Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 767.
Haikuwa na ubishi kabisa Roma aliweza kuona namna ambavyo Lekcha uwezo wake ulivyokuwa umeongezeka , kwa mahesabu ya haraka haraka ilikuwa tayari ni mwaka na Roma alishangazwa kwa namna ambavyo Lekcha ameimarika na ukweli ni kwamba hakuwa binadamu , alionekana kama kiumbe ambacho kipo katika umbo la nishati.
Aoiline upande wake alikuwa amechanguka na alionekana alikuwa akihangaika sana kujilinda na ngao ya kijini , yaani ilionekana uwezo wa kushambulia hakuwa nao zaidi ya kujilinda.
Nywele zake zilizokuwa za kirembo zilikuwa zimejikunja kunja kunja huku gauni lake likiwa limechanika chanika, mikia yake yote tisa ilikuwa ikionekana na kuwa kama kinga kwake.
Kama sio kwa uzuri wake wa uso ingekuwa ngumu kudhania mwanamke huyo alikuwa na hadhi kubwa kati ya majini wa jamii ya Mbweha.
Wawili hao pia walionekana kuhisia uwepo wa Roma na mara baada ya kumuona akishuka kutoka juu haikuwa kwa Aoiline tu lakini hata kwa Lekcha mwenyewe alikuwa katika hali ya mshangao.
“Ni wewe!, Wewe mjinga hukuweza kufanikiwa kutoka wakati ule?”Aliongea Aoiline akipandisha sauti na ni wakati uleule alifanya uchunguzi wa haraka haraka wa kumkagua Roma na uso wake ulikunja ndita.
“Embu subiri kwanza… naona uwezo wako umeimarika sana!?”Aliongea akiwa katika hali ya hamaki.
Roma nae alikuwa kwenye mshangao baada ya kugundua watu hao walikuwa katika floor hio kwa mwaka mzima wakiendelea kupigana.
“Hahaha…Hades wewe mpuuzi muoga muoga umekuja wakati muafaka, usije ukakimbia awamu hii wakati ukijiona unataka kufanya hivyo”
Lekcha alionekana kufurahi mno kama vile ameokota hela na ari yake ya kutaka kupigana ilipanda maradufu , nguvu ya Ant- matter ambayo ilikuwa ni kama mlima iliweza kuongezeka zaidi na zaidi.
Roma alijua wakati huo sio wa kujielezea na aliruka na kwenda kutua upande aliopo Aoiline huku akijilinda na Chaos Cauldron.
“Nitajielezea baadae , kwasasa rekebisha hali yako ya kimwili na niachie nidili na hili”Aliongea Roma.
Aoiline hakuwa msichana mdogo ambaye uwezo wake wa kufikiria ni mdogo , ijapokuwa uwezo wake ulikuwa ukizuiwa na kanuni za kifizikia za ulimwengu huo lakini uono wake haukuwa mdogo.
Hivyo alipanga kumpatia Roma nafasi kudili na maswala yao , isitoshe Lekcha alifika katika ulimwengu huo kwasababu ya ugomvi wake na Roma na yeye ni kama alinunua vita hio.
“Kijana, mimi Master wako nimeweza kushindana na huyu mshenzi kwa zaidi ya mwaka sasa hivyo usiniangushe”Aliongea.
Aoline alimwangalia Roma kwanzia chini na hali isiokuwa ikielezeka ilionekana katika uso wake na aliishia kutoa tabasamu hafifu sana na kisha alisogea pembeni kuangalia pambano.
“Sijawahi kuwaza juu ya uwezo wako lakini ushaanza kuniwazia vibaya , ngoja nikuonyeshe kwamba nilichokuwa nikifanya huko nje hakikuwa kitu cha kupuuzwa”Aliwaza Roma.
Kutoka kuwa chokoraa anaelala chini ya daraja mpaka kuwa mtu mwenye nguvu wa kuweza kushindana na Aoiline kwa zaidi ya mwaka mzima si jambo dogo na Roma alijikuta akimkubali Lekcha bila ya wasiwasi , maana uwezo wake sio wa kawaida.
Wakati Roma akiingia ulimwengu wa majini pepo na kukutana na Aoiline kwa mara ya kwanza alishindwa kabisa kushindana nae , lakini Lekcha aliishi katika ulimwengu huo kwa muda mfupi sana lakini alikuwa ameweza kupandisha uwezo wake kwa viwango vya juu hivyo kwake aliona kabisa hakuwa mtu wa kawaida lakini hata hivyo Roma wakati huo uwezo wake sio wa kawaida na alitaka kumuonyesha Lekcha maana ya nguvu halisi.
Unaweza kusema kwamba Lekcha alifika katika uwezo huo kwasababu ya Roma kumsukumia Kizwe kwake.
Yaani kama Roma asingempa adhabu Kizwe ya kubakwa na machokoraa basi ni hakika Lekcha asingeweza kukutana na Kizwe na hatimae kumuua Yan Buwen na kurithi uwezo wake.
Roma hakutarajia athari ya kile alichokifanya ingemfikisha katika hatua hio, wanasema kila unachokifanya leo kina athari mbeleni na ndio ambacho Roma aliweza kushuhudia na kwa namna yoyote ile kwasababu yalikuwa maamuzi yake wakati ule hakuwa na budi ya kuyakabili matokeo.
“Kwa vyovyote vile kwasababu Mungu amenileta na kukutana nae hapa ,, basi ni wakati wa kuhitimisha huu uhusiano mbaya kwa mikono yangu miwili”Aliwaza tena Roma.
“Inaonekana umekula vitu vingi ndani ya huu mnara”Aliongea Roma akiwa na tbaasamu.
“Kuna haja ya kuuliza , au ndio ushaanza kuniogopa , hivi unadhani mwaka wote niliokuwa ndani ya huu mnara nilikuwa napoteza muda , ijapokuwa nimeshindwa kumuua huyo mbweha lakini ilikuwa ni swala la muda tu .. majani ya kiroho na matunda yaliopo ndani ya huu mnara yamenifanya kuwa wa tofauti kabisa”Aliongea Lekcha akiwa katika hali ya kujiamini kabisa.
“Basi tuchukulie hii ni bahati maana hata mimi nimekuwa wa tofauti kuliko mwanzo , ngoja tuone nani alikuwa akipoteza muda”
Mara baada ya Roma kuongea tu mazingira yaliokuwa yakimzunguka ni kama vile yanaganda na kusababisha msuguano mkali wa elementi za hewa na kufumba na kufumbua radi ya Zambarau ilianza kujitengeneza kama vile ni transfoma la umeme linapiga shoti ambazo ziliruka kwa kunyongorota kama umbo la nyoka.
“Radi ya zambarau!!!”
Aoline ambaye alikuwa akiangalia kwa mbali alimaka huku akiingia katika tafakari nzito, ni kitu ambacho hakutegemea kukiona kwa Roma.
Roma licha ya kuonyesha karata yake hio kwa Lekcha hakubadilika hata kidogo na aliishia kutoa tabasamu la dharau katika uso wake na mkono wake ulibadilika na kuwa kama mkono wa chuma uliotengenezwa na nishati ya Ant- Matter, Shoti za nguvu ile zilikuwa zikitisha mno na ziiongezeka kila sekunde na kutaka kummeza Roma.
Ilikuwa ni sawa kusema mwili wa Lekcha kwa wakati huo ulikuwa ni nguvu ya Ant Matter na ilionekana ni kama vile alikuwa ashapata ufuno wa namna ya kuendeleza kuziongeza maradufu.
Kama sio kwa mnara huo kutokuwa wa kawaida , nguvu ambayo alikuwa akidhalisha Lekcha mnara huo ungekuwa umedondoka muda mrefu sana.
Roma ili kupambana na nguvu ile ya nishati isio maada palepale alibadilisha radi ile na kuwa kama mkuki na kisha alimrushia Lekcha ule mkuki kumchoma.
Nguvu ya radi haikuwa ya kawaida kabisa pia , ijapokuwa nishati ya Lekcha kila ilipokutana na radi ambayo huundwa na maada kulitokea ‘annihilation’ yenye nguvu kubwa kiasi kwamba uwiano ulikosekana.
BOOM, BOOM, BOOM!
Mlipuko mkubwa wa nishati zote mbili kukataana ulikuwa mkubwa mno na ulilipuka katika mfululizo na shambulizi la Lekcha likawa limesabaratishwa namna hio
Lekcha macho yake yalionyesha hali ya kukasirika , hakuamini shambulizi lake hilo ambalo alikuwa ameliongezea nguvu kwa muda mrefu lingeweza kusambaratishwa na nguvu ya radi.
Roma alikuwa mjanja mara baada ya kusambaratisha pigo la Lekcha alikuwa ameongezea nguvu kubwa mno shambulizi lake na mara baada ya mlipuko kutokea mshale mwingine uliweza kutoka na kumpata Lekcha katika kifua na kutengeneza shimo lakini hakukuwa na damu yoyote ilioweza kutokea zaidi ya nishati ambayo iliziba shimo lile haraka sana .
“Hey ..hahaha…Good .. what a powerfull move”Lekcha aliongea kwa kingereza huku akitingisha kichwa chake na kushika eneo la kifua chake ambacho kilitobolewa.
“Inasikisha kwamba huwezi kuniua kizembe namna hii na viradi vyako”
Roma aliishia kukunja sura , aliamini pengine shambulizi la radi lingeweza kumyeyusha lakini ilionekana nguvu ya Ant Matter ilikuwa kubwa mno na kufanya mwili wa Lekcha kuwa na kinga ilio imara.
Lekcha mara baada ya kupona palepale macho yake yalibadilika na aligeuka na kuwa kama lichuma lililotengenzwa kwa uji uji na ilikuwa ni kama mwili wake unaungua kwa shoti na kuzisambaza katika eneo lote.
Roma hakutaka nishati zile kumpata na alijikinga kwa kutumia Chaos Cauldron , chungu kile ni kama kilikuwa kikisubiria fursa hio kwani ile roho ya mnyama iliokuwa ndani yake iliweza kujitokeza kuonyesha ukali wake na kani kubwa ya mvutano ilidhalishwa na kutaka kummeza Lekcha.
“Aaah..ni yale yale , unadhani nitakuogopa kwa kutumia hilo lijichungu lako?”
Lekcha alitoa kicheko kama mwehu na bila ya kukwepa chungu kile alikisogelea na kukivaa na mara baada ya kufikiana na mwili wa Lekcha alilipuka kama bomu la nyuklia.
“Bang!!
“Hoooo…!!!
Ile nafsi ya Chaos ilinguruma kwa sauti kubwa mara baada ya kufunikwa na mlipuko wa nishati ile isiokuwa ya kawaida na kisha kiliachiwa na Lekcha alirudi katika umbo lake la kawaida.
Roma alijikuta akishangazwa na kitu kile , Dhana hio ya Cauldron ilikuwa imeunganishwa na nguvu zake na kama kikipigwa na kuathirika na yeye alikuwa akiumia.
Kilichomshangaa Roma ni mara baada ya roho ile ya mnyama kujificha mara baada ya kuachiliwa na nguvu ya nishati ya ant- matter na hii ilimaanisha kwamba Lekcha alikuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba Dhana hio imekuwa sio tishio kwake tena.
“Unashangaa nini wewe ndio unaefuatia baada ya kuharibi chungu chako”Aliongea Lekcha.
Ilikuwa ni muda uleule Lekcha alitengeneza ngome ya nishati ya Ant- Matter na kuifanya iwe ni kama gunia na kutaka kumfunika nalo Roma.
Roma alishangazwa, nishati ile nyingi haikumtoka Lekcha bali ilikuwa ni kama vile ameitengeneza katika mazingira , yaani likuwa ni kama vile yeye alivyokuwa na uwezo wa kukusanya nishati za mbingu na ardhi ndio alichokifanya Lekcha.
“Nenda kuzimu mshenzi wewe”
Lekcha aliongea kwa sauti na palepale lile boma la nishati alilotengeza lilipuka na kuwa kama vile ni fataki na zile cheche zote kumvaa Roma huku zikiwa zimechanganyika na nguvu nyingine ambayo Roma hakuweza kuitambua lakini ambayo ni hatarishi.
Lekcha alikuwa akibweka kama vile alikuwa kwenye maumivu , chuki yake yote ya zaidi ya miaka aliokuwa nayo zidi ya Roma alionekana aliiwekeza katika ngurumo aliokuwa akitoa
Muonekano wake ulikuwa umebadilika kabisa na kuwa kama mtu mwingine na alionekana kabisa alikuwa akipambana kwa ajili ya kulipa kisasi.
Yaani ile hamasa aliokuwa nayo wakati akipambana na Aoiline ilikuwa ni tofauti wakati huo alivyokuwa akipambana na Roma.
Roma hakutaka kuwa mzembe , aliamua kukiongezea nguvu chungu chake na kisha akakipa kazi ya kunyonya nishati ile ya Ant Matter ili kuipunguza nguvu isimdhuru kwa kiasi kikubwa.
Lakini hata hivyo hakikuweza kuimeza yote na pale ilipomwangukia ilimfanya kujihisi ni kama vile anashambuliwa na nyuki.
Maumivu aliokuwa akihisi hapo yalikuwa ni mara mbili na yale ambayo aliyahisi wakati akiwa ndani ya kizimba cha Dhana ya mafuvu na misumari tisa ya Joka.
Katika hali hio ya kupambana na nguvu kubwa hata ule ugonjwa wake ni kama vile umeshituka kiasi cha kufanya macho yake kuanza kubadilika rangi na kuwa ya kijani..
“Arghh…!!”
Roma alitoa mguno mkubwa mno huku mishipa yake ya damu ni kaa vile inataka kumpasuka na mwili wake ulionyesha hali ya kutaka kupitia mabadiliko , ilionyesha ni dhahiri virusi ambavyo vilikuwa vimelala kwenye mwili wake viilitaka kuamka na kumfanya kuwa jitu.
Lakiini hata hivyo lilikuwa shambulizi dogo sana la kuweza kummaliza Roma kwani maumivu yale ni kama vile yalimfungua ubongo na kujikuta akiingiwa na utashi wa kutaka kufanya shambulizi kubwa zaidi.
“Radiii…!!
Roma alibweka na palepale kimbuka cha nishati ya nguvu ya mbingu na ardhi kilijikusanya juu na kugeuka kuwa moto wa zambarau na wa bluu na mara baada ya kuunganika tu radi ilimshukia Lekcha kutoka pande zote na kuanza kupambana na ile nishati ya Ant- Matter.
Roma nguo hakuwa nazo tena kwenye mwili wake na alikuwa yupo uchi kabisa na mwili wake ni kama vile unapigwa na shoti ya radi kwani ulikuwa ukitetema sio mchezo.
Wakati radi ikishambuliana na nishati ile ya nguvu isiokuwa maada Roma alishuka chini kama vile ni kimondo na mara baada ya kujipigiza chini aliweza kutengenza wimbi kubwa mno la nishati ya nguvu za kijini liloambanta na nguvu ya radi na kumshambulia Lekcha kwa chini.
Roma hakuishia palepale alifyatuka kama mshale huku akiwa amekunja ngumi na kumsogelea Lekcha kwa kasi na kumchapa ngumi ya kichwa iliokuwa na uzito wa tani nyingi mno.
“Pfff!!”
Lekcha alijikuta akipokea mashambulizi matatu kwa wakati mmoja na kufanya nguvu yake ya nishati ya anti-matter kusambaratika lakini wakati uleule ikiyeyushwa na shoti za radi.
Roma mpango wake ulikuwa mwepesi , alijua nishati ya Lekcha ilikuwa na kikomo na kwasababu dunia ki asili ni maada basi uwezo wa Lekcha kuidhibiti nguvu hio ilimhitaji uwezo mkubwa hivyo alimshambulia Lekcha kwa kasi kusambaratisha nguvu zake huku akitumia shoti za umeme wa radi kuziyeyusha ili zismrudie.
Mashambulizi yale ya haraka yalimfanya Aoiline aliekuwa akiangalia kwa mbali kuwa katika hali ya kutokuamini kile alichokuwa akiona.
Alikuwa ni jini wa uwezo wa juu sana ambaye alishawahi kuwepo na alikuwa ameona vitu vingi na mbinu nyingi ambazo majini wanazotumia lakini havikumshangaza , lakini upande wa Roma kila alichokuwa akifanya kilikuwa kipya kwake na kumfanya kushangaa.
Unachopaswa kuelewa hata ukiwa ndani ya mnara huo bado sheria za ulimwengu wa mapeppo zilikuwa zikitumika hapo hivyo kufanya uwezo wake kuwa wa chini , lakini sasa kama kwa nusu ya uwezo wake aliweza kupigana na Lekcha kwa mwaka mzima lakini hakufanya shambulizi kubwa kama ambalo Roma amefanya bali alimuona ameimarika nje ya matarajio yake.
Hivyo kimahesabu ni kwamba Roma na yeye alikuwa akitumia nusu ya uwezo wake na moja kwa moja aliona lazima Roma atakuwa amemuacha mbali sana hata kama akitoka katika ulimwengu wa kawaida na kurudiwa na uwezo wake wote.
Mbaya zaidi alichoona ni kwamba Roma anaonekana uwezo wake huongezeka kila ndani ya dakika.
“Huyu kijana ubora na utimamu wa kimwili unafaida kubwa kwake, kautoa wapi huo mwili?”Alijiwazia.
Aoiline aliamini mwili wa Roma ndio chanzo cha kuweza kufunikiwa kwa muda mfupi na alimfananisha na ukoo wa majini joka wa zama zile.
Kadri ambavyo Roma hakuwa akimpa nafasi Lekcha kujikusanya ndio ambavyo alikuwa akizidi kupoteza nishati yake ya Ant- Matter na ilichukua muda mfupi ilionekana Lekcha alibakiwa na nguvu kidogo sana.
Nishati ya Ant matter inaweza kuwa na nguvu lakini ni ghali sana , hii inamaanisha kwamba ni muda mwingi sana unahitajika kwa ajili ya kuikusanya tofauti na nishati ya mbingu na ardhi ambayo mara nyingi haina kikomo ili mradi tu ubongo wako unafanya kazi vizuri, hasara kubwa ya nishati hio ni kwamba asili yake sio ya kidunia hivyo huharibika kwa kasi.
Lakini sasa wakati Roma akiwa na mawazo kwamba amemzimisha Lekcha mpaka kuwa dhaifu Lekcha alirudi katika umbo la kawaida na kumfanya Roma amuone ni kama ndoto ambayo hawezi kuifuta.
Lekcha mara baada ya kurudi katika umbo la mfanano wa kibinadamu alianza kukunja shingo yake kama vile anaweka mwili sawa kana kwamba anamwambia Roma pigo zako ni za kitoto.
“Vipi tena bwana mdogo Roma Ramoni A.k. a Hades dhaifu, hicho ndio ambacho unaweza kujivunia , hii radi yako inaonekana kuwa na nguvu kweli lakini athari zake kwangu ni ndogo”Aliongea Lekcha huku akitoa tabasamu la uovu.
Roma moyo wake ulisinyaa , alidhania akitumia mahesabu ya kikanuni ya nishati ya nguvu hio anaweza kummaliza Lekcha kwa kumshambulia bila kukoma kwa kasi lakini ilionekana kuna kitu ambacho hakukitambua kutoka kwa Lekcha.
“Roma usichokijua na wasichokijua wanasayansi ni kwamba wakati wa nishati ya matter na anti matter zinapogongana hakutokei kitu kinachoitwa Annihilation kama wanavyoamini bali asilimia mia moja kunatokea nishati nyingine yenye tabia tofauti , nishati hii ndio ilionifanya uwezo wangu kuimarika maradufu kadri nilivyokuwa nikipambana na yule Mbweha , bomu la nyuklia ambalo hutengenezwa kwa kurutubisha viini vya atomu ni sawa na asilimia moja tu ya nishati inayotokea wakati wa kugongana kwa nishati hizi mbili , hivyo ninao uwezo wa kuharibu kisiwa kwa kukadiria tu uwezo nishati ninayotaka itokee , sasa hebu jiulize gunduzi yangu hii ndio nataka kuiajaribisha kwako”
Aliongea Lekcha na palepale alitengeneza kitenesi cha nguvu ya nishati ya Ant-Matter na kukirusha aliposimama Roma kwa kasi.
Roma alitaka kutumia Chaos Cauldron kuweza kukijikinga na shambulizi lile lakini Chaos alionyesha hali ya kunywea kutokana na ukubwa wa shambulizi lile.
Roma alijikuta akikosa chaguo lingine na kung’ata meno yake kwa hasira na kisha palepale kwa spidi ya haraka sana alichoropoa lile Shoka kutoka katika hifadhi yake ya pete.
Inasemekana katika ulimwengu wa majini kulikuwa na Dhana kumi na saba ambazo zilikuwa na nguvu sana enzi hizo na kati ya Dhana hizo ni Shoka hilo la Pangea ambalo halikueleweka namna linavyofanya kazi , kuna tetesi kwamba linaweza kuingia katika shimo jeusi la anga na kutoka.
Kitu kingine ni kwamba nguvu yake pia ni kama ilivyokuwa kwa Cauldron, shoka hilo linaonyesha uwezo wake kulingana na uwezo wa mtumiaji. Lakini kitu cha uhakika ni kwamba Shoka hilo lilikuwa na uwezo wa kuchana anga na kwenda kinyume na kanuni za anga.
Katika kanuni za kifizikia kutoka kwa mgunduzi Einstein anasema anga ni kama kitambaa, ijapokuwa hakumaanisha kitambaa kama kitambaa lakini ndio namna rahisi ya kuelewa kwamba anga linaweza kuharibika kikanuni.
Sasa Shoka hilo lilikuwa na uwezo wakuchana hiko kitambaa ambacho ni kama anga sasa kwa kukiuka sheria za anga.
Unaweza kushangaa hizi Dhana zinafanyake kazi lakini teknolojia ambayo ipo nyuma yake ni nje ya uelewa wa fahamu za kibinadamu na hata viumbe wenye akili sana kama majini na hata miungu hawakuwa wakijua siri iliopo nyuma ya uhunzi wa Dhana hizo..
Chukulia mfano safu ya ulinzi ya gereza la Roho katika miliki ya Hongmeng mpaka wakati huo sio Athena wala kiumbe chochote aliweza kujua teknojia ya safu hizo za ulinzi zinafanyaje kazi.
Hivyo hata kwa Roma mwenyewe hakuwa akijua namna Dhana hizo zilivyotengenezwa alichokuwa akijua ni namna ya kutumia tu.
Sasa Roma aliamini kwasababu kanuni za anga hazikufanya kazi vizuri katika ulimwengu huo kutumia Shoka hilo ambalo linaenda kinyume na kila sheria ya asili ndio tumaini pekee la kuhimili nguvu ya Ant- matter.
Kitendo cha Shoka lile kutua katika mkono wa Roma na kuliingizia nguvu za kijini lilibadilika palepale muonekano wake na zile herufi ambazo zilikuwa zimechorwa katika Shoka hilo ziling’aa.
Ijapokuwa lilionekana kama shoka la kawaida lakini uzito wake haukuwa wa kawaida na pengine hata Rose ambaye yupo mwishoni mwa levo ya Nafsi asingeweza kulishika mkononi.
Kwa namna ambavyo liliamshwa na nguvu za mbingu na ardhi za Roma ilikuwa ni kama vile shoka hilo lilikuwa likitawaliwa na nafsi lakini ukweli ni kwamba hakukuwa na nafsi yoyote , ilikuwa ni kama kifaa tu ambacho kimelala na muda huo kimepata nishati na kuingia katika matumizi.
Roma hata yeye ndio inakuwa mara yake ya kwanza kujaribisha shoka hilo na kitendo cha kuamka kwake ile sehemu aliosimama ni kama vile upepo unakimbia , msisimko ulioweza kutoka ilikuwa ni kama vile kiumbe mwenye nguvu sizizokuwa za kawaida anawavamia.
“Arghh…!!!”
Roma alipiga yowe na kwa kutumia nguvu zake zote za kijini aliinua lile shoka juu na kisha akalipigiza chini ndani ya sekunde.
BOOM
Wimbi la nguvu iliotokana na shoka hilo ilikuwa ni kama vile inakwenda kutenganisha mlima wa gereza la nafsi za giza na kuziachia.
Shambulizi lile la Lekcha mara baada ya kugongana na msisimko wa nguvu ya lile shoka mwanga wake ulibadilika katika rangi zisizokuwa zikihesabika na shambulizi lake nikama vile limetumbukia kwenye shimo.
Aoiline ambaye alikuwa mbali aliweza kuhisi msisimko usiokuwa kawaida kutoka kwa nguvu ya nishati ya Ant-matter iliotengenezwa na Lekcha , aliamini kama Lekcha angetumia shambulizi hilo kumshambulia basi angepatwa na majeraha makubwa mno, lakini sasa alishangaa pale Roma akitoa kitu kilichomwacha mdomo wazi.
Licha ya kwamba aliishi miaka mingi hakutegemea kuona Roma angeweza kumiliki kitu cha ajabu kama hicho , alikuwa akisikia kuhusu shoka hilo lakini hakuwahi kuona katika uhalisia.
Unajua bwana majini wengi wana historia kama ilivyokwa binadamu lakini utofauti wa majini na binadamu ni kwamba majini wa zamani walikuwa na akili nyingi sana na kufanya vitu vya ajabu kuliko hawa wa sasa lakini kwa sisi binadamu uwezo wetu wa akili unaongezeka kulingana na muda.
Yaani wakati binadamu akiendeea kutafuta siri za dunia kwa kupanua uwezo wa kufikiria upande wa majini wao wanataka kufikia levo za kufikiria za watangulizi wao.
Sasa katika vitabu vya kihistoria vya majini walikuwa wakisoma uwepo wa Dhana kumi na saba na kati ya Dhana hizo ni Chaos Cauldron , Shoka la kipangea , kioo cha nafsi, Fimbo ya muujiza na zinginezo lakini licha ya kuishi miaka mingi sana hakuwahi kushuhudia hizo Dhana.
Sasa alijjiuliza Roma amewezaje kumiliki Dhana mbili kati ya Dhana kumi na saba za kihistoria. Alijiambia huyu mtoto katoa wapi vitu hivyo.
Lakini licha ya kuwa kwenye mshangao hakuonyesha hali ya kufurahi mara baada ya kuona nguvu halisi ya shoka hilo , hakujali nguvu yake itauathiri vipi mnara lakini alitaka kuona matokeo tu.
Ile sehemu ambayo amesimama Roma kulionekana hali ambayo haikuwa ikielezeka ilikuwa ni kama vile kataratasi ya nailoni linaungua katikati na kutengeneza ufa katikati.
Roma mwenyewe alishangazwa na kitu kile na palepale wazo lilimwingia na kuhamaki na kujiambia kwahio kuchanika kwa anga ndio kupo hivi.
Roma alishangazwa na jambo hio radi yake ilikuwa ikileta machafuko lakini shoka hilo ilionekana ni kweli ilikuwa ikiharibu anga na kumfanya yeye kuwa kati , yaani ni kama lile shoka linaharibu anga na wakati huo huo kunatengenezeka anga lingine jipya ambalo ndio anaonekana yupo yeye sasa.
Roma alijua kabisa anga la ulimwengu huo sio ‘Parallel dimension’ kama ilivyokuwa kwa ulimwengu wa majini watu, bali ni tofauti kabisa ndio maana ukiwa katika huo ulimwengu huwezi kufanya mawasiliano kwa namna yoyote ile na ulimwengu wa kawaida, pili kanuni zake za anga hufanya kazi kitofauti.
Kama anga la uimwengu huo lilikuwa la kawaida basi majini hao wasingeweza kufungiwa kirahisi hivyo.
Moja kwa mmoja ilimaanisha kwamba Shoka hilo lilikuwa na sheria zake za ufanyaji kazi.
Kuna kitu kilikuwa kikimwambia kuna uwezekano wa Roma kubadilisha utendaji kazi wa ulimwengu huo kwa kutumia hilo shoka , ikimaanisha kwamba ameshikilia ufunguo ambao unaweza kuruhusu njia ya kutokea.
Yaani ni kama ilivyokuwa kwa mfalme Wuja mkuu wa majoka kutengeneza Dhana ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza njia ya kutokea ulimwengu wa kawaida ndio ambavyo Roma alihisi uwezo wa shoka lake ulivyo.
Shambulizi ambalo Lekcha aliamini kwamba linaweza kuharibu kisiwa lilisambatatishwa na Sururu la Roma na moja kwa moja alijihisi kukasirika mno kwani hakutegemea hilo.
“Haiwezekani… Hadae nasema haiwezekani ukapangua shambulizi langu namna nyepesi hivyo”
Lekcha aling’aa meno yake kwa hasira, nguvu yake ya nishati ambayo ilikuwa kama dhoruba baharini ilijikusanya upya katika mkono wake na kwa mara nyingine alijaribu kumshambulia Roma.
Roma baada ya kuona utukufu wa shoka lake hali ya kujiamini iliongezeka na kujiambia yes ni muda wa majaribio na palepale alifyeka anga na shoka lake kutengenza wimbi lingine la mchaniko uelekeo wa shambulizi la Lekcha.
Shambulizi la Lekcha lilikuwa kubwa kweli lakini shoka lile liliteneneza hali ya kuyumba kwa anga hivyo kufanya shambulizi lake kusambaratika , kwa bahati nzuri ni kwamba anga lina nguvu ya kinishati kubwa sana hivyo hata kama shoka hilo lilikuwa na uwezo wa kubadilisha utedaji kazi wa kawaida wa anga ilikuwa ni eneo dogo tu hivyo athari zake zilikuwa katika mzingo mdogo na pia ile sehemu ambayo huonekana kuharibika inarudi upya kwa kasi.
Lekcha alikasirika mno mara baada ya kuona ana mashambulizi yenye nguvu lakini bado hakuweza kumfanya chochote Roma kutokana na shoka lake na aliamua kupotezea kila kitu na kuanza kukusanya kiwango kikubwa cha nishati ya ant matter.
Roma alijua Lekcha yupo katika hali ambayo ni ngumu kumuua , alikuwa ni kama nishati na ili kumaliza lazima kuyeyusha nishati yake hivyo alitumia Chungu , radi na shoka kushambulia kwa wakati mmoja.
Wakati huo ni kama Cauldron imeweza kutambua uwepo wa shoka na hali ya roho ile ya mnyama kujiamini ilirudi.
Wakati huo sasa katika floor hio ukiangalia kwa juu ni kama vile kuna nishati mbili ambazo zilikuwa zikivamiana huku watu waliokuwa wakidhalisha nishati hizo hawaonekani.
Aoiline aliekuwa akiangalia pambano hilo uwezo wake ulikuwa umerudi lakini hata hivyo hakutaka kuingilia.
Sio kwamba hakutaka lakini nguvu ya kimauaji iliokuwa ikimtoka Roma ilimfanya kuona kabisa hana haja ya kuingilia.
Lakini hata hivyo Roma asingependa maana katika maisha yake hakupenda kumtumia mwanamke kama chombo cha mafanikio yake ndio maana tokea amuache Aoiline ndani ya mnara huo roho iikuwa ikimsuta.
Kadri Roma alivyokuwa akishindana na nguvu ile ya Ant-Matter ni kama vile kichwa chake kinakuwa kizito mno kiasi kwamba ule ugonjwa uliokuwa umempotea ulianza kurudi kwa kasi na kufanya macho yake kuwaka taa nyekundu.
Ilikuwa ni kama vile ile nishati ya Ant- matter inashitua hali flani ya utendaji wa mwili wake.

SEHEMU YA 768.
Wakati huo huo vita hio ikiendela katika ngome ya makao makuu ya kambi ya kitafiti ya Zeros organisation alionekana Madam Dyana akiwa na tabasamu la aina yake usoni huku akiangaia kitu kwenye skrini , ilikuwa ni kama vile alitamani kuona kitu cha namna hio kwa muda mrefu.
Dyana ni mwanamama ambae ni Chief wa kitengo cha usimamizi wa maendeleo ya mpango LADO yaani idara ya PLMC.
Kitengo hicho kwa muda mrefu sana kilikuwa kimya sana na hakukuwa na dalili yoyote ya taarifa kutoka kwa ajent wao na hata wale wanasayansi ambao walikuwa wakihusika walikuwa wakilala tu muda mwingi lakini siku hio ilionekana kuwa tofauti katika miezi mingi.
Licha ya kwamba ulimwengu ulikuwa katika hali ya sinfofahamu lakini kazi zilikuwa zikiendelea kawaida ndani ya kambi hio na ukweli ni kwamba ubize ulikuwa umeongezeka kwa kiwango kikubwa sana.
Sasa ni miezi kadhaa tokea Dyana kupokea maagizo kutoka kwa mheshimiwa Barack Mabo.
Unajua katika jumuia yoyote ambayo inahusisha viumbe binadamu lazima kuna wale ambao wana mtazamo tofauti na hio ilionekana ndani ya umoja wa Zeros organisation.
Inaaminika kwamba Barack Mambo ndio moja ya wanachma wa vyeo vikubwa ndani ya jumuia hio ya siri tena akiwa mkuu chini ya The First Black lakini ndio mtu pekee ambaye alikuwa na mawazo tofauti na malengo ya Zeros.
Mpango LADO ni mpango ambao una sahihi yake na sio kwake tu karibia kwa maraisi wote waliopitia katika nyumba nyeupe mpango huo hujumuishwa katika viapo vyao ili kuulinda na kuudumisha.
Ki uhalisia haukuwa mpango mbaya kwani malengo yake yalikuwa wazi , malengo ya mpango LADO hayakuwa kwa ajili ya kumtengeneza ajent mwenye nguvu pekee lakini ukweli ni kwamba ni mpango ambao uliundwa kwa ajili ya kupata binadamu mwenye DNA tofauti, yaani kwa lugha nyepesi kilichokuwa kikilengwa ni kutengeneza kizazi kipya.
Illuminat ndio jamii ambayo ‘ideology’ yake imepewa kipaumbele katika zeros organisation kuliko jamii yoyote ile , waliamini ili dunia izidi kuwa salama kuelimika kwa binadamu lazima kuendane na kasi ya muda na ili hilo kufanikiwa lazima kuwepo binadamu wenye uwezo tofauti wa kufikiria na huo ndio utakuwa mwanzo wa gunduzi mpya tofauti na mwendelezo wa teknolojia zilizopo.
Upande wa Ant-Illuminat wao umoja wao ulianzishwa kupinga ‘ideology’ za Illuminat kwamba ii dunia iendelee kuwa salama maendeleo ya teknolojia yanatakiwa kuendelea katika spidi sawa na ukuaji wa kifikra wa kibinadamu , yaani kusiwe na ‘hacking’ ya aina yoyote ile ya kujaribu kuharakisha ukuaji wa kufikiria kwa binadamu.
Sasa Barack Mabo katika mawazo hayo mawili yeye ni vuguvugu, ikimaanisha kwamba nusu anakubali ajenda za illuminat na nusu anakubali ajenda za Ant-Illuminat na hili ndio ilimfanya kujikuta kuwa na mawazo tofauti.
Kati ya watu ambao anafanana nao kimawazo ni Dyana mwanamama ambaye ndio aliepewa jukumu la usimamizi wa maendeleo ya mpango LADO.
Sasa ni miezi kadhaa tokea yatokee mabadiliko ya hali ya hewa duniani , moja ya watu ambao hawakuwa na utulivu na kile kilichokuwa kikiendelea alikuwa ni yeye.
Na wasiwasi ulimfanya kufanya vikao vingi sana na wadau wengi kuzungumzia kile kinachoendelea na nia halisi ya viumbe hao kutoka sayari nyingne zidi ya binadamu.
Ijapokuwa ni kweli Athena aliwahakikishia kwamba ili kuibadilisha dunia kutoka katika hali ya sasa ya Dystopia na kwenda kuwa ulimwengu wa Utopia kuna kafara itahitajika lakini bado haikutosha kumuamini moja kwa moja na kutokufanya chochote au kutokuchukua tahadhari.
Ieleweke kwamba Athena licha ya kuanzisha umoja huo hakuwahi kujionyesha hadharani na hata pale alipokuwa akijionyesha ni katika hali ya kuogofya pengine hii iliwafanya watu kuwa na imani dhaifu juu ya mipango yake.
Ukweli ni kwamba hakuanzisha Zeros kwa njia ya moja kwa moja bali ni binadamu wenyewe ambao walitoa pendekezo na yeye akaingiza ushawishi wake na mwisho wa siku ikaonekana ni kama yeye alieanzisha.
Sasa Barack Mabo na wanachama wengine walikuwa katika vikao vya kila siku na ajenda kubwa iliokuwa ikizungumziwa katika vikao hivyo ni kufumbua fumbo gumu ambalo Athena amelitega.
Fumbo lenyewe ni kwamba kama Athena alikuwa na nguvu kubwa kwanini akataka mpango LADO kufanikiwa kwa silimia mia moja na kumfanya Roma kuendelea kuwa na nguvu kila uchao.
Yaani viongozi hao na wanasayansi hao waliona kabisa hakukuwa na uhusiano wowote uliopo kati ya mipango ya Athena na kupanda madaraja ya ki uwezo kwa ajent Thirteen.
Athena aliwaambia kufanikiwa kwa Roma ni kwa ajili ya kutengeneza uzao mpya , binadamu ambaye atakuwa na uwezo wa kufikiria tofauti lakini kwanini inaonekana ni kama vile Athena anataka kuua binadamu wote.
Yamkini ni kwamba binadamu hao ambao wanajiita ndio watu waliokuwa karibu na mwishoni mwa piramidi la uongozi wa dunia walikosa majibu , walikosa majibu kutokana na kwamba waliekuwa wakimuuliza maswali hakuwepo na hakujisumbua hata kujitokeza kwao.
Walijikuta kama vile ni viumbe ambavvyo vimetelekezwa kwani hali ya dunia ilizidi kuwa mbaya lakini hakukuwa na majibu kwamba hali hio ingedumu kwa muda gani na matokeo yake ni nini ,walijuliza je hali hio ndio dunia ambayo Athena anataka kutengeneza lakini kimahesabu wanaonna hakuna namna Athena akawa na nia nzuri kwa binadamu.
Mwisho wa maamuzi ya vikao ndio wengine wanashauri kujengwa kwa Safina kuokoa binadamu asipotee , huku kundi la watu wakipinga pendekezo hilo na kutaka kushindana na miungu.
Moja ya watu ambao waliona kujenga Safina sio suruhu ni mstaafu Barack Mabo na kutokana na kuwa na mawazo ya tofauti aliamini mtu mmoja pekee ambaye anaweza kutatua kitendawili kilichokuwa kikiwasumbua wengi ni Hades pekee kwani alikuwa ni nusu binadamu na nusu viumbe hao.
Sasa ule wakati ambao walikuwa wakitamani Roma aingilie kati ndio wakati ambao Roma ametoweka ghafla tu na asijiulikane alipo.
Ni muda wa mchana usiokuwa na jua nchini Marekani , licha ya kwamba dunia ilikuwa katika hali ya baridi kali lakini baadhi ya raia waliokuwa wakijiweza kiuchumi hawakuwa na hali mbaya.
“Dyana nipe ripoti , naamini simu hii sio ya bure kuna matokeo chanya?”Aliongea Raisi Barack Mabo akiwa nyumbani kwake na hio ni mara baada ya simu yake kuita na kupokea kwa haraka haraka.
“Ndio mheshimiwa tumeweza kupata dalili ya mabadiliko ya kimwili ya Ajent 13 na taarifa zimeingia katika mfumo wetu dakika chache zilizopita”
“Nini! Dyana unamaanisha mmepata Hades?”
“Mheshimiwa tokea tuanze kutafuta taarifa za Hades alikopotelea ni leo tu mifumo yetu imeonyesha uhai , vijana walikuwa macho kutokokosa hata viashiria kidogo ndani ya mfumo na juhudi zao za kuwa macho leo hii zimezaa matunda, inaonekana Hades yupo katika hali ya mapambano makali na signal za sayansi ya Devine light zimetuma taarifa hatujui kwa uhakika ni nini kinaendeea na katika lango lipi la anga lakini ni dalili nzuri”Aliongea Dyana na Mheshiimiwa Barack Mabo alionekana kuonyesha hali ya mabadiliko kidogo katika wasiwasi wake.
“Dyana nataka kujua kama Hades anaweza kurudi?”
“Mheshimiwa ili mradi yupo hai naamini atarudi , ndio tegemeo letu kwasasa kujibu maswali ya kinachoendelea, Barrack mpaka sasa umeshindwa kuwaamini watu wa Vatican?”
“Sio kama siwaamini lakini wamekuwa ni watu wa njama sana na mitego , wanasema kuna unabii unaopaswa kutimia ndio maana hawachukui hatua yoyote lakini mpaka leo hii hawatupi maelezo”Aliongea na kumfanya Dyana kutulia.
“China na Japani msimamo wao upoje , nasikia hawakushiriki katika vkao vyote vya kimataifa vya dharula lakini walikuhitaji kama mjumbe wao”Aliongea na kumfanya Barrack Mabo kukumbuka namna alivyofuatilia kikao cha viongozi wa China.
*****
Wiki kadhaa ndani ya Zhongnahai Beijing kulikuwa na kikao kizito ambacho kilihusisha viongozi wote wa juu wa taifa hilo na wale wastaafu waandamizi(Country senior’s).
Kiongozi mkuu namba moja mwandamizi ndio ambaye alikuwa akiongoza kikao hicho , pembeni yake kulikuwa na viongozi akiwemo Li Moshen waziri wa ulinzi , YangChen mkuu wa majeshi , Cai Yuncheng mkuu wa kikosi cha wachawi na Ning Guanyao ambaye ni waziri mkuu hao ni baadhi tu.
Katika watu waliokuwa na wasiwasi ndani ya kikao hicho ni Cain Yuncheng huyu ndie ambaye ni kama anahusika na utendaji wa Hongmeng katika ulimwengu wa kawaida na wasiwasi wake ni kwamba Hongmeng inaweza kukosa nguvu kutokana na kwamba Anjiu mkuu wa miliki ya Xia alikuwa akiwashambulia.
Ijapokuwa baridi ilikuwa kali sana ndani ya taifa hilo lakini China ni moja ya nchi ambazo zina hakiba kubwa ya chakula lakini pia limeeendelea katika urahisishaji wa social service delivery kwa raia wake.
Yaani haikuwa na haja kwa raia kutoka nje kwa ajili ya kwenda sokoni wala dukani bali teknolojia ilirahisisha kazi hio hivyo kufanya nchi hio yenye watu wengi zaidi duniani kwa mara ya kwanza kuonekana kama vile haina watu.
Bila shaka sio kwamba watu wote hawakutoka , kuna wafanyakazi walitoka lakini ilikuwa kwa tahadhari maalumu na hata wale wenye vipato kidogo walikuwa wakisaidiwa.
Baada ya kimya kirefu cha mkuu wa nchi hio hatimae alianza kuongea.
“Hatuwezi kuendelea kukalia mikono yetu zaidi , kwanzia sasa tutajitegemea sisi wenyewe na sio wengine”Aliongea lakini hakuna ambaye aliongea kwani wote walikuwa kimya wakimwangalia , licha ya kwamba dunia ilikuwa katika hali isiokuwa ya kawaida lakini tabasamu halikumtoka.
“Kutokana na janga hili linaloendelea nchi yetu yote na hata kwa binadamu tunapitia changamoto , kama unachochote cha kuongea waziri Ning tafadhari sema, kwanini upo kimya sana siku hizi?”
“Mheshimiwa ulimwengu wa majini sasa hivi upo kwenye machafuko kutokana na vita inayoendelea , miliki ya Xia kwa kutumia watu wao ambao wamefikia levo ya radi wanajaribu kuvamia miliki nyingine , ikumbukwe Xia ipo ndani ya bara la Asia na kwa muda mwingi wamekuwa na wivu na Hongmeng , je uhakika tunao kama wakiiteka Hongmeng hawatotaka kuchukua nafasi yao na kuingilia maswala yetu?”
“Usiwe na wasiwasi , hawawezi”Alijibu Raisi na kisha akaendelea.
“Ijapokuwa miliki ya Xia imepanda na kuwa na nguvu ndani ya ulimwengu wa majini kuliko miliki zote , kutumia nguvu zao kutaka kuingilia maswala ya ulimwengu wa kawaida hakutowasaidia chochote , zaidi ya kujiingiza hatarini kwa kuwachokoza wajumbe wa muungano wa ulinzi wa dunia na ulimwengu wao,sidhani wanaweza kuwa wajinga hivyo”
Mara baada ya kutajwa wajumbe wa ulinzi wa umoja kila mmoja alionyesha hali ya msisimko.
Haikuwa kwa majini tu ambao walikuwa wakijua uwepo wa umoja wa ulinzi wa dunia , ukweli ni kwamba historia hio haijawahi kufutika katika uso wa dunia tokea siku ambayo viumbe kutoka sayari nyingine kutua duniani.
Ni wajumbe hao hao wa umoja ndio waliohusika na ambao waliendelea kushikilia ulinzi wa usalama wa dunia.
Katika hali kama hio ya dunia kuwa hatarini na vilevile kupotea kwa Roma kitu pekee ambacho binadamu wenye kuelewa siri ya uwepo wa wajumbe hao waliomba waingilie kati.
Walinzi wa dunia au The Guardians jukumu lao kubwa ni kuhakikisha dunia inaendelea kuwa salama na wajumbe hao wa ki’umoja hawakujali maswala ya nchi na nchi , ukweli ni kwamba hawakujihangaisha na maswala ya kiserikali ya kibinadamu wala majini.
Hawajali Israeli kumvamia Mpalestina wala Mchina kumvatia Mtaiwani au Mrusi kumvamia Ukraine , ajenda yao kuu ni kulinda uwiano wa usalama wa kidunia hii ikimaanisha katika malango yote ya dunia , iwe ni ulimwengu wa kawaida ama ulimwengu wa ajini pepo au ulimwengu wa majini watu lakini vilevile kuzuia jamii moja ya viumbe kushambulia viumbe wengine.
Majini wa Panas , walitakiwa kubakia Panas na majini wa Xia walitakiwa kubakia Xia na kama wataamua kushambuliana wao kwa wao hakuna tatizo lakini kama watashambulia binadamu na kutaka kuteka nchi ndio tatizo hutokea ambalo lilipaswa wajumbe hao kuingilia.
Lakini kilichokuwa kikiwasumbua sio serikali ya China tu bali serikali zote ambazo ziikuwa zikijua historia ya uwepo wa watu hao ambao haikueleweka ni majini , binadamu au malaika ni kwamba hawajui walikuwa na ajenda gani na pili hawafahamika kwa sura ni wakina nani na wanatokea nchi gani au wanaishi nchi gani.
Inasemekana ni matiafa makubwa duniani tu ambao wameweza kukutana na mmoja ya wajumbe hao yaani Mkuu namba moja na mara nyingi alijitokeza kwao kwa ajili ya kutoa onyo tu na haikuwa vinginevyo.
Nchi pekee ambayo ni ndogo na mkuu namba moja alijitokeza kwa kiongozi wake ni Rwanda tu na hio yote ni kutokana na Jeremy kushikirikiana na miliki ya Panas kutaka kuingilia maswala ya kibinadamu,
Mtu binafsi tu ambaye aliweza kukutana na mkuu namba moja ambaye huunda baraza la usalama wa ulimwengu ni Roma pekee.
Ki ufupi ni kwamba Master Namba moja mwenyewe alikuwa na nguvu sana kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kukutana na raisi wa Urusi kwa kutumia sura ya Singanojr na vilevile akakutana na raisi wa Korea Kaskazini kwa sura ya mtu mwingine , ili mradi amefikisha ujumbe haikujalisha ni sura ya nani inatumika.
Sasa Raisi wa China na baadhi ya watu tofauti tofauti ndio walijua siri hio ya uwepo wa hivyo viumbe lakini hawakujua ni wakati gani watachukua hatua hivyo tofauti na kusubiri waendelee kuteseka ni bora kujitegemea wao kwa wao.
Wakati kikao hicho kikiendelea upande mwingine Raisi Barack Mabo alikuwa akifatilia kila kitu, ni kama alipewa ruhusa ya kuangalia namna kikao hicho kinavyoendelea.
Ukweli ni kwamba Raisi Barak Mabo alikuwa akiamini kwamba wajumbe hao wa ulinzi wa dunia walikuwa na mawasiiano na taifa la China na hio yote ni kutokana na uwepo wa Hongmeng lakini matokeo yake ni kwamba hata raisi mwenyewe wa China hakuwa na mawasiliano nao lakini licha ya hivyo Barack Mabo hakumuamini na ndio maana mheshimiwa alimpa nafasi ya kuangalia kikao chake na vongozi wake waandamizi ili aweze kuamini maneno yake.
“Mheshimiwa dunia nzima ipo katika hili janga la baridi na miungu wanaendelea kutukandamiza , Hongmeng ambao ni tegemeo letu wenyewe wapo na matatizo , je hakuna uwezekano wowote wa hawa walinzi kutusaidia ?”Aliuiza mkuu wa kikosi cha uchawi.
“Bado hamjanielewa tu nilichojaribu kuwaelezea..?”Aliongea na kisha akawaangalia mmoja mmoja na kisha alivuta pumzi na kuendelea.
“Sio mimi tu ambaye nimejaribu lakini wenzangu wengi wamejaribu lakini hakuna uwezekano wowote ambao nimeweza kuwasiliana nao”
“Kwaho hii inamaanisha hawana mpango wa kusaidia binadamu?”Aliuliza Ning.
“Hilo sijui lakini na wenyewe wana falsafa yao mpaka kuamua kuingilia maswala ya kibinadamu, pengine wanaona dunia haipo hatarini”
“Hawana lolote hao nina uhakika wanawaogopa miungu”Aliongea waziri mkuu Ning kwa hasira.
“Waziri chunga mdomo wako”Aliofokewa na mheshimiwa Raisi
“Kila kitu kinatokea kwasababu maalumu mheshimiwa waziri , mzunguko wa kimaisha unatafsiriwa kutoka kuzaliwa mpaka kufa , uwezekano wa hawa watu kuwepo ni kweli lakini haijalishi kama wapo au hawapo , hatua ambayo binadamu tumefikia haijatokana na wao , ni kwa maarifa yetu na upumbavu wetu wenyewe , dunia ilipofikia sio kwa msaada wa kiumbe chochote bali ni sisi binadamu wenyewe na ndio sisi ambao tunapaswa kuipambania kurudi katika hali yake ya kawaida”Aliongea mkuu wa majeshi.
“Mr Yang upo sahihi katika hali kama kila taifa linataka kujitegemea hatuna budi na sisi kujua namna ya kujilinda”
Kwa mheshimiwa Barack Mabo ilikuwa ni kama vile anaangalia filamu , alichokuwa akitarajia hakukipata ijapokuwa kwa namna flani alijua ni kweli kuna uwepo wa hao viumbe lakini bado hakuamini.
Na swali hata yeye kwake lilibakia je ni kweli kama inavyosadikika kwamba kuna viumbe wasiofahamika wanaojiita walinzi wa dunia kama wapo ni lini watajitokeza na ni viumbe wa namna gani.
Mpaka mwisho hakuwa na majibu na alijikuta akirudi nchini kwake akiwa mnyonge.

SEHEMU YA 768.
Ilikuwa ni vita ya wanaume wawili na ingekamilika vizuri kama mmoja kati wao angeshinda bila kuongezewa nguvu ndio maana Aoiline hakutaka kuingilia.
Vita hio ya Roma na Lekcha ilikuwa sio ya kawaida kabisa iliojaa mizungusho , kurushiana makombora ya nishati na kuoteana.
Radi ya zambarau na bluu ndani ya mnara huo ilikuwa ikipiga mara kwa mara lakini katika floor hio ya kwanza haikufika
Roma alizidi kuwa jasiri kila sekunde ilivyokuwa ikisonga na alijiua licha ya kwamba akili yake ni kama vile imetawaliwa na mdudu na kufanya macho yake kubadilika rangi mara kwa mara lakini uungu wake ulikuwa imara mno na haikuwa kama kipindi cha nyuma ambapo hakuweza kujitawala kiakili.
Roma aliweza kuhisi mwili wake ukipitia maumivu mara baada ya kupigwa na mlipuko wa nishati ya ant-matter na kuhisi kupoteza kiasi flani cha nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi lakini hata hivyo alijiponyesha kwa haraka sana.
Kwa jinsi mwili wake ulivyokuwa ukifanya kazi , illikuwa ni kama vile alikuwa na mawasiliano na kila kiungo cha mwili , hata pale seli ambazo zilikufa na kujitengeneza zingine ni kama vile alikuwa akijua kinachofanyika.
Hisia za namna hio katika wakati huo zilikuwa ni za kipekee sana na ilimfanya kuhisi ulimwengu uliokuwa mbele yake ulikuwa sio , ilikuwa ni kama vile yupo katika lango jipya la anga.
Kila kitu ambacho kilionekana kuwa halisi katika macho yake ni tofauti..
“Hahaha…”
Roma wakati akiwa anahangaika ni kama vile alipata utashi flani hivi uliomfanya kucheka na hakujua hata ni kwa namna gani alisogea na hakujali ni shambulizi gani ambalo Lekcha atampiga nalo.
Kwa wakati huo upande wa Roma vita hio haikuwa ya kifo na uhai bali furaha mpya ili ujaza moyo wake, ni kama vile alikuwa akifurahia kinachoendelea katika wakati huo.
“Mvulana mjinga huyu … anacheka nini sasa”
Hata kama uwezo wa kufikiria wa Aoiline ni mkubwa kuliko wa Roma lakini hakuweza kuelewa ni kitu cha namna gani Roma alikuwa akipitia , hakuelewa hisia zake zilikuwa zikimaanisha nini.
Baada ya muda mfupi Aoiline alikunja ndita na aliangalia juu katika sehemu walipokuwa wakipambana Lekcha na Roma.
Kipande cha anga katika eneo waliopo ni kilikuwa kikiharibika kwa kasi , kwa macho ya kawaida unaweza usione kinachoendelea lakini kwa macho ya kijini au ya kiuungu lazima uone kinachotokea na kufanya nishati ya Ant-Matter aliokuwa akizalisha Lekcha kuwa na mawasliano na ulimwengu wa nje ya mnara hhuo.
Ilikuwa ni mnara huo umetengeneza ufa ambao ulikuwa ukipitisha hewa kwa juu.
“Hii nii…”
Aoiline aliwaza lakini macho yake yalichanua kama vile alikuwa ametegemea kitu ambacho kinakwenda kutokea.
Roma ambaye alikuwa akipambana na Lekcha alikuwa akicheka kama vile ni kichaa na uso wake ulikuwa umejaa hali ya kujiamini, hali flani ya utambuzi na ukuu kama vile ni mtawala mbele ya watawaliwa.
Lekcha ambaye alikuwa akipambana na Roma alijikuta akikasirika sana mara baada ya kutumia njia zote kujaribu kumfikia Roma kimashambulizi na kushidwa , kilichompa kero zaidi moyoni ni namna ambavyo Roma hakumchukulia siriasi.
“Siwezi kushindwa , siwezi kushindwa nimetoka mbali kufika hapa siwezi kushindwa leo , lazima nikumalize leo Hades”
Lekcha alibwatuka kama vile ni kichaa lakini sauti yake ilimezwa na ngurumo ya radi kubwa sana ambayo ilisikika kutoka nje ya mnara.
BOOM!!
Ilikuwa ni sauti kubwa ya kuumiza masikio ambayo ni kama vile mnyama ananguruma katika lindi la ukiwa wa milele au kama vile ni Mungu anafungua makufuli ya mateso k wa viumbe wake binadamu.
Ilikuwa ni ngurumo ambayo haikuwa ya kawaida , ambayo kwa haraka haraka haikuwa na asili ya mnara huo na kufanya waliokuwa wamesikia ni kama vile masikio yao yanasikia Kengele ya tahadhari .
Na ile sehemu ambayo walikuwa wamesimama Roma na Lekcha palikuwa na tundu ambalo limejitokeza kwa juu kupitia kwenye ule ufa ambalo lilikuwa na mawasiliano na ulimwengu wa nje.
“Hio ngurumo ya Dhiki ya mapigo elfu moja ya radi!! , Aisee huyu mtoto hazuiliki , kijana umefanikiwa vipi kuelewa haraka hivi tamaduni zetu na kupanda levo kila unapokuwa kwenye changamoto?”
Ailione ambaye alikuwa tayari amekwisha kupitia adhabu ya mapigo mengi ya radi alikuwa akijua kani ya radi ya mapigo mengi , alikuwa amepitia adhabu ya mapigo zaidi ya elfu moja hivyo asingeweza kushindwa kujua kinachoendelea.
Lakini sasa umri wa Roma ni miaka ishirini kwenda therathini kitu ambacho sio cha kawaida kwa umri huo kuweza kusababisha radi ya mapigo mengi.
Alijiambia mtoto huyo ambaye alionekana kuwa na tamaa ya pesa na maisha ya anasa haijalishi nini amefanya au wapi ametokea uwezo wake wa kutambua siri za mbingu na ardhi ni mkubwa mno kiasi kwamba unamfanya yeye mwenyewe kuona wivu.
Lekcha alijikuta akihamaki kwani hakutgemea mabadiliko ya namna hio.
Alikuwa akielewa kuhusu radi na mateso yake tokea siku ambayo aliweza kuuvaa mwili wa mkuu wa majoka mfalme Wuja , ijapokuwa alikuwa akijiamini kutokana na nguvu yake ya nishati ya Ant -matter lakini hakuwa na uhakika kama anaweza kupona kama atapigwa na radi ya mapigo elfu moja.
“Muda wowote radi itafika ndani ya hili eneo , je bado unataka kuendelea kushindana na mimi?”Aliuliza Roma huku akiona ishara ya wasiwasi kutoka kwa Lekcha
Lekcha alijikuta akiona ni kama vile anadhalilishwa na aliishia kutoa tabasamu la kejeli akionekana hataki kushindwa.
“Inaonekana umekasirisha anga na muda wowote radi inakuja kukupa adhabu yako ,hivi wewe mwenyewe unao uwezo wa kupona kabla ya kuniuliza , nina ngungu ya ant-matter ambayo inawea kulinda mwili wangu , unadhani radi hio itaweza kunifanya nini?”Aliongea Lekcha kwa kujiamini.
Roma hakuwa akipanga kumkasirisha Lekcha ukweli ni kwamba alijua kumdhibiti Lekcha lilikuwa ni swali la muda tu.
Hata kama hatomuua Lekcha Roma bado alikuwa na uwezo wa kutumia shoka lake na kumfungia katika space crack au kumpoteza mazima katika malango ya anga.
Lakini kwasababu Lekcha alionekana kuwa na hamu ya kupitia uzoefu wa nguvu ya radi akiwa na yeye hakuona haja ya kumjali
Mara baada ya kusita kidogo palepale alikiita chungu chake cha maafa kwa mara nyingine lakini hakutumia kwa ajili ya kujikinga na radi ambayo inatarajia kushuka alisimama na kisha alikizibia na mwili wake
Yaani alichokifanya Roma ni tofauti kabisa na mwanzo , kwani ili kupita dhiki hio ya mapigo mengi alitakiwa kukiweka chungu hicho juu ake kama kinga lakini awamu hio ni kama anakilinda chungu hicho na radi.
Kitendo kile kilimfanya Aoiline kuwa katika hali ya mshangao na alitaka kumuuliza Roma anajitafutia kifo lakini mara baada ya kufikiri kwa haraka alioneakna kupata wazo ambalo Roma anajaribu kufanya na macho yake yalijaa mshituko na kuamua kukaa kimya akitarajia namna Roma anavyokwenda kupita dhiki hio.
Upande wa nje mnara wote ulifunikwa na dhoruba ya wingu zito mno kiasi kwamba ni hakika wale ambao wapo karibu na mnara huo wasingewea hata kuuona kwani ulifunikwa mpaka kwenye maji na ni cheche tu na ngurumo ambazo zilikuwa zikisikika.
Katika ile floor ambao walikuwepo Roma ile ufa ambao umejitengeneza ulionekana muda wowote unakwenda kuporomoka kutokana na presha ambayo inajiandaa kuingia ndani.
Hali ya giza ilizidi kuongezeka ndani ya mnara na hakukuwa na mwanga tena kama mwanzo.
Roma upande wake hakuwa na muda tena wa kumfirikia Lekcha , ukweli ni kwamba aliacha kabisa kupambana nae.
Kulikuwa na nafasi ndogo sana kwa Lekcha kuweza kukwepa radi ile kwani alikuwa amekaribiana sana na Roma.
Ilionekana ni dhahiri baada ya Dhiki hio ambaye atafanikiwa kutoka hapo wa kuipita hio dhiki basi moja wa moja anaweza kuwa mshindi.
Boom!!
Palepale mwanga ulionekana ndani ya eneo lile mara baada ya shoti ya radi iliokuwa katika mwanga wa rangi ya fedha(silver), yaani ni mwanga ambao haukuwa mweupe sana wala mweusi sana.
Shoti ile ilianza kidogo kidogo na kwa nje ilikuwa ni kama vile anga linashambulia ule mnara na radi na kutaka kuangusha kwani wingu lilikuwa likizunguka kwa kasi kubwa mno , ni kama vile kuna panya yupo shimoni na paka anatafuta namna ya kupita ndo ilivyokuwa kwa namna wingu hilo lilivyokuwa likizunguka kupata upenyo wa kumpa Roma anachostahili.
Kitendo kile kilifanya mnara wote kuwa na hali flani ya umeme ambao ulikuwa endelevu , yaani ni radi ambayo haikukoma ni kama vile umeme umewashwa kutoka mawinguni na kuingia ndani ya mnara huo.
Upande wa Roma na Lekcha walikuwa wamefunikwa na shoti za radi ambazo ni kama hazina mpango wa wa kuwaachia na kuwafanya hata miili yao isionekane.
Zile nguvu za nishati ya Ant-Matter ambazo zilikuwa zimesambaa zote ziliyeyushwa na shoti za radi na kupotea mara moja , ikionekana kabisa hakuna uwezekano wa kuhimili nguvu yake.
“Arghhhh…uwiii!!”
Lekcha alipiga yowe kubwa mno la kilio cha kusaga meno na hio yote ni kutokana na kuyeyuka kwa kasi kwa nishati yake ya Ant Matter na kugeuka mvuke ambao ulipotelea angani. Alikuwa akibabuka kama vile ni magamba ya mti.
Upande wa Roma hakuonyesha ishara yoyote kama alikuwa akipitia maumivu .
Ukweli ni kwamba ile radi ilikuwa imemfunika Roma sio kwamba ilikuwa ikimshambulia lakini ni kama vile ilikuwa ikimzingira na kushidwa kupita katika mwili wake hivyo kutokumsambabishia maumivu yoyote.
Ilikuwa ni kama vile inamuogopa Roma kumshambulia kabisa tofauti na ilivyo kwa Lekcha.
Katika mkono wa kulia wa Roma alikuwa akibadilisha kwa kiwango kikubwa nishati za mbingu na ardhi na kutengeneza moto wa rangi nyeusi huku mkono wa kulia alikuwa ametengeneza kiwango kikubwa cha moto wa rangi ya bluu.
Moto ule ulikuwa ukimzingira na kutengeneza kitu kama gamba la radi ya rangi ileile ambayo ilikuwa ikisukumana na ile ya radi ya Dhiki.
Yaani ilikuwa ni kama vile nguvu ambayo Roma anadhalisha ilikuwa ikikataana na dhiki ile ya radi ndio maana ilitengeneza ‘magnetic field’ ambayo ilifanya radi ile kumzunguka Roma na kutokumgusa.
Ushawahi kuona filamu ambayo binadamu yupo msituni na anakutana na Dubu na yupo katika hali ya kutoweza kukimbia na anafumba macho kusubiria kuraruliwa na lile Dubu lakini ajabu mnyama yule aina ya Dubu anapiga magoti na kukusujudia basi hali hio ilikuwa ni kama vile kwa radi ile ya mapigo mengi.
Kitendo cha Roma kudhalisha moto mweusi na bluu na kisha kuunganisha kulimfanya kuweza kutengeneza radi yenye tabia sawa na ile ya Dhiki na kumfanya isihindwe kumsogelea.
Kifizikia kilichokuwa kikitokea ni sheria ya Ki’Electrostatic , sheria ambayo inaelezea kwamba kunapotekea chaji mbili zinazofanana ziwe aidha ni chanya au hasi ili mradi ziwe zimefanana basi zitakataana na kama zikitofautiana zitavutana.
Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema hakuna mvutano wowote kati ya mwanaume na mwanaume bali kuna mvutano mkali ambao huleta madhara pale mwanamke na mwanaume wanapokutana sasa chukulia radi aliotengeneza Roma ni radi dume na iliotaka kumuadhibu ni radi dume pia hivyo ki asili zitakataana.
Sasa ni kwamba kabla ya radi hio kushuka Roma alishajua kwamba akiunganisha elementi za moto mweusi na moto wa bluu atatengeneza shoti ya radi ya rangi ya fedha ambayo ndio rangi hio hio ya Dhiki.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba radi ya mapigo tisini na tisa ilikuwa na rangi yake na radi ya mapigo tisa ilikuwa na rangi yake vilevile na radi ya mapigo mia tisa tisini na tisa ilikuwa na rangi yake vilevile.
Utofauti huu wa rangi inamaanisha namna inavyotokea kuna utofauti mkubwa wa elementi za chaji.
Roma hakuhitaji chungu kujilinda na radi tena hio yote ni kwamba anao uwezo tayari wa kutengeneza radi ya rangi ya silver kwa kuunganisha moto wa rangi nyeusi na moto wa rangi ya bluu na matokeo yake ni kwamba akawa anafanana na radi ya mapigo mia tisa tisini na tisa na kama sheria kifizikia ya asili inavyosema radi ile ilimtambua Roma kama mwenzake kutokana na kudhalisha nguvu inayolingana na kwake na matokeo yake ilishindwa kumdhuru.
Upande wa Lekcha yeye ni kama vile alikuwa Chanya na radi ilikuwa hasi na sheria ya asili inaelezea kwamba ikitokea nguvu mbili hazifanani basi zitavutana na ikitokea hizo nguvu mbili moja ni dhaifu basi itamezwa na ile iliokuwa na nguvu.
Hivyo ant Matter ilikuwa ni dhiafu na radi ilikuwa na nguvu hivyo moja kwa moja nishati ile ilifunikwa.
Radi ile ilikuwa ni endelevu , pengine ni aina ya radi ambayo binadamu wa kawaida hajawahi kuishuhudia na kadri ilivyokua ikiendelea kushambulia upande wa Roma alikuwa akipitia steji mbili muhimu sana ambayo ya kwanza ni Soul Evolution(Kukua kwa nafsi) na pili ni Soul Cleansing(Usafi wa nafsi) ambazo steji hizi zote mbili ukiziunganisha majini wanaita Ubatizo wa moto wa mbingu(heavenly fire baptism) ama ubatizo wa radi katika lugha ya kibinadamu.
Ukumbuke majini hawaiti radi kama radi bali kwao radi ni sawa na moto wa mbingu au moto wa Mungu na wao wanaamini kwamba moto wa mbingu ndio huwatengeneza au ni kama chanzo cha kukua kwao.
Katika hatua za juu kabisa za uwezo wao au unaweza kusema levo ambazo majini wa viwango vya juu sana ambao walipitia ni katika hatua ya ubatizo wa moto wa mbingu.
Lakini sasa tokea enzi zile hakuna jini ambaye ashafanikisha kupitia hatua ya ubatizo wa moto.
Roma hakupata faida ya kusafishwa kwa nafsi au kukua kwa nafsi pekee bali pia alipata usafisho wa mwili , yaani ni kama vile mwili wake uliondolewa kitu ambacho kilikuwa kikimsumbua kwa muda mrefu na kumfanya kuzidi kuwa imara.
“Hatimae imetokea… huyu mtoto amekwisha kupata ufunuo wa radi ya mapigo mengi na namna unavyotokea , hii radi ya kimungu haina tena madhara kwake zaidi ya kuwa ndugu aisee sijatarajia baada ya maisha yangu marefu kushuhudia kitu cha namna hii”Aliongea Aoiline mwenyewe .
Huku hisia mbalimbali zikipita katika moyo wake , ilionekana kwamba ukiachana na Roma kuweza kujua siri ambayo ipo katika adhabu ya mapigo tisini na tisa ya radi lakini pia alikuwa amefahamu siri iliopo nyuma ya mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi.
Kwa mtu wa kawaida anaweza kusema kwanini majini waogope radi ilihali Roma anaweza kuwaambia siri ya radi hizo lakini ukweli ni kwamba ili waweze kufanikisha hilo lazima wakaanze moja katika hatua za uvunaji wa nishati za anga kwa kutumia mbinu ya andiko la urejehso.
Roma aliweza kudhibiti siri ya radi hizo kutokana na kwamba alikuwa amepitia njia ndefu ya mafunzo hayo ambayo ndio kama msingi na hii ilimpelekea kuwa na uwezo wa kutengeneza moto adimu sana ambayo una elementi zote za kutengeneza radi , mfano wa moto wa bluu , maji ya kiroho na moto mweupe.
Siraha za namna hio ni majini wachache sana ambao wanaweza kutengeneza au hakuna kabisa ndio maana tokea mwanzo miliki zote za majini watu zilikuwa zikimuwekea Roma njama ya kutaka kumpa siri hio.
Ikumbukwe kwamba katika hatua za andiko la urejesho mbinu ya hatari zaidi ni ile ya kufa na kufufufuka , yaani steji ya kifo na uhai.
Kwahio basi mpaka muda huo Roma aliweza kupitia hatua muhimu ambayo ya kwanza ni mapigo tisa ya radi ambayo steji hii alitumia uwezo wa mwii wake kujiponyesha kwa haraka na andiko la urejesho , hatua ya pili ya dhiki ni mapigo tisini na tisa ambayo aliyapata katika mnara huo wakati wa kutoka kwa msaada wa Cauldron na hatua ya tatu ni mara baada ya kumshuhudia Anjiu akipitia levo ya mapigo ya radi alikuja kufahamu siri ya kutengeneza radi ya zanbarau na hatua nyingine ni hio ya sasa ya kupitia mapigo mia tisa tisini na tisa lakini awamu hio hakuumia zaidi ya kwamba aliidhibiti ile radi kwa kujifananisha nayo ili sheria ya asili(law of nature) ifanye kazi.
Wakati Roma akifurahia namna ambavyo radi ya mapigo mengi ilivyokuwa ikimzunguka na kuendelea kunyonya nishati yake Lekcha yeye alikuwa katika kilio cha kusaga meno.
Ilikuwa ni ngumu sana kwake kujiokoa katika hali ambayo alikuwepo , iapokuwa radi ya Zambarau ilikuwa na uwezo wa kuharibu mwili wake lakini ukubwa wa nguvu ya ant matter iliuwa na uwezo wa kumrejesha lakini awamu hio radi ya rangi ya fedha haikuwa mchezo kabisa , sio tu kuharibu mwili lakini pia ilianza kuharibu na nafsi yake.
Haikujalisha nishati ya Ant Matter ilikuwa na nguvu namna gani lakini hakuweza kulinda kitu muhimu sana ambacho ni roho au nafsi , ilimaanisha kwamba Lekcha alianza kukosa ufahamu wa kujiendesha na kuwa kichaa na kadri sekunde zilivyokuwa zikisonga angepotea moja kwa moja.
Alijitahidi kukusanya kiwango kikubwa cha nishati kulinda roho yake lakini hakufua dafu kwani nishati yake ilikuwa na kikomo lakini kwa mapigo elfu moja ya radi hakukuwa na kikomo cha ukubwa wake.
Aliweza kuona kabisa nguvu ya radi hio ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi kuvumilia tena na kifo kilikuwa kikimsogelea kwa kasi ya 5G.
BOOM
Awamu ya pili kubwa zaidi ya pigo la radi ilishuka , haikueleweka pigo moja lina uzito wa nguvu kiasi gani kukamilisha hesabu ya 999 lakini ni dhahiri mapigo yasingekuwa moja moja.
Roma alikuwa katika hali ya furaha ya ubatizo wa radi hio na mabadiliko ya kiakili aliokuwa akipitia ilimfanya kumpotezea kabisa Lekcha aliekuwa akilia kama mtoto.
Ajabu ni kwamba ni nje ya mahesabu ambayo Roma alitarajia kwani alipitia mapigo matatu tu ambapo kila pigo moja lilidumu kwa dakika kumi na tano.
Haikueleweka ni kwa namna gani majini waliweza kutoka na hesabu ya mapigo tisini na tisa katika awamu tatu lakini kutokana na ukubwa wa radi hio na nguvu yake Roma aliamini inawezekana awamu tatu kukamilisha mapigo yote mia tisa tisini na tisa.
Mara baada ya dakika kumi na tano kumalizika za pigo la mwisho hali ya hewa ilirudi katika hali yake ya kawaida kwa kasi sana.
Na hata ule mwanga wa rangi ya silver ambao ulidumu ndani ya mnara huo kwa dakika arobaini na tano ulirudi katika hali ya kawaida.
Hali ya hewa ndani ya mnara huo ilikuwa ni harufu flani hivi kama ya baruti iliochanganyika na kuungua kwa mimea na kuyeyuka kwa baadhi ya dhana zilizopo ndani humo.
Roma alivuta pumzi nzito na kisha alishuka taratibu na kukanyaga floor hio ambayo ilikuwa imepata moto , chungu cha machafuko kilimzhuguka Roma kwa namna flani hivi ya kumlaki kikimuelezea kwamba licha ya kumkinga na radi lakini pia kimefaidika .
Roma palepale aliamua kuficha Shoka lake la kimaajabu na chungu kile kwani hakuwa na uhitaji navyo kwa muda huo.
Mwili wake ulikuwa ukitoa harufu flani hivi isiokuwa ikielezeka lakini kwa mbali ni kama vile kuna cheche za shoti zilizokuwa zikionekana katika mwili wake uliokuwa umetuna kwa mazoezi.
Hakuwa na nguo hata moja wakati huo alikuwa uchi wa mnyama na kwanzia vidoleni mpaka chini alikuwa akitoa shoti za umeme na ilikuwa ni kama vile mwili wake unapo kwani shoti zile zilikuwa zikififia.
Roma alishangazwa na nguvu ya radi hio lakini alijua kabisa hapo sio mwisho , inasemekana majini wa enzi hizo walipitia mpaka hatua ya mwisho kabisa ya mapigo 9999 , sasa alijiuliza kama ni hivyo waliwezaje kupita hatua hio au na wao walikuwa kama yeye tu walijifananisha na radi hio na matokeo yake radi ilifuata kanuni ya asili.
Roma mara baada ya kuwaza kwa muda hatimae sasa akili yake iliwaza kuna Lekcha na aligeuka palepale na alipoangalia sehemu Lekcha alipo aliona vijicheche kwa mbali ambavyo vilikuwa vikipotelea.
Kama ilivyo kwa Roma mwili wake kupoa upande wa Lekcha alikuwa amerudi kawaida na mwili wake ulikuwa umepoa kabisa kwa kupoteza nishati yote ya Ant-Matter.
Ilionekana radi yote ilikuwa imekula nishati yake na kumbakisha mweupe na kuwa kama binadamu wa kawaida tu.
“Hukutakiwa kuwa na kiburi…. Vinginevyo ungeweza kupata nafasi ya pili , isitoshe mwili wako unaonekana kutokuwa wa kawaida”
Roma aliongea huku akitembea kumsogelea Lekcha aliekuwa akitetemeka kama vile mgonjwa wa Malaria kali.
Lekcha aliepiga goti alijikuta akivuta pumzi nyingi na kisha kwa unyonge aliinua kichwa chake , alikuwa amefubaa kama karatasi lakini hata hivyo hakupoteza ile hali ya ukejeli kwenye uso wake , ilikuwa ni kama vile hakujali tena kifo.
“Acha kunionyesha hio tabia yako ya kujiona unajua kila kitu , hivi unajua kinachonifanya kukuchikia zaidi ni nini , kinachonifanya ni kuchukie sana ni tabia yako ya majigambo”
“Inaonekana una chuki binafsi zidi yangu lakini niwe tu mkweli sijawahi kukuchukulia kama tishio kwangu lakini hata hivyo umenishangaza , sijui kuhusu mengine lakini kitu ninachojua ni kwamba sijali namna yoyote ile unavyonifikiria”
“Hahahaha… , kwaio ndio unajigamba , naona mwishoni nimekushindwa kama alivyoshindwa yule mjinga Yan Buwen na mjinga wake Denisi , mpaka mwishoni inaonekana hakuna ambaye anakuweza na yamkini hapo mwenyewe unajihisi sio wa kawaida lakini Roma ngoja nikuambie kitu , mimi Lekcha a.k.a Joseph Bikindi hujanishawishi juu ya uwezo wako wala siwezi kukubali, hata kama nikifa siwezi kukuruhusu ujione shujaa au kukufanya ufikirie umeniweza .. kitu pekee ambacho kimenifanya kuwa katika hali ya kushindwa ni bahati basi , najiuliza kwanini sikuwa na bahati ya kupata fursa ya kukutana na master ambaye ni mzuri kwangu , kwanini niligeuzwa na kuwa mtumwa , kwanini kuna watu nyuma yako ambao wapo tayari kukusaidia ,, Hades umefanikiwa hayo yote kwasababu bahati ilikuangukia na ukawa upande mzuri , tokea ulivyozaliwa Mungu alishakuandikia utafanikiwa kwa kutuchukulia sisi kama ngazi , lakini hebu jiangalie sasa hivi unavyojiona mwenyewe, sio juhudi zako pekee zilizokufikisha hapo mwanaharamu wewe”
Lekcha alitumia kadri ya uwezo wake wote kuongea kwa sauti lakini hata hivyo sauti yake ilionekana kunyongea sekunde hadi sekunde.
Roma aliishia kucheka kivivu kama vile ashajichokea hata kumgusa Lekcha lakini hata hivyo hali flani ilionekana katika macho yake mara moja.
“Huu ni muda wa wewe kuacha kuwa mpumbavu , najua haina maana kukuelewesha tena lakini nikuambie tu wewe ni moja kati ya maadui zangu ambae umechukua muda mrefu , ukweli sio kwamba nakuchukia kihiivyo , kabla roho yako haijauacha mwili wako nataka nikuambie kitu ,, pengine ulichosema ni kweli kwamba ni neema za Mugnu zilizonifikisha leo hii lakini unaweza kushangaa kwamba wakati wewe ukiwa mwanafunzi mzuri na kinara shuleni kwenu, unaependwa na walimu kwangu mimi sikuwa hata na uhuru wa kuitwa chokoraa .. hivi unadhani umeshindwa na mtu ambae alikuwa na kila kitu , ngoja nikuambie umeshindwa na mtu ambaye hakuwahi hata kujua alikuwa na familia wala ni wapi alizaliwa , mtu ambaye alitegemea nyama ya binadamu kuishi , mtu ambaye alikuwa ni sehemu ya majaribio ya kisayansi ambayo maumivu yake sio ya kawaida , kwasababu tu ya kupoteza ndugu na kuwa kilema ndio useme Mungu amenipendelea , ninachomshukuru Mungu leo hii kunipa nafasi ya kuendelea kuishi mpaka leo hii licha ya changaoto zote nilizopita na hii ndio tofauti yako na yangu , unaamini Mungu kanipendelea lakini mimi namshukuru kwa kunipa nafasi ya kuishi”
Machozi ndio dalili pekee ya uhai iliomtoka Lekcha na mara baada ya kuvuta pumzi ndefu palepale nywele zake zilianza kubadilika rangi na kuwa nyeupe na hatimae rangi ya kijivu na ngozi yake ikakauka na kujikunja na hatimae kukosa sifa ya ubinadamu na uhai wake ulionekana ndio unafikia mwisho taratibbu taratibu.
Katika uso wake huo ambao ulikuwa ni kama udongo hali ya furaha, huzuni na makasiriko iliweza kuonekana na alionekana kuwa wa tofauti sana kuliko mwanzo , hakuna neno ambalo liliweza kutoka katika kinywa chake kana kwamba alikuwa akisubiria wakati wake wa mwisho.
Roma aliendelea kumwangalia Lekcha jinsi alivyokuwa akibadilika rataribu kadri nishati ya ant-matter ilivyokuwa ikipotea hewani na palepale alivuta pakiti ya sigara kutoka katika hifadhi yake ya anga na kuchomoa moja.
“Vipi nikupatie moja?”Aliuliza Roma, ndio kitu pekee ambacho alikuwa na uwezo wa kumpatia Lekcha muda huo katika hatua zake za mwisho.
“Pengine hujawahi kuvuta sigara ghali kama hii maisha yako yote”Aliongea Roma na kisha alichuchumaa na kumshikisha Lekcha ile sigara na alisita kidogo na hatimae Lekcha alionekana kuishikilia japo kwa taabu na kisha akaitumbukiza katika mdomo wake, mara baada ya Roma kuiwasha Lekcha alivuta moshi kidogo tu na kushikwa na kikohozi kilichomfanya sifara kudondoka.
“Naona unanikejeli , nimepokea hii sigara kwasababu inaonekana ya thamani sana na ingesikitisha nikifa kabla ya kuonja moshi wake … usijione wewe ndio mtu pekee ambaye umepitia mengi na una uzoefu wa kuishi maisha ya kifahari”
Roma alivuta kwanza moshi na kuupuliza hewani na kisha alitoa tabasamu huku akiona kiwango cha mwisho mwisho cha nishati ya Ant-Matter kikipotea katika mwili wa Lekcha.
“Kama ningekuwa mtu mkarimu pengine ningekupatia bia ya ya thamani kubwa lakini nimekupa sigara kwani ndio kitu pekee cha thamani ndogo nilichokuwa nacho”Aliongea Roma na kumfanya Lekcha kutoa tabasamu la dhati lisilo na unafiki kwa mara ya kwanza mbele ya Roma.
Muda huo ndio aliweza kufika Aoiline kwani alijitenga mbali sana na eneo hilo na mara baada ya kutua alimwangalia Roma kwa namna ya kushangazwa nae.
Alimwangalia namna ambavyo Roma alikuwa akiwasha sigara moja baada ya nyingine huku akiangalia namna ambavyo Lekcha anavyochukuliwa na Israeli mtoa roho.
Roma baada ya kuona hakuna tumaini lolote kwa Lekcha alisimama na kisha alimsogelea Aoline na ni muda uleule aliruhusu radi kumpiga Lekcha na akageuka kuwa majivu na huo ndio ukawa mwisho wake.
“Inaonekana angalau mwishoni chuki yake zidi yako imempotea”Aliongea Aoiline.
“Labda , kumalizana nae ni kama kuagana na kipindi kingine cha maisha yangu , Ni nani ajuaye kinachonisubiri mbele”
Aliongea Roma huku akitoa tabasamu hafifu kana kwamba ashaona nini kinamngojea huko duniani.
ITAENDELEA.
Sawa 768
 
[emoji1635][emoji1635][emoji3590]
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI :SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 773.
Afande Kweka na familia nzima kwa ujumla ilikuwa katika hali ya furaha , hata Raisi Senga ambaye alikuwa ametulia muda wote alijikuta akikunja viganja vya mikono kwa namna ya kufurahi.
Hakukuwa na shaka kwamba wote walikuwa na wasiwasi mara baada ya kupotea kwa Roma.
Ukweli ni kwamba kwa kipindi chote hicho raisi Senga na Afande Kweka walikuwa wakitembelewa na watu wengi sana na wengi wao walikuwa ni viongozi wa juu wa nchi zilizoendelea ikiwemo China , Japani , India , Ufaransa na Marekani na wote hao walikuwa wakiulizia habari za Roma.
Katika wakati wa hatari kama huo binadamu wote matumaini yao waliyaweka kwa Roma kama muokozi wao.
Hata familia hio kukusanyika ndani ya eneo hilo ilikuwa ni katika kufanya ibada maalumu ya kumuombea Roma.
Raisi Senga kipindi cha nyuma alikuwa mzito sana pale linapokuja swala la Roma lakini katika kipindi cha muda mfupi alikuwa ameamka sana.
Pengine ni kutokana na kukosa mtoto wa kiume kwani katika uzao wake mrithi wake ambaye alikuwa akimuona kwa wakati huo ni Roma pekee kwani mke wake Damasi alikuwa ashapita katika wakati wa kuzaa tena.
Ashley licha ya kwamba alikuwa na akili na ni tegemezi lakini bado alikuwa ni mwanamke ambaye leo au kesho atataka kuanzisha familia yake na ukoo mwingine.
Roma moyo wake ulijisikia joto mara baada ya kuona namna ambavyo mama yake alikuwa akimngojea kwa mapenzi makubwa.
“Usilie mama yangu , nitakuelezea kila kitu , nipo sawa”Aliongea Roma akiwa na tabasamu , ilimchukua juhudi kumtuliza Blandina.
Sasa wote macho yao yalikuwa kwa Roma na ni wakati ambao waliweza kugundua kulikuwa na mwanamke mrembo wa kutisha alieambatana nae.
Ijapokuwa Aoiline alijitahidi kuuficha uzuri wake kwa kutumia nguvu za kijini lakini hakuacha kutamanisha kwa macho , ilikuwa ni ngumu kwa binadamu wa kawaida kutoa macho kwake.
Kwa bahati nzuri ni kwamba watu wote waliokuwa ndani ya eneo hilo sio wale wa kawaida , walikuwa ni watu walioelimika hivyo hawakumkodolea macho sana, hata hivyo ilikuwa ni kama imezoeleka kwani Roma alikuwa na wanawake warembo sana.
“Huyu dada ni…”
Blandina alimchukulia Aoiline kwa matamanio na kutokumkubali kwa wakati mmoja , aliotea pengine kupotea kwa Roma ni kutokana na kula bata na huyo mrembo.
Tabasamu la uchungu lilimvaa Roma na kwa haraka sana kusafisha hewa alimtambulisha Aoiline na kutokana na hali ilivyo Roma hakuona haja ya kuficha kama Aoiline sio binadamu bali ni jini ambaye alimsaidia sana kipindi cha mwisho alichopotea.
Pengine kwa familia za kawaida kama ungemtambulisha mwanamke kama huyo ni jini wangetimua nduki lakini Afande Kweka aliishi na Zenzhei mwanamke jini kwa muda mrefu sana na ilikuwa ni kama washaanza kuchukulia viumbe hao ni wa kawaida.
Bila shaka haikuwa kwa familia nyingine , ilikuwa kwa familia ya Roma tu ambayo sio ya kawaida ndio walioona mambo ni ya kawaida.
Afande Kweka alishangazwa mno mara baada ya kusikia huyo mrembo ni jini jamii ya mbweha wa mikia tisa ambaye ameishi umri wa miaka elfu hamsini , kutokana na urembo wake ilikuwa ngumu kwake kuamini.
Blandina hatimae lilimshuka mara baada ya kugundua Aoiline sio mpenzi wa Roma , vinginevyo hakujua ni kwa namna gani angeongea na mke mwana yaani Edna.
Aoiline ni kama hakuwa na ‘interest’ na maongezi ya binadamu na alikuwa bize kushika kitabu hiki na kile pamoja na vifaa vya kieletroniki kwa namna ya kuvishangaa.
Mara baada ya Roma kuelezea kila kitu katika safari yake ya ajabu hatimae kila mmoja alivuta pumzi lakini mtu kama Ashley na Damasi walikuwa katika hali ya mshangao mkubwa , hakuna ambaye alikuwa akiamini kulikuwa na ulimwengu mwingine lakini kwa namna moja simulizi ya Roma ni kama ilikuwa ikiwaambia kwamba kulikuwa na mbinguni au Akhera sehemu ambayo Mungu huishi hivyo kiimani Damasi aliimarika zaidi.
Upande wa Ashley yeye alikuwa ni mwanasayansi ,ijapokuwa hakushangaa sana lakini ni moja ya binadamu ambao wamejazwa na shauku ya kuthibitisha vitu kisayansi.
“Roma je Edna na wengine washafahamu umerudi?”Aliuliza Blandina.
“Hapana , nimekuja nyumbani kwanza mara baada ya kutokea ulimwengu wa majini watu”
Jibu lake lilimfanya Blandina kuwa na furaha na ile hali ya huzuni ilikuwa ishampotea kabisa , kwa Blandina Roma alikuwa ni mtoto tu haikujalisha anapitia mapigo mangapi ya radi au ni majukumu ya namna gani alikuwa nayo.
“Nilijua tu mtoto wangu una akili , nani angejua ungeniwazia mimi wa kwanza na kuja kunitembelea”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kuona aibu kidogo maana mama yake alikuwa akimchukulia kama Lanlan na kitendo kile kilimfanya Aoiiline kuishia kucheka
Baada ya maongezi kidogo ya kutaniana ya hapa na pale Afande Kweka alichukua nafasi yake kuongea.
“Roma unapaswa kuwaambia umerudi mapema , maana kuna kitu kimetokea huko kisiwani wakati ukiwa haupo”
“Mhmh , inawezekana vipi , niliacha majini watatu wenye utaaalamu wajuu kulinda , sidhani kuna binadamu ambaye ana uwezo wa kuwashinda”Aliongea Roma akiwa amekunja sura.
“Hakuna alieumia , Princess Clark alichukuliwa na jeshi la umoja wa Ulaya na Marekani …”Aliongea Blandina na kuanza kuelezea kile kilichotokea.
Roma muonekano wake ulibadilika palepale , hakuwa akijali chochote kuhusu maswala ya Safina lakini alikasirika mara baada ya kumchukua Clark kinguvu licha ya kwamba walikuwa wakijua alikuwa ni mwanamke wake.
“Ashley sidhani kwa akili zako umeachwa hivi hivi tu , una projekti gani kwa sasa?”Aliuliza Roma.
Ukweli ni kwamba ni kama vile ameshikwa na hatia kwani alikuwa ni mdogo wake lakini walikuwa wakikaa pamoja mara chache sana , lakini hakupaswa kulaumiwa kwani Ashley alikuwa ni mtu bize hususani tokea atoke kwenye mikono ya Profesa Clark na kujitegemea katika maswala ya utafiti.
“Ashley kwa sasa yupo chini ya ya serikali katika utafiti wa maswala ya tiba”Aliongea Damasi.
“Unaweza kuambatana na mimi kuelekea kisiwani , Mwalimu wako amefungua maabara kule inaweza kukusaidia zaidi kama mtakuwa karibu”Alipendekeza Roma.
“Asante Bro lakini kwasasa nimeamua kujitegemea , ndio namna pekee ya kuonekana kuliko kuendelea kuwa chini ya kivuli cha Profesa”
“Mjukuu wangu yupo sahihi ni wakati wake wa kuifikiria Tanzania kwanza”
“Mzee unavyoongea ni kama vile mimi siifikirii Tanzania , anyway naona huku mmebarikiwa joto wakati nchi nyingi zikitaabika”
“Ni kweli lakini haimaanishi kwamba hatupo kwenye hofu , tafiti zinaonyesha mpaka miezi saba kupita kuna uwezekano na Afrika kuanza kuganda , sisi ni tofauti na wazungu na watu wa Asia kama hili likitokea inamaanisha tutaathirika zaidi kwani miili yetu haiendani na baridi kali”Aliongea Raisi Senga kwa mara ya kwanza na Roma aliishia kutingisha kichwa.
Wazungu wao wanasifika katika kuhimili baridi na miili yao imeumbwa kwa staili hio lakini upande wa Afrika wenyewe uwezo wao ni kustahimili joto, ndio maana mazingira ya uzunguni sio ya baridi sana wala ya joto sana hii ilimaanisha joto hata likishuka katika nyuzi sifuri tu Waafrika wengi wangepoteza maisha.
Maongezi yaliendelea kwa muda mfupi sana kabla ya Roma kuaga, maana alikuwa na hamu ya kuona familia yake na mtoto wake.
Wakati akitaka kutoka Afande Kweka alimsimamisha na kisha akamshika beganin.
“Mtoto kinachoendelea sio swala la utaifa bali ni swala la maisha ya binadamu , kadri nguvu zako zinavyokuwa kubwa ndo wajibu wako unavyokuwa mkubwa na kwasababu ya hili hakuna ambaye atakulazimisha kubeba majukumu yote , kama utajikuta upo njia panda , usiathiriwe na maoni ya watu na wewe fuata moyo wako kufanya maamuzi, hakikisha tu hujutii kwa lolote lile”Aliongea Afande Kweka.
Roma alijikuta akikaa kimya kwa dakika kadhaa akifikiria maneno yake na mwishowe alitingisha kichwa chake akionyesha kukubali.
Blandina aliishia kumpungia mtoto wake wa pekee kana kwamba alishaelewa kinachoendelea katika majukumu anayoenda kukabiliana nayo na aliishia kuwaangalia mpaka walipopotelea katika upepo wa macho yake na kuishia kufuta machozi.
*****
Katika eneo la visiwa vya wafu joto lilikuwa ni nyuzi sifuri kwa visiwa vyote na barafu ilikuwa imeifunika bahari lakini upande wa visiwani theluji ilikuwa kidogo sana.
Lakini hata hivyo miti mingi na mimea ilikuwa imekwisha kukauka tayari na kufanya kisiwa hicho kuonekana kama ardhi isiokuwa na kitu.
Upande wa wana visiwa walikuwa ndani ya nyumba zao na uzuri ni kwamba nyumba zao zilikuwa zimejengwa kwa ajili ya kutunza joto kwa kuchoma kuni na kuwasha AC.
Na bahati nzuri ni kwamba chakula walikuwa nacho kingi kama cha akiba hivyo hawakuwa na wasiwasi na maswala ya chakula.
Bi Wema , Sui na Qiang Xi wote walikuwa wamehamia katika makazi ya Roma ya ngome kwasababu kulikuwa na jenereta kubwa ambalo lilitosha kuzalisha kiwango kukubwa cha joto lakini pia ukubwa wa ngome hio uliwafanya kuishi bila shida yoyote.
Ijapokuwa Tanzania kulikuwa na joto lakinni waliona ni kheri kuendelea kuishi ndani ya kisiwa hicho wakimsubiri Roma kwani waliona ndio namna pekee wanaweza kuwa salama zaidi.
Sasa wakati huo wanawake hao walikuwa wamekaa katika meza ya chakula ikiwa ni nyakati za usiku , ijapokuwa chakula kilichokuwa kimeandaliwa hakikuwa cha kifahari kama ilivyokuwa kawaida lakini bado kilikuwa cha kutamanisha lakini kwa bahati mbaya wote walionekana kukosa hamu ya kula hivyo kumpa uwanja Lanlan wa kushughulika na share zao.
Lanlan alikuwa amekaa katikati na pembeni yake alikuwepo Edna ambaye mara kwa mara alikuwa akimfuta midomo kwa kutumia kitambaa na kisha kumlisha mboga za majini licha ya kwamba alikuwa akikataa, uwepo wa mtoto ndani ya familia hio ilifanya hali iwe ni ya amani.
“Edna dunia ndio inafika mwisho na Hubby hajulikani alipo , kwanini huonyeshi wasiwasi wa aina yoyote ile , hata Da’Neema ameshindwa kuvumilia na kinachoendelea na kwenda kufanya tahajudi kwenye basement , lakini wewe upo na amani kabisa na unamlisha Lanlan”Aliongea Mage ambaye uvumilivu ulimshinda kwani ni Edna pekee ambaye ni kama vile inachoendelea huko Duniani hakikuwa kikimuhusu.
Edna alimwangalia Mage na kutoa tabasamu hafifu na kisha hakutoa jibu na kuendelea kumlisha Lanlan mboga za majini.
“Miss Edna anaweza kuonekana hana wasiwasi lakini yupo kama wengine tu ni kwamba tu haonyeshi waziwazi kile anachojisikia , ndivyo alivyo”Aliongea Bi Wema akijaribu kumtetea.
Maneno yake yalifanya wengine wote kucheka , kutokana na kukaa na Edna kwa kipindi kirefu ni kama walijua hakuwa hivyo kwa makusudi bali ndio tabia yake.
Walimheshimu kwani kwa kipindi chote ambacho Roma hakuwepo ni kama ndio aliekuwa kiongozi.
“Mommy Where is sister Lati?”Lanlan aliuliza akimaanisha yu wapi jini Latina , Lanlan hakuwa akiogopa kabisa majini hao , tokea siku wampeleke Uingereza kucheza na Ujerumani alikuwa akiwaita dada licha ya kwamba walikuwa na umri zaidi ya miaka elfu mbili.
“Atakuwa hapa kisiwani , kwanini unauliza?”Aliongea Edna.
“Da’Lati ameniahidi atanipeleka kwao nikacheze lakini ni siku nyingi tu hatimizi ahadi”Aliongea.
“Anatakiwa kuwepo hapa kisiwani kwa ajili ya kulinda kila mmoja , hawezi kuondoka kwenda nyumbani na wewe kwa ajili ya kucheza , unapaswa usubiri mpaka baba yako arudi sawa”Aliongea Edna huku akichezea kichwa chake.
“When is Daddy coming back then?”Aliuliza akimaanisha ni lini sasa baba anarudi.
“Baba yako….”Edna alionekana akifikiria lakini palepale macho yake yalichanua.
“Baba yako naona tayari amekwisha rudi”
Mara baada ya kauli hio watu wawili walitokeza nje ya Ngome hio na kuanza kutembea kuelekea upande wa mlango mkubwa
Wanawake ndani ya ngome hio waliweza kuhisi kitu na wote walilirupukwa na furaha.
Muda uleule wale majini pepo watatu waliweza kutokea katika upande mmoja , ilionekana hata wao waliweza kuhisi ujio wao.
Kutokea kwa Roma kulisababisha kila moja kupatwa na hali ya kihisia , mara baada ya kuushinda mshituko wao wa mwanzo wote walionekana kushangilia kwa furaha , warembo hao walishindwa kuzuia machozi yao na wasiwasi wao uliokuwa umewashika kwa wiki kadhaa zilizopita.
Roma mara baada ya kuona machozi yao na wasiwasi wao alijikuta akishikwa na hatia na alifosi tabasamu.
Licha ya kwamba alikuwa na uwezo wa juu sana wa nishati ya mbingu na ardhi lakini jasho liliweza kuonekana katika paji la uso wake.
“Nimerudi , naomba mnisamehe nilipatwa na ajali na kuwasababishia mawazo”Aliongea Roma akiwa katika hali ya utulivu na wote waliishia kutingisha vichwa.
Roma aliishia kutoa tabasamu huku akimkagua mmmoja baada ya mwingine , alishindwa kuzuia aibu yake kwani kutoweka kwake ni kama vile mwanaume aliekimbia majukumu.
Mara baada ya kukutanisha macho yake na Edna kwa dakika kadhaa aliweza kugundua ndio mwanamke pekee ndani ya makazi yake ambaye alikuwa katika hali ya utulivu , ilikuwa ni kama vile alijua Roma angerudi mapema tu.
Pengine alipaswa kufurahi kutokana na utulivu wa Edna lakini ajabu ni kwamba alijikuta yeye ndio anaona wasiwasi zaidi.
“Daddy where did you run off to play , did you bring a present for me?”Aliuliza Lanlan akimaanisha baba yake alikimbilia wapi kucheza na je amemletea zawadi.
Joto lilimshika Roma kwenye moyo wake na alijikuta akiinama na kumbeba juu juu na kumbusu binti yake shavuni.
Tokea siku aitwe baba fikra zake zilikuwa zimebadilika mno , wakati alipokuwa katika ulimwengu wa jicho la anga alimuwazia mno binti yake , uhusiano wa damu kati ya mtoto na baba alikuja kugundua sio wa kawaida kabisa.
“Kabla ya kuomba zawadi napaswa kumuuliza mama yako kama ulikuwa mtoto mtiifu”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kumwangalia Edna kwa macho ya kubembeleza asimseme vibaya mbele ya baba yake
Muonekano wake uliwafurahisha watu wazima waliokuwa wakimwangalia na hali ilionekana kubadilika kutokana na Lanlan.
Wote walijikuta wakijituliza na kumsogelea Roma na kumuuliza kile kilichokuwa kimetokea.
Bila shaka walikuwa wamekwisha kumuona Aoiline tokea muda mrefu , wakati macho yao yanatua kwa mrembo huyo ambaye amevalia mavazi ya kitamaduni ilikuwa nguvu kwao kujituliza , alikuwa mrembo kama Edna lakini aliekuwa akitamanisha zaidi.
Aoiline hakujali kabisa namna wanavyomwangalia na alikuwa bize kushangaa mapambo ndani ya ngome hio , macho yake yalionyesha furaha mara baada ya macho yake kukutanisha na runinga kubwa mbele yake pamoja na mfumo wa kisasa wa mziki.
Roma aliwaambia kila mmoja kutulia kwenye kiti chake ili aweze kuwaelezea.
Lakini kabla ya hayo upande wa Latina , Winu na Yunu walikuwa wamesimama nje ya ngome hio bila ya kuingia ndani , ilionekana ni kama vile walikuwa kwenye mshituko na mara baada ya kupungua ndio waliingia ndani kwa tahadhari mno.
Majini jamii ya Mbweha walikuwa na uwezo wa kipekee wa kuweza kutambuana wao kwa wao , kuweka katika lugha nyepesi ni kwamba wanao uwezo wa kunusa harufu kama mbwa.
Ijapokuwa hawajawahi kukutana na Aoiline lakini waliweza kumtambua kutokana na harufu yake na uwezo wake mkubwa wa nguvu za kijini.
Lakini sasa jambo hilo limetokea ghafla sana kwao mpaka wanashindwa kuamini.
Majini hao watatu waliishia kusimama kwenye Korido huku macho yao yakimwangalia Aoiline ambae alikuwa bize kuangalia mapambo ya nyumba kwa mbali , hawakuthubutu kupiga hatua na waliishia kushikilia magauni yao kwa nguvu huku wakitetemeka na macho yao yakianza kubadilika rangi .
Kutokana na muonekano wao Roma aliona aachane kwanza na maswala yake na aliamua kumgeukia Aoiline.
“Hey , Aoiline si umesema unataka kukutana na wana ukoo wenzako , hao hapo ndio wana ukoo wa mbweha kutoka Braki”
Mara baada ya Latina na Wenzake kumsikia Roma akitaja jina la Aoiline miguu yao ilikosa nguvu na wote walipiga magoti chini.
“Mhenga..!!!!”(Haha I mean Ancestor)
Mabadiliko ya hali yaliwafanya waliokuwa ndani ya eneo hilo kushangaa , hawakuaini mwanamke huyo mrembo hivyo ni mtangulizi wa majini jamii ya Mbweha.
Moja kwa moja walimwangalia Roma kwa macho ya shauku na ilimfanya Roma aelezee kile ilichotokea katika ulimwengu wa majini pepo
Muda huo ndio Aoiline alirudi katika hali ya kawaida na kuwageukia vitukuu wake.
“Mnaweza kusimama , nilikuwa nikishangaa vitu vya hapa ndani , vimekaa kimaajabu ajabu na kuishia kupotezea vitu vingine , mnaitwa nani?”Aliongea Aoiline.
Majiini hao watatu walisimama kwa umakini mkubwa na kisha wakajitambulisha.
Majini hao watatu kwa mara ya kwanza walionyesha hali ya kuogopa na kuwafanya binadamu waliokuwa wakiwaangalia kuona kama vile wamekutana na mtu wa heshima kubwa.
Muda uleule katika hali ya kutambuana Aoiline ndie aliekuwa wa kwanza kubadilisha macho yake na yakawa ya kijani na wale watatu wengine wote walibadilisha macho yao na yakawa ya kijani lakini mng’ao wa macho yao haukuwa mkali kama wa Aoiline ikionyesha damu yake ilikuwa safi zaidi yao.
“Nimewaangusha sana kama kiongozi wa ukoo kwa zaidi ya miaka elfu hamsini lakini nimefurahi kuona mmeweza kurithi damu yetu , nina shukuru kwa kuona kile nilichokuwa nikiwazia hakijatokea”Aliongea
“Hapana hapana , wewe ndio mtangulizi wetu na utukufu wetu , kukua na kuanguka kwa ukoo wetu hakutegemeani na wewe pekee , tumekuwa tukiamini upo hai na kuanzia sasa tunakuhitaji utuongoze katika levo za juu”Aliongea na kumfanya Aoiline kutabasam.
“Msiniite Mhenga , kwani naonekana mzee?”
“Ah .. haana , hatujamaanisha hivyo”Majini hao warembo waliogopa kumkasirisha Aoiline.
Aoiline alikaa katika Sofa na kisha akamgeukia Roma.
“Dogo sina haraka sana kuongea na wana ukoo wenzangu , si una maswala muhimu ya kuongea , endelea”
Muda huo huo Neema na Magdalena pamoja na wanawakewengine waliokuwa wakivuna nishati za mbingu walitokea na kusalimiana nae na kisha kuketi kusubiri simulizi ya Roma huko alikotoka.
Roma alielezea kila kitu huku akiruka matukio ya XiaoXiao kadri awezavyo pamoja na wale mapepo na roho za giza kutoka ulimwengu wa jicho la anga na alielezea kwanini amechelewa kurudi, mwishonni aliulizia kilichompata Clark.
Ukilinganisha kati ya Clark na kushuka kwa joto la Dunia Roma alikuwa na wasiwasi na mpenzi wake zaidi.
“Hubby wakati ambao hukuwepo tumeweza kufanya uchunguzi na tumeweza kugundua Marekani na Muungano wa Ulaya wamejenga kambi kubwa ya kijeshi katika nyanda za juu za milima ya Ethiopia , joto ndani ya nchi hio lipo juu tofauti na maeneo yote ya dunia na halina watu wengi , lakini pia usafirishaji kuingia nchini huko ni rahisi , wanapanga kujenga safina ndani ya nchi hio na kisha kuipeleka majini , tunaamini Clark atakuwa huko.. alienda kwasababu walimtishia kuua binadamu ndo maana , vinginevyo angekuwa amekwisha kurudi ukilinganisha na uwezo wake”
“Safina ya Nuhu ? huo ni uongo wa kujifariji tu , kwa teknolojia iliopo haina maana kama miungu wanapanga kuua binadamu wote , hata Clark hawezi kushindana na miungu kwa teknolojia”
Alikuwa na uwezo wa kuhisia namna uungu wa Hades ndani yake ulivyoimarika , kama angetumia kanuni za anga angekuwa na uwezo wa kumshina hata jini Anjiu bila ya kutumia uwezo wa kijini.
Roma aliona kama hali itaendelea hivyo basi uwezo wake unaweza kufikia juu zaidi , pengine angefikia katika levo inayolingana na uwezo wake wakati huo wa mapigo mengi ya radi.
Hivyo moja kwa moja Roma aliamini kuna uwezekano wa Poseidon uwezo wake wa kutumia kanuni za anga kufika sawa na mapigo elfu tisa tisini na tisa ya radi.
Sasa kutokana na hisia hizo bado hakuwa na ile hali ya kujiamini kushindana na miungu hio ana kwa ana hata kama alikuwa tayarii ashapitia mapigo mengi ya radi.
Roma aliamini pale miungu kusema walikuwa na asilimia ishirini mpaka theratini ya uwezo wao , kipindi ambacho viumbe hao wanatua hapa duniani nguvu zao zilizima kutokana na kwamba hawakuwa na miili yao kamili lakini pia moyo wa Gaia haukuwa hai.
Unapaswa kuelewa katika sayari yao Moyo wa Gaia uliendelea kuwa hai na ilikuwa ni kama chanzo cha wao kuishi , yaani kama ilivyo hapa duniani kutegemea oksijeni na jua kuishi basi kwao mti Mama ambao kiini chake ni moyo wa Gaia ndio ilikuwa sehemu ya uhai wao na utimamu wao.

SEHEMU YA 774,
Mara baada ya kumsikia Roma kukosa kujiamini kupambana ana kwa ana na miungu walijikuta nyuso zao zikisawijika , ingawa walijua kinachoendelea kitaishia katika vita kati ya binadamu na miungu lakini hawakutarajia kama Roma hatokuwa na ujasiri wa kupambana nao wakati huo.
“Kwahio tunafanya nini , je tutaendelea kuangalia joto likishuka zaidi na zaidi?”Aliuliza Nasra katika hali ya wasiwasi.
“Tuachane na hili kwanza , ninapaswa kumrudisha Clark kwanza na aachane kupoteza muda kujenga hio safina , ni muhimu zaidi kwake kuwa hapa kwani usalama wake utakuwa mkubwa”
Warembo hao hawakuwa na pingamizi , hawakuthubutu kufanya maamuzi wakati Roma hakuwepo lakini sasa alisharudi na wangefuata kila maamuzi atakayo fanya.
Upande wa Aoiline hakutaka kuendelea kupoteza muda mbele ya Roma na alichukuana na majini wenzake na kisha walipotea kuelekea ulimwengu wa jangwa tenganifu.
Roma hakuwa na wasiwasi nini kitatokea mara baada ya urudi kwake katika ukoo wake , haikujalisha majini pepo jamii ya mashetani watalichukulia vipi swala hilo kwa kutowasaidia kurudisha wakuu wao lakini wasingemfanya chochote isitoshe Aoiline alitoka katika ulimwengu wa majini pepo kwa nguvu zake.
Mara baada ya kutafuta uelekeo wa kambi ya jeshi kunakojengwa hio Safina aliamua kuelekea huko akiwa peke yake.
Maeneo mengi ndani ya Ethiopia yalikuwa yakipatikana katika nyanda za juu zaidi ya mita elfu nne kutoka usawa wa bahari , kulikuwa na vyanzo vinne vya mito ikiwemo mto Atbarah.
North Atlantic Organisation(NATO) na jeshi la Urusi walichagua eneo hilo kujenga kambi ya kijeshi kutokana na sababu kuu mbili , mosi ukiachana na vyanzo vikubwa vya maji walikuwa na uwezo wa kutengeneza njia kutoka juu milimani kwenda upande wa baharini hivyo isingekuwa ngumu kuihamisha safina kutoka eneo la matengenezo.
Roma mara baada ya kufika katika nyanda za juu na kuangalia upande wa baharinni aliweza kuona meli nyingi za kivita zilizokuwa zimeegeshwa zikiwa zimewekewa mifumo ya kivita ya Aegis.
Nchi zote duniani ukiachana na taifa la China walikuwa wamefanya muungano wa pamoja , hivyo wanajeshi waliokuwwepo walikuwa ni wengi mno , yaani kwa jicho moja tu aliweza kugundua walikuwa ni zaidi ya wanajeshi milioni moja ndani ya eneo moja.
Roma alichunguza mazingira ya kambi hio kabla ya kushuka chini.
Karibu na mlimani kulikkuwa kumezungushiwa ukuta mkubwa mno wa chuma kigumu ambao urefu wake ulikuwa ni kama mita mia moja , geti tu lilikuwa na upana wa mita mia tatu.
Roma mara baada ya kujitokeza na kukanyaga juu ya ndege iliokuwa ikiendeshwa na mfumo wa nyuklia palepale wanajeshi wengi waliweza kumuona.
“Simama hapo hapo , wewe ni nani?”
Mwanajeshi alieonekana kama na miaka hamsini hivi alievalia sare za jeshi la maji aliongea akiwatangulia wanajeshi kadhaa wa ngozi nyeusi.
Roma hata hakuwajali na hakujisumbua kuongeleshana nao , mara baada ya kutembea mpaka mbele ya geti aliruka mita kama kumi na mbili hivi kwenda juu na kisha alirusha ngumi katikati lile geti.
“Thudd !!!
Mshindo ulikuwa mkubwa mno kiasi cha kutetemesha mlima na mawe makubwa yalianza kuporomoka kwenda chini na kuwashitua wanajeshi waliokuwa upande wa chini.
Roma akiwa na uso wa kutisha aliweza kutengeneza tobo kubwa tu kwenye geti lile , shimo ambalo lilikuwa na upana wa mita kumi , iliwezekana kutokana na kwamba alitumia nguvu za kijini.
Mara baada ya kutengeneza shimo lile aliingia ndani na kuwaacha wale wanajeshi wakiwa wamebung’aa wasiamini wanachoona.
Eneo ambalo lilikuwa limechimbwa katika mlima huo lilikuwa kubwa mno kiasi cha kumshangaza Roma
Ilikuwa ni kama vile wametengeneza ulimwengu mwingine kabisa ghafla tu, juu kabisa walionekana kubadilisha uelekeo wa maji kwa kutengeneza bwawa kubwa ambalo lilionekana lilifungwa mitambo ya kuzalisha umeme.
Upande wa juu kabisa kulikuwa kumejengwa kitu meli sio meli wala ndege sio ndege kitu chenye ukubwa wa meli ya kivita ya Marekani
Ilikuwa ni kama vile Roma anaangalia filamu za kisayansi , kwani kila kitu kilionekana katika umbo la kushangaza na kubwa licha ya kwamba unaweza kujua moja kwa moja pengine ni Manowari.
Kila kitu kilichokuwa kimetengenezwa hapo ndani ilikuwa ni kwa ajili ya kutengeneza malighafi za ujezi wa Safina.
Kulikuwa na watu wengi mno ambao kila mmoja alikuwa bize , kulikuwa na watafiti , wafanyakazi na wasimamizi.
Roma alishangazwa kwani ilionyesha binadamu alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchimba pamoja na kujenga , kwani usingeamini kama eneo hilo limechimbwa na kujengwa ndani ya siku chache tu , haikuwa projekti ndogo hata kidogo.kambi hio unaweza kuiita ya kimiujiza .
Kwasababu ya Roma kuingia kimabavu king’ola kilianza kupiga makelele katika eneo lote na taa mbalimbali za tahadhari kuwanza kuwaka.
“Tuu tuuuu… Attention !, Everyone! Attention! , Everyone An Intruder has breached the perimeter!!”
Wakati wafanyakazi wakishangaa upande wa wanajeshi na siraha zao walikimbia kutoka pande zote kumsogelea Roma.
Palepale aliweza kujua hali ilikuwa ngumu kuliko alivyokuwa ametarajia kwani sio binadamu pekee ambao walikuwa ndani ya hilo eneo.
Kundi kubwa la watu waliokuwa na ngozi kama ufinyanzi walisogea , walikuwa ni wanajeshi wa daraja la juu wa kabila la wanywa dam.
Nyuma yao kulikuwa na kundi lingine la watu ambao wote walikuwa na nguvu za ziada walikuwa ni Werewolves moja ya maadui wakubwa wa Vampire na walikuwa wamechomoza kucha zao zilizorefuka kwa ajili ya kumrarua Roma.
Kilichomshangaza zaidi hata wavatican na Wajihad walikuwepo hapo ndani na wanachama wa Bunge la Giza.
Tabasamu la kichekesho lilimvaa Roma mara baada ya kundi kubwa kumzunguka , ilikuwa ni hali iliompa ufahamu wa vitu vingi sana.
Binadamu waliweza kujenga na kuchimba eneo kubwa namna hio kutokana na msaada ya Werewolves , Blood race na watu wa nguvu za ziada.
Mfamo wachawi kutoka Uingereza chini ya Merlin Magic Association walikuwa na uwezo wa kutumia uchawi wao kupasua miamba hivyo kufanya zoezi la uchimbajij kuwa jepesi zaidi , upande wa Wolverines na Vampires walikuwa na uwezo wa kubeba vitu vizito ambavyo mashine na binadamu hawawezi kubeba.
Kati ya kundi lote wa kwanza kujitokeza mbele yake ni wanywa damu na mmoja kati yao aliweza kumtambua Roma.
Alikuwa ni mwanamke mrembo wa kuita aliefahamika kwa jina la Lilith ambaye Roma ashawahi kuonja mbususu yake.
“Everyone stop , it’s His Majesty Pluto”Aliongea Lilith kwa nguvu akimaanisha waache kwani ni Mfalme Pluto.
Lilith alikuwa katika hali ya mshangao mara baada ya kumuona Roma lakini akili ilimrudia na kutoa maagizo ya haraka
Muda huo huo ma’prince wa kundi la wanywa damu na wazee wa jamii ya Wolverines pamoja na majemadari wa jeshi walisogea
Kati yao Roma alikuwa akiwatambua kwani alikuwa ni Sargaras baba yake Lilith , Mkurugenzi wa FBI Baloteli na Fodesa Mkurugenzi wa DGSE na wote hao walimjua Roma.
Lakini walkuwa na wasiwasi mnno kwani hawakujua nia iliomleta Roma ndani ya hilo eneo.
Roma mara baada ya kuona wanajeshi hao ambao walikuwa katika madaraja tofauti tofauti alishindwa kujizuia kuwaza.
“Tch , nilikuwa nikidhania Jihad , Vatican na Bunge la Giza siku zote watakuwa maadui, kusingekuwa na wakati wa amani kati ya Wolverine na Vampires , lakini vile vile FBI wasingekubali kuonekana pamoja na KGB , inaonekana uhalisia umeniaminisha tofauti , haha..yaani wote nyie mnashirikiana?”Aliongea Roma huku akitabasamu kifedhuli.
Viongozi wa juu walikuwa washajua kuonekana kwa Roma ndani ya eneo hilo kwani wanamtambbua kama Hades sehemu ya miungu, sasa kutokana na ukinzani uliotokea kati ya miungu na binadamu walijikuta wakiwa na wasiwsi.
“Your Majesty Pluto it isn’t appropriate for you to show up here”Aliongea Sargaras akimaanisha sio vizuri kwa Roma kujitokeza hapo.
“Sargaras hivi jeraha lako ulilopata kipindi ile limekwisha kupona , lile jeraha sio rahisi kuponyeka kwa muda mfupi”Aliongea Roma.
“Bado sijapona kabisa lakini siwezi kuendelea kulala , kupotea kwa kizazi cha binadamu kunaweza kusababisha kupotea pia kwa wanywa damu”
“Mfalme Pluto ijapokuwa wewe ni sehemu ya miungu lakini bado ni binadamu , tafadhari usifanye mambo kuwa magumu kwetu , tunajua uwezo wako ni mkubwa lakini tutapambana kama ni swala la kutufanya tuishi..”Aliongea Lilith akiwa na hali ya huzuni kwenye macho yake lakini mikono yake haikulegea katika kushikilia siraha yake.
“Nyie watu mnafikiria mbali , sijaja hapa kupigana na nyie bali kumchukua mwanamke wangu na kumrudisha nyumbani , Niambieni Clark yupo wapi? Mbona sihisi uwepo wake?”
Ijapokuwa Roma alikuwa na hasira kwa nchi hizo kushirikiana na kumlazmisha Clark kufanya vitu asivyopenda lakini alikuwa ni mwelewa kwa binadamu kupigania uhai wao
Lakini kwasababu asharudi hakutaka kuangalia tu Clark akiteseka ndio maana alifika hapo kumchukua.
Lakinji katika wakati huo hali ya wasiwasi ilimvaa mara baada ya kushindwa kupata msisimko wa nishati za mbingu na ardhi kutoka kwa Clark.
Mara baada ya kusikia swali lake watu wale walionekana kuwa na hali ya wasiwasi katika macho yao.
“Kuna kilichompata Clark?”Aliuliza Roma mara baada ya kuona wanaangaliana tofauti na kujibu swali lake.
“Your Majesty we cant hide it from you , Princess Clark was Abducted”Aliongea Lilith akimaanisha kwamba hawawezi kumficha Roma kwani Clark alitekwa.
Muonekano wa Roma ulibadilika palepale na ukawa ni wa kugopesha , macho yake yalipita kwa kila mmoja aliekuwa ndani ya hilo eneo na kuwasabibishia jaso kuwatoka.
“Unamaanisha nini ?”
“Ilitokea wiki tatu zilizopita , adui alivunja katika kambi yetu na kumchukua Clark , tulishindwa kujua amewezaje kufanya hivyo lakini kulingana na alivyokuwa akisafiri na kutoa msisimko ni mtu mwenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi , kwani Clark alifurukuta kidogo tu na nguvu zake zote zilifungiwa”Aliongea Sargaras.
Roma wasiwasi ulimvaa palepale na alijiuliza au ni majini kutoka ulimwengu wa majini watu au ni majini pepo kutoka Braki?”
“Mfalme Pluto hatukuweza kutoa taarifa kuhusu hili mapema kwasababu hatukujua wapi ulipo , ujenzi wa Noah Ark unaendelea kuwa malengo yetu hata baada ya kupotea kwa Clark , hatutaki kuwa na kikwazo kwani tunakimbizana na muda “General aliekuwa kwenye mavazi ya kijseshi aliongea.
Roma aliona haitokuwa na maana kuwa na wasiwasi , ilionekana ni kweli kuna mtu amemteka Clark lakini nia zao hazikuwa zikifahamika lakini hata hivyo alijua atakuwa sawa kwani kama wangetaka kumuua wasingemteka hivyo ilimaanisha kuna kitu walitaka kutoka kwake
“Bado mnaweza kuendelea na ujenzi bila ya uwepo wake?”
“Princes Clark ashamaliza kutengeneza Blueprint za Noah Ark , ijapokuwa kuna taarifa ndogo ndogo zilizobakia zinazohitaji mahojiano tunajiamini katika kumaliza ujenzi ndani ya muda kutokana na nguvu ya watu kutoka pande zote za dunia”
Jibu hilo lilimshangaza Roma na kujiuliza inamaana Clark ameweza kusanifu ujenzi wa Meli hio kubwa ya kivita , au ni kwamba alishawaza kutengeneza kitu kama hicho hapo kabla.Roma alijiuliza nini kipo katika akili ya mwanamke huyo.
Licha ya wasiwasi wake Roma alijua hawakuwa kipaumbele kwake kwa wakati huo , alipaswa kutafuta njia ya kujua wapi alipo Clark , ili mradi yupo duniani alijua lazima atampata.
Kuhusu Moyo wa Gaia alijiambia lazima apate suluhisho pia ili kuokoa binadamu.
Roma kabla ya kutaka kuondoka sauti iliongea kutoka nyuma yake na kumfanya asimamae.
“Mfalme Pluto je utatusaidia?”Alikuwa ni Lilith alieuliza ni kama anataka kujua kama Roma atakuwa upande wa Binadamu.
Licha ya kwamba ujenzi ulikuwa ukiendelea vizuri lakini walijua fika tatizo sio tu kushuka kwa joto lakini vipi kama miungu hio ikaamua kuua binadamu wote.
Watu kama Sargaras walikuwa washaona uwezo wa Roma hivyo walihisi kufahamu matokeo ya mapigano na miungu mingine.
Kila mmoja alimwangalia Roma kwa kusubiria jibu lakini upande wa Roma alijikuta akipatwa na hisia ambazo hakuwahi kuzipata hapo kabla.
Zamani hakuona kuna utofauti wowote kwa kuwa sehemu ya miungu au kuwa sehemu ya binadamu , alikuwa ni Roma Ramoni binadamu lakini pia mwenye uungu unaomuweka katika sehemu ya miungu.
Ilikuwa ndio wakati sasa akili yake inamwambia kwamba miungu na binadamu ni viumbe viwili tofauti
Katika ulimwengu wa wanyama , viumbe viwili tofauti vinaweza kuishi pamoja kwa miaka muda flani lakni upo uwezekano wa moja kati ya viumbe hao kuwa na nguvu kubwa na kutaka kumla aliekuwa kiumbe dhaifu kutokana na njaa.
Sasa ilikuwa ni swala la muda hata kwa miungu hao , ilikuwa ni muda wao wa kuamsha uwezo wao na kutokana na kwamba washakuwa na nguvu ilikuwa ni swala la muda tu kutaka kuwala binadamu ambao ni wadhaifu na ni swala ambalo halihusiani kabisa na mambo ya maadili wala sentimentals(hisia).
Roma alitaka kuongea lakini neno halikumtoka na alichoweza kutoa ni pumzi iliojaa wasiwasi.
Hali ya masikitiko ilikuwa imemvaa mara baada ya kushindwa kutoa jibu ni upande gani alipo , lakini sio kosa lake kwani ni kama alikuwa akijua nini kitatokea kama atataka kupigana na kundi lote hilo la miungu ambao wana uwezo wao asilimia mia moja.
Roma hakutoa jibu wala hakugeuka nyuma na aliondoka katika eneo hilo kurejea visiwa vya wafu.
Wakati akiwa njiani alijitahidi kupunguza mwendo ili kurudisha mudi yake lakini sasa dakika ambayo anaingia katika anga la visiwa vyake aliweza kuhisi kuna kitu hakipo sawa na kumfanya apige hatua kubwa kuingia katika ngome.
Katika eneo la sebuleni ndani ya ngome hali ya hewa ilikuwa kinzani yenye kutisha , wanawake hao na ndugu walikuwa wamekaa wote wakimwangalia mwanaume wa ajabu aliekuwa mbele yao
Mwanaume huyo alikuwa amekaa kama bosi katika nafasi ambayo Roma hukaa siku zote kama kiongozi wa familia.
Mwanaume huyo alikuwa akishaganza mno kwani ukiachana na kuwa na uwezo mkubwa wa kijini usiotamithilika , kwanza alikuwa mzee hakuwa na nywele wala nyusi usoni , yaani alikuwa ni kama vile ni Skeleton lililopata mwili kwa bahati mbaya lakini hata hivyo alionekana kwa mbaali kuwa Handsome.
Roma mara baada ya kupiga jicho vizuri aliweza kuona mwanaume yule alikuwa ameshikilia ile bangiri ambayo Edna alipewa na Afande Kweka kama ishara ya kuwa mkwe wa familia.
ITAENDELEA.
Hatariiii
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 774.
Roma aliishia kukunja sura mara baada ya kuona bangiri ya Edna ikiwa katika mikono ya yule mtu wa maajajbu, kwa jinsi mtu yule alivyokuwa ameishikilia ni kama vile ni kitu cha thamani kubwa sana kwake.
“Hubby umerdi .. huyu mzee alikuwa akikusubiria”Aliongea Edna mara baada ya kumsogelea Roma akiwa ameshikilia Lanlan.
Pengine ni Edna pekee ambaye alikuwa katika hali ya utulivu , ilikuwa ni kama vile hakujali sana kutembelewa na mtu ambaye hakuwa akimjua.
“Kwanini amechukua bangiri yako?”Aliuliza Roma.
“Ameichukua sekunde tu mara baada ya kufika, hatuna uwezo wa kudili nae”Aliongea Edna huku akionyesha tabasamu la uchungu
Roma alimchunguza Lanlan na kila mmoja na alipatwa na ahueni mara baada ya kuona hawana tatizo lolote.
“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma na yule mtu wa kushangaza aliinua kichwa chake na kumwangalia na kisha akatoa cheko.
“Kijana hupaswi kuongea na mtu mzima kwa ukorofi namna hio”Aliongea yule mzee huku akigeuzia macho kwenye ile bangiri.
“Hio bangiri ni ya mke wangu naomba uirudishe”Aliongea Roma anbaye alionekana hayupo katika hali ya furaha lakini hakumpokonya kwa nguvu kutokanaa sababu maalumu.
“Kauli yako inashangaza hii bangiri pia ni ya mke wangu”Aliongea yule mzee na kufanya kila mmoja kushangaa akiwemo Roma mwenyewe.
“Ijapokuwa upo juu katika levo ya mapigo mengi ya radi , kuna uwezekano mkubwa usiniweze , hivyo nakusihi kistaarabu rudisha bangiri hio kwa mke wangu kabla hujanikasirisha”
Kauli ya Roma iliwashangaza kila mmoja aliekuwa humo ndani ukweli ni kwamba walijua huyo mzee alikuwa na uwezo wa kijini lakini hawakujua ni katika levo ipi.
Sasa muda mchache uliopita waliweza kusikia kutoka kwa Roma alikuwa amepanda levo mpaka mapigo mengi ya radi na waliamini hakuna binadamu ambaye anaweza kuwa na uwezo mkubwa kuliko yeye lakini ajabu ametokea mtu mwenye uwezo mkubwa.
“Naona upo katikati ya levo ya mapigo mengi ya radi lakini umeweza kutambua levo ya uwezo wangu , inaonekana haupo chini yangu sana likija sawala la ufahamu wa mbingu na ardhi”Aliongea yule mzee huku akimwangalia Roma kwa namna ya kuridhika.
Roma mara baada ya kupata maelezo machache kutoka kwa Aoiline na pamoja na uwezo wake mkubwa wa utambuzi aliweza kupata uwelewa wa haraka sana wa kutambua levo hata ya mtu ambaye yupo juu yake, ni hivyo tu ameshindwa kukusanya nishati ya kutosha kupanda levo mpaka mwishoni mwa mapigo mengi hivyo yupo katikati.
Ilimshangaza pia kuona mzee huyo alikuwa akimsifia kwa dhati kabisa , ilikuwa ni kama mwalimu anavyompongeza mwanafunzi.
“Wewe ni nani lakini , kwanini umekuja kunitafuta?”Roma aliendelea kuuliza huku akiwa amekunja ndita.
Yule mwanaume alisimama kutoka katika sofa na kisha alitembea kumsogelea Roma , hakujali kuwa mstaarabu katika kumwangalia Roma.
“Hakuna kubwa lililonileta nimekuja tupimane uwezo”Aliongea na ni muda ulule alikuwa ashafanya shambulizi kwa kumshika Roma kola ya shati.
Roma macho yake yalipanuka kwa mshangao mara baada ya kugundua ameshindwa kumkwepa.
Spidi ambayo mtu huyo alitumia inaweza kuonekana ya kawaida kwa mtu wa kawaida lakini kwake ilikuwa ya ajabu kwani haikumtoa katika eneo alilokuwa amesimama mpaka akafikiwa
Hata kwa wanawake wa Roma walishangaa kwani mwanaume huyo kwa macho alionekana alitumia spidi ndogo sana lakini kwa Roma bado alishindwa kumkwepa.
“Hii sio sehemu nzuri ya sisi kupigana , nitakupa lift”Aliongea yule mwanaume na palepale alimsukuma Roma kama mpira kumtoa nje ya ngome hio.
Roma alijikuta akisukumwa na nguvu isiokuwa ya kawaida kwenda kilomita kadhaa juu angani akiwa hana uwezo wa kujidhibiti.
Muda ambao aliweza kujiimarisha angani mwanaume yule alikuwa ashatoka kwenye ngome na kumfikia huku akimwangalia na tabasamu usoni .
Muda huo huo Roma aliweza kutambua mtu huyo hakuwa na uadui na yeye na ilionekana yupo hapo pekee kwa ajili ya kushindana nae na kama sio hivyo angeweza kumshambulia tokea mwanzo wakati alipokuwa amezubaa.
“Hili eneo lina uwazi wa kutosha na hatutoweza kuumiza watu wa visiwani kama tutakuwa makini”Aliongea yule mtu na palepale alikunjua mikono yake kwa kumpa ishara ya kuanza pambano , yaani alifanya kama vile wanamisumbwi wanavyopeana ishara ya kuanza kushambuliana.
Ijapokuwa Roma alikuwa tayari kupambana lakini bado alikuwa na wasiwasi na ufunuo wa kisiraha wa huyo mtu lakini hata hvyo hakuwa mwepesi kushindwa na alijiambia atampiga kwanza na baada ya hapo watakaa chini na kuongea.
Nguvu ya mbingu na ardhi karibu yao ilianza kuzunguka kwa kasi mno na kusababisha upepo mkali mno na dakika ileile vitu vyeusi vyeusi viliweza kujitengeneza katika anga kwenye umbo flani hivi kama la farasi.
Waliokuwa wakiangalia kwa chini walikuwa na uwezo wa kuona umbo hilo la rangi nyeusi la kushangaza na kuwafanya wanawake wa Roma kushikwa na mshituko
Ijapokuwa walijua uwezo wa Roma ni mkubwa kwa kuweza kufikia levo ya mapigo mengi ya radi lakini hawakutegemea mashambulizi ya mtu yule kuwa ya aina yake kwani hapo walipo ni kama wanahisi nguvu flani ambayo inataka kuharibbu dunia.
Roma na yeye hakuwa nyuma alikuwa tayari ashatengeneza mashambulizi ya uharibufu kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake.
“Hivi unadhani unaweza kunitisha na aina hio ya mashambulizi?”Aliuliza yule mzee.
“Acha kujiamini kwa kupitiliza”
Aliongea Roma na muda uleule aliita radi ya rangi ya zambarau kutoka kwenye kiwingu kilichojitengeneza juu angani.
“Rumble….”
Radi zile zilikunjana kama vile ni vinyoka nyuka ikionekana inajikusanya nguvu na kutengenza mwanga mkali chini ya bahari wa rangi ya bluu na zambarau.
Radi ile mara baada ya kumshukia yule mtu alonekana kuipotezea kwani hakujali kabisa na aliacha impige.
Roma alishangazwa na jambo lile na alijiuliza au hana spidi ya kukwepa shambulizi lake.
“Haileti maana ninaweza bado kuhisi nguvu zake hazijadhoofika hata kidogo au inawezekana.. hapana
Roma moyo wake ulisinyaa , dakika ambayo aliingiwa na hsia zisizozakawaida alishapokea pigo kutoka nyuma.
Thud !!
Ukiachana na sauti kubwa ya kishindo , uzito uliompiga mgongoni ulikuwa ni wa tani nyingi sana kiasi cha kumpeleka chini kama furushi.
Alikuwa kama mshale namna ambavyo aliruka lakini Roma alijiimarisha kwa kukimbia umbali mrefu katika juu ya bahari.
Lilikuwa ni pigo kubwa sana kwake ambalo lilimfanya kujihisi ni kama vile viungo vyake vimepasuliwa pasuliwa na kidogo tu ateme damu.
Roma mwili wake kisayansi ulikuwa na uwezo wa kuhimili mapigo makubwa lakini teke ambalo alipokea kutoka kwa mtu huyo wa maajiabu lilikuwa limeambatana na nguvu ya nishati ya levo za mapigo mengi ya radi , bila kusahau mzee huyo alikuwa ameweka umakini wote katika miguu yake hivyo kusababisha nguvu kubwa sana kuzidi hata ya mapigo mengi ya radi.
Roma alijikuta akiona nyota nyota na nishati zake za mbingu na ardhi mara baada ya kusambaratishwa na kile kiwingu cha radi pia kilipotea.
Alijikuta akihema kama mbwa mara baada ya kurudi tena angani huku akiwa na hali kubwa ya makasiriko na ilidhihirika katika macho yake.
“Unakitafuta kifo”Roma alibweka.
“Hakuna namna , hata kama una ufunuo mkubwa wa mashambulizi huwezi kushindana na mimi kutokana na kwamba huna uzoefu wa kutosha… naona kukutafuta kwangu tupigane kushaanza kuniboa ..bado nakuona ni mdogo sana na inaonekana haikufai kubeba majukumu makubwa”Aliongea
“Acha kuongea upuuzi nenda moja kwa moja kwenye pointi yako wewe ni nani?”
Roma hakutaka kutumia uwezo wake wote kushindana na huyo mzee kwani aliogopa anaweza kumua lakini alijutia kuwa na huruma.
“Kwanini unajifanysiha kama mtoto ambaye hataki kukubali kushibdwa baada ya kushindwa , bado huelewi tu kwamba haijalishi kama ni radi ya Zambarau au ya rangi ya fedha au hata radi ya nyekundu huwezi kunishinda kwasababu huwezi kunifikia na mashambulizi yako , mtu yoyote akifikia katika levo flani za mbingu ukali wa kisu hauna maana tena zaidi ya mbinu, kisu chako kinaonekana kuwa na makali mara mia moja kuliko cha kwangu lakini ujuzi wako ni mdogo , radi yako inaweza kufanya kazi zidi ya wanaojiita watu wa ulimwengu wa majjini watu kwasababu uelewa wao ni mdogo kuliko wako .. lakini ukijilinganisha na mimi nimekuacha mbali kwa vitu vingi sana”
Roma alijikuta akifubaa mara baada ya kuona pengine huyo mtu ana pointi , hio ilikuwa ni kwasababu hata Aoiline kule ujinini alimfanyia kitu ambacho kilimfanya kujua mbinu zake ni ngumu sana kueleweka , kipindi cha nyuma hakuelewa kuhusu hilo na wala hakulipa kipaumbele mara baada ya kuamini kwasababu uwezo wa kushinda anao haina haja lakini sasa alikuja kugundua kwamba katika mapigano ya levo za juu anaweza asishinde kwani atakuwa amekosa mbinu licha ya uwezo alikuwa nao.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Roma siraha anazo lakini hana mbinu nzuri y a kutumia hizo siraha kumshambulia Adui ndio alichomaanisha huyo mzee , hivyo akijikuta katika mashambulizi ya levo ya juu siraha zake zinaweza zisilete madhara kwa adui kwani hana mbinu ya kuwashambulia nazo.
Ni sawa sawa una Kombora lako la nyuklia hapa Tanzania na unataka kushambulia Marekani lakini huna mbinu ya kulifikisha Marekani.
Lakini hata hivyo Roma hakutaka kushindwa kizembe namna hio , radi ya mapigo mengi ya rangi ya silver ilianza kumzunguka kwa kasi kubwa sana kama shoti za umeme na kutengeneza kitu kama ngao vile , ilikuwa ndio radi halisi ya mapigo mengi.
Kadri ilivyokuwa ikiongezeka palepale mnyororo wa radi wa urefu kama wa mita kumi uliweza kujitokeza mkononi mwake , ulikuwa ukinesa nesa kama nyoka.
“Oh! Naona wewe ni mtu ambaye hukubali kushindwa kirahisi nimependa lakini kwa bahati mbaya huwezi kushinda zidi yangu”Aliongea yule mtu huku macho yake yakisinyaa.
Roma hakutaka kutoa jibu na palepale alipiga hatua kwenda mbele na aligeuza ile radi na kuwa boriti akiwa na nia ya kumpiga nayo yule mtu na kumuua hapo hapo , hakuwa na haja tena ya kumjua ni nani.
Radi ile ya rangi ya silver ilikuwa ni kama vile ni mabawa ya samaki na ilifanya kila ilichokuwa ikielekezwa.
Radi hio iliokuwa ni kama mnyororo unaokwenda kumfunga jambazi ilichana anga kwa spidi kali mno , ijapokuwa radi za kutengeneza hazikuwa na nguvu kubwa kama zile zinazoshuka kutoka mawinguni kiasili lakini uwezo wake wa kuzikontrol na kuzichezesha atakavyo ulikuwa ni mkubwa.
Lakini sasa kwa namna zote alizojaribu kushambulia yule mtu alipotea ile sehemu aliolenga na kutokea sehemu nyingine
Yaani ni kama Roma alikuwa akitegwa arushe na bwana yule apotee na pigo lake kupita na hali hio ilimfanya kuzidi kuchanganyikiwa.
Ndani ya dakika kumi na tano Roma aliweza kutengeneza mashambulizi matano ambayo yote hayakuweza kumpata mshindani wake.
Hata warembo wake waliokuwa wakiangalia shindano hilo waliweza kuona radi tu lakini hawakuweza kuona mtu akidhulika nazo.
Kwa Roma ilikuwa ni kama vile amekutana na Master wake na anamwambia ajaribu kumshambulia lakini kila shambulizi Master ana kwepa na kumfanya kujikatia tamaa.
Yule mtu aliishia kutoa tabasamu la uchokozi huku akimwangalia Roma kama mtoto.
“Umeelewa sasa , kama nilitaka kukimbia ningekuwa nishafanya hivyo muda mrefu na hata usingejua , kama ningetaka kukushambulia wakati ulipokuwa ukizubaa ningekuwa nishafanya hivyo na usingeweza kukwepa shambulizi langu , kama mimi ni adui yao ninaweza nisikuue lakini nina uhakika kwamba usingeweza kunifanya chochote”
“Aina yako ya mshambulizi mbona kama yanafanya watu kuchanganyikiwa?”Aliuliza Roma na kumfanya yule mzee kushangaa kidogo.
“Inaonekana angalau umeweza kurudi ila kwa bahati mbaya umekosea , ufunuo wangu wa kimashambulizi ni kweli unafanana na ule wa kumfanya mtu kuchanganyikiwa lakini utakuwa ni mwepesi sana kama upo hivyo pekee”
Roma alishangaa kidogo na alionekana kukumbuka kitu dakika chache zilizopita.
“Ni Deviation? Kwasababu kila kitu kinabadilika na hata kwa kanuni za ulimwengu pia zinabadilika , ufunuo wako ni ushahidi wa dunia kubadilika hivyo kufanya wengine kuchanganyikiwa”Aliongea Roma.
“Deviation? Hehe hilo ni jina la kipekee lakini unapaswa kujua kwamba sio kwamba najaribu kukuficha ukweli ni kwamba tu ufunuo wa mtu wa nishati za mbingu na ardhi hauelezeki kwa maneno”Aliongea lakini Rima pia alikuwa akijua hilo.
Nishati za mbingu na ardhi mara nyingi ukishafikia katika mwanzo wa levo ya utambuzi ambayo ni levo ya nafsi unachopata ni kitu kama maono , sasa maono hayo yanakuwa kama hisia flani hivvi ambazo unashindwa kuziweka katika maneno.
Njia rahisi ya kuthibitisha hili ni kupitia wachungaji wanaotumia nishati za mbingu na ardhi kujaribu kuombea watu , ile hali inayompata yule anaeombewa mpaka kudondoka chini ndio ambacho kinatokea katika ufunuo wa nishati za mbingu na ardhi ni vitu ambavyo havielezeki yaani unajua tu ni kama vile unatunukiwa.
Lakini jambo moja la kufurahisha ni kwamba kadri unavyopanda viwango vya juu vya uelewa wa siri ya nishati za mbingu za ardhi unaweza kutatua fumbo la ufunuo wa aliechini yako.
Roma anashindwa kuelewa ufunuo wa mtu aliekuwa akipambana nae kwasababu alikuwa amemzidi kila kitu.
Sasa Roma alijua hakuna uwezekano ambao anaweza kumshinda mtu aliekuwa mbele yake na hata kama atumie Dhana asingeweza kufanikiwa kama nishati zake za mbingu na ardhi zimeshindwa .
“Basi acha kuzunguka zunguka na niambie wewe ni nani”Aliongea Roma mara baada ya kuzima radi yake na kurudi kawaida akionyesha hana mpango wa kushambulia.
“Acha kuwa na wasiwasi , ni muda wa kukaa wakati tukiongea”Aliongea yule mtu huku akiwa na tabasamu na kufumba na kufumbua wote waliweza kufika katika ngome kwa mara nyingine.
Roma aliishia kukunja ndita lakini aliamua kumkubalia tu na mara baada ya wote kukaa chini katika eneo la sebuleni ni kama sasa yule mtu aliweza kumuona Lanlan aliekuwa katika mikono ya Edna.
“Katoto jina lako si Lanlan , hebu njoo hapa kwanza nina zawadi yako”Aliongea yule mzee.
Kibonge huyo aliishia kupesha tu ijapokuwa hakuwa akimjua mtu huyo ni nani lakini alikuwa amejifunza kutoka kwa baba yake kutokukataa zawadi hivyo alitoka katika mikono ya Edna.
Edna hakumkatalia kana kwamba aliona hakuna tatizo ambalo litampata Lanlan.
“Mjomba ni zawadi gani hio ,je ni kitu cha kula?”Aliongea Lanlan mara baada ya kwenda kusimama mbele ya yule mwanaume.
Katika macho ya kila mmoja bwana yule alitoa bangiri kutoka katika hifadhi ya pete iliokuwa na vigoroli vya kung’aa sana ambavyo ni kama madinni ya rubi lakini sio rubi.
“Inavutia mno…”Sophia aliekuwa kimya muda wote aliongea
Wote waliangalia haraka haraka kuona kama ilikuwa ni Dhana lakini palepale waliweza kugundua madini yaliotumika ni yale yale yaliotumika kutengenezea ile bangiri , ijapokuwa ni kitu kama Dhana lakini ni ngumu kujua kiwango cha nguvu yake.
Hali ya kukata tamaa ilionekana katika macho ya Lanlan , alipenda vitu vizuri lakini bangiri haikuwa ikivutia zaidi kama kitu cha kula.
Mwanaume yule aliweza kuona mabadiliko ya LanLan na alishia kucheka na kumfinya Lanlan mashavu yake.
“Huna shukrani wewe kibonge”
Licha ya kuongea hivyo alikuwa akimvalisha Lanlan ile bangiri.
“Hii Bangiri inaitwa Hufe na ilitengeenzwa kuvutana na hii bangiri ya Fehu, haya majina aliyataja mke wangu wakati huo na ni lugha ambayo hamuwezi kuielewa lakini maana yake ni Hufe nakuombea maisha marefu kwa mwanaume na Hefu nakuombea maisha marefu kwa mwanamke”
“Hebu subiri sana umesema bangiri ilikuwa ya mke wako , huyo mke wako ni nani?”Aliuliza Roma.
“Kijana mjinga sana wewe , unafikiri ilitua kwenye mikono ya familia yenu bahati mbaya tu , mimi na mke wangu kwako wewe sisi ni mababu zako , jina langu naitwa Mzee Yasu kutoka miaka elfu nne iliopita”
“Hebu acha utani basi au ndio unapendwa kuitwa mababu tu kisa una nguvu za mbingu na ardhi”Aliongea Roma alikuwa hana mshangao kama ilivyo kwa wengine.
Lakini sasa yule mtu hakujali sana maneno ya Roma ya kutokumwamini na palepale sijui alifanya nini lakini ile bangiri iliokuwa kwenye mkono wake ilitoa rangi ya kijani na ile ya Lanlan ilitoa pia rangi ya kijani na zilipokutana hewani zilitengeneza picha kama ya binadamu aliekuwa kama ndege kutokana na mabawa na ilidumu kwa dakika chache tu na kupotea na hali ikawa kimya kama vile hakuna kilchotokea.
“Dhana ya kiuungu hio!!”
Roma alishangazwa na jambo hile , ilikuwa ndio ni Dhana ya kiuungu yaani hio ni Dhana tofauti na Dhana za majini ni Dhana ambayo ina roho ya kiuungu ndani yake unaweza kuitwa Dhana za kimalaika.
“Ni miaka elfu nne imepita hatimae gurudumu la upepo na moto vimekutana”
“Gudurudumu la moto na upepo!!”
Kila mmoja alishangazwa na maneno yake , vitu vingi vilikuwa vimetokea na kila aliemsikia hakuweza kuelewa mara moja.
“Unaamnisha gurudumu la upepo na moto ambalo alitumia jini Nezha katika kuwashambulia miungu?”Aliuliza Roma.
“Hehe eti kuwashambulia miungu , ulichosikia wewe ni hadithi tu za kufikirika lakini hii bangiri pamoja na mwenzake nguvu yake ni ya Gurudumu la upepo na moto, Dhana ya kiuungu ambayo Master wangu mimi ndio alinipatia na nikampatia mke wangu kama zawadi lakini kwa bahati mbaya alikuwa ni binadamu wa kawaida ambae uwezo wake ulikwa wa kawaida hivyo alifariki miaka elfu nne iliopita…Ukitaja neno Gurudumu la moto na upepo inaweza kuwa Dhana yenye nguvu lakini kwa mtu ambaye uwezo wake ni mdogo inakuwa ni bangiri ya ulinzi tu… hizi bangiri zikiungana na ndio inakamilika kutoka kuwa zana na kuitwa Dhana. wakati wa kutafuta familia yenu nilifuata tu msisimko wa hii bangiri ndio maana ilinifikisha hapa”
Kwa maelezo yake ni kama iliwafanya wamuamini na kumwangalia kwa heshima awamu hio.
“Ila inawezekanaje ukwa unaishi wakati wewe ni binadamu..inamaana umeishi kwa kuangalia wengine kufa kwa miaka yote hio?”Aliuliza Roma.
“Umekosea sijawahi kuishi katikati ya binadamu kwa wakati wote , kuhusu wapi nimetokea sitoweka wazi kwa faida yako , babu yako alipaswa kukuelezea kwanini DNA za mwilini mwako tokea unazaliwa ni tofauti na binadamu wa kawaida na sio kwako tu kwa familia nzima”
“Yule mzee anapenda kuongea ujinga kama wewe tu .. lakini kama kweli wewe ni sehemu ya mababau zetu kwanini umejitokeza sasa hivi au ndio upo hapa kwa ajili ya kunisaidia kutokana na matatizo yanayonikabili ..tena umesema unae Master , je huyo Master wako mpaka sasa bado anaishi na kama alikuwa na uwezo wa kukupatia hii Dhana ya kiuungu ya Gurudumu la upepo na moto unaonaje na mimi ukinipa hizo Dhana zenye nguvu pengine zinaweza kusaidia kupandisha joto la dunia .. unapaswa kujua sasa hivi binadamu wanakufa je hampo tayari kuokoa dunia, mimi nipo njia panda imekuwa ngumu kwangu kudili na binadamu na miungu kwa wakati mmoja , Athena ni mjanja sana na siwezi kushindana nae”Aliongea Roma na kwa jinsi alivyokuwa akiongea kwa kutia huruma iliwafanya warembo wake kuangua kicheko
Lakini licha ya hivyo mzee Yasu alionekana kutojali sana tabia ya Roma ya kubembeleza bembeleza.
“Nini napaswa kukuambia ? kidogo tu unichanganye”Aliongea na kisha alisimaa na akaendelea kuongea.
“Kinachoendelea ni janga la kinabii la hatima ya binadamu , wewe ndio utacheza katika nafasi ya kuamua kuishi kwao au kufa kwao , sijaja hapa kwa matakwa yangu mwenyewe na kabla ya kuja hapa niliomba ruhusa kwa wakubwa ili kupimana na wewe ki uwezo , itakuwa ni vizuri zaidi kama nitakuwezesha kuimarika lakini siwezi kukusaidia kupigana na maadui zako , sio kwasababu sipo tayari bali ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wangu?”
Tabasamu usoni mwa Roma lilipotea palepale mara baada ya kuona maelezo yote hayo hayaeleweki.
“Naona unanitania , sio kwamba wewe ni dhiafu kuliko mimi na kama hili likiendelea kila mtu juu ya uso wa dunia atakufa lakini bado tu wewe na huyo unaemwita sijui Master wako hampo tayari kusaidia , je mnataka kuniona nikifanya mazungumzo na miungu , mpenzi wangu ashapotea na napaswa kumtafuta sina muda wa kujali maswala ya binadamu mimi”Aliongea Roma kwa hasira.
Roma mwanzoni alifurahi mara baada ya kugundua kuna watu wenye nguvu kama yeye tu katika uso wa dunia kama Aoiline ataendelea na msimamo wake wa kutotaka kujali kinachoendelea na kukataa kusadia, Roma aliona kuna wengine wangekuwa tayari kutoa msaada lakini hao wanaojiita sijui walinzi wa dunia wanaonekana kutokujali kabisa.
Sasa alijiuliza wanafanya nini ili hali wanajua hana nguvu ya kutosha lakini wanamtaka yeye mwenyewe ndio akadili na miungu , kwa vigezo vipi? Roma aliionekana kukasirika sana.
Mara baada ya Edna na wengine kusikia mpenzi wake amepotea walishajua lazima atakuwa anamzungumzia Clark na kila mmoja aliingiwa na wasiwasi kwani ni kama hali inazidi kuwa mbaya zaidi na zaidi.
Licha ya Roma kuonyesha hasira zake waziwazi , upande wa yule Mzee Yasu alionekana katika utulivu , ilionekana ni kama alitegemea Roma kuwa katika hali hio.
“Kwanza kabisa mambo mengine sio marahisi kama unavyoyaona wewe , wakati tukiwa tunatokea katika mazingira yenye mitazamo tofauti ki asili lazima tutakuwa na maoni tofauti , pili punguza presha mwanamke wako atakuwa sawa lakini hatorudi kwako mpaka saa ya mwisho ya hili janga kuisha”
“Kwahio wewe ndio uliemteka Clark , unajaribbu kufanya nni?”
Roma alikuwa na hasira mmno na alitamani kumpiga mzee huyo palepale lakini ndio hivyo tu hakuwa na uwezo wa kushinda ndio maana aliishia kukasirika.
“Wakati sahihi ukiwadia utajua kila kitu , unachokabiliana nacho hakiepukiki mtoto , umechagua njia yako mwenyewe na utatakiwa kufanya maamuzi ya mwisho , unatakiwa kukumbuka kwamba maamuzi yako ndio yataamua hatima ya binadamu , najua uliweza kufanya maamuzi na kuwa na nguvu lakini kwasasa kila kitu kinategemeana na wewe unapenda au hupendi , hivyo acha kujisumbua kuniuliza neno ‘Kwanini’ wakati unajua jibu kwa maswali mengi”
Dakika ambayo alitamka maneno hayo uso wa Roma ulizidi kuwa mweusi na aliishia kukunja ngumi yake huku akishindwa kuongea neno.
Yasu mara baada ya kumwangalia Roma kwa muda kidogo alianza kukagua wanawake wake mmoja baada ya mwingine na macho yake yalikuja kukwama katika sura ya Rufi.
“Ninaweza nisikusaidie katika maswala mengine lakini huyu mwanamke wako mwili wake una kiwango kikubwa cha nishati ya Yin na inaonekana anakutegemea wewe ili uje kumponyesha sumu iliopo ndani ya mwili wake , ninaweza kukusaidia kumponyesha sasa hivi”
Mara baada ya sentensi yake hio mkononi ilionekana karatasi lililokunjwa kunjwa na ilionekana lilikuwa na maandishi ya mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi na alimrushia Rufi.
“Hio ni mbinu ya kubadilisha Yin na Yang unachotakiwa kufanya ni kutumia asili ya mwili wako kufumua meridiani za mwili wako na utafikia hatua ya kutengeneza uwiano, majini wengi hawajui kwamba mwili wako ni mzuri sana kwa kuweza kupanda daraja katika levo za juu , kama utafuata maelekezo yote katika hio karatasi nakutabiria mazuri”
Rufi aliangalia karatasi lile na alionekana kuwa na furaha kubwa mno kiasi cha kufanya macho yake kuwa mekundu , hakuamini kama ilikuwa ni kweli anakwenda kuvuna nishati za mbingu na ardhi kama wenzake.
Mzee Yasu hakuongea zaidi kwani mara baada ya kutoa ishara flani ya kuaga alimgeukia Lanlan na kisha akatoa tabasamu flani hivi la matumaini na kisha akaondoka.
Roma hakuweza kumzuia kuondoka hapo kwani hata hivyo asingeweza kumzuia kwa lolote.
Wakati huo wanawake wote walikuwa wakimwangalia , waliona Roma alikuwa katika hali ya hatari muda huo na walitaka kuonyesha namna walivyokuwa na wasiwasi juu yake.
“Hubby unapanga kufanya nini , je unataka kwenda kuwatafuta miungu katika Ncha ya Kaskazini?”Aliuliza Edna.

SEHEMU YA 775.
Roma alijikuta akimwangalia mke wake katika macho ambayo yalikuwa na hisia ambazo hazikuwa zikielezeka , ilikuwa ni kama vile kuna kitu anakitafuta lakini mwishowe aliishia kuonyesha hali ya majonzi na kukata tamaa hali iliomfanya kulazimisha tabasamu.
“Nataka kwanza kukaa chini na kufikiria ,,hebu kwanza niangalie hio mbinu ambayo Rufi anakwenda kuanza nayo katika kuvuna nishati za mbingu na ardhi, isije yule mzee akawa amedanganya”Aliongea Roma na palepale alimsogelea Rufi na kisha akachukua ile karatasi na kukariri maneno yote yaliokuwepo.
Dakika chache mbele Roma alionekana kukunja sura huku akitafakari na kisha alimwangalia Rufi kwa uso wa tumaini na kumtingishia kichwa cha kukubali.
“Inaonekana huyo mzee amefanya kitu , hii mbinu inashangaza mno na ya upekee , naona kipenzi chetu Rufi anaenda kuvuna nishati kama wengine..”Aliongea Roma huku akiwa na tabasamu.
Roma alijiambia kama Rufi ataweza kupanda levo kile kitu kilichokuwa kikimuumiza kichwa kwa muda mrefu hatimae kitakuwa kimeisha
Kwake ilikuwa ni kama kupatwa na hali ya joto katika baridi kali..
******
Ni kilomita kadhaa juu ya bahari ya Hindi Mzee Yasu alionekana akipita ndani ya eneo hilo bila ya kujulikana uelekeo wake ni kwenda wapi.
Lakini sasa muda ulele aliweza kuonyesha wasiwasi katika uso wake na kumfanya kuinua mkono na kujaribu kushika hewa iliokuwa mbele yake.
“Thud..!!!
Kilikuwa ni kishindo kikubwa kilichoweza kusikika katika hewa , , ilikuwa ni kama vile juu angani mbele yake kulikuwa na ukuta ambao ulimfanya kushindwa kuendelea kusonga mbele.
Ni kama ukuta huo ulikuwa hapo kwa muda mrefu na kama sio kujaribisha na mkono pengine angeweza kujigonga kwa nguvu na kurudishwa nyuma.
Lakini kwa bahati nzuri ni kwamba ukuta huo ulionekana kuwekwa na mtu ambaye alionyesha kutaka kumzuia ambaye hakuwa na uadui na yeye.
Sasa kutokana na uwezo wake kulikuwa na watu wachache sana ambao wanaweza kumtengenezea ukuta kama huo na kumzuia hivyo kwa haraka sana aliweza kujua aliemfanyia hivyo ni nani.
“Mkuu kwanini unataka kunisumbua , wewe ni mkuu mwenye karama kubwa kama ilivyo kwa kizazi cha Master wangu , si ni kujishushia hadhi kujaribu kumtega mtu mdhaifu kama mimi”Aliongea Yasu huku akionyesha hali flani ya kunyenyekea.
Ijapokuwa alishindwa kumjua aliemuwekewa mtego wa kumzuia ni nani lakini hakutaka kujifanya kijogoo.
Kufumba na kufumbua , mwanamke mrembo sana mwenye nywele zilizokuwa zikipeperushwa na upepo alijitokeza akiwa amezungukwa na mawingu , alikuwa mzuri kama malaika wa kike.
Mwanamke huyu hakuwa mwingine bali ni Aoiline jini jamii ya mapepo wa Mbweha wa mikia tisa.
Wakati huo hakuonekana yule mwanamke mchangamfu bali aliekuwa kauzu na siriasi.
“Dogo vipi , mkufunzi wako yupo wapi , nataka unipeleke kwake”Aliongea Aoiline akimwitwa Yasu Dogo
Upande wa Yasu alikuwa katika kiwewe mara baada ya kuhisi msisimko usiokuwa wa kawaida umemzunguka.
Master wake alikuwa sahihi , ukiachana na yeye mwenyewe kulikuwa na Mbweha wa mikia tisa ambaye alikuwa na uwezo wa juu sana , kwa jinsi alivyokuwa akijisikia ni kama vile yupo mbele ya Master wake, aliwaza hivyo Yasu.
Ilikuwa ni kama vile mtoto amesimama mbele ya jitu kubwa la miraba minne na angeuliwa pengine kwa teke moja tu.
Ukweli ni kwmaba Roma hajawahi kumuona Aoiline akitoa msisimko wa aina hio , ni kwamba Aoiline hajawahi kufanya hivyo mbele ya Roma.
“Madam , Mkufunzi wangu ametarajia hili na ameniambia nitakutana na wewe njiani na wakati huo nitapaswa kukupeleka kwake , hivyo huna haja ya kuomba ruhusa yangu”Aliongea Yasu.
Aoiline alikunja sura na aliondoa mkanamizo wa nguvu ake za kijini na kumwangalia Yasu kwa mshangao kidogo .
“Kwahio unasema master wako ameonyesha nia ya kutaka kukutana na mimi?”
“Ndio amesema ana shukrani kubwa kwako kwa kutoingilia hali ya dunia ilivvo kwa sasa , amesema pia wewe ndio mtu pekee unaemjua vizuri kwa miaka elfu hamsini na zaidi..”Aliongea Yasu na kwa mara ya kwanza Aoiline alionyesha hali flani ya aibu za kike lakini iliodumu kwa sekunde chache tu na kumpelekea hata Mzee Yasu mapigo yake ya moyo kusimama.
Yasu hakuamini angeweza kuona mwanamke mrembo wa namna hio , lakini hata hivyo kwa miaka yote elfu nne alioishi alikuwa na hamu mno ya kukutana na Aoiline kwani alishazisikia habari zake nyingi.
Alijiambia ni Master wake tu pekee ambaye ana uwezo wa kuvumilia kutokuonana na mrembo wa naman hio kwa miaka mingi namna hio.
“Kama ni hivyo ongoza njia , nataka kuona huyo mzee aliamua kujifichia wapi maana nimetafuta dunia nzima bila ya kumuona”Aliongea Aoiline
Yasu hakutaka kuthubutu kumchelewesha mrembo huyo hata kwa sekunde na palepale alimpa ishara kisha akageuza na kupaa kuelekea upande wa mashariki.
Walikuwa wakisafiri kwa spidi kali sana na ndani ya sekunde tu walikuwa washatokezea upande mwingine wa dunia katika ardhi ya kitropical ndani ya kisiwa cha Jamaica kwa Walatini huko.
Hiko kisiwa kilionyesha kutokuwa na maendeleo makubwa kulikuwa na makazi ya watu wachache sana yaliokuwa yakionekana na asilimia kubwa ya nyumba zilijengwa kwa nyasi na matope , karibia wakazi wote ni Wamerika wa kihindu.
Aoiline macho yake ya kijjini yalisafiri katika eneo lote hilo na alionyesha kushangaa kiasi.
“Mkufunzi wako ndio anaishi hapa?”Aliuliza
Sio kwamba Aoiline alikuwa akidharau hayo maeneo lakini hakuweza kuamini mtu ambaye ana chaguzi nyingi kuamua kuishi katika eneo kama hilo.
Kubwa zaidi ni kwamba kile ambacho kisiwa hicho ilikuwa ikijivunia nacho hakikuwepo tena kutokana na dunia kupoteza joto, misitu iliokuwa ikionekana ilikuwa ni swala la muda tu kupotea.
Jamaica ilikuwa na hali ya joto pia lakini ilikuwa ni swala la muda tu na sehemu hio kuganda kwa baridi
Yasu aliishia kutingisha kichwa kumwitikia Aoiline na kisha aliendelea kusonga mbele.
Katikati ya kisiwa hicho karibu na upande wa Kaskazini kulikuwa na mwinuko mkubwa kama bonde, mita mia tatu usawa wa bahari na juu yake kileleni kulikuwa na vijumba vidogo vya matope vilivyokuwa vikionekana.
Usipo angalia makini usingedhania kama eneo hilo kuna binadamu ambaye anaishi.
Dakika hio hio alionekana mwanamke ambaye amevaa nguo kwa kujifunga na matambara hivi kama wale watu wa zama za kale huku nywele zake ndefu akionekana kuzibana na kibanio cha mti.
Alionekana kuwa katika umri wa miaka therathini hivi au arobaini na alikuwa na umbo matata sana na muonekano , ni kwamba tu mavazi yake yalikuwa yameuficha ule uzuri na kumfanya kuonekana kama maskini.
Mara baada ya Yasu kutokeza akiwa na Aoiline yule mwanamke aliweka chini kikapu kilichotengenzwa kwa mianzi na alisugua mikono yake kwenye nguo zake kabla ya kugeuza uso wake na kumwangalia Aoiline.
Ijapokuwa hakutabasamu lakini aliinamisha kichwa chake kwa namna ya heshima kumsalimia Aoiline.
“Salamu kwako Madam”
Mara baada ya kusalimia aliendelea na shughuli yake , alionekana alikuwa bize kupangilia dawa aina ya mizizi ili ikauke lakini ukweli ni kama hajafurahishwa na ujio wa Aoiline.
Aoiline alimwangalia yule mwanamke hasa umbo lake kwa macho ya kidadisi na kumwangalia Yasu katika tabasamu.
“Huyu ni mwanafunzi mwandamizi mwenzako?”Aliuliza.
“Haha.. ndio jina lake anaitwa Li Xuemei ni binadamu mtangulizi wa ukoo wa Li kutoka China , ni mtu mkimya sana lakini anakuheshimu tafadhari usijali sana tabia yake”Aliongea Yasu.
“Hehe.. ananipotezea kama vile nimemuibia bwana , kama ningekuwa nimekasirika asingekuwa hai mpaka sekunde hii na hata Master yako hawezi kunizuia”
Licha ya muonekano wake wa uchangamfu na tabasamu lake kwenye uso lakini hakutoa macho kwenye mlango wa kutokea wa nyumba iliokuwa mbele ake.
Hali ya kihisia ilionekana katika macho yake kwa wingi mno.
Ni muda huo huo mwanaume alionekana akitoka nje ya kijumba hicho cha matope.
Alionekana kuwa wa kawaida sana kwa macho ya kibinadamu , akiwa na makadirio ya umri kama miaka hamsini hivi , alikuwa ni kama msomali au tuseme muarabu na nywele zake zilikuwa fupi na tabasamu hafifu sana lilionekana katika uso wake , ukimwangalia kwa ukaribu lazima ungejua ni Handsome ni hivyo tu alionekana kama vile amekosa matunzo.
Ukweli ni kwamba kwa muoneano wake hakuna mrembo yoyote ambaye angempenda hasa wale wanawake wanaoangalia maokoto zaidi kwani alikaa kama vile ni mkulima wa Tumbaku alieishi kijini ambaye anavuta tumbaku hio hio.
Miguuuni alikuwa amevalia viatu kama ndara rangi nyeusi pamoja na kanzu iliokuwa imefubaa sana ya rangi ya ugoro.
Wanasema umdhanie kumbe sie ndio kilichokuwa kikiendelea kwa wewe binadamu ungemuona ni binadamu ambae hatamanishi lakini wataalamu au watu wenye uwezo wa juu sana wa mafunzo ya kijini wangejua huyo mtu sio wa kawaida.
Wasifu wake halisi ulikuwa umezikwa chini kabisa ya bahari na ulikuwa ni wa kipekee sana.
Mwanaume huyo alionekana kama mpita njia ndani ya mtaa na mwanamke alikuwa ni kama malaika alieshushwa kutoka mbinguni.
“Za siku nyingi Aoiline!?”
Mwanaume ndio aliekuwa wa kwanza kuvunja ukimya mara baada ya kuangaliana na mrembo huyo kwa muda mrefu.
Sauti yake ilikuwa ya kizee tofauti kabisa na muonekano wake, ni salamu nyepesi lakini ilimfanya mrembo Aoiline macho yake kuwa mekundu kama vile anataka kulia.
Ghafla tu upepo ulianza kuvuma kwa kasi na nguvu za kijini zilianza kujikusanya katika eneo walilosimama, zilikuwa ni nguvu kutoka kwa Aoiline.
Na ilikuwa ni kama vile juu ya kilele hicho kumetegeshwa mabomu mia moja ya nyuklia ambayo yanakwenda kulipuka mara baada ya sekunde kumaliza kuhesabu , jambo ambalo lilimfanya Li Xuemei na Yasu kushangaa mno.
Uwezo wa jini Aoiline ulikuwa sio kitu ambacho wanaweza kuelewa kwa fahamu zao , wawili hao walikuwa wakipata shida kuvuta pumzi kutokana na mkandamizo unaotokea na walishindwa hata kusoge kwani ni kama wameshikwa na jinamizi.
Ulikuwa ni mkandamizo wa kisheria ambao upo nje ya fikra zao, kama sio Aoiline kujizuia pengine kisiwa hicho kingeporomoka.
Dakika hio hakueleweka kilichotokea lakini yule mwanaume alipotea alipokuwa amesimama na alipokuja kuibukia alikuwa mbele ya mwanamke mrembo Aoiline na kuweka mkono wake kwenye bega lake kwa namna ya kumtuliza na ndio wakati ambao ule mkandamizo uliokuwa ukitokea ni kama vile umeshikiliwa na mwanamume huyo.
“Ine kwanini unafanya hivi , kama unataka kuniona haina haja ya kuwa hivi”Aliongea akifupisha jina la Aoiline na kutaja ine.
“Kwanini nisiwe hivi Sharif , umenitelekeza kwa miaka elfu hamsini kisa tu ya majukumu kwangu ilikuwa sawa lakini kwannini ulinidanganya kuhusu jina lako na wasifu wako , kwanini nisiwe hivi au unataka kusema kila kitu ilikuwa ni mipango yako , au niliona vitu vile kwa bahati mbaya … kwanini hukuniambia wewe ni binadamu tena mtangulizi wa Koo ya Sharif , mshenzi weweulipaswa kufa muda mrefu sana”.
“Najua unachojisikia mara baada ya kupita kizingiti kwa mguu mmoja, nadhani umeona maandishi niliokuachia juu ya paa la mnara , lakini juu ya yote unapaswa kuelewa nia yangu haikuwa mbaya , je unataka yaliopita yakuendeshe?”Aliongea mwanaume aliefahamika kwa jina la Sharf.
“Upo sahihi nimepita mnara na mguu mmoja lakini usisahau ninao mguu mwingine”
“Nilidhani utakuwa umebadilika baada ya miaka yote hio lakini upo vilevile , kama sikosei ungeweza kupita kwenye mnara muda mrefu lakini ukaacha kufanya hivyo”
“Hata kama ningetaka kupita nisingechagua mbinu kama yako ..”Aliongea na kisha alijitahidi kujituliza kwa kuvuta pumzi nyingi.
“Sitaki kuendelea kuongea vitu vinavyonikasirisha haikidhi nguvu zangu kwa mzee kama wewe”
Alionekana ni kam ameyegemea kauli hio na aliinua kidole chake kumnyooshea Aoiline.
“Wewe..”
“Nini! , unadhani nashangaza , unataka kuniona nikiendelea kulia lia mbele yako na kushindana na wewe , sitaki kuua wanafunzi wako kwani najua kujifurahisha mwenyewe vinginevyo nisingeishi miaka yote katika ulimwengu wa majini pepo”Aliongea Aoiline na kumpa jicho la pembeni kwa kujiona hayumbishwi na hisia na kisha aliingia ndani ya kibanda cha mzee huyo.
Eneo lote lilikuwa likinuka madawa tu huku kuta za kijumba hicho zilionekana kujengwa lwa tamaduni za makabila ya eneo hilo.
Sharif aliingia ndani akiwaacha wanafunzi wake nje.
“Nilifika kisiwani hapa miaka ishirini iliopita , nilikuwa natembea tembea tu huko na huko na ndipo nilipo kuja kukutana na mtoto mdogo ambaye ameng’atwa na nyoka , kwa bahati nzuri mama yake alikuwa akiomba msaada na kwasababu nilikuwa mnyonge kipindi hicho niliona bora nijichangamshe kwa kumuokoa huyo mtoto , nilimsaidia kumponyesha kwa baadhi ya dawa za mitishamba na baadae wakazi wakaamua kunipatia chakula na eneo kama shukrani , hali ya hewa ya hii nchi ni nzuri na tulivu kiasi cha kunifanya kuamua kuweka makazi yangu hapa na kujikusanyia mimea misituni na kusaidia wanakijiji .. ni miaka mingi ijapokuwa kwa watu kama sisi inaweza kuwa siku chache lakini kwa binadamu ni muda mrefu”
“Ndio maana nilishindwa kukupata mara baada ya kukutafuta mara kibao , nadhani kwasababu ya uwezo wako kuwa mkubwa kiasi kuliko wa kwangu ndio maana nilishindwa kukupata lakini kulingana na uelewa wangu nilienda katika maeneo ambayo niliamini ungekuwepo lakini sikukuona , kwahio unataka kusema umebadilika ndio maana umeamua kuja kuwa dokta katika eneo kama hili”Aliongea Aoiline.
“Nilitaka kubadilisha mazingira na vitu ninavyofanya , unajua kutokana na uwezo wangu inaboa kukaa bila cha kufanya”
“Mh ndio ipo hivyo..”Aliongea Aoiline na ghafla tu alihama alipokuwa amesimama na kutokezea mbele ya Sharf na kumkodolea macho karibu zaidi na kufanya pumzi zao kugusana.
“Kwahio kujipa huu muonekano ndio kusema unainjoi maisha , huonekani mzee sana wala kijana lakini una sura mbaya , usiniambie sauti yako imezeeka mara baada ya miaka elfu hamsini”
“Nisingekumbuka kabisa kama usingeongea sasa hivi , nilijibadilisha katika huu muonekano na katika hii sauti mara baada ya kuanza projekti maalumu ya kufundisha binadamu namna ya kuvuna nishati ya mbingu na ardhi miaka elfu nne iliopita”
“Oh..! Unamaanisha hao watoto wawili hapo nje au kuna wengine?”Aliuliza Aoiline na Sharif alisogea mpaka kwenye kijikabati na kisha alimimina chai ambayo ni dawa ya kijani kwenye kikombe na kumpatia Aoiline.
“Ni stori ya kufurahisha sana , nitakuelezea siku nyingine ila ni maamuzi magumu nilioyafanya mara baada ya kutoka katika ulimwengu wa majini na kukutana na kiumbe ambae anabakia kutokuwa na jina mpaka leo hii ..nimefanikiwa kufundisha binadamu makabila yote , mzungu , Mchina , Mwafrika .Waraabu na kuendelea lakini kwa bahati mbaya walioweza kufanikiwa kunielewa ni watatu tu”
“Unamaanisha hao wawili hapo nje , kama ni hivyo wa tatu yupo wapi?”
“Ndio ni hao wawili hapo nje kuhusu mtu wa tatu ni Mwarabu na anapambana kuendesha jamii yake , ni swala la muda tu utaweza kukutana nae”Aliongea.
Ilionekana walikuwa na mambo mengi sana ya kuongea , kwani walitumia muda mrefu sana na Aoiline alionekana kufurahi baadhi ya stori alizokuwa akiongea.
Yasu na Li Xumei hawakuwaingilia , ukweli ni kwamba ni mara ya kwanza kwa Master wao kuongea kwa muda mrefu namna hio.
“Unaweza ukashangaa lakini wanafunzi wangu wote wamejipatia umaarufu mkubwa kipindi hicho na wameandikwa katika historia lakini mambo mengi yalivumishwa tofauti na kile walichofanya , kwa mfano Li Xumei alifahamika kama Nuba katika stori za kichina na Yasu alivuma kama Walumbe ndani ya Afrika , baada ya kuridhika nao niliwaachia kazi ya kuangalia Gereza la Roho na kulinda binadamu zidi ya majini watu wasivamie dunia… hawakufanya chochote kile kinachohusiaa na maswala ya siasa”
Waliongea kwanzia mchana mpaka siku iliofuata , walionekana kukummbusiana mambo mengi yaliopita.
Siku iliofuatia wakazi wa kisiwa hicho waliweza kufika na kumfanya Aoiline na Sharif kutoka.
Mzee Yasu aliweza kuona mwanaume mmoja wa kizungu ambae ngozi yake ilikuwa na vijidoti doti vyeusi , alikuwa ni mtoto wa mkuu wa ukoo afahamikae kwa jina la Chriss.
Watu wa visiwa hivyo walikuwa wakiwachukulia Sharf na wenzake kama ndugu , hawakujua kama walikuwa na uwezo wa kupaa au kufanya maajabu , yaani ki ufupi hawakuhisi chochote kutoka kwao.
“Chris kuna tatizo?”Aliuliza Yasu kwa lugha ya kingereza.
“Dokta Yasu kuna habari mbaya , haraka mnapaswa kuondoka kwa boti kuelekea bandari iliopo upande wa kusini Magharibi , jeshi la Ulaya limeingia kisiwani na wanapanga kugeuza hiki kisiwa kama kambi yao , baba na wazee wanajaribu kuwazuia kwa kuongea nao lakini nadhani ni swala la muda tu mazungumzo kuvunjika .. baba kaniambia niwajulishe muondoke kabla hamjachelewa , kama wataanza kuua watu na kuiba tutapigana nao mpaka kufa lakini nyie wengine hampaswi kufia hapa”Aliongea kwa haraka haraka.
Ilionekana ni kama vile dunia imerudi katika enzi ile za ukoloni kwani wazungu walikuwa wakilazimisha vitu lakini awamu hii haikuwa kwa ajili ya kuchukua mali bali kwa ajili ya kupata hifadhi.
Yasu na Li Xuemei waliishia kuangaliana kabla ya kuchuuguza kisiwa hicho kwa uwezo wa kitambuzi na kweli waliweza kuona meli za kivita upande wa Kaskazini.
Walikuwa hawana tabia ya kuangalia usalama hivyo walishindwa kuona meli hizo kabla.
Katika hali ya dunia inavyoenda ilikuwa ni sawa kwa wazungu kutaka kuvamia kisiwa hicho kwani kilikuwa ni moja ya maeneo yenye joto na kipo chini ya Serikali ya Jamaica nchi ambayo haina uwezo wa kujilinda na uvamizi.
Dunia ilikuwa kwenye machafuko na hakuna aliekuwa akijali ni nchi gani inavamia nchi ipi.
Lakini sasa hapo kisiwani watu wake walikuwa hawajaendelea kabisa na ilikuwa ni swala la muda kuuliwa wote kama watataka kuingai vitani kwani siraha zao zilikuwa za kawaida sana.
Yasu na mwenzake waliishia kukunja sura kwani Aoiline na Master hawakuwa wametoka bado nje lakini wakati wakijuliza cha kufanya ndio muda ambao waliweza kutoka.
Ilionekana ni kama vile Sharif alikuwa amemlegeza mrembo Aoiline kwani hakukuonekana dalili ya chuki , ki ufupi alionekana kuwa na furaha.
Yasu na Xumei walionekana kushangaa mara baada ya kuona Master wao alikuwa amebadilika muonekano na kuwa kijana kabisa , palepale waliamini lazima itakuwa ndio sura halisi ya Master wao.
Upande wa Chriss alionekana kuwa katika hali ya mshangao mara baada ya kuona watu wawili ambao hakuwa akiwajua wakitoka nje ya nyumba hio.
Yasu na Xumei waliishia kutoa heshima mbele yao na kabla hawajaeleea kinachoendelea Sharif alivunja ukimya.
“Tumewasikia”
“Je unataka tuchukue hatua , nina uhakika watu wa kisiwa hawatojua sisi ndio tunahusika”Aliongea Yasu tena kwa lugha ya kiswahili akionekana alikuwa na mpango wa kutaka kuvamia hizo meli za kijeshi.
“Haina haja , kwasababu Chriss ametuambia tuondoke , basi tunapaswa kuondoka”
“Aa..!”
Wanafunzi hao wawili wa Sharf walionekana kushangaa , ijapokuwa hawajali sana maisha ya watu wa visiwa hivo lakini walikuwa wamewafahamu na kuzoeana nao kwa miaka mingi
Lakini mara baada ya Sharf kuwaambia hivyo , ilikuwa ni kama agizo kwao na hakuna ambaye alikuwa na uwezo wa kukataa na kwa haraka waliishia kuwaaga wale binadamu wa kawaida na kisha walitokomea upande wa kusini magharibi.
Unadhani wana Ajenda gani hao na kinachoendelea
Inayokuja Anjjiu na Wenzake wanamuomba Roma hifadhi baada ya miliki zote kuvamiwa na kupigwa kama ngoma unadhani Roma atawakubalia.
ITAENDELEA
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1635][emoji3590]
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZ: SINGANOJR

Mono no aware ILIPOISHIA:
Roma alivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha aliinama chini na kumkumbatia Lanlan na kumbusu shavuni na kisha akasimama na kumwnagalia Edna. “Mpenzi ni….”
“Usije ukathubutu ”
Kabla hata hajamaliza sentensi Edna ashabwatuka na kumnyooshea Roma kidole huku akionyesha mabadiliko.
Uso wake ulikuwa siriasi mno na alionekana kuwa kauzu isivyokuwa kawaida , alikuwa ni barafu.
Mabadiliko yake na namna alivyofoka iliwaogopesha kila mtu ndani ya hilo eneo lakini palepale waliweza kuona kitu katika macho ya Roma.
Roma muonekano wake ulibadilika mno wakati akiwa anamwangalia mke wake , ilionyesha alikuwa na majonzi na hali ya kuomboleza kwa namna alivyokuwa akimwangalia Edna.
Ni sawa na pale unapomwangalia mpendwa wako akiwa hospitalini huku ukijua hana muda mrefu wa kuishi ndio namna Roma alivyokuwa lakini haikueleweka muonekano wake unahisia za namna gani.
“Lakini sijaongea chochote mke wangu…”Roma aliongea kwa kusita.
“Najua unachopanga kufanya hata usiponiambia , nakukataza kwenda kupigana na miungu Roma”Aliongea tena na kutaja jina la Roma kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu sana kuonyesha namna gani alikuwa akisisitiza , kwa jinsi alivyokuwa akiongea ni kama swala hilo halina mjadala.
Roma aliishia kukunja ndita , ijapokuwa siku zote alikuwa akiwasikiliza wnawake wake lakini akiamua lake hakuna wa kumzuia.
“Edna I have made a decision , take care of Lanlan , I’ ll came back as soon as possible”Aliongea Roma akimaanisha Edna mwangalie Lanlan kwani ashafanya maamuzi na atarudi mapema iwezekanavyo.
Edna alionekana kutetemeka na kauli hio na haikujulikana kutokana na woga wa Roma kuwa hatarini au hasira , ghalfa tu alisogea mbele na kumshika Roma mkono.
“Roma mume wangu naomba tafadhari usiende , Please don’t go , kwa ajili yangu na mtoto naomba usiende”
Edna alibembeleza na alikuwa amebadilika akiwa ameinamisha kichwa chake chini na ilikuwa ni kama vile anaogopa kukutanisha macho na Roma.
Lanlan aliekuwa akiangalia alikuwa aking’ata lips zake kwa wasiwasi kwani aliona muda wowote mama yake na baba yake watagombana hivyo hakuweza kuongea chochote, upande wa Roma aliishia kutoa kicheko cha kivivu mno.
“Nilikuwa na chembe ya kusita dakika chache zilizopita lakini sasa nadhani napaswa kwenda , kuna vitu napaswa kukabiliana navyo mapema au baadae..”
Edna mkono wake ulitetemeka na kinyonge sana alimwachia Roma na kupiga hatua moja kurudi nyuma.
“Naomba umwangalie Lanlan , napaswa kwenda Edna”Aliongea Roma na kisha alimshika Edna mkono kwa sekunde na kisha akauchia na akapotea palepale.
Upande wa Edna alikuwa ni kama mwanamke ambaye haamini kilichokuwa mbele yake , aliishia kukosa nguvu na kidogo tu angekaa chini , ilikuwa ni kama vile kitendo cha kumwachia Roma mkono ni kama vile alikuwa yupo tayari kwenye maisha yake kuacha kila kitu lakini sio kumwachia Roma lakni mwisho wa siku alikuwa amemuacha.
Wakati warembo wengine wakiwa na wasiwasi juu ya usalama wa Roma Edna yeye alionyesha hali ya huzuni kama vile hatomuona tena.

SEHEMU YA 780.
Ni katika ulimwengu wa majini watu ndani ya miliki ya Hongmeng , hali iliokuwa ikiendelea katoka miliki hio ilikuwa ni ya kutisha.
Yale majengo mazuri na makubwa ambayo yalikuwa fahari ya miliki hio yalikuwa yamebakia vifusi.
Eneo lote lilikuwa ni vumbi na michanga iliochanganyika damu na viungo vya miili , kilichokuwa kikionekana ilikuwa ni maana halisi ya eneo la vita.
Licha ya hali hio ya kusikitisha katikati ya eneo hilo upande wa angani kulikuwa na jengo ambalo limezungukwa na miale ya mwanga ambao mwezi sio mwezi ni kama mwanga wa platinumu ule ambao haujakolea .
Naam eneo hilo ndio linapatikana Gereza la Roho na majini pepo, ndio.sehemu pekee ambayo miungu wameshindwa kuiangusha kutokana na uimara wake.
Sasa katika safu hio ya ki ulinzi ya mwanga wa dhahabu wanaonekana watu wa tatu wakiwa wamesimama , ilikuwa ni kama vile wamefanya kazi kubwa sana na ishara flani za kukata tamaa zilikuwa zimegubika nyuso zao .
“Hepheastus una uhakika hii mbinu itafanya kazi??”Mwanamke mrembo Rozu kwa jina la kijini na Hera kwa jina la viumbe kutoka sayari nyingine aligeuka na kumwangalia Monk aliekuwa pembeni yake na kumuuliza.swahi hilo.
Mwanaume ambaye alikuwa na kipara alievalia Kissaya mavazi maalumu ya kimonk alikuwa ndio Master Yanyuni ambae mwili wake inaishi nafsi ya Hephaestus, nafsi kiumbe kutoka sayari nyingine ambae wasifu wake ni mungu wa moto.
Kwenye mikono yake alikuwa ameshikilia gurudumu la kuwaka waka ambalo lilionekana ni Dhana yenye maandishi ya herufi ambazo hazikutafsirika.
Lakini kama Sharif na Aoiline wangeona herufi hizo wangezitambua mara moja ni lugha ya wajumbe wa Mkuu wa Enzi, lugha ambayo ilitumika miaka mingi iliopita wakati wa wajumbe hao kufika duniani kwa misheni maalumu.
“Numekuwa katika hiki kisiwa kwa muda wa miaka mia tatu na niliishi kwa kufanya utafiti wa namna ya kuvunja hili gereza kila siku, Busara na hekima iliotumika kujenga sio ya kawaida na ni ngumu mno na hatuwezi kutumia nguvu kulivunja, hata kama tukiweza kutengeneza upenyo msukumo wa presha ndani yake utalifunga ndani ya sekunde tu, ukweli ni kwamba tukifanya hivyo kutatokea misukosuko ambayo itafanya ulinzi wake kuimarika zaidi, lakini nilikuja kugundua njia pekee ya kufanikisha hili ni wakati wa presha ya safu yenyewe kuwa chini na hii ni kwasababu ni kama herufi zilizowekwa ndani yake ni kama programu maalumu.Kwahio nilitumia miaka yangu mingi kukusanya vitabu vya kale ambavyo vina tafsiri mbalimbali ya maandishi hayo na nilipo fanikiwa ndio nikatumia miaka mia moja mingineyo kutengeneza hii Dhana nilioipa jina la Reverse Dhamachakra, Hii Dhana haiwezi kufungua hii safu ya ulinzi mara moja lakini inao uwezo wa kupunguza kasi ya ufanyaji kazi mpaka kwenye hatua dhaifu na hapo ndipo presha ya nishati iliopo ndani ya gereza itapungua na kumfanya Zeus kutoka”
“Hehe..mbona ni maajabu hivyo Hephaestus, kama umefanikiwa kwanini unaendelea kusimama? “
“Hatuwezi kuharakisha, nishaona kwamba muda muhimu wa kugeuka ni mchana na safu hii inakuwa haipo imara wakati huo kutokana na kujaa kwa wingi wa nishati chanya, itakuwa ni salama zaidi nikiingiza mfumo wangu wa Reverse Dhamachakra kwani tutakuwa salama muda huo”
“I don’t care about anything that you said as long as Zeus can come out soon. Humph. I don’t want that b*tch to be so arrogant”Aliongea Hera akisema hajali chochote ambacho amesema ilimradi Zeus aweze kutoka mapema... Anasema hataki yule mal*ya(Athena) kuwa na kiburi.
“Muone unavyoongea Hera, hata kama Zeus mpenzi wako wa zama akitoka hawezi kukufanya wa kwanza kabla ya Athena, siku zote nguvu inatawala, haina maana kuendelea kumuonea wivu, Kila kitu kipo usawa wa kiganja chake, ashakushinda muda mrefu tu”Aliongea Hermes na kumfanya Hera kumwangalia kwa ukauzu na wakati anataka kusema jambo mara alikunja sura baada y kuhisi kitu.
"Nilikuwa nimeboreka lakini kwa bahati nzuri kuna wapuuzi wamejileta hapa kujitafutia kifo" Aliongea Hera.
"Nitawaacha mshughukike nao maana ni ngumu mimi kupigana" Aliongea Hephaestus , mawazo yake yote yalikuwa kwenye Gereza hilo la Roho kwa ajili ya kumruhusu Zeus kutoka hivyo hakufikiria sana kuhusu binadamu.
"Hehe... hutopata nafasi hata hivyo hawa viumbe dhaifu hivi kuwachangia wote ni kupoteza muda"
Palepale Hermes mabawa yake yalichanua kwa kujitokeza kusiko julikana huku mkono wake ilionekana siraha ya Caduceus.
Waliofika hapo ni Anjiu na kundi lake la majini , walikuja hapo haraka sana wakiwa zaidi ya majini mia moja huku wengi wao wakiwa katika levo ya Maji ya Barafu.
"Sikuwahi kufikiria viumbe dhaifu kama nyie mtajileta kwenye uwanja wa kifo badala ya kukimbia" Aliongea Hermes
.Majini hao pamoja na baadhi ya binadamu wenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi walikuwa wamekasirika mno na kwa jinsi walivyokuwa wakionekana ilidhihirisha ni namna gani wapo kwa ajili ya kupigana kufa na kupona.
Macho ya Anjiu yalitua katika uso wa Monk Yanyu hususani katika kifaa alichokuwa ameshikiria mkononi na uso wake ulizidi kukunjamana.
"Ile Dhana ni Dhamachakra na imetengenezwa kwa kufanana na maelekezo ya herufi za safu ya ulinzi , hofu yangu kuna uwezekano wa Dhana hio kudhoofisha mfumo wa safu ya ulinzi , hatupaswi kuruhusu hilo litokee" Aliongea Anjiu akiwaambia wenzake, master Shagoni na majini wengine.
"Umeeleweka kwahio tinachopaswa kufanya ni kumshambulia huyo mzee na para lake"
"Yanyu wewe mshenzi mwanaharamu kabisa , siamini kama umepotoka kiasi cha kusaliti sisi marafiki zako wa zaidi ya miaka mia moja, leo ndio mwisho wa uhai wako"
Wale wa miliki ya Hongmeng ndio waliongea hivyo na waling’aka huku wakitoa Dhana zao kwa ajili ya kushambulia.
"Mnaongea ujinga"
Kabla ya Shombeli na kundi lake hawajashambulia , Hermes alikuawa tayari ashajitokeza mbele yao kufumba na kufumbua tu.
Dhana yake ya Cadeceus ilikuwa ikifanana na nyoka , ni kama alama flani hivi zinazotumiwa sana sana katika kutambulisha hospitali lakini muda huo zana hio ikikuwa ni Dhana kwani ilikuwa hai na macho ya nyoka yalikuwa yaking’aa kama rubi.
Dakika hio wale majini walijikuta wakinywea kama vile walikuwa wamegeuka na kuwa barafu , na kitu pekee walichoweza kufanya ni kuzungusha macho yao kama vile wanajichunguza kitu kilichowashikilia.
Lakini ilikuwa ni dakika hio hio waligeukana wao kwa wao na kuanza kushambuliana.
"Shit wameshalogwa na yale macho ya nyoka na kuchukuliana kama maadui"Aliongea Anjiu na palepale bila ya kuchelewa nguvu nyingi za nishati ya mbingu na ardhi zilimtoka na kugeuka moto wa radi ya zambarau huku ukiungana na moto wa kijini wa Ndege wa dhahabu wa miguu mitatu, hakuishia hapo tu aliita pepo lake la ndani la kijeshi na kuliruhusu kwenda kumvaa Hermes.
"Hehe... naona unapaniki wakati bado hata sijaanza "Aliongea Hermes na palepale alizungusha ile fimbo yenye nyoka wa kimaajabu juu hewani na kumtupia Anjiu ndoto ya ukichaa.
Anjiu alionekana alikwisha kujiandaa tayari kwani aliruhusu pepo lake kumlipukia Hermes mbele yake.
Boom!!
Ikiambatana na sauti ya kuumiza masikio mlipuko ule wa pepo la kijeshi ulitengeneza wingu flani kama vile ni milipuko wa fataki unaotoa moshi mweusi.
Ilitokea ndani ya sekunde tu palepale mlipuko ule ulijikusanya na kugeuka tena na kuwa kama kivuli cha moshi kinachofanama na jini Anjiu.
Lakini sasa ilionekana alichofanya Anjiu kilileta faida kwani Shombeli na wenzake ufahamu wao ulirudi na kuacha kushambuliana na kumwangalia Hermes kwa macho makali, lakinj wakati huo huo wakiwa na hofu mara baada ya kugundua walikuwa wametupiwa uchawi wa uchizi.
Uchawi wa Hermes pengine usingekuwa na madhara kwao zamani lakini mara baada ya kuamka kwa Moyo wa Gaia nguvu zake zilizidi nguvu ya kiroho ya nishati za mbingu na ardhi ndio maana aliweza kuwachanganya.
"Tsk..Tsk..Huwa sipendi mtu kuharibu mipango yangu"
Bila kutarajia Hermes alitokeza nyuma ya Anjiu akiwa na sura iliokunjamana kwa hasira ile nyoka iliokuwa kwenye Dhana yake ya Cadeceus ilikuwa ni kama imepata uhai na ilipanua mdomo wake kama Cobra na kumlenga Anjiu kichwani.
Ni muda huo huo wale majini walipata kuelewa Hermes waliekuwa wakimuona mbele yao hakuwa uhalisia bali macho yao yalikuwa yakiwadanganya.
Hali hio ilikuwa ni uthibitisho kwamba uwezo wake ulikuwa mkubwa kuliko majini wote waliokuwa hapo.
Anjiu uso ulimfubaa kwani adui yake spidi yake ilikuwa ya juu sana kiasi cha kushindwa kumkwepa mapema.
Dakika ileile nguvu za kijini zilitoka na Aura ya siraha iliokuwa katika rangi ya bluu ilijitokeza kutoka kusikojulikana , ilikuwa kama vile ni wimbi la sauti kwani siraha ile ilikusanya nguvu kubwa na kumshambulia yulq1e nyoka.
"Madaraja 27 ya nafsi ya upanga ,Mpasuko wa kibuli!!"
Ilikuwa ni bahati kwa Anjiu kwani Shagoni alikuwa makini kuangalia kilichokuwa kikiendelea nyuma ya Anjiu na kumzuia Hermes na shambulizi lake.
Hermes mara baada ya kuona nyoka wake alikuwa amefyekwa na kusambaratishwa kwa kugeuzwa poda alionyesha namna gani hajapendezwa na jambo hilo , ijapokuwa nyoka wake alipona haraka na kujitokeza katika Dhana yake lakini bado ilimkasirisha kwani shambulizi lile lilikuwa ni kummaliza Anjiu moja kwa moja lakini likafeli.
"Una spidi kali ya kushituka"
Aliongea Hermes lakini pale umbo lake ni kama linagawanyika kutengeneza mazingara ya sura yake danganyifu kila mahali , ilikuwa ni ngumu kujua ni yupi ni uhalisia.
Shagoni na siraha yake ya kimaajabu ilizunguka hewani na kutengeneza Aura ya bluu katika mzunguko mkubwa na kushambulia yale mazingara ya sura ya Hermes kwa spidi kubwa.
Majini wengine pia hawakubakia kuangalia kizembe kwani walitumia uwezo wao wote kudili na yale mazingara ya sura.
Hatimae Hermes halisi aliweza kutokeza tena .
"Hivi mnadhani mnaweza kunishinda kwa kunichangia kimashambulizi?"Aliongea Hermes aliekuwa juu zaidi hewani akiwaangalia majini hao kwa chini na tabasamu la Dhihaka. "Madaraja 32 upinde wa Aura ya mchomoo!!!" Bila ya kusita Shagoni alirusha siraha yake ambayo iliweza kutoa mng'ao wa rangi nyekundu , alikuwa ameunganisha Aura ya siraha ile pamoja na nishati za mbingu na ardhi na kufanya itengeneze joto kali kama la kuchomelea chuma .
Siraha ile iliokuwa kama upinde ilimsogelea Hermes kwa kasi na kumchoma kwa kutoboa mwili wake ndani ya sekunde tu.
Alitema damu nyingi huku akishangaa ameshindwa vipi kukwepa shambulizi hilo.
Mara baada ya pigo hilo kwenda kwa Hermes morali ya majini iliamka palepale na wengine walienda mbali hata kuanza kupiga makofi wakionyesha kwamba safari yao ya mapambano sio ya bure.
Lakini sasa kilichotokea ndani ya sekunde kilisinyaza mioyo yao.
Hermes aliinua kichwa chake haraka na kisha aliwaangalia kwa tabasamu ka kifedhili, na damu iliokuwa mwenye midomo yake ilipotea kimaajabu.
"Samahanini , lakini hii damu pia na yenyewe ni feki"
Kwa Shagoni aliona alikuwa amemshambulia Hermes na kufanikiwa lakini ukweli ni kwamba alikuwa ni kama yupo kwenye usingizi wa pono na anaota.
Haikuwa kwake tu majini wote walikuwa wakiona maluweluwe ya ubalisia wa Hermes , kila kitu kilikuwa ni udanganyifu.
Hawakuamini kama Hermes alikuwa na uwezo huo wa kutengeneza udanganyifu na kuwaotesha ndoto kila mmoja.
Hera ambae muda wote alikuwa akiangalia pambano alionekana kuboreka na alitaka na yeye kuingia vitani.
"Vizuri , Mercury inatosha sasa kuwachezea akili waue wote"
"Hehe Hera lakini bado sijamaliza kucheza , haifurahishi kuwaua wote kwa haraka" Aliongea Hermes.
"Kama hutofanya hivyo nitawaua mwenyewe"
Tabasamu la kishetani lilijichezesha kwenye lipsi zake na palepale ghafla tu ulionekana upinde mkubwa wa dhahabu kwenye mikono yake.
Ulikuwa ni upinde ambao haukuwa na kamba kama ilivyo kwa upinde bali kulikuwa na kitu kama uzi wa moto uliokuwa umejifunga katika ncha zote za upinde na kutengeneza kitu kama kamba na kutoa msisimko ambao haukuwa wa kawaida , kwa haraka haraka kwa majini ambao wana elimu kubwa wangeweza kugundua ni Dahana ya Wajumbe wa mkuu wa enzi .
"Oh! Hapana , huo si upinde wa Dhana ya machweo!!?"Moja ya jini mzee levo ya maji ya kiroho aling'aka .
"Siamini macho yangu Panas kutoa hio hazina kwa msaliti"
"Hakuna aliejua nafsi ya miungu inaishi ndani yake , ni udhalimu wa namna gani huu!?"
Dhana hio inaitwa upinde wa Uungu wa Machweo , inasemekana ilipewa jina hilo na majini kutokana na uwepo wa malaika(mjumbe wa mkuu wa enzi) wa zama hizo ambae alitumia upinde huo kuzamisha jua kwa kulishambulia na mshale unaotoka katika upinde huo..
Majini wa jamii ya Panas wanaamini Hoyi Malaika mkuu ndie aliekuwa akihusika kuleta machweo yaani kuzama kwa jua.
Sasa hizo ni imani tu kama imani nyingine kwa majini , sasa Dhana hio ilikuwa ni kama urithi kwa majini wa jumba la kifalme huko miliki ya Panas , ijapokuwa kwao ni Dhana ya kiimani wanaamini nguvu yake imeshuka kutokana na kuharibika lakini hata hivyo ni Hazina ambayo mrithi aliefuatia ni Rozu.
Sasa Dhana hio ilikuwa na nguvu kubwa mno licha ya kwamba nguvu yake imeshuka.
Moja ya tabia yake kubwa Dhana hio ni kwamba inao uwezo wa kufanya mashambulizi yasiokuwa na kikomo ya kiroho .
Kama ilivyo kwa maji ya upako kuathiri roho ndio tabia ya upinde huo na nguvu yake ni mara mbili ya levo nishati za mbingu na rdhi kwa mtumiaji na kwa anaeshambuliwa.
Kwahio ni kama.Dhana hio ilikuwa na uwezo wa kuharibu kila kitu.
"Natumia Dhana ya majini kushambulia majini , nadhani utakuwa mwisho wenu mzuri"Aliongea Hera huku akitoa tabasamu la dhihaka na mikono yake ilishikilia ule uzi wa upinde na kuvuta.
Dakika ileile ule upinde ulianza kukusanya kiasi kikubwa cha nishati ya mbingu na ardhi na hali ya joto ndani ya eneo hilo ilizidi kuongezeka na ghafla tu mshale wa moto rangi ya Dhahabu ulionekana na kuanza kutishia kuunguza anga kwani ile sehemu ilicheza cheza kama vile ni gesi inayosamba angani.
Tukio hilo linaweza kuonekana la kitaratibu sana lakini lilitokea ndani ya sekunde tu na kufanya majini wote kuwa na wasiwasi.
Swoosh !!!.
Sauti ya mkato ya kitu iliweza kusikika na palepale mshale ule ulishatoka katika ule upinde ukimlenga jini mzee aliekuwa katika levo ya maji ya upako.
Mzee yule wa kijini alionekana kujiamini kupambana na ule mshale kwani alikusanya kiasi kikubwa cha mbingu na ardhi na ilionekana alikuwa akipanga kukwepa kwa wakati mmoja.
Lakini sasa akiwa katika kiwewe aligundua hakuwa na uwezo wa kusogea kwa namna yoyote ile kila alipojaribu kufanya hivyo.
“Inawezekana vipi hii!!
Alijikuta akimaka ndani kwa ndani huku akiangalia mshale ule ukimsogelea na hatimae kumfikia na kumtoboa.
Mshale ule mara baada ya kumtoboa yule jini haukupita bali uligeuka kama moto na kuunguza kila kitu na ni ndani ya sekunde tu jini yule aligeuka cheche zilizosambaa angani.
Majini walioshuhudia tukio lile walikumbwa na hofu isio na kifani.
Ukweli ni kwamba licha ya mshale wa upinde huo kuwa na nguvu lakini kama utafanikiwa kukwepa huwezi pata madhara na ndio mbinu pekee ya kupambama na Dhana hio.
" Ni ujinga kiasi gani mnao , yaani unajiona jini wa levo ya maji ya upako unaweza kushindana na nguvu ya kanuni za anga??" Aliongea Hera kama vile yule jini hajafa.
Hermes aliishia kuchezesha ulimi wake tu huku akizungusha kichwa , kikawaida alikuwa ashajua Hera ametumia kanuni za anga kumshikilia yule jini asisogee ili mshale wake umshambulie.
Kwahio ilimaanisha Hera alikuwa akirusha mshale kulenga shabaha ambayo haisogei.
Mara baada ya kuona kazi yake ni njema alitoa tabasamu la kifedhuli huku akiwaangalia Shagoni na Anjiu.
"Umekuja hapa kwa ajili ya kuongoza watu wako
katika kifo , je unajiona unaweza , nawaonyesheni namna gani maisha yenu hayana thamani kwa kujitia ujasiri mbele ya sisi miungu"
Mwishoni mwa.sentensi yake alianza kucheka kama kichaa lakini hakutingishika hata kidogo.
Dakika ileile alianza kutengeneza mishale ya moto na kuendelea kuwashambulia Anjiu na wenzake .
Mishale hio ilikuwa ikitoa sauti kama ya makombora na kusambaratisha majini.
Ijapokuwa walikuwa katika levo ya maji ya barafu kupanda lakini mbele ya Dhana hio ya upinde wa machweo hakuna ambae alikuwa na kinga.
Hawakuweza hata kujitengenezea vizuizi kwani waliishia kuungua na moto lakini hata hivyo walikufa huku wakionyesha hawakuwa wakijutia maamuzi yao ya kuja kupambana.
Muonekano wa Anjiu na Shagoni ulikuwa katika hali ya kusawijika , ijapokuwa hawakutegemea kushinda udogo wa uwezo wao zidi ya miungu ulikuwa ni nje ya fikra zao.
Uwezo wa Hera pekee unaweza kukadiriwa kama utaufananisha na mbinu za mbingu na ardhi kufikia levo ya mapigo mengi ya radi au juu kidogo , alikuwa na nguvu kuliko majini watu wote.
Yaani miungu wengine hawakuhitaji hata kuingia kwenye mapambano Hera pekee anatosha kusambararisha jamii hizo zote.
"Ni kweli tupo hapa kwa ajili ya kifo . je hii ndio hatima ya jamii yetu kuwa na mwisho mbaya hivi??"
Mawazo mbalimbali yalipita katika akili zao , hata kwa Anjiu ambaye alikuwa amepitia uzoefu mwingi kwenye maisha yake hakuweza kusaidika zaidi ya kuwa mnyonge mbele ya hatari iliokuwa mbele yao.
Ndani ya dakika chache tu majini karibia wote walikwisha kuuliwa na kubakia wasiozidi kumi na mbili akiwemo Shombeli , Anjiua , Umini na baadhi ya waliokuwa na uwezo wa juu lakini hata hivyo hakuna aliethubutu kushambulia.
Madhaliliko na aibu haikutosha kuelezea hisia zao wakati huo , ilikuwa ni zaidi ya majonzi ni kwa namna gani walikuwa dhaifu.
"Ni kwa bahati mbaya show ndio inakaribia ukingoni , mmefurahi ?, Hehe.. naona mmebakia wachache sana na hamuwezi kuniondolea hamu yangu ya kuua”.
Baada ya kuongea hivyo upinde wake alieulekezea kwa Anjiu.
"Unaweza kuleta ukinzani lakini kwangu ni kama mtoto mdogo anaeanza kutambaa"Aliongea Hera.
Mwishoni mwa sentensi yake aliachia mshale ambao ulikuwa na nguvu kubwa kuliko yote aliokuwa amerusha mwanzo.
"Whoosh!!
Anjiu alifumba macho yake kana kwamba alikuwa akijaribu kuvuta kumbukumbu nzuri za maisha yake yote wakati huo akisubiria kifo.
Lakini sasa palepale ulisikika mngurumo kama wa radi huku upepo wa ajabu ukifyeka lile eneo na ajabu kwao ni kwamba Anjiu alionekana mzima.
Moto ule wa mshale ulipotawanyika ndipo walipoweza kuona kuna mtu amesimama mita kadhaa alipo Anjiu "Romaa..!!!" Majini walimaka
"Hades" Miungu ilimaka.

END OF SEASON 26.

NILIEMDHANIA NI KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI : SINGANOJR

Mono no.Aware.

SEASON 27.

SEHEMU YA 781.
Miungu walikumbwa na hali ya mshangao mara baada ya kujua mgeni aliefika hapo alikuwa ni Roma Ramoni Au Hades.
Ni muda huo huo waliweza kumuona akishusha mkono chini , ilionekana alitumia mkono wa kulia kuzuia shambulizi hilo.
"Seriously ? Nimechelewa kwasababu nilikuwa nikifikiria kuhusu maisha lakini naona kuna majini wachache sana waliobakia , ni nini hiki , kwanini nyie watu mnaua fasta fasta namna hii , ni tofauti kabisa na kwenye filamu za mapigano ,
au ndio tuseme mmejifunza kutoka kwangu?"Aliongea Roma katika mawazo yake.
Isitoshe athari za kujitokeza kwake haukuwa mkamilifu.
Lakini kwa bahati nzuri wale wakubwa walikuwepo na Roma aliona kama Hera atawaua kutoka wa hadhi ya chini kwenda juu basi atakosa mahali pa kulilia.
“Hades, what is the meaning of this?”Aliuliza Hera akimaanisha hio ni maana gani lakini kwa muonekano wake ni kama hana nia ya kukaa chini na kuongea na Roma yaani alikuwa kishari zaidi.
"Wewe ndio Hera? ,Tsk , Tsk siamini ni nafsi nyingine ya miungu inayoishi ndani ya jini yenye kubeba chuki ya wazi , sio mbaya angalau wewe kuliko huyo popo mwenzako Hermes .... U’mrembo kupindukia , naona ulichagua mtu mzuri kwa ajili ya kuuvaa mwili wake ,kama sio nafsi yako kuishi ndani ya huo mwili pengine miliki ya Panas ingejipatia mkwe wa matawi ya juu"
"Unaongea nini wewe?" Aliuliza Hera ambaye alionekana kukasirika.
Alijiuliza huyu mtu katokea wapi na kuanza kuongea ujinga.
"Relax. I’m just joking to lighten up the mood. It’s too tense here.”Aliongea Roma akisema anachangamsha hali.
"Hehe..Hades acha kumtania Hera , uwezo wake unalingana na wa Poseidon ,hivyo nakusihi kufikiria kwanza ni kiwango gani cha uwezo Poseidon amepona , umekuja kufanya nini hapa , weka wazi??"Aliongea Hermes.
"Sio swala kubwa lililonileta , nimeona tu nyie watu mmesababisha matatizo ya kutosha na hakuna haja ya kuendelea kwenda mbali"
"Oh , kwahio unapanga kufanya nini??"Aliuliza Hera.
"Nilikuwa nikisubiri sana uongee hivyo , nilikuwa nikiwaza kuwakusanya wote kwa pamoja na itakuwa vizuri zaidi na Athena akiwepo ili tujadiliane namna ya kurudisha hali kawaida katika meza ya mazungumzo , kwanza tutapaswa kuzingatia namna ya kuzuia joto kutoshuka zaidi na zaidi , kwasababu watu wengi watapotea na isitoshe kuwa na dunia ya barafu haifurahishi na muhimu zaidi nitatoa wapi nyama kwa ajili ya binti yangu kama wanyama wote watapotea?, pia hatupaswi kuhusisha binadamu wa kawaida katika hili , hebu tukaeni chini sisi kwa sisi na tuone ni kwa namna gani tutapata suluhu , mimi nitabakia neutral ili mradi nitaona kila upande umepata haki, sitaki kumsaidia yeyote , mnaonaje je mpango wangu ni wa akili ??"
Maneno ya Roma yalionekana kusababisha miungu hao kuwa na muonekano usioelezeka , tofauti na kuita mpango huo ni wa akili wao waliona ni wa kijinga.
"Hades kama upo hapa kucheza , tafadhari rudi kisiwani kwako na ukaendelee na maisha yako ,
vinginevyo tutaamini wewe ni msaliti wa sisi miungu kwa kuamua kuungana na binadamu"Aliongea Hera.
"Hey hii ni mara yetu ya kwanza kukutana , kwanini kuongea maneno ya kuudhi hivyo, ,si nishawaelezeni hakuna haja ya kwenda mbali kama haifaidishi pande zote" Aliongea Roma akiwa na tabasamu.
"Acha kuongea ujinga , una chaguzi mbili , kwanza kaa pembeni na angalia bila kuingilia , pili tusaidie kuua hili kundi la viumbe wenye sura mbaya".
Muda uleule presha ya mwanamke huyo iliotokana na nguvu za kanuni za anga ilimtoka na kuzingira eneo lote , Anjiu na wenzale walijikua wakiwa katika mshangao mara baada ya kugundua hawakuwa na uwezo hata wa kutingisha vidole.
Hio ndio ilikuwa nguvu hlisi ya kanuni za anga ambayo miungu walikuwa na uwezo kuitoa kwa kutumia ufahamu wao wa kiroho.
Hermes na Hephaestus wote walionyesha nyuso za majigambo kana kwamba walikuwa wakiamini uwezo wa Hera unatosha.
Ilikuwa ni kwasababu ukiachana na Zeus na Athena , Poseidon na Hera ndio miungu waliokuwa na uwezo wa juu zaidi kuliko wengine wote.
Hata Hades wa zamani hakuwa na uwezo wa kumshinda Hera , sasa kwa Roma ambae alirithi nusu ya uungu wa Hades alikuwa hatoshi kabisa kushindana na Hera.
Kuhusu uwezo wa Hera wa nishati za mbingu na Ardhi hawakufikiri sana kwani Hera ni kama anaunganisha uwezo huo pamoja na uwezo wa kanuni za anga kitu ambacho kinamfanya moja kwa moja kuwa juu ya Roma hata kama amepitia mapigo mengi ya Radi.
Gepu dogo tu katika uwezo huo ni kubwa mno na haliwezi kuzibwa kirahisi.
Roma alipata kuonyesha muonekano wa kusumbuka na aliishia kulamba lips zake mara mbili , wakati kila.mmoja akionesha hali ya wasiwasi yeye alivuta pakiti ya sigara kutoka hifadhi ya pete na kuiwasha.
Mara baada ya kuiwasha aliweka taratibu mdomomi , ilimchukua sekunde chache tu kutoa sigara na kiberiti, ilimpa.shida kidogo kuwasha sigara kutokana na upepo na baridi lakini alifanikiwa.
Roma palepale alipiga pafu la moshi na kisha akalimeza na kulitoa puani .
Majini wale ambao walikuwa katika hali ya kujikatia tamaa walijiuliza huyu mtu amekuwa addicted kiasi gani na sigara mpaka kuwaza kuvuta muda huo wa hatari bila ya wasiwasi. "Haha.. msinifikirie vibaya , sio kwamba nipo addicted na sigara bali ni kwamba nina wasiwasi sana nyakati hizi , hivyo navuta ganja kidogo kujituliza"
[emoji769]Hades achana na maswala yako ya kujitakia umaarufu, umefanya vya kutosha na ni muda wako wa kurudi" Aliongea Hermes.
Roma aliishia kulamba lipsi zake kidogo na kisha alivuta pafu mbili za moshi na akatupa ile sigara huku akitoa moshi mwingi puani kama gari moshi na kuwaangalia kwa muonekano uliosawijika.
"Kama nilivyosema mwanzo mnapaswa kuacha mambo yenu ya kutesa binadamu mara moja"
"Do you truly believe I won’t attack you, Hades? The Gods’ revival is unstoppable, and no one is allowed to stand in its path!”
"Unadhani siwezi kukushambulia Hades? ,Ufufuo wa miungu hauzuiliki na hakuna wakusimama katika njia yake".Aliongea Hera.
Roma uso wake ulibadilika palepale na kuzidi kuwa mweusi na mara ileile msisimko wa kimauaji ulimvaa na alianza kuogopesha na hakukuwa na tone la utani katika macho yake , alikuwa amebadilika tofauti sana na mwanzo.
"Wewe Ajuza , nimekuita Hera kwasababu nilikuwa nikijaribh kuonyesha heshima , hupaswi kutokunielewa ilihali hatujawahi kuonana , jina langu ni Hades lakini ukiachana na hilo naitwa Roma Ramoni , Naongea tena ni aidha muache mara moja na tuongee au niwaue wote tuone kama hata mtaweza kuhamia katika miili mingine ,nadhani huelewi jambo moja , sijaja hapa kwa ajili ya mazungumzo wala kubembeleza mtu...Maneno yangu ni sheria ya mbingu na kama hutaki kutii kufa .."Miungu wote walijikuta wakipauka kutokana na hasira anazoonesha Roma.
"Ukaidi huu , unathubtu vipi kuongea na mimi namna hio ilihali ni binadamu mdhaifu uliepata nusu ya uungu wetu, hakuna wa kukuokoa leo hii , na nakwenda kukuonyesha ni kwa namna gani huna umuhimu wowote kwetu"Aliongea Hera kwa hasira.
Anga kumzunguka Roma ghafla tu lilibebeshwa kurasa za anga zaidi ya elfu moja huku Hera akijaribu kufanya shambulizi kwa kutaka kumfunga funga Roma.
Wakati huo huo ile Dhana ya upinde wa machweo katika mikono yake ulikuwa umeshikia mshale wa moto kumlenga na ulikuwa na nguvu mara nne ya alivyokuwa akishambulia majini.
"Nenda!!"
Mshale ule uliomlenga Roma eneo la moyo uliachiliwa na kuwa kama vule ni boriti ya mwanga wa laser inamsogelea kwa kasi.
Kutokea mwanzo mpaka mwisho Roma hakuwa amesogea hata inchi na akiwa na macho yake angavu aliangalia namna mshale ule unavyotoka katika upinde ule kumsogelea.
Lakini sasa sekunde tu ambayo mshale ule ulionekana kuufikia mwili wake radi ya rangi ya silver ilionekana kulipuka kutoka katika mwili wake kama shoti.
Boom!!
Nguvu ya mshale ule wa upinde wa Dhana ya machweo ulinywea mara baada ya kukutana na nguvu halisi ya radi yenye nguvu mara elfu moja kasoro moja na kusambaratishwa kabisa.
Unachopaswa kuelewa hata radi ya zambarau tu ni hatari sana mbele ya miungu sembuse nguvu ya radi hio ya silver , radi ambayo ni adimu sana kuonekana duniani imetoka katika mwili wa Roma kwa namna ya ajabu hivyo.
"Ni radi ya rangi ya Silver !!! ..Haiwezekani, umewezaje lujua siri ya radi ya aina hio?" Hera alionekana kuhamaki asiamini anachokiona,ule utukufu wa neema yake ya ki uwezo ilimpotea palepale.
Ilikuwa ni kama vile hakutarajia Roma anaweza kupanda levo haraka namna hio.
Walikuwa na mbinu za kupambana na radi ya zambarau lakini nguvu ya radi ya mapigo mengi ni kama hawakuwahi kuifikiria, hata kama uwezo wao unaweza kufikia ule wa Zeus au Athena.
Roma alipiga hatua moja mbele.,.muonekano wake ni wa kiutawala zaidi , kana kwamba alikuwa akimiliki ulimwengu wote na anao wezo wa kudhibiti kinachotokea kati ya mbingu na ardhi.
Ni dakika hio hio ni kama wingu juu angani limeitikia wito na lilijikusanya kwa kasi na kuanza kuzunguka huku mingurumo ikiwa ni ya juu sana.

Zile kurasa elfu moja za vizuizi vya anga ziliungua kama vile karatasi inavyoungua na kusambaratika.
Radi ya mapigo mengi ilianza kuomyesha mbwembwe zake juu mawinguni na wingu lilianza kushuka chini kwa kasi kama kimbunga na kutishia kuharibu kila kiumbe kilichopo chini yake.
Hera hali ya wasiwasi na ya kusita ilimvaa na hakuweza kufikiria tena kupambana na Roma ambae uwezo wake ni kama vile anatawala viumbe wote.
"Hephaestus usisubri tena fanya sasa hivi na kwa haraka"Aliongea Hara.
Hephaestus mungu wa moto alielewa amri na palepale alisogelea safu ya gereza ile sehemu dhaifu na kuchomeka Dhana yake ya Reverse Dhamachakra kwa ajili ya kumsaidia Zeus kutoka.
Shombeli na wenzake walikumbwa na wasiwasi mara baada ya kuona Yanyu anachotaka kufanya na kuanza kumpigia makelele Roma.
"Mzuie .., Mzuie haraka anaharibu safu ya ulinzi huyo"
Good work bro
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR

Mono no Aware.

ILIPOISHIA
Lakini muda uleule wakati akijiandaa kutumia uwezo wake wote Athena alitoa sauti ya kumzuia.
"Subiri kwanza dakika moja"Sauti yake ilionekana kubadilika haikuwa ya kikauzu na ya kiadui kama.mwanzo.
"Nini tatizo , hautaki tena kupigana??"
Athena alionekana kuwa kimya kwa.muda , kwa kile kinachoweza kuelezeka kama hali ya kusita.
"Kama nilivyosema kama utatumia uwezo wako wote inamaanisha mmoja wetu atakufa lakini je upo tayari kuniona nikifa mbele ya macho yako?"Aliuliza Athena.
"Haha.. unamaanisha nini??"
Roma alihangaika kukwepesha macho yake na Athena , alikuwa akionyesha kumdhihaki lakini hakuweza kuishinda nguvu ya kutaka kuzidi kumwangalia uso wake ambao ni kama umefunikwa na kiwingu muda wote lakini licha ya hivyo ilifanya mtu yoyote kuhisi Athena ni mrembo bila ya kumuona.
Lakini palepale ili kumjibu Roma swali lake Athena aliamua kuonyesha muonekano wake.
Roma aliangalia uso wake kidogo tu tena kwa mbali na hakuona macho yake yalikuwa yakimdanganya , ilikuwa ni sura ya mwanamke mrembo ambae alikuwa akimjua kiasi kilichopelekea mshituko katika moyo wake.
Kwa miungu waliokuwepo ambao walikuwa wakiujua ukweli tokea mwanzo waliishia kukumbwa na huzuni juu ya Roma.
Lakini Hera na Hermes ni kama vile wanataka kumwambia Roma msemo wa 'kiko wapi' , yaani walikuwa na sura zenye tabasamu la dhihaka.
"Heh..haha..haha..ah""
Roma mwili wake ulitingishika , mabega yake yalishuka na kichwa chake alikishusha chini huku akitoa kicheko kwa namna ya kujicheka mwenyewe pengine kujidharau , kicheko ambacho unaweza kukitafsiri kama kilio , ilikuwa ni kama vile amekuwa chizi na aliishia kutingisha kichwa kama mtu asiekubaliana na ukweli.
Mwishowe macho yake yaligeuka mekundu na haikuchukua muda machozi yalianza kujitengeneza katika mboni zake.
Roma alikuwa akishindana na kilio cha kwikwi kwa kukizuia na kumfanya kuonekana kama kuna kitu kimemkaba kooni , alijitahidi kujizuia lakini alionekana kushindwa.
Hali ile ya huzuni , majonzi na maumivu kwenye macho yake iliwafanya baadhi ya miungu kama vile Aphrodite na Artemis kushindwa kuzuia machozi.
Hakukuwa na ishara ya huzuni wala furaha katika sura ya Athena na alichokifanya ni kupaa na kwenda kutua mbele ya Roma akiwa katika hali ya utulivu .
Muda huo Aegis na Pallas alikuwa ashavirudisha katika hifadhi na hio ni kwasababu alijua ameshinda vita.
Kma alivyotabiri tokea mwanzo haijalishi mwanaume huyo atapanda levo kiasi gani na kuwa na nguvu lakini mwisho wa siku hataweza kumshambulia.
Athena katika hali ya utulivu alimwangalia Roma ambae alikuwa ameficha kichwa chake kwa kuangalia chini akiwa katika hali ya maumivu yasioelezeka na palepale alichanua mikono yake na kuizungusha katika kiuno cha Roma huku mwili wake ukimwegamia.
“I knew it. I know you couldn’t bring yourself to hurt me, am I right?”
"Nilijua tu , nilijua hutoweza kuniumiza , si kwel ??"
Alinusa harufu ya marashi anayoyajua na kumfanya kuhisi kitu kimemkaba kooni na ghafla tu alimsukuma Athena mbali na mwili wake kwa mkono mmoja na kisha mkono huo huo ukashilia kidevu cha mwanamke huyo na kuzungusha kichwa chake kwa kumkagua.
Macho yao yaligongana , wakati ya Roma yakiwa ya hasira ya kwake ni kama maji ya barafu kwenye friji, ni sawa na kusema moto na barafu vimekutana.
Ilikuwa ni ngumu mno kuelezea hali aliokuwa nayo Roma.wakati huo, alijiona ni kama vile amegeuka kichaa lakini kwa wakati mmoja hakuweza kuendelea kuwa kichaa.
Athena hakuleta ukinzani wowote na alimuacha mwanaume huyo kumfanya atakacho.
Ukauzu wake , urembo wake ulikuwa ukitisha usiohimilika kwasababu ya mkandamizo aliokuwa akitoa lakini pia hadhi ya jina lake.
"E... Edna kwanini unanifanyia hivi , si nilikuomba ...ukae nyumbani na kumwangalia mtoto , Kwanini .. kwanini unafanya hivi.."Roma alijitahidi kumeza mate huku mkono uliomshikilia Edna ukitetemeka.
Ishara ya huzuni ilionekana hatimae kwa mbaali katika uso ambao ni kama haiwezekani , uso wa mrembo Edna , kope zake zilicheza huku mboni ya macho yake ikiwa katika eneo moja.
"Na mimi nilikusihi ..nilikuomba sana ..nilikubembeleza Roma usije ila hukutaka kunisikia"Aliongea Edna mara baada ya kung'ata lipsi zake.

SEHEMU YA 784.
Roma hakuwahi kutamani maisha yake yawe ya udanganyifu au kwamba pengine asingekuwa wa ulimwengu huu hapa Duniani. Hata kama utoto wake ulikuwa mgumu zaidi, utu wake ulimhimiza kutotelekeza uhai.
Lakini katika wakati huo ishara hafifu ya kifo ilijionyesha katika macho yake , ni ishara iliokuwa katika muundo wa uchomvu wa mwili na akili , uchomvu uliokithiri na wasiwasi ulioanza kula mizizi ya vyanzo vya uhai katika mwili wake.
Udanganyifu , uongo na unafiki . Maisha yake ni kama yamepoteza muelekeo na maana sekunde ambayo mwanamke Athena alipoonyesha sura yake.
Roma alijikuta akimwachia Athena na kurudi hatua mbili nyuma kwa kujikongoja halafu akamwangalia mwanamke huyyo kwa uso kama wa mtu mjinga. Wote waliangaliana bila ya kusemezana neno.
Umbali mchache Aphrodite ambaye alikuwa akitoa tayari machozi alijikuta akimgeukia Artemis.
“Hades , he … he seems to have known all along?”Aliuliza mbona ni kama Hades alikuwa akijua muda mrefu.
“Nafikiri hivyo pia , kwa nilichowasikia , inaonekana Athena alikuwa akijua Hades alikuwa akifahamu kila kitu wakati ambao tulikuwa tukidhania tumemficha kisawasawa”Alijibu Artemis .
“Nyie Hera na Hermes ndio mliomwambia sio?”Aliuliza Poseidon huku akiwaangalia kwa macho ya ukali.
“Ni mimi , nilimwambia muda mrefu tu lakini kipindi kile sikujua kama aliweza kuniamini”Aliongea Hermes huku akitoa kicheko.
“Kwaniin ulifanya hivyo?”Aliuliza Aphrodite.
“Si kila kitu kipo wazi , hata kama Hades alijua angeendelea kufuata ramani aliowekewa na Athena kupita kwasababu nyepesi tu hakuamini ukweli niliomwambia , kama angemuacha Athena mara baada ya kujua hili ingemaanisha kwamba mipango yake yote imefeli tokea mwanzo, nyie hamuoni hili swala linasisimua , kumfanya kuwa na wasiwasi huku akiamini anachokiwaza hakiwezi kutokea hatimae kimetokea…”
“Hermes ulienda mbali sana?”Apollo aliongea akiwa amekunja sura.
“Huh! Mbali kivipi? ,nilichofanya ni kuongeza tamthilia kidogo tu na chumvi chumvi kwa mhusika mkuu , nyie wanafiki kama kweli mngekuwa mnamjali Hades kwanini mlimficha ,nikijilinganisha na nyie bora hata mimi nina nafuu”Mara baada ya kuumbuliwa na Hermes wote walifunga midomo yao.
Ni kweli kabisa kila kitu kilikuwa kishajulikana muda mrefu sana, labda tu kama Roma asingekuja kuwa na hisia za kweli za kimapenzi kwa Edna asingeweza kufika hatua hio bila ya kujali uhusiano wa Edna na Athena upo vipi.
Kila hatua aliopiga Athena ilikuwa ni kumfikisha mahali alipofikia siku hio.
Kuchukua uwezekano wa mwanaume ambae alikuwa ametabiriwa kuwa na nguvu ya kubadili mpango mkubwa wa ufufuaji wa kabila la miungu kwa kumfanya mmoja wao.

Bila shaka mtu wa kawaida angejua juu ya hilo pengine angesema Athena ana fanya vitu visivyo na maana kwasababu tu kwa uwezo wake pamoja na wa miungu kama wataungana ingekuwa rahisi kumuua Roma.
Lakini kwa miungu hao walikuwa wakifikiria tofauti na watu wa kawaida , walikuwa wamejaaliwa akili kubwa ndio maana hawakumhukumu Athena kwa maamuzi yake tokea mwanzo.
Waliamini hakuna kitu ambacho Athena alifanya na kikawa hakina msingi kwasababu kwao alikuwa ni mwanamke aaeona mbali kuliko wengine wote.
Lazima tu kutakuwa na taarifa ambayo hakufunuliwa kwa asilimia mia moja katika unabii aliopata kitu kilichomfanya kukaa chini na kuandaa ramani ndefu ya miaka mingi iliomhusisha Roma ili kumfikisha katika hatua hio.
Kwa lugha nyepesi ni kama unaweza kusema Athena alikuwa akishindana na unabii.
Miungu waliweka imani zao kwa asilimia mia moja kwa Athena na katika uhalisia alikuwa ameishi katika matarajio yao.
Roma alionekana hakuwa na hamu tena ya kupigana na ufufuo wa miungu umebakia kidogo tu kukamilika.
Mara baada ya Roma kumwangalia Athena kwa muda mrefu , muonekano wake ulibakia tunduwaza(Daze), kama kwamba alikuwa amepoteza nafsi yake.
“Kabla sijaondoka naomba nikuulize swali moja?”Aliongea Roma kinyonge.
Athena alionekana kama ametarajia nini angeuliza , kwa kuchezesha vidole vyake tu kifaa kilichofanana na taji rangi ya majivu ,kiinachong’aa kama kioo kilionekana katika mikono yake , lakini bado ajabu ule ukijivu wake ulijaa msisimko wa kifo.

“Unataka kujua nimewezaje kujificha kwako bila ya kuonyesha ishara yoyote ?, hili ndio jibu langu”Aliongea huku akimnyooshea Roma kile kifaa kama taji kuangalia kisha akaendelea kuongea.
“Hades wa zamani alinikubalia ombi langu nusu kufuata mipango yangu na ili kuonyesha dhati yake ndipo aliponitunuku ‘Helmet of invisibility’ na kisha kukutunuku wewe nusu ya uungu wake kama nilivyohitaji … hiki kitu unaweza kukiita kama Dhana iliowahi kuwepo yenye uwezo wa kificha kila kitu , labda tu nitake mtu kuona , ila kama sio hakuna mtu yoyote ambae anaweza kuniona wala kuhisi uwepo wangu na kuona sura yangu halisi”
Miungu walihuzunika mara baada ya kuona Helmeti hilo , waliamini Hades wa Zamani alijitoa kafara kwa ajili tu ya kufufua miungu.
Ukweli ni kwamba tokea mwanzo Hades hakuonyesha waziwazi alikuwa akikataa mpango wa kufufua ndugu zake , alichokuwa na wasiwasi nacho ni athari zitokanazo na mpango huo na alifuata yote akiamini katika unabii.
“Ndio maana haishangazi ..nakumbuka ulipoondoa uungu kutoka katika Hollygrail , kile kitabu cha teknolojia ya Thanatos na Jiwe la Kimungu ..sikuweza kuhisi kitu chochote ambacho hakikuwa sawa , kumbe kilichokuwa kikikulinda ni hio Siraha ya maajabu. Haha..”
Roma alijikuta akikumbuka nyakati zile ambazo Athena aliweza kunyakua Hollygrail mara baada ya mnada kuvuruugika , lakini vilevile alikumbuka namna ambavyo alipoteza kile kitabu cha Thanatos kule Ufaransa lakini pia jiwe la Kimungu nchini Tanzania.
Matukio yote hayo yalitokea katika kipindi ambacho hakuwa karibu na Edna , wakati ananyakua Hollygrail kutoka katika mikono ya vampire Moses, Edna alimuacha Mlimani City , wakati anapokonywa kitabu cha Thanatos, Edna alimuacha katika gari , wakati anapokonywa jiwe la Kimungu Edna alikuwa kazini.

Roma aliishia kutoa tabasamu lililojaa uchungu na kinyonge alijikuta akigeuka na kisha palepale akatoweka , akipotezea macho ya kila mmoja yaliokuwa yakimwangalia.
Kwa wale waliokuwa na macho ya kijini na yasiokuwa ya kawaida waliweza kumuona namna anavyopotea katika upeo wake na ilikuwa ni kama mgongo wake muda wowote utapeperushwa na upepo.
Athena nae aliangalia na kuishia kukunja ndita kidogo ashindwe kuongea neno lakini Aphrodite upande wake hakuweza kujizuia kutokuongea.
“Athena , aren’t you worried abour Hades?”Aliuliza akimwambia je hana wasiwasi juu ya Hades.
Athena alifumba macho yake na kuvuta pumzi nyingi kama kwamba anatafuta harufu mbaya na kisha akaongea:
“Anapaswa kuwa peke yake kwa sasa , hawezi kwenda kinyume na sisi tena”
“Hilo sio tatizo , ninachomaanisha je humjali tena?”Aliongea Aphrodite mwenye mawazo.
“Nani!!?”Alifungua macho yake.
“Kila kitu nilichofanya katika miaka elfu ishirini yote ni kufanikisha kufufua roho za wenzetu zilizopotea na kurudisha uzao wetu , huyu ndio mimi iwe anakubali au kukataa hakuna kitakachobadilika iwe leo au kesho”Aliongea kikauzu akiwa hana ishara ya hisia zozote juu ya aliomfanyia Roma.
“Wewe…”Aphrodite alitaka kuongea lakini alijikuta akipaliwa kutokana na hasira na aliishia kusema:
“Sitaki kupoteza pumzi zangu kwako”
Athena upande wake alionekana hakuwa na chochote cha kumwambia na macho yake yote yalikuwa yakiangalia uungu ambao unazaliwa juu ya Mti Mama, alionekana akiwa amepotelea katika mawazo na hakuna ambae alijua anafikiria nini.
Majini wale wa miliki za Hongmeng na Xia haraka sana na wao walikimbia mara baada ya kumuona Roma akiondoka.
Ukweli walioweza kushuhudia uliwayumbisha na wao na hawakutuhubutu kukaa hapo hata kwa sekunde , hawakutaka kufa kusiko kwa maana.
Kama majini ambao nyumbani kwao ni ulimwengu wa majini walikuwa na mawazo pia , hakuna aliewahi kutarajia miungu kumzidi nguvu Roma , tumaini la binadamu na wao lilikuwa katika kiganja cha mkono wa Athena.
Hakuna mtu jasiri duniani ambaye anaweza kufanya maamuzi ya haraka ya kuua mke wake au watoto wake hivyo ni kama walielewa kile Roma anachopitia.
Hatima ya binadamu ni kama ilionekana imejulikana na kifuatacho ni mwisho wake.
*****
Katika eneo la kujitegemea la anga lenye mandhari nzuri na ya kushangaza kulikuwa na kundi la watu pia waliokuwa wakiangalia kila kitu kilichokuwa kikitokea ncha ya kaskazini katika kitu kama kioo kilichokuwa mbele yao.
Pengine katika akili za kawaida mtu akikuambia kuna akhera au mbinguni usingeweza kumuelewa kutokana na kukosa uthibitisho lakini uwepo wa eneo hilo kama mtu angeingizwa hapo pengine angeweza kuamini.
Clark ambae alikuwa amekaa katika kiti cha jiwe alijikuta akiinuka kwa kurupuka mara baada ya kuona Athena alikuwa ni Edna.
Wakati huo alipoweza kuona namna hali aliokuwa nayo Roma mpenzi wake alijikuta akishindwa kujizuia na kuanza kulia kilio cha kwikwi huku akiwa ameficha uso wake.
Alikuwa akijua fika umuhimu wa Edna katika maisha ya Roma na uzito wake katika moyo wake .
Katika ulimwengu huu maumivu makali sana yanayoweza kumpata mtu ni pale unapoumizwa na mtu uliempenda sana.
Ilikuwa ni kama Clark anahisi maumivu anayopitia Roma ndani ya moyo wake , ilikuwa ikiuma sana kwake na hakupata picha alichokuwa akipitia mpenzi wake.
Mara baada ya kumpiga macho Athena Chuki kali iliibuka katika macho yake.
Upande mwingine Sharif na wenzake walionekana walikuwa wakiujua ukweli muda mrefu sana na Aoiline ambae ni kama ndio kwanza anafahamu alionekana kutoshangaa,.
“Huyu kijana ni mjinga kukimbia”Aliongea Sharif asieleweke hisia zake zipoje kwani hakuonyesha ishara yoyote.
“Unadhani kila mtu ni kama wewe ambae unajikuta mkatili kwa unao wapenda? , watu wote sio kama wewe kuweza kuondoa hisia na mawazo kwa haraka yawe mazuri au mabaya”Aliongea Aoiline huku akimwangalia Sharif kwa macho ya dhihaka na Sharif hakujali dhihaka zake.
“Nilitarajia hili hata hivyo tokea mwanzo. Kuipita changamoto ya namna hii sio lelemama na niliweza kujua haya yote kutoka kwa barua walioacha Wajumbe wa mkuu wa Enzi katika mnara ndio nikaelewa kila kitu , hata hivyo usijali , nitamfuata mwenyewe , matumaini yangu ni kutokukuharibu nguvu zake kubwa”Aliongea Sharif.
“Master , awamu hii Hephaestus amefanikiwa kuzima nguvu ya safu ya ulinzi hivyo haitochukua muda mrefu Zeus kutoka pamoja na kundi la roho za majini wabaya , kama Roma ataendelea kusita sita kama hivi kuwashughulikia miungu , kwanini tusianze kuimarisha hali ili majini wasije kugeuza dunia kuwa kuzimu?”Aliongea Mzee Yasu.
“Kama Roma hatarudiwa na akili zake inamaanisha kwamba ni kudra za Mkuu wa enzi juu ya binadamu kutofanikiwa kuepuka hili janga , haileti tofauti iwe ni sasa au baadae , au ni majeruhi wachache au wengi, lakini kama unataka kuingilia unaweza kwenda , majini pepo wabaya wa zamani sio kama wanyama wakali tena , ni mizimu yao tu iliobakia katika nguvu kidogo, wanaweza kuwadhuru binadamu lakini sio majini watu”Aliongea Sharif.
Yasu na Xumei walijikuta wakishangaa , Sharif hakuwepo katika kundi la wanafunzi hao na haikueleweka alienda wapi.
Licha ya kujua Master wao hakuwahi kujali uhai wa binadamu lakini hawakuwahi kuwaza angeonekana kutojali kabisa.
Lakinni hata hivyo haikumaanisha Sharif alikuwa mtu mbaya , ilikuwa ni kwamba katika ulimwengu huu hakuna kitu kama Uovu na wema , kila kiumbe kilichopo katika uso wa dunia kina maana na sababu juu ya uwepo wake na isitoshe alikuwa ni kama ishara ya muunganiko wake na binadamu lakini vilevile alikuwa ishara ya muunganiko wake na Wajumbe wa Mkuu wa enzi.
“Sharif naona unawaogopesha wanafuzi wako , hehe.. wamekuwa pamoja na wewe kwa miaka elfu mbili lakini bado hawakufahamu vizuri, hawatokuwa na uvumilivu zaidi kama utaendelea kuongea maneno mengi ambayo ni kinyume na ulimwengu”Aliongea Aoilie huku akicheka kishambenga.
Sharif na yeye alicheka lakini hakuwa na nia ya kuelezea zaidi na kilichowapata ni upepo tu kwani alipotea palepale.

SEHEMU YA 785.
Kitendo cha Sharif kupotea katika eneo hilo kioo kilichokuwa mbele yao kilichokuwa kikionyesha kiachoendelea katika ncha ya Kaskazini kilipotea pia kana kwamba hakikuwepo kabla.
Clark ambae alikuwa kimya muda wote ghafla tu alimpigia magoti Aoiline huku macho yake yakiwa mekundu.
Aoiline macho yake yalimsinyaa kutokana na kitendo cha Clark na alimwangalia kwa tabasamu lililojaa uchokozi.
“Msichana unafanya nini?”Aliuliza.
“Najua unao uwezo wa kunitoa hapa na kunipeleka katika ulimwengu wa kawaida …”Clark alisaga meno , chuki aliokuwa nayo wakati huo ilikuwa ni ngumu kujificha.
Aoiline mrembo huyo wa kimaajabu alishika unywele wake na kuuzungusha kwa aina isioelezeka huku akiwa na tabasamu pana la kutojali chochote.
“Je ni kweli unao uwezo wa kubadilisha hali yote inayoendelea huko nje na uwezo wako?”
“Mimi sijui, lakini sijawahi kumuona akiwa katika majonzi namna ile tokea nimjue , nashindwa hata kudhania ni kiasi gani cha maumivu anachopitia , anatia sana huruma nashindwa kujizuia kulia kwa ajili yake”
“Uwezo wa kukutoa hapa ninao lakini sitofanya hivyo..”
“Kwanini?, Haupo upande wa Roma?”Aliuliza Clark kwa mshangao maana aliamini Aoiline na Roma ni marafiki na angemjali kwa kile anachopitia.

“Napendeea kuamini mpenzi wako ataweza kukabiliana na hatima yake yeye mwenyewe tokea nilipokubaliana na mipango yote ya Sharif, hivyo sitofanya mambo kinyume , hii ni imani niliokuwa nayo zidi yangu mwenyewe na ambayo ninayo zidi ya Roma”Aliongea Aoiline mara baada ya kutingisha kichwa.
Anaweza kuwa katika upande wa Roma lakini anataka apate ufumbuzi wa matatizo yake mwenyewe bila ya msaada wa nje.
Mara baada ya kuona usiriasi aliokuwa nao machoni kwake alijikuta akinywea na kuinamisha kichwa chake chini na kukaa kimya.
****
Upande mwingine ni masaa machache tokea kikao kizito kumalizika nchini Tanzania , kikao hiki kilikuwa kimeongozwa na Shekhe Idris kiongozi wa hadhi wa Ant- Illuminat..
Ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni juu ya mchoro wa unabii , kila mmoja ambae alihudhuria kikao hicho alikuwa katika hali ya kuhamanika pengine yote hayo yametokana na juu ya ukweli waliokuwa wameusubiria kwa muda mrefu sana.
Haikuwa hivyo tu kwa wanachama hao wa umoja huo bali vilevile kikao kingine kilifanyika jijini Nairobi kilichowakutanisha wanachama wote wa Hadhi ya juu wa Zeros Organisation , kikao hicho kilifuatana na kile cha umoja wa kimataifa kitakachoongozwa na Katibu mkuu wake Clelia Allisanto.
Katika kikao cha Zeros wanachama wote wa ngazi za juu kutoka jamii nyingi za siri na viongozi wakubwa wa mataifa yalioendelea walionekana kuwa na sura zilizokuwa zikifanana na zile za waachama wa Umoja wa Ant-Illuminat.
Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema wanachama wa umoja wa Illuminat walikuwa sawa kimuonekano na wanachama walewale wanaoenda kinyume na wao yaani Ant- Illuminat.
Swali ni moja tu je ni Ajenda zinazofanana zimejadiliwa katika vikao hivyo , swali hilo lilikuwa gumu kujibika mara moja kutokana na usiri uliokuwepo kati ya kikao cha Dar es salaam na kikao cha Nairobi.
Lakini kitu kimoja ambacho pengine kilionekana kuwa cha tofauti baina ya sura za watu hio ni kama kulikuwa na hali ya tumaini katika nyuso zao.
Ni dakika chache katika kuhitimika kwa kikao hicho , yaani wakati wa kikao cha Umoja wa mataifa kikianza moja ya tukio kubwa ambalo lilikuwa likitarajiwa ni juu ya kiongozi mkuu wa The Holly See kuongea kupitia Vidio call katika mwanzo wa kikao hicho.
Jambo hili pengine ni la kawaida kwani licha ya kiongozi huyo kukosa haki ya sheria ya kura katika baraza la Umoja lakini alikuwa na cheo cha uangalizi na maoni yake yalikuwa yakisikilizwa.
Tokea dunia ianze kuingia katika hali ya hatari ya kupotea kwa kiumbe binadamu Kiongozi huyo hakutoa msisimamo wake juu ya kile kinachoendelea wala maoni yoyote , ki ufupi ni kwamba hakujitokeza hadharani licha ya kwamba kwa siri sana , taarifa ambazo hazikuwa wazi baadhi ya wanajaeshi wake walikuwa wakishiriki katika ujenzi wa Safina huko nchini Ethiopia.
Sasa kwa mara ya kwanza Kiongozi huyo anajitokeza na mara hio ya kwanza ni katika kikao cha cha umoja ambacho ni cha mwisho kufanyika kitakachohusiana na namna ya kuokoa binadamu.
Kati ya watu ambao hawakuwa na shauku ya kujua kinachokwenda kuzunguzwa na kiongozi huyo ni Mheshimiwa Barack Mabo , hakuwa na shauku kwasababu alikuwa akitarajia kile ambacho kitasemwa.
Wakati mengi yakiendelea yeye pia alikuwa jijini Nairobi huku akijinasibu ni wa asili ya nchi hio lakini kwa siri na yeye alikuwa na mipango yake.
Na hakuwa na siku moja wala mbili alizokuwepo nchini hapo , ukweli ni kwamba ilijulikana kwa wengi alikuwa Nchini Narobi na familia yake lakini mara nyingi na kwa siri alionekana nchini Tanzania huku akijitahidi kuweka ukaribu na familia ya Kweka , yaani familia anayotokea Roma ilikuwa ni kama vile alikuwa akitaka kujua kinachoendelea mara baada ya kurudi kwa Roma.
Alikuwa na taarifa hizo lakini hakuwa na mwendelezo wa taarifa ya kila siku ya juu ya kile anachokifanya Roma kwa ajili ya kuokoa binadamu, haikuwa kwake tu pengine kwa viongozi wote walipata taarifa za kile kinachoendelea katika maisha ya Roma.
Akiwa ndani ya Hoteli kubwa simu yake ya mkononi iliita na kwa papara sana alipokea mara baada ya kuona namba ya mpigaji.
“Mheshimiwa nilikuwa nikisubiria simu yako kwa hamu kubwa”Aliongea yeye kabla wa upande wa pili hajaongea lakini licha ya hivyo upande wa pili ni kama alikuwa akisikia pumzi ya mtu pasipo neno.
“Barack wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na sipendi kukuficha , taarifa zilizonifikia si nzuri hata kidogo juu ya hatima ya kila mtu, nimepokea taarifa nzuri na mbaya ndani ya mpishano wa dakika sabini”.
Mara baada ya kauli hio Mheshimiwa Barack licha ya kuonyesha hamaniko lakini bado hamu yake ya kujua anacholenga mpiga simu haikumtoka.
“Nakusikiliza Shii..”Aliongea kwa sauti hio ikionekana kutaja jina lenye kusikika Kimandari.
“Roma alierejesha tumaini letu ndani ya dakika themannini zilizopita amegeuka na kuturudisha mwanzo mwa mioyo yenye wasiwasi mara baada ya kuona sura ya Adui yake mkubwa”Aliongea upande wa pili kwa kingereza kilichosikika sio cha kuzaliwa bali cha kujifunza kutokana na rafudhi.
“Naamini kashafanikiwa kuona sura ya Athena , lakini swala hili linaingiliana vipi na Adui”Aliuliza Barrack lakini licha ya swali lake alionekaa kuwa katika hali ya kawaida.
“Ni kama ilivyotarajiwa Barrack, hii ni taarifa yangu ya mwisho ya kuwa chanzo cha taarifa za kile kinachoendelea kwako”Mara baada ya kauli hio simu ile ilikatwa.
Barrack aliangalia jina la Xi likipotea katika simu yake na tofauti na kuwa na wasiwasi alionekana kuwa mwenye kufikiria na hazikuchukua dakika hata moja alifungua app ya simu na kisha alionekana kuingiza namba flani na ndani ya sekunde ileile aliweka sikioni.
“Diana nadhani una majibu juu ya kazi niliokupatia?”Aliongea Barrack.
“Amesema kuna utofauti katika muonekano wa picha mheshimiwa”Aliongea kwa lugha ya kingereza.
“Unataka kumaanisha nini kusema hivyo?”
“Ni mjuzi wa hali ya juu katika kukumbuka taarifa ndogo ndogo alizoziona mara moja tu na kuziweka katika mchoro , nimekutumia faili mheshimiwa Mstaafu”Sauti ya mwanamke aliefahamika kwa jina la Diana aliongea na hata hakuongea neno zaidi, Mheshimiwa alizama upande wa eneo la ishara ya taarifa zilizoingia katika app hio hio iliotengeezwa kwa teknolojia ya ‘BlockChain’ kwa ajili ya maswala ya ki ulinzi.
Dakika ileile kioo cha simu yake kilijaa faili ambalo lipo katika mfumo wa picha na alikodoa macho kusoma kila taarifa inayoonekana katika picha hio.
Picha ile ni ileile ambayo alionekana Athena akimuonyesha msichana mdogo Naira alietokana na Proiect Pro Human katika bara la barafu ncha ya Kusini mwa dunia.
Picha ya unabii unaweza kuiita hivyo , ni picha ambayo humuonyesha mwanamke aliekalia kiti cha kimalkia huku akionyesha tabasamu na chini yake kuna wenye kumuonyeshea heshima kwa namna ya kumsujudia.
“Kila ninachofanya ni kuhakikisha tabasamu la huyu mwanamke halikauki”Pengine ndio kitu cha pili yake kukumbuka kabla hata ya kuanza kuchora picha hio.
Naam kwasababu ni mtu mmoja tu alieonyeshwa picha hio basi moja kwa moja tunamjua ni Naira na hii inatuongezea kuamini kutokana na mwanamke Diana aliekuwa kwenye simu na Mheshimiwa Barrack Mabo.
Mheshimiwa huyo alionekana kuongea mwenyewe katika nafsi yake lakini simu mbili zilizoingia mfululizo zilimfanya aache kuyakiminika katika faili hilo na kugeuza sura yake kwa simu zinazoingia.
Moja ilikuwa ni ya Shekh Idriss na nyingine ilikuwa ni kutoka kwa Clellia na ilimfanya Mheshimiwa kuonyesha tabasamu .
“Katika nyakati kama hizi ndio umuhimu wangu huonekana baada ya kuwa mstaafu”Alijiwazia na akapokea kwanza ya Clelia.
“Ni Tofauti na mchoro wa Unabii Clellia, maelezo yako yanafanana na ya Naira wote mmedanganywa na Athena”Aliongea Mheshimiwa na upande wa pili haukuongea sana na simu ilikatwa na palepale aligeukia mtu mwingine aliekuwa akimpigia.
“Idriss nadhani haina haja ya kunipigia ilihali Ajenda katika vikao vyote zilikuwa sawa”Aliongea Mheshimiwa huku akivuta glass ya mvinyo na kuketi kwenye sofa.
“Sijataka kujua taarifa ya kikao cha jumii yenu , katika nyakati hizi ni rahisi kupata taarifa katika kipindi cha utulivu”
“Kama ni hivyo ni taarifa ipi unataka kutoka kwangu, nje ya mkataba wetu?”
“Uthibitisho wa unabii”
“Unabii wa picha alioonyesha Athena ni tofauti na Unabii uliowakilishwa kwetu leo na Vatican, maelezo ya Clellia Allisanto na Naira yanafanana”Aliongea , ilionekana hakuwa na haja ya kumficha tena Idriss.
Ukweli ni kwamba licha ya kuwa na nia nzuri ya kujiingiza katika jamii zote mbili na kuwa mwanachama alifanya yote hayo kwa ajili ya kujitengenezea thamani.
Kiongozi huyo alikuwa tofauti na maraisi wengine wastaafu , wakati wao wakijilimbikizia mali yeye hakupenda uthamani wake kutafsiriwa na kiasi cha pesa bali siri anazobeba ndio maana alijitahidi kujijengea Koneksheni na watu wenye kumweleza taarifa na sio wenye kumpa utajiri, moja ya watu hao ni Raisi wa China ambae alikuwa na muunganniko mkubwa na majini kutokana na kwamba alitawala nyuma yake wakiwepo jamii ya Hongmeng.
Sasa taarifa za Roma kukimbia uwanja wa mapambano ndio alizoweza kusikia kutoka kwa mtu alieitwa Shii yaani Xi ambae alionekana ni rafiki yake kulingana na namna walivyoongea.
Raisi huyo mstaafu ni moja ya wanachama wa Hadhi waliohudhuria kikao cha Zeros ambapo moja kwa moja ungesema ni kikao cha Illuminat kutokana na jamii hio kuwa na nguvu katika umoja huo.
Mheshimiwa alimuelezea namna mchoro ulivyokuwa na kwa maelezo yake ilionekana tofauti ya mchoro huo haikuwa kubwa picha waliopewa mwanamke hana tabasamu na mbele yake hakukuwa na wenye kumsujudia , alikuwa ni kama Malkia asie na taifa la kutawala lakini licha ya hivyo alionekana hajanuna bali alikuwa ameridhika huku macho yake yakimwangalia mwanaume aliekuwa mita kadhaa kulia kwake , ndio mtu pekee alieonekana katika mchoro.
Haikuwa rahisi kutafsiri mchoro huo kama unavyosemekana ni wa kinabii lakini pengine watu wenye maarifa wangeweza kuuelezea.
Picha nyingine ambayo ni kulingana na maelezo ya Clelia na Naira, picha ilionekana mwanamke akitabasamu lakini mwanaume aliemfanya mwanamke kuridhika katika picha ya mwanzo hakuonekana katika picha hio.
“Idriss leo nimekuwa mtiifu kwako tokea nilipofahamu wewe ni moja wapo ya walinzi wa dunia”Aliongea Barrack.
“Haibadilishi kitu juu ya wasifu wangu , hii ni simu yangu ya mwisho kwako” na simu palepale ilikatwa lakini Barack Mabo hakuonyesha kubadilika.
“Ni muda wa kujiongezea ushawishi juu ya jambo hili , ni muda wa kurejea nchini kwangu kueneza maneno ya ujasiri”Aliwaza na kisha palepale aliwasha runinga.
Kwa namna moja alionekana kufurahishwa na matokeo , picha mbili za unabii zinazotofautiana ni kama zilimpa furaha.
“Hii ndio ilikuwa sababu tokea mwanzo nilishindwa kumuua huyu msichana licha ya kuwa ndani ya taifa dogo kama Tanzania, alikuwa ni kila kitu ya kila kinachoendelea”Aliongea mwenyewe na ni kama alionekana kukumbuka nyakati zake za uongozi alivyotoa maelekezo ya Edna kufa kwa ajili ya kulinda siri ya Mpango LADO.

*******
DAR ES SALAAM SIKU SABA MBELE.(Seven days later in Dar es Saalam)
Hali ya hewa ndani ya jiji la Dar es salaam haikuwa mbaya sana , joto bado lilikuwa la kawaida na halikuwa limevuka nyuzi joto sifuri lakini lilikuwa la chini sana kuvunja rekodi..
Serikali ya Tanzania ilikuwa imetuliza ghasia zote ambazo zilitokea ndani ya jiji hilo na sasa hali ya amani ilikuwa imerejea lakini hata hivyo haikuwa kama siku za kawaida kwani wanajeshi wengi pamoja na polisi walikuwa kila mtaa kuhakikisha hakuna uhalifu wowote.
Kitu pekee ambacho raia waliongeza umakini nacho ni kuingia katika nyumba za ibada , haikuwa kwa waislamu wala wakristo kila mwananchi alionyesha jitihada za kuhudhuria ibada kulingana na ratiba za dini yake , hata wale ambao hawakujua milango ya nyumba za ibada walikuwa watiifu kuhudhuria kwa wakati pengine kuzidi hata wale ambao walikuwa ni wahudhuriaji wazuri.
Kila mtu aliekuwa na nia yake , wengine ilikuwa ni hofu ya kile kinachoendelea wengine waliamini katika unyakuo.
Ijapokuwa jiji hili halikuwa na baridi kali kama maeneo mengine lakini ukweli ni kwamba kulikuwa na baridi ambayo ilifanya watu wajifungie ndani, yaani kitu pekee ambacho hakikuonekana baadhi ya jiji hilo ni kama mvua ya theluji tu ambayo ilipatikana katika maeneo ya nyanda za juu.
Sasa moja ya sehemu ambazo zilikuwa hazina watu ni ndani ya hoteli ya JR mita kadhaa inapopatikana Club B.
Ilikuwa ni kama vile wenye hoteli yao walikuwa wamfukuza wagenni ndani ya hoteli hio kwani hakuonekana mtu ndani ya eneo la Bar kama ilivyozoeleka.
Katika kona ya eneo hilo alionekana mwanaume ambaye alikuwa na mavazi ambayo hayakuwa katika mkao mzuri , ilikuwa ngumu kusema mtu huyo alikuwa ni masikini kutokana na muonekano wake lakini ni rahisi kusema mtu huyo hakuwa katika hali nzuri ya kimawazo yaani kama kichaa kwa namna anavyogugumia chupa za bia huku mbele yake zikitawanyika chupa tupu.
Alikunywa kimimiika chote kilichokuwa kwenye chupa kwa pupa kama mtu anaelazimisha kulewa na mpaka aliposhusha chupa ile aliishia kucheua na muda huo alikuwa ni kama mtu wa kawaida tena mbele ya macho ya mtu anaemfahamu.
Alikuwa ni Roma ambae amerudi Dar mara baada ya kuzurula kwa siku mbili mfululizo katika maeneo ambayo hayakufahamika , alikuwa amechafuka mno.
Eneo alilokaa lilikuwa ni lile lile ambalo aliweza kukutana na mwanamke mrembo Edna kwa mara ya kwanza akimdhania ni kahaba.
Muda ulikuwa umeenda na mazingira yalikuwa yamebadilika lakini kumbukumbu za eneo hilo kwao hazikuweza kubadilika , zilikuwa kumbukumbu za kupuuza lakini tamu kwa wakati mmoja.
Lakini wakati huo kwa Roma eneo hilo alilichukulia kama sehemu ambayo ndio mwanzo mwa udanganyifu.
Roma alikuwa ametumia Dhana ya jani la upofu kubadili sura yake ili aonekane tofauti pamoja na kuficha uwezo wake , kwani hakutaka usumbufu wa mtu yoyote wala kuonana na mtu yoyoyote.
Yeye mwenyewe ndio alikuwa mhudumu na vinywaji kwani aliinuka na kuchukua vinywaji na kurudi navyo na kisha kuendeleza kazi , ilikuwa ni kama alitaka kukaa kama mlevi maisha yake yote.
Eneo hili ukweli ni kwamba halikuwa na watu sio kwasababu ya kukosa wateja bali hoteli hio ilifungwa kutokana na hali ya ki usalama wa jengo lenyewe kwani kulitokea mtitio wa ardhi mita kadhaa kutoka ulipo msingi wa jengo na ishara za ufa wa hoteli hio ndio ulifanya hoteli hio ifungwe kwa muda.
Roma muda huo alitamani angekuwa binadamu wa kawaida ili alewe kiasi kwamba asielewe hata kinachomtokea katika mazingira ya kawaida pengine kufa kabisa maumivu yampotee.
Lakini kila mara sura ya Lanlan na familia yake ilipokuja katika fahamu zake alitaka kuishi lakini bado aliona kuishi ni kubaya zaidi ya kifo.
Eneo hilo lilikuwa kimya mno na hakuna mtu ambae anaweza kumuona Roma aliejikalia kwenye kona kama angeingia ndani ya eneo hilo kutokana na giza na alikaa hapo kwa muda mrefu sana kama binadamu aliekosa tumaini kabisa.
Ikiwa ni katikati ya mchana siku ya saba tokea kupatwa na Janga la moyo na siku tao tokea aingie ndani ya jengo hilo kivuli cha mtu alievalia kanzu kilionekana ndani ya eneo hilo akitembea kwa hatua hafifu kumsogelea Roma.
Roma aliekuwa amelala kwenye Sofa ilikuwa ni kama vile hajamuona mtu huyo , ki ufupi ni kwamba hakujali ni mtu au ni mzimu wa mtu.
Mtu yule alisogea mpaka kwenye Sofa alilolala Roma na alisimama bila ya kuongea neno kwa dakika kadhaa na mara baada ya kuona Roma hakuwa na nia ya kuamka aliishia kutoa tabasamu lililojaa wasiwasi.
“Mbona unakuwa mjinga , umekutana na yule mwanamke kwa muda mchache sana kama ilivyo kwa kumbukumbu zako juu yake , haina haja ya kung’ang’ania juu ya swala dogo namna hii”Aliongea Sharif kama vile ni baba anaejaribu kumfokea mtoto.
Roma alijigeuza kwenye sofa lile na kugeukia upande mwingine huku akijjikunyata.
“Potea mbele yangu”Roma aliongea na hakuonekana kutaka kuongea neno lingine zaidi.
Sharif au Master namba moja hakufanya chochote zaidi ya kutabasamu , ilionekana Roma hakuwa amelewa licha ya kwamba alionekana kama mlevi , hivyo hata kama hajajitambulisha yeye ni nani ilionekana Roma ashamtambua tayari.
Ki uhaisia haikuwa ngumu hata kujua uwezo wa Sharif kwani Roma alikuwa ametumia Dhana ya jani la upofu na kama Sharif angekuwa na uwezo mdogo asingeweza kumpata Roma kirahisi.
Sharif hakujali ujeuri wa Roma , ukweli ni kwamba hakujali kabisa namna watu wanavyomchukulia na aliishia kutingisha kichwa na kisha aliketi kwenye sofa kando ya Roma.
“Kama methali zinavyosema, mtu na asivutiwe na sura tu bali aone ukweli ndani ya moyo , vilevile mtu asifungwe na ukweli wa moyo na hata aikatae sura”Aliongea Sharif.
“Nimesema Ondoka”Roma aliongea huku akionyesha hali ya kukereka , hakujali Sharif alikuwa na nguvu kiasi gani na alikuwa na nani bali hakutaka kuonana na mtu yoyote yule.
ITAENDELEA
Hakika Ni kazi nzuri sana
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.
MTUNZI: SINGANOJR .
Mono no Aware

SEHEMU YA 786.
Roma sauti yake ilionekana kubadilika na kuonyesha zaidi hali ya kukasirika mara baada ya kuona anasumbuliwa na Sharif.
Alijiambia anaongea nini huyo na methali zake, muonekano ?, ukweli wa moyo?, Kama angekuwa mtu wa dini na angeambiwa aelezee upendo na chuki na yeye angejiuliza swali kama vyote hivyo vipo kweli kwanini ana mahusiano mengi na mikwamo mingi.
Sharif alijikuta akibakia mdomo wazi na aliona ni kama ujinga kwani kijana mdogo kama huyo ndio kwanza yupo kwenye miaka ishirini kuelekea therathini na licha ya kuwa na uwezo usio na mipaka bado ni mtoto tu na kama ataongea kwa namna anavyongea na Aoiline basi anaweza asimsikilize.
Kuhusu Roma kumwambia aondoke wala hakujali sana na mara baada ya kuwaza kwa akika kadhaa alionekana kuwaza kitu na kutingisha kichwa chake kwa mara nyingine.
“Kulingana na utafiti wa kibinadamu juu ya dunia ya kale , Kimondo chenye uzito wa zaidi ya tani trilioni moja kilidondoka duniani miaka milioni sitini na tano iliopita , spidi ya kimondo hiki inakadiriwa kuwa zaidi ya kilomita elfu themanini na tano kwa saa na nguvu yake ni sawa na kulipua vichwa milioni therathini vya mabomu ya nyuklia kwa wakati mmoja, Binadamu wanaweza wasielewe hili lakini kuna uwezekano wa aina ya kimondo cha namna hio kuigonga dunia kila baada ya miaka milionni kumi na kuharibu kabisa sayari ya Dunia , vilevile vimondo vya ukubwa wa wastani upande vinaweza pia kudondoka duniani muda wowote.
Ni miaka elfu hamsini tu iliopita wakati dunia iliopoingia katika vita kali ya majini na binadamu mpaka Wajumbe wa Mkuu wa Enzi kuingilia kati, kipindi hiki ndio wakati ambao Kimondo kilidondoka eneo la jangwa eneo ambalo sasa ni sehemu ya taifa la Marekani , jimbo la Arizona , baada ya kimondo hiki kufika ardhini kilirusha mawe tani milioni mia saba sabini na tano kwenda angani na kutengeneza shimo kubwa ambalo lilikuwa na upanda wa takribani kilomita saba na mita zaidi ya mia kwenda chini , sehemu hii ndio leo hii hufahamika kwa jina la Bariger Crater.
Wakati huo hiki kimondo kilikuwa na ukubwa futi mia tatu therathii ambazo ni sawa na ndege za sasa , baada ya kudondoka kilisababisha joto zaidi ya nyuzi 1600 , joto ambalo liliyeyusha mawe , mchanga na takataka zilisafiri kwa umbali maili sita kwa spidi mara tatu ya risasi , na kwa spidi hio watu wote wlaiokuwa karibu pamoja na wanyama miili yao ilitobolewa na kuvunjika mifupa hata pasipo ya kujua”
Sharif aliongea muda mrefu na haikueleweka alikuwa akielekea wapi katika mazungumzo yake lakini habari hizo zilimfanya Roma asimwambie andoke.
Roma taratibu sana alijinyanya na kukaa kitando na kisha akamwangalia Sharif ambaye alikuwa na uso uliopambwa na tabasamu.
“Ni kitu gani lakini ambacho unakusudia kusema kwa stori yako hii?”\Aliuliza Roma.
“Naona hatimae umevutiwa na kile ambacho nakusudia kuongea, si ndio?”Aliuliza Sharif.
“Kama sio kwasababu ya wewe kuwahi kuniokoa , ningepigana na wewe hata kama ilimaanisha sikuwezi”Aliongea Roma huku sauti yake ikiwa na hali ya mikwaruzo huku akimwangalia Sharif kwa macho makali kama vile ni mbwa mwitu.
“Oh!Umejuaje niliwahi kukuokoa?”Aliuliza Sharif.
“Wakati Yan Buwen alipofanikiwa kuunganisha nishati ya Ant Matter na mwili wake na kupambana nae, ilikuwa ni wewe ambae ulitawala mwili wangu na kutengeneza radi ya Zambarau na haikuwa mara moja , ijapokuwa sauti yako imebadilika lakini siwezi kusahau namna nilivyokuwa nikisikia sauti yako katika akili yangu , kama sijakosea ni wewe pia uliemfana yule mzee kumteka Clark , Wewe ndio Master namba moja”Aliongea Roma na kumfanya Sharif kutingisha kichwa.
“Naona hujalewa na hii inamaanisha hujakata tamaa bado”
“Ninaweza kuwa ziadi ya unavyowaza”Aliongea Roma na palepale alitawanyisha chupa za bia ambazo zilikuwa kwenye meza na mara baada ya kupata iliokuwa na kinywaji aligida yote kiasi kwamba ilimfanya hata kumwagikia kwenye kifua chake lakini hakujali.
“Haha..nini kingine ambacho unajua kuhusu mimi , kwanini usiongee nikakusikiliza?”Aliongea Sharif huku akimwangalia Roma na matarajio.
Roma alicheua kwanza kinywaji alichokunywa kwa pupa na kisha macho yake yalisinyaa kana kwamba alikuwa amelewa.
“Kama nipo sahihi , wewe utakuwa mtu ambae Aoiline alikuwa akizungumzia , wakati nilipokuwa katika ulimwengu wa majini pepo alisema nilikuwa nikifanana kwa kiasi flani na mtu mmoja na alimfikiria huyo mtu mara baada ya mimi kutumbia mbinu ya Andiko la urejesho wa Azimio , hii inamaanisha ni mtu anaetumia mbinu kama yangu”
“Mtaalamu ambae anaweza kumfanya Aoiline kumfikiria lazima atakuwa na nguvu kuliko mii na kwako wewe kuweza kudhibiti mwili wangu kwa kuuazima na kisha kuita radi ya mapigo tisini na tisa bila ridhaa yangu , huyo mtu lazima atakuwa ni wewe.
Aoiline ni jini mtaalamu wa kihistoria ambae aliingia katika ulimwengu wa majini pepo miaka elfu hamsini iliopita , kwa umri wako lazima angalau utakuwa unalinfana nae au umemzidi kidogo , kama wewe ni mtu ambae unaweza kupambana nae au kumshinda kabisa basi lazima utakuwa angalau katika levo ya mapigo elfu tisa tisini na tisa ya radi , zaidi ya yote na uelewa wako wa mbinu ya Andiko la urejesho wa azimio basi kuna uwezekano mkubwa wewe ndio mtu wa kwanza kutumia mbinu hii kama sio kuigundua na kama ni hivyo basi isingewezekana kwa namna yoyote kumshindwa Zeus na Athena miaka elfu ishirini iliopita wakati wanafika duniani , kuna uwezekano wa aina mbili , mosi kuna uwezekano hukushiriki vita ya miungu na majini , pili uliwaacha moiungu wote kumi na mbili makusudi kabisa licha ya kwamba ulkikuwa na uwezo wa kuwaua wote..”
Macho ya Sharif yalichanua kadri ambavyo Roma alikuwa akiongea na aliishia kutingisha kichwa hapa na pale huku akiwa na tabasamu la ajabu usoni mwake.
“Ndani ya ulimwengu wa majini watu niliweza kupata kopi ya andiko la urejesho wa Azimio lakini jina lilikuwa tofauti , kama mawazo yangu yapo sahihi basi kuna uwezekano hii mbinu ilisambazwa kwa viumbe wote wa dunia wanao onekana na wasio onekana kwasababu maalumu ya kumtafuta mtu ambae anaweza kujua siri yake”
“Mtu alietengeneza Andiko hili alijua vizuri nguvu yake ,lakini licha ya hivyo kauonyesha kujali kama watu au viumbe wabaya kujifunza na hili linanipa jibu kwamba mgunduzi alikuwa akijua vizuri kabisa ni ngumu mo kwa viumbe kujifunza mbinu hii kutokana na ugumu wake lakini aliishi katika tumaini siku moja itatokea mtu ambae ataweza kujifunza na kupita levo zote”Roma aliendelea kuongea na akaendelea.
“Na hili ndio ambalo lilifanya mbinu hii kujulikana kwa majina tofauti tofauti kati ya binadamu na viumbe wasioonekana na haya yote ni kwa ajili ya kupata mrithi ambae atafikia juu kabisa mwa levo zote ili kutimiza lengo flani , kama nilichootea kipo sahihi basi sababu inayokufanya kuwa mbele yangu saa hii ni kwasababu mimi ndio kiumbe pekee niliefanikiwa kuzijua siri zote za andiko la urejesho na kuyafkia mafannikio , binadamu ambae unapanga kumchagua …”
“Paah ! Paah!!”Sharif alijitkuta akipiga makofi kwa nguvu mara mbili huku akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake.
“Sio mbaya , katika sehemu zote ulizoongea umepatia , hii mbinu licha ya kwamba sijaigundua mimi lakini imechukua nguvu zangu nyingi kuielewa juu ya siri zake na hata kuirahisisha jina ambalo uliipatia mbinu hii ndio jiina hilo hilo ambalo mbinu hii inafahamika, Andiko la Urejesho waAzimio”
“Tofauti kubwa kati ya mbinu zote za kuvuna nishati za mbingu na ardhi na nyingine zote zinazotumiwa na viumbe wa aina zote wenye nguvu ni kwamba mbinu nyingine zinamtengenezea mvunaji njia ya kupita na hatimae kufikia mwisho na kupata ufunuo mpana , lakini mbinu ya Andiko la urejesho wa Azimio inamuonesha Mvunaji kwanza mwisho wa safari ulivyo kabal ya kuianza safari na njia ambayo mtu atatumia kupita mpaka kufikia huo mwisho alioona ni juu yake yeye mwenyewe kuitafuta , ki ufupi ni kwamba ni aidha kupata mafanikio katika hatua ya kwanza au kutumia maisha yao yote kujaribu kusiku kwa faida”
“Katika kipindi cha miaka elfu kumi yote kulikuwa na baadhi ya watu wachache sana tena binadamu ambao waliweza kufanikiwa kujua maana ya Andiko hili ni nini lakini nikiwalinganisha na wewe umewaacha mbali mno , Mastar wako Tang Chi alipata mafanikio ya juu juu ila huwezi kumlinganisha na wewe”Aliongea Sharif lakini Roma hakuonyesha ishara ya furaha wala huzuni.
“Hebu acha kuzunguka zunguka , ni ipi nia yako kamili kwa kufanya na kuongea haya yote?”Aliuliza Roma akiwa siriasi.
“Je unajua ni vimondo na magimba mangapi yanatosha kuharibu uhai wa dunia ambayo yameweza kuikaribia dunia katika miaka elfu hamsini iliopita?”Aliuliza.
“Wewe si umesema mwenye ni kila baada ya miaka milioni kumi”
“Hio ni nadharia tu , ni kama hesabu za Probability na uwezekano huo ni mdogo , lakini haiondoi uwezekano wa magimba na vimondo kuipiga dunia katika kipindi cha muda mfupi tu , kati ya miaka elfu hamsini iliopita na sasa , kimondo kilichosababisha Barringer Crater kuna kubwa zaidi angalau mara ishirini ya kimondo kile na kama kikipiga hapa duniani , inatosha kabisa kuibaribu dunia yote na kufuta uhai”
“Kama ni hivyo si ingekuwa miaka elfu hamsini iliopita ndio maisha yageanza?”Aliuliza Roma.
“Sababu ya Magimba hayo ya anga za juu hayaifikia dunia ni kwasababu ya mimi kama Mjumbe wa mkuu wa Enzi”Aliongea.
“Wewe…!!!”Roma alionekana kufikiria kitu lakini aliona ni nguvu kuvuta taswira.
“Kwahio unataka kusema kwmaba unao uwezo wa kupindisha muelekeao wa vimondo visifikie dunia , hebu acha kunitania , kama ni hivyo si utakuwa na uwezo wa kuupoteza hata mwezi?”
“Unaonekana kushangaa na hii inamaanisha huna imani yoyote nje yako tofauti na uwezo wako pekee , ukweli ni kwamba Wajumbe wa mkuu wa Enzi ambao waliacha dunia na kwenda nje galaksi nyingine wanao uwezo hata wa kuharibu sayari”
Roma alikuwa ni kama anaona muonekano wake mwenyewe , ilikuwa ni dhahiri alikuwa katika bumbuwazi lakini ilionekana ni kama vile Sharif hakuwa akitaniana nae.
Roma alijiuliza maswali mengi juu ya Wajumbe wa mkuu wa Enzi, Galaksi nyingine , alijiambia kwahio hao wakuu wa enzi tuseme wameenda nje ya anga la kawaida , yaani katika mbingu nyingine.
Mara baada ya kumuonaRoma akiwa katika hali ya Bumbuwazi aliona lazima atakuwa ameenda mbali katika maneno yake hivyo alimpa ishara Roma kutosisimkwa na mwili sana na kumsikiliza taratibu taratibu.
Sharif alijiweka sawa kama mtu ambae anakusanya mawazo yake na mara baada ya muonekano wake wa kawaida kurudi alianza kumwelezea kila kitu kuhusu Wajumbe wa mkuu wa Enzi , stori ambayo inaanzia juu ya yeye mwenyewe ni nani haswa.
****
Miaka elfu hamsini iliopita Sharif alikuwa ni mtoto wa kiume aliezaliwa nje ya ndoa ambae alikuwa amechanganya damu , akizaliwa na mama ambae ni binadamu wa kawaida na jini jamii ya mapepo , kutokana na kuzaliwa nje ya ndoa na binadamu ilimfanya kutohesabika kama mtoto mwenye umuhimu ndani ya familia ya baba yake Sharif.
Ikumbukwe kipindi hichi ni wakati ambao binadamu , majini pepo na majini watu walikuwa wakiishi pamoja , yaani kabla ya vita na utenganisho wa jamii hizo na hii ilifanya hata kwa majini pepo kuwa na koo zenye majina ya kufanana na za binadamu leo hii , hivyo Sharif alitokea katika ukoo wa Sharif kutokea bara la Asia yaani Uarabuni.
Ndani ya familia ya Majini Sharif , Sharif uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi ulikuwa mdogo sana zaidi ya kichekesho , mdogo zaidi hata kwa wadogo zake ambao walikuwa ni majini kamili.
Kitu ambacho familia ya Majini Sharif hawakukifahamu ni kwamba Sharif kilichosababisha uwezo wake kuonekana mdogo sio kama alikosa kipaji au elimu bali ni kwamba uwezo wake wa akili ulikuwa mkubwa zaidi kuliko familia nzima , kipindi hichi alikuwa ni kama mtoto ambae alipata maono tayari hivyo mbinu yake ya mafunzo ilikuwa ni tofauti kabisa na ndugu zake.
Mara baada ya kutengwa sana na familia kwa kuonekana mzigo alijifanyisha kufa wakati wa vita ya viumbe wa dunia na hapo ndipo alipoweza kujitenga na familia yake kwasababu ilijua alifariki walimsahau.
Haikueleweka alikuwa na elimu gani wala ufunuo wa namna gani , kwake ilikuwa ni kama Mungu akujie ndotoni na akuonyesha Akhera au Mbinguni kulivyo lakini akuambie shika hili andiko na elewa maana yake ili kuijua njia ya kufika Uzimani yaani Akhera au Mbinguni , hiki ndio kilichomtokea Sharif.
Sharif ambae alikuwa kama binadamu wa kawaida alikuwa tayari ashaingia katika kituo cha juu kabisa cha levo ya mapigo elfu kumi ya radi wakati ambao Aoiline Jini jamii ya Mbweha alipoanza kuupata umaarufu miaka elfu hamsini iliopita.
Ukweli ni kwamba licha ya Sharif mweyewe kutoweza kukutaa ana kwa ana na Wajumbe wa mkuu wa Enzi lakini alikuwa ashawafikia ki uwezo au pengine kuwapita kabisa na alifikia katika levo ambayo ilimuwezesha kufungua malango ya kwenda kwenye Galaksi nyingine ambako Mkuu wa Enzi na wajumbe wake huishi.

Wakati Sharf anafikia levo ya juu kabisa akiwa amejitenga alijikuta akipata uwezo wa kuweza kusafiri katika eneo lolote juu ya dunia , ikiwemo kuingia katika gereza la roho na kutoka ambalo lilitengenezwa na Wajumbe wa mkuu wa enzi , pamoja na kuingia ulimwengu wa kimaajabu wa majini pepo , pamoja na ulimwengu wa jicho la Anga kipindi hicho bado ulimwengu huo haujafahamika bado .
Katika matembezi yake hayo alikuja kujifunza ulimwengu wote wa aina tano umeungana katika sayari moja ya dunia kwa nama ya kipekee.
Mkuu wa Enzi pamoja na wajumbe wake ilionekana walitumia uwezo mkubwa sana wa akili kutengeneza kitu kama hicho.
Na wakati wa utenganisho kuanza kulikuwa na majini wengi wabaya ambao walikuwa wamefungiwa katika gereza la roho lakini kutokana na nguvu kubwa za giza walifanya ulimwengu wa majini wwatu kulemewa
Hivyo ndipo Wajumbe wa mkuu wa enzi walipotengeneza malango ya anga ambayo huunganisha ulimwengu wa jicho la anga na Gereza la roho na kuanza kunyonya nguvu za giza kuzijaza katika ulimwengu huo.
Kwa bahati nzuri ni kwamba nishari hasi inao uwezo wa kunyumbulishwa na kutengeneza radi ya zambarau hivyo walitumia nguvu zilezile za kwao za giza kutengeneza radi katika mnara ili kuzuia majini hao wasitoroke
Mambo haya yote yalifanyika kwa ajili ya usalama wa binadamu kwani kipindi hicho ndio wakati wao uliwadia wa kuondoka duniani na kurudi walikotoka
Walikuwa na uwezo wa ajabu mno zaidi ya nguvu za nishati ya mbingu na ardhi hivyo kuwa na uwezo wa kusafiri kwenda katika mbingu nyingine kabisa ya kushangaza.
Lilikuwa ni jukumu lao kulinda dunia kwa wakati huo lakini haikuwa kazi yao kulinda dunia milele hivyo mara baada ya kumaliza misheni yao walipaswa kurudi.
Misheni yao kubwa ilikuwa ni kwa ajili ya kuendeleza kizazi cha binadamu hivyo walipaswa kuhakikisha dunia sehemu ambapo ni nyumbani kwao panakuwa salama.
Hivyo majini wale wabaya walifungiwa gerezani na wale ambao walionekana kuwa wajanga wakawekewa mtego wa mnara ili kuwavuta kwenda kwenye ulimwengu mwingine
Sasa haya yote yalijulikana kwasababu waliacha maandiko juu kabisa ya mnara wa maajabu.
Ijapokuwa ulimwengu hizo zilionekana kama gereza lakini nia kubwa ya Mkuu wa Enzi kupitia wajumbe wake ni kutenganisha viumbe hatari na binadamu wa kawaida.
Viumbe wa dunia walikuwa ni majini watu , Majini pepo na binadamu na Mkuu wa enzi kupitia wajumbe wake alipanga kuacha mtu ambae anapaswa kuwa mwangalizi wa dunia na mtu ambae alichaguliwa kwa wakati huo ni Sharif lakini hata hivyo hakumpa misheni hio moja kwa moja.
Katika mnara wa Anga kuliwachwa nyaraka za lugha ilioandikwa na wajumbe , naraka hizo zilikuwa zikielezea mtu yeyote ambae ataweza kupitia mapigo tisini na tisa ya radi ya Zambarau na kufika kileleni mwa mnara , iwe ni binadamu , iwe ni jini mtu , iwe ni jini pepo kutoka ulimwengu wa majini pepo ilimaanisha nguvu yake ni kubwa ya kukidhi kigezo cha kurithi cheo cha Uangalizi kwa niaba ya Mkuu wa Enzi.
Ukweli ni kwamba Roma yeye ni Special case kutokana na uwezo wake mkubwa mno , kwanza kabisa mwili wake ulikuwa timamu mno kwa kwa kufanyiwa sayansi nyingi na kupata mabadiliko , pili aliweza kubahatika kumiliki Dhana ya Cauldron ambayo iitumiwa na Wakuu wa Enzi kumfungia mnyama Chaos.
Sababu ya Mkuu wa Enzi kupitia wajumbe wake kuacha nyaraka ya maelekezo juu ya mnara wa anga ilikuwa ni kama misheni ya kukidhi vigezo kwa mtu ambae anapaswa kuwa Mwangalizi kwa niaba.
Mkuu wa enzi aliamini mtu yoyote ambae ataweza kufika katika mnara huo na kuvuka Dhiki ya mapigo ya radi basi moja kwa moja inamaanisha anakaribiana ki uwezo na wajumbe wake hivyo anatosha kuwa mwangalizi.
Hivyo kwa lugha nyepesi ni kwamba wajumbe walikaribiana ki uwezo na mtu yoyote atakaefanikiwa kuingia katika mnara na kufika kileleni na hii ipo hata kwa Aoiline pia.
Wote ambao hufanikiwa kufika katika mnara huo kwa maelekezo ya nyaraka hizo wanapaswa kufanya chaguzi, mosi ni kuchukua Dhana ya Ngoma ya kinaoni na kuondoa radi inayowazuia majini pepo kutotoka katika ulimwengu wa majini pepo , pili ni kuiacha ngoma hio ili kuendelea kutenganisha binadamu na Viumbe hao hatari.
Ilikuwa ni kwa ajili ya kuwapa viumbe wote nafasi sawa , iwe ni majini watu , iwe ni binadamu wenye uwezo wa kuvuna nishati za mbingu na ardhi au majini.
Kama angetokea kiumbe chochote kikawa na nguvu na kuua binadamu basi ilimaanisha hio ndio hatima yao , hivyo hivyo kwa majini pepo.
Sasa Sharif ndio wa kwanza kabisa kuingia katika ulimwengu wa majini pepo kupitia mnara na hio yote ilikuwa ni kutokana na shauku yake tu.
Wakati huo mnara huo ulikuwa wazi masaa yote na miaka yote na haikuwa kila baada ya miaka sitini.
Mara baada ya kudhurula ndani ya ulimwengu huo wa majini pepo kwa muda hatimae aliamua kuondoka kwa kuingia katika floor ya kwanza ya mnara wa mbingu na kupanda juu hatua kwa hatua akipitia mapigo ya radi mpaka kileleni, alikuwa na uwezo mkubwa hivyo ilikuwa rahisi kwake.
Sasa mara baada ya kufika katika kilele cha mnara huo ndipo alipokutana na nyaraka zilizoachwa hapo kwa makusudi maalumu na palepale alijua yeye ndio wa kwanza kama kiumbe wa dunia kufika hapo.
Na ndipo alipokuja kupta ufahamu juu ya uwepo wa viumbe hai kabla ya binadamu katika uso wa dunia ambao walipotea mara baada ya Dunia kupigwa na kimondo , alipata kujua pia ni Mkuu wa Enzi na wajumbe wake waliokuwa wakihakikisha dunia inakuwa salama kwa kupindisha magimba makubwa kutoka angani ili yasiingie katika mzingo wa dunnia.
Haikueleweka kwanini Mkuu wa Enzi alikuwa akijali sana viumbe wa Dunia , haikueleweka kwanini alikuwa akiwalinda lakini mara baada ya Sharif kusoma barua hio alijua kwanzia siku hio amekuwa Mwangalizi wa usalama wa dunia, yaani amekuwa kama Mjumbe wa Mkuu wa Enzi licha ya kwamba ni nusu binadamu nusu jini.
Kila yoyote ambae angeweza kufika kilele cha mnara huo ilimaanisha alikuwa na uwezo wa kuibeba misheni na sio hivyo tu anao uwezo pia wa kuchukua nguvu ya Ngomba kama uwezo huo wanao.
Mwanzoni Sharif mara baada ya kupata misheni mpya alitaka kupotezea , lakini badala yake aliona lazima dhamiri ingemfunga milele hivyo moja kwa moja aliamua kukubali misheni yake na kwanzia hapo ndipo alipoitwa Master namba moja.
Alikuwa na uwezo hata wa kuondoka ndani ya hii syaari lakini hakufanya hivyo na aliamua kuishi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini kwa ajili ya kutii maagizo ya mkuu wa enzi.
Lakini Sharif hakuwa na mpango wa kuwa Master namba moja milele , hakuwa akiataka kuwa muangalizi milele na alipaswa kuondoka na kuwafuata Wajumbe wa mkuu wa enzi na ili kuondoka misheni ilikuwa ni kutafuta mrithi wake ambae angeendeleza alipoishia
Kwa lugha nyepesi ilikuwa ni kwamba misheni yake ilipaswa kuisha mara tu baada ya kupata mrithi.
Sasa siku hio hio ambayo aliingia katika mnara huo tayari alikuwa ashaandaa mpango wa kutafuta mrithi , yaani siku ambayo anapata isheni ndio siku ambayo alianza kuanza juu ya kupata mrithi wake.
Sharif alichukua ufunguo wa ulimwengu wa jicho la anga , yaani ile hazina inayofanana na kokoto ya umbo la mviringo na kisha ndipo alipotoka na kurudi ulimwengu wa binadamu.
Wakati anatoka tayari vita baina ya viumbe wa dunia ilikuwa ikiendelea bado na kutokana na uwezo wake aliamua kuzamia katika miliki ya majini chotara yaani Panas na kujiita jina linalofanana na jamii hio lakini licha ya kuwa na uwezo mkubwa hakujionyesha kabisa.
Ilikuwa ndio kipindi hiko hiko aliweza kukutana kwa mara ya kwanza na mrembo Aoiline ambae ndio yupo juu ki uwezo na kuzoeana lakini kwa bahati mbaya wakati huo tayari alikuwa na misheni hivyo ilikuwa ngumu kuwa nae kimapenzi , ijapokuwa mwanamke huyo alikuwa mrembo na alionyesha kila dalili ya kupendwa lakini alimkataa.
Aoiline alikuwa ni jini mwenye akili sana na alikuwa na uwezo wa kukisia mambo mengi hata yale ambayo Sharif hakumweleza na ili kutokuwa kikwazo kwa Sharif aliamua kutorokea kwa hiari yake katika ulimwengu wa majini pepo.
Aoiline hakuvutwa a mnara kama ilivyokuwa kwa majini wengine bali yeye mwenyew kwa hiari yake aliacha ndugu na kupotelea kwenye ulimwengu wa majini pepo.
Sharif hakutaka kumzuia Aoiline kutokana na kwamba alikuwa na vitu vingi vya kufanya.
Sharif ili kumaliza vita aliamua kuwavuta majini pepo wengi kuingia katika ulimwengu wa jicho la anga na mara baada ya kufika huko alijilipua kimaigizo huku akiwaua wote na ndipo walipogeuka mizimu baadae.
Kitendo alichokifanya Sharif katika ulimwengu huo wa jicho la Anga ulifanya kutengeneza upenyo kupitia ulimwengu wa ajini watu kwa kila baada ya miaka mia moja.
Kwasababu alichukua Hazina iliokuwa ni ufunguo unaounganisha ulimwengu wa jicho la anga na mnara geti lilijifunga na kupelekea nguvu hasi ya kutosha kutoingia katika mnara na hatimae kwenye Dhana ya ngoma kirahisi pamoja na kushikiria geti la mnara kwa upande wa majini pepo hivyo kusababisha mnra huo kufunguka kila baada ya miaka sitini kipindi maalumu ambacho Ngoma hio imekusanya nishati za kutosha kushikilia geti la mnara kuwa wazi.
Mara baada ya kutoa hazina hio alirudi katika asili yake sasa ambayo ni familia ya Sharif na kuacha hazina hio pamoja na ujumbe kwa kuwaeleza ili kurudisha wenzao ambao wamepotea yaani wale aliolipua katika jiccho la Anga na ambao wamemezwa na mnara basi Hazina hio ndio njia na hakueleza ni kwa namna gani ni njia na alifanya hivyo kutokana na kwamba aliamini hatima ndio itaamua.

Sharif yeye liacha hazina hio katika mikono ya ndugu zake akichukulia kama zawadi kwao lakini wakati huo akikisia kwamba kama itaokea majini pepo wataiteka miliki ya majini watu hivyo kuna uwezekano wa hazina hio ikafanya kazi kwa kufungua lango , kitu kama kilichomtokea Roma wakati ule , ilikuwa ni kama kitu kilichopangwa ambacho hakiwezi kubadilishika.
Sasa miaka elfu therathini ilipita ya Sharif kuendelea kufanyia kazi misheni aliopewa na kimya kimya aliendelea kuangalia ndugu ake wakati huo huo akiisaidia dunia katika kudili na mambo hatarishi.
Lakini kadiri alivyokuwa akiishi alikuja kugundua alikuwa akizidi kuongezeka ki uwezo maradufu huku binadamu , majini pepo na majini watu wakizidi kupoteza uwezo .
Majini pepo ambao walibakia katika ulimwengu wa kibinadamu ili kuepuka kushambuliwa na majini watu walienda kujichimbia katika ulimwengu wa jangwa tenganifu huku wakiaha Hazina katika ulimwengu wa binadamu wakiamini hio ndio sehemu waliopotea ndugu zao na kama walivyoambiwa ndio njia ya kuwarudisha basi tokea hapo waliifanya kama Dhana ya imani yao.
Upande wa majini watu Sharif pia aliona ni upuuzi mtupu kwani hakukuwa na wapanda levo zaidi ya udanganyifu tu.
Kitendo cha majini kupoteza uwezo kila kukicha ilimfanya kuwa na wasiwasi kama itakuja siku kupata mrithi na kujiuliza kama kuna hata haja ya viumbe hao kubakia katika dunia.
Alijjiuliza maswali mengi na wakati huo moja ya maswali hayo ni je kuwaacha binadamu kuwa watawala wakuu wa dunia kama ilivyoamuliwa na Mkuu wa enzi na kuwatenganisha na majini pepo.
Kadri ambavyo alikuwa akipanda levo ni kama alikuwa akijiweka mbali zaidi na viumbe wa binadamu , alichojali ni usalama wa dunia tu na sio usalama wa binadamu au majini.
Lakini kabla hata hajajua majibu ya maswali yake ikiwa imepita miaka elfu therathini ndipo viumbe kutoka sayari nyingine walitua duniani.

SEHEMU YA 787.
Sharif kwa muda mrefu alikuwa ashajua juu ya kabila la viumbe hao licha ya kwamba hakuwahi kufika katika sayari ya Mars.
Tofauti na kuwa na wasiwasi juu ya ujio wa hawa viumbe alijikuta akifurahi.
Likija swala la nguvu na uwezo miungu walikuwa na nafasi kubwa hapo kutokana na kwamba walizaliwa wakiwa na uungu ambao unawawezesha kuzitambua kanuni za anga.
Uwezo wa namna hio ni kama zawadi kutokana na kuwa na nguvu kubwa mno.
Kitu kingine kilichowapatia faida miungu ni uwezo wao wa kuhamisha nafsi zao kutoka mwili mmoja kwenda mwingine , hivyo walikuwa wakiishi muda mrefu kuliko binadamu.
Ijapokuwa miungu walikuwa na uwezo wa chini kuliko wajumbe walikuwa na uwezo wa kutegemea miili yao tu kusafiri kutoka katika sayari moja kwenda nyingine lakini ilikuwa ngumu kwa majini pamoja na binadamu kusafiri kutoka sayari moja kwenda nyingine na kuweza kupona na adha ya anga labda tu mtu awe levo ya mapigo elfu kumi ya radi.
Kitu kingine ambacho kilionekana kuwa faida kwa miungu ilikuwa ni kwamba wameungana pamoja kifikra yaani miungu yote kumi na mbili na walikuwa na mama mmoja wa kiuungu hili liliwapelekea kupunguza mingongano ya ndani licha ya kwamba kuna kutoridhika kati yao.
Ustaarabu katika sayari ya Mars chini ya miungu ulikuwa umeendelea mno kuliko hata wa dunia ya sasa.
Kama ugefananisha ustaarabu wa miungu na wa sasa wa kibinadamu ni kama vile ndio kwanza tupo katika zama za mawe, miungu walikuwa wa moja na hakukuwa na utofauti wa kidini wala kimsimamo ni kama wote walikuwa na mawazo sawa, ilikuwa ni sahihi kuita ulimwengu wao ni wa kiutopia.
Sasa mara baada ya sayari yao kushindwa kusapoti maisha na mti Mama kunyauka mahai sahihi walipoona ni pakukimbilia ni sayari ya Dunia lakini walijua fika miili yao haiendani na mazingira ya dunia kwa muda mrefu na hapo ndipo maauzi yalipofanyika kuhamisha nafsi zao na uungu wao kwenda kwa nafsi za binadamu.
Miungu kumi na mbili kutokana na kwamba walikuwa ndio uzao wa kwanza wa mti walikuwa na nguvu kubwa na walifanikiwa kuziteka nafsi za binadamu na kutawala miili yao , lakini ndugu zao ambao hawakuwa na nguvu kubwa kama wao waliishia kumezwa na nafsi za binadamu.
Sasa mara baada ya vita kuanza kati ya majini watu na miungu upande wa Sharif yeye alikaa pembeni kuangalia kinachoendelea na hakusaidia upande wowote.
Ijapokuwa Sharif alikuwa na uwezo wa kuua miungu hao kirahisi tu ikiwemo Athena na Zeus lakini hakuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Na hio ni kwasababu tokea zamanni alikuwa ashaacha kuingalia dunia kwa mtazamo wa kawaida , binadamu na miungu wote waliishi katika anga na mhimili wao ni sayari zao , ni rahisi kusema wote wana haki ya kuishi katika anga hivyo Sharif aliona hata wao wana haki ya uhai ndani ya mhimili wa sayari ya dunia na hakutaka kutofautisha viumbe kwa kuwaita Alliens.
Kipindi hicho ndio ambapo Sharif wazo lilimwingia na kuona kama dunia itatawaliwa na miungu basi moja kwa moja misheni yake inaweza kufikia mwisho.
Aliona kabisa miungu walikuwa na uwezo wa kulinda dunia na isipotee kwa kugongana na magimba au vimondo na wakati huo huo ustaarabu wao ulikuwa umekuwa sana kuliko hata ilivyokuwa binadamu.
Ukumbuke kipindi hichi miungu wakati wanashuka binadamu hawakuwa hata wakijua gari ni nini na walitegemea miguu yao kusafiri.
Sharif katika misheni yake ilikuwa ni kulinda viumbe wa dunia wasipatwe na majanga ya nje ya dunia lakini sio kuwafanya binadamu kuwa juu ya viumbe wegine au kuwa chini ya viumbe wengine , alijua kama miungu watakuwa ndio viumbe wenye nguvu zaidi ya binadamu kutokana na maendeleo yao basi wasingepoteza rasilimali za dunia katika kupambana wao kwa wao bali wangefikiria namna ya kuendeleza dunia jambo ambalo si baya.
Wajumbe wa mkuu wa enzi walikuwa tayari wamekisha andaa kila kitu , kulikuwa na safu ya ulinzi wa gereza la roho kwa ajili ya mashetani , mapepo na mazimwi kutokana na kwamba hawakutaka kuwaua wote na kutokana na hilo Sharif aliona hata kabila la waliostaarabika la miungu Mkiuu wa enzi na wajumbe wake wataweza kuwavumilia , isitoshe ndio walikuwa wakitafuta mahali pa kuishi.,
Ukweli ni kwamba Sharifi wakati huo alikuwa katika kujiluliza kwingi kama angeweza kufanya maamuzi hayo angeenda kinyume na mipango ya mkuu wa enzi lakini kwasababu hayakuwa maamuzi rahisi basi aliamua kuangalia kwanza kitakahotokea.
Katika miaka iliofuata ya miungu kufanikiwa kutawala baadhi ya miili ya kibinadamu , Sharif aliweza kugundua ni miungu wamepoteza miili yao na hawawezi kuendeleza kizazi chao.
Kitendo cha miungu kutelekeza miili yao ilimfanya Sharif kuingia katika uchunguzi na alichokuja kugudua kilimshangaza sana , ilionekana miungu hawakutegemea jua moja kwa moja kwa ajili ya kuishi na miili yao kusapoti maisha bali walitegemea jua kwa njia isiokuwa ya moja kwa moja.
Sharif alifungua miungu waliishi chini ya mti na huo mti kazi yake ilikuwa ni kubadilisha nishati ya jua kuwa nishati tofauti ambayo husapoti miili yao na kuwapelekea kuzaliana na mti kuwatunuku uungu.
Mara baada ya sayari yao kukubwa na janga lililowafanywa wakimbie Astreus moja ya viumbe hao aliamua kuficha moyo wa Gaia katika teknolojia ya kipekee na kuja nayo duniani , moyo wa Gaia ilikuwa ni kama mbegu ya mti huo.
Sasa Sharif mara baada ya kufanya utafiti wake wa chini chini alikuja kugundua mengi , alishangaa mara baada ya kugundua ni kweli mti maa ndio ulikuwa chanzo cha nguvu za miungu lakini nguvu zao walizipata kwa gharama ya nishati ya sayari yao kiasi cha kuipelekea kupoteza sifa ya uhai kwa spidi kubwa sana.
Ufumbbuzi wa jambo hilo ulimfanya kusita na mpango wake wa kuwafanya miungu kuwa juu ya binadamu
Alijua kama miungu wangepatia dunia kuitawala ni swwala la muda tu kuupata moyo wa Gaia na kisha kuufufua na kupanda Mti Mama tena ili kuarudisha uzao wao.
Misheni yake ilikuwa ni kulinda dunia na kama jambo hilo angeruhusu ilikuw ani kama anaangalia dunia ikiangamia.
Sharif ambae alikuwa na cheo cha uangalizi kutoka kwa Mkuu wa Enzi alijikuta akishindwa kufanya maamuzi ya moja kwa moja aidha kuwapa ukuu miungu kuitawala dunia au kuendelea kulinda ustaarabu uliopo wa kiumbe binadamu.
Wakati huo huo aliikuwa akiataka kuungana na wajumbe kwa Mkuu wa enzi haraka iwezekanavyo lakini hakuwa na uwezo wa kuondoka duniani kabla misheni yake haijaisha baada ya kupata mrithi.
Hivyo ilimpelekea Sharif kuchukua hatua kama Mwangalizi na kisha kuwaza maswala mengine baadae.
Alijifanyisha ni jini mtu kutokea Hongmneng kwa kubadili muonekano wake pamoja na uwezo wake kuushusha kidogo na hivyo kumfanya awe moja ya kiumbe jini mtu mwenye nguvu kubwa.
Baada ya kujifanyisha anapigana na Zeus alimtega na kumwingiza katika ulimwengu wa majini watu na kisha akamfungia katika gereza la roho huku Athena akimwahia huru makusudi.
Kufungiwa kwa Zeus ilimaanisha miungu kukosa nguvu ya kivita kwa asilimia hamsini na kushindwa kutamba mbele ya majini watu hivyo wakaona waache vita na hapo ndipo ulipotokea mkataba wa The Gods Treaty .
Maongezi hayo kati ya Roma na Master namba moja yalidumu kwa muda mrefu sana tokea mhana mpaka usiku.
Roma kadri alivyokuwa akimsikiliza Sharif akielezea historia hio ya miaka mingi alijikuta akkishindwa kujizuia na kutoa tabasamu hafifu.
“Dogo hivi unadhani kwa yote ambayo nimefikiria na kufanya ilikuwa ni kupoteza muda?”
“Sidhani kama ilikuwa ni kupoteza muda , kwako wewe haikujalisha ni binadamu , majini au miungu walikuwa ni kama kunguni tu ambao hupambana wao kwa wao na wewe ulikuwa ukiifurahia vita yao , haikujalisha maamuzi yako yalikuwaje lakini mwisho wa siku kila kitu ni juu yako”Aliongea Roma na kumfanya Sharif kuoekana ni kama vile ametegemea jibu la aina hio.
“Kama kweli hicho ndio unachofikiria , kwanini ukamuacha Athena ili hali ulikuwa na uwezo wa kufanya hivyo , kama hutaki kumua unafanya nini hapa peke yako?, unazo nguvu za kufanya maamuzi yoyote yale lakini bado upo hapa kujisahaulisha , vitu nilivyofanya vinaweza kuwa nikupoteza juhudi zangu lakini ni angalau kuliko chaguzi uliofanya
Mara baada ya neno Athena kutamkwa macho ya Roma yalicheza huku akikunja ngumi yake na kihisia alikosa mhimili lakini mara baada ya kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa alionekana kutulia , kwani bado alikuwa katika bumbuwazi juu ya maneno ya Sharif.
Roma alijiuliza hata kama ni kweli anao uwezo wa kufanya maamuzi yoyote je ni maamuzi ambayo anaweza kufanya kirahisi.
“Muunganiko wangu na hii sayari pamoja na viumbe vyote hai ni kama muunganiko wako na Athena , ijapokuwa ni toafuti lakini kuna uhusiano , umeshindwa kufanya maamuzi kwa sababu ya mwanamke mmoja , je unadhanni ilikuwa rahisi kwangu kufanya maamuzi kwa niaba ya viumbe wote?”
Awamu hio Roma hakuonyesha kumcheka ni kama kwa namna flani alikuwa akizielewa hisia zake , lakini kwa wakati mmoja alikuwa amekasirika kwasababu alijua nia yake kwake.
“Umefanya mambo mengi na bado ukasubiri kwa miaka elfu ishirini je ni kwasababu ulishindwa kufanya maamuzi wewe mwenyewe , ndio maana unataka mimi ndio niamue ni nani anapaswa kuitawala dunia?”Aliuliza Roma na Sharif aliishia kutingisha kichwa asikatae.
“Ndio , unaweza chukulia hivyo , lakini haya sio maamuzi yangu ni hatima yako kama unabii ulivyotabiriwa , wewe ndio mtu pekee ambae utaathiri matokeo”Aliongea Sharif.
“Nini kilichopo nyuma ya huu unabii ambao Athena ameshikilia , je atakuwa alikujua tokea mwanzo na uwezo wako na misheni yako, lazima utakuwa unajua kila kitu kuhusu Athena alichokifanya lakini ukamuacha tu makusudi , je ni kweli?”Aliuliza Roma huku akisaga meno yake.
“Dogo haina haja ya kuwa na hasira ,najua kila kitu unachotaka kufahamu na nisikilize nitakuambia taratibu , nimekuja kwako kuondoa hali ya kuchangayikiwa kwenye moyo wako …”Alionekana kuvuta pumzi na akaendelea.
“Kinachosemekana kama unabii pengine mtu ambae anaweza kukielewa ni Athena mwenyewe, lakini ninaweza kufanya makisio kwa kuangalia tu uungu wake , inasemekana karama ya unabii ndio upekee wa uungu wake , kwa kutegemea tu kanuni za anga anao uwezo wa kujua nini kitatokea baadae , inaweza kuwa ni sekunde ijayo ,dakika , siku , miaka na hata zaidi ya milenia ya wakati ujao …”
Njia pekee ambayo humfanya hupta huo unabii ni kitu ambacho anakifahamu yeye mwenyewe na hakuna mtu anaeweza kuelewa , ni kama sisi tu tunavyopata ufunuo , hata hivyo ukubwa wa athari za mtu , eneo au elementi nyingine za unabii wake katika anga ndio nguvu yake ya kiroho inavyotumika sana , isitoshe mbinu hio ya unabii mkubwa unatokana na kanuni za anga”
Kwa maneno mengine kama Athena atataka kutabiri kesho ya mtu wa kawaida basi ni sawa na kutumia chembe ya nguvu yake ya kiroho lakini kama atata kutabiri kesho yangu haiwezekani.. hii ni kwasababu nimepanda na kuwa juu ya kanuni za anga ambazo anazifahamu , sipo kwenye dimension sawa na yeye
Hatas kama atataka kukutabiria wewe Roma Ramoni itakuwa ngumu mno kwake , hio ni kwasababu wewe Roma wa sasa umebadilika sana tofauti na zamani , unabii wake ulikuwa sahihi tu kabla ya wewe kuingia levo ya mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi , unabii wake ni kama unafamna kujua unafikiria nini na unataka kufanya nini katika sekunde inayofuata hivyo kama utapigana nae atashindwa kuyatabiria mashambulizi yako hivyo hatojisumbua kutumia uwezo wake wa kutabiri na atashindana na wewe bila ya hira yoyote”
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Athena anaonekana kuwa na nguvu kutokana na kwamba anao uwezo mkubwa wa kutabiri tukio litakalotokea ndani ya sekunde moja kuendelea na hii inamfanya kuweza kukudhibiti kabla hata hujafanya shambulizi lakini kama mtu ana uwezo wa juu na yupo juu ya kanuni zake za anga basi moja kwa moja unabii wake unakuwa sio sahihi, alikuwa akimuweza Roma kutokana na kwamba alikuwa na uwezo wa kumtabiria na kujua kila kitu atakachofanya lakini hio yote ilikuwa ni kipindi kabla hajapitia mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi.
“Kwahio Athena hajui kabisa wewe ni nani?”Aliuliza Roma.
“Hapana , ijapokuwa hawezi kutumia unabii wake kukadiria uwezo wangu pamoja na wasifu wangu lazima atakuwa anajua uwezo wangu kupitia njia zingine , ukweli ni kwamba ashajua muda mrefu nitakubali kila kitu anachofanya hivyo hakuwa na haja ya kunitaja kwa yoyote , ni kama tu alivyoweza kuupata moyo wa Gaia , ijapokuwa alishindwa kutabiri eneo husika utakapotokea lakini alikuwa na uelewa ulikuwa ndani ya Taifa la Korea na wewe ndio utakuwa kama ramani kwake”
“Kama mimi wa sasa nitajiweka katika levo ambayo atakuwa na uwezo wa kufanya unabii sahihi , je atakuwa anajua kama unabii huo ni sahihi?”Aliuuliza Roma na kumfanya Sharif kuangau kicheko.
“Ukweli ni kwamba mbingu yake ya utabiri mkuu ishathibitishwa muda mrefu sio sahihi”
“Unamaanisha nini kusema hivyo?”Aliuliza Roma akiwa katika mshangao.
“Umenisikia vizuri , unabii wake mkuu wa Athena sio sahihi kwa asilimia mia moja , kuna mbinu za moja kwa moja za kuharibu utabiri wake kuliko kwenda mbali kwa kujiweka katika levo anayoweza kutabiri”Aliongea na kumfanya Roma kuonekana kuchanganyikiw .
“Ili kufanikisha hilo ni kumhusisha yeye mwenyewe kama kipengele cha unabii”Aliongea Sharif na kumfanya Roma kuwa na ufahamu unaokuja kwa mbaali.
“Athena ndio wa kwanza , mtu anawez akusema ni yeye pekee anaejua kila kitu anachotabiri kwa ukamilifu , hii inamaanisha kwamba ikiwa anataka kuathiri mustakabali wa jambo , anachohitajika kufanya ni kurekebisa tu baadhi ya hatua alizokuwa amepanga kuchukua na historia itabadilika yenyewe na mustakabali utafuatia”
“Kama ni hivyo , uliposema unabii wake haupo sahihi miaka kadhaa iliopita , je ni kwasababu alifanya kitu ambaho hakupwaswa kufanya?”Aliuliza Roma.
“Upo sahihi , ni kipindi kilichopita ambacho kinakuhusisha wewe zaidi, Athena hakutarajia atakuzalia mtoto na kumfanya ahame mwili mapema”Aliongea Sharif na ilikuwa ni kama ameshusha bomu.
“Unasema nini!!”Roma alijikuta akishindwa kuedelea kukaa na kujikuta akisimama huku macho yake yakimtoka wakati akuongea.

“Lanlan ?! , unamaanisha Seventeen alikuwa…”Aliuliza Roma kwa kuchanganyikiwa lakini Sharif alikunja nne kwa pozi murua.
“Hivi bado hujawahi kuwaza , hakukuwa na hali isiokuwa kawaida wakati ulipokuwa nae ?,Seventeen ni mwanamke ambae Athena alitawala mwili wake wakati akiwa hatua za mwisho za uhai wake , yote haya alikuwa ni sehemu ya unabii wake wa mwanzo”
Roma alijikuta akipata picha ya Lanlan kulazimisha Edna kuwa mama yake mzazi kila muda na Roma kukumbuka wakati ambao Edna alikuwa akitamka maneno ya Seventeen aliowahi kuongea.
Roma alikuwa na hisia za namna hio lakini mara baada ya kuthibitisha kwa masikio yake ilifmanya ajione ni kama amepigwa na radi.
“Sina uhakika unabii wa Athena wa mwanzo ulikuwaje lakini nilikuwa nikimwangalia hatua kwa hatua , ni wazi kabisa mara baada ya kuhamia katika mwili wa Seventeen hakutaka kabisa kuwa karibu na wewe lakini alishindwa kutabiri wakati atakapoamka katika mwili wa Seventeen tayari ana hisia za kimapenzi kwako na kubeba mimba yako”
“Unapaswa kuelewa kanuni za anga hazina athari yoyote mbele ya mapenzi ya kibinadamu ambayo huvuka nafasi na muda , upendo ni hisia nyeti ambazi hata miungu na akili zao zote wameshindwa kuelewa , ndio nguvu ya ajabu ambayo binadamu anayo ambayo haipo chini sana na uungu wa miungu”
Athena anaweza kutabiria kila kitu isipokuwa tu upendo anaokaribia kukutana nao , kwani mapenzi ya kibinadamu kadri yanavyosababisha hisia kali ndivyo unavyokosa maana na mantiki , Wakati Athena nafsi yake inaamka katika mwili wa Seventeen tayari alikuwa ni mjamzito na mtoto wako na ni wakati alipokuwa amezama baharini , labda unaweza kujiuliza kwanini aliamua kujificha kwa kutumia helmeti , kuzaa mtoto na kisha kumkabidhi kwa Tang Chi , lakini hayo yote yalibadilisha historia nzima , mapenzi ya kweli na mtoto ambae hakupaswa kuwepo kwenye maisha yake ilimfanya kufanya chaguzi nyingine ili kurekebisha makosa ya unabii wake wa mwanzo”
“Hembu subiri”
Roma alionekana kuingialia maneno ya Sharif huku akiwa na muonekano ambao una wasiwasi.
“Kama uyasemayo ni kweli , si inamaanisha Edna tokea mwanzo hakuwa ni Athena na hata Seventeen hakuwa Athena wakati tulipoanza kupendana pia?”Roma aliuliza na kumfanya Sharif kutingisha kichwa kukubaliana nae na palepale kumfanya Roma kupambwa na tabasamu la ahueni.
“Asante kwa kuniambia haya .. tafadhari endelea ..nataka kujua kila kitu”
Muda huo alonekana kuwa na furaha kana kwamba amezaliwa upa , miale ya mwanga ilipiga katika maisha yae na kufukuza kiza chote.
Iwe ni kwa Edna na pacha wake Seventeen hao wanawake wote wlaikuwa ni halisi , hawakuwa udanganyifu uliotengenezwa na Athena.
Ukweli ni kwamba hakuwa na chuki na Athena kwasababu yalikuwa ni maamuzi yake ammbayo yaliwezesha Lanlan kuzaliwa.
Kwa sababu zozote zile Roma hakutaka kuvuta taswira ni kwa namna gani Seventeen angejisikia kama angepoteza uhai akiwa na mtoto tumboni kama Athena asingeamua kumzaa.
Kwa ufupi ni kwamba Athena ili kuhakikisha anachotaka kitokee ni sahihi atafanya vitu ambavyo vinachangia mustakabali wa tukio husika , udhaifu mkubwa wa unabii wake ni pale tu anaposhindwa kujitabiria yeye mwenyewe , kitendo cha kushindwa kujitabiria mwenyewe ilimtokea kufanya kitu ambacho hakupaswa kufanya ambacho ni kumzaa Lanlan ambae ni mtoto wa Roma.
Yaani Athena alipanga kuutawala mwili wa Seventeen kwa kuhamisha nafsi yake na uungu wake lakini ikumbukwe kuhamisha nafsi kutoka kwenye mwili mmoja kwenda kwa mwingine sio kitu kinachotokea mara moja , nafsi inapohama hulala kwa kipindi cha muda flani na kisha ndipo huamka , kuwahi au kuchelewa inategemeana sana na uwezo wa uungu wao.
Sasa Athena mara baada ya kuhamisha nafsi yake kwenda kwa Seventeen kutokana na kushindwa kujitabiria wakati anaamka katika mwili wa Seventeen tayari alikuwa mjamzito wa Roma na ndio kipindi ambacho Seventeen anakaribia kupoteza uhai mara baada ya kuzama baharini wakati wa kulipuliwa na bomu na kundi laTakamagahara
Hivyo ni kama Athena alivaa mwili ambao ulikuwa ni mjamzito tayari a tofauti na kuua kiumbe kilichokuwa tumboni aliaamua kulea ujauzito kwa siku kadhaa na kisha akajifungua na baada ya hapo ndipo alipoenda kumkabidhi Lanlan kwa Tang Chi ili kumpelekea Roma , hivyo ni sawa kusema Seventeen na Athena walishikiana kumzaa Lanlan , Seventeen kama Seventeen alimpenda Roma na kubeba ujauzito wake , huku Athena yeye akarithi ujauzito wa Seventeen na kumzaa Lanlan.
Sasa ili kurekebisha unabii ambao Athena alitaka utokee alifanya maamuzi mengine na pengine ndio maamuzi yalioacha akaamua kuuvaa mwili wa Edna pacha wake Seventeen, Roma anafurahi kwa kuona kwamba tokea mwanzo Edna na Seventeen walikuwa halisi na kama walimpenda walimpenda kweli kabla ya kupoteza nafsi zao kwa Athena.
“Nadhani sasa unaweza kudhania ni kipi Athena alifanya ili tu kusahihisha makosa ili apate matokeo ya unabii wa mwanzo kuliko mustakabali ambao huamuiwa na hatima , ingawa kuhamisha nafsi inahitaji nguvu nyingi mno za kiroho lakini mwili wa Seventeen ulikuwa ukipoteza uhai taratibu na hata kama angekurudia ingekuwa tayari amekwisha chelewa kubadilidha unabii na katika maamuzi ya mwisho nipo Athena alipojikuta hana jinsi na kumtumia mtu ambae anaweza kuirudisha hitimisho la unabii wake wa mwanzo na mtu huyo ni Edna na alihama punde tu mara baada ya kuuachia mwili wa Seventeen , aliona kwasababu Edna na Seventeen ni mapacha wa kufanana basi anakuwa mtu sahihi kabisa wa kutengeneza mustakabali wa kesho ambao utakuwa sawa na unabii wake , hivyo maamuzi hayo alifanya mara baada ya kosa la mwanzo
Unapaswa kuelewa ugumu uliopo kuhamisha nafsi kwenda kwa mtoto ni tofauti na kwenda kwa mtot , bila kusahau anahamisha nafsi yake akiwa na asilimia ishirini tu ya nguvu zake zote
Ijapokuwa alikuwa na helmet la kumfanya asionekane na kuhama kimya kimya lakini ilikuwa haiwezekani kuamka mara moja na kwa kukamilika hivyo alichoweza kufanya ni kuufufua uungu wake tu katika mwili wa Edna huku akiitumia nafsi yake kumdhibiti Edna kila muda akihitaji
Wakati Edna anakuja katika hii hoteli sio yeye bali alikuwa ni Athena ambae alicheza na akili ya Edna , alitaka kuwakutanisha na kusababisha kilichotokea baadae , lakini hata hivyo kila kilichowatokea ilikuwa ni wewe na Edna katika uhalisia na sio Athena”
“Athena hakutaka kuhatarisha mpango wake kwa kumgundua mapema ndio maana hakutaka kuupandisha uungu wake wote katika mwili wa Edna ili kumtawala kikamilifu kwa muda mrefu , hivyo kuna muda aliuteka ufahamu wa Edna na mwili wake na kukutana na washirika wake akiwemo Yan Buwen , Athena hakumtawala sana Edna na mara zote aliibadilisha sura yake na kuonekana kama Mzungu mwanadada maarufu ambae ana historia nae nadhani unamjua”Aliongea.
“Clelia Allisanto”Aliongea Roma na hapo sasa ni kama akili yake inakaa sawa vizuri lakini kidogo akionekana kuchanganyikiwa Dorisi alisema alikutana na mwanamke alieitwa Clelia Allisanto wakati huo huo Edna alikutaa na mwanamke alieitwa Clelia Allisanto wakati Athena alikuwa akiishi ndani ya mwili wa Edna wakati huo
“Bila shaka kila kitu kilihotokea kati yako na Eda kilikuwa katika mipango ya Athena kutimiza unabii wake na ndio hizo hatua mlizokuwa mkipiga pamoja ndio zilizomuwezesha kufanikisha kurudisha hitimisho la unabii wake , lakini awamu hii hakutaka kuzembea kama alivyozembea kwa Seventeen baada ya kuchelewa kuamsha ufahamu wake bali aliamua kuwa macho wakati akiwa amejificha ili asifanye kosa tena , lakini hata hivyo kwasababu ya haraka kipindi cha muda wa kujihamisha ulikuwa mfupi sana na kwasababu hakutaka kulala tena kufuta kumbukumbu za Seventeen ndio maana ni kama Edna amekuwa na kumbukumbu zake ndio maana ilitosha kwa binti yako kuamini Edna ni mama yake mzazi , kwa maana hio nafsi ya Edna ina sehemu ya nafsi ya Seventeen ambayo imetokana na haraka za Athena”
Maneno yake yalimfanya Roma mapigo yake kwenda mbio mno kwasabu alikuwa amejua kitu amabcho hakutaka kukifikiria mwanzo.
“Kwahio unamaanisha Athena wa sasa .. ah namaanisha Edna licha ya nafsi yake kutawaliwa na Athena yeye pamoja na Seventeen hawajapotea , si ndio unachomaanisha?”Aliuliza Roma.
“Sahihi , ukweli ni kwamba kipindi ambacho Edna ameweza kutawala nafsi yake lazima kuna wakati alijihisi ana tatizo la akili lakini hakuweza kuongea chochote kutokana na nafsi ya Athena kumzuia , licha ya kwamba alikuwa akijua nafsi yake ilikuwa imetekwa ni kama kuna mtu mwingine katika akili yake lakini asingeweza kuongea chochote kwani Athena anamlinda, lakini sasa hivi ni tofauti kutokana na kufufuka kwa Moyo wa Gaia basi nguvu zake zote zitamrudia na atakuwa na uwezo wa kuzizima nafsi zote mbili za mapacha hao na kumiliki mwili wake kikamilifu na kwa kile ninachojua , miungu wote wakuu kumi na mbili hawawezi kupoteza kumbukummbu kila wanapohamisha nafsi zao lakini wanapoteza kwanza nafsi ya mwili uliopita kabla ya kuamka ambayo ni ya mmiliki wa mwili na ndio maana huchelewa kuamka hata kwa zaidi ya miaka ishirini kulingana na nguvu ya nafsi husika , lakini kwasbabau Athena alikuwa na haraka aliamua kulazimisha kuamsha nafsi yake kwa haraka katika mwili wa Edna na hakuwa na muda tena wa kufuta nafsi ya Seventeen , ndio maana utaona kuna muda mkeo ni kama anaropoka kitu alichofanya Seventeen lakini ni mara moja moja kutokana na kwamba ufahamu wake umekwisha kupotea hivyo nafsi yake inakuwa kama mtu ambae yupo ndotoni , haijalishi atakuwa makini namna gani lakini kuna muda atakuwa anatamka maneno kama vile anaota “
Roma sasa alielewa na ndio maana Edna kuna muda alikuwa kama Seventeen mtupu , iijapokuwa walikuwa mapacha lakini haikumaanisha walikuwa wakifanana , lakini hata hivyo Roma ni kama tumaini lilimwingia.
“Kwa maneno mengine kama nitaweza kufuta nafsi ya Athena nitaweza kufufua nafsi za wote wawili Edna na Seventeen”
“Haha.. aisee wewe ni mjinga”Sharif alijikuta akicheka huku akiatgisha kihwa chake , ni kama alikuwa akijua Roma anawaza nini.
“Unafikiri itakuwa rahisi , Athena ashatarajia utafikiria hivyo , alifanya makusudi kutozima nafsi zote mbili ili kuungana nazo , sasa hivi ni mtu katika nafsi tatu ndani yake, kwa maneno mengine labda tu Athena yeye mwenyewe aisalimishe nafsi yake na kufa , lakini chochote ambacho unapanga kuifanyia nafsi yake basi hivyo hivyo utaimiza nafsi ya Edna na Seventeen , Athena kafanya yote haya makusudi kabisa ili tu usije ukamgusa mpaka mipango yake itimie”
Maelezo hayo yalikuwa ni kama boriti ya radi ya bluu kwa kumfanya Roma matumaini yake yote kupot3ea.
Nini kitafuta usikose
ITAENDELEA.
[emoji1635][emoji1635][emoji1635][emoji3590]
 
Moja kati ya Riwaya za HOVYO na Kipumbavu kuwahi kusoma ni hii...Riwaya ndefuu haina kichwa wala miguu,,mtunzi anajaza matukio mengii mradi iwe ndefu isio na tija

Elfu 10 yangu nililopa bora ningenunua Malaya tu nipunguze uzito
Hii simulizi inahitaji utimamu wa akili ili kuielewa,,,,,,so naweza kusema umeamua kusoma kitu ambacho sio level yako
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

MTUNZI: SINGANOJR

WATSAPP: 0687151346

Mono no aware

SEHEMU YA 788.
Roma alijikuta akiweka tabasamu kama vile alikuwa amekula kitu kichachu , ilikuwa ni kama vile alikuwa amepoteza uwezo wake wote.
Kila kitu kilirudi mwanzo , asingeweza kumgusa Athena ambae alikuwa ameshikilia mwili wa Edna kwasababu alishajua Athena alikuwa ni Edna na Seventeen.
Wakati akiona furaha kuona nafsi zote mbili yaani Edna na Seventeena wanaishi , wanawake ambao walikuwa na umuhimu mkubwa kwake lakini ilimpa msongo wa mawazo kuona kwamba hakuna namna ya kuwaokoa wote kwa pamoja.
Kadri Roma alivyowaza ndio alivyojiona anaweza kupata ukichaa na mwishoni alijikuta akijichapa vibao vya kichwa na mikono yake yote na kuanza kugugumia kwa kutoa mngurumo kama wa mnyama mkali.
Roma alichangua nywele zake kwa kujikuna kichwa huku machozi ya moto yakiloanisha uso wake.
Aliona uwezo wake hauna faida kama hawezi kumuokoa mama mtoto wake na mke wake.
Sharif hakuongea neno na alimwangalia Roma tu akipunguza hasira zake na alichokuwa nacho ni tabasamu tu akimsubiria Roma kutulia.
Dakika chache mbele Roma alionekana kuimarika kihisia na aliinua kichwa chake na kumwangalia Sharif na macho makavu.
Sasa kutokana mambo kufikia hatua hio na yeye pia ni kama amepata mwanga.
Ki ufupi ni kwamba huu mchezo wa zaidi ya miaka elfu ishirini uliokuwa ukichezwa ni kama wa kubahatisha tu kwa wote wawili Athena na Sharif.
Sharif alihitaji kutafuta mrithi wa kuendeleza alipoishia kama maelekezo ya mkuu wa enzi lakini alitaka mrithi wake ndio aamue ni nani anapaswa kuitawala dunia , binadamu au miungu?.
Upande wa Athena pia alikuwa akijua mtu ambae alimfungia Zeus nyakati zile alimwachia yeye makusudi kabisa na hata kama apambane nae hamuwezi.
Lakini wakati huo huo ni Sharif ambae alikuwa akimwangalia tu Athena kuendeleza mipango yake bila ya kuingilia huku akijua kwasababu Athena anao uwezo wa kusafiri mbele ya muda kinabii basi ni swala la muda tu kujua njia ya kufufua miungu.
Wakati Athena akimtumia Roma kama njia ya kufanikisha mipango yake na Sharif alikuwa akimtumia Athena kumtafutia mrithi.
Sharif hakuwa na uwezo wa kutabiri yajayo , alikuwa na uwezo wa kulinda dunia tu hivyo alitumia uwezo wa Athena kumtafutia mrithi wake.
Yaani ki ufupi ni kwamba kila mtu alikuwa na mpango wake , Hades wa zamanni alikuwa na mpango wake kichwani licha ya kwamba hakupinga moja kwa moja ufufuo wa ndugu zake , Athena pia alikuwa na mipango yake ya kukamilisha ufufuo wakati huo huo Sharif yeye alikuwa na mipango yake kwa kuwatumia miungu kumtafutia mrithi.
Wote kwa pamoja walikuwa wakitumiana isipokuwa tu Athena yeye alikuwa akifanya kazi kwa njia isiokuwa ya moja kwa moja kutimiza mipango yake.
Ki ufupi ni kwamba yanayowatokea binadamu msababishi mkuu ni Sharif , maana yeye ndio aliemuacha Athena kutimiza mipango yake yote bila kuingilia ili tu aje kumsaitia kupata mrithi.
Roma ambae tokea mwanzo akili yake ilitengenezwa , maisha yake kurefushwa ndani ya mpango LADO na hata kuja kujifunza mbinu ya andiko la urejesho na kulielewa kwa viwango vya juu alikuwa akihesabika kama mrithi ambae alimridhisha master namba moja.
Ijapokuwa Sharif hakujisumbua sana kuhusu nani atashinda katika vita baina ya viumbe wa dunia na miungu yeye hakutaka kuona mrithi aliemchagua akishindwa na Athena kwasababu tu ya hisia zake za kimapenzi , alitaka awe kama yeye ambae aliamua kuachana na kila matamanio yake yote kama vile kumpotezea Aoiline ili mradi kutii maagizo ya mkuu wa enzi kupitia wajumbe wake.
Kwa namna nyingine unaweza kusema pia ni shindano kati ya Aoiline na Sharif kujua nani ambae alifanya maamuzi sahihi miaka elfu hamsini iliopita.
Athena upande wake aliamini kwamba Roma atapotezea usalama wa binadamu kwasababu tu alikuwa amekufa na kuoza kimapenzi kwa wanawake hao wawili yaani Seventeen na Edna , hata kama atajua kwamba alimdanganya na kumtumia asingeweza kuchukua hatua ya kumuua yeye katika mwili wa mpendwa wake.
Kwahio Athena na yeye alikuwa akicheza kamari ambapo kufanikiwa ama kutokufanikiwa kulitegemeana na maamuzi ya Roma.
“Kwa maana hii , vitu vyote ambavyo nilikutana navyo wakati wa kukutana na Edna vipo ndani ya mpango wa Athena ili tu kurudisha matokeo ya unabii wake wa mwanzo?”Aliuliza Roma kwa sauti nzito.
“Kama nilivyokwisha kusema , alihitaji kufanya marekebisho ya makosa yake , mwanzoni kama Seventeen asingekufa mbele ya macho yako basi ungeendeleza ukichaa wako wa kuua watu dunia nzima na kwa maana hio ni swala la muda tu ungekuwa tatizo kwa dunia nzima kwa kupanikisha watu na mataifa mbalimbali na kugeuka adui wa binadamu’
“Lakini ukiachana na hayo , kwasababu mimi sio yeye ninaweza kukisia kiasi kidogo tu cha mipango yake yote , lakini bado lazima itakuwa ni kutokana na ramani ya unabii wake wa mwanzo , kwa maana kwamba uwezo wako ungeendelea kuwa mkubwa sana kutokana na kupigana kusiko isha , lakini mwisho wa siku hakuna alietarajia kama Seventeen atakukimbia akiwa na mtoto kutokana na mapenzi yake ya dhati kwako, akiamini kukuacha utaacha kuua na kutubu na kutokufa mwishowe , mara baada ya kurudi kwako Tanzania uliamua kuishi maisha ya kawaida na ukaacha na tamaa za kuona damu kitu ambacho Athena hakukitarajia kabisa .Haukua mtu ambae unaweza kuacha kuua kirahisi na kuzembea bila kazi yoyote maisha yako yote, haikuwa mipango ya Athena kukuona ukiwa hivyo”
“Hivyo basi mara baada ya kushughulikia swala la Lanlan , Athena hakujali tena kurudisha nguvu yake yote ya kiroho na moja kwa moja akaingia katika mwili wa Edna , mara baada ya kukutana na wewe katika sura ya Edna aliamua kutumia unabii wake kukutengenezea njia za kupita , mwanzoni alikuwa akimtumia Yan Buwen kupitia jiwe la kimungu ambae aliwezesha kuitumia nishati ya Ant – matter na kukuletea ushindani mkali lakini kuna vitu havikumridhisha kuhusu Yan Buwen na akatabiri kifo chake kwa kumuingiza Joseph Bikind(Lekcha) ambae alishamuandaa muda mrefu ambae ndio alikuwa hatari zaidi ya Yan Buwen na ulikuwa ni mpango mujalabu sana kumchagua Lekcha maana ulijikuta ukipambana nae mpaka ukaja kuingia kwenye ulimwengu mwingine kupitia mnara.
Yan Buwen kwa upande wake utafiti wake ulikuwa ni kutengeneza miungu feki kwa kukusanya nguvu ya kiroho kutoka katika Dhana mbalimbali ikiwemo Hollygrail, Thanatos na kadhalika ili tu kuimarisha Clone ya sura yako lakini mpango huu ulionekana kubuma kutokana na kwamba haukuchangia vizuri kwenye matokeo ya unabii wake hivyo aliupotezea mara baada ya mtafiti mwingine aliemwandaa kupitia Project Pro Human kufanikiwa kugundua sayansi ya kutumia elementi za dunia tofauti na nishati ya Ant-matter kufufua moyo wa Gaia, hivyo kwa lugha nyepesi alipotezea tafiti zote za Yan Buwen”
Kila sentensi alioongea ilikuwa ni kama ngurumo ya radi katika masikio ya Roma , ijapokuwa alikuwa amejiandaa lakini hakuamini Athena alikuwa amefanya mambo mengi namna hio kwa siri.
Roma aliona alikuwa amepitia katika hatari nyingi lakini zote alikuwa amezipita , kuna hata muda mtu alievaa joho la rangi nyeusi na mask alimuokoa kule Australia pengine yote hayo yalikuwa ni maagizo ya Athena.
Ilikuwa sahihi kabisa kwa Roma kuwaza hivyo , mwanzoni alihitaji Roma kuua sana tu kama kichaa ili kuwa na maadui wengi na kupitia changamoto hizo za maadui uwezo wake ungeendelea kuimarika maradufu sana , lakini mapenzi ya Seventeen kwenda kwa Roma yakamuokoa pale mwanamke huyo alipoamua kumuacha Roma baada ya kuona hana nia ya kuachana na ukichaa wake wa kuua.
Roma mara baada ya kushuhudia kifo cha Seventeen kwa macho yake kule kuua kulipoa kabisa mara baada ya kujua nia ya Seventeen kupitia janga la namna ile.
Kipindi haya yanatokea Athena alikuwa usingizini lakini haikumaanisha kwamba mipango yake ilikuwa haiendelei lakini kutokana na kutosimamia njia za unabii wake baada ya kuamka ndio anaona kabisa unabii wake unavyopaswa uwe umebadilika.
Mchoro wa Unabii ambao alimuonyesha Naira ndio ilikuwa ni hatima ya unabii wake , kama alivyosema katika kauli yake kipindi wanaongea sura ya mwanamke katika mchoro ule haikupaswa kuondoa tabasamu , kadri picha itakavyokuwa katika tabasamu ilimaanisha ndio namna ambavyo unabii wake unaenda sawa sawa , lakini baada ya kuamka pengine mwanamke hakuwa katika tabasamu na alikuwa amenuna kama mchoro wa unabii uliotolewa na Vatican.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Athena alikuwa akishindana na unabii , alikuwa akishindana na hatima ya binadamu , alikuwa akishindana na hatima ambayo aliwekewa Roma kuja kuwa mwangalizi baada ya Sharif.
Ni dhahiri kabisa kulikwepo na unabii wa Roma kukidhi vigezo vya kuwa mwangalizi kwa kumrithi Sharif, unabii huo Athena aliufahamu lakini akaamua kuubadilisha kwa kubadilisha matukio yanavyoenda na hatimae historia.
Sasa kifo cha Seventeen hakukitarajia lakini vilevile hakutarajia ujauzito wa Seventeen , hakutarajia Roma ataacha kuua kama alivyokuwa mwanzo na kurudi Tanzania na kuwa mbeba mizigo na kuishi katika chumba kimoja cha kupanga.
Hivyo ili kurekebisha makosa akaamua kumuingia Edna akijua fika ni pacha wa kufanana wa Seventeen na akamtumia Edna kumfanya Roma apende kama alivyompeda Seventeen.
Kitendo cha Roma kupenda ilimaanisha kabisa lazima awajibike kwa wale ambao anawapenda kwa maswala yote ikiwemo ulinzi na hapo ndipo alipomuingiza Yan Buwen kuwa tisho la usalama wa watu wake wa karibu , alijua kadri ambavyo Yan Buwen atakuwa tishio ndio Roma atajitahidi kupandisha uwezo wake ili kumlinda anao wapenda.
Kwahio ukiachana na kwamba Athena alilenga tafiti za Yan Buwen kumsaidia katika kufufua miungu vilevile alitumia tamaa za kimwili za Yan Buwen kumletea Changamoto Roma , pengine Yan Buwen alijua mrembo Athena alikuwa akimpenda Roma au alikuwa akimhadaa kumuonyesha alikuwa akimpenda Roma ndio maana Yan Buwen kujenga kinyongo kikali zidi ya Roma.
Lakini baadae Naira kupitia tafiti zake aligundua mbadala wa kufufua moyo wa Gaia kwa kutumia elementi za dunia nje ya nishati ya Ant- matter
“Kuna kitu kingine kilichonivutia sana wakati wa kuangalia haya yote ni kwamba , kati ya miungu watatu yaani Hera , Hephaestus na Hermes hawampendi Athena na ndio maana Hera aliamua kwanza kujifunza mbinu za nishati ya mbingu na ardhi na kisha akahamia katika mwili wa jinni na kujifunza mbinu ya kutabiri ambayo haikuwa nzuri sana kama ya Athena ambae alizaliwa na Karama hio lakini hata hivyo bado ilikuwa na maajabu yake kwani iliweza kutabiri mambo mengi ya baadae kwa usahihi
Hawa wote hawakuchagua miili ya majini na ya Vampire bila sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kuongeza umri wa kuishi bila kuhama hama katika miili mingine kuepuka kulala muda mrefu , walifanya hivi ili kuvuruga mpango wa Athena wa kutafuta Moyo wa Gaia ulipo wakati Athena akiwa usingizini akisubiria kuamka katika mwili mwingine , baadae wakifanikisha wamuue Athena kama kiongozi , nadhani umesikia kuwa Athena ana uwezo wa kutawala fahamu za miungu wa chini yake , hio ni moja ya sabababu ya kutaka kumuua lakini kwa bahati mbaya mipango yao ilifeli”
“Kwa mfano kuhusu ile Dhana feki ya Magical Girdle ulikuwa ni mpango ambao waliamini kama Edna atakuwa hatarini Athena atakosa jinsi na kuonyesha uwezo wake kumlinda Edna na hapo wewe baada ya kufika eneo la tukio ungeweza kumuona Athena katika mwili wa Edna lakini Athena alijizuia mpaka mwisho na hakumsaidia Edna na ikatokea tu ukawa umefika ndani ya muda , haikuwa hivyo tu waliamua pia kumtumia Chriss kutaka kumuua Edna lakini kwa bahati nzuri Athena alishafahamu hila hio na kumtumia moja ya mshirika wake kumlinda Edna”Aliongea Sharif na sasa Roma ni kama anapata majibu.
“Vipi kuhusu Ant- Illuminat na Hades wa Zamani?”Aliuliza Roma kwa shauku mara baada ya kukumbuka kitu muhimu.
“Tunaelekea huko taratibu…Kulikuwa na siku nyingine pia nadhani unakumbuka mara baada ya Hermes kuingilia akitaka kukuzuia kumuua Denisi , ule pia ulikuwa ni mpango wao tokea mwanzo wa kutaka kuvuruga mpango wa Athena , mwanzoni kama ungemuua Denisi mdogo wako ingekuwa ngumu kwako kukubali kurudi katika familia ya ukoo wako na ungekuwa upande mwingine tofauti na serikali ya Tanzania ambayo inaongozwa na baba yako lakini Athena bado hakutaka kuingilia lakini mwishowe aliamua kutengeneza mpango mwingine ambao utamfanya Denisi kupoteza uhai”
“Kuhusu Ant- Illuminat kusudi la mwanzo la kuanzishwa kwake sio kama la sasa , kama ilivyo kwa Freemason kusudi la mwanzo la kuanzishwa kwake sio kama la sasa”
“Unamaanisha nini?”
“Illuminat ilianzishwa chini ya ushawishi wa miungu hili sitoongelea sana maana lipo kibinadamu zaidi lakini linahusiana na maswala ya kidini zaidi na haliingiliani sana na wewe , vilevile Ant- Illuminat ilianzishwa chini ya ushawishi wa miungu na ilikuwa juzi tu zaidi ya miaka elfu moja iliopita , Hades wa zamani na Athena walicheza karata nyingi sana katika kuanzishwa kwa umoja huu lakini wote walikuwa wakilenga shabaha moja , Athena na Hades wa zamani waliamua kugeuzana maadui wa faida na hili lilikuwa moja wapo ya ombi la Athena ukiachana na kukupatia uungu wake na Dhana ya helms of invisibility , unachopaswa kuelewa tu Hades alikuwa neutral katika kufufuliwa kwa miungu na yote ambayo amefanya Hades yalikuwa maombi ya Athena , kuna muda ili ufikie malengo unahitaji mshindani ambae hana hila tofauti na walivyo Hera na wenzake na huyo ndio Hades alivyokuwa kwa Athena”
“Athena alisumbuka sana kuweka mambo sawa kwa ajili ya kudumisha unabii wake lakini hata hivyo kulikuwa na baadhi makosa madogo madogo lakini napaswa kumkubali kwani licha ya changamoto zote aliweza kuzishinda na kukuruhusu ufikie levo kubwa ya mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi mpaka leo hii tena ndani ya muda mfupi tu lakini wakati huo huo kunifanya mimi kuvutiwa na uwezo wako na kukupa fursa ya kufanya maamuzi”
“Bora hara nisiwe na hizo nguvu , wewe mwenyewe umeshindwa kufanya maamuzi na ndio unataka mimi nibebe lawama?”Aliongea Roma akiwa na tabasamu.
Sharif alisimama akiwa na tabasamu lisiloelezeka na kisha alimshika Roma bega kwa kulipiga piga.
“Dogo umekosea , nilishafanya maamuzi miaka elfu ishirini iliopita ambayo ni kuwa Neutral kwa pande zote , sitokulazimisha kwa lolote kama utaamua kumtetea Athena na kuacha kupigana ni sawa tu , nimekuja hapa siku hii kwa ajili ya kukueleza ukweli ambao unastahili kujua , kuhusu mengine ni juu yako na hatima ya binadamu pia, misheni yangu ilikuwa ni kulinda dunia na sio binadamu moja kwa moja wala kuingilia imani zao na matendo yao , vilevile kwa miungu sikupaswa kuwaingilia”
Mara baada ya kuongea kauli hio Sharif aligeuka na kupotea kama upepo bila kuacha ishara yoyote nyuma.
Hata kwa Roma aliekuwa na uwezo wa juu hakuweza kujua amepotea potea vipi kwani ni kama ameyeyuka.
Hatimae Lounge ya bar hio katika hoteli ya JR ilirudi kimya kwa mara ningine , Roma alijikuta akiegamia sofa akiangalia mwanga hafifu wa taa uliokuwa ukimulika kana kwamba anaushangaa.
*****
Ilikuwa ni nusu mwezi tokea kuharibiwa kwa mfumo wa kiutendaji wa ulinzi wa Gereza la Roho ambalo hufungia miungu na majini , Dhana ya Reverse Dhamachakra ilionyesha kufanikisha lakini wakati huo ile kasi yake ilionekana kupungua.
Ule mng’ao wake wa Dhahabu haukuwa mkali kama mwanzo , kulikuwa na msisimko mdogo sana uliokuwa ukitoka katika Dhana hio na wakati huo nguvu nyingi hasi ilikuwa imejikusanya katika eneo dhaifu la ulinzi wa safu ya gereza hilo.
Muda huo miungu tisa walikuwa wakiangalia sehemu hio Dhaifu kana kwamba kuna kitu wanachokisubiria.
“Haijawa na matokeo mazuri sana lakini hio safu haiwezi kushikilia kizuizi kwa muda mrefu”Aliongea Hephaestus kwa kujiamini.
“Naona unajigamba sasa , wewe huoni ni kama hili swala linachukua muda mrefu na kutupotezea muda tu hapa?”Aliuliza Ares akiwa kachukia.
“Haina maana hata nikikuelezea kwasababu punguani kama wewe unachojua ni kupigana tu na haujui hata nguvu ya ulinzi wa Gereza unavyofanya kazi”Aliongea Hephaestus akimwangalia Ares kwa macho ya dhihaka.
Ares kauli ile ilimkasirisha sana na alitaka kumshikisha adabu Hephaestus lakini jicho baya na la kikauzu la Athena lilimtuliza na kisha alimgeukia Hephaestus akimpa ishara asimchokoze mwenzake na kusababisha matatizo yasio na maana , akiwa amenyoosha mkono wake juu angani alionekana kushikilia kitu flani.
Kiumbe kilichovalia mavazi meusi kilionekana palepale , alikuwa ni Mtu mwenye Mask na alionekana kuhangaika kujinasua kutokana na kushikwa na mikono ya Athena kupitia kanuni za anga.
“Nisamehe mimi .. sina nia mbaya kujificha”
Miungu wengine hawakuwa na macho ya kuona kama ya kwake hivyo hawakuweza kuhisia uwepo wa mtu na waliishia kushangaa kuona Athena kakamata mtu.
“Hivi ulidhani sitokuona kwa kujificha mbali?”
“Sikutaka kuwasumbua ndio maana nikaangalia kutokea mbali”
“Athena hicho ni kiumbe gani , mbona kama sio binadamu wala jini?”Aliuliza Aphrodite kwa mshangao
Athena mara baada ya swali lile alimwachia yule mtu mwenye Mask.
“Unaweza kujionyesha sasa , haina haja ya kuendelea kujificha kwenye Mask”Aliongea Athena.
Mara baada ya kauli ile kutoka kwa mtukufu Athena kiumbe kile hakikutaka kuchelewa hata sekunde na ilikuwa ni kama vile umetokea moto ghafla kama wa kipepo ulioanza kuyaunguza mavazi yake na ile Mask.
Punde tu kitu cha ajabu cheusi kama ukungu kiliweza kuonekana mbele ya miungu.
Ilikuwa ni kama ukungu mweusi uliozunguka kile kiumbe na kufanya iwe ngumu kuona sura , ijapokuwa walikuwa wakiona umbo la kibinadamu lakini ile sehemu ambayo ilipaswa kuwa kichwa kulikuwa na kitu kama fuvu.
Kiumbe hicho chenye muonekano wa kutisha kiliwafanya miungu kupiga hatua moja nyuma huku wakikunja sura kama wameingiwa na kichefu chefu.
“Kwa miaka kadhaa iliopita hiki kiumbe kimekuwa kama njia ya mawasiliano kati ya Zeus na mimi ni jini aliezaliwa katika umbo la kivuli ambae kwasasa ni Mzimu wa jini mkubwa wa kipepo aliewahi kuwepo , ijapokuwa huu mzimu una uwezo mkubwa kulinganisha na levo ya maji ya upako lakini upo vizuri kwenye kujificha na kuwa katika sura tofauti tofauti”Aliongea Athena.
“Ni mzimu wa jini la kale?! , imewezekana vipi kutoka katika gereza la roho?”Hera aliuliza kwa mshangao
“Haha.. haha.. hahaha…ukweli ni kwamba sio kama nimetoka nje lakini mimi ni moja ya majini pepo wa tofauti sana”Aliongea huku akitoa kicheko cha ajabu mno.
Miungu palepale waliweza kuelewa ilionekana mzimu huo uliweza kutoka nje ya gereza kwasababu ya kuwa na miili mwili
Wakati jini Kivuli anazaliwa alikuwa na mwili wa kawaida na wa kivuli , miili yote ilikuwa chini ya udhibiti wake na ilikuwa na uwezo sawa .
Sasa mwili wa kawaida ili mradi tu utakuwa hai basi ule wa kuvuli unaweza kuwa popote.
Miaka mingi iliopita wakati wajumbe walipokuwa wakitenganisha majini pepo watukutu katika gereza la roho Jini Kivuli alikuwa akijua hana uwezo wa kuwashinda hivyo alijiengua kutoka katika mwili wake wa kivuli ambao ulikuwa na uwezo wakujificha na akajifanyisha amekufa kwenye vita , sasa mara baada ya mwili wake mkubwa kufungiwa katika gereza alitafuta namna ya kurudia mwili kivuli ambao ameuacha nje.
Wajumbe hao licha ya uwezo wao haikumaanisha kwamba walikuwa wameondoa majini yote kwa kuyafungia ndio maana hata yale walioyabakisha waliyawekewa mtego , majini walikuwa wengi mno karibia dunia nzima , sasa mwili kivuli ulibakia nje wakati roho ikiwa katika mwili mkubwa na mara baada ya muda mfupi alikuwa na uwezo wakuifanya roho yake ya nje kuwasiliana nae kutokana na kuwa na miili inayofanya kazi ndani na nje , sasa hapo ndipo mwili kivuli uliwasiliana na Athena na mwili wa kawaida uliwasiliana na Zeus na muda mwingine alitumia mwili wa kivuli kwa ajili ya kufanya maelekezo ya Athena bila hata ya kwenda mwenyewe.
“Umelificha hili swala vizuri sana , kumbe ulikuwa na mawasiliano na Zeus muda wote huo hatuambiani?”Aliuuliza Hera akionyesha jambo hilo lilivyokuwa chungu kwake.
“Tumeanza kuwasiliana miaka miwili iliopita , kwasababu Kivuli alikuwa mbali na mwili wake mkubwa hivyo alikuwa na wasiwasi wa kukutana na majini watu ambao wataweza kumuua , ilichukua miaka elfu kumi kuweza kupona katika hali ya kifo , kabla ya hapo sikuwa nikijua hali ya Zeus ndani ya gereza”
“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Zeus amewashinda majini pepo wote wa zama za kale na mishetani ndani ya gereza , kwahio ndio kwamba tuna vijakazi wa kutosha tu sasa hivi?”Aliuliza Hermes na tabasamu la kifedhuli.
“Ninachojua majini pepo wengi na jamii ya mashetani hawajazaliwa kutoka katika miili kamili na hata uwezo wao unaenda taratibu taratibu na mara nyigine walikuwa wakivaa miili ya binadamu au wanyama kuonekana lakini kwa huyu Kivuli mpaka kufikisha levo inayolingana na maji ya kiroho ni lazima liwe ni la kipekee , majini pepo wengi ni wabaya wa sura na wanatisha mno kama unataka wawe vijakazi wako unaweza kuwatumia”
Jini Kivuuli alisikiliza ki uwoga woga na ilikuwa ni kwa bahati mbya hakuwa na uwezo wakuonyesha muonekano wa kibinadamu vinginevyo maelezo ya Athena yangemfanya kuonekana na aibu.
Ilikuwa kweli kabisa baadhi ya majini pepo na wale mashetani waliohesabika kuwa na nguvu kubwa waliweza kuuliwa na wajumbe wa mkuu wa Enzi makumi elfu ya miaka iliopita.
Lakini ukiachana na machache ambayo yalikuwa yamefungiwa ndani ya geereza hilo uwezo wao ulikuwa ni kidogo sana , sasa tofauti na kuendelea kushikiliwa na gereza hilo ni kheri kuwa huru hata kama watadhalilishwa na miungu.
“Kwa uwezo wa Zeus ni kawaida kuweza kuwashinda majini pepo wote wafungwa na kuwa mfalme lakini nina wasiwasi na mwili wake wa sasa , amewezaje kuishi katika mwili mmoja kwa miaka elfu ishirini yote , maana hawezi kutoka nje na kuhama kwenye mwili mwingine?”Aliuliza Apollo.
“Ana njia zake , utajua akishatoka”Alijibu Athena.
*****
Upande mwingine upepo wa baridi kali ulikuwa ukivuma juu ya bahari ya Meditterranian , wingu la kijivu lilikuwa limefunika anga lakini walisimama na hakuna upepo ulioweza kuwapeperusha.
Anjiu na majini wenzake kumi walipata kurudi kisiwani kwa Roma na habari za Edna kuwa Athena na ilikuwa ni kama bomu kwa kila mtu.
Hatimae wanawake hao walijua ni kwanini mara kwa mara Edna alionekana kumuacha Lanlan na kupotea.
Kuhusu Roma mhimili wa familia alikuwa amepotea na haikujulikana alikuwa wapi na iliwafanya kuwa na mawazo.
Kitendo cha kukosa wazazi wake wote kwa muda mmoja ilimletea Shida Lanlan na kusumbua kwa siku kadhaa lakini mwishowe Neema , Rose na wanawake wengine ilibidi watoe taarifa nyumbani kwa Afande Kweka na Blandina ambae mara baada ya kusikia habari hio alifanya safari ya kuja kisiwani na hakuwa peke yake hata Afande Kweka aliamua kutembelea kisiwani.
Blandina alikasirika mno mara baada ya kusikia Edna alikuwa ni Athena , aliona mtoto wake alikuwa akichezewa akili lakini ukiachana na mawazo yake mengine aliiishia kumlaumu Edna na kumuita kila jina baya.
Wanawake hao hawakupendezwa kusikia kauli za Blandina lakini walikaa kimya kwani hawakuwa na uhakika kama Edna alifanya hayo yote kwa akili zake , hakuna aliejua ukweli.
Walichojisikia ni huzuni kwa ajili ya Roma na hivyo ilipelekea kuwa na chuki kiasi zidi ya Edna.
Kwa Blandina Edna hakuwa na umuhimu mkubwa kama ilivyo kwa mtoto wake na hio ni kutokana na kwamba ndio mtoto pekee aliekuwa nae.
Alilalamika huyo lakini mwisho wa siku aliacha mwenyewe na sasa alichokuwa akitaka kusikia ni taarifa za Roma alipo tu , kila siku alikuwa akihimiza majini waliokuwa ndani ya kisiwa hicho na hata wanajeshi wa The Eagles kumtafuta Roma.
Lakini mwisho wa siku hakuna ambae aliweza kumpata kama Roma mwenyewe ndio aliamua kujificha , hata Sauron au Anjiu hawakuweza kumpata , lakini waliendelea kutafuta kutokana na maagizo yalitoka kwa mama yake Roma.
Upande wa Afande Kweka alikuwa hana wasiwasi wowote ni kama vile hakujali kile kilichomtokea Roma na alifikiria mbinu tu za hapa na pale za kumchekesha Lanlan.
Lakini Lanlan licha ya kwamba alifurahi uwepo wa babu yake lakini bado hakuwa na amani na hata ile hamu ya kula ilikuwa imempotea.
Kila mtu alikuwa katika wakati mgumu lakini sasa siku mbili baadae ghafla tu hali ilibadilika.
Ilikuwa ni vivuli tu ambavyo vilionekana vikisafiri kwa kasi kwenye anga kama vimondo vikisambaa kila uelekeo .
Mara baada ya Anjiu , Shombeli na wengine kuona tukio hilo walijikuta wakikamaa sura mara baada ya kuona hali imekuwa ya hatari.
“Majini pepo na mashetani wamevamia ulimwengu wa kawaida , Gereza la roho limefunguka!!”
Waliongea wote kwa kumaka wakiambizana.

SEHEMU YA 789.
Ni siku chache mbele tu hali ilikuwa imebadilika na kuwa mbaya zaidi , katika anga la China na majirani zake wingu kubwa lilikuwa limetanda , licha ya kwamba ilikuwa mchana ilikuwa ni kama usiku.
Ki uhalisia ni kwamba ilichukua nusu siku kwa kila eneo ndani ya dunia ambalo lina watu kubadilika na kuwa katika hali ya kutisha namna hio mara baada tu ya Gereza la Roho kuvunjwa.
Watu ambao walikuwa wakiepuka kwa namna yoyote baridi kali la kuumiza mifupa hawakuwa na uelewa juu ya janga la asili kwanini limetokea na kutisha hivyo.
Lakini wakati wakijiuliza kwanini joto kushuka licha ya jua kuonekana angani wanakuja kujua sio kitu kirahisi tu kama kushuka kwa joto.
Yale mapepo ambayo watu wa kawaida hawawezi hata kuelewa yalianza kuonekana moja baada ya nyingine katika sayari yote ya dunia , halikuwa ni swala la Afrika wala Ulaya tena , mapepo yalikuwa kila mahali.
Yale mapepo na maskeletoni ambayo watu waliishia kuyaona kwenye filamu sasa yalikuwa mbele ya macho yao mubashara, ilikuwa ni taharuki juu ya taharuki.
Wakati mengine yakipita tu na kuingia misituni mangine yalichagua kuingia binadamu na kuwashambulia na kufanya damu kila mahali kutapakaa.
Licha ya kwamba yalikosa miili lakini uwezo wao wa kuchanganya akili za binadau na kushambuliana wao kwa wao ulikuwa mkubwa sana.
Yaani ilikuwa ni swala la kumvamia huyu binadamu na kisha kumuua biadamu mwingine na kuacha mwili , ilikuwa ni kama binadamu wamegeuka mazombi.
Kama ingesemekana dunia ilikuwa ikitaka kuingia katika kizazi cha barafu na binadamu kuwehukwa na akili basi picha iliokuwa ikionekana ilikuwa ni zaidi ya neno kifo.
Awamu hio haikuwa swala la matajiri tu wala masikini , kila mtu alikuwa ni mhanga.
Kitu kikubwa ambacho watu walikuwa wakifanya mbele ya Maskeletoni hayo pamoja na mizimu hio ya kipepo ni aidha kuomba sana au kuswali wasivamiwe na mapepo kugeuka vichaa au kusubiria kifo mbele ya maskeletoni.
Hali ilibadilika ghafla sana hata wale watu waliokuwa na akili za ziada walishindwa kuelewa wala kufanya utafiti ya kinachoendelea na ilikuwa ni kujiuliza maswali ni nini kinaendelea huku wakihaha.
Majini watu kutoka miliki za kijini walijua uhatari wa hali mara baada tu ya kugundua ni wale majini waliokuwa katika gereza la roho.
Majini wa miliki ya Hongmeng hawakuwa wajinga kulinda gereza hilo la roho kwa miaka mingi vizazi na vizazi lakini hakuna ambae alitegemea ni karne hio gereza hilo litafunguliwa.
Punde tu Shombeli , Umini na wengine waliamua kujigawa na kusambaa kila kona ya dunia kwa ajili ya kushambulia majini pepo hao.
Kutokana na nguvu za majini hayo zilikuwa katika levo za nafsi na wengi wao akili zao zilikuwa chini haikuwa ngumu kudili nao na pengine ndio kitu cha pekee cha kushukuru.
Majini walishambulia mapepo hayo licha ya kwamba walijua dunia ni kama inafikia mwisho wake , lakini walijiambia kama wanaweza kuchelewesha basi watafanya hivyo.
Upande wa wanawake ambao walikuwa wakimsubiria Roma walichoka na wao mara baada ya kutokuonekana kwake na hawakuwa na jinsi ya kumsubiri tena na wale ambao walikuwa tayari katika levo ya nafsi waliungana na majini kushambulia hio mizimu , mapepo na maskeletoni.
Kutokana na kuwa na Dhana nyingi za kimaajabu ambazo Roma aliwapatia hawakupata shida sana ya kudili nayo lakini baadhi ya majini pepo wale wa kale walionekana kuwa ngumu sana kudili nao kutokana na uzoefu wao wa kivita na akili kubwa kama alivyokuwa jini Kivuli na wengine walikuwa katika levo yake.
Ndani ya siku mbili tu taarifa zilirudi majini zaidi ya miambili walishakufa kwa kuuliwa na baadhi walirudi wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana huku wakiwa wamewekewa sumu ya ajabu katika miili yao
Mwishoni Anjiu na wenzake wenye uwezo wa juu walitoa maagizo kama itatokea kuna mzimu au jini pepo lenye nguvu kubwa sana basi taarifa itolewe na wao wataenda kudili nalo , ijapokuwa sio njia salama lakini ndio iliokuwa imebakia.
Dunia ilikuwa imebadilika kutoka kuwa barafu na sasa ilikuwa ni kuzimu.Haikujalisha ulikuwa mfanyakazi wa kawaida , tajiri , mrembo , star au kiongozi wa siasa au mwanajeshi wa nyota zote kila mtu alikufa kifo kibaya aidha kwa kushambuliwa na maskeletoni au kuwehushwa akili.
Wengi ambao walisalimika ni wale ambao walijijengea nguvu ya kiroho kwa muda mrefu kupitia kusali na kuswali pamoja na wale wenye ushirikina wenye nguvu na wanaojjimilikisha majini roho, majini jamii ya watu walioshindwa kupata miili na kubakia viumbe wanapandisha levo zao kupitia binadamu..
Mpaka kufikia muda huo ni kama udhaifu wa binadamu zidi ya viumbe wasioonekana umedhihirika, maana makombora na bunduki hazikufanya kazi.
*****
Ni katika taifa la China upande wa kusini , jiji hilo ambalo lilikuwa likipendeza nyakati za usiku muda huo kilichokuwa kikionekana ni maiti za biadamu na wanyama ambazo zimesambaa kila mahali.
Mji ulikuwa kimya mno na hakukuwa na dalili hata ya ndege anaepaa angani , maduka makubwa ya nguo , viwanda na magari yalikuwa yametelekezwa .
Taifa kubwa kama la China ambalo limeendelea hawakuwa na kinga zidi ya baridi kali ilioikumba dunia , pengine ndio nchi ambayo imeathirika sana kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu , hali ilikuwa ikisikitisha kweli.
Sasa katika mitaa hio ambayo ilikuwa kimya mwanaume mweusi ambae alionekana kuchafuka kama chokoraa akiwa ameshikilia chupa ya Whiskey alionekana kutembea katikati ya mtaa.
Mwanaume huyu alionekana kama mlevi ambae hana makazi maalumu.
Naam huyu ni Roma Ramoni ambae alikuwa akidhurula kwa siku nyingi mno katika kila taifa bila sababu za msingi .
Tokea aachane na Sharif Roma hakujua ni wapi aelekeee wala maamuzi gani afanye.
Mara baada ya kukaa katika ile hoteli kwa usiku mmoja asubuhi kulivyokucha alitoka akiwa hana wazo lolote katika akili yake na ndipo alipoanza kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine , alianza bara la Afrika lote na kisha alijikuta akiwa ulaya na akaingia Asia, kwa namna ambavyo alikuwa akidhurula ni kama kuna kitu ambacho alikuwa akitafuta.
Sasa katika mitaa ya vijiji baadhi vya nchi hio ya Wachina Roma aliweza kuangalia namna ambavyo mizimu ilivyokuwa ikihaha huku na huko ikishambulia binadamu.
Lakini Roma hakujali hata pale aliposhuhudia binadamu wakinyonywa damu na nafsi zao kuibiwa, Roma alijifanyisha kipofu kabisa.
Mambo yote hayo kwake ni kama hayakuwa yakimuhuisu kabisa .
Majini pia ni kama yalikuwa yakijua Roma alikuwa na uwezo mkubwa na kwa utashi wao waliweza kusogea mbali bila kumsogelea.
Katika kila majiji aliopita kilichokuwa kikimvutia ni vinywaji tu vitu vya thamani vilivyotelekezwa kwake havikuwa na maana tena, alikuwa akiogopa kuacha kulewa kwani angeanza kufikiria ni kipi anapaswa kufanya , ki ufupi ni kwamba alikuwa akijisahaulisha kile kinachoendelea kupitia pombe.
Boom!!!
Ghafla tu mlipuko mkubwa ulitokea kutoka katika moja ya jengo la makazi mita kadhaa kutoka alipo.
Moshi mwingi ulionekana ukisambaa angani na ni palepale aliweza kuona mtu alievalia mavazi ya bluu akijitahidi kujitoa katika kifusi cha mchanga na matofali.
Sekunde chache mbele walionekana majini wawili mwanaume na mwanamke wameshikilia siraha ndefu wakimkimbilia mwanaume wa kibinadamu ambae amefunikwa na kifusi kumsaidia na wakimuuliza kama alikuwa ameumia.
Mwanaume alievalia suti ya rangi ya bluu uso wake ulikuwa mweusi na kulikuwa na dalili za damu kumtoka midomoni lakini aliishia kusugua meno yake akionyesha ishara kwamba hakuna tatizo , muonekano wake wa kuvumilia maumivu ulikuwa tofauti na ishara zake ..
Roma alisimama kwenye kona ndani ya mtaa akiangalia tukio hilo na palepale kulikuwa na hali tofafuti katika macho yake na alionekana kusita lakini hakuweza kusaidia zaidi ya kusimama tu.
Muda huo huo msichana ambae amvalia gauni la pink ambae ni jini mtu alionekana kumuona Roma ambae amesimama kwenye kona mbali na wao na alianza kumpigia makelele Roma..
“Usisogee hapa ni hatari , ondoka kabisa eneo hili”
Kabla msichana yule kukamilisha sentensi yake mwanaume aliekuwa pembeni yake alimkemea.
“Dada kuwa makini”Aliongea
Kutoka ndani ya jengo hilo lilitoka puto kubwa kama baluni jeusi ambalo lilianza kufuka moshi kuelekea mbele ya wale watu.
Yule mwanaume alisimama mbele ya yule mwanamke na siraha iliokuwa mikononi mwake ilimtoka kwa kuelekea upande wa lile puto.
“Bro Zomu kuwa makini , hilo ni shambulizi la sumu”
Mwanaume aliekuwa katika mavazi ya suti alipiga yowe akipotezea kuumia kwake.
Om! Wah ! Pah ! mi Hum!!
Yule mwanaume aliekuwa katika mavazi ya bluu alianza kunena kwa lugha ya kibudha maarufu kama mantra kama vile alikuwa akiimba.
Mwanaume yule alikunja ngumi yake na huku akitoa uchawi wa kufuta nguvu ile ya kipepo na kulipiga lile puto.
“Bang!!”
Sauti ya ajabu iliweza kutoka katika lile puto la ukungu na palepale ni kama vile lilibadilika na kuanza kutoa miale ikionekana ni kama linataka kupasuka.
Lakini ni dakika hio hio jitu la ajabu ambalo lilikuwa na mwili wa ukungu lilijitokeza kwa kuibukia kwenye lile puto.
Jitu hilo lilikuwa na mapembe mawili kwenye kichwa chake , midomo kama kipande cha chapati uliozungukwa na sharubu ndefu kama za chui, macho mekundu kama damu na mwili kama wa simba , juu ya mkia wake kulikuwa na vitu kama ufagio wa ajabu ambao ulifanya lizidi kuogopesha.
Jitu lile lilitoa tabasamu la ajabu mno la kutisha na kuanza kuchezesha mkia ule juu angani na kutengeneza wimbi ambalo liliwatupia mbali wale watu.
Watatu hao walionekana kutokuwa na nguvu za kutosha kupambana na mzimu huo na waliishia kutema damu.
Lile lizimwi liling’aka kwa sauti kwa namna ya majigambo huku likitoa moshi kama wa gari wenye sumu kwenda chini , kucha zake zililianza kurefuka na lilijiandaa kunyofoa shingo ya yule msichana na kunyonya damu yake.
Mara baada ya kuona mzimu huo wa jini pepo ukimsogelea yule mwaamke ilimfanya aogope sana kiasi cha sura yake kupauka alichoweza ni kufumba macho yake akikisubiria kifo.
Kabla ya tukio lile la kutisha kutokea , walichoweza kusikia ni mbweko wa maumivu kutoka kwa mzimu ule.
“Ghrrrrrrrr…!!!”
Moto uliokuwa kama nyoka nyoka ulionekana kuuzingira ule mzimu na kufanya uanze kutapa tapa lakini bado lilionekana kushindwa kujinasua kutoka kwenye kuyeyushwa na ule moto.
Kufumba na kufumbua lilipotea kama mvuke na kukawa kimya na ajabu ni kwamba ule moto ulinyonya ule moshi wote wenye sumu a kuwafanya wale watu kupumua vizuri
Watu hao watatu waliangalia kwa bumbuwazi kile kilichotokea na mpaka moto ule unapotea na kurudiwa na akili waliweza kuona yule mtu ambae alionekana kama chokoraa akiwaangalia
“Nyie wote watatu hata kama muungane mtakuwa na uwezo angalau wa maji ya kawaida lakini bado tu mnajaribu kushindana na pepo ambalo lipo levo ya maji ya barafu, kwanini ya kujisumbua kama mnataka kufa”Aliongea Roma na kisha aligeuza akitaka kuondoka.
Mwanaume na mwanamke walikuwa ni majini na walifahamika kwa jina la Zomu na Zato ambao walikuwa ni washirika wa miliki ya Kekexil, mwanaume alievalia nguo za bluu alikuwa ni binadamu mwenye mafunzo ya kijini aliefahamika kwa jina la Feilo.
Kama isingekuwa kwa watu hao kumchukulia kama rafiki na yeye pia kuwahukulia kama marafiki Roma asingejali kabisa kuhusu maisha yao.
“Hey! Subiri”
Zomu alijikuta akisimama licha ya kusita sita na kujikaa kumuita Roma .
Feilo na Zomu walisimama pia kwa haraka , neema ya kuokolewa uhai wao haikuwa jambo jepesi hivyo hawakutaka kudharau.
“Asante broo kwa kuokoa uhai wetu , naweza kujua jina lako , pengine nikipata nafasi naweza kukulipa fadhila baadae?”
Zomu alimpita Roma kwa mbele na kumwangalia usoni kwa namna ya kunuia au kutokunuia.
Roma alichukua chupa yake ya Whiskey na kupiga pafu moja na kisha alipunga mkono.
“Haina haja ,ondoka nipite”
Alimsukuma Zomu na kisha aliendelea zake kutembea kuingia katikati ya mji.
Lakini kabla hata hajapotelea Zomu aliita kwa nguvu,
“Bro Xiao Cheni!!”
Roma alishangaa kuitwa jina hilo na aliishia kusimama kama kagandishwa.
“Nipo sahihi , ni Braza Xiao Cheni”Aliongea kwa furaha na kumfanya Zato na Feilo kushangaa na kuuliza nini kinaendelea.
Wote watatu kwa haraka walimzingira Roma na kumwangalia kutoka juu mpaka chini kwa kupokezana.
“Umesema mimi ni nani?”Alimuuliza Zomu.
“Acha kujificha basi Braza ..tena nimekosea napaswa kukuita Braza Roma hehe..”
Awamu hio Roma aliona inashangaza na kjiuliza Zomu kamjuaje , ijapokuwa alikuwa katika muonekano wake wa kawaida lakini hawajawahi kuonana.
“Usishangae Braza , ni mara baada tu ya wewe kuondoka kipindi kile tuliweza kujua wewe ni nani halisi , kipindi kile uliweza kuvuruga miliki ya Kekexil na ukaeda pia kufanya katika miliki ya Xia , kila mtu anajua ulichofanya , ijapokuwa ulimwengu wetu wa kijini sio mdogo lakini sio mkubwa sana pia , ilikuwa rahisi kwetu kusikia habari zako , tulikutafuta sana na jina lako halikufahamika katika miliki zote hivyo tulijua ulitumia jina feki , ilikuwa ngumu kwetu kutokujua kulingana na matukio , kipindi kile ulitupatia vidonge vya kutosha na kama ukizingatia jambo lile sio majini wa kawaida ambao wana uwezo huo , sisi ni ni majini wa chini sana katika ulimwengu wetu na ilishangaza mtu kama wewe kutujali , kipindi kile hatukuweza kugundua uwezo wako halisi na hata sasa tumeshindwa kugundua na kama umeweza kuuficha namna hii na kuonekana wa kawaida lazima itakuwa ni wewe , kubwa zaidi ni muonekano wako wa kiafrika hehe”
Roma mara baada ya kusikiliza maelezo ya Zomu aliona kweli haikuwa ngumu kujua , kulikuwa na watu wachache sana wenye sura nyeusi ambao wana mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
“Kaka ni kweli ni yeye , Roma Ramoni?”Aliuliza mrembo Zato akimwangalia Roma kana kwamba amepata Hazina ya thamani ya juu sana.
Feilo ni kama alikuwa amekabwa na kitu kooin na kushindwa kuongea neno , jina la Roma Ramoni lilikuwa maarufu sana kama hadithi za mashujaa wa kale.
Miaka ishirini na saba au nane tu alikuwa ndio binadamu aliekuwa juu zaidi kuliko binadamu wote , binadamu mwenye uwezo wa kuingia ulimwengu wa majini na kufanya anavyotaka na kisha kuogopesha miungu kwa uwezo wake , haikuwa rahisi kuwa wa kawaida mbele ya binadamu mwenzake mwenye uwezo wa kutisha hivyo.
Roma alijua hakuna haja tena ya kujificha na aliishia kutoa cheko akiwaagalia.
“Nadhani ni Mungu alietukutanisha , naomba nichukue nafasi hii kuwapa ushauri , achaneni na maswala ya kujiingiza kwenye maji machafu , bado ni wadhaifu mno na machoweza ni kudili na mizimu ya uwezo wa wastani tu lakini sio hio yenye uwezo wa juu wa akili”
“Hata kama hatuyawezi lazima tupambane , bila ya sisi kujitokeza vipi kuhusu binadamu wa kawaida?”Aliongea Zato kwa hasira.
“Ndio sisi wote watatu tumeamua kuungana kuua majini pepo popote pale , ijapokuwa uwezo wetu sio mkubwa kama wakubwa zetu lakini tunaweza kujitahidi pia”Aliongea Feilo
“Rom,… Bro nadhani hutojali nikikuita kwa jina lako , ulikuwa umeenda wapi siku zote hizo , familia yako kule kisiwani wana wasiwasi kufa , kila mtu sasa hivi anajua mke wako ndio Athena lakini kukimbia sio suluhisho , angalau unapaswa kurudi , lazima kutakuwa na njia kama mkishirikiana pamoja kimawazo”
“Ni kweli kabisa ni bora hata utudanganye sisi , lakini kama umeweza kutuokoa inamaanisha unaweza kumuokoa kila mtu , acha kupoteza muda wako”Aliongea Zato akiwa na wasiwasi.
“Kama ni rahisi hivyo ningeshafanya muda mrefu ,, hamuwezi kuelewa hata hivyo , kuna baadhi ya vitu haviwezi kufanyika hata kama unao uwezo”Aliongea Roma kwa kucheka kivivu na baada ya hapo alimshika Zomu bega akitaka kumpita.
Mrembo jini Zato alionekana kukasirika na palepale alimsogelea Roma na kumshikilia mkono wake kwa ngugvu.
“Huruhusiwi kukimbia tena , hivi wewe ndio Roma kweli ambae unavumishwa kila kona , mtu ambae haogopi mbingu na ardhi , ndio tuseme unamuogopa mke wako katika hali hatarishi kama hii ya kifo na uhai , hivi wewe ni mwanaume kweli?”
“Zatoo..”
Zomu alionekana kuogopa mno Zato kumkasirisha Roma na haraka sana alitaka kumzuia asiongee ujinga.
“Kaka kwani nimekosea nini , binadamu wanateseka dunia nzima lakini hebu muone huyu mtu mwenye uwezo wa kubadili kila kitu kaamua kukimbia na kunywea , mbaya zaidi anaikwepa hata familia yake , anajua kabisa ni kosa kujificha lakini bado anafanya , nyie mnamuonaje si mtu muoga muoga?”
Roma uso wake ulikuwa umebadilika na kutisha , maneno ya Zato yalionekana kuwa kama kisu kikali ambacho kinatonesha jeraha la moyo wake na kisha kulimwagia chumvi .
Zomu na Feilo walijikuta wakikosa usemi , ukweli ni kwamba hata wao waliona aibu juu ya matendo ya Roma lakini hawakuwa na ujasiri wa kumwambia wazi wazi.
Zato palepale alimuachia Roma na kufuta machozi yake na kisha alipotea na alipoibukia alikuwa na mtoto mdogo ambae ana umri wa miaka mitano au sita hivi , mchina aliefungwa fungwa na jaketi zito mno , macho yake yalionekana kuvimba kutokana na kulia sana.
Alikuwa ni msichana na alionekana kuogopa mno na ilishangaza kuwepo ndani ya hilo eneo , muonekano wake ulikuwa ni wa mduao wakati wa kuangalia watu hao.
“Unajua ni kipi amepitia huyu mtoto wakati tunafika hapa , bibi yake ndio mtu pekee aliekuwa nae na wazazi wake inaonekana wamekimbia, ule mzimu umenyonya damu ya bii yake mpaka akawa mkavu , kama sio kilio cha huyu mtoto ingekuwa ngumu kugundua kulikuwa na mzimu maeneo haya na kama tusingejitokeza ndani ya muda nini kingemtokea?, wapo watu kama mia tu ambao wana mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi na kuna majini pepo vichaa zaidi ya elfu moja dunia nzima , wewe si una binti pia , kwahio mtoto wako ndio wa thamani kuliko wa wengine , kama watoto ambao wangeweza kukua watakufa kwasababu yako basi aliewaua sio haya mazimwi bali ni wewe na ubinafsi wako na uoga”
Roma aliishia kumwangalia yule mtoto mdogo anaetia huruma kwa woga huku maneno ya Zato akigonga ngoma za masikio ake kama vile ni mwangwi ndani ya bonde.
Akili yake ilikuwa ni kama inamwambia Lanlan ndio alikuwa mbele yake na alikuwa akimlilia kwa woga.
Roma macho yake yaligeuka na kuwa mekundu huku akiwa na aibu na aliishia kukunja ngumi yake huku akijitahidi kujidhibiti hisia zake kwa kutoa pumzi nzito.
“Kila mtu anafikiri umepatwa na shida ndio maana umeshindwa kurudi mapema lakini inaonekana ni tofauti na mawazo ya kila mmoja .. hata kama unaniona kama mjinga mimi sijali , mimi Zato leo hii nitaongea na wewe kwa kuvaa uhusika wa mwanamke binadamu.. kama ningekuwa mke wako basi nisingeshukuru kwa wewe kunikimbia kwa kuogopa kuniumiza ,, naona ni kama tusi kuolewa na mwaname muoga kama wewe ambae anaogopa kukabiliana na uhalisia na kuishia kujificha, ”
Mara baada ya kuongea Zato palepale alipotea na waliweza kumuona akingia kwenye jengo hilo la makazi.
Zomu na Feilo waliishia kuangaliana na nyuso zisizo za kawaida huku wakionekana kutabasamu kwa wasiwasi.
Ijapokuwa maneno ya Zato hayakuwa mazuri na yalijaa ukiburi lakini kwa kawaida walielewa alikuwa na hasira.
Kwa jini kama huyo wa kike , Roma alikuwa ni kama somo ambalo amelipenda kwa siri lakini anakuja kugundua mtu ambae ni kama shujaa alikuwa havumiliki, ni sawa kwake tu kuwa na hasira.
Isitoshe alikuwa ni jini na maisha yake hayakuwa yakijali sana kuhusu binadamu lakini alikuwa na huruma kumzidi hata Roma ambae ni binadamu.
“Bro , dada yangu ameenda mbali lakini hana nia mbaya na wewe , tunaelewa hili sio jambo rahisi kwako , lazima kuna vitu ambavyo hatuvijui na ni wewe tu unaevijua lakini hata hivyo haijalishi nini kitatokea kwa binadamu na sisi majini lakini tutaishia kukutegemea wewe kama tumaini letu la mwisho , ni sisi kutokuwa na uwezo na kama tukifa basi ndio hatima yetu”Aliongea
“Unajua nini bro , mara nyingi nakuzungumzia , umekuwa sehemu ya maneno yangu kila siku , sisi wote tunakuonea wivu kwa kijana mdogo kama wewe tena binadamu kufikia levo hio , imefikia mpaka hatua kuota vipi kama uwezo wako ungekuwa wangu… ningekuwa mkubwa na wa kuheshimika kiasi gani haha… tunajua ni ujinga lakini tutafanya nini kama ndio kitu tunachoweza kujifariji nacho , lakini siriasi kabisa tunakuonea wivu kwa kuwa na uwezo huo na bahati kitu ambacho hatuwezi kuwa nacho , haijalishi ni maamuzi gani utafanya lakini matumani yetu ni mimi na Feilo kutokukuchukia kama wengine , tunaweza tusiwe kitu mbele yako lakini kwa sisi ni heshima kuwa na koneksheni na mtu kama wewe…”
Zomu na Feilo waliishia kuonyesha tabasamu na kuacha kuongea kisha na wao walizipiga hatua kuingia kwenye jengo la makazi kwa ajili ya kumtafuta Zato .
Roma aliishia kusimama eneo moja kwa muda akionekana kuwaza na kiini cha macho yake kilikuwa kikicheza mno kama vile upungufu wa melanin.
Baada ya muda mfupi Roma aliishia kutoa kicheko kama cha kujionea huruma na kuinua uso wake kuagalia anga.
Roma alitupa Chupa ya Whiskey alioshikilia mkononi na palepale alipotea katika mtaa ule.
Punde tu katika visiwa vya wafu maili laki moja na elfu nane mbali Roma alikuwa ashabadili na kuwa katika unadhifu na palepale alipotea na kuibukia katika ngome yake.
Katika Floor ya kwanza Dorisi , Yezi , Najma , Nasra na wengine walionekana kuwa kwenye mkao kama vile wapo kikaoni.
Lanlan yeye alikuwa amekaa na babu yake akionekana kusikiliza baadhi ya hadithi za zamani .
Kitendo cha ghafla cha Roma kujitokeza kiliwashitua wote lakini Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kupiga makelele.
“Dadiiii…!!!”
Roma aliangalia warembo wake na ndugu zake huku akiwa na macho ambayo ni kama anataka kutoa mahozi na aliishia kumkumbatia binti yake ambae alimrukia kifuani kwa furaha.
Roma keshafanya maamuzi , unadhani atafanikiwa kumrudisha mke wake?
Asante
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Vanity of vanities , all is vanity

SEHEMU YA 793.
“Zeus..!1”
Roma moyo ulimsinyaa , alijiuliza inamaana wimbi la sauti ambalo ni kama lilikuwa likitaka kuharibu anga lilitoka kwa Zeus?, ni palepale alipata kujua lazima sauti aliokuwa akiisikia kwenye akili yake ilipitia kwenye uungu wa Hades
Wakati huo mara baada ya kusikika kwa sauti, radi ya rangi ya dhahabu na bluu yenye urefu wa zaidi ya futi kumi ilipasua anga kama ilivyokokotwa kutoka kwenye kitu kisichoweza kuonekana na kwenda moja kwa moja kupasua radi na mawingu ambayo yalikuwa chini ya udhibiti wa Roma.
Mkono imara ulijitokea kutoka mawinguni na kunyakua shoti ya radi bila kujeruhi ule mkono kwa namna yoyote licha ya kwamba radi ile ilionekana kuushambulia ule mkono.
Ndani ya sekunde tu lile wingu lote lilitawanyika na hatimae mwili wa miraba minne ulionekana juu angani.
Alikuwa na ndevu ndefu nyeupe ambazo zilikuwa zikipeperushwa na upepo huku mashavu yake yakiwa na kingo kama za mawe pamoja na kona zake.
Macho yake yote mawili ni kama yametawaliwa na umeme na kufanya yatoe mng’ao wa ajabu ambao mweupe sio mweupe ni kama rangi ya majivu.
Mwili wake ulikuwa umesitiriwa na joho la rangi nyeupe lenye mikono mifupi ilioacha wazi mikono yake , huku misuli yake iliotuna ikionekana waziwazi na ilikuwa ni kama vile mwili wake wote umejaa kutu.
Roma aliishia kutoa macho yake tu asiweze kuamini , aliekuwa juu yake ni kama hakuwa amebadilika kabisa , kama alivyokuwa miaka elfu mbili iliopita.
Imewezekana vipi?
Miungu wote ambao walikuwa wamepoteza miili yao mara baada ya kuja duniani na kuvaa miiili ya binadamu, alishangaa mara baada ya kumuona Zeus akiwa na mwili wake wa awali.
Mara baada ya miungu kushuka hawakukaa hata siku moja wote waliamua kuivamia miili ya binadamu na kutelekeza ya kwao lakini kwa wale ambao walikuwa na uwezo wa juu ikiwemo miungu kumi na mbili waliweza kuishi nayo kwa muda mfupi kidogo kabla ya kuhamia katika miili ya binadamu.
Inasemekana Zeus ndio ambae alidumu katika mwili wake kwa muda mrefu na aliingia na mwili wake katika gereza la Roho.
Ndio maana muda huo Roma anashangaa ameweza vipi kutohamia katika mwili mwingine na kuishi na mwili wake licha ya kwamba katika mazingira ya dunia haiwezekani.
Alijiuliza je kulikuwa na sababu ya kipekee ndani ya gereza la Roho ambayo ilimfanya kuishi na mwili wake tofauti na mazingira ya dunia, maana kwa anavyoonekana ni kama haikuwa swali bali jibu.
“Kuwa na uungu wa Hades halafu kuwa adui wa miungu hustahili kabisa uungu wake na haustahili kabisa kuwa sehemu ya miungu , leo nitakuuwa na radi hii iliopo kwenye mikono yangu”Aliongea Zeus akimwangalia Roma kwa macho makali..
Na mara baada ya kauli hio aliinua mkono wake mkubwa juu na bila ya kuchezesha chezesha aliachia radi yote kutoka kwenye mikono yake kumshambulia Roma.
Mara baada ya miungu kuona tukio hilo wengine walikuwa katika hali ya heshima kwa Zeus na wengine walikuwa na furaha.
Ilionekana walikuwa wakijua fika kama Zeus ataamua kuingilia kati, Roma hana nafasi ya kushinda tena.
Roma spidi yake ilikuwa kubwa mno , hata kama ni radi ya Zeus haikuwa rahisi kutokuiona kwa macho yake na kabla radi ile haijamtoka Zeus alikuwa tayari ashajiandaa kukwepa.
Lakini sasa mara baada ya Roma kusogea upande mwingine kwenye hewa akijua kabisa amefanikiwa kukwepa shambulizi lile alipigwa na boriti tatu nyingine za radi na kusababisha mlipuko mkubwa wa shoti.
BOOM!
Roma alishindwa kuamini na hakujua ni nini kinaendelea , ilikuwa ni ile radi imetoka alipokuwa amesimama na kumfuata alipokuwa amehamia na kuvunja ukuta wake na kisha kumshambulia.
Ilikuwa ni kama vile radi ile ilikuwa na ufahamu kwamba atasogea hivyo ilibadilisha uelekeo bila ya taarifa.
Mwili wake wote ulionekana kuungua kwa kiwango cha juu cha joto, huku viungo vya ndani vikionyesha kuumia pia na kujinyonga nyonga, alishindwa kuzuia sauti zaidi ya kupiga yowe.
Maumivu hayo yalikuwa makubwa mno kuliko yale yaliosababishwa na siraha ya Athena wakati wa kumshambulia.
“Arghh..!!”
Roma macho yake ni kama yanapasuka na ni kama anajua sasa nama maumivu halisi ya radi yanavyokuwa
Mwili wake ni kama unaelekea kupalalaizi huku maumivu ni kama yameungana na mwili wake na kumfanya akitamani kifo kuliko kuendelea kuishi.
Uwezo wa Zeus ni sawa na kusema ulikuwa wajuu kiasi kuliko ule wa Athena , jambo ambalo lilimaanisha shoti ya radi yake ilikuwa na nguvu mara mbili na ya jini au mtu aliepitia mapigo elfu kumi ya radi.
Sasa Roma uwezo wake ulikuwa katika mapigo mengi ya radi na pengine ni sawa na kusema ni bahati kwake hajafa mara baada ya kupigwa na radi hio , ilimuwia vigumu kupona haraka kuliko mwanzo.
“Athena kwanini unasita sita, radi yangu itamfanya kuwa dhaifu , tumia mkuki wako kumchoma eneo la moyo na kisha tukiondoe kichwa chake”Aliongea Zeus.
Alikuwa akimwangalia Roma kwa madharau kutokana na kushindwa kwake kusogea huku akiongea na Athena.
“Huna haja ya kunifundisha cha kufanya”Aliongea Athena na palepale aliishikilia vyema siraha yake.
Roma alijikuta akipatwa na kiwewe mara baada ya kuona Zeus na Athena wanataka kumchangia kumshambulia .
“Sikutugemea kuishi lakini siwezi kufa bila ya kupambana”Aliwaza Roma.
“Ni mapema sasa kuniua”
Roma aliongea kwa nguvu akionyesha tabasam lake la ukichaa wakati akiwa anavumilia maumivu ya pigo la mwanzo.
Alikusanya mawingu kwa kasi ya ajabu ili kuanza kutengeneza radi na wakati huo huo alitoa Shoka lake na kumshambulia nalo Zeus.
Lakini sasa kumsogelea Zeus kwa ajili ya kumshambulia halikuwa swala jepesi hata kidogo kwani Athena ni kama alikuwa ashamtabiria ni njia gani Roma atapita na alitumia ngao yake ya Aegis kumzuia.
Bang!!!
Sauti kubwa ya kishindo ilisikika, radi pamoja na shoka lile viligongana na Ngao ya Aegis na ni ndani ya sekunde hio hio Athena alitoa ile ngao na kilichomkuta Roma ni pigo lingine la radi kutoka kwa Zeus.
BOOM!!
Shambulizi lingine la radi ya dhahabu lilimpata Roma na kufanya harufu ya kuungua kwa mwili kusambaa na Roma alijikuta akipiga yowe la maumivu huku akidondoka kutoka angani kama kimondo.
Radi ya Zeus kama ilivyosimuliwa na wagiriki inaweza kumshambulia adui na pasionekane mahali pa kujificha.
Radi hio ilikuwa na uwezo wa kumfuata adui eneo lolote hata kama ajaribu kukwepa vipi, hivyo ni sawa na kusema siku zote lazima ifikie shabaha, sasa ukijumlisha na uwezo wa Athena katika kutabili ilikuwa hatari kabisa kwa Roma.
Pengine dakika chache zilizopita alikuwa na uwezo wa kushambulia Mti Mama lakini muda huo ni kwamba hata uwezo wa kujilinda alikuwa hana na hata kama aamue kupokea mapigo ya Zeus kama alivyoamua kupokea ya Athena basi anaweza kuuliwa mara moja.
Haikushangaza kabisa kwani ki uwezo anaanza Zeus na kisha anaingia Athena lakini mara nyingi watu wanasema Zeus na Athena wapo levo sawa ila kinachomfanya Zeus kuwa juu zaidi ni kwamba Athena anao uwezo mkubwa wa kujilinda huku Zeus akiwa na uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi.
Kwa mfano kama ikatokea Zeus na Athena wakapambana inaweza asitokee mshindi kutokana na utofauti wao, Athena hatoweza kumshambbulia Zeus kutokana na kwamba hana mashambulizi imara na wakati huo huo Zeus kama atamshambulia Athena mashambulizi yake hayatopita kutokana na Athena kumiliki Aegis , ngao yenye uwezo mkubwa sana wa kukinga mashambulizi mengi.
Mpaka kufikia hatua hio ni kwmaba Roma hakuwa na uwezo wa kushambulia tena , kwani akishambulia Athena tayari ashatabilia mashambulizi yake na kuyakinga na ngao yake wakati huo huo Zeus radi yake ni kama ina ufahamu wakati wa kumshambuilia.
“Nadhani huu ni mwisho ambao hujautarajia?”Aliuliza Athena na sauti ya kikauzu huku akiwa na hali ya kihisia isiokuwa ikielezeka.
Roma ambae alikuwa akidondoka kutoka juu angani alijitahidi kutingisha kichwa chake kwa taabu.
Athena alikuwa na uwezo wa kumuongelesha Roma kutokana na kwamba alikuwa akishuka na Roma sambamba, tofauti ni kwamba Roma alishindwa kujizuia kudondoka wakati Athena ni kama anamfatilia Roma kwa karibu.
Sasa wakati alipomaliza kuuliza kwa kauli hio aliinua mkuki wake akinuia kumchoma nao Roma eneo la moyo.
“Sio kirahisi hivi , siwezi kufa kirahisi”Roma aliongea kwa sauti iliojaa maumivu.
“Kweli..?”
Muonekano wa Athena ulikuwa katika utulivu sana , yaani ni kama vile hana uadui na Roma lakini mikono yake ilikuwa tofauti.
“Pfff..!”
Mkuki wa Pallas uliokuwa ukitoa mng’ao wa rangi ya bluu ulikuwa tayari ushamchoma Roma eneo la kifuani kuingia kwenye moyo wake lakini hata hivyo haukuweza kupita kama ambavyo kila mmoja alitarajia .
Kabla Athena hajafanikiwa kumchoma kifuani , Roma alikuwa ashafanikiwa kuushikilia ule mkuki kwa nguvu usipite japo ya kwamba ulimchoma nchi kadhaa kuingia ndani lakini hakujali.
Damu ya moto ilimtoka Roma mkononi na kwenye kifua chake na kusambaa.
“Hatimae nimekukamata … Mkuki wako hatimae nimeushikilia na usione unaweza kuuchukua kutoka kwangu kirahisi”Aliongea Roma huku macho yake ni kama vile yanataka kumtoka pengine ni kutokana na maumivu.
“Kwel?”Athena aliuliza kana kwamba Roma alikuwa akiongea vitu visivyo na maana.
Sekunde iliofuata Athena alimbutua Roma na mguu wake kwa nguvu zote.
“Bang!!
Muda ambao Roma aliweza kusikia sauti ya kishindo alikuwa ni kama vile amegeuka kuwa satilaiti akiizunguka dunia huku yeye mwenyewe akijizungusha katika mhimili wake , kichwa chake kilipindishwa kwa angle mia na sitini na kwenda kuvaa mlima wa barafu.
Miungu wote waliweza kuona namna Roma alivyoenda kuvamia mlima wa barafu na kudidimia ndani asionekane kwa nje.
Athena alirudisha siraha yake iliokuwa imechafuliwa na damu na kuishia kuangalia sehemu ambayo Roma ametumbukia
“You… you can’t win against us”Athena alionekana kumung’unya maneno kwa lugha ya kingereza akimaanisha Roma hawezi kushinda zidi yao.
Zeus alieshikilia kitenesi cha shoti ya radi hatimae aliweza kufika juu ya barafu na alijikuta akikunja sura yake.
“Uungu wake unapotea kwa haraka sana!”Aliongea.
Miungu wengine na wao pia walifika kwenye barafu na waliweza kugundua pia uungu wa Hades unaisha kwa spidi kubwa mno
Ilikuwa ni kama kibatari ambacho kishaishiwa na mafuta na muda wowote kinakwenda kuzima na hio ndio namna uungu wa Hades ulivyokuwa ukipotea na palepale Christen machozi yalimjaa.
“Hades..!.ni kweli umeamua kumuua?”Aliongea Christen akimlaumu Athena akidhania amemuua Roma.
“Hapana, Aphrodite hebu tumia hisia zako kwa umakini, ijapokuwa uungu wake unapotea lakini mkandamizo wa nishati za mbingu na ardhi…”
“Uwezo wake unaongezeka … huyu mwanaharamu anatumia nafsi ya mnyama kuunyonya uungu wa Hades na kuubadilisha kuwa nishati za mbingu na ardhi”Aliongea Hera kwa kupaniki.
“Nini?!”Wengine wote sasa ni kama wanajua kinachotokea na kupiga kelele huku Zeus akiishia kumwangalia Athena.
“Hio ni mbinu yake nyingine?”Aliuliza Zeus lakini Athena hakukubali wala kukataa na wahenga wanasema kimya ni jibu hivyo moja kwa moja ilieleweka bila ya neno.
Dakika hio mlima wa barafu ambao ulikuwa katika hali ya utulivu ulianza kutingishika kwa nguvu kama vile unataka kuporomoka na ikafuatia wimbi ambalo lilikuwa likitoka chini yake.
Ni kitendo cha sekunde tu mlima wote wa barafu ulipasuka na kurusha mapande ya barafu juu angani kwa mita kadhaa na palepale Roma aliweza kuonekana tena ikiwa ni kama vile hakuwa ameumizwa eneo lolote.
Lakini muda huo miungu hao hawakuweza kabisa kumjua Roma kama mwenzao tena kwani uungu wa Hades ulikuwa ushamtoka kabisa.
Mtu ambae alikuwa mbele yao hakuwa tena Hades bali alikuwa ni binadamu mkamilifu mwenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Roma sio Hades tena kwani jina hilo lilitokana na nusu ya uungu wa Hades, hivyo ni sawa na kusema Roma amerudi kuwa Denisi binadamu kamili aliezaliwa duniani.
Uungu ndio mzizi wa miungu au unaweza kusema ndio asili yao ambao hubeba uwezo wao wa hali ya juu sana na kuwafanya kuwa na nguvu kubwa ya kiroho mpaka kuwawezesha kuhama kutoka katika mwili mmoja kwenda katika mwili mwingine.
Chaos ni mnyama wa machafuko ambae anao uwezo wa kumeza kila kila kitu ndani ya ulimwengu, hivyo hata kwa uungu ni kitu ambacho kinaweza kumezwa na Chaos kutokana na kwamba uungu hubeba nguvu ya kiroho ambayo chanzo chake sio ardhi bali ni ulimwengu(Universe).
Roma aliamua kufikiria nje ya boksi na akaamua kuitumia nafsi ya Chaos kuumeza uungu wa Hades ambao alikuwa akimiliki kwa ajili ya kupandisha uwezo wake kwa levo ya juu zaidi ndani ya muda mfupi.
Mara baada ya kufufuka kwa moyo wa Gaia uungu wa Hades na wenyewe ni kama ulikuwa unapona na kufikia uwezo ambao ni sawa na mapigo elfu moja ya radi.
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba Roma alikuwa na uwezo wa kutumia kanuni za anga na kama utamfananisha na mtu anaevuna nnishati za mbingu na ardhi basi ni katika levo ya mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi uwezo ambao ni wajuu sana.
Sasa unapaswa kuelewa mara baada ya Chaos kumeza uungu wa Hades aliugeuza kuwa nishati ya mbingu na ardhi ambayo moja kwa moja ilienda kwa Roma.
Sasa katika mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi Roma alikuwa levo ya mapigo mengi ya radi huku upande wa kanuni za anga ni hivyo hivyo , kwa lugha nyepesi ni kama Roma ameunganisha uwezo wake wote kuwa kitu kimoja yaani alichanganya uungu wa Hades na nishati ya mbingu na ardhi.
Zamani ilimpasa Roma kutumia kanuni za anga peke yake na vilevile nishati za mbingu na ardhi peke yake , lakini muda huo vyote vilikuwa pamoja mara baada ya kufanikiwa kuubadilisha uungu kuwa nishati ya mbingu na ardhi.
Ukweli ni kwamba hio ndio mbingu ya kipekee ambayo Roma alifanya na miungu hawakutarajia kabisa.
Maana kitendo cha kufanya hivyo ni kama Roma kaamua kuachana na amswala ya kanuni za anga kwa ajili tu ya kuongeza uwezo wake.
Bila hata ya maelezo kutoka kwa Athena miungu hao walijua ni namna gani uwezo wa Roma umeongezeka na kuwa wa kutisha.
“Mkandamizo wa nguvu zake ni mkubwa mno , nashindwa hata kuangalia ni levo gani kafikia, ukijumlisha na uwezo wake wa mwanzo naogopa kusema kwasasa kafikia levo ya mapigo elfu kumi ya radi”Aliongea Hera akiwa na wasiwasi .
Roma sasa ni kama amekidhi vigezo vya kupambana na Zeus na Athena kikamilifu..
******
Sharif , Aoiline na wengine wote walikuwa wakiangalia kilichokuwa kikitokea katika ncha ya kaskazini kwa kutumia kioo cha maajabu.
Clark mwanzoni alijua Roma ameshindwa vita na kumfanya aanze kulia lakini mara baada ya kumuona mpenzi wake akisimama tena akiwa na uwezo uliongezeka haraka hakuweza kujizuia na kushangilia kwa furaha.
“Hehe .. huyu mtoto hatimae amegundua kwanini Hades alimwachia nusu ya uungu wake bila fahamu , alipaswa kujua siri hii mapema kama angeacha kujali sana maswala ya wanawake…”Aliongea Sharif.
Moja ya sababu kubwa ya Athena kumuomba Hades kutii takwa lake na kumwachia Roma uungu ni kwasababu tu alitaka kuweza kumtabiria kirahisi hata kama apande levo za juu sana , ilikuwa rahisi kumtabiria Roma kupitia uungu kuliko akiwa binadamu kamili.
Yaani kwa lugha nyepesi uungu wa Hades katika mwili wa Roma ilikuwa ni njia ya mawasiliano ya kinabii kati ya Roma na Athena.
Kulingana na maelezo ya Sharif kitendo cha Roma kufikia levo ya mapigo elfu moja ya radi ilimaanisha Athena hana uwezo tena wa kumtabiria lakini ajabu ni kwamba Athena bado alikuwa na uwezo wa kumtambiria Roma hio yote ni kutokana na uungu wa Hades ambayo ni njia ya mawasiliano.
Sababu ya pili Athena kutaka Roma aachiwe uungu ni kwa ajili ya kumfanya kuwa sehemu yao.
Ikumbukwe mara baada ya Athena kufika duniani aliweza kuangalia nini kitakuja kutokea mbeleni na kupitia unabii wake aliweza kugundua ni binadamu Roma Ramoni atakaeweza kuzuia mipango yake ya kufufua ndugu zake.
Sasa kwanzia miaka elfu ishirini iliopita Athena alikuwa akipambana na unabii kwa kubadilisha historia.
Kitendo cha kutaka Hades kumpatia Roma uungu ukiachana na dhamira ya kutaka kumtabiria kwa urahisi lakini vilevile alitaka kumfanya mmoja kati yao.
Lakini kitu ambacho Athena hakukifahamu ni kwamba Hades alikubaliana nae kirahisi akiwa na ajenda nyingine kabisa, kwa Athena Roma alipewa uungu kwa ajili ya kurahisisha mipango yake kwa Hades wa Zamani alimwachia Roma uungu wake kwa ajili ya kukwamisha mipango ya Athena.
Hivyo Roma kutumia uungu kupandisha uwezo wake ndio kete ya mwisho ambayo Hades wa Zamani alitarajia Roma kuicheza ili kuja kumshinda Athena na wenzake lakini hata hivyo hakumwambia Roma juu ya siri hio, ni kama alimpa mtihani wa kugundua yeye mwenyewe.
Hayo yote Sharif aliyajua tokea mwanzo wa mpango LADO unaanzishwa na yeye pia hakutaka kumpatia Roma siri hio kama anao uwezo wa kupandisha mara mbili uwezo wake kupitia uungu wa Hades.
Sasa Roma alishindwa kugundua siri hio mapema kutokana na Christen mpenzi wake Hades wa zamani kuwa rafiki yake, pengine kama asingekuwa na mfungamano wa kirahifi na Christen angeweza kugundua siri hio mapema sana.
Sasa Sharif alikuwa kwenye mshangao mara baada ya kuona Roma anazidi kushambuliwa na Athena na Zeus bila ya kutumia uwezo wake wote, yaani uungu wa Hades, alijiuliza au bado hajajua siri hio.
Sharif hakuwa mjinga kumtaka Roma apambane licha ya kwamba kimahesabu levo aliokuwa amefikia kulinganisha na wapinzani wake ni ndogo lakini ukweli ni kwamba hakuwa akibahatisha , alikuwa akijua tokea mwanzo njia pekee ya Roma kushinda ni kutumia Chungu chake kuubadilisha uungu kuwa nishati za mbingu na ardhi na kupandisha uwezo wake kwa haraka.
Aoiline macho yake yalicheza na haikujulikana anafikiria nini na aliishia kuangalia kioo bila ya kuongea neno.
Xumei na Mzee Yasu walikuwa na furaha , ijapokuwa walikuwa wakiyaheshimu maamuzi ya mwalimu wao kwa kuwapa binadamu na miungu nafasi sawa , wao walikuwa bado ni binadamu na walitamani kuona Roma anawaua miungu wote na dunia kubakia salama.
Sharif alikuwa ni kama Hades wa zamani tu wote walikuwa Neutral , Sharif hakutaka kuwazuia miungu kutokuitawala dunia kama uwezo huo wanao lakini pia hakutaka kujisumbua kama binadamuw atashindwa kulinda dunia yao.
Kama miungu wangeshinda na Mkuu wa Enzi kutokuingilia basi moja kwa moja Dunia ingekuwa chini ya miungu , kama binadamu wangeshinda kwa kuilinda sayari yao basi pengine ndio mapenzi ya Mkuu wa enzi, na moja kwa moja uangalizi angemkabidhi Roma
Hakukuwa na haja ya kati y a miungu kuwa na muangalizi kwani alijua fika wanao uwezo wa kuilinda sayari lakini kwa binadamu wote waliwakilishwa na Roma hivyo kama Roma angeshinda ilimaanisha ndio yeye kati ya binadamu wote mwenye uwezo wa kuilinda dunia.
*****
Muda huo namna ambavyo miungu walimwangalia Roma haikuwa ikielezeka kama walikuwa wakihisi kitu cha namna gani kwenye mioyo yao.
Mara baada ya kupoteza uungu, Roma alikuwa sasa amekuwa adui yao kikamilifu , hata kwa Apollo na Poseidon ambao walikuwa na urafiki na Roma hawakuwa na huruma nae tena.
Walikuwa wakimchukulia kama mwenzao kwasababu ya uungu wake na sio kwasababu alikuwa binadamu.
Lakini kubwa zaidi kwa wakati huo ni kwamba Roma alikuwa tishio kubwa kwa ajili ya ufufuo wao.
“Inavutia sana kwa ulichofanya , ni kheri kuua binadamu aliekamilika kuliko kumuua kaka yangu Hades”Aliongea Zeus huku akitoa kicheko kizito.
Upande wa Roma ni kama vile hakuwa akimsikia Zeus anachoongea na alikuwa amefumba macho yake huku akichanua mikono yake kama vile anaomba baraka kutoka juu mawinguni.
Ni dakika hio hio waliweza kuhisi kitu cha ajabu , kutoka kila pande nguvu kubwa ya kiroho ilikuwa ikijikusanya kumsogelea Roma.
Roma alikuwa ni kama sumaku na kuanza kuvuta kila aina ya nguvu ya kiroho iliokuwa karibu yake
Nguvu hio ya kiroho ilimwingia Roma na kubadilika kuwa nishati ya mbingu na ardhi na kuzidi kufanya sehemu ambayyo Roma amesimama kuwa na upepo mkali unaomzunguka kama kimbunga.
Kitendo cha upepo mkali kumzunguka Roma ilifanya kuwa ni kama Dhoruba ya kimbunga kikali na kufanya hewa kusukumwa kwenda juu angani kwa spidi kubwa , hatimae sehemu ambayo Roma alikuwa amesimama hakukuwa na hewa ya aina yoyote ni sawa na kusema Roma alikuwa ndani ya Ombwe(vacuum)
“Hii ni hatua ya mwisho ya mapigo ya radi , levo elfu tisa mia tisa tisini na tisa ya radi, levo ya mwisho wa Dhiki na mwanzo mwa ufunuo mkuu”Aliongea Hera ambae ni kama sauti imempotea.
Hakuwahi kushuhudia radi ya levo hio na inakwenda kuwa mara yake ya kwanza , ukweli ni kwamba ni majini wachache sana ambao wameshuhudia radi ya mapigo elfu kumi na wengi wao waliamini ni ngano tu katika vitabu.
“Ukali wa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi kumzunguka ni kama chuma kigumu , hii ndio levo ya mwisho kabisa ya ufahamu wa mbingu..”Aliongea Hephaestus akiwa katika mshangao.
“Inaonekana hii levo ya dhiki ya mwisho haitokei kwa kukusanya mawingu , hicho kizingia cha nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi kinataka kufanya nini?”Aliuliza Apollo kwa mshangao.
“Mnashangaa nini sasa , tumieni nafasi hii kabla Dhiki haijaisha , muueni”Aliongea Hermes.
Zeus ni kama amekumbuka cha kufanya na palepale aliongezea nguvu ya radi iake na kuirusha katika eneo ambalo Roma amesimama.
“Chwiiiii….!!!”
Dakika ambayo radi ile inataka kumkaribia Roma ilizuiwa na kizuizi ambacho hakionekani na kusababisha msuguano kama vile ni wa breki a gari uliopelekea mlipuko.
“Ule ni ulinzi wa kiroho?!”Hera aliuliza akiwa katika hali ya mshangao mkubwa
“Hicho kizingia kimemzunguka tayari na inaonekana ni kama ulinzi”Aliendelea kuongea.
Miungu walikumbwa na mshangao mkubwa mara baada ya kuona radi ya mapigo elfu kumi ilikuwa na tabaka lake la kumlinda mpitia Dhiki.
Kizingia cha mkusanyiko mkubwa wa nguvu ya kiroho ilikuwa ni tabaka la ulinzi kwa mtu yoyote au jini anaepitia mapigo ya levo ya mwisho wa Dhiki ili asiwe na mawasiliano na ulimwengu wa nje na isitokee yoyote wa kufaidika.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba radi hio inampata yule tu ambae anapitia mapigo hayo na si vinginevyo na ombwe ambalo limetengezwa na kizingia hicho ni kama njia maalumu ambayo radi itapita.
Ukweli ni kwamba sio kama radi hio inataka kumlinda Roma au nini bali ili radi hio kuweza kutokea lazima kuwe na mkondo maalumu , ni kama mfereji au useme njia maalumu ya radi hio kupita.
Roma alikuwa amesimama kwenye ombwe hilo la kisingia akiwa ametulia kabisa huku macho yake akiwa ameyafumba , ni kama vile alikuwa amesahau kila kitu kinachoendelea ulimwengu wa nje.
“Uzio umeweza kuzuia radi kupita , inamaana huo ulinzi una nguvu kiasi hicho”Walishangaa.
Hata radi ya Zeus ambayo ilisifika kwa ukali haikuweza kupita au kusababisha mtingisho wa aina yoyote ile
Miungu hao hatimae washajua hawana uwezo wa kumshinda Roma akiwa ndani ya kizingia na waliishia kuangalia namna anavyopitia mapigo ya radi.
Zues uso wake ulikunjamana , macho yake yaliwaka mwanga na aliongea kwa sauti.
“Kwasababu mambo yamefikia hatua hii , basi na tuogeni utukufu wa Mama Gaia na turudi katika miili yetu ya Titani”Aliongea Zeus.
Miungu walimwangalia kwa mshangao mkubwa kutokana na maamuzi yake.
“Zeus ni lazima kufanya hivyo ..tutakula nguvu nyingi kutoka kwenye Mti Mama na uungu unaochipua utanyauka na kuzuia roho nyingine kuchelewa kufufuka”Aliongea Poseidon kwa uangalifu.
“Naunga mkono , hata kama atafanikiwa kupita levo ya mapigo elfu kui ya radi uwepo wako na Athena ukijumlisha na sisi haina haja ya kurudi katika miili yetu ya Titan”Aliongea Hera.
“Na tuanzeni , tunahitaji kurudi katika miili yetu ili kumaliza hii vita”Aliongea Athena ambae alikuwa kimya muda wote.
Miungu walijikuta wakishangaa na kwasababu alioengea ni Athena basi waliamini kuna sababu hivyo maamuzi ya Zeus kutokupingwa na wengine.
Ijapokuwa baadhi yao waliona haina haja ya kwenda mbali hivyo lakini kilichokuwa mbele yao ni vita ambayo hawapaswi kushindwa.
Mwishowe miungu wote walifanya maamuzi na kupaa mpaka kwenye kilele cha mti mama na kutengeneza duara.
Sekunde ileile miungu wote walianza kutoa miale ya mwanga na anga kuwazunguka lilianza kupinda pinda na kucheza huku eneo la katikati nguvu ya kiroho ikichemka kwa kasi kubwa.
Kadri walivyokuwa wakiendelea kiasi kingi cha nguvu ya kiroho kiliungana na Mti Mama na palepale mwanga wa dhahabu uliokuwa kama uji uliwafunika wote hata wasiweze kuonekana kwa nje.
Muda huo huo upande wa Roma ambaye alikuwa kwenye kisingia cha nguvu ya kiroho hakushituka hata kidogo licha ya kujua kila kitu kinachoendelea nje yake, alikuwa amezama kwenye utambuzi wa Adhabu ya mapigo ya radi.
Roma alikuwa akiitikia wito wa mapigo elfu kumi ya radi na kupanua ubongo wake kukwea katika mbingu za ufahamu , kujua asili ya vitu vyote na kutafuta uthibitisho.
Upande wa miungu walikuwa tayari washafanikuwa kuunganisha ufahamu wao na mti mama na miili yao ilizidi kufuka miale ya mwanga.
Katika anga hilo ndani ya ncha ya kaskazini hatimae sauti zilipaa angani na kugonga huku na huko mawinguni, zilikuwa ni sauti za wimbo ambazo lugha yake haikufahamika.
Hio ndio lugha ya miungu waliokuwa wakitumia.ilikuwa ni ushairi(Ode) ambao miungu pekee ndio wanaoweza kuelewa.
“Wakati wa kuyeyuka kwa barafu juu ya Olympos , ukuu wa mungu utatanda ulimwenguni kote, tutauvaa utukufu wa ardhi na kuzisikiliza sauti za ngurumo ya radi , mambo yote chini ya utawala wa kifalme wa miungu milele ivukayo kesho, Hiki ni kizazi cha Titani”
Waliimba kwa kurudia rudia maneno na kufanya dunia yote sauti zao kusambaa kwa kasi sana.
Na muda uleule mti ule ulianza kufuka mwanga wa rangi ya Dhahabu na kuvamia juu ya duara walilotengeneza miungu , huku mwanga ule ni kama vile unazama mwilini na kuungana.
Miili ya miungu ilikuwa ni mwanga kulingana na aina ya nishati na kufanya kila mtu kung’aa kwa namna ya kipekee , huku ming’ao yao ikiendelea kuongezeka na kupanuka na nguvu yao ya kiroho ilizidi kuongezeka maradufu na kufanya mkandamizo wa hewa kuwa mkubwa kuliko isivyokawaida.
Mwili wa rangi ya Dhahabu na bluu ulionekana kutoka kwa Zeus , mwili wa jitu kabila la Titani , Zeus ndio aliekuwa wa kwanza kubadilika na ndani ya sekunde tu alikuwa ni jitu likubwa mno.
Mara baada ya kunyanyua mguu wake na kukanyaga juu ya bahari barafu yote ilipasuka pasuka vipande vipande na wimbi alilosababisha lilitengeneza Tsunami.

SEHEMU YA 794.
Ili kurudiwa na uwezo wao asilimia mia ilikuwa ni lazima warudi katika miundo yao ya Kititani , ilikuwa ndio njia moja tu ya kujipandisha ki uwezo zaidi na zaidi.
Ndani ya dakika chache tu mti wote ulipoteza nishati ya kutosha kwa kuwavalisha miungu miili yao kupitia uungu.
Ijapokuwa walikuwa wamekosa damu ya Titani kama ilivyokuwa kwa miili yao ya awali Mti mama ulikuwa na uwezo wa kuwapatia nguvu ileile.
Kitendo hicho kingeweza kusababisha mti kuathirika na kusababisha uungu uliokuwa ukihipua kunyauka kwa kiasi kikubwa lakini hilo ni swala ambalo miungu hawakutaka kulifikiria kwa wakati huo.,
Walihitajji nguvu ya kutosha kwa ajili ya kumdhibiti Roma ambae anapitia levo ya mwisho ya mapigo ya radi.
Kilichokuwa kikiogofya ni kwamba ukijumlisha na mwili wa kititani wa Zeus , miungu wote wlaikuwa wamebadilika kutoka katika miili ya kibinadamu na kuwa katika maumbvo yenye nguvu kubwa.,
Kama ambavyo binanamu huitwa binadamu , jini kuitwa jini na malakka kuitwa malakika ndio ilivyokuwa kwa iungu hawakuwa binadamu tena walikuwa ni Watitani.
Walikuwa na maumbo marefu mno ni kama vile viuno vyao ndio vinatenganisha mbingu na ardhi
Kila dakika walivyopiga hatua walisababisha wimbi kubwa la upepo na kila dakika walivyochezesha mkono ilikuwa ni Dhoruba.
Mara baada ya miungu yote kuzunguka mti ,mti huo haukuwa mkubwa tena.
Kitu kingine cha ajabu zaidi ni kwamba Dhana zao walizokuwa wakimiliki na zenyewe zilikuwa zimeongezeka ukubwa , haikujalisha ni Athena ngao yake au upinde wa Apollo na Artemis kila kitu kiiongezeka ukubwa kulingana na miili yao.
Bila shaka kama hazikuongezeka basi zisingeweza kuitwa Dhana za kititani.
Kuwa katika miili ya kititani iliwapa uwezo wa juu sana wa kutengeneza mashambulizi , kitu kikubwa zaidi miungu hao walikuwa wakipata bado nishti kutoka kwenye mti mama.
Jua , bahari , madini na kila kitu kingine ni rasilimali za kulisha siraha zao na ngao zao pamoja na miili yao.
Miili yao ilikuwa ni nishati , haikuwa miili ya nyama kama ya kibinadamu , ilikuwa ni kama wamegeuka na kuwa mwanga lakini katika maumbo ya watu.
Lekcha na wao kulikuwa na tofauti kidogo tu , pengine Lekcha alikuwa na mwili wa nishati wa Ant matter lakini wao walikuwa na miili ya kinishati inayotokana na Mti mama , nishati ambayo ilionekana kabisa wanapaswa kuipata ili kuendelea kuishi.
Pengine siku mmoja nishati ya dunia itaisha lakini wasingejali , pengine wangeweza kutafuta sayari nyingine na kurudisha uhai wao kama waivyovamia dunia.
Sasa kitendo cha miungu hao kupata miili yao ya kinishati , miili ya Titani inawafanya kuwa katika muonekanno wao wa awali isipokuwa tu kwa Zeus ambae mwili wake alionekana kuudumisha hivyo kumfanya kuwa na mwili wa damu na sio wa nishati kama wenzake.
Hera alikuwa amevalia taji la shaba huku mwili wake wote ukitoa mwanga wa rangi ya Cyani, mkonno wake wa kulia mkubw aulikuwa umeshikilia Golden Apple huku vazi lake likifanana na mng’ao wa mwanga aliokuwa akitoa.
Viumbe hao kwa jinsi walivyokuwa wakitoa mwanga wa ajabu pengine unaweza kuwafananisha na malaika kwa jinsi walivyosimuliwa tofauti tu ni kwamba walikuwa na maumbo makubwa kuliko malaika lakini kwa jinsi wlaivyokuwa wakitoa mngao wa kuumiza macho inaweza kuwa moja ya sifa ya kufanana.
“Kwasababu aaendelea kupitia Dhiki , tutamshabulia kwa uwezo wetu wote na pengine tunaweza kuvunja kizuizi kinachomlinda”Aliongea Hera,
Mara baada ya kubadilika katika maumbo yao ya kititani sauti zao ni kama zinatoka juu angani na kufanya sauti kusambaa umbali mrefu sana kama sio dunia nzima.
“Hatuwezi kuvunja , ilishapangwa kufanikiwa kufikia katika levo hio ya mwisho wa dhiki ya radi”Sauti ya Athena iligonga ngoma zao a masikio
Athena yeye alikuwa akitoa mng’ao mtakatifu wa rangi ya fedha , nywele zake ndefu zilionekana kuwa laini kupita kiasi zilizojisokota kwa kutengeneza mawimbi , alidhihirisha ushujaa na kufanya sura yake isichoshe kuangalia.
Kama malaika alikuwa amevalia na yeye gauni la kitambaa cha hariri huku eneo la kifuani kukiwa na mchoro wa jani la mzeituni , alinyoosha mikono yake na kuinua ngao ya Aegis usawa wa kifua chake na Siraha ya Pallas upande wa kulia , chuma hicho kilitoa mngao na msisimko unaoendana na mwili wake.
“Unaweza kuona nani anakwenda kushinda ?”Aliuliza Poseidon ambae alikuwa ameshikilia Chusa kubwa ya meno matatu.,
Mfale huyo wa bahari alikuwa katika muonekano usiokuwa ukivutia m nywele zake zilikuwa zimetapakaa na alikuwa na mwili mkubwa unaotoa mng’ao wa rangi ya bluu , alikuwa na mgogo wenye ncha kali kama vile ni mnyama wa baharini , kuanzia kwenye kiwiliwili kwenda chini alikuwa na umbo kama la nyoka wa baharini.
“Mimi na Zeus katika miili yetu uwezo wetu ni sawa na kusema levo a mapigo elfu kumi ya radi , uwezo wa Roma mara baada ya kuipita Dhiki ni sawa na wa kwetu au uliongezeka kidogo , kwa adui wa uwezo huo pamoja na kutokuwa na uungu unabii wangu hauwezi kuwa sahihi”Aliongea Athena akimjibu Poseidon,
“Haiwezekani , haijalishi ni kwa spidi kiasi gani uwezo wake unaongezeka hawezi kufikia mwisho mwa levo mwa mapigo elfu kumi ya radi “Aliongea Hephaestus mungu wa moto.
Alikuwa na nywele ambazo ni kama vile zinawaka moto akiwa nusu mtupu na mwili wake wa rangi ya shaba , alikuwa na utimamu wa kutosha wa kimwili na misui yake imepinda pinda kama jiwe huku akiwa na makovu kama vile yamechongwa katika mwili wake makusudi , upande wa hini kabisa alikuwa amevalia suruali ambayo imeunganisha na vyuma kwa namna flani hivi kama magamba.
Ijapokuwa alikuwa jitu kubwa sana, muonekano wake ni kama ulikuwa ukiadilika badilika na kumfanya kuwa mwepesi kama mwewe.
“Wewe Hephaestus kwanini usijaribu na hilo nyundo lako kuvuruga Dhiki yake?”Aliongea Hermes huku akitoa kiheko.
Tofauti ya Hermes na wengine ni kwamba hakuwa na mwili mkiuubwa na alikuwa na muonekano kama wa binadamu lakini sura yake ikiwa imezidi uzuri kimuonekano , alikuwa na kiuno chembamba mno, alikuwa ni kama vile amevaa vazi la kutengenea ambalo limeunganishwa na mbawa.
Hakuwa mpana sana bali alikuwa mrefu kwenda juu na kumfanya kuonekana kuwa mwepesi zaidi.
“Unadhani nashindwa kufanya hivyo , kwanini uwezo wa sisi Titanni kuwa mdogo mbele ya binadamu?”Alliongea Hephaestus kwa jeuri na palepale aliinua lishoka lake juu ambalo liliweza kushika moto mara moja na kuanza kuyeyusha anga.,
Faida nyingine ya miili ya kititani ni kwamba miili yao imeunganishwa na namna kanuni za anga zinavyofanya kazi , mashambulizi yao hayakuhitaji kutumia kanuni za anga kwa nia maalumu bali anga lenyewe ndio huwapatia nguvu.
Ni kama Hephaestus alivyoinua tu nyondo yake palepale ilishika moto na kuana kuunguza anga,
“Nyundo ya moto mtakatifu”
Hephaestus aliruka huku akifyatua lile linyundo na kulifanya lionekane ni kama linadondoka mahali Roma alipo , nyundo hio ilienda moja kwa moja kuvamia kizingia kilichomfunika Roma.
BOOM!!!
Mshindo mkubwa wa sauati uliweza kusikika mara baada ya kizingia kutingishika , nguvu yake ilisambaa kila kona
Wimbi hilo lililoambatana na moto liliyeyusha barafu yote iliokuwa katika nha ya kaskazini na kuwa bahari kikamilifu,
Lakini bado tu licha ya kizingia hicho kupigwa na kanuni za anga kupitia nyundo hakikuharibika wala kusogea hata kidogo
Hephaestus aliishia kukunja sura na miungu wengine pia walikuwa katika hali ya mshangao.
“Ni tabia gani ya ki elementi imetumika kutengenezea nguvu ya kiroho mpaka kutfengeneza kizuizi chenye nguvu namna hio kiasi cha kutoarhirika na kanuni za anga?”Aliuliza Hera.
Upande wa Roma alikuwa akijua mabadiliko ambayo yametokea upande wa ncje na uwezo wa miungu ulikuwa umeongezeka katika levo nyingine kabisa na wanajarbu kuigilia Dhiki yake,
Lakini ujio wa radi ya mapigo elfu kumi ulimfanya kutojali sana kile kinachoendelea
Katika Ombwe la mfereji uliotengenezwa na nguvu za kiroho hali ya giza ilitanda huku msukumo wa mawimbi ya hewa yakiongezeka na msisimko wa nguvu ya ajabu ulivamia ndani yake.
Kadri msisimko wa nguvu ya kimaajabu kungezeka ndivyo namna uzio uivyoendelea kuimarika zaidi na zaidi , kisingia kilizidi kuzunguka kwa kasi kubwa mbo na kufanya mfereji wa ombwe kuzidi kwenda angani
Roma aliweza kuhisi mvutano wa hali ya juu mno wa nguvu ya ajabu na tabasamu la ahueni lilijjionyesha kwenye midomo yake
“Kwahio kumbe ipo hivi”Roma alijisemesha moyoni.
Dakika ileile ilikuwa ni kama vile nyoka mweusi anashuka kutoka juu angani kupitia lile ombwe la mfereji na kufanya iwe kitu cha ajabu mbo kwa miungu wote waliokuwa katika eneo hilo.
Ukiachana na Sharif na Aoiline wlaiokuwa katika ulimwengu unaojitegemea hakuna ambae alitarajia radi ya mapigo elfu kumi ni nyeusi.
Radi hio yenye rangi nyeusi ya kimaajabu ilionekana kama vile ni wino na urefu wake ulifanya kuwa kama kamba nyeusi ndefu inayoheza cheza kutoka juu mawinguni,
Kilichowashangaza zaidi ni kwamba , radi hio nyeusi ilishuka bila ya ngurumo , yaani hali ilikuwa tulivu mno na ilikuwa ni kama hakuna kilihokuwa kimetokea.
Mandhari yalikuwa ya kimaajabu kwa wote na walizidi kuona ni maajabu mara baada ya pigo la radi kumfikia Roma bila ya sauti kabisa.
Waliweza kumuona Roma ndani ya ombwe la mfereji akiwa amezingirwa na ile radi nyeusi.
Radi hio haikutoa mwanga kama radi nyingine , ki ufupi ni kwamba unaweza kusema sio radi ni kitu kingine kabisa
Ukichana na mfereji huo mazingira yanayozunguka eneo hilo yalikuwa hayajaaathirika hata kidogo hata bahari iliokuwa chini ya Roma ilionekana kuwa tulivu.
“Hii ndio radi ya mapigo elfu kumi kwanini ni nyeusi?”Aliuliza Hermes lakini ilikuwa wazi miungu wote waliokuwa ndani ya hilo eneo hawakuwa na majibu.
Roma ambae alikuwa amezingirwa na kiza cha radi nyeusi ni kama vile alikuwa kwenye ulimwengu mwigine kabisa.
Akiwa amefumba macho yake aliruhusu radi ile nyeusi kuungana na mwili wake kidogo kidogo.
Alizuia pumzi na kuindoa akili yake katika mazingira ya mbingu na ardhi , alikuwa pia amezuia nishati za mbingu na ardhi kutofanya kazi .
Katika macho yake alichoweza kuoa ni anga lisilokuwa na mwisho , Roma aliweza kugundua alikuwa katika kundi la nyota za galaksi ya Milk way.
Nyota alizokuwa akiona zilitoa mingao ya kucheza cheza kama vile ni madini ya thamani kubwa yaliokuwa gizani.
Ulimwengu ulikuwa katibu yake na kumpa hali flani ya ukawaida ambayo hakuwahi kuihisia hapo kabla , katika eneo ambalo akili yake ilikuwa mwili wake ni kama vile ulikuwa ukijongea bila shida yoyote na kumfanya kusafiri mamilioni ya maili ndani ya sekunde tu.
Alikuwa ni kama samaki anaeogelea katika maji mengi au ndege anaepaa angani , ulimwengu aliokuwa ulimshangaza sana.
Radi ile iliendelea kuwa endelevu ikimzunguka kana kwamba inamlaki Roma . haikumletea maumivu yoyote wala usumbufu.
Lakini sasa Roma kila alipojaribu kuishikilia na mkono wake alishindwa kabisa
“Nini nakosa , bado nashidwa kuidhibiti?”Roma alijiuliza.
Katika radi hio Roma alikuwa akiona kabisa nishati za aina tatu ambazo ni kama anazijua
Nishati ya moto wa Zambarau , moto wa rangi ya bluu na moto wa rangi ya samawati”
Ni radi au moto wa rangi tatu ambao umetokana na elementi za moto , maji na nishati ya hasi na chanya lakini ajabu ni kwamba nishaati zote tatu zilionekana kuungana pamoja na kutengeneza radi hio nyeusi.
Kuungana kwa moto wa zambarau na bluu kunatengeneza radi ya mapigo tisini na tisa , kuungana kwa moto wa bluu na samawati ilitengeneza radi ya mapigo elfu moja ya radi
Je kuna uwezekano wa radi ya mapigeo elfu kumi kutokea kwa kuunganishwa kwa elementi zote tatu za moto ? hapana…
Kwa akili zake za haraka aliwez akuhisi kuna kitu cha ziada kilihokuwa katika hio radi ya kimaajabu , ilikuwa na nguvu zaidi kuliko elementi zote tatu za rangi ya moto.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kutokea kwa radi hio nyeusi ni unganiko la nguvu za aina nne na kufanya radi hio kuvuka vizuizi vya kanuni ya nafasi na muda na nguvu yake ni kama ufunguo wa kuvunja vizuizi vyote vya mbingu na ardhi na kumfanya kuingia katika ulimwengu wa anga.
Roma alikumbuka swali la Clark akimuuliza je anao uwezo wa kupaa kwenda anga za mbali bila shida yoyote na alimjibu kwamba hawezi kwasababu hana nishati ya kutosha kuishi katika anga za mbali
Sasa radi ilikuwa mbele yake ilikuwa ni kama ufunguo wa kumuwezesha kwenda anga za mbali
Bila kujielewa Roma alikuwa ameingia katika mbingu nyingine yenye ufumbuzi tofauti na muda ulikuwa umesimama na kanuni za anga ni kama hazifanyi kazi katika mbingu hio.
Alikuwa ni yeye na ulimwengu ulikuwa wake, ilikuwa ni kama amefanaishwa na ulimwengu wa anga za mbali.
Taratibu kila kitu katika ulimwengu wake wa kawaida kilipotea , miungu waliokuwa wakimshambulia , Mti mama , bahari , hewa , dunia , anga na kila kitu kilipotea.
Hata zile nyota ambazo zlikuwa akiangalia zilianza kupotea tena katika ufahamu wake na hakuona tena , lakini sasa hata kama kila kitu kilikuwa kikipotea katika ufahamu wake hata muda kusimama lakini kila kitu kilikuwepo licha ya kuonekana kutokuwa na athari zozote,
Hio ndio ilikuwa ni asili ya anga tokea mwanzo , hio ndio ilikuwa ni nishati ya awali kabisa iliokuwa imefunika kila kitu ikiwemo dunia na sayari nyingine.
Roma kwa haraka sana alihisi ni kama alikuwa na macho manne ambayo mawili yametokea ndani kabisa katika nafsi yake, yaani ilikuwa ni kama vile kuna mtu anaemfunilia kila kitu kilichokuwa mbele yake.
Kila kitu alichofahamu kuhusu ulimwengu kilibadilika kabisa kutoka katika ujazo mpaka kuwa mtupu na tena kutoka kuwa mtupu mpaka ujazo.
Radi ya mapigo mengi ilikuwa imebadilika mara moja kutoka kutokushikika mpaka kushikika.
Kwa kutingishika tu hatimae aliweza kurudi kutoka uliwengu wa ufahamu mpaka katika uhalisia na kilichofuatia ni tabasamu la kutoka katika ujinga lililopamba uso wake na alianza kucheka kwa furaha kubwa kiasi cha kumfanya atingishike mwili na taratibu akayafumbbua macho yake.
Katika ombwe la mfereji ile nguvu ya kimaajabu ni kama ilihisi kitu na kuanza kujikusanya kwa kujitosheleza.
Kizingia kilichokuwa kikimzunguka kilianza kupotea taratibu na hatimae kabisa na kufanya iwe ni kama hakuna kilichotokea na amani ikarudi duniani.
Jambo hilo liliwashangaza miungu kwa mara nyingine , radi ya mapigo elfu kumi haikuwa kama matarajio yao kwani ilipiga mara moja tu na kisha kupotea.
“Hapo tunaweza kusema kafanikiwa ?”Aphrodite aliuliza akiwa na muonekano usioelezeka.
Kama alivyopewa utu wa jina la mapenzi na urembo hakika alikuwa na muonekano wa kuvutia mno , alitoa mng’ao wa rangi ya dhahabu , mtu anaweza kumsifia kwa kumfanya kielelezo cha ustadi safi , gauni lake la hariri nyeupe lilipambwa na udarizi wa maua yaliochanua na ndege wa dhahabu anaeruka , kiunoni alikuwa amefunga mkanda wa dhahabu ambao ulikuwa na utajiri wa mchoro wa kuvutia mno, mkanda huo ndio ulipewa jina la Magical Girdle.
“Nashindwa kuhisi mkandamizo wowote kutoka kwenye nguvu ya nishati na mbingu , hivyo ninaamini atakuwa amefanikiwa kupita Dhiki kwa asilimia mia moja”Aliongea Zeus akimjibu Aphrodite.
“Vyovyote vile , hii ndio vita yetu ya mwisho”Aliongea Ares.
Ares alikuwa ni kama vile ni mwanavita wa zama zile za kale , ukiachana na mkuki wake mrefu wa chuma alikuwa amevalishwa mwili mzima na cchuma kizito na kumfanya aonekane pua tu.
“Wote kaeni pembeni katika hili na mlinde mti mama , mimi pekee na Zeus ndio tupo na uwezo wa kupambana nae , kama tukipoteza nyie msipoteze muda wa kupambana nae”Aliongea Athena akimwangalia Roma,
Watitani hao wote hususani Hera na Poseidon walionekana kukasirishwa na maneno ya Athena , ijapokuwa uwezo wao haukulingana na wa Zeus na Athena lakini pengine walilingana na jini wa levo ya mapigo elfu kumi ya radi mara baada ya kujibadilisha kuwa mwili wa nishati , kubwa zaidi Hera alikuwa na mti wa matunda ya shufaa na kila tunda moja linaweza kumsaidia kufukuza aina yote ya mashambulizi.
“Acha kujiona unaweza kila kitu , umeshakiri wewe mwenyewe huna uwezo wa kumtabiria , nini kinakufanya uamini una uwezo wakushindana nae ukijumlisha na alivyo na akili , ukweli wa kwamba amefanikiwa kuigia katika levo ya mapigo elfu kumi ya radi na akapita moja kwa oja anatakuwa katikati mwa levo ya mwisho wa Dhiki, hebu achaneni na huyo malaya anachoongea na tumuueni huyu mwanaharamu na kuiharibu kabisa nafsi yake ili ajue ni kosa gani amelifanya kuua uungu wa Hade”Aliongea Hera.
Mara baada ya kutaja kuua uungu wa Hades , viumbe hao wote wa kititani waliharuka kwa hasira na kutupia pembeni wasiwasi wao na kumnyooshea Roma siraha zao.
Apollo alikuwa amekwisha kurudi katika umbo linalofanana na mngao wa madini ya almasi na bahari kumzunguka iliana kugeuka mvuke kutokaa na mngao wake kuwa na joto kali.
Artemis na yeye alikuwa katiak umbo la kititani na alitoa mngao mweupe kama wa mwezi , katika kiichwa chake amejifunga kibanio cha rangi ya dhahabu huku nywele zake ni kama vile zina umeme kwa namna inavyocheza cheza. amevalia gauni refu kama vile ni la harusi huku akimshambulia Roma kupitia Selene, bahari chini yake ilikuwa imeganda kutokana na nishati ya ubaridi aiokuwa akitoa.
Poseidon , Ares , Hephaestus na Hermes wote waliinua siraha zao wakipgana kummaliza Roa na pigo moja.
Nishati ya anga ilijikusanya karibu yao na kutengeneza umbo la chusa linalotoa mngao wa rangi ya bluu iliokolea , upande wa mungu wa vita Ares alikuwa ni kama vile anadidimiza anga katika eneo alilosimama Roma huku Caduceus ikiana kumtengenezea Roma ndoto na kuingilia usikivu wake.
Ukimtoa Aphrodite pekee , miungu wote ni kama wamepamba kutumuia uwezo wao wote kushambulia , hata hivyo hakuna wa kumlaumu kwani siraha yake ya magical girdle haikuwa kama siraha zao ambazo zinafanya mashambilizi ya moja kwa moja , hivyo kumfanya kuwa mnyonge kati yao.
Ares ambae alichujuliw akama mdhaifu sasa alikuwa na uwezo sawa na mwishoni wa mapigo mengi ya radi na kwa kuagalia tu miungu wote walionekana uwezo wao wakutumia kanuni za anga umeimarika maradufu.
Zaidi sana ni kwamba miungu wote walijua mashambulizi ya rasha rasha hayana maana hivyo walihitaji mbinu yakinifu ambayo inaweza kumzimisha Roma na kumtengenezea majeraha makubwa.
Mara baada ya kuona hakuna wa kumsikiliza Athena hakutaka kuongea lolote na aliinua siraha yake a kisha wakapenda ishara na Zeus na ghafla tu alimsogelea Roma kwa spidi kwa ajili ya kumshambulia.
[emoji3590][emoji1635]
 
Kila mtu alijua nafsi ya Roma imekwisha kupotea mara baada ya kuachana na mwili lakini maajabu yake ni kwamba ilionekana ilinasa katika hicho kioo kama sio kushikiliwa.
“Katika vitabu vyetu inasemekana kwamba kioo cha nafsi kina uwezo wa kusafiri kupita katika ombwe kwenda anga za mbali na kurudisha muda nyuma na nafasi , hivyo inaonekana mara baada ya kumtambua Roma kama Master wake, kilizuia muda na nafasi kwa nafsi ya Roma isiondoke duniani”Aliongea Aoiline.
Maneno yake yalitokana na vile walivyojifunza , majini walikuwa na siri nyingi sana kuhusu ulimwengu wa anga za mbali na maajabu ya dunia , sasa kile ambacho amesoma ndio kilichokuwa kikitokea katika macho yake.
Dakika ileile ni kama vile ule mwanga wa rangi saba ulikuwa ni lift kwani uliishusha nafsi ya
Roma mpaka kwenye maiti yake taratibu sana.
Kitendo cha kuamka kwa nafsi katika mwili wake na Andiko la urejesho palepale lilianza kufanya kazi yake ya kimiujjiza.
Awamu hio kila kitu kilienda vizuri kwani Roma sio kwamba alikuwa akizuia Andiko la urejesho wa Azimio usifanye kazi.
Muda uleule upepo ulianza kuongezeka katika eneo ambalo Roma mwili wake umelala na nguvu ya kiroho ilitawala kwa kiasi kikubwa na damu ambayo imeshaganda ilipata moto kwa mara nyigine na nishati za mbingu na ardhi iliamka kwa kasi kubwa na kufanya senta ya mwili wake kutuna na kusinyaa kama vile ni jipu.
Dakika chache eneo la kifua chake paliziba kabisa huku ikionekana moyo wake kupona na kuanza kudunda kwa mara nyingine chini ya nguvu ya kimaajabu ya kutisha ya Andiko la Urejesho wa Azimio.
Edna aliishia kuduwaa akiangalia kile kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake , hakupepesa macho hata kidogo akiogopa alichokuwa akiangalia kitatoweka na kubakia kuwa ndoto.
Ukweli ni kwamba hakuthubutu hata kupiga kelele na aliishia kuziba mdomo wake na mkono , huku machozi yakiendelea kumtoka mfufulizo, huku uso wake wa kirembo ukiwa mwekundu kama yai , hakuthubutu kuonyesha furaha yake kwa makelele.
Wakati kila mmoja akiwa katika hali hio ya kushangaa hatimae Roma aliweza kupona kabisa na hakuonekana tena kama maiti bali kama mtu alielala usingizini.
Kifua chake na tumbo lake vilipanda na kushuka ikionyesha amerudiwa na pumzi na hatimae aliyafumbua macho yake.
Kana kwamba alikuwa katika hali ya furaha mara baada ya sura ya kwanza kuiona akifumbua macho ni Edna alinyanyua mkono wake na kumfuta Edna machozi.
“Hehe.. Babe wife , usiwe na hasira hivi , sio kama nilikuwa nikifanya utani kwa kujifanyisha kufa , kidogo tu nipoteze uhai moja kwa moja awamu hii”
Edna hatimae hakutaka kuzuia tena hisia zake na kwa haraka sana alimnyanyua Roma kwa nguvu zake zote na kumsimamisha na kisha alipitisha mikono yake katika shingo na kuanza kuangua kilio akijilaza kifuani.
Kwa wakati huo , akili yake haikufanya kazi , hakuweza kuelezea namna gani anajisikia zaidi ya kutoa kilio cha furaha.

SEHEMU YA 798
Muonekano wa Roma kwa upande wake ulikuwa ni ule ulionekana kuwa na mawazo kidogo, aliishia kuinua mdomo wake juu kama mtu ambae amekosa pumzi.
“Okey , Okey … Edna Darling , najua unafuraha .. lakini imekuwaje ukawa na nguvu nyingi kiasi hichi ?Ouch .. nashindwa kupumua..”
Roma alikuwa hajui acheke ama alie kwani Edna alikuwa amemkaba mno shingo yake kama kwamba anataka kumnyonga , hivyo kumfanya kushindwa kupumua vizuri.
Kwa bahati nzuri hakuwa hatarini kiafya , alijiambia kama angerudi kuwa hai na kisha kunyongwa na mke wake kutokana na kumbatio angejisikia vibaya sana.
Edna hatimae alimuachia huku macho yake yakiwa na machozi , aliishia kupiga mapaja yake huku akiendelea kulia kwa kwikwi akikosa hata ujasiri wa kumgusa Roma tena.
“Bado tu unapenda kunichezea , kwanini unapenda kucheza na akili yangu , nani kakuambia ujiue , wewe ni mtu mbaya sana .. kwanini ulitaka kumtelekeza mtoto wetu na kuondoka mwenyewe….”
Edna alishindwa kabisa kujizuia kuacha kulia , ule ukauzu wake wote ulikuwa umeshampotea na kwa wakati huo alikuwa mwepesi kihisia kama ua ambalo litadondoka na kunyauka muda wowote.
Roma alichoweza kufanya ni kuishia kumkumbatia na kumpiga piga mgongo wake kwa namna ya kumtuliza , kulikuwa na dalili za kukosa cha kufanya muda huo kutuliza hali aliokuwa nayo mke wake lakini hata hivyo alikuwa na furaha kuona namna ambavyo mke wake alikuwa akimpenda.
Tukio hilo liliwafanya Aphrodite na Artemis kutoa machozi , ilikuwa ni kama vile jua limepotea milele na vilevile hakukuwa na baridi kwa wakati mmoja.
Hatimae Roma aliweza kumfanya Edna kuacha kulia na kukigeukia kioo ambacho bado tu kilikuwa kikielea Angani.
Kioo hicho na nafsi mara baada ya kupungiwa mkono na Roma kiliacha kuendelea kutoa ile miale ya rangi na kurudi katika ukubwa wa kawaida na kisha kilidondoka kutoka juu na kwenda kutua katika mikono ya Roma.
Kila mtu aliekuwa katika eneo hilo alimwangalia Roma akifanya mambo hayo yote , kwao kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni miujiza ,walikuwa wakijiuliza inakuwaje kioo cha namna hio kufanya miujiza kuurudisha uhai wa Roma.
Baada ya Edna kufuta machozi hatimae na yeye alikodolea macho kioo hicho ambacho kilikuwa katika mikono ya mume wake kwa macho ya shukrani.
Ni kama alikuwa akitaka kusema asante kioo kwa kumrudisha mume wangu hai.
“Hey ,Asante kwa msaada wako Lumiel, nadhani tutakuwa marafiki wazuri kuanzia sasa na baadae , umeyaokoa maisha yangu hivyo nitahakikisha unaishi maisha mazuri , sitokufanyia ubaya na urafiki wetu utadumu katika wema, sawa?”
“Lumiel?!”
Kila mtu aliekuwa hapo akiwemo Sharif walikuwa na muoneknao usio kuwa wa kawaida mara baada ya kusikia kioo hicho kikiitwa na Roma jina la Lumiel.
Kioo kile kilionekana kuelewa maneno ya Roma kwani kilitoa miale yote saba kwa namna ya kuitikia na kumfanya Roma kucheka.
“Haha.. jina linaweza kuwa sio zuri kimatamshi lakini libebeba maana kubwa , Nuru ya mkuu wa Enzi. Ila kwanzia sasa nitafupisha jina lako na kukuita Lumi, unaonaje juu ya jina hili?” Roma alikuwa akiongea na kile kioo na baada ya kuuliza hilo swali kilitoa mwangaza tena.
Watu wote walishikwa na butwaa kwa namna ambavyo Roma alikuwa akiwasiliana na kioo hicho , katika mazingira ya kawaida ilikuwa ni kama vile mtu anawasiliana na Roboti ambalo linatumia akili mnamba(AI) .
“Hubby inamaana hiki kioo kina kuelewa unachoongea ?”Aliuliza Edma ambae alikuwa na shauku kubwa , hata kama alikuwa tayari na maarifa yote ya Athena katika akili yake , hakuwa akijua kioo hicho kilikuwa ni nini.
Lilikuwa swali ambalo hata Sharif na Aoiline pia walikuwa nalo na waliishia kumwangalia Roma ili kusikia jibu lake.
“Dahh .. nimejikuta nikiwa bize na rafiki yangu Lumi na kusahau kilichotokea..”Aliongea Roma kwa kujipiga paji la uso kama vile kuna kitu amesahau na palepale ndipo alipoanza kuelezea kila kitu.
Kumbe hata kwa Roma mwenyewe alijua tayari amekwisha kufa lakini mara baada ya nafsi yake kutoka Roma alijihisi ni kama vile yupo ndotoni , kwani alijikuta akiwa katika ulimwengu mwingine ambao ni kama vile Kioo hicho cha nafsi ni mlango wa kuingilia na kutoka.
Ulimwengu huo aliokuwepo ni ule wa nafsi , yaani kwa lugha nyepesi ni kama vile alikuwa katika ulimwengu ambao nafsi huhifadhiwa baada ya kifo kwa kukusanywa na kioo hicho.
Sasa mara baada ya kufika katika ulimwengu huo ambao ni kama haukua na ardhi yaani chini ni anga na juu ni anga alisikia sauti ikisemezana nae na iligeuka ni nafsi hio ya Dhana hio ya mkuu wa Enzi ndio iliokuwa ikimuongelesha.
Nafsi hio ilimwambia kwamba imepata ruhusa kutoka kwa mmiliki wake wa awali kumtambua yeye kama Master wake na msaidizi mkuu kwanzia sekunde moja katika mazingira ya sayari ya dunia , yaani ulimwengu wa binadamu na hio ndio sababu ambayo kioo hicho cha nafsi kirudisha nafsi ya Roma na kuurejsha uhai wake kwa ajili ya kumtambua.
Sababu kuu ya kupata ruhusa ya kioo hicho kumtambua Roma ni kutokana na kwamba alifikia upeo mwingine ambao ndio kiumbe pekee kutoka duniani aliefikia upeo huo juu ya siri za ulimwengu.
Lakini hata hivyo kama Roma asingekuwa na kioo hicho tokea mwanzo kutoka katika Jicho la anga angekuwa amekufa kweli hata kama ameweza kufikia katika upeo huo .
Sasa kutokana na uwezo wa Roma kioo hicho ambacho kilikuwa katika mikono ya Roma kiliamua kuomba ruhusa kumtambua Roma kama Master wake na msaidizi.
Sasa ilionekana ni kama kulikuwa na maelezo mengi sana juu ya kioo hicho kwanzia kwa mtu alieomba ruhusa lakini kwa upande wa Roma hakuwa na kingine zaidi cha kuelezea kwani nafsi ya kioo hicho haijamwambia bado.
Sasa Roma aliona kila kitu kilichotokea mara baada ya kifo chake wakati akiwa katika miliki ya kioo cha nafsi , mwanzoni alitaka kutoka mapema na kurudi lakini nafsi ya kioo hicho ilikuwa na maelezo mengi ya kumwambia hususani uwezo halisi wa kioo hicho ukiachana na kushikilia nafsi.
Kila mmoja aliesikia alijikuta akishangazwa na jambo hilo , kwani kioo hicho kilionekana kuwa na uwezo wa maajabu mno.
“Nadhani sijakosea kabisa kuweka matumaini yangu makubwa kwako tokea mwanzo , hatimae umenifanya nijivunie , unaiisikiaje kufikia katika huo upeo?”Aliuliza Aoiline.
“Nimeelewa kwa namna flani tu hivi kwa msaada wa Dhiki ya mapigo Elfu kumi ya radi , vingineyo ingekuwa ni ngumu sana kuja kufikia katika huu ufunuo nilio nao sasa”
“Upeo na ufunuo gani , mbona mnaongea kimafumbo mafumbo?”Aliuliza Edna ambae alionekan kukunja sura , huku akionekana kutopenda namna ambavyo Aoiline alikuwa akimwangalia Roma kwa macho ya matamanio huku akiongea vitu ambavyo haelewi.
“Ninachomaanisha ni kwamba , ufunuo ambao mwanzoni nilikuwa nao kikomo chake ilikuwa ni katika mazingira ya dunnia pekee , upeo wako ukishatoka katika mazingira ya dunia au Parrallel Space ni kitu kingine kabisa , kwa mfano moja ya upeo ambao nimepata ni Maada giza(Dark Matter) kuwa asili halisi ya ulimwengu wote, uelewa huu umenileta karibu zaidi na ufunuo wa kihisia usioelezeka ambao ni wa ki-Cosmic zaidi , unaweza kuita ufunuo wa anga za mbali wa kinishati”
Roma aliongea kwa kutumia fasihi zaidi , ilikuwa ni kama kuna kitu anajaribu kuficha na kuwafanya waliokuwa wakimsikiliza wasielewe kabisa.
Lakini hata hivyo kuna kitu kimoja ambacho miungu waliweza kuelewa , ukweli wa kwamba Roma alikuwa na uwezo wa kubatilisha kanuni zote za anga kwa kuwa tu na uwezo wa kudhibiti radi nyeusi ambayo ilikuwa na mchanganyiko wa maada nyeusi , kwao lilikuwa jambo la kushangaza.
Radi nyeusi ilikuwa na nguvu ambayo yenyewe ilitokana na mchangyaiko wa radi kama radi na maada nyeusi , sasa ukija katika uhalisia wa Maada nyeusi , ni aina ya njia ambayo humfanya mtu kuona zaidi.
Yaani kwa lugha nyepsi ni sawa na watu wote mue katika chumba chenye giza lakini Roma peke yake ndio mwenye uwezo wa kuona kila mtu aliekuwa ndani katika chumba hicho bila kutumia mwanga , hio sio kwasasababu alikuwa na nguvu za kimaajabu lakini ni kwasababu alikuwa na uwelewa wa namna giza linavyokuwa na asili yake.
Sasa unachopaswa kuelewa kuvuna nishati ya mbingu na ardhi kupitia mbinu ya andiko la urejesho ni kama njia, ni sawa na muumini wa dini yoyote anaambiwa ukitenda mema na kushika sheria zote za dini utafikia uzimani au Akhera.
Sasa basi kama Radi ya mapigo elfu moja ndio mwisho kabisa wa safari ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi kinachofuata kuanzia hapo ni hatua ya kwanza ya ufunuo mkuu , sasa hapa ndio kina kuja kitu kama sehemu ya kwanza ya ufunuo , sehemu ya pili ya ufunuo mkuu na sehemu ya tatu ya ufunuo mkubwa.
Roma alikuwa katika sehemu ya pili ya ufunuo mkuu huku upande wa Sharifu yeye alikuwa katika sehemu ya kwanza ya ufunuo mkuu. “Inaonekana ni mimi ambae sikuweza kuiona nuru mapema , kuna ufunuo wa aina tofauti tofauti katika upeo wa kidunia na ufunuo huo wote humpeleka mtu katika mwisho mmoja ambao ni ufunuo wa Anga , ni kitu ambacho sikukukielewa mapema lakini huo ndio ukweli”Aliongea Sharif,
“Sasa hivi tayari Roma amekidhi vigezo na anaweza kushika majukumu yako kwanini usiwe na furaha , angalau unaweza kuondoka duniani na kuiendea njia nyingine”Aliongea Aoiline.

Sharif alijua mbweha huyo alikuwa akimtania lakini hata yeye pia alikuwa amefikiria mambo mengi , ukweli wa kwamba Roma alikuwa ameweza kufikia upeo huo kupitia njia ya upendo na kifo ilimfanya kuelewa mambo mengi , kitu ambacho ni kama alielimika.
“Umeshinda , sipo vizuri sana kama wewe lakini pia nataka kukushukuru , kwanzia sasa nadhani
ni muda wangu wa kuondoka kwa amani”Aliongea Sharif.
“Kama unataka kuondoka unaweza kuondoka lakini kabla ya yote hakikisha unarekebisha ulinzi wa gereza la roho na kusafisha hali ambayo umeisababisha mwenyewe , haya yote yametokana na mipango yako hivyo sitaki kukusaidia kurekebisha makosa uliofanya”
Sharif alijikuta akikosa cha kufanya na kujiambia huyu mtoto hakuwa tena akimuogopa kama mwanzo kwasababu muda huo ni kama wanalingana ki uwezo na ukiburi umeongezeka mara mbili kiasi kwamba anaanza kumpa maagizo.
“Nitarekebisha Gereza la Roho , sio kazi ngumu hata hivyo lakini hayo mapepo yanahitaji watu kuyakamata na kuyaharibu , hivyo siwezi kudili nayo moja baada ya lingine , kuhusu athari zilizopita dunia na joto kushuka sana ….”Aliwageukia miungu na kisha akatoa tabasamu.
“Nitamwalika mtu mmoja ambae anaweza kurudisha nguvu ya uhai wa dunia haraka iwezekanayo”.
Kauli hio ni kama iliwafumbua akili miungu na kujua alichokuwa akimaanisha.
“Dionysus!, Unafahamu Dionysus alipo ?”Aliuliza Hera ambae alikuwa na shauku ya kusikia jibu.
“Ni nani huyo sus’..”Aoiline aliuliza akishindwa kutamka jina.
“Ni Dionysus moja ya miungu kumi na mbili waliofanikiwa kuhamisha nafsi zao wakati ule , huyu mwenzao hapendi kabisa kupigana na anapendelea amani , hivyo siku zote alikuwa ni mwenye kujificha , lakini uungu wake una uwezo wa kipekee unaofahamika kama; ‘Uzao mpya’ , pia ana vitu viwili mno vya kuvutia , cha kwanza ni Ngozi ya Mbweha ambayo huvaa , ngozi ambayo ina uwezo wa kimaajabu wa kuotesha mimea na kingine ni Kikombe cha Divai ambacho kina uwezo wa kugeuza maji yote kuwa divai ya uhai na pale inapomwagikia mimea hukua kwa haraka sana , muda ambao atatoka , haitochukua muda mrefu kwa mimea yote kurudi katika hali ya kawaida na kutokana na dunia kuendelea kupata joto basi kila kitu kitarudi kama ilivyokuwa mwanzo”
“Sina haja sana na hicho kikombe cha Divai , lakini hio ngozi ya Mbweha, ikitokea nikiiona ninamuua”Aliongea Aoiline.
Miungu hao walijikuta wakipatwa na wasiwasi , lakini kwa Roma na Edna walijua fika Aoiline alikuwa mbweha hivyo lazima afurahiswe na kusikia ngozi ya mbweha.
“Wapi Dionysus amejificha ?, nimemtafuta kote bila ya mafanikio?”Aliuliza Edna ambae ni kama Athena anaeuliza.
“Roma na Aoiline mnamjua fik..”Aliongea Sharif.
“Sisi ?, nimeishi miaka elfu hamsini ndani ya ulimwengu wa majini pepo namjulia wapi mim..”
“Ndio kiongozi wa majini pepo mashetani wa anga katika miliki ya msitu wa mianzi Zambarau , jina lake ni Master Zao”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.
“Kumbe ni yeye , imekuwaje sijawahi kuona kitu cha tofauti kutoka kwake?”
“Uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi sio mdogo , hivyo haikuwa ngumu kwake kuficha uungu wake “Aliongea na kisha akamwangalia Edna.
“Kuhusu unabii wa Athena hawezi kufika katika ulimwengu wa majini pepo , lakini ukiachana na hivyo Zao aliamua kujificha yeye mwenyewe hivyo ingekuwa ngumu kumjua , hata mimi mwenyewe nisingempata kama nisingekuwa nawafatilia ninyi wote”
Roma aliona Master Zao alikuwa ni mwigizaji mzuri sana , alimfahamu fika kwani ndio aliekuwa rafiki wa Master wake Tang Chi na kulingana na wote kufanana tabia ndio maana wakawa marafiki wakubwa.
Hata kipindi kile cha shindano la kuingia mnarani mara baada ya kumuona Aoiline , alijifanyisha kuwa muoga kumbe yote ilikuwa ni maigizo tu ya kutotaka kugundulika ili mradi aendeee kujificha.
Lakini sasa kwa vyovyote vile vita imeshaisha na miungu walikuwa tayari kupotezea kila kitu na kuianza siku mpya wakiwa pamoja na binadamu.
Roma alikumbuka vyema Sharif alikuwa amemfcha Clark , hivyo alimwamrisha kumrudisha na kwa Sharif asingeendelea kumshikilia Clark hivyo aliahidi atarudishwa kisiwani.
Hatimae Roma aliridhika na matokeo yote na kisha alimshika mkono mke wake na kumkonyeza.
“Wife ni muda wa kruudi nyumbani sasa”Aliongea na kumfanya Edna atoe tabasamu lake tamu na kutingisha kichwa kukubali.
Dakika hio hio kama ilivyokuwa kwa Sharif na Aoiline walivyofika katika eneo hilo ndio namna ambavyo Roma na Edna walipotea mara baadaa ya anga kutengeneza shimo na kutumbukia.
Upande wa miungu waliuchukua Moyo wa Gaia na kuurudisha kama mwanzo ulivyokuwa chini ya miliki ya familia ya Yezi kule Korea na kisha wakampatia Poseidon kwa ajili ya kuuhifadhi.
Kisha wote kwa pamoja waliangaliana kwa kutabasamu kuoneysha hali za ahueni katika macho yao, ilikuwa ni wakati wa kufikiria upya maisha yao yajayo katika mazingira ya dunia.
Amani hatimae ikarudi.
Aoiline na Sharif walipaa mpaka juu angani zaidi na kuiangalia dunia kwa chini huku wakijaribu kuhisi joto la jua ambalo ni kama sasa limerudi katika ubora wake huku wakijaribu kuyawazia matendo yao yote na uzoefu wote waliopitia kwa miaka mingi ya hapa duniani.
“Aoiline , unadhani nini kimesababisha huyu mtoto kunipita na kushinda?”Aliuliza Sharif akionekana kama vile ni mwenye hali ya mkanganyiko ni kama hakuwa akiamini Roma ameweza kumpita ki upeo na kuwa chini yake.
“Au ni kwasababu sina elimu kubwa kuliko yeye
, haiwezekani anishinde ili hali ni mimi niliorahisisha mbinu ya Andiko la urejesho , au ni kwasababu ilipangwa , au ni kile kioo au nini , mbona nashindwa kuelewa?”
Aoiline alijikuta akimwangalia Sharif ambae alionekana kuchangayikiwa , kwa muda huo alimuona mwanaume huyo ni kama amerudi katika wakati ule ambao ndio kwanza anakutana nae.
“Ukweli ni kwamba kwa mtazamo wangu , ambae ameshinda sio Roma , sio hatiima yake au kioo cha nafsi au wewe..”
“Kama ni hivyo ni nani ameshinda?”Aliuliza kwa mshangao kidogo.
Alinyoosha mkono wake na kisha kuchukuwa wa Sharif na kisha kupitisha vidole vyao kwa namna ya kuunganisha.
“Its love!”
Alijibu akisema ni mapenzi au upendo ndio ambao ameshinda na kisha wawili hao wakiwa wameshikana mikono waliangaliana kwa tabasamu na kisha wakapotea pamoja.
******
TEN YEARS LATER (MIAKA KUMI BAADAE).
Ni katika ulimwengu wa majini pepo , ulimwengu ambao ki asili hujulikana kama ulimwengu wa majini pepo wa milenia.
Sasa katika miliki ya msitu wa mianzi zambarau upepo ulikuwa ukivuma na kutengeneza sauti kama ya wimbo na harufu yake kuvutia pua kwa wale waliokuwa wakiivuta.
Hali hio ya upepo ilichangayika na harufu nzuri ya mvinyo uliokuwa umejaa kilevi cha hali ya juu.
“Nimeshinda , Haha, Braza Chi , inaonekana hii
pombe ya kijani ni ya kwangu kwa ajili ya kunywa”
Wanaume wawili walionekana wakicheza mchezo wa Chess juu ya jiwe huku mshindi alikuwa akijipatia kikombe cha mvinyo wa kijani.
Watu hao walikuwa ni Master Chi na Master Zao ambae sasa jina lake lingine ni Dyonysus mungu wa divai.
Katika miezi kadhaa walikuwa na utaratibu wa kucheza michezo mbalimbali ile ambayo Zao alikuwa akiijua na ambayo Chi alimfundisha
Zao , katika mchezo ambao Zao hakuujua ni wa Chess na baada ya kufundishwa kwa muda alionekana kuelewa na hatimae kwa mara ya kwanza aliweza kumshinda Master Chi.
Sasa kwasababu ambazo hazikuwa zikielezeka , siku hio Master Chi alijikuta kila mchezo ambao alijaribu kucheza na Zao alifungwa na kunywa pombe yote iliokuwa na thamani kubwa.
Sasa kikombe cha mvinyo wa kijani ndio pekee ambacho kilikuwa kimebakia na mara baada ya kuona Zao anakaribia kukipeleka mdomoni alimzuia.
“Hey , hebu tulia kwanza”
“Ah , Braza Chi ndio kwamba hutaki kukubali kushindwa”Aliongea Zao ambae kwa wasiwasi alirudisha kile kikombe chini.
“Braza Zao huu mvinyo wa kijani ni zawadi nilioletewa na mjukuu wangu Lanlan alipokuja kunitembelea mwezi uliopita , ukinywa wote nitakuwa sijauonja hata kidogo , nakubali kushindwa lakini nikikuacha uumalizie nitaenda kinyume na nia yake nzuri kwangu , unaonaje kama nikikupatia aina nyingine ya pombe kufidia hii?”
“Unataka kunipa ile tuliozoea , kama naitaka si bora nitengeneze mwenyewe”
“Unatoa wapi ujasiri wa kunikumbusha hili swala , umekuwa ukinificha kwa muda mrefu kumbe muda wote ulikuwa mungu wa mvinyo , hapana huwezi kunywa huu mvinyo tena”Aliongea Master Chi kwa hasira.
“Acha zako hizo Braza basi , si miaka kumi imepita mpaka tumalize hili swala , inakuwaje bado una kinyongo tu ..”
Miaka kumi iliopita , Sharif alifika katika ulimwengu wa majini pepo na kumchukua Dyonysus kwa ajili ya kurudisha hali ya kimaisha katika sayari ya dunia na hapo ndipo Master Chi alifahamu rafiki yake ni sehemu ya miungu.
Sasa kilichomkasirisha Tang chi ni kwamba siku zote alijiona yeye ndio yupo vizuri kwenye kutengeneza mvinyo lakini matokeo yake Zao ndio alikuwa bingwa .
Kwa mwaka mzima Dyonyus alitumia Dhana zake katika kuifanya Biosphere ya dunia kurudi katika hali yake ya kawaida na baada ya hapo ndipo aliporudi ulimwengu huo wa majini pepo na kuendelea kunywa kujigalagaza na rafiki yake Master Chi.
Wote wawili walikuwa wakifanana tabia hawakutaka kufanya chochote zaidi ya kulewa.
Dakika hio hio wakati wakiendelea kulumbana juu ya kikombe cha pombe, kulikonekana kitu kikubwa umbo la koni cha rangi ya silver kikipaa kuja eneo hilo la msitu wa mianzi ya Zambarau kwa spidi kubwa sana.
Muoneknao wa kifaa hicho ilikuwa ni kama vile ni kisahani hasa kwa spidi yake na kufumba na kufumbua kilishafika katika mazingira ya wale wazee walipo na kilitoa mwanga mkali kutoka eneo la chini na kuanza kushuka taratibu katika mstari mnyoofu(Vertical line) na eneo la juu lilibadilika rangi kutoka silver na kuwa kama kioo na kisha mlango wake ukafunguka.
Msichana mmoja mrembo sana wa ajabu alishuka kutoka kwenye kifaa hicho na kukanyaga chini , alikuwa ni makadirio ya miaka kumi na moja au kumi na tatu hivi.
Alikuwa na mashavu yalionona , huku akiwa amevalia Tshirt ya bluu , Denim Short(Kaptura fupi hivi kama jeans) na Sneaker za rangi ya bluu , yalikuwa ni mavazi yalio jaa ujana ule wa kisasa zaidi na kilichomfanya kupendeza zaidi ni namna shepu yake ilivyokuwa ikianza kuchepua kwa kasi.
Sekunde ambayo Master Chi alimuona msichana huyo mrembo alimpotezea kabisa Zao na kutoa tabasamu la furaha huku akisimama.
“Are you here to visit me again , Lanlan?”Aliongea Master Chi huku akiwa ameipanua mikono yake.
Msichana huyo ambae alikuwa akivutia sana hakuwa mwingine ni Lanlan ambae alikuwa amekwisha kukua na kurithi uzuri wote wa mama yake na zaidi ya kumpita kabisa, jina lake kamili ni Lanlan Roma Ramoni Kweka.
Ukizungumzia uzuri wa Lanlan ni sawa na kusema amerithi kutoka kwa Edna au Seventeen lakini hata hivyo pengine ni mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi yamemfanya kuwa tofauti sana , alikuwa na nywele ndefu mno kama vile ni mzungu na uso wake ulituna kidogo na kumfanya kupendeza zaidi.
Ijapokuwa hakuwa m’cute kama alivyokuwa mdogo lakini alikuwa ni pisi kali na classic , shukrani zimwendee Edna kwa malezi mazuri.
“Grandpa!”
Lanlan alitabasamu huku akimkimbilia babu yake na kwenda kukumbatia kwa nguvu.
“Grandpa are you gambling with Mr Drunkard?”Aliuliza akimaanisha anacheza kamari na Mr mlevi.
“Hehe, ndio tena ninatia huruma maana nimekuwa nikipoteza sana kila mchezo , Lanlan , umekuja na mvinyo mwingine leo?”Aliuliza Master Chi kwa furaha.
“Naona nimeshakuwa chupa ya mvinyo katika macho yako siku hizi?”Aliongea Lanlan lakini licha ya kuongea hivyo alichezesha mkono wake na palepale alitoa chupa za mvinyo kutoka hifadhi ya pete na kumuwekea katika meza.
“Nimemuibia baba hizi chupa za Dalmore kutoka katika hifadhi yake , nimesikia kutoka kwa babu Ron ni ghali mno zaidi ya paundi elfu kumi kwa chupa moja , Babu hakikisha ukimaliza unaficha chupa Dady asije kuziona , akiona lazima atanisemea kwa mama tena”Aliongea huku akimtingisha Master Chi mkono wake.
Wanaume hao wawili waliitikia haraka haraka kama vile wanataka kunywa haraka kilevi hicho.
Baada ya kukagua chupa hizo huku wakimsifia Lanlan kwa kuleta zawadi hio nzuri hatimae walitaka kujua kilichomleta, kwani ni mwezi uliopita tu alikuwa amekuja kutembea hivyo ni lazima alikuwa na ujumbe.
“Lanlan kuna kingine umekuja nacho?”Aliuliza MasterChi.
“Mr Mlevi leo nimekuja hapa kwa ajili yako ,
Mommy ameniambia nikufikishie taarifa Auntie
Clark na Sis Naira wameshamaliza kujenga Spaceship kwa ajili yenu , iwe unataka kubaki duniani au kuondoka ni juu yako lakini unapaswa kukutana na wenzako kwanza”Aliongea Lanlan.
“Mbona mapema hivyo?, sitaki kuondoka hapa duniani mapema hivi , lakini nadhani napaswa kuwaaga , lini wanatarajia kuondoka”
“Tunaweza kuondoka wote sasa hivi , unachopaswa ni kumrukia Kibonge wangu na tuondoke”Aliongea akinyooshea kijindege chake alichokuja nacho.
Ndege hio ilikuwa ni teknolojia mpya ya Ant- Gravity ambayo ilivumbuliwa na Clark miaka saba iliopita , spidi yake ilikuwa ni kubwa mnno na ilikuwa na uwezo wa kusafiri kuingia katika ulimwengu wa majini pepo na wa binadamu.
Sasa kutokana na ulimwengu huo kutokuwa na anga la kawaida usafiri wa aina hio ulihitajika.
Sasa kindege hicho kilijengwa maalumu kwa mtu mmoja moja na spidi yake kutokana na ukubwa ilihitaji angalu nishati za mbingu na ardhi kukidhibiti.
Sasa kutokana na kwamba akiwa mdogo wengi walikuwa wakimwita kibonge aliamua kuiita kindege chake hicho Chubi yaani kibonge.
Master Zao hakuwa na pingamizi na alitaka rafiki yake Master Chi kumsindikiza , hivyo wote watatu walipanda katika ndege hio ya Lanlan na kisha wakaondoka kuelekea ulimwengu wa binadamu.
Miaka kumi iliopita Aoiline na Sharif waliondoka pamoja , safari yao ilikuwa ni kutaka kuzijua zaidi siri za anga za mbali na kwanzia hapo ni kama kila kitu katika dunia kilikuwa chini ya Roma,
Kitu cha kwanza alichofanya mara baada ya kuwa Mwangalizi ilikuwa ni kuondoa ngoma katika mnara wa anga na kuwaruhusu majini pepo ambao walikuwa wakiishi katika ulimwengu wa majini pepo kuwa na uwezo wa kusaifiri kutoka na kurudi katika ulimwengu huo.
Binadamu walikuwa washajua tayari hawakuwa peke yao kama watawala wa dunia bali kulikuwa na viumbe wengine kama vile majini wa jamii zote tatu hivyo hawakuwa na woga tena.
Roma aliwaambia pia kulikuwa na viumbe wegine kutoka sayari ya Mars waliwahi kupata kufika duiani ambao hujiita miungu kama walivyosimuliwa katika hadithi za wagiriki na kwa mara ya kwanza dunia ilijua kwanini kulikuwa na uwepo wa hadithi hizo kumbe yote hayakutokea duniani bali ni sayari nyingine.
Sababu ya Roma kuwafanya binadamu kujua juu ya uwepo wa viumbe wengine ilikuwa ni kuwaandaa kisaikolojia kwa kuwambia kama hawatochukua hatua basi wataishia kuwa chini ya viumbe wengine,waliopo na ambao wanaweza kufika.
Alijua kama wataelewa muda wowote wanaweza kukumbwa na janga kama ambalo lilitaka kuwatokea basi watapiga hatua ya kujua namna ya kujilinda.
Chini ya utawala wa dunia wa Roma hakuna jini wala kiumbe chochote kilichotuhubutu kuleta fujo katika ulimwengu wa binadamu na hio ni kutokana na kwamba kulikuwa na sheria maalumu katika kila mpaka kati ya ulimwengu na ulimwengu.
Majjini pepo walibakia katika miliki yao ya kijini pepo lakini walikuwa na uwezo wa kufika katika ulimwengu wa binadamu , hivyo hivyo kwa binadamu walikuwa na uwezo pia wa kufika katika ulimwengu wa majini pepo na ikawa hivyo kwa majini watu.
Miliki za Hongmeng , Xia , Panas na Kekexil zilijengwa upya, majini waliokuwa wakiishi katika ulimwengu wa jangwa tenganifu na wenyewe walipewa ruhusa ya kutembelea katika ulimwengu wa majini watu , na binadamu.
Ndani ya muda mfupi ulimwengu wa binadamu ulibadilika mno na hatua za kimaendeleo ziliongezeka kwa kasi mno kuliko ilivyokuwa mwanzo,majini walikuwa na siri nyingi na siri hizo walishirikiana na binadamu na kufanya uelewa wa binadamu kuongezeka kwa haraka.
Hakukuwa na siri tena juu ya uwepo wa ulimwengu wa majini watu , wa majini pepo , binadamu walijua yote hayo.
Kwa sheria maalumu iliwawezesha binadamu kuamua kujifunza kanuni za mbingu na ardhi na hata kuchagua aidha aombe uraia wa miliki flani au abakie katika ulimwengu unaonekana.
Ki ufupi ni kwamba hata baraza la umoja wa kimataifa ambalo lilikuwa chini ya Clellia Allisanto lilitambua rasmi jamii za viumbe wasionekana na walipewa siti yao.
Mashulenni somo la kuvuna nishati za mbingu na ardhi kwa ajili ya kujikinga na magonjwa na kuishi muda mrefu liliingizwa katika mitaala ya mataifa mengi na msisitizo kuwekwa.
“Lanlan maamuzi ambayo baba yako alifanya wakati ule yalikuwa sahihi mno na inaonekana faida zake sasa hivi”
Aliongea Master Chi mara baada ya ndege hio kuingia katika ulimwengu wa binadamu na kuona baadhi ya binadamu ambao walikuwa na uwezo wa kupaa.
Binadamu walijikuta wakijua haikuwa na maana sana kutengeneza makombora kwa ajili ya kuuana wao kwa wao , yote waliona ni mambo batili na kupoteza rasilimali za dunia tu, ki ufupi ni kwamba binadamu aliufikia upeo mwingine kabisa.
Wale waliokuwa wakiamini katika Dini waliimarika sana kwani walitumia dini zao kuvuna nguvu za kiroho kupitia mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi.
Ki ufupi ni kwamba ulimwengu ulikuwa ni nusu Utopia , ijapokuwa matatizo hayakuwa yakikosekana baina ya watu lakini angalau amani ilikuwa kubwa zaidi kuliko mwanzo.

“Ndio , baba yangu ni shujaa , tatizo Bichwa kubwa anamwita mjinga”Aliongea na kuwafanya watu hao kucheka.
Dakika chache mbele ndege hio ilikuja kutua katika Visiwa vya wafu miliki inayotambulika kama ya Roma, haikuwa visiwa vya wafu tena bali ilikuwa ni kama taifa ambalo lilipewa jina kama miliki ya Roma.
Roma alionekana alikuwa akisubiria tayari na alikuwa nje amevalia mavazi yake ya rangi nyeupe upande wa shati na sandals za ngozi , kwa alivyokuwa akionekana utadhani sio baba mzazi kwa Lanlan , alikuwa akionekana kijana zaidi kuliko mwanzo.
“Master naona umekuja na Mzee
Zao?”Aliongea Roma huku akipitisha mkono wake kwenye shingo ya Master Chi.
“Hebu kuwa na maadili, ndio maana mtoto wako wa kiume anakwita mjinga”Aliongea Master Chi akijitoa kwa Roma na kumfanya Roma kumwangalia Lanlan ambae alikuwa akijifanyisha hajasikia chochote.
“Chubi , naona ulikuwa ukinichoma bila ya kujua tena?”
Ijapokuwa Lanlan hakuwa kibonge tena , Roma hakuona haja ya kubadilisha namna alivyokuwa anamwita.
“Lakini ndio Bichwa kubwa anavyokwita , usinilaumu mimi?”Aliongea Lanlan
“Inaonekana nakudekeza sana kama mama yako anavyosema , unadhani sijui mama yako Seventeen alikupatia zile bangiri , haya rudisha hapa ,hutakiwi kucheza na moto”
“Hapana , Mama Seventeen amesema ninaweza
kucheza nazo nitakavyo, ukizuchukua nitamwambia siku nyingine”
Roma midomo yake ilicheza mara baada ya kukumbuka namna tabia za Seventeen zilivyo wakati akiamka katika nafsi ya Edna.
“Master nina uwezo wa kuwadhibiti watoto
wengine lakini huyu kanishinda”Aliongea Roma
.
Upande wa Lanlan ambae alikuwa akicheka alitoa zile bangiri mbili na kisha aliziingizia nishati ya mbingu na ardhi na palepale zilibadilika na kuwa kama magurudumu yaliomvaa kiunoni na alianza kupaa kwenda angani.
“Aisee , ni mdogo mno lakini tayari ashapita
mapigo tisini na tisa ya radi ya
Zambarau…”Aliongea Master Zao.
“Mafanikio yake yanaridhisha , kati ya watoto wangu wote Lanlan ndio ambae ameoneysha uwezo mkubwa , Rusi amefanya vizuri pia na sasa ameingia levo ya nafsi siku chache zilizopita”
“Rusi yupo levo ya nafsi , lakini si ana umri wa miaka saba tu!!?”Aliongea Master Chi , alikuwa akiwajua watoto wote wa Roma kwani walikuwa wakimwita babu.
Furaha ya Roma haikujificha kwenye uso wake , lilikuwa jambo la kujivunia kama mzazi .
“Hivi huyo Rusi ndio mtoto wa kiume wa Rose sio ?”Aliuliza Zao.
“Ndio tofauti na wenzake yeye anapenda kuwa mwanajeshi , ijapokuwa hayupo vizuri kama Lanlan kiakili lakini anajuhudi kubwa na laiti
Lanlan angekuwa na nusu ya juhudi alizonazo Rusi angekuwa amepiga hatua kubwa , Lanlan tabia yake ya kupenda kula na maisha ya bata yanamrudisha nyuma”.
“Inatosha sasa , hebu ongoza njia nimechoshwa na majigambo yako”Aliongea Master Chi na kumfanya Roma kucheka.
Ijapokuwa uwezo wake ulikuwa umefikia hatua ya juu sana lakini aliweza kufanikisha kupata watoto kupitia kwa Edna , Rose na Clark lakini ajabu pia Amina na yeye alikuwa mjamzito.
Upande wa Edna yeye alipata watoto mapacha ambao hawafanani yaani ikiwa ni wa kike na wa kiume , Roma siku ambayo Edna alijifungua salama alifurahi mno kiasi kwamba alienda kushangilia juu angani kidogo tu agongane na Space station.
Miaka saba iliopita Rose alijifungua mtoto wa kiume huku Clark yeye akijifungua mtoto wa kike , ndani ya muda mfupi tu Roma alikuwa na watoto wakike watatu na wa kiume wawili na alikuwa akitegemea mmoja kutoka kwa Amina ambae mimba yake ilikuwa changa.
Wanawake wengine licha ya kuwa na wivu lakini walijitahidi sana kufanikisha uwezo wao ili na wao wapate watoto.
Lakini hata hivyo Roma hakuwa na haraka kwani walikuwa na muda mrefu wa kuishi.
Waliongea huku wakitembea na ndani ya muda mchache tu waliweza kufika katika bandari iliokuwa upande wa Kaskazini magharibi ya ksiiwa hicho kikubwa.
Upande huo ndio mahali ambapo familia yake ilikuwepo wakifurahia maisha pamoja na miungu wote.
Mara baada ya kumuona Roma ameongozana na wageni hao walisalimiana nae kwa ishara ya kirafiki.
Upande wa baharinni kulikuwa na chombo kikubwa mno chenye muonekano wa kimaajabu kilichofanana na UFO.
“Master Chi karibuni”Aliongea Edna ambae alikuwa amevalia gauni la chiffoni na aliwakaribisha Master Chi kwa heshima.
Ule ukauzu wa Edna ulikuwa ushampotea mara baada ya kujifungua watoto mapacha na umbo lake liliongezeka mno , ki ufupi alikuwa amenenepa japo hakupoteza mpangilio.
“Haha.. Edna kwanini naona kila mtu tayari yupo hapa , au hii ndio sherehe ya kuagana na ndugu zetu hawa”Aliongea Master Chi akicheka.
Aliuliza hivyo kwasababu wanawake wa Roma hawakuwa wakiishi tena kisiwani , alikuwa ni Edna tu mara nyingi ndio anakuwa yupo kisiwani na mume wake na kama wataonekana kisiwani ni nyakati za wikiend tu.
Clark yeye alikuwa maarufu sana katika sayansi hivyo licha ya kuwa na maabara katika Kisiwa hicho mara kwa mara alikuwa katika mataifa tofauti tofauti akifundisha katika vyuo vikuu.
Lakini licha ya wanawake hao kuwa mbalimbali watoto wa Roma wote walikuwa wakiishi na baba yao chini ya uangalizi wa Edna.
[emoji1635][emoji1635]
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

SEHEMU YA 799.
“Kila mtu amekuja kwasababu sio muda wa kuagana , kama ingekuwa hivyo wasingefika maana inahuzunisha”Alijibu Edna.
“Haha.. upo sawa”Aliunga mkono Master Zao. “Hey , Dionysus! Mbona unapoteza muda tena , hebu tuletee mvinyo uliotengeneza , Roma ni mbahili mno anatumia pombe ya bei chee kwenye hii sherehe”Aliongea Ares ambae ni kama vile anafoka , ilionekana hakuwa ameridhishwa na aina ya vinywaji ambayo vimeandaliwa na Roma.
“Unaongea upuuzi , huo ni mvinyo mzuri tu , kwa uwezo wako wa kuhimili kilevi ni kuingia hasara tu kama nitakupatia mvinyo wangu wa gharama kubwa”Aliongea Roma.
“Seriously , yaani muda si mrefu tunaondoka lakini bado unakuwa mbahili hivyo , Tsk tsk”Ares hakutaka kujisumbua kujibishana na Roma hivyo aliendelea kumuomba Zao mvyinyo ambao ametengeneza.
Mapema tu sherehe ilianza na kila mmoja alianza kuongea huku wakifurahia vinywaji na chakula.
Habari kuu zilizokuwa zikiongelewa ni juu ya kuondoka kwa miungu kwenda sayari nyingine.
Dionysus hakuwa tayari kuondoka na Athena pia, hivyo ni miungu nane tu ambao walikuwa wakiondoka.
Miaka tisa iliopita Clark alitoa pendekezo la ujenzi wa Spaceship ili miungu kutafuta sayari ambayo ina mazingira mazuri ya kufufua moyo wa Gaia.
Miungu walikubaliana na wazo la Clark , haikujalisha sayari ya Dunia ilikuwa nzuri kiasi gani lakini bado haikuwa ni sayari yao.
Pendekezo la Clark juu ya ujenzi wa Spaceship hio ilitokana na kioo Cha nafsi.
Moja ya kazi kubwa ya Kioo cha Nafsi ni kuwa na taarfa zote za anga za mbali na sayari zake na nyota zake.
Inasemekana kwamba kioo hicho kilikuwa na uwezo wa kuangalia sayari za mbali ambazo zipo miaka zaidi ya elfu moja ya mwanga.
Sasa kwa msaada wa kioo cha Nafsi Roma aliweza kugundua uwepo wa sayari nyingi sana ambazo zilikuwa na muonekano wa kimazingira unaofanana na dunia na sayari kubwa mara mbili ya dunia, aliweza hata kugundua baadhi ya uwezo wa miezi ambayo inasapoti maisha.
Haikuwa hivyo tu Roma aliweza kugundua vitu vingi sana kwa muda mchache sana kuhusiana na anga za mbali , aliweza kugundua baadhi ya uwepo wa viumbe wengine waliopo nje ya galaksi.
Sasa katika sayari zote ambazo aligundua moja wapo ya sayari iliokuwa karibu zaidi ndio ambayo ilikuwa na mazingira ya kusapoti maisha na haikuwa imetawaliwa , kwa maana ya kwamba haikuwa na viumbe wenye akili zaidi ya wanyama.
Roma yote hayo hakuwa na haja hata ya kusafiri kwenda anga za mbali , kwake ilikuwa ni kama anaoteshwa tu juu ya mazingira hayo kupitia msaada wa kioo.
Sasa ili kufika katika sayari hio ambayo aliona inawafaa ilihitajika tu usafiri wa kuelekea huko ambao ni SpaceShip huku kioo kikitumika kama ramani na kisha angekirudisha kioo hicho duniani.
Miungu wangeweza kufika katika sayari hio na kwa kupitia uwezo wao wangeweza kufufua Mti Mama na kuzaliana.
Bila shaka mawazo hayo hayakumjia Roma yeye mwenywe , ilikuwa kwake ni kama wazo ambalo liliwasilishwa na Mkuu wa enzi kupitia kioo hicho ndio maana alifanya maamuzi.
Ijapokuwa Roma alikuwa na uwezo wa kwenda anga za mbali kusalimiana na marafiki zake lakini bado aliona aandae sherehe ya kuwaaga kabisa , isitoshe mahali wanakoelekea ni mamia ya miaka ya mwanga.
Mamia ya miaka ya mwanga sio umbali mdogo , kwa teknolojia ya Roketi pengine ni zaidi ya miaka elfu moja mpaka kufika mwisho wa safari lakini kupitia teknolojia mpya yote hayo yaliwezekana kwenda umbali mrefu kwa muda mchache.
Mara baada ya kunywa na kula Venus(Aphrodite) alimsogelea Roma na kumpiga busu la shavuni na lipsi zake zilizopakwa rangi.
“Roma , don’t you have anything to say to me now that I’m leaving?”Aliongea Christen akimwambia Roma kwamba hana cha kumwambia wakati huo anataka kuondoka.
Muda huo Roma alikuwa akihangaika na steki ya nyama kwenye sahani na aliinua uso wake kumwangalia mrembo huyo kwa hali ya kusita.
“Ni kipi ninachoweza kukuambia sasa, Uwe na safari njema “
“Unadhani nataka kusikia hio kauli , unaonaje ukija chumbani kwangu usiku wa leo kabla ya kuondoka?”Aliongea huku akiweka mapozi ya kumtega Roma.
Kitendo hicho kilimfanya Roma homoni zake kuanza kuongezeka kwa kasi na aliishia kumeza mate akisita kutoa jibu la ombi kwa mrembo huyo.
“Wapi unataka kwenda usiku?”
Dakika hio hio Edna alikuwa ashasogea , ni kama alijua nini kinataka kutokea lakini licha ya hivyo alikuwa na tabasamu usoni.
“Wife hamna ninapoenda , alikuwa akimaanisha usiku anga ni la bluu sana hivyo kama tunaweza kutembea?”Roma alijibaraguza.
“Oh!, ndio hivyo?”Edna aliongea huku akipiga pafu laChampagne iliokuwa kwenye glasi yake na kumwangalia Christen kwa macho yaliojaa ukali.
“Athena nakuonea sana wivu”Aliongea Christen mara baada ya kumsogelea Athena na kisha akampita baada ya kuona ombi lake haliwezi kutimia.
“Halafu wewe hebu niambie , umelala wapi usiku wa jana , Rose alianiambia uliondoka hotelini kwake mepema tu”
“Nilienda kumwangalia Sophia na maandalizi yake ya Show”
Baada ya hali ya dunia kutulia Sophia alirudi katika maswala yake ya usanii na alikuwa maarufu mno karibia dunia nzima na kambi yake kubwa ilikuwa ni nchini Tanzania.
“Kama ulienda kwa Sophia kwanini ulirudi nguo zako zikitoa harufu ya perfume ya
Recho?”Aliuliza Edna huku macho yake ni kama yalikuwa yakiiangalia akili ya Roma. “Babe , umejuaje ni marashi ya Recho?”
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa amebadilika sana , katika kipindi cha muda mfupi alikuwa na wanawake ambao hawakuwa wakifahamika mmoja wapo alikuwa ni Recho , Benadetha na Nadia.
Wanawake hao hawakuwa na haja kubwa ya kutambulika kama mahawala wa Roma na waliendelea kufanya kazi katika kampuni ya Vexto, kwa Recho ambae alishaolewa na kuachika hakupenda tena kuwa na mwanaume na alifurahia kuchepuka na Roma ambae alikuwa akimpatia vitu vingi ikiwemo vidonge na mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi , upande wa Benadetha ilikuwa hivyo , Nadia yeye japo hakuridhika na kuwa mchepuko wa siri lakini kutokana na mapenzi makubwa aliokuwa nayo kwa Roma aliona angalau inatosha , taasisi yake binafsi ya kisheria ilikuwa ikifanya kazi kubwa sana na alikuwa na mikataba na kampuni kubwa katika usimamizi wa maswala ya kisheria ikiwemo kampuni ya Vexto na Kanani.
“Unadhani nilimpatia zawadi ya marashi ambayo hakuna anaeyatumia bila sababu ?”Roma alijikuta sura ikimshituka kumbe ulikuwa mtego.
“Edna Darling , nimekukubali kuja na mbinu hio, I’m so impressed”
“Fanya mambo yako ukidhania sijui , najua unachokifanya na Mkurugenzi wa tawi langu nchini Japani Tannya , na juzi tu ulikuwa na Lilith ….”
Roma hakutaka kumsikiliza tena zaidi ya kumziba mdomo .
“Nakuomba mke wangu , tafadhari acha kuongea tena juu ya haya maswala , kwanini usinifungie kama adhabu , sitokudanganya tena, nimekosa mimi Babe”
“Najua tabia yako ya kuuchezea mwili wangu wakati Seventeen na Athena wakijitokeza wakati nikiwa nimepumzika , ijapokuwa hawawezi kukudhibiti lakini naona kila kitu katika fahamu zao”
“Nimeelewa , nimeelewa mke.. najua nafsi zote tatu ndani yako ni kitu kimoja”
Edna ndio aliekuwa mtawala kamili wa nafsi tatu lakini kuna muda mwingine akichoka ni kama nafsi hizo huamka kwa wakati wake, katika kipindi chote aligundua akili yake inapata utulivu kama atawaacha Seventeen na Athena kuutumia mwili wake hivyo ndio maana akitaka kupumzika anaizima nafsi yake.
Sasa upande wa Roma alikuwa akitumia fursa wakati nafsi hizo zikiwa zimeamka kufanya yale ambayo Edna hayapendi , sio kwamba hakupenda kufanya na Edna lakini ukweli ni kwamba Roma alikuwa akimhofia zaidi Edna kuliko hata Athena na Seventeen , pengine ni kutokana na upekee wake.
Roma alifurahia siku ambazo nafsi hizo zikuwa zinafanya kazi kwani maisha ni ya amani lakini hata hivyo kuna muda alipatwa na mawazo kwani tabia ya Seventeen ilikuwa tofauti kabisa na ya Edna.
Seventeen akiamka atampa Lanlan kila anachotaka , hata bangiri zile za ulinzi Lanlan alipewa na Seventeen , ki ufupi ni Seventeen aliemfanya Lanlan kupenda kula bata kuliko kitu chochote na hakujali matokeo ya tabia yake kwa Lanlan ili mradi impe furaha.
Upande wa Athena yeye nafsi yake iliongoza kwa kuwa na aibu na Roma akimuona mwanamke huyo ameamka anamtoa nje kwani wakati wa kale machezo akifika kileleni lazima kutokee tetemeko kiasi cha kumfanya Roma aogope nyumba yake itaporomoka.
Upande wa Edna alirudi kikamilifu kwenye biashara zake na alifufua ndoto yake ya kuifanya kampuni ya mavazi kuwa kubwa mno na swala hili liloimfanya kufanya biashara mpaka na miliki za majini ya Kibra na Panas.
Ki ufupi alipenda kufanya kazi sana na kumfanya kutokuwa karibu zaidi na Roma ndio maana ilimpa nafasi Roma ya kuwatembelea wanawake zake.
Lakini licha ya hivyo alikuwa na mbinu zake za kumfatilia kila mahali bila hata yeye mwenyewe kujua.
Muda huo wakati Edna anataka kumchimba
Roma juu ya tabia yake alibadilika palepale mara baada ya kuona msichana wa miaka saba alievalia gauni akisogea maeneo hayo huku akiwa ameshikilia boksi la vikeki.
“Nyromi wewe mtoto , kwanini unakula keki zangu , haya tema haraka , tema”
Nyromi , Naomi au Nyomi ni jina la kiebrania ambalo Roma alichagua kumpatia binti yake sababu kubwa ni kutokana na Naomi kufanana kila kitu na Edna haikuwa muonekano tu bali mpaka tabia na hisia alizokuwa akipata akimwangalia biti yake huyo ndio sababu ya kuja na jina hilo.
Kulingaa na Bi Wema ambae alishuhudia ukuaji wa Edna anasema kama Naomi angezaliwa miaka ishirini iliopita basi kusingekuwa na ubishi wa kuwa pacha wa Edna, ki ufupi ni kwamba Edna alijipiga kopi tu na kumleta Naomi Duniani.
Wote walifanana katika vyakula wanavyopenda na kufanya muda mwingi kugombana, kwani Edna akinunua keki zake anakuta zimeliwa zote.
Jambo hilo lilifanya watu wengi kucheka mno ugomvi unapotokea kutokana na tabia zao.
Dakika ambayo Naomi alijua tayari ameshakamatwa alichukua keki iliobakia kwenye kiboksi na kuibugia yote mdomoni bila ya kujali mdomo ulikuwa mdogo.
“Si nilikupatia za kwako , kwanini unakula na zangu , unatafuta kupigwa mbele ya wageni?”Licha ya kufoka kwake Naomi ambae ni kama sasa amefanya jambo la kujivunia alimwangalia mama yake kwa macho ya kijasiri.
“Mama.. mama anatia aibu kugombania chakula na mtoto..”
“Wewe..”Edna alikuwa na hasira na alimsogelea Naomi na kumfinya shavu.
“Haya tema , tema nakuzuia kumeza , tema..”Licha ya kushikilia shavu Naomi alionyesha ukiburi wake na kukataa kutema na kufanya wageni kucheka.
Tabia zao zilimfanya Blandina kama mama mkwe kuona aibu mbele ya mjukuu wake na mke mwana.
“Wifey .. usiwe na hasira hivyo , nitakununulia vingine , Nyromi ni mtoto ambae haelewi kitu lakini vilevile ni binti yako…”
“Kwahio akiwa binti yangu ndio anifanyie hivi?”
“Ndio kama mama yao ni wa kawaida”Roma aliwaza lakini hata hivyo aliamua kumaliza hali hio.
“Unaonaje kama nikimuadhibu na mazoezi ya masaa mawili , Wife punguza jazba ashazimaliza zote hata hivyo”
Wakati wakiendelea kuongea kumaliza hali hio mtoto mdogo wa kiumbe alievalia suti ya ugoro na tai nyekundu juu ya shati jeupe aliishia kutingisha kichwa huku akiendelea kula chakula kwa uma.
“Aunt Clark .. naona kabisa kama sisi wawili tusingekuwa sehemu ya hii familia , ukiunganisha IQ zao matokeo yatakuwa ni hasi .. Baba anafikiria na kichwa cha chini, mama na dada mbele ya vijikeki wanakuwa wajinga ..moyo wangu unauma nikiwaangalia na inanipa changamoto kuona namna nilivyo na majukumu makubwa”
Maneno aliokuwa akiongea huyo mtoto hayakulingana na umri wake,ijapokuwa alikuwa mzuri wa sura na mpole lakini alikuwa akiongea kama mtu mzima.
Alikuwa amevalia miwani kubwa ambayo haikuwa na kioo , yote hayo ilikuwa ni kwa ajili ya maonyesho tu.
Huyo alikuwa ni pacha wake Naomi afahamikae kwa jina la Rube au Rubchen jina la kijerumani ambalo lilimaanisha kichwa kikubwa.
Sababu za Roma kumwita Kichwa kikubwa ni kutokana na kwamba alionyesha dalili ya kuwa Jiniasi tokea akiwa na mwezi mmoja tu.
Tokea apate ufahamu wa kujitegemea Rube hajawahi kupenda kukaa karibu na Roma wala mama yake , muda wote alikuwa karibu na Clark ambae alipenda kujifunza vitu vingi kutoka kwake na hakuchagua cha kujifunza , iwe ni mambo ya anga , bailojia au Jiografia alijifunza kwa spidi kubwa mno.
Clark alikuwa akimpenda sana Rube kutokana na akili yake yenye uwezo wa ajabu na alimfundisha kwa moyo wote huku akitegemea makubwa kutoka kwake , lakini upande wa Roma ilimpa mawazo.
Rube ndio mtoto wake wa kwanza lakini licha ya hivyo hakuonyesha kumpenda kabisa na kumuona yeye hana akili na Clark pekee ndio ambae aliona ni mtu wa kufatishana nae.
Ijapokuwa Rube alijua baba yake ni mtu mwenye uwezo mkubwa na nguvu lakini hakukubali uwezo wake , yeye aliamini katika maswala ya sayansi pekee na mambo ya kuvuna nishati kwake hayakuwa kipaumbele na aliona ni ujinga.
Roma alijaribu kumtaka Rube kujifunza namna ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi lakini alikataa na mwishoni aliamua kumwacha afanya anavyotaka.
Katika ujenzi wa Spaceship Naira kutoka idara ya sayansi ya Zeros alitoa mchango wa teknolojia mpya ya injini lakini mara baada ya utafiti wake kufanyiwa uchambuzi na Rubeni kulionekana kuna mapungufu mengi na yote yalizibwa na mtoto huyo , hivyo kwa lugha nyepesi ni kama injini ya Spaceship ilitengenezwa kwa mchango wa Rube.
“Upo sahihi Rube , muda mwingine naona kama vile nimekuzaa mimi na kuna namna baba yako alifanya miujiza yake na ukazaliwa na Sister Edna”Aliongea Clark alievalia koti la maabara.
“Hata wewe umeona , mimi mwenyewe najiuliza kwanini kuna utofauti mkubwa wa IQ na Naomi?”Aliongea Rube.
Lakini muda huo msichana mdogo ambae alikuwa akila Ice Cream pembeni alionekana kutofurahiswa na Clark .
“Am I not your Daughter ?Do you not want me anymore?”Aliuliza msichana ambae alikuwa na muonekano kamili wa kizungu.
Alikuwa na nywele nyingi mno za rangi nyeusi na macho yake ya Bluu , alikuwa ndio mtoto mdogo zaidi wa kike ambae amezaliwa na Clark , kitu pekee ambacho pengine Roma aliona amerithi ni Komwe la Ashley, ki ufupi ni kwamba rangi na macho alirithi kwa Clark lakini sura yake alikuwa akifanana mno na Ashley mdogo wake Roma.
Binti huyo alifahamika kwa jina la Dami na hio ni kutokana na namna ambavyo alionekana wakati akiwa mdogo , Dami alikuwa na mashavu yaliotuna kama Andazi ndio maana Roma akaibuka na hilo jina.
Clark mara baada ya kuona binti yake anavyotia huruma aliishia kucheka na kumpakata huku akimchokoza kwa kufinya mashavu yake.
“Kwaninni nisikutake tena , wakati unaonekana mzuri hivi , unajua kuimba na kucheza na pia unaweza kunichora bila ya kunikosea , kaka yako Rube anajaribu kutania tu”Aliongea kwa kumbeleza na Rube alitingisha kichwa kukubaliana na Clark kumtuliza msichana huyo mdogo ambae alionekana kutaka kulia.
Dami licha ya kwamba mama yake alikuwa mwanasayansi mkubwa lakini yeye hakupenda kabisa maswala ya sayansi , alipenda mno sanaa kuliko kitu chochote kile.
Alipenda kuimba , kucheza na kuchora , alikuwa na uwezo wa kuchora kitu bila ya kukikosea kwa kuona mara moja tu na pia alikuwa na uwezo wa kuigiza namna ya kuimba na kucheza kwa kujifunza mara chache sana.
Dami ndio ambae alionekana kuwa mpole kuliko wote , ijapokuwa alionekana kama ana uwezo mdogo wa kuchanganua sentensi zenye zaidi ya maana lakini alionekana atakuja kuwa mwanasanaa mkubwa sana.
Clark hakutaka kumlazimisha binti yake kufanya kile anachokifanya , hata hivyo aliridhika na kile ambacho kinaonyeshwa na Rube.
Kinachofurahisha zaidi Dami ni namna ambavyo ana ukaribu mkubwa na Lanlan , walikuwa wanapendana mno pengine ni kutokan na wote wawili kupenda kula na maisha yao kutojali sana vitu vingi.
Dakika chache wakati stori zikiendeea Lanlan aliweza kufika huku akiita kwa nguvu jina la baba yake .
“Dad , Dad , Dad , I want to eat sashimi”
“Sister Lanlan!!”Dami furaha yake yote ilichipua mara baada ya kumuona Lanlan ambae ameshikilia Samaki mkubwa aina ya Tuna(Jodari).
“Dami hii ni zawadi yako”Aliongea Lanlan huku akitoa Kombe(conch) kutoka katika hifadhi yake ya pete na kumpatia mdogo wake, aina hio ya kombe huweza kutumika kutengenezea mziki kwa kupuliza.
“You are the best Sister Lanlan”Kaliongea kwa furaha huku kakiruka ruka wakati huo Edna ni kama ameamka sasa kwani muonekano wake ulibadilika, kitendo cha kumuona Lanlan akiwa na samaki wa aina hio alijua fika Lanlan anaendeleza tabia yake ya kuzama baharini kwenye kina kirefu cha maji.
“Lanlan mbona huchoki kusababisha matatizo , mara ya mwisho Rusi alikuambia umpitishe kwenye Dhiki ya radi ya zambarau kwa kumshambulia nayo na kweli ukafanya hivyo , kama isingekuwa kwa Dhana alizokuwa nazo , mdogo wako angekuwa ashafariki”Alifoka Edna.
“Sikufanya makusudi , na sitofanya tena”Lanlan aliishia kuinamisha kichwa chake chini.
Hakutaka habari hio izungumziwe kabisa , kwani mara baada ya tukio hilo alipatwa na hofu kubwa kwa namna ambavyo Rusi alikuwa ameunguzwa na radi hio.
Kitendo hicho kilimfanya Rose kufoka mno na Edna alimpiga Lanlan mpaka akalia , hata Roma ambae alikuwepo hakuingilia kabisa.
Ndio hivyo tu walikuwa ni familia na Rusi alijua sio makosa ya Lanlan peke yake , yeye ndio ambae alikuwa na shauku ya kuona namna Dhiki ya radi ilivyokuwa na Lanlan hakuona mbaya kumuonjesha mdogo wake.
“Inatosha sasa Edna , hilo swala lishapita na Rusi ashapona , haina haja ya kuendelea kumfokea nalo Lanlan”
“Sio kosa la Sister Lanlan , ni kwasababu sikumsikiliza baba na kuwa na wasiwasi juu ya kupanda levo ndio maana nikapata shauku”
Rose alimpatia mwanae jina la Rusi kama mbadala wa neno Utulivu , kutokana na changamoto alizopitia katika maisha yake kukutana na Roma ilikuwa mwanzo wa utulivu ndio maana kuweka kumbukumbu sawa akaamua kumwita mtoto wake Rusi yaani Utuliivu , Rusi ni msemo katika lugha ya Bengali huko Bangladesh.
Katika watoto wote wa Roma, Rusi ndio ambae alikuwa na ndoto za kumfikia baba yake katika mafunzo ya nishati ya mbingu na Ardhi , angefanya chochote kile ili mradi kiwe kinahusiana na maswala ya kuvuna nishati. Lakini licha ya ya umakinni wake mkubwa spidi yake ya kupanda levo haikuwa kama ya Lanlani na swala hilo lilimpa mawazo na hata kutamani kutafuta njia ya mkato.
“Inatosha sasa , leo ni siku ya furaha utamfunza vizuri muda mwigine , halafu Lanlan ni mtoto wetu wa kwanza kwanini unakuwa mkali sana kwake hivyo?”
“Ushasema ni mtoto wa kwanza ndio maana nakuwa mkali , nisipokuwa mkali utamharibu kwa kupenda kumdekeza “Aliongea Edna.
Roma aliishia kunyamaza na kisha alimkonyeza Lanlan na Dami kumfuata nyuma wakamtengeneze samaki na Lanlan alimpa ishara na Rusi na wote walimkimbhilia baba yao.
Baada ya kuona watoto hao wanamfatisha Roma Edna aliishia kuangaliana na Rose na kuishia kutabasamu.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kizazi cha Roma mara baada ya kuwa mwangalizi , ijapokuwa kwake alikuwa akichukulia familia yake kama familia nyingine lakini watoto wake walikuwa wakiangaliwa kwa jicho pekee mno , ni kama dunia ilikuwa ikisubiria kuona ni namna gani kizazi hicho kitabadilisha maendeleo ya binadamu kwa haraka.
Isitoshe Mpango LADO haukuwa kumfanya Roma kuwa na nguvu tu na kuweza kuwa na nguvu ya kuwashinda miungu bali pia kizazi chao ilikuwa ni sehemu ya mipango hio.
Na kama ilivyotarajjiwa , licha ya kwamba watoto hao walikuwa na hobi tofauti tofauti lakini mustakabali wa maisha yao ulikuwa ukisubiriwa na msisimko mkubwa na hasa hasa macho yalikuwa kwa Rubcheni ambae muda wote aliambatana na Clark na hata kuvumbua teknolojia mpya ya injini ya Spaceship.
Moja ya watu waliokuwa wakitamani kufanya kazi na watoto wa Roma ni Naira Mkurugenzi wa kitengo cha sayansi cha dunia cha Zeros.
Miaka kumi iliopita makao makuu ya kitafiti ya
Zeros yaliondolewa kutoka katika umoja wa Zeros organisation ambao ulivunjwa na kuingizwa kama kitengo maalumu cha maswala ya kitafiti kinachodhibitiwa na umoja wa Mataifa.
Naira ambae ndio aliekuwa mwanasayansi kinara wa taasisi hio alipewa ukurugenzi kamili wa kuendesha taasisi hio na makao hayo makuu hayakuwa siri tena, ijapokuwa hayo yote yalifanyika chini ya mapendekezo ya Roma kama njia ya kuboresha usalama wa dunia lakini hakutaka kuingilia moja kwa moja maswala ya kibinadamu.
Majukumu ya Roma kama mwangalizi hayakuwa kufuatilia binadamu wanafanya nini bali ni kuzuia majaribio yota hatari ambayo yanaweza kupelekea dunia kutokuwa salama, hivyo hata maswala ya jamii za siri hakujihusisha kabisa na aliacha ziendelee kama ilivyokuwa mwanzo.
Naira aliweza kukutana na Dorisi na ilikuwa ni furaha kwa wawili hao kukutana na kumfanya Dorisi sasa kujihisi amepata ndugu , ijapokuwa kukutana kwa Dorisi ndio ilikuwa mwanzo wa kujua sababu ya vifo vya wazazi wake lakini kwa namna moja ama nyingine alifurahi aliweza kufuta ule mkanganyiko aliokuwa nao muda mrefu.

SEHEMU YA 800.
Mwezi mmoja baadae hatimae miungu iliacha dunia na kuelekea sayari nyingine kupitia Spaceship , tukio ambalo lilishuhudiwa na dunia nzima huku pongezi zikienda kwa Clark , Naira na Rubeni wafanikishaji wa teknolojia hio.
Upande wa Roma hakuwa na majuto ya kuagana na marafiki zake , licha ya macho makali ya Edna ya kumfatilia , Roma alifanikisha kwenda kuweka kumbukumbu nzuri na Christen, lakini haikujalisha alikuwa makini namna gani lakini Edna aliweza kujua kupitia uungu wa Athena na kumfanya Roma wiki nzima kumbembeleza mke wake amsamehe kwa magoti.
Hatimae wanawake wote wa Roma walirudi katika majukumu yao ya kimaisha kwa kuondoka kisiwani wakimuacha Edna pekee katika Ngome.
Roma pekee ndio mtu ambae hakuwa na kazi rasmi ya kufanya lakini hio haikumaanisha kwamba alikuwa amekaa kizembezembe.
Ukiachana na kufuatilia kwa ukaribu ukuaji wa watoto wake na elimu zao lakini pia alisafiri kila kona ya dunia kuangalia maendeleo ya sayari yalivyo.
Ukweli kitendo cha kuwaruhusu binadamu kuvuna nishati za mbingu na ardhi ni kama ilimuongezea jukumu lingine la kuhakikisha hakuna ambao wanatumia mbinu hizo kufanya uharifu., hivyo akiona wale ambao wanataka kudhuru binadamu kwa namna yoyote ile alikuwa akiwaua.
Kuhusu kulinda anga na matishio ya mbali kioo ndio kilikuwa kama darubini yake angani ya kumjuza , ukweli ni kwamba kazi yake haikuwa ngumu sana kama ilivyokuwa kwa Sharif ambae hakuwa na Dhana hio.
Hakutafuta pia mrithi kama Sharif alivyofanya bali yeye aliona ana miaka mingi ya kuishi na bado ni kijana hivyo swala hilo atalifanya baadae.
Neema licha ya kuzidi kutajirika kwa kufanya biashara ya Vidonge lakini vilevile aliweza kuitwa bibi baada ya Donyi kujifungua mtoto na Kassimu , jambo hilo lilimfanya kuwa na mawazo, lakini hata hivyo alikuwa na furaha kwa ajili ya binti yake.
Magdalena alipandishwa cheo na kuwa
Kamanda mkuu wa kitengo cha Wachawi nchini Tanzania na alikuwa ndio msimamizi wa maswala yote yanayohusiana ulimwengu unaonekana na ule usioonekana.
Mage yeye aliingizwa katika kitengo cha usalama wa taifa kama mkuu wa idara ya sera za kigeni hivyo alifanya kazi karibu zaidi na raisi.
Upande wa Afande Tobwe alipandishwa cheo na kuwa katibu mkuu wa wizara ya ulinzi huku Afande Maeda yeye aliteuliwa na kuwa mkuu wa majeshi.
Najma ambae mwanzoni alitaka kuwa mwanasiasa aliachana na maswala hayo na alifanywa mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya kimisaada ya Blandina Foundation ambayo iliingia katika maswala ya ushirikiano na taasisi ya Edna Foundation iliokuwa chini ya Suzzane, hivyo ilimfanya Najma muda mwingi kusafiri akiwa na Blandina.
Janga ambalo lilitokea miaka iliopita lilifanya watoto yatima kuwa wengi hivyo ni kama kazi ya watoto waliohitaji misaada iliongezeka.
Athena kupitia mwili wa Edna aliweza kumpatia Dorisi robo ya kiasi cha hela zote alizokuwa nazo pamoja na Naira na kiasi kilichobakia kiliingizwa katika mfuko wa maendeleo ya jamii dunia nzima.
Nasra alijiunga na benki ya dunia kama makamu wa raisi Afrika ya mashariki na kusini na Dorisi aliendeleza biashara za wazazi wake kwa mtaji aliokuwa nao , biashara ya uchimbaji wa madini ,biashara hio ilimfanya Dorisi kusafiri mpaka katika ulimwengu wa majini kwa ajili ya kukusanya madini.
Rufi na Amina waliungana pamoja na kufungua kampunni ya mawasiliano, wakati huo Amina alikuwa akitambulika kama sehemu ya majini wa Mbweha katika miliki ya Braki na alifika na kutambulishwa kabisa, ijapokuwa haikuwa na umuhimu sana lakini ilifanyika hivyo ili wanamiliki hao kujiweka karibu na Roma.
Upande wa Rufi yeye licha ya kufanya kazi katika kampuni lakini kupitia mwili wake ulivyokuwa alifanikiwa kupanda levo kwa haraka sana na kuwapita Rose , Clark na wengine wote kasoro Edna tu ambae alikuwa na uungu wa Athena jambo ambalo lilimshangaza sana Roma.
Yezi alirudi Korea na kupewa urithi wake na kuanzisha vyuo binafsi vinavyofudisha namna ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi, ndani ya muda mchache tu kwa kuchanganya na urithi aliopata aliweza kuwa tajiri mwenye pesa nyingi mwanamke katika bara la Asia, aliweza hata kumpita Edna likija swala zima la utajiri.
Mataifa mengi ya Afrika yaliingia katika hatua nyingine kabisa ya kimaendeleo na moja ya mataifa yaliopiga hatua kwa haraka ni Tanzania, Raisi Senga kwa kupitia ushawishi wake aliweza kubadilisha katiba , ambayo ilimpa nafasi ya kugombea uraisi mara nne.
Kutokana na kukubalika kwake na sapoti kubwa kwa familia aliweza kushinda kila awamu hivyo kuwa raisi wa kwanza nchini Tanzania kutawala muda mrefu zaidi ya miaka kumi.
Raisi Jeremy upande wake kwa kushirikiana na majini wa Paasi waliofanikiwa kukimbia alianza kujenga upya miliki hio na miliki nyingine hazikumwingilia sana kutokana na kwamba walihofia Roma anaweza kuingilia kati kutokana na mke wake kuwa na uhusiano na Jeremy.
Upande wa Afande Kweka maisha yake yalikuwa ni yale ya kizee , kucheza na wajukuu , hakujutia kwa maamuzi yake yote alioyafanya miaka mingi iliopita kumhusisha Roma(Denisi) katika mpango LADO, aliona alifanya maamuzi sahihi kabisa hasa kwa kwa kuwa na vitukuu wengi namna hio wenye akili kubwa.
Upande wa Omari aliteuliwa kama raisi wa chama cha wavuna nishati za mbingu na ardhi duniani na hio yote ni kutokaa na kupata sapoti kubwa kwa Roma , wale ambao waliona hafai walinyamaza wakimhofia Roma.
Ukweli ni kwamba uwezo wake haukuwa mkubwa sana , Omari alikuwa amepitwa hata na Lanlan ki uwezo lakini licha ya hivyo Roma aliamini huko mbeleni atakuja kuimarika nakushawishi kila mmoja kuwa raisi wa ushirika wake.
Upande wa XioXiao alikuwa akifika mara kwa mara kisiwani kwa Roma , ijapokuwa mara zote alifika kwa kisingizio cha kutaka kucheza na Lanlan pamoja na kuvuna nishati pamoja lakini alikuwa akitafuta nafasi kumtega Roma , alijua fika Roma ni mwanaume tu na siku moja lazima ataingia kwenye mtego wake.
Lakini hata hivyo alikuwa na furaha , mama yake alikuwa akiishi na baba yake na walikuwa wameirudisha miliki yao kama ilivyokuwa mwanzo japo sio kwa asilimia mia moja.
Roma alijua fika mipango ya Xiao Xiao lakini kutokana na kumhofia mke wake hakufanya lolote.
Wale wanafunzi wa Sharif , yaani Mzee Yasu na
Xumei wenyewe walipotea kusikojulikana na Roma hakujisumbua kuwatafuta akijua lazima wameenda kujichimbia kwa ajili ya kuelewa namna ya kufikia levo ya mapigo elfu kumi ya radi, ni Shekhe Idriss tu ambae alikuwa ndio kiongozi wa umoja wa Ant-Iluminat mara baada ya kutawazwa rasmi na Edna ambae alikuwa akitegemewa kama kiongozi, ijapokuwa sera zilikuwa zimebadilika lakini walikuwa ndio wamiliki wakubwa wa Project Binamu Island.
Dunia ilirudi katika hali yake ya Amani kabisa na maisha yakaendelea na ilikuwa ni kama hakuna kilichotokea,
Umoja wa kimataifa ulitangaza Safina ambayo ilikuwa ikijengwa huko Ethiopia kukamilishwa na kisha kufungwa injini zilizotumika katika Spaceship ya miungu na kisha kutumwa anga za mbali kwa ajili ya utafiti na kupitia taasisi ya Zeros hilo lilifanikiwa kwa asilimia mia moja.
Serikali ya Tanzania ilimpatia Roma kisiwa cha Mbudya kama zawadi kwa ajili ya ujenzi wa makazi.
Edna kupitia kampuni yake ya ujenzi alijenga hekalu la kifahari la kutosha familia yote ya Roma na ilikuwa ni sehemu maalumu kwa ajili ya mapumziko yao ya mara kwa mara , japo hawakuishi hapo moja kwa moja.
Roma alihakikisha watoto wake wanasoma katika shule moja ili wasitengane kutokana na kuzaliwa na mama tofauti tofauti , lakini pia aliwaacha kusoma katika shule zenye mchangayiko wa wanafunzi wengine wa kawaida ili kushirikiana na jamii.
Maimuna aliweza kurudi na kusimamia biashara za ukoo wake baada ya Tannya kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Vexto tawi la Japani.
****
Ilikuwa ni siku ya tatu yaani tarehe nne baada ya Mwaka mpya, mwanga wa jua uliingia kupitia dirisha na kuyagusa mashavu ya Roma na kumfanya atoke usingizini.
Roma alinyoosha mkono wake bila ya kufumbua macho yake akijaribu kumtafuta Edna na aligundua ashaamka tayari na ilimfanya kuangalia saa na kuona ni saa kumi na mbili na nusu.
“Huyu mwanamke hajui kabisa kuinjoi maisha, ukute ashaenda kazini tayari”Aliwaza Roma.
Aliondoa blanketi na kushuka chini akiwa hana nguo yoyote mwilini , usiku wa jana alicheza na mke wake mpaka usiku wa manane na kuishia kulala akiwa amemkumbatiaa bila ya kuoga.
Roma alivaa boksa tu na kisha alitoka chumbani na kuegamia kwenye uzio akiangalia chini sebuleni.
“Lanlan kula hizi tambi , nimekutengenezea kwa ajili yako , ni tamu sana”Aliongea Bi Wema ambae alikuwa amevalia Apron.
Lanlan mara baada ya kuwekewa sahani hio yenye tambi hakutaka kupoteza muda maana alikuwa ashameza mate vya kutosha.
“Bi Wema unamdekeza sana Lanlan kwa kumpa kila anachotaka , halafu tena sasa hivi ni asubuhi”Bi Wema hakujali maneno ya Edna kabisa huku akiwaangalia watoto wakila chakula kwa furaha.
Edna aliishia kutoa pumzi na kumgeukia Rube ambae alikataa kula tambi alizowekewa na Bi
Wema.
“Rube is the best , he knows how to follow a balanced diet and only eat eggs and drink milk in the morning”Aliongea Edna akimshika kichwa Rube ambae ameshikilia kikombe cha maziwa.
“Ni kwasababu kama mtu akila na akashiba kabisa tena ikiwa ni asubuhi anasababisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuhitaji kiasi kikubwa cha damu hivyo kufanya ubongo kuchoka haraka , Mimi kama mwanasayansi mkubwa ambae dunia inanitegemea , siwezi kukifanya kichwa changu kiathiriwe na chakula”
“Also Mother, can yoo stop touching my head , I am not a kid anymore”Aliongea Rube huku akimwangalia Edna akimaanisha hataki kuguswa kichwa kwani sio mtoto.
Tabasamu ambalo lilikuwa katika uso wa Roma lilipotea na kujiambia huyu mtoto anamaanisha nini lakini hata hivyo aliondoa mkono wake kiabu aibu.
“Unaongea ujinga gani Rube , kwahio wewe ni mtu mzima kama sio mtoto?”Aliongea Edna lakini hata hivyo aliishia kugeuzia macho yake kwa pacha yake Rube yaani Nyromi na kumwangalia namna ambavyo alikuwa akinywa chai kimapozi kama vile ni Princess.
“Naomi! Why are still eating so slowly ? you will be late for school”Aliongea Edna lakini Naomi alitingisha kichwa.
“Mom , you told me to be a lady! A lady should not gobble down food or else I will look rude..”Aliongea kimapozi kwa jinsi alivyo ilionyesha atakuja kusumbua sana mbeleni kwa maringo.
“Mh , unajifanyisha mtiifu lakini mbona hukuwa hivyo wakati ukila keki zangu , hebu muone.. na ole wako nilete zigine uniibie”Aliongea lakini Naomi aliishia kumtolea Edna mdomo.
“Bi Wema hebu kaangalie haka katoto , kwanini kazaliwa kuwa adui yangu , kwanini ananifanyia hivyo asubuhi yote hii , akikua je , mimi nafanya nini?”
Bi Wema aliishia kutabasamu tu na aliishia kutingisha kichwa bila ya kumuunga mkono Edna.
Hata hivyo alikuwa ashazoea na tabia za hao wawili , Naomi yeye alikuwa tofauti kabisa na dada yake Lanlan ambae alikuwa akipenda kujali mambo yake lakini Naomi atahakikisha anafanya kila kitu kumkasirisha Edna.
“Haha…”
Roma ambae alikuwa amesimama floor ya juu akiangalia kinachoendelea alishindwa kujizuia na kucheka na kumfanya Edna ainue macho yake na kumwangalia kwa ukali.
“Unacheka nini , vaa nguo zako kama umeamka , unadhani unaonekana vizuri ukiwa na hio boksa tu?”
Roma aliishia kutingisha kichwa kwa haraka huku akimnyooshea kidole gumba Naomi .
Roma hakuwa na haraka , mara baada ya kurudi chumbani aliingia kwenye jakuzi na kufurahia maji ya moto na mpaka anakuja kutoka Bi
Wema alishaondoka kupeleka watoto shule.
Ukweli ni kwamba alikuwa akishinda huko huko maana Roma akili za watoto wake alikuwa akizijua hivyo hakutaka watoroke.
“Honey , hivi unadhani Naomi atasumbua sana akishangia katika ule umri .. kulea sio kazi rahisi , mwenyewe hapa nikimfikiria Rube kichwa kinauma .. yaani kila siku atakimbilia kwenye maabara ya Clark utadhani ndio mama yake ,mpaka najiuliza isije ikawa Clark anampa madawa , inakuwaje kuwa na mtoto aina yake ,,, Hey! unafanya nini?”Edna kabla hata hajamaliza kulalamika alijikuta akibebwa juu juu na Roma.
“Hubby naomba tuache..nataka kwenda kazini”
“Babe Edna wewe ndio umekosea, nani kakuambia uanze kulalamika kuhusu watoto asubuhi yote hii , mimi niliona namna ambavyo unafurahisha kama mama nakujikuta nikitamani mtoto mwingine”
“Ah … basi nitaacha , acha kwanza niende kazini
, unajua leo tunapaswa kwenda kuandaa mazingira kwa ajili ya harusi ya Ashley… napaswa kuandaa zawadi…”
“Ushachelewa.. zawadi tutafuta wote…”Edna alijitahidi kujitetea lakini haikuleta maana tena.
“Basi tufanye kwa nusu saa tu .. usizidishe baada ya hapo ?”
“Unaonaje dakika arobaini..”
“Hapana , nusu saa tu”
Roma aliishia kusugua mano yake na kujiambia vyovyote vile nitafanya tu , pengine anaweza kunogewa na kusahau muda.
Dakika arobaini baadae Edna ndio ambae alikuwa hataki Roma aondoke mapema , alikuwa akihema kama vile roho inataka kumtoka lakini licha ya hivyo alijihisi yupo ulimwengu mwingine.
Upande wa Roma alikuwa kama mnyama ambae hachoki na alipeleka moto kisawa sawa , walianzia kitandani mpaka sakafuni na hatimae masaa mawili yalipita.
Edna baada ya kumaliza hakutaka kuendelea kubakia hivyo , alijua amechelewa lakini alihitaji kwenda kazini.
“Umeona sasa nimechelewa , ni makosa yako”Alilalamika Edna huku akikwepesha macho kidogo na Roma huku akijitahidi kufunga vifungo vya shati lake.
“Unataka kufanya nini?”Aliuliza Edna akirudi nyuma mara baada ya Roma kushika shati lake tena huku akivifungu vile vifungo.
Roma hakuongea na Edna alikuja kugundua alikuwa amekosea kufunga vifungo hivyo kiasi cha kuvipishanisha, kitendo kile kilimfanya
Edna kumwagalia Roma kwa macho ya mahaba.
“Nenda sasa kafanye kazi ukiwa mpya ..”Aliongea Roma mara baada ya kumaliza kuweka nywele za mke wake vizuri pamoja na koti lake.
Edna alipepesa macho kidogo na kisha alipanua mikono yake na kumsogelea Roma na kisha akambusu kwenye lips.
“I love you so much Honey” Edna aliongea huku akitabasamu na macho yake yalivyokuwa ni kama vile anataka kulia lakini haikuwa hivyo.
“Nakupenda sana mke wangu , nina furaha sana kuwa na wewe,Na ibarikiwe ile siku niliokudhania…”Kabla Roma hajamalizia alifinywa , Edna hakutaka kabisa kusikia kauli ya kudhaniwa kahaba , hata hivyo kila kitu kilikuwa wazi siku ile akili yake ilikuwa na mdudu.
“Tutaelekea wote kwenye harusi ya Ashley, baadae unifuate tukaangalie nguo zetu”Aliongea Edna na Roma aliitikia kwa kutingisha kichwa akiwa na tabasamu lakini ni muda huo huo simu ya Edna iliita.
“Nimechelewa , Matilda anapiga simu , Bye Honey”Aliongea Edna akimaanisha Mkurugenzi wa kampuni ya JR anapiga simu, kampuni ya JR chini ya uongozi wa Matilda iliweza kufanya vizuri mno , yote hayo ni baada ya Matilda kufuata ushauri wa Edna.

MWISHO
ASANTENI KWA KUIFUATILIA MWANZO MWISHO , KWA AJILI YA REFERENCE NITAFUTE WATSAPP 0687151346

ALL APRECIATION TO MY MENTOR : Ron Timm -PATH OF DAO.(Ingia google search ' Path of Dao' ,nstagram@pathofdaoqiqong).

INSPIRED BY MY ALL TIME FRIEND: LUANG JIZI(A.k.a flatbread)

SPONSORED BY : VOLAR MEDIA
Clear
 
Hatari
 
Mtu si mtu yyte ajaribu kunitumia hii riwaya yote kabisa inform of pdf kama ako nayo
 
Back
Top Bottom