Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Hamza mara baada ya kuongea hivyo , palepale alisimama kwa ajili ya kuondoka , lakini muda huo Rehema ambae alikuwa amebeba kikombe cha kahawa kwa ajili ya Hamza aliingia na alishangaa kumuona Hamza anataka kuondoka.


“Mr Hamza unaondoka baada ya kufika tu?”Aliongea na Hamza alichukua kikombe kile na bila kujali kahawa ilikuwa ya moto ama ya baridi aliipiga yote kwa mkupuo kama maji na kisha akampatia kikombe chake.


“Sister Rehema , asante kwa jitihada zako , ila mimi ndio naondoka hivyo”


“Mr Hamza tafadhari usikasirike! Mzee Mboma ndio alivyo , ila tunahitaji sana msaada wako. Mimi naamini Afande Simba na Afande Himidu kukualika hapa ni kwasababu wanazo sababu zao za msingi”Aliongea Rajabu.


“Balozi huna haja ya kuwa na wasiwasi. Kwasababu nilishakubaliana na Himidu, nitatimiza baadhi ahadi zangu. Lakini kutokana na baadhi yenu tofauti ya kuongea kuhusu ushirikiano ila mnaanza kunihoji, sioni haja ya kuendelea kubakia hapa”Aliongea Hamza na Balozi Rajabu alikuwa na wasiwasi mno.


“Mzee Mbomba ni vizuri ukimwomba radhi Mr Hamza”


“Muache aondoke kama anataka , lazima amechaguliwa kwasababu za kindugu . Kama hana vigezo kwanini tumlazimishe. Kwa uzee wangu huu nishaona watu wengi wa aina yake. Kama wasiwasi ni juu ya ulinzi nitaweka mpango mzuri kwa kushirikiana na majasusi ndani ya Kitengo cha usalama . Pili Baraza la maksi licha ya kuwa la siri lakini pia limeundwa kwa ajili ya kuimarisha amani duniani baina ya makundi , sidhani kama itatokea mtu akataka kutuvamia bila sababu”


“Mzee.. kwanini ni mgumu sana kuelewa…” Balozi alishindwa kujua cha kufanya baada ya kuona Hamza ameshaondoka tayari na haraka sana alimpa maagizo sekretari wake kumsindikiza Hamza.


Katika kikao hicho Balozi alizidi kumshutumu Mboma , kwamba alifanya makusudi kumfanya Hamza kuondoka. Akienda mbali na kusema hata kama Hamza amechaguliwa kutokana na koneksheni na Mshauri mkuu hakupaswa kuongea kwa namna ya kumdhalilisha.


Ukweli ni kwamba watu wote wlaiokuwa katika kikao hicho walikuwa na mtazamo sawa na Mboma. Walikosa tu ujasiri wa kuelezea hisia zao , ila Hamza alionekana wa kawaida sana licha ya kuwa maarufu kupitia tukio la Kisiwani Chole.


Walipata kusikia tu habari za kisiwani na hakuna hata mmoja hapo ambae aliona Hamza akipambana moja kwa moja.


Mboma upande wake hakujali kile ambacho Balozi anaongea na aliishia kukunja midomo kumkejeli , akiamini kabisa alichofanya ni sahihi.


Upande wa nje Rehema alifanikiwa kumuona Hamza akitaka kuingia kwenye taksi na alimwita kwa kumkimbilia.


“Mr Hamza tafadhari usijali sana juu ya kilichotokea. Wote tunamjua mzee Mboma ni mtu anaeongea bila ya kufikiria , hususani likija swala la ukaribu wako na Himidu”Aliongea.


“Kuna tatizo gani mimi kuwa na ukaribu na Himidu?”Aliuliza Hamza


“Afande Mboma alikuwa moja ya watu waliokuwa wakiaminiwa sana na Afande Simba , lakini baada ya kutokea kwa Himidu nafasi yake ilichukuliwa na akaanza kujiona sio wa muhimu tena mbele ya wakubwa. Hakuwahi kupenda namna ambavyo Himidu alipanda cheo haraka haraka mpaka kufikia kuwa mshauri mkuu”Aliongea Rehema.


“Ndio maana , kumbe nimejiingiza katika ushindani wao?”Aliongea Hamza akitingisha kichwa lakini hata hivyo aliona hayo hayamuhusu. Kwanza mwanzoni hakutaka hata kushiriki na ni hila tu za Afande Simba.Ila hata hivyo hakutaka kuweka mambo moyoni kutokana na kile ambacho Mboma alisema kuhusu mpango wa jeshi kutaka kugawa baadhi ya taarifa zinazhohusianisha teknolojia ndani ya Earth Axis, aliona kuna haja ya kuwa siriasi kwani lolote lingetokea, ingekuwa hasara kwa serikali na wasingeridhishwa nae.


Hamza hakujali sana , alipanga kufuatilia swala hilo kwa namna anayoijua yeye, hivyo palepale aliagana na Rehema ambae alikuwa akiomba radhi kwa niaba ya Mboma mpaka anatia huruma.


Hamza hakupanga kurudi hotelini na badala yake alimpa uelekeo mwingine dereva nje kabisa ya jiji mpaka kumfanya dereva yule kushangaa kidogo.Wakati akiwa njiani, Hamza alipokea simu kutoka kwa Afande Himidu.


“Bosi nimesikia kilichotokea . Mboma ni mtu mgumu sana kuelewa licha ya cheo chake na ni mtu wa kukuza hata vitu vidogo visivyo na maana,naomba usimzingatie sana”


“Nawezaje kukasirika kwa kitu kidogo namna hio? Unawaza sana na wewe”Aliongea Hamza huku akicheka.


“Haha.. bosi nilikuwa na wasiwasi tu utaacha kunisaidia ndio maana. Bosi kama sio uwepo wako ndani ya Tanzania sidhani tungekuwa na amani mpaka sasa”Aliongea Himidu.


“Wewe ni muhuni sana , kwahio kumbe hili kongamano lenu lina mpango mwingine wa kugawa siri za Earth Axis lakini ukakaa kimya. Au ulitaka nije kuyajulia hukuhuku?”


“Haha.,. samahani sana bosi , tumeamua kuvujisha taarifa za Earth axis makusudi kurahisishia kazi , ila naamini kwa uwezo wako hakuna tatizo kabisa”


“Hakukuwa na utofauti hata ungeniambia mapema. Ila taarifa mlizowabebesha hawa wanajeshi ni kama kuwashikisha kiazi cha moto”


“Upo sahihi , ila taarifa ambazo tumetoa ni za juu juu sana kuhusiana na mazingira na mfumo mpya wa viwanda na mbinu nyingine za kuboresha zaidi maisha ya binadamu . Hata kama watuibie hawataweza kutengeneza siraha za hatari. Hivyo sidhani kutakuwa na shida kubwa”


“Lazima itakuwa mbinu uliofikiria , mnataka kutoa ushirikiano wa kugawa teknolojia ambayo haihusiani na mambo ya siraha ili kujiimarisha kidiplomasia na kuongeza ushawishi wenu katika siasa ili msiwe wanyonge katika kupambana na nchi kubwa kama Amerika. Himidu hata kama hii mbinu yako itafanya kazi pointi ya msingi ni kwamba , hata wakijua mnachotaka kugawa hakina uhusiano na utengenezaji wa siraha na mambo mengine , unadhani watakubali?. Lazima watafikiri mnajaribu kuwasaidia China na Urusi mahasimu wao wakubwa kiuchumi na kijeshi ili kujijenga, hivyo sidhani kama watakubali kupitwa kirahisi ?”


“Ndio maana tunakutegemea wewe bosi , mazungumzo haya yakikamilika, tutakuwa na washirika wengi kutoka mataifa makubwa na mikataba mingi itasainiwa. Na kwanzia hapo tutakuwa hatuna hofu tena kama taifa dogo, hata kama tukiwa katika ushirikiano mbaya na America lakini bado tutakuwa na sapoti ya kutosha kujilinda kutoka kwingine. Wasiwasi wangu ni kama ambavyo nimekwambia bosi , tunahofia kabla ya makubaliano, taarifa za Earth Axis zitakuwa zimekwisha kuvuja mahali tusipotaka zifike kupitia mashushu wao ndani ya jeshi letu na kama kila mtu akiwa na hizi taarifa za kiteknolojia zitakosa thamani na itakuwa ngumu kufanya makubaliano na haya mataifa na wakakubali”Aliongea na kumfanya Hamza kutaka kucheka.


“Tabu zote hizo ni kwa ajili ya kutaka kunufaika mwenyewe na Earth Axis! Unadhani utaweza kuificha mpaka mwisho , si mshirikiane tu ?”


“Bosi mpango sio kwa ajili ya kuhimili mpaka mwisho , tunachotaka ni kupata muda wa kutosha wa kujijenga , tukifikia hatua ya kuwa na teknolojia ambayo hakuna mwingine alienayo, hakuna taifa litaweza kutugusa kirahisi. Hii ni bahati yetu kuinuka kiuchumi kama taifa na Arika nzima. Licha ya kwamba itakuwa safari ndefu yenye vikwazo vya kila namna”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo , alionekana kuwa katika hali ya kuwaza , ukweli alichokuwa akimaanisha Himidu ni kwamba wanahitaji muda wa kutosha kwa ajili ya Yulia kukwamua kila taarifa iliopo ndani ya Earth axis.


Aliona Yulia alikuwa na kazi ngumu sana, maana kwa mpiganaji kama yeye alichoweza zaidi ni kuufanya mwili wake kuwa imara zaidi na kufikia levo za juu lakini sio katika maswala ya teknolojia.


“Bosi ..”Aliita Himidu mara baada ya kuona Hamza ameacha kuongea na alishindwa kujua anachowaza ndio maana aliita kwa nguvu.


“Bosi lazima utakuwa umekasirika si ndio?”


“Hapana , kuna kitu nilichokuwa nikifikiria , ila niseme umenipa hamasa”Aliongea Hamza


“Hamasa gani bosi?”


“Kufunuliwa ni chanzo cha hamasa , usiulize sana, na usiwe na wasiwasi, japo sipendi kuwasaidia katika mipango yenu ila kwa ajili yako sina jinsi zadi ya kwenda kuonana na Roho Mchafu”


Himidu mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akishangaa na palepale alianza kucheka.


“Haha… , boss kweli unashangaza mno , umefikiria la maana sana. Kwasababu upo Paris sio mbaya kuonana mshikaji wetu , usisahau kunifikishia salamu zangu kwa Roho mchafu”


Hamza hakuendelea hata kujibishana na Himidu tena na palepale alikata simu ile.


Taksi ile iposimama Hamza ni kama alikuwa nje kabisa ya jiji la Paris kutokana na eneo hilo kuwa kama limetelekezwa hivi.
Majengo mengi yaliokuwa katika eneo hilo yalikuwa ni yale ya kale na yenye kuota uozo.


Hamza mara baada ya kusogelea upande wa kulia kuingia katika majengo , watu wengi walikuwa wakimnyooshea vidole na ilionekana walikuwa wakiongea kwa kumtukana.


Lakini hata hivyo Hamza hakuonekana kujali kabisa na aliendelea kutembea kukata mitaa na mara baada ya kuingia katika uchochoro wa nyumba mbili pande kwa pande ndio jinsi aeneo hilo lilivyozidi kuwa tulivu na watu kutoonekana.


Hamza alitembea katika uchochoro huo bila ya wasiwasi , akionyesha alikuwa akijua anakoelekea na dakika chache mbele aliweza kutokezea kwenye uzio uliokuwa na geti kubwa la chuma la rangi nyeusi.


Getini hapakuwa na mlinzi , hivyo Hamza alipita na ile anafika ndani aliweza kukuta eneo kama vile ni mapokezi ya hotelini ndani ya jengo hilo lililoenda hewani na kulikuwa na mtu eneo la Kaunta , mzee hivi mzungu, aliekuwa amelala fofofo na kupiga miayo , ilionekana alikuwa amelewa pombe chakali.


Pembeni ya kaunta kulikuwa na vyungu vya maua ambavyo mimea yake ilionekana kukauka kutokana na kukosa maji . Kulikuwa na vipisi vingi vya sigara katika vyungu hivyo.


Ni eneo ambalo lilikuwa na uchafu ambao sio wa kawaida na giza tupu na hio yote ni kutokana kati ya taa chafu za glasi ambazo zimening’inizwa, ni mbili tu ambazo zilikuwa zinawaka na mwanga wake ulikingwa na kutu.


Hamza baada ya kusogea kwenye lile eneo la kaunta alipeleka mkono na kuvuta kitabu kilichokuwa pembeni ya yule mlevi , lakini ile anavuta tu mwanaume yule mzungu alikikandamiza na mkono wake bila kuinua uso kuangalia nani anavuta kitabu huku akiendelea kupiga usingizi.


Hamza aliishia kutoa tabasamu na kujiambia huyu mzee lazima atakuwa anaota na palepale hakutaka kumchelewesha kwani alivuta kile kitabu kwa nguvu na kumsukuma na kumfanya adondoke chini kama furushi na palepale ndio alishituka na kujua kumbe kulikuwa mgeni.


Alisimama haraka haraka na kumwangalia Hamza na kisha alichukua karamu na lile daftari.


“Unaitwa nani?”Aliuliza kwa kifaransa.


“Hamza”


“Sijui linavyoandikwa , hebu andika mwenyewe”Aliongea na kumsogezea Hamza karamu na daftari.


Hamza alitamani kucheka kwa visingizio vya mzee huyo , lakini hata hivyo aliandika jina lake.


“Raisi wako yupo?”Aliuliza Hamza na mzungu yule mara baada ya kusikia Hamza akiuliza hivyo alimwangalia kwa macho ya uchunguzi.


“Unamtafuta raisi wangu kwa ajili ya kukumbushia yaliopita?”


“Ndio , sisi ni mrafiki”


“Lakini ametoka”Aliongea.


“Ameenda wapi?”Aliuliza Hamza akiona hakuwa na bahati.


“Mbugani”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo , alionekana kukumbuka kitu palepale na kutabasamu.


“Kama ni hivyo nitamsubiri”Aliongea na palepale yule mzungu alinyoosha kidole kuelekea kwenye korido iliokuwa na giza.


“Chukua huo uelekeo kwenda mbele , utaona ofisi ya Raisi , unaweza kuingia na kupumzika”Aliongea yule mzungu bila kujali Hamza ni nani na Hamza mara baada ya kuondoka palepale aliendelea kulala.


Hamza alichukua korido hio mdogo mdogo akijali mambo yake na mara baada ya kutembea ndani zaidi hatimae aliweza kukuta eneo ambalo kulikuwa na bendera mbalimbali zilizosimamishwa pembeni , pamoja na medali zilizofungiwa kwenye kabineti za makabati ya vioo.


Kama mtu angeangalia medali hizo kwa umakini, asingekosa maneno haya: World number one Assassin Guild - Baffold (Shirika namba moja duniani la Wauaji - Baffold), World Ranking of Assassins (Cheo cha Dunia cha Wauaji), Golden Blade Awards (Tuzo ya Upanga wa Dhahabu), World Assassin Guild (Shirika la Dunia la Wauaji), Best Trade Union – Baffold Annihilations (Muungano Bora wa Biashara – Baffold Annihilations), Assassin Guild Lifetime Achievements Awards – Asmuntis (Tuzo za Mafanikio ya Maisha ya Shirika la Wauaji – Asmuntis), Honorary Chairman of the Assassin's Society – Asmuntis (Mwenyekiti wa Heshima wa Jumuiya ya Wauaji – Asmuntis).


Ilikuwa ni kawaida sana kwa kundi la kimauaji kupokea medali za aina hio , hasa kwa yale ambayo yanashikiria namba moja duniani.


Asilimia kubwa ya bendera ambazo zimening’inizwa zilikuwa ni kutoka kwa wateja ambao waliridhika na kazi na namna ya kushukuru kwa kazi nzuri mara nyingi hutuma bendera ya nchi misheni ilipofanyikia na kukamilika.


Kadri wingi wa bendera ulivyo ilimaanisha idadi ya waliokufa , ambao wengi wao ni viongozi wakubwa wa kisiasa na matajiri. Kulikuwa na bendera hadi ya Tanzania katika makabati hayo.


Hamza wakati huo akikagua hizo medali na bendera macho yake yalionyesha kuwa na hali ya majuto na kuridhika , akisifia ndani kwa ndani kwa kusema Roho mchafu umefanya kazi nzuri ya kuendeleza kuwa mchafu.


Ukiachana na medali hizo pamoja na bendera , kulikuwa na vyumba tofauti katika korido hio , vingi vikiwa ni vya mafunzo , Gym na hata swimming pools.


Kwa bahati ukiachana na maeneo mengi kuwa machafu eneo la mafunzo ya kulenga shabaha lilikuwa safi mno.


Hamza mara baada ya kusogea ndani ya eneo hilo kuchungulia aliweza kuona watu wengi wa kila rangi watoto na watu wazima wakiwa bize kujifunza namna mbalimbali za kimafunzo na kwa macho ya haraka tu walionekan mafunzo yao sio kwa ajili ya ulinzi bali kummaliza mtu.


Hamza alitembea kuvuka eneo hilo na kwenda ndani zaidi katika mlango wa mbao , usiokuwa na loki kabisa na kisha akausukuma na ile anaingiza mguu mmoja kuingia ndani , mwili ulimsisimka kwa kuhisi hatari , lakini hakujizuia na kukubali kile kinachokwenda kumtokea.


Na pale pale kisu kikali kiliwekwa shingoni kwake na aliekuwa amemuwekea kisu hicho alikuwa ni mwanamke alievalia nguo za kininja za kumbana huku akiwa hana utani hata kidogo.endelea nayo bure:- SEHEMU YA 186
Simulizi imekaa unyama sana Big up Bro
 
186.
Gwiji mwenye hadhi ya nyota kumi.


Alikuwa ni mwanamke aliechanganya rangi lakini kwa namna alivyokuwa akionekana ni ngumu kusema ni Shombeshombe kutokana na umbo lake la kibantu. Ilikuwa ngumu pia kukubali mwanamke mwenye umbo namba nane namna hio anaweza kuwa ninja.


Mwanamke huyo alijua vyema kujificha na Hamza hakuweza kuhisia uwepo wake mpaka pale alipowekewa kisu shingoni, ikionyesha ni kwa kiasi gani alikuwa na uwezo.


“Wewe ni nani?” Mwanamke yule aliuliza huku akionekana kuwa siriasi mno , lakini kwa wakati mmoja sauti yake haikuwa ikichukiza masikioni.


Hamza aliishia kuvuta pumzi ya ahueni huku akitoa tabasamu kama vile mtu anajaribu kukumbuka kitu na kisha palepale taratibu taratibu aligeuka na kumwangalia.


“BlackFog hujanitambua?”


Hamza mara baada ya kuongea hivyo hatimae mwonekano wake ulijionyesha wote mbele ya yule mwanamke na kisu ambacho alikuwa amewekewa shingoni kilidondoka chini palepale na kutoa mlio.


“My God! My Prince!?”


Black Fog palepale kwa hamasa kubwa alishuka chini kupiga goti na mguu mmoja lakini Hamza alimuwahi na kumzuia.


“Inatosha sasa , tumefahamiana tokea ukiwa mdiogo , haina haja ya kuwa hivi kila tunapoonana”Aliongea Hamza huku akimchunguza “Umekuwa mtu mzima sasa mpaka nimeanza kukusahau, hasa namna ulivyokuwa mrembo”


Hamza mara baada ya kuongea vile, kauli yake ilionekana kumgusa mwanamke huyo na alijawa na shauku.


“Mfalme unauhitaji mwili wangu?”Aliuliza.


Hamza mara baada ya kusikia swali hilo alishindwa kujizuia na kujihisi ajabu.


“Mara hii tu nimegeuka na kuwa mfalme na unataka kunipa mwili wako? Si tulikubaliana mimi ni kaka yako , kama huwezi tena kuniita kaka niite Hamza”Aliongea.


“Wewe ni mfalme napata wapi uthubutu wa kukuita kwa jina lako au kaka?”Aliongea Black Fog huku macho yake yakiwa katika hali ya kulegea.


Hamza alishindwa kuvumilia mwonekano huo , kipindi cha nyuma mwanamke alikuwa akimwangalia kwa mwonekno huyo alikuwa akitaka kulala nae.


Black Fog ni mwanafunzi wa Asmuntis lakini vilevile alikuwa ni binti yake ambae alimwasili, kipindi ambacho Hamza alikuwa na miaka kumi na tatu Black Fog alikuwa na miaka nane.


Ni hivyo tu Hamza alikua kiakili haraka na katika umri wa miaka kumi na tatu alishaanza kufanya misheni mbalimbali na kuwa katika daraja sawa na Asmuntis ambao walikuwa wakubwa kwake ki umri.


Miongo kadhaa iliopita , Black Fog na Asmuntis walitembea kuzunguka dunia nzima pamoja, wakati ambao Hamza yeye aliongoza kundi la wenzake katika mapambano na wavuna nishati ya mbingu na ardhi na kwanzia hapo hawakuonana kwa muda mrefu. Siku ambayo Hamza alikuja kukutana kwa mara nyingine na Black Fog alikuwa ameshakuwa mtu mzima na kuwa mwanamke mrembo anaetamanisha, msichana ambae Hamza alijiambia kama angemkuta Club asingemuacha salama.


Lakini kutokana na msichana huyo kuwa mwanafunzi na binti kwa Asmuntis Hamza alimkwepa na hakutaka kabisa kumgusa.


“Nishastaafu tayari , unaweza kuniita tu kwa jina langu usiwe na wasiwasi, niite Hamza au kaka inatosha , sijawahi penda mtu kuniita mfalme nadhani wote mnajua?”Aliongea Hamza na kumfanya Black Fog kuwa na mwonekano wa kushangaa kidogo.


“Kwahio naweza kukuita Kaka kweli?”


“Ndio , nimekupita miaka mitano ki umri sidhani kuna haja ya kuwa na wasiwasi”Aliongea Hamza na kumfanya Black Fog kulamba lips zake na kisha palepale alinyoosha mkono kuelekea katika masofa akimpa Hamza ishara ya kuingia na kukaa.


Hamza alifanya hivyo na kwenda kukaa kwenye sofa huku Black Fog akifunga mlango.


Hamza alijua mwanamke huyo atampa kinywaji chochote kama mgeni , lakini alienda kukaa na yeye pembeni yake tena karibu kabisa kiasi cha mapaja yao kugusana. Hamza alikuwa akihisi harufu nzuri ya marashi kutoka kwa Black Fog.


“Kaka…!”Sauti nzuri na nyororo ya Ukungu ilisikika , huku mkono wake ukishuka katika paja la Hamza.


Mwanamke huyo alikuwa na mikono milaini mno , ijapokuwa ilikuwa ni mikono ambayo imeshikilia aina mbalimbali za siraha kwa miaka mingi lakini mikono yake bado iulikuwa misafi na laini ya kuamsha hisia za mwanaume.


Sasa kitendo c ha mwanamke huyo kumgusa , alijihisi msisimko kwa hali ya juu, zilikuwa ni hisia ambazo mara nyingi anazielewa sana hususani akiwa karibu na mwanamke na hali hio ilimfanya kuhisi ajabu kwani ilikuwa ni tofauti sana na nyuma alipokuwa karibu na mwanamke huyo.


“Nini kimekutokea?”Aliuliza Hamza akibabaika huku akijitahidi kujituliza.


Fog hakuonyesha kujali kabisa mwonekano wa Hamza , ilikuwa ni kama amejiandaa kwa muda mrefu siku mwanaume huyo akijitokeza basi anakwenda kujiachia ilivyo. Kwani palepale cha kwanza alimwegamia Hamza na kisha alinyoosha mkono wake na kuondoa kibanio cha nywele zake na kufanya ziporomoke chini kwenye mebaga yake na kwa namna zilivyokuwa nyeusi na zenye matunzo makubwa ilifurahisha macho ya mwanaume rijali.


Hamza alijikuta akimeza mate mengi , utafiti unasema uzuri wa mwanamke huonekana kupitia kwenye kona za macho ya mwanaume na hiko ndio ambacho Hamza alikuwa akipitia. Black Fog alikuwa akivutia mno.


“Unajua miaka mitatu iliopita nililia sana baada ya Master kuniambia umeondoka na hajui wapi umeenda?”Aliongea Black Fog kwa deko huku akisugua mapaja ya Hamza kimahaba kabisa.


“Mwanzoni sikuwa na uwezo wowote wa kimapigano , lakini nilivyokuja kuwa na uwezo ushaondoka tayari …”Aliendelea kuongea kwa kujitilisha huruma na kumfanya Hamza kucheka.


“Sikuwa hata nikijali uwezo wako , kutokujua kwako kupigana ilikuwa swala la kawaida tu kwa mwanamke”


“Lakini Kaka unakumbuka miaka kumi iliopita , kwasababu ya kushindwa kujifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi , Master alinipa adhabn ya kufanya mafunzo ya ziada katika bonde la moto..?”Aliongea mwanamke huyo na kumfanya Hamza kukumbuka na palepale alianza kucheka.


“Asmuntis alikuonea sana kipindi kile , ulikuwa na miaka kumi tu lakini akaamua kukutupia katika bonde la moto bila ya kujali kuna wanyama..”


“Na ni wewe uliekuja kunitoa na hata kuniokoa kwa kuua mbwa mwitu waliokuwa wakitaka kunirarua na kisha tukachoma nyama yao na kula”Aliongea Black Fog huku macho yake yakiwa yamejaa mahaba mazito.


“Ilikuwa ni kama bahati tu kipindi kile , nilikuwa nikipita na nilishangaa kukuona”


Hamza wakati huo alikuwa zake katika misheni na alikuwa akifukuzana na watu ambao walienda kujificha katika korongo la moto , lakini hakutegemea wakati huo Black Fog alikuwa ametupiwa pia katika hilo bonde kwa kupewa adhabu.


Kwasababu alikuwa ni mdogo na mtoto wa rafiki yake hakutaka kumuacha na alimlinda mpaka akamtoa , jambo ambalo lilimkasirisha Asmuntis kwa kuona Hamza anajifanyisha baba huruma na kuharibu adhabu aliompatia Black Fog na hapo ndio walianza kupigana lakini Asmuntis alibakia akishangaa baada ya kugundua Hamza alikuwa amemzidi uwezo.


“Muda mwingine bahati ni maajaliwa , sijui watu wengi wanalichukuliaje, lakini kwangu mimi wewe ni mtu mwenye roho nzuri dunia nzima. Master alinilea kwa ajili ya kuwa muuaji, lakini kama wewe usingekuwepo ningepoteza maisha muda mrefu”


“Huwezi kusema bahati ni majaliwa , kama ni mtu mwingine angefanya kama mimi tu kukusaidia”Alijitetea Hamza.


“Kwanini huyo mtu mwingine hakujitokeza na ukawa wewe? Ilikuwa imepangwa uwe wewe ndio maana” Mwanamke huyo kadri alivyokuwa akiongea ndio namna sauti yake ilivyozidi kubadilika.


Hamza alijikuta akivuta pumzi nyingi kutokana na mkono wa mrembo huyo ulikuwa ukipandiswa taratibu na kugusa maeneo yenye msisimko mkubwa.


“Inatosha sasa Fog. Naona staili yako ya kunikaribisha ni ya pekee sana”Aliongea Hamza huku akitabasamu kizembe lakini ni kama amepandisha kichaa cha ninja huyo kwani palepale alisimama na kisha alimkalia Hamza kwa kuingiza miguu yake katika mapaja.


Hamza alijikuta akigugumia baada ya kuhisi sehemu ambayo mwanamke huyo aliokalia ndio ile ile muhimu sana kwake kama mwanaume na kitendo cha Fog kuendelea kujisugua ilimfanya kuhisi uvumilivu unakwenda kumshinda.


“Mimi sio mtoto, naona kabisa mwili wako unaniambia unanipenda?”Aliongea huku akijipinda pinda kwa kulegea kama nyoka.


Hamza aliishia kuangalia kiuno kilaini cha mwanamke huyo na uvumilivu ulimwishia lakini bado hakuwa radhi , hivyo alimshika na kumuondoa juu yake.


“Fog hatuwezi kufanya hivi”Aliongea Hamza.


“Kwanini!?;Aliongea huku akimwangalia Hamza kwa macho ya huzuni “Mwili wangu ni msafi , kama wasiwasi wako ni juu ya ujuzi wangu nimeupata kwa kusoma na sijawahi kufanya hivi kwa mwanaume mwingine, kwasababu nilikuwa nikiiongojea siku ambayo nitakupatia kila nilichokuwa nacho..”


Hakika hakutegemea msichana ambae alimsaidia miaka kumi iliopita angetokea kumpenda kwa kipindi chote hicho.


Ingawa kwa Hamza ilikuwa ni kama bahati kupendwa na mwanamke wa namna hio na mrembo , lakini bado alikuwa mwanafunzi na kama binti kwa Asmuntis . hivyo hakutaka kudharau ukaribu wao.


“Hio sio sababu , wewe ni mwanafunzi wa Asmuntis, unaweza kumchukulia kama mwalimu tu lakini yeye anakuchukulia kama mtoto wake. Chochote kikitokea baina yetu, si nitaweka rehani mahusiano yetu. Wewe ni mtoto bado haina haja ya kuendelea kuwa muuaji na hakuna haja pia ya kuendelea kuniona mimi pekee kama mwanaume..”Kabla Hamza hajamaliza kuongea Fog alimzuia.


“Master kasema inawezekana! Nilimuuliza mwenyewe na kaniambia ili mradi nimekubali mwenyewe hawezi kukufanya chochote”Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akipaliwa na mate na kuanza kukohoa.


Hakuamini mwanamke huyo angemwambia ujinga huo master wake.


“Lakini…”Hamza alitaka kuongea lakini alizuiwa.


“Uwezo wangu kitandani ni mzuri tu usiwe na wasiwasi, nimejifunza mno kujiandaa na hii siku”


“Sio swala la uwezo wako , ninachomaanisha ni kwamba nimebadilika sana siku hizi , sitaki kukufanya kama mwanamke wa kupita , hata kama kutatokea kitu baina yetu lazima kuwe na msingi wa kimapenzi kati yetu. Pia nimekwisha oa tayari na kutokana na hilo nipo makini sana kuliko mwanzo”Aliongea Hamza akijitahidi kwa uwezo wake wote kujitetea kwasababu mwenyewe alikuwa na wasiwasi , alijua fika kama ingeendelea hivyo ataweza vipi kujizuia.


Fog mara baada ya kusikia kauli ya Hamza macho yake yaliingiwa na unyonge na mshangao kwa wakati mmoja.


“Umekwisha kuoa?”


“Ndio , kuna mambo yalitokea tu ndio maana sikufanya harusi”Aliongea Hamza.


“Kwahio siwezi hata kuwa mpenzi tu?”


"Acha kuwa hivyo basi, acha asili ichukue nafasi yake. Hatujakutana kwa muda mrefu, pengine ni kwa sababu hujakutana na mwanaume zaidi yangu, ndiyo maana unahisi mimi ni sahihi kwako."


"Haiwezi tokea, naujua moyo wangu, najua fika wewe ndiye ninayekutaka," aliongea, na palepale alifumba macho yake na kuinama kwa ajili ya kumkiss Hamza.


Hamza upande wake hakumzuia, alijua vyema kama atamsukuma, alihisi hata yeye pia atasikia maumivu.


Mara baada ya kumkiss Hamza mdomoni, mwanamke huyo alisimama na kumwangalia Hamza.


"Nitakusubiri mpaka siku utakayoanza kunipenda mwenyewe, lakini usinifanye nisubirie kwa muda mrefu kwa sababu nimeshakupenda tokea miaka kumi iliyopita."


Hamza, mara baada ya kusikia hivyo, alitamani kulia. Alijiambia kama ni baraka zimemzidia sasa, lakini kwa wakati mmoja ni kama alimuonea huruma huyo mrembo kwa kugonga hodi kwenye mlango ambao si sahihi.


"Tutoke kwanza, nataka kuonana na Roho Mchafu. Kama hajarudi, nitamfuata huko huko," aliongea Hamza, na Fog alionekana kusita.


"Bado nataka kuwa na wewe kwa muda mrefu kidogo, isitoshe ni muda mrefu hatujaonana, nitakusindikiza kwenda kuonana na Master."


Hamza hakuwa na haraka, lakini alihofia kuwa peke yake na huyo mwanamke kwa kuona ni hatari zaidi.


"Sikujua kama utakuja mapema, nikiwapigia watu na kuwapa taarifa ya ujio wako nadhani haitachukua muda watajazana hapa," aliongea Black Fog wakiwa wametoka nje.


"Kuna zaidi ya Assassin mia ndani ya hili eneo na kwa kusanyiko la viongozi wakubwa ndani ya Paris. Harakati zenu zikionekana, Wizara ya Ulinzi lazima watashitukia na kuhisi kuna kitu mnachopanga kufanya," aliongea Hamza, na muda huo waliweza kufika katika lile eneo la mapokezi.


Hamza aliweza kumuona yule mzee aliyemkuta mwanzo, lakini pia alionekana kijana mdogo mwingine aliyeshikilia simu akionekana kuichezea.


"Ni wa kina nani hawa? Maana kwa ninavyowaona sio maninja?" aliuliza Hamza.


"Huyo mzee ni mwalimu wa Master na huyo mtoto ni mpwa wake," aliongea Fog.


"Mwalimu wa Roho Mchafu?" Hamza alijikuta akishangaa kwa sekunde na palepale alionekana kukumbuka jambo.


"Huyu mzee ni Vessa?" aliuliza Hamza akiwa kama haamini. Vessa alikuwa ni mmoja wa maninja wa mwanzo kabisa wa daraja la juu kuwahi kutokea katika uso wa dunia. Ni sawa kusema alikuwa akikaribia daraja la ugwiji, la sivyo asingekuwa mwalimu wa Asmuntis au Roho Mchafu.


"Ndio, lakini kwa sasa ni mtu wa kulewa tu na kutafuta wanawake. Alipotimiza umri wa miaka hamsini na tano alipata jeraha kubwa alipokuwa katika misheni na kufanya mwili wake kulemaa. Master aliamua kumleta hapa ili kumalizia uzee wake," aliongea Fog.


Asilimia kubwa ya maninja wote hawakuwa na mwisho mzuri. Hata kama hawatokufa, kadri walivyokuwa wakizeeka na uwezo wao pia hupotea na kuwa dhaifu kuliko hata binadamu wa kawaida, na hiyo yote ni kutokana na kwamba asilimia kubwa wanatumia dawa za kuimarisha nguvu za kimwili.


Kitendo cha Asmuntis kumleta mzee huyo kukaa katika eneo hilo, si kwa sababu ya kumheshimu kama mwalimu, bali ilionekana dhahiri ni kwa ajili ya kujilinda kupitia uzoefu wake.


Hamza alimwangalia yule kijana mwingine aliyekuwa akichezea simu na alionekana kuwa teja kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya.


"Asmuntis hajali mpwa wake kuwa teja wa madawa ya kulevya?"


"Huyo achana naye. Kama asingekuwa ndugu yangu wa pekee ningeshamuua muda mrefu, hana mchango wowote zaidi ya kuwa mzigo."


"Huna haja ya kuwa na wasiwasi namna hiyo juu ya uwepo wao. Nina uhakika Master wako kaamua kuwaacha hapa kwa sababu bado anapanga kuwatumia."


"Kuwatumia? Hawa ni kama mzigo tu na kazi ni kuchezea hela, sioni kama wana faida yoyote."


"Wapo hapa kama kielelezo; mtu yoyote ambaye anafanya mafunzo ya uninja akiwaona lazima atapata onyo kutoka kwao. Ukiwa muuaji siku zote si tu umakini unaohitajika, lakini vilevile unapaswa kuwa mvumilivu na mwenye kujizuia nyakati nyingine; la sivyo, ukitoka nje ya mipaka ya kazi yako hutokuwa binadamu tena zaidi ya mzimu unaotembea."


Black Fog mara baada ya kusikia maelezo hayo, alionekana kuelewa maana ya Hamza na alitingisha kichwa palepale.


Wawili hao walitoka nje ya jengo hilo na kuanza kupita mitaa miwili mpaka mitatu. Baadhi ya mateja na vibaka baada ya kumuona Mrembo Black Fog walionyesha heshima yao kwa ishara ya kumhofia. Wengine waligeuza vichwa vyao pembeni wakiogopa kabisa kukutanisha macho.


Jambo hilo lilimfanya Hamza kutamani kucheka. Ilionyesha Black Fog alikuwa akiwashikisha adabu maana si kwa kumhofia huko.


Mara baada ya kutoka nje ya mtaa, waliingia katika msitu wenye miti mifupi mifupi, na walitembea umbali kidogo tu, waliweza kumuona mwanaume mzungu aliyekalia katika kiti kilichochakaa.


Alikuwa ni mfupi ila mnene mwenye nywele ambazo zilianza kubadilika rangi kutoka kuwa nyeupe na kuwa kama kijivu hivi, zilikuwa zimechanguka na namna zilivyokuwa ndefu zilimfunika mpaka usoni.


Alikuwa amekaa chini akikodolea macho upande mmoja huku pembeni yake kukiwa na chupa nyingi za pombe zilizokuwa tupu na baadhi ya kopo za nyama.


Hakuwa katika mazingira mazuri hata kidogo, kutokana na kuzungukwa na nzi pamoja na mbwa waliokuwa wakila nyama ambazo alikuwa akiwatupia.


Mbwa hao licha ya kuonekana kama wale wasio na wamiliki lakini walionekana kumzoea huyo mzee. Ilikuwa pia ngumu kujua mwanaume huyo alikuwa katika hali ya furaha au majonzi.


Kama isingekuwa kwa mwanaume huyo kuwa katika mavazi mabaya na kutojipenda, kwa mwonekano wa sura yake tu angekuwa msafi, angevutia sana wanawake wengi; alikuwa ni mtanashati aliyekosa matunzo.


"Roho Mchafu, hilo koti lina zaidi ya miaka kumi tokea ulinunue, kwa nini hujalibadilisha?" aliongea Hamza huku akicheka.


Ijapokuwa mwanaume huyo alikuwa ashasikia hatua za miguu zikisogea upande wake, hakugeuka hata kidogo kama vile hakujali, lakini mara baada ya kusikia sauti ya Hamza, palepale alishituka kwa nguvu.


Palepale alimkodolea Hamza na macho yake ya rangi ya bluu na alionekana kama vile alikuwa akitetemeka.


"My Prince!"


Asmuntis palepale alipiga goti na mguu mmoja na kuweka mkono wake kifuani.Hamza alisogea na kisha alimshika bega kwa kumgonga gonga.


“Ni kama nilivyotea utakuwa unalisha mbwa na paka huku msituni , hujabadilika kabisa kama mwanzo. Una huruma kwa mbwa na paka kuliko kwa binadamu”Aliongea na kumfanya Asmuntis midomo yake kucheza. Kwake yeye kitendo hicho ilikuwa ni sawa na kutabasamu.


Asmuntis sifa yake kubwa alikuwa akipenda sana wanyama , ni rahisi kwake kumuua mtu kuliko kumuua mbwa. Ilikuwa ngumu kwa mtu yoyote kuamini muuaji kama huyo alikuwa ni kiongozi wa kupigania haki za wanyama.


Ukiachana na kazi yake ya uninja , kazi yake nyingine ilikuwa ni kulisha wanyama na hata asilimia kubwa ya pesa anazopata katika kazi zake alikuwa akitoa msaada kwa taasisi mbalimbali za kutunza wanyama ili mazingira yao kuboreshwa.


“Bosi ni kweli umekuja kushiriki katika baraza la Maksi? Sikudhania utashiriki katika kilele cha kikao cha Magwiji?”Aliongea Asmuntis.


“Kikao cha Magwiji , unamaanisha nini? Mimi nipo hapa kwasababu ya kitengo cha Malibu kuniomba niwasaidie na pia nilipanga kukutana na Washikaji zangu nyie”Aliongea Hamza na kumfanya Asmuntis kutokuelewa.


“Inamaana hujui kinachoendea , sio kama upo hapa nchini kutokana na mwaliko?”


“Mwaliko gani!?”Aliuliza Hamza akiwa amechanganyikiwa.


“Kutokana na miaka mitano iliopita ulimuua Mr Black, nafasi yake imekuwa wazi tokea wakati ule . Kingine bosi umetoweka kwa zaidi ya miaka mitatu hivyo jamii ya baraza la watoa maksi wameona itakuwa ni vizuri kukaa chini na kufanya upembuzi kuona kama bado unastahili cheo cha nyota kumi za ugwiji . Sasa ili kudai upya cheo cha Nyota kumi za Ugwiji , Sytor Association wameitisha kikao cha magwiji kwa ajili ya majadiliano. Kwa ufupi ni kwamba wameitisha kikao kwa kualika Magwiji wote wakubwa duniani ambao watapiga kura kumchagua mtu mwingine wa kushikilia hadhi ya Gwiji mwenye nyota kumi. Mmi nilidhania ujio wako hapa Paris ni kwasababu umepokea mwaliko kwa ajili ya kikao hichi , sijategemea kukosa kwako mwaliko”


“Nilishasema nimestaafu tokea mwanzo , kwanini wanitumie mwaliko , pengine pia wanadhani nimekuwa dhaifu kuliko mwanzo hahaha..”


Hamza hakujali kabisa kuhusu hilo , lakini kusikia kuhusu kikao hicho cha magwiji alijikuta akivutiwa.


Miaka kumi nyuma Hamza alimuua Mr Black ambae alikuwa akishikilia cheo cha Gwiji mwenye nyota kumi na ilikuwa ni baada tu ya vita takatifu kumalizika katika ulimwengu wa siri. Sasa kitendo cha kumuua Mr Black maana yake alirithi cheo chake , lakini kutokana na kutokuonekana kwake kwa zaidi ya miaka mitatu ilionyesha ni kama Hamza ametekeleza cheo hicho ndio maana watu wa Baraza la Maksi wameona ni vyema kama wataitisha kikao cha magwiji kumchagua mtu ambae atarithi cheo hiko.


Asmuntis mara baada ya kumwangalia Hamza kwa namna ya kumchunguza alijikuta akishangaa.


“Bosi kwanini sihisi chochote katika mwili wako , unaonekana kutokuwa na nishati za mbingu na ardhi kabisa?”Aliongea.


“Nilishapoteza nguvu za nishati za mbingu na ardhi muda mrefu tu na sijavuna kwa muda mrefu hivyo ni sawa tu kutohisi chochote”


“Nini!” Asmuntis alishikwa na mshangao wa kauli hio kiasi cha kuanza kutetemeka. Hata kwa Black Fog aliekuwa hapo alishangaa pia.


“Kaka! Unasema huna nishati za mbingu na ardhi kwenye mwili wako kabisa?”


“Kuna haja ya kushangaa namna hio, si swala tu la kutojifunza tu?”


“Ndio maana hukushituka muda ule wakati nakushambulia , mimi nilidhani uliniacha nikushambulie tu kumbe umekuwa…”Aliongea Black Fog huku mtoto wa kike chozi likimtoka akishindwa hata kumalizia kusema Hamza amekuwa mdhaifu.


“Bosi kwa taarifa ambazo nilisikia wakati wa mapigano yako na Mr Black, ingawa uliweza kumshinda na kumuua lakini ulijeruhiwa mno na ndio maana hukuwa na jinsi na kuamua kustaafu. Sikuamini niliposikia lakini sikutegemea ulipoteza mpaka uwezo wako wa nishati za mbingu na ardhi?”


“Mchafu hebu tulia…” Hamza hakujua hata namna ya kujielezea na hakujua alie ama acheke katika hali hio.


“Bosi huna haja ya kuongea , najua namna ya kufanya,” aliongea Asmuntis akiwa siriasi “Nitatunza siri hii usiwe na wasiwasi , hata kama umepoteza uwezo wako bado wewe ni bosi wetu. Mimi Azzle , Leviathani, Mameni, Berly , Murphy na Sally wa kisiwani Toharani na washikaji zako ambao tupo hai hatuwezi kukutelekeza. Ni wewe ulietuleta pamoja na kupambana kwa ajili ya kujilinda . Sasa hivi ni wakati wetu kuungana na kukulinda wewe”


Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Asmuntis na namna ambavyo yupo siriasi alitamani kucheka kwa nguvu lakini kwa wakati mmoja alitamani kulia vilevile. Hio ilikuwa ndio maana halisi ya urafiki wa kufa na kuzikana , haijalishi upo katika hali gani ,huwezi kuwaacha ama kuachwa na wenzako.


Hamza alifikiria kwa sekunde kadhaa kuhusu hilo na palepale aliona haina haja ya kujielezea . Alijiambia muda wa kuwashangaza washikaji zake upo wa kutosha.


Kufikiria hivyo aliona swala hilo linavutia mno na lilimpa hamasa iliomfanya kusikia furaha katika moyo wake, lakini hata hivyo aliguswa na maneno ya Asmuntis a.k.a Roho mchafu.


“Pepo mchafu chukulia kama vile hujajua mimi mshikaji wako nimekuwa dhaifu. Nipo hapa kwa jaili ya kukuomba msaanda , nataka utumie baadhi ya watu wakanisaidie suala langu mjini”Aliongea Hamza.


“Bosi wewe niambie tu ni nani unataka afe, nitakamilisha ndani ya saa chache”Aliongea Asmuntis bila kugwaya.


“Sina mpango wa kumuua mtu yoyote. Nimeahidiana na Murphy kusaidia kitengo cha Malibu katika baraza la Maksi na pia kuangalia kuhusu msaliti ndani ya kitengo. Nataka utume watu wenye akili kadhaa ili wawe wanachukua maagizo kutoka kwangu”.


“Kama ni hivyo , basi usiwe na wasiwasi . Nipe usiku mmoja tu nitakamilisha kila kitu”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa kukubaliana nae.


“Nahisi njaa sasa baada ya kupata ninachokitaka , unajua mgahawa wowote mzuri ndani ya hili eneo?”


“Hapana , nitakuchukua twende tukale mbali na hapa”Aliongea Asmuntis na kumfanya Hamza kutaka kucheka , walimwita roho mchafu kutokana na tabia yake ya kupenda kuishi katika maeneo machafu. Lakini licha ya hivyo alijali wageni wake ndio maana alitaka kumchukua Hamza kwenda eneo lingine.


Baada ya kutoka katika huo msitu waliweza kufika nje kabisa ya eneo hilo na kuingia katika mgahawa uliojengwa kwa mbao , uliokuwa na mazingira mazuri.


“Bosi napanga kutuma watu kuja kwa ajili ya kukupatia ulinzi. Ijapokuwa watu hawajui hali uliokuwa nayo kwasasa lakini bado una maadui wengi”Aliongea Asmuntis.


“Ndio , nimekuwa mdhaifu sana siku hizi , unapaswa kutuma vijana wenye nguvu za kutosha kwa ajili ya kunilinda”Aliongea Hamza na kumfanya Asmuntis kumwangalia Black Fog.


“Chukua watu kadhaa ukamlinde bosi”


Black Fog mara baada ya kusikia hivyo alijawa na furaha na haraka sana alitingisha kichwa kukubali.


Hamza mara baada ya kusikia hivyo , kichwa chake kilianza kuuma palepale , kama angejua mwanamke huyo ndio anakwenda kupewa jukumu hilo angekataa tokea mwanzo.


Lakini kuona namna Black Fog alivyokuwa na furaha hakutaka kumkatalia.


Hamza alikula pamoja na Asmuntis na kuendelea kupiga soga mpaka jua lilipozama ndio alipoaga na kuondoka.


Asmuntis aliishia kumwangalia bosi wake kwa huruma akipanda kwenye taksi huku ikionyesha ni dhahiri alijua Hamza alikuwa akipitia wakati mgumu kwa kukosa nguvu na kuwa binadamu wa kawaida .


“Kesho asubuhi utaanza safari ya kwenda mjini , hakikisheni mnamuonyeshea bosi heshima na hamumsumbui”Aliongea Asmuntis, alikuwa akijua Hamza alikuwa ameoa pia.


“Sawa Master , nitaenda kuandaa safari sasa hivi”


“Nenda”


Mara baada ya pale Black Fog aligeuka kuwa ukungu mweusi na kupotea katika macho ya Asmuntis.
 
Muda ule Asmuntis alitoa simu ndogo ya batani na kuingiza namba flani na kisha aliweka sikioni na ndani ya dakika tu simu ile iliunganishwa na upande wa pili na sauti yenye mikwaruzo ilisikika.


“Wewe mtu mchafu wa roho unanitafutia nini usiku wote huu?”


“Umesikia kuhusu habari za bosi?”


“Boss? Haha.. umeshaonana na bosi tayari. Niliongea nae jana tu hapa najua yupo Paris kwa ajili ya kushiriki katika Baraza la Maksi. Na mimi najiandaa kuja huko, kesho tutaonana muda si mrefu”Aliongea Aziza au Azzle kwa furaha kubwa.


“Siongelei kuhusu hilo mimi m naongelea kuhusu uwezo wa bosi wa nishati za mbingu na ardhi ..”


“Kuna shida gani kuhusu uwezo wake , ameingia katika levo nyingine au? Kama ni hivyo hilo sio swala la kushangaa , bosi amekuwa na kipaji kikubwa sana tokea mwanzo”


“Hapana, bosi hana uwezo wowote”Aliongea Asmuntis na upande wa pili kimya kilitawala.


“Ni watu wangapi wanajua kuhusu hili?”


“Sina uhakika , lakini kwa namna mpaka sasa hakuna ambae amelipa kisasi nahisi bado hawajazinyaka habari. Tunapaswa kufanya hili swala kuwa siri , hususani tusiwaambie Leviathan m Beryl na wengine kujua kilichomtokea. Wana midomo mipana wale muda si mrefu tukiwaambia taarifa zitasambaa”.


“Naunga mkono kuhusu hili , lakini hata kama wakijua sidhani watawerza kusambaza, ila kwasasa tufanye hivyo, Sikudhania mapigano yale na Mr Black yangemfanya kupoteza uwezo wake. Wewe kiumbe mchafu unaenuka hakikisha unamlinda bosi vizuri mpaka nifike. Vinginevyo nitakupiga nyundo na kuchangua ubongo wako”


“Najua cha kufanya hata kama usiponiambia . Mtu yoyote atakaethubutu kugusa hata unywele wa bosi hatoliona jua na mwezi tena”.


*****


Hamza hakujua kutoweka wazi kuhusu uwezo wake mpya umewafanya Asmuntis na Aziza kuwa na wasiwasi kama vile walikuwa wakiingia vitani kwa mara nyingine kwa kuogopa kuna jambo linakwenda kutokea.


Kwa Hamza aliamua kutowaambia kwasababu za kimatani tu kwani alikuwa akifahamu uhusiano wao ni ngumu kuvunjika kwasababu ye yeye kukosa uwezo wake . Kingine pia hakudhani kama kuna mtu angeweza kujaribu kumchokoza. Hakuvutiwa pia na cheo cha Nyota kumi za Gwiji na alikuwa tayari kukipoteza , hakujifunza mapigano kwa ajili ya watu wengine kumkadiria levo aliopo.


Hamza mara baada ya kurudi hotelini , taa ndani ya chumba cha Regina zilikuwa zikiwaka bado licha ya kuwa usiku sana. Hamza alikuwa amelewa kidogo hivyo mudi yake ilikuwa nzuri na alipanga kutumia fursa kufanya mahaba na Regina.


Lakini sasa baada ya kugonga na kujitambulisha kama ni yeye, Regina alimpotezea palepale.


“Wife , Mke wangu fungua mlango , kwanini unanipotezea?”Aliongea Hamza akiwa amesimama kwenye mlango akiwa hana cha kufanya.


Mara baada ya kusimama mlangoni kwa dakika kama moja hivi , Regina hatimae alifungua mlango kidogo.


“Ondoka zako , usinisumbue”


Hamza mara baada ya kusikia kauli hio iliojaa ukauzu , mapigo yake ya moyo yalikita kwa nguvu.


“Wife kwani tatizo ni nini? Nimekukasirisha saa ngapi tena?”Aliuliza.


“Ulikuwa umeenda wapi siku nzima?”


“Nilienda Louvre na baada ya kutoka nikaenda kuonana na marafiki zangu”


“Marafiki gani , lazima ulikuwa kwa wanawake zako, si ndio?”Aliongea Regina huku akivuta mdomo.


Hamza alijikuta akishikwa na wasiwasi na hakujizuia kuhisi labda Regina alijua mchana alitoka na Nyakasura na kwenda shopping.


“Wife hebu acha kuniangalia hivyo , sikwenda kwa mwanamke yoyote”Aliongea Hamza akijitetea.


“Wewe ni mwanaume ambae hujali kabisa kuhusu ahadi zako , sitaki kukuona mimi , piss off , usinisumbue nina kazi”Aliongea na kisha palepale alifunga mlango kwa hasira.


Hamza aliishia kusimama nje ya mlango akiishia kukuna kichwa na kufikiria ni ahadi gani ambayo hakutimiza , baada ya kufikiria kwa sekunde palepale alikumbuka na alijipiga kwenye paji la uso wake kwa kujilaumu kusahau kwake.


Alikuwa amemwahidi Regina kumtembeza katika jiji hilo jana yake na kutokana na hilo Regina aliongeza siku za kukaa hapo , lakini alikuwa amesahau kabisa na matokeo yake alikuwa akinywa pombe na rafiki yake mchafu na kurudi hotelini kwa kuchelewa.


Hamza alijikuta akijilaumu na hapo hapo alipanga namna ya kuikabili hio hali , lakini hata hivyo alijua Regina alikuwa na hasira na hata kama akimbembeleza ingekuwa bure tu.


Aliishia kurudi katika chumba chake akiwa na hali ya unyonge. Hakujua cha kufanya na palepale aliingia katika mtandao wa Watsapp na kumtumia ujumbe Eliza baada ya kuona yupo online.


Hamza: “Lizzy unafanya nini?”


Eliza: “Ndio nimemaliza kupika hapa, vipi hujalala tu mpaka sasa hivi?”


Hamza: “Hapana! Nimekumiss.”


Eliza: “Mh! Mimi sikuamini wewe, upo na mkeo Regina honeymoon huko unapata wapi muda wa kunimisi?”


Hamza: “Honeymoon gani tena? Tuna siku mbili tu hapa ila huko kukasirika kwake sasa.”


Eliza: “Nini kimetokea kwani, umemkosea tena Mkurugenzi?”


Hamza: “Nilisahau ahadi yangu kwake ndio maana,..”


Eliza: “Ndio maana, wanawake wanajali sana ahadi hata kama ni ndogo kiasi gani, kwanini usimwambie ulipokuwa, pengine anaweza kukuelewa. Ukimwacha akiendelea kuwa na hasira ndio atakavyozidi kukasirika. Ijapokuwa Regina amepitia mengi wakati akiwa mdogo lakini baada ya kuwa chini ya babu yake na bibi yake alidekezwa mno, ndio maana ni mwepesi wa kukasirika usipomchukulia siriasi.”


Hamza: “Eliza sasa wewe unaona nifanye nini?”


Eliza: “Mbona ni rahisi sana, upo ndani ya jiji la Paris tayari na kuna maduka mengi ya kifahari, unaweza kwenda na kumnunulia mkoba au viatu vizuri na kisha kumpatia kama zawadi, wanawake huwa tunapenda vitu kama hivyo.”


Hamza: “Lakini mke wangu ni tajiri tayari, kama akipenda vitu kama hivi anaweza kununua tu, unadhani anaweza kufurahishwa na kitu ambacho anaweza nunua?”


Eliza: “Wewe ni mjinga, zawadi inahusiana vipi na mtu kuwa tajiri ama kutokuwa tajiri. Kama umemnunulia wewe unadhani itakuwa sawa na akinunua mwenyewe?”


Hamza: “Kwahio ninachopaswa ni kumnunulia nitakachoweza bila kujali anaweza kununua au lah?”


Eliza: “Naona umeelewa sasa? Mimi nataka kuosha vyombo nipumzike, tutachat kesho ukiwa na muda.”


Hamza: “Vipi kuhusu wewe, unapenda nini, nitakununulia zawadi nije nazo?”


Eliza: “Sitaki chochote mie, wewe mnunulie tu bosi.”


Hamza: “Nishaelewa tayari, hata kama unasema hutaki napaswa tu kukununulia.”


Eliza: “Hahahaha…”


Mara baada ya kuchati na Eliza kwa dakika kadhaa , hatimae kichwa cha Hamza kilipata amani kidogo na alipanga kesho kukipambazuka akamnunulie Regina zawadi kumbembeleza.


Asubuhi mara baada ya kufanya mazoezi kidogo alioga na kuvaa nguo zingine na kisha alitoka nje na ile anafungua tu alikutana na sura ya mwanamke mrembo alievalia gauni la rangi ya pink na mkoba wa Chanel na viatu vya high heels. Alikuwa amependeza haswa na ilikuwa ngumu kuamini alikuwa ni yule ninja maarufu afahamike kwa jina la Ukungu mweusi(Black Fog).


“Mbona umependeza namna hio , una mtoko nini?”Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu.


“Kaka Hamza! Nipo hapa kwa ajili ya kukulinda , nimevaa hivi ili kuwa karibu yako kama msaidizi”Aliongea Miss Ukungu na kumfanya Hamza ashindwe kujizuia na kucheka.


“Mimi pia ni msaidizi na wewe unataka kuwa msaidizi wangu? Hebu acha hizo , nitakutambulisha kwa mke wangu kama mdogo wangu, sawa”Aliongea Hamza na kumfanya Miss Ukungu kushikwa na aibu za kike.


“Sawa kaka! Ninaenda kuwa dada yako leo”Aliongea kwa lugha ya kiswahili japo lafudhi yake haikuwa imenyoosha.


Professional killer’s mara zote wanakuwa na mafunzo mbalimbali tofauti na yale ya kimapigano , walikuwa wakifunzwa mbinu mbalimbali za kuwafanya kuishi katika mazingira ya kila namna bila kujali tamaduni husika na hio huwafanya kujua lugha zote kubwa duniani. Kiswahili ndio moja ya lugha kubwa ndani ya Afrika hivyo alikuwa amejifunza tayari, hivyo haikumshangaza Hamza kwa mwanamke huyo kujibu kwa kiswahili, lakini mapozi yake katika kutamka maneno hayo yalimfanya Hamza kukosa neno , hakuamini alikuwa akijua swaga za wanawake wa kiswahili.,


“Wewe mtoto usije kuleta tu mchezo , unajua ninachomaanisha”Aliongea Hamza kumtahadharisha huku akimzodoa kwa kidole kwenye paji lake. Licha ya wasiwasi wake wa uwepo wa mwanamke mrembo kama huyo lakini kwa wakati mmoja alifurahi kuwa nae karibu maana walikuwa wamezoeana.


“Nimekuelewa Bro , Nitakuwa dada yako mzuri. Ijapokuwa mama yangu ni mzungu lakini baba yangu ni Mwafrika wa Ethiopia, wote tumechanganya rangi hivyo ni rahisi kuaminika mimi na wewe ni ndugu”


“Umeshajua baba yako ni Mwafrika wa Ethiopia! Naona umefanya utafiti kujua asili yako, nakumbuka kipindi Asmuntis anakuokota ulikuwa huna kumbukumbu ya chochote zaidi ya jina lako tu”


Night Fog mara baada ya kusikia hivyo alionekana kukosa furaha ghafla na palepale alibadilisha mada.


“Kwahio kaka tunaenda wapi sasa hivi? Master kaniambia nikufuate kila utakapoenda , kama hutaki nionekane naweza kukulinda kwa siri”


“Kwa namna ulivyopendeza hivi , itakuwa ni hasara kunilinda kwa siri. Wewe nifuate ni muda wa kupata Breakfast huu na kisha nataka niende dukani kwa ajili ya kununua mikoba mizuri na viatu”


“Unataka kumpa mkeo zawadi?”


“Umejuaje?”


“Kwasababu na mimi ni mwanamke , lakini pia inawezekana unapeleka kwa mpenzi wako mwingine”Aliongea na kumfanya Hamza kugusa pua yake kwa kushikwa na haya.


“Roy kwasababu wewe ni mwanamke unaonaje ukinipeleka kwenda kuchagua?”Aliongea Hamza akitaja jina la Black Fog.


Msichana huyo alikuwa akiitwa Rhoda ila walifupisha kwa kumuita Roy, ndio jina ambalo alipewa na wazazi wake, wakati Asmuntis anamuokota alichokuwa akikumbuka ni jina lake tu.


Black Fog maana yake ni Ukungu mweusi , Rhoda wakati anajifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi aliweza kupata ufunuo wa ukungu mweusi , mbinu ambayo ilimfanya kutembea gizani bila ya kuonekana na katika ulimwengu wa kimauaji alifahamika zaidi kwa Nickname yake hio ya Black Fog , lakini jina lake la kawaida ndio Roy au Rhoda.


“Bro kwasababu hujui ununue aina ipi , kwanini usinunue aina zote , isitoshe kwa hadhi yako na utajiri uliokuwa nao unaweza kuwaamrisha watu wa kampuni wakuletee”


“Upo sahihi , kwanini nimesahau, ni swala tu la kuongea na Mzee Pilnault awaambie wafanyakazi wake kuniletea kila aina ya bidhaa mpya”


Rhoda mara baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa Hamza alijikuta akiangua kicheko na kumfanya azidi kupendeza.


“Bro nimejikuta nikigundua umebadilika sana , ule ujivuni wako umepotea lakini umezidi kuvutia , ni ngumu kuamini umekuwa wa kawaida na unahangaika kumfurahisha mwanamke. Wakati ule na chao chako cha Prince ulikuwa ni kupiga simu tu na kutoa amri”


“Sikuzaliwa kuwa mjivuni , ni kwasababu ya Master wako na wenzake walinibadilisha tabia”


“Hahaha..”


“Ila sidhani kama itakuwa sawa kununua kila aina waliokuwa nayo , nitaongea na Pino achague baadhi tu aniletee, wewe unaonaje?”


“Wewe ndio mwenye kauli ya mwisho Bro”


Hamza mara baada ya kuona maamuzi yake yamekaa vizuri kuhusu swala la zawadi , palepale alichukuana na Roida na kushuka chini kwa ajili ya kifungua kinywa na muda huo alitumia kumpigia Pino.


“My Prince, nilikuwa nikisubiria simu yako kwa hamu zote . ila bado sikutegemea kama utanipigia kweli”Alisikika mwanaume upande wa pili


“Mzee Pino , ulikuwa ukisubiria simu yangu!?”


“Ndio , najua tukio muhimu katika ulimwengu wa siri linaanza hapa Paris mwezi huu , kwasababu ya cheo chako nilikuwa na uhakika lazima ungeshiriki. Vipi haujafika tu Paris , nataka nikukutanishe na mtoto wangu”Aliongea Mzee Pino kwa kifaransa.


“Oh ! Kumbe sijawahi kukutana na mtoto wako eh?”


“Ndio na muda wote ametamani sana kuonana na wewe na kukushuruku kwa ulinzi wako”


“Kama ni hivyo unaonaje ukifanya hivi , nina uhitaji na mikoba ya kike, viatu na vitu vingine kwa ajili ya kumpatia mke wangu. Si familia yako ni moja ya wamiliki wa Gucci na Bottega? Itakuwa vizuri kama utanikusanyia bidhaa zote mpya na nzuri kwa ajili ya zawadi na uje nazo ili tupate chakula cha mchana pamoja”


“Itakuwa heshima kwangu kama mke wako atapenda bidhaa zetu mpya. Itakuwa ni baraka sana kwetu! Lakini naomba kuuliza ni wapi mlipo ili niweze kuwafikia ndani ya wakati”Aliuliza na Hamza palepale alimtajia hoteli waliofikia na kumwambia kama ana kazi anaweza kufanya hata jioni lakini Mzee huyo alimwambia anao muda wa kutosha na hayupo bize.


Kwasababu Regina alikuwa na ratiba ya kwenda kwenye kampuni asubuhi , angerudi mchana hivyo ni muda sahihi wa kuonana. Baada ya kupata Breakfast Hamza alitembea na Roida kuzunguka zunguka katika maeneo ya Champs -Elysees.


“Nilisahau kukuuliza jana , vipi kila kitu kipo sawa ndani ya Baffold?”Aliuliza Hamza akitaka kujua hali za jamaa zake.


“Mzunguko wetu unazidi kukua kila mwaka , Wauaji wengi wanataka kujiunga na kundi letu , hivyo tumeweka vigezo vikubwa sana kwa ajili ya kudahili. Ndani ya miaka hii miwili tumechukua watu wachache sana. Master anasema hataki kuchukua watu wengi ili kuendeleza hadhi ya Baffold kama ulivyoiacha”


“Hahaha.. halikuwa hata katika daraja la juu wakati naondoka , lakini naona Master wako amefanya kazi kubwa kulikuza”


“Ni kwasababu kipindi kile hukutaka kuwa muuaji ndio maana halikuwa katika daraja la juu. Vinginevyo Master asingeshika namba moja kama ilivyosasa”Aliongea mrembo Ukungu.


“Vipi kuhusu wewe? Upo nafasi gani katika kuua?”


“Nimemuangusha tu Master , nipo nafasi ya tisa?” Hamza mara baada ya kusikia hivyo kidogo tu ateme kawaha aliokuwa akinywa.


“Umeshafika levo ya tisa! Wakati Master wako akiwa katika umri wako alikuwa chini kabisa kuliko wewe. Ki ufupi kwa spidi yako umemzidi mno”Aliongea Hamza.


























SEHEMU YA 187.


Hamza aliweza kukadiria uwezo wa Rhoda kuwa katika levo ya Ukaidi wa asili , levo hio ilikuwa ni mwanzo mwa levo ya nafsi na kufikia hatua hio sio jambo dogo hata kidogo.


Lakini kuingia katika topten ya maninja tena nafasi ya kumi , halikuwa swala jepesi ambalo linategemea mafunzo ya nishati peke. Ilihitajika mbinu nyingi sana za kimauaji vinginevyo ni ngumu kufikia katika daraja alilokuwepo.


“Lakini kaka wewe wakati ukiwa una miaka ishirini tu , tayari uliweza kushinda vita takatifu na kutengeneza jamii ya Inferno ya daraja S na kisha hata kutunukiwa nyota kumi za ugwiji. Nikijaribu kujilinganisha na wewe najiona kama punje katika mchanga”


“Ah! Tatizo mwalimu wako ni Roho mchafu , ni sawa tu kuwa na uwezo kumzidi yeye , inatosha kabisa na huna haja ya kujilinganisha na mimi , hata mimi nilikuwa chini ya watu vilevile , ukijumlisha na bahati yangu”


“Naonekana mdhaifu , pengine ndio maana hunipendi”Aliongea Black Fog.


“Hebu acha kuwa mjinga , wewe ni mdogo wangu wa hiari kwanini nisikupende”Aliongea Hamza akimfinya shavu.


Rhoda mara baada ya kuona Hamnza hakuwa akidanganya aliishia kuvuta pumzi ya ahueni huku tabasamu likipamba uso wake.


“Napenda sana kazi ya kuua , huwa naifurahia mno”


Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akikosa usemi na kuona kweli Asmuntis ameweza kupandikiza roho chafu kwa msichana mrembo kama huyo , inakuwaje binadamu afurahie kumuua mwenzake?.


Wakati wakiendelea kutembea mara tu watu wawili walionekana mbele yao na kumfanya Hamza kuvutiwa nao , lakini kwasababu Hamza alikuwa katika hali ya kulindwa hakutaka kufanya chchote na vilevile hakutaka kumfanya Roida kutumia uwezo wake hivyo hakuongea chochote , lakini ni muda ule uso wa mwanamke huyo ulibadilika mara baada ya kuhisi kitu kisichokuwa cha kawaida na urembo wake ulipotea palepale , ilikuwa ni kama ni mtu mwingine kabisa sio yule wa mwanzo.


“Bro kuwa makini , kuna kitu sio cha kawaida hapa”Aliongea na wala Hamza hakuonyesha kushangaa sana.


“Nini tatizo?”


“Angalia hatua saba mbele yetu kuna mwanaume alievalia koti la rangi ya kahawia na mwanamke alievalia koti la rangi nyeupe ni watu wa Metal Tide, Gray na Helena”Aliongea Black Fog.


“Kweli! Unawafahamu?”


Hamza alikuwa akilijua kundi la kimasenari lenye kauli mbiu yao a ya Uaminifu wa ndani , kundi hili la Metal Tide ni la daraja A, ni kundi ambalo nusu linajitegemea na nusu ipo chini ya wizara ya ulinzi.


Masenari wao hutokea dunia nzima na walinufaika na ruzuku za serikali ya nchi ya Mafuvu. Lilikuwa kundi muhimu sana kwa misheni ambazo Serikali ya Kifaransa haikutaka kuhusisha wanajeshi wake wa moja kwa moja ndio hutumia kundi hilo.


Jina la Metal Tide inasemekena lilitokana na siraha iliotumiwa na Knight Templar aliemjeruhi mfalme wa Ufaransa kabla ya kuchinjwa hadharani miaka mingi iliopita , wengi wanaamini kundi hili lilikuwa na muunganiko na jamii ya siri ya Knight Templar ambao wamekuwa na kisasi na serikali ya Ufaransa.


Kiongozi wa kundi hilo la kimasenari alifahamika kwa jina la Gonzalez maarufu kama Goliathi wa chuma. Aliaminika kuwa muumini mkuu wa jamii ya Wicca akichanganya mafunzo yake ya kuvuna nishati na nguvu za kichawi. Lakini tokea awe kuiongozi wa kundi hilo mara nyingi sana watu waliokuwa na mashaka na uwezo wake. Alikuwa kiongozi kwasababu ya uwezo wake wa kimapigano lakini bado iliaminika hakustahili hata nyota moja ya Ugwiji.


Jambo hilo la watu kumshuku halikumfurahisha kabisa Gonzalez , lakini vilevile alikuwa akiogopa kupambana na Magwjini kwa kuhofia uwezo wake ni mdogo.


“Bro , kutokana na sasa hivi umepoteza uwezo wako nina uhakika Gonzalez akizipata hizi habari atataka kuomba kushindana na wewe ili aingie katika daraja la Hadhi ya Ugwiji , unapaswa kuwa makini sana , mimi na wenzangu tutahakikisha unapata ulinzi wa kutosha”Aliongea Fog.


Hamza kusikia hivyo alitamani kucheka lakini aliona atashitukiwa kama anaigiza kuwa dhaifu , hivyo aliishia kutingisha kichwa kukubali .


“Sawa , lakini sina uhakika kama watatafuta ugomvi na mimi”


“Ngumu kusema, baada ya pambabo lako na Mr Black wengi waliamini uliamua kustaafu kutokana na kupata majeraha makubwa , kwa mantiki hio lazima Gonzalez atakuwa anajua hali uliokuwa nayo na anapanga kutumia kama nafasi”Aliongea Fog na muda huo Gray na Helena waliwasogelea


“Black Fog ni bahati sana kukutana na wewe hapa”Aliongea mwanaume mweusi aliekuwa na kipara huku akionyesha meno yake yote nje.


Metal Tide na Baffold yote yalikuwa makundi katika ulimwengu wa siri , utofauti tu ni kwamba Baffold ni Hitman Guild , wakati Metal Tide ni kundi la kimasenari kama ilivyo kwa The Eagle’s au Blackwater. Ni mara chache sana makundi haya kuingia kwenye mgogoro kutokana na utofauti wao wa kikazi.


“Haiwezi kuwa bahati kwasababu hatuna ukaribu”Aliongea Black Fog kikauzu.


“Miss Fog hata kama hatuna ukaribu lakini tunafahamiana , wote sisi ni watu wa ulimwengu wa siri na nakubali uwezo wako katika ulimwengu wa wauaji, unaonaje tukikaa chini na kuongea kidogo huku tukipata kinywaji”


“Not interested”Aliongea Fog.


“Bro ni kama nakufananisha hivi , nahisi nishawahi kuona picha yako sehemu ila sikumbukji”Aliongea Gray huku akimwangalia Hamza na Helena palepale na yeye alionyesha kushangaa kimaigizo.


“Ahh! Gray wewe ni mjinga , unamsahau vipi Lucifer! Mfalme wa kuzimu. Samahani sana mkuu Lucifer”Aliongea Helena kinafiki na palepale yeye na Gray kama vile wametoka ndotoni walimsalimia Hamza kwa heshima lakini aliwazuia.


“Nishastaafu , haina haja ya kunionyeshea heshima wakati mmeanza kuniita na majina ya utani”


“Sir mafanikio yako ni makubwa mno , tunakukubali sana . Je upo hapa kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha Magwiji?”Aliuliza Helena.


“Sijui maana sijapata mwaliko wowote , na pia nimekwisha kustaafu , sidhani kama kuna haja mimi kushiriki”


“Sir kama usipoenda itakuwa ni hasara kwa Kikao. Kwa niaba ya wenzetu wote ndani ya Metal Tide tunakukaribisha Paris”Aliongea Gray


“Kama mmemaliza naomba muondoke tafadhari , acheni kumsumbua mfalme wangu”Aliongea Fog akionekana kukosa uvumilivu kabisa.


“Hehe.. Black Fog mbona una wasiwasi sana. Sisi tunaonyesha tu furaha yetu kukutana na Mtaalamu , Gwiji wa hadhi ya nyota kumi. Au haturuhisiwi?”


“Sire naomba unipe nafasi ya kukukaribisha makao makuu yetu ya Metal Tide . Mkuu wetu anakukubali sana , nina uhakika atakukaribisha kwa ukarimu mkubwa sana”


“Niko bize kwasasa hivyo tunaondoka”Aliongea Hamza akikataa mwaliko ule.


“Oh .. basi sio mbaya”Aliongea Gray huku akiwaangalia Hamza na Roida wakiondoka katika macho yao na ile walivyoona wamewaacha kwa umbali mrefu waliangaliana.


“Gray hujahisi chochote , nahisi kabisa amekuwa wa tofauti”Aliongea Helena.


“Ni kweli kabisa, ile hali ya ujivuni imepotea kabisa . Kimantiki kwa mtu kama yeye asingetaka hata kuongea na watu kama sisi na hata kumtania kwa kumuita Lucifer . Kingine sijaweza kuhisi msisimko wowote wa nishati za mbingu na ardhi kutoka kwake , unadhani atakuwa feki?”


“Labda itakuwa kweli kuhusu ule uvumi! Nasikia mara baada ya vita yake na Mr Black alipoteza nishati za mbingu na ardhi”Aliongea Helena kwa hamasa.


“Nadhani itakuwa kweli kabisa vinginevyo Black Fog asingekuwa siriasi namna ile . Tuendelee kufuata maagizo ya kiongozi wetu kuujua ukweli vizuri”Aliongea Gray na kumfanya Helena kutoa tabasamu la uovu na palepale alitoa simu yake na kupiga namba flani..


******


Katika hoteli ya Four Season , Regina alionekana ndio kwanza anarudi kutoka kwenye kampuni. Mara baada ya kuingia katika chumba chake alitupia mkoba wake pembeni na kuvua koti lake na kisha alijilaza kitandani akivuta pumzi nyingi.


Alijihisi upweke ndani ya chumba hicho kikubwa na alishindwa kujizuia kumkumbuka Hamza kama mshenzi mmoja hivi ambae baadala ya kumbeleza akaamua kumpotezea na bado hata hakuhangaika kumtafuta tokea asubuhi. Kadri alivyokuwa akimuwazia ndio alivyozidi kumchukia.


“Ameenda wapi huyu mshenzi?” Aliongea huku akitoa simu yake kutoka kwenye mkoba akipanga kumpigia, lakini mara baada ya kufikia jina lake alisita na alianza kujiuliza kwanini ampigie kama mtu hajali.


Regina alijikuta akisaga meno kwa hasira na kuweka simu pembeni , huku kwa wakati mmoja akihisi njaa kali na palepale hakuwa na jinsi na kuchukua simu ya hoteli na kupigia jikoni, alihisi uvivu kwenda kula peke yake.


Ile anataka kupiga simu kengele ya chumbani kwake iligonga na alijua ni Hamza huyo na alijiandaa kumfokea na kumnunia lakini ile anafungua alishangaa kuona ni Meneja wa hoteli akiwa amesimama na tabasmu pana usoni.


“Miss Regina , sorry to bother you”Aliongea yule meneja kwa kingereza.


“It's nothing, what's wrong?”


“Well, Mr. Francois Pino and Mr. Henry Pino, they said they would give you a present. They are already downstairs. May I ask if they can come up?”Aliongea Meneja akimaanisha kwamba watu wanaofahamika kwa jina la Fanco Pino na Henry wana zawadi zake na wapo chini wakiomba kama wanaweza kupandisha kumpatia.


Regina mara baada ya kusikia majina hayo ni kama alishawahi kuyasikia na mara baada ya kufikiria kwa kina akili yake ilifanya kazi na kumfanya awe na wasiwasi kidogo.


“Unamzungumzia Pino wa familia ya Pinault na mwanae au ni watu gani?”Aliuliza Regina kwa shaka.


“Ndio , nadhani utakuwa unawafahamu? Wametoa maagizo kabisa kwamba mlengwa wanaemtafuta ni wewe. Ni tajiri Pinault mwenyewe kutoka Kering, tajiri maarufu anaefahamika dunia nzima”Aliongezea munyu meneja huyo , huku akimwangalia Regina kama vile haamini kama kweli ndio mlengwa.


Regina alijihisi ni kama ubongo wake umekuwa mdogo ghafla . Haijalishi alikuwa na akili kiasi gani , hakuweza kujua kwanini tajiri namba moja katika ulimwengu wa fasheni amekuja mwenyewe hotelini kwa ajili ya kumpatia zawadi.


Ni kweli Regina alikuwa na utajiri wa Dollar Bilioni kumi akiwa manamke wa kwanza kwa Afrika , lakini asingeweza kujilinganisha kabisa na mtu kama Francois Pino ambae familia nzima inamiliki zaidi ya Dolar bilioni mia na ushee. Ukweli kwa tajiri kama huyo pesa ilikuwa ni utambulisho tu wa mali zinazoonekana ambazo anamiliki , lakini sirini nani anajua ni kiasi gani anamiliki.


Cha kushangaza zaidi ni kwamba tajiri huyo na mwanae wamekuja mpaka hotelini hapo na kuomba kabisa kuonana nae kwa ajili ya kumpa zawadi kwa kupandisha chumbani kwake.


Ifahamike kwamba hata kama Regina angeomba kufanya kazi na kampuni yao , asingeweza kabisa kukutana na tajiri huyo zaidi ya wafanyakazi wake tu. Regina aliishia kudhibiti hisia zake na kisha alitingisha kichwa.


“Nashuka kuonana nao”


Aliongea Regina akiamini itakuwa heshima kama yeye ndio ataenda kukutana nao na sio wao kuja kuonana nae.


Meneja hakuwa na maswali mengi na palepale alimchukua Regina na kushuka nae.


Ile wanafika katika ukumbi wa aneo la mapokezi , Regina alijikuta akishangazwa na kile kilichokuwa mbele yake.


Katikati ya ukumbi huo kulikuwa na sehemu ambayo ilikuwa na package nyingi sana mikoba na zote zilikuwa ni za kifahari kutokea katika kampuni ya kering.


Regina licha ya kutokuwa na muda wa kutembelea sana maduka ya kifahari , lakikini hakuwa mshamba wa bidhaa halisi za Gucci na Bottega, kwa haraka sana aliweza kugundua thamani ya kila bidhaa iliokuwa ndani ya hilo eneo. Kwa mahesabu ya haraka haraka aliamini itakuwa ni zaidi ya Euro milioni nne na zaidi.


Kulikuwa na mabodigadi wa kizungu kulia na kushoto waliokuwa wakitoa ulinzi kwa bidhaa hizo.


Kulikuwa na mwanaume mzee hivi na mwingine wa makamo waliokuwa wamesimama na walijawa na tabasamu mara baada ya kumuona Regina.


“Mr Pino! Mimi ndie unaenitafuta?”Aliuliza Regina baada ya kuwatambua maana ni kama hakuwa na uhakika kama yeye ndio kweli anatafutwa.


“I am honored to be of service to you, madame, and I hope you will enjoy these gifts.”Aliongea Pino akionyesha ishara ya heshima.


“Mr Pino tafadhari naomba usiwe hivyo , mimi ni mfanyabiashara wa kawaida kabisa , nadhani mtakuwa mmenifananisha na mtu mwingine”Aliongea Regina kwa wasiwasi na hali ile ilimfanya yule mzee kuona Regina hakuwa na uelewa wowote kuhusu Hamza ni nani.


“Samahani sana Madam kwa kutokupa maelezo ya kutosha , tupo hapa kwa maagizo ya mume wako. Tupo pia na miadi ya kuonana na Mr Hamza kwa ajili ya chakula cha mchana , nadhani utaelewa kila kitu akishafika hapa”Aliongea.


“Unamaanisha hizi zawadi zimetoka kwa Hamza?” Aliuliza Regina akiwa katika mshangao mkubwa na palepale alijikuta akijua ni hisia gani zimtawale. Alijiuliza ni surprise ngapi ambazo Hamza ataendelea kumfanyia mpaka kuja kuacha. Mr Alec, Dokta Ronicas na Paco walitosha kabisa kumshitua moyo wake lakini awamu hio ni Tajiri mkubwa duniani tena na mwanae?.


Japo ni kweli Hamza alishamwambia anajuana na watu wengi maarufu ambao wanaweza kumsaidia katika biashara zake , lakini Regina hakuwahi kuwaza kati ya watu hao ni tajiri huyo.


Kilichomfanya zaidi Regina kujisikia vibaya ni kwamba Pino na mtoto wake wote walikuwa wakimuonyeshea heshima kwa kumnyenyekea.


“Mr Pino samahani naomba kuuliza , Hamza ni nani kwani , imekuwaje ukwa mnafahamiana?” Aliuliza na kumfanya Mzee Pino kushikwa na haya kidogo.


“Kitu pekee tunachoweza kusema ni kwamba Hamza ni mfadhili wetu . Tumeweza kuilinda kampuni yetu zidi ya washindani wetu kwa msaada wake” Regina mara baada ya kusikia hivyo alishangaa na kujiuliza Hamza amefanya nini mpaka kulinda kampuni hio, kwa uwezo upi?.


“Madam , hizi zawadi zipelekwe chumbani kwako au sehemu nyingine?”Aliuliza Mzee Pino.


“Mr Pino , hizi zawadi ni nyingi sana , sidhani kama zitatosha katika chumba changu , pia sidhani kama Hamza ndio aliezichagua”Aliongea Regina.


“Hapana , hizi zawadi ni Mr Hamza mwenyewe aliezichagua”Aliongea Mr Pino akimpigia pasi Hamza.


“Lakini hata kama ni yeye kweli zitajaa chumba kizima na kuacha nafasi au..” Regina kabla hajamaliza Mzee Pino alimgeukia Meneja.


“Kuna chumba kingine kipo wazi?”


“Ndio , kuna kingine”


“Andaa chumba hicho kwa ajili ya Madam na hizi zawadi zitapelekwa katika chumba chake”Aliongea Pino.


Kama mtu angesikia kinachoendelea hapo angemuona huyo mzee amegeuka kuwa kichaa , yaani chumba cha mamilioni ya hela anataka kukigeuza kuwa stoo ya kuhifadhia zawadi?.


Lakini mtu huyo alietoa maagizo ni tajiri mkubwa ndani ya nchni ya mafuvu, hivyo meneja hakusita hata kidogo na aliondoka kwa ajili ya kuandaa chumba hiko.


Regina siku zote alijiambia alikuwa akijua kutumia hela , lakini mara baada ya kuona jambo hilo alijiona ni wakawaida sana.


“Madam , walinzi wetu watazipeleka zawadi hizi , ni matumaini yangu utazipenda”Aliongea Pino kwa heshima na mpaka muda huo hakujua ajibu nini maana hata yeye mwenyewe alikuwa akijiuliza mwanaume aliemuoa ni nani .


“Ayaa Mzee Pinoo!!”


Muda huo sauti kutoka nje ilisikika , alikuwa ni Hamza aliekuwa akiingia ndani ya hoteli hio akiongozana na Roda.


Hamza mara baada ya kumuona mzee huyo alicheka kwa furaha na kumsogelea.


“Samahani kwa kukawia kurudi , nilitoka mara moja”Aliongea Hamza akionekana kutojali kabisa vitu vilivyokuwa kwenye sakafu , kwake yeye alijua Mzee Pino ni mtaalamu hivyo haikuwa na haja ya kuangalia ameleta nini.


Muda ule Mzee Pino alitaka kupiga kelele na kuita Prince , lakini alijizuia mara baada ya kukumbuka uwepo wa Regina katika eneo hilo na haraka sana alimshika mkono mwanae Henry na kumsalimia Hamza kwa pamoja.


“Mr Hamza!”


“Huna haja ya kuwa hivyo mbele ya ndugu yako kama mimi”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu kabisa na kumshika Mzee Pino na mwanae Henry mabega.


Kilichowashangaza watu ni kwamba licha ya Hamza kuonekana mdogo , lakini alikuwa ni kama mtu mzima kwa mzee huyo na mwanae.


“Mr Hamza , nimezisikia habari nyingi zako kutoka kwa baba , natumaini siku za usoni nitaweza kuwa na mchango mdogo kwako”Aliongea Henry.


“Hakuna shaka kabisa , unaonaje ukimtumia mke wangu mara moja moja baadhi ya bidhaa mpya kila zinapotoka nchini Tanzania , nina uhakika atafurahi”Aliongea Hamza huku akimkonyeza Regina.


Regina mara baada ya kuona namna Hamza alivyokuwa akijiachia mbele ya watu hao aliamini hakuwa akiota na kila kitu ni kweli.


“Nitatuma hela kwa ajili ya kununua , sidhani itakuwa vizuri kupokea bure tu”Aliongea Regina.


Hamza aliweza kuona maneno ya Regina hayana ukweli wowote maana namna alivyoangalia walinzi hao wakibeba zawadi hizo kuzipeleka juu , alionekana kuwa na shauku kubwa.


Wanawake wanapenda zawadi za kifahari mno , ni rahisi sana kumlegeza mwanamke kupitia zawadi kuliko maneno.


Kwa macho ya Regina Hamza aliona kabisa Eliza alikuwa sahihi , haikujalisha mwanamke ni tajiri kiasi gani , lakini siku zote hupenda kupokea zaidi zawadi hata kama anao uwezo wa kununua. Maneno bila vitendo haikutosha kwasababu mwanamke siku zote anataka kuona kile mwanaume anachomfanyia na sio kile anachoambiwa.


Muda huo Roida alisogea mbele ya Regina kwa ajili ya kumsalimia.


“Hello , Sister Regina!”


“You are ..” Muda huo ndio sasa Regina aligundua Hamza alikuwa ameongozana na msichana ambae silika yake haikuwa ya kawaida hata kidogo. Na alishindwa kujizuia na kumwangalia Hamza na macho makali.


“Mbona humtambulishi?”


“Wife huyu ni dada yangu wa hiari , anaitwa Rhoda . Mwalimu wake ni rafiki yangu .. najua maelezo hayajitoshelezi lakini nitakuelezea vizuri badae”Aliongea Hamza.


“Sister Regina wewe ni mrembo mno , ni mara yangu ya kwanza kuona mwanamke mrembo sana kutoka Afrika kama wewe , ndio maana Kaka Hamza amekubali kukuoa”Aliongea Roida kwa dhati kabisa na Regina mara baada ya kuona tabasamu la msichana huyo alijikuta akivuta pumzi ya ahueni. Alimuona kama msichana mdogo wa kawaida ambae pengine ni kweli ni mdogo wake Hamza.


Asichokijua Regina ni kwamba mwonekano aliokuwa akionyeshewa na Black Fog ulikuwa ni wa maigizo tu.


“Na wewe pia ni mrembo mno, naona umechanganya rangi kama Hamza, wewe ni raia wa nchi gani?”Aliuliza Regina.


“Baba yangu ni Mwafrika wa Ethiopia , Mama ni Mgiriki”Aliongea.


“Oh! Wewe ndio uliefika kumtembelea Hamza asubuhi na kutoka nae?”Regina alitaka kujua ni wapi Hamza alienda asubuhi asubuhi.


“Ndio , nilimsindikiza kwa ajili ya kumsaidia kukuchagulia zawadi zako . Amehangaika kweli. Dada niseme tu umebarikiwa mno kwa kuwa na mume bora kama Hamza”


“Kumbe!”Regina alijikuta akimwangalia Hamza na kidogo alijisikia amani. Hata ile hali ya kumchukia Hamza ilimpotea.


Hamza mara baada ya kuona pasi ambazo Roda anampigia zilimfikia vilivyo alishindwa kujizuia na kumuonyeshea kidole gumba.


“Hehe mke wangu , mbingu na ardhi ndio mashahidi zangu muda wote nakufikiria wewe tu , lakini wewe unadhani nimetoka kwa ajili ya kwenda kutafuta mwanamke , nilijisikia uchungu kweljanai ”Aliongea Hamza huku akijifanyisha kuwa na huzuni.


“Huaminiki kwasababu una mambo mengi ya chini chini yanaendelea. Ila nimeamini maneno ya Roida, anaonekana kuwa msichana mpole na msafi. Sijui hata kwaniniu anakujali nyang’au mkubwa kama wewe”


Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo alitaka kucheka kwa sauti , huku akijiambia laiti Regina angeona mambo ambayo Black Fog alikuwa akiyafanya jana kumtega , Regina angedondosha jicho.


Mzee Pino na mwanae hawakutaka kula chakula katika hoteli hio , hivyo waliungana na Hamza na Regina na kuingia kwenye Roll Royce kuelekea katika hoteli yao ya kifahari kwa ajili ya chakula.


Upande wa Regina aliona anapoteza muda sana , kwani bado alikuwa akitakiwa kushiriki katika Party ambayo imeandaliwa na wafanyabiashara. Mzee Pino mara baada ya kusikia maelezo ya Regina kuhusu kushiriki alionekana kuelewa jambo.


“Madam unzungumzia tafrija ilioandaliwa na familia ya Alice sio? Henry pia amealikwa katika hio sherehe na anaenda kuwakilisha kampuni yetu ya Kering , kama hutojali tutakupeleka moja kwa moja”Aliongea lakini Regina aliatingisha kichwa kukataa.


“Mr Pino licha ya uhusiano wako na Hamza , sitarajii kutumia ukaribu wenu kwa ajili ya maswala yangu ya kibiashara , nataka kutumia uwezo wangu binafsi kushinda deal”Aliongea Regina.


“Lakini Madam kuna madaraja ukifikia kama mfanyabiashara , muda mwingine huwezi kufanya kila kitu kwa uwezo wako binafsi”


“Ni kweli ila nataka kujaribu kuona ni umbali kiasi gani naweza kwenda kwa uwezo wangu binafsi”


“Mzee Pino , tafadhari usije ukaingilia maswala ya kibiashara ya mke wangu , maana hapendi”Aliongea Hamza.


Mara baada ya baba na mwana kusikia hivyo hawakuongea zaidi na badala yake waliingia Dining kwa ajili ya chakula mpaka kumaliza.


Baada ya Mzee Pino kuondoka , upande wa Black Fog aliaga pia kwamba anaondoka , lakini hakuondoka bali alijificha tu asionekane kwa Regina.


Regina na Hamza walirudi chumbani. Regina aliishia kuangalia maboksi na mifuko ndani ya chumba hiko na kuona ni kama bado yupo ndotini.


“Wife umependa zawadi zangu?”Aliuliza Hamza huku akimshika Regina kiuno huku akiwa na tabasamu.


Lakini ghafla tu Regina aligeuka na kumwangalia Hamza kwa macho makali.


“Wewe na Rhoda nini kinaendelea kati yenu?”
 
Hundred Shadows.


Hamza alijikuta akishangazwa na swali lile kwani hakuwa amejiandaa kabisa kama Regina angeuliza, alidhania yalikuwa yameisha pale pale.


“Wife, si nilishakuambia yule ni mdogo wangu wa hiari.”


“Wewe! Nilikubali kishingo upande pale kwasababu ya wageni. Hivi unadhani mimi ni mjinga? Yaani utoke naye asubuhi halafu uje uniambie eti mmetoka kuchagua zawadi. Unadhani mimi ni mtoto wa miaka mitatu kwamba nitakubaliana na kila unachoongea?”


Hamza alijikuta akishindwa kujua namna ya kujitetea, hakudhania Regina angeweza kugundua kuna kitu kinachoendelea kati yake na Roda. Ukweli, aliamini katika uigizaji wake pale Regina asingejua kitu, lakini matokeo yake Regina alionekana alikuwa akiwachora tu.


“Wewe na huyo mdogo wako mnadhani mimi ni mjinga, kwamba nitaamini kila mnachoongea?” Aliongea Regina huku akimkodolea Hamza kama vile alikuwa akisoma mawazo yake.


“Wife, hebu acha kufikiria mbali. Ni kweli hakuna kilichotokea kati yetu.”


“Najua kwasasa unasema kweli maana kwa mtu uliekosa aibu kama wewe huwezi kuficha kama kweli kuna kilichotokea,” aliongea Regina na Hamza hakutaka kuendelea na mada hiyo hivyo alicheka na kuingizia kitu kingine.


“Mke wangu, hebu tuachane na hayo kwanza, unaonaje ukiangalia ni zawadi gani zitakuvutia zaidi. Angalia kama kuna gauni unaweza kuvaa usiku wa leo kwa ajili ya Royal Ball invitation.”


Regina alikuwa na shauku kuhusu zawadi hizo hivyo hakutaka kuendelea na mada hiyo pia. Isitoshe alimfahamu Hamza, alikuwa muhuni na amekubali kuishi naye hivyo hivyo kibishi.


“Kwasababu ya mzee Pino nitaangalia, ila sio kama najali sana vitu kama hivi,” aliongea akigeuka na kuanza kuangalia vitu vile akiwa amechuchumaa.


Kulikuwa na nguo, mikoba, viatu na baadhi ya vito vya thamani ya juu sana, na alitoa kimoja baada ya kingine. Kadri alivyokuwa akikagua zawadi hizo uso wake ulijaa furaha huku macho yaking’aa. Alifurahishwa zaidi na aina ya mikoba ambayo ameletewa na kumfanya achizike na kioo kwa kujigeuza geuza.


“Hamza, unaonaje urembo wa huu mkoba, mbona ni kama mnyororo wake ni mrefu sana?” aliuliza Regina akiwa kwenye kioo.


“Kwako wewe kila utakachovaa kinakupendeza na huo mkoba ni mzuri pia sioni tatizo.”


“Vipi na hili gauni? Naona kama vile chini limepwaya sana mwilini?”


“Ni zuri sana kwa umbo lako, ukivaa lazima litakupendeza.”


“Kwahiyo kama nikivaa hili nitumie na mkoba upi? Naona kama huu wa njano haviendani hivi...”


“Mimi mwenyewe sijui chochote sana kuhusu mavazi ya wanawake...” aliongea Hamza huku akikuna kichwa.


“Kwanini upo hivyo wewe? Nakuuliza ni kipi hapa kitanipendeza sijakuuliza ujuzi wako kwenye mavazi ya wanawake?”


“Nadhani hilo la rangi nyekundu litakukaa zaidi vizuri na huo mkoba.”


“Mh! Mimi naona hili la pinki ndio zuri zaidi, hili jekundu ni kama litanifanya nionekane mzee.”


“Kama ushachagua hilo tokea muda mrefu, kulikuwa na haja ya kuniuliza?”


“Hivi wewe kwanini unakosa uvumilivu?” Aliongea Regina huku akikunja sura.


“Wife, wewe endelea kuchagua, mimi naenda kupumzika kidogo.”


“Kwahiyo unachukia kuwa na mimi hapa sio? Kunisaidia kuchagua kipi nivae ndio unajihisi kuchoka?”


“Sijamaanisha hivyo, kwanini nichukie kuwa na wewe mke wangu?”


“Huna haja ya kujielezea, kila kitu kipo wazi. Kama umenichoka huna haja ya kuendelea kubakia na mimi, nenda kamtafute Roda,” aliongea kihasira na kisha aligeuka na kuendelea na uchaguzi wake.


Hamza kuona vile hakutaka kuondoka tena na alitembea na kumkumbatia Regina kwa nyuma.


“Mke wangu...”


“Ondoka!”


“Sitaki kuondoka, nataka kuwa na wewe.”


“Si umesema unaenda kupumzika? Sitaki kukusumbua hivyo wewe ondoka zako tu, huna haja ya kujisumbua,” aliongea huku akijipinda pinda kutoka katika kumbatio la Hamza. Lakini hakupewa nafasi hiyo kwani Hamza alikaza mikono.


“Mke wangu usiwe na hasira basi. Ijapokuwa sijui sana kuhusu mitindo ya kimavazi, ila nitakusaidia kadri ya uwezo wangu kuhakikisha unapendeza,” aliongea Hamza kwa sauti ya kubembeleza.


“Sema mke wangu, mwonekano wako unavutia mno na hizi nguo ni kama umetengenezewa kuvaa wewe tu.”


Regina ambaye alikuwa ameshikilia sketi mara baada ya kusikia maneno hayo alijikuta akitabasamu kisirisiri kwa furaha.


“Wewe ni muongo, umeweza hata kuniigizia wewe na yule mwanamke na kuniona mimi mjinga.”


“Mke wangu, achana na hayo yaliopita,” aliongea Hamza akihofia Regina ataanza kukumbuka na kukasirika tena.


“Utajua mwenyewe ila jua tu umenifanya nisiwe na furaha na wewe tena.”


“Wife, nifanye nini uwe na furaha?” aliuliza Hamza na pale pale macho ya Regina yalichanua.


“Unajali sana mimi kuwa na furaha?”


“Lazima nijali furaha yako, mke wangu.”


Mara baada ya kusikia hivyo, aligeuka na kumwangalia Hamza usoni.


"Basi nataka unisaidie kuchagua vazi kwa ajili ya kwenda kwenye party leo usiku," aliongea Regina, na kumfanya Hamza aangalie nguo zilizokuwa chini hapo.


Hamza alijiambia kuwa kama angejua, asingemruhusu Mzee Pino kuleta nguo nyingi namna hiyo. Lakini kwa sababu alitaka kumfurahisha Regina, aliishia kung’ata meno na kumsaidia mrembo huyo kuchagua.


Mara baada ya kuchagua karibu nguo zote zilizokuwa hapo, Regina alionekana kutoridhika, na walitoka kwenda kwenye chumba kingine kuangalia zingine.


Hamza, baada ya kuingia kwenye chumba hicho cha hoteli na kukuta zawadi nyingi, alitamani kumpigia simu Mzee Pino na kumfokea.


Baada ya kuchagua kwa muda mrefu, hatimaye Regina alipata vazi ambalo lilimridhisha na kumkaa vizuri mwilini. Katika mavazi yote waliyochagua, kutokana na uzuri wake, Hamza hakuelewa kwa nini Regina alichagua vazi la namna hiyo.


"Wife, hii kazi ni zaidi ya kupigana na watu zaidi ya mia moja," aliongea Hamza akiwa ameshika kiuno na kuvuta hewa ya ahueni.


Regina muda huo alikuwa na tabasamu pana akijigeuza-geuza kwenye kioo.


"Nani kakuambia uvunje ahadi yako, uliniahidi mwenyewe ungenitembeza lakini ukapotezea."


"Wife, tatizo ulikuwa na kazi, ningekutembeza vipi?"


"Kazi visingizio tu, wewe sema hutaki kutoka na mimi kwa sababu hupendi usumbufu wangu."


Hamza alimwangalia mwanamke huyo namna ambavyo amevimba mashavu na kujikuta akicheka.


"Wife, nimegundua siku hizi unazidi kupendeza na kuvutia; kipindi kile tulipokutana kwa mara ya kwanza hukuwa kama hivi, ulikuwa kauzu mno."


"Wakati tunakutana hatukufahamiana, na kwenye kampuni nisingekuwa kama hivi la sivyo wafanyakazi wasingenichukulia siriasi," aliongea, na Hamza alitingisha kichwa kukubali.


"Nakubali, ila napenda ulivyo sasa hivi. Sweet and silly wife haha..." Hamza aliongea hivyo, na Regina aligeuka kujiangalia kwenye kioo kana kwamba anaangalia mwonekano wake unaendana na maneno ya Hamza.


"Unavyoongea ni kama umenigeuza kuwa rafiki yako uliyezoeana naye miaka mingi."


"Nikikufanya rafiki vibaya? Kwanza, marafiki wenyewe unao?"


"Ninao wa kutosha tu. Wewe unadhani sina marafiki? Eliza, Prisila, Yonesi wote ni marafiki zangu," aliongea Regina huku akikunja mikono yake na kuendelea, "Nina rafiki yangu wa karibu sana ambaye yupo Spain kwa muda mrefu, hata yeye ananiona nimebadilika na kuwa kama mtoto," aliongea kwa kulalamika.


Hamza hapo hapo alimshika mkono na kumvuta kwake, na kufanya wote wawe wamekumbatiana mbele ya kioo.


"Wewe unafanya nini sasa?"


"Wife, unajua napenda namna unavyobadilika kutokana na mazingira; napenda namna ulivyokauzu kwa watu kama CEO, lakini kwangu unakuwa kama mtoto," aliongea Hamza. Regina hakujitoa katika kumbatio lile, badala yake alijiangalia pia kupitia kioo namna Hamza alivyo mkumbatia kwa nyuma.


"Kweli! Kwa hiyo unapenda nikiwa kama mtoto, eh?"


"Sana, kwa watu wengine kuwa kauzu na bosi, ila kwangu nataka uwe mtamu kama sukari."


"Mh! Kwa hiyo nyie wanaume mnapenda wanawake wa hivyo?" Aliuliza Regina huku akiwa na aibu kidogo.


"Sijui kuhusu wengine; ninachojua ni kwamba nakupenda zaidi unavyokuwa karibu yangu na kuniganda."


"Unamaanisha nini kukuganda! Ni kwa sababu ya kutaka kujua ulipo siku hizi ndio maana unasema nakuganda; unataka niwe na wewe muda wote?"


"Ndio, natamani kuona ukaribu wetu ukizidi kuongezeka siku hadi siku," mara baada ya kusema hivyo, aliinamisha kichwa chake na kumkisi chini ya sikio lake la kulia.


Regina kuona hivyo alianza kujipinda.


"Unafanya nini?"


Hamza hakujibu na badala yake aliendelea kumkisi Regina kutoka sikioni na kushuka mpaka shingoni.


Kitendo kile kilimfanya Regina kuanza kushikwa na msisimko wa hali ya juu na kumfanya avute hewa nyingi huku macho yake yakilegea.


Hamza hakuishia pale, alimsukumiza kwenda kuegamia Wardrobe na kuendelea kumkisi taratibu taratibu...


Regina alijikuta pumzi zikianza kuisha na kujaribu kumsukuma Hamza, lakini nguvu zilikuwa kidogo sana.


"Mke wangu, wewe ni mzuri mno," aliongea Hamza huku akiupapasa uso wa mrembo huyo na kuvuta pumzi nyingi.


Regina mwili ulizidi kupata moto; hakuwahi kupandwa na hisia za ajabu namna hiyo na kumfanya ashindwe kufanya chochote kama zuzu.


Hamza, mara baada ya kumkisi tena, hakukataa na badala yake alianza kutoa ushirikiano huku akisikilizia msisimko wa mikono ya Hamza iliyokuwa ikitalii mwilini mwake.


Hamza alimbeba Regina juu juu na kumuweka kitandani, na alipokuwa akitaka kufungua vifungo vya shati lake, kengele ya chumba hicho ilianza kulia.


"Mkurugenzi!" Alikuwa ni Josh aliyeita.


"Bosi Regina, muda umewadia, upo ndani?"


Hamza aliishia kujitoa juu ya Regina, na mrembo huyo alijikuta akipaniki kidogo kisha kukaa kitako.


Hamza muda huo alikuwa akimtukana ndani kwa ndani Josh kwa kuja wakati mbaya, ilihali yeye alipanga kumlegeza Regina na hatimaye kumega tunda.


"Pumbavu zako Joshua!"


"Jiandae uvae suti haraka, tunaondoka," aliongea Regina, ambaye alianza kujiweka sawa.


"Wife, unaonaje baadae tukirudi tukiendelea..." aliongea Hamza kwa unyonge.


"Don't push yourself too far!"


Hamza alijikuta akinywea na kujiuliza imekuwaje amebadilika tena na kuwa mkali. Regina mara baada ya kumwangalia Hamza alivyonyongea aligundua maneno yake yalionekana kuwa makali.


“Namaanisha usiwe na haraka, tunacho cheti cha ndoa hivyo sisi ni wanandoa halali. Ukiendelea kunifurahisha fursa haitoacha kujitokeza.”


“Mke wangu, kwa sababu umesema hivyo nimepata ahueni, nitahakikisha nakufurahisha ili nipate fursa. Ila wife, upo vizuri hapo kiafuani.”


Hamza mara baada ya kuongea hivyo, Regina alishikwa na aibu kiasi cha kumpiga Hamza teke.


“Kaa kimya! Na acha kuongea ujinga.”


Hamza alijikuta akiwa na furaha ndani kwa ndani, baada ya kugusa eneo muhimu sana kwenye mwili wa mrembo huyo.


Hamza mara baada ya kufungua mlango, Josh alionekana kushangaa baada ya kumuona lakini alipotezea haraka haraka na kuweka muonekano wa kiume.


“Pole kwa kazi Mr. Hamza.”


“Asante Meneja na pole kwa kusubiria muda mrefu,” aliongea Hamza na Josh aliishia kuangalia maboksi ya zawadi yaliokuwa kwenye sakafu na alijikuta akiwa katika hali ya mshangao mkubwa.


“Mr. Hamza hivi ni…”


“Usiulize maswali yasiohitajika. Nenda kanisubirie kwenye gari nakuja,” aliongea Regina na kumfanya Josh atingishe kichwa kuondoka baada ya kuona Regina amekuwa mkali.


Hamza aliishiwa na maneno; tabia ya Regina kubadilika ilimfanya kuonekana ni namna gani alikuwa na zaidi ya nafsi moja.


“Nenda kabadilishe uvae suti, unamwangalia nani?” aliongea Regina akimkodolea macho Hamza.


“Sawa naenda,” aliongea Hamza huku akitabasamu kizembe.


Dakika kumi na tano mbele, Regina na Hamza walikuwa ndani ya gari wakielekea Paris Intercontinental Hotel kwenye tafrija.


Mara baada ya kufika nje ya hoteli hiyo, kulikuwa na magari mengi ya kifahari na watu wengi waliovalia mavazi ya bei ghali walishuka na kuingia katika hoteli hiyo, harufu ya eneo hilo ilikuwa ni ile ya ukwasi wa pesa nyingi.


Alice’s Party ndio jina rasmi la tafrija hiyo na ni sherehe ambayo hukusanya matajiri na wanasiasa wakubwa. Ingawa ilikuwa ya watu binafsi, ilikuwa ni muhimu sana kwa watu wengi kuhudhuria kwa ajili ya kujenga koneksheni za kibiashara.


Katika biashara, ukifikia daraja fulani biashara zako zinategemea zaidi koneksheni na watu. Ijapokuwa mara nyingi katika sherehe kama hiyo hakuna mikataba ya kusainishana, ilikuwa ni fursa ya kufahamiana na matajiri wengi na wafanyabiashara.


Sasa kwa kampuni ya Dosam, kama wangetaka kuimarisha na kustawisha kampuni yao katika soko la Ulaya, sherehe kama hiyo ilikuwa ni fursa kubwa.


Waandaaji walimpatia Regina mwaliko wa sherehe hiyo kwa kutambua uwezo wake, lakini kuhusu suala la ushirikiano wa kibiashara ingetegemea na juhudi zake mwenyewe.


Hamza na Regina mara baada ya kuonyesha Royal Ball Invitations Card, waliruhusiwa kupita na kuingia ukumbini pamoja. Hawakusimama hata sekunde; wahudumu waliwasogezea champagne na kila mmoja akachukua.


Muda huo huo, waliweza kuona mwanaume na mwanamke, weusi walioshikana mikono wakiingia ndani ya eneo hilo.


Mwanaume alikuwa amevaa mavazi ya suti na tai nyekundu, na mwanamke alikuwa mrefu mwenye nywele zilizoachia mabegani. Wote wawili walionekana kuwa na umri wa miaka thelathini hivi.


Mwanaume yule alionekana kumtambua Regina na kumpungia mkono, huku kwa wakati mmoja akiwa na tabasamu la kumkejeli.


“Nimesikia kutoka kwa wafanyakazi wako na wewe umekaribishwa kwenye sherehe hii, nilidhani wamekosea, ila sikutarajia ni kweli utakuja hapa,” aliongea yule mwanaume.


“Mkurugenzi Zuberi, sikujua na wewe upo hapa Paris. Umekuja kwa maagizo ya bodi ya wakurugenzi au upo mapumzikoni?” aliuliza Regina, na kwa haraka haraka ilionekana kama kuna uhasama kati yao.


Hamza alimfikiria kwa kina bwana huyo na jina lake na alionekana kukumbuka kuwa Eliza alishawahi kumzungumzia.


Kilimanjaro Group ilikuwa ni kampuni kubwa yenye makazi yake ndani ya jiji la Mwanza. Inasemekana mwanzilishi wa kampuni hiyo aliishi nje ya nchi kwa miaka mingi, na alivyorudi nchini ndio alifungua kampuni hiyo ambayo ilijihusisha na masuala ya mabenki, Real Estate, burudani, na mahoteli. Ni moja ya kampuni kubwa ndani ya Tanzania.


Ikumbukwe kampuni ya Dosam pia ilijihusisha na mahoteli, Real Estate, ujenzi, na mitindo, hivyo moja kwa moja ilikuwa katika ushindani na kampuni ya Kilimanjaro.


Miaka kadhaa nyuma, Kilimanjaro ilikuwa ni moja ya kampuni kubwa ndani ya Tanzania, lakini mara baada ya Regina kushika hatamu ya uongozi wa kampuni, ilipigwa gepu kubwa mno kutokana na staili ya kibiashara aliyokuwa nayo Regina. Suala hilo lilifanya mambo kuwa magumu kwa Zuberi Daffa ambaye alikuwa ni mkurugenzi.


Zuberi Daffa mara nyingi kila alipokuwa akifanya kosa alikuwa akilinganishwa na Regina katika vikao vya wakurugenzi wa bodi kwa kuambiwa hakuwa akijua kufanya biashara.


“Bosi Regina, asante kwa wasiwasi wako kwangu. Nakupa pole kukutaarifu nipo hapa nchini kwa ajili ya kusaini mkataba na Mzee Kaird na Brewer. Uchokozi wako wa kibiashara umekuwa motisha kwangu kukamilisha hili.”


“Bado ndio kwanza unaingia hapa kwa ajili ya sherehe na unasema unataka kusaini mkataba. Unadhani Kaird na Brewer watakubali kufanya ushirikiano na Kilimanjaro?” aliongea Regina na muda huo mwanamke aliyekuwa ameambatana naye alicheka kidogo na kuongea:


“Kumbe wewe ndio Regina. You don't seem as smart as the rumors say you are. Don't you know me?” aliongea.


“Napaswa kukufahamu?” aliuliza Regina kwa kijeuri.


“Mhmh!” Aliguna huku akifyatua nywele zake kimapozi kurudisha nyuma. “Naitwa Hamissa Nganjilo! Hujawahi kusikia jina langu?”


“Hapana,” alijibu Regina bila ya kuwa na tofauti yoyote ya kimwonekano.


Mwanamke yule alionekana kushangazwa na jibu la Regina lakini alijizuia kutokuonyesha utofauti.


“Basi sina haja ya kujielezea sana kama haunifahamu. Wewe ni aina ya wafanyabiashara ambao hamjui kujichanganya na watu, hivyo ni kawaida hujawahi kusikia jina langu. Nataka nikukumbushe tu kwa nia njema kwamba usije kwenda kujidhalilisha mbele ya Mr. Kaird na Brewer usiku wa leo. Hatupo hapa kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara tu, lakini vilevile ni watu tunaofahamiana nao. Sidhani kama unaweza kutuzidi mimi na mpenzi wangu,” aliongea kwa maringo lakini hata hivyo mwonekano wa Regina haukubadilika.


“Ijapokuwa sikujui wewe ni nani, ila kama mmemaliza sis mnaweza kuondoka.”


“Mhh! Naona una kiburi kama inavyosemekana. Ila kwa sababu unashindwa kuyachukulia maneno yangu kwa uzito basi subiri uone.”


“Misa, huna haja ya kuongea naye sana. Huwezi jua bosi wetu Regina ana mpango wake wa kupata mkataba...” aliongea Zuberi huku akicheka.


“Darling, ulichosema ni sahihi, haina haja ya kusumbuka naye,” waliongea na kisha yule mwanamke alimwangalia Regina kwa mapozi, mavazi yake, na mkoba wake na kisha hakuongea zaidi na kufuatana na mpenzi wake.


Hawakumjali kabisa Hamza aliyekuwa pembeni ya Regina, pengine walijua lazima ni msaidizi tu ama mlinzi, wakiamini Regina bado alikuwa ni single.


“Wife, huyu dada ni kutoka kampuni ya Multimedia Group, kampuni ya habari iliyotanda Afrika nzima mpaka Ulaya?” aliuliza Hamza.


“Kumbe umemjua? Inaonekana karatasi nilizokupatia kwenye ndege ulizisoma?” aliongea Regina.


“Nilizichungulia tu,” aliongea Hamza akijichekesha kizembe na kisha alionekana kufikiria kidogo.


“Kwahiyo huyu Hamissa ni mkurugenzi mtendaji wa Tanzania Multimedia, mtoto wa tajiri Fredi Nganjilo, si ndiyo?” aliuliza Hamza, akimfanya Regina kutingisha kichwa huku akinywa kidogo Champagne kabla ya kujibu.


“Inaonekana Zuberi, ili kujiingiza katika soko la Ulaya baada ya kufeli awamu iliyopita, ameamua kumtumia binti wa Mzee Nganjilo. Kampuni ya Kilimanjaro ni kubwa sana kwa Tanzania na ipo chini ya ubia wa watu wengi. Licha ya Zuberi kuwa mkurugenzi, familia yake inajitahidi sana kumbakiza katika uongozi ili kuendeleza ushawishi wao; vinginevyo, mpaka sasa angeshafukuzwa muda mrefu na bodi.”


Kampuni ya Kilimanjaro ukubwa wake ulitokana na umiliki wa watu wengi; kwa familia ya Daffa, walikuwa na umiliki wa asilimia kumi na tatu pekee, na ndiyo hiyo ambayo walitumia kumfanya Zuberi mtoto wao kuwa Afisa Mtendaji Mkuu. Kwa lugha nyepesi, nafasi ya Zuberi ni kama ya kuteuliwa, na ikitokea wamiliki wa kampuni hawaridhishwi naye, wanaitisha tu kikao cha bodi na kupiga kura ya kumuondoa na kumteua mwingine.


“Kwahiyo, wife, wewe una biashara gani ambayo unashindana nao hapa Paris?” aliuliza Hamza.


“Wanataka pia kufungua thieta, kumbi za sinema na kutengeneza pia. Kaird na Brewer ndiyo matajiri wakubwa kwenye maswala ya utayarishaji wa filamu mbalimbali kwa sasa. Kama wakikubaliana kushirikiana na sisi, ili mradi tuna kiasi cha pesa cha kutosha, maana yake moja kwa moja nitaingia katika ubia wa kibiashara. Lakini kama Zuberi akifanikisha kabla yangu, itakuwa ngumu sana kwangu kuwekeza katika maswala ya filamu; labda nifikirie fursa nyingine.”


“Kwani Multimedia Group wana nguvu sana kiasi cha kufanya kampuni mbili za Ufaransa kufanya nao kazi?” aliuliza Hamza akiwa bado haelewi.


“Kama ni miaka mitatu iliyopita, pengine isingekuwa kama sasa hivi. Katika miaka mitatu iliyopita, kampuni ya Multimedia wamewekeza sana katika soko la Ulaya kwa kununua kampuni za burudani nyingi na kuwapelekea kuwa na ukaribu sana na mastaa wengi, ikiwemo waigizaji, waandishi na wawekezaji wengi. Kwa hiyo, ukiachana na hela, kampuni ya Brewer na Kaird ni rahisi kuichagua Kilimanjaro kutokana na umaarufu wa Multimedia ambao ungesaidia kukuza mauzo.”


“Sasa kama ni hivyo, wewe utashindaje hapo? Unaonekana kujiamini mke wangu.”


“Ijapokuwa ni kweli Multimedia ni kampuni kubwa na ina mastaa wengi ndani ya Ulaya, lakini sio wote. Nipo hatua moja nyuma dhidi yao, hivyo ninachopaswa kufanya ni kutafuta hao ambao hawapo chini yao. Isitoshe, biashara ya burudani ni pana sana; kuna kampuni nyingi duniani ambazo naweza kufanya nazo kazi, ni swala la kuchagua tu itakayonifaa. Ujio wangu hapa sio kwa ajili ya kazi, bali kwa ajili ya kufahamiana tu na Mr. Brewer na Mr. Kaird. Kama ingekuwa kibiashara basi, ni kama walivyosema, siwezi kushinda.”


“Mimi ninachoona kuhusu Zuberi, mtazamo wake umelenga zaidi hadhi yake na sio kile ambacho anakwenda kufanya. Nina uhakika kama ukiweka mipango yako vizuri lazima Brewer na Kaird watakuchagua wewe.”


“Ni kweli, hata mimi pia nina uhakika huo, lakini nguvu ya Multimedia Group sio ya kudharauliwa. Kwa sasa sina kete za kutosha kucheza wakati wa mazungumzo, hivyo nafanya vitu kwa umakini mkubwa.”


“Wife, mwenzako yeye anatumia koneksheni kwa ajili ya kukamilisha dili, kwanini usiniache nikitumia koneksheni zangu kukufanikishia…” Kabla Hamza hajamaliza kuongea, alizuiwa na Regina.


“Unadhani siwezi kushinda mkataba bila koneksheni, mbona kama unanidharau?”


“Wife usifikirie vibaya. Najua unao uwezo, hivyo sitoingilia kabisa. Tunafanya nini baada ya hapa? Au ndio tuanze kuwatafuta Kaird na Brewer?”


“Nataka kula chochote kwanza na baada ya hapo tunaenda kuwatafuta. Kama Herry Pinault akija na ikaonekana nina ukaribu nao, mambo hayatakuwa mazuri,” aliongea Regina, na Hamza alishindwa kuongeza neno na kuamua kuheshimu mawazo ya Regina.


Mara baada ya kukaa na kuanza kula, Regina alikula kidogo tu na kisha alichukua glasi ya Champagne na kumuacha Hamza.


“Bro, kwanini upo mwenyewe?” sauti ilisikika katika masikio ya Hamza. Alikuwa ni Rhoda aliejitokeza mbele yake. Mrembo huyo alikuwa amevaa na kupendeza mno jioni hiyo. Umbo lake lilizidi kujichoresha kutokana na mavazi yake na kumfanya atamanishe. Kilichompagawisha Hamza ni pasua la gauni.
 
“Black Fog, unafanya nini hapa? Mke wangu akituona tupo pamoja, nitakosa namna ya kujielezea,” aliongea Hamza.


“Si tushamwambia mimi ni mdogo wako wa hiari. Sidhani kama kutakuwa na tatizo,” aliongea Black Fog akidhani Regina alikuwa mwepesi kudanganyika.


Hamza muda huo hakujua acheke ama alie, lakini pia hakutaka kuelezea kinachoendelea, vinginevyo Rhoda angegundua kuwa Regina ni mtu mwenye hila sana.


Hamza alifikiria kwa dakika na palepale aliona amwambie tu ukweli mwanamke huyo kwamba hakuhitaji ulinzi wake. Hakujua mrembo huyo ninja angejisikiaje akigundua Hamza alikuwa akimwingizia, lakini hakujali maana ni swala la muda tu na angeweza kushuhudia uwezo wake. Lakini sasa, ile anataka kumwambia, Hamza alinasa hali ya msisimko kwenye mwili wake ikiashiria kuna mtu alikuwa akimwangalia kwa lengo la kutaka kumuua.


Hamza aliishia kusinyaza macho yake; hakudhania kuna mtu atakuja mpaka ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kutaka ugomvi, hata hivyo haikumpa hofu baada ya kuhisi mtu huyo alikuwa wa kawaida sana.


“Naelekea toileti,” aliongea Hamza.


Muda huo na Rhoda aliweza kuhisi kitu hakipo sawa na alimwangalia Hamza kwa wasiwasi kidogo.


“Hata mimi naenda,” aliongea na kumfanya Hamza kukosa tena la kufanya na kujiambia hili eneo ni dogo mno mpaka na Black Fog kuinusa hatari.


“Mimi naenda msalani tu, haina haja ya kwenda pamoja, sawa?”


“Hapana, ni kwasababu nahisi nia ya mauaji ndani ya hili eneo, kwasababu huna nishati za mbinu na ardhi huwezi kuhisia hivyo nina wasiwasi wanakulenga wewe.”


“Kama kweli kuna mtu anataka kuniua, basi haina haja ya kunifuata maliwatoni.”


“Bro usiwe na wasiwasi kabisa, nitashia tu nje, sitoingia ndani. Nimemuahidi Master nitakulinda kwa namna yoyote ile kuhakikisha usalama wako, sitaki kuona ukipatwa na lolote baya,” Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyo namna alivyokuwa siriasi alikosa namna ya kumkatalia.


“Basi hakuna shida, tunaweza kwenda.”


Maliwato yalikuwa upande wa pembeni kabisa kiasi kwamba watu waliokuwa eneo la mapokezi hawakuweza kuona upande huo kabisa.


Hamza bila ya kugeuka alitembea na kwenda kuingia ndani ya eneo hilo, wakati huo Black Fog akibakia nje.


Hakukuwa na watu wengi ndani ya maliwato hayo. Hamza ile anataka kujisaidia aliweza kuona watu wawili waliovalia suti na sura zilizojaa usiriasi wakisogelea upande huo kama vile hawakuwa na habari nae.


Kwa professional killer ni rahisi sana kufoji jina na kadi ya mwaliko na kuzamia kwenye sherehe kama hiyo kwa urahisi kabisa, vinginevyo matajiri wasingetumia hela nyingi kwa ajili ya kujihakikishia usalama.


Muda huo Hamza pia alikuwa katika hali ya maswali mengi akijiambia ni nani anataka kumuua, isitoshe alikuwa amestaafu na alifika hapo bila ya kujitambulisha na hata watu wa baraza la maksi hawakumpatia mwaliko.


Hamza mara baada ya kufikiria kwa kina aliweza kuunganisha doti juu ya kile kilichotokea mchana na wasiwasi wake wote aliuelekeza kwa kundi la kimasenari linaloongozwa na Gonzalez.


Ilikuwa ni rahisi kwa mtu kama Gonzalez kutuma watu kuja kumjaribu ili kujua tetesi za mfalme wa kuzimu kupoteza uwezo wake wa kuvuna nishati za mbinu na ardhi ni kweli.


Kutokana na hilo, Hamza aliona haina haja ya kuwashambulia yeye tena. Kwasababu watu hao wametumwa kwa ajili ya kumjaribu basi ni sawa kuendelea kujifanyisha dhaifu hadi mwisho na muda ukiwadia Gonzalez mwenyewe atajitokeza tu na ndio utakuwa wakati mzuri wa kumshikisha adabu. Vinginevyo kama atapigana na watu hao aliowatuma, Hamza alihisi ni kujikosea heshima sana.


Yaani aonyeshe uwezo wake kwasababu ya watu dhaifu waliokuja kumjaribu, aliona hapana na hiyo yote ni kutokana aliamini kwa uwezo aliokuwa nao Black Fog angetosha kabisa kuwadhibiti wauaji hao.


Mwanaume na yule mwanaume waliachiana mikono mara baada ya kuingia washroom na mmoja alielekea upande wa wanawake, huku mwingine akiingia alipo Hamza.


Kitendo cha kuingia ndani ya eneo hilo, ni kama wamejiingiza kwenye mtego wa Black Fog.


Mmoja akiwa mbele na mwingine nyuma, wote kwa pamoja walifanya shambulizi, huku mkononi wakionekana kushikilia visu vidogo na macho yao yalibadilika kuwa ya kawaida na kuwa yale yenye ukatili wa hali ya juu.


Black Fog alikuwa amejiandaa pia na aliishia kutoa sonyo lenye ukali wa hali ya juu na kwa wepesi mkubwa sana aliruka na shambulizi la teke na kumpiga yule mwanaume mkono wake ulioshikilia kisu na kufanya kidondokee pembeni.


Yule mwanamke mara baada ya kuona shambulizi lile, haraka sana alisogea akidhamiria kumshambulia Black Fog shingoni kupitia nyuma, lakini ile anamsogelea karibu Black Fog aligeuka na teke katika angle ya 180 na kufyatua kile kisu chake pembeni.


Yule muuaji alionekana kushangaa kwani hakutegemea Black Fog angekuwa na uwezo wa kufanya shambulizi la namna hiyo.


Wasichokijua ni kwamba Black Fog alikuwa ni uzao wa Asmuntis muuaji mkubwa duniani. Black Fog licha ya kuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi lakini vilevile alikuwa na mafunzo ya juu sana ya Aikido.


Kwa lugha nyepesi, Black Fog alikuwa na mafunzo ya Aikido, Nishati za Mbingu na Ardhi, na pia ya uninja, muunganiko wa kujilinda na kushambulia ambao amejifunza tangu akiwa mdogo.


Mwanaume yule muuaji alitaka kutumia mwanya kuingia bafuni na kumshambulia Hamza, lakini kilichomtokea ni kwamba kisigino cha kiatu cha high heels kilitoboa ubongo wake. Shambulizi hilo lilikuwa na ustadi wa hali ya juu sana kwani Black Fog hata hakugeuka; kwa namna umbo lake lilivyo na wepesi wa miguu yake, ilikuwa vigumu kuamini kuwa alifanikiwa kufanya shambulizi la aina hiyo.


Wakati huo huo, alitumia mkono wake kudaka kisu alichokifyatua kwenda hewani na kukitumia kumchoma yule mwanamke kwenye paji la uso, na hivyo ikawa mwisho wake. "Kwa uwezo mdogo namna hii, mnataka kushindana na mimi? Mmejitoa kafara wenyewe," aliongea huku akimwachia yule mwanamke adondoke chini akiwa hana uhai.


Hamza aliishia kumwangalia mwanamke huyo bila kuonyesha hisia zozote; Rhoda hakuwa Rhoda aliyemzoea. Alikuwa na hali ya ukatili wa juu sana, na hata baada ya kutekeleza mauaji hayo hakuonekana kushikwa na hatia hata kidogo.


Baada ya kukamilisha kuua, alienda kwenye mlango wa kutokea, akaweka kibao cha Cleaning Up, kisha akarudi ndani na kwa haraka sana aliwabeba wale maiti wote na kuwaingiza kwenye choo cha wanaume, akiweka vichwa vyao kwenye sinki ili damu isidondoke chini. Baada ya kuwaingiza, alisafisha damu iliyokuwa chini kwa kutumia dekio kwa haraka sana na kuondoa viashiria vyote vya damu. Eneo hilo likawa kama hakuna kilichotokea.


Baada ya pale, alivuta uzi mwembamba kutoka kwenye gauni lake, kisha kwa mbinu ya kipekee sana, aliuloki ule mlango kwa ndani kiasi kwamba ukijaribu kufungua kutoka nje haukufunguka. Mpaka hapo, ilikuwa vigumu mtu kujua kuwa ndani ya choo hicho kulikuwa na maiti zimesukumwa kwenye sinki.


Hamza upande wake hakuwa akiangalia tu; alikuwa akihesabu muda na aligundua kuwa kila kitu kilikamilika ndani ya dakika mbili—kuanzia kuua, kusafisha, hadi kufunga mlango. Aliishia kutikisa kichwa chake kwa kuridhika.


"Ah! Naona mchafu hakupoteza muda wake kukufundisha. Umefanya kazi nzuri," aliongea Hamza huku akicheka.


"Bro, mimi ni ninja namba tisa duniani, siwezi kuwa dhaifu," aliongea Rhoda.


"Haha. Nisamehe kwa kusahau kuwa mdogo wangu Rhoda ni damu changa kwenye ulimwengu wa wauaji."


"Napenda unavyoniita kwa jina langu la kawaida. Niite hivyo kuanzia sasa," aliongea Rhoda, akimfanya Hamza kumwangalia jinsi alivyobadilika kutoka kwenye ukatili hadi kuwa msichana wa kawaida kabisa.


"Sawa sawa, ni muda wa kurudi sasa," aliongea Hamza, na Rhoda alitabasamu, akajiweka vizuri, na kufungua mlango. Wakaanza kurudi kwenye ukumbi.


Walipokuwa wakitoka, alikuwapo mfanyakazi wa usafi aliyekuwa akielekea upande wa maliwatoni ,mbele yao akiwa anasukuma kitoroli, akionekana kama mtu wa kawaida sana. Lakini kwa Hamza, mtu huyo alikuwa tofauti. Alikuwa na mafunzo ya juu ya Nishati za Mbingu na Ardhi, hata kuliko Black Fog. Namna Hamza alivyogundua hili ni kutokana na utashi wake unaotokana na uzoefu. Upande wa Black Fog, kutokana na kuua watu wawili, alikuwa ameshusha uwezo wake wa kunasa hatari, hivyo hakuweza kugundua hali hiyo.


Hamza palepale aligundua jambo: mwanzoni hata yeye alishangaa kwa nini wale wauaji waliotumwa walikuwa dhaifu sana kumbe walikuwa kama chambo tu. Muuaji halisi alikuwa huyo aliyekuwa akijifanya mfanya usafi. Yote hii ilikuwa ni mbinu ya kumpumbaza Black Fog ili umakini wake upungue.


Hamza baada ya kuona jambo hilo, hakuona haja ya kumwambia Black Fog. Alijiambia hilo ni suala ambalo atadili nalo yeye mwenyewe, hivyo kumzubaisha pia yule muuaji. Hamza aliendelea kuongea kawaida na Rhoda kwa kucheka na ile wanapishana na yule mtu wa usafi. Palepale yule mwanaume alilipukwa na nishati za mbingu na ardhi wa levo ya nafsi na kwa haraka sana alitoa silaha yenye mchanga tatu mfano wa chusa kwenye kile kitorori. Matendo yake yalikuwa ya haraka sana kulinganisha na spidi aliokuwa nayo Black Fog.


Hamza aliishia kupumua huku akijiambia inaonekana Black Fog haikuwa ameiva sana. Kuwa mdogo na kukosa uzoefu ilimfanya iwe rahisi kudanganyika. Mawazo hayo ya Hamza yalikuwa ndani ya sekunde tu, lakini sasa ile anataka kufanya shambulizi alihisi kivuli cheusi kikimpita mbele ya macho yake.


“Black Fog!!”


Hamza alijikuta macho yakimtoka palepale, na ile ni baada ya yule muuaji alivyotaka kumshambulia, Black Fog alikuwa ashapotea upande wake wa kulia na kuhamia upande wa yule muuaji alipokuwepo.


Spidi ya mwanamke huyo ilikuwa kubwa kiasi kwamba Hamza alishindwa kumuona vizuri. Kitu pekee alichoweza kuona ni kama kulikuwa na ukungu mweusi uliokuwa umemzingira Rhoda na kuonekana kama vile amegeuka na kuwa radi nyeusi.


Bam!


Muuaji yule hakuwa hata na muda wa kushitukia shambulizi hilo kwani alishambuliwa eneo la kifuani na kumfanya arushwe mbali huku akiwa ni kama amepigwa na shoti ya umeme. Hakukuhitajika shambulizi la pili kwani torori lile lilimmaliza palepale baada ya kujigonga nalo vibaya na kumfanya avunjike mbavu kadhaa.


Arggg! Mwanaume yule aliishia kutoa mguno wa maumivu makali huku akitema damu nyingi chini, alikuwa kwenye mshangao akishindwa kuamini kile kilichotokea. Kwa spidi ambayo Black Fog alitumia ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba imevuka ile ya ubinadamu wa kawaida wa mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi.


“Rhoda, wewe!” Hamza pia alikuwa katika mshangao wa spidi aliokuwa nayo Black Fog.


Ngumi hiyo aliopigwa nayo muuaji huyo, Hamza alijiambia kama ni yeye mwenyewe asingeweza kuikinga, ijapokuwa isingemuumiza kutokana na nguvu yake ya mwili lakini itoshe kusema kwa mtu wa levo yake kuweza hata kumshambulia tu inamaanisha uwezo wako ni mkubwa sana.


Muuaji yule wakati akijaribu kuvuta pumzi ili kusimama, Black Fog palepale alichomoa nyota kutoka kwenye gauni lake na kisha aliunganisha na nishati ya mbingu na ardhi na kuirusha na moja kwa moja kuzama katika shingo ya yule muuaji na kufa palepale.


Muda huo Hamza aliweza kuhisi kulikuwa na tatizo katika mwili wa Black Fog na kumshikilia.


“Rhoda uko sawa?” Aliuliza kwa wasiwasi baadaya kumuona akilegea.


“Nipo sawa Bro, ngoja niuchukue huu mwili nikaufiche stoo.” Aliongea lakini Hamza alishika mkono wake kupima msukumo wa damu na aligundua ulikuwa chini mno.


“Bado tu unasema upo sawa, unaonekana kutumia nguvu nyingi sana kufanya hili shambulizi. Mwili wako umekosa uhimili wa kuidhibiti spidi yako ni kwa bahati tu meridiani zako hazijaharibika,” Aliongea Hamza.


“Bro, umegundua!” Aliuliza Black Fog kwa mshangao.


“Hata kama sina mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, utaalamu wangu wa tiba ni mkubwa mno wa kuweza kuona una shida,” Aliongea Hamza.


Hamza alielewa anachomaanisha, lakini hata hivyo hakuweza kuua kama mrembo huyo alikuwa na uwezo wa kuzuia shambulizi lile. Lakini kwa namna moja alifurahia kuona kitu ambacho hakuwa akikifahamu kuhusu Black Fog na alijiambia lazima kuna mambo hakuwa akiyajua tokea mwanzo kuhusu mwanamke huyo.


Hamza alimpa ishara Rhoda ya kutofanya chochote na kwa haraka haraka aliuchukua ule mwili na kuuburuza mpaka kwenye chumba cha stoo na kuuficha na mashuka. Baada ya kumaliza alisafisha haraka haraka na kisha alimchukua Black Fog mpaka kwenye floor ya pili ya jengo hilo la hoteli kwenye balconi.


“Rhoda hebu niambie, umewezaje kufanikisha ile spidi. Kama sikosei Asmuntis hana aina hii ya mafunzo, si ndio?” Aliuliza Hamza.


“Bro tafadhali usije kumwambia Master kuhusu hili.”


“Kwanini?”


“Kwasababu Master kanikataza kutumia mbinu ya Hundred Shadows. Kama akigundua ataniadhibu vikali.”


“Hundred Shadows! Unamaanisha hii mbinu ndio inaitwa hivyo?”


“Ni Master ndio aliniambia inaitwa hivyo, ila hata mimi mwenyewe sijui...” Palepale Rhoda alianza kumwelezea Hamza kila kitu kwa kurahisisha.


Kwa maelezo ya Rhoda ni kwamba ni Asmuntis ambaye alimlazimisha kujifunza mbinu hiyo ya Hundred Shadows na kutokana na kumhimiza na kukosa uvumilivu ilimpelekea Rhoda kufikia levo ya juu.


Wakati wakiwa katika mazoezi kama sehemu ya mafunzo Rhoda alijihisi ni kama vile mwili wake umetawaliwa na umeme na kufanya spidi yake kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana kiasi cha hata yeye kutotambua na kutokana na hilo alimshambulia Asmuntis kutaka kumdhuru.


Ikumbukwe Rhoda bado ni mdogo sana wa umri wa miaka kumi na nane tu wakati huo na mafunzo yake ya nishati za mbingu na ardhi hayakuwa yamefikia katika daraja la ukaidi wa asili na kuzaliwa kwa mwili mpya. Hivyo licha ya kwamba shambulizi lake lilimfikia Asmuntis lakini hakuweza kumdhuru kutokana na kwamba Asmuntis alikuwa na mafunzo ya juu ya nishati za mbingu na ardhi kumzidi.


Lakini sasa baada ya shambulizi hilo moja, matokeo yake ni kwamba mishipa ya damu ndani ya mwili wa Rhoda ilipasuka na kumfanya kuvuja damu nyingi jambo ambalo lilimchukua zaidi ya miezi minne mpaka kuja kupona, tena kwa maumivu makali.


Kutokana na hilo, tokea siku hiyo, Asmuntis hakumtaka Rhoda kutumia mbinu hiyo kabisa kwa kuamini ilikuwa na madhara makubwa katika mwili wake.


Maelezo ambayo yamekosekana ni kwamba licha ya Asmuntis kumfundisha mbinu hiyo, lakini uwezo ambao Rhoda aliupata ulikuwa ni wa ajabu ambao haukuweza kuelezeka kama ni kitu alichopata kutoka nje au ni kipaji kilichokuwa ndani ya mwili wake na kiliamka baada ya mafunzo hayo.


Hivyo kwa sababu hakukuwa na maelezo ya kutosha kutokana na uwezo waliokuwa nao Rhoda njia rahisi ilikuwa ni kutokutumia mbinu hiyo tena.


“Master pia kasema pengine ni kutokana na mwili wangu hauwezi kuhimili mbinu ya Hundred Shadows na labda nitaweza kuitumia baada ya kufika levo ya ukamilifu wa mwili, lakini sijui itanichukua muda gani mpaka kufikia daraja hilo la mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi. Naamini siku ambayo mwili wangu utaweza kuhimili mbinu ya Hundred Shadows nitakuwa nimemzidi Master ki uwezo.”


“Sio tu kumzidi itakuwa ni kumuacha mbali kabisa, ile ngumi yako haikuwa ya kawaida hata kwangu inaweza kuwa ngumu kuhimili,” Aliongea Hamza.


“Bro si kwasababu huna mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, ni sahihi tu kutoshindwa kuihimili,” Aliongea na kumfanya Hamza kukosa neno na kushikwa na haya.


“Anyway, ninachoweza kusema mbinu yako ni hatari mno. Kwa sasa pumzika haina haja ya kujilazimisha kunilinda,” Aliongea Hamza.


Rhoda ingawa hakutaka kumuacha Hamza mwenyewe bila ya ulinzi , lakini hakuwa na nguvu za kumlinda, ndio maana aliishia kutingisha kichwa chake tu kukubaliana nae.


“Basi kaka naomba usimwambie Master kama nimepata majeraha”Aliongea Black Fog akionekana kumhofia master wake.


“Usiwe na wasiwasi hata kama akitaka kukupa adhabu nitakulinda mwenyewe”


“Ni kweli ! Sasa hivi nina kaka wa kunilinda”Aliongea huku akitabasamu kinyonge na kisha alimsogelea Hamza na kumkumbatia na hakuishia kumkumbatia tu, alimkisi shavuni.


Hamza alijikuta akishitushwa na busu hilo na ile anataka kuongea Black Fog alimuwekea kidole mdomoni.


“Usiwazie sana , hii ni kama ishaRa ya mdogo wako kuongeza ukaribu na kaka yake”Aliongea mrembo huyo na kisha alimkonyeza Hamza na kushuka ngazi kuelekea chini.


Hamza aliishia kutoa tabasamu huku akitingisha kichwa chake. Mawazo yake muda huo alijiambia ili kumsaidia Black Fog, ngoja kwanza baraza la ugawaji wa maksi lipite na kisha atamwelekeza mbinu yake mpya ya mafunzo ya kuamsha nishati ya mwili.


Alikuwa na uhakika kama angejifunza mbinu hio ingekuwa rahisi kwake kuhimili nguvu ya hundred shadows.


Ukweli Hamza alikuwa na shauku pia ya kutaka kujua ni asili gani ya kimwili imemuwezesha Rhoda kuamsha uwezo mkubwa wa aina hio. Ikumbukwe mafunzo yote yawe ni ya nishati za mbingu na ardhi au yale ya kuamsha nguvu za asili ya mwili yote lengo lake ni kugundua siri za kimwili ziliozojificha. Hakuna nguvu yoyote ambayo inamwingia bindamu kutoka nje bali nguvu hio imejificha ndani ya miili yetu na ni kukosa tu namna ya kuweza kuiamsha.


Kama ilivyo kwa Nyakasura , uwezo wake ulitokana na damu yake ya kifoeniksi , maana yake ni kwamba mafunzo anayofanya sio kwa ajili ya kujiongezea nguvu bali ni kwa ajili ya kuelewa uwezo wake.Hivyo hivyo hata kwa Rhoda alipaswa kupata mafunzo ya kuelewa uwezo wake , kila mtu huzaliwa na uwezo wake wa kipekee na ni ngumu kuigwa na mwingine hivyo lengo la Hamza ilikuwa ni kutaka kumfanya mwanamke huyo kuelewa maana halisi ya uwezo wake ni ipi na vipi ataweza kujithibiti.


Hamza alijifikiria kwa muda na palepale aliona ni muda sasa wa kurudi ukumbini kwa ajili ya kumtafuta Regina , aliondoka muda na hakuwa akijua Regina alikuwa akiendeleaje katika maongezi yake na matajiri hao wa kizungu.
 
Prince of hell(Lucifer.)


Hamza alishangaa kumuona mke wake akiwa amesimama na wafanyabiashara mashuhuri waliovalia suti zilizowapendeza, akiongea nao. Hamisa na Zuberi pia walikuwa pamoja na Regina. Kundi hilo la watu lilikuwa limegubikwa na tabasamu, lakini kama ungesikiliza kwa ukaribu, ungejua kinachoendelea hapo ni kama kuna mdahalo uliokuwa ukiendelea.


“Samahani sana Miss Regina, nilishakaa chini na kufanya maongezi na kampuni ya Kilimanjaro Group kwa ajili ya ubia wa kibiashara. Kampuni yetu ina mkataba mmoja tu wa kusaini, hivyo hatutoweza kushirikiana,” aliongea mwanaume mtanashati mwenye ndevu nyingi.


“Mister Kaird bado hujaona mpango wetu katika ushirikiano huu lakini bado unatukataa mapema hivi. Huoni kwamba ni kushindwa kuwajibika vyema kama kiongozi wa kampuni na kwa wafanyakazi wenzako?” Aliongea Regina akiwa na hali ya ukauzu machoni mwake, hakutegemea watu hao wangeweka umakini wao wote kwa Zuberi na Hamisa kutokana na kufahamiana tu.


“Miss Regina, nimekuwa katika biashara ya burudani kwa muda mrefu sana, na sio mimi tu, baba na babu pia walikuwa katika biashara hii kwa zaidi ya miaka sitini. Kama kampuni, tunajua biashara hii inavyoenda, hivyo mipango yote ni ileile tu hakuna jipya. Sioni kuna ulazima wa kuangalia mpango wako kwani hautokuwa na tofauti kubwa na wa hawa,” aliongea Karid.


“Kwangu mimi naona maneno yako yamekosa uwajibikaji kwa kujifungia katika njia moja. Kwanini mnataka kufanya kazi na kampuni changa kutoka nchi zinazoendelea? Kwa sababu mnataka kuondoa mtuwamo na kufanya soko la Ulaya kupanuka zaidi. Kama ukichagua kampuni ya Kilimanjaro kwa sababu ya kupigiwa debe na Kampuni ya Multimedia, naona hakuna tofauti na kucheza kamari, njia ambayo inakosa ubunifu na kuogopa kuanzisha vitu vipya.”


“Regina hebu punguza ujuaji, unasemaje mpango wetu sio mzuri kuliko wa kwako? Unahisi timu yetu iliyokaa chini na kutengeneza huu mpango haina ubora kama ilivyo kwa kwa timu ndani ya kampuni yako?” Aliongea Zuberi akiwa na ukauzu usoni.“Mr. Karid anajua sana hii biashara kuliko wewe na amekupa muda wa kuongea kwa sababu ya kukuonyeshea heshima”


“Ni kweli, kwa muonekano wako Regina ni kama vile hutaki kushindwa, ndio maana unaongea vitu ambavyo havina msingi hapa. Kila mtu ana njia zake za kibiashara, kwanini unalazimisha?” Aliongea Hamisa.


“Sina muda wa kupoteza kuongea na nyie, nataka kumuuliza Mr. Kaird swali moja tu. Mr. Kairid, una uhakika hutojutia kuangalia mpango wa kampuni yangu?” Aliuliza Regina, akimfanya Mr. Kaird kutoa kicheko cha kujivunia.


“Miss Regina, nadhani nishaweka kila kitu wazi, najua ni mshirika yupi ambaye kampuni yetu inamuhitaji.”


“Okay.”


Regina, mara baada ya kupewa jibu hilo, alimgeukia mwanaume mwingine wa kizungu wa makamo, ambaye alikuwa amevalia suti yenye maua-maua huku nywele zake nyeusi akiwa amezichana kwa kuzirudisha nyuma.


“Mr. Brewer, is your company also thinking the same way as Kaird?”Aliuliza Regina akimaanisha kwamba je bwana huyo anafikiria sawa kama ilivyo kwa Kaird.


“Mr. Brewer, tumekutana jana na tumeongea kwa furaha kubwa juu ya makubaliano ya kibiashara tunayokwenda kuafikia. Ndani ya miaka mitano ijayo, asilimia kubwa ya brand kubwa tutakuwa sehemu ya wawekezaji,” aliongea Zuberi akiingilia kwa namna ya kumkumbushia.


“Mr. Zuberi, ni kweli jana tulikuwa na mazungumzo mazuri, lakini bado sijafikia maamuzi.” Mara baada ya kuongea hivyo, Regina macho yake yalichanua.


“Mr. Brewer, kama haujafikia katika maamuzi, inamaanisha kwamba pendekezo lao halijajitosheleza kwa asilimia mia moja. Naomba kama una nafasi, tupate muda wa kukaa chini na kuongea juu ya mpango wa kampuni yangu katika siku moja au mbili zijazo,” aliongea Regina na kumfanya Brewer kuonyesha kusita kidogo.


“Miss Regina, tuachane na hayo kwanza, kwa sasa nataka kukuuliza swali moja.”


“Unaweza kuuliza, Mr. Brewer.”


“Mtaji wenu wa uwekezaji unaweza usiwe mkubwa sana au mdogo kuzidi wa kampuni ya Kilimanjaro, huna msingi wa kibiashara hapa nchini na pia hauna rasilimali za moja kwa moja za kutumia. Nini kinakufanya kujiamini kwamba tukikaa chini na kuongea nitachagua kampuni yako na kuwaacha Kilimanjaro? Kukurahisishia, jaribu kuelezea kwa ufupi faida zitakazopatikana katika kampuni yako kuzidi Kilimanjaro Group. Ukiugusa moyo wangu, nipo tayari kukubali miadi na wewe na kukaa chini kwa ajili ya mazungumzo.”


Regina mara baada ya kuulizwa vile alijikuta akikaa kwa muda akionekana kufikiria.


Upande wa Zuberi aliona Regina alikuwa amekosa jibu na kumfanya aanze kucheka.


“Mr. Brewer, swali lako linaonekana kuwa gumu sana kwa Bosi Regina. Ni dhahiri kabisa hakuna faida kubwa utakayopata kuzidi kampuni yetu.”


Hamza, hata yeye swali lile lilimfanya kutaka kujua Regina atalijibu vipi. Kama Regina hakutaka msaada wake wala kutegemea koneksheni yake, alitaka kujua ni kipi kinachomfanya kutaka kujiamini.


Regina muda ule alionekana kumaliza kufikiria na kufanya kuinua mikono yake na kuiweka kifuani.


“Ukifanya na sisi biashara, utakuwa na faida nyingi…” aliongea na kufanya watu wote waliokuwa wakisikiliza kukaa kimya. Zuberi na mpenzi wake Hamisa walionyesha kejeli, wakiamini chochote atakachojibu hakiwezi kumridhisha Brewer. Kaird naye alionekana kutaka kusikia jibu la Regina.


“Kwanini?” aliuliza Brewer.


“Naamini wote mnajua maendeleo ya kampuni yetu ni makubwa sana katika kipindi cha miaka michache iliyopita na pia kuna utofauti mkubwa kati yangu na wao,” aliongea Regina na kisha alimnyooshea mkono Zuberi.


“Mr. Zuberi ni loser. Miaka iliyopita baada ya kushindwa alilikimbia soko la Ulaya na sasa amerudi kwa njia ya kuomba msaada, maana yake hakuwa na uwezo wa kusimama yeye mwenyewe kama yeye baada ya kupata changamoto. Mimi Regina ni wa tofauti. Nimekuwa na ushindi mkubwa katika kuanzisha biashara katika maeneo mageni kwangu na sijawahi kutegemea koneksheni kutoka kwa yoyote. Ninachotafuta ni mtu wa kufanikiwa naye na sio wa kunisaidia nifanikiwe. Pengine watu wangehofia kushirikiana na mimi kwa kuona mafanikio yangu yatachukua muda, lakini kufanikiwa ni lazima. Kwenye makampuni makubwa, kiongozi hahitajiki kujua maswala yote ya kiufundi, hana haja ya kujua namna ya kuuza bidhaa. Anachotakiwa kujua ni namna ya kuwa mshindi na sio kukimbia pale changamoto zinapojitokeza. Biashara ni kama mchezo, ukijitoa maana yake umeshindwa na maksi anapewa nyingine. Hivyo kwa ninavyoona hapa Zuberi ni yuleyule alieshindwa miaka iliopita na kama akipata changamoto kuna asilimia kubwa atakimbia”


Zuberi mara baada ya kusikia hivyo, sura yake ilijikunja na aliishia kunyonga tai yake kwa hasira.


“Regina, hebu acha kuongea ujinga, sikukimbia. Kampuni yetu ya Kilimanjaro itaendelea na ubia wa kibiashara hapa nchini na faida itaonekana.” Licha ya Zuberi kuongea hivyo, Regina alimpotezea kabisa.


“Mr. Brewer, je nimekupa sababu ya kueleweka?” aliuliza Regina na palepale Brewer alianza kucheka na kisha akanyoosha mkono kumpatia Regina.


“Miss Regina, inaonekana utu wako wa ndani unavutia zaidi ya muonekano wako wa nje. Msaidizi wangu atawasiliana na wewe kwa ajili ya kupanga muda wa kukutana,” aliongea, na kauli yake ilimfanya midomo ya Regina kucheza wakati huo wakiwa wameshikana mkono na Brewer.


Zuberi muda huo alikuwa akisaga meno yake kwa hasira, lakini kwa sababu Brewer amekwisha kusema, ingekuwa ukorofi kujaribu kuingilia maamuzi yake, hivyo aliishia kukaa kimya.


Muda huo, Kaird alionekana macho yake kushangaa baada ya kuona mtu ambaye alikuwa akimfahamu akikaribia eneo walipo.


“Mr. Leibson, sijatarajia kama ungekuja kwenye hii sherehe. Ah!, naona umeongozana na binti yako mrembo, Miss Barbara,” aliongea Kaird kwa uchangamfu.


Mwanaume ambaye alisogea katika eneo lao alikuwa ni wa makamo aliyevalia miwani ya rangi ya brown. Alionekana kuwa kati ya miaka arobaini hivi, mrefu mwenye mwili ulioshiba akiwa amevalia suti yenye michirizi ya rangi nyeupe.


Mikono ya mwanaume huyo ilikuwa imejaa vito vya thamani kuanzia saa alovalia, cheni ya mkono na pete. Shingoni pia alikuwa na mkufu wa almasi uliokuwa ukimeta meta. Kila mtu aliyemuona mwanaume huyo akiingia alimwangalia kwa husudu. Watu wengi walitamani kumsogelea lakini walikuwa na hofu, hivyo waliishia kusita.


Pembeni ya mwanaume huyo alikuwa ni msichana mdogo mwenye nywele za kiblonde. Alikuwa mrembo mwenye umri makadirio ya miaka ishirini hivi. Alikuwa amevaa gauni la mkato wa chini rangi ya njano huku shingoni akiwa na mkufu uliokuwa ukimeta meta.


Licha ya bwana huyo kusikia sauti ya Kaird ikimwongelesha, hakujisumbua hata kujibu zaidi ya kuguna tu.


Ni Barbara ambaye alitoa tabasamu na kumpa salamu.


“Hello, wewe ni Kaird?” aliuliza mrembo huyo, Barbara.


“Ndio, ndio, ni heshima kwangu, Miss Barbara, unanifahamu.”


Muda huo Zuberi alimwangalia Hamisa kwa shauku, akionekana hakuwa akiwafahamu huyo mzungu na binti yake.


“Huyo Leibson ni nani?”


“Inamaana humjui Mr. Leibsoni, hujawahi kuisikia Innova Chemicals?”


“Unamaanisha huyo ni tajiri Joris Leibson! Anayehusishwa kumiliki kampuni ya kutengeneza silaha ya Thunder?” Zuberi alionekana kushangaa, na Brewer aliweza kusikia mazungumzo yao.


“Sio kuhusishwa—ndiye mmiliki mkuu wa kampuni ya Thunder. Kwa nje, ni bosi wa kampuni kubwa ya kemikali ya Innova, lakini anaingia kwenye tatu bora ya wauza silaha wakubwa ulimwenguni. Katika moja ya kauli zake za hivi karibuni, aliongea hakuna silaha ambayo anakosa kwenye ghala zake. Yule Barbara ni binti yake na anasafiri naye popote. Ukimkosea Barbara, umemkosea yeye pia na kinyume chake,” aliongea Brewer.


Kwa sifa hizo, ilikuwa ngumu kumsogelea Leibsoni. Kufanya biashara ya silaha si jambo rahisi linaloweza kufanywa na kila mtu. Nchi kubwa haziwezi kukuona unanunua na kutengeneza silaha na kusafirisha utakavyo.


Kampuni ndogo kama Dosam, Kilimanjaro, na Multimedia, bajeti yao ya mwaka inaweza kuwa ni jaribio moja au mawili ya kombora.


Muda huo, baada ya matajiri kumuona Leibson, wengi walimsogelea na kuanza kuongea naye huku wakiwekeza nguvu zao kumfurahisha Barbara.


Regina alijikuta akiwa katika hali ya kushangaa jinsi watu walivyokuwa wakimshobokea tajiri huyo.


“Kwanini wanamchangamkia namna ile, biashara zao zinahitaji koneksheni ya mtu kama yeye?” alizungumza Regina huku akimgeukia Brewer.


“Mr. Brewer, naona hata wewe unatamani kwenda kusalimiana naye,” aliongea Regina, na kumfanya Brewer kutingisha mabega huku akicheka kidogo.


“Miss Regina, uzoefu wako katika hii biashara ni mdogo sana. Wafanyabiashara wa silaha hawauzi silaha tu. Ndio watu wanaogusa uchumi wa dunia moja kwa moja, kwa sababu wao ndio wachochezi wakubwa wa vita. Bila vita, biashara zao haziendi vizuri, na bila silaha vita haiwezi kutokea. Unaowaona hapa, asilimia kubwa ni matajiri ambao biashara zao zimesambaa dunia nzima. Sehemu waliowekeza ikitokea vita, maana yake watapata hasara kubwa sana, lakini vilevile inaweza pia kuwa fursa kwao. Mtu kama Leibson anaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa dunia kwa njia zake. Katika orodha ya namba za simu utakuta ni mawaziri wakuu, marais na hata wakuu wa jeshi wa nchi nyingi. Biashara ya kutengeneza silaha na kununua inahitaji mtaji mkubwa sana. Maana yake ni kwamba, ukiachana na uwekezaji wake, kuna hela za serikali pia anazozozungusha,” alizungumza Brewer kwa kirefu.


“Kumbe ipo hivyo... ila kwanini na wewe usiende kusalimiana naye? Wewe ni moja ya matajiri pia hapa nchini, si ndio?”


“Ni kweli naweza kwenda kusalimiana naye, lakini hebu angalia watu wote hao. Mpaka kujiminya na kwenda kutoa salamu nitatumia nguvu kubwa na inaweza kunitokea ya Kaird, kuishia kupotezewa. Labda niwe na umiliki wa asilimia hamsini wa soko la Ulaya ndio mtu kama yeye anaweza kuniangalia,” aliongea Brewer.


Wakati huo, Leibson aliyekuwa amemshikilia Barbara mkono alianza kupiga hatua kusogelea upande wao. Kitendo kile kilimfanya Brewer kuwa na wasiwasi na haraka sana akaweka kola yake ya shati vizuri.


Watu wote walikuwa wakimwangalia Leibson anakosogelea. Ukweli ni kwamba watu wengi walishangazwa na ujio wake kwani hadhi yake ilivyo, ni ngumu mtu kama huyo kuja katika sherehe kama hiyo, hivyo maswali yalikuwa mengi.


“Haha... Mr. Leibson ni heshima kwangu…” Brewer alikuwa na uhakika Leibson alikuwa akija kusalimiana naye, ndiyo maana alijichangamsha kwa kunyoosha mkono kwa ajili ya kusalimiana naye, lakini badala ya kupokea mkono ule, alienda moja kwa moja kusimama mbele ya Regina na midomo yake ilionekana kucheza kama mtu aliyekuwa akizuia tabasamu.


“This should be Miss Regina. It's my pleasure to meet you in Paris. I'm Leibson, and the one over here is my daughter, Barbara." Alijitambulisha kwamba yeye ni Leibsoni na aliyeambatana naye ni binti yake Barbara, na ana furaha kukutana na Regina.


Ukweli ni kwamba kulikuwa na watu weusi wachache sana ndani ya sherehe hiyo. Asilimia kubwa ya weusi walioonekana walikuwa ni wahudumu.


Tukio la Leibsoni kumsogelea mwanamke mrembo wa Kiafrika ambaye hakuwa akijulikana kwa watu wengi lilishangaza wengi na kufanya eneo lote kutulia na kuacha sauti ya band ya violini kusikika pekee.


Kaird na matajiri wengine walihisi ni kama macho yao yalikuwa yakiwadanganya. Waliishia kupepesa macho huku nyuso zao zikiwa katika hali ya maswali.


Kuhusu Zuberi na Hamisa haikuwa na haja ya kuelezea sana, maana mwonekano wao ni kama watu walionyweshwa pombe ya kienyeji.


Brewer hakuwa hata na muda wa kujisikia vibaya kupotezewa. Maana alikuwa katika mshituko mkubwa.


Tajiri na bintiye waliokuwa wakipokea salamu za watu kivivu ndani ya eneo hilo, kumsogelea mtu na kuanzisha maongezi wao tena kwa mwanamke wa ngozi nyeusi kutoka nchi isiyoifahamika sana, tena kwa kuongea kwa upole, ni suala lisilo la kawaida.


Ukweli ni kwamba si tu kwa watu hao ambao hawakuelewa kile kinachoendelea, bali kwa Regina pia hakuwa akijua nini kinaendelea. Aliishia kushikana mkono na Leibsoni akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa.


"Mr. Leibson, seems to be meeting for the first time. Do you know me?” aliongea Regina baada ya kujituliza akiuliza kama ni mara yao ya kwanza kukutana na kama anamfahamu.


“Ni kweli ni mara yetu ya kwanza kukutana, lakini nafahamiana na bwana karibu yako kwa muda mrefu sana. Miss Regina, inawezekana kukukaribisha wewe na mwenza wako kwenye balkoni kwa ajili ya maongezi?” Aliongea Leibson huku akimwangalia Hamza kwa macho ya ishara fulani hivi.


Hatimaye Regina aliweza kuamka katika ndoto na kumgeukia Hamza aliyekuwa kimya muda wote nyuma yake na kuona alikuwa akiangaliana na Leibson kwa tabasamu hafifu.


Mwonekano wa Hamza ulikuwa ni kama vile ujio wa Leibson hapo si swala kubwa sana kwake.


Ukweli ni kwamba Leibsoni, mtu aliyemtaka kusalimiana naye ni Hamza. Lakini kwa mtu mjanja kama Leibson hakutaka kuonyesha nia yake wazi. Kama angemsalimia Hamza moja kwa moja ingezua maswali mengi kutokana na kwamba tokea mwanzo hakuna mtu yoyote aliyeonekana kumjali Hamza. Hivyo njia ya kuficha nia yake ilikuwa ni kumsalimia Regina kwanza.


Regina alikuwa katika hali ya mshituko. Alikuwa akizidiwa na shauku zaidi na zaidi juu ya mume wake. Kwanini huyu mwanaume anafahamiana na muuza silaha? Ndio swali ambalo liliibuka katika kichwa chake. Lakini hata hivyo, uwezo wa Regina wa akili ni mzuri sana hivyo aliijua nia ya Leibson mara moja.


"Bila shaka tunaweza kuongozana," aliongea Regina.


Wakati watu wakiendelea kuwa katika hali ya mshangao, Regina, Hamza, Leibson na binti yake walitembea kwenye ngazi kuelekea floor ya pili kwenye balkoni. Kulikuwa pia na watu kadhaa waliokuwa wakijua kinachoendelea kama vile mtoto wa Mzee Pino yaani Henry Pinault, ambaye muda wote alikuwa akiwaangalia bila ya kuongea neno.


Asilimia kubwa ya watu ambao walikuwa wakimfahamu Hamza hawakumsogelea Regina kwa sababu Hamza ametangaza asitokee mtu wa kumsaidia Regina kupitia koneksheni.


Sasa baada ya Leibson kusogea ni kama wote walipata sababu ya kuwasogelea kwa mara nyingine, hivyo walijipanga kwenye ngazi wakisubiria washuke ili wasalimiane nao.


"Prince of Hell! Nimesikia sifa zako nyingi Lucifer. Naitwa Leibson, rafiki wa rafiki yako kutoka ulimwengu wa siri. Huyu ni binti yangu Barbara. Barbara onyesha heshima zako kwa mrithi wa utawala wa kuzimu," aliongea Leibson.


Barbara ambaye muda wote alikuwa na tabasamu la kuvutia, aliweka usiriasi na kisha alishikilia gauni lake kwa kulipandisha juu na kusinyaa kidogo kuonyesha heshima.


"Sir Lucifer! Nimezisikia habari zako nyingi," aliongea Barbara na kumfanya Hamza kuinua glasi yake ya champagne.


"You're welcome. I know you have a good relationship with Big Mamen. In this world, besides the enemy, you're also friends. So you can do as you wish." ("Karibu sana, najua una uhusiano mzuri na Big Mamen. Kwenye dunia hii mbali na kuwa maadui lakini vilevile ni marafiki, hivyo unaweza kufanya unavyotaka") aliongea Hamza, akimaanisha kwamba Leibson licha ya Big kuwa marafiki lakini pia ni maadui likija suala la biashara za silaha maana ni washindani.


Regina mapigo yake yalikuwa yakidunda kwa spidi mno. Ingawa uso wake ulionekana kuwa wa kawaida, lakini mara baada ya kusikia maneno ya Leibson alipatwa na mabadiliko ya ghafla. Kwenye kichwa chake maneno yaliyokuwa yakijirudia ni "Prince of Hell," "Lucifer!" Alijiuliza majina hayo yanamaanisha nini, au Hamza ndiye anavyoitwa nje ya nchi. Lakini bado alijiuliza kwa alichoelewa, "Lucifer" maana yake ni shetani na "hell" maana yake ni kuzimu. Je, majina hayo yalikuwa yakimaanisha nini mpaka kuitwa hivyo? Ilikuwa ngumu kufikia hitimisho kuamini Hamza alikuwa akiitwa Lucifer kama uwakilishi wa shetani.


Regina alikuwa katika hali ya kuhamaki huku akijiuliza inakuwaje taikuni wa biashara ya silaha kama huyo kumsalimia Hamza kwa namna ya upole, tena kwa namna ambavyo alikuwa akiongea ni kama vile hakuwa na ukaribu na Hamza na ndio mara yao ya kwanza kukutana.


Maswali mengi yaliibuka katika kichwa cha mrembo huyo na alihisi uchizi wa kutaka kujua Hamza ana cheo gani, kwanini kila siku anamshangaza tu.


Hamza pia alijua Regina baada ya hapo angejawa na maswali mengi sana, lakini kwa sababu ya Leibson aliona haitokuwa na haja ya kuendelea kumficha. Isitoshe wawili hao walikuwa ni wanandoa hivyo ni suala la muda tu kumwelezea Regina yeye ni nani haswa na sifa zake ni zipi.


"Wife nitakuelezea baadae..." aliongea Hamza akimwangalia Regina ambaye alikuwa na viashiria vya jasho kwenye paji la uso.


Regina aliishia kuminya lipsi zake tu, alihisi kukosewa kwenye moyo wake. Alikuwa na zaidi ya miezi minne tokea afahamiane na Hamza lakini bado tu hakuwa akimjua.


"Ijapokuwa nimefahamiana na Greed Mameni kwa kuchelewa lakini namkubali sana na yeye pia ananikubali na uhusiano wetu ni mzuri. Muda mwingine mtandao wake wa kibiashara unanisaidia sana kukamilisha dili zangu na vilevile nyanja zangu muda mwingine zinamsaidia na yeye. Niimesikia pia Mameni atashiriki katika Baraza la Maksi na pengine tutakutana tena," aliongea Leibson.


"Sire, ujio wangu leo umetokana na intelijensia yangu kunitaarifu wewe na mke wako Miss Regina mngeshiriki katika hafla hii, ndio maana nimekuja na binti yangu kwa ajili ya kutoa salamu zetu."


"Sir Lucifer nimesikia habari zako nyingi, simulizi yako juu ya vita takatifu ni moja ya sababu kubwa za mimi kutamani kukutana na wewe siku moja. Sikutarajia utakuwa mdogo hivi," aliongea Barbara.


"Kuhusu hayo kwangu sio kumbukumbu za kujivunia. Mimi sio mfanyabiashara wa silaha, kwangu mimi Vita ni uhai na kifo na sio fursa ya kibiashara. Nipo hapa leo usiku kwenye sherehe hii kama msindikizaji, mke wangu ndio muhusika mkuu hivyo sitaki kuchukua nafasi yake, tuongee kuhusu biashara," aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kumfanya Barbara kucheka kichini chini huku akimwangalia Regina.


"Miss Regina una bahati kubwa sana kuolewa na mtu maarufu kama yeye,Gwiji mtaalamu wa hadhi ya juu" aliongea Barbara, na Regina aliishia kulazimisha tabasamu pekee huku akiendelea kujiuliza, Mameni ni nani, Vita takatifu inahusu nini na umaarufu wa Hamza unatokana na nini?


Regina akili yake ilikuwa na maswali mengi na hakuwa na namna ya kuuliza, kitu pekee alichoweza kufanya ni kuwa mvumilivu.


"Your Excellency, naomba utuwie radhi, nadhani hatujawasumbua kwa usiku wenu wa leo. Kama ukipata muda tafadhali karibu nyumbani kwetu ili utupatie nafasi ya kukushukuru na kuonyesha ukarimu wetu," aliongea Leibson.


"Tutaongelea hayo baadae, ngoja kwanza tumalizane na maswala ya Baraza la maksi, maana kuna mambo mengi ya kushughulikia," aliongea Hamza akikataa ukaribisho wake kwa ukarimu. Hakutaka kujiweka karibu na wafanyabiashara wa silaha.


Wanne hao walikaa juu hapo kwenye balkoni wakiongea kwa dakika kadhaa na kisha walirudi chini. Upande wa Leibson na mwanae hawakurudi kabisa ukumbini kwani waliondoka moja kwa moja ikionyesha ujio wao ilikuwa ni kwa ajili ya kuonana na Hamza pekee.


Lakini sasa Regina ambaye alikuwa amebakia, alijikuta akiwa staa wa usiku huo kwa kuangaliwa na watu wengi.


Kila mtu alikuwa na swali, walishamjua Regina ni mfanyabiashara kutoka Afrika, lakini hawakujua ni kwanini Leibson akataka kuongea nae.


Hivyo matajiri mmoja baada ya mwingine walimsogelea wakijaribu kumdodosa kiaina. Tabia yao ilikuwa imebadilika mno dhidi ya Regina. Hata kama wengine walikuwa katika biashara tofauti kabisa na anazofanya Regina lakini walimsogelea na kutaka kujenga ukaribu.


Kutokana na hilo Regina alijikuta akiwa bize mno na hakuwa na muda wa kuongea na Brewer tena.


Upande wa Brewer alikuwa na wasiwasi mno na hakutaka bahati yake kumpotea, hivyo alijiminya katika kundi la watu mpaka kumfikia Regina.


"CEO Regina usisahau kushirikiana na sisi, kesho asubuhi na mapema nitakutumia barua pepe," aliongea Brewer.


Kabla ya hapo Brewer alipanga msaidizi wake ndio awasiliane na Regina, lakini baada ya tukio la Leibson aliona alishikilie hilo suala mwenyewe. Hakutaka kufanya kosa na kupoteza fursa adhimu kama hiyo ya kushirikiana na mtu anayefahamiana na taikuni Leibson. Kwanza alishukuru hakumuonyeshea Regina dharau kama ilivyokuwa kwa Kaird.


Upande mwingine Kaird uso ulikuwa umempauka. Alikuwa na hasira kiasi kwamba meno yake yalishindwa kuachana.


Upande wa Zuberi alikuwa katika hali ya mshangao mkubwa, hakujua inakuwaje Regina akafahamiana na muuza silaha ulimwenguni, tajiri Joris Leibson. Alijiambia, laiti ningejua nisingemdharau Regina tokea mwanzo.
 
“Mr. Kaird, usiwe na wasiwasi, hata kama Regina ana koneksheni kubwa, lakini nikuhakikishie tutafanya kazi nzuri tuki…”


Zuberi alitaka kumfariji Kaird lakini kabla ya kumaliza sentensi yake, Kaird aliingilia;


“Haina haja, Mr. Zuberi, hatuna mpango tena wa kufanya kazi pamoja. Makubaliano yetu tuliokubaliana mwanzo nayafuta kuanzia sasa,” aliongea Kaird huku aking’ata meno kwa hasira.


“Nini! Kwanini unaenda kinyume na maneno yako?” Wote Hamisa na Zuberi walijikuta sura zikiwafubaa na kushindwa hata kujua nini waongee.


“Hatukusaini mkataba wowote baina yetu, haiwezi kuhesabika kama ahadi. Sitaki kushirikiana na nyie, sio kwasababu hamna vigezo bali sitaki kumkasirisha Bosi Leibsoni.” Mara baada ya kuongea hivyo haraka haraka alisogelea upande aliokuwepo Regina.


Akiwa na sura iliyojaa soni, alimsogelea Regina na kumuomba ushirikiano upya.


“Miss Regina, nitazingatia ombi lako kwa umakini, naona hali ya kampuni yako ni nzuri zaidi kwa sisi kushirikiana.”


Regina muda huo alikuwa bize kudili na watu waliokuwa wakimsalimia na wengi wao walikuwa ni mabosi wa makampuni makubwa. Mara baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Kaird, aliishia kukunja sura kidogo.


“Sorry, Mr. Kaird. I am no longer interested in cooperating with you guys,” aliongea akimaanisha havutiwi tena kushirikiana nao.


Ijapokuwa alitarajia jibu hilo, lakini bado alishikwa na mawazo. Mara baada ya Zuberi na Hamisa kuona hilo, walijikuta wakishikwa na hasira mno kiasi cha kutaka kutapika damu. Yaani Kaird alikuwa radhi kuachana nao na aende kuomba kwa Regina ambako alijua angekataliwa?


Walijihisi takataka muda huo; hakuamini kuungana kwake na Multimedia hakukuwa na ushawishi mkubwa kwa tajiri kama Kaird.


Kutokana na jambo hilo, Zuberi na mpenzi wake hawakuwa na hamu tena ya kuendelea kukaa katika sherehe hiyo, hivyo haraka haraka walitembea kinyonge, wasithubutu hata kumwangalia Regina usoni.


Ukweli ni kwamba Regina tokea mwanzo hakuwachukulia kama washindani. Malengo yake ilikuwa ni kudili na matajiri wakubwa wa biashara, na Brewer na Kaird ilikuwa ni mwanzo tu.


Henry na baadhi ya watu wachache waliokuwa wakimfahamu Hamza walisimama nae huku wakiongea.


“Sir, sio kwamba tunamsaidia Madam, ni kutokana na ushawishi wa Leibsoni ndiyo maana,” aliongea Henry huku akicheka.


“Na hili ni swala ambalo siwezi kuamua tu, mnaweza pia kujumuika na nyie. Nina uhakika mke wangu hawezi kukasirika,” aliongea Hamza akimwangalia mke wake aliyekuwa bize akiongea na wazungu.


Mpaka sherehe inakuja kutamatika, Regina alikuwa amepata mwaliko kutoka kwa zaidi ya makampuni ishirini na wote walitaka kushirikiana naye kibiashara.


Kama Henry na yeye angeonyesha kufahamiana na Regina, pengine mialiko ingekuwa mingi zaidi.


Mwanzoni Regina alitaka kujihusisha na kampuni ambazo alipendezwa kufanya nazo kazi, lakini mwishowe kampuni yake ni kama imegeuka na kuwa keki na kila mtu aliitaka.


Wakati wakiwa njiani kwenye gari kurudi hotelini, Regina alikuwa amefumba macho yake akionekana kupumzika, hakuongea neno lolote na Hamza.


Baada ya kufika hotelini, Regina alihisi kuchoka sana. Alikaa kitandani huku akivuta pumzi kwa nguvu. Kulikuwa na hali ya jasho kwenye paji la uso wake.


Hamza aliangalia mwonekano wa mwanamke huyo na pale pale alionekana kugundua, ijapokuwa Regina alionekana kutulia kidogo lakini kiuhalisia ilikuwa stress kuongea na watu wengi namna ile ambao hakuwa akiwajua.


Hamza aliishia kutoa tabasamu hafifu na kisha alikaa kitandani na kunyoosha mkono wake akitaka kumtuliza Regina, lakini mwanamke huyo alimkwepa kwa kusogea mbali.


“Wife, nini tatizo? Una hasira na mimi kwa kilichotokea? Haikuwa makusudi pale, sikujua yule Leibsoni angekuja kunitafuta, mimi mwenyewe hata sikuwahi kumfahamu. Si unaona Henry na wengine ambao nilifahamiana nao hawakuthubutu kukusogelea kwa sababu ya kuheshimu maamuzi yako,” Hamza aliona ajitetee na Regina aligeuza kichwa chake na kumwangalia.


“Nani kasema nimekasirika?”


“Kama sio hivyo…”


“Niambie, wewe ni nani kwanza?” aliongea Regina na kumfanya Hamza kushangaa kwani katika macho ya Regina ni kama vile ndio kwanza wanaanza kufahamiana.


“Nataka kujua Mameni ni nani, Vita Takatifu ni nini, kwa nini wanakuita Lucifer, na Prince mrithi wa utawala wa kuzimu ni jambo gani. Leo ni siku ya kuniambia, sidhani kama kuna haja ya kuendelea kunificha,” aliongea Regina kwa uzito, akimfanya Hamza kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa.


“Mameni ni mshikaji wangu, zaidi ya ndugu, ni mfanyabiashara mkubwa wa kuuza na kusambaza silaha duniani. Ana mtandao mzuri wa usafirishaji, na kwa sababu Leibsoni pia ni mfanyabiashara, wamekuwa marafiki. Kuhusu mimi, niliwahi kuwa kiongozi wa juu wa jumii ya siri ya Inferno, inayojulikana pia kama Hellfire Club. Kutokana na nafasi yangu, nilipachikwa majina ya utani kama Selafi, Lucifer, mfalme wa kuzimu, na Prince. Kuhusu jina Lucifer, ni kutokana na chimbuko lenyewe la jumuia hii; ukifuatilia historia, utaelewa ninachomaanisha. Kuhusu Vita Takatifu, hiyo ni hadithi ndefu yenye mfululizo wa maswali mengi. Wife, nitamtafuta mtu atakayeandaa taarifa kwa mtiririko mzuri ili uelewe. Siwezi kuelezea yote usiku huu,” aliongea Hamza, akimfanya Regina kupatwa na mshtuko na moyo wake kuenda mbio baada ya kusikia hayo.


“Na vipi kuhusu jina la ‘Gwiji Mtaalamu wa Juu’? Kwa nini wanakuita hivyo?” aliuliza Regina.


“Hayo pia ni majina ya sifa walizonipa. Ukweli ni kwamba sijali sana; kama ningekuwa najali kuhusu majina na vyeo, nisingerudi Tanzania na kuwa msaidizi katika kampuni yako,” alijibu Hamza, na Regina alimwangalia huku akitabasamu kwa dhihaka.


Hamza alikuwa bado ni yuleyule. Ingawa kulikuwa na mambo ya kushangaza kuhusu maisha yake, lakini angalau alikuwa mkweli. Mara baada ya kufikiria kwa muda, uso wake ulitulia, kisha akavimbisha mashavu.


“Nilisema nitajitahidi mwenyewe kupata ubia wa kibiashara, lakini umeharibu kila kitu.”


“Wife! Ningejua vipi kama Leibsoni atakuja na kuvuruga kila kitu?” alijibu Hamza kwa kujitetea.


“Sijali, yote ni kwa sababu yako. Kwa macho yao, wanaona kama mimi ni mwanamke ninayefanikiwa kupitia uhusiano wetu. Hili linanikasirisha, sitaki tena kwenda na wewe kwenye hafla kama ile. Mimi ndio ninakulipa mshahara, lakini wanadhani unanisaidia,” aliongea Regina kwa hasira, kisha akaelekea mezani na kujimiminia glasi ya maji akanywa yote kutuliza hasira.Hamza hakujua acheke au alie; aliguna tu muda huo.


“Ni kweli kabisa. Mshahara wangu napata kutoka kwako, wao wanakusingizia tu. Na kuanzia sasa, nitawatangazia wasifanye biashara na wewe kwa kutanguliza jina langu,” aliongea Hamza huku akiongeza utani, jambo lililomfanya Regina kumwangalia kwa uzito.


“Lazima unanicheka moyoni, ukidhani siwezi kufanya lolote bila msaada wako, hasa ukizingatia namna Hamisa na Zuberi walivyokuwa wakinicheka mbele ya wale matajiri.”


“Hamna, wife, sijawahi kufikiria hivyo. Niliweza kuona jinsi ulivyomjibu Brewer pale. Ulikuwa na ujasiri, na nilifurahi sana kukuona vile,” aliongea Hamza.


“Kweli!” Aliuliza Regina kimashaka.


“Kweli kabisa, kama nakudanganya mke wangu, nipasuliwe na radi.” Ile anamaliza kuongea kauli hiyo tu, ngurumo nzito ilisikika nje kiasi cha kufanya jiji hilo la Paris kuwa kama vile anga lake linataka kudondoka.


Regina macho yalimtoka kutokana na tukio hilo. Upande wa Hamza alizubaa, na kama hakuamini, haraka sana alisimama na kwenda kuchungulia dirishani kwa kuvuta pazia, na hapo ndipo alipoweza kuona wingu zito likiwa limetanda angani. Ilikuwa ni usiku sana, na ilionyesha mvua muda wowote itaanza kunyesha.


Hamza aliishia kukuna kichwa chake kwa wasiwasi huku akilaani ngurumo hiyo, ijapokuwa mara nyingi mvua inayoambatana na ngurumo ilinyesha kipindi cha masika, lakini kulikuwa na dalili mvua hiyo itakuwa kubwa.


Hamza mara baada ya kugeuka aliweza kumuona Regina akimwangalia huku anamcheka. Mrembo huyo alionekana kufurahia kuumbuka kwake, lakini alifurahishwa na tabasamu lake.


“Wife, hii ngurumo haihusiani kabisa na kuapia kwangu, nazungumzia radi kama radi na sio ngurumo,” aliongea Hamza akijielezea.


“Huna haja ya kuongea, kwa sababu Mungu tayari ashanipatia jibu ninalotaka. Wewe endelea tu kunidharau, isitoshe ni kweli nakutegemea, na mpaka sasa mambo yamebadilika, hivyo siwezi kufanya chochote.”


Baada ya kuongea hivyo, alijilaza kitandani huku akijiwekea mto na na kufumba macho .


“Nimechoka, nataka kulala. Unaweza kwenda kuendelea kucheza huko nje mwenyewe.”


Hamza akiwa na tabasamu lililojaa uchungu alijirusha na yeye kitandani pembeni ya Regina.


“Mke wangu, usiwe hivyo basi. Wengine wanaweza kuona unanitegemea, lakini mimi najua ukweli unajitegemea mwenyewe. Usiwe na hasira basi.”


“Mimi sina hasira,” aliongea Regina huku akiwa amefumba macho yake.


“Mimi siamini kama huna hasira. Sikutegemea kabisa yule mshenzi Leibsoni angetokea namna ile.”


“Nishasema tayari sina hasira sawa. Kwanza sina haki ya kuwa na hasira kwa mtu kama wewe mwenye cheo cha Lucifer, mfalme kutoka kuzimu. Mfanyabiashara yoyote mdogo kama mimi siwezi kuzuia kufaidika kwa uwezo wako. Nikikukasirikia si nitaonekana kama mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri?”


“Wife, usiendelee basi kuongea hivyo. Kadri ninavyokusikia ndivyo ninavyozidi kupaniki. Hebu fumbua kwanza macho yako na uniangalie. Macho yangu yanaongea ukweli kuliko mdomo wangu, angalia utaona mwenyewe.”


Regina aliishia kufumbua macho yake na kisha aligeuza uso wake na kumwangalia Hamza usoni.


Waliishia kuangaliana, na Regina alinyoosha mkono wake na kuuweka katika sura ya Hamza na kumfanya bwana huyo mapigo yake kudunda kwa nguvu. Ilikuwa ni adimu sana kwa mrembo kama huyo kuchukua hatua kama hiyo.


“Nishakuambia sina hasira, kwanini bado huniamini? Unadhani sikuamini au ni kweli unanidharau kwenye moyo wako? Ukweli, muda mwingine najihisi labda nina maringo na ukiburi ila najua unanijali mno. Lakini hata hivyo, nataka kufanya kitu ambacho nitajivunia uwezo wangu. Sio jambo baya kwanza kumtegemea mwanaume. Ukiangalia kuna wanawake wengi sana ambao wanategemea waume zao kufanya kila kitu na wanaishi vizuri tu kwa furaha. Najua pia mimi ni mwanamke na napaswa kukutegemea, lakini siwezi kuigiza uhalisia kwani tayari mimi ni tajiri. Kulinganisha na hao wanawake wengine, sidhani kama kutaka kujifanyia kitu kwa uwezo wangu kunaniondolea kigezo cha kuwa mke mwema. Wewe unaonaje?” aliuliza Regina.


Hamza alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha, na pale pale alishika mkono wa Regina.


“Mke wangu, kama huu ndio mtazamo wako basi nimefarijika. Lakini pia jua tu, siku moja ukiamua kutaka kunitegemea na kutaka kukaa tu nyumbani na kuwa kama wanawake wengine, siwezi kukudharau. Ninayekupenda ni wewe; kwangu mimi haijalishi una utajiri kiasi gani au cheo kipi katika kampuni.”


“Ndio, naelewa. Ukweli baada ya kukutana na wewe na pia kufahamiana na watu unaojuana nao kama ilivyo kwa Mr. Leibsoni, leo nimejikuta nikifikiria sana. Kwako wewe urithi nilioachiwa ni mdogo sana, na linaweza kuwa swala ambalo hata hujali. Lakini ndio urithi ambao babu na bibi wameniachia. Nataka kuiendeleza kampuni kwa sababu ya kuheshimu juhudi zao. Lakini vilevile kuna wafanyakazi kibao ambao wanategemea kuendesha maisha yao kupitia kampuni. Hivyo haiwezekani nikawa mwanamke ambaye ninachojua ni kununua na kula tu. Tukiwa kama hivi nichukulie mimi kama mimi na usijali sana kuhusu kazi yangu, sawa,” aliongea Regina na kauli yake ilimfurahisha Hamza moyoni.


Kwa namna walivyokuwa wakiangaliana usoni, urembo wa Regina ulivutia sana macho katika angle hiyo. Kilichomfurahisha zaidi ni haiba ya upole aliokuwa nayo.


Muda huo wakati akiwa amejilaza kitandani akimsikiliza mke wake, alijihisi kuwa mwanaume mwenye bahati dunia nzima na mke wake ni mrembo kuliko wanawake wote.


“Wife, nataka kusikia ukiniita mume wangu au Hubby. Mimi nimekuwa nikikuita mke kwa muda mrefu,” Hamza alijiambia ni wakati wa kugongelea chuma kikiwa bado ni cha moto. Regina mara baada ya kusikia hivyo, alijirembulisha.


“Sitaki, hujanichumbia bado nikakubali kuwa mke wako kihisia.”


“Ah! Basi kama ni hivyo, kuanzia sasa nitafikiria namna ya kukuchumbia,” aliongea Hamza na kumfanya Regina kuvimbisha mashavu.


“Hamza, unataka kweli kuoa mwanamke kama mimi? Hujali kubadilika badilika kwangu na hasira za karibu?”


“Wife, muda kama huu kwanini unauliza swali kama hilo? Tumefahamiana kwa muda mrefu sasa na kufanya mambo mengi, kuna siku uliwahi kuona nikionyesha dalili ya kutokukupenda?”


“Basi niambie umenipendea nini? Si una wanawake wengi tena warembo tu. Hata kama nimewazidi kidogo uzuri, lakini wamenizidi kwenye vitu vingine?” aliuliza Regina akiwa na shauku.


Hamza alipitisha mkono na kuvutia kichwa cha Regina na kukiweka kifuani kwake. Jambo hilo lilimfanya Regina kutetemeka maana ni mara yake ya kwanza, na kwa wasiwasi aliuliza.


“Unafanya nini?”


“Shiii! Sikiliza kwanza,” aliongea Hamza huku akilengesha sikio la Regina karibu na moyo wake.


“Unasikia mapigo yangu ya moyo?”


“Mh! Mbona yapo mbio sana?”


“Ndio. Kabla sijakutana na wewe, sijawahi kuwa na mwanamke ambaye ananifanya mapigo yangu kunienda mbio kama wewe. Kwangu mimi sijali unabadilika badilika wala una hasira za karibu,” aliongea Hamza na Regina mara baada ya kusikia sauti hiyo ya besi alishindwa kujizuia na kutega vizuri sikio lake.


Lakini ni muda ule ngurumo kubwa ilisikika kwa mara nyingine na mvua kubwa ilianza kunyesha.


Regina aliyekuwa ndani ya chumba hicho alichoweza kusikia ni sauti za matone ya mvua na upepo akiwa amemlalia Hamza kifuani.
Endelea kusoma kwenye jukwaa la fasihinet , kwanzia hiki kipande kwenda mbele ni bure:- SEHEMU YA 192
 
Back
Top Bottom