Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.



MTUNZI: SINGANOJR.



SEHEMU YA 174.

She is my wife.​

Ukaribu wa Regina na Hamza ulizidi kuimarika , mara baada ya kutoka kuonana na Lamla. Regina alipendekeza watoke Out pamoja kama familia pamoja na Shangazi ,wazo ambalo licha ya kumshangaza Hamza kuona Regina kapata vipi wazo hilo lakini pia lilimfurahisha.

Baada ya kutoka kazini Regina alikwisha mpigia simu Shangazi na kumwambia asihangaike kupika usiku kwani wanaenda kula katika hoteli ya hadhi ya nyota tano na Shangazi hakupinga, hata kama alipendelea kula chakula anachopika mwenyewe lakini kwa ajili ya Hamza na Regina kuwafanya kuwa pamoja zaidi alikubali.

Siku iliofuata Regina aliwahi kurudi kutoka kazini na alimwambia Hamza alikuwa akitaka kupika siku hio hivyo waende Supermarket pamoja kununua mahitajhi. Japo wazo hilo lilimtisha Hamza kutokana na uzoefu alioupata mara ya mwisho kutokana na chakula alichopika Regina lakini hakuwa na namna ya kukataa.

Wakati wakiwa Supermarket waliweza kukutana na Eliza ambae pia alikuwa ananunua mahitaji ya kwenda kupika nyumbani na Regina alishangaa , lakini ndio alikuja kujua Eliza alikuwa amehamia karibu na mtaa anaoishi.

Kwasababu Eliza alikuwa peke yake, Regina alipendekeza waende wakapike nyumbani chakula cha pamoja , Ijapokuwa Eliza alisita kutokana na uhusiano wake na Hamza , lakini Regina alionekana kutojali sana juu ya mahusiano yao na alitaka aende kama mfanyakazi mwenzake.

Hio ilikuwa pona ya Hamza kula chakula kibaya siku hio kwani Eliza alimfundisha Regina kupika chakula kitamu.

Usiku Hamza alimsindikiza Eliza mpaka nyumbani kwake , ambapo hakuondoka mpaka alipohakikisha amepasha mwili joto na kazi ilifanyika haswa. Na Eliza aliishia kumsifia Hamza kwa uwezo wake mkubwa kitandani.

Hamza pia hakusahau kuendelea kumlegeza Regina taratibu taratibu , siku hio wakiwa wameketi juu ya jumba lao sehemu maalumu ya kumpizikia Hamza hakuwa nyuma kuelezea hisia zake.

“Wife unajua mwanzo nilikuwa nikivutiwa zaidi na mwonekano wako , lakini sasa hivi nadhani kuna kitu kingine zaidi kinachonivutia . Nakupenda sana tena zaidi ya sana . Hata kama uwe mzee sitoacha kukupenda”Aliongea Hamza akiwa na Regina wakati wakicheza Karata.

“Mh! Acha maneno mengi maana najua wewe ni muongo sana”Aliongea Regina ambae hakujizuia kusikia furaha moyoni lakini hakutaka kuionyesha.

“Kwanini nidanganye, kama sikupendi kweli , nipigwe na radi mpaka nife”Aliongea.

“Unanipendea nini , chakula nilichopika ni kibaya . Siku ile ulijikaza hata kukimaliza lakini ukadanganya na kusema ni kitamu , Wewe kama sio muongo ni nani sasa?”Aliongea Regina akishindwa kujizuia kujifananisha na Eliza ambae alipika chakula kitamu jana yake mpaka Shangazi kumsifia.

“Wife inamaana huelewi? Ijapokuwa chakula unachopika kina radha ya tofauti sana lakini umepika kwa ajili yangu , hisia ninazopata ni kubwa tofauti na kusema chakula ni kitamu. Hisia nilizopata ndio utamu wenyewe na sio kupitia ulimi ila moyo wangu”Aliongea Hamza kwa dhati kabisa.

Regina aliekuwa kama mtoto wakati huo alijikuta akishikwa na aibu za kike , huku akijiambia mbona hata kama maneno ya Hamza yamejaa sukari nyingi lakini bado yanafurahisha kusikiliza.

“Basi nitakuwa nakupikia kila siku?”Aliongea Regina akifanya makusudi kumtania, lakini alimfanya Hamza mwili kumkakamaa na kujikuta akicheka.

“Hilo ni wazo zuri sana mke wangu! Lakini kwa jinsi ulivyokuwa bize haina haja ya kunipikia kila siku , unaonaje mara moja haha..”

“Nilijua tu unanichezea akili , hutaki kula chakula changu , naondoka sitaki kukuona tena”Aliongea Regina kwa hasira huku akitupa karata chini na kutaka kukimbilia ndani.

Lakini ile anapita tu Hamza alisimama na kumkumbatia kwa nyuma na kuweka mdomo wake karibu na sikio na kufanya Regina kuhisi pumzi ya joto katika masikio yake.

“Regina nakupenda sana”Aliongea Hamza na kauli hio ilimfanya Regina kutetemeka.

“Niachie , sikuamini mimi”

“Nakupenda , nakupenda sana , usikasirike basi”Aliongea Hamza kwa sauti ya kubembeleza na alimfanya Regina kulegea.

“Sio kama nakukasirikia , najikasirikia mimi mwenyewe kwa kutokujua kupika, halafu kutokana na hasira zangu za karibu hamniambii ukweli”

“Wife mbona mimi naona upo kawaida tu, Kwanza una moyo mzuri , ukiachana na kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini nje ya biashara maisha yako ni simple sana”Aliongea Hamza huku akijiambia muda mwingine mwanamke akiwa na hasira za karibu ndio anavutia zaidi.

“Wewe nichukulie tu kama mtoto mdogo ila mimi najijua mwenyewe , muda mwignine hata sitaki kukasirika ila najikuta tu basi ..”Aliongea Regina kilegevu.

Hamza aliishia kucheka na kisha palepale alimgeuzia na kunyoosha mkono wake na kushika uso wake kwa namna ya kupapasa , akishindwa kuamini mwanamke mrembo na kauzu kama Regina muda huo alikuwa kama msichana wa kawaida.

Pengine muda huo Regina alikuwa katika umri wake na sio umri wa ukubwa wa akili yake.Alikuwa katikati ya miaka ishirini hivyo ni kawaida kwa mwanamke wa aina yake kuwa na aibu.

“Mbona unanikodolea macho wewe mjinga?”Aliongea Regina huku akishikwa na haya kwa namna Hamza anavyomwangalia.

“Wife unaonaje nikikununulia Doughunut?”Aliuliza Hamza akipotezea kile alichokuwa akipanga kufanya.

“Sitaki Doughnut sasa hivi , nataka matunda”Aliongea Regina na Hamza alitingisha kichwa na kumwambia asubiri akayalete.

Baada ya Hamza kutoka na matunda na kula waliendelea na kucheza karata lakini muda ule Regina alimkumbuka Shangazi.

“Kwanini tusimuite na Shangazi aje tucheze nae pia?”

“Shangazi yupo chumbani kwake , inaonekana kalala , halafu anaonekana hayupo sawa tokea ile jana tukutane na yule Mzee kule hotelini”Aliongea Hamza akikumbuka walikutana na Mzee mmoja ambae alionekana kufahamiana na Shangazi wakati walipokuwa Dinner.Mzee huyo alikuwa ameambatana na baba yake Irene.

“Hata mimi nimeona kitu ile siku , pengine walikuwa na mahusiano ya karibu zamani”Aliongea Regina.

Hamza pia alielewa , lakini kwasababu Shangazi hakuongea chochote hawakuona haja ya kuuliza na waliendelea kukaa juu hapo wakishuhudia jua kuzama.

“Hii ni siku yetu ya kwanza kuona jua la mwisho wa mwezi likizama , nina furaha sana mke wangu tupo pamoja”Aliongea Hamza huku macho yake yakiangalia jua linaloelekea magharibi.

Hamza wakati akiwa hana hili wala lile alijikuta akihisi lipsi zikigusa shavu lake. Haikujulikana Regina alitoa wapi ujasiri lakini kwa mara ya kwanza alichukua hatua na kumbusu Hamza shavuni.

Baada ya busu hilo la haraka Regina alikuwa n a aibu mno kiasi kwamba aligeuka pembeni akishindwa kumwangalia Hamza usoni.

Hamza alihisi ni kama moyo wake umepigwa na shoti ya umeme na alimwangalia Regina kwa mshangao na bila ya kuongea neno , palepale aligeuka na kumkumbatia na kumkiss kwa nguvu.

Ilikuwa ni picha nzuri kwa mwanamke mrembo kama Regina kukisiwa na kijana Mtanashati Hamza , wakimulikwa na miale ya kuzama kwa jua.

******

Ni ndani ya kisiwa cha Barry huko Wales Uingereza. Ndani ya hoteli ya Gileston Manor Luxury B&B, alionekana Serena alievalia gauni jepesi la hariri na Bikini , akiwa amelalia kiti na kunywa taratibu mvinyo huku akiangalia mafataki yaliokuwa yakirushwa upande wa baharini.

Pembeni yake alikuwepo mtaalamu wa mambo ya SPA na alikuwa akimfanyia masaji kwenye miguu yake.

Muda huo mwanaume mweusi alievalia Bathrobe alitoka ndani ya hoteli hio .

“Tutaendelea kukaa hapa kwa muda gani?”Aliuliza yule mwanaume kwa lugha ya kingereza.

“Haraka ya nini? Kwa mandhari ya hapa na hoteli kama hii ya kifahari watu wengine wasingetaka kabisa hata kuondoka mapema. Unapaswa kunishukuru kwa kukuleta hapa bure”Aliongea bila ya kugeuka.

“Mimi Saidi Adamson , sipo hapa kwa ajili ya kula bata . Ninachotaka ni kisasi , nataka kuchukua kila kitu nilichopoteza”Aliongea Saidi huku macho yake yakiwa na hisia za hasira mno.

“Nadhani kichwa chako kimepigwa teke na punda. Hamza mpaka sasa kutokana na kutofanikisha kutupata lazima atakuwa makini mno . ukiharakisha utaishia kukamatwa tu bila kufanya chochote. Unadhani Hamza ni mjinga akuache tu uondoke baada ya kujua mpango wako wa maroboti . Akikukamata sahau kabisa kuhusu kisasi chako atatumia moto wa jehanamu kuisambaratisha nafsi yako”Aliongea Serena.

“Kama ni hivyo kwanini umenileta huku? Si walisema watanipa nafasi ya kuinuka tena?”

“Embu acha kuwa na wasiwasi na angalia mandhari nzuri iliopo mbele yetu , ulimwengu huu umejaa vitu vizuri sana lakini sisi binadamu tunachukulia kawaida”Aliongea Serena lakini bado hakumshawishi Saidi.

“Kama ni hivyo basi nipe hata malengo yako , naboreka kukaa hapa siku nzima bila cha kufanya”Aliongea na kumfanya Serena kugeuza kichwa na kumwangalia.

“Kuna malighafi ya thamani ya juu sana ambayo Hamza ameniibia , lakini mpaka sasa sijajua ni wapi ameficha . Nilikaa Tanzania kwa ajili ya kutafuta hizi malighafi lakini sikupata viashiria vyvoyote . Kwanza nisaidie niweze kupata hivi vitu na nitakupatia nafasi ya kumuua”.

“Ni malighafi gani hizo , si uzitafute aidha kwa kumteka hata mwanamke wake au kuingia ndani ya nyumba yake kimya kimya”

“Mpango mbovu huo , kuna haja gani ya kuchukua hatari kubwa namna hio, sitaki kujiingiza kwenye ulimwengu wake ambao kutokufa ndio sheria. Nimekuokoa ni wakati wako wa kunilipa . Kama utanisaidia kuweza kupata hivyo vitu viwili nitakupatia rasilimali nzuri ambazo zitakusaidia kuweza kutimiza malengo yako”Aliongea na macho ya Saidi yalichanua palepale na tabasamu la uovu lilimtoka.

“Kwa suala kama hili , umepata mtu sahihi kabisa. Ninaweza kukusaidia ila sina uhakika kama utanisaidia”

“Oh! Pata kwanza hivyo vitu na tuone kitakachotokea”Aliongea Serena huku akicheka.

NB: Usisahau kuhusu zile Fuwele hapa.

******

Hamza alikuwa na furaha kubwa jinsi ukaribu wake na Regina ulivyongezeka siku ya jana . Licha ya busu lile hakuna kingine kilichotokea, Lakini hata hivyo Hamza aliona japo ni ngumu sana kumlegeza Regina lakini mwisho wa safari ya kumuweka kifuani kwake haikuwa mbali sana.

Baada ya kifungua kinywa Hamza alimwambia Regina anapanga kwenda Morogoro kutembelea watoto maana kila mwezi mpya unapoingia kituo hicho kinakuwa na utaratibu wa kufanya usafi na kupanda maua na shughuli nyingine nyingi.

Regina mara baada ya kusikia hivyo , alimkubalia na upande wake alipanga kubakia nyumbani tu siku hio.

Ile anafika Morogoro wakati akitoka kwenye taksi nje ya geti , Hamza aliweza kuona tukio ambalo lilimfanya ashangae.

Aliweza kuona mwanamke wa kizungu alievalia koti la leather akidondoka chini . Alikuwa ni Crow mlinzi.

Crow alikuwa amepokea kichapo kutoka kwa mwanamke mrefu alievalia koti la rangi nyekundu huku nywele zake zikiwa zimeachia na kufunika mabega yake yote . Alikuwa ni Nyakasura.

Hamza mara baada ya kuona vile haraka haraka alishuka kutoka kwenye gari na kukimbilia kwenda kumsaidia Crow.

“Nyakasura unafanya nini?”Aliongea Hamza kwa sauti. Crow mara baada ya kumuona Hamza alipotezea maumivu yake na kutaka kupiga goti chini kutoa saluti lakini Hamza alimzuia.

“Achana na saluti , nini kinaendelea hapa?”Aliuliza Hamza akiwa na shauku maana hakutegemea kumuona Nyakasura hapo kituoni.Hakuacha kuwaza labda yupo hapo kwa ajili ya kutafuta ugomvi na yeye.

“Huyu ni mtu wako? Ndio maana , mimi nilijua ni ninja anataka kuniua?”Aliongea Nyakasura.

Crow aliishia kung’ata meno yake na kisha kuelezea kinachoendelea. Ilionekana kwa ajili ya kumlinda Prisila, Crow alisafiri nae mpaka Morogoro lakini Nyakasura alikuwepo ndio aliweza kumgundua ndani ya kituo hicho na alimshika na kumtoa nje na kumrushia chini.

“Ni mlinzi nimemuweka kumlinda Prisila, Wewe hujaona hana nia ya kimauaji kwenye macho yake?”Aliuliza Hamza akiamini Nyakasura lazima alikuwa akifanya makusudi.

“Mimi inanihusu nini , kwani nimemuua au tu unataka kumkingia kifua mtu wako?”Aliongea kwa kejeli.

Hamza hakutaka kushindana na mwanamke huyo , hivyo alimpa ruhusa Crow kuondoka kwanza.

“Halafu wewe unafanya nini kwanza hapa?”

“Ni kwenu hapa kwani? Kama unaweza kuja unadhani mimi siwezi?”Aliongea akionekana hana furaha.

“Nishawahi kuwa hapa hapo mwanzo na leo nipo kwa ajili ya kusaidia usafi . Wewe sababu yako kuja hapa ni ipi?”

“Nimekuja kukuangalia ukifanya usafi”

Hamza alijikuta akishindwa kuongea neno , alitamani kumpasua kichwa chake maana hakuweza kuelewa ubongo wake unavyofanya kazi.

“Usiniambie ushaanza kufa na kuoza kimapenzi juu yangu ndio maana umefanya makusudi kuja huku kuniona”Aliongea Hamza na tabasamu la kumchokoza lakini kauli yake ilimfanya Nyakasura macho yake kubadilika na kuonyesha ukali.

“Yaishe natania tu , sijui sababu yako ila kama unataka kuwa hapa unaweza , mimi naingia ndani”

Hamza alitembea kuingia ndani ya kituo hicho na Nyakasura alimfuata nyuma nyuma.

Watoto wengi mara baada ya kumuona Hamza walimkimbilia kumlaki kwa furaha , lakini mara baada ya kumuona Nyakasura walionekana kumshangaa . Maana licha ya uzuri wake hawakuwa wakimfahamu.

“Hamza karibu!”Aliongea Mzee Hizza akiwa ameshikilia mafagio na alionekana kufuta jasho wakati akimwita Hamza.

Hamza mara baada ya kumuona mzee huyo alionekana kushangaa , maana alikuwa amekonda mno.

“Mzee ulikuwa ukiumwa , maana naona mwili wako umepungua sana”

“Kila mtu ananiuliza mimi hivyo , mniache sasa , Prisila na yeye alionekana kuwa na wasiwasi . Niko sawa kabisa nilienda hata hospitalini kufanya uchunguzi”Aliongea lakini Hamza bado hakuonekana kuridhika.

“Mzee naweza kushika mkono wako niangalie mapigo yako?”

“Usiwe na wasiwasi . Tutaongea nikishamaliza kukabidhi hizi fagio . Ingia ndani ukamsaidie Prisila”

“Nachukua dakika chache tu”

“Hamza niko sawa lakini kwanini unakadhania kuonyesha kama naumwa ? Nina watoto wengi hapa wananihitaji kwanini nitanie kuhusu afya yangu?”

Hamza mara baada ya kusikia hivyo hakuongea zaidi , vinginevyo angeonekana kama analazimisha mzee huyo kuonekana alikuwa mgonjwa.

“Basi sawa mimi ngoja niingie ndani”Aliongea Hamza lakini muda huo huo Prisila alitoka ndani akiwa ameshikilia Mop . Mara baada ya kumuona Hamza akiwa ameambatana na Nyakasura alionekana kushangaa.

“Hamza. Imekuwaje ukaja na Nyakasura?”

“Unamjua?”Aliuliza Hamza kwa kushangaa

“Ndio”Alijibu Prisila na kumsogelea Nyakasura.

“Nyakasura , vipi umekuja kunitafuta?”

“Hapana , nimekuja kupigana na huyo?”Aliongea huku akimnyooshea kidole Hamza.

“Hey! Unaongea nini , kwanini tupigane tena?”

“Kama hutaki na mimi sitaki , kwani siruhusiwi kukutafuta ninapotaka?”

“Kunitafuta? Unanipenda au?”

“Kukupenda kwa Nyo**! Hata kama wanaume wote wafe dunia nzima siwezi kupenda mwanaume kama wewe mimi”Aliongea huku akimshusha Hamza na kumpandisha.

“Prisila ashawahi kukutafuta huyu mwanamke?”Aliuliza Hamza akiamini kuna kitu hakipo sawa na Prisila alitingisha kichwa na alitaka kuongea kitu lakini aliingiliwa na Prisila.

“Wewe umekuwa mtumwa wake , kwanini unajibu kila anachokuuliza?”Aliongea Nyakasura na kumfanya Prisila ashindwe kujua namna ya kujibu.

“Nyakasura kwani ulikuwa ukinitafuta?”

“Hapana”

“Kumbe! Ila mimi kuna kitu nataka kukuuliza”

“Mimi sijui”Aliongea

“Lakini hata hujajua ninachotaka kuuliza ni nini”

“Mimi sijui chochote hivyo usiniulize?” Mara baada ya kuongea hivyo alikimbilia upande wa kulia kwake na kwenda kukaa kwenye bembea.

Hamza alijikuta akihema kwa masikitiko tu , kwa mwonekano wa Nyakasura ni sawa na kusema alikuwa katika umri sawa na Prisila lakini alionekana kuwa na mambo ya kitoto kuliko isivyokawaida.

“Prisila tuingie ndani tukaendelee”Aliongea Hamza , aliona uvivu kumfuatilia huyo mwanamke kichaa na alipanga kumsaidia Prisila kufanya usafi wakati wakiongea.. Lakini sasa ile wanaingia ndani Nyakasura aliwasogelea kama upepo na kusimama mbele.

“Mnaenda wapi?”

“Wewe unadhani tunaenda wapi kama sio kufanya usafi , Wew huoni kila mtu anafanya kazi hapa? Au una ukichaa wa asubuhi asubuhi?”Aliongea Hamza kwa kufoka.

“Acha kuniita kichaa, usidhani nashindwa kuunguza hiki kituo”Aliongea kwa hasira

“Unguza uone”Aliongea Hamza alionekana kuchukia pia baada ya kuona vitisho vyake vya kipuuzi.

Prisila mara baada ya kuona kinachoendelea kinaweza kuibua mengine , haraka sana alisimama katikati.

“Jamani acheni kugombana , hili ni swala dogo sana. Hamza twende kufanya usafi. Dada wewe huna haja ya kufanya usafi , kwanini usicheze na watoto , kwa urembo wako naamini watakupenda kwa haraka”

“Upo sahihi, mimi pia ni mwepesi kupenda binadamu hivyo na watoto watanipenda . Ila nacheza nao vipi?”

Prisila aliishia kufosi tabasamu , mwanzoni alidhani Nyakasura ni aina ya wanawake wagumu kuelewa lakini muda huo alimuona kama mdogo wake.

Yule mtoto pale anaitwa kwa jina la utani la Bando , kwanini usiende kucheza nae , anapenda mchezo wa Draft “Aliongea Prisila na kuangalia upande huo na aliweza kuona mtoto wa kike wa kike akiwa anacheza draft peke yake.

Baada ya Nyakasura kwenda kucheza na watoto Hamza na Prisila waliingia ndani kuanza kufanya usafi sakafuni pamoja na kusafisha madirisha.

“Hamza , hisia zangu zinaniambia huyu Nyakasura anajua kuhusu uwezo wangu wa ajabu”

“Kwanini unaongea hivyo?”Aliuliza Hamza.

“Unakumbuka nilikuambiaga siku ile niliweza kumkimbia Saidi kwasababu ya mwili wangu kushika moto?. Ukweli tokea nikiwa mtoto nilikuwa nikipenda sana kucheza na moto na hata niweke mkono karibu na miale sijawahi kuungua kabisa na kama nina kovu au mikono yangu ni migumu nikiweka karibu na moto inalainika..”Aliongea Prisila kwa kirefu na Hamza baada ya kukumbuka alijikuta akishamgaa , alikuwa ashasahau kabisa kuhusu hilo suala.

“Wewe umajuaje Nyakasura anaweza kuwa kama wewe?”Aliuliza Hamza na hapo ndipo Prisila alivyochukua jukumu la kuanza kumhathia Hamza tukio la Nyakasura kuunguza mpira.

Mara baada ya kusikiliza maelezo yote , aliona pengine hisia za Prisila ni kweli. Hamza palepale alijiuliza au Prisila msichana aliemfahamu tokea akiwa mdogo anaweza kuwa na damu ya kiphoenix , kama ni hivyo imekuwaje baba yake akawa ni Profesa Singano. Hamza alijihisi alichokuwa akiwaza ni ujinga.

“Prisila kuhusu swala lako naona ni siriasi sana . Inaweza kuwa laana au baraka lakini hatujui mpaka sasa , hivyo usiwe na haraka ya kuanza kumuuliza Nyakasura , niache nilifanyie uchunguzi mimi mwenyewe”Aliongea

“Mh! Najua .. mimi pia nahisi kuogopa lakini nataka kweli kujua kuhusu kutokuwa kawaida , nimeishi kwa hofu tokea nikiwa mdogo na Baba anaonekana kunificha kitu”

Hamza palepale hakutaka kupoteza muda na alimpigia simu Sally na kumpa maelekezo ya kumfanyia uchunguzi Nyakasura kuangalia kama kuna uhusiano wowote na Prisila.

“Prisila una kitu chochote unachomiliki ambacho sio cha kawaida ulichoachiwa na mama yako?”Aliuliza Hamza.

“Kwanini unaniuliza hivyo. Nina kidani ambacho niliambiwa nilikutwa nacho shingoni”Aliongea Prisila huku akimuonyesha Hamza.

Hamza aliangalia kidani kile na alionekana kushangaa kidogo kwani madini yake yalionekana kutokuwa ya kawaida.

Alikipiga picha na kisha akamtumia Sally na kumpa maelekezo mengine kufuatilia kama kuna uhusiano wowote wa muundo wa kidani hicho na Nyakasura.

Baada ya mawasiliano hayo Hamza alimwambia Prisila asifikirie sana kuhusu hilo swala. Hivyo waliendelea kufanya usafi mpaka mchana wakati wa chakula ulipowadia.

Muda ule wanatoka walisikia kilio cha mtoto na Hamza mara baada ya kugeuka aligundua ni Bando ndie aliekuwa akilia na walikimbilia upande huo kuona kinachoendelea.

Nyakasura alikuwa amekaa huku uso wake ukionekana kutokuwa na furaha akimwangalia mtoto huyo kwa namna ya kushindwa kumbembeleza

“Acha kulia nitakulipa draft lako”

“Wewe ni mtu mbaya, unatisha ..”Aliongea yule msichana huku Bando akiendelea kulia

“Nini kimetokea?”Aliuliza Hamza. “Bando ni huyu dada kakuchokoza?”

“Nimemchokoza saa ngapi mimi wakati nilikuwa nikicheza nae draft?”Aliongea Nyakasura lakini Bando alimkimbilia Hamza na kuendelea kulia.

“Ameunguza draft kimazingaombwe wakati nikielekea kushinda”Aliongea

Prisila na Hamza mara baada ya kusikia hivyo , walijikuta wakishangaa na kujiuliza inakuwaje mtu acheze draft na mtoto mdogo na baada ya kushindwa anaunguza Draft.

Ilikuwa bahati watu walikuwa bize . Kama wangeona kilichotokea wangepaniki na kumdhania Nyakasura ni Jini.

“Sikufanya makusudi.. nilijikuta tu nikiwasha moto”

“Nyakasura wewe umeshindikana . Inamaana kila anaekushinda utataka kumuunguza , kama unaendesha gari mtu akikupita utaunguza gari yake?”

“Nani kasema nasafiri kwa kutumia upuuzi unaoitwa gari mimi. Nitembee na hayo magari yenu yenye mwendo wa kinyonga , nikitaka kufika mahali ni sekunde tu kwa uwezo wangu”

“Mimi nauliza swali sijali kama unaendesha gari au unafanya nini?”Aliongea Hamza kwa sauti akiona Nyakasura anamfanyia makusudi kutoelewa anachomaanisha.

Upande wa Prisila aliishia kumfariji Bando kwa kumfuta machozi .

“Sikupendi wewe dada Unatisha”Aliongea Bando.

“Hata mimi sikupendi ! Unalia nini sasa ?”Aliongea Nyakasura akimfokea Bando akionekana amechukia.

“Nyakasura hebu tulia acha kufokeana na mtoto”

“Binadamu wadhaifu sana , kitu kidogo tu analia. Nishachoka kukaa hapa hapafurahishi naondoka zangu”Mara baada ya kuongea hivyo hakujali kabisa angemshitua Bando kwani aliyeyuka na kumfanya Bando macho kumtoka.

Upande wa Hamza alihisi kitu kikiongea katika masikio yake na kumfanya anyooshe mkono na palepale kwenye mikono yake alonekana akiwa ameshikilia karatasi.

Ilionekana Nyakasura alisahau kumpatia Hamza karatasi hio na alitumia uwezo wake kumpatia hata kwa mbali.































SEHEMU YA 175.

Hamza alifungua karatasi ile na aligundua ilikuwa ni nyaraka iliotokea kwa Afande Simba , ikiwa na maelekezo na mpangilio wote wa safari ya kwenda kushiriki Baraza la Maksi.

Hamza aliishia kuhema tu , hakutamani kwenda kushiriki lakini kwasababu alikuwa amekwisha kukubali , alijikuta akiwa hana jinsi. Aliona ngoja achukulie kama muda wa kwenda kukutana na marafiki zake wa zamani.

Baada ya chakula cha mchana mambo madogo madogo yalimaliziwa na sasa kituo chote kilionekana kuwa kisafi mno.

Wadeni aliwataka Hamza na Prisila kubakia mpaka jioni lakini Prisila alikuwa na miadi na Hamza pia alipanga kuonana na Dina kabla ya kuanza safari ya kwenda Ulaya na Regina.

****

Usiku sana Hamza alipanga kurudi nyumbani akitokea kwa Dina , aliona licha ya muda kusonga sana ni kheri kurudi hata kwa kuchelewa maana kulikuwa na tofauti kubwa kati ya kutokurudi na kurudi kwa kuchelewa.

Lakini muda ambao alikuwa akitoka kwenye mgahawa wa Dina aliweza kugundua kulikuwa na mwanaume aliekuwa ameegamia gari kwenye maegesho akiwa amevalia kofia na ilikuwa ni kama alikuwa akimsubiria.

Hamza hakuwa na haja hata ya kumjua ni nani kwani palepale kwa furaha alimwita yule mtu.

“Himidu mbona ghafla tu upo hapa?”Aliuliza Hamza na kumfanya Himidu kutabasamu.

“Bosi unakula sana maisha kwa uzuri wa hawa warembo wako nina uhakika Sally huko kisiwani tayari ashakuchukia”

“Haha. Hebu achana na hayo , najua ujio wako una sababu”Aliongea Hamza huku akichukua sigara kutoka kwa Himidu na kuvuta moshi.

“Unaonaje tukienda kwenye mgahawa wowote kwa ajili ya chakula . Ndio nimetua na sijapata chochote”Aliongea Himidu na Hamza hakuwa na pingamizi kwani aliendesha gari mpaka kwenye mgahawa wa Jenna na walifanikiwa kuagiza chakula walichotaka , hawakuacha kuagiza na vinywaji.

“Bosi nimejikuta nikikumbuka kipindi kile tulipokuwa Sipolia . Ile barafu sio mchezo . Hii nyama choma ni kama ile usiku wa njaa kali lakini ghafla tu ulikuja kwenye kambi ukiwa na ng’ombe mzima. Utamu wa ile nyama siwezi kusahau maisha yangu yote”Aliongea Himidu akikumbuka mbali. Na kumfanya Hamza kuishia kutabasamu tu.

“Himidu unaonekana kama una jambo juu ya safari ya kwenda Ulaya?”

“Bosi unadhani isingekuwa hivyo ningekuja kukuvamia usiku usiku?”

“Ni kwasababu nilionana na Nyakasura mchana , kwanini usingenitumia tu ujumbe kupitia yeye?”

“Bosi ijapokuwa Nyakasura uwezo wake ni mkubwa sana na nitegemeo kwetu lakini kuna baadhi ya vitu hatuwezi kumwambia moja kwa moja”Aliongea.

“Kumbe! Unataka kusema kuna kitu kinachoendelea juu ya msaliti ndani ya jeshi?”Aliuliza Hamza.

“Bosi kweli wewe ni noma kuelezea kidogo tu ushang’amua kila kitu.Umejuaje nazungumzia msaliti?”

“Kama nikishindwa kung’amua swala dogo kama hili kwanini niwe bosi wako sasa?”Aliongea Hamza huku akicheka na Himidu aliona ni sahihi.

“Kwahio Himidu unamaanisha katika kitengo muhimu cha Malibu kuna msaliti na Simba hamjui?”.

“Ni kwasababu hatuna uhakika . Mimi na Afande Simba tunaamini kuna msaliti ndani ya kitengo anaevujisha taarifa zetu. Unajua kwa kipindi cha muda mrefu tumekuwa tukifanya upepelezi kujua nguvu ya ushawishi ndani ya serikali kutoka kwa watu wa Binamu ili kupata muunganiko na Umoja wa kisiri wa Imani ya Bluu”

“Hawa watu wa imani ya bluu sio ndio ambao wana makanisa yamesambaa Africa nzima ?”

“Ndio, wengi wanayaita Makanisa ya Wabrazili. Unajua maswala yanayohusiana na dini ni ngumu sana, Binamu ni wajanja sana kuna uwezekano mambo yanayoendelea mipakani wao ndio wasababishajij lakini bado hatuna uhakika kutokana na kutokuwa na ushahidi wa moja kwa moja”

“Kama mnawatilia shaka Kanisa la Wabrazili na Binamu kwanini msipandikize mashushu ndani ya umoja wao? Au mlioingiza waliuliwa?”

“Ndio maana tunaamini kuna msaliti ndani ya kitengo . Tumeingiza mashushu ndani ya kisiwa cha Binamu zaidi ya mara tano lakini wote waligundulika na kupoteza maisha”Aliongea Himidu.

“Inaonekana kweli kuna msaliti kati yenu. Kwa nguvu aliokuwa nayo Simba kusimamia majasusi wa siri kuzamia taasisi yoyote ni jambo rahisi sana. Lakini uhusika wa Binamu hapa ndio changamoto maana wapo karibu sana na vitengo vya serikali ya Kimarekani maa pengine ndio wanakovujishia taarifa”

“Ndio maana mpaka sasa bado hatujatangaza nani anaenda kushiriki mashindano ya baraza la maksi. Kwasababu msaliti hatumfahamu , Nyakasura licha ya kuwa na uwezo mkubwa lakini hajui namna ya kutofautisha nani ni msaliti na nani sio msaliti kutokana na kuwa wa tofauti na sisi. Hivyo ujio wangu hapa ni kukuomba utusaidie tufahamu nani ni msaliti kati yetu”

“Kama hata wewe Himidu umeshindwa kumjua nani ni msaliti , mimi nitawezaje kumfahamu?”

“Bosi wewe uwezo wako wa kumsoma mtu ni mkubwa mno , pili mimi ni ngumu kujua maana nipo ndani ya mfumo , mtu wa nje anaweza kuona vitu kwa uharaka zaidi. Bosi kama sio uwezo wako wa kugundua wasaliti sidhani ungeshinda ile vita takatifu”Aliongea

“Naona ushaanza kunisifia sasa . Ila usiwe na wasiwasi awamu hii nitawasaidia bure tu kumkamata anaewasaliti”

“Bosi tuna mipango mingi ya kupiga hatua kama taifa na kama siri zinaendelea kuvuja kirahisi inakuwa kikwazo kwetu. Tunakutegemea katika hili”Aliongea

Baada ya kupata Nyama choma na Himidu , Hamza aliweka walioongea moyoni lakini hata hivyo Himidu alimkabidhi majina ya viongozi wote ambao watasafiri kwenda kushiriki baraza la Maksi na waliamini kama kuna msaliti basi kati ya hao lazima mmoja wapo atakuwepo.

Wasiwasi wa Himidu ni kwamba mipango mingi ya jeshi iliokuwa ikiendelea ilikuwa ikivuja nje ya nchi . Mfano swala tu la Profesa Ndiswe kuwa shushu wa Kimarekani na kusaidia kuiba Earth Axis , halikuwa swala la rahisi bila mkono ndani ya Jeshi.

Maana yake ni kwamba moja ya viongozi wakuu wa kitengo kuna mmoja ni msaliti na ndio huyo walietaka kumfahamu kabla ya kupiga hatua zaidi. Alichokifanya Himidu ni kuteua wale wote ambao anawatilia shaka kuwa katika msafara ili ikiwa kuna msaliti Hamza aweze kumfahamu, maana kwa namna yoyote angejidhihirisha tu akiwa nje ya macho ya jeshi.

Hamza mara baada ya kurudi nyumbani alitumia kusoma nyaraka ya siri aliopatiwa na Himidu kukariri sura na majina ya viongozi wote wa kijeshi na kisha akachoma karatasi hio.

Mpaka kufikia hatua hio , aligundua alikuwa na mambo mengi ya kufanya akifika Ulaya kuliko alivyowaza mwanzo. Alipaswa kufanya kazi kama msaidizi wa Regina na vilevile kushiriki katika baraza la Maksi na pia kufuatilia msaliti.

******

Siku moja mbele hatimae Hamza na Regina walipanda ndege kuelekea jiji la Parisi nchi ya Mafuvu na kama kawaida walikaa daraja la kwanza kabisa.

Linda hakuwa sehemu ya safari hio, aliomba likizo fupi kwa ajili ya mchakato wa kumtambulisha mpenzi wake kwao pamoja na mchakato wa kutoa mahari hivyo asingeweza kusafiri.

Kwanza Hamza aliona hio ni fursa pekee ya kuwa na Regina karibu na kumfanyia utundu wake bila ya kuangaliwa na Linda.Maana alijua kama Linda angekuwepo Regina asingetaka michezo ya aibu.

Upande wa Regina hakuwa akijua Hamza alikuwa na kazi nyingine ndani ya nchi hio ya Mafuvu.

Walikuwa wamepanda Turkish Airlines, mhudumu wa ndege aliewapokea alikuwa ni mzungu mrembo sana , aliekuwa kati ya umri wa miaka therathini kwenda arobaini hivi , licha ya umri mkubwa alionekana ni aina ya wale wanawake wanaojipenda.

Hamza kama kawaida yake alikuwa mcheshi mno na aliongea na mhudumu huyo wa ndege kwa lugha ya kikwao na kufanya mwanamke huyo kuvutiwa na maongezi.

Regina mara baada ya kuona Hamza alivyokuwa bize , akiongea na mwanamke huyo alijikuta akijikalia zake kimya , akikosa kabisa mudi ya kuangalia nyaraka za kibiashara.

Baada ya mhudumu kuondoka Regina alitoa furushi la nyaraka na kumuwekea Hamza.

“Pitia hizo nyaraka ili angalau ujue tunachokwenda kufanya”Aliongea

“Wife wewe ukijua inatosha . Mimi nitakuwa tu bodigadi wako basi au mtafsiri”

“Soma angalau ujifunze , kwani huna malengo yoyote kwenye maisha yako”

“Wife kama hata chuo nimeacha mwishoni , unadhani naweza kuwa na malengo gani? Mimi nipo nipo kwanza”

“Sio swala la elimu au kumaliza chuo , ukiwa kama msaidizi wangu , tukikutana na hao wazungu lazima watajaribu kuuliza maswali kama msaidizi kukupima . Ukikosea utanitia aibu”Aliongea

“Kwahio unasema nje ya nchi mimi sio kama mume wako bali msaidizi wako pekee?”Aliuliza Hamza akiwa amenyongea na Regina mara baada ya kuona hivyo alijikuta akilegeza.

“Lakini wewe unajua mahusiano yetu yalivyo. Siwezi tu kukutambulisha kama umenioa. Isitoshe hukunichumbia vizuri nikakubali bali kulikuwa na biashara katikati”Aliongea.

“Wife kwahio unasema nikikuchumbia vizuri utanikubalia? Na tukifunga ndoa tunaweza kutangaza uhusiano wetu kwa watu si ndio?”Aliongea na kumfanya Regina kuona aibu kidogo.

“Mimi sijui , si unapaswa kunibembeleza ili nikubali kama wanavyofanya wengine , naweza kukataa kwanza ila hatimae nikakubali”

“Unamaanisha nini kukataa kwanza? Kwahio unamaanisha napaswa kukuchumbia mara mbili ndio unikubalie . Babe unajua tayari sisi ni wanandoa na tumajisajili kabisa , sidhani kama itakuwa vizuri kunizungusha kiasi hicho , nikikuchumbia mara ya kwanza nikubalie siku hio hio”

“Kwahio unadhani nina masharti mengi . Una wanawake kibao na ushukuru tu sijaitaka talaka . Kama hutaki kunibembeleza mpaka nikubali acha, kwanza sitaki harusi mimi”Aliongea Regina akiwa amenuna na Hamza alitamani kujilamba kibao. Alikuwa ashaandaa mpango wake wa kukubaliana na kila kitu ili kumlegeza lakini muda huo ameanza kwenda kinyume.

“Wife nimekosea , ninatamani pia kuona ukinikubalia na kunipa kidole nikuvishe pete . Ngoja nitafikiria namna nzuri ya kukufanya unikubalie”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kuishia kuvuta mdomo akionekana hataki kumsikiliza tena.

“Wife unapendelea staili ipi nikikuchumbia ? Tayari wewe ni tajiri nadhani pete ya almasi haitokuwa na thamani kubwa kwako”Aliuliza Hamza na Regina alichukua Earpod zake na kuziweka sikioni.

“Acha kuniita mke , mke mimi sio mkeo k wanza nasikiliza mziki”Aliongea hivyo lakini Hamza aliona bado matumani yapo, maana Regina licha ya kuweka earphone hizo sikioni lakini hakuwa ameweka mziki maana yake bado alitaka kumsikiliza.

“Wife unaonaje nikatengeneza Pete kubwa yenye karati zaidi ya mia za madini ya almasi?”

“Pete yote hio ya nini , itanishinda kuivaa mbele za watu , kama naitaka kama pambo naweza nunua tu”Aliongea.

“Basi nitakupatia almasi kama almasi utengeneze mikufu , Bracelet hata taji la almasi . Nikufanye umeremete kama Malkia”

“Bado havitakuwa na thamani maana naweza kununua na hela zangu , kwahio hakuna kitu chochote ambacho siwezi kununua ambacho huwezi kunipa?”

“Tatizo kila kitu ambacho kinatumika kuchumbia vinanunuliwa na hela na uwezo huo unao .. au tufanye nitakupatia Antique au mchoro maarufu”

“Yaani wewe uchizi , nani anachumbia na Antique siku hizi au mchoro?”Aliongea Regina kwa mshangao kidogo tu jicho lingedondoka chini.

“Kwahio unapenda nini?”

“Mimi mwenyewe sijui , kama vipi usinichumbie tu kabisa, kwanza mwenyewe unaonekana hutaki , hata hivyo sitaki kufanya harusi na wewe mimi. Mambo ya harusi yanachosha mno , kuanza kutafuta gauni , ukumbi , sijui mpiga picha na kualika wageni. Halafu watu wakisikia naolewa na mwanaume mwenye sura mbaya kama wewe watanicheka mpaka basi”

“Ah! Wife nani ana sura mbaya , acha kukufuru uumbaji wa Mungu ujue!”

“Mimi sijali , nenda kamuoe mwanamke mwingine , sitaki kuolewa na wewe mimi”Aliongea Regina akionekana kususa.

Hamza alimwangalia mrembo huyo lipsi zake zilivyokuwa nyekundu na palepale aliona atumie nguvu na alimshika Regina na kulazimisha Kiss.

Regina aling’atwa na Hamza kwa dakika moja na mwanzo mwisho alishindwa kumsukuma Hamza na kumuacha tu aendelee kufanya anachofanya huku akitoa ushirikiano.

Hamza mara baada ya kumwachia alimshika nywele zake kwa kuzipapasa huku akimwangalia namna alivyo iva kama yai la kienyeji.

“Regina kwanini mate yako ni matamu mno , ni kama una kiwanda cha asali mdomoni?”Aliongea Hamza akimtania.

Regina alishindwa kuvumilia na aliishia kuchukua nyaraka kwenye kimeza na kuanza kumpiga nazo Hamza na kisha akamwekea mkononi.

“Soma hizo nyaraka kisha nikuulize maswali”

“Ah! Wife hakuna haja ya mimi kuzisoma bwana , Kwani si wajasiriamali wadogo wadogo unaoenda kukutana nao?

Aliongea Hamza huku akijua fika wafanyabiashara wengi wa Ulaya ni wazee na hakuna idea mpya ambayo hawajawahi kusikia, hivyo kujielezea sana ni kupoteza muda.

“Kwanza nina marafiki wengi Ulaya yote naweza kuongea nao na kualika watu bora zaidi kwa ajili yako na ukafanikisha suala zima la kujipanua kibiashara”Aliongea Hamza kwa sifa kabisa sio kama alikuwa akijigamba , ila alijua fika kwa mfanyabiashara yoyote ili kuweka mzizi katika masoko ya kigeni inachukua muda sana na lazima uanze hatua kwa hatua ya kujenga koneksheni.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Regina anaenda kufanya maongezi na wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuwekeza kwao na hakuwa mzoefu , Hata kama wajasiriamali hao watajua anao mtaji wa kutosha hawawezi kumpatia nafasi kutokana na kutokea Africa.

Lakini kama Hamza akitumia marafiki zake , ingekuwa ni njia ya mkato na rahisi zaidi kufanikisha , kwasababu mbele ya tajiri yoyote hasa wazungu wanachokitaka ni kile kitu ambacho hawawezi nunua.

Regina mara baada ya kusikia kauli hio , uso wake ulijaa usiriasi.



“Sitaki unisaidie kupitia koneksheni zako , kwanza sijui nani unamjua , lakini kama nitatumia koneksheni zako kujiimarisha kibiashara , si itaonekana sina uwezo binafsi . Hata kama ukifanya hivyo sidhani kama nastahili”

“Wife kuna haja ya kuwa hivyo? Unadhani ulimwengu wa sasa unaenda bila koneksheni , watu wanaonekana kufanikiwa wamepita milango mingi ya nyuma . Mimi na wewe ni mume na mke ni kawaida kutumia koneksheni zangu kukusaidia. Sio wewe tu wengine wengi wanafanya hivyo”

“Wengine ni wengine mimi ni mimi , kwanini unanifananisha na wengine?”Aliuliza Regina kwa kiburi.

Hamza mara baada ya kuona msimamo wake , hakutaka kumlazimisha tena, aliona pengine Regina alikuwa na sheria zake mwenyewe katika biashara hivyo hakutaka kwenda mbali.

“Basi nakuahidi sitowatafuta na kuwatambulisha kwako , lakini ikitokea ukakutana na mfanyabiashara ambae nafahamiana nae usije kunilaumu”Aliongea.

“Ili mradi kuna sababu ya msingi ya ushirikiano haina shida, ila kama anakubali tufanye biashara sio kwasababu ya uwezo wangu bali kwa urafiki wenu siwezi kubali”Aliongea Regina.

“Sawa , mimi nitakufauta tu na kuwa msaidizi wako mtiifu , ondoa shaka kabisa”

“Inafurahisha namna unavyojiongelea kama mtu maarufu vile, Si mtu mkubwa unaefahamiana nae ni Master Alec na Dokta Ronicas tu? Kuna matajiri wengine unaofahamiana nao , maana unavyoongea ni kama vile una urafiki na Katibu mkuu wa umoja wa mataifa”Aliongea Regina huku akitabasamu kwa kumchokoza.

Hamza alijiambia Katibu wa umoja wa mataifa ndio nani kwanza, hata hivyo hakutaka kumwelezea sana mrembo huyo na kubakia kimya.Isitoshe hakuwa mtu anaependa umaarufu.

Nusu saa mbele Regina aliacha kuuliza maswali na alipitiwa na usingizi.Namna alivyokuwa amepotelea usingizini alizidi kuwa mrembo.

Hamza aliishia kuomba blanketi ktuoka kwa mhudumu na kisha kumfunika na mhudumu alionekana kumwonea Hamza wivu.

"Sir, your girlfriend is so beautiful.”Aliongea mhudumu kwa kingereza akimsifia Regina.

“She is my wife.” Alijibu Hamza akiwa na tabasamu na kumfanya mhudumu kushangaa na kumpa hongerea ya kuwa na mke mrembo sana.

ITAENDELEA USIKOSE.
 
Back
Top Bottom