SEHEMU YA 145
Ni kwa Zaidi ya dakika kumi na tano alizotumia profesa Clark katika kumpima Roma kwa kutumia CT Scan na ndipo alimpomruhsu kutoka ndani ya mashinne hio ,hakuishia katika vipimo vya aina moja tu bali aliendelea kumpima na baadhi ya vipimo vingine kama vile kuchukua damu yake na kuipima , Profesa Clark alionekana kuwa vizuri katika kazi yake.
“Alright Roma kwa hivi vipimo vya Damu itanichukua muda mpaka kumaliza , ila kwa upande wa Ubongo wako niseme kwamba kuna mabadiliko makubwa sana”
“Mabadiliko kivipi Clark?”
“Uvimbe unaonekana kupungua ukubwa wake , mara ya mwisho kabla ya kurudi Tanzania uvimbe ulikuwa na ukubwa kwa Sentimita tano lakini sasa hivi zimebakia tatu , kwa spidi hii nakadiria baada ya mwaka mmoja huenda ukawa huru na saratani ya ubongo”Aliongea Profesa na kumfanya Roma atabasamu.
“Are you Sure?”
“Yeah unaweza kuangalia mwenyewe ubongo wako unavyofanyakazi”Aliongea huku akimuonesha kwenye skrini namna ubongo wake ulivyokuwa ukionekana.
“Kila siku ninavyoangalia ubongo wako unavyofanya kazi najikuta kushindwa kuzoea”aliongea Profesa na kumfanya Roma amwangalie kwa sekunde kadhaa na kisha kugeukia kwenye Skrini.
“Unadhani nini kimesababisha uvimbe kupungua Clark?”
“Bado sijajua ila mara ya mwisho nilivyokupima kule Japan mpaka leo tena nilivyokupima nimegundua huenda kumesababishwa na aina ya mazingira mapya ambayo unaishi, japo sina uhakika sana, na nitajua Zaidi baada ya kupima viwango vya Homoni vilivyopo kwenye damu yako”Aliongea na kumfanya Roma kutingisha kichwa.
“Clark kuna jambo labda sijawahi kukueleza ila kuna siku niliweza kushindwa kujizuia na nilijikuta nikirudi katika hali yangu ya Zamani lakini jambo la kushangaza ni kwamba Edna baada ya kunikumbatia niliweza kurudi kwenye hali ya kawaida”Aliongea Roma na kumfanya Clark awe na mshangao.
“Unaongea kweli juu ya hilo?”
“Yeah ilikuwa ni siku kuna jamaa mmoja alikuwa akihadithia haya mambo ya Vita na nikamuonya asiendelee na hakunielewa na nilijikuta nikibadilika pasipo ya mimi kupenda na nikwambie tu nilishindwa kabisa kujizuia na kama sio Edna huenda ningeua siku ile”
“Kwahio unamaanisha mkeo ndio alikufanya ukarudi katika hali yako ya kawaida?”
“Yeah kitu kama hicho”Aliongea Roma na kumfanya Profesa Clark kushangaa kidogo na kufikiria kwa wakati mmoja.
“Au huenda ni kwasababu mkeo anafanana na Seventeen ndio maana uliweza kujizuia?”
“Sidhani kabisa Clark, nadhani nishawahi kukuhadithia kwanini Seventeen alijirusha baharini akiwa na ujauzito wangu?”
“Kwasababu kadri alivyokuwa akikusihi uache kuua watu na kuwa mkatili kama mnyama wewe ulizidisha kuua na alivyoona huna mpango wa kuacha roho yako ya kikatili ndio alivyoamua kujirusha baharini akiwa mjamzito”Aliongea Profesa Clark huku akitabasamu , alionekana alikuwa akikumbuka vyema hisrtoria ya Maisha ya Seventeen na Roma.
“Umenikumbusha sana Mbali Clark , najutia sana kumpoteza Seventeen huenda sasa hivi ningekuwa na mtoto wa miaka minne”
“Ni kweli ila yaliopita yashapita na uzuri ni kwamba ushampata Seventeen mwingine”Aliongea huku akitabasamu.
“Sidhani…”Aliongea Roma na kumfanya Clark kushangaa.
“Kwanini unamaanisha hivyo?”
“Ndoa yangu ni ya mkataba”Aliongea Roma huku akisogelea kiti kilichokuwa pembeni na kukaa akiwa amevalia Boksa tu na Clark na yeye alikaa kwenye kiti cha pembeni na Roma alianza kumhadithia namna ambavyo alikutana na Edna.
“Hahahaha……Hahaha..!!!”
“Roma utaniua…jamani mbavu zanguu …”
“Unacheka nini sasa ..?”Aliongea Roma huku na yeye akitabasamu.
“Unajua mara ya kwanza nilivyosikia Ashley ananiambia juu ya wewe kuoa nilishangaa sana, nikasema huenda umeacha tabia yako , maana ninavyokumbuka kipindi ulivyokuwa unakuja Uingereza ulikuwa ukihudumia wanawake kumi na sita kwa wakati mmoja, lakini Stori yako imenifurahisha sana”
“Sehemu gani imekufurahisha Zaidi?”Aliongea Roma huku kikumbuka Maisha yake ya nyuma aliokuwa akiishi , ni kweli kabisa maneno ya Clark alivyokuwa akisema, kwani Roma kwake wanawake kilikuwa kitu cha kawaida sana na kufanya ngono ilikuwa ni kama sehemu ya hitaji lake muhimu kwa siku , alikumbuka namna mbavyo alikuwa akizungukwa na wanawake kibao Zaidi ya kumi na akifanya nao mapenzi kwa wakati mmoja na kuwaridhisha.
“Sehemu ilionifuarahisha Zaidi ni ulipomdhania Edna kama Kahaba na kumuweka begani na kumpeleka Geto , lakini paliponifurahisha Zaidi ni uliponiambia ulivyoona Damu kwenye shuka ukadhani yupo kwenye Period , ninavyomuona mkeo na nikifikiria hilo tukio…hahaha,,Sikufahamu mnahistoria ya aina hio”Aliongea Clark na alionekana kufurahia kweli.
“Yeah ilikuwa hivyo…..”
“Mh!!Ila sidhani kama ni swala ambalo limetokea bahati mbaya Hades”Aliongea na kumfanya Roma ashangae.
“Unamaanisha nini?”
“There is no Such Coincidence ….. huwezi kunidanganya Roma,Naamini kwa asilimia mia moja ulirudi Tanzania ukiwa unafahamu uwepo wa Edna”AliongeaClark na kumfanya Roma atabasamu.
“Haingii akilini kabisa…..kwa nguvu uliokuwa nayo Duniani ni lazima ulipata taarifa ya uwepo wa Edna Tanzania mapema tu na ni moja ya sababu iliokurudisha , huenda pia ulidhania Edna ni Seventeen ndio maana ukarudi Tanzania na juu ya kuitafuta familia yako huenda ikawa ni kisingizio tu ,nakumbuka kabisa ulisema mwili wa Seventeen haukuwahi kuonekana licha ya kwamba alijirusha baharini?”Clark aliongea huku akionekana kama mtu ambaye ana uhakika na maneno yake .. alimwangalia Roma kwa namna ambavyo alikosa majibu ya haraka na kuona maneno yake huenda ya kawa na ukweli kama alivyofikiria.
Mrembo huyu ambaye alikuwa na taaluma kubwa sana, likija swala la kuunganisha mambo alikuwa na uwezo mkubwa sana , hakuweza kuamini Eti Roma alirudi Tanzania na akakutana na mwanamke anaefanana na Seventeen na kisha wakafunga ndoa , kwake hilo halikuwa la kawaida kabisa na alijua fika huenda wakati Roma anaianza safari ya kurejea Tanzania , alikuwa akijua uwepo wa Edna tayari ndani ya taifa la Tanzania.
Kabla Roma hajamjibu Clark juu ya makisio yake simu yake ilianza kuita na akasogelea suruali yake na kuitoa na baada ya kuangalia jina aliona ni Diego.
“Your Majesty! Habari za muda huu?”
“Salama Diego , kuna taarifa gani?”
“Ni juu ya Yan Buwen Mfalme Pluto”
“Nipe Ripoti”
“Tumeweza kumfuatilia kwa ukaribu sana na tukagundua ni kwanini yupo Tanzania”
“Mmegundua nini?”
“Kwanza kabisa tumepata kugundua uwepo wa BSL-4 laboratory”
“BSL 4 lab ndanii ya Tanzania!!?”
“Ndio Mfalme tumeweza kupata faili linalohusiana na uwepo wa maabara hio ya kisasa ndani ya Tanzania kwa kudukua tarakishi ya waziri wa Sayansi na Teknolojia”Roma alijikuta akishangaa na kumwangalia Clark kwa wakati mmoja.
“Diego elezea Zaidi”
“Mfalme jambo ambalo limenifanya tujue huenda ndio nia halisi ya Yan Buen kuwepo Tanzania ni kwamba, mtu aliekuwa akiendesha shughuli zote ndani ya maabara hio ni Profesa Shelukindo na siku ya jana ndani ya makazi ya mheshimiwa kigombola kulikuwa na kikao cha siri sana kilichokuwa kikiendelea , tulishindwa kujua kikao hiko kinahusu nini , lakini wahusika wakuu waliokuwa ndani ya kikao hiko ni Mheshimiwa Kigombpla mwenywe , Mkuu wa majeshi Afande Tozo ,Yan Buwen , IGP wa Tanzania pamoja na Waziri wa Sayansi na tunakisia kikao hiko kinahusiana na kinachoendelea ndani ya maabara hio”
“Kwanini mnakisia hivyo?”
“Kwanza kabisa Mfalme namna ambavyo tuliweza kupata faili linalohusiana na maabara hio ni kupitia tarakishi ya Waziri wa Sayansi na Teknolojia na hio ni baada ya Bram kuweka Kirusi ndani ya tarakishi yake na hii ni baada ya Waziri kutumia Tarakishi yake kufungua faili lililokuwa likihusiana na Maabara hio na jambo la kufurahisha ni kwamba faili hilo lilikuwa limehifadhiwa kwenye ‘Flash Disk’ , na sisi tulitumia mwanya huo kupandikiza kirusi ndani ya Flashi hio”
“Na baada ya kupandikiza kirusi kwanye Flashi mkagundua nini?”
“Flashi hio alikabidhiwa Yan Buwen na hivyo moja kwa moja ndio tukaona huenda kuna jambo linaendelea ndani ya hio maabara , Tumekupigia kutaka kupata maelekezo yako Zaidi “
“Mnafikiria kufanya nini?”
“Tunapanga kuzamia ndani ya hio maabara kwani mpaka sasa tumepata eneo ilipo”Aliongea upande wa pili na kumfanya Roma afikirie kidogo.
“Diego kazi mliofanya mpaka hapo intatosha msiendelee Zaidi”
“Lakini Mfalm…”
“Najua shauku yako Diego ila kinachoendelea kinahusianana mambo ya Anti Matter Energy”Aliongea Roma na kimfanya Diego kutulia kwa dakika na Roma alijua kabisa lazima bwana huyo atakuwa kwenye mshangao.
SEHEMU YA 146
“Diego najua unachofikiria ila kwa sasa nataka ufatilie jambo moja tu”
“Ndio mfalme”
“Fuatilieni mfahamu imekuwaje Tanzania wakaweza kujenga aina hi ya Maabara hapa nchini nataka kujua kama kulikuwa na kibali kutoka Marekani au Umoja wa Mataifa kupitia WHO”
“Sawa Mfalme lakini hio teknolojia kama itaingia kwenye mikono ya watu wabaya haitoleta shida mfalme?”Aliongea Diego na kumfanya Roma atabasamu kidogo.
“Diego Stop Being Greedy ninachotaka mfanye kwa hapa Tanzania ni kufatilia mambo yote yanayohusiana na usalama wa watu wangu wa karibu lakini pia nipate kumjua The Doni ni nani, Mimi sina hofu hata nisikie Urusi imerusha Bomu la nyuklia kwenda Ukraine kama halinihusu kwangu ni la kipuuzi tu na napaswa kupotezea”Aliongea Roma na kisha kukata simu na kumwangalia Clark.
“So Yan Buwen yupo Tanzania kwa ajili ya kupata Tafiti za Profesa Shelukindo?”
“Yeah nina uhakika na hilo , ila sidhani ni juu ya tafiti hizo tu”
“Unamaanisha nini?”
“Inaonekana anapanga kuishi Tanzania kwa muda mrefu Zaidi”Aliongea na Profesa alishangaa kidogo.
“I am Surprised with presence of BSL 4 Lab in Tanzania”
“Nimeshangaa pia hata mimi na ninaamini kwa asilimia moja Marekani inahusika na uwepo wake”Aliongea Roma na Clark pia kutingisha kichwa kukubaliana nae.
Ukisikia BSL 4 kirefu chake ni ‘Biosafety level Four’ sasa Duniani maabara hupewa madaraja kutokana na usalama wake , kuna daraja la kwanza mpaka la nne , hili daraja la nne ndio linaenda kwa jina la ‘BSL 4 labs’ hizi ni maabara ambazo ni chache sana duniani ,na maabara hizi zinahusisha tafiti ambazo ni ‘Deadly’ yaani kwa maneno marahisi ni kwamba zinahusisha tafiti ambazo sio salama kabisa kwa Maisha ya binadamu mfano halisi ni aina ya virusi ambavyo bado havijapatiwa dawa zake hivyo aina hio ya virusi vinahifadhiwa kwenye maabara ya daraja hilo la nne na tafiti zake hufanyika humo , kujenga maabara aina hio ndani ya taifa ni gharama kubwa sana kutokana na teknolojia inayotumika katika maswala ya hewa na mazingira na hii ndio maana Roma akashangaa kuona Tanzania kuwa na aina hii ya maabara ndani ya taifa ambalo halina maendeleo makubwa , kwani maabara hizi kwa dunia zipo kwenye mataifa yalioendelea kama vile Marekani , China , Ufaransa na Australia
******
JULY 2014
Hii ilikuwa ni miaka kadhaa nyuma siku ambayo Mheshimiwa Barrack Mabo alifika Tanzania na kufanya Tanzania kuweka historia ya kutembelewa na kiongozi mkubwa duniani ,sasa usifikiri raisi mkubwa duniani akatoka Marekani mpaka Tanzania kwa ajili ya kutembelea taifa dogo lenye amani kama Tanzania , kuna mambo makubwa sana ambayo yalimleta mheshimiwa huyu Tanzania.
Sasa muda wa saa nne kamili za usiku mheshimiwa Kigombola alikuwa na kikao na mheshimiwa Barrack Mabo ikulu, na hio ni katika mfuliulizo wa vikao hivyo tokea raisi huyu kufika Tanzania.
“Unamjua huyo?”aliuliza Mheshimiwa Barrack huku akimpa mheshimiwa Kigombola picha.
“Yeah huyu ni raia wetu ambaye anaendelea kuiheshimisha Tanzania kimataifa”Aliongea Mheshimiwa Kigombola huku akiangalia picha ya Profesa Shelukindo na kumfanya mheshimiwa Barrack kutabasamu.
“Ni kweli kabisa , huyo naweza kusema ni ‘Recarnation’ ya Mwanasayansi Einstein , licha ya kwamba hamfikii ila kwa uwezo wake huenda akafikia levo zake”Aliongea huku akitabasamu na kunywa mvinyo kidogo uliopo kwenye glasi.
“Ni kweli ila sidhani kama atamfikia Einstein.. tusimpe kichwa Zaidi”aliongea mheshimiwa Kigombola na mkumfanya Mheshimiwa kutabasamu kidogo.
“Ni kweli kabisa ila kwa upande wangu nina mategemeo makubwa kwake na sio mimi tu kwa wadau wote wa mwaswala ya Sayansi wanamategemeo makubwa kutoka kwake na ndio maana napanga kuwekeza nguvu zangu zote kwake”
“Unamaanisha nini mheshimiwa?”
“Najua mpaka sasa hivi unaelewa kuwa The Doni bado antusumbua na kila mara ninavyokumbuka nguvu za huyo mwanaharamu silali kwa amani kabisa , haiwezekani niwe raisi wa taifa kubwa kama Marekani halafu nikatishiwa nguvu na mtu asieonekana”Aliongea kwa hisia kubwa na Mheshimiwa Kigombola na yeye akaungana nae.
“Kigombola Profesa Sheliukondo ndio mtu pekee ambaye anaweza kututoa kwenye kifungo cha muda mrefu”
“Kivipi mheshimiwa kam umeniacha na siamian mtu kama Profesa Shelikindo anaweza kumdhidi The Don”
“Inawezekana kabisa kama tutakuwa na nguvu kubwa kuliko yeye na ndio maana nimekuja Tanzania”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa Kigombola kushangaa.
“Nadhani twende moja kwa moja mheshimiwa nipo kizani”
“Kigombola unachopaswa kunisaidia ni sapoti yako pekee , nina mpango wa kujenga maabara kubwa ya kisasa hapa Tanzania ambayo itagharimu Zaidi ya Dollara milioni ishirini”Aliongea na kumfanya mheshimiwa kushangaa mno.
“Usishangae sana Kigombola nina maanisha ninachokuambia na jambo ninalokuambia hapa litakuwa ni siri na mtu ambaye ataiendesha hii maabara ni Profesa Shelukindo”
“Kwahio unamaanisha Maabara ikiisha Profesa atarudi Tanzania?”
“Ndio atarudi Tanzania kwa kisingizio cha kuachana na maswala ya kitafiti lakini akirudi Tanzania ataendelea kwa siri na kuna jambo kubwa naamini atalitimiza na hilo likitimia ni muda wa sisi kutoka katika vifungo vya The Doni”Aliongea na kumfanya mheshimiwa Kigombola kutabasamu na kuona mheshimiwa anapointi kubwa sana.
“Nitakusapoti katika hili mheshimiwa , nitaandaa mazingira ya eneo”Aliongea mheshimiwa na kumfanya Mheshimiwa Barrack kutabasamu.
“Mpaka sasa hivi nishaandaa mazingira tayari ninachotaka siku chache baada ya mimi kuondoka hapa nchini usaini baadhi ya nyaraka kutoka kwa muwekezaji atakayejitambulisha kwa jina la Malcom”aliongea mheshimiwa Barrack na kumfanya mheshimiwa Kigombola kutingisha kichwa kwa kukubali.
Sasa baada ya siku kadhaa Mheshimiwa kurudi nchini kwake kampuni moja kubwa ya utafiti kutoka Venice Italy inayofahamika kwa jina la INNOVA ikiongozwa na mkurugenzi wake anafahamika kwa jina la Malcom Thadeo ilingia Tanzania.
“Mheshimiwa nimekuja kwa maelekezo ya Mheshimiwa”aliongea Thadeo mara baada ya kupitia hatua zote za ukaribisho ikulu.
“Karibu sana Malcolm unaweza kunipa hizo nyaraka nizipitishie macho kwa dakika kadhaa hatua inayofuatia iendelee”Aliongea Mheshimiwa Kigombola na Malcolm alitoa karatasi na kumpatia mheshimiwa Kigombola na kuanza kuzipitia. Lakini mheshmiwa kadri alivyokuwa akiendelea kusoma alijikuta akishangaa.
“Kwanini mnataka sehemu ambayo ishaanza kujengwa , Da es Salaamu ina maeneo mengi ya wazi ambayo ninaweza kuwapatia , kuna ulazima maabara hii kujengwa sehemu hii?”aliulia Mheshmiwa Kigombola.
“Ndio mheshmiwa , dhumuni kubwa la kutaka sehemu hio ni usalama na usiri wa maabara hii ndani ya Tanzania , tukijenga nje sehemu nyingine itafanya macho ya watu wengi kuelewa kile kinachoendelea”Aliongea Thadeo na kumfanya mheshimiwa awaze kidogo.
“Okey! Nitaidhinisha swala hili hapa hapa , lakini kuhusu kuanza kwa ujenzi nadhani ni mpaka nitakapoweka mambo sawa na kampuni inayohusika na ujenzi wa jengo hili, na inaweza ikachukua siku kadhaa kwa ajjili ya mazungumzo ya kuvunja mkataba , maana jengo hili linakaribia kuisha”
“Hakuna shida kabisa mheshimiwa kwasasa tutasubiria jibu kutoka kwako ili timu yetu ya ujenzi iendelee , kuhusu hilo jengo kama mkataba wetu unavyosema , litaendelea kuwa chini ya serikali lakini Ardhini itakuwa ni mali yetu”Aliongea na kumfanya mheshimiwa kushangaa.
“Nilijua mnataka maabara kuwa kwenye hili jengo kumbe mnataka kujenga kwenda chini?”
“Ndio tutajenga kwenda chini , kama nilivyosema mheshimiwa Project hii ni siri sana na hatua zote za kuifanya ibakie siri zinachukuliwa na ndio maana tutajenga kwenda chini na wakati huo huo jengo likiendelea kumaliziwa kwenda juu , tukikamilisha kazi yetu ya ujenzi basi jengo linaweza likafunguliwa na taratibu zingine za kiserikali ndani ya jengo hilo kuendelea”Aliongea na Mheshimiwa Kigombola kukubaliana nae.
Baada ya siku kadhaa kupita tokea Maongezi ya Malcolm kufanyika ndani ya Ikulu siku ya asubuhi aliingia mwanamama mfanyabiashara mkubwa mrembo , huyu hakuwa mwingine ali alikuwa ni CEO wa kampuni ya VEXTO.
“Karibu sana Rahel”
“Asante sana mheshimiwa nimeshangazwa na wito wako ndani ya ikulu”
“Ni kweli Raheli lakini wewe ni mfanyabiashara mkubwa ambaye taifa linakutegemea , nadhani ni jambo la kawaida kwa mwanasiasa kama mimi kutaka kuonana na wewe”Aliongea huku akitabasamu na Rahel alirudisha tabasamu.
“Rahel niende moja kwa moja ili nisipoteze muda , najua kazi hii ilitakiwa kufanywa na Waziri ila kutokana na ukubwa wa jambo lenyewe ndio maana nimekuita Ofisini”
“Sawa mheshimiwa unaweza kwenda moja kwa moja”Aliongea Raheli kwa kujiamini , siku hii mwanamama huyu alikuwa amevalia suti yake nyeusi na blazia kwa ndani , alikuwa amependeza haswa na kumfanya kuonekana mremnbo Zaidi mbele ya mheshimiwa Kigombola na hata Raisi huyu kuzidi kumtamani kimapenzi , ukweli Mheshimiwa alishatupiga ndoano zake kwa Raheli mara kibao licha ya kujua mwanamama huyo mahusiano yake na Raisi Jeremy wa Rwanda na Raheli alimchomolea Mheshimiwa Kigombola.
Mheshimiwa alichukua faili lililokuwa kwenye meza na kisha akatoa karatasi na kumpatia Raheli na kuanza kusoma na kadri mwanamama huyu alivyokuwa akiendelea kusoma macho yake yaliongezeka ukubwa.
“Mheshimiwa kwanini unataka kuvunja mkataba wakati hakuna kosa lolote ambalo limefanyika kwa upande wangu na isitoshe jengo limekamilika kwa Zaidi ya asilimia sabini na pia tupo ndani ya muda?”
Aliongea CEO Rahel kwa kuweka uso wa usiriasi na Mheshimiwa Kigombola aliona mabadiliko hayo kutoka kwa mwanamam huyo na alichokifanya ni kuwa wakawaida tu , alijua kazi ya kuvunja mkataba ilikuwa ni ngumu kwani ilikuwa ikikiuka vigezo vingi vya kibiashara na ndio maana alijipanga kabla ya kumuita Raheli ofisini kwake ikulu.
“Raheli unaweza usinielewe , lakini jambo ambalo ninakuambia lakini ninaweza kusema kwamba kuna maswala ya kiserikali ambayo ni siri nisizopaswa kuzitoa nadhani wewe ni mfanyabiashara unaelewa ,na kuhusu gharama za kuvunja mkataba zitalipwa mara mbili yake , nadhani itakuwa ni faida mara mbili ya ujenzi mzima wa hili jengo”
“Mheshimiwa ninachozungumzia hapa sio swala la faida kwa kampuni bali ni swala la Taswira ya Kampuni na isitoshe hii karatasi inaelezea wafanyakazi wangu wote kutoendelea kufanya kazi kwenye huu mradi”.
“Kama nilivyokwisha kusema Raheli , kampuni yako ina utendaji mzuri sana na hilo nimeliona , lakini kwakua swala hili linaigusa serikali moja kwa moja , huna budi ya kutii, na Sheria za mkataba siku zote zinaeleweka na serikali imezingatia hilo na tumeamua kuvunja mkataba , sidhani kwamba ni swala ambalo unaweza kukataa Rahel ni maswala ya kibiashara tu”Aliongea Mheshimiwa .
Hivyo ndio ilivyokuwa , licha ya Raheli kutotaka kuvunja mkataba , lakini mwishowe alikubali , asingeweza kupishana kauli na viongozi wa juu wan chi , kwani biashara zake ili zifanikiwe alihitaji sana mhimili na mazingira mazuri ya kuendelea kufanya biashara nchini , lakini licha ya Raheli kukubaliana na mheshimiwa juu ya kuvunja mkataba , mwanamama huyo hakuweza kufurahishwa na jambo hilo na mbaya Zaidi kilichomfanya kukasirika Zaidi ni ni kwamba baada ya kuvunja mkataba ,kampuni yake haikutambulika kama sehemu ya ujenzi wa jengo hilo ambalo lilikuwa kama nembo ndani ya jiji laDa Es Salaam na hili kuikosesha heshima kampuni yake ya ujenzi,
SEHEMU YA 147
Hatimae siku saba zilipita Profesa Clark alikuwa asharudi tayari nchini kwake baada ya kusindikizwa na Roma mpaka uwanja wa ndege.
Roma baada ya kuhakikisha Profesa Clark ashapotelea kwenye macho yake aligeuza na gari yake kuelekea nyumbani, ilikuwa ni siku ya ijumaa hivyo hakutaka kwenda kazini na ukweli pia karibia wiki yote hakuwa ameenda kazini lakini hakusahau pia kutoa taarifa kwa Benadetha.
“Roma usije ukaachana na Edna , inaonekana ni Zaidi ya tiba kwako”Ilikuwa ni kauli ya Profesa Clark wakati wa kuagana na kumshangaza Roma kwani Profesa hakutoa maelezo Zaidi.
Baada ya kufika nyumbani muda huo wa saa tano hakukuwa na mtu na hakushangaa kwani Asubuhi wote walitoka kwa pamoja , Bi wema na Sofphia wakienda kumsaidia Edna kurudi nyumbani na yeye kuelekea uwanja wa nedege kumsindikiza Clark.
Roma hakukaa sana , akiwa eneo la Sebuleni Edna alieongozana na Sophia pamoja na Bi Wema waliingia ,Roma alisalimiana na mke wake kama kawiada.
“Roma naomba tukaongee kwenye chumba changu cha kujisomea”aliongea Edna huku akipandisha ngazi na Roma hakujali sana , alifuata nyuma nyuma mpaka ndani ya chumba ambacho Edna hutumia kusomea na kufanyia baadhi ya kazi zake za kiofisi akiwa nyumbani.
Edna baada ya Roma kuingia ndani , alichukua mkoba wake na kuingiza mkono na kisha akaibuka na ile pete na kisha akamkabidhi Roma.
“Asante imenisaidia sana unaweza sasa kuichukua”Aliongea Edna kwa sauti ya chini.
“Wife nadhani umeshuhudia nguvu ya hio pete , kwanini usikae nayo kwani inaweza ikakusaidia?”
“Hapana siwezi kukaa na kitu ambacho sio cha kwangu”aliongea Edna kwa sauti kavu na kumfanya Roma atoe Tabasamu la uchungu.
“Ushasahau kama sisi tumeoana Edna , kilicho chako ni changu na changu ni cha kwako”Aliongea Roma huku akiwa ametabasamu lakini Edna hakujali maneno yake , ukweli hakuwa tayari kukaa na pete hio kabla hata ya kujua ni kwanini ina nguvu , lakini Edna pia hakutaka kumlazimisha Roma kumwambia historia ya Maisha yake ya nyuma , alitaka Roma atakapotaka mwenyewwe kufanya hivyo ndio asikilize lakini sio kumlazimisha kuongea , kuna muda alikuwa akimini huenda pia kuna sababu Roma hakutaka kumwambia juu ya Maisha yake ya nyuma. Lakini Edna alikuwa na shauku kubwa , alitamani Roma aongee tu , alikuwa akitaka kujua kwanini anaitwa Queen Persephone.
Roma hakuona haja ya kubishana jambo dogo hivyo na Edna , aliamua kupokea pete hio , kwanza alijua pete hio haina thamani kubwa sana kwa Edna kwani mwanamke huyo amelelewa kujitegemea na sio kutegemea watu wengine.
Upande mwingine , ndani ya hoteli ya nyota ya Landmark . hoteli iliokuwa ndani ya maeneo ya Ubungo , alionekana Jestina mke wa Tajiri Azizi akiingia ndani ya hoteli hio na gari yake aiana ya Range.
Baada ya mwanamama huyu kuegesha gari yake sehemu maalumu aliingia moja kwa moja ndani ya eneo la mapokezi.
“Karibu Mgeni wetu”Aliongea dada wa mapokezi mara baada ya Jestina kufika eneo hilo.
“Asante nipo hapa kwa ajili ya kuonana na mgeni katika chumba namba 103”Aliongea mwanamama huyu na mhudumu yule aliangalia kwenye tarakishi yake kwa dakika na kisha akamgeukia.
“Una miadi naye mama?”
“Ndio , unaweza kupiga simu na kumwambia Jestina amefika”Mhudumu yule alifanya kama alivyoambiwa na kupiga simu na baada ya kuongea kwa dakika moja alimpa ishara ya heshima Jestina na kumruhusu.
Dakika chache mbele mama huyu alikuwa akitoka nje ya Lift na kwenda moja kwa moja kusimama kwenye chumba namba mia na tatu ndani ya floor ya tisa na kugonga na mlango na ukafunguliwa baada ya nusu dakika.
“Jestina karibu sana”Ilikuwa ni sauti ya mwanamama mtu mzima alieonekana kwenye mlango huo na kumkaribisha Jestina.
“Asante sana MamaTheresia”Alijibu na moja kwa moja akenda kukaa kwenye masofa yaliokuwa ndani ya chumba hiki cha hadhi na akafuatia Mama Thereisia.
Alikuwa ni mama mtu mzima hivi lika la miaka arobaini hivi , lakini alionekana ni aina ya wamama wanaojipenda kwani licha ya kuwa ni mweusi ,lakini Ngozi yake bado haikuwa na mikunjo mingi kumfanya aonekane kuzeeka.
“Niambie Jestina nimeshitushwa na namna ulivyowasiliana na mimi na kutaka tuonane kwa siri”A;liongea huyu mwanamama huku akijaza wine kwenye Glasi na kumpatia jestina.
“Ni kweli na nikutokana na umuhimu wa jambo lenyewe”aliongea na Mama Theresia alivuta pumzi na kukaa vizuri kwa ajili ya kumsikiliza Jestina.
“Unaweza kwenda moja kwa moja Jestina tusipoteze muda sana”
“Nahitaji msaada wako Mama Theresia , nataka umsaidie dada yangu Blandina kutoka kwenye kifungo”aliongea huku akianza kuonyesha hali ya huzuni , lakini kumshangaza Zaidi Mama Theresia .
“Unamaanisha nini , Blandina si Ashafariki , mbona unanichanganya…”
“Blanidna yupo hai Mama Theresia na nishaonana nae , nimekutafuta ili nikueleze ukweli wote kwani najua urafiki wenu wa muda mrefu kabla ya kupotea kwake”Aliongea Jesrina na kumfanya Mama huyu kushangaa mno , lakini Jestina hakujali , alikuwa akitegemea mshangao kutoka kwake na ndio maana alitoa barua ile alioandika Blandina na kumkabidhi mama huyo na kuanza kusoma.
Mama Theresia kadri alivyokuwa akisoma alijikuta mikono yake ikitetemeka huku machozi yakianza kuonekana kwenye macho yake , nadhani aliguswa sana na alichokuwa amekisoma kwenye hio barua.
“Hii ni ya kweli Jestina?”
“Ndio Mama Theresia”Alijibu na mwanamama huyu alifuta machozi kwa mkono na kisha akamwangalia Jestina ni kama hakuwa akiamini vile.
“Blandina kwanini alichukua maamuzi ya hivi unajua siamini kabisa Jestina , nimekutana na Maina Zaidi ya mara tatu na hata kuonyesha ishara yoyote ya kunifanya nimfahamu ameshindwa? , kwnini sikuweza kutambua”
“Sio wewe tu hata mimi nilishangaa na kuumia kwa wakati mmoja , najiona kama mkosaji , nampenda dada yangu sana na sitaki kumuona akiendelea kuteseka na ndio maana niko hapa,Mama Theresia tunapaswa kumsaidia Blandina…”
“Lakini Jesrina hujanieleza kila kitu kuhusu upande wa familia yenu , hasa baba yako , kwanini asimsaidie yeye?”
“Baba ashaonana nae na anaonekana hana mpango wa kumsadia kabisa dada yangu na kwa taarifa nilizokuwa nazo sasa hivi ni kwamba kafungiwa ndani ya ikulu , jambo hilo linaniumiza sana”aliongea kwa huzuni na kumfanya Mama Theresia afikirie kidogo.
“Kwahio unataka nikusaidie vipi juu ya hili maana ni swala zito na mimi mpaka muda huu siamini kabisa , naona kama nina anagalia sinema”
“Nahitaji unisaidie kwa kumfikishia taarifa Raisi Senga , Yule ni kaka yako itakuwa rahisi kumueleza”Aliongea na kumfanya Mama Theresia akumbuke mahusiano yaliokuwepo kati ya Blandina na kaka yake na alijikuta akitoa macho,
Alianza kukumbuka namna ambavyo kaka yake aliweza kuomboleza kifo cha Blanisna mara baada kupata taaridfa ya ndege ya M Airline kupotea, alikumbuka pia namna ambavyo Senga alivyokuwa na urafiki wa karibu na Raisi Kamau Kamau wa Kenya , aliona kama swala hili Senga akalifahamu juu ya usaliti uliofanywa na watu hao wawili aliokuwa akiwajali , hakuweza kujua ni nini kitamkuta raisi Senga na aliona hata ombi ambalo Jestina alikuwa akiomba kwake lilikuwa la hatari sana.
“Jestina hili swala ni ngumu sana kufanyika , maamuzi ambayo Blandina ameyachukua yalikuwa magumu san ana naweza kusema yalikuwa sio ya busara ,swala hili linaweza kumletea mshituko kaka yangu , hapana hatuwezi kufanya kama unavyopendekeza ,Blandina anapaswa kuwajibika kwa matendo yake”
“Naelewa hili Mama Thereisa , lakini unafikiri Senga atakaa kwenye Giza mpaka lini , ukweli utakuja kumfikia tu , lakini pia naamini dada yangu anasababuu kubwa juu ya kuchukua maamuzi alioyafanya , hatupaswi kumlaumu ila tunapaswa kumsaidia , hebu fikiria mapenzi aliokuwa nayo Blandina kwa Senga , hivi ulifikiria ilikuwa rahisi kwake kujificha kwa miaka yote hio, unafikiri ni swala rahisi lazima kuna sababu kubwa ambayo dada hajanieleza na nataka kumsaidia, na wewe ni rafiri yake tunapaswa kumsaidia”
“Hapana Jestina hatupaswi kua na haraka hivi , hili swala ni kubwa na Senga ni raisi wa hii nchi , jambo baya likimkuta nchi itayumba”
“Vipi kama nikikueleza kama Denisi yupo hai?”Aliongea Jestina na kumfanya mama huyu kutoa macho , hakuelewa ni nini anamaanish.
“Lakini si barua inajieleza Denisi amekufa na ajali ya ndege ndio maana Blandina akajificha,Denisi gani tena unamzungumzia?”
Jesrina hakutaka maelezo sana , alichokifanya ni kutoa simu yake na kisha akaenda upande wa picha na kufungua picha mbili alizopiga na kumsogelezea simu Mama Theresia na kumuonyesha haikuelewa alizipiga muda gani.
“Mume wangu siku ya jumapili alienda kumuonyesha baba yako hizo picha na kwa jinsi nilivyoweza kufatilia Mohamedi picha hizo kapatiwa na Raisi Jeremy wa Rwanda na hizo picha ni za Denisi zote , ya kwanza ni kipindi akiwa Malaysia kwenye matibabu na ya pili yake nasikia ilipigwa akiwa Marekani”Aliongea Jestina kwa haraka haraka na kumfanya Mama Theresia kushangaa mno na kuendalea kuzoom hizo picha ni kama hakuwa akiamini.
“Unataka kumaanisha kama Denisi yupo hai?”
“Ndio maana unaona hizo picha na swala hili linafahamika mpaka kwa baba yako”Aliongea na kumfanya mwanamama huyu kutoa macho
“Nenda picha ya tatu”aliongea Jesrina na Mama Theresia akaslide na hapo hapo ikaonekana picha ya mwamba Roma Ramoni alieonekana na mreambo Edna na picha hio ilionekana kupigwa siku ya Edna alipoenda kwenye sherehe ya kumpongeza kijana Kassimu mtoto wa Tajiri Azizi.
Unahisi The Doni atakuwa nani?????
ITAENDELEA KABLA YA SAA TANO USIKU KIPANDE KIMOJA AU VIWILI , STAY TUNED.