Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Mtumishi Madonna


“Mwanaume ana sura mbili , sura ya kabla na baada ya ndoa” By Regina


Hamza yeye kama yeye hakuwa na wasiwasi na sumu hio, kutokana na mafunzo yake ya kuimarisha mwili ni ngumu sana kuathirika , hivyo wasiwasi wake ulikuwa kwa Airami.


“Princess , usivute hewa!”Aliongea Hamza kwa nguvu , ingawa alimwambia asivute hewa lakini shambulizi hilo lilikuwa la haraka mno hivyo ilikuwa ni ngumu kama hajavuta sumu hio hata kidogo.


Hamza hakujali kitu kingine tena na palepale alichomoka kwenye siti yake na kurudi nyuma na kumkunyakua Airami na kisha akafungua mlango na kukimbia nae nje licha ya moshi ule.


Lakini licha ya kufanikiwa kumtoa , Airami alikuwa ashavuta hewa kama mara mbili hivi ya moshi ule wa sumu na ilimfanya Hamza kuanza kuwa na wasiwasi na umakini wake kupungua.


“Hamza… na. najisikia vibaya”Aliongea Airami kwa sauti ya unyonge akionesha alikuwa katika maumivu.


“Usiongee ndio unajipa shida zaidi”Aliongea Hamza kwa nguvu lakini alikuwa amechelewa kwani palepale Airami alipoteza fahamu.


Hamza aliishia kusaga meno kwa hasira , kama angejua watu hao wangechukua hatua mapema ya kutaka kuwaua na sio kuwakamata angefanya kitu mapema, hakujua kama walikuwa na watu kila kona.


Bang! Bang! Bang!”


Nyuma yake ilikuwa ni mirindimo ya risasi , watu wale wa Sinagogu walibadilisha uelekeo wa siraha zao na kuanza kumshambulia Hamza.


Hamza alitumia mwili wake kukinga risasi zile , ili kuhakikisha Airami hazimfikii.


Mara baada ya kuona wameishiwa risasi , Hamza hakutaka kuzembea na palepale alimuweka Airami chini na kisha kwa spidi ya juu aliwasogelea wale polisi feki na kuwashambulia na ngumi za kichwa.


Wauaji wale hawakujua kwanini Hamza hakuwa ameathirika licha ya kuvuta hewa ya moshi wa sumu , lakini hawakupewa nafasi hata ya kujua kwani Hamza aliwaua palepale.


Licha ya kuwaua kirahisi,Hamza hakuwa na furaha hata kidogo na hio yote ni kutokana na Aira kuvuta sumu ile na walikuwa mbali na mjini. Aliona hata kama angemuwahisha hospitalini anaweza asimuokoe.


Hamza hakuamini kama mwnamke mrembo kama Airami , mtoto wa mfalme alikuwa anakwenda kufa kizembe namna hio.


“Pumbavu zenu wasinagogu.. mnachokifanya sio ubinadamu kabisa!”Alilaani Hamza. Ingawa alimuona Airami kwa muda mchache sana lakini alitokea kumpenda.


Hamza aliishia kutuliza hasira iliokuwa ndani ya moyo wake na palepale alijiambia atafanya la kuwezekana kumuokoa Airami. Lakini sasa ile anageuka kusogelea sehemu aliokuwa amemlaza chini, Airami hakuonekana. Hamza aliishia kupepes na hata kujifikicha macho yake kuona vizuri lakini Airami hakuonekana pale.


“Airami!, Princess?” Hamza aliita kwa nguvu lakini Airami ambae alikuwa alipoteza fahamu na kisha kutoweka hakusikika wala kuonekana, ilikuwa ngumu kuamini alikuwa amekimbia mwenyewe wakati alimuona kabisa akiwa katika hali ya kupoteza fahamu.


Hamza alijiuliza au kuna mtu ambae amemchukua Airami , lakini licha ya kujiuliza swali hilo alikataa maana ilikuwa ngumu kutoweza kujua uwepo wa mtu kupitia hisia zake.


Hamza alijihisi ni kama anaona maluweluwe na kuanza kujiuliza ni hali gani hio iliokuwa ikiendelea?.


Aliishia kusimama katika sehemu moja akiwa ameshika kiuno huku akiangaza kulia na kushoto kama anaweza kuona chochote lakini hakupata hata dalili.


Muda ule alianza kuzunguka kwa spidi kujaribu kumtamfuta katika mzingo wa kilomita moja , lakini hakuweza kumuona kabisa wala kuona viashiria vyake.


Hamza alihisi ubaridi kusambaa mgongoni mpaka kwenye nyayo za miguu yake na palepale alishindwa kujifikiria na kujiambia au Airami aliekuwa nae alikuwa ni udanganyifu wa macho?, Au ni jini?.Hamza alijiambia kama sio mzimu wala jini anaitafsiri vipi hio hali?.


Hamza alijiamulia zake kurudi barabarani tu akipotezea kumtafuta tena , ki-uhalisia kutokana na uwezo wake usiokuwa wa kawaida angeweza kuelewa hali hio hata kwa viashiria vidogo , lakini kilichotokea kilikuwa nje kabisa ya uelewa wake na ndio maana alionekana kuwa katika hali isioelezeka.


Aliishia kutoa sigara kwenye mfuko wake na kuiwasha ili kujaribu kujituliza na baada ya kupiga moshi kidogo , palepale alitingisha kichwa na kupotezea kabisa swala lile na kuona ni muda wa kurudi hotelini.


Kutokana na gari ile aliokuwa akitumia kuharibika , hakuwa na jinsi zaidi ya kutumia ile ya polisi.


Mara baada ya kufika mjini aliegesha gari pembeni ya barabara na kisha alianza kutembea kuitafuta hoteli ilipo.


Baada ya kufika katika mlango wa chumba cha Regina, aliangalia saa yake ya mkononi na aligundua ilikuwa ni saa tisa za usiku , hivyo hakujua kama Regina alikuwa amelala au yupo macho.


Hivyo alitega sikio kusikiliza sauti kutoka ndani na aliweza kusikia sauti ya TV na pale ndio alijua lazima Regina bado atakuwa macho hivyo aligonga mlango na kujitambulisha.


Regina mara baada ya kujua ni Hamza haraka haraka alifungua mlango, akionekana katika mavazi ya kulalia.


“Vipi wewe? Hujaumia eh?”Aliuliza kwa kujali.


Hamza alionekana kushangaa . Alidhania Regina angemchunia kama kawaida yake maada bado hakuwa katika maelewano mazuri wakati anaondoka , lakini ilikuwa tofauti , kwani Regina alionekana kumjali.


“Niko sawa , naumiaje kwa mfano”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.


Regina alimwangalia mwanaume huyo kwanzia miguuni mpaka kichwani na mara baada ya kuthibitisha hakuwa na tatizo , alitoa pumzi ya ahueni.


“Lakini Hamza seriously! Una nini wewe , kama ni mlipuko si ungeuacha tu ulipuke wewe unakuhusu nini mpaka kwenda kuangalia? Nchi hii ina kila aina ya wakimbizi unajua ni wapi bomu linaweza kutokea , ukilipukiwa je?”Regina alilalamika.


“Upo sahihi mke wangu , nitakuwa makini siku nyingine .. Ila ukiachana na mlipuko nimekuja kwa kuchelewa kwasababu ya kitu kingine?”


“Kitu gani?”Aliuliza Regina huku akipepesa macho na Hamza alioneakna kusita kidogo.


“Muda umeenda sana na kesho unapaswa kwenda kwenye kampuni , pumzika mapema”


“Hapana! Nalala vipi wakati hujamaliza kuongea . Isitoshe kuna mlipuko huko nje na nimeona pia kupitia taarifa ya habari Princess Airami ametekwa. Ndio kilichonifanya nikusubiri mpaka sasa hivi”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kufurahi.


“Wife , kwahio ulikuwa ukinisubiria kweli? Unaonekana kunijali”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kushikwa na aibu za kike.


“Usibadili mada.Wapi ulikuwa umeenda?”Aliuliza na Hamza kwa wasiwasi aliona amwambie tu.


“Ni kama ulivyoona kwenye taarifa ya habari , ukweli nilikuwa nikiwafuatilia hao watekaji”


“Ah! Kwahio umewakamata sasa?”.


“Wife unaonaje kwanza nikiingia ndani , nitakuambia taratibu”


Muda huo ndio Regina alijua kumbe walikuwa wamesimama mlangoni,aliiishia kumruhusu Hamza kuingia ndani.


Mara baada ya kutumia mashine maalumu ndani ya chumba hicho kutengeneza kahawa alimpatia Hamza kikombe na ndio Hamza alivyoanza kumhadhitia Regina kuhusu umoja wa imani ya siri ya Sinagogu na ibada zao na kitendo cha kutaka kumtoa kafara, Princess Airami.


Hamza alimwambia Regina kinachomshangaza na kumchanganya ni kutokana na kupotea kwa Princess Airami.


“Ulikuwa ukiota au! Hata kama asingevuta moshi wa sumu mtu mwenye mwili wa nyama ni ngumu kupotea”


“Ni kweli ndio maana nakuambia wewe mke wangu. Mwenye najiuliza maswali mengi hapa kama kuna shida katika akili yangu, unaonaje ukinifinya kidogo pengine nipo ndotoni”


Regina aliekuwa amekaa juu ya kitanda akiwa amening’iniza miguu aliishia kumwangalia Hamza kwa kumchunguza.


“Wala hata sikufinyi, kwanza umesema umeua watu wengi , utakuwa mchafu bado na pengine una damu zao”


“Sikuwa na jinsi , wale watu walikuwa ni kama mazombi , kama nisingewaua ni swala la muda tu kudhuru watu wengine. Wewe unadhani damu waliokuwa wakinywa wameitolea wapi? Nina uhakika sio damu kutoka hospitalini”Aliongea Hamza kwa uhakika.


Regina aliishia kutingisha kichwa kukubali na palepale mboni za macho yake mazuri zilicheza.


“Vipi kuhusu huyo Princess… Ni kweli ni mrembo sana? Nimesikia kutoka kwenye taarifa ya habari ndio mwanawake mrembo zaidi duniani na hajawahi kutoka ndani ya tano bora tokea akiwa na miaka kumi na tano , huku akishika nafasi ya kwanza mara tatu mfululizo. Imenifanya kuingia mtandaoni kujaribu kuona picha zake lakini ajabu sikuona hata moja na karibia zote ambazo zilisimekana kuwa zake amevaaa shera.”


Hamza alivyosikia namna Regina alivyokuwa akiongea kwa sauti ya unyongea alitamani kucheka kwa nguvu.


“Wife acha kusikiliza propaganda kutoka kwa wanahabari , nina uhakika kama sio maswala ya upendeleo wewe ndio ungekuwa namba moja duniani . Huyo Princess hakufikii hata kidogo”Aliongea Hamza akiwa siriasi lakini kwenye moyo wake alikuwa akiomba msahamaha ndani kwa ndani.


“Samahani sana Princess Airami , sijui umekufa ama upo hai. Ila sina jinsi kwasasa zaidi ya kumsifia mke wangu”


Regina mara baada ya kusikia hivyo alishindwa kuizuia furaha yake.


“Unaongea upuuzi , nakuwaje wa kwanza duniani? Uzuri wangu ni wa tofauti sana na hawa watu weupe”Aliongea Regina.


“Ni kweli , lakini kwa upande wangu sijawahi kuona mwanamke mzuri kama wewe mke wangu”


“Mh! Kama kweli mimi mzuri kwanini bado una hangaika na wanawake wengine huko nje?”Aliongea Regina huku akivuta mdomo.


Hamza alifurahishwa na mwonekano wa Regina muda huo na alijiambia ‘Kazi nzuri Hamza’. Ukweli ni kwamba Regina anapokuwa katika hali ya furaha na mwepesi wa kuongea nae anapendeza zaidi na kumfanya mtu yoyote kumpenda kama ilivyo kwa Airami.


“Wife kwa jinsi ulivyokuwa na hasira na mimi muda ule ? Kwanini bado unaonekana kunijali , nimeshangaa?”Aliuliza Hamza.


“Kwahio unataka niendelee kukasirikia?”


“Hapana , mke wangu kipenzi naomba usiwe na hasira , unajua unanifanyta nakuogopa?”


Regina alimwangalia Hamza alivyokuwa na wasiwasi na kuishia kutingisha kichwa kusikitika.


“Hamza , hivi ni kweli nakasirika haraka? Naonekana kama mtu mgumu hivi eh?”


Hamza alitamani kusema ndio , lakini aliona akiongea hivyo ni sawa na kulipua bomu.


“Hapana , mimi huwa naona mara nyingi ukikasirika una sababu ya msingi”


“Mhh! Huna haja ya kuongea uongo , mwenyewe najua siku za hivi karibuni nina wasiwasi sana , sijui hata ni kwanini. Sijawahi kuwa hivi hapo kabla “Aliongea Regina kwa sauti ya chini huku akisugua kikombe cha kahawa alichoshikilia mkononi kama vile kilikuwa na uchafu.


“Wife hata usijali kabisa , najua sio kama una hasira , bali ni kutokana na kujaribu kuwa mwelewa juu yangu”Aliongea Hamza kwa furaha.


“Nimekuwa nikijijengea kujiamini sana tokea nikiwa mdogo , kwa msichana kama mimi ambae nipo chini ya miaka therathini na kisha kuwa mkurugenzi , kama nisipoonyesha kujiamini ni nani ambae anaweza kuniamini? Ndio maana babu alikuwa akiniambia tokea nikiwa mdogo nina kipaji ambacho wengine hawana na njia pekee ya kuendelea kujiamini ni kuiamini akili yangu. Hivyo ndio nilivyokuwa nikiwaza siku zote na kuona watu watanipenda kupitia uwezo na mafanikio yangu. Lakini mara baada ya kukutana na wewe kila kitu naona ni tofauti baada ya kuona wanawake warembo na wenye sifa hata kunizidi wakionyesha kuvutiwa na wewe sana bila hata kujitambulisha kwao. Lakini nilipoanza kuona nilivyokudhania ni tofauti na vile ninavyokujua pamoja na watu wengi unaofahamiana nao kuwa wenye hadhi za juu , najiona hata ule uwezo wangu wa akili ambao ulikuwa ndio msingi wa kujiamini kwangu umenipotea , najiona kuwa mjinga na nashindwa kujizuia kuwa na hisia za kuona mimi sifai kuwa mke wako..”


“Wife kipi kinakufanya ufikirie hivyo? Mimi na wewe hatuna utofauti mkubwa unaowazia, ni kwamba tu uzoefu wangu wa kimaisha ulikuwa wa tofauti , hivyo ni kawaida kukutana na watu wengi na hicho sio kigezo cha kuitambua hadhi ya mtu. Unachoongea wewe ni ule mtazamo wa kwamba Prince anapaswa kumuoa Princess na Masikini anapaswa kumuoa masikini mwenzake. Mapenzi hayapo hivyo kabisa , kumpenda mtu hakuhitajiki kigezo cha nani ni tajiri na nani sio tajiri. Ndio ni kweli sipingi kuna baadhi ya watu wanaochagua kabisa nani wa kumuoa au kuolewa nae ila hio ni kutokana na kupunguza lile gepu la kimazingira. Lakini hebu angalia sasa hivi kuhusu sisi , wewe unadhani kuna kasoro yoyote , si tunaendana vyema tu na tunaelewana?”Aliongea lakini haikutosha kumwondolea Regina wasiwasi.


“Mimi naogopa, nahisi kabisa ni kama unataka kunichezea tu na pengine baada ya kuona sina jipya na labda nimezeeka utaenda kutafuta mwanamke mzuri zaidi yangu na kumpenda na kunisahau kabisa. Najua kabisa wapo wanawake wengi warembo kunizidi mimi ambao wanazaliwa kila siku na kadri umri wangu unavosogea ndio wanavyoniacha mbali..”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo , aliona mwanamke huyo ni mjinga mno kiasi cha kufanya moyo wake kuuma. Aliishia kukaa kitandani karibu yake na kupapasa kichwa chake.


“Wife kwahio unaniona mimi ni mtu wa aina hio. Kama kweli nipo na wewe kwa kigezo cha uzuri pekee kwanini nikubali kutia sahihi cheti cha ndoa. Nakupenda ndio maana nimefanya vile na hata kama nipigwe kila siku nikane mapenzi yangu kwako, siwezi. Hivyo hivyo kama kweli sijakupenda basi siwezi kukupendi hata kama unipatie kila nitakachohitaji ndani ya uwezo wako. Hivyo hebu acha kufikiria mambo ya kijinga , nimepitia mengi sana na siku niliokubali kusaini kile cheti cha ndoa sikukurupuka , nilishafanya maamuzi ya kuwa na wewe kwa namna yoyote ile”


“Kweli..!”Regina alionekana kusita.


“Ndio , Wife hebu acha kuniogopesha kwa kunifananisha na mtu mbaya basi”Aliongea Hamza na Regina alionekana kuwa kimya kwa muda mfupi na palepale alivuta pumzi na kuzishusha.


“Kwahio unaniambia napaswa kujiamini , vinginevyo naweza nisiwe mimi, si ndio?”Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa.


“Una moyo wangu tayari ,hivyo unapaswa kujiamini”Aliongea Hamza na Regina alishindwa kuzuia tabasamu la aibu.


“Ila nikiwa na hasira huwa nakutisha eh?”


“Sanaa, ndio maana hata muda huu tunaongea nawaza nisije kuongea kitu ambacho kitakukasirisha”Aliongea Hamza na muda ule Regina alinyoosha mkono na kushika kidevu cha Hamza kwa kumpapasa kimahaba.


“Muone sasa ulivyo mjinga , nilitaka tu unibembeleze ndio maana, nikiona unanibembeleza ndio nitajua unanipenda kweli na kunijali”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akigundua kumbe hio ndio sababu. Wanawake ni viumbe ambao wana mitego sana.


“Haha.. kwahio kumbe pale nilipaswa kukubembeleza tu, lakini kama kukubembeleza ni kwa staili hii si nitachoka. Uwezo wangu wa akili ni mdogo na nashindwa kufikiria namna ya haraka ya kukubembeleza , kwangu kubembeleza ni ngumu kuliko kuua na kupigana” Regina mara baada ya kusikia hivyo hakufurahi.


“Wewe unaona uvivu wa kunibembeleza kwasababu umeshanioa bila ya kunichumbia. Wanaume huwa mna sura mbili ,sura ya kabla na baada ya ndoa, na ndio ninachokiona sasa hivi”.


“Hapana wife , nitakubembeleza sana kwanzia sasa hivi”Aliongea Hamza akijitetea.


“Haina haja , Usije hata kunichumbia kwa ajili ya harusi maana nitakataa. Haya ndio maisha yetu yatakavyokuwa . Upo radhi kwenda kubembeleza mwanamke nje lakini kwangu unaona inachosha”


Mara baada ya kuongea hivyo aliweka kikombe chini na kupandisha kitandani na kujifunika na blanketi gubigubi.


“Unaweza kwenda, nimechoka nataka kulala”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo alitamani kutoa kilio palepale. Mabadiliko ya haraka haraka ya Regina yalimshangaza mno.


“Wife nimechoka sana , unaonaje nikilala hapa hapa?”


“Wewe toka!” Regina alifoka.


Hamza alijiambia ya nini ngoma za masikio kunipasukia , aliishia kujiinua kivivu na kurudi chumbani kwake.


Alijua Regina sio kama alikuwa na hasira bali alitafuta tu sababu ya kumuondosha ndani ya chumba chake. Mwanamke huyo ni kama alikuwa na pepo.


Muda ulikuwa umeenda sana na Hamza hakuona hata haja ya kulala , hivyo mara baada ya kujiegesha kidogo tu njaa ilimshika na alitamani angepata chochote kuchangamsha tumbo , lakini alisubiria kukuche.


Muda huo pia aliona ni vizuri pia kuongea na Himidu kuhusu suala zima la umoja wa Sinagogu , ili kuwafanya kuwa makini sana. Maana kile alichokishuhudia aliamini pengine kinaendelea ndani ya Tanzania.


Mara baada ya kumwambia Himidu kilichotokea , Mshauri mkuu huyo alisema sio rahisi kudili na makanisa ya Wabrazili moja kwa moja kutokana na kwamba ni mpaka wapate ushahidi kwamba wapo chini ya Sinagogu , hivyo wataandaa mpango maalumu , lakini kabla ya hapo anapaswa kupeleka taarifa hio kwa wakuu wake.


Hamza alijua Himidu yupo sahihi kwasababu nchi haikuwa yake na maswala ya kidini huwa si mepesi kudili nayo maana yanagusa wananchi moja kwa moja.


Baada ya kukata simu palepale aliona njia nzuri ya kupoteza muda ni kuchukua mazoezi na zoezi alilofanya ni ile ile mbinu yake ambayo alikuwa akiita Mdundiko wa jinni kichaa.


Ukweli ni kwamba aliamini uwezo wake ulikuwa mkubwa zaidi kabla ya kuvua nguvu za nishati ya mbingu na ardhi miaka mitatu iliopita.


Kama angeendelea na mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi na kisha akaja kukutana na Nyakasura, Asingeweza kumshinda mwanamke huyo.


Nyakasura ni aina ya watu ambao wamezaliwa na nishati za mbingu na ardhi kwenye miili yao tayari na wanachofanya ni kuziamsha tu na binadamu kama yeye atakachojivunia ni juhudi pekee.


Hamza yeye mtazamo wake ulikuwa ni tofauti kidogo , aliamini binadamu mwili wake una nguvu ya asili kama ilivyo kwa Nyakasura kuzaliwa na damu ya nishati ya moto.


Hivyo kuachana na mafunzo hayo ili kuwa ni kwa ajili ya kuvuna nguvu ya asili ya mwili na mazingira. Aliamini binadamu ni kiumbe ambacho hakijawepo katika uso wa dunia kuwa wa kawaida . Kama ambavyo wanahistoria wanaangazia binadamu alianza kuwa kama mnyama na kadri muda ulivyosogea ndio alibadilika , hivyo aliamini pia binadamu wa sasa bado hajafikia hata robo ya safari ya mabadiliko yake na pengine mabadiliko yanachukua muda mrefu kumtokea binadamu kutokana na kuridhika. Hivyo Hamza hakutaka kuridhika , alitaka kuharakisha mabadiliko ambayo binadamu anaweza kuyafikia kwa karne kadhaa mbele. Hivyo hakutaka kupoa.


Hamza hakupata mawazo hayo kwasababu ni yeye ndio kagundua kuwaza namna hio , kulikuwa na uthibitisho wa uwepo wa binadamu wenye uwezo wa hali ya juu sana ambao , hawakuwahi kuaminika uwepo wao katika akili za kibinadamu zaidi ya hadithi pekee.


Ijapokuwa hata yeye hakuwahi kukutana na hao Magwiji , lakini aliamini wapo na kama hawapo walikuwepo. Sasa mpango wa Hamza ni kuivuna asili ya mwili wake ili kufungua code za uwezo wa mwili wake na kufikia levo ya Ugwiji.


Imani yake ilimwambia kama kweli hao magwiji wapo basi ataweza kukutana nao akifika levo zao pekee na hio ndio asili na tabia ya watu wa juu. Ni kama ilivyo kwa watu waliokuwa juu kimadaraka hukaa meza moja na wenzao walio na madaraka ya juu ., Hivyo Hamza aliamini akifikia levo ya Ugwiji lazima magwiji watajitokeza kutaka kupimana nae.


Asubuhi na mapema Hamza alishuka katika mgahawa wa hoteli hio kwa ajili ya kufingua kinywa. Hakumsumbua Regina kwa kuamini kutokana na kuchelewa kulala basi usingizi utakuwa haujamwishia. Lakini ile inafika saa tatu Regina alianza kumpigia Simu.


Hamza alihisi pengine Regina ana tatizo , hivyo haraka haraka alikimbilia kwenda chumbani kwake na mara baada ya kufunguliwa mlango , Regina alikuwa katika mavazi ya kulalia bado na hata kuoga ilikuwa bado.


“Wife ni ni tatizo?”Aliuliza Hamza.


“Angalia mwenyewe”Aliongea Regina huku akimpa Hamza nafasi ya kuona Tv ndani. Palepale Hamza aliweza kuona taarifa ya habari ambayo ilimsahngaza na kumfanya mwili wake kushikwa na ubarafu.


Katika taarifa hio ilisema kwamba Princes Airami amepatikana. Kulingana na maelezo ya mtoa taarifa , ni kwamba watekaji hawakufanikiwa kwa silimia mia moja kumteka Princess. Anasema kwamba Princess alitekwa mwanzo lakini mara baada ya mtekaji kupoteza uangalifu alikimbia mpaka pale polisi walipofanikiwa kumpata asubuhi.


Familia ya mfalme na serikali ya Ufaransa wanapongeza juhudi za watu wote waliokuwa wakihakikisha kupatikana kwa Princess. Huku jeshi la polisi likiahidi litaendelea kufanya uchunguzi kugundua ni nani amabe alipanga njama za utekaji huo.


“Wewe si ulisema jana Princess alitoweka baada ya kuvuta hewa ya sumu na ulikuwa na uhakika amekufa? Kwahio ulikuwa ukinidanganya , mbona bado yupo hai?”


Hamza alikuwa katika kihoro , alikuwa na zaidi ya miaka ishirini na tano na muda huo kwa mara ya kwanza ndio anajihisi zile ngano za uwepo wa mizimu pengine ni kweli.


“Wife jana ni kama nilivyokuambia…. Nashindwa kuelewa imekuwaje” Hamza alihisi ni kama jambo hilo halikuwa likiwezekana.


“Inawezekana ulikutana na Princess feki wewe! Au alibadilishwa kuonekana ndio yeye . Kuna matukio ya watu wakubwa duniani ambao hutumia mbinu ya kujibadilisha ili kukwepa utekaji”Aliongea Regina.


“Kwamba walikuwa wawili? Lakini kama unachosema ni kweli alikuwa feki , vipi mbona hata maiti yake ilipotea? Kingine inawezekana vipi awe mrembo vile? Kama alifanya hivyo kulikuwa na haja ya kutafuta mtu mwenye urembo wa aina ile?”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kuguna.


“Jana nimekuuliza na ukasema ni wa kawaida , lakini naona kabisa sasa hivi unashindwa kuficha hisia zako”


Hamza palepale aliona mambo yanaelekea kuharibika na haraka haraka alibadilisha topiki.


“Mke wangu suala la muhimu ni kufanya uchunguzi na kujua kwa hakika nini kinaendelea au wewe unaonaje? Inawezekana niliekutana nae jana ni halisi na waliempata sasa hivi ndio feki na kama ni feki basi moja kwa moja atakuwa ni mwanachama wa Sinagogu. Na kama ni hivyo unadhani ni hatari kiasi gani kwa kile atakachofanya?”


Regina mara baada ya kusikia hivyo aliona aendane na Hamza kubadilisha tu mada.


“Hata kama ni feki , utafanya nini? Utawezaje kugundua isitoshe ulisema ndio mara yako ya kwanza kukutana nae”


Hamza pia hakujua anaenda kufanya uchunguzi vipi , lakini alijiambia lazima afuatilie hilo suala. Kwenye maisha yake hajawahi kuchezewa akili namna hio. Tabia yake haikumruhusu kuishi bila majibu anayoyataka.


“Wife naomba leo nisikusindikize kwenda kwenye kampuni . Naenda kuonana na huyu Princess”


“Kuonana nae! Kivipi utaweza kumuona?”


“Sikosi namna . Wife wewe usiwe na wasiwasai kabisa , ni princess tu huyo na sio kwamba naenda kuvamia ikulu , haiwezi kuwa ngumu”Aliongea Hamza , ingawa Regina alikuwa na wasiwasi lakini aliona amruhusu Hamza baada ya kuona alikuwa akijiamini vya kutosha.


“Usije tu kusababisha matatizo , sitaki kuja kukamatwa hapa Paris”


“Hilo lisikupe shaka kabisa . Naweza kamatwa Afrika na kushikiliwa kwa muda mrefu lakini sio Ulaya. Ninafahamiana na watu kibao wenye madaraka”


Regina alitaka kumwambia aache tambo , lakini mar baada ya kukumbuka mambo ya Hamza katika masaa machache yaliopita , alihisia kabisa hakuwa akidanganya.
 
Hamza mara baada ya kutoka hotelini hapo , alichukua uelekeo wa Louvre. Alikumbuka Princess Aira aliongea kuhusu sherehe za kukata utepe na kuna uhakika ilikuwa ni katika eneo la Louvre kama ratiba zake hazitakuwa zimebadilishwa.


Hamza mara baada ya kufika katika eneo hilo maalumu la makumbusho ni kama hisia zake zilivyomwambia kwani aliona walinzi wengi wakiwa wanaimarisha ulinzi. Watu wa kawaida hawakurhusiwa kabisa kuingia.


Hamza hakuwa na haraka kabisa. Alitembea kwa kuzunguka majengo hayo , akijaribu kuchunguza ili kama anaweza kupata eneo ambalo hawezi kuonekana na kurukia. Alisimama kwenye kona akiwa anasubiri.


Nusu saa mbele magari meusi yalifika ndani ya eneo hilo yakiwa na watu wengi maarufu na matajiri ambao wengi wao walikuwa katika mavazi ya kifasheni na kuvutia raia wengi na baadhi ya watalii.


Mara baaeda ya gari ya katikati ya Mercedenz Benz kusogea kabisa eneo hilo la Louvre Meusium, mtu ambae aliekuwa akimfahamu alishuka kutoka garini.


Alikuwa amevalia shati la chiffoni rangi nyeupe, Sketi ya Dark green na koti la suti lenye michirizi ya rangi nyeupe mkononi . Alikuwa mrefu mwenye umbo la kuvutia la umisi .


Alikuwa ni Princess Airami na muda huo alikuwa amefunika kichwa chake na kofia flani hivi wanzovaa sana Princess wa kimagharaibi iliokuwa imezungushiwa na kitambaa cha melimeli. Licha ya kutokuonekana sura vizuri, Hamza aliweza kuona kabisa huyo ni yule yule ambae amekutana nae jana usiku.


Hamza alijiuliza nini kinaendelea , imekuwaje yule princess ambae jana alipoteza fahamu akawa huyo?.


Hamza alitupa pembeni espresso aliokuwa ameshikilia na kisha palepale alianza kupita hatua kusogelea upande ule katika jeno la makumbusho ambalo Aira wasaidizi wake waliingia.


Muda ule mara baada ya kuona walinzi wawili mlangoni walikuwa hawaaangalii upande wake , haraka sana aliongeza nguvu katika miguu yake na kufanya mwili wake kuwa kama mshale na kupita walinzi kwa spidi kubwa na hawakuweza kuona chochote.


“Hey! Hujahisi kama kuna kitu kimepita?”Aliuliza mlinzi mmoja na kumfanya mwenzake pia kuonyesha hali ya kuchanganyikiwa.


“Nimehisi tu wimbi la upepo?”


“Haha.. nadhani ni pombe ya jana bado ipo kichwani”Aliongea na wote walicheka.


Wakati wakiongea , upande wa Hamza alikuwa ashafanikiwa kujipenyeza ndani ya jumba hilo la makumbusho.


Kutokana na ushombeshombe wake na pia kuvalia suti na namna ambavyo alikuwa akitembea kwa kujiamini ndani ya jengo hilo , ilikuwa ngumu kwa mtu ambae hakuwa akimfahamu kumtilia shaka.


Mara baada ya kufika katika aneo la mapumziko , sehemu maalumu kwa wageni muhimu , aliweza kuona mabodigadi wanne wakiwa wamesimama kwa nje kuhakikisha ulinzi kwa kutembea kwenda mbele na kurudi nyuma.


Ijapokuwa kulikuwa na njia nyingi za kuweza kujipenyeza ndani , Hamza hakutaka kupoteza muda hivyo alitembea kwa kujiamini kusogelea mlango ule.


“Wewe ni nani?” Bodigadi wa kizungu alievalia miwani nyeusi aliuliza.


Kwasababu Hamza likuwa akitembea kwa kujiamini , bodigadi yule hakuonyesha fujo , akiamini Hamza pengine ni mtu mzito.


“Mimi ni rafiki yake princess Airami , jina langu naitwa Hamza”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.


“Una urafiki na princess?!” Aliuliza mlinzi yule akionekana kushangaa na wote waliangaliana.


“Samahani tunapaswa kwanza kuthibitisha kama unachoongea ni kweli”Aliongea Bodigadi yule mwenye miwani ya jua na kisha kupitia simu ya upepo alitoa ripoti kwa watu waliokuwa ndani ya chumba.


“Madam Mtumishi!, kuna mtu hapa nje amejitambulisha kwa jina la Hamza anasema ni rafiki yake Princess.. ndio… Sawa”


Mara baada ya kukata simu ile , yule bodigadi aliinua sura yake na kumwangalia Hamza.


“Samahani Mr! Princess hakufahamu , tafadhari ondoka katika eneo hili”


“Kweli! Labda atakuwa amesahau jina langu , mwambie ni Hamza kutokea Tanzania”Aliongea Hamza kwa sauti.


“Please Leave!”Aliongea yule bodigadi huku usiriasi ukiongezeka.


Hamza aliishia kusinyaza macho yake tu akishindwa kujua ni kweli Airami hakumfahamu au alikuwa akiigiza kutokumfahamu makusudi tu.


Lakini licha ya hivyo Hamza hakutaka kulazimisha , maana aliamini sio kama Princess huyo angetokomelea huko ndani . Alipanga kusubiri mpaka atoke ndio ajihakikishie kama kweli alikuwa akiigiza au ni kweli hakuwa akimfahamu.


Baada ya kusubiri kwa takribani nusu saa hatimae msafara wa Airami ulianza harakati za kutoka.


Chini ya safu mbili za walinzi . Princess Airami aliweza kuonekana. Ingawa alikuwa amejifunika na kitambaa kama shera kuzunguka kofia yake , lakini Hamza alikuwa na uhakika na macho yake , huyo alikuwa ni Airami wa usiku wa jana bila shaka.


Muda huo Hamza hakusita tena kwani palepale alifanya maamuzi ya kuziba kwa mbele.


“Wewe ni nani?”


“Mzungukeni Princess!”Aliongea kiongozi wa walinzi haraka sana mara baada ya tukio la Hamza kusimama mbele yao.


Hamza mwonekno wake haukubadilika kabisa na muda huo alimwangalia Princess.


“Princess Airami, ni kweli hunitambui?”Aliuliza.


Kundi la wahudujmu mara baada ya kusikia lafudhi ya Hamza walijikuta wakiangaliana na ni kama walipatwa na hali ya ahueni wakiamini pengine sio muuaji.


Princess upande wake baada ya kuitwa jina lake na Hamza hakukuwa na mabadiliko makubwa na kupitia upenyo wa walinzi alimwangalia Hamza kwa umakini.


“Please excuse me sir, who are you?” Aliongea Princess akimuuliza Hamza kama yeye ni nani.


Hamza mara baada ya kusikia sauti yake , aliitambua vyema , ilikuwa ni sauti hio hio aliweza kusikia jana usiku bila shaka, lakini kwanini mwanamke huyo anasema hamtambui?.


“Princess Airami jina langu ni Hamza . Hukuiona vizuri sura yangu ile jana usiku wakati tunarudi Paris?”Aliendelea kuuliza Hamza.


“Sijawahi kukuona popote. Mr labda utakuwa umenifanananisha?”


Moja ya mhudumu wa kike alievalia miwani yenye flemu zilizobandikwa madini ya dhahabu aliingilia


“Harakisheni na mumkamate huyo mtu , anaweza kuwa sehemu ya watekaji wa jana usiku”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo alishindwa kujizuia na kuishia kushangazwa na kauli hio.


“Nyie watu nadhani mnatania , kama ningekuwa mtekaji ningekuija katika eneo kama hili kujiingiza mtegoni mwenyewe?”


“Nyie watekaji ni wajanja mno . Lazima upo hapa kimbinu. Princess ni mtu mkalimu sana lakini bado nyie watu msio na huruma mnajaribu kumteka na kumdhalilisha , uovu wenu hausameheki”Aliongea kwa kingereza na palepale walinzi walimsogelea Hamza kwa kasi na kutaka kumkamata.


Hamza aliishia kuwakwepa mara mbili mfululizo na kuwafanya mabodigadi hao kudondoka chini. Princess Airami mara baada ya kuona tukio hilo alionekan kushangaa kidogo.


“Madonna haina haja ya kumkamata , anaonekana kuwa mtu mzuri , tuondokeni”Aliongea Airami.


“Princess una roho nzuri sana , hii ndio maana unakaribisha watu wengi wasio na nia nzuri kuchukulia faida . Ila niamini mimi huyu mtu ni jambazi na lazima tumkamate ili tujue kwa undani stori nzima ya wasinagogu na kwanini wamekuteka?”


“Haina haja , tupo hapa kwa ajili ya kushiriki sherehe za kukata utepe na zitaanza muda si mrefu , tuondokeni haina haja ya kusumbuana nae”Aliongea Airami na kwa Hamza alivyomsikia mwanamke huyo, ilikuwa ni kama kweli kabisa hakumfahamu.


Hamza hakutaka kuamini kabisa kama Princess mrembo ambae alimuokoa jana alikuwa feki na huyo ndio halisi.


Baada ya Madona kuona Princess anaomba sana kwa Hamza kuachwa alikubali huku akimuonya asijekuwasogelea tena na palepale walianza kutembea kutoka.


Hamza alionekana kutokuwa na jinsi mpaka wakati huyo , kwasababu alishajitambulisha na Princess huyo kamkataa , hakuona haja ya kuendelea kulazimisha.


Hamza muda ule wakati anataka kuondoka ndani ya jengo hilo la makumbusho alihisi kuna kitu hakipo sawa na alijiuliza ni kitu gani , ila hakupata jibu.


Muda ule wakati anasogelea mlangoni alijikuta akikutana na mchoro wa Monalisa uliotundikwa ukutani na mara baada ya kuangalia mchoro ule, tabasamu la Monalisa ni kama lilikuwa linamkejeli kwa kushindwa kujua kitu ambacho kipo wazi kabisa.


Hamza palepale alijikuta akisimama na kufumba macho yake na kujiuliza tena swali , ni kitu gani nimeshindwa kuona , alianza kufuatilia kila kitu kilichotokea muda huo na kila neno alilosikia.


Baada ya dakika moja ya kufikiria palepale macho yake yalichanua akionekana kuna kitu kimemwingia akilini.


“Kumbe…!”Hamza alijikuta akiongea hivyo huku tabasamu la uchungu likimvaa.


*****


Nje ya lawns(bustani) makundi mbalimbali ya wanahabari walioshikilia kamera na maiki walionekana kusubiri.


Baada ya kuona kundi la watu maarufu na matajiri wakitoka , kamera zilianza kumulika mfululizo. Na hatimae Princess Airami alijitokeza wa mwisho na hapo ndipo kamera zilivyozidi kupiga makele ya Kacha , kacha.


Ijapokuwa tukio hilo lilikuwa ni maalumu la kukaribisha kazi ya kisanaa mpya ndani ya makumbusho hayo , lakini watu walikuwa wamewekeza umakini wao kwa princess sana.


Hususani tukio la kutekwa kwake jana usiku , waandishi wengi walitaka kujua kama alikuwa amejeruhiwa kwa namna yoyote ile.


Mara baada ya hotuba fupi. Curator na baadhi ya viongozi wa Paris, walionekana kufahamu Princess hakupenda kuonyesha sura yake kwa watu. Hivyo waliishia kumshukuru kwa kushiriki kwake na palepale walianza taratibu za kukata utepe.


Lakini muda ule vitu kama vitenesi vya chuma vilitua ardhini na kuanza kusogea uelekeo alipokuwepo Airami na watu wengine na ilichukua sekunde tu palepale vitu vile vilipasuka na kufuka moshi mzito na kubadilisha hali ya hewa kabisa ya eneo hilo la sherehe za kukata utepe.


Muda ule vilio na mayowe yalianza kusikika kutoka kwa watu mbalimbali , huku wengine wakidondoka chini na kupelekea kukanyagwa na wenzao na kusababisha eneo lote kuwa na hali ya juu ya tafrani.


“There's an intruder!" Quick, cover the princess and retreat!”Aliongea Madonna msaidizi mkuu na kisha palepale alimshika Airami mkono na kukimbia nae.


Mabodigadi walimkimbilia kwa nyuma wakiwa wametoa siraha zao kushambulia yoyote atakaekuwa kikwazo.


Lakini sasa moshi ule ulikuwa mzito mno na kufanya watu kukimbia kimbia hovyo na kuwafanya wale mabodigadi kuzongwa na sekunde chache tu hawakuweza kumuona Madonna na Princess kwenye macho yao.


Katika eneo la kutokea , Madonna alionekana akiwa na Princess wakikimbia.


“Madonna , tunaenda wapi huku?”Aliuliza Princess kwa kupaniki.


“Princess hii ndio jia ya kujiokolea ambayo tuliiandaa ikiwa chochote kitatokea . Tafadhari nifuate g kuna gari ipo mbele kwa ajili yako’”Aliongea Madonna lakini ni muda ule aliweza kuona mtu akijitokeza mbele yake.


“Kwanini ni wewe tena?”Aliuliza kwa mshangao na chuki. Aliekuwa amejitokeza mbele yake alikuwa ni Hamza.


Hamza alikuwa ameshikilia sigara na mdomo wake huku akimwangalia Madonna na tabasamu ambalo halikuwa tabasamu.


“Madam Mtumishi , unampeleka wapi Princess na haraka zote hizo?”


“Kuna dharula na tunapaswa kumuondoa hapa haraka . hebu toka njiani”Aliongea Madonna huku akitaka kukimbia na Princess kwa mara nyingine.


Lakini Hamza alimzuia kwa mkono huko akitoa sigara ile mdomoni na kuitafuna ili izimike.


“Mbona huku hakuna jia yoyote ambayo inaonekana ni ya kumuokoa, maana kama ndio njia sahihi ningeona gari maalumu ya kumchukua Princess na badale yake gari niliona pale mbele ni zile za kutekea watu”Aliongea Hamza na mara baada ya Madona kusikia vile alionekana kushituka kidogo lakini alificha hali ile haraka..


“Unaongea nini wewe , hebu pisha njia”Aliongea kwa kufoka.


“Nadhani unajua vizuri ninachoongelea. Kwanza huna haja ya kuharakisha maana watu watatu ambao walikuwa ndani ya gari , wanaume wawili na mwanamke mmoja , wote wameshapoteza uhai”


Madonna mara baada ya kusikia hivyo alijua ni kwa namna gani hawezi kuendelea tena na sura yake ilijikunja palepale na kuwa mbaya kama kalishwa sumu, huku akimwangalia Hamza kwa macho ya tahadhari.
 
Pepo mchafu.


Madona alionekana sasa kuelewa ni kwa namna gani asingeweza kuendelea, na sura yake ilibadilika ghafla, akimwangalia Hamza kwa wasiwasi.


“Wewe ni nani?” aliuliza.


“Nadhani nilishakwambia kuwa mimi ni rafiki yake Princess, lakini wewe ukadhani natokea Umoja wa Sinagogu,” Hamza aliongea huku akionyesha mwonekano wa kejeli.


Madona alikakamaa, na ingawa sura yake iliendelea kubadilika, alijitahidi kujiweka sawa.


“Sijui unachoongea,” aliongea, huku Princess Airami akimwangalia Madona kwa macho yaliyojaa mshangao wa kugundua jambo.


“Madona, ni kweli ulisema Sinagogu! Lakini katika kumbukumbu zangu, sijasema kuwa walioniteka walikuwa Wasinagogu,” Princess Airami aliongea, na Madona alijikuta akishituka, jambo lililomfanya Hamza kucheka.


“Nadhani sasa umejua ni kwa namna gani umejichanganya hadi kujidhihirisha mwenyewe. Sidhani kama kuna mtu mwingine kati yangu na Princess anayejua waliomteka walikuwa Umoja wa Sinagogu. Ulitoa maagizo nikamatwe kwa sababu ulitaka kujua siri za Sinagogu, lakini kwa mtu kama wewe ambaye ni mtumishi tu, si jambo rahisi kuzungumza… na sasa hivi ghafla tu umekimbilia upande huu ukisema ndio njia ambayo Princess alipaswa kupita kujiokoa ilihali hata walinzi wengine hawaijui,” Hamza aliongea kwa lugha iliyoeleweka kwa Princess.


Ingawa Princess Airami alikuwa na mshituko, hakuwa mjinga, na haraka sana alionyesha kukatishwa tamaa na Madona na kumwangalia kwa fadhaiko.


“Madona, kwa nini umeamua kunisaliti? Nilikuchukulia kama dada yangu na kukufanyia mazuri, kwa nini?” Madona, baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Airami, macho yake palepale yalijawa na chuki.


“Kunifanyia kwako mazuri kuna umuhimu gani kwangu? Mtu pekee ninayemtii ni Mfalme Mkuu Devasi! Na kwa kuwa mpango wangu wa kukuchukua umeshindikana, ni muda wa kukamilisha mpango B,” aliongea, na palepale akaanza kucheka kwa nguvu, kisha akamsogelea Airami na kumshika.


“Kuwa makini, ana bomu!”


Hamza aliongea wakati ambapo tayari alishamfikia Airami na kumkwepesha kutoka kwa Madona huku akimpiga Madonna teke lililomfyatua kama mpira.


“Boom!”


Teke hilo liliambatana na mlipuko ambao ulipasua korido nzima ya jengo la Louvre na kusambaza vipande vya matofali. Huku sanamu kadhaa za thamani kubwa ziliharibiwa pia.


Hamza alimkumbatia Airami kwa nguvu huku akimkinga kwa mgongo wake, akihakikisha kuwa wimbi la bomu hilo halimdhuru, na vipande vya mawe vilivyokuwa vikiruka vilisababisha nguo zake kuchanika.


Akiwa pale, aligeuza macho yake na kuangalia korido hiyo iliyoharibika, akijikuta akishikwa na hofu, na kujiuliza, Devasi ni mtu wa namna gani hata kumfanya mtu msomi kama Madona kujitoa mhanga kwa kuvalishwa bomu!?.


“Princess Airami, ulisema mwenyewe jana kuwa kuna msaliti kati ya watu wako. Inaonekana ni watu hatari sana,” Hamza aliongea huku akimshika mkono Airami na kuanza kutembea naye.


Airami alikuwa katika hali ya hofu, uso wake wa kirembo ukionyesha dalili za kupoteza rangi yake.


“Asante sana, asante sana Sir. Kama si wewe, ningekufa leo,” Airami aliongea kwa shukrani huku akinamisha kichwa na kumtazama Hamza kwa wasiwasi.


“Hujaumia?” aliuliza.


“Hapana, ni kidogo sana, usijali,” Hamza aliongea kwa furaha. “Lakini kwa nini leo uko kihadhi kiasi hiki? Sio kama jana usiku.”


“Jana usiku!?” Airami alionekana kuchanganyikiwa, macho yake yakipepesa, jambo lililomfanya Hamza kumshangaa.


“Airami, acha maigizo. Tumefahamiana tangu jana, kwa nini unaigiza kutonifahamu?” Hamza aliongea, lakini Aira alionekana kutojua kitu.


“Sir, ni kweli sikufahamu, ukiendelea hivi unanipa wakati mgumu,” aliongea, jambo lililomfanya Hamza kujikuna kichwa kwa mawazo.


“Kuna kitu unajaribu kunificha. Jana uliwezaje kupotea ghafla namna ile?”


“Sijui unachoongea kabisa,” Airami aliongea kwa sura ya unyonge ila akiwa siriasi.


Wakati huo, walinzi wa Airami walikimbia wakielekea upande huo huku wakiita jina lake. Hamza alihisi kuwa kama angeendelea kubaki pale, wangeweza kumdhania vibaya. Kwa hiyo alimwangalia Airami kwa kumkazia macho.


“Naondoka, ila najua kabisa wewe ni yule wa jana. Hutaki tu kukubali, ila muda si mrefu nitakuja na ushahidi.” Baada ya kusema hivyo, Hamza alichukua fursa ya umati wa watu na kutoka nje ya Louvre.


Baada ya kufika katika duka moja la nguo, Hamza hakujali mshangao wa muuza duka. Haraka sana alichagua nguo, akaenda kuzivaa, kisha akalipia na kuanza safari ya kurudi hotelini.


Alipofika hotelini, alikumbuka kuwa Regina alikuwa ameenda kwenye kampuni kwa ajili ya kikao, hivyo alikuwa ameboreka sana kuwa peke yake. Alitaka kwenda kutafuta mgahawa ili ale, kisha arudi kulala. Lakini aliposhuka chini, alimuona mwanamke aliyevaa nguo nyekundu ambaye alimtambua.


Alikuwa ni mwanamke aliyevaa gauni nyekundu na viatu virefu vya kisigino. Hakuwa na hereni wala mapambo mengine ambayo wanawake hupendelea kuvaa. Alikuwa ni Nyakasura, na jinsi alivyokuwa amesimama, ni kama alitaka kila mtu anayeingia na kutoka ndani ya hoteli hiyo amuone.


Kadri ulivyomwangalia Nyakasura, mwonekano wake ulikuwa ukibadilika-badilika, jambo lililowafanya wanaume wengi kumkodolea macho kwa tamaa. Hamza alimtambua mara alipokuwa akitoka kwenye lifti, lakini hakumsogelea mara moja kwa sababu kulikuwa na mwanaume mmoja mzungu aliyekuwa akijaribu bahati yake.


Lakini Nyakasura alitumia lugha aliyoifahamu na kuanza kumwongelea vibaya yule mwanaume kwa kejeli, jambo lililomfanya yule mwanaume mtanashati kufyata mkia na kuondoka.


Kitendo hicho kilimfanya Hamza kushindwa kuzuia tabasamu. Alitabasamu kwa sababu ni kama vile kitu hicho alitaka Nyakasura afanye.


“Unamwangalia nani?” aliuliza huku akimwamgalia Hamza kwa chuki kutokana na tabasamu lake. Kwa tafsiri yake, aliona Hamza alikuwa akimkejeli.


“Wewe unaonaje?”


“Angalia mtu mwingine,” aliongea.


“Hakuna shida , endelea na ratiba zako basi”Aliongea Hamza huku akimpita lakini kitendo kile kilimfanya Hamza kuhisi msisimko na palepale alimuwahi maana alijua atawasha moto.


“What the F*ck!” Hamza aliongea huku akimshika mkono na kuangalia kulia na kushoto kuona kama watu hawajaona kitu cha ajabu.


Lakini muda huo Hamza akiwa ameshikilia mkono huo aliishia kung’ata meno kwa nguvu kutokana na mkono wake kuungua kama vile alikuwa ameshika chuma cha moto. Lakini kutokana na watu kuwaangalia aliishia kutoa tabasamu la kizembe akijifanyisha kila kitu kipo sawa.


“Hey! Mrembo tabia yako ya kutaka kuwasha moto kila sehemu sio nzuri. Unadhani ukiunguza hii hoteli utakuwa sawa. Hata kama una damu ya kiphoenix viongozi hawawezi kukuacha salama”


Nyakasura aliishia kumwangalia Hamza namna alivyoshikilia mkono wake bila kuuachia na sura yake ilibadilika na kuiva.


“Mshenzi !”Aliongea kwa ukali akimpa ishara amuachie.


Hamza alijikuta akishikwa na haya na palepale alimwachia mkono wake.


“Sijakushika makusudi, nilikuwa na wasiwasi utawasha moto na kufanya watu wakuone kama kiumbe wa ajabu”


“Kwani najali , nilichotaka ni kukuunguza basi”.


“Kwa mtu aina yako kuwa na mtu kama mimi ambae unaweza kushindana nae si ndio vizuri. Ukishaniunguza utabakiwa na nini?”


“Kuna vitu vingi ninaweza kuwa navyo sio lazima uwe wewe . Nikiboreka naunguza nyumba ninayoishi au naigeuza swimming pool kuwa mvuke ..”


Hamza alijiambia huyu mrembo roho yake ni kama damu yake , lakini hakutaka kuonyesha alichokuwa akimuwazia.


“Niambie kwanini upo hapa ?”


“Nimekuja kukutafuta”


“Kwanini unitafute?”


“Nimekuja kukuchukua. Himidu kasema nikupeleke ukaonane na watu wa Malibu . Anataka tufahamiane pia upate kuelezwa mpangilio wote wa tukio zima . Sijajua kwanini mtu kama wewe wa nje wanataka ukutane na sisi lakini kwasababu Himidu na Simba ndio wamesema sina jinsi kukuchukua na kwenda kukutana nao”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo na kuona hakuwa na kitu cha kufanya aliona akubali.


“Sawa tuelekee huko”


“Nifuate”Aliongea Nyakasura akigeuka kimaringo na kuanza kupiga hatua kutoka nje ya hoteli hio.


Hamza alijua wanaenda kupanda gari ambayo imeandaliwa na kitengo cha Malibu , lakini alishangaa kuona Nyakasura akitoa simu yake na kufungua App ya Lifti kuita taksi.


“Nyakasura si ni kama upo mapumzikoni tu! Kwanini Malibu hawajakuandalia usafiri?”Aliongea Hamza akijiuliza kwa uwezo wa Nyakasura kwanini Malibu wasimwandalie gari.


“Sijataka wanipe gari! Kuna tatizo kwani?”


Hamza aliishia kutingisha kichwa na kisha muda ule alimfuata mwanamke huyo na kuingia kwenye taksi na kuondoka , lakini maelezo ya uelekeo wanaoenda aliotoa Nyakasura ulimshangaza Hamza.


“Nyakasura tunaenda Shopping mall kufanya nini? Au unataka kusema tunakutana ndani ya mall?”


“Kinchokusumbua nini kwani? Ninaanza kwenda ninapotaka kwanza. Unawapaenda sana hao watu mpaka unataka kukutana nao haraka? Kuongozana na mwanamke mrembo kama mimi unapaswa ujivunie, Ila sikulazimishi kama hutaki unaweza kuondoka”


Hamza alijihisi ni kama anaona kivuli cha Regina katika sura ya Nyakasura. Ijapokuwa mke wake kidogo alikuwa akichagua maneno ya kuongea lakini sio kama huyo kiumbe.


“Sawa mama , tunaweza kwenda unapotaka kwanza”Aliongea Hamza maana hakutaka kusumbuana nae.


Nyakasura aliishia kumpotezea Hamza na kuchezea simu yake mpaka wanafika na ile wanashuka nje ya Lafayette Shopping mall, Nyakasura alimgeukia Hamza.


“Lipia nauli!”


“Kwanini nilipie wakati wewe ndio uliita usafiri , kwanini usilipie juu kwa juu?”


“Mwanaume unapaswa kumgharamikia msichana kama mimi. Au wewe sio mwanaume?” Aliongea kwa kejeli.


Hamza alitaka kusema mimi sio mwanaume ndio, lakini alishikwa na hofu ya Nyakasura anaweza kumuunguza dereva, hivyo aliishia kutoa Euro na kushuka nje ya gari.


Mara baada ya kuingia ndani ya shopping mall hio , Nyakasura alikuwa ni kama mnyama alietolewa bandani . alikimbia hapa na pale kuchagua chagua kwa furaha kubwa.


Hamza aliishia kutingisha kichwa kwa masikitiko , ilikuwa ngumu kuamini huyo ndio mtu pekee aliekuwa akiaminiwa na kitengo chote cha Malibu kama mlinzi. Licha ya utofauti wake na binadamu wa kawaida lakini alikuwa na asili ya tabia ya kike ndani yake , ile ya kutaka kununua nunua vitu.


Nyakasura alitembea zaidi ya maduka sita ya kifahari na kununua kila kilichomvutia macho , alinunua mikoba nguo na viatu vya brand kubwa kama Givency , Parisiani , dior , Gucci na kuendelea bila kujali gharama.


Kila alichonunua akimaliza alitoa kadi ya benki ya rangi nyeusi iliodarizwa na dhahab na kuipitisha katika kimashine maalumu. Hamza aliitambua kadi hio ni Black Card ambayo hifadhi yake ya hela si chini ya bilioni tatu za kitanzania.


Hamza upande wake alikuwa akifuatisha tu kama mfanyakazi , akipokea kila kilichokuwa kinanunuliwa.


Mara baada ya kuridhika na manunuzi , walifika eneo la kukamata midoli na mashine maalumu na palepale Nyakasura macho yake yalichanua.


“Unajua kutumia hii mashine au wewe ni Mshamba?”


Hamza alijua kama wakianza kucheza na mchezo huo watapoteza muda mwingi sana.


“Mimi mshamba ndio , unaonaje tukiondoka kwanza nikaonane na watu wa kitengo cha Malibu kabla muda haujaisha?”Aliongea na kauli yake haikumfurahisha Nyakasura hata kidogo.


“Kwanini upo hivyo?”


“Nipo vipi?”


“Nimenunua kila kitu kwa hela yangu na huna ulichonifanyia , lakini nakuambia kuhusu kunikamatia mdoli hata mmoja unanikatalia. Hufai hata kidogo”Aliongea huku kiini cha mboni ya macho yake kubadilika na kumtia Hamza wasiwasi.


“Unajitilisha huruma ya nini sasa. Mimi sio mpenzi wako kwanini nikufanyie hayo yote?”Aliongea Hamza.


“Mpaka uwe mpenzi wangu ndio unisaidie . Usiponikamatia hata mmoja naunguza mashine”Aliongea akiwa siriasi na Hamza aliishia kukunja sura huku aking’ata meno. Aliona hakuwa na jinsi zaidi ya kumkamatia mdoli kama anavyotaka.


Ukweli ni kwamba aliona Nyakasura bado akili yake haijakomaa licha ya uwezo wake. Na vitu ambavyo anaweza kufanya havitabiliki kabisa .


Hamza alitumia zaidi ya lisaa kufanikisha kukamata mdoli mmoja na muda huo ndio simu ya Nyakasura ilivyoita na alivyopokea alionekana kuwa siriasi.


“Sawa..”


Nyakasura aliishia kukata simu kwa hasira na kumwangalia Hamza


“Simba kasema twende sasa hivi ukakutane na hao watu”Aliongea kinyonge na jambo lile lilimshangaza Hamza.


“Nyakasura uwezo wako ni mkubwa kuliko wa Simba , kwanini bado unamsikiliza kwa utii namna hio?”


“Sio kama namtii! Ni kwamba sitaki akiwasiliana na baba na kuanza kunisnitch”


“Baba yako!?”


Hamza alijikuta akiwa katika shauku , alitamani kuona familia ya Nyakasura ilivyo. Kwake ni kama yalikuwa maajabu na aliamini pengine kukutana na familia hio angejua kuhusu uwezo wa Prisila una uhusiano gani na Nyakasura.


Upande wa Nyakasura alionekana kama kujutia kile alichoongea na palepale, mwonekano wake ulibadilika na kuwa wa kikauzu.


“Jali mambo yako na acha maswali” Hamza aliishia kuishiwa na maneno na kujiambia moyoni kama hataki kujibu si hataki , kuna haja ya kubadilika na kuwa kama mbuzi.


Mara baada ya kutoka nje ya shopping mall , waliita taksi ambayo iliwachukua moja kwa moja mpaka kwenye hoteli ambayo timu ya kitengo cha Malibu walikuwa wakiishi.


Hamza mwanzo alifikiria timu hio ya wanajeshi wangewekwa katika hoteli ya fahari ya juu lakini ilikuwa kinyume chake . Ilionekana dhahiri walifanya maamuzi hayo kutokana na athari za kiusalama.


Baada ya kufika Hamza alidhania Nyakasura angeongozana nae kuingia ndani ya hoteli hio lakini ilikuwa tofauti.


“Unaweza kwenda sasa. Narudi zangu hoteli kulala”


Hamza aliishia kushangaa na kujiuliza kumbe majini nayo yanalala.


“Sio kama unaishi hapa na wenzako?”


“Nani aishi kwenye hoteli mbaya kama hio. Wanakaa wenyewe”Mara baada ya kuongea alimpa ishara dereva kuondosha gari.


Hamza aliishia kusimama nje ya hoteli hio kama sanamu , alijiambia ni kweli alimkubalia Simba kudili na hilo swala. Lakini kwanini ni kama amegeuka mtumwa ghafla?.


Alijiuliza kama Nyakasura hakuwa na mpango wa kushiriki kwenye kikao hicho, kulikuwa na sababu ya kumsumbua vyote vile? Alijihisi ni kama amezidi kuwa mpole ghafla kiasi cha watu kuanza kumchezea.


“Habari kaka. Utakuwa Mr Hamza si ndio?”


Hamza aligeuka na aliweza kuona mwanamke mweusi wa makamo,kama miaka arobaioni hivi. Alikuwa na nywele fupi na amevalia jacketi refu na suruali, pamoja na miwani ya macho. Alikuwa na sura ya upole mno.


“Ndio dada. Wewe ni..”


“Naitwa Rehema Mndeme ila unaweza niita tu Ray. Mimi ni Katibu muhtasi wa Balozi Rajabu. Nipo hapa kukupokea”Aliongea .


Hamza palepale alikumbuka katika ile orodha ya majina ambayo Himidu alimpatia, jina la Balozi Rajabu Salumu lilikuwepo, ambae licha ya kufahamika kama Balozi lakini vilevile alikuwa ndio chifu kitengo cha Malibu anaeshughulika na maswala yote ya kitengo katika bara la Ulaya kwa kushirikiana na idara ya mambo ya nje.


“Wewe ni mkubwa kwangu hivyo nitakuita Sister Ray”Aliongea Hamza na kumfanya Rehema kutabasamu na kisha palapale aliongoza njia kuelekea ndani.


Mara baada ya kufika floo ya sita ambayo ilikodishwa nzima kwa ajili ya kitengo hicho . Hamza alipata kuona Ma ajenti wengi wakizunguka huku na huko kuimarisha ulinzi. Walionekana kuwa na mafunzo ya hali ya juu.


Ndani ya chumba cha mikutano , kulikuwa tayari na watu zaidi ya kumi wanaume na wanawake wakiongea. Asilimia kubwa ya watu waliokuwa ndani ya eneo hilo walikuwa na umri kuanzia miaka therathini na kupanda. Ni wachache sana waliokuwa na umri wa miaka ishirini.


Mwanaume ambae alikuwa amekaa mwisho wa meza , aliekuwa na nywele ziliozojaa mvi ndio aliekuwa kiongozi wa msafara .


“Balozi! Hamza amekwisha wasili”Aliongea Katibu Rehema.


Balozi aliweka karatasi alizokuwa ameshikilia mkononi chini na kisha alisimama na kumsogelea Hamza kumpatia mkono.


“Mr Hamza , tumekusikia sana kutoka kwa Afande Simba na Mshauri mkuu na wote hapa tunafahamu wewe ni mtaalamu wa juu sana katika mapigano. Hii ndio mara yangu ya kwanza kukuona na sijadhania utakuwa mdogo hivi”Aliongea.


“Balozi Rajabu Asante kwa Ukarimu! Ila mimi ni kama Korongo pori tu, sina msaada mkubwa lakini kwasababu Himidu kaniambia nije nimeona nimpe heshima yake” aliongea Hamza na pale alionyeswa pakukaa.


Asilimia kubwa ya wanajeshi wa kitengo cha Malibu waliokuwa ndani ya eneo hilo , walikuwa wakimwangalia Hamza kwa shauku na maswali mengi. Ni kama hawakuwa wakiamini alikuwa na uwezo mkubwa wa kuaminiwa hadi akachukua nafasi ya Nyakasura.


“Baraza la maksi litafanyika siku chache zijazo . Nimesikia kutoka kwa Himidu ukiachana na kikao rasmi , sina haja ya kushiriki katika maandalizi mengine na nyie , si ndio?”


“Ni kweli kabisa Mr Hamza na ukaribisho wako hapa sio kwa ajili ya maandalizi , tumeona kwasababu tunakwenda kufanya kazi pamoja,itakuwa vizuri tukifahamiana mapema ili isiwe ngumu siku ya tukio.Wengi wetu hapa ni mara yetu ya kwanza katika kushiriki katika kongamano hili na tumesikia wewe unao u zoefu mkubwa , hivyo tungetamani kuuliza na kupata majibu ya maswali machache”


Mara baada ya Balozi kuongea hivyo , palepale alianza kutambulisha watu wote katika meza kwa majina na vyeo vyao . Nusu yao wote walikuwa ni wanajeshi ndani ya kitengo cha Malibu na wengine walikuwa ni Secret service agent kutoka TISA(Tanzania intelligence security agency) na wapo hapo kama wawakilishi wa usalama.


Mtu ambae alikuwa na madaraka makubwa zaidi ndani ya eneo hilo ukiachana na balozi, alikuwa ni Amoni Mboma maarufu kama Afande Mboma. Alikuwa ndio mkuu msaidizi wa idara ya siri ndani ya TISA. Licha ya kuwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa lakini vilevile alikuwa na mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi kuliko watu wote waliokuwa katika eneo hilo.


Kwa mpangilio wa madaraka, Mboma alikuwa namba mbili baada ya Balozi Rajabu, utofauti ni kwamba tu alikuwa ni kama kapteni na pengine alibeba siri nyingi kuliko hata ilivyo kwa balozi.


“Mr Hamza kwasababu unaonekana kama una haraka , basi sitozunguka sana na nitaenda moja kwa moja. Sababu tuliokuitia hapa ni kwasababu tuna matumaini utatusaidia. lakini niwie radhi kwasababu mpaka sasa sijajua ni kwa namna gani unakwenda kutusaidia”aliongea Afande Mboma huku akijikakamaza na kisha akaendelea.


“Awamu hii ushiriki wetu katika Baraza la maksi unakwenda kuwa wa tofauti na vipindi vyote tulivyoshiriki . Siku hizi taifa letu linamiliki Earth Axis , kitu ambacho kimetafutwa sana baada ya vita ya pili ya dunia mpaka sasa.


Sababu ya kwanza , ushiriki wetu ni kwa ajili ya kulinda hadhi ya nchi na jeshi letu. Sababu ya pili ni kwamba tunahitaji kushiriki katika mazungumzo ya kidiplomasia ya aina zote ili kujihakikishia hatuna maadui wengi.


Tatu na muhimu zaidi tutaangalia uwezekano wa kushirikiana na taasisi kubwa kutoka katika maeneo mengine ya nchi kubwa kwa ajili ya matumizi mazuri ya teknolojia kutoka ndani ya Earth Axis. Katika misheni hii usiri mkubwa unahitajika na kwasababu ni misheni inayohusisha taarifa nyingi adimu za kiteknolojia kutoka kwenye Earth axis, juhudi kubwa itakuwa kwenye swala zima la ulinzi kwani ni hakika jambo hili linamuweka kila mmoja wetu hapa katika uhatari, hususani kipindi hicho ambacho tupo katika mgogoro na Pentagon.


Ukweli mpaka sasa sijajua ni kwasababu gani Mkuu wa majeshi pamoja na Himidu wamekualika. Labda ni kutokana na ushindi uliotupatia kule kiswani Chole. Na kama ni hivyo tunashukuru sana kwa mchango wako, lakini hata hivyo uwepo wako inamaanisha tutakwenda kuwa wakali zaidi”


“Mzee Mboma! Hamza ametusaidia kiuungwana kabisa kule Chole, lakini kwa maneno yako kwanini ni kama vile unamdhalilisha na kuonyesha kama hastahili kuwa hapa??”Aliongea Balozi.


“Sio kama namdhalilisha , kitu ambacho sielewi mpaka sasa, kwanini wanasema Hamza anaweza kusaidia kulinda watu wetu na kulinda taarifa . Mnapaswa kuelewa kikosi cha Zero Delta alichopambana nacho hakukuwa na mtaalamu hata mmoja. Hata kupitia washirika wao walituhakikisha hawakutuma wale wanajeshi wa juu kabisa. Tumekuja hapa na Nyakasura hivyo hata kama itokee watumie wataalamu wa hali ya juu kimapigano hakuna wa kumuweza . Lakini kwanini imani yote ipo kwa Hamza na sio kwa Nyakasura?. Mimi aona kama tukimtegemea Hamza na tukashiriki baraza la maksi hatokuwa na msaada zaidi ya hasara tu”.


Hamza alimsikiliza bwana huyo bila hisia zozote , hakuongea neno,ukweli ni kwamba kwa kiasi flani wasiwasi aliokuwa nao Mboma ni ubinadamu kutokana na kwamba ilikuwa ngumu kwa Himidu na Simba kutoa taarifa zake kwa wepesi. Hivyo ni kama hakuna ambae alikuwa akijua uwezo wa Hamza upo vipi na ni kawaida kuhoji.


Waliona inawezekana Hamza kweli ni mtaalamu , lakini ni mtaalamu tu kama mwanajeshi aliefunzu ukomandoo bila nguvu za ziada.


“Afande Mbona unachojaribu kumaanisha ni kwamba uwepo wangu unaweza kuwa mzigo kwenu si ndio?” Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu ambalo halikuwa tabasamu.


“Mr Hamza usikasirike . Mzee Mboma ni mwepesi kuonyesha wasiwasi wake ila sio kwa nia mbaya. Wasiwasi wake ni kama tunaweza kuingia matatizoni”Aliongea Balozi Rajabu.


“Mr Hamza naheshimu sana mashujaa na watu wenye nguvu. Wewe ni shujaa ulieshinda vita kule kisiwani Chole . Lakini awamu hii hatuijui nafasi yako katika kampeni yetu na ni kwa namna gani unaenda kutusaidia” Aliongea Afande Mboma.


“Ukweli hata mimi sjiui naenda kuwasaidia vipi?”Aliongea Hamza akiwa hana wasiwasi kabisa na kauli yake hio ilimfanya kila mmoja aliekuwa katika kikao hicho kumwangalia mwenzake wa pembeni.


“Labda ni kwasababu nina marafiki wengi wa kimataifa na kama lolote litatokea wanaweza kusaidia . Ila tu kama kampeni yenu itaenda sawa na hakuna chochote kitakachotokea na hakuna nchi wala taasisi ambayo itajiingiza na kuibua usumbufu , maana yake sitofanya chochote” Aliendelea kuongea.


“Mr Hamza una ushahidi gani wa kutuaminisha kwamba una koneksheni ya kutosha kimataifa?. Operesheni yetu awamu hii ni kama tunatembea katika barafu nyembamba. Nchi na taasisi kubwa duniani wanatuangalia kwa ukaribu sana.”


“Mzee Mboma kama unataka nikuthibitishie kuhusu hilo ,muda sina. Sipo hapa kwa ajili ya kuomba kushiriki na nyie. Niwaambie tu sivutiwi kabisa na hilo baraza la maksi. Hivyo kama mnaona kuambatana na mimi kutawaongezea mzigo, basi sidhani kama kuna haja ya kuendelea kushirikiana, najitoa kiuungwana tu”Aliongea Hamza
 
Hamza mara baada ya kuongea hivyo , palepale alisimama kwa ajili ya kuondoka , lakini muda huo Rehema ambae alikuwa amebeba kikombe cha kahawa kwa ajili ya Hamza aliingia na alishangaa kumuona Hamza anataka kuondoka.


“Mr Hamza unaondoka baada ya kufika tu?”Aliongea na Hamza alichukua kikombe kile na bila kujali kahawa ilikuwa ya moto ama ya baridi aliipiga yote kwa mkupuo kama maji na kisha akampatia kikombe chake.


“Sister Rehema , asante kwa jitihada zako , ila mimi ndio naondoka hivyo”


“Mr Hamza tafadhari usikasirike! Mzee Mboma ndio alivyo , ila tunahitaji sana msaada wako. Mimi naamini Afande Simba na Afande Himidu kukualika hapa ni kwasababu wanazo sababu zao za msingi”Aliongea Rajabu.


“Balozi huna haja ya kuwa na wasiwasi. Kwasababu nilishakubaliana na Himidu, nitatimiza baadhi ahadi zangu. Lakini kutokana na baadhi yenu tofauti ya kuongea kuhusu ushirikiano ila mnaanza kunihoji, sioni haja ya kuendelea kubakia hapa”Aliongea Hamza na Balozi Rajabu alikuwa na wasiwasi mno.


“Mzee Mbomba ni vizuri ukimwomba radhi Mr Hamza”


“Muache aondoke kama anataka , lazima amechaguliwa kwasababu za kindugu . Kama hana vigezo kwanini tumlazimishe. Kwa uzee wangu huu nishaona watu wengi wa aina yake. Kama wasiwasi ni juu ya ulinzi nitaweka mpango mzuri kwa kushirikiana na majasusi ndani ya Kitengo cha usalama . Pili Baraza la maksi licha ya kuwa la siri lakini pia limeundwa kwa ajili ya kuimarisha amani duniani baina ya makundi , sidhani kama itatokea mtu akataka kutuvamia bila sababu”


“Mzee.. kwanini ni mgumu sana kuelewa…” Balozi alishindwa kujua cha kufanya baada ya kuona Hamza ameshaondoka tayari na haraka sana alimpa maagizo sekretari wake kumsindikiza Hamza.


Katika kikao hicho Balozi alizidi kumshutumu Mboma , kwamba alifanya makusudi kumfanya Hamza kuondoka. Akienda mbali na kusema hata kama Hamza amechaguliwa kutokana na koneksheni na Mshauri mkuu hakupaswa kuongea kwa namna ya kumdhalilisha.


Ukweli ni kwamba watu wote wlaiokuwa katika kikao hicho walikuwa na mtazamo sawa na Mboma. Walikosa tu ujasiri wa kuelezea hisia zao , ila Hamza alionekana wa kawaida sana licha ya kuwa maarufu kupitia tukio la Kisiwani Chole.


Walipata kusikia tu habari za kisiwani na hakuna hata mmoja hapo ambae aliona Hamza akipambana moja kwa moja.


Mboma upande wake hakujali kile ambacho Balozi anaongea na aliishia kukunja midomo kumkejeli , akiamini kabisa alichofanya ni sahihi.


Upande wa nje Rehema alifanikiwa kumuona Hamza akitaka kuingia kwenye taksi na alimwita kwa kumkimbilia.


“Mr Hamza tafadhari usijali sana juu ya kilichotokea. Wote tunamjua mzee Mboma ni mtu anaeongea bila ya kufikiria , hususani likija swala la ukaribu wako na Himidu”Aliongea.


“Kuna tatizo gani mimi kuwa na ukaribu na Himidu?”Aliuliza Hamza


“Afande Mboma alikuwa moja ya watu waliokuwa wakiaminiwa sana na Afande Simba , lakini baada ya kutokea kwa Himidu nafasi yake ilichukuliwa na akaanza kujiona sio wa muhimu tena mbele ya wakubwa. Hakuwahi kupenda namna ambavyo Himidu alipanda cheo haraka haraka mpaka kufikia kuwa mshauri mkuu”Aliongea Rehema.


“Ndio maana , kumbe nimejiingiza katika ushindani wao?”Aliongea Hamza akitingisha kichwa lakini hata hivyo aliona hayo hayamuhusu. Kwanza mwanzoni hakutaka hata kushiriki na ni hila tu za Afande Simba.Ila hata hivyo hakutaka kuweka mambo moyoni kutokana na kile ambacho Mboma alisema kuhusu mpango wa jeshi kutaka kugawa baadhi ya taarifa zinazhohusianisha teknolojia ndani ya Earth Axis, aliona kuna haja ya kuwa siriasi kwani lolote lingetokea, ingekuwa hasara kwa serikali na wasingeridhishwa nae.


Hamza hakujali sana , alipanga kufuatilia swala hilo kwa namna anayoijua yeye, hivyo palepale aliagana na Rehema ambae alikuwa akiomba radhi kwa niaba ya Mboma mpaka anatia huruma.


Hamza hakupanga kurudi hotelini na badala yake alimpa uelekeo mwingine dereva nje kabisa ya jiji mpaka kumfanya dereva yule kushangaa kidogo.Wakati akiwa njiani, Hamza alipokea simu kutoka kwa Afande Himidu.


“Bosi nimesikia kilichotokea . Mboma ni mtu mgumu sana kuelewa licha ya cheo chake na ni mtu wa kukuza hata vitu vidogo visivyo na maana,naomba usimzingatie sana”


“Nawezaje kukasirika kwa kitu kidogo namna hio? Unawaza sana na wewe”Aliongea Hamza huku akicheka.


“Haha.. bosi nilikuwa na wasiwasi tu utaacha kunisaidia ndio maana. Bosi kama sio uwepo wako ndani ya Tanzania sidhani tungekuwa na amani mpaka sasa”Aliongea Himidu.


“Wewe ni muhuni sana , kwahio kumbe hili kongamano lenu lina mpango mwingine wa kugawa siri za Earth Axis lakini ukakaa kimya. Au ulitaka nije kuyajulia hukuhuku?”


“Haha.,. samahani sana bosi , tumeamua kuvujisha taarifa za Earth axis makusudi kurahisishia kazi , ila naamini kwa uwezo wako hakuna tatizo kabisa”


“Hakukuwa na utofauti hata ungeniambia mapema. Ila taarifa mlizowabebesha hawa wanajeshi ni kama kuwashikisha kiazi cha moto”


“Upo sahihi , ila taarifa ambazo tumetoa ni za juu juu sana kuhusiana na mazingira na mfumo mpya wa viwanda na mbinu nyingine za kuboresha zaidi maisha ya binadamu . Hata kama watuibie hawataweza kutengeneza siraha za hatari. Hivyo sidhani kutakuwa na shida kubwa”


“Lazima itakuwa mbinu uliofikiria , mnataka kutoa ushirikiano wa kugawa teknolojia ambayo haihusiani na mambo ya siraha ili kujiimarisha kidiplomasia na kuongeza ushawishi wenu katika siasa ili msiwe wanyonge katika kupambana na nchi kubwa kama Amerika. Himidu hata kama hii mbinu yako itafanya kazi pointi ya msingi ni kwamba , hata wakijua mnachotaka kugawa hakina uhusiano na utengenezaji wa siraha na mambo mengine , unadhani watakubali?. Lazima watafikiri mnajaribu kuwasaidia China na Urusi mahasimu wao wakubwa kiuchumi na kijeshi ili kujijenga, hivyo sidhani kama watakubali kupitwa kirahisi ?”


“Ndio maana tunakutegemea wewe bosi , mazungumzo haya yakikamilika, tutakuwa na washirika wengi kutoka mataifa makubwa na mikataba mingi itasainiwa. Na kwanzia hapo tutakuwa hatuna hofu tena kama taifa dogo, hata kama tukiwa katika ushirikiano mbaya na America lakini bado tutakuwa na sapoti ya kutosha kujilinda kutoka kwingine. Wasiwasi wangu ni kama ambavyo nimekwambia bosi , tunahofia kabla ya makubaliano, taarifa za Earth Axis zitakuwa zimekwisha kuvuja mahali tusipotaka zifike kupitia mashushu wao ndani ya jeshi letu na kama kila mtu akiwa na hizi taarifa za kiteknolojia zitakosa thamani na itakuwa ngumu kufanya makubaliano na haya mataifa na wakakubali”Aliongea na kumfanya Hamza kutaka kucheka.


“Tabu zote hizo ni kwa ajili ya kutaka kunufaika mwenyewe na Earth Axis! Unadhani utaweza kuificha mpaka mwisho , si mshirikiane tu ?”


“Bosi mpango sio kwa ajili ya kuhimili mpaka mwisho , tunachotaka ni kupata muda wa kutosha wa kujijenga , tukifikia hatua ya kuwa na teknolojia ambayo hakuna mwingine alienayo, hakuna taifa litaweza kutugusa kirahisi. Hii ni bahati yetu kuinuka kiuchumi kama taifa na Arika nzima. Licha ya kwamba itakuwa safari ndefu yenye vikwazo vya kila namna”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo , alionekana kuwa katika hali ya kuwaza , ukweli alichokuwa akimaanisha Himidu ni kwamba wanahitaji muda wa kutosha kwa ajili ya Yulia kukwamua kila taarifa iliopo ndani ya Earth axis.


Aliona Yulia alikuwa na kazi ngumu sana, maana kwa mpiganaji kama yeye alichoweza zaidi ni kuufanya mwili wake kuwa imara zaidi na kufikia levo za juu lakini sio katika maswala ya teknolojia.


“Bosi ..”Aliita Himidu mara baada ya kuona Hamza ameacha kuongea na alishindwa kujua anachowaza ndio maana aliita kwa nguvu.


“Bosi lazima utakuwa umekasirika si ndio?”


“Hapana , kuna kitu nilichokuwa nikifikiria , ila niseme umenipa hamasa”Aliongea Hamza


“Hamasa gani bosi?”


“Kufunuliwa ni chanzo cha hamasa , usiulize sana, na usiwe na wasiwasi, japo sipendi kuwasaidia katika mipango yenu ila kwa ajili yako sina jinsi zadi ya kwenda kuonana na Roho Mchafu”


Himidu mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akishangaa na palepale alianza kucheka.


“Haha… , boss kweli unashangaza mno , umefikiria la maana sana. Kwasababu upo Paris sio mbaya kuonana mshikaji wetu , usisahau kunifikishia salamu zangu kwa Roho mchafu”


Hamza hakuendelea hata kujibishana na Himidu tena na palepale alikata simu ile.


Taksi ile iposimama Hamza ni kama alikuwa nje kabisa ya jiji la Paris kutokana na eneo hilo kuwa kama limetelekezwa hivi.
Majengo mengi yaliokuwa katika eneo hilo yalikuwa ni yale ya kale na yenye kuota uozo.


Hamza mara baada ya kusogelea upande wa kulia kuingia katika majengo , watu wengi walikuwa wakimnyooshea vidole na ilionekana walikuwa wakiongea kwa kumtukana.


Lakini hata hivyo Hamza hakuonekana kujali kabisa na aliendelea kutembea kukata mitaa na mara baada ya kuingia katika uchochoro wa nyumba mbili pande kwa pande ndio jinsi aeneo hilo lilivyozidi kuwa tulivu na watu kutoonekana.


Hamza alitembea katika uchochoro huo bila ya wasiwasi , akionyesha alikuwa akijua anakoelekea na dakika chache mbele aliweza kutokezea kwenye uzio uliokuwa na geti kubwa la chuma la rangi nyeusi.


Getini hapakuwa na mlinzi , hivyo Hamza alipita na ile anafika ndani aliweza kukuta eneo kama vile ni mapokezi ya hotelini ndani ya jengo hilo lililoenda hewani na kulikuwa na mtu eneo la Kaunta , mzee hivi mzungu, aliekuwa amelala fofofo na kupiga miayo , ilionekana alikuwa amelewa pombe chakali.


Pembeni ya kaunta kulikuwa na vyungu vya maua ambavyo mimea yake ilionekana kukauka kutokana na kukosa maji . Kulikuwa na vipisi vingi vya sigara katika vyungu hivyo.


Ni eneo ambalo lilikuwa na uchafu ambao sio wa kawaida na giza tupu na hio yote ni kutokana kati ya taa chafu za glasi ambazo zimening’inizwa, ni mbili tu ambazo zilikuwa zinawaka na mwanga wake ulikingwa na kutu.


Hamza baada ya kusogea kwenye lile eneo la kaunta alipeleka mkono na kuvuta kitabu kilichokuwa pembeni ya yule mlevi , lakini ile anavuta tu mwanaume yule mzungu alikikandamiza na mkono wake bila kuinua uso kuangalia nani anavuta kitabu huku akiendelea kupiga usingizi.


Hamza aliishia kutoa tabasamu na kujiambia huyu mzee lazima atakuwa anaota na palepale hakutaka kumchelewesha kwani alivuta kile kitabu kwa nguvu na kumsukuma na kumfanya adondoke chini kama furushi na palepale ndio alishituka na kujua kumbe kulikuwa mgeni.


Alisimama haraka haraka na kumwangalia Hamza na kisha alichukua karamu na lile daftari.


“Unaitwa nani?”Aliuliza kwa kifaransa.


“Hamza”


“Sijui linavyoandikwa , hebu andika mwenyewe”Aliongea na kumsogezea Hamza karamu na daftari.


Hamza alitamani kucheka kwa visingizio vya mzee huyo , lakini hata hivyo aliandika jina lake.


“Raisi wako yupo?”Aliuliza Hamza na mzungu yule mara baada ya kusikia Hamza akiuliza hivyo alimwangalia kwa macho ya uchunguzi.


“Unamtafuta raisi wangu kwa ajili ya kukumbushia yaliopita?”


“Ndio , sisi ni mrafiki”


“Lakini ametoka”Aliongea.


“Ameenda wapi?”Aliuliza Hamza akiona hakuwa na bahati.


“Mbugani”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo , alionekana kukumbuka kitu palepale na kutabasamu.


“Kama ni hivyo nitamsubiri”Aliongea na palepale yule mzungu alinyoosha kidole kuelekea kwenye korido iliokuwa na giza.


“Chukua huo uelekeo kwenda mbele , utaona ofisi ya Raisi , unaweza kuingia na kupumzika”Aliongea yule mzungu bila kujali Hamza ni nani na Hamza mara baada ya kuondoka palepale aliendelea kulala.


Hamza alichukua korido hio mdogo mdogo akijali mambo yake na mara baada ya kutembea ndani zaidi hatimae aliweza kukuta eneo ambalo kulikuwa na bendera mbalimbali zilizosimamishwa pembeni , pamoja na medali zilizofungiwa kwenye kabineti za makabati ya vioo.


Kama mtu angeangalia medali hizo kwa umakini, asingekosa maneno haya: World number one Assassin Guild - Baffold (Shirika namba moja duniani la Wauaji - Baffold), World Ranking of Assassins (Cheo cha Dunia cha Wauaji), Golden Blade Awards (Tuzo ya Upanga wa Dhahabu), World Assassin Guild (Shirika la Dunia la Wauaji), Best Trade Union – Baffold Annihilations (Muungano Bora wa Biashara – Baffold Annihilations), Assassin Guild Lifetime Achievements Awards – Asmuntis (Tuzo za Mafanikio ya Maisha ya Shirika la Wauaji – Asmuntis), Honorary Chairman of the Assassin's Society – Asmuntis (Mwenyekiti wa Heshima wa Jumuiya ya Wauaji – Asmuntis).


Ilikuwa ni kawaida sana kwa kundi la kimauaji kupokea medali za aina hio , hasa kwa yale ambayo yanashikiria namba moja duniani.


Asilimia kubwa ya bendera ambazo zimening’inizwa zilikuwa ni kutoka kwa wateja ambao waliridhika na kazi na namna ya kushukuru kwa kazi nzuri mara nyingi hutuma bendera ya nchi misheni ilipofanyikia na kukamilika.


Kadri wingi wa bendera ulivyo ilimaanisha idadi ya waliokufa , ambao wengi wao ni viongozi wakubwa wa kisiasa na matajiri. Kulikuwa na bendera hadi ya Tanzania katika makabati hayo.


Hamza wakati huo akikagua hizo medali na bendera macho yake yalionyesha kuwa na hali ya majuto na kuridhika , akisifia ndani kwa ndani kwa kusema Roho mchafu umefanya kazi nzuri ya kuendeleza kuwa mchafu.


Ukiachana na medali hizo pamoja na bendera , kulikuwa na vyumba tofauti katika korido hio , vingi vikiwa ni vya mafunzo , Gym na hata swimming pools.


Kwa bahati ukiachana na maeneo mengi kuwa machafu eneo la mafunzo ya kulenga shabaha lilikuwa safi mno.


Hamza mara baada ya kusogea ndani ya eneo hilo kuchungulia aliweza kuona watu wengi wa kila rangi watoto na watu wazima wakiwa bize kujifunza namna mbalimbali za kimafunzo na kwa macho ya haraka tu walionekan mafunzo yao sio kwa ajili ya ulinzi bali kummaliza mtu.


Hamza alitembea kuvuka eneo hilo na kwenda ndani zaidi katika mlango wa mbao , usiokuwa na loki kabisa na kisha akausukuma na ile anaingiza mguu mmoja kuingia ndani , mwili ulimsisimka kwa kuhisi hatari , lakini hakujizuia na kukubali kile kinachokwenda kumtokea.


Na pale pale kisu kikali kiliwekwa shingoni kwake na aliekuwa amemuwekea kisu hicho alikuwa ni mwanamke alievalia nguo za kininja za kumbana huku akiwa hana utani hata kidogo.endelea nayo bure:- SEHEMU YA 186
 
Raia mmeuchuna kimya utadhani mi ndo nna Arosto pekeyang
Mzee unadai kama unalipia?
Wakati kitu chenyewe ni Kwa hisani tu ya mwandishi,ukiona anachelewa lipia utumiwe namba hiyo apo juu,watu wanakua na shughuri nyingine za kuwaingizia kipato sio mda wote awaze kukuletea wewe simulizi ya bure hapa.
 
Mzee unadai kama unalipia?
Wakati kitu chenyewe ni Kwa hisani tu ya mwandishi,ukiona anachelewa lipia utumiwe namba hiyo apo juu,watu wanakua na shughuri nyingine za kuwaingizia kipato sio mda wote awaze kukuletea wewe simulizi ya bure hapa.
Naelewa procedure mkuu that's why I'm begging ivi unadhani ningekuwa na hiyo pesa ningejisumbua kupiga kelele hapa kwenye jukwaa? Sometimes ina muencourage mwandishi na kuona kuna wafuatiliaji makini though nishawahi kulipia episode za mwanzo ila kusomea simuizi apa jf kuna raha yake,
Au na ww arosto zinakuchanganya ukiona notification unahic ni singano?
 
Mzee unadai kama unalipia?
Wakati kitu chenyewe ni Kwa hisani tu ya mwandishi,ukiona anachelewa lipia utumiwe namba hiyo apo juu,watu wanakua na shughuri nyingine za kuwaingizia kipato sio mda wote awaze kukuletea wewe simulizi ya bure hapa.
Pia naomba utengue kauli hiyo mi sijadai ila nimeomba tu huruma ya mwandishi indirect way, tuliza kipwinto🤗
 
Back
Top Bottom