakini ilimpa msongo wa mawazo kuona kwamba hakuna namna ya kuwaokoa wote kwa pamoja.
Kadri Roma alivyowaza ndio alivyojiona anaweza kupata ukichaa na mwishoni alijikuta akijichapa vibao vya kichwa na mikono yake yote na kuanza kugugumia kwa kutoa mngurumo kama wa mnyama mkali.
Roma alichangua nywele zake kwa kujikuna kichwa huku machozi ya moto yakiloanisha uso wake.
Aliona uwezo wake hauna faida kama hawezi kumuokoa mama mtoto wake na mke wake.
Sharif hakuongea neno na alimwangalia Roma tu akipunguza hasira zake na alichokuwa nacho ni tabasamu tu akimsubiria Roma kutulia.
Dakika chache mbele Roma alionekana kuimarika kihisia na aliinua kichwa chake na kumwangalia Sharif na macho makavu.
Sasa kutokana mambo kufikia hatua hio na yeye pia ni kama amepata mwanga.
Ki ufupi ni kwamba huu mchezo wa zaidi ya miaka elfu ishirini uliokuwa ukichezwa ni kama wa kubahatisha tu kwa wote wawili Athena na Sharif.
Sharif alihitaji kutafuta mrithi wa kuendeleza alipoishia kama maelekezo ya mkuu wa enzi lakini alitaka mrithi wake ndio aamue ni nani anapaswa kuitawala dunia , binadamu au miungu?.
Upande wa Athena pia alikuwa akijua mtu ambae alimfungia Zeus nyakati zile alimwachia yeye makusudi kabisa na hata kama apambane nae hamuwezi.
Lakini wakati huo huo ni Sharif ambae alikuwa akimwangalia tu Athena kuendeleza mipango yake bila ya kuingilia huku akijua kwasababu Athena anao uwezo wa kusafiri mbele ya muda kinabii basi ni swala la muda tu kujua njia ya kufufua miungu.
Wakati Athena akimtumia Roma kama njia ya kufanikisha mipango yake na Sharif alikuwa akimtumia Athena kumtafutia mrithi.
Sharif hakuwa na uwezo wa kutabiri yajayo , alikuwa na uwezo wa kulinda dunia tu hivyo alitumia uwezo wa Athena kumtafutia mrithi wake.
Yaani ki ufupi ni kwamba kila mtu alikuwa na mpango wake , Hades wa zamanni alikuwa na mpango wake kichwani licha ya kwamba hakupinga moja kwa moja ufufuo wa ndugu zake , Athena pia alikuwa na mipango yake ya kukamilisha ufufuo wakati huo huo Sharif yeye alikuwa na mipango yake kwa kuwatumia miungu kumtafutia mrithi.
Wote kwa pamoja walikuwa wakitumiana isipokuwa tu Athena yeye alikuwa akifanya kazi kwa njia isiokuwa ya moja kwa moja kutimiza mipango yake.
Ki ufupi ni kwamba yanayowatokea binadamu msababishi mkuu ni Sharif , maana yeye ndio aliemuacha Athena kutimiza mipango yake yote bila kuingilia ili tu aje kumsaitia kupata mrithi.
Roma ambae tokea mwanzo akili yake ilitengenezwa , maisha yake kurefushwa ndani ya mpango LADO na hata kuja kujifunza mbinu ya andiko la urejesho na kulielewa kwa viwango vya juu alikuwa akihesabika kama mrithi ambae alimridhisha master namba moja.
Ijapokuwa Sharif hakujisumbua sana kuhusu nani atashinda katika vita baina ya viumbe wa dunia na miungu yeye hakutaka kuona mrithi aliemchagua akishindwa na Athena kwasababu tu ya hisia zake za kimapenzi , alitaka awe kama yeye ambae aliamua kuachana na kila matamanio yake yote kama vile kumpotezea Aoiline ili mradi kutii maagizo ya mkuu wa enzi kupitia wajumbe wake.
Kwa namna nyingine unaweza kusema pia ni shindano kati ya Aoiline na Sharif kujua nani ambae alifanya maamuzi sahihi miaka elfu hamsini iliopita.
Athena upande wake aliamini kwamba Roma atapotezea usalama wa binadamu kwasababu tu alikuwa amekufa na kuoza kimapenzi kwa wanawake hao wawili yaani Seventeen na Edna , hata kama atajua kwamba alimdanganya na kumtumia asingeweza kuchukua hatua ya kumuua yeye katika mwili wa mpendwa wake.
Kwahio Athena na yeye alikuwa akicheza kamari ambapo kufanikiwa ama kutokufanikiwa kulitegemeana na maamuzi ya Roma.
“Kwa maana hii , vitu vyote ambavyo nilikutana navyo wakati wa kukutana na Edna vipo ndani ya mpango wa Athena ili tu kurudisha matokeo ya unabii wake wa mwanzo?”Aliuliza Roma kwa sauti nzito.
“Kama nilivyokwisha kusema , alihitaji kufanya marekebisho ya makosa yake , mwanzoni kama Seventeen asingekufa mbele ya macho yako basi ungeendeleza ukichaa wako wa kuua watu dunia nzima na kwa maana hio ni swala la muda tu ungekuwa tatizo kwa dunia nzima kwa kupanikisha watu na mataifa mbalimbali na kugeuka adui wa binadamu’
“Lakini ukiachana na hayo , kwasababu mimi sio yeye ninaweza kukisia kiasi kidogo tu cha mipango yake yote , lakini bado lazima itakuwa ni kutokana na ramani ya unabii wake wa mwanzo , kwa maana kwamba uwezo wako ungeendelea kuwa mkubwa sana kutokana na kupigana kusiko isha , lakini mwisho wa siku hakuna alietarajia kama Seventeen atakukimbia akiwa na mtoto kutokana na mapenzi yake ya dhati kwako, akiamini kukuacha utaacha kuua na kutubu na kutokufa mwishowe , mara baada ya kurudi kwako Tanzania uliamua kuishi maisha ya kawaida na ukaacha na tamaa za kuona damu kitu ambacho Athena hakukitarajia kabisa .Haukua mtu ambae unaweza kuacha kuua kirahisi na kuzembea bila kazi yoyote maisha yako yote, haikuwa mipango ya Athena kukuona ukiwa hivyo”
“Hivyo basi mara baada ya kushughulikia swala la Lanlan , Athena hakujali tena kurudisha nguvu yake yote ya kiroho na moja kwa moja akaingia katika mwili wa Edna , mara baada ya kukutana na wewe katika sura ya Edna aliamua kutumia unabii wake kukutengenezea njia za kupita , mwanzoni alikuwa akimtumia Yan Buwen kupitia jiwe la kimungu ambae aliwezesha kuitumia nishati ya Ant – matter na kukuletea ushindani mkali lakini kuna vitu havikumridhisha kuhusu Yan Buwen na akatabiri kifo chake kwa kumuingiza Joseph Bikind(Lekcha) ambae alishamuandaa muda mrefu ambae ndio alikuwa hatari zaidi ya Yan Buwen na ulikuwa ni mpango mujalabu sana kumchagua Lekcha maana ulijikuta ukipambana nae mpaka ukaja kuingia kwenye ulimwengu mwingine kupitia mnara.
Yan Buwen kwa upande wake utafiti wake ulikuwa ni kutengeneza miungu feki kwa kukusanya nguvu ya kiroho kutoka katika Dhana mbalimbali ikiwemo Hollygrail, Thanatos na kadhalika ili tu kuimarisha Clone ya sura yako lakini mpango huu ulionekana kubuma kutokana na kwamba haukuchangia vizuri kwenye matokeo ya unabii wake hivyo aliupotezea mara baada ya mtafiti mwingine aliemwandaa kupitia Project Pro Human kufanikiwa kugundua sayansi ya kutumia elementi za dunia tofauti na nishati ya Ant-matter kufufua moyo wa Gaia, hivyo kwa lugha nyepesi alipotezea tafiti zote za Yan Buwen”
Kila sentensi alioongea ilikuwa ni kama ngurumo ya radi katika masikio ya Roma , ijapokuwa alikuwa amejiandaa lakini hakuamini Athena alikuwa amefanya mambo mengi namna hio kwa siri.
Roma aliona alikuwa amepitia katika hatari nyingi lakini zote alikuwa amezipita , kuna hata muda mtu alievaa joho la rangi nyeusi na mask alimuokoa kule Australia pengine yote hayo yalikuwa ni maagizo ya Athena.
Ilikuwa sahihi kabisa kwa Roma kuwaza hivyo , mwanzoni alihitaji Roma kuua sana tu kama kichaa ili kuwa na maadui wengi na kupitia changamoto hizo za maadui uwezo wake ungeendelea kuimarika maradufu sana , lakini mapenzi ya Seventeen kwenda kwa Roma yakamuokoa pale mwanamke huyo alipoamua kumuacha Roma baada ya kuona hana nia ya kuachana na ukichaa wake wa kuua.
Roma mara baada ya kushuhudia kifo cha Seventeen kwa macho yake kule kuua kulipoa kabisa mara baada ya kujua nia ya Seventeen kupitia janga la namna ile.
Kipindi haya yanatokea Athena alikuwa usingizini lakini haikumaanisha kwamba mipango yake ilikuwa haiendelei lakini kutokana na kutosimamia njia za unabii wake baada ya kuamka ndio anaona kabisa unabii wake unavyopaswa uwe umebadilika.
Mchoro wa Unabii ambao alimuonyesha Naira ndio ilikuwa ni hatima ya unabii wake , kama alivyosema katika kauli yake kipindi wanaongea sura ya mwanamke katika mchoro ule haikupaswa kuondoa tabasamu , kadri picha itakavyokuwa katika tabasamu ilimaanisha ndio namna ambavyo unabii wake unaenda sawa sawa , lakini baada ya kuamka pengine mwanamke hakuwa katika tabasamu na alikuwa amenuna kama mchoro wa unabii uliotolewa na Vatican.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Athena alikuwa akishindana na unabii , alikuwa akishindana na hatima ya binadamu , alikuwa akishindana na hatima ambayo aliwekewa Roma kuja kuwa mwangalizi baada ya Sharif.
Ni dhahiri kabisa kulikwepo na unabii wa Roma kukidhi vigezo vya kuwa mwangalizi kwa kumrithi Sharif, unabii huo Athena aliufahamu lakini akaamua kuubadilisha kwa kubadilisha matukio yanavyoenda na hatimae historia.
Sasa kifo cha Seventeen hakukitarajia lakini vilevile hakutarajia ujauzito wa Seventeen , hakutarajia Roma ataacha kuua kama alivyokuwa mwanzo na kurudi Tanzania na kuwa mbeba mizigo na kuishi katika chumba kimoja cha kupanga.
Hivyo ili kurekebisha makosa akaamua kumuingia Edna akijua fika ni pacha wa kufanana wa Seventeen na akamtumia Edna kumfanya Roma apende kama alivyompeda Seventeen.
Kitendo cha Roma kupenda ilimaanisha kabisa lazima awajibike kwa wale ambao anawapenda kwa maswala yote ikiwemo ulinzi na hapo ndipo alipomuingiza Yan Buwen kuwa tisho la usalama wa watu wake wa karibu , alijua kadri ambavyo Yan Buwen atakuwa tishio ndio Roma atajitahidi kupandisha uwezo wake ili kumlinda anao wapenda.
Kwahio ukiachana na kwamba Athena alilenga tafiti za Yan Buwen kumsaidia katika kufufua miungu vilevile alitumia tamaa za kimwili za Yan Buwen kumletea Changamoto Roma , pengine Yan Buwen alijua mrembo Athena alikuwa akimpenda Roma au alikuwa akimhadaa kumuonyesha alikuwa akimpenda Roma ndio maana Yan Buwen kujenga kinyongo kikali zidi ya Roma.
Lakini baadae Naira kupitia tafiti zake aligundua mbadala wa kufufua moyo wa Gaia kwa kutumia elementi za dunia nje ya nishati ya Ant- matter
“Kuna kitu kingine kilichonivutia sana wakati wa kuangalia haya yote ni kwamba , kati ya miungu watatu yaani Hera , Hephaestus na Hermes hawampendi Athena na ndio maana Hera aliamua kwanza kujifunza mbinu za nishati ya mbingu na ardhi na kisha akahamia katika mwili wa jinni na kujifunza mbinu ya kutabiri ambayo haikuwa nzuri sana kama ya Athena ambae alizaliwa na Karama hio lakini hata hivyo bado ilikuwa na maajabu yake kwani iliweza kutabiri mambo mengi ya baadae kwa usahihi
Hawa wote hawakuchagua miili ya majini na ya Vampire bila sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kuongeza umri wa kuishi bila kuhama hama katika miili mingine kuepuka kulala muda mrefu , walifanya hivi ili kuvuruga mpango wa Athena wa kutafuta Moyo wa Gaia ulipo wakati Athena akiwa usingizini akisubiria kuamka katika mwili mwingine , baadae wakifanikisha wamuue Athena kama kiongozi , nadhani umesikia kuwa Athena ana uwezo wa kutawala fahamu za miungu wa chini yake , hio ni moja ya sabababu ya kutaka kumuua lakini kwa bahati mbaya mipango yao ilifeli”
“Kwa mfano kuhusu ile Dhana feki ya Magical Girdle ulikuwa ni mpango ambao waliamini kama Edna atakuwa hatarini Athena atakosa jinsi na kuonyesha uwezo wake kumlinda Edna na hapo wewe baada ya kufika eneo la tukio ungeweza kumuona Athena katika mwili wa Edna lakini Athena alijizuia mpaka mwisho na hakumsaidia Edna na ikatokea tu ukawa umefika ndani ya muda , haikuwa hivyo tu waliamua pia kumtumia Chriss kutaka kumuua Edna lakini kwa bahati nzuri Athena alishafahamu hila hio na kumtumia moja ya mshirika wake kumlinda Edna”Aliongea Sharif na sasa Roma ni kama anapata majibu.
“Vipi kuhusu Ant- Illuminat na Hades wa Zamani?”Aliuliza Roma kwa shauku mara baada ya kukumbuka kitu muhimu.
“Tunaelekea huko taratibu…Kulikuwa na siku nyingine pia nadhani unakumbuka mara baada ya Hermes kuingilia akitaka kukuzuia kumuua Denisi , ule pia ulikuwa ni mpango wao tokea mwanzo wa kutaka kuvuruga mpango wa Athena , mwanzoni kama ungemuua Denisi mdogo wako ingekuwa ngumu kwako kukubali kurudi katika familia ya ukoo wako na ungekuwa upande mwingine tofauti na serikali ya Tanzania ambayo inaongozwa na baba yako lakini Athena bado hakutaka kuingilia lakini mwishowe aliamua kutengeneza mpango mwingine ambao utamfanya Denisi kupoteza uhai”
“Kuhusu Ant- Illuminat kusudi la mwanzo la kuanzishwa kwake sio kama la sasa , kama ilivyo kwa Freemason kusudi la mwanzo la kuanzishwa kwake sio kama la sasa”
“Unamaanisha nini?”
“Illuminat ilianzishwa chini ya ushawishi wa miungu hili sitoongelea sana maana lipo kibinadamu zaidi lakini linahusiana na maswala ya kidini zaidi na haliingiliani sana na wewe , vilevile Ant- Illuminat ilianzishwa chini ya ushawishi wa miungu na ilikuwa juzi tu zaidi ya miaka elfu moja iliopita , Hades wa zamani na Athena walicheza karata nyingi sana katika kuanzishwa kwa umoja huu lakini wote walikuwa wakilenga shabaha moja , Athena na Hades wa zamani waliamua kugeuzana maadui wa faida na hili lilikuwa moja wapo ya ombi la Athena ukiachana na kukupatia uungu wake na Dhana ya helms of invisibility , unachopaswa kuelewa tu Hades alikuwa neutral katika kufufuliwa kwa miungu na yote ambayo amefanya Hades yalikuwa maombi ya Athena , kuna muda ili ufikie malengo unahitaji mshindani ambae hana hila tofauti na walivyo Hera na wenzake na huyo ndio Hades alivyokuwa kwa Athena”
“Athena alisumbuka sana kuweka mambo sawa kwa ajili ya kudumisha unabii wake lakini hata hivyo kulikuwa na baadhi makosa madogo madogo lakini napaswa kumkubali kwani licha ya changamoto zote aliweza kuzishinda na kukuruhusu ufikie levo kubwa ya mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi mpaka leo hii tena ndani ya muda mfupi tu lakini wakati huo huo kunifanya mimi kuvutiwa na uwezo wako na kukupa fursa ya kufanya maamuzi”
“Bora hara nisiwe na hizo nguvu , wewe mwenyewe umeshindwa kufanya maamuzi na ndio unataka mimi nibebe lawama?”Aliongea Roma akiwa na tabasamu.
Sharif alisimama akiwa na tabasamu lisiloelezeka na kisha alimshika Roma bega kwa kulipiga piga.
“Dogo umekosea , nilishafanya maamuzi miaka elfu ishirini iliopita ambayo ni kuwa Neutral kwa pande zote , sitokulazimisha kwa lolote kama utaamua kumtetea Athena na kuacha kupigana ni sawa tu , nimekuja hapa siku hii kwa ajili ya kukueleza ukweli ambao unastahili kujua , kuhusu mengine ni juu yako na hatima ya binadamu pia, misheni yangu ilikuwa ni kulinda dunia na sio binadamu moja kwa moja wala kuingilia imani zao na matendo yao , vilevile kwa miungu sikupaswa kuwaingilia”
Mara baada ya kuongea kauli hio Sharif aligeuka na kupotea kama upepo bila kuacha ishara yoyote nyuma.
Hata kwa Roma aliekuwa na uwezo wa juu hakuweza kujua amepotea potea vipi kwani ni kama ameyeyuka.
Hatimae Lounge ya bar hio katika hoteli ya JR ilirudi kimya kwa mara ningine , Roma alijikuta akiegamia sofa akiangalia mwanga hafifu wa taa uliokuwa ukimulika kana kwamba anaushangaa.
*****
Ilikuwa ni nusu mwezi tokea kuharibiwa kwa mfumo wa kiutendaji wa ulinzi wa Gereza la Roho ambalo hufungia miungu na majini , Dhana ya Reverse Dhamachakra ilionyesha kufanikisha lakini wakati huo ile kasi yake ilionekana kupungua.
Ule mng’ao wake wa Dhahabu haukuwa mkali kama mwanzo , kulikuwa na msisimko mdogo sana uliokuwa ukitoka katika Dhana hio na wakati huo nguvu nyingi hasi ilikuwa imejikusanya katika eneo dhaifu la ulinzi wa safu ya gereza hilo.
Muda huo miungu tisa walikuwa wakiangalia sehemu hio Dhaifu kana kwamba kuna kitu wanachokisubiria.
“Haijawa na matokeo mazuri sana lakini hio safu haiwezi kushikilia kizuizi kwa muda mrefu”Aliongea Hephaestus kwa kujiamini.
“Naona unajigamba sasa , wewe huoni ni kama hili swala linachukua muda mrefu na kutupotezea muda tu hapa?”Aliuliza Ares akiwa kachukia.
“Haina maana hata nikikuelezea kwasababu punguani kama wewe unachojua ni kupigana tu na haujui hata nguvu ya ulinzi wa Gereza unavyofanya kazi”Aliongea Hephaestus akimwangalia Ares kwa macho ya dhihaka.
Ares kauli ile ilimkasirisha sana na alitaka kumshikisha adabu Hephaestus lakini jicho baya na la kikauzu la Athena lilimtuliza na kisha alimgeukia Hephaestus akimpa ishara asimchokoze mwenzake na kusababisha matatizo yasio na maana , akiwa amenyoosha mkono wake juu angani alionekana kushikilia kitu flani.
Kiumbe kilichovalia mavazi meusi kilionekana palepale , alikuwa ni Mtu mwenye Mask na alionekana kuhangaika kujinasua kutokana na kushikwa na mikono ya Athena kupitia kanuni za anga.
“Nisamehe mimi .. sina nia mbaya kujificha”
Miungu wengine hawakuwa na macho ya kuona kama ya kwake hivyo hawakuweza kuhisia uwepo wa mtu na waliishia kushangaa kuona Athena kakamata mtu.
“Hivi ulidhani sitokuona kwa kujificha mbali?”
“Sikutaka kuwasumbua ndio maana nikaangalia kutokea mbali”
“Athena hicho ni kiumbe gani , mbona kama sio binadamu wala jini?”Aliuliza Aphrodite kwa mshangao
Athena mara baada ya swali lile alimwachia yule mtu mwenye Mask.
“Unaweza kujionyesha sasa , haina haja ya kuendelea kujificha kwenye Mask”Aliongea Athena.
Mara baada ya kauli ile kutoka kwa mtukufu Athena kiumbe kile hakikutaka kuchelewa hata sekunde na ilikuwa ni kama vile umetokea moto ghafla kama wa kipepo ulioanza kuyaunguza mavazi yake na ile Mask.
Punde tu kitu cha ajabu cheusi kama ukungu kiliweza kuonekana mbele ya miungu.
Ilikuwa ni kama ukungu mweusi uliozunguka kile kiumbe na kufanya iwe ngumu kuona sura , ijapokuwa walikuwa wakiona umbo la kibinadamu lakini ile sehemu ambayo ilipaswa kuwa kichwa kulikuwa na kitu kama fuvu.
Kiumbe hicho chenye muonekano wa kutisha kiliwafanya miungu kupiga hatua moja nyuma huku wakikunja sura kama wameingiwa na kichefu chefu.
“Kwa miaka kadhaa iliopita hiki kiumbe kimekuwa kama njia ya mawasiliano kati ya Zeus na mimi ni jini aliezaliwa katika umbo la kivuli ambae kwasasa ni Mzimu wa jini mkubwa wa kipepo aliewahi kuwepo , ijapokuwa huu mzimu una uwezo mkubwa kulinganisha na levo ya maji ya upako lakini upo vizuri kwenye kujificha na kuwa katika sura tofauti tofauti”Aliongea Athena.
“Ni mzimu wa jini la kale?! , imewezekana vipi kutoka katika gereza la roho?”Hera aliuliza kwa mshangao
“Haha.. haha.. hahaha…ukweli ni kwamba sio kama nimetoka nje lakini mimi ni moja ya majini pepo wa tofauti sana”Aliongea huku akitoa kicheko cha ajabu mno.
Miungu palepale waliweza kuelewa ilionekana mzimu huo uliweza kutoka nje ya gereza kwasababu ya kuwa na miili mwili
Wakati jini Kivuli anazaliwa alikuwa na mwili wa kawaida na wa kivuli , miili yote ilikuwa chini ya udhibiti wake na ilikuwa na uwezo sawa .
Sasa mwili wa kawaida ili mradi tu utakuwa hai basi ule wa kuvuli unaweza kuwa popote.
Miaka mingi iliopita wakati wajumbe walipokuwa wakitenganisha majini pepo watukutu katika gereza la roho Jini Kivuli alikuwa akijua hana uwezo wa kuwashinda hivyo alijiengua kutoka katika mwili wake wa kivuli ambao ulikuwa na uwezo wakujificha na akajifanyisha amekufa kwenye vita , sasa mara baada ya mwili wake mkubwa kufungiwa katika gereza alitafuta namna ya kurudia mwili kivuli ambao ameuacha nje.
Wajumbe hao licha ya uwezo wao haikumaanisha kwamba walikuwa wameondoa majini yote kwa kuyafungia ndio maana hata yale walioyabakisha waliyawekewa mtego , majini walikuwa wengi mno karibia dunia nzima , sasa mwili kivuli ulibakia nje wakati roho ikiwa katika mwili mkubwa na mara baada ya muda mfupi alikuwa na uwezo wakuifanya roho yake ya nje kuwasiliana nae kutokana na kuwa na miili inayofanya kazi ndani na nje , sasa hapo ndipo mwili kivuli uliwasiliana na Athena na mwili wa kawaida uliwasiliana na Zeus na muda mwingine alitumia mwili wa kivuli kwa ajili ya kufanya maelekezo ya Athena bila hata ya kwenda mwenyewe.
“Umelificha hili swala vizuri sana , kumbe ulikuwa na mawasiliano na Zeus muda wote huo hatuambiani?”Aliuuliza Hera akionyesha jambo hilo lilivyokuwa chungu kwake.
“Tumeanza kuwasiliana miaka miwili iliopita , kwasababu Kivuli alikuwa mbali na mwili wake mkubwa hivyo alikuwa na wasiwasi wa kukutana na majini watu ambao wataweza kumuua , ilichukua miaka elfu kumi kuweza kupona katika hali ya kifo , kabla ya hapo sikuwa nikijua hali ya Zeus ndani ya gereza”
“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Zeus amewashinda majini pepo wote wa zama za kale na mishetani ndani ya gereza , kwahio ndio kwamba tuna vijakazi wa kutosha tu sasa hivi?”Aliuliza Hermes na tabasamu la kifedhuli.
“Ninachojua majini pepo wengi na jamii ya mashetani hawajazaliwa kutoka katika miili kamili na hata uwezo wao unaenda taratibu taratibu na mara nyigine walikuwa wakivaa miili ya binadamu au wanyama kuonekana lakini kwa huyu Kivuli mpaka kufikisha levo inayolingana na maji ya kiroho ni lazima liwe ni la kipekee , majini pepo wengi ni wabaya wa sura na wanatisha mno kama unataka wawe vijakazi wako unaweza kuwatumia”
Jini Kivuuli alisikiliza ki uwoga woga na ilikuwa ni kwa bahati mbya hakuwa na uwezo wakuonyesha muonekano wa kibinadamu vinginevyo maelezo ya Athena yangemfanya kuonekana na aibu.
Ilikuwa kweli kabisa baadhi ya majini pepo na wale mashetani waliohesabika kuwa na nguvu kubwa waliweza kuuliwa na wajumbe wa mkuu wa Enzi makumi elfu ya miaka iliopita.
Lakini ukiachana na machache ambayo yalikuwa yamefungiwa ndani ya geereza hilo uwezo wao ulikuwa ni kidogo sana , sasa tofauti na kuendelea kushikiliwa na gereza hilo ni kheri kuwa huru hata kama watadhalilishwa na miungu.
“Kwa uwezo wa Zeus ni kawaida kuweza kuwashinda majini pepo wote wafungwa na kuwa mfalme lakini nina wasiwasi na mwili wake wa sasa , amewezaje kuishi katika mwili mmoja kwa miaka elfu ishirini yote , maana hawezi kutoka nje na kuhama kwenye mwili mwingine?”Aliuliza Apollo.
“Ana njia zake , utajua akishatoka”Alijibu Athena.
*****
Upande mwingine upepo wa baridi kali ulikuwa ukivuma juu ya bahari ya Meditterranian , wingu la kijivu lilikuwa limefunika anga lakini walisimama na hakuna upepo ulioweza kuwapeperusha.
Anjiu na majini wenzake kumi walipata kurudi kisiwani kwa Roma na habari za Edna kuwa Athena na ilikuwa ni kama bomu kwa kila mtu.
Hatimae wanawake hao walijua ni kwanini mara kwa mara Edna alionekana kumuacha Lanlan na kupotea.
Kuhusu Roma mhimili wa familia alikuwa amepotea na haikujulikana alikuwa wapi na iliwafanya kuwa na mawazo.
Kitendo cha kukosa wazazi wake wote kwa muda mmoja ilimletea Shida Lanlan na kusumbua kwa siku kadhaa lakini mwishowe Neema , Rose na wanawake wengine ilibidi watoe taarifa nyumbani kwa Afande Kweka na Blandina ambae mara baada ya kusikia habari hio alifanya safari ya kuja kisiwani na hakuwa peke yake hata Afande Kweka aliamua kutembelea kisiwani.
Blandina alikasirika mno mara baada ya kusikia Edna alikuwa ni Athena , aliona mtoto wake alikuwa akichezewa akili lakini ukiachana na mawazo yake mengine aliiishia kumlaumu Edna na kumuita kila jina baya.
Wanawake hao hawakupendezwa kusikia kauli za Blandina lakini walikaa kimya kwani hawakuwa na uhakika kama Edna alifanya hayo yote kwa akili zake , hakuna aliejua ukweli.
Walichojisikia ni huzuni kwa ajili ya Roma na hivyo ilipelekea kuwa na chuki kiasi zidi ya Edna.
Kwa Blandina Edna hakuwa na umuhimu mkubwa kama ilivyo kwa mtoto wake na hio ni kutokana na kwamba ndio mtoto pekee aliekuwa nae.
Alilalamika huyo lakini mwisho wa siku aliacha mwenyewe na sasa alichokuwa akitaka kusikia ni taarifa za Roma alipo tu , kila siku alikuwa akihimiza majini waliokuwa ndani ya kisiwa hicho na hata wanajeshi wa The Eagles kumtafuta Roma.
Lakini mwisho wa siku hakuna ambae aliweza kumpata kama Roma mwenyewe ndio aliamua kujificha , hata Sauron au Anjiu hawakuweza kumpata , lakini waliendelea kutafuta kutokana na maagizo yalitoka kwa mama yake Roma.
Upande wa Afande Kweka alikuwa hana wasiwasi wowote ni kama vile hakujali kile kilichomtokea Roma na alifikiria mbinu tu za hapa na pale za kumchekesha Lanlan.
Lakini Lanlan licha ya kwamba alifurahi uwepo wa babu yake lakini bado hakuwa na amani na hata ile hamu ya kula ilikuwa imempotea.
Kila mtu alikuwa katika wakati mgumu lakini sasa siku mbili baadae ghafla tu hali ilibadilika.
Ilikuwa ni vivuli tu ambavyo vilionekana vikisafiri kwa kasi kwenye anga kama vimondo vikisambaa kila uelekeo .
Mara baada ya Anjiu , Shombeli na wengine kuona tukio hilo walijikuta wakikamaa sura mara baada ya kuona hali imekuwa ya hatari.
“Majini pepo na mashetani wamevamia ulimwengu wa kawaida , Gereza la roho limefunguka!!”
Waliongea wote kwa kumaka wakiambizana.




SEHEMU YA 789.
Ni siku chache mbele tu hali ilikuwa imebadilika na kuwa mbaya zaidi , katika anga la China na majirani zake wingu kubwa lilikuwa limetanda , licha ya kwamba ilikuwa mchana ilikuwa ni kama usiku.
Ki uhalisia ni kwamba ilichukua nusu siku kwa kila eneo ndani ya dunia ambalo lina watu kubadilika na kuwa katika hali ya kutisha namna hio mara baada tu ya Gereza la Roho kuvunjwa.
Watu ambao walikuwa wakiepuka kwa namna yoyote baridi kali la kuumiza mifupa hawakuwa na uelewa juu ya janga la asili kwanini limetokea na kutisha hivyo.
Lakini wakati wakijiuliza kwanini joto kushuka licha ya jua kuonekana angani wanakuja kujua sio kitu kirahisi tu kama kushuka kwa joto.
Yale mapepo ambayo watu wa kawaida hawawezi hata kuelewa yalianza kuonekana moja baada ya nyingine katika sayari yote ya dunia , halikuwa ni swala la Afrika wala Ulaya tena , mapepo yalikuwa kila mahali.
Yale mapepo na maskeletoni ambayo watu waliishia kuyaona kwenye filamu sasa yalikuwa mbele ya macho yao mubashara, ilikuwa ni taharuki juu ya taharuki.
Wakati mengine yakipita tu na kuingia misituni mangine yalichagua kuingia binadamu na kuwashambulia na kufanya damu kila mahali kutapakaa.
Licha ya kwamba yalikosa miili lakini uwezo wao wa kuchanganya akili za binadau na kushambuliana wao kwa wao ulikuwa mkubwa sana.
Yaani ilikuwa ni swala la kumvamia huyu binadamu na kisha kumuua biadamu mwingine na kuacha mwili , ilikuwa ni kama binadamu wamegeuka mazombi.
Kama ingesemekana dunia ilikuwa ikitaka kuingia katika kizazi cha barafu na binadamu kuwehukwa na akili basi picha iliokuwa ikionekana ilikuwa ni zaidi ya neno kifo.
Awamu hio haikuwa swala la matajiri tu wala masikini , kila mtu alikuwa ni mhanga.
Kitu kikubwa ambacho watu walikuwa wakifanya mbele ya Maskeletoni hayo pamoja na mizimu hio ya kipepo ni aidha kuomba sana au kuswali wasivamiwe na mapepo kugeuka vichaa au kusubiria kifo mbele ya maskeletoni.
Hali ilibadilika ghafla sana hata wale watu waliokuwa na akili za ziada walishindwa kuelewa wala kufanya utafiti ya kinachoendelea na ilikuwa ni kujiuliza maswali ni nini kinaendelea huku wakihaha.
Majini watu kutoka miliki za kijini walijua uhatari wa hali mara baada tu ya kugundua ni wale majini waliokuwa katika gereza la roho.
Majini wa miliki ya Hongmeng hawakuwa wajinga kulinda gereza hilo la roho kwa miaka mingi vizazi na vizazi lakini hakuna ambae alitegemea ni karne hio gereza hilo litafunguliwa.
Punde tu Shombeli , Umini na wengine waliamua kujigawa na kusambaa kila kona ya dunia kwa ajili ya kushambulia majini pepo hao.
Kutokana na nguvu za majini hayo zilikuwa katika levo za nafsi na wengi wao akili zao zilikuwa chini haikuwa ngumu kudili nao na pengine ndio kitu cha pekee cha kushukuru.
Majini walishambulia mapepo hayo licha ya kwamba walijua dunia ni kama inafikia mwisho wake , lakini walijiambia kama wanaweza kuchelewesha basi watafanya hivyo.
Upande wa wanawake ambao walikuwa wakimsubiria Roma walichoka na wao mara baada ya kutokuonekana kwake na hawakuwa na jinsi ya kumsubiri tena na wale ambao walikuwa tayari katika levo ya nafsi waliungana na majini kushambulia hio mizimu , mapepo na maskeletoni.
Kutokana na kuwa na Dhana nyingi za kimaajabu ambazo Roma aliwapatia hawakupata shida sana ya kudili nayo lakini baadhi ya majini pepo wale wa kale walionekana kuwa ngumu sana kudili nao kutokana na uzoefu wao wa kivita na akili kubwa kama alivyokuwa jini Kivuli na wengine walikuwa katika levo yake.
Ndani ya siku mbili tu taarifa zilirudi majini zaidi ya miambili walishakufa kwa kuuliwa na baadhi walirudi wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana huku wakiwa wamewekewa sumu ya ajabu katika miili yao
Mwishoni Anjiu na wenzake wenye uwezo wa juu walitoa maagizo kama itatokea kuna mzimu au jini pepo lenye nguvu kubwa sana basi taarifa itolewe na wao wataenda kudili nalo , ijapokuwa sio njia salama lakini ndio iliokuwa imebakia.
Dunia ilikuwa imebadilika kutoka kuwa barafu na sasa ilikuwa ni kuzimu.Haikujalisha ulikuwa mfanyakazi wa kawaida , tajiri , mrembo , star au kiongozi wa siasa au mwanajeshi wa nyota zote kila mtu alikufa kifo kibaya aidha kwa kushambuliwa na maskeletoni au kuwehushwa akili.
Wengi ambao walisalimika ni wale ambao walijijengea nguvu ya kiroho kwa muda mrefu kupitia kusali na kuswali pamoja na wale wenye ushirikina wenye nguvu na wanaojjimilikisha majini roho, majini jamii ya watu walioshindwa kupata miili na kubakia viumbe wanapandisha levo zao kupitia binadamu..
Mpaka kufikia muda huo ni kama udhaifu wa binadamu zidi ya viumbe wasioonekana umedhihirika, maana makombora na bunduki hazikufanya kazi.
*****
Ni katika taifa la China upande wa kusini , jiji hilo ambalo lilikuwa likipendeza nyakati za usiku muda huo kilichokuwa kikionekana ni maiti za biadamu na wanyama ambazo zimesambaa kila mahali.
Mji ulikuwa kimya mno na hakukuwa na dalili hata ya ndege anaepaa angani , maduka makubwa ya nguo , viwanda na magari yalikuwa yametelekezwa .
Taifa kubwa kama la China ambalo limeendelea hawakuwa na kinga zidi ya baridi kali ilioikumba dunia , pengine ndio nchi ambayo imeathirika sana kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu , hali ilikuwa ikisikitisha kweli.
Sasa katika mitaa hio ambayo ilikuwa kimya mwanaume mweusi ambae alionekana kuchafuka kama chokoraa akiwa ameshikilia chupa ya Whiskey alionekana kutembea katikati ya mtaa.
Mwanaume huyu alionekana kama mlevi ambae hana makazi maalumu.
Naam huyu ni Roma Ramoni ambae alikuwa akidhurula kwa siku nyingi mno katika kila taifa bila sababu za msingi .
Tokea aachane na Sharif Roma hakujua ni wapi aelekeee wala maamuzi gani afanye.
Mara baada ya kukaa katika ile hoteli kwa usiku mmoja asubuhi kulivyokucha alitoka akiwa hana wazo lolote katika akili yake na ndipo alipoanza kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine , alianza bara la Afrika lote na kisha alijikuta akiwa ulaya na akaingia Asia, kwa namna ambavyo alikuwa akidhurula ni kama kuna kitu ambacho alikuwa akitafuta.
Sasa katika mitaa ya vijiji baadhi vya nchi hio ya Wachina Roma aliweza kuangalia namna ambavyo mizimu ilivyokuwa ikihaha huku na huko ikishambulia binadamu.
Lakini Roma hakujali hata pale aliposhuhudia binadamu wakinyonywa damu na nafsi zao kuibiwa, Roma alijifanyisha kipofu kabisa.
Mambo yote hayo kwake ni kama hayakuwa yakimuhuisu kabisa .
Majini pia ni kama yalikuwa yakijua Roma alikuwa na uwezo mkubwa na kwa utashi wao waliweza kusogea mbali bila kumsogelea.
Katika kila majiji aliopita kilichokuwa kikimvutia ni vinywaji tu vitu vya thamani vilivyotelekezwa kwake havikuwa na maana tena, alikuwa akiogopa kuacha kulewa kwani angeanza kufikiria ni kipi anapaswa kufanya , ki ufupi ni kwamba alikuwa akijisahaulisha kile kinachoendelea kupitia pombe.
Boom!!!
Ghafla tu mlipuko mkubwa ulitokea kutoka katika moja ya jengo la makazi mita kadhaa kutoka alipo.
Moshi mwingi ulionekana ukisambaa angani na ni palepale aliweza kuona mtu alievalia mavazi ya bluu akijitahidi kujitoa katika kifusi cha mchanga na matofali.
Sekunde chache mbele walionekana majini wawili mwanaume na mwanamke wameshikilia siraha ndefu wakimkimbilia mwanaume wa kibinadamu ambae amefunikwa na kifusi kumsaidia na wakimuuliza kama alikuwa ameumia.
Mwanaume alievalia suti ya rangi ya bluu uso wake ulikuwa mweusi na kulikuwa na dalili za damu kumtoka midomoni lakini aliishia kusugua meno yake akionyesha ishara kwamba hakuna tatizo , muonekano wake wa kuvumilia maumivu ulikuwa tofauti na ishara zake ..
Roma alisimama kwenye kona ndani ya mtaa akiangalia tukio hilo na palepale kulikuwa na hali tofafuti katika macho yake na alionekana kusita lakini hakuweza kusaidia zaidi ya kusimama tu.
Muda huo huo msichana ambae amvalia gauni la pink ambae ni jini mtu alionekana kumuona Roma ambae amesimama kwenye kona mbali na wao na alianza kumpigia makelele Roma..
“Usisogee hapa ni hatari , ondoka kabisa eneo hili”
Kabla msichana yule kukamilisha sentensi yake mwanaume aliekuwa pembeni yake alimkemea.
“Dada kuwa makini”Aliongea
Kutoka ndani ya jengo hilo lilitoka puto kubwa kama baluni jeusi ambalo lilianza kufuka moshi kuelekea mbele ya wale watu.
Yule mwanaume alisimama mbele ya yule mwanamke na siraha iliokuwa mikononi mwake ilimtoka kwa kuelekea upande wa lile puto.
“Bro Zomu kuwa makini , hilo ni shambulizi la sumu”
Mwanaume aliekuwa katika mavazi ya suti alipiga yowe akipotezea kuumia kwake.
Om! Wah ! Pah ! mi Hum!!
Yule mwanaume aliekuwa katika mavazi ya bluu alianza kunena kwa lugha ya kibudha maarufu kama mantra kama vile alikuwa akiimba.
Mwanaume yule alikunja ngumi yake na huku akitoa uchawi wa kufuta nguvu ile ya kipepo na kulipiga lile puto.
“Bang!!”
Sauti ya ajabu iliweza kutoka katika lile puto la ukungu na palepale ni kama vile lilibadilika na kuanza kutoa miale ikionekana ni kama linataka kupasuka.
Lakini ni dakika hio hio jitu la ajabu ambalo lilikuwa na mwili wa ukungu lilijitokeza kwa kuibukia kwenye lile puto.
Jitu hilo lilikuwa na mapembe mawili kwenye kichwa chake , midomo kama kipande cha chapati uliozungukwa na sharubu ndefu kama za chui, macho mekundu kama damu na mwili kama wa simba , juu ya mkia wake kulikuwa na vitu kama ufagio wa ajabu ambao ulifanya lizidi kuogopesha.
Jitu lile lilitoa tabasamu la ajabu mno la kutisha na kuanza kuchezesha mkia ule juu angani na kutengeneza wimbi ambalo liliwatupia mbali wale watu.
Watatu hao walionekana kutokuwa na nguvu za kutosha kupambana na mzimu huo na waliishia kutema damu.
Lile lizimwi liling’aka kwa sauti kwa namna ya majigambo huku likitoa moshi kama wa gari wenye sumu kwenda chini , kucha zake zililianza kurefuka na lilijiandaa kunyofoa shingo ya yule msichana na kunyonya damu yake.
Mara baada ya kuona mzimu huo wa jini pepo ukimsogelea yule mwaamke ilimfanya aogope sana kiasi cha sura yake kupauka alichoweza ni kufumba macho yake akikisubiria kifo.
Kabla ya tukio lile la kutisha kutokea , walichoweza kusikia ni mbweko wa maumivu kutoka kwa mzimu ule.
“Ghrrrrrrrr…!!!”
Moto uliokuwa kama nyoka nyoka ulionekana kuuzingira ule mzimu na kufanya uanze kutapa tapa lakini bado lilionekana kushindwa kujinasua kutoka kwenye kuyeyushwa na ule moto.
Kufumba na kufumbua lilipotea kama mvuke na kukawa kimya na ajabu ni kwamba ule moto ulinyonya ule moshi wote wenye sumu a kuwafanya wale watu kupumua vizuri
Watu hao watatu waliangalia kwa bumbuwazi kile kilichotokea na mpaka moto ule unapotea na kurudiwa na akili waliweza kuona yule mtu ambae alionekana kama chokoraa akiwaangalia
“Nyie wote watatu hata kama muungane mtakuwa na uwezo angalau wa maji ya kawaida lakini bado tu mnajaribu kushindana na pepo ambalo lipo levo ya maji ya barafu, kwanini ya kujisumbua kama mnataka kufa”Aliongea Roma na kisha aligeuza akitaka kuondoka.
Mwanaume na mwanamke walikuwa ni majini na walifahamika kwa jina la Zomu na Zato ambao walikuwa ni washirika wa miliki ya Kekexil, mwanaume alievalia nguo za bluu alikuwa ni binadamu mwenye mafunzo ya kijini aliefahamika kwa jina la Feilo.
Kama isingekuwa kwa watu hao kumchukulia kama rafiki na yeye pia kuwahukulia kama marafiki Roma asingejali kabisa kuhusu maisha yao.
“Hey! Subiri”
Zomu alijikuta akisimama licha ya kusita sita na kujikaa kumuita Roma .
Feilo na Zomu walisimama pia kwa haraka , neema ya kuokolewa uhai wao haikuwa jambo jepesi hivyo hawakutaka kudharau.
“Asante broo kwa kuokoa uhai wetu , naweza kujua jina lako , pengine nikipata nafasi naweza kukulipa fadhila baadae?”
Zomu alimpita Roma kwa mbele na kumwangalia usoni kwa namna ya kunuia au kutokunuia.
Roma alichukua chupa yake ya Whiskey na kupiga pafu moja na kisha alipunga mkono.
“Haina haja ,ondoka nipite”
Alimsukuma Zomu na kisha aliendelea zake kutembea kuingia katikati ya mji.
Lakini kabla hata hajapotelea Zomu aliita kwa nguvu,
“Bro Xiao Cheni!!”
Roma alishangaa kuitwa jina hilo na aliishia kusimama kama kagandishwa.
“Nipo sahihi , ni Braza Xiao Cheni”Aliongea kwa furaha na kumfanya Zato na Feilo kushangaa na kuuliza nini kinaendelea.
Wote watatu kwa haraka walimzingira Roma na kumwangalia kutoka juu mpaka chini kwa kupokezana.
“Umesema mimi ni nani?”Alimuuliza Zomu.
“Acha kujificha basi Braza ..tena nimekosea napaswa kukuita Braza Roma hehe..”
Awamu hio Roma aliona inashangaza na kjiuliza Zomu kamjuaje , ijapokuwa alikuwa katika muonekano wake wa kawaida lakini hawajawahi kuonana.
“Usishangae Braza , ni mara baada tu ya wewe kuondoka kipindi kile tuliweza kujua wewe ni nani halisi , kipindi kile uliweza kuvuruga miliki ya Kekexil na ukaeda pia kufanya katika miliki ya Xia , kila mtu anajua ulichofanya , ijapokuwa ulimwengu wetu wa kijini sio mdogo lakini sio mkubwa sana pia , ilikuwa rahisi kwetu kusikia habari zako , tulikutafuta sana na jina lako halikufahamika katika miliki zote hivyo tulijua ulitumia jina feki , ilikuwa ngumu kwetu kutokujua kulingana na matukio , kipindi kile ulitupatia vidonge vya kutosha na kama ukizingatia jambo lile sio majini wa kawaida ambao wana uwezo huo , sisi ni ni majini wa chini sana katika ulimwengu wetu na ilishangaza mtu kama wewe kutujali , kipindi kile hatukuweza kugundua uwezo wako halisi na hata sasa tumeshindwa kugundua na kama umeweza kuuficha namna hii na kuonekana wa kawaida lazima itakuwa ni wewe , kubwa zaidi ni muonekano wako wa kiafrika hehe”
Roma mara baada ya kusikiliza maelezo ya Zomu aliona kweli haikuwa ngumu kujua , kulikuwa na watu wachache sana wenye sura nyeusi ambao wana mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
“Kaka ni kweli ni yeye , Roma Ramoni?”Aliuliza mrembo Zato akimwangalia Roma kana kwamba amepata Hazina ya thamani ya juu sana.
Feilo ni kama alikuwa amekabwa na kitu kooin na kushindwa kuongea neno , jina la Roma Ramoni lilikuwa maarufu sana kama hadithi za mashujaa wa kale.
Miaka ishirini na saba au nane tu alikuwa ndio binadamu aliekuwa juu zaidi kuliko binadamu wote , binadamu mwenye uwezo wa kuingia ulimwengu wa majini na kufanya anavyotaka na kisha kuogopesha miungu kwa uwezo wake , haikuwa rahisi kuwa wa kawaida mbele ya binadamu mwenzake mwenye uwezo wa kutisha hivyo.
Roma alijua hakuna haja tena ya kujificha na aliishia kutoa cheko akiwaagalia.
“Nadhani ni Mungu alietukutanisha , naomba nichukue nafasi hii kuwapa ushauri , achaneni na maswala ya kujiingiza kwenye maji machafu , bado ni wadhaifu mno na machoweza ni kudili na mizimu ya uwezo wa wastani tu lakini sio hio yenye uwezo wa juu wa akili”
“Hata kama hatuyawezi lazima tupambane , bila ya sisi kujitokeza vipi kuhusu binadamu wa kawaida?”Aliongea Zato kwa hasira.
“Ndio sisi wote watatu tumeamua kuungana kuua majini pepo popote pale , ijapokuwa uwezo wetu sio mkubwa kama wakubwa zetu lakini tunaweza kujitahidi pia”Aliongea Feilo
“Rom,… Bro nadhani hutojali nikikuita kwa jina lako , ulikuwa umeenda wapi siku zote hizo , familia yako kule kisiwani wana wasiwasi kufa , kila mtu sasa hivi anajua mke wako ndio Athena lakini kukimbia sio suluhisho , angalau unapaswa kurudi , lazima kutakuwa na njia kama mkishirikiana pamoja kimawazo”
“Ni kweli kabisa ni bora hata utudanganye sisi , lakini kama umeweza kutuokoa inamaanisha unaweza kumuokoa kila mtu , acha kupoteza muda wako”Aliongea Zato akiwa na wasiwasi.
“Kama ni rahisi hivyo ningeshafanya muda mrefu ,, hamuwezi kuelewa hata hivyo , kuna baadhi ya vitu haviwezi kufanyika hata kama unao uwezo”Aliongea Roma kwa kucheka kivivu na baada ya hapo alimshika Zomu bega akitaka kumpita.
Mrembo jini Zato alionekana kukasirika na palepale alimsogelea Roma na kumshikilia mkono wake kwa ngugvu.
“Huruhusiwi kukimbia tena , hivi wewe ndio Roma kweli ambae unavumishwa kila kona , mtu ambae haogopi mbingu na ardhi , ndio tuseme unamuogopa mke wako katika hali hatarishi kama hii ya kifo na uhai , hivi wewe ni mwanaume kweli?”
“Zatoo..”
Zomu alionekana kuogopa mno Zato kumkasirisha Roma na haraka sana alitaka kumzuia asiongee ujinga.
“Kaka kwani nimekosea nini , binadamu wanateseka dunia nzima lakini hebu muone huyu mtu mwenye uwezo wa kubadili kila kitu kaamua kukimbia na kunywea , mbaya zaidi anaikwepa hata familia yake , anajua kabisa ni kosa kujificha lakini bado anafanya , nyie mnamuonaje si mtu muoga muoga?”
Roma uso wake ulikuwa umebadilika na kutisha , maneno ya Zato yalionekana kuwa kama kisu kikali ambacho kinatonesha jeraha la moyo wake na kisha kulimwagia chumvi .
Zomu na Feilo walijikuta wakikosa usemi , ukweli ni kwamba hata wao waliona aibu juu ya matendo ya Roma lakini hawakuwa na ujasiri wa kumwambia wazi wazi.
Zato palepale alimuachia Roma na kufuta machozi yake na kisha alipotea na alipoibukia alikuwa na mtoto mdogo ambae ana umri wa miaka mitano au sita hivi , mchina aliefungwa fungwa na jaketi zito mno , macho yake yalionekana kuvimba kutokana na kulia sana.
Alikuwa ni msichana na alionekana kuogopa mno na ilishangaza kuwepo ndani ya hilo eneo , muonekano wake ulikuwa ni wa mduao wakati wa kuangalia watu hao.
“Unajua ni kipi amepitia huyu mtoto wakati tunafika hapa , bibi yake ndio mtu pekee aliekuwa nae na wazazi wake inaonekana wamekimbia, ule mzimu umenyonya damu ya bii yake mpaka akawa mkavu , kama sio kilio cha huyu mtoto ingekuwa ngumu kugundua kulikuwa na mzimu maeneo haya na kama tusingejitokeza ndani ya muda nini kingemtokea?, wapo watu kama mia tu ambao wana mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi na kuna majini pepo vichaa zaidi ya elfu moja dunia nzima , wewe si una binti pia , kwahio mtoto wako ndio wa thamani kuliko wa wengine , kama watoto ambao wangeweza kukua watakufa kwasababu yako basi aliewaua sio haya mazimwi bali ni wewe na ubinafsi wako na uoga”
Roma aliishia kumwangalia yule mtoto mdogo anaetia huruma kwa woga huku maneno ya Zato akigonga ngoma za masikio ake kama vile ni mwangwi ndani ya bonde.
Akili yake ilikuwa ni kama inamwambia Lanlan ndio alikuwa mbele yake na alikuwa akimlilia kwa woga.
Roma macho yake yaligeuka na kuwa mekundu huku akiwa na aibu na aliishia kukunja ngumi yake huku akijitahidi kujidhibiti hisia zake kwa kutoa pumzi nzito.
“Kila mtu anafikiri umepatwa na shida ndio maana umeshindwa kurudi mapema lakini inaonekana ni tofauti na mawazo ya kila mmoja .. hata kama unaniona kama mjinga mimi sijali , mimi Zato leo hii nitaongea na wewe kwa kuvaa uhusika wa mwanamke binadamu.. kama ningekuwa mke wako basi nisingeshukuru kwa wewe kunikimbia kwa kuogopa kuniumiza ,, naona ni kama tusi kuolewa na mwaname muoga kama wewe ambae anaogopa kukabiliana na uhalisia na kuishia kujificha, ”
Mara baada ya kuongea Zato palepale alipotea na waliweza kumuona akingia kwenye jengo hilo la makazi.
Zomu na Feilo waliishia kuangaliana na nyuso zisizo za kawaida huku wakionekana kutabasamu kwa wasiwasi.
Ijapokuwa maneno ya Zato hayakuwa mazuri na yalijaa ukiburi lakini kwa kawaida walielewa alikuwa na hasira.
Kwa jini kama huyo wa kike , Roma alikuwa ni kama somo ambalo amelipenda kwa siri lakini anakuja kugundua mtu ambae ni kama shujaa alikuwa havumiliki, ni sawa kwake tu kuwa na hasira.
Isitoshe alikuwa ni jini na maisha yake hayakuwa yakijali sana kuhusu binadamu lakini alikuwa na huruma kumzidi hata Roma ambae ni binadamu.
“Bro , dada yangu ameenda mbali lakini hana nia mbaya na wewe , tunaelewa hili sio jambo rahisi kwako , lazima kuna vitu ambavyo hatuvijui na ni wewe tu unaevijua lakini hata hivyo haijalishi nini kitatokea kwa binadamu na sisi majini lakini tutaishia kukutegemea wewe kama tumaini letu la mwisho , ni sisi kutokuwa na uwezo na kama tukifa basi ndio hatima yetu”Aliongea
“Unajua nini bro , mara nyingi nakuzungumzia , umekuwa sehemu ya maneno yangu kila siku , sisi wote tunakuonea wivu kwa kijana mdogo kama wewe tena binadamu kufikia levo hio , imefikia mpaka hatua kuota vipi kama uwezo wako ungekuwa wangu… ningekuwa mkubwa na wa kuheshimika kiasi gani haha… tunajua ni ujinga lakini tutafanya nini kama ndio kitu tunachoweza kujifariji nacho , lakini siriasi kabisa tunakuonea wivu kwa kuwa na uwezo huo na bahati kitu ambacho hatuwezi kuwa nacho , haijalishi ni maamuzi gani utafanya lakini matumani yetu ni mimi na Feilo kutokukuchukia kama wengine , tunaweza tusiwe kitu mbele yako lakini kwa sisi ni heshima kuwa na koneksheni na mtu kama wewe…”
Zomu na Feilo waliishia kuonyesha tabasamu na kuacha kuongea kisha na wao walizipiga hatua kuingia kwenye jengo la makazi kwa ajili ya kumtafuta Zato .
Roma aliishia kusimama eneo moja kwa muda akionekana kuwaza na kiini cha macho yake kilikuwa kikicheza mno kama vile upungufu wa melanin.
Baada ya muda mfupi Roma aliishia kutoa kicheko kama cha kujionea huruma na kuinua uso wake kuagalia anga.
Roma alitupa Chupa ya Whiskey alioshikilia mkononi na palepale alipotea katika mtaa ule.
Punde tu katika visiwa vya wafu maili laki moja na elfu nane mbali Roma alikuwa ashabadili na kuwa katika unadhifu na palepale alipotea na kuibukia katika ngome yake.
Katika Floor ya kwanza Dorisi , Yezi , Najma , Nasra na wengine walionekana kuwa kwenye mkao kama vile wapo kikaoni.
Lanlan yeye alikuwa amekaa na babu yake akionekana kusikiliza baadhi ya hadithi za zamani .
Kitendo cha ghafla cha Roma kujitokeza kiliwashitua wote lakini Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kupiga makelele.
“Dadiiii…!!!”
Roma aliangalia warembo wake na ndugu zake huku akiwa na macho ambayo ni kama anataka kutoa mahozi na aliishia kumkumbatia binti yake ambae alimrukia kifuani kwa furaha.
Roma keshafanya maamuzi , unadhani atafanikiwa kumrudisha mke wake?
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

CREATOR: SINGANOJR

SEHEMU YA 790.

“Yaliokuwako ndio yatakayokuwako ,yaliotendeka ndio yatakayotendeka, wala jambo jipya hakuna chini ya jua .Je! kuna jambo lolote ambalo watu husema juu yake , Tazama , ni jambo jipya?,Hilo limekwisha kuwako , tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi(Mhubiri 1:9-10)”
Mara baada ya kusikia habari za kurudi kwa Roma , wanawake wote pande zote za dunia wakipambana na mapepo , mizimu na maskeleton walirudi mara moja Visiwa vya wafu.
Blandina alilia sana kwa furaha akiishikilia mikono ya mwanae huku akimsihi asifanye jambo lolote la kijinga na kuuona ukweli waziwazi na kutoendelea kufanywa kipofu na Athena.
Roma aliishia kutingisha kichwa kukubaliana nae na mwishowe kumfanya Blandina mama yake ambae hakupata usingizi kwa muda mrefu kwenda kulala sasa kwa amani kufidia siku zote alizokuwa macho.
Upendo wa familia na wapenzi wake ulimfanya Roma kuhisi hali isioelezeka , kulinganisha na siku ziliozopita katika hali hio upendo huo ulikuwa na nguvu kuliko kitu chochote.
Hakuna aliemuuliza Roma alikuwa wapi , wala anachopanga kufanya ni nini na hata kama Roma hakupanga kumtaja Edna hakuna ambae angethubutu kutaja jina lake.
Roma upande wake alimfariji Bi Wema na kumwambia kwamba Edna hajafa ni kwamba tu hawezi kuamka kwa muda.
Bi Wema alielewa alichokuwa akimaanisha Roma na alijisikia vizuri japo kidogo tu , isistoshe alikuwa akiogopa nafsi ya Edna imeuliwa na Athena , alihisi maumivu makali kwa kipindi chote kwa kudhania ameshindwa kumlinda Edna kama alivyopewa jukumu na wazazi wake na ndio imekuwa kwaheri.
Ron , Sauron , Makedon na viongozi wa juu wa jeshi la The Eagles waliokuwa karibu na Roma walifika haraka wakiwa na wasiwasi na Roma alikutana nao na kufanya kikao cha muda mfupi huku akiwapa maelekezo ya siri ambayo hakuna mwanafamilia alieweza kuyajua.
Lakini kwa kuangalia nyuso za wazungu hao wakati wakitoka nje ya ukumbi wa kikao haikuwa ngumu kuelewa jambo ambalo Roma alikuwa akiongea nao lilikuwa siriasi mno.
Wakati wa usiku Roma aliamua kujituliza na kukaa katika ukumbi wa chakula na familia yake yote na kupata chakula cha usiku.
Lanlan alikaa karibu na baba yake na aliuliza ni wapi mama yake alipo mara kwa mara lakini Roma alichoweza kusema ni kwamba mama yake atarudi muda wowote , Kibonge huyo alikuwa na uelewa mkubwa mno wa akili na nikama kuna tatizo kwa mama yake lakini angalu kwa muda huo hamu yake ya kula imerudi.
Roma akiwa ndio anamalizia kula alionekana kukumbuka kitu na palepale aliweza kutoa siraha za kimaajabu kutoka katika hifadhi yake ya pete ambazo zlitoka nazo ulimwengu wa jicho la Anga.
Dhana na siraha hizo ziliwafanya wanawake wote kubung’aa kwa mshangao mkubwa.
Roma alisema akiwa na tabasamu kwamba anaomba msahama kwa kuwafana kuwa na wasiwasi kwa siku kadhaa na hakurudi nyumbani mapema hivyo amewalerea zawadi kufidia.
Kitendo cha Sui kuona Roma anawapatia wasichana hao Dhana za kale kama vile anagawa chakula , alijikuta akielewa uzito wa hali na kidogo tu apaliwe,
Alijua Roma alikuwa akihangaika huko na huko kutafuta hazina kama hizo lakini hakuja kuwazia Roma atakuwa tajiri namna hio.
Kwa Sui ambae ni jini pesa majengo na mambo yaayoonekana hayakuwa utajiri kwake , majini utajiri wao haukupigwa kwa kiasi gani cha pesa wanachomiliki bali kwa Dhana , ziwe Dhana zilizotumiw ana watangulizi wao au Dhana zilizotumiwa na wajumbe wa mkuu wa enzi.
Kwa wingi wa Dhana ambazo Roma anamiliki ni sawa na kusema ni utajiri wote waliokuwa nao miliki zote za majini katika ulimwengu usioonekana.
Ijapokuwa Dhana hizo zina thamani kubwa lakini kitendo cha Roma kuwapatia siraha hizo iliwafanya wapatwe na wasiwasi , ni kama washajua ni nini Roma anapanga lakini waliishia kutoa tabasamu na kupokea.
Baada ya chakula Roma alienda vyumba vya ardhini na kisha alitumia Chaos Cauldron na kuanza kutengeneza vidonge vya daraja la juu sana kwa kutumia malighafi zote alizokuwa nazo na kisha alivigawa vidonge hivyo katika makundi kulingana na idadi ya wanawake wake.
Mara baada ya kumaliza swala hilo Roma alirudi juu na akaingia katika humba cha Lanlan na kumwangalia binti yake ambae amelala baada ya kushiba , alimkodolea maho kwa muda mrefu na kisha alishikwa nywele zake na kumbusu kwenye paji la uso na kisha akaondoka.
Roma alivuta pumzi nyingi na kufanya unyevunyevu uliokuwa katika macho yake kupotea , haraka sana Roma alionyesha tabasamu la kifedhuli na kisha alisogelea chumba cha Rose na kuingia ndani.
Pengine huo unaweza kuwa usiku wa ajabu kwa Roma maisha yake yote.
Wanawake wote ndani ya ngome hio walikuwa na wofa kufa kutokana na ukichaa wa Roma.
Rose , Nasra , Amina , Neema , Dorisi , Magdalena , Mage , Najma na Yezi wote baada ya kuwa na Roma kitandani walitolewa katika vyumba vyao na kwenda kutupiwa kwenye kitanda kikubwa katika chumba cha Master.
Mwishonni hata kwa Yezi na Sophia ambao bado hawakuwa wameonja tunda lililokatazwa walikamatwa na Roma na bila aibu wakatupiwa juu ya kitanda.
Wanawake hao walishajua ni nini Roma anachotaka kufanya lakini ilikuwa ngumu kwao kukabiriana na uhalisia kirahisi.
Kati yao kulikuwa na wale ambao washashughulikiwa kwa wakati mmoja lakini awamu hio wanawake kumi na moja pamoja wamekusanywa sehemu moja walikuwa wakielekea kupatwa na ukichaa.
Wengine walikuwa wamevalia vyupi tu wengine magauni ya kulalia , wangine walivurugiwa muda wao wa kuvuna nishati , kila kitu kilikuwa tafrani.
Waliishia kuangaliana wakiwa na aibu mno na hawakujua nini chakufanya , aidha wakasirike au wacheke , waliona maji yamezidi unga.
Upande wa Roma makusudi alitengeneza ngao katika chumba hicho ili isionekane hata mmoja ambae atakimbia , hakuna ambae alikuwa na uwezo wa kuvunja ngao yake kwa namna yoyote ile.
Mara baada ya wote kukusanywa kitanda kilionekana hakitoshi na Roma alikuwa na uso uliojaa tabasamu la kifedhuli na alijirusha katikati ya fusi hilo la wanawake na kusababisha vilio.
Roma aliishia kusugua ngozi laini za wanawake hao kama vile anaogelea , haikuwa na haja ya kuangalia kwani wote walikuwa ni wake na alikuwa akimbusu huyu na kisha kuhabia kwa huyu na hakujali ni nani.
Ndani ya masaa mnne mbele wanawake wote aibu zilishawatoka tena na akili zishawacharuka , hata Yezi na Sophia ambao ndio mara yao ya kwanza walijikuta wakinogewa.
Roma alikuwa ni kama ameamua kufanya komesha maana ilikuwa ni vita, ilikuwa ni kama vile yupo miaka ile ambayo binadamu hakuwa amestaarabika.
******
Asubuhi hatimae kijua hafifu kiliweza kuingia ndani ya humba hicho kukubwa.
Roma alikaa kitandani kutoka katikati na mara baada ya kuona wanawake wengi namna hio aliishia kutingisha kichwa kwa kujisitikia na kujicheka mwenyewe.
Aliona kabisa kucheza rafu na wanawake hao kwa zaidi ya kumi alikuwa amezidisha.
Chumba kilijaa harufu nzito mno na ukweli ni kwamba hakuna ambae alikuwa amelela , wote walikuwa wakijifanyisha wapo usingizini lakini Roma mwenyewe alilijua hilo na palepale alionekana kutoa kijichupa kwenye hifadhi yake ya pete kilichokuw ana unga unga wa rangi ya kijani na kwa kutumia nishati ya mbingu na ardhi alisambaza poda ile hewani na wote walijikuta wakipoteza fahamu kwa kulala usingizi mzito.
Baada ya hapo Roma alisimama akaingia bafuni na kuoga na kisha akabadili mavazi mengine na kisha aligeuka na kuwaangalia.
“I am sorry babies .. no matter whether I Live or die , I cant escape this is my destiny”
Mara baada ya kuali hio hakuangalia nyuma tena na alipotea palepale akionyesha kabisa amekwisha kufanya maamuzi.
*****
NORTH POLE
Kadri macho yalivyozidi kuona , mti Mama kivuli chake kilikuwa kimetanda na kufanya iwe ni kama bahari ya njano , ilikuwa ni kama vile matawi yake hayakuwa na mwisho.
Juu kabisa ya mti huo Roma aliweza kuonekana akitokea kwa spidi kubwa.
Na ikiwa ni kama vile wamefahamu ujio wake Athena na miungu wengie ni kama vile wanatapikwa na anga na kutokea mbele kwa umbali flani.
Ilikuwa ni wazi kwa Athena unabii wake mkuu ulimtabiria Roma atarudi hivyo kufanya miungu hao kutokuwa na mshangao.
Kulikuwa na hisia zisiosomeka katika nyuso zao pekee , haikuwa kwa Venus au Artemis , au kwa Poseidon na Ares kila mmoja alikuwa katiika muoekano ambao haukuwa ukisomeka anawaza nini.
Ni kama wanatoa taarifa ya kwamba kubadilika kwa dunina ni swala ambalo halizuiliki.
Athena uso wake ulionekana kuwa katika hali ya utulivu kabisa , Edna na Seventeen licha ya kwamba nafsi zao zilikuwa hai lakini zilikuwa chini ya utawala wa Athena.
Ukiburi wake haukutaka kuyumbishwa na jambo ambalo limepangwa kutokea.
Upande wa Roma na yeye alionekana kuwa katika hali ya utulivu kabisa , tokea afikirie safari ya kufika hapo tayari alikuwa ameshajituliza.
Akiwa na tabasamu hafifu aliwaangalia marafiki zake wa kitambo ambao wakati huo walikuwa ni kama watu wageni machoni pake.
Mwishoni kabisa maho yake yalisimama kwa mmoja ambae alimsaidia kumpatia utulivu wa akili , sura ya kirembo ambayo si rahisi kusahaulika , mwanamke ambae alimpata kwa kumdhania ni kahaba.
“Bado tu umekuja?”Aliongea Athena kwa sauti ya chini.
“Nadhani unabii wako umetabiri ujio wangu hapa , je umetabiri nini kitatokea leo hii?”Aliuliza Roma akiwa na tabasamu hafifu.
“Ningekuwa na uwezo huo..nisingetumia nguvu nyingi kuandaa kila kitu , nimefanya kila kitu ndani ya uwezo wangu”Aliongea Athena na kumfanya Roma macho yake kuangaza ndani ya eneo hilo.
“Mtu muhimu naona haonekani hapa , Zeus bado tu hajatoka?”Aliuliza Roma.
“Mh , kwa uwezo wetu tuliokuwa nao haina hata ya Zeus kutoka , huna uwezo wa kushinda hata kidogo”Aliongea Hera kwa dharau.
Roma macho yake yalisinyaa na kwa umakini kabisa aliangalia mazingira kupitia uwezo wake nusu wa uungu na alijikuta akishangaa
“Zeus yupo ndani ya huo Mti?”Roma aliongea kwa mshangao mkubwa.
Roma alishangaa mara baada ya kugundua mtu ambae ana nguvu kubwa mno na asiemfahamu alikuwa amejikusanya juu ya tawi la Mti mama, mtu huyo nguvu zake hazikuwa kidogo kuliko za Athena.
Ilionekana kupitia Zeus na lile tunda ambalo lilichipuka katika mti huo ni kama kifaa ha kukusanya nishati za dunia na kuzibadilisha kisha kunyonywa na mti huo kkwa spidi kubwa kuliko mwanzo.
Ni sawa na kusema uwezo wa Zeus ulikuwa ukirahisisha ufiifuo wa nguvu za mti huo kwa spidi kubwa.
“Naona umeweza kuona?, Uungu wa Zeus ndio ulikuwa wa kwanza kuzaliwa kutoka mtini , ana muunganiko wa kipekee na mti mama , Zeus anasaidia mti huu kupona kwa haraka na ndani ya siku chache zijazo roho zote zilizopotea zitajikusanya juu ya mti na kuzaliwa upya katika miili ya miungu”Aliongea Hera.
“Kwahio tunapaswa kupambana haraka haraka ili huu mti usiendelee kukua kwa muda mrefu?”Aliuliza Roma akishika paji la uso wake kwa mawazo.
“Hades!”
Aphrodite alipiga hatua mbele , macho yake yalikuwa kama ya mwanamke aliepandwa na hasira a ilionekana alikuwa akishindana na wasiwasi wake.
“Ni kweli unataka tufikie huku , hatutakuwa familia sekunde ambayo utashambulia”Aliongea.
“Nilijaribu kuepuka kufanya chaguzi lakini nimegundua siwezi kukaa nje ya hili , samahani sana Christen , ilikuwa furaha sana kuwa na rafiki kama wewe ..lakini kuanzia leo hii mimi naitwa Roma Ramoni Kweka binadamu niliezaliwa na kukua katika dunia , wewe ni Aphrodite kiumbe kutoka sayari ya Mars hivyo usiwe na huruma tena”
“Umeongea vizuri sana , staili yako nimeipenda na kama unataka kupigana basi pigana acha kuzunguka zunguka , sogea sasa”Aliongea Ares huku akitoa cheko kubwa na palepale uungu wake ni kama ulibadilika na kuwa nguvu ya kiroho na anga lilianza kucheza kama bendera inapeperushwa na upepo na ghafla tu mkuki wa mungu huyo wa vita ulionekana.
Hata kama Ares alikuwa wa mwisho likija swala la nguvu lakini alikuwa na uwezo unaolingana na nguvu ya mapigo elfu moja ya radi kutokana na kufufuka kwa mti.
“Kwasababu umeamua haina haja ya kujizuia tena”Aliongea Apollo akijiangaa kushambulia pamoja na wenzake.
Apollo , Artemis na Hephaestus ambao walikuwa na uwezo wa juu kuliko Ares kwa haraka sana walionyesha uwezo wao mkubwa kupita levo ya mapigo mengi ya radi.
Ukiachana na Hera na Poseidon ambao uwezo wao ni kupita wa Apollo na wenzake Zeus na Athena walikuwa tayari washaonyesha uwezo wao wote ambao ukifananisha na mbinu za ardhi na mbingu ni mwanzoni mwa mapigo elfu kumi ya radi.
Nguvu hio kubwa ya kanuni za anga na usaidizi wa Mti Mama ilimzunguka Roma kama wimbi kubwa la bahari.
Siraha mbalimbali zilikuwa mikononi wa miungu , iwe ni Hellius , Selene , Nyundo , Mjeledi na nyoka wa vichwa viwili zote zilikuwa tayari kushambulia.
Kitendo cha Athena kuita siraha zake ikiwemo ngao ya Aeigis na mkuki Pallas anga lote la Ncha ya kaskazini ni kama linataka kudondoka.
Achana na Hera na Poseidon , ilikuwa ni msuguano wa hali ya juu mno wa anga , kwa mtazamo wa Roma mtu au jini aliefikia katika levo ya mapigo elfu kumi ya radi ndio anaweza kupambana nao.
Roma uwezo wake ulikuwa ukiiongezeka kwa kasi lakini bado alikuwa katikati mwa levo ya mapigo elfu moja ya radi , kwa wakati huo miugu ambao walikuwa na uwezo wa chini ni kama alilingana nao ki uwezo kinadharia.
Lakini uso wa Roma haukuonyesha hofu , ukiahana na kuwa na utulivu hakuyumba hata kidogo.
“Njooni wote kwa pamoja , hamniwezi mkiwa mmoja mmoja”
Mara baada ya Roma kuongea mawingu yaliosababisha ngurumo yalijikusanya kutoka pande zote , radi ya rangi ya silver ilianza kucheza cheza bila kutulia kuzunguka mwili wake.
Maneno ya Roma yaliwafanya miungu waone ni kama kichekesho ,ingawa hawakuamini Roma kuwa mdhaifu lakini hawakutarajia anataka kuwashambulia na radi ya mbingu.
Unachopaswa kuelewa licha ya kwamba Athena ndio pekee anaeweza kushindana na radi lakini haikumaanisha miungu wengie watakufa baada ya kushambuliwa nayo , kingine Roma anaweza ashindwe kuwashambulia.
“Hahahaha.. naona ukiburi hakuishia , adhani ukishapigwa kidogo ndio adabu itakushika , huwezi kukubali hitimisho lililotimia juu ya kufeli kwa binadamu”
Ares aliongoza na mkuki wake wa mungu wa vita ulionekana ghafla tu ukirushwa na kusimamisha anga kuzunguka eneo Roma aliposimama , alikuwa amesimaamisha muda ili kumfanya Roma asisogee huku mkuki ule ukifanya kazi na kumsogelea Roma kwa kasi kulenga kifua.
Katika mapigano ya namna hio , mbinu za kujionyesha onyesha hazikufanya kazi na nguvu halisi ndio kila kitu , kadri wepesi wako ulivyo ndio ufanisi wako.
Roma hakukwepa wala kupangua , alifungua kiganya chake na kubadilisha nguvu za mbingu na ardhi na kuwa radi na kisha alipasua anga ambalo lilikuwa limeshikilia na akaishikilia ile siraha moja kwa moja.
Miungu wote walishangaa , hata kama Ares uwezo wake ulilingana na wa Roma ilikuwa ni ngumu mno kuelewa siri ya mbinu ya nishati za mbingu na ardhi ambayo ina uwezo wa kusambaratisha anga lililosimama kutoka katika siraha ya Ares kirahisi namna hio.
Roma mara baada ya kuishikilia ule mkuki wa Ares aliuurusha kumrudishia akiwa ameunganisha na radi juu yake , Ares hakuthubutu kuidaka siraha yake na alikwepa ikapita kwenda angani.
Katika sekunde iliofuata miungu hawakuona haja ya kuangalia , walijua fika Roma hakuwa akiongea tu , iliaminika kwamba kama hawatopambana kwa kushirikiana basi hawatoweza kumzuia Roma kutokuharibu mti wao.
Hawakutaka kuona mti wao unaharbiwa wakati umefikia hatua hio.
Ghafla tu mshale wa jua , mshale wa nguvu ya kupatwa kwa mwezi , ndoto danganyifu na moto vilidondoka kwa pamoja kumshambulia Roma.
Roma uwezo wake wa kupambana ulitokana na majaribio mengi ya kifo na uhai , ijapokuwa amefikia katika levo inayomuhitaji maamuzi ya haraka lakini alikuwa na uwezo wa juu wa kuendana na mashambulizi.
Mwili wake wote ulikuwa umezingirwa na radi iliokuwa ikimzunguka kama kimbunga na kuendelea kuvunja kila mtego wa anga aliowekewa.
Roma aliita hungu cha maafa na kumpa amri nafsi ya mnyama kumeza kila mashambulizi yanayomsogelea kutoka pande zote na kuyageuza kuwa nishati ambayo inamfaa Roma.
Ingawa ilionekana Hera na Poseidon kuwa na uwezo mkubwa kuliko Roma kinadharia lakini kwasababu ya radi ya nguvu mara elfu moja ilikuwa sumu kwao walirudi nyuma.
Athena alieshikilia ngao ya Aegis alikuwa akizuia kila mashambulizi ambayo yalisogelea mti mama mara kwa mara na hakuonekana kushiriki katika vita hio kwa kukurupuka.
Vita ilikuwa ni kubwa mno , Roma alikuwa akikabiliana na mashambulizi yasiokuwa ya kawaida na mbingu mbalimbali lakini licha ya hivyo hakuonekana kuwa dhaifu
Dakika chache walikuja kujua Roma alikuwa akitegemea mashambulizi yao makubwa ili kukilisha chungu chake na kupandisha uwezo wake.




SEHEMU YA 791.
Waliona kama itaendelea hivyo muda mfupi tu Roma atafikia mwishonni mwa levo ya radi ya mapigo mengi.
Iisitoshe elementi za anga ambazo zilikuwa zikigeuzwa na miungu kupitia kanuni zao za anga zilikuwa kubwa mno kulinganisha na uchawi wa majini.
Kama ni chakula basi ni sawa na kusema mashambulizi yao ni chakula cha daraja la juu chenye kila aina ya virutubisho mbele ya Cauldron.
Poseiodon mara baada ya kuona hali hio ilikuwa ngumu kwake kumdhibiti Roma na aliita chusa(Trident), ilikuw ani kama vile kivuli cha rangi ya bluu kinadondoka kutoka juu angani kama kimondo na kudondoke bahari ya barafu na kuipasua vipande vipande na hatimae ile chusa ilionekana kutoboa.
“Boma la kiposeidon!!!!”
Aliongea kwa nguvu na palepale barafu zote zilizokuwa zimefunikwa maji zilitawanyika na maji ya baridi kali yalionekana hini yake.
Mlipuko huo haukuwa na athari zozote kwa Mti mama , mizizi yake haikuwa imeshikiliwa na bahari bali ilikuwa imeenda sana chini kupita miamba.
Punde tu nyoka wa baharini walijitengeneza kutoka katia maji hayo na kufnyatuka kuelekea angani huku wakiachama kumlenga Roma na kileChungu.
Kila pale chungu kilipotaka kumeza nyoka hao wa kibaharini walionekana kukwepa kana kwamba walikuwa hai na kusababisha roho ya uovu ya chaos kugeuka geuka bila mafanikio.
Roma palepale alipata ufahamu , ingawa nyoka hao walikuwa wameitwa kupitia kanuni za anga na vilevile wametokana na elementi za dunia kama atatumia radi kushambulia basi zitamiliki radi yake na kuwa na nguvu zaidi.
Kwa msaada wa majoka hayo ya baharini ilimfanya Roma kuhama hama na kumtenganisha na nafsi ya Machafuko na ghafla tu ni kama uwezo wa miungu umepanda mara mbili.
Kila mara Poseidon alipopunga hewani chusa yake kulitokea wimbi kubwa la sauti , sauti hizo ni kama vile simulizi juu ya mnyama mkubwa wa baharini ambae alishwahi kuwepo na kumfanya Roma kuhisi ukichaa.
Roma hakujisaidia na aliishia kukunja sura kwani hisia zake ni kama zinacheza cheza na alishidwa kuepuka mashambulizi kadhaa.
Miungu hawakujjizuia tena kushambulia kwa kumheshimu mshindani wao pamoja na kutotaka tatizo katika ufufuo wa ndugu zao walimshambulia kisawa sawa.
Mishale ya moto wa jua , mishale ya mwanga mweupe kama mwezi na Nyundo ya moto vyote vilimpiga Roma na kumwachia makovu.
Kwa bahati nzuri Roma aliweza kupona kwa haraka kupitia Andiko la urejesho wa azimio na hakupatwa na majeraha lakini aliona kama hali ikiendelea hivyo nni swala la muda tu atafikia hatua hawezi kupona.
Hera aliunganisha kanuni zake za anga na nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi huku akiwa ameshikilia upinde wa machweo na kuendelea kumshambulia roma na mishale kwa nguvu kubwa mno.
Hio mishale sio tu kuwa na nguvu ya ajabu ya kanuni a anga lakini pia ilibeba athari za nishati ya mbingu na ardhi na kuwa na nguvu ya mishale miwili kwa wakat mmoja na hilo lilimfanya Roma kuwaza.
Katika eneo ambalo Roma alikuwa amesimama anga lake lilikuwa likilipuka huku miale ya mwanga ikitokea.
Ijapokuwa Roma alikuwa na namna ya kulinda mwili wake lakini nguvu ya miungu haikuwa ya kudharauliwa kabisa na alikuwa ametumia nguvu nyingi katika kujilinda na kukwepa mashambulizi , hakukuwa na amna ya yeye kushambulia.
“Duuh , huyu jamaa ni mgumu mno , inakuwaje bado yupo hai tu?”Mkonno wa Hera ulishaachia mishale mfufulizo kama dhoruba lakini bado anaona Roma hakuwa amedhulika kabisa na hakujizuia kukasirika.
Usiwe na wasiwasi , kadri tukavyoendelea hivi ni swala la muda tu atashindwa kujilinda , kwa uwepo wa huu mti nguvu zetu hazina kikomo”Aliongea Hephaestus akiwa ameshikilia nyundo yake ambayo ilikuwa imepata moto na kuwa nyekundu.
Lakini unadhani Roma alikuwa na mpango wa kuwaacha wafikirie upuuzi wa namna hio , mwanzoni alikuwa akiwaza kumaliza vita hivo kupitia radi lakini aliona hawezi hivo hakutaka kujisumbua kuficha vitu tena.
Palepale Roma aliamua kuchoropoa shoka lake la rangi ya shaba ambalo lilikuwa na upanda wa futi kumi kutoka katika hifadhi ya pete.
Ilikuwwa ni Dhana ya Wajumbe wa mkuu wa Enzi iliofahamika kwa jina la Pangea lakini baadae ikaja kutumiwa na jini pepo mmoja aliefahamika kwa jina la Pangu , jini huyo mara baada ya kupata Shoka hilo alijigamba kwamba yeye ndio alitenganisha mbingu na ardhi kupitia shoka hilo.
Roma alifoka na kwa nguvu ya sauti yake alipigisha hewani lile shoka pande zote.
Yale majoka ya bahari ambayo yalitaka kumshambulia Roma yalisambatasiwa mara moja na hayakurudi upya kama mwanzo na kugeuka maji ambayo yalidondoka baharini.
“Nini!!!... inaawezekana vipi , ukuta wangu haufanyi kazi”Poseidon alimaka.
Hephaestus na Hera ambao walikuwa wamesoma elimu ya majini na hadithi zao walijikuja nyuso zao zikisawijika , walibung’aa wasiamini kama ni kweli wanashuhudia shoka hilo.
“Inawezekanaje , lile nni shoka la Pangea , si ilisemekana lilipotea na Pangu, kwanini lipo katika mikono ya huyu mtoto?”Hera alipiga kele
Miungu wengine pia walionyesha hali za kushangaa , licha ya kwamba hawakuwahi kusikia uwepo wa hilo shoka lakini walijua siraha ya Roma ilikuwa ikitisha mno.
Wote walijikuta wakimwangalia Athena na ilionekana ni kama alikuwa ametarajia swala hilo kutokana na utulivu wake na alionekana kabisa alifahamu hawezi kumdhibiti Roma kwa muda ndio maana alisubiri akiwa pembeni.
“Bitch , kwanini hujaongea chochote kama ulijua fika ana hii Dhana?”Aliongea Hera kwa hasira
“Ungefanya nini hata kama ningekuambia?”Aliulia Edna kikauzu na kumfanya Hera kuishiwa na pumzi kwa kukosa neno.
Upande mwingine Roma alikuwa tayari katika matumizi ya Shoka na alilazimisha miungu kurudi nyuma kwa kulifyatua mara chache tu.
Haikujalisha ni aina gani ya sheria za anga zinatumika , ili mraadi tu iwe ni sheria za anga basi Shoka hilo lingefanya kazi yake.
Miungu walijua mbele ya shoka hilo kubwa katika mikono a Roma mashambulizi yao hayana nguvu yoyote kama vile wanatupa mayai kwenye jiwe.
“Pumbavu bora hata ingekuwa Dhana nyigine kwanini kati ya Dhana zote liwe hili Shoka lenye kuweza kupangua kanuni za anga ?”Hera alijikuta akisugua meno na alionekana kukosa jinsi zaidi ya kupunguza mashambulizi yake.
Mbinu zao zote za mashambulizi lazima zitokee kwenye neno sheria ya nafasi katika anga lakini kwa bahati mbaya shoka hilo lilitengenezwa na Wajumbe wa mkuu wa enzi kwa ajili ya kuharibu sheria hizo.
Kwa maneno mengine ni kama miungu wanatumia nafasi ya anga kama matofali na kujenga ukuta ambapo bumu liwe kama shoka la kubomoa ukuta wao ndio kilichokuwa kikitokea.
Haijalishi utajenga ukutwa wako kwa uimara wa naa gani lakini ukikutana na bomu lazima uporomoke.
Viumbe hao hatimae walijua kwanini Athena alimuona Roma kama mshindani wake licha ya kwamba alionekana kuwa na uwezo wa hini kidogo kuliko yeye.
Kwa matumizi ya shoka hilo kwenye mikoo ya Roma hila zote za Athena zinaweza sizifanye kazi pia.
“Hamuwezi kushindana na Shoka hilo la kipangea , lindeni Mti Mama mimi nitapigana nae”Aliongea Athena.
“Acha majigambo , hivi unadhani kupambana mwenyewe ndio utakuwa na uwezo tofauti na jumla yetu?”Aliongea Hera kwa hasira
Athena hakuongea neno na palepale alirusha ngao ya Aegis iliokuwa kwenye mikono yake.
“Bang
Ilitokea sauti kali ya kuumiza kama mshindo baada ya Shoka kugongana na ngao ya Athena kiasi cha kuifanya itoa mlio wa kulalamika.
Ambae amelidwa kutoka kwenye shambulizi hio alikuwa ni Hera ambae alikuwa bize kujibizana na Athena
Hera alifubaa mara baada ya kujua kama sio Athena kumuokoa angekuwa vipande vya nyama kwa kushambuliwa na hilo shoka , alijikuta akikosa jinsi na kutuliza hasira zake.
Mara baada ya miungu hao kuona tukio hilo walijua ni Athena pekee ambae anaweza kuhimili mapigo ya Shoka na Roma ambae yupo levo ya mapigo mengi ya Radi.
Kundi hilo kwa haraka sana walirudi nyuma na kumuachia Athena nafasi ya kupambana na Roma.
Roma alikuwa ashajua lazima kutakuwa na hio mechi na hakuonyesha utofauti wowote.
Mara baada ya kuona Roma anamsogelea kwa kasi na ngao yake pamoja na mkuki kwa kutokuwa na furaha kabisa usoni alifyatua shoka lake hewani
Lakini kabla hata shambulizi lile halijamfikia Athena alionekana kuhama kimaajabu tena kabla hata Roma hajafanikiwa kumalizia kufyatua shoka
Uwezo wake wa kitabiri hatimae ulionyesha faida zake muda huo , hata kama Aqthena hakuwa na uwezo wa kuona kila kitu kitkaacho tokea haikumwaannisha kwamba hawezi kutabiri nia ya mashambulizi ya Roma.
Mkuki wa pallas uliokuwa kwenye mikono yake uling’aa na mwanga wa ajabu wa bluu ulionekana na ulikwepa wimbi na shambulizi la shoka na kama shoti ulimsogelea Roma kwa kasi
Athena alihofanya ni kuunganisha maelfu ya matabaka ya anga kutoka kwenye parallel space na kisha akaunganisha na nguvu ya Pallas a kutengeneza nguvu kama vile ni Tsunami na kumgonga Roma kwa nguvu.
BOOM!!
Roma alipigwa na nguvu kubwa ya wimbi mgongoni lenye uzito wa tani zaidi ya laki moja na kufyatuuliwa kama vile ni mpira na ilikuwa ni rasha rasha ya mtu kutema damu angani ilioweza kuonekana.
Hata miungu hawakuamini , Roma pia alijikuta akishikwa na mshituko kwani ilikuwa ni raundi moja tu na ameshambuliwa nama hio.
Ukweli ni kwamba kama isingekuwa kwa mwili wa Roma ulivyo kwa mtu mwingine angekuwa amebakia vipande vipande kama sio uji uji
Roma alifurumushwa kilomita kadhaa huku akijjitahidi kujituliza na kuanza kuhema kw anguvu kama mbwa , aliishia kufuta damu zilizokuwa zikimtoka mdomoni na kuishia kutoa tabasamu la ukauzu akimwangalia Athena.
“Inaonekana umedhamiria kabisa kuniua”Aliongea Roma akimwangalia Athena ambae yupo katika sura ya kirembo ya mke wake.
Tabasamu ambalo Roma alikuwa nalo ni chungu huku uso wake ni kama ule wa mtu anaonyesha malalamishi.
Upande wa Athena alikuwa katika utulivu , gauni lake jeusi lilikuwa likipeperushwa na upepo na nywele zake ndefu zilifika mpaka kwenye mashavu yake.
“Na wewe si unataka kuniua ..nilidhani kwa ajili ya Edna na Seventeen hautoniua lakini sijategemea utakuwa mkatili hivi”
Roma majeraha yake yaliweza kupona kwa haraka na sasa aliweza kunyoosha mwili wake.
“Ukweli ni kwamba sina haja ya kukuua , angalau mashambulizi yako yananifanya none nafasi ninayo”
Athena aliishia kukunja ndita kiasi kama vile alikuwa akijaribu kuelewa Roma anamaaisha nini lakini haraka sana alishatarajia Roma anachotaka kwenda kufanya.
“Wewe mwanaume kichaa..”:
Athena muonekano wake ulibadilika palepale na alionekana kuonea kitu ambacho kiliwafanya miungu wengine kutokuelewa.
Ndani ya dakika hio hio Roma alionekana kucheka kama kichaa na kumuacha Athena peke yake.
Alichukua shoka lake la kipangea na kukimbia moja kwa moja mpaka katikati ya mti , Roma aliamua kupotezea swala la kujilinda mara baada ya kugundua mashambulizi ya Athena hayawezi kumuua na badala yake aliona aanze kucharanga mti na shoka lake ili kuudondosha.
Shoka lile lilikuwa na uwezo wa kuzivunja kanuni za anga ikiaanisha kwamba ingekuwa ngumu sana kwa miungu kulinda Mti Mama kudondoshwa na yeye.
Lakini katika mchakato huo Roma mwenyewe angeshambuliwa na miungu , alipanga kuvumilia hata kama maumivu na majeraha yatakuwa siriasi namna gani , ili mradi hawezi kufa na mpango wake kufanikiwa basi hakuna tatizo.
Mi9ungu kwa haraka sana waliamua kutumia kaununi za anga na kutengenza matabaka zaidi ya elfu moja kuwa ngao za anga wakijaribu kuzuia shoka kugusana na mti.
Lakini shoka lile lilikuwa ni kama kisu cha moto kinachokata plastiki wakati wa kudili na kanuni a anga.
Ngao hio ya anga hakuweza kuzuia shoka kupita kwani ilipasuliwa mara moja.
“Unadhani nitakuacha ufanikiwe?”
Athena alikuwa katika kiwango cha juu ha hasira , huku sauti yake ikiwa ya kikauzu kama vile ni barafu ya kuumiza mifupa na kufumba na kufumbua alikuwa tayari ashafika mbele ya Roma huku ngao yake ya Aegis ikimtoka mikononi mwake na dude kubwa rangi ya silver lilianza kuonekana mbele ya ngao ile.
Fuvu la Medusa , mwanamke aliesimuliwa kuwa na vichwa vya nyoka alionekana katikati ya ngao ile kana kwamba amerudi uhai , wale nyoka kichwani walionekana kuheza cheza huku ikiwa ni kama wanangea.
Inasemekana Medusa macho yake meusi yalikuwa yakitoa mng’ao wa rangi ya damu ya mzee huku yakiwa kama mashimo yaliojaa damu.
Roma alihisi kutetemeka kusiko kwa kawaida huku akiwaza tabia ya nguvu ya uchawi wa Medusa kugeuza mtu kuwa jiwe , alikuwa akielewa kwmaba hapaswi kuangalia macho yale ya damu hivyo kwa haraka aligeuza kichwa chake mbali.
Medusa alifahamika kama jitu la kutisha ambalo lilikuwa na nguvu huko katika sayari ya Mars , halikuwa kama ambavyo alivumishwa kwenye hadithi za wagiriki lakini ilikuwa ni kweli kwaba macho yake yalikuwa na uwezo wa kimaajabu wa kumgeuza mtu jiwe.
Medusa alikuja kuuliwa na shujaa wa sayari ya mars afahamikae kwa jina la Perseus na baada ya hapo akakata kichwa chake na kwenda kumtunuku Athena kwa ajili ya kuweka kwenye ngao ake.
Kitendo cha kuufanya uchaawi wa Medusa kuwa hai ilimpatia Athena nafasi ya kufanya shambulizi.
Athena alionekana kama vile ni kivuli cheusi huku akirusha ile siraha ake ya Pallas na kutengeneza mwanga wa bluu wa kimaajabu na kuufyatua kuelekea upande wa Roma.
Kitendo cha Roma kugeuza kichwa chake alihisi chembechembe za anga zisizokuwa zikihesabika zikimzunguka kuanzia kwenye mikono ake kama vile ameutumbukiza kwenye majij ya bahari.
“Arghhh..”
Roma alipigwa na wimbi la uhakika kwa mara nyingine na kufyatuliwa na kutokana na maumivu makali alijikuta akitoa kilio , ilikuwa ni kama vile mkono wake wa kulia umepondwa na aliishia kubiringita huku vipande vya nyama vilivyomtoka vikigeuka uji.
Athena alitabiria namna ambavyo Roma angekwepa shambulizi lake na katika eneo lilelile ambalo akili yake ingemwambia angesimama alirusha pigo na alimpiga kwa nguvu zake zote .
Roma alikuwa kwenye maumivu makali lakini hakuwa na nia ya kuacha , haraka sana aliponyesha mwili wake na kuushambulia mti mama bila ya kupumzika.
Chaos pia alijaribu kumpunguza kasi Athena na miungu lakini licha ya miungu kuwa rahisi kuzuiwa lakini kwa Athena ilikuwa tofauti .
Haikujalisha ni radi au Shoka Athena alikuwa akitabiri mashambulizi hayo na kukwepa na muda huo huo kurudisha shambulizi.
Mapigano hayo makali yalidumu kwa dakika chache tu huku wakipigana kwa raundi zaidi ya mia moja lakini mwishoni Roma ndie aliojnekana kuumia zaidi.
Pengine kama sio uwezo wa Roma kupona kwa haraka nafsi yake ingekuwa ishaharibiwa muda mrefu.
Lakini hata kama Roma alikuwa na uwezo wa kutumia nishati ya mmbingu na ardhi bila kikomo kulikuwa na mwisho wa uvumilivu, alikuwa akipata majeraha kila sekunde na kutopona kwa haraka na damu ilikuwa ikimtoka sana.
Roma alijua kabisa hana uwezo wa kuvunja kizuizi cha miungu kwa spidi hio na angeshindwa mapema tu kabla ya kutimiza lengo , hivyo aliona atumie mbinu nyingine.
Roma alipata wazo palepale na alibadilisha uelekeo akikimbia kuelekea upande wa bahari ya Arctic chini
Barafu ambayo ilisambaratishwa na Poseidon muda huo ilikuwa imejikusanya na kutengeneza mlima.
Roma alitumbukia katika kina cha maji kwa mamia ya mita na akapotea kabisa.
“Anafanya nini?”Hermes alijikuta akikunja sura kwa muda.
Uso wa Athena ulikuwa mkavu na alitumia uwezo wake wa kanuni za anga kutengeneza shimo katika maji hayo ili kuona hini yake sehemu ambayo Roma alitumbukia.
Roma ni kama amekitoa kafara chungu cha maafa kwani kilitoa sauti kama tanuru la moto kikijaribu kushambulia mti mama lakini ilikuwa ngumu kwa Chaos kufanikiwa.
Mbinu ya Roma ilikuwa nyepesi sana , kwasababu hakuwa na uwezo wa kukata mti basi aliona akachimbe na kuharibu mizizi yake na kama mizizi ikifa utanyauka wenyewe bila hata ya kushambuliwa.
Faida kubwa ya kushambulia mizizi katika kina kirefu cha maji ni kwamba kama miungu watataka kumzuia Roma basi wataishia kumshammbuulia kwa kutuma mashambulizi na ndio hayo hayo mashambulizi ambayo yyangeharibu mizizi.
“Kwa msaada wa nafsi ya mnyama wa mahafuko Cauldron njoo na uozeshe mizizi ya mti”
Athena ni kama alishajua nini Roma anataka kufanya lakini hakuona njia bado ya kudili na hali hio kwa muda.
Hio ndio moja ya udhaifu wa unabii wake , hata kama utaweza kumwambia nini kitatokea mbeleni lakini anaweza asibadili kitu.
Alichoonyshwa kinatokea sio kitu ha baadae ambacho angepata muda wa kupanga namna ya kutatua tatizo lakini alipatiwa sekunde tu na unabii wake
Mara baada ya kujua hawezi kuchelewa hata sekunde , Athena alichoweza kufanya ni kukiuka sheria na kutengeneza shimo la anga kutoka juu kwenda chini na kisha kupasua mfumo wa miamba ili kumfukuza Chaos.
Roma alikuwa ashatarajia hilo litatokea na alitumia shoka kuharibu mzito wa kanuni za anga wa Athena wakati huo juu angani radi zilianz akupoiga kwa kasi mno.
Boom , Boom
Juu ya bahari ngurumo zilizoambatana na radi zilipiga mfululizo na matokeo yake ni kama maji yameshika umeme na nguvu ya nishati za mbingu na ardhi.
Kitendo hicho kiliwafanay miungu kutogusa maji ya bahari kutokana na kukosa ngao kama Aegis hivyo wataathirika.
Lilikuwa tukio la kutisha kwelikweli namna wingu lilivyofunika bahari na kushambulia maji ya bahari kama vile Mungu ameunganisha umeme kati ya mbingu na ardhi.
Athena alitengenza nafasi na kwenda nusu kina ambacho amefikia Roma na kugundua alikuwa tayari ashaharibu mzingo wake wa kanuni za anga na maji yaliokuwa katika eneo hilo yamejaa umeme wa radi. Na hatiimae ndio alipata kujua kila kitu.
Roma kutumia Cauldron kuozesha mizizi ilikuwa hatua ya kwanza na ya pili ni kuyageuza maji ya bahari kuwa radi ambayo itashambulia mti.
Ijapokuwa Athena hilo ni jambo ambalo aliona linakwenda kutokea ndani ya dakika chache kulingana na unabii wake lakini alikosa namna ya kukabiliana nalo kwani hakuwa na uwezo wa kumuua Roma mara mmoja.
Uso wa Athena ulizidi kuwa mbaya lakini hakuwa na nguvu tena , ki ufupi kazidiwa ujanja na Roma , mara baada ya kuita ngao yake ya Aegis ili kujilinda aliishia kurudi juu ya bahari akiepuka kuyeyushwa na radi iliosambaa katika maji.
“Khaa… mti unaathirika na radi ?”Poseidon alipiga makelele
Athena mara baada ya kugeuza macho yake aliweza kuona moja ya matawi yalikuwa yameshambuliwa na radi lakini hata hivyo sehemu ndogo ya matawi haina athari sana kwa ukubwa wa mti huo.
Lakini Roma alikuwa akiendelelea kuunganisha mti huo na radi kutokea chini , yaani alikuwa akizalisha radi chini ya maji na kuziingiza katika mti na kusafiri kwenda juu na kusababisha mti ulioshikilia matawi kuanza kuharibika na ile ishati iliokuwa katika mngao wa dhahabu kupungua.
“Ni ngumu kuzuia hili , anao uwezo wa kutawala radi na mawingu anavyotaka na ikamtii , hivyo hii radi haiwezi kuzuilika kabisa”Aliongea Hephaestus akiwa na huzuni.
“Damn ….tatizo ni kwamba huyu mtoto ni ngumu sana kumuua lakini tunaweza kuelekeza uwezo wotu wote kujilinda”Aliongea Hera huku akisaga meno.
“Nilijua haitokuwa rahisi kudili nae , haijaisha bado , msiwe na wasiwasi sana”Aliongea Athena ambae alikuwa na maho kama nyota.
Miungu walishangaa kwanza kabla ya kushangaa zaidi.
Dakika hio hio mwili wa mti huo ghafla tu ulianza kutoa nishati kubwa mno na kutengeneza mzunguko kama wa kimbunga wa rangi ya Dhahabu kuanzia katikati ya mti.
Ilikuwa ni kama vile kiwanda cha kutengenezea mabomu ya nyuklia kinalipuka na mabomu yake katika eneo moja tu na wimbi la msukumo lilianza kusukuma maji yote mbali kwenda chini.
Kama utaangalia kwa juu ungeweza kuona maji yote ambayo yalikuwa yamezzingira mti huo yamepotea ndani ya sekunde kwa maili kadhaa.
Walioweza kusukumbwa na kimbunga hizo cha msukumo ni Roma na chungu chake
Ilikuwa ni kama vile bahari imegeuka lijimkono likuubwa na kumtupia Roma mbali na hakuweza hata kujizuia kwani nguvu hio haikuwa ya kawaida hata kidogo.
Roma akiwa angani akipeperushwa na kimbunga alijikuta ni kama kuna sauti imeingia katika akili akili yake na kusikia sauti nzito ikiongea na fahamu zake kwa lugha ya kimaajabu na pengine ameweza kutafirisi kupitia uungu wa Hades.
“Those who disobey the oracle , be punished”
 
Back
Top Bottom