Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Ila wabongo😅😅
Mmepewa link kbs ya kujimiminia venye mnataka lakn bado mnaweka MB za 2000 kuja kusoma kipande kimoja wakt ukilipia tokeni hyo 2000 unasoma mpk ujichokee 🙌🙌
 
Kuna kitu unatuficha mdau😅🤣😅🤣🤣🤣🤣😅🤣🤣🤣🤣
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI :SINGANOJR.

SEHEMU YA 178.

Al-Maestro.

Hamza akiwa katika hali ya usiriasi , alinyanyua ngumi yake na kumuonyesha Mahmoud.

“Utakula nyama kwa hiari yako au unataka kula ngumi? Nitahesabu mpaka tatu chagua.. moja … mbili “

Mahmoud alionekana mdogo kama piritoni na hata ongea yake ilikuwa ni ya kigugumizi.

“Nitakula nyama , nitakula nyama”Aliongea na haraka sana alichukua nyama mbichi na kwa kujikaza na kichefu chefu aling’ata pande.

“Ng’ata pande kubwa kubwa , usipoimaliza yote ndani ya dakika moja , nitaanza kuvunja miguu yako”Aliongea Hamza.

Mahmood alikuwa akilia . Machozi yalitengeneza mfereji kabisa huku akitafuna nyama mbichi na kilio cha kwikwi , akijutia kumchokoza kichaa kama Hamza.

Mwanzoni aliwaza Hamza ni Mwafrica tu ambae amekuja matembezini kama ilivyo kwa watalii wengine. Isitoshe siti ambayo walibook ndani ya mgahawa huo ilikuwa ni ya kawaida sana . Lakini nani angejua atageuka kuwa kama hivyo!.

Mahmood aliendelea kutafuna nyama mbichi na hakuthubutu hata kupumua . Alijilazimisha kumaliza pande lote ndani ya dakika, alijihisi kichefu chefu , lakini Hamza alichukua pande lingine la nyama ya Bata mzinga na kumuwekea.

“Hebu malizia na hiki kipande kidogo cha nyama ya Bata mzinga , nyama yake ni laini sana , hivyo maliza ndani ya dakika moja”Aliongea Hamza huku akiwa na tabasamu , lakini tabasamu lake kwa watu wengine lilionekana kama vile ni tabasamu la shetani.

Mahmood alitamani kuacha lakini kila alipoangalia ngumi ya Hamza aliishia kujikakamua na kuendelea kula.

Mara baada ya kumaliza kula nyama ile, Hamza alichukua Ini la Bukini ambalo halijaiva na kumuwekea kwenye mdomo wake huku akimwambia Mahmood atamalizia na matunda baadae.

Watu kuangalia tu midomo ya Mahmood iliojaa damu ya nyama walijikuta wakihisi kichefu chefu.

Meneja kuona vile , aliona hali haipaswi kuendelea vile na haraka sana alifanya mawasiliano na mwenye mgahawa kuwahi kurudi ili kutatua suala hilo.

Upande wa Regina alikuwa na wasiwasi wa kitu kimoja , alijua kama Prince Maxim atafika , nini kitamtokea Hamza?.

Muda huo aliokuwa akiwaza kundi la wanausalama waliovalia suti na visikilizishi masikioni waliingia kwa kasi kutoka nje.

Mara baada ya Mahmood kuona kundi la hao wanausalama palepale alijikuta akiona waokozi wake wamewasili hatimae na ujasiri ulimrejea palepale na kusimama.

“Kaka , kaka niko hapa, niokoe”

Aliingia mwanaume alievalia kanzu ambae pia alikuwa na kiremba kichwani huku akiwa amevalia cheni kubwa ya madini ya Almasi na Dhahabu . Alikuwa akisindikizwa na ulinzi mkali mno na uso wake ulikuwa na ile hali ya hadhi ya juu.

Regina na wengine wote walimfahamu mtu huyo ni nani. Alikuwa ni Kaiser Maxim, mtu ambae alionekana mara nyingi katika taarifa za habari.

Max hata yeye alikuwa katika moja ya Club karibu na maeneo hayo. Alikuwa katikati ya mazungumzo ya kibiashara na mataikoni wakubwa wakati akipokea distress signal kutoka kwa mdogo wake na ndio kwa haraka sana aliongoza kundi hilo la walinzi kufika hapo.

“Wewe ni nani na unathubutu vipi kudhalilisha familia yetu?”Aliongea kwa kufoka kwa kutumia lugha ya kingereza.

Kundi lote la wanausalama walitoa siraha zao na kuzikoki tayari kwa kushambulia.

Fomesheni yao ya ulinzi iliwaogopesha kila mtu kasoro Hamza tu ambae alikuwa katika hali ya utulivu kabisa.

Mahmood palepale aliona sasa ni muda wa kutamba na kumshikisha adabu Hamza , hivyo kwa haraka sana alikimbilia upande wa kaka yake.

Lakini sasa ile anakimbia kumsogelea kaka yake chakula kilichokuwa tumboni kwake kiliamka na alishindwa kujizuia na kujikuta akitapika damu nyingi iliochanganyika na vitu vya njano kwa spidi kama ni bomba la maji limepasuka.

Maxim ambae alitaka kumsogelea mdogo wake alijikuta akirudi nyuma kukwepa matapishi yale . Kitendo hicho kilimfanya kuona ni udhalilisho wa kiwango cha juu sana kwa familia ya kifalme ya Saebia na alijikuta akizidi kuwa na hasisra zidi ya Hamza.

“Wewe ni nani na umemfanya nini mdogo wangu?”Aliuliza kwa hasira.

Hamza kama kawaida yake hakuwa na wasiwasi na alitemeba kutoka ndani ya chumba hiko binafsi huku akipishana na mitutu ya bunduki iliokuwa imeelekezwa kwake.

“Muulize mdogo wako atakuhadithia kwanini nimefanya hivi . Hasira zangu sasa zimeisha naona ni muda wa kuondoka”Baada ya kuongea hivyo alimsogelea Regina.

“Tuondoke zetu”Aliongea

Regina alikuwa na wasiwasi bado lakini aliishia kutingisha kichwa na kumfuata Hamza.

Josh alifuata nyuma nyuma pia na kila kiungo ndani ya mwili wake kilikuwa kikitetemeka , alishukuru tu hakujikojolea, maana kwenye maisha yake hakuwahi kuwa katika mazingira ya kunyooshewa bunduki nyingi namna hio.

“Yaani unataka kuondoka baada ya kumdhalilisha mdogo wangu? Mvunjeni miguu”Aliongea Maxim kwa sauti.

Kundi la wale wanausalama haraka sana walielekezea bunduki zao kulenga miguu ya Hamza na ile wanataka kulipua Hamza alikuwa ametoweka mbele yao na kujikuta wakigeuza vichwa vyao kumtafuta alipo na hapo ndipo walipongudua alikuwa tayari mbele ya Maxim.

Kila mtu aliona ni miujiza imetokea kwa namna Hamza alivyotoweka na kuibukia eneo lingine na kumkaba Maxim shingo.

“Samu-kum”(Your highness!)

Walinzi wale walijikuta wakimaka na kuongea kwa sauti kwa lugha ya kiarabu.

“Kaka!” Mahmood nae alijikuta akishikwa na ukichaa na kupiga makelele”Wewe mwanaharamu usiniambie unataka kumuua Crown Prince? Unataka kusababisha vita?”Aliendelea kuongea Mahmood.

Maxim ujasiri ulimpotea palepale na macho yake yalishikwa na woga, lakini hadhi yake kama Mfalme Tarajiwa ilimfanya kujikakamua.

“Kama unao uwezo wa kuniua niue , ila siwezi kukuogopa”Aliongea kwa ujasiri wa kiarabu.

Meneja wa mgahawa huo alikuwa akiogopa kiasi kwamba alianza kuhema kwa shida. Huyo alikuwa ni Crown Prince mfalme mtarajiwa wa nchi ya Saebia , moja ya watu matajiri na wenye ushawishi mkubwa duniani. Lakini Hamza amemshika shingo kama vile ameshika shingo ya kuku.

Kama angemuua lisingekuwa swala tu la kukamatwa na kwenda jela , lingekuwa swala pia la kuibua mgogoro baina ya mataifa bila kujalisha Hamza ni raia kutoka nchi gani.

Regina alihisi ni kam moyo wake unataka kumtoka . Alijikuta akiacha kujali kitu chochote na alimsogelea Hamza na kumshika mkono kwa kubembeleza.

“Hamza mwachie . unachotaka kufanya ni jambo la hatari”Aliongea.

Hamza aligeuza kichwa chake na kumwangalia na alivyoona namna alivyofubaa na hali ya woiga iliomshika aliishia kulazimisha tabasamu.

“Usiwe na wasiwasi nitadili na hili swala”Aliongea

“Wewe.. unajaribu kufanya nini kwani?” Regina alikuwa ni mfanyabiashara tu , haijalishi vipi asingetaka kumchokoza mtu kama Prince Maxim maana hata nchi yake inaweza kumtelekeza.

“Usiwe na wasiwasi , hakuna kibaya kitakachokukuta”Aliongea Hamza akimtaka Regina kutulia na palepale aligeuka na kumwangalia Maxim na tabasamu ambalo halikuwa tabasamu.

“Kwahio unasema huogopi kifo?”Aliuliza Hamza huku akimwangalia kwa macho ya kejeli.

“Ndio”Aliongea huku uso wake ukiwa mwekundu.

“Sio mbaya naona angalau una kifua. Haishangazi kwa Azzle kukubali kuwa mshauri wa mfalme wa Saebia”Aliongea Hamza huku akimwachia Maxim.

Hali ya mshangao ilimshika Maxim palepale huku ikifuatiwa na hali ya kutokuamini.

Walinzi wale mara baada ya kuona Hamza amemwachia Prince walitaka kushambulia lakini Maxim aliwapa ishara ya kutulia.

“Msishambujlie”Aliongea

Walinzi hao walijikuta wakishangaa na kujiuliza Prince amekuwa mjinga? Hio si ndio fursa ya kumdbiti huyo muuaji?.

Maxime macho yake yalionekana kuchanua na alishusha sauti yake chini na kumuuliza Hamza;

“"Mister, you …. You know the State Al--Maestro?”Aliuliza akitaka kufahamu kama Hamza anafahamiana na mtu anaeitwa Al--Maestro ambae jina lake ni Azzle kama Hamza alivyotaja.

Ukweli ni kwamba swala hilo lilikuwa nyeti mno. Al=Maestro ni mtu ambae alikaribishwa ikulu miaka miwili iliopita na cheo chake kilikuwa cha siri ndani ya jumba la kifalme.

Watu wanaofahamiana na huyo Al--Maestro ukiachana na Maxim mwenyewe wengine ni watu wa juu zaidi wa maswala ya kiusalama na kwa mtu kama Mahmood hakuwa akifahamu jina la Azzle. Pengine alimuona ndani ya jumba la kifalme mara moja ila hakumjua kazi yake na jina lake ni nani.

Sababu ni moja tu mtu kama huyo ikifahamika katika serikali za nchi nyingine kubwa kama mtu huyo anatumikia familia hio ingeleta paniki sio tu kwa mataifa makubwa lakini kwa rasi ya uarabuni yote kwa kumuogopa. Kwasababu historia ya mtu huyo ya mafanikio yake ilikuwa ikifahamika wazi mpaka akapewa jina la Shujaa wa Vita ya rasi.

Upande wa bwana huyo kukaribishwa makao makuu ya nchi na mfalme sio kwasababu ya maswala ya kivita lakini ni kwa ajili ya kuilinda familia ya kifalme kupitia matishio mbalimbali , lakini pia alipewa cheo cha Mwalimu wa taifa na kazi yake ni kumwandaa kimaarifa na kibusara Prince Maxim kwa ajili ya utawala wake ujao.

Sasa mtu kama Hamza kujua siri ya taifa kama hivyo, halikuwa swala jepesi jepesi kwa mtu wa kawaida kulifahamu , ilihali hata serikali ya Marekani haijui.

“Namjua ndio , lakini sikuwahi kujua kwanini alikubali kuwa Mshauri wa mfalme labda uniambie wewe. Kwa ajili yake nitawasamehe leo hii”Aliongea Hamza.

Hamza aliona ni swala la kawaida kwa kaka mkubwa kulinda hadhi ya familia yake ma kumsaidia mdogo wake , hivyo hakuona haja ya kumdhuru na yeye pia.

“Sir una urafiki na Mshauri wa Mfalme? Kama kweli una urafiki nae basi wewe sio mtu wa kawaida. Kwaninii sijawahi kukuona Saebia hata siku moja?”Aliuliza Maxim.

“Kama sijakutana na huyo mtu kwa miaka mitatu , kwanini unione ndani ya Saebia?”

“Lakini najuaje kama kweli una urafiki na Mshauri wa mfalme?”Aliongea Maxim huku akikunja sura.

“Ushaanza kuongea ujinga sasa . Nishaawaambia kama isingekuwa kwa Azzle mnadhani wewe na mdogo wako mngetoka hapa mkiwa hai?”Aliongea Hamza.

Pembeni Mahmood alikuwa asharudiwa na pumzi , maana alitapika mpaka kizunguzungu kikamshika na mara baada ya kusikia maneno ya Hamza alionekana kutokuelewa kinachoendelea.

“Kaka anamzungumzia nani?”Aliuliza.

“Hebu kaa kimya. Huyu bwana anaweza kumfahamu mtu ambae yupo karibu sana na familia ya kifalme, mtu muhimu sana kwetu”

“Nani huyo kaka , mbona sielewi?”Aliuliza

“Ni Azzle shujaa wa vita ya rasi”Aliongea kwa kumnong’oneza Mahmood.

“Nini!” Ijapokuwa Mahmood hakuwahi kumuona Azzle ana kwa ana, lakini alishawahi kusikia jina lake kutokana na umaarufu wake.

“Kaka haiwezekani , unajua watu kutoka Africa wanajua sana kudanganya wakiwa katika hatari”Aliongea asiamini.

Hata Maxim mwenyewe alikuwa na shaka kama Hamza alikuwa akifahamiana na Aziza(Azzle au Azazel). Isitoshe maneno ya Hamza hayajanyooka kabisa.

“Mr subiri kidogo , nitampigia Mshauri mkuu wa mfalme kuthibitisha”Aliongea huku akitoa simu yake na kujiandaa kupiga simu.

Hamza alishindwa kuongea chochote . Kama ni kipindi cha nyuma angekuwa ashaua tayari , lakini muda huo alikuwa amebadilika na alikuwa akizingatia sana matokeo.

Hata hivyo aliona sio mbaya kwa Azzle kupigiwa , angetumia nafasi hio kusalimiana nae.

Haikuchukua dakika nyingi mawasiliano yaliunganishwa

“Al--Maestro samahani kwa usumbufu … Ni kwamba kuna bwana mmoja hapa kutokea Africa anasema mnafahamiana .. Ah . sawa , unataka kuongea nae? , Oh sawa sawa Al--Maestro..”

Maxim hakuongea zaidi , hata hakumtambulisha Hamza kwa jina lake alisema tu mtu kutoka Africa lakini Azzle alionekana kufahamu mara moja na kuambiwa ampatie huyo mtu simu.

Hamza aliishia kutabasamu tu , aliona bwana huyo akili yake ilikuwa ikifanya kazi mno kama mwanzo kama maneno machache hivyo yamemfanya kuotea ni yeye.

Hamza alichukua simu ile na kabla hata hajaongea chochote sauti upande wa pili ilisikika.

“Bosi ni wewe?”

Hamza mara baada ya kusikia sauti hio alijikuta akipumua kwa ahueni.

“Umejuaje ni mimi?”Aliuliza Hamza . Ijapokuwa sauti ya Azzle ilionyesha kuwa katika utulivu lakini pia ilikuwa na kitetemeshi.

“Sally alinipigia simu juzi . Aliniambia anahitaji msaada wa kumtafuta mjane wa Dokta Genesha , Serena. Nimesikia pia unakuja Ulaya na nilikuwa nikikusubiria kwa hamu tuonane”Aliongea Azazeli au Azzle.

Hamza palepale alielewa, ilionekana washikaji zake wote walikuwa na taarifa anaenda kushiriki kwenye baraza la Maksi.

“Sawa nimekuja Ulaya , ila usije nitafuta maana sitaki usumbufu. Nimekuja kwa muda mfupi tu na nitarudi tena Tanzania kuendelea na maisha yangu. Msimamo wangu ni uleule mimi ni mstaafu”

“Tatizo bosi vijana wangu wote wamejiandaa kukupokea , wewe ni kama mwalimu wao moyoni na wanatamani kujifunza chochote kutoka kwako”

“Azzle nimesema hapana , sawa?”Aliongea Hamza huku akishindwa kujua acheke ama alie “Tangu lini nikawa mwalimu , kwanza kundi lako la kimasenati si linafanya vizuri tu?”

“Ni kutokana na msingi uliotujengea ndio maana tunaendelea kufanya vizuri, Kama sio kwa kutumia jina lako nisingeweza kukusanya wanajeshi wengi kutoka pande zote za dunia. Watu wamejiunga na Barhams kwasababu wanataka kukutumikia wewe na sio mimi. Bosi kwahio huna mpango kabisa wa kurudi?”Aliuliza kwa shauku.

“Bosi najua unasita lakini ulimwengu umebadilika sana , hata kama ukirudi sio kwamba tutazunguka na kuhama hama . Tunaweza kuwa na furaha pamoja”Aliendelea kuongea.

“Kama ulivyosema ulimwengu umebadilika ndio maana nimefanya maamuzi mengine . Isitoshe kila maamuzi ninayofanya yana sababu zake”Aliongea Hamza.

“Kama unasema hivyo bosi , sina jinsi , nitaendelea kulinda kazi yako na hadhi yako kwa nguvu zangu zote”

“Basi sawa , tuachane na hayo kwanza na ongea na huyo Prince wako mjinga aache kunisumbua”Aliongea Hamza na kumrushia simu Maxim.

Kutokana na lugha waliokuwa wakitumia Maxim na wengine wote hakuna alekuwa akijua ni kitu gani wanaongea , lakini bado alihisi hali ya heshima kutoka kwa Azzle kwenda kwa Hamza.

Alijiuliza kama ulikuwa ni urafiki tu kwanini bado ni kama Azzle alionekana mdhaifu kwa Hamza.

“Al--Maestro. Napaswa kufanya nini?”Aliuliza.

“Kama sio kwa Mfalme baba yako kunialika kuwa mwalimu wako , ungekuwa mfu dakika hii , Samu-kum

“Unamaanisha nini?”Alishangaa.

“Kama sio kwa ajili yangu , huyo bwana alieyeko mbele yako,angeshakuua wewe na mdogo wako bila wasiwasi , na asingejali kuhusu wasifu wako hata kidogo , hata kama angekuua mfalme asingethubutu kuweka rehani familia ya kifalme kwa ajili ya kulipa kisasi”Aliongea Aziza Al-Maestro kikauzu.

Aliongea kwa kuchuja sana maneno yake , kwa maana nyingine Hamza aliekuwa mbele yao alikuwa akitoa vitisho tu na hakutaka kwenda mbali kwa kujali uwepo wake.

“Huyu mtu ni nani?”

Swali hilo liliibuka katika kichwa cha Maxim , maana ilikuwa ni ngumu mtu anaemheshimu kama Al-Maestro ana mtu wake pia anaemheshimu zaidi , tena mtu mwenyewe akiwa kijana zaidi , palepale halmashauri yake ilifanya kazi na macho yalimtoka. Au ndio yeye?.

Jasho jepesi lilianza kumtoka huku akimwangalia Hamza kwa wasiwasi na kidogo tu angedondosha ile simu kwa woga.

“Asante sana Al-Maestro .. ndio najua sasa kosa langu”Aliongea na kisha palepale alikata simu huku sura yake ikijawa na radhi.

“Sir naomba unisamehe sana sana . Kaka yangu amefanya jambo baya na kufanya wewe na watu wako kupata usumbufu . Kama hujaridhika unaweza kuendelea kumuadhibu”

“Aaah Kakaa!!” Mahmood alishituka “Una uhakika na unachofanya, kwanini unamsaidia yeye na sio mimi?”

Regina , Meneja wa mgahawa na wengine walikumbwa na hali isioelezeka. Walijiuliza kwanini hali imegeuka kwa nyuzi 180 baada ya simu moja tu? Na badala yake ni Crown Prince Maxim aliekuwa akimuogopa Hamza!.

Maxim aliishia kumwangalia mdogo wake kwa macho makali na palepale alishika kichwa chake na kumuinamisha chini.

“Piga magoti na omba msamaha , la sivyo nitakuua hapa hapa”

Hakuwa na jinsi , hilo ni swala ambalo lilikuwa likigusa usalama wa taifa na kwa ufalme mzima na hakutaka kufa kwa ujinga wa mdogo wake.

Kwenye ulimwengu huu kuna nguvu ambazo huwezi kushindana nazo iwe ni kwa hela au madaraka , Max aliyafahamu hayo yote na aliona kama Hamza ndio moja ya zile nguvu anazofahamu basi hakuna namna zaidi ya kuomba huruma, la sivyo watakuwa hatarini kama wakiungana na kushambuliwa.

Ijapokuwa Mahmood ni mwenye kiburi , lakini siku zote alijua kaka yake sio mtu wa utani . Aliona swala hilo litakuwa siriasi kuliko alivyofikiria na licha ya kutopenda aliishia kupiga magoti chini na kumuomba msamaha Hamza na Regina.

Regina aliishia kuziba mdomo kwa mshangao huku macho yakiwa yamemtoka.Ni kama alikuwa ndotoni akiombwa msamaha na Prince wa Saebia.

Mrembo huyo alijikuta akimwangalia Hamza na aligundua alikuwa mtulivu kabisa na hakuonyesha wasiwasi kama kwamba alikuwa amezoea.

Mshituko ambao Hamza alimpelekea Regina haukuwa wa kawaida kabisa, ulikuwa umefikia daraja ambalo ni ngumu kufikiria. Licha ya kuishi na Hamza aliungana na wengine wote na kujiuliza Hamza ni nani?. Alikumbuka kwenye ndege Hamza alisema anafahamiana na wafanyabiashara wengi wakubwa na yeye aliona zilikuwa tambo tu lakini muda huo haikuwa hiari yake kuamini tena.

Bwana Joshua aliishia kufikicha macho yake pekee na kuendelea kujificha ili kutoka usingizini. Hakutaka kuamini Hamza ndio msaidizi wa Regina.

“Tuondoke . Hili swala limeisha ila inasikitisha hatujashiba”Aliongea Hamza akimwangalia Regina ambae alikuwa katika mshangao.

Regina hakujali tena alikuwa ameshiba au hajashiaba , akili yake muda huo ilikuwa ikizunguka . Alitamani kuondoka haraka katika hilo eneo na kwenda kutulia kufikiria upya.

Mwanamfalme Maxime alimpisha Hamza na alimsindikiza kabisa mpaka nje na ile wanatoka tu gari aina ya Cadillack Kare nyeusi ilisimama mlangoni na mwanaume katika mavazi ya upishi alishuka haraka sana.

Yule mzee wa kizungu mara baada ya kumuona Hamza macho yake yaligubikwa na machozi ya furaha na alikimbia akitaka kupiga magoti na kuongea lakini Hamza alimuwahi akihofia bwana huyo ataongea kitu ambacho hapaswi kuongea.

“Mathayo za siku nyingi?”Aliongea akimshika mkono huku akimpa ishara ya kutomwita kwa majina yake. Mathayo palepale aliangalia kundi la watu waliokuwa nyuma ya Hamza na alionekana kuelewa na palepale alitingisha kichwa.

“Ndio Sir, ni muda mrefu hatujaonana , nimekumiss sana . Wewe Bernadi hebu acha kushangaa na uje usalimiane na huyu mtu wa heshima”

Kijana Bernard haraka sana alisogelea kwa kukimbilia alipo baba yake na kutoa salamu kwa heshima.

“Salamu kwako Mr , Mimi na baba ni heshima kubwa kupata ugeni wako katika mgahawa wetu”Aliongea.

Muda huo meneja wa mgahawa na kundi la wahudumu walisogelea . na sasa walionekana kuamini Hamza alikuwa akifahamiana na wapishi hao.

Prince Maxima alionekana sasa kukubali zaidi na alimwangalia Mahmood kwa chuki kwa kumharibia koneksheni yake. Alijiambia kama sio kwa ujinga wake angejenga ukaribu na Hamza.

Aliamini kuwa na urafiki na mtu kama huyo ingekuwa na faida kubwa kwa familia yao ya kifalme na kwa uongozi wake ujao.

“Sir! Umefanikiwa kupata chakula? Tumekuja haraka haraka na tumekosa muda wa kukuhudumia”Aliuliza Bernard

“Nimekula kidogo tu , ili kuelewa zaidi mnapaswa kumuuliza meneja wenu”Aliongea Hamza na muda ule Mathayo alimwangalia Mahmood.

“Your Royal Highness , nilijua utaelewa maana yangu kwa kutoa maagizo waandaliwe chakula . Sikutarajia bado utaendelea kuwachokoza”Aliongea na Mahmood aliishia kuinamisha kichwa chake chini kwa aibu akitamani kuwe na shimo atumbukie.

“Sir naomba unipe nafasi mimi na baba yangu tukuandalie chakula.Limekuwa hitajio letu la muda mrefu, siku moja kukuhudumia”Aliongea Bernard.

Meneja na wahudumu walishangazwa na kauli hio , siku zote mabosi zao ndio waliokuwa wakibembelezwa na watu kupika lakini leo hii wao ndio wanabembeleza mtu kumpikia.

“Itakuwa usumbufu sasa , na mgahawa umechafuka tayari , msiwe na wasiwasi tunaweza kununua chochote hata Mcdonalds na kula”Aliongea Hamza.

Watu wa pembeni kidogo tu watapike damu , yaani mpishi wa nyota tatu za michellin anaomba kukupikia halafu unakataa na kusema unataka kwenda kula Mcdonalds. Yanaweza kuwa maneno ya Hamza kutotaka kuwasumbua wapishi hao , lakini ilikuwa tafsiri nyingine kwa mpishi.

“Tafadhari Sir , Nyumba yetu ipo karibu na hapa , kwanini tusiende, tutaharakisha chakula ndani ya muda”Aliendelea kubembeleza.

Regina ambae alikuwa nyuma ya Hamza alishindwa kuvumilia baada ya kutafsiriwa na Josh na alisogea mbele na kumshika Hamza mkono.

“Hebu acha kuwa hivyo , huyo ni mpishi wa daraja la juu duniani na anaomba kukupikia kwanini unamuumiza kwa kumkatalia”Aliongea kwa kiswahili.

SEHEHMU YA 178.

Ukweli ni kwamba Regina alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua Hamza ana hadhi gani kiasi cha kuifanya familia ya kifalme kutoka Saebia na wapishi hao kuwa na wasiwasi namna hio? Hivyo aliamini pengine anaweza kumfahamu Hamza zaidi kama angeenda nyumbani kwa Mathayo kwa ajili ya chakula.

“Sawa, nitakusikiliza wewe twende nyumbani kwa Mathew”Aliongea Hamza akimkubalia Regina.

Hamza alichukuana na Regina na kuingia ndani ya Cadillac , Kuhusu Josh yeye alisikia aibu kuongozana nao na alisema atataungulia kurudi nyumbani , isitoshe aliona watu ambao walialikwa kwenda nyumbani kwa wapishi hao ni Hamza na Regina pekee.

Joshua alizingatia hadhi yake, kama angeng’ang’ania kuongozana nao basi ataonekana kama mtu ambae hajui kusoma mazingira.

Hamza alifurahia pia uamuzi wake maana uwepo wa bwana huyo ulimzuia kumchokoza Regina.

Wakiwa njiani Mathayo aliuliza kumjua Regina ni nani hasa na mara baada ya kusikia Regina ni mke wa Hamza yeye na mtoto wake walishangaa mno na haraka sana walimsalimia tena kwa heshima.

“Ms Regina tafadhari tusamehe kwa kutokukufahamu , hatukutegemea utakuwa mke wa Mr Hamza , ni heshima kwetu kukutana na wewe”Aliongea Mathayo.

Regina alionekana kuzidiwa na heshima hio , kwenye maisha yake hakuzoea hisia za kunyenyekewa tena na waznngu . Muda huo alijiona kama Cinderella ambae amekwea hadhi ghafla na kuwa Princess.

Ingawa Regina alikuwa tajiri lakini bado alikuwa ni mwanamke wa kawaida ambae hajawahi kuwa katika daraja la kunyenyekewa.

“Mr Paco huna haja ya kuwa hivyo , mimi ni mfanyabiashara wa kawaida, hata msijali sana”Aliongea Regina kwa kingereza.

“No, you are the wife of this lord, you must be incomparably respectful!”Alikazia Mathew akimwambia Regina anastahili heshima kwa kuwa mke wa Hamza.

Regina alijikuta akijichokea mara baada ya kusikia hivyo . Aliishia tu kumwangalia Hamza kinyonge.

“Hamza wewe ni nani kwani?”Aliuliza kinyonge.

“Wife achana nao hao , ni sahihi kwao kukuonyeshea heshima , unaweza kubali tu”Aliongea Hamza , aliona ghafla tu kumwelezea Regina yeye ni nani isingewezekana, maana hakujua pa kuanzia na alimwambia wataongea siku nyingine.

Regina aliona Hamza hakuwa tayari kumwambia yeye ni nani bado.Alihisi uchungu lakini hakutaka kuuliza zaidi.

Mara baada ya kufika nyumbani kwa Mathayo , nyumba yake ilionekana kama Apartment usanifu wa ki-baroque. Lilikuwa jengo la orofa tatu na lote ilikuwa ni miliki ya Paco familly.

Muda ambao Hamza na Regina walishuka kutoka kwenye gari , wanawake watatu walitoka wakiongozana na mtoto kuwakaribisha na Mathew aliwatambulisha mmoja baada ya mwingine . Wa kwanza kumtambulisha alikuwa ni mke wake Agani kisha binti yake na Mke wa mtoto wake . Ijapokuwa wanawake hao hawakufahamu ubini wa Hamza lakini Mathew aliwapa maelekezo kumkaribisha kwa ukarimu mkubwa kwani ni wageni wa heshima.

“Agani unajua huyu Mr Hamza ndio mtu ambae nilikuwa nikikuambia sana , Mtu muhimu kwangu ambae alinisaidia sana na biashara yangu ya migahawa? Kama isingekuwa yeye mgahawa wetu ungenyakuliwa na wezi muda mrefu na tusingekuwa na maisha tulionayo sasa”Aliongea Mathayo akiwa na ari kubwa.

Agani mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akimaka kwa mshangao .

“Kumbe mfadhili wetu ni mdogo kiasi hiki?”

Familia hio walikuwa wakijua kilichotokea kipindi cha nyuma kidogo . Na kutokana na hilo kila mmoja alitoa tabasamu la ukarimu kuonyesha shukrani zao kwa Hamza.

Upande wa Regina hakuelewa chochote kwasababu lugha iliokuwa ikitumika ni kifaransa.

“Mnaongea nini?”Alimuuliza Hamza.

“Ni kuhusu Mathew , alikuwa maarufu kwa muda mrefu sana hivyo matajiri wengi walimtaka kuwa mpishi wao binafsi. Mathew hakutaka kwani alihitaji kuendelea na biashara yake ya mgahawa nakuwa karibu na familia yake hivyo aliwakatalia. Sasa kipindi flani kuna bwana mmoja tajiri hivi alitaka kununua mgahawa wake kinguvu na kumtaka Mathew kumfanyia kazi chini yake . Lakini kwa bahati nzuri au mbaya huyo tajiri nilikuwa na kinyongo nae na nikaamua kumsaidia Mathew na ndio tukaja kufahamiana”

“Ukweli kwangu sijali sana. Wao wananichukulia kama mfadhili lakini mimi niliona niwasaidie tu bure”.

“Kulikuwa na haja ya kwenda mbali hivyo kwa ajili tu ya kumfanya mpishi wao?”Aliuliza Regina.

“Haha..Wife wewe huelewi ndio maana. Kuna watu wanahisi wakishakuwa ni matajiri na wenye madaraka, wanadhani wanaweza kupata kila kitu na ikitokea wamekosa watatumia kila namna . Vinginevyo wataonekana vipi kuwa matajiri?”Aliongea Hamza

Regina aliishia kupepesa macho tu , ijapokuwa mwonekano wa Hamza ulikuwa ni tulivu lakini aliona Hamza alikuwa tofauti kipindi cha nyuma. Vinginevyo familia hio ya Paco wasingekuwa na shukrani namna hio.

Mara baada ya kuingia sebuleni , Bernard na Mathew haraka sana waliingia jikoni . Isitoshe walikuwa wapishi na kwao majukumu kama hayo hawakuyachukulia kama ya mwanamke, na nyumbani walikuwa na kila viungo walivyohitaji kwa ajili ya kupika chakula kitamu. Hawakuishia kulisha watu tu vyakula vitamu lakini vilevile walijitahidi kulisha familia zao chakula kitamu pia.

Hamza na Regina walikaribishwa ndani na wanawake hao , lakini walishangaa hao wazungu hawataki kukaa na badala yake waliishia kusimama pembeni tu kwa heshima. Regina mara baada ya kuona hivyo hakujisikia vizuri hata kidogo.

“Jamani kaeni , kwanini mmesimama?”

“Cheo cha Mr Hamza ni kikubwa mno , bila ya ruhusa yake hatuwezi kuthubutu kukaa nae meza moja”Aliongea Agani.

Hamza kusikia hivyo alijikuta akiishiwa na maneno , aliona mbona ni kama wanamtia wasiwasi Regina tu , aliishia kuwapa ishara ya kutokujali.

“Mimi sijawazuia kukaa , mkiendelea kusimama hivyo sidhani tutaweza kula chakula kwa amani”

“Asante Sana Mr Hamza”Aliongea Agani akimchukua mtoto wake na kukaa chini , akifuatia Mke mwana.

Nyumba ya Mathew ilikuwa imepambwa kwa tamaduni za kifaransa zaidi, mtindo wake ulikuwa ni ule wa zamani lakini wenye kupendeza macho mno.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Regina kuingia kwenye nyumba ya mfaransa . Kuangalia tu mapambo na finishing kila kitu kilikuwa kipya kwake. Alikuwa akijiamini hivyo alianza kuongea na Agani na kwa bahati nzuri wote walionekana kufahamu kingereza.

Haikuchukua muda mrefu Mathew na Bernard walianza kuandaa vinono mezani , kulikuwa na kila aina ya chakula ikionyesha ni kwa namna gani walikuwa siraisi sana na chakula, mpaka kuwa na mahitaji mengi namna hio nyumbani.

Regina mara baada ya kuona chakula hiko , alijikuta akiona kilipendeza macho zaidi ya kile alichoona kule mgahawani.

“Agani nenda kalete Romanee conti yangu ya thamani kubwa ile kwa ajili ya Mr Hamza na mke wake Ms Regina”Aliongea Mathew na kisha palepale alimwangalia Hamza kwa tabasamu “Mr Hamza ninazo chupa za Romanee-Conti za umri wa miaka kumi na tatu kwenye hifadhi yangu na huu ndio muda muafaka wa kuzifungua , ukija tena nipo tayari kukupatia kama zawadi”Aliongea.

Hamza hakuwa masikini , alikuwa ameonja kila aina ya mivinyo na hakujali pia thamani yake . Lakini siku hio kwasabau ya Regina aliona ngoja mrembo huyo aonje radha yake.

Romannee-Conti huwa zinazalishwa chupa elfu tano mpaka elfu sita tu na ni maarufu sana na watu matajiri walipambana kuzipata. Ijapokuwa Regina alikuwa tajiri lakini alitokea Tanzania na kwa hulka yake sio mtu mwenye kuwa exposed sana na mambo ya namna hio. Lakini kwa nchi kama hio ya Ufaransa kwa matajiri kunywa vitu adimu ndio hadhi na furaha kubwa.

Chupa moja mara tu baada ya kufunguliwa ilijaza harufu nzuri ndani ya eneo hilo. Ilikuwa ni harufu kama ya maua ambayo ilisisimua mapafu.

Wakati wa kumiminwa kwenye glasi ilikuwa imebadilika rangi yake, nyekundu ilikuwa imeiva kiasi kwamba ilikuwa kama nyeusi na wekundu ulionekana kwenye michirizi yake pekee na kuifanya kweli ionekane ilikuwa ya thamani.

“Come, let's all drink a little. Good wine needs to be shared in order to taste good.”Aliongea Hamza akimaanisha mvinyo mzuri uwe ni ule wa kugawana ili radha yake kuwa tamu.Aliwakaribisha na wanafamilia hao ili pia waonje.

Mathayo na wenzake walikubali lakini walijizuia kunywa kwa wingi , walikuwa ni kama wanaionja tu.

Regina upande waka hakuwa mpenzi sana wa vileo . Ila kuona namna mvinyo huo unavyovutia alishindwa kujizuia na kunywa kiasi na alijikuta akishangaa huku tabasamu likimtoka.

“Hamza hii wine ina radha ya Strawberry kabisa , Ndio wametumia kutengenezea?”Aliongea Regina kwa kiswahili akishindwa kuzuia furaha yake.

Familia haikumwelewa kabisa anachoongea , lakini kupitia tabasamu la Regina waliona kabisa alikuwa ameipenda. Lakini kwa wakati mmoja wakivutiwa na tabasamu la Regina maana ni kama ua linalochanua katikati ya jangwa.

Upande wa Hamza mara baada ya kusikia kauli hio ya Regina alijikuta akicheka. Mwonekano wa Regina ulikuwa ukifurahisha mno na ilimchekesha zaidi baada ya kuona sababu ya mvinyo kuwa na radha ya strawberry ndio maana anaona ni mtamu zaidi, alimuona kama mtoto jambo lililomfanya kufurahi zaidi.

“Mke wangu kumbe unakuwa mshamba muda mwingine . Unafananisha vipi wine na radha ya strawberry . Hio inatokana na mchakato wa kuitengeneza , huwa kuna radha ya kiasili inajitokeza yenyewe . Muda mwingine mvinyo unaweza kunukia harufu ya waridi , muda mwingine unanukia maganda ya miti , vyote hivyo haimaanishi imetengenezwa kwa aina ya mimea, ni ufundi tu”Aliongea Hamza.

“Sasa mimi nayajulia wapi yote hayo wakati sijawahi kuonja wine ya hivi..”Aliongea huku akivuta mdomo.

“Hata mimi sijawahi kuonja , lakini kwasbabu najua mchakato wa kutengeneza wine ndio maana najua”Aliongea Hamza na Regina alikunywa tena.

"It's really delicious!”

“Wife taratibu , unapaswa kuiweka mdomoni kwanza ndio uimeze”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kuona kweli utamu ulikuwa ukimchanganya na kuonekana kama vile alikuwa akinywa maziwa.

Muda ule Hamza aliwaambia Mathew mke wake ni kichaa wa Strawberry na mara baada ya Mathew kusikia hivyo palepale alionekana kupata wazo.

“Ms Regina , Kijana wangu ametengeneza keki ya Strawberry juzi . Nadhani utaipenda”Aliongea na Regina mara baada ya kusikia hivyo macho yalichanua.

“Keki ya Strawberry! Hio nadhani itakuwa tamu zaidi’Aliongea na Bernard palepale alisimama.

“Ngoja nikakuletee”Aliongea.

“Thank you”

“It’s my honor”Aliongea Bernard na kisha kwenda kumletea Regina.

Regina alionekana kuwa na furaha kuliko vile alivyotarajia Hamza na aliona wazo la kuja kwa Mathew kwa ajili ya chakula lilikuwa sahihi mno.

Hamza aliona pengine nyumbani Regina hakuthubutu kupumzika sio kwasababu hakutaka bali kutokana na presha kubwa ya kazi na matarajio ambayo wengi wanayatarajia kutoka kwake , hivyo inamfanya kutoonyesha upande wake wa pili.

Nje ya nchi . alikuwa amezungukwa na watu ambao ndio kwanza anafahamiana nao na hawakuhusiana na kazi , hivyo hakujali ni mkurugenzi tena. Hali hio ilimfanya kujiachia mno na kuzidi kuvutia.

Usiku wa kwanza wa chakula cha usiku ndani ya nchi ya Mafuvu. Ingawa ni kwa kuchelewa sana lakini kilikuwa cha kuridhisha mno.

Regina mara baada ya kupewa keki ya Strawberry furaha yake iliongezeka zaidi na kumfanya aonekane kama malaika. Tabasamu lake usoni ni kitu ambacho Hamza alitamani kuona kila siku.

“Methew na Bernard chakula cha leo kimemfanya mke wangu kumuona akiwa na furaha kubwa kwa mara ya kwanza , napanga kwenye harusi yetu niwaalike kuwa wapishi”Bernard na baba yake mara baada ya kusikia hivyo walilipukwa na furaha mno. Ilikuwa ni heshima kubwa sana kwao.

Hamza aliongea kwa kingereza kabisa ili kumfanya Regina kuelewa na mrembo huyo mara baada ya kusikia aliishia kuona aibu kidogo huku akijiweka bize na chakula . Aliona aibu hata ya kumwangalia Hamza usoni, alikuwa kama msichana wa darasa la saba ambae kwake mapenzi ni kitu kipya kabisa.

Baada ya chakula Hamza na Regina walirudi hotelini kupitia gari ya Mathew.

Kwasababu ilikuwa tayari ni usiku sana Hamza alimshika mkono Regina akiwa hawana wasiwasi kabisa wa kuonekana kwa watu na kuingia ndani ya lift.

“Umeridhika na chakula cha leo?”Alimuuliza Regina wakiwa ndani ya lift.

“Ule mvinyo na ile keki ni vitamu mno..”

“Haha..unanifurahisha unavyochizika na strawberry. Yaani vyakula vyote vile vilivyokuwa vitamu kwako wewe ile keki ndio tamu zaidi. Inabidi nikununulie kikapu kabisa cha matunda na siku nyingina haina haja ya kuwasumbua Mathew kupika vitu vingi”Aliongea Hamza.

“Pale hata sikuwa nikielewa kifaransa mlichokuwa mkiongea , halafu unajua kabisa mimi sio mpenzi wa nyama”

“Kwa staili hii utakosa kula vitu vitamu sasa kwa kuendelea kung’ang’ania strawberry tu . Unapaswa kuonja baadhi ya vyakula vingine na utajikuta unagundua ulimwengu una vyakula vitamu nje ya matarajio yako”Aliongea Hamza lakini kauli yake ni kama ilimkumbusha Regina matukio ya siku hio.

“Mhh! Kwani kuna ubaya gani nikipenda kula Strawberry , nimezaliwa na mama maskini na sijazoea vyakula vya bei ghali , sipendelei Cavier sijui white truffle na vinginevyo . Kama hupendi ninachopenda siku nyingine nenda mwenyewe”Aliongea Regina huku akitoa kwa nguvu mkono wake kwa Hamza.

Hamza alijikuta akipatwa na mawazo , hio haikuwa nia yake kuongea hivyo.

“Wife usinielewe vibaya nilichoku…”

“Huna haja ya kujielezea najua hadhi yangu ni ya chini sana na sio kama wewe , Kila mtu unaefahamiana nae ni maarufu na mtu wa kuheshimika, kwanzia washonaji nguo , Madaktari , wapishi hata Mwanafalme wa Saebia anakuonyeshea heshima… Ila mimi ni mwanamke wa kawaida sana najua kuongea kingereza tu .. lakini wewe mwenzangu kila unaefahamiana nae ni mtu mzito . Kupenda kwangu kula Strawberry , keki za strawberry na donati nimemkosea nani mpaka unikejeli . Unanidharau kwasababu ya hobi yangu ya kimasikini?”

Hamza alijikuta akikosa maneno , alijiuliza yametokea wapi hayo , si sekunde chache zilizopita walikuwa na furaha . Kwanini ghafla tu anaonyesha kisirani.

“Wife.. usiwe na hasira , sijamaanisha hiyo..”

“Nishakuambia usijielezee! Mimi najua kabisa unanidharau , unaniona mimi ni mwanamke mshamba na mjinga”

Muda huo lift ilifika katika floor husika na Regina alitoka kwenye lift na kumwambia Hamza asimame hapo hapo asisogee.

“Naenda kupumzika , usije kunifuata”

Hamza asingekubali kutii alichoongea . Aliona anapaswa kujielezea vizuri la sivyo usingizi hautopanda.

Ukweli hata yeye hakujua ni wapi alikosea na alikuwa katika mshangao wa usiku wao mtamu kugeuka na kuwa mchungu ghafla.

Wahenga wanasema moyo wa mwanamke ni kama sakafu ya bahari. Ilikuwa ni kweli, hivyo Hamza alijitoa ufahamu na kuanza kuomba msamaha licha ya kutojua kosa lake.

“Wife nisamehe , nimekosea mimi jamani …..sitorudia tena , punguza jazba, sikuwa nikidharau hobi yako , Wife wewe ni muhimu sana kwangu, nashukuru sana Mungu kunikutanisha na wewe…”

“Sitaki hata kusikia , kwanzia tunakutana mpaka sasa unaniona mshamba , wakati nadharau baiskeli yako ulikuwa ukicheka ndani kwa ndani kumbe ina thamani ya gari . Unanifanya najiona mjinga kila saa”

Hamza alijikuta akishindwa hata kujielezea , ilikuwa ngumu kwa wakati ule kumwelezea baiskeli ilikuwa na thamani kutokana na historia yake na aliona hata kama angeelezea Regina asingeelewa , hivyo hivyo kwa zile nguo na mengineyo.

Hamza hakupata mawazo kwasababu Regina kakasirika , alipatwa na mawazo kwasababu hakujua namna ya kumbembeleza.

“Wife ni kweli nilikosea , unaonaje ukinifokea tu au nipige basi. Ila tu usiwe na hasira , sasa hivi unaweza kula chochote unachotaka na sitokuuliza..”Aliongea Hamza akiwa na tabasmu la kizembe.

“Mimi sitaki kukusikiliza , naenda kupumzika . Kwaheri”akiwa na uso wa ukauzu aliingia ndani ya chumba chake na kufunga mlango.

Hamza aliishia kusimama kwenye mlango akitamani kugonga , lakini mara baada ya kuona hana cha kuongea , alijikuta akiondoka kimya kimya kuelekea kwenye chumba chake. Alikuwa akihisi majonzi kwenye moyo wake huku akijiuliza mara mbili mbili , kosa lake ni niini ? Mbona kama kila kitu kilikuwa sawa ? Kwanini huyu mwanamke ghafla tu kakasirika.

Hamza hakuwahi kujua kwenye maisha yake atakuwa katika hali kama hio, tokea siku ambayo alikutana na Regina alikuwa tayari ashampenda lakini ndio anagundua ilikuwa ngumu sana kumfurahisha Regina kuliko alivyokuwa akimfurahisha Eliza kwa vitu vidogo tu . Regina alikuwa mgumu mno kueleweka zaidi ya Irene msumbufu.

Alimuona Regina ni kama Nyakasura , tofauti yao ni kwamba tu mwingine sio binadamu wa kawaida .

Hamza alijiambia kwanini bado tu anamtaka sana Regina kama mkwe wake . Maisha yake yangekuwa marahisi kama Eliza ndio angekuwa mke wake. Kufikiria hivyo alijikuta akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa na aliishia kutoka kwenye balkoni na kupunga upepo.

Hamza asichokujua , Regina ambae aliingia chumbani kwake alikuwa na wasiwasi mno.

Regina alikuwa amekwisha kuvua koti lake na alikuwa ameshika eneo la kifua chake karibu na moyo.

“Regina kwanini upo hivi jamani , si alikuwa akitania tu , kulikuwa na haja ya kupaniki..”

Regina alijikuta aking’ata lipsi zake huku akiangalia mlango. Alitaka kumsikia Hamza akigonga na kuendelea kumbembeleza.

Muda ule alijikuta aking’ata kidole huku macho yakilegea.

“Ukinibembeleza tena kwa dakika tatu. Usiku wa leo nitakupa nafasi…”Aliongea Regina kwenye akili yake huku akisubiria kwa hamu Hamza kugonga mlango.

Lakini mara baada ya kusubiria kwa zaidi ya dakika tano hakusikia mlango ukigongwa na aliamini Hamza alishaenda kulala na alijikuta hasira ikimvaa palepale.

“Hamza wewe ni mjinga sana , yaani ndio umeondoka bila kunibembeleza . Inamaana hujali nimekasirika ..”Regina alijikuta akijirusha kitandani kwa hasira huku akipiga ngumi mto.

“Yaani mtu mzima kabisa ila tu huelewi .. Ananidharau huyu lazima. Hamza nakuchukia , nakuchukia sana mshenzi wewe”

Alijikuta akikaa huku akianza kutingisha viatu vyake vya high heels akiendelea kujiongelesha.

“Usipo kuja chumbani kwangu usiku huu , kesho sitokuongelesha”

*****

Nusu saa mbele Regina alikuwa bafuni akioga na ile anatoka alisikia mlango wa chumbani kwake ukigongwa na palepale tabasamu lilimvaa baada ya kuamini lazima atakuwa ni Hamza.

“Nani?”Aliuliza.

“Wife ni mimi”Hamza aliongea kwa sauti.

Regina mara baada ya kusikia hivyo alijikuta aking’ata lipsi zake kwa furaha . Alikuwa amejifunga taulo tu na kila kitu kilikuwa wazi na alijifikiria kuvaa nguo nyingine ili asionekane kama anamtamanisha.Lakini Regina aliona ngoja ampe nafasi Hamza ya kuufaidi uzuri wake.

Endelea hapa:- SEHEMU YA 180
 
Shukran
 
Ndio hiyo sarafu siyo ndio shida nalipaje nauliza inakuwaje
Mm menyewe nimeshindwa nimejaribu kubuy now inagoma labda tulipie kwa lipa namba then yeye azifungue kulingana na account ya mtu.
 
Back
Top Bottom