Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 54

Kutoka Osaka mpaka ilipokuwa kambi iliokuwa ikifahamika kwa jina la Hastiti hapakuwa mbali na chopa ilitumia dakika kumi na tano tu kua angani.

Muda wote ambao Sophie na Shira kuwa angani , walikuwa wakimshangaa Roma ,hawakuwa wakielewa kwanini mtu aliekuwa uchi mbele yao dakika kadhaa nyuma alionekana kuheshimika sana mbele ya Meja Suzuki , lakini pia hawakuwa wakielewa kwanini Meja Suzuki alikuwa akimwita mwanaume aliekuwa mbele yao Hades, walikuwa na maswali mengi yaliokuwa yamewajaa kwenye vichwa vyao , kwao Roma alikuwa akionekana kawaida sana kwenye macho yao na kitu pekee ambacho hakikua cha kawaida kuhusu Roma ni ukubwa wa dudu lake tu, lakini pia hawakuwa wakiamini kama Roma ndio aliowaokoa,Laiti wangeshuhudia mziki alioufanya Roma wakati wakiwa kwenye maboksi wasingekuwa na maswali ya aina hio.

Licha ya Sophie kuwa katika hali mbaya kimavazi , urembo wake haukua umejificha , alionekana kuwa mrembo kweli kiasi kwamba hata kwa Dorisi hakuwa akimfikia , na kwa kumwangalia tu Sophia ni dhahiri kwamba utagundua mmoja ya mzazi wa Sophie ni mwarabu kutokana na nywele zake.

“Kanaonekana kuwa karembo , kwanini muda ule sikuwa nimekaangalia vizuri”Aliwaza Roma wakati wakiwa wanakaribia ilipo kambi ya Hastiti nje kidogo na jiji hili la Osaka.

Chopa ilitua kwa ustadi katika uwanja mdogo wa Hastiti , licha ya uwanja huu kuonekana mdogoi lakini ulikuwa ukitosha kabisa kwa ndege kubwa kutua , ilikuwa yapata saa nane za usiku lakini ndani ya eneo hili ni kama mchana kutokana na taa aina ya ‘Spotlight’ zilizokuwa zimefungwa kwa kuzungushwa eneo zima la kambi kumulika.

Kitendo cha Roma kukanyaga Ardhini tu , alimuona mwanamke akimkimbilia , alikuwa ni Dorisi, aliekuwa kwenye mavazi yake yale yale , licha ya kwamba Roma alikuwa amemuacha akiwa amechomwa sindano ya sumu na Kisu Mvunjiko , lakini hapa alionekana kuwa katika hali ya uzima wa afya.

Roma alijikuta akitabasamu mara baada ya kumuona mrembo Dorisi ,Mrembo huyu alionekana alikuwa na wasiwasi kweli , walikumbatiana na kufanya watu waliokuwa eneo hili wawaangalie kwa macho ya tofauti , huku Shira na Sophia wakiwa ni wenye kushangazwa na uzuri wa Dorisi , licha ya kwamba Sophia alikuwa mzuri lakini alikiri Dorisi alikuwa mzuri.

“Wanaonekana wanapendana sana”Aliwaza Sophie.

“Bebii Dorisi naona umepona”Aliongea Roma huku akiwa na tabasamu kama kawaida yake.

“Nilikuwa na wasiwasi sana , roho ilitaka kunitoka , nilikuwa nikiwaza kama jambo baya likikutokea nitamwambia nini Edna, na mimi nitaishi vipi”

Aliongea Dorisi na kumfanya Roma amkumbuke mke wake Edna , kwani tokea afike Japani hawakuwa ni wenye kuwasiliana hata kwa ujumbe wa meseji , hawakupigiana simu kujuliana hali wanandoa hawa wa mkataba.

Roma alijikuta akijisikia vibaya , licha ya kwamba yeye hakuwa amempigia mke wake simu lakini aliona Edna alipaswa kumpigia yeye , kwani Edna alikuwa na taarifa zote za kile kilichokuwa kikiendelea Japani.

“Hakuna jambo linaweza kunipata Dorisi , hupaswi kuwa na wasiwasi mimi hakuna kiumbe kinachoweza kunidhuru kwenye hii dunia”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi atabasamu , kwa namna ambavyo Roma alikuwa akiongea usingedhania kama ni yule aliekuwa akifanya mambo ya kutisha masaa kadhaa nyuma , huyu alikuwa Roma wa kawaida ambaye mtu yoyote angemuangalia asingeyumbishwa na uwepo wake, kwani alikuwa wa kawaida sana.

“Dadii..” Aliita Sophine mara baada ya kumuona baba yake aliekuwa akiingia ndani ya sehemu hii ya uwanja wa ndege na akamkimbilia na wakakumbatiana huku Sophie akianza kulia kwa kwikwi .

“My Daughter ,I am so Sorry I Could’nt Protect you”Aliongea mzee huyu huku akionekana kujutia kwa kuruhusu tukio la kutekwa kwa mtoto wake , aliona yeye ndio msababishi kwani hakuwa makini na usalama na mtoto wake.

Balozi Ramadhani Shabani alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Japani , alikuwa ni mwanaume ambaye ukimwangalia tu utajua alikuwa na umri usiokuwa ukipungua miaka arobaini hivi , alikuwa ni mwanaume mweusi tii jambo ambalo lilimshangaza Roma , inakuwaje Baba yake Sophia kuwa mweusi sana halafu Sophia kuwa mzuri kiasi hiko , kwani Rangi ya Sophia na ya baba yake havikuwa vikiendana ila Roma alijiambia moyoni huenda Mama yake Sophia ni mweupe , hivyo hakutaka sana kujisumbua na mawazo hayo kwanza ni maswala ambayo hayakuwa yakimhusu.

“Hades naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa kumuokoa mwanangu , sijui ni zawadi gani nikupatie , kwani kama Sophia angepelekwa Korea Kaskazini sijui ningemuangalia vipi mke wangu”

Roma alimwangalia mzee huyu na kwa maneno yake tu alijua huyu mzee watakuwa ni wale wanaoendeshwa na wake zao , wale wanaume wanaopenda kupitiliza ,kiasi kwamba hata wakosee wao mara nyingi ndio wanapiga magoti kuomba msamaha.

“Mzee kama unanishukuru kwa kumuokoa mwanao unaonaje,ukiwa mkwe wangu kabisa” Aliongea Roma na kumfanya Sophia aone aibu na hapohapo akili yake ikakumbuka dudu ya Roma .

“Kuhusu hilo Hades nitalifikiria”.

“Karibu sana Hades , kwenye kambi yetu , na ninafuraha ya kukutana na wewe , naitwa kanali Sotoko”Aliongea bwana mmoja kijana, baada ya kuwasogelea Roma ,Dorisi na Balozi waliokuwa wakisalimiana.

“Ooh!Kanali nafurahi kukufahamu pia na ni vyema umekuja kunipokea , kabla ya mambo mengine kuendelea Kanali nina njaa sio ya kawaida , unaonaje ukitoa amri nifanyiwe mpango wa chakula , kabla hamjanipeleka kuonana na Kapteni Kisu Mvunjiko”

Kanali alitabasamu na kuwapa ishara vijana wake waliokuwa mita kadhaa kutoka alipo yeye na kisha wakaondoka na walionekana walienda kuandaa chakula kama alivyokuwa ameongea Roma , kwani Roma alikuwa akiongea na Afande Sotoko kwa lugha ya kijapani.

Baada ya kama nusu saa kupita ,Roma alikuwa ameshikilia bakuli lake la Tambi. Huku pembeni yake akiwa amesimama mpishi aliekuwa na hotpoti kubwa ambalo lilionekana dakika chache zilizopita lilikuwa limejaa.

Mpishi huyu muda wote aliikuwa ni mwenye kutoa macho ya mshangao kutoka na uwezo wa Roma kula , hakuamini kama hotipoti zima la tambi ambalo amekuwa akizoea kuwekea watu watano lilikuwa linaisha.

Roma baada ya kumaliza bakuli la nne alimwambia mpishi amalizie tambi zilizokuwa kwenye hotpoti , na mpishi alifanya kama alivyoagizwa na baada ya Roma kukabidhiwa bakuli lake , alimwangalia Kanali Sotoko aliekuwa ameketi pembeni kwenye masofa alionekana na yeye ni mwenyekushangazwa na uwezo wa Roma kula chakula kingi halafu anaonekana kawaida , alijiuliza bwana huyu ni mtu au ngombe , ila hakutaka kuonesha kama alikuwa akimfikiria vibaya Hades , kwani alikuwa amepewa maelekezo kutoka uongozi wa juu kumpa heshima.

“Kanali nadhani ni muda wa kunipeleka kwa Kapteni Kisu Mvunjiko nina machache ya kumuuliza”.

“Sir pluto vijana washaandaa utaratibu tayari nasubiria umalizie”

“Nitaenda nakula taratibu Kanali tunaweza kuelekea maana sitaki kupoteza muda , kesho nina safari ya kurudi Tanzania nimemmisi mke wangu”

Aliongea Roma na kumfanya Kanali ashangae , ndio alishangaa kwasababu muda mfupi uliopita Roma alikuwa amekumbatia na kuonyeshana mapenzi kama yote na Dorisi , inakuwaje sasa anamwambia amemmisi mke wake , ila hakutaka kuongea chochote , walinyanyuka na kuelekea nje huku Roma akiwa na Bakuli lake akitembea huku anakula , jambo ambalo liliwafanya wanajeshi waliokuwa kwenye Korido hizi za kambi kumshangaa Roma kwa tabia yake , mshangao wao kwa Roma ni kama heshima..

Wanajeshi waliokuwa na vyeo mbalimbali walikuwa wamejipanga kwa mstari kumuangalia Hades wakati akipita , walikuwa na taarifa zote za ujio wa Hades ndani ya kambi yao na wakaona hio ndio nafasi yao ya kumuona mtu ambaye ana umaarufu mkubwa sana duniani ndani ya majeshi yote , Pluto , Mrithi wa kiti cha mfalme wa Kuzimu na mmiliki wa pete ya Hades.

Ni ndani ya gereza ndani ya kambi hii , Mlango ulifunguliwa na mwanajeshi aliekuwa akihusika na ulinzi na kumruhusu Roma na Kanali Sotoko waingie ,

Kapteni Kisu mvunjiko alionekana katika hali ya majeraha mengi mno , alionekana alikuwa amepitia mateso makali sana ndani ya saa chache zilizopita na hata Roma alipoingia hapo ndani , licha ya kwamba alikuwa ni mwenye kuonyesha wasiwasi baada ya kutambua mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni Hades, lakini hakuweza hata kunyanyuka wala kusogea mahali alipokuwa amekaa.

Roma alikaa kwenye kiti kilichokuwa hapo ndani na kuendelea kula Tambi zake bila habari na ndani ya dakika kama tano hivi alikuwa amemaliza na sasa aligeuza shingo yake na kumwangalia Kapteni Kisu Mvunjiko.

“Okey! Kapteni kisu tusipoteze muda , sitaki kuondoka kwenye hili taifa na nikaacha deni nyuma , utaniambia kila kitu na nikishamaliza nisikufiche nitakuua”

“Hades niombe Radhi kwa kuingilia lakini huyu ni mtuhumiwa wetu na mpaka sasa yupo chini ya Jeshi tunakuruhusu kumuhoji lakini sio kumuua”.

“Afande kama mnamjali sana Kapteni Kisu hapa mimi sina shida , ila mimi bila ya kuua ndani ya taifa hili siondoki , sitaki kudaiwa na sitaki kumdai mtu , mimi nchi yenu nawadai kifo cha Kapteni kisu , ila kama kwenu Kapteni kisu ni muhimu nitafutieni mwanajeshi yoyote hapa kambini nimuue na deni langu litakuwa limeisha” Afande Sotoko alijikuta akitoa jasho .

“Hades sio kwamba tunaumuhimu sana na Kapteni Kisu , ila tokea tulipoanza kumuhoji hakuna ukweli wowote ambao ameongea mpaka sasa”

“Sasa kama shida ni hio kwanini uwe na wasiwasi , nitamfanya atapike kila kitu hapa kama unachukua kalamu na karatasi andaa kabisa na nikimaliza nitamuua”

Kanali Sotoko aliona hakuwa na maamuzi ya mwisho juu ya swala hilo , aliona kwanza awasiliane na wakuu wake na alifanya hivyo kwa kutoka nje , huku Roma akibakia na Kapteni kisu Mvunjiko.

“Kapteni kisu usiwe na wasiwasi nitahakikisha kifo chako kutokuwa cha maumivu kama utaniambia mwenyewe kila kitu na usije ukafikiria kunidanganya maana nina mbinu nyingi za kujua ukweli sawa”Aliongea Roma huku akimgusagusa nywele Kapteni Kisu kama mtoto ambaye anabembelezwa alale .

Kapteni kisu alimwangalia Roma kwa wasiwasi mkubwa sana, lakini licha ya kuwa na woga alijiambia katika nafsi yake hatoongea ukweli wowote na yupo radhi kufa.

Baada ya dakika tatu Afande Sotoko alirudi.

“Nipe ripoti Afande mnaniruhusu nimuue au mtanipatia mwanajeshi yoyote cheo cha kapteni nitulize kiu yangu na tumalizane nirudi zangu kwa mke wangu?”Aliuliza Roma.

“Hades Mkuu wa majeshi kakupa nafasi ya kufanya kile unachotaka kufanya ilimradi Kapteni kusu mvunjiko atapike siri zote”.Roma alitabasamu.

“Okey! Kapteni kisu nadhani ushasikia mwenywe kutoka kwa Kapteni , sasa hivi mimi ni kama Mungu kwako , ninaweza kukuweka hai na ninaweza pia kuruhusu kifo chako , lakini pia ninaweza kukupa kifo cha maumivu lakini pia ninaweza kukupatia kifo kisichokuwa na maumivu katika chaguzi unatakiwa kuchagua vitu viwili tu kifo cha maumivu au kifo ambacho sio cha maumivu”

“Naomba uniue tu siwezi kuongea chochote”.

“Nina asilimia mia moja wewe ni shushu kutoka Korea Kaskazinina huenda wewe ni sehemu ya jeshi lao na sifa ya kipuuzi ambayo wanaaminishwa dunia ni kwamba , wanajeshi wa Korea Kaskazini mnajua kuvumilia mateso ya aina yoyote, hio sifa kwangu ni ya kipuuzi na nikwambie tu huwezi kuvumilia mateso ambayo nitakupatia”Aliongea Roma na Kisu mvunjiko licha ya maneno hayo hakuonekana kuyumba kwa aina yoyote ile alijiambia kwenye nafsi yake hizo Zote ni tambo za Hades na haongei chochote.
 
SEHEMUYA 55

YOKOTA AIR BASE-JAPAN

Ni ndani ya makao makuu ya jeshi la anga la Marekani nchini Japani , ndani ya ukumbi mkubwa uliozoeleka kwa kufanyia mikutano , alionekana mkuu wa majeshi wa Japani na maafisa wakuu wa jeshi la Japani na wa Marekani wakiwa wamezunguka meza kubwa, na kwa namna ambavyo wamekaa walionekana kuwa na kikao ambacho kinaendelea.

Mbele kabisa ya meza kulikuwa na Skrini kubwa ambayo ilikuwa ikionyesha chumba cha mahojiano moja kwa moja kutoka Hastiti , huku pembeni akiwa amesimama mzungu mmoja ambae ameshikilia Tablet(kishikwambi) yake , huku maafisa hawa wakiwa wanamuangalia bwana huyu ambaye amevalia nguo za kawaida tofauti na watu wote waliokuwa ndani ya chumba.

“Naitwa Meja Stanlaus Homer , nipo hapa kwa ajili ya kutoa maelekezo ya kile kinachoendelea katika chumba cha mahojiano kutoka kambi ya Hastiti, mahojiano ambayo yatakwenda kufanywa na Hades , hii ni fursa kwetu hapa kujua aina ya mateso ambayo Hades hutumia pale anapomhoji adui , nitaelezea kwa kila kitu kitakacho kuwa kinaendelea”

Aliongea Meja Stanlaus huku akionekana kujiamini, alionekana alikuwa ameshiba taarifa ambazo zinamhusu Hades, na baada ya kutoa utambulisho huo mfupi aliruhusu sauti ya Hades kusikika ndani ya chumba hiki huku maafisa hawa wakiangalia kile kinachoendelea.

“Kapteni kisu , unajua kwanini naitwa King Of hell?”Kapteni Kisu hakuongea chochote.

“Ni kwasababu kila kiumbe kinachokufa kinakuwa chini ya utawala wangu, na kwasababu mimi ni Mungu wa kuzimu vilevile ninaweza nikakataa baadhi ya raia , hivyo hata wewe hapa ninaweza nikakuua kwenye huu ulimwengu unaoonekana kwa mateso makali na nikakukataa kwenye ulimwengu wa kuzimu … kwa hio utakuwa unakufa na kufufuka , ni rahisi kukuambia nitakutesa mpaka ufe halafu na kufufua tena nakutesa unakufa nakufufua tena”Aliongea Roma na kufanya maafisa wa jeshi watabasamu kwa biti hilo.

“Kwa hio Kapteni nieleze ukweli wote nikupe kifo cha kistaarabu ujistukie tu upo kuzimu , au nikupe kifo cha maumivu ambacho nitahakikisha ukiwa kuzimu bado unahisi maumivu”

“Niue siwezi kuongea chochote”

Aliongea Kapteni kisu mvunjiko na Roma akatabasamu na kisha akamsogelea na kumuingizia vidole viwili masikioni na kuanza kumminya kwa nguvu , na kadiri ambavyo Roma alikuwa akimminya ndivyo kapteni alivyoanza kutoa kilio , alionekana kuhisi maumivu makali sana kiasi kwamba alitoa ukulele , lakini bwana huyu bado hakuonyesha kuongea na Roma pia hakuonyesha kuacha na alijikuta akizimia kwa maumivu na Roma akamuwekea viganja mashavuni kwa sekunde kumi na akashituka tena na maafisa wa jeshi wakamgeukia Stanlausi , walionekana walikuwa wakitaka maelezo.

“Hiyo inaitwa ‘Endless Energy Restoration’ ni nguvu inayopatikana kati ya mbingu na ardhi kwa kufanya ‘Meditation’ na hii nguvu Hades aliipatia wakati akiwa kwenye mafunzo ya ‘Martial Art’ kwenye Shaolini Tempo za kichina , ni Hades pekee ambae ameweza kufikia mzunguko wa juu wa kufyonza nguvu hii inayozalishwa kati ya mbingu na ardhi na hili ndio jambo ambalo linamfanya Hades kuwa tishio kwa ‘Master’ wote wa mafunzo ya kimapigano wa matempo ya kichina,na mpaka sasa hakuna ‘Master’ yoyote kutoka China anaeweza kupigana na Hades kwa nguvu za kichawi na ‘Martial Art’”Aliongea na kuwafanya washangae na kuendelea anachokifanya Hades.

Licha ya mateso makali ambayo Kapteni Kisu alikuwa akifanyiwa na Roma hakuwa tayari kuongea na hili lilimshangaza Roma mwenyewe na mpaka akajiuliza kuna sababu gani ya mtu huyu kuwa na moyo mgumu kiasi cha kuvumilia mateso yake , lakini licha ya ugumu huo wa Kapteni Kisu hakukubali kushindwa.

“Ngoja kwanza nimpeleke kuzimu , akikutana na wafu ataongea tu”

Aliwaza Roma na kisha akamuwekea vidole kwa mara nyingine na hapa ndipo Kapteni Kisu alivyoanza kutetema , alionekana akiwa akishindana na kifo na uhai , lakini licha ya mateso hayo hakuwa tayari kuongea , alitamani kufa, na zilichukua sekunde therathinni tu , alinyooosha miguu na kukakamaa na alionekana amekufa , na hili swala liliwafanya maafisa hawa wa jeshi kutoa macho kwa mshangao.

“Sh**t sisi ni wapumbavu tumeacha amemuua , haya sasa tumekosa taarifa muhimu sana kwa jeshi letu,tutakuwa jeshi la kwanza duniani kwa kuwa wapuuzi”

“ Brigedia Shomboto kaa chini tuliza mshono Alah!”Aliongea Mkuu wa majeshi kwa hasira na alionekana hakupendezwa na uropokaji wa Brigedia Shomboto.

Roma baada ya kutulia dakika mbili aliona hizo zinatosha sana kwa Kisu Mvunjiko kuiona kuzimu , alimuwekea viganja tena na baada ya dakika tano ,Kapteni kisu mvunjiko alishituka tena , huku akionekana ni mtu ambaye kama alikuwa akikimbizwa ndotoni , kwani alikuwa akihema mno.

“Hehe…. Kapteni nadhani umepaona palivyo?”

‘Naomba usiniue tafadhari nipo tayari kuongea”. Roma alitabasamu nakuona Zoezi lake limefanikiwa

Maafisa wa jeshi wakamgeukia Meja Stanlausi , walionekana kutaka maelezo ya kile kilichotokea.

“Hapo Hades amempeleka katika falme yake ambayo haionekani kwa macho(realm) na anachokifanya ni kumuingizia nguvu ya kimiujiza mtu na kufanya viungo vyote vya mwili kupoteza mawasiliano na mtu kuonekana kama amekufa lakini akili ya mtu ikiendelea kufanya kazi , unaweza ukashangaa ni kwanini hili linawezekana, ila jibu ni kwamba Hades ana nguvu nyingine aliopata kutoka kwa mfalme Pluto , nguvu hio inaitwa ‘Divinity of light’ hii ni nguvu ambayo inampa uwezo wa kumfanya mtu akili yake kufanya kazi wakati akiwa amekufa, sasa baada ya Hades kuua mawasiliano ya viungo vyote vya mwili ,sasa Hades kwa kutumia ‘Divinity of Light’ anaweza kuifanya akili yako kuwa katika falme yake(realm) na kwa jinsi nilivyoona kwa Kapteni kisu ni dhahiri Hades alimpeleka sehemu zinazotisha katika falme yake”Aliongea na kuwafanya maafisa hawa kushangaa na kujiuliza Hades katoa wapi mambo yote hayo.

“Ongea kwanza kapteni , umekuwa mtu wa kwanza kuvumilia mateso yangu kwa muda mrefu mpaka nikakupelea kutalii kuzimu na kurudi”.

Kapteni Kisu alionyesha uwoga wa hali ya juu kiasi kwamba aliwafanya maafisa hawa wa jeshi waangaliane ,unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba wakuu hawa wajeshi walikuwa Tokyo Okinawa na Hades alikuwa Honshu –Osaka Hastiti Military base.

“Naipenda sana nchi yangu ya Japani, lakini licha ya kuipenda hii nchi nampenda Zaidi mtoto wangu , yote nimefanya kwa ajili ya kumuokoa mtoto wangu”Aliongea Kisu kwa hali ya huzuni huku akianza kububujikwa na machozi.

“Mtoto wangu wa kike kashikiliwa nchini Korea Kaskazini na nimefanya yote ili kumuokoa asije akanyongwa”

Hapa ndani maafisa wote walishangaa ,Kapteni Kisu alionekana kuwa kwenye maumivu mengi , aliangalia juu dalini.

“Kihoi mwanangu naomba unisamehe baba yako , najua nitakaposema haya yote ndio mwisho wako na wangu …..”

Aliongea kwa masikitiko makubwa na Mkuu wa jeshi pale alitoa maagizo kwa taarifa za kihoi kutafutwa haraka, na muunganiko wa kimajukumu wa jeshi hili ulionekana kuwa vizuri kweli sio kama Tanzania unakuta kutafuta taarifa mtandao uko ‘slow’, kwani ilichukua dakika mbili tu taarifa za Kihoi zilianza kuonekana kwenye Tv hilo la hapo ndani ya chumba cha mikutano , huku Skrini ikigawanywa mara mbili , sehemu ya kulia ni video inayomuonyesha Roma na Kapteni kisu kwenye chumba cha Mahojiano na upande wa pili ni taarifa za Kihoi .

Alikuwa ni msichana mdogo sana mrembo aliekuwa kwenye gauni jeupe, alionekana kuwa na mchanganyiko wa mataifa mawili, yaani Korea na Japani na hii ilimfanya mtoto huyo kuwa mzuri na mabwana hawa walishangazwa na muonekano wa huyo Binti katika picha , kwa maelezo yaliokuwa kwenye Skrini yalisomeka kuwa Kihoiu mama yake ni Raia wa Korea Kaskazini.

“Kwa hio Kapteni ilikuwaje mtoto wako akafika Korea Kaskazini?”Aliuliza Roma

“Mama yake ni raia wa Korea Kaskazini , mwanzoni wakati nakutana na mama yake Kihoi ni nchini Korea Kusini nilipokuwa kwenye misheni maalumu ya kijeshi , na misheni yangu ilinifanya kuonana na Mama yake Kihoi mara kwa mara kutokana na kwamba alikuwa akiuza Bar na uhusiano wetu ndipo ulipoanzia ,tulikula bata sana ndani ya jiji la Seoul mpaka misheni ilipoisha na mimi kurudi hapa nchini ,baada ya miaka mitatu ya kupotezana na mama yake Kihoi ndipo siku moja alinitafuta na kunieleza juu ya uwepo wa mtoto wangu jijini Seoul na akanipatia ‘Anuani namba , nilijaribu kumuuliza yeye yuko wapi , hakujibu na kukata simu na hapo ndipo nilipofanya safari ya kwenda Seoul kumfatilia mtoto wangu , lakini licha ya kufika sehemu husika kama Anuani ilivyoonesha Anuani ambayo alinipatia mama yake Kihoi, sikuweza kumpata nilitumia majirani kuweza kumtafuta , lakini kila aliekuwa akinipa taarifa hazikuwa ni za kueleweka baada ya kutafuta sana nilishindwa kumpata Kihoi na kukata tamaa na ndipo niliporejea nchini , lakini ajabu ni kwamba nilikaa siku tatu tu nikatafutwa na mtu aliejitambulisha kwa jina la Kim Deshen kutoka Korea Kaskazini na kunieleza mama yake Kihoi alikuwa ni ‘Spy’ nchini Korea Kusini na wamegundua kuwa amezaa mtoto akiwa kazini jambo ambalo ni kinyume na sheria na ili kutoa mfano kwa wengine mama yake Kihoi ashanyongwa , huku Kim akiniambia kuwa taarifa nzuri ni kwamba washamrudisha Kihoi na kama anataka asinyongwe kama mama yake inabidi nifanye kile wanachonieleza na hapo ndipo nilipokuwa ‘Spy’ rasmi ndani ya jeshi langu la taifa langu ninalolipenda”Alisimulia Kapteni kisu mkasa wake.

“Okey Kapteni Kisu , stori yako inaonekana kusikitisha sana ila mimi hayo hayanihusu , kifo bado kipo palepale ila kutokana na Kihoi hana hatia ngoja nikusaidie juu ya hilo”Aliongea Roma na kisha akamgeukia Kanali.

“Nahitaji kuongea na mkuu wa Majeshi wa Kotea Kaskazini sasa hivi nadhani jeshi lina namna ya kuwasiliana nae”

Aliongea Roma akiwa siriasi na Kanali alishangaa na kumuona Roma kama Mwehu , lakini palepale Mkuu wa majeshi alitoa amri ya Mkuu wa majeshi wa Korea Kaskazini atafutwe na aunganishwe na Hades, kilikuwa kitendo cha dakika kadhaa tu simu iliunganishwa na makao makuu ya jeshi la Korea Kaskazini

Baada ya simu kupokelewa simu ya Kanali ilitoa mlio na akapokea

“Mpe Hades simu”Na Kanali alimpatia Hades.

“Mnaonekana kufatilia ninachofanya hapa ndani mbwa nyie mnaoniangalia”Aliongea Hades na kisha akaweka simu sikioni.

“Oi! Mjeda ni mimi Hades”

Aliongea Roma na kuwafanya maafisa hawa watoe macho na kujiuliza inakuwaje Roma anaongea na Mkuu wa majeshi wa Korea kaskazini kama mshikaji wake maana mkuu wa majeshi wa Korea kaskazini alikuwa akisifika kwa Roho mbaya ndani ya Korea Kaskazini yote.

“Haha.. !Pacha ni wewe nasikia umeoa…?”.

Roma alionekana kuongea na mkuu wa Majeshi kama mshikaji wake , walioneakna wawili hao kuwa na stori yao iliopelekea kufahamiana.

“Okey! Hades hatutaki kukukasirisha , licha ya kwamba dunia inatuona kama watu wenye roho mbaya lakini sisi tunashukrani kwa kile ulichotufanyia na kwa mtu yoyote ambaye anafanya wema juu ya nchi yetu, kinachotutofautisha sisi na wao ni mtazamo wa kisheria tu hakuna mengine , lakini pia nia yetu ya kujitegemea wametufanya kuwa maadui ,Kihoi ataachwa hai , lakini naamini Hades unajua cha kufanya juu ya taifa letu”.

“Tuko pamoja , swala hili nataka liishe kidemokrasia Zaidi”

“Hakuna shida Hades,Japani hatuna ugomvi nao , ni marafiki wetu wa siri , ila kwenye urafiki kuna kukoseana na kusameheana naamini nitaongea na mkuu wa majeshi na tutayajenga”

Na hapo simu ilikatwa na kile Hades alichoongea na mkuu wa majeshi wa Korea Kaskazini walisikia maafisa hawa kila kitu.

Kapteni aliongea kila kitu na katika mazungumzo yake , alisema Watu wa Dhorua nyekundu walimtishia kumfichua kama shushu kwa jeshi na hapo ndipo walipompa maelekezo ya kutengeneza misheni feki kwa ajili ya kumpeleka Roma kwenda kupambana na Tzeng.

Kuhusu kutekwa kwa Sophia na Shirani , alisema ni swala ambalo hakuwa akilitambua na hakuhusika nalo na haikueleweka kwanini walikuwa kwenye hio boti na alionekana kuongea ukweli na Roma akamwamini na swali likabaki ni kwanini Hirashia na Sophie wakatekwa , kwani wanadada hao wote wawili hawakuwa na jambo kubwa ambalo lingekuwa linahitajika kwa Korea Kaskazini , kwani Hirashia alikuwa ni mwimbaji wa nyimbo za kitamaduni za Japani na Sophie na yeye alikuwa ni msaanii pia wa nyimo za kileo, lakini pia licha ya hivyo jeshi la Korea Kaskazini walionesha kutokuhusika na jambo hilo.

Kapteni kisu Mvunjiko alihukumiwa na Hades kwa kukiuka sheria namba moja ya Hades ya kutumia watu wake wakaribu kumpata na kwa mtu yoyote anaevunja sharia kwa Hades hakuwa na huruma kwa watu hao na adhabu yake kubwa ni kifo.



******

Ni siku nyingine kabisa Roma akiwa na Dorisi , walionekana kuwa ndani ya ndege kubwa ya kifahari ‘Private’ ambayo ilikua ikiwarudisha Tanzania na Ndege hii ilikuwa imetolewa na Serikali ya Japani kwa ajili ya kuwarudisha kutokana na mchango wa Hades kumuokoa mtoto wa waziri mkuu Shirani.

Roma licha ya kwamba mke wake hakuwa amemtafurta tokea aingie Japani na sasa anarudi , katika moyo wake alikuwa amemkumbuka mno , licha ya kwamba alikaa siku tatu japani , lakini kwake ilikuwa kama ni Mwezi , alitamani sana kumuona Edna hakuelewa kwanini amemmisi hivyo.

Safari ilikuwa ni kama ndoto kwa Dorisi , hakika hakuwahi kuwaza atakuja kutumia ndege kubwa ya kifahari kama hio kwenye maisha yake , alitamani safari isiishe aenendelee kubaki na Roma.

Mwanadada huyu alionekana kuwa na huzuni , kwani alijua Roma anarudi kwenye mikono ya mke wake na sasa kuonana kwao kutakuwa ni kazini na nafasi za kuchepuka za Roma na ni hapo mpaka amkumbuke.

“Wapendwa wetu mnapaswa kufunga mikanda , tunakaribia kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam”Roma alimwangalia mwanamke huyu mrembo wa kijapani na kisha akafunga mkanda pamoja na Dorisi.

Ni muda wa asubuhi ambao Roma na Dorisi walitoka nje kabisa ya jengo la wageni la uwanja huu, kwa muonekano wa Roma ni kama alikuwa akitokea Bukoba, ila Dorisi alikuwa amependeza mno na Begi lake la kuvuta kiasi kwamba alikuwa kivutio kwa watu waliokuwa eneo hili.

Roma moyo wake uliikuta ukipiga Paah! Baada ya kumuona Edna aliekuwa amependeza mno akiwa anawapungia mkono huku akiwa na miwani ya jua…
 
SEHEMU YA 56

Edna aliekuwa amesimama akiwapungia mkono Dorisi na Roma , alikuwa na hisia ambazo hakuweza kuzielewa mwenyewe , kwani siku kadhaa alionekana kumkumbuka sana Roma na kutamani arudi haraka , licha ya kwamba hakuwa amempigia simu, lakini alitaka kufanya hivyo mara kibao , kila alipokuwa akitaka kupiga aliishia kughaili hakujua ni kwanini kuna nguvu mbili zilizokuwa zikishindana ndani ya moyo wake na kutokana na nguvu ya kutotaka kumpigia Roma kuwa kubwa aliishia kutokumpigia, lakini licha ya hivyo alikuwa akimkumbuka sana na sio yeye tu hata kwa Bi wema walitokea kumkumbuka sana Roma na waliweza kujua umuhimu wake ndani ya nyumba.

“Kwanini akiwa mbali namkumbuka sana na kutamani kumuona , ila akiwa karibu yangu sipendi kumuona tena”Ni mawazo aliokuwa nayo Edna mara baada ya Roma na Dorisi kuwafikia.

“Bebi unaonekana kunimisi mumeo sana , naamini siku nzima tutaitumia kuonesheana mapemzi”

Aliongea Roma huku akiweka tabasamu usoni baada kukumbatiana na Edna alifanya hivyo tu kwasababu Dorisi alikuwa mbele yao ,Edna hakutaka ijulikane kama ndoa yake na Roma ni ya Mkataba na hakuna mapenzi katikati yao , aliona kama ikijulikana Dorisi na wanawake wa Roma wanaweza wakamchukua Roma na ndoa kufa kabla ya muda aliopanga kuachana na Roma .

“Niilikumisi sana”Aliongea Edna kwa aibu za kike , kwake ndio mara ya kwanza kumwambia mwanaume amemmisi.

“Nimekumisi pia mke wangu”Aliongea Roma lakini Edna aliishia kutabasamu tu na Edna alimgeukia sasa Dorisi.

“Dorisi karibuni tena nyumbani na hongereni kwa kufanikisha jambo kubwa kwa kampuni , lakini pia niwape pole kwa kila kitu kilichotokea”.

“Asante Sana , Shukrani ziende pia kwa Roma kwani ndio alifanya kazi yote kwa asilimia kubwa na kama isingekuwa kwa yeye sijui nini kingetokea kwa kampuni”Aliongea Dorisi mbele ya Roma na Edna licha ya kwamba alikuwa akichemka ndani kwa ndani kwa wivu lakini hakutaka kuficha kile anachojiskia,Roma alimwangalia Dorisi na kisha akamkonyeza na akamgeukia mke wake.

“Mke wangu ni zawadi gani umeniandalia kwa mchango wangu kwa kampuni?”.

“Nimekuandalia chakula”Aliongea Edna na kumfanya Dorisi na Roma washangae .

“Hehe..Bebi nadhani kitakuwa kitamu kuliko cha siku ile”Aliongea Roma na Edna hakufurahia neno hilo ni kama alioua Roma alikuwa akimkejeli.

Wakati wakiwa wamesimama wanaongea , mara uliingia msafara wa gari za Raisi Senga ndani ya uwanja huo na kuwafanya Roma ,Dorisi na Edna wasogee pembeni.

“Simamisha gari”Aliongea mheshimiwa Senga na mlinzi wa pembemi alishikilia sikio namna ya kuwasiliana.

“Gari ya mheshimiwa inasimama , narudia gari ya mheshimiwa inasimama na itifaki za kiusalama kwa mheshimiwa zichukukuliwe”

Aliongea afisa usalama huyu na hapohapo gari zilisimama na watu waliokuwa ndani ya hili eneo walikaa pembeni .

Baada ya mheshimiwa kushuka , aliwasogelea Edna ,Roma na Dorisi waliokuwa wamesimama upande wa kushoto.

Na wao baada ya kuona kwamba gari ya mheshimiwa ilisimama kwa ajili ya wao, Edna ndio aliekuwa wa kwanza kumsogelea mheshimiwa huku walinzi na wao wakimtangulia mheshimiwa, afisa usalama hawa walionekana kuwa makini na kazi yao.

“Morning! Mr President”

“Morning Edna nimefurahi kuwaona kabla sijaelekea safairi yangu , nadhani kukutana kwenu ni Baraka kwa safari ninayoendeea”Edna alitabasamu.

“Asante sana mheshimiwa kwa kuona kukutana kwetu ni Baraka , na nakuombea mafanikiio”

“Asante sana Edna”Huku aiwageukia Roma na Dorisi waliokuwa nyuma ya Edna.

“Morning Mr President”Alisalimia Dorisi kwa Heshima.

“Morning Dorisi”aliongea Meshimiwa na kumfanya Dorisi atabasamu na kujisikia vizuri kwa kuitwa kwa jina lake , kwani hakujua kama mheshimiwa alikuwa akimfahamu lakini alishangaa mheshimiwa kamfahamu vipi.

“Mr Roma , nasikia wewe na Dorisi mmekuwa na mchango mkubwa sana kwa Vexto kwa kufanikisha dili nono , niwape hongera sana , mafanikio ya Vexto ni maendeleao ya taifa kwa ujumla , asanteni kwa mara nyingine”

“Mheshimiwa huna haja kunishukuru, mimi sjiafanya kwa ajili ya taifa , nimefanya kumfurahisha mke wangu tu ili azidi kunipenda hayo mengine ni ya ziada”

Aliongea Roma na kumfanya mheshimiwa atabasamu ila Edna alikunja sura alitamani amfinye Roma palepale maana aliona anaongea upuuzi, na hata kwa Dorisi aliona kauli ya Roma haikuwa na maana ila hakutaka kuonesha hali yoyote ya kutokufurahia.

“Mheshimiwa nikutakie safari ya mafanikio kwa ajili ya taifa letu”.

“Asante sana Edna”

Mheshmiwa Senga aliwaacha Edna na yeye akaendelea na safari yake.

“Kabwe nipe ripoti”Aliongea Mheshimiwa mara baada ya kuingia kwenye ndege hii kubwa ya shirika la ATCL.

“Mheshimiwa hii ndio ripoti iliotoka kwa balozi Ramadhani Japani”Aliongea Kabwe huku akimpatia mheshimiwa Senga Kishikwambi na mheshimiwa alianza kuangalia taarifa hio ambayo ilimfanya macho yake kuwa makubwa kwa kuoneysha mashangao.

kwenye Tablet ilikuwa ikionyesha picha mbalimbali za Roma akiwa Kambi ya jeshi Hastiti , lakini kulikuwa na picha ambazo Roma alipiga na mheshimiwa Waziri mkuu wa Japani.

“Kila taarifa ya Roma inayonifikia kila siku inakuwa sio ya kawaida , inanishangaza sana sina taarifa zote zinazomuhusu , hili swala linaniumizakichwa sana Kabwe , hebu jitahidi kuwasiliana na watu wakubwa ndani ya Marekani tuweze kupata mwanga kuhusu huyu mtu”

“Sawa mheshimiwa nitalifanyia kazi”

“Vipi kuna taarifa yoyote ya Dorisi kuwasiliana na baba yake?”.

“Mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote ya Dorisi kuwasiliana na baba yake mheshimiwa , lakini tumegundua kitu ambacho hakipo sawa”.

“Nieleze, hayo mambo ambayo hayapo sawa ndio nayataka”.

“Mheshimiwa Dorisi anatumia ‘Black Card’ kufanyia malipo”

“Hebu elezea vizuri ni kipi hakipo kawaida kabwe”

Kabwe alivuta pumzi na kuona kweli maelezo hayo hayakuwa yanatosha , kwani mheshimiwa Senga licha ya kuwa Raisi wa wananchi wa Tanzania , ila Elimu yake ilikuwa ni ya kufoji vyeti na siri hio waliokuwa wakiijua ndani ya Taifa la Tanzania ni watu wachache sana.

Ndio mheshimiwa Senga aliishia kidato cha sita tu na akarudi nyumbani kwao Songea na kuanza kuuza viazi vya kuaanga, na kwa wananchi wa Songea ukweli ni kwaba hawakua na taarifa za kutosha kuhusu raisi Senga , kwani Senga baada ya kuuza uza Chipsi huko Matalawe Songea baada ya kumaliza kidato cha sita Songea boys, aliondoka na kwenda kusiko julikana na siku ambayo anarudi tena Songea alikuwa na ukwasi mkubwa wa Pesa huku akiwa ameoa mwanamke aliekuwa akifahamika kwa jina la Blandina na mpaka kupata mtoto wao wa kwanza walikuwa wakiishi Songea na hata kampuni ya usafirishaji wa mizigo ilianzia hapo hapo Songea na ndio kampuni ambayo ilimpa utajiri wa haraka kwa kipindi hicho kwani alikuwa akipokea tenda nyingi sana kutokana na umiliki wa magari makubwa aina ya Scania.,

Baada ya mheshimiwa Senga kujiunga ndani ya siasa , watu walishangaa Senga kuwa mhitimu kutoka chuo kikuu katika masomo ya ‘political’ kutoka chuo kikuu cha Syndey Australia kwa ngazi ya Degree(Shahada) na Masters(uzaamili) na vyeti vyake vilikuwa ni halali kabisa.

“Mheshimiwa Black Card ni aina ya kadi ambazo zinatolewa kwa mwaliko maalumu na Benk ya Uswis hapa nchini kupitia tawi la Botswana ,Kwa inavyojulikana duniani kote benki hazijaweka vigezo maalumu vya mtu kupatiwa Black Card, na akaunti ya kibenki kukidhi vigezo hivyo ni kuwa na kiwango cha matumizi ya pesa yasiopungua bilioni mbili za kitanzania”Aliongea Kabwe.

“Kwa hio Kabwe unamaanisha kwamba ni ngumu sana kwa Dorisi kumiliki akaunti hio? ,ijapokua nahisi muunganiko wa Dorisi na The Don hapa nchini , lakini nashindwa kupata uthibitisho Kabwe , ila nina uhakika wa asiliamia mia moja Dorisi ni mtoto wa The Doni”

“Hilo linawezekana kwa Dorisi mheshimiwa”

“Kwa hio mmejaribu kufuatilia mmiliki wa Akaunti ya Dorisi?”

“Ndio mheshimiwa tumejaribu , lakini kutokana na sheria kali za kibenki za Swiss Bank, wamekataa kutupatia taarifa”.

“Endeleeni kumfuatilia kwa karibu sana , nilikuwa nina mpango wa kumuweka karibu kama mchepuko wangu , lakini naona ni hatari Zaidi kwangu , kwani The Doni anaweza kunishitukia mipango yangu mapema na Senior kanishauri juu ya hili na mimi pia nimeona ni jambo jema , na pia hata kama ningefanya hivyo yule mpuuzi anaonekana kumchanganya Dorisi na mapenzi yake feki”aliongea mheshimiwa.

“Sawa mheshimiwa , lakini kwanini tusijaribu kumuuliza Senior kama anaweza kutupatia taarifa zinazomuhusu Roma , yule anakonekeshini kuliko wewe”Aliongea Kabwe.

“Senior amekuwa mgumu sana kunieleza juu ya Taarifa zinazomuhusu Roma na mara nyingi amekuwa wa kuniambia nihakikishe sifanyi jambo lolote kuwa katika upande mbaya na Roma”Kabwe alionekana kumuelewa mheshimiwa na maongezi yao yaliishia pale ndege ilipoanza kupaa mheshimiwa Senga alikuwa akielekea nchini Kenya kwa ziara yake ya siku moja.

“Roma jifunze kuwa na majibu mazuri basi unapoongea , hasa na watu wakubwa duniani , nakuambia hivyo sio kama nimekasirika , lakini itakusaidia sana pale ambapo utahitaji msaada mbao unahiraji Koneksheni , hivyo ndio dunia inavyoenda”

“Mke wangu , wewe usiwe na wasiwasi , na isitoshe sijamjibu vibaya mheshimiwa , nikweli nafanya haya yote kwa ajili yako , wanasiasa siku zote wana maneno matamu matamu kukuvutia lakini kwangu ni tofauti”.

“Lakini hio ndio maana ya siasa , unafikiri mwanasisasa anatakiwa kuongeaje?”

“Mke wangu , najua tumeoana , lakini hujawahi kujua nini napenda na kipi sipendi”

“Kwa hio wewe unapenda nini na kipi hupendi?”

“Hehe.. mke nitajibu nusu ya swali lako , mpaka nijue umenipikia nini?”

“Haya jibu”

“Kwenye mambo ambayo sipendi moja wapo ni wanasiasa ..mwanasiasa siku zote ni mtu muongo na mimi nachukia uongo”

“Unachukia uongo , je wewe husemi uongo?”

“Mimi siwezi kusema uongo ,pasipo na sababu , nitadanganya kwa muda tu lakini nitaishia kwenye kusema , ukweli na nafanya hivyo kama mtu ambae anapaswa kuujua ukweli hatoweza kunielewa hata nikimwambia hivyo , au pale ninapoona hawezi kuhimili ukweli , lakini nitaishia kumwambia ukweli mwisho wa siku”

“Hebu nniambie mpaka sasa tokea tusajili ndoa yetu ambayo hata mwezi haujaisha , je kwenye kipindi cha muda wote tumekuwa mume na mke kihalali ni wanawake wangapi umelala nao?”Aliuliza Edna na wakati huu walikuwa wakikaribia kuingia ndani ya nyuumba yao wanayoishi Kigamboni.

NITAPOSTI SIKU YA JUMAPILI TENA NITAKUWA OFFLINE JF KWA MUDA HUO

ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 72 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]eti roma anaonekana kama vile ametoka bukoba
 
ubarikiwe sana singanojr
 
Shukrani sana Mkuu umefanya jumatano yangu kuwa tulivu kabisaaaaa[emoji4][emoji4][emoji4]
 

.
 
duuuuuh mpka jumapili na mzgo umekolea ivi
 
Dah singanojr mkuu fanya mambo huku naona Alhamis haiendi kabisaaa[emoji58][emoji58][emoji58] tuonee huruma kidogo Mkuu
 
Katika utunzi wa riwaya pendwa nadiriki kusema upele umepata mkunaji. Unatisha mwamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…