NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware.
SEHEMU YA 715.
Tulipoishia:
Roma amefanikiwa kurudi upya kwenye ulimwengu wa majini watu na kufika katika makao makuu ya miliki ya Xia kwa ajili ya kumuokoa Rufi , katika harakati za kuingia bila kujulikana anamuua Jinni ambaye ni Mlinzi afahamikae kwa jina la Cheli na kisha anachukua uhusika wake , mara baada ya kuingia ndani hatimae akijifanyisha kufanya Doria lakini anashitukiwa na anaambiwa asimame hapo hapo alipo.
Roma alikuwa ashahisi akisogelewa kwa muda mrefu lakini hakutegemea kama jini huyo angemuamrisha kusimama tena kwa sauti kubwa , mara baada ya kugeuka aliweza kuona jini mzee ambaye amevalia joho la rangi nyeusi akiwa na nywele ndefu za rangi nyeupe.
Uso wake ulikuwa ni ule wa kujiamini na alikuwa akimwangalia kwa namna ya ajabu , ni kama vile mwewe anavyoangalia vifaranga na kumfanya Roma kuwa na wasiwasi.
Alikuwa ni jini ambaye yupo katika levo ya maji ya barafu na Roma aljiambia huyo sio mwepesi wa kudili nae mara moja.
Roma palepale akijiepusha kujulikana aliinamisha kichwa chake chini kama ishara ya heshima.
Huyo jini mzee alifahamika kwa jina la Lao , ndio ambaye alifika ulimwengu wa kawaida na kumkamata Rufi akiwa na Lahani, kazi yake ndani ya makao makuu hayo alikuwa ni Mtumishi Kiongozi.
Mara baada ya kumuona Roma anaelekea upande ambao haukuruhsiwa kufanyiwa doria pamoja na kuongea na walinzi kila mara ilimfanya kumshuku.
Walinzi wote ndani ya eneo hilo walikuwa wakisimamiwa na yeye mwenyewe na alijua huyu mtu anaefahamika kwa jina la Cheli , alikuwa ni jini wa kawaida ambaye anafanya kazi chini ya familia ya kiongozi mkuu wa miliki.
Master Lao alikuwa akimjua Cheli ni moja wapo ya majjini waliopo mwishoni mwa levo ya nafsi ambao ni waaminifu na hawawezi kuonekana wakitembea tembea sehemu ambazo hawaruhusiwi.
“Cheli kwanini umekuja huku eneo ambalo sio lako?”Aliuliza mara baada ya kumona hamsalimii , Roma hakutaka kusalimia kwani hakutaka kugundulika.
“Nastahili adhabu kwa kukiuka majukumu yangu?”Aliongea Roma huku akijifanyisha kuwa muoga.
“Nyanyua kichwa chako na ongea na mimi ukiwa unaniangalia”Aliongea huku akipiga hatua kumsogelea Roma karibu huku akitoa nguvu ya kijini ya kuogofya.
Upande wa Roma alionyesha kuathirika na muonekano wa Mtumishi Lao lakini kwa wakati huo alikuwa akiongea na moyo wake , alijiambia hilo eneo ni katikati ya makao makuu ya miliki hii anaweza kumuua ndio lakini lazima ataamsha walinzi wakuu ndani ya eneo hilo na mpango wake wa kumuokoa Rufi ungefeli au kuingia hatarini.
“Kwanini hunipigii saluti?”Aliongea na palepale Roma kwa haraka aliinua mkono wake na kumpa saluti yake.
“Umesahau mimi ni nani?”Aliongea Mtumishi Lao huku akizidi kuhisi kuna kitu hakipo sawa kuhusu Cheli , mlinzi huyo mara nyingi alikuwa akipiga sautli lazima ataje jina lake , lakini kitendo cha kutotaja jina ilimaanisha kwamba hakumfahamu , sasa alijiuliza inawezakaje.
Lao alishakuwa Mtumishi ndani ya familia ya viongozi wa miliki kwa muda mrefu sana , ni zaidi ya miaka mia moja na yeye mwenyewe umri wake ilikuwa ni miaka mia mbili , hivyo asilimia tisini ya majini wote wanaoshi ndani ya miliki hio walikuwa wakimfahamu.
Roma alijikuta akipatwa na jasho la ubaridi , hali ilikuwa ikiendelea kuwa mbaya na kama ataendelea kubakia hapo angeweza kumtambua.
“Wewe sio Cheli , niambie wewe ni nani?”Aliongea na palepale alinyanyua mkono wake na kufanya nguvu za kijini kuendelea kumtoka kwa wingi na alikuwa tayari kumkamata Roma.
Lakini muda ule Roma akili yake ilikwisha kucheza tayari na alishapata mpango wa kumaliza hio hali.
“Guru Master!!!”
Aliongea Roma na palapele alinyoosha kidole nyuma yake akijifanya kama vile yupo kwenye mshangao kwa kuona mtu nyuma.
Ijapokuwa ameishi miaka mingi lakini hakuwa akijua hila za kibinadamu za kutoroka na ndio alichomfanya kwa kujifanyisha kushangaa mtu aliekuwa nyuma yake na aligeuka kweli kwani alikuwa akitegemea kumuona Laofi.
Baada ya kugeuza kichwa chake aliishia kulaani katika kichwa chake na kujiona ni mjinga kwani kama kweli Laofi amekaribia basi angeweza kuhisi uwepo wake , akiwa na hasira aling’ata meno yake na kumgeukia Roma lakini Roma alishaondoka mbele yake na kukimbia.
“Unathubutu vipi kukimbia?”Aliongea kwa hasira na palepale aligeuka kama kivuli na kumpandia Roma hewani na kuanza kumfukuzia.
Roma wakati huo alikuwa akitumia nguvu ya kijini katika levo ya nafsi hivyo spidi yake ilikuwa ndogo na ingemuwezesha kukamatwa na jini ambaye yupo katika levo ya maji ya barafu hususani kwa mtaalamu kama Lao.
Baadhi ya majini wa levo za juu pia waliweza kumshuhudia Mtumishi Lao kumfukuzia jini ambaye yupo katika levo ya nafsi lakini hawakujisumbua kumsaidia wakiamini kwamba kwa uwezo wake ataweza kummudu , shukrani kwao Roma aliona kabisa hio ndio nafasi ya kujitoa katika hali hio ya mtego.
Upande wa majini walinzi waliokuwa katika levo ya nafsi na baadhi waliopo katika levo ya moto wa njano walitaka kujichukulia sifa kwa kwenda kumsaidia Mtumishi lao hivyo waliunga nyuma katika kumfukuza Roma.
Upande wa Roma hakuwa na wasiwasi , ilimradi hakukuwa na jini ambalo lipo levo ya maji ya upako ingekuwa rahisi kudili na majini hao wa levo ya chini , hivyo alijiambia anapaswa kukimbia kwenda mbali kadri awezavyo.
Kufumba na kufumbua Roma alikuwa zaidi ya kilomita ishirini mbali na makao makuu ya miliki ya Xia na upande wa Master Lao alikuwa akimfukuzia kwa kasi na kumsogelea karibu.
Palepale Lao alitoa tabasamu la kifehdnuli na kisha alitoa mjeledi wa mkanda rangi ya silver ambao una urefu kama futi saba hivi kwenye hifadhi pete yake , ulikuwa na mafundo fundo yalifungwa kwa namna ya kiajabu.
Wale walinzi waliokuwa wakifatilia nyuma mara baada ya kuona Dhana hio ya mjeledi wote walijikuta wakitoa kicheko cha furaha.
“Huyu mwizi hana bahati , Mtumishi kashatoa tayari
Dhana yake ya Mjeledi wa ngurumo ya radi , ile ni
Dhana ya daraja la kati na ina nguvu ya kueleweka”
“Nishawahi kusikia mjeledi wa ngurumo unaweza kushambulia na kuzuia , nguvu yake ni sawa na Dhoruba ya radi lakini kwa bahati mbaya sijawahi kuona ikitumika”
“Tokea siku nyingi nilikuwa nikitamani kuonyesha uwezo wangu , lakni wezi ni adimu sana kuja makao makuu ya familia ya viongozi , nadhani hata leo nimekosa nafasi”
Walinzi walikuwa wakiongea huku wakiamni Roma anakwenda kupoteza pambano , wote kwa pamoja walipunguza spidi wakiona haina maana ya kukimbia kwa spidi.
“Ewe mwizi onja radha ya mjeledi wangu wa ngurumo ya radi!!!”
Muda huo mara baada ya Master Lao kuona umbali kati ya Roma umekuwa mfupi aliunganisha mjeledi wake ule na nguvu za kijini na palepale ulianza kuwaka moto na kutoa shoti kama za radi huku ukiambatana na ngurumo.
Shoti zile za radi zilikuwa na spidi mno kwani zilimsogelea Roma kwa spidi , ilikuwa ni kama vile ule mkanda unaongezeka urefu wake lakini haikuwa hivyo ilikuwa ni kutokana na nguvu ya kijini ambayo imetumika hivyo zile Radi ndio zilionekana kama vile mkanda umeongezeka.
Upande wa Roma muda huo alijikuta akishangazwa na Dhana ile ambayo inatoa moto kama radi vile.
Ili dunia kubalansi asili yake ilitengenezwa na nguvu za aina mbili zinazopingana lakini kuvutana kwa wakati mmoja , Ying and Yang , Chanya na Hasi , maji na moto, mbingu na ardhi n.k.
Elementi nyingine za dunia kama vile Dhahabu miti , ardhi na upepo vyote vimewezekana kutokana na nguvu mbili ambazo hazifananani lakini kuvutana.
Hivyo likija swala la Dhana na Nishati za mbingu na Ardhi asilimia kubwa elementi ambazo hutumiwa na majini ni maji na moto.
Asilimia kubwa ya majini wa kawaida hawawezi kutumia radi ambao wenyewe huita moto wa mbingu(Heavenly fire) lakini wanao uwezo wa kutumia nguvu zao za kijini katika kubadilisha nishati ya kiroho ili kucheza na maji na moto hata zaidi ya hapo.
Kuna baadhi ya mbinu za kucheza na moto na maji na kuzalisha kitu kingine kabisa na kuwa na nguvu kukaribiana na radi, kwa mfano mbinu ya majini wa kikaskazini ifahamikayo Dark ice soul ambayo hutumiwa zaidi na Hongmeng , hio ni mbinu ambayo imetokana kati ya kufungamanishwa roho na barafu.
Lakini sasa ukizungumzia elementi za radi ni za kipekee sana , radi hutokana na elementi zote mbili za moto na msunguano wa maji ya barafu katika mawingu.
Kwahio mchanganyiko wa hasi na chanya siku zote unakuwa ni hatari sana na ndio asili ya Adhabu ya mapigo tisa ya radi ambayo nguvu yake inakuwa ni zaidi ya nishati za mbingu na ardhi.
Kama sio hivyo pengine Zeus asingeweza kuwapiga majini kwa kutumia siraha yake ya ngurumo miaka elfu ishirini iliopita , ijapokuwa Zeus siraha yake haikuwa na nguvu kama mapigo tisa ya radi ngurumo lakini ilikuwa ni kitu ambacho kina athari kubwa kwa majini.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba majini wanaoogpa sana Radi kuliko kitu chochote kile na ndio Dhiki yao kubwa wanayoihofia sana.
Roma alijua radi ambayo inatoka katika mjeledi wa Lao ni radi ya kawaida kabisa ambayo imetengenezwa kwa kunyumbulisha elementi za dunia hivyo haiwezi kulingana na ile inayotoka juu mawinguni lakini hata hivyo hakutaka kuidharau nguvu hio.
Sasa Roma mara baada ya kuona sasa yupo mbali na miliki ya Xia hakutaka tena kuficha uwezo wake wa kijini , nishati ya mbinu na ardhi ya andiko la urejesho wa azimio ili uzingira mwili wake na kutengeneza kinga na mara baada ya shoti zile za radi kugusana na mwili wake ulitokea mlipuko ambao ulisambartisha nguvu ile ya radi.
“Ina,, inawezakanaje..!?”
Mzee huyo jini alijikuta akikosa muda kabisa wa kuchukua hatua , alikuwa amechelewa kuepuka na alijikuta akianza kuhema , alijaribu kuzungusha mkanda wake ule wa kimjeledi ili kumrushia Roma boriti za shoti ya radi.
Roma aliangalia shoti hizo ambazo zinamsogelea zikiwa katika rangi ya bluu na alitoa tabasamu la kejeli na palepale alijiambia sio mbaya angalau alikuwa akitafuta sura yenye cheo ili kuweza kumtafuta Rufi ndani ya makao makuu hayo bila kushitukiwa na amejileta mwenyewe.
Dakika ileile alikiita chungu cha maafa na kikatokea na kuanza kumeza zile shoti zote za radi na palepale nguvu ya mnyama ilitengeneza nguvu ya kani mvutano na kuushikilia mwili wa jini Lao.
Jini Lao alijikuta akiogopa mno , alijitahidi kujiokoa akimbie lakini alishindwa kabisa , ilikuwa ni kama vile
mtu anavyotumbukia kwenye shimo na hakuna pa kushikilia , alitumia nguvu zake zote za kijini kujishikilia lakini nguvu ya roho ya mnyama ilikuwa kibwa mno.
“Wewe … wewe ni nani?! , hebu niachiliee”Aliongea kwa kutetemeka huku akiwa na hasira mno kiasi cha kufanya uso wake kuwa mwekundu , katika maisha yake hakuwahi kutoa kilio cha kuomba kuachiliwa kama hivyo kwa miaka yote mia moja.
Roma hakutaka kujisumbua sana na aliangalia walinzi
ambao ameambatana nao kumfukuzia na walionyesha dalili za kutaka kukimbia na Roma hakutaka kuwapa nafasi na palepale aliachilia moto wa rangi ya Zambarau uliogeuka kama vinyoka na kushambulia majini wote hao ambao walikuwa katika levo ya nafsi na moto , waligeuzwa majivu palepale.
Master Lao mara baada ya kuona tukio hilo palepale alijikuta akikosa ujasiri tena wa kujiokoa , mtu anaepambana nae uwezo wake ulikuwa ni hatari mno na ilimkumbusha paleplae uwezo wa mkuu wao wa miliki jini Anjiu.
Roma mara baada ya kuhakikisha majini wale amewaua na hakuna ijini mwingine karibu hakutaka kumeza jini Lao na chungu chake hivyo alimsogelea karibu zaidi.
“Nadhani nimesikia wakikuita Mtumishi mkuu , nadhani wewe ndio unaefahamika kwa jina la Lao?”Aliongea Roma.
“Kwahio vipi kama ndio mimi , umetoa wapi ujasiri wa kutaka kuingia katika ngome ya miliki ya Xia, kama una akili ni bora ukaniacha niende zangu ,
haijalishi uko vizuri kiasi gani lakini huwezi kumshinda Master wa miliki ya Xia”Aliongea kwa sauti.
“Haha.. unachekesha , yaani ulitaka kuniua halafu unaniambia nikuachie , hivi akili yako imeota kutu kutokana na kuzeeka?, kama unataka kuendelea kuishi , fanya kama ninavyosema , jibu maswali yangu yote kwa uaminifu na nikimaliza nitakuondolea nguvu zako za kijini na kukugeuza paka na kukuacha uende zao , ukikaidi nitakuminya mpaka unabakia hewa”
Alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira huku akijaribu kujiondoa katika mvutano wa chungu lakini kila alivyojaribu hakuona namna kabisa ya kujiokoa.
Ijapokuwa alikuwa katika levo ya maji ya barafu lakni Roma alikuwa katika levo ya juu kabisa ya mzunguko kamili wa mapigo tisini na tisa ya radi zambarau na Dhana yake ilikuwa ni ya daraja la juu kabisa ya kihistoria , hakuna jini lolote hata ambalo lipo katika levo ya maji ya upako kuweza kuepuka kama tu halina Dhana ya daraja la juu, hivyo kwa lugha nyepesi kwa Mtumishi Lao hakuwa na uwezo wowote wa kujiokoa.
“Acha kujaribu bahati yako , ninaweza kukua kwa kukunja kidole tu”Aliongea Roma akiwa siriasi.
Master Leo alijiambia hata kama uwezo wake wa kijini ukiondolewa ataweza kuendelea kuishi na anaweza kuwa chini ya uangalizi wa familia ya mkuu wa majini kama kiinua mgongo cha kuwahudumia kwa zaidi ya miaka mia moja , alijiambia hata kama akigeuka paka au kiumbe chochote anayo nafasi ya kujifunza na kurudisha mwili wake na kuendelea na maisha,
“Okey , uliza maswali yako?” Hatimae alikubali.
“Je wakuu wa miliki ya Xia wamemkata Rufi wa miliki ya Kekexil?”
“Huh!?”
Master Lao hakutegemea swali hilo kutoka kwa Roma , alitegemea angekwenda kumuuliza mbinu za mafunzo ya kijini au siri za miliki hio.
“Hilo ndio swali lako , kwanini unamuulizia , umetokea miliki ya Kekexil?”
“Acha kuongea ujinga na jibu maswali yangu , Rufi yupo wapi , na anaendeleaje?”Aliongea Roma kwa mara ya pili na palepale jini Lao aliingiwa na wazo na kutoa tabasamu la kifedhuli.
“Ndio unajaribu kumuokoa Rufi , hehe.. kama unataka kumuokoa usije kunigusa maana atakufa kwa uhakika”
Lao alijiambia angekuwa juu zaidi kama angemtumia Rufi kumtishia Roma lakini asichokijua Roma alikuwa mjanja tena zaidi ya neno lenyewe na alikasirika sana baada ya kuona jini huyo anamtishia maisha kwa kutumia mtu mwingine.
Palepale aliondoa kile chungu na kisha akamkaba shingo jini Lao kwa nguvu na kuachia nguvu ya kijini ya daraja la juu zaidi .
“Pumbavu zako , unathubutu vipi kunitishia , unafikiri mimi ni mtoto wa miaka mitatu kwamba ni rahisi kunidanganya?”
Msisimko wa kimauaji ambao ulikuwa ukimtoka
Roma ulibadilisha hali ya hewa na kumpelekea jini Lao kuhisi ubaridi , kidogo tu ajikojolee , kwenye maisha yake hakuwahi kukutana na adui amezingirwa na nguvu ya vifo kama Roma , nguvu hio mara nyingi hutokana na mtu ambaye ameua sana zaidi ya maelfu ya watu.
Kabla hajaomba hata msamaha kwa kumchokoza Roma alijishutikia mkono wake ukichomolewa begani na kufanya damu nyingi zimtoke.
Roma hakuishia kwenye kunyofoa mkono wake tu kwani palepale aliruhusu na nguvu ya moto kumtoka na kuanza kumuunguza jini Lao.
“Arhggggg…!!!”
Baada ya kuona mkono wake umenyofolewa macho yake yalijawa na ukali huku akiendelea kupiga yowe la maumivu.
“Nitakuuliza kwa mara nyingine , Rufi yupo wapi?”Aliongea Roma huku awamu hio sauti yake ikibadilika na kuwa nzito mno.
“Yupo … yupo katika chumba cha stoo kwenye jengo la kutengenezea vidonge.. bado yupo hai?”
“Jengo la kutengenezea vidonge ndio lipi?”
“Lipo kusini kutoka Jumba la Jade , ni jengo lenye ghorofa tatu kwenda juu , kuna alama za kimaandishi katika jengo hilo hivyo itakuwa rahisi kugundua , yupo chumba floor ya tatu”
“Wewe unaweza kwenda bila shida , je kuna vizuizi vyovyote kuinga katika jumba hilo la utengenezaji wa vidonge , kuna walinzi wangapi?”
“Mimi kama Mtumishi mkuu wa Jumba la mkuu wa miliki ninaweza kuingia na kutoka nitakavyo , walinzi wataondoa safu ya ulinzi na unachotakiwa kufanya ni kuwaambia wakufungulie mlango , ndani kuna mzee mmoja tu ambaye anahusika kutengeneza vidonge na hakuna mwingine zaidi”
Lao alionekana kushika adabu na kujibu kila maswali , alijua kabisa uwezo wake ungeondolewa lakini hakutaka kupoteza kiungo kingine cha mwili wake.
“Umejibu vyema , swali lingine la mwisho ni majini wangapi ambao wapo levo ya maji ya upako au zaidi ndani ya miliki ya Xia?”
Roma alikuwa na wasiwasi na jambo hilo , kama kutakuwa na zaidi ya watano basi atapaswa kuwa makini zaidi na zaidi na pia ingekuwa ngumu zaidi katika kumuokoa Rufi.
Kwani hata kama atamtoa kwenye chumba hicho basi atapaswa kumlinda huku wakati huo akitafuta njia ya kuondoka , Chungu cha kijini bado hakikuwa katika uwezo wake wote hivyo asingeweza kuwashambulia wote kwa pamoja halafu wakati huo akimpa ulinzi Rufi.
“Kuna wazee watatu , Mkuu wetu namba moja Mzee
Anjiu , Mkuu wetu namba mbili Master Zianji na Guru Mzee Laofi”
Roma alifurahi na kuona hakutakuwa na hatari kubwa
.
“Nimejibu maswali yako yote naomba uyarehemu maisha yangu tafadhali”Aliongea kwa kubembeleza na Roma hakuuliza maswali mengi zaidi.
“Yaani nikuachie , nadhani umekua kipofi kwa kuishi muda mrefu , hivi unafikiri muwindaji anaweza kuachia kitoweo kichague kufa au kuishi?” “Muongo mkubwa wewe’Aliongea kwa hasira .
“Crack!!!”
Roma kwa kutumia nguvu ya kijini palepale aliivunja shingo yake na Lao kupoteza maisha palepale na hakupata hata nafasi ya kumjua Roma ni nani haswa.
Roma baada ya kufanya muaji alitoa pete yake ya hifadhi na kisha akavaa mavazi yake na kuchukua Dhana yake ya Ngurumo , baada ya kuangalia hifadhi yake aliweza kuona baadhi ya vitu ambavo ni kama zawadi kutoka kwa miliki hio na hakujua matumizi yake hivyo aliachana navyo.
Kulikuwa na kifaa kimoja tu ambacho aliweza kukishangaa , ni chupa ndogo ambayo ndani yake ilikuwa na kimiminika cha rangi ya damu ya mzee na hakikuwa na harufu , Roma alitumia nguvu ya kijini ya utambuzi na aliweza kugundua kina nguvu kubwa ya giza.
Aliona pengine sio kitu kiziuri hivyo alifunika mfuniko wake na kisha akatupia kwenye hifadhi yake bila maswali mengi.
Baada ya kuunguza maiti yake na kuwa majivu alibadilisha muonekano wake na kisha uwezo wake wa kijini kwenda levo ya maji na kisha alianza safari ya kurudi makao makuu kama Mtumishi Lao.
Safari yake ya kurudi haikuwa na shida kubwa kwani alikuwa akitumia sura ya Master Lao ambaye anacheo kikubwa tu ndani ya makazi hayo makuu ya miliki.
Walinzi mara baada ya kumuona hawakuonyesha tofauti yoyote zaidi ya heshima na walimwita mtumishi kiongozi.
Upana wa makao makuu hayo ulikuwa ni mkubwa mno kiasi kwamba ni ngumu kujua wale walinzi waliondoka hawajarudi.
Roma mara baada ya kuzunguka zunguka ndani ya makazi hayo ya majiini hatimae aliweza kufika mbele ya jengo ambalo lina alama juu ya jengo la kutengenezea vidonge.
Alitumia uwezo wake kuchunguza eneo hilo na hatimae aliweza kupata uwepo wa Rufi ndani ya jengo hilo lakini hata hivyo alijua hatakiwi kuzembea hususani katika wakati huo muhimu , alijifanyisha kuwa na utulivu na kwa kujiamni alianza kutembea kuusogelea mlango.
Majini walinzi ambao walikuwa na muonekano wa kizee walikuwa wamesimama mlangoni , wote wakiwa katika levo ya maji yya upako , nywele zao wote zilikuwa nyeupe , ijapokuwa walipewa vyeo vya wazee wa miliki lakini walimpa heshima Mtumishi Lao. “Jambo gani limekuleta katika jengo la utengenezaji wa vidonge Mtumishi usiku usiku , je Mkuu wetu kuna chochote anachotaka?”Aliuliza mmoja huku akiwa na uso uliojaa bashasha.
Roma hakuwa na uvumilivu hata kidogo na kujiambia kwanini wasifungue tu mlango , maswali mengi ya nini, lakini hata hivyo aliamua kujibu.
“Ndio”
SEHEMU YA 716.
“Kuwa mtumishi hakika ni kazi yenye ubize sana , sio tu kwamba unapaswa kuongoza wafanyakazi ndani ya makao makuu lakini vilevile unapaswa kumhudumia mkuu wetu”Aliongea yule mwingine.
Roma aliona ni kama vile wanamchawia na aliishia kutoa pumzi ya ahueni na kisha akatoa tabasamu.
“Nina timiza wajibu wangu tu kama Mtumishi, kwenu nyie marafiki zangu naombeni mnifungulie mlango”
“Oh bila shaka tusamehe kwa kukuchelewesha Mtumishi”Waliomba radhi na kisha waliondoa kizuizi katika mlango kwa kutumia nguvu zao za kijini na palepale mlango wenyewe bila kuguswa ulifunguka.
Roma mara baada ya kuingia katika chumba kikubwa cha kwanza alikuwa akihisi nguvu kubwa ya kiroho katika hewa.
Sakafu yake yoto na kuta mpaka madirisha madini ya Jade ndio yametumika katika ujenzi ili kuzuia nguvu za kiroho kutoka nje, katika floo ya kwanza tu kulikuwa na rundo la mimea na viungo vingi ambavyo vilipangiliwa katika mtiririko wa kueleweka.
Lakini kwa kulinganisha Jumba jeupe la miliki ya Kekexil na miliki hio haikuwa na hazina kubwa ya madawa.
Kwa mfano tu katika lile Jumba Jeupe kulikuwa na floor tano zote ambazo zimetumika katika kuhifadhia mimea ya kimadawa, likija swala la aina , kiasi , ubora na uadimu wa mimea na vidonge Xia hawapandi hata kidogo kwa Kekexil.
Ilionekana kila miliki ilikuwa na aina yake ya utajiri kwa ajili ya kuishi , miliki ya Kekexil ilisifika kwa kuwa na madawa lakini miliki hio ilisifika kwa kuwa na utajiri wa madini ya jade .
Ukweli ni kwamba Roma alijua hata kama aliwaibia Kekexil ingewachukua tu angalau mwaka kurudisha kila kitu sawa.
Muda huo ndani ya floo hio wazee wawili walikuwa wapo makini wakitengeneza vidonge kwa kutumia moto wa rangi ya njano na nyekundu , lakini pia kulikuwa na vijakazi ambao walikuwa wakipangilia mimea na viungo.
Mara baada ya kumuona Roma majini hao waliinamisha vichwa vyao kuonyesha heshima , ilionekana Master Lao sio tu kuwa maaruf lakini alikuwa na cheo kikubwa ndani ya makao makuu ya miliki hio zaidi ya utumishi.
Kwasababu Roma hamu yake ni kumuona Rufi hakutaka kabisa kuongea nao sana na alifuatisha ngazi kuanza kuelekea juu , lakini dakika hio hio aliweza kushuhudia mwanamke wa kijini akitokea juu kuja chini akiwa ameambatana na mzee mwingine ambaye alikuwa amevalia mavazi kama vile ni Monk.
“Niwie radhi sana sana , sio kama nakuwa mkatili lakini kuna awamu ya kwanza tu ambayo imekamilika ya vidonge vya daraja la juu na tayari nishavitawanya kwa watu muhimu ndani ya familia kulingana na maagizo ya Lodi mkuu mwenyewe , kama awamu nyingine ikikamilika ninakuahidi wewe utakuwa ni wa kwanza , mimi ni mwanaume wa vitendo”
“Oh ,.., haina haja ya kuwa siraisi hivyo Cheluni , ninataka vidonge hivyo kwa ajili ya kijana wangu Lahani , sina uelewa mume wangu anafikiria nini kwa kutompatia mtoto wake vidonge vya daraja la juu
wakati anajua anatarajia kufikia levo ya maji meupe”Aliongea yule mwanamke akionyesha huzuni.
“Hakika unampenda sana kijana wako , nimevutiwa lakini nadhani mkuu wetu anatamani kuona Lahani anapita levo hio kwa nguvu zake mwenyewe kwasababu mwanzoni amemeza vidonge vingi , kama ataendelea kutegemea vidonge kupanda levo itamletea madhara huko mbeleni na atapata tabu kwenye kupanda levo za juu zaidi kutokakna na msingi wake ktuokuwa imara”Waliendelea kuongea na dakika hio hio waliweza kufika katika floor ya chini.
“Oh … Mtumishi nakuoa upo hapa , kuna maagizo yoyote kutoka kwa Mkuu wetu?”Aliuliza jini aliefahamika kwa jina la Cheluni.
Roma alikuwa na wasiwasi na kwa bahati nzuri alikuwa ashasikia majina yao vinginevyo asingewafahamu ni wakina nani.
Mwanaume huyo alifahamika kwa jina la Cheluni na alikuwa ndio anaesimamia jengo hilo na alikuwa kwenye levo ya maji ya barafu na inawezekana akawa ndio mwenye nguvu zaidi ukiachana na wale ambao wapo tayari katika maji ya upako.
Kuhusu huyo mwanamke mrembo alikuwa ni mke wa Mkuu wa miliki hio Lodi Anjiu na kwa maelezo ya Sui ilikuwa sahihi kabisa alikuwa mwishoni mwa levo ya maji meupe.
“Mzee Chuleni nimekuja kuchukua vidonge kwa ajili ya mkuu wangu”
“Kumbe , basi mimi ndio namsindikiza mke wa mkuu wetu na nitakufuata kuchukua vdonge , subiri kidogo Mtumishi”
Roma alitingisha kichwa chake huku akitamani waondoke tu , lakini kwasababu ameambiwa asubiri hakuona haja ya kwenda juu peke yake kwani angehatarisha misheni yake.
Muda uleule mara baada ya mke wa Anjiu , bibie Anjiu Leiana kumpita, Roma aliweza kunusa harufu yake ya marashi na yalikuwa yakifurahisha pua mno.
Kilichomshangaza zaidi Roma ni kwamba mrembo huyo mara baada ya kukutananisha nae macho alimkonyeza na ilikuwa ni wazi kabisa alikuwa akijilengesha.
Ijapokuwa ilitokea ndani ya sekunde tu wakati wengine hawajaona lakini Roma hakuamni kile kilichotokea , alikuwa katika sura ya Mtumishi wa makazi hayo na alijiuliza inawezekana vipi mke wa bosi mkuu wa miliki hio kumtega mtumishi au wana mambo yao ya siri yaliokuwa yakiendelea.
Roma aliishia kukunja sura na hakutaka kujisumbua sana alichokuwa akipaswa kufanya hapo ni kumtamfuta Rufi na sio vinginevyo na kisha kuondoka.
Jini Cheluni mara baada ya kumtoa nje Jini Leiana alirudi ndani kwa haraka na kisha alichukuana na Roma mpaka floor ya pili .
Roma mara baada ya kufika katika floor hio aliweza kuona vidonge vingi ambavyo vilikuwa vimepikwa na kuhifadhiwa katika shelfu , kulikuwa pia na majini wa levo ya maji barafu waliokuwa wakilinda katika kila kona , ki ufupi ni eneo ambalo lilikuwa na ulinzi mkali sana.
Roma palepale alijua mtumishi Lao alimdaganya , maana alidhania ni kweli hakuna walinzi lakini eneo hilo ulinzi wake sio wa kawaida na alijua kama atamtoa Rufi lazima agesababisha vurugu kubwa mno , kutokana na wingi wao alijua angepoteza muda kupambana nao mpaka muda ambao majini wa levo ya maji ya upako watakapo fika.
“Mtumishi naweza kujua ni vidonge gani unahitaji kwa ajili ya mkuu wetu?”
“Oh .. Master anahitaji vidonge Washa kumi”
“Vidonge washa kumi!! , hivi si kwa ajili ya mapambano ya ana kwa ana , au anawapatia wanajeshi wetu wanaondoka?”
“Master hakuniambia ni kwa ajili ya nini lakini ninadhani ni kwa ajili hio”
Cheluni alikuwa akiuliza tu kwa ajili ya shauku na sio kwamba hakuwa akimwamini Mtumishi , muda ule alimchukua Roma mpaka katikati ya chumba na kulikuwa na jiwe kubwa ambalo limekaa kama meza na mara baada ya kuorodhesha vidonge ambavyo Roma alihitaji alimwambia asaini.
Roma hakutegemea utaratibu huo , ilionekana walifanya hivyo ili kuzuia majini wasichukue vidonge bila utaratibu maalumu.
Ilikuwa bahati kwa Roma aliweza kuona sahihi ya Lao pembenni yake na aliigizia vilevile ilivyo kwa kutumia nguvu za kijini hivyo hakushitukiwa
Baada ya utaratibu ule alitoa kichupa cha rangi ya kijani ambacho ndani yake kuna vidonge nane vya Washa na kisha kumpatia Roma.
“Tushamalizana Mtumishi , tuondoke sasa”Aliongea huku akimpa ishara lakini Roma palepale alisimama akuonyesha hajamaliza..
“Mzee Cheluni kuna jambo lingine kuhusiana na msichana ambae yupo floor ya tatu?”
“Msichana ambae yupo floor ya tatu … unamzungumzia Rufi mfungwa wetu?” “Ndio , Mkuu kaniambia nimpeleke pia ana maswali anataka kumuuliza”Aliongea Roma na kumfanya Cheluni kuonyesha mshangao.
“Rufi tayari amekwisha kukabidhiwa kwa baraza la wazee na yalikuwa ni maamuzi yake , ashaanza kutumika tayari katika majaribio ya vidonge kwanini anamuhitaji tena , si tulimuuliza maswali yetu yote?”
Roma alijikuta akipandwa na jazba na kauli hio , ilionekana walimtesa Rufi katika kumuuliza maswali na hali hio ilimtia mashaka atakuwa katika hali gani.
“Imekuwa ngumu kujua sababu ya maagizo ambayo nimepewa na mkuu wetu , mmi natii tu maagizo yake kwa kumpeleka”
Cheluni palepale alionyesha ishara za wasiwasi juu ya Roma kwani hakuwa mjinga , alijua namna ambavyo Lao mtumishi anavyoongea ni tofauti kabisa siku hio lakini hakuweza kuona nini tatizo kwani alikuwa ni yeye
“Unaweza kumtoa hapa kwa kupata kibali kutoka kwa wazee wenyewe au upate ruhusa kutoka kwa Guru Laofi , mimi Cheluni sijawahi kufanya makosa katika kulinda hili eneo , sitaki kuingia katika historia kwa kuwa wa kwanza kukiuka sheria , Rufi ana thamani kubwa kwa miliki yetu na nina vidonge bado vya kufanyia majaribio nione ukali wa sumu yake , siwezi kumruhusu kirahisi kuondoka ndani ya jengo hili nitapata wakati mgumu kutoa maelezo mbele ya baraza la wazee”
Roma alikuwa na hasira alijua vyema asingeweza kuharakisha kwenda juu bila ya kujua hali yake Rufi , pengine anaweza kumuingiza katika hatari zaidi kama atakurupuka.
“Unaonaje tukifanya hivi , sitoondoka nae lakini
utanipeleka na nimuulize maswali machache tu na kumuacha?”
Dakika hio hio ambayo Roma alitamka kauli hio alijutia palepale kwani ilimfanya Cheluni kuzidi kuwa na wasiwasi.
“Mtumishi , Rufi ni mfungwa na yupo chini ya baraza la wazee ,Mkuu wetu na wewe pia mnaelewa hili , unaonekana kutaka sana kuonana nae , ni maagizo ya mkuu kweli?”
“Mzee Cheluni unamaanisha nini? , ninachofanya ni kumpunguzia mkuu wangu mzigo , ila kwasababu unanikataza kwenda basi nitaenda kuchukua kibali kutoka kwa mkuu mwenyewe”
Cheluni alimwangalia Roma machoni kama vile kuna kitu ambacho anatafuta lakini Roma hakuonyesha hali ya hofu na wote waliangaliana usoni.
Mwishowe Cheluni hakuona tofauti yoyote kutoka kwa Roma , mwanzoni alijua labda mtu aliekuwa mbele yake sio Mtumishi kutokana na makosa ya wazi anayoyafanya lakini alionyesha kuridhika.
“Kama ni hivyo Mtumishi nenda kalete kwanza kibali cha maandishi na nitakupatia huyo mwanamke , sio tu wewe hata mtoto wa Mkuu na mke wake hawawezi kumtoa humu bila ruhusa”
Bwana huyo alionekana kuwa imara kwenye msimamo wake na yote hayo ni kwasababu Lao Mtumishi alikuwa akichukuliwa ni kijakazi licha ya cheo chake.
Lao hakuwa mrithi wa moja kwa moja katika familia ya wakuu wa miliki na hakukuwa na uwezekano wa kulazimisha kufanya kitu.
Roma mara baada ya kukataliwa alijikuta akizidi kuwa na wasiwasi na alitamani kuharibu jengo zima lakini alijua akikurupuka kimaamuzi itamuweka Rufi katika hali mbaya, ilikuwa ni bahati kwake tu kwamba Rufi alikuwa hai mpaka wakati huo.
“Rufi naahidi nitakutoa ndani ya hili eneo mapema tu , naomba uvumilie kwa muda mfupi”Aliwaza Roma akikodolea macho jengo hilo na kisha akaondoka.
Roma hakutaka kuendelea kujifanyisha ni Lao Mtumishi tena kwani angegundulika muda si mrefu , katika akili yake alikuwa akikumbuka maneno ya Cheluni kwamba Guru Laofi ndio ambaye ana uwezo wa kumchukua Rufi bila hata ya ruhusa , hivyo wazo lake mara moja lilimwingia akilini , aliona kitu pekee cha kufanya ni kumuua huyo Laofi na kisha kuchukua uhusika wake , ijapokuwa ingekuwa ngumu kutokana na kwamba yupo katikati mwa levo ya maji ya upako lakini alijiambia atajitahidi kwani ndio njia pekee ya rahisi.
Baada ya mpango huo Roma alianza kuulizia wapi alipo Master Laofi ili tu kumdanganya na kumpeleka eneo la mbali na kisha kumuua.
Wazo hilo lilikuwa kichaa kutokana na uwezo wa Laofi lakini kwa Roma ni wazo la kawaida , kwake yeye mtu ambaye anawazia sana matokeo hawezi kufanikiwa kwenye maisha yake.
Dakika chache mara baada ya Roma kukata kona aligundua kuna anaemfatilia kwa nyuma na hio ni mara baada ya kunusa harufu ya marashi.
Majini wanakuwa na marashi ambayo sio ya kawaida kabisa hasa majini wakike na Roma pua zake ziliweza kunasa harufu hio na dakika hio hio aliweza kusikia sauti nyororo ikimwita.
“Unaenda wapi Mtumishi Lao?”
Mrembo jini Leiana alitokezea mbele ya Roma , alikuwa ni mweupe sana na midomo myekundu kama vile inavuja damu huku macho yake yakiwa ni yale ya kuita.
Mwanaume wa kawaida hawezi kuhimili mvuto wa mwanamke huyo , isitoshe hata hivyo sio wa kawaida lakini kwa Roma kutokana na kuwa na nguvu za kijini alikuwa vizuri kwenye kuhimili mvuto wake.
Licha ya kwamba Roma hakujua uhusiano uliokuwepo kati ya Mtumishi Lao na Leiana kutokana na uzoefu wake alijua tu lazima kuna mahusiano ya siri yanaendelea.
“Madam , siendi popote , je kuna maagizo yoyote unataka kunipatia?”Aliongea Roma kwa heshima na kauli yake ile iliamsha kicheko cha nguvu kutoka kwa Leiana na kisha alimsogelea karibu Roma na kuanza kugusa kifua chake na vidole vyake kama vile anatafuta uvimbe.
“Acha woga basi , hakuna mtu anaetuona hapa , nadhani ulinielewa nilivyokukonyeza nilimaanisha nakusubiria nje au mpango wako ni kunipotezea siku hizi?”
“Ni kwamba…”Roma alijikuta akishikwa na mshangao na alijiambia kinachokwenda kutokea ni usumbufu , ilionekana huyo mzee aliechukua sura yake licha ya kuonekana mtiifu lakini alikuwa ni muhuni.
Kwa Leiana alionekana yupo tayari kwa ajili ya kufanya ngono na mpenzi wake wa siri lakini upande wa Roma hakuwa na mudi ya kufanya mapenzi na jini kwa mara ya pili..
“Bibie ,,, ninapaswa kupeleka kwanza vidonge kwa mkuu wangu”Aliongea Roma akitafuta namna ya kumkimbia lakini kauli yake ilimfanya Leiana kukasirika kiasi cha kusambaza nguvu za kijini.
“Pumbavu zako unaweza kumdanganya Cheluni lakini sio mimi , Anjiu amejifungia kwa siku nyingi akiendelea na mafunzo na hajawahi kutoka nje anakuagiza vipi vidonge , hii sio mara yako ya kwanza kutumia janja ya aina moja kuiba vidonge , hebu acha maigizo tayari upo kwenye kundi moja na sisi na huwezi kukimbia , usiniambie unataka kunipotezea sasa hivi na kuendelea kuwa mbwa wa familia, kama kweli wewe ni mtiifu na mwaminifu kwanini ukakubali kufanya mapenzi na mimi nilivyokutega ile siku , unataka nimwambie Laofi uongo wako akakusemee , naamini utakufa kabla hata hujajielezea”Aliongea maneno mengi akionekana kukasirika.
Roma alijiuta akishangaa na palepale akili yake ilicheza , ashajua Laofi , marehemu Lao Mtumishi , Leiana na pengine Zianji wote ni kundi moja.
Anjiu ndio sehemu ya master kumi mwenye nguvu katika miliki yote ya kijini lakini nani angeamini kama familia yake yote inamsaliti.
Kutokana na meneno ya Leiana Roma aliona ni ngumu kumkataa kwa nguvu kwani hakuwa na sababu na juhudi zake zote hizo alizofanya zingekuwa bure.
“Bibie acha zako , najua nini cha kufanya”Aliongea Roma
“Mhmh … bora unajua “Aliongea huku akiweka uso wake kama vile anatia huruma , uwezo wake wa kubadilika kihisia ulikuwa mkubwa mno kuliko hata spidi ya kufunua kurasa ya kitabu , alikua na kila sifa mara awe kama vile ni mtoto wa darasa la saba , mara awe mtu mzima , muda mwingine awe mama.
“Nilijua unataka kuniacha mara baada ya kuona uchi wangu , hivi unajua ni kwa kiasi gani ningeumia , tafadhari usinifanyie hivyo tena”Aliongea huku akishika sura ya Mtumishi feki kwa kuiparaza kistaarabu kabisa huku akirembua macho yake.
Roma aliishia kumeza mate hakuwa akimtamani licha ya kwamba alikuwa mzuri na hakutegemea tokea mwanzo wawili hao kuwa na mahusiano ya kimapenzi licha ya kwamba Leiana ni mke wa mkuu wake, Roma alijiambia huku sio ujinini bali ni mitaa ya madanguro.
Hata hivyo Roma aliamini uwezo wake wa kuigiza uhusika wa mtu mwingine na mara baada ya kuthibitisha hakuna anaewaangalia palepale alimshika mrembo Leiana kiuno na kutokana na gauni lake kuwa jepesi alikuwa akihisi ulaini wa ngozi yake.
“Hehe … hatimae mtumishi amegeuka mtundu”Aliongea huku akipiga kibao mkono wa Roma kimahaba.
“Wewe mkorofi hapa sio mahali salama , hebu twende kwenye Banda la Wingumbingu, nina kazi siriasi na wewe usiku huu”
Roma alijiuliza Banda la Wingumbingu ndio wapi , hakuwa na uelewa maana ni mgeni na alijifanyisha tu kwamba anaelewa eneo hilo.
“Hakuna tatizo mrembo wangu , wewe tangulia na
nitakufuatisha”Aliongea
“Unajifanya upo makini , unajua tunapaswa kwenda kila mtu kivyake lakini kwa leo haina haja maana Anjiu amejifungia kuendelea kuvuna nishati , hana muda wa kutusumbua”Aliongea na palepale alipaa kuelekea upande wa mashariki.
Roma alifuata nyuma nyuma kwa spidi ya kawaida na ilikuwa ngumu kuonekana kwani kulikuwa na giza.
Haikupita hata nusu dakika waliweza kufika eneo ambalo ndio kuna banda linaloitwa Wingumbingu.
Ni kama Gazebo mtindo wa nyumba iliojengwa kwa kutumia mianzi katikati ya bwawa , usanifu wake ulikuwa ni ule wa kawaida na kuzunguka eneo hilo kulikuwa na maua mengi sana ya kupendeza ilionyesha dhahiri ni eneo la mapumziko..
Ilikuwa ni sawa kuwepo kwa maneno kama hayo , isitoshe ulimwengu wa kijini una eneo kubwa kuliko wakazi wake.
Mara baada ya kuingia ndani , Leiana alimrukia Roma na kuanza kubusu lipsi zake kwa pupa bila ya kujali ndevu za Lao mtumishi.
Baada ya kuanza shambulizi kwa kuweka ulimi wake ndani ya midomo ya Roma alianza kutoa miguno ya kimahaba na kumfanya Roma kuona majini wana hisia kali kuliko hata binadamu kwani mara ya mwisho wakati akiwa na jini Manyani hata yeye ndio alienzisha mashamblizi.
Roma alijiambia leo tena ameletwa eneo hilo kwa nguvu kwa ajili ya kufanyishwa ngono na jini lenye umri zaidi ya miaka mia , alijiambia au ni kwamba Mungu anaelewa hobi yake sana ndio maana anajitahidi kumbariki.
Lakini Roma akili yake ilikuwa ikimuwaza Rufi tu kwa wakati huo , ijapokuwa Leiana alikuwa mrembo lakini hakuwa tayari kufanya nae chochote.
Muda huo Roma aligundua eneo hilo ni mbali kutoka makazi na kama angeamua kumuua huyo mwanamke katika eneo hilo basi ingekuwa ni rahisi bila hata ya kushitukiwa na kisha kwenda kumtafuta Laofi.
Dakika hio hio wakati akiwaza hatua ya pili ya kuchukua , Leiana aliacha kile alichokifanya na kuanza kulamba lipsi za Roma.
“Wewe mtukutu tutatulia kwanza kwasasa , watafika muda si mrefu , nitakuhudumia baada ya biashara yetu kuisha”
Maneno hayo yalimfanya Roma kushangaa ndani kwa ndani , na kujiambia inamaana kuna wengine wanaokuja ndani ya eneo hilo na ndio maana akasema kuna biashara ya siriasi , lakini alijisikia vizuri na alitamani Laofi ndio awe anafika bila kukosa ili mpango wake uwe mwepesi.
SEHEMU YA 717.
Hazikupita dakika hata mbili tayari Roma alihisi ongezeko la nguvu za kijini katika eneo hilo na mkandamizo wao ulimfanya kujua mmoja wapo alikuwa katika levo ya maji ya upako katikati na mwingine alikuwa mwanzoni pia mwa levo ya maji ya upako.
Ilikuwa ni kama alivyotamani iwe , kwani jini mwenye maringo Laofi alievalia joho staili ya wachina wanapofunga ndoa maarfu kwa jina la Chanqsan , alikuwa ametangulizana na Zianji ambaye yeye alivalia joho staili ya kanzu nyeupe iliofungwa na mshipi kiunoni kama Shemasi.
Roma alianza kusitasita , na kujiambia majini wa levo ya maji ya upako kwa wakati mmoja ndio wamefika , umbali kati ya eneo hilo na ngome ya familia ya mkuu wa majini ni karibu sana.
“Kama nitapigana nao hapa sidhani kama nitawaua mara moja , vipi kama mmoja akipigana na mimi na mwingine kukimbia kuomba msaada nitakuwa nimekwisha , nadhani sina jinsi zaidi ya kusubiri na kutafuta nafasi ya kumtoa jini Laofi ndani ya hili eneo kwenda mbali na kisha kumuua”Aliwaza Roma.
“Hahaha… nadhani tumekuja muda mbaya na kuharibu mnachokifanya na Mtumishi wetu”Aliongea Laofi huku akiingia kwenye kijumba hicho.
Leiana alitoa tabasamu murua na palepale alijirusha na kwenda kutua kwenye kifua cha Mzee Guru Laofi na kujikunja kama vile hana mfupa.
“Ndio kwamba Mzee Guru umeshikwa na wivu?”
“Vipi kama nikisema ndio , utakuwa na furaha?”Aliongea huku akitoa tabasamu la kifedhuli huku utukutu ukijioneysha kupitia macho yake na palepale alipeleka mkono wake na kuanza kuminya maembe dodo ya Leiana.
Upande wa Zianji mara baada ya kuingia ndani ya eneo hilo hakuonyesha mshangao ni kama vile hakuwa akijali kinachoendelea.
Yaani alivyomwangalia shemeni yake ni kama vile anaangalia mwanamke kahaba.
Roma kila kilichokuwa kikiendelea hapo ndani hakujua acheke au alie , ilionekana Zianji sio tu kwamba Laofi alikuwa chini yake lakini pia Mtumishi marehemu alikuwa chini yake kutokana na kuwatunzia siri.
Sasa Roma alijiuliza imekuwaje Anjiu jini mkuu wa miliki ya Xia kushindwa kuelewa kinacheondelea au ni kwamba wapo vizuri katika kuigiza au alikuwa bize sana na maswala ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
“Vizuri hebu tuingieni kwenye maswala ya siriasi ya biashara zetu kwanza na baada ya hapo nitamla huyu horny b**tch”aliongea Laofi na kisha akamwachia Leiana na kumgeukia Roma.
“Mtumishi maendeleo yanakwendaje kuhusiana na kazi tuliokupatia?”
Roma alijikuta akichanganyikiwa , kazi!, Kazi gani hio hakujua ni kazi gani na aliishia kuonyesha utulivu tu.
“Imekamilika”Aliongea.
Ukweli ni kwamba kuigiza katika mazingira hatarishi kama hayo ilikuwa ni ujasiri usiokuwa wa kawaida.
Jini Laofi na jini Zianji wote walionyesha mshangao na kisha kuangaliana mara baada ya kusikia jibu la Roma huku wasiwasi ukionekana kwenye nyuso zao.
“Umemaliza!!? , usituambie umemaliza kutumia damu yote ya mnyama wa kishetani , si nilikueleza mapema kwamba licha ya kwamba ina nguvu kubwa itahitajika siku au mwezi katika kujikusanya mwilini, bila ya kuitumia kidogo kidogo kwa miaka miwili mfululizo haiwezi kuleta athari kwa jini mwenye nguvu kama Anjiu, nilikuelekeza unatakiwa kutumia tone tu la damu ili kuzuia harufu yake , kiasi cha damu tulichokupatia ni kwa matumizi ya miezi mwili mitatu hivi kwanini umeharakisha kuimaliza yote , vipi kama Anjiu akigundua tunamuwekea , juhudi zote zitakwenda na maji”
“Damu ya mnyama wa kishetani!!!?”Swali lilijitokeza katika kichwa cha Roma na palepale alikumbuka maongezi yao kule msituni, alikumbuka pia kimiminika cha damu ya mzee alichokiona katika hifadhi ya Mtumishi Lao.
“Kwahio hio damu ya mnyama wa kishetani kapewa mtumishi Lao kwa ajili ya kumuwekea Anjiu kutokana na ukaribu wao , ni kwamba tu sijui athari zake zikoje”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake.
Roma palepale alibadilisha muonekano wake ili kuonyesha kama alikuwa akitania.
“Msiwe na wasiwasi , nilichokuwa nikimaanisha ni kwamba kazi inaenda vizuri”
Mara baada ya kuongea kauli ile wote watatu walionyesha kuwa na ahueni na Laofi alimsogelea Roma na kumpiga piga begani.
“Endelea kufanya kazi nzuri Mtumishi , tunajua ni ngumu kufanya hila mbele ya Anjiu lakini ndio nafasi yetu ya pekee kummaliza , tunakiasi kidogo tu cha hio damu kutoka Kekexil , ilisemekana ni ya miaka mingi iliopita hivyo inawezekana hiko ndio kiasi kidogo cha mwisho kilichobakia , unatakiwa kuitumia vizuri na mara baada ya Anjiu kutawaliwa na hio damu tutapambana nae na wakati huo tutaweza kumuondoa madarakani , Wewe mtumishi hatimae utaachana na kazi yako ya ukijakazi na kuwa moja ya wazee wanaoheshimika , kizazi chako kijacho hakitakuwa cha vijakazi bali kizazi tukufu”
Kwa haraka haraka masharti hayo yalionekana kweli kuleta tamaa lakini hata hivyo Roma alijua kilichomfanya Mtumishi Lao kumsaliti bosi wake ni kwasababu ya mtego aliowekewa na Leiana , mtego
wa kimapenzi la sivyo asingeweza kumsaliti , mwanamke huyo alikuwa mrembo sana wa kumpagawisha kila mwanaume wa kijini.
“Asantte kwa uungwana wako Guru Mzee , ni heshima kwangu”Aliongea Roma na kumfanya Leiana kubetua mdomo.
“Mtumishi hebu fikiria ulimuona Lahani akikuwa hatua kwa hatua tokea alivyotoka Palao na anakuchukulia kama babu yake na mara baada ya Anjiu kufariki Lahani atachukua madaraka , je si na wewe cheo chako moja kwa moja kitapanda?”
Roma alitabasamu na kumwangalia jini huyo , hakushangaa matendo yake kumbe yote hayo anafanya kwa ajili ya kumfanya mtoto wake kuwa na cheo kikubwa , lakini hata kama Lahani atakuwa na cheo moja kwa moja atakuwa kama kiongozi kivuli tu na nyuma ya pazia watakao ongoza miliki hio ni Laofi na Zianjji.
“Ukweli ni kwamba Mtumishi nimekuitia hapa kwa sababu nyingine , ninatamani unisaidie kupata taarifa kwa ajili yangu”Aliongea Laofi.
“Nipe maagizo yako Guru”Aliongea Roma.
“Siku chache zilizopita mara baada ya wewe kwenda kumkamata Rufi pamoja na Lahani huko duniani , Anjiu alimwita kiongozi wa koo ya Wang , jini
Wang Mian hapa makao makuu baada ya hapo Wang Mian alimchukua binti yake na kwenda nae ulimwengu wa kawaida lakini sijui kuna kipi kinaendelea , wala sababu ya kwenda ulimwengu wa kawaida ni ipi”Aliongea Laofi.
Roma alijifanyisha kushangaa pia lakini palepale sasa alikuja kugundua nini kilichotokea.
Kwahio kitendo kile cha kumfanya yeye kwenda kutoa andiko lake la urejesho ulikuwa ni mpango wa Jini Anjiu na mtu aliekutana nae ndio jini aliefahamika kwa jina la Wang Mian.
Roma aliijiuliza kama ni hivyo kwahio kupotea kwa mtoto wa Master wake Magdalena ilimaanisha amerudi huku ujinini , lakini kama walidanganya kwanini alikuwa na kitu ambacho kilimtambbulisha kwa Tang Luyi , yaani kile kidani, lakini pia kwanini amepotea bila ya kuaga, kuna mpango gani unaendelea ndani ya hio miliki mpaka kufanya janja hio ili tu kupata andiko lake.
“Wasiwasi wetu ni kwamba tukio lile linahusiana na binti yake XiaoXiao mtoto wa binadamu mwanamke kutoka ulimwengu wa kawaida , kitu pekee ambacho kinamuunganisha Anjiu na ulimwengu wa kawaida ni binti yake na mwanamke binadamu aliemzalia mtoto , ijapokuwa hadhi yake ni ya chini lakini bado ni mtoto wa Anjiu , likija swala la kurithi kiti cha mfalme na yeye pia anayo nafasi ili mradi tu Anjiu
awe na uthibitisho mama yake alikuwa ni bikra na hana makando makando mengine”
“Kuongezea , baada ya Xiao kurudi kutoka duniani uwezo wake wa kijini uliongezeka kwa kasi mno , nadhani kuna mambo mengi ameweza kjifunza alivyokuwa ulimwengu wa kawaida na kipaji chake ni kizuri na hahitaji kidonge kuweza kuingia levo ya nafsi , tukio hili limewafanya baraza la wazee kumwangalia Xiaoxiao kwa ukaribu zaidi , kama atafanikiwa kupata ufunuo wasiwawasi wetu Gurusi Mkuu lazima atamwangalia kwa jicho lingine na kama Anjiu akifa bado kutakuwa na usumbufu wa nani arithi kutokana na uwepo wake…”Aliongea Leiana kwa kirefu.
Roma alishangaa kidogo alikuwa akikumbuka siku ya kwanza mara baada ya kufanya maongezi na Xiaoxiao chini Tanzania katika fukwe ya Kawe alimwambia alikuwa Tanzania kwa ajili ya kumtafuta mama yake ambaye ni binadamu kutoka Afrika, ukiachana na hayo pia alikuwa na hasira na Xiaoxiao kwa kuamini pengine ndie alivujisha taarifa ya uwepo wa Rufi nchini Tanzania
Kwa haraka haraka aliona pengine XiaoXiao ana kipaji kikubwa cha akili ndio maana uwezo wake unapanda kwa haraka lakini alimshusha vyeo kutokana na tukio la Rufi kutekwa.
“Kama ni hivyo Guru na Master Zianji ni kipi ambacho mnataka nifanye?”
“Ni rahisi sana , tunachotaka kujua ni kitu gani Anjiu amemwambia Wang na binti yake kufanya , wewe ndio mtu wake wa karibu nina uhakika atakuambia kitu , kama utafeli unaweza kutumia cheo chako cha utumishi na kwenda kuongea na kiongozi wa familia ya wang , tunachotaka kujua ni ubini wa mama yake XiaoXiao katika ulimwengu wa kawaida na baada ya hapo ndio tutajua namna ya kudili nae , kama ni mwanamke kicheche tutaachana nae lakini kama ni mwanamke ambaye anacheo huko duniani tutahitajika kufanya kitu”
Roma palepale mawazo yake yalikuwa wazi sasa , kwahio ilimaanisha XiaoXiao mama yake mzazi sio Mwafrika kama alivyoambiwa bali alikuwa ni Master yake Magdalena, Tang Luyi kutoka ngome ya Tang, lakini swali kama ni hivyo vipi kuhusu Wang mian ambaye Tang Luyi alisema ndio mwanaume aliekuwa nae katika mahusiano.
Roma hakuelewa lakini hata hivyo aliona akubaliane na maagizo hayo kwa muda , isitoshe sio kama anaenda kuyafanyia kazi kwani yeye siio mtumishi. “Nimekuelewa nitalifanyia hili kazi nikisharudi”
“Wewe mtukutu haina haja ya kuwa na haraka , nataka kwanza uniahidi utalifanyia hili kazi kwa juhudi zako zote , huyo Chotara ni wa kawaida kuliko dume langu Lahani”Aliongea Leiana huku akiwa mbele ya Roma na kuongea kwa sauti ya kimapozi akitumia mbinu ya ziada kumshawishi Roma mtumishi feki.
Laiti wangelijua mtu wanaeongea nae ni feki , sijui wangelichukuliaje swala hilo, mpaka hapo ilimaanisha Roma alikuwa akijua uchafu wote unaoendelea katika miliki hio.
“Hehe … kwa hali hii nadhani shemeji yangu hawezi kuendelea kuvumilia zaidi”Aliongea Zianji huku akimwangalia Leiana kwa kejeli na kisha alimshikilia na kumrushia kitandani.
“Hey taratibu basi tabia yako kila siku unanifanyia fujo”Aliongea lakini sura yake ilionyesha kuhitaji fujo zenyewe.
Yaani ilionekana wanaume wote watatu walikuwa chini ya himayya yake , anawahonga penzi huku akihakikisha mpango wa kumfanya kijana wake kuwa mrithi unakamilika.
Dakika chache mbele Leiana hakuwa na nguo hata moja mwilini na alipandiwa juu juu na Zianji na kuanza kupelekewa moto , alikuwa na ngozi nyororo mno na kitendo kilichokuwa kikifanyika kilimfanya Roma kuwa na njaa kali.
Lakini hata hivyo alishindwa kuchukua hatua na Laofi ambaye alikuwa pembeni alikuwa akimwangalai kwa wasiwasi.
“Kwanini Mtumishi wetu leo anaonekana kama vile hana mudi”Aliongea Laofi huku akimshika Roma bega.
“Ni kwasababu Master Zianji anaendeleza kazi hivyo sitaki kumwingilia?”Aliongea Roma akijitetea.
“Una matatizo gani wewe leo? , sijawahi kukuona ukiwa na huo upole kwa miaka mitatu yote …. Kwani huyu mwanamke si tunamfanyaga wote watatu kwa pamoja , hebu anza kazi Mtumishi acha mambo yako bwana , unastahili kupata huo utamu , halafu si hobi yako ni kupitia njia ya uwani wewe… sehemu hio ni ya kwako peke yako leo hii haiguswi na mtu”Aliongea Jini Laofi huku akitoa kicheko.
Roma alijikuta akipagwa na kujiuliza kwa mshangao ‘ Njia ya uwani’ , aliona kabisa majini hao walikuwa wanafanana kabisa na binadamu mambo yao.
“Pumbavu inamaana mtumishi Lao yeye alikuwa
akipendelea kumchezea huyo mke wa bosi wake kupitia njia ya uani!!?”
Laofi ambaye alikuwa akitoa kicheko cha furaha alikuwa tayari akisaula na dakika chache mbele alijiunga, staili aliowekwa Leiana ilishangaza pengine bado haijagunduliwa na watenda Dhambi wa dunia kwani licha ya kuingiliwa na watu wawili kwa mpigo lakini njia ya Uwani ilikuwa haijaguswa na kumpa uhuru mtumishi kundelea.s
Leiana mara baada ya kuona upande mwingine hakuna mtu alionyesha kukasirika mno na kumwangalia Roma.
“Wewe mshezi unashangaa shangaa nini , hebu njoo
, inaumiza kusubiri ujue”
Roma alijiambia mwanamke kahaba kama huyo imekuwaje akawa mke wa mkuu wa miliki , Roma licha ya kushangazwa na kitendo hicho lakini hata yeye mwenyewe hakuwahi kuwa mtakatifu na alitoa tabasamu la kifedhuli na kusaula haraka haraka.
“Arghhh… ndugu Mtumishiii… leo yamekuwaje mbona kila kitu chako ni tafauti”Alilalama Leiana mara baada ya ujazo usiokuwa wa kawaida kumwingia.
“Hehe … mambo ya vidonge vya Tinya hayo”Aliongea Roma akijitetea na mwanamke yule aliishia kutingisha kichwa chake tu akionyesha kuridhika.
“Pumbavu zako wewe mshezi, yaani umejipatia vitu vizuri lakini umetuweka gizani”Aliongea Zianji.
Mpambano ambao ulimfanya Roma kujihisi yupo ndotoni ulimalizika ndani ya nusu saa , ukweli ni kwamba Roma alitumia nguvu za kijini kumaliza haraka lakini kwa namna moja ama nyingine hakuchukulia zoezi hilo kama Adhabu , alijipa kisingizio cha kufanya yote hayo kwa ajili ya misheni hivyo ki ufupi ni kwamba aliinjoi.
Mara baada ya kazi kukamilika Leiana alijirusha ziwani na kujishafisha na baada ya hapo kila mtu alirudi katika usiriasi wake kama kawaida na kila mmoja alichukua njia ya kurejea makao makuu .
Roma alifuata nyuma nyuma ya Laofi mpaka ngomeni na mara baada ya Laofi kuachana na Zianji , Roma alizunguka na kwenda kutokea kwa mbele.
Laofi mara baada ya kumuona Roma akija upande wake akiwa na tabasamu alionyesha hali ya kushangaa.
“Kwanini umenifuata mpaka huku , si nilikuambia hatupaswi kukutana mara kwa mara tukiwa wenyewe tu ili kuepuka kushitukiwa kabla ya damu haijaisha , Anjiu mpaka sasa bado ni tishio kwetu”
“Guru nimeona nitumie fursa hii kukualika kwenda kukuonyesha kitu”Aliongea Roma na kumfanya Laofi kushangaa.
“Ni kitu gani kwanini hukuongea kabla hatujarudi?”
“Nakuamini wewe tu ndio maana sikutaka kuongea mbele ya wenzetu”
Laofi hakuwa na tatizo na uongo wake kwasababu
Zianji na Leiana walikuwa na ukaribu wa kindugu na Anjiiu ni rahisi kumuua lakini Laofi yeye alikuwa tofauti alikuwa akimchukia sana Anjiu kwa viwango vya juu.
Hio ni kwasababu Anjiu na baba yake waliiba cheo chake na baba yake kwa hila zao na wao ndio walipaswa kuwa warithi wa kiti cha ukuu wa miliki.
“Niambie ni kitu gani hicho?”Aliongea Laofi huku akikunja sura.
Roma palepale alitoa kidonge cha daraja la juu kabisa kutoka kwenye hifadhi yake , kidonge hicho mara baada ya kutoa kilisambaza nguvu ya kijini isiokuwa ya kawaida na kiling’aa kama vile ni dhahabu iliomulikwa na tochi , ni kidonge ambacho alitengeneza siku ya jana yake kwa kutumia mimea alioba Kekexil na kilikuwa cha ajabu kwani alitumia kanuni ya andiko la Malkia wa Tushani , zawadi ambayo alipatiwa na Aoiline.
“Hicho nii….”Jini Laofi alishindwa hata kuongea vizurf kutokana na hali ya mshangao na mshituko na palepale alisogea na kumpokonya Roma
“Kidonge Poyana!!!, umetoa wapi hiki kidongea , kanuni ya kutengeneza aina ya hivi vidonge imekwisha kupotea miaka mingi iliopita , hakuna kabisa kidonge cha namna hii katika ulimwengu wa kijini , isitoshe ‘pureness’ ya hiki kidonge inaaminika kuwa ni kamilifu, ni kitu cha thamni kubwa ambacho miliki yetu haiwezi kutengeneza”
Ilikuwa ni haki yake kuonyesha mshangao na msisimko huo kwasababu kidonge hicho ndio hutumiwa na majini ambao wanataka kuvuka levo ya nafsi kwenda levo ya Dhiki na sio tu kwamba kinakuvusha lakini pia kinasaidia katika kuhimili maumivu ya Dhiki.
“Siku mbili zilizopita nilienda kukamilisha kazi moja hivi na ndio nilivyokuja kusimama katika ardhi moja ya theruji upande wa kaskazini , kilichonifanya kusimama ni kwamba kipande cha ardhi katika eneo hilo kilikuwa ni cha tofauti kabisa kutokana na ishara ya nguvu za kijini zilizokuwa zikitoka , nguvu yake ya kiroho katika eneo hilo ilikuwa ni ya kutisha na ndio ilinifanya kuanza kutafuta sababau ni nini maana sio kawaida na nilipoangalia ndipo nilipokutana na maboksi ya vidonge , ilionekana ni kama uzio wa ulinzi wa vidonge hivyo ulifungunka na kufanya eneo hilo la hifadhi ya vidonge kuwa wazi , nina uhakika ni hazina ambayo iliachwa na majini wa enzi , sikutaka kuficha hivi vidonge na niliamua tu kuficha katika maeneo ya karibu na ndio nilivyorudi huku kwa haraka kwa ajili ya kukuambia”
“Kweli!!!?”
Jini Laofi alikuwa katika kiwango cha juu cha mshangao , alipatwa na msisimko mno kiasi cha meno yake kucheza , aliona ni kitu ambacho hakiwezekani lakini hakuwa na tatizo la kutokuamni ilihali alikuwa ameshikilia kidonge hicho adimu mikononi mwake .
“Sasa kama ni hivyo kwanini umeamua kuniambia , ungeamua kuficha au kuweka kwenye hifadhi yako na hakuna jini ambae angegundua?”
“Guru Mzee ukweli ni kwamba vidonge hivi sidhani kama vingenisaidia , kipaji changu kipo ukingoni na tayari mimi ni mzee , ninachotamani ni kuona uwezo wako unapanda ili kuwa na nafasi ya kumshinda Mkuu wetu Anjiu , nitaridhika kama nikichukua kiasi kidogoo tu na kuhusu kuviweka katika pete yangu sikuweza kupata huo ujasiri”
Laofi liishia kufumba macho yake kana kwamba anaingia kwenye tafakari na mara baada ya kuwaza hatimae macho yake yalionyesha hali ya tamaa.
Alijiambia kwasababu Lao uwezo wake ni wa chini basi hana mpango wa hila anaomwandalia na hata kama ikiwa hivyo ni rahisi kudili nae.
“Vizuri kama nitaviona kwa macho yangu ninaahidi kukupatia zawadi kubwa…. hehe Mtumishi ongoza njia nikajionee mwenyewe”
Laofi alikuwa ashajua Mtumishi aliekuwa mbele yake ana kasoro, mara nyingi alipenda kujiita Kijakazi mwanajeshi au mfuasi lakini siku hio hakutaja kabisa maneno hayo kama ilivyotabia yake.
Lakini bado nguvu ya Jani la upofu ilikuwa kubwa mnno na hakujua utofauti wowote wa kimaumbile kutoka kwa Roma.
Roma yupo ndani ya mtego wa jini mkuu Anjiu , Laofi na yeye kaingia mtegoni unadhani atachomoka??
.