hamimahmad894
Member
- Sep 9, 2024
- 11
- 11
Mchawi yaan siku umekamilisha kuiandika yote tangazo lako moja tu linatosha kwan naisubir sanaAu kama vipi na wewe usichukulie ahadi zangu siriasi. Simple
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchawi yaan siku umekamilisha kuiandika yote tangazo lako moja tu linatosha kwan naisubir sanaAu kama vipi na wewe usichukulie ahadi zangu siriasi. Simple
Sasa unasoma ya nini na umejuaje maringo ya mwandishi kama humfuatilii jaribu kuheshimu kazi ya mtu boss huenda wewe unasoma kujiburudisha lakini yeye anaendesha maisha yake kupitia huu uandishi kwahyo lazima awe na strategies za kuingiza pesa kupitia kazi zake za sanaa.Simulizi mbaya mwandishi ana linga
U'r the best 🙏SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.
MTUNZI:SINGANOJR
SEHEMU YA 141
Don’t die
Yulia hakuwa na uhakika jinsi ya kuhisi katika moyo wake, maana alihisi kama hakuna kitu alichojisikia. Hakuhisi shukrani wala chochote, alilaumu Hamza kwa kutoa Earth Axis. Alijua fika kwamba suala hilo likifika kwa viongozi, lisingekuwa na tofauti na kuisaliti nchi kwa sababu ya mwanamke.
Hata hivyo, katika akili ya Hamza, Yulia ni muhimu zaidi kuliko Earth Axis.
"Hamza, wewe ni mjinga! Ngoja viongozi wa juu wa nchi wasikie ulichokifanya, uone kama wanawake wako uliowaacha Dar watakuwa salama," aliongea Yulia huku aking'ata meno kwa hasira na kumfanya Hamza kuishia kujikuna kichwa.
"Hili lishakuwa tatizo sasa, unaonaje nikimfukuzia? Pengine ninaweza kumkamata na kumpokonya?"
"Kumfukuzia! Kama hatukuweza kumfukuzia wakati akiwa kwenye macho yetu, unadhani kila mtu anaweza kuwa mjinga kama wewe na kukuamini?" alilalama Yulia.
"Hey! Yulia, hebu acha kuzidisha. Ijapokuwa mimi ni mvumilivu sana kwa wanawake wangu, lakini kuna mpaka hupaswi kuvuka," aliongea Hamza mara baada ya kuona Yulia ni kama anataka kumkosea heshima.
Yulia alikuwa na hasira kiasi kwamba aliishia kumpiga ngumi Hamza kifuani.
"Nazidisha kivipi! Sio tu kwamba natamani kukufokea, natamani kukuua pia. Kuna haja gani ya kuishi bila ya kuwa na Earth Axis? Unadhani wakuu watatuacha salama?"
"Kwa hiyo tufanyaje? Mimi niliwazia usalama wako kwanza," aliongea Hamza na alikuwa akimaanisha; alihofia kama asingewapatia hicho kitu basi Yulia angedhurika kweli.
Mara baada ya kufikiria kuhusu alichokifanya kwa mara ya pili, aliona pengine maamuzi yake hayakuwa sahihi.
Yulia, mara baada ya kusikia maneno ya Hamza, alimwangalia kwa sekunde kadhaa na kisha hakujali tena kukasirika.
"Njia ya kutatua hili tatizo ninayo, lakini kuanzia sasa hivi unapaswa kunisikiliza kila nitakachokuambia," aliongea Yulia na Hamza kutingisha kichwa.
Hamza, tokea mwanzo, alijua Yulia kwa namna alivyokuwa na akili, lazima kuna njia anayo ya kuweza kuitumia kuirudisha Earth Axis. Ndiyo maana aliitoa bila shida.
"Hakuna tatizo, nitakusikiliza kuanzia sasa," aliongea Hamza.
Yulia hakuwa na haraka kabisa, na palepale aligeuka na kusogelea sehemu ambayo Bertha alikuwa amedondokea. Alichuchumaa na kugeuza uso wa Bertha ambao ulikuwa umetapakaa damu.
"Madaktari wetu wapo wapi?" aliuliza Yulia.
"Kanali Yulia! Madaktari wetu mmoja amefariki na mwingine ameumia," aliongea mwanajeshi aliyekuwa pembeni.
Yulia pia alikuwa ni mwanajeshi mwenye cheo maalumu cha Ukanali, na hiyo yote ni kutokana na mchango wake jeshini katika upande wa sayansi na teknolojia.
Hamza, mara baada ya kusikia kauli hiyo, aliishia kukunja sura na kisha palepale alisogea na kuchuchumaa pia kuangalia hali aliyokuwa nayo Bertha kwa kushika mkono wake.
"Ameumia ndani kwa ndani na kutoa damu, lakini sio tatizo kubwa sana. Mbinu yake ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ina nguvu sana ya kumsaidia kuimarisha afya yake na kuponya majeraha kwa haraka. Pia ashafikia levo ya nafsi huyu ambayo ni ya ukaidi wa asili. Ndani ya siku tano au kumi, atakuwa amepona kabisa," aliongea Hamza.
"Wewe unajuaje?" aliuliza Yulia.
"Ninaweza kuua na kuponya pia," alijibu Hamza.
"Una uhakika?" aliuliza Yulia akiwa na wasiwasi na kumfanya Hamza kucheka.
"Yulia, tangu lini ukawa na wasiwasi juu ya watu wengine?" aliuliza Hamza.
Yulia alijua ni kweli alikuwa tofauti na mwanzo; aina hiyo ya hisia asizozielewa ilisababisha moyo wake kuwa katika machafuko.
"Acha kuongea ujinga. Sitaki kuingia katika matatizo na viongozi wake kwa sababu yangu," aliongea.
"Kama ni hivyo basi sawa," alijibu Hamza bila kuongezea neno na akaishia kumwangalia mwanamke huyo kwa tabasamu.
Yulia hakuthubutu kumwangalia Hamza usoni. Aliishia kusimama na kisha akaanza kutembea.
"Nifuate, ni muda wa kurudisha mashambulizi," aliongea.
Hamza alimwangalia mwanamke huyo kwa nyuma na namna nywele zake zilivyokuwa zikisambazwa na upepo. Macho yake yalichanua pale pale, kisha akaifuata nyuma yake.
Wawili hao walirudi ndani ya maabara ile ya kijeshi. Watu waliokuwa ndani ya maabara hiyo walishaokolewa nje na kambi yote ilikuwa tupu.
Yulia aliwasha mfumo wa dharura wa umeme, na mara moja tarakilishi zote pamoja na skrini ziliwaka upya ndani ya sekunde chache, na kufanya eneo lote kupambwa na mwanga unaobip na kuzima kwa namna ya kupendeza macho.
"Sababu ya kuchagua kujenga maabara hii katika kisiwa cha Chole ni kwa sababu eneo hili kuna mkondo mkubwa wa bahari ambao tumeutumia kutengeneza chanzo cha umeme wa dharura. Hivyo, hata kama laini kubwa ya umeme ikiharibika, umeme unaopatikana unatosha kabisa," aliongea Yulia huku akipangusa kioo kikubwa kilichokuwa upande wa kushoto akimuonyesha Hamza mitambo ya kuzalisha umeme iliyofungwa chini ya maji.
Hamza, baada ya kuchunguza mfumo ule wa kutengeneza umeme, macho yake yalichanua baada ya kuona sio wa kawaida kabisa. Walitembea upande mwingine wa juu kabisa na Hamza alishangazwa na aina ya keyboard ndogo sana ambayo ilikuwa kama kishikwambi, aliyoanza kuitumia kuendesha kila aina ya skrini bila shida yoyote.
"Hii aina yako ya keyboard, inafanya vipi kazi kudhibiti maabara nzima?" aliuliza Hamza, akimfanya Yulia kuinua kidole chake na kuelekezea kichwani.
"Hii keyboard nimeunganisha na mawazo yangu, ninachoamua kitokee, kinatokea," aliongea.
"Mh! Kwa staili hiyo, hata kama mtu akijaribu kuvamia na kutaka kuiba tafiti zako, itakuwa ngumu sana," aliongea Hamza huku akitingisha kichwa chake.
"Ulidhani mke wako mwenye IQ ya 180 anaweza kunizidi. Ni kwamba tu sijawahi kujali sana maswala ya kupima uwezo wangu wa akili au kujiunga na hizo taasisi za kijinga jinga."
"Kwahiyo unasema unamzidi mke wangu?"
"Bila shaka namzidi kila kitu likija suala la kutumia akili, au unataka kunishindanisha naye?" aliongea Yulia.
Hamza alitingisha mabega na kisha alitembea na kumkumbatia Yulia kwa nyuma.
"Darling, vipi kwanza kuhusu mpango wako wa kurudisha mashambulizi?"
"Hebu niachie kwanza wewe mshenzi," aliongea Yulia huku aking'ata lipsi zake. Alikuwa amekosa neno juu ya matendo ya Hamza.
"Nimeshakuambia uache kuniita mshenzi, la sivyo haitakuwa habari nzuri kwako," aliongea Hamza akiwa siriasi, lakini Yulia hakuongea neno na aliendelea kuweka umakini kwa kile alichokuwa akifanya.
Baada ya kama dakika kumi ya kuandika kwa haraka, kitufe cha rangi nyekundu kilitokeza katika skrini, na alibonyeza. Palepale, ramani ya baharini ilionekana huku kukiwa na mzunguko wa radar ukifanya kazi.
"Unajaribu kufanya nini? Usiniambie unajaribu kutafuta manowari yao kupitia radar. Wametumia EMP kuingilia mawasiliano."
"Wewe unachozungumzia ni radar zile za zamani, lakini mimi radar ninayotumia hapa ni teknolojia mpya kabisa na inatumia teknolojia ya Gravity detector, na natumia kuskani juu ya uso wa maji kuona ni upande gani ilipo," aliongea Yulia.
"Kwahiyo unachomaanisha ni kwamba kama manowari yao itakuwa juu ya maji, uzito wa maji katika eneo husika utakuwa tofauti na utofauti huo unamaanisha ndiyo eneo walipo?"
"Ni kama hivyo, lakini ulichoongea wewe ni nadharia tu. Hii teknolojia bado utafiti wake sijaukamilisha na sina uwezo wa kuskani umbali mrefu na kutoa majawabu sahihi. Kama wako mbali sana na hapa, sina uhakika kama itafanya kazi," aliongea.
Hamza aliweza kuelewa kiasi nadharia juu ya teknolojia hiyo, hata hivyo, asingeweza kujua kila kitu. Kama alichoelezea ni sahihi kwa asilimia mia moja, basi Yulia hakuwa genius.
“Manowari tatu!” Yulia aliongea huku akikunja sura.
“Kama kuna manowari tatu, kazi ishakuwa ngumu tayari hii. Tutajuaje ni ipi imebeba Earth Axis?” aliendelea kuongea, akimfanya Hamza kuangalia manowari hizo kwa umakini.
“Ninaamini ambayo ipo karibu zaidi na kisiwa ndiyo imeibeba,” Hamza aliongea.
“Unajuaje? Au unadhani colonel Bird hawezi kwenda mbali na ile suti yake? Isitoshe pia wana drone maalumu ambazo zinaweza kuwapeleka kwenye manowari ya mbali,” Yulia aliongea, na kumfanya Hamza kutingisha kichwa kuonyesha kukubaliana, lakini pia kujutia.
“Nilifanya makosa kumkabidhi,” Hamza aliongea.
Yulia, baada ya kusikia kauli hiyo ya masikitiko kutoka kwa Hamza, kidogo tu atapike. Yeye kama mwanasayansi, kitu ambacho alikuwa akichukia ni kuotea jambo bila kuwa na sababu za kimantiki.
“Hebu kuwa siriasi basi! Uwezo ambao ninao ni kukupeleka katika manowari yao moja, na kama si sahihi basi tutakuwa tumefeli,” Yulia aliongea.
“Unadhani ni kipi tutafanya sasa? Katika dunia hii kila kitu tunaotea tu, na kinachofanyika ni kuelemea upande ambao tunaona kuna asilimia kubwa za ushindi. Halafu pia najua saikolojia ya wanajeshi, hivyo sidhani kama nimekosea,” Hamza aliongea.
“Ni tofauti na unavyowaza. Nisipofanikiwa kuirudisha Earth Axis sitoweza kukulinda dhidi ya kitakachokutokea,” Yulia aliongea.
Hamza alikubaliana naye na kuona kama atajijengea uadui na nchi, hawezi kuwa salama na labda kitu atakachofanya ni kuichukua familia yake na kukimbia nchi.
“Yulia, si umesema unao uwezo wa kunipeleka kwenye submarine? Nafikaje?” aliuliza Hamza.
“Submarine yao inatembea kwa spidi ya kilomita tano kwa saa, ni ngumu kuwapata kwa njia ya maji. Hata kwa ndege itakuwa ngumu kuwazuia maana submarine yao ina mfumo wa kujilinda na makombora,” Yulia aliongea, kisha akamgeukia Hamza akiwa na uso uliojaa usiriasi.
“Kwahiyo unapaswa kufika eneo walipo moja kwa moja, na baada ya hapo itakuwa juu yako,” Yulia aliongea.
“Kama ni hivyo, nitafikaje moja kwa moja walipo kutoka hapa? Ni kifaa gani natumia?” Hamza aliuliza.
“Mpango wangu ulikuwa ni kukuonyesha tu majaribio yangu, na sikuwahi kudhania utahusika moja kwa moja,” Yulia aliongea na palepale alitembea na kuingia kwenye chumba kingine kilichokuwa kimefungwa kwa mfumo maalumu.
Hamza alishangazwa na kile kilichokuwa mbele yake. Kulikuwa na kifaa kikubwa kilichojengwa kwa chuma kigumu chenye mwonekano wa silver. Kifaa hicho kilikuwa na nguzo mbili pembeni za chuma, na katikati kulikuwa na duara kubwa lililokaa kama yai.
Ilikuwa ni kifaa kilichotengenezwa kufanana kabisa na ngao ya Taifa, yaani kulia na kushoto ilikuwa ni kama watu wamesimama na kushikilia ngao iliyo na tundu kubwa katikati. Nyuma ya kifaa kile kulikuwa na chupa kubwa lililounganishwa, lilikuwa kubwa mno kama yale matanki ya kuhifadhia mafuta ya petroli.
“Unakwenda kuwa binadamu wa kwanza kwenda kutumia hii teknolojia. Ukweli ni kwamba unaweza kuwa chaguo sahihi zaidi kuanza kutumia wewe kama sehemu ya majaribio yake,” Yulia aliongea huku macho yake yakiwa yamechanua kwa ari kubwa.
“Hii teknolojia nimeipa jina la Space Jumper au unaweza kusema Space warping Device,” Yulia aliongea.
“Nini!?” Hamza alihisi ni kama hakusikia vizuri kile alichoongea mwanamke huyo. Ijapokuwa alikuwa amezoea kuona vitu vikubwa vya kushangaza na alikuwa na uwezo wa kuishi maisha marefu katika hatari kuliko mtu yeyote, lakini alizidi kushangazwa na Yulia.
“Kwahiyo unasema hiki kifaa kazi yake ni kumfanya mtu kuweza kuteleport?” Hamza aliuliza.
“Ndio, na huna haja ya kuwa na wasiwasi. Nishaifanyia majaribio hii teknolojia kwa kutumia mawe, panya, na ngedere. Ijapokuwa nilifeli kwa angalau mara mia katika majaribio, lakini nilifanikiwa mara ya mwisho. Hiki kifaa kazi yake ni kukutoa eneo moja kwenda lingine mara moja tu, na kwa fitness ya mwili wako huwezi kupata shida yoyote,” Yulia alieleza.
Hamza alijikuta mwili wake ukisisimka huku akishikwa na jasho la ubaridi baada ya kugundua ukweli. Ni muda huo aliweza kujua mwanamke aliyekuwa mbele yake alikuwa akiogopesha kuliko alivyofikiria.
“Umewezaje kutengeneza kifaa kama hiki? Ni kanuni gani ya kifizikia imekuwezesha? Aina hii ya kiteknolojia imepita teknolojia ya kawaida ya kibinadamu tokea kustaarabika kwake,” Hamza aliuliza.
“Hata kama nikikuelezea, unaweza usielewe. Lakini kitu pekee ninachoweza kukuambia ni kwamba hii teknolojia sio mimi niliyeigundua. Nilichokifanya ni kutumia ramani iliyokuwepo na kutengeneza kwa malighafi za hapa hapa,” Yulia aliongea na kumfanya Hamza kutoa macho.
“Usiniambie umeweza kutengeneza hiki kitu kwa sababu ya Earth Axis?” Hamza aliuliza na kumfanya Yulia kuvuta pumzi nyingi. Kisha palepale alitembea na kwenda kumshika Hamza shingoni kwa mbele, na kutokana na Hamza kumzidi kirefu, alijirefusha na kufikia upande wa sikio lake.
“Watu wengi wanachokijua ni kwamba Earth Axis ni kitu muhimu sana, lakini hawajui thamani yake ipoje. Ukweli ni kwamba Earth Axis ni kama kitabu kinachoelezea historia ya ustaarabu wa jamii ulioendelea zaidi kuliko wa kwetu binadamu. Kwasasa ni mimi pekee ninaweza kutafsiri na kuielewa, ndiyo maana unaona kila kitu kilichopo ndani ya hii maabara ni kigeni kwenye macho yako. Ikitokea kifaa hiki kikatua katika mikono ya watu wabaya na wakaelewa maana yake, nadhani unajua nini kitakwenda kutokea,” Yulia alieleza.
Muda huo moyo wa Hamza ulikuwa ukidunda kwa kasi mno, alijua kwanini Himidu hakutaka kumwambia chochote kuhusu majaribio haya yanahusu nini zaidi ya kumwambia kwamba atapata faida kama atahusika katika haya majaribio kwa kuja kutoa ulinzi katika eneo hilo, lakini kumbe alichokuwa akifukuzia na kufanyia kazi kwa siri ni kitu zaidi ya sayansi na teknolojia.
"Nadhani nimeelewa sasa, tuanze kazi," aliongea Hamza huku akilazimisha tabasamu.
"Hauogopi? Hii ndio mara ya kwanza naenda kufanya majaribio ya space jump na mwanadamu."
"Kuogopa! Licha ya kujua lugha nyingi na kushindwa hata kuzihesabu, kwangu neno woga ni neno ambalo sijawahi kuijua maana yake katika uhalisia."
"Hee wewe! Endelea na majigambo tu," aliongea Yulia akivuta mdomo na kisha aligeuka.
"Ngoja nikuletee vifaa vya kupigia mbizi," aliongea.
"Haina haja, hata kama huwezi kunipeleka moja kwa moja mpaka ndani ya submarine, mwili wangu una uwezo wa kutosha wa kupiga mbizi bila shida, isitoshe kutumia hivyo vifaa ni kuniongezea mzigo."
"Acha ukichaa basi, unajiona umekuwa superman?"
"Unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unanifikisha zilipo manowari zao na sitokuangusha," aliongea Hamza kwa kujiamini.
"Ni kama nilivyosema, sina uhakika asilimia mia moja kama naweza kukuingiza moja kwa moja ndani ya manowari zao, kutokana na urefu wake ni mkubwa sana na sijawahi kuufanyia majaribio, unaweza kupasuka ukiwa njiani," aliongea lakini Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa wala kugopeshwa na maneno yake.
"Najua huwezi kuniacha nife, wakati tayari ushakufa na kuoza kwa ajili yangu," aliongea na kauli ile ilimshitua kidogo Yulia na pale pale aligeuka na kusogelea kile space jumper.
"Yulia, hata kama nisipoweza kurudi, kumbuka kuwaambia wakubwa zako nimekufa kwa ajili ya taifa, naomba usifanye mambo kuwa magumu kwa mke wangu na wengine," aliongea Hamza na kumfanya Yulia kung'ata lipsi zake bila kugeuka na kuendelea kuandika vitu kwenye keyboard.
"Hilo halitokuwa jukumu langu sasa," aliongea.
"Ninaamini utafanya kama nilivyosema," aliongea Hamza.
Yulia aliendelea kutumia mkono wake kuunganisha maumbo kwenye skrini pamoja kama maduara hivi na kisha kwa kutumia ramani alitengeneza target ya eneo ambalo Hamza anakwenda kutua na kisha alimgeukia Hamza na kumwangalia na alivyoona amekaa sehemu sahihi mbele ya mdomo wa kifaa kile alitingisha kichwa na kisha akageuka na kubonyeza kitufe.
"Utamezwa na kifaa na kutemwa ndani ya sekunde kumi tu, siwezi kusema ni hisia gani utapata wakati huo kutokana na kwamba wewe ndio binadamu wa kwanza kufanya haya majaribio. Good luck," aliongea.
Hamza alitingisha kichwa na kisha akafumba macho yake akiacha kufikiria kitu chochote.
Yulia alivuta pumzi nyingi na kisha alibonyeza kitufe cha rangi ya njano na pale pale yale maumbo aliokuwa ameyaunganisha katika skrini yalianza kujiunganisha kwa namna ya ajabu huku sauti ya kieletroniki ikisikika.
"Space Jump Device 0.17 has entered operational mode. Fusion reactor power is fully online... Initiating lock on target's 3D spatial coordinates..."
Dakika ileile ndani ya lile tanki mwanga ulionekana ukija kutoka ndani ya fusion reactor ukiwa unazunguka kwa spidi kubwa, mzunguko ule wa nishati uliokuwa ukionekana mbele yake ulitosha kutingisha dunia kutokana na ukubwa wa teknolojia yake. Kuwa na teknolojia ya kudhibiti wingi wa nishati kama hiyo ilikuwa ni kama kudhibiti nishati ya dunia, ilikuwa ni nishati safi ambayo inaweza kugeuza uchumi wa dunia.
Hamza pale pale alielewa kwanini Yulia alikuwa na ujasiri wa kusema kifaa hicho kina uwezo wa kumteleport mtu, kumbe ni kwa nguvu ya hiyo nishati.
Ni sawa na kusema teknolojia ya Yulia ilikuwa kubwa na hatari zaidi ya teknolojia ya nyuklia bila kuuma maneno.
"Ten... nine... eight..."
Sauti ya kieletroniki ilianza kuhesabu kwa kurudi nyuma, sehemu ambayo alikuwa amesimama Hamza alikuwa ashapotea tayari kwa kumezwa na mwanga, mkono ule wa chuma ulikuwa ukizunguka kwa spidi kubwa sana. Kitendo cha kuhesabu kumalizika palepale ule mwanga wa kile kifaa ulipungua kwa namna fulani ya kuzama kwenda ndani ya ile chupa kubwa na kupotea kabisa, na kila kitu kilirudi katika hali yake ya kawaida.
Yulia mara baada ya kufika juu ya Transmission Platform kumwangalia Hamza hakuonekana kabisa na aliishia kuongea maneno ya chinichini.
"Don’t die."
Katikati chini ya maji ndani ya manowari ya kijeshi isioweza kuonekana kabisa kutokana na teknolojia yake, wanajeshi wengi wa Delta Zero walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wakinywa na kula.
"To our fallen comrades! Their sacrifice was worth it! We got the Earth Axis! Long live America!" aliongea Kanali Bird akiwa amesimama juu na glasi ya mvinyo, akiwapa ishara wanajeshi wenzake ya kugongesheana cheers kama namna ya kuwaenzi wenzao walioweza kujitoa muhanga katika misheni hiyo na kufanikisha kuipata Earth Axis.
Wanajeshi hao hawakuwa na huzuni, licha ya kwamba wenzao walikufa, lakini mafanikio walioweza kufanikisha waliona sio bure na ndio maana walijazwa na vicheko wakati wakifurahia pombe.
"Kanali, naomba kuuliza swali. Hiki kitu kinachoitwa Earth Axis ni nini hasa? Tumepoteza wanajeshi wetu wengi kwa ajili ya kukipata lakini hatujui hata maana yake," mwanajeshi mmoja aliuliza na Kanali Bird alitingisha kichwa kuonyesha hajui.
"Hata mimi sijui ni nini hasa, hata Jenerali Smith hajui. Nilichoweza kusikia tu ni kwamba baadhi ya maraisi waliohudumu katika uongozi ndio wanajua kuhusu siri yake."
"Kumbe ni kitu cha siri namna hiyo, ndio maana tumetumika sisi katika kushambulia," aliongea mwingine.
"Nilimsikia General Smith akiongelea kuhusu hili na kusema Earth Axis ilionekana kwa mara ya kwanza nchini Ethiopia na ikapotea, ila baadaye ikaonekana tena nchini Cyelon lililokuwa koloni la Waingereza. Baada ya Vita ya Pili ya Dunia, Malkia Elizabeth alituma wanajeshi kwenda Cyelon kuirudisha, lakini ilipotea tena na habari yake ikaishia hapo kwa miaka mingi. Baada ya hapo, Serikali ya Marekani ilinusa uvumi wa uwepo wa hiki kitu na utafutaji ulianza mpaka ilipobainika miaka ya hivi karibuni ipo Tanzania," aliongea.
"Kanali, imewezekanaje Watanzania wakawa na kitu kama hiki kwenye mikono yao baada ya kupotea huko cyelon kama ulivyosema?" aliuliza mwenzake. Cyelon ilikuwa ni Sri Lanka.
"Hakuna anaye fahamu mpaka sasa imekuwaje Tanzania wakawa wamiliki wa Earth Axis," wanajeshi wote walionekana kusikiliza kwa umakini mkubwa.
Lakini muda huo wote waligutushwa na king’ora kilichoanza kutoa sauti kwa nguvu.
"Du... Du... Du... Du..."
"Tunakaribia kushambuliwa," wote walihamaki.
SEHEMU YA 142.
Wanajeshi hao walijikuta wakishangaa kwa kuona kitu ambacho hakiwezekani kabisa kutokana na teknolojia ya manowari yao.
“Imewezekanaje mpaka tukashambuliwa? Ina maana rada imeshindwa kufanya kazi yake?” waliuliza, maana kutokana na mfumo wao wa rada, kama adui angekuwa anaisogelea manowari yao, wangeweza kumuona akiwa umbali wa maili hata tano.
“Hapana, sio shambulizi, kuna mtu amevamia manowari yetu,” aliongea mwanajeshi mwingine aliyekuwa akiongoza mtambo huku akiangalia skrini iliyokuwa ikionyesha ramani yote ya manowari yao huku wakitoa macho kuona kuna mtu yupo ndani ya manowari yao wakijiuliza ameingiaje.
Isitoshe, walikuwa chini ya maji kwa zaidi ya mita mia nne.
“Kanali, kuna mtu kavamia ndani ya manowari yetu na sasa yupo upande wa store na anasogelea kuja uelekeo wetu,” aliongea bwana aliyekuwa akiangalia kitu cha rangi nyekundu kilichokuwa kikisogea katika ramani ya manowari hiyo.
“Kaingiaje ingiaje?”
“Haijulikani, lakini baadhi ya wanajeshi wetu wamekufa tayari,” aliongea mwingine akionyesha kamera ambazo wanajeshi walionekana wakiwa chini.
Muda huo, sauti ya upepo ilianza kusikika kupitia simu zao kutoka kwa wanajeshi waliokuwa upande mwingine.
“Requesting support, requesting support!”
Kanali, mara baada ya kusikia sauti za vijana wake kuomba msaada, alijikuta akirusha ile glasi aliyokuwa ameshikilia mkononi ukutani na ikapasuka palepale.
“Everyone, get into first-class combat readiness! Go back and support!” Aliamrisha wanajeshi wake kujipanga katika mtindo wa daraja A ili kushambulia.
Lakini sasa, wakati wanajiandaa kuondoka, ghafla eneo walilokuwepo mwanga wake ulizimika mara moja na kukawa giza.
“Hii ni hatari, huyu mtu anajaribu kuharibu manowari yetu...”
Kanali Bird sura iligeuka na kuwa ya kijani palepale na palepale alichukua kiboksi kilichokuwa na kodi maalumu.
“Naenda kuvaa suti yangu ya kijeshi, ipandishe manowari juu ya maji, ni muda wa kumuua huyu mvamizi na kisha kuondoka hapa,” -.
Aliongea na palepale wanajeshi wote walianza kukimbia kuelekea kila uelekeo huku kapteni wa manowari hiyo akifanya kazi ya kuipandisha manowari hiyo juu ya maji.
Wanajeshi wale, baada ya kukimbilia uelekeo wa eneo la mvamizi alipo, walijikuta wakikunja sura mara baada ya kuona wanajeshi wenzao zaidi ya wanne wakiwa chini tayari. Palepale waliweza kumuona mwanaume shombeshombe akitumia ngumi na mateke na chuma kuharibu manowari yao.
Hamza, mara baada ya kumezwa na ile mashine ya Yulia, alijikuta tu yupo ndani ya manowari hiyo ya kijeshi upande wa stoo. Hisia alizopata ni kama vile alikuwa ndotoni kwani ni ndani ya sekunde tu alikuwa kisiwani na wakati huo alikuwa eneo lingine kabisa.
Hamza alijua fika Yulia hakuwa amemdanganya hata kidogo. Aliamini lazima ni kweli Earth Axis ni kitu ambacho ni kutoka kwa viumbe wenye akili sana. Hata kwa akili gani angekuwa nazo, Yulia asingeweza kutengeneza kitu cha maajabu namna hiyo, hivyo ndivyo Hamza alivyofikiria.
Wanajeshi wale wa Delta Zero mara baada ya kumuona Hamza akiwa mbele yao hawakuthubutu kutumia bunduki zao wala ile mionzi kutokana na kwamba wangeharibu manowari. Hivyo, kwa spidi kubwa walimsogelea kupambana naye kwa kutumia nguvu. Na Hamza hakujali sana, isitoshe hilo ndio eneo ambalo alikuwa vizuri zaidi. Katika uchochoro mdogo wa manowari hiyo alipigana na wanajeshi hao mpaka wakaanza kuwa wekundu.
Kila Hamza alivyoshambulia, alikuwa akiharibu pia manowari hiyo mpaka pale alivyotengeneza ufa. Kutokana na presha ya bahari kuwa kubwa, maji yalitoboa na kuanza kuingia ndani kwa spidi kubwa. Kadri maji yalivyokuwa yakiingia ndani, vyuma vilishindwa kushikilia vizuri na kusababisha sehemu nyingi kuanza kuvuja.
Kwa spidi ya kuonekana kwa macho, manowari hiyo ilianza kuharibika kwa kasi kubwa.
“Huyu ni kichaa, hivi hajui hii meli ina kinu cha nyuklia?”
“Pumbavu zake, yupo wapi?”
Kutokana na maji mengi yaliyokuwa yakiingia, iliwapa ugumu wanajeshi kushindana na Hamza na aliishia kushindana na maji kujilinda wasipoteze maisha, huku Hamza akiwatoroka bila ya kuacha nyayo.
Licha ya Hamza kutowahi kuingia katika aina ya manowari hiyo yenye mfumo wa nyuklia ndani yake, lakini tayari alikuwa ameingia katika manowari nyingi sana tu. Hivyo, alikuwa akielewa namna muundo wake ulivyo na ramani yake kwa ujumla.
Mpango wake ni kutafuta wapi Earth Axis ilipohifadhiwa, na moja kwa moja aliamini lazima itakuwepo katika chumba cha Colonel Bird. Hivyo, Hamza uelekeo wake ulikuwa ni kutafuta ni wapi Colonel Bird atakuwa anahifadhi suti yake.
Hivyo, dakika ambayo maji yaliingia ndani, Hamza alitumia nafasi hiyo kwenda ndani zaidi ya vyumba vya manowari hiyo kutafuta Earth Axis. Isitoshe, aliona kama atashambuliwa pande zote na washambuliaji akiwepo Colonel Bird, basi inaweza kumpa shida sana kushinda, isitoshe teknolojia ya suti yake ilikuwa kubwa mno.
Kitu kingine pia alihofia ni Colonel Bird kutoroka na Earth Axis kutoka ndani ya manowari hiyo, ndiyo maana aliona aharakishe maana akitoweka, maana yake na mpango utakuwa umefeli.
Kanali Bird aliingia katika chumba maalumu ambacho suti yake ya kijeshi huihifadhi katika eneo maalumu ili kuendelea kujicharge. Mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho maalumu, alivyotoka nje alikuwa tayari amebadilika na kuwa katika umbo la roboti.
Baada ya miale ya mwanga kutoka upande wa eneo la kichwa chake, palepale aligeuka pembeni na kubeba kile kiboksi chenye Earth Axis na kujiandaa kutoka nje ya manowari hiyo ambayo ilishaanza kuonyesha dalili ya kuzama. Lakini ni dakika hiyo hiyo mtu aliingia ndani ya eneo alipo na kumgonga kwa nyuma. Kilichosikika ni sauti ya peng. Kanali Bird na suti yake alifyatuliwa na kwenda kujigonga kwenye kuta na kuharibu mpaka mlango wa kutokea nje, lakini bahati nzuri suti yake ya chuma haikuweza kuharibika, hata hivyo alishikwa na mshituko wa aina yake.
Tokea aanze kuivaa hiyo suti kama mwanajeshi maalumu wa Delta Zero, hajawahi kupigwa na shambulizi la kushitukiza kama hilo mpaka kudondoka chini.
“Wewe ni nani?” Aliongea huku akisimama na kugeuka nyuma, na alishituka mara baada ya kugundua aliekuwa mbele yake ni Hamza.
“Ni wewe tena!?” Aliuliza huku moyo wake ukianza kusukuma damu kwa spidi akiwa anamshangaa.
“Umewezaje kufika hapa?”
“Sipo hapa kucheza mchezo wa swali na jibu, Earth Axis ni kitu ambacho siwezi kukuruhusu uondoke nacho,” aliongea Hamza
“Wewe ni mwanajeshi wa Kitanzania?” Aliuliza Kanali huyo maana bado hakuamini kama Tanzania inaweza kuwa na mwanajeshi mwenye nguvu kama Hamza.
Hamza hakujibu swali lake, badala yake alipiga hatua mbele na kisha akaushika mkono wa kiroboti wa Kanali Bird. Kwa staili matata sana ya Judo, mkono ule aliweka kwenye bega lake na kuuvuta kwa nguvu. Kutokana na chumba hicho kuwa kidogo kwa saizi ya suti hiyo kugeuka, mkono ule uliharibika palepale kwa kupinda.
Shambulizi lile lilimuacha Bird katika mshituko mkubwa na kujiuliza kama mtu huyo alikuwa binadamu kweli. Haikuwa swala rahisi kuharibu mkono wa suti yake kwa staili ya Judo kama vile anashindana na binadamu wa kawaida.
Hakutaka kufikiria mara mbilimbili, kule kujiamini anaweza kumdhibiti Hamza haraka kuliisha na aliona ampe heshima inayostahili kwenye kupambana naye. Ijapokuwa alishambuliwa mara mbili na Hamza, hata hivyo suti yake haikuharibika sana zaidi ya kuachia kidogo eneo la kiungio chake cha bega. Hivyo kwa spidi kubwa alifyatuka na kumsogelea Hamza ili kumpiga ngumi.
Hamza palepale alikwepa kwenda kushoto na kisha alitumia mkono wake wa kulia kupiga suti ile eneo la kifuani kwa nguvu zake zote na kumfanya Kanali kufyatuliwa tena na kwenda kujipigisha kwenye ukuta kwa mara nyingine na kusababisha cheche.
“Mbona hutumii hayo mashambulizi yako ya mionzi kama ulivyofanya? Hata kama suti yako hiyo ya kijeshi ni silaha hatari lakini ni ngumu kunishambulia mtu kama mimi,” aliongea Hamza mara baada ya kuona ni kama Bird anajaribu kuwa makini.
Bird aliishia kubakia kimya kama mtu ambaye hakuwa na jibu. Kitendo cha Hamza kuharibu sehemu muhimu za manowari hiyo ilisababisha iwe ngumu kurudi juu na suala hilo lilimtengenezea udhaifu Afande Bird, kwani suti yake haikuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi akiwa chini ya kina kirefu cha maji na hata kama angesema atoke nje asingekuwa na uwezo wa kuogelea akiwa na suti hiyo mwilini.
Kutokana na hilo, Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa, alijiambia ili mradi hakuna uwezekano wa mwanajeshi huyo kuingia katika manowari nyingine, hawezi kumtoroka kwa namna yoyote ile.
“You are an expert, a powerful warrior. We can negotiate whatever you want,” aliongea Kanali Bird mara baada ya kuona uwezo wake wa kushinda ni mdogo. Aliona njia pekee ni kumshawishi huyo mwanajeshi kushirikiana naye kwa kumtajia chochote anachotaka.
“Nadhani unajua nchi na jeshi letu vinathamini sana watu wenye uwezo mkubwa,” aliongea akiendelea kuongea.
“Unataka kunihonga?” Aliuliza Hamza.
“Hapana, nakualika kuwa sehemu ya kambi ya watu wa haki, kambi maalumu yenye mchango mkubwa katika uhuru na maendeleo ya binadamu kwa ujumla,” aliongea.
“Kama unataka kunihonga, unapaswa kujua gharama unayopaswa kulipa haiwezi kuwa ndogo.”
Wewe ongea tu, ni kiasi gani cha pesa unahitaji au ni nguvu kiasi gani unahitaji, tunaweza kuongea kila kitu,” aliongea Kanali akiona lazima kuna uwezo wa kumshawishi huyo bwana. Isitoshe, kwa namna alivyoonekana kuwa na asili ya uzungu ndani yake, alimuona ni kama mwenzao.
“Sitaki hela na sitaki nguvu vilevile. Ninachotaka ni Earth Axis,” aliongea Hamza huku akinyooshea mkono kiboksi alichoshikilia Kanali, na kauli yake ilimwacha Bird bila usemi.
“Inaonekana kama hutaki maongezi na mimi,” aliongea, na palepale alikunja ngumi na kufanya kwenzi za vidole vyake zifyatue mionzi kumlenga Hamza.
Aliona kama asipotumia siraha za suti yake, uwezo wa kumshinda Hamza utakuwa mdogo sana. Hivyo, aliona tofauti na kuogopa kuharibu meli hiyo zaidi kwa kutumia silaha zake, ni bora ajaribu.
Kutokana na ukaribu uliokuwepo, ilionekana kama shambulizi lile halikwepeki. Lakini Hamza, kwa spidi ya hali ya juu, alisogea nyuma ya ukuta wa chuma huku akijitahidi kadri awezavyo kuepuka mlipuko.
Boom, Boom, Boom.!!
Mionzi ile ilikuwa kama kombora kwani baada ya kugusana na chuma ilitoa mlipuko mkubwa ambao ulibaribu kebini nzima na kuzifanya sehemu hiyo kuwa na mrundikano wa vyuma.
Ijapokuwa aliweza kuepuka mionzi ile, ilifanikisha kushambulia mabomba ya mfumo wa gesi na hewa ya oksijeni na kufanya kuwe na mfululizo wa milipuko. Milipuko hiyo ilikuwa kama jehanamu inayotaka kummeza Hamza mzima mzima.
Kutokana na mlipuko ulivyotokea na eneo ambalo Hamza alipokuwa amesimama, Kanali Bird aliona kabisa ashamdhibiti mvamizi huyo na kuhusu moto, aliona kabisa hauna athari yoyote kwake kutokana na kuwa ndani ya suti.
Lakini sasa, dakika ileile Hamza alivyotoka katika lindi la moto, alikuwa na spidi ya radi na alimrukia Kanali Bird kwa kumlenga bega lake kwa nyuma.
Kanali Bird aliishia kutoa mshangao akijiuliza Hamza amewezaje kupona mlipuko ule. Licha ya kuvamimiwa kwa nyuma, aliweza kumuona Hamza vizuri kupitia kamera na kugundua hakuwa na majeraha yoyote.
Hamza hakujali mshangao wa mwanajeshi huyo. Kutokana na spidi yake aliyoruka, aliweza kutua vyema katika bega lake na kisha kwa mikono yake yote alishika lile helmeti na kulivuta kwa juu huku akinguruma kama simba.
Kanali Bird alishindwa kujua Hamza alikuwa akitaka kufanya nini, lakini dakika ileile ishara ya hatari ilianza kujionyesha katika suti yake.
“Shit!!”
Kabla hata hajachukua hatua, Hamza aliweza kunyofoa lile helmeti kwa juu na kusababisha cheche nyingi mno.
Uso uliopauka wa Kanali Bird hatimaye uliweza kuonekana wazi bila helmeti. Alikuwa katika hali ya mshituko wa matendo ya Hamza na kumfanya ashindwe hata kuongea neno zaidi ya kumwangalia kama kiumbe cha kutisha.
“Bila ulinzi wa hili helmeti lako, huwezi kufanya chochote,” aliongea Hamza.
“Monster… You’re a monster, just where did you come from?” aliongea kwa sauti ya kitetemeshaji.
“Selaphinii!” aliongea Hamza.
“Wewe ni…” Macho ya Kanali yalimtoka lakini Hamza hakumchelewesha kwani kabla hata hajamaliza sentensi yake, Hamza alimshambulia kwa kumlenga kichwani na palepale kichwa kiligeuka kifusi cha nyama.
Kabla Kanali hajadondoka na suti yake ya chuma, Hamza alipiga sarakasi murua kabisa na kudaka kile kiboksi kilichokuwa kwenye mikono yake. Kisha, kwa spidi ya hali ya juu, alijirusha nje ya maji kupitia mlango wa dharura wa kujiokoa na manowari ile ililipuka palepale.
Upande wa kisiwani Chole, mawasiliano yalikuwa yamerudishwa, na meli nyingi zilizokuwa mbali zilisogea kiswani hapo na kukizunguka, huku kazi kubwa ya kuzima moto na kurudisha hali katika utulivu ikifanyika kwa spidi kubwa sana.
Upande wa Yulia, yeye alikuwa ndani ya CR ya kijeshi akiendelea kurekebisha mifumo iliyoathirika. Herbert alikuwa amesimama kando ya Yulia akiwa na uso usioelezeka na alikuwa akimsumbua Yulia kwa maswali ya kutaka kujua ni wapi Hamza alipo.
“Umempeleka wapi? Au umetumia Space Warp device?” aliuliza, lakini Yulia aliendelea na shughuli zake huku akimpotezea.
“Yulia, hivi unajua unakiuka sheria? Nani karuhusu ubadili mpango mzima wa majaribio?” Herbert alibweka na kumfanya Yulia kuhisi kama ngoma zake za masikio zinataka kupasuka.
“Unatoa wapi muda wa kunipigia makelele? Kwanini usifikirie namna ya kwenda kujielezea kwa wakubwa? Si ni wewe uliefanya maamuzi ya kukabidhi Earth Axis kwa adui.”
“Acha kunisingizia, sijafanya kitu kama hicho,” alijitetea.
“Kuna ushahidi na ushahidi, ni bure tu hata ukijifanya kuwa mjanja.”
“Huo ushahidi umetoka wapi? Yulia, acha kunisingizia kitu ambacho sijafanya,” aliongea huku akiwa na wasiwasi.
“Ushasahau ndani ya hii kambi kuna umeme wa dharura, kila kitu ulichofanya katika lift ya dharura kimerekodiwa na kamera, na kwa taarifa yako, bodigadi wako Pima bado yupo hai. Ijapokuwa ulimsariti, lakini bahati ilikuwa upande wake. Hamza alimsaidia.”
“Nini!?” Herbert uso uligeuka na kuwa mkaa palepale na ishara ya chuki iliuvaa uso wake.
“Vipi, unataka kunishambulia ili kuua ushahidi?” aliuliza Yulia mara baada ya kuona mabadiliko ya Herbert na kuona nia yake.
“Kama unataka kuniua sawa tu, ila nikwambie kila kitu kilichotokea hapa kitafika makao makuu. Hata kama uamue kumuua Pima na mimi, ni bure tu.”
Jasho lilianza kumtoka Herbert mfululizo huku akionyesha tabasamu la unyonge.
“Yulia, tumefahamiana kwa muda mrefu na tumefanya kazi pamoja. Sio hivyo tu, nishawahi hata kuwa mchumba wako. Naomba ulipotezee hili swala na lisiende makao makuu. Ukinisamehe katika hili, naahidi nikija kuwa mrithi wa babu, utapata faida kubwa sana.”
“Kama hutaki kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, ondoka mbele yangu mara moja nikiwa nakuruhusu na usije kunisumbua tena,” aliongea Yulia.
Herbert alihisi kudhalilika sana lakini hakuwa na chakufanya zaidi ya kinyonge kuondoka ndani ya eneo hilo. Lakini wakati huo, mwanajeshi aliingia kwa haraka.
“Naripoti Afande…” Mwanajeshi huyo alitaka kutoa ripoti kwenda kwa Afande Herbert lakini mara baada ya kuona sura yake ilivyo, alimpotezea na kisha alimsogelea Yulia.
“Kanali Yulia, rada yetu imeweza kunasa uwepo wa manowari inayosogelea upande wa kaskazini-magharibi mwa kisiwa,” aliongea.
Herbert mara baada ya kuona mwanajeshi huyo akimpita na kutoa taarifa hiyo moja kwa moja kwa Yulia alijikuta akizidi kukunja sura. Ilionyesha dhahiri kila mwanajeshi aliye kuwa katika kisiwa hicho alikuwa akimdharau na cheo chake cha kusimamia kila kitu kuhusu majaribio hayo kimeenda moja kwa moja kwa Yulia.
“Ni manowari yetu?” aliuliza Yulia.
Tumethibitisha sio moja ya manowari yetu! Kuna haja ya kushambulia?” aliuliza. Yulia alitingisha kichwa kukataa.
“Hapana! Iache isogelee fukwe, hakuna anaeruhusiwa kushambulia bila idhini yangu,” aliongea.
Ijapokuwa mwanajeshi huyo hakuelewa kwanini, alipokea maagizo hayo na kisha akaondoka. Yulia hakuwa na muda wa kuendelea kukaa ndani ya CR (Command Room) na alitoka nje na kutoa maagizo kwa jeshi la ulinzi wa majini huku wakielekea upande wa manowari inaposogelea.
Herbert macho yake yaliishia kuchanua, huku akionyesha hali ya wasiwasi. Upande wa fukwe, magharibi mwa kisiwa hicho, wanajeshi walikuwa washajipanga tayari kwa kila aina ya siraha kushambulia. Yulia alikuwa ameshafika na alikuwa amesogea karibu akiangalia uelekeo wa maji uliojaa giza. Ilichukua kama dakika kumi na tano hivi hatimaye manowari ndogo ya kijeshi ilianza kuonekana taratibu juu ya maji na funiko la juu yake lilifunguliwa na mtu aliweza kuonekana akitoka.
“Kanali, hii inaonekana si manowari ya mashambulizi licha ya kuwa ya America,” aliongea mwanajeshi mmoja. Upande wa Yulia, uso wake ulikuwa umepambwa na tabasamu.
“Amefanikiwa,” aliongea.
“Nani?” wanajeshi wote waliosikia kauli hiyo walijikuta wakishangazwa na kauli hiyo.
“Shusheni siraha zenu chini, Hamza amefanikiwa kuirudisha Earth Axis.”
Wanajeshi hao waliishia kuangaliana na palepale walimkumbuka yule mtaalamu aliemuokoa Yulia, kumbe alikuwa akiitwa Hamza.
“Kumbe ni yeye! Basi ni muda wa kumkaribisha kisiwani.”
Kundi la wanajeshi wenye vyeo vya ukapteni waliongea wakiamini maneno ya Yulia na palepale siraha ziliweka pembeni na boti zilisogezwa karibu ili kumruhusu Hamza kupanda kurudishwa ufukweni.
Upande wa Hamza, mara baada ya kutoka katika manowari hiyo, aliishia kwanza kujivuta kunyoosha mgongo kama mtu ambaye ametoka usingizini.
“Ni muda mrefu sijaendesha submarine,” alijiwazia.
Hamza alikuwa na mafunzo ya kila aina ya udereva. Alikuwa na uwezo wa kuendesha ndege, manowari, meli za kawaida, vifaru, na hata meli kubwa za kivita.
ITAENDELEA- WhatsApp: 0687151346
Daah hatariSHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

Kweli asee atukumbuke na sisiKesho ni km wikiend tu tukumbuke mkuu
Mpaka bi dada shunie ammwite.Kweli asee atukumbuke na sisi