SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU
MTUNZI:SINGANOJR .
SEHEMU YA 139.
EARTH AXIS.
“Moja ya kosa kubwa binadamu alilofanya tokea kuwa na upeo mkubwa wa akili ni kuudharau mwili wa kibinadamu na kuona kwamba kuuchakachua ndiyo kuongezea nguvu. Siri za uwezo wa binadamu zilizofichwa katika miili ya kibinadamu ni kitu ambacho huwezi kufikiria kabisa.”
*****
Haikuwa mshangao wa kuokolewa tu, lakini vilevile alishangaa jinsi Hamza aliwezaje kufika hapo ndani ya muda mfupi, wakati wanajeshi ambao walikuwa wamepewa jukumu la kumlinda walikuwa wakikimbilia nje kuokoa maisha yao kwa kukimbia mbali na moto.
“Umewezaje kufika hapa?” aliuliza Yulia kwa mshangao.
“Nimeruka na kukimbia mpaka nikafika hapa. Vipi, akili yako imepata matatizo? Kwanini unauliza swali la kijinga?” aliongea Hamza huku akicheka.
“Kwahiyo umekuja kuniokoa?” aliuliza Yulia ambaye pumzi yake ilikuwa ikitoka kwa kasi sana.
“Wewe unaona nimekuja kufanya nini?”
“Kwanini? Hata kama una uwezo, sio rahisi kujitoa muhanga na kuja hapa juu kuniokoa?” aliongea Yulia.
“Hilo sio swali tena. Nimekuja kwa sababu ushakuwa mpenzi wangu,” aliongea Hamza huku akianza kumpapasa kutoa vumbi nywele zake.
“Unadhani nilivyokuwa nikikuambia nakufanya kuwa mwanamke wangu, nilikuwa nikikutania?”
Yulia alijikuta akiwa kimya baada ya kusikia hayo. Tokea mwanzo, alidhani Hamza alikuwa akicheza naye na hakuwa na nia ya dhati juu yake. Isitoshe, alikuwa mgonjwa wa akili, asiyekuwa na uwezo wa kupata hisia, mgonjwa asiejua mapenzi yakoje. Kwa lugha nyepesi, kama Hamza angeamua kucheza naye na kisha kumuacha, asingekuwa na maumivu kwa sababu hakuwa na hisia zozote; alikuwa binadamu lakini kama roboti, hisia pekee alizokuwa nazo ni zile za furaha na hasira.
Lakini sasa, matendo ya Hamza yalimfanya Yulia kushikwa na hisia mchanganyiko.
Hamza muda huo hakuwa na muda wa kujali ni kitu gani mwanamke huyo anafikiria wala kuhisia.
“Afande, angalia nyuma yako.”
Bertha alikuwa katika hali ya kushangaa baada ya kuona kumbe Hamza na Yulia walikuwa wakifanya mapenzi alipokuwa anaingia chumbani kwa Yulia na kukuta kumevurugikana. Sasa baada ya Hamza kumwambia angalia nyuma, alikumbuka alikuwa bado akipigana.
Palepale alikusanya nguvu zake zote za nishati ya mbingu na ardhi na kuzielekeza kwenye mkono, akiunganisha na ngumi na kumpiga yule mwanajeshi eneo la kichwa kabla hajamgusa Bertha na visu vyake. Ngumi ile ilikuwa na uzito usiokuwa wa kawaida, kama vile amegongwa na chuma; eneo la kichwa chake lilibonyea huku jicho lake likitoa cheche za umeme. Licha ya hayo, mwanajeshi yule wala hakufa, na kwa kitendo cha kuruka tu alipotea ndani ya eneo hilo.
“Ana spidi ya hatari,” aliongea Bertha huku akiugulia maumivu ya mkono.
“Hawa wanajeshi wametengenezwa vipi? Kwanini wanaumiza sana licha ya kuwa nusu binadamu, nusu roboti?” aliongea Bertha, na kumfanya Hamza kusinyaza macho yake huku akimwangalia Bertha.
“Kwa kiwango ulichopo, kupigana na mwanajeshi wa aina ya Delta Zero na kumfanya akimbie, nakupa pongezi. Unaonekana sio mwepesi,” aliongea Hamza.
“Unajua nipo kiwango kipi? Wakati huna hata nishati ya mbingu na ardhi kwenye mwili wako, unaonekana sio wa kawaida na wewe,” aliongea Bertha kwa kuhamaki.
Bertha alijua kulingana na kanuni za mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, mwanajeshi akiwa na uwezo wa kuona kiwango ulichopo, maana yake amekuzidi. Binadamu yoyote anapozaliwa, anakuwa tayari na nguvu ya nishati za mbingu na ardhi, hii ni asili yake. Kitendo cha kujifunza kuamsha nguvu ya mwili maana yake ni kuilandanisha na nishati ya mazingira na kutengeneza uwiano; hapo ndipo mtu huvunja vizuizi au siri zilizokuwa ndani ya mwili wake. Mtu akifanikiwa hapo, maana yake anaweza kufanya mambo nje ya hiari ya asili yake.
Inasemekana kwamba watu wa enzi ya kale waliweza kuishi kwa muda mrefu kutokana na kuzaliwa na kiwango kidogo cha uchafu mwilini. Hata wale waliendeleza kujisafisha siku hadi siku kwa ku
'synchronize', nishati ya asili ya miili yao na nishati ya mbingu na ardhi waliweza kuongeza umri wao wa kuishi maradufu kwa kufikia daraja la nafsi au daraja la matengenezo mapya ya mwili au daraja la Ukaidi wa mbingu.
Hata hivyo, ni watu wachache sana walioweza kufanikisha jambo hilo na waliishi licha ya historia zao kupotea. Kilichofanya siri ya uvunaji wa nishati kupotea mwanzoni ni kutokana na kuibuka kwa mbinu nyingi sana za mafunzo hayo, ambazo yalikuwa na uwezeshaji tofauti tofauti. Mfano, hata sasa baada ya siri ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kurudi upya, watu wanatumia mbinu tofauti tofauti. Mfano, Bertha alikuwa akitumia mbinu ya Holy Fire, au Levithian ambaye alitumia mbinu ya kutunisha mwili.
“Ninaamini utakuwa wewe ndiye pekee wa umri mdogo kuweza kufikia kiwango hicho katika shirika la Holy Fire,” aliongea Hamza.
“Upo sahihi. Ukiachana na Master wangu, mimi ndiye ninayeendelea kufikia kiwango cha juu,” aliongea Bertha kwa kujivuna.
“Naona bodyguard wako sio mwepesi,” aliongea Hamza na kumfanya Yulia kutingisha kichwa, maana hakutaka maongezi hayo kuendelea ndani ya eneo hilo ambalo limegeuka kama jehanamu kwa joto.
Baada ya hapo, Hamza alimbeba juu na kisha alijirusha kioo kwenye cha cha dirisha la jengo na kutokomea nje.
“Ahhhhhhh..!”
Yulia alijikuta akitoa kilio kutokana na tukio hilo na aliishia kumkumbatia Hamza kwa nguvu zake zote wakiwa wanadondoka kutoka hewani kwenda chini.
“Holy shit, anajaribu kufanya nini?” Aliongea Bertha kwa mshangao na hakutaka hata kujua kinachoenda kuwatokea ni nini, kutokana na moto kumsogelea kwa kasi palepale na yeye alijirusha uelekeo huo, ijapokuwa mafunzo yake hayakuwa katika levo ya juu, lakini hakuogopa pia urefu wa jengo na ardhi.
Hamza upande wake mara baada ya kuporomoka kwa kasi, ile anakaribia kutua ardhini spidi yake ilipungua na kutua taratibu sana na kumuweka Yulia chini na palepale walisogelewa na kundi la wanajeshi.
“Madam, imekuwa kheri sana upo salama,” kila kamanda aliongea kwa kupatwa na ahueni hazina ya Taifa Yulia alikuwa hai.
Upande wa Yulia bado alikuwa kwenye mshituko wa kudondoka kwenye ghorofa, na mara baada ya akili yake kumrudia na kusikia maneno ya wanajeshi hao aliishia kukunja sura tu.
“Kwahiyo mnasema hili eneo hata mawasiliano yanashindwa kufanyanyika?” Aliuliza Yulia.
“Ndio, kwanzia tukio lianze mawasiliano yalianza kupotea kwanza.”
“Itakuwa wametumia EMP, jeshi la Marekani teknolojia yao ya Electromagnetic Pulse ipo juu sana kuliko nchi yoyote, lakini hata hivyo inafanya kazi kwa muda tu,” aliongea Hamza.
“Nadhani walifanya hivi ili kutoruhusu mawasiliano kutoka nje, nina uhakika ndani ya maabara kuna kinachoendelea, mnasubiri nini hapa kimbieni kwenda chini mkalinde majaribio yetu,” aliongea Yulia lakini Hamza alizuia.
“Subirini msiende.”
Kundi hilo la wanajeshi walishangazwa na kauli hiyo, walikuwa wakimsikiliza zaidi Yulia lakini baada ya kumsikia Hamza akiongea hivyo ni kama walianza kujiuliza yeye ni nani, walimshangaa baada ya kumuona akiruka kutoka juu ya ghorofa na kutua chini bila ya majeraha tena akiwa amembeba Yulia, aina hiyo ya uwezo haikuwa kawaida kwa wanajeshi hao.
“Mbona unawazuia, hivi unajua kwanini serikali ilitumia hela nyingi kujenga maabara, unajua ni nini kimefichwa, kama kikichukuliwa na hawa Wamarekani upo tayari kuwajibika?” Aliongea Yulia kwa wasiwasi mkubwa.
Hamza palepale alimnyooshea kidole Bertha na kufanya wale wanajeshi wamgeukia na kumwangalia.
“Wote hapo hamjafikia levo aliokuwa nayo huyo mwenzenu, lakini yeye anao uwezo wa kudili na mwanajeshi mmoja tu pekee tena kwa tabu, kama huko chini wapo zaidi ya kumi maana yake mnajipeleka kufa na sio kwenda kufanya kitu.”
Yulia aliishia kubung’aa, ijapokuwa alikinzana nae lakini alijua Hamza alichoongea ni ukweli mtupu.
Haikuwa tu uwezo wa wanajeshi hao, lakini siraha walizokuwa wakitumia zilikuwa zimeendelea sana katika teknolojia yake.
“Kwahiyo tunapaswa kufanya nini, hatuwezi kusimama tu hapa na kusubiri bila kufanya kitu?” Aliongea Yulia.
“Kama hawawezi kwenda mimi ninaweza kwenda kudili nao,” aliongea Hamza akiwa anatingisha mabega.
“Wewe! Peke yako unataka kwenda?” Aliuliza Yulia kwa mshangao wa kutokuamini.
“Haha... Kwani si ndio maana Malibu wamenileta hapa, si ili kudili na hali kama hizi?” Aliongea Hamza na kisha alinyoosha mkono wake na kumshika Yulia uso.
“Kuwa mtoto mzuri na nisubirie hapa.”
Mara baada ya kuongea kauli hiyo alikimbia na kuzama ndani ya hoteli iliyokuwa ikiwaka moto.
Wanajeshi wote waliokuwa katika eneo hilo walimwangalia Yulia kwa mshangao, wakishindwa kujua namna ya kuitafsiri hali hiyo, walijiuliza tangu lini Yulia akawa romantiki hivyo mbele ya mwanaume.
Akili ya Yulia ilikuwa ikifanya kazi vizuri, licha ya kwamba moyo wake ulikuwa ukidunda kwa kasi na aliishia kuwaangalia wanajeshi hao bila ya wasiwasi wowote wala aibu.
“Mnamkodolea macho nani, shughulikieni swala la mawasiliano haraka iwezekanavyo na muwasiliane na meli zetu za jeshi zilizopo karibu, nina uhakika hawa wavamizi watakuwa wamekuja hapa na meli ya kivita au manowari,” aliongea na wanajeshi wale haraka sana walikubali maagizo na kugawanyika.
Bertha yeye aliishia kusimama pembeni ya Yulia, hakutaka kwenda mbali tena maana kidogo tu angeshindwa kumuokoa bosi wake kama sio Hamza na kutokana na uzembe wake aliishia kukunja ngumi na kung’ata meno kwa hasira.
Mpango ulikuwa ni kuingia katika maabara ya chini ya ardhi kwa kutumia lifti ya hoteli hiyo. Ijapokuwa kulikuwa na zaidi ya njia moja ya kuingia ndani, Hamza alikuwa akiitambua njia hiyo pekee kutokana na kuitumia mara ya kwanza.
Hivyo, Hamza aliingia katika lifti na aliweza kuona wanajeshi kibao wa Kitanzania waliokuwa wamelipuliwa na bomu na kuungua na moto.
“Haha... naona kuna wanajeshi wengine wanajitakia kifo,” aliongea Kapteni Jasoni, na palepale aliinua silaha yake ya M4 Carbine Colt, ambayo ni maalum kwa kikosi chao.
Silaha hiyo mwanzoni ilifahamika kuwa na uzito wa kilo tatu, lakini wakati huo ilikuwa imeboreshwa zaidi na kuwa na uzito wa zaidi ya kilo tano. Umbali wake wa kulenga shabaha ulikuwa umeongezeka kutoka mita mia sita mpaka kufikia mita mia nane, na vilevile ilikuwa na uwezo wa kufyatua zaidi ya risasi moja.
“Tututututututu.”
Mara baada ya kufyatua risasi kadhaa, Jasoni aliridhika na kisha akashusha silaha yake chini.
Lakini sasa, dakika ambayo anashusha silaha ile chini, aligundua mwanajeshi wa Kitanzania aliye mbele yake hakuwa ameumia hata kidogo na bado alikuwa akitembea kumsogelea.
"How could this be… I missed!?" Jasoni hakuamini macho yake. Mdunguaji wa daraja la kwanza kama yeye, ndio maana alichaguliwa kujiunga na kikosi hicho cha kwanza, uwezo wake wa kulenga shabaha ulikuwa wa kiwango cha juu sana katika kutekeleza mauaji ya umbali mrefu.
“Damn it.”
Jasoni alijikuta akishikwa na aibu mbele ya wanajeshi wenzake na alianza kumshambulia tena Hamza. Lakini Hamza hakusubiria kushambuliwa tena. Palepale kabla hata Jasoni hajafyatua, alikuwa ashapotea alipokuwa amesimama na kuibukia mbele yake na kuipokonya kwa nguvu ile bunduki ya M4 na kumpiga nayo kichwani.
Bam!
Silaha hiyo iligongana na kichwa cha Jasoni mpaka ikapinda na kusambaratika, lakini helmeti la Jasoni halikupata madhara makubwa zaidi ya kuonyesha mikwaruzo michache.
"Shit, ni mwanajeshi wa mbinu za kale huyu!!" aliongea Jasoni.
Wamarekani hawakuamini kabisa katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi. Waliamini katika teknolojia na walizichukulia mbinu hizo siku zote kama mbinu za kale.
Jasoni, mara baada ya kujua ni aina gani ya adui anapambana naye, palepale alitumia mkono wake wa roboti na alitengeneza nishati ya mionzi na kumshambulia nayo Hamza. Lakini Hamza alikwepa mionzi ile na kwa spidi kubwa aliushika ule mkono na kuugeuzia uelekeo wa mwanajeshi mwenzake. Kitendo cha kutoa mionzi ile kilisababisha sauti ya kuchomelea chuma, yule mwanajeshi mwenzake kichwa chake kilitoboka palepale na kumfanya Hamza acheke.
“Bado inaonekana udhaifu wenu upo kichwani, ijapokuwa mahelmeti yenu yametengenezwa na chuma cha pua, lakini bado hayashikilii vizuri kwenye kichwa.”
“Damn African boy, go to hell,” aliongea Jasoni kwa hasira mara baada ya kuona amemshambulia mwanajeshi mwenzake na alitaka kumuua Hamza palepale.
Mkono wake mwingine ulichomoa visu kuelekea kichwa cha Hamza, lakini Hamza alijua ugumu wa chuma cha pua ulivyo. Hata kama alikuwa na mwili mgumu, ni ngumu kupona katika mishale hiyo ya visu. Hivyo, kwa ustadi wa hali ya juu sana, alikwepa visu vile huku akimpiga mtama maridadi sana Jasoni na kumfanya adondoke chini kwenye lifti. Hakuishia hapo tu; alikishika kichwa chake na kukipigisha kwenye sakafu kwa nguvu zake zote mara kadhaa mpaka Jasoni akapoteza uhai palepale.
Mara baada ya kuona Jasoni amekufa, mwanajeshi mwingine aliinua mkono wake akitaka kuwasiliana na wengine, lakini Hamza hakumpa hiyo nafasi. Alimsogelea kwa spidi na aliushika ule mkono wenye kifaa cha mawasiliano na kisha alitumia uzito wa ngumi yake kumshambulia kichwani mara tatu.
Kutokana na uzoefu alioupata kwenye kumshambulia Jasoni, Hamza alilenga lile helmeti kwa ufanisi wa hali ya juu na kulibonyeza kwa kutengeneza shimo katikati. Baada ya kumuua na mwanajeshi yule palepale, aliruka chini na kuingia kwenye shimo kwenda vyumba vya ardhini.
Kama Bertha angeona tukio hilo, angeshikwa na mshangao mkubwa, kwani yeye alitumia nishati ya mbingu na ardhi kushambulia yule mwanajeshi lakini alishindwa kumletea madhara, lakini Hamza alitumia staili ileile lakini aliweza kuua wanajeshi wote tena bila ya kutumia nishati za mbingu na ardhi zaidi ya nguvu za mwili wake tu.
Hamza hakuzubaa, alijua chini huko wanajeshi wa Delta Zero wapo makini kufuatilia kila adui anayeingia hapo ndani, na ilikuwa kama alivyotarajia kwani ile anatua na risasi zilianza kumsogelea mfululizo. Wanajeshi wale waliokuwa wakilinda eneo la kuingilia wote macho yao ya kushoto ya kifaa yalikuwa yakimpa shabaha ya Hamza alipo na kufanya risasi zao zisikose, lakini spidi ya Hamza ilikuwa sio ya kawaida kabisa na kufanya risasi zao zisimguse kabisa.
"Captain Craig! Someone had entered! The enemy is very nimble, so we cannot shoot him down at the first moment!" Mwanajeshi mwingine hakupanikishwa na uwezo wa Hamza na alitoa taarifa palepale baada ya kuona ni ngumu kudili na mtu kama Hamza.
Cleig na wenzake walikuwa mbele ya mlango wa kielektroniki na walikuwa bize kufanya
decryption ya mlango wa chuma kizito, Profesa Ndiswe akiwa ndiye kiongozi wa mchakato huo. Sasa mara baada ya kusikia taarifa hizo, sura yake ilionyesha mshangao.
"Kama ni hivyo basi Jasoni na wenzake wamekwisha kufa, mtu wa aina hio ni ngumu kushindana nae, msipigane kumuua bali mchelewesheni," aliongea Cleig na kisha palepale alimgeukia Ndiswe.
"Profesa, utafanikiwa kweli naona kama tunatumia muda mrefu?"
"Unafikiri nataka kutumia muda mrefu, hii maabara imefungwa na nywila mia tisa tisini na nane na ina njia elfu tisa mpaka kuifungua na kufikiria Earth Axis.
If I didn't steal their decryption algorithm, you wouldn't even be able to decrypt it when you die!" aliongea Profesa huku haraka haraka akiendelea kuchezesha vidole vyake kwenye kijikeyboard huku akilaani na paji lake la uso lilikuwa limejaa jasho.
"Shenzi kabisa, muda ni mchache sana, mngenileta mapema pengine ningefanikisha mapema, acha lawama," aliongea.
"Huna muda wa kuongea, unapaswa kufanya jambo, mpaka kukuingiza hapa tumetumia akili nyingi na juhudi kubwa, vijana wetu pia wamepoteza maisha
," aliongea Cleig lakini palepale ile
lock ilitoa sauti ya kubip na rangi ya kijani.
"Success!"
Profesa alifurahi kufanikiwa kufungua mlango huo wa chuma na kumfanya Cleig macho yake kuchanua, muda uleule aligeuka na kuangalia mlango huo wa chuma ukijifungua tataribu.
"If I wasn't worried about activating the destructive device, I could have gone in! Let's go! Bring the earth's axis back!" aliongea Cleig, akimaanisha kwamba kama isingekuwa ni kuhofia kifaa cha kuharibu hiyo maabara angefosi kuingia.
Wote watatu haraka haraka waliingia ndani ya maabara hiyo, kilichokuwa mbele yao ilimfanya hata Cleig aliyezoea kuona teknolojia iliyoendelea kushikwa na mshituko mkubwa.
Kila kifaa kilichokuwa hapo ndani kilikuwa na teknolojia ambayo sio ya wakati huu, vilikuwa ni vifaa vya ajabu mno kimuundo na kufanya iwe ngumu kwao kuelewa vina kazi gani.
Eneo lote la ukuta kuzunguka kulikuwa na skrini zilizokuwa zimewashwa na kuonyesha aina mbalimbali ya michoro, ni aina ya michoro ambayo mwanasayansi wa kawaida asingeweza kuelewa.
"Acheni kushangaa maana hata mimi mwenyewe sielewi zaidi ya Yulia ambaye ndio anajua kila kitu kuhusu Earth Axis, haya ndio matokeo ya utafiti wake na ni yeye peke yake anaejua Tanzania nzima, siku zote wanaofika hapa ni wakaguzi tu na mimi alinileta mara moja lakini hakunielezea
," aliongea kwa masikitiko Profesa.
"Hizi ni siraha au, mbona ni kama ndege, vingine sijui ni kama nini tu?" aliongea Cleig akitamani kukuna kichwa lakini aligundua alikuwa na helmeti.
"Only by getting the Earth's axis and doing our own research will we be able to find out the answer! Fast! The earth's axis is the innermost part!" aliongea Profesa, akimaanisha kwamba watapata majibu ikiwa tu wataichukua Earth Axis na kwenda kufanya utafiti wao.
Mara baada ya kuongea hivyo hawakusimama tena, palepale walikimbia kwenda ndani zaidi kwenye njia na walifika katika eneo maalumu kama jukwaa hivi.
Kulikuwa na mwanga wa miale ya umeme, muundo wa neti ya mbu ilivyo. Miale ile ilikuwa ni umeme wenye shoti kubwa na katikati yake kulikuwa na jiwe linalotoa rangi kama vile kuna kitu kilichokuwa kimewekwa juu yake ila kimeondolewa.
“Nini kinaendelea? Mbona sioni hiyo
Earth Axis? Ilitakiwa iwe hapa,” aliongea Profesa Ndiswe kwa namna ya kuchanganyikiwa.
Cleig aliishia kugonga mara mbili paji la uso wake na palepale jicho lake lilitoa mionzi na kuskani eneo lote. Alikuja kuishia katika eneo la ukuta ambao ulionekana kama haukuwa wa kawaida, na palepale aliinua mkono wake na kufyatua mionzi.
“Ziiii, ziiii.” Sauti kama ya kuchomelea chuma ilisikika na chuma kilichokuwa katika eneo lile kilikatika na kutengeneza tundu kwenda ndani zaidi.
“Ah! Kumbe kuna milango mingine ya siri kuingilia hili eneo, hawa Waafrika wameyajuaje haya yote?” aliongea Ndiswe kama vile yeye hakuwa Mwafrika.
“Inaonekana kuna mtu amefika hapa na kuichukua
Earth Axis mapema kabla yetu, lakini hakuna kingine kilichochukuliwa. Maana yake ni kwamba aliyechukua alikuwa na haraka, atakuwa hajaenda mbali, ngoja tumfukuzie,” aliongea. Na pale palepale wawili hao waliingia kwenye lile tundu na kuanza kufuatilia wasiomjua.
Kwa sababu Ndiswe hakuwa mwanajeshi, alishindwa kukimbia sambamba na wenzake, hivyo mwanajeshi aliye nyuma alimbeba begani kama vile ni nzi kwa wepesi, na safari ikaendelea.
Baada ya Cleig kuongoza kundi hilo kukimbia, ghafla alisimama na kisha aligeuza uso wake kulia.
“There's a reaction from the heat! We'll take a shortcut!” aliongea akimaanisha kwamba kuna viashiria vya joto hivyo wapite njia mkato.
Mara baada ya kuongea vile, palepale alitumia ile mionzi na kukata chuma na kutengeneza tundu lingine. Baada ya kuingia na kukimbia kwa mita kama mia mbili hivi mbele, walijikuta ni kama wanapanda mlima na ile wanakimbia hatimaye waliweza kuona eneo lililokuwa kama jukwaa juu yao. Mara baada ya kufika juu yake, waligundua ilikuwa ni lift iliyokuwa ikitumia mfumo wake pekee wa umeme. Ilionekana ilitengenezwa kwa nyakati za dharura kama hizo.
Muda uleule walimuona mtu akikimbilia mbele yao kuwahi kwenye lift, na Profesa Ndiswe alimfahamu.
“Ni Hebert Kijazi yule, moja ya viongozi wa huu utafiti,” aliongea.
Hebert alikuwa ameshikilia kiboksi flani kidogo kilichokuwa na kioo kama simu juu yake. Mara baada ya kuona amefikiwa na wavamizi, alijikuta akishikwa na mshituko wa hali ya juu. Alibonyeza kwa nguvu lift ile kufunguka, na ilivyoleta upenyo kidogo tu, aliweka mkono kuilazimisha kufunguka kwa haraka.
“Na huyu ana mafunzo ya nishati za mbingu!” aliongea Cleig huku akiachia tabasamu.
Hakuna taifa lililokuwa likidharau wanajeshi wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kama wanajeshi wa kitengo cha Zero Delta; walikuwa wametengenezwa maalumu kwa kudili na wanajeshi wa uwezo huo.
Hebert alikuwa akitetemeka mno. Baada ya lift kufunguka, palepale alibonyeza kwa haraka vifute ili ijifunge na kuondoka, lakini sekunde ambayo mlango ulijifunga palepale ulipigwa bomu na kuchanguka.
“Hebert Kijazi, kutoka familia ya mzee Kijazi, moja ya familia zenye nguvu kubwa hapa Tanzania,” aliongea Ndiswe huku akicheka.
“Profesa Ndiswe, umeamua kushirikiana na adui na kuisaliti nchi yako?”
“Nimetengenezwa kuwa Mtanzania, ila sijawahi kuwa raia wa Tanzania. Acha kuongea ujinga wa kuuza nchi. Leta ulichoshikiria maana huna uwezo wa kushindana na Kapteni Cleig,” aliongea Ndiswe.
“Huna haja ya kuongea kwa sauti, Ndiswe,” aliongea Cleig na palepale alimsogelea Hebert, akiwa amekunja ngumi na visu vilichomoka kwenye kwenzi ya vidole vya mkono ule wa roboti kumlenga Hebert kichwani.
Hebert aliweza kutumia mafunzo yake ya kijeshi kukwepa shambulizi lile, lakini nguo zake zilichanika na kumfanya kushikwa na jasho la ubaridi.
“Zero Delta Squadron!” aliongea Hebert huku akiwa ni kama amepata akili baada ya kuona chapa katika mavazi ya Cleig, na palepale akakakamaa mwili akijua kabisa kuwa hakuwa na uwezo wa kushindana na Cleig.
“Huu umeshaanza kuwa usumbufu, kufa,” aliongea Cleig, hakutaka tena kuendeleza mchezo wa panya na paka na palepale aliachia mionzi kummaliza Hebert.
Hakuwa mzembe vilevile, kwani aliweza kuikwepa kiustadi sana ile mionzi, lakini hata hivyo, hakuweza kukwepa yote na kuishia kuumia kwenye mbavu huku akitawaliwa na joto kali sana. Hofu ilizidi kumvaa kila hatua aliokuwa akipiga Cleig kumsogelea.
“Acha kunishambulia, acha kunishambulia, nipo tayari kukupatia hiki kitu, naomba uniache hai,” aliongea.
“Sawa, leta hapa,” aliongea Cleig akiacha kushambulia.
SEHEMU YA 140.
Hata kama ni mimi, ningefanyaje? Kiufupi, Hebert hakuwa na namna na aliishia kuinua kile kiboksi kumsogelezea Cleig huku akitanguliza maneno ya ushawishi kuachwa hai.
“Mimi ni mtoto wa kwanza na mkubwa katika familia ya Mzee Kijazi, kati ya familia kubwa hapa nchini. Nikifanikiwa kuwa kiongozi wa familia baada ya babu yangu, nitakuwa kati ya watu wenye nguvu kubwa ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Ikiwa mtaniacha hai leo, nawahakikishia kutakuwa na faida kubwa kwenu. Nitawapa kila aina ya ushirikiano,” aliongea.
“Hahaha… una mbinu nzuri za maneno. Tunapenda watu wa aina yako,” aliongea Cleig, akishirikiana na Profesa Ndiswe na kuanza kucheka.
Hebert alitoa tabasamu la ushirikiano na kisha kile kiboksi alikiweka kwenye sakafu. Kisha akarudi nyuma na kuingia kwenye lift nyingine ambayo haikuharibika.
“Axis of Earth...! We've finally gotten our hands on it. We've accomplished our mission!” aliongea na kisha palepale aliinua macho yake na kumwangalia Hebert.
“Stupid cowardly bastard, leave the elevator here to us!” aliongea akimwita Hebert mjinga na mwanaharamu muoga na kumtaka aiache lift maana ni ya kwao kuikwea.
“Naombeni msiniue, nimeshawapa kila kitu. Ninaweza kuwapa na hela pia, ninazo nyingi,” aliongea Hebert.
Hebert alitaka kupona kwa namna yoyote, akiamini kwamba hata kama akipoteza kitu muhimu kama hicho, mradi siku moja atakuja kuwa mrithi wa familia yake, atapata madaraka makubwa zaidi kuliko kupoteza
Earth Axis. Licha ya kuona kwamba kama angeweza kuokoa
Earth Axis isiibiwe angeweza kupatiwa heshima kubwa na nchi, lakini hakuwa tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kitu hicho.
Muda huo, lift iliweza kugunduka na kumfanya ageuke.
“Bosi! Kumbe ulikuwa huku? Nilijua tu umekimbia huku kwa ajili ya kulinda
Earth Axis,” aliongea Pima.
Hebert alishikwa na mshangao, na palepale wazo lilimwingia katika akili yake. Kabla Cleig hajachukua hatua ya kudili na Pima, alimuwahi palepale.
“Pima,
Earth Axis imeshachukuliwa na ipo kwenye mikono ya huyo bwana. Fanya namna tuirudishe,” aliongea.
Pima mara baada ya kusikia kauli hiyo, aliona kabisa bosi wake amemkubali tena na palepale aliitikia kwa ari kubwa.
“Nimekuelewa bosi,” aliongea na kisha alikaa mkao wa mapigano, hali iliyomfanya Cleig apambwe na tabasamu la dhihaka.
Pima alimsogelea Cleig kwa ustadi mkubwa na kushika mkono wake. Lakini mara baada ya kuushika ule mkono, alihisi kuna kitu hakipo sawa. Ilikuwa kweli, kwani visu vilifyatuka na kumchoma kwenye kiganja cha mkono wake, na kusababisha damu nyingi kumtoka.
“Arghhhhh!!! Bosi kuwa makini!” aliongea huku akigeuka nyuma akijua kwamba kushambuliwa kwake na bosi wake atakuwa hatarini, lakini ajabu ni kwamba Hebert alikuwa ashaingia kwenye lift na ilikuwa ikianza kujifunga huku akiwa na tabasamu la kumkejeli.
Sura alioweza kuona Pima ni ile ya kumkatili. Hebert aliamua kumtumia Pima kama chambo ili kujiokoa.
“Bosi umeamua...” Alishindwa hata kumalizia sentensi yake baada ya kugundua alikuwa ametumika kama chambo tu.
Alijikuta uso wake ukishikwa na huzuni kubwa na alishindwa hata kugundua Cleig ameshakwisha kumsogelea na alikuwa akipanga kummaliza palepale kwa kumpiga ngumi ya kichwa. Kama ingefanikiwa kumfikia, maana yake angepoteza maisha palepale.
Lakini ikiwa imebakia nchi tu kurushiwa ngumi ile, kitu kama kifurushi lilimgonga Cleig.
Bam!
Cleig alishindwa kuhimili shambulizi lile na alijikuta akirushwa na kwenda kujigonga kwenye ukuta, na kushindwa kumshambulia Pima.
Pima palepale alishituka kutoka katika mshangao na mara baada ya kuinua uso wake na kuangalia kile kilichotokea, aligundua aliyemuokoa ni Hamza.
“Mr Hamza!!!”
“Wewe ni mjinga mno. Unadhani nani kawapatia hicho kiboksi? Nadhani umeshuhudia wewe mwenyewe akikimbia. Tokea mwanzo alitaka kukuona ukifa, halafu unadhani ni mtu ambaye anaweza kukupokea upya,” aliongea Hamza.
Pima aliishia kung'ata meno yake kwa hasira kubwa kiasi cha damu kuanza kumtoka. Aliishia kuchuchumaa chini na kuanza kupiga ngumi chini kama kichaa huku machozi yakimtoka.
Cleig aliepigwa mpaka kwenda kutengeneza shimo kwenye ukuta. Alisimama kwa mara nyingine huku akimwangalia Hamza kwa mashaka.
“You’re the one who killed Jason and the others!?” (Wewe ndio uliemuua Jasoni na wengine?)
“Simjui Jasoni mimi, ila mmeenda mbali sana. Kama mngekuja tu na kuchukua kilichowaleta nisingeingilia kwa kuja huku,” aliongea Hamza.
Muda uleule, mwanajeshi aliyekuwa amembeba Profesa Ndiswe aliinua mkono wake na kumshambulia Hamza kwa mionzi kutoka nyuma yake. Muda ambao mwanajeshi yule alidhani anakwenda kufanikiwa, ilikuwa ni kama Hamza alikuwa na macho kwenye kisogo kwani alisogea pembeni na shambulizi likapita.
“Shambulia! Electric lock!” aliongea Cleig.
Mara baada ya mwanajeshi kusikia kauli hiyo, alimsogelea Hamza palepale na vitu kama minyororo vilifyatuka kutoka kwenye mikono yake, kutaka kumfunga Hamza kama vile alikuwa ni Spiderman. Hamza alipiga sarakasi matata sana na kukwepa minyororo ile, lakini Cleig alikuwa ashafyatua minyororo mingine na kumuunganishia huko huko hewani.
Dakika ile minyororo inakutana na Hamza ilikuwa ni kama moto umegusana na moto, kwani minyororo ilianza kuzunguka na kutengeneza kitu kama
magnetic field.
“Mr Hamza!!”
Pima baada ya kuona tukio hilo alishindwa kabisa kuzuia mshituko wake. Aliona palepale wanajeshi hao wote walikuwa wakishambulia kitimu na vifaa vyao vilikuwa hatari sana na sahihi kwa asilimia kubwa.
“Go to hell!!”
Cleig alicheka kama kichaa mara baada ya mwanga mweupe kusafiri katika ule mnyororo wa umeme uliomtengenezea Hamza
electric lock. Hamza licha ya kuwa na mwili mgumu, alijisikia maumivu makali mpaka mwili ukahisi ganzi. Hata hivyo, upande wa Cleig akijua anakwenda kushinda pambano, hali ile ilimshangaza.
“Inawezekanaje hii? Ameweza kuhimili?” aliongea kwa mshituko.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba lock hiyo ilikuwa ikitumia mkondo mkubwa wa umeme na ikigusana na mtu ni sekunde tu kufa, tena kwa kugeuka jivu.
Hamza alifungua macho yake na palepale aling'ata meno kwa nguvu. Kisha alipanua mikono yake, na mtego ule wa umeme ulisambaratika palepale na kumfanya Cleig kupiga hatua kurudi nyuma kwa mshangao mkubwa.
Hamza nguo zake zote zilichanika na kilichoonekana ni michirizi miekundu katika ngozi yake. Alikuwa akisikia maumivu makali lakini hakupata majeraha makubwa.
“You… You’re not human. You have also been modified!?” (Wewe… Wewe si binadamu. Pia umebadilishwa!?)
Cleig aliongea kwa mshituko, akiona Hamza hakuwa binadamu, akiwa ni kama wao tu kwamba ametengenezwa.
Tokea awe mwanajeshi, hajawahi kuona mtu wa kawaida akiweza kutoka katika mtego wa
electric lock. Hamza hakuwa na muda wa kupoteza nao; kwa spidi ya hali ya juu alikuwa ashamfikia Cleig na kumpiga ngumi nzito ya paji la uso mara tatu.
Bang! Bang! Bang! Boom! Kichwa cha kapteni kililipuka palepale.
“Kapteni!”
Mwanajeshi aliyebaki hakujisikia vizuri kabisa na alipanga kujilipua kama silaha yake ya mwisho ikitokea mpinzani kamzidi nguvu. Hata hivyo, Hamza alijua fika kwamba mwanajeshi huyo mmoja ana bomu la nyuklia ndani yake, hivyo hakumpa nafasi ya kujilipua. Alimfikia na kumshika shingo yake kwa mkono mmoja na mwingine alimpiga karate ya shingo na kumfanya shingo yake kupinda na damu nyingi kumtoka palepale.
Hamza hakushia hapo; alimpiga ngumi na ilikuwa ni kama anapiga tikiti kwani alidondoka chini huku helmeti lake likitengeneza ufa mkubwa.
Hamza alijikuta akipumua kwa nguvu huku akimwangalia Profesa Ndiswe aliyebaki.
“Nadhani wewe uliebaki ni rahisi kukupiga na ngumi moja tu kukuua kuliko wenzako,” aliongea.
Profesa Ndiswe alikuwa katika hali ya woga usiokuwa na kifani. Namna wanajeshi hao walivyokufa hakuwahi kudhania katika maisha yake, na alijikuta akikaa chini na kuanza kutetemeka kama vile alikuwa amekumbwa na shambulio la moyo.
“Umewezaje? Kikosi cha Delta Zero ni top secret ndani ya jeshi la Kimarekani. Miili yao imebadilishwa na kuaminika ni wanajeshi hatari kuwahi kutokea katika uso wa dunia, na wapo zaidi ya elfu kumi, ila wewe ume…”
“Moja ya kosa kubwa binadamu alilofanya tokea kuwa na upeo mkubwa wa akili ni kuudharau mwili wa kibinadamu na kuona kwamba kuuchakachua ndiyo kuongezea nguvu. Siri za uwezo wa binadamu zilizofichwa katika miili ya kibinadamu ni kitu ambacho huwezi kufikiria kabisa,” aliongea Hamza, na hakumpa nafasi bwana huyo kushangazwa na maneno yake. Palepale alimpiga teke la kichwa na akapasuka.
Hatimaye, mwamba Hamza Mzee alikigeukia kiboksi cha Earth Axis na kukiokota. Mara baada ya kumuona Pima akiwa amekaa chini kwa udhaifu mkubwa, alimsogezea na kisha alimpa mkono.
“Upo tayari tuondoke zetu?”
“Nimeumia tu mkono, sio tatizo kubwa,” aliongea na kisha alimwangalia Hamza kwa wasiwasi. Alishika mkono wake na kusimama.
“Nimeokoa watafiti wengi kwenye maabara. Kama nguvu unazo za kutosha, nenda kawasaie waweze kutoka. Nina wasiwasi bado wanajeshi wa Delta Zero wapo ndani ya hiki kisiwa. Ngoja nikaone kinachoendelea huko nje,” aliongea, na kisha Hamza alizama kwenye ile lift iliyokuwa imeharibika na kupotea juu.
“Aisee huyu mtu kweli haogopi kifo!” aliongea Pima kwa mshangao, na kuanza kuangalia maiti za wanajeshi zilizokuwa chini.
“Huyu mtu ni nani huyu?” alijikuta akiwaza huku akijiambia alikuwa na bahati sana wakati alivyokuwa akipigana na Hamza; hakukuwa na chuki kubwa vinginevyo angekuwa sehemu ya wafu.
Nje ya hoteli, Herbert alifanikiwa kutoka akiwa amechafuka kwa vumbi.
“Hebert!”
“Kapteni!”
Kundi la wanajeshi, mara baada ya kumuona Herbert, kila mtu aliita kwa mshituko na walimsogelea kwa haraka, kumzunguka na kumpa huduma ya kwanza kwa majeraha yake. Herbert aliishia kupiga makelele wakati wa huduma ya kwanza.
“Nimeliabisha taifa langu, nimewaangusha viongozi wetu,” aliongea.
“Bosi, nini kilichotokea?”
“Hebert, umeenda chini kwenye maabara. Vipi kuhusu Earth Axis?” Aliuliza Yulia kwa wasiwasi mkubwa.
“Naomba unisamehe Yulia, maadui walikuwa wengi na nisingeweza kuwashinda wote peke yangu.”
“Ni wanajeshi wangapi wa Delta Zero waliongia?”
“Jumla yao ni kumi, na wote walikuwa wakiniandama mimi. Nilifanya makosa na kushindwa kuipata Earth Axis.”
“Kumi!?”
Yulia na Bertha waliangaliana kwa mshangao mkubwa, wakiwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja. Walishangaa kwa sababu mwanajeshi mmoja tu wa Delta Zero alitosha kumsumbua Bertha. Sasa kama wapo kumi, si maana yake watamuweza Bertha ndani ya sekunde tu? Kulingana na uwezo wa Bertha,alikuwa juu zaidi kuliko Herbert, kitendo cha kusema wapo kumi na kufanikiwa kuwatoroka kilikuwa kama hakikubaliki mara moja katika vichwa vyao.
“Hebert, una uhakika wanajeshi waliokuwa wakikufukuza wapo kumi na ni kikosi cha Delta Zero?” Aliuliza Yulia.
“Yulia, najua ni makosa yangu kushindwa kuilinda Earth Axis. Nitawajibika kwa yote yaliotokea,” aliongea.
“Afande Herbert peke yake asingeweza kuilinda Earth Axis. Madam, kama utatulaumu, lawama zielekezee kwetu. Sisi ndio tumeshindwa kufanya chochote,” maafisa kadhaa wa jeshi waliongea wakimtetea Herbert. Mwanzoni kulinda kisiwa hicho pamoja na tafiti zake zote ilikuwa ni kazi yao, lakini kutokana na ukubwa wa adui pamoja na silaha zao, hawakuwa na maana tena kushindana na adui. Kitu pekee walichoweza kufanya ni kuzima moto, kuokoa na kurudisha mawasiliano.
“Jamani, naomba tusiongelee hili zaidi. Ni makosa yangu na siwezi kumbebesha mtu lawama. Kilichobaki sasa hivi, tujikusanye wote na kwa nguvu zetu za pamoja, ni muda wa kurudisha Earth Axis katika mikono yetu kutoka kwa adui,” aliongea.
“Upo sahihi kamanda, bado hawajaondoka. Tuharakishe kuzuia kila eneo la kutokea,” maafisa hao waliongea wao kwa wao, wakihamasishana, na walijigawa palepale kutimiza kazi.
“Yulia, wewe ni mtu muhimu sana kwa taifa. Nitakuchukua na kukupeleka sehemu salama,” aliongea Herbert, akiwa amemsogelea Yulia.
“Kama unataka kuondoka, nenda mwenyewe; huna haja ya kunichukua,” aliongea Yulia kwa ukauzu.
“Yulia, nafanya hivi ili kukulinda. Najua sikufika kukulinda kwa wakati, lakini siwezi kukuacha tena. Kukutelekeza ni kutelekeza mapenzi yangu kwako.”
“Mapenzi!! Unachotaka ni kukimbia, huna lolote. Wewe unaweza kuondoka tu. Kuna mtu namsubiri hapa mpaka atoke,” aliongea Yulia.
“Kuna mtu unamsubiri? Ni nani huyo?”
Kabla hata hajatoa jibu, waliona kitu kinachovuma kama mashine kutoka angani. Kilionekana kuwa ni kitu kilichokuwa kama duara hivi na kilikuwa kikizunguka kwa spidi kubwa. Mara baada ya wanajeshi kusikia mvumo huo, wote waliangalia juu na waliweza kuona mtu alievalia mavazi meusi akishuka kutoka angani juu ya kifaa kile.
Alikuwa mwanajeshi wa Delta Zero alievalia suti ya chuma, akiwa na chata la triangle kwenye kifua chake. Kwa namna vazi lake lilivyokuwa, ilionyesha ni jinsi gani lilikuwa na ulinzi wa kumkinga na mashambulizi.
“Ni kitu gani kile!?” Kundi la wanajeshi wa Kitanzania walijikuta wakiwa kwenye mshangao. Ilikuwa mara yao ya kwanza kuona jambo la namna hiyo.
“Sambaeni wote, msilundikane sehemu moja,” aliongea Yulia kwa sauti kubwa, lakini wanajeshi wale walileta ubishi na kuhamasishana.
“Tumshughulikieni huyu.”
Waliongea na palepale wanajeshi kadhaa walioshikilia RPG waliosogea na kujiweka katika mkao wa kushambulia. Kisha wakaachia mabomu.
Woosh.. Woosh!!
Mabomu yale kama roketi yalimsogelea mwanajeshi huyo na kumpiga, kisha kulipuka.
Boom!!
Baada ya kulipuka, kile kifaa alichokuwa akisafiria kama drone kiliharibika, na vyuma vyake kudondoka chini.
“Tumefanikiwa!” waliongea kwa shangwe, lakini hali ilikuwa tofauti kwa Yulia.
“Kimbieni!”
Wanajeshi wale hawakuelewa kwa nini wakimbie ilihali walishamshinda adui kutoka hewani, lakini kilichowatokea baada ya hapo walijutia ushamba wao. Yule mwanajeshi alishuka kutoka kwenye eneo lililolipuka na kutua chini akiwa hana jeraha hata kidogo. Hakupoa kwani eneo la kichwa chake, palipovalishwa kitu kama miwani ya wapiga mbizi, ilitoa mionzi iliyo washambulia wanajeshi mara moja na kufa palepale.
Ile mionzi ilikuwa ni hatari mno, na jinsi alivyoshambulia na kuwaua ndani ya sekunde karibia wanajeshi wote ilitisha.
“Kumbe ni kweli walifanikiwa kutengeneza suti ya mashambulizi,” aliongea Yulia kwa mshangao.
“Bosi, kuwa makini!”
Bertha aliongea na kwa spidi kubwa alimkinga Yulia na ngao ya nishati za mbingu na ardhi. Lakini licha ya hivyo, alijikuta akitema damu kutokana na nguvu ya shambulizi lile.
“Hili jitu lina nguvu inatisha,” aliongea kwa mshangao, maana mwanajeshi huyo alikuwa tofauti kabisa na yule aliyeshambuliana naye mwanzo.
“Bertha, upo sawa? Hiyo suti yake haitegemei akili kwenye kushambulia; ndiyo silaha hatari kutengenezwa duniani,” aliongea Yulia, akimwangalia Bertha aliyeonekana akitema damu.
“Mkurugenzi, ungeongea mapema sasa. Nilijua shambulizi lake ni la kawaida tu.”
“Hata mimi ndio mara yangu ya kwanza naiona sasa hivi. Nilisikia uundaji wake lakini sikuwahi kuthibitisha. Ila si wamepata tayari Earth Axis, kwanini wametuma mwanajeshi aliyevaa suti hatari kama hii?” aliongea Yulia, akiwa haelewi ni vipi jeshi la kimarekani walivyoachia wazi kadi yao muhimu kama hiyo.
Muda huo, yule mwanajeshi katika ile suti alipiga hatua kumsogelea Yulia.
“Miss Yulia, I am Colonel Bird of the Delta Zero Team. I hope you can cooperate with me. If you want to resist, I can only break your arms and legs…” aliongea akijitambulisha kama Afande Bird na kusema anamtaka Yulia kutoa ushirikiano, la sivyo atamvunja miguu na mikono.
“Mzuieni haraka, hatuwezi kuruhusu amchukue Yulia!” aliongea kwa nguvu Hebert baada ya kuona lengo la yule mwanajeshi lilikuwa ni Yulia.
Lakini wanajeshi waliokuwa wamebakia, hawakuwa na ujasiri tena wa kumsogelea yule mwanajeshi; hata Hebert mwenyewe hakuwa na ujasiri wa kufanya chochote zaidi ya kujishika kifua.
“Wajinga nyie Watanzania, kwa hii suti yangu ya chuma hata mlete vifaru hamuwezi kunifanya lolote,” aliongea na kisha aliachia miale ya mionzi, akilenga baadhi ya wanajeshi waliobakia na wakafa palepale.
Yulia sura yake ilifubaa; mpaka dakika hiyo alijua kama atakimbia, matokeo yatakuwa mabaya zaidi.
“Acha kuua wanajeshi wasio na hatia. Nipo tayari kuondoka na wewe,” aliongea Yulia.
“Yulia, hapana!”Aliongea Hebert.
“Mkurugenzi, wewe kimbia. Nitamchelewesha kwa kupigana naye,” aliongea Bertha kishujaa, akitokezea mbele. Palepale alikusanya nishati za mbingu na ardhi na kutumia mbinu yake ya ufunuo wa moto mtakatifu.
“Naona unatumia mbinu ya holy fire!!” aliongea Kanali Bird bila ya kusogea nchi wala kuonyesha hofu zaidi ya uwezo wa Bertha.
“Nyakati za wanajeshi wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi zimekwisha; teknolojia na itamalaki,” aliongea Bird huku akimpiga Bertha ngumi ya tumbo, kumfyatua hewani huku akitema damu nyingi na kujingonga kwenye mnazi.
“Berthaa!!!”
Yulia alishindwa kuvumilia na kuliita jina la bodigadi wake. Ingawa hakuwa amefahamiana na bodigadi huyo kwa muda mrefu, kitendo cha kujitoa mhanga kuokoa maisha yake kilimgusa.
Tokea dakika ambayo Hamza alitokea na kuleta machafuko kwenye ulimwengu wake usio na hisia, kuna kitu kilikuwa kimebadilika sana. Kulikuwa na kitu kipya kinachoanza kumea katika moyo wake.
Afande Bird wala hakujali kama Bertha alikuwa mzima au amekufa. Palepale alimsogelea Yulia na kumshika shingo yake.
“Yulia, tunaondoka pamoja.”
Yulia macho yake yalikuwa mekundu pekee; pumzi ilianza kumtoka kwa shida. Moyo wake ulikuwa umejaa huzuni kubwa lakini hakuweza kufanya lolote. Muda ule alitamani kugeuka nyuma na kuona muujiza wa Hamza kujitokeza tena na kumsaidia.
Lakini ni kama matamanio yake yalijibiwa, kwani palepale sauti aliokuwa akitamani kusikia iligonga masikio yake.
“Afande roboti, hebu subiri kwanza, nina kitu mnachotaka hapa.”
Yulia mara baada ya kusikia sauti hiyo, mwili ulimsisimka. Colonel Bird aligeuka mara moja, pamoja na kundi la wanajeshi waliosalimika, wakiuongozwa na Hebert.
“Earth Axis! Umefanikiwa kuipata?” aliongea Yulia kwa mshangao.
Wanajeshi pia walijikuta wakishikwa na ari mpya mara baada ya kuona Earth Axis ilikuwa kwenye mikono ya Hamza. Hakuna aliyeweza kufikiria kwamba mwanajeshi huyo asiyefahamika angeweza kutoka akiwa hai, tena akiwa ameokoa kitu muhimu kama hicho.
“Ni bahati kwamba sijafeli, lakini ni bahati mbaya umeshakamatwa,” aliongea Hamza.
“Vipi kuhusu wanajeshi kumi wa Delta Zero?”
“Wanajeshi kumi kutoka wapi? Walikuwa wapo watatu pekee pamoja na msaliti Ndiswe, na nimewaua wote,” aliongea Hamza, akifanya kila mtu kushangaa. Palepale waligeuka na kumwangalia Hebert.
Hebert aliishia kuangalia chini kisha alijifanyisha kuwa katika hali ya maumivu na kuanza kukohoa. Kitendo kile kilimfanya Hamza kuelewa kinachoendelea, na alimwangalia.
“Yaani umepata hadi ujasiri wa kudanganya wenzio kwa kujigamba kulikuwa na wanajeshi zaidi ya kumi ilihali mwanajeshi mmoja tu anaweza kukuua?” aliongea Hamza kwa kejeli, jambo lililomfanya Hebert hasira kumpanda maradufu. Lakini hakuongea chochote.
“Muachie huyo mwanamke na nitakupatia hiki kitu,” aliongea Hamza.
“Hamza, acha ukichaa. Unajaribu kufanya nini?” aliongea Yulia kwa mshangao.
“Unadhani nafanya nini? Nakuokoa kipenzi changu,” aliongea Hamza.
Baada ya kusikia kauli hiyo, wanajeshi wote walijua uhusiano wa Hamza na Yulia.
Hebert uso ulizidi kuwa mweusi na mkono mmoja aliishia kukusanya mchanga kana kwamba umemkosea.
“Kupitia mfumo wangu wa utambuzi nimeweza kuona uwezo wako; hakika uwezo wako sio wa kawaida, lakini kipi kinakupa ujasiri kuona unaweza kunishinda na mimi?”
“Vipi? Unataka kujaribu?” aliongea Hamza, na lile roboti mtu macho yake yalitoa miale miekundu kwa dakika kadhaa kisha ikafifia.
“Kwa leo sio muda sahihi. Mpango wetu wa awali ni kuipata Earth Axis. Ukinipatia hicho kiboksi, nitamwachia Yulia.”
“Najua wanajeshi wa Kimerekani mnasifika kwa ujanja, ila nipo tayari kukuamini awamu hii. Nina uhakika hutotaka kuiabisha nchi yako,” aliongea Hamza, akisogea na kuweka kile kiboksi kwenye ardhi.
“Hamza, nakuomba usifanye hivyo. Unajua hata Earth Axis ni kitu gani mpaka uwapatie?” aliongea Yulia kwa masikitiko makubwa.
“Sijui chochote kuhusu hicho kitu, lakini hakijalishi ni kitu gani, sio muhimu kwangu kama wewe,” aliongea Hamza.
Kauli yake ile ilimshangaza Yulia; ni kama muda umeganda ghafla.
“Vizuri sana kijana, hakika unajua kupenda,” aliongea Afande Bird, kisha alisogelea kile kiboksi na kukichukua, kisha akamwachia huru Yulia.
Baada ya Afande Bird kupata kitu muhimu kama hicho, hakujali tena. Palepale aligeuka, miguu yake ghafla ililipuka miale ya moto na kumfyatua kwenda angani.
Wanajeshi walitamani kumshambulia lakini alikuwa ashapotea tayari angani.
“Spidi ya ajabu kweli! Kwanini anaonekana kama roketi?”
“Aisee, inamaanisha teknolojia ya roketi imeendelea kiasi hiki?” Wanajeshi walijikuta wakiongea wao kwa wao, wakiwa hawaamini.
Hamza hakujali alichopoteza. Palepale alimsogelea Yulia na kumshika.
“Yulia, hujaumia popote?” aliuliza Hamza.
“Earth Axis ipo wapi?” aliuliza Yulia, ambaye hakuwa na hisia zozote kwenye macho yake.
“Earth Axis niitoe wapi tena? Si umeshuhudia mwenyewe nikimpa yule roboti mtu?”
“Acha maigizo basi. Kwa ninavyokujua, lazima umempa boksi tupu pale,” aliongea Yulia akiamini kwamba Hamza ametumia mbinu.
“Unadhani ingewezekana kumpa boksi tupu? Ile suti teknolojia yake ni ya hali ya juu, ina macho ya X-ray na unaweza kuona kama ndani kuna kitu au hakuna. Sikuona hata haja ya kujifanya mjanja. Uhai wako ni muhimu zaidi,” aliongea Hamza.
“Kweli umempatia? Wewe mshenzi, ni akili gani hiyo?”
“Sikuwa na jinsi. Sikuona haja ya kuhatarisha maisha yako.”
“Mimi ni nani mpaka niwe muhimu kwako? Nadhani una matatizo kwenye akili yako wewe,” alifoka Yulia.
“Nimeshakwambia wewe ni mrembo wangu tayari. Bado unasahau kauli yangu, unadhani natania?”
Yulia hakuwa na uhakika wa jinsi ya kuhisi katika moyo wake, maana alihisi kama hakuna kitu alichojisikia. Hakuhisi shukrani wala chochote, alilaumu Hamza kwa kutoa Earth Axis.
Alijua fika kwamba suala hilo likifika kwa viongozi, lisingekuwa na utofauti na kuisaliti nchi kwa sababu ya mwanamke.
Hata hivyo, katika akili ya Hamza, Yulia ni muhimu zaidi kuliko Earth Axis.