Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU​

MTUNZI:SINGANOJR​

SEHEMU YA 176.

Prince Mahmood​

Baada ya masaa kadhaa kuwa hewani hatimae waliweza kutua ndani ya jiji la Paris katika nchi ya mafuvu.

Kampuni ya Dosam ilikuwa na tawi lake la kibiashara ndani ya jiji hilo,ijapokuwa lilikuwa dogo na kuwa na wafanyakazi wachache , kwa ujio wa Regina ililazimu wafanyakazi wote kuwa katika hamasa ya juu.

Watu waliofika Airport kumpokea Regina alikuwa ni meneja wa tawi hilo na baadhi ya wafanyakazi wa juu . Meneja wa tawi hilo alifahamika kwa jina la Joshua Mzena. Alikuwa ni raia wa Tanzania ambae ni mkazi wa kudumu ndani ya nchi ya Ufaransa.

Alianza kufanya Paris chini ya ubalozi wa Tanzania na baadae ndio alifanywa kuwa meneja wa kampuni hio tanzu, ijapokuwa umri wake ulikuwa ni zaidi ya miaka arobaini lakini alionekana kuwa ni mtu mwenye kujijari mno kwani alionekana kama kijana wa miaka therathini. Pia alikuwa mtanashati mwenye urefu wa zaidi ya mita moja na nukta nane.

Regina alikuwa amefanya kazi kama CEO wa kampuni kwa muda wa miaka mitano na alikutana na Josh ana kwa ana mara mbili tu , mara nyingi waliwasiliana kupitia Vidio Conference.

“Mkurugenzi tulikuwa tunawasubiri kwa muda mrefu sasa”Aliongea Josh pamoja na wenzake wakati wakisalimiana na Regina ambao ndio wanatoka katika jengo la wanaowasili.

Regina alikuwa amevalia Blauzi ya rangi nyeupe na Sketi ya Dark blue iliomfika magotini na koti la rangi ya kaki kwa nje . Ijapokluwa alikuwa amevalia miwani ya jua lakini silika yake na umbo lake la urefu vilimfanya kuwa sehemu ya macho ya wengi ndani ya uwanja huo wa ndege.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hio Tanzu kumuona CEO ana kwa ana , walionekana kuhamasika lakini pia kulikuwa na hali ya mshangao katika macho yao , hususani kwa baadhi ya raia wa nchi hio.

Regina aliishia kupeana mkono na Meneja na wafanyakazi wote na kisha palepale alianza kuongea kwa kingereza maana hakuwa akifahamu kifaransa.

“Mmejitahidi mno , ila haikuwa na haja ya kujisumbua kwa kuja watu wengi namna hii , isitoshe tutaonana kwenye kampuni wakati wa mchana”Aliongea.

“Haha.. CEO hii ndio ishara ye heshima ambayo tunaweza kukuonyeshea kwa niaba ya wafanyakazi wote 136 wa kampuni.Nakumbuka mara ya mwisho wakati tunaonana ana kwa ana ilikuwa ni miaka miwili iliopita na sasa hivi umerudi tena ukiwa ni CEO na Mwenyekiti hongera sana”Aliongea Josh akiwa na tabasamu.

Regina alikuwa ashazoea maneno ya kusifiwa mara nyingi hivyo hayakumgusa sana.

“Tuondokeni kwanza , tutaanzia kufikia hotelini”Aliongea Regina.

“Sawa” Josh aliitikia na muda huo alimwangalia Hamza na tabasamu na kisha akaongea.

“Wewe kama sikosei utakuwa Hamza Msaidizi , si ndio? Mimi jina langu naitwa Joshua Mzena , wengi wanafupisha kwa kuniita Josh tu , nimesikia sana kuhusu habari zako kwa muda mrefu”Aliongea

Hamza alijiwazia palepale hajafanya kazi kwa muda mrefu ndani ya kampuni ya Regina , inakuwaje huyo bwana akasema amesikia jina lake muda mrefu , isitoshe hata ndani ya kampuni kwa kipindi alichohudumu hajafanya kazi kubwa.

“Meneja Josh, nimesikia pia wewe ni moja ya wafanyakazi muhimu ndani ya kampuni ya Dosam baada ya Regina . Shukrani kwako sasa hivi kampuni ya Dosam inafahamika nje ya nchi . Nimelisikia jina lako kwa muda mrefu pia”Aliongea.

“Haha. Mr Hamza unanipaka mafuta kwa mgongo wa chupa , nawezaje kupokea hizo sifa ilihali sisi ni kama walinzi tu ndani ya kampuni na kazi yote anafanya Mkurugenzi. Tumefeli kutoa mchango mkubwa na kumsambabishia mkurugenzi kuweka juhudi kubwa . Kila siku tunamshukuru Mkurugenzi kwa kuendelea kutuvumilia na imetufanya kuwaza ni namna gani tunaweza kulipa ukarimu kwake”

Hamza mara baada ya kusikia hivyo alitamani kucheka , ilionekana bwana huyo alikuwa akiujulia uchawa sio kawaida maana sio kwa kulirudia rudia jina la Mkurugenzi mara nyingi katika sentensi moja.

Muda ule Regina na Hamza walitemba na kwenda kuingia kwenye gari Mercedes-Maybach S680 na kuchukuliwa mpaka kwenye hoteli ya Four Seasons karibu na mtaa wa George Avenue.

Four Season ni moja ya hoteli ya kifahari ndani ya jiji la Parisi , kwa utajiri wa Regina hawazii kabisa ni siku ngapi za kukaa ndani ya hoteli hio. Isitoshe kwake yeye ni mchumi zaidi , asilimia kubwa ya mabilionea walikuwa na majumba nje ya nchi lakini yeye hakuwa na nyumba yoyote nje ya nchi.

Hamza mara baada ya kuingia ndani ya hoteli hio alidhania wataenda kukaa ndani ya chumba kimoja , lakini Regina aliagiza vyumba viwili, huku akichagua chumba cha kifahari na upande wa Hamza chumba chake kilikuwa cha kawaida . Lakini hata hivyo Hamza hakujali sana , alijiambia akitaka si ataenda tu kumgongea na kuingia ndani na kuichukulia fursa ya kuja Parisi na mrembo huyo.

Hamza alijiambia piga chini safari hio ya Parisi ndio ya kuimarisha uhusiano wake na Regina.

Mara baada ya kuweka mizigo, Regina hakuwa na muda wa kupumzika. Baada ya kubadilisha alipanga kwenda ofisini kwa ajili ya kikao na wafanyakazi haraka iwezekanavyo.

Hamza hakupinga na haraka za Regina ambae hakujali alikuwa ndani ya jiji la mapenzi lakini bado anawazia kazi tu.

Wawili hao waliweza kufika ofisini , makao makuu ya tawi la kampuni hio na walipokewa na Joshua vizuri tu na kikao kiliendelea na kuisha saa moja kamili za jioni.

“Mkurugenzi baada ya kusikiliza mafundisho yako , tumepata kujifunza vitu vingi mno . Tumeweza kufanikiwa kujua vipi ni vipaumbele vyetu na malengo kwa kazi zinazotusubiria!. Ni muda wa chakula cha usiku huu na kwa kujishusha Mkurugenzi naomba unipe nafasi ya kuwakaribisha wewe na Msaidizi wako kwenye mgahawa niliokwisha kuweka oda, ni moja ya migahawa maarufu sana ndani ya Paris na nilifanya booking miezi miwili iliopita”Aliongea Josh na kumfanya Regina kumwangalia Hamza.

“Unaonaje?”Aliuliza na Hamza alionekana kutokuwa na pingamizi.

“Meneja mgahawa unaozungumzia ni ule wa kule Square?”Aliuliza Hamza na kauli yake ilimfanya Josh kushangaa

“Ndio Bwana Hamza , umejuaje? Ni pale Place des Vosges ndani ya Marais district”

“Kumbe! Sema nina njaa sana , hebu simamisha gari kwanza ,nimeona pale wanauza hotdog ninue nipunguze njaa wakati tukiendelea na safari”Aliongea Hamza(Hotdog ni aina ya Soseji).

Baada ya dereva kusimamisha gari , Hamza alishuka haraka haraka na kwenda kunua hotdogs mbili na kurudi huku akitafuna.

“Tuondoke sasa”Aliongea

Regina aliishia kukunja sura tu maana baada ya kuingia nazo harufu ilijaa ndani ya gari.

“Hamza ushawahi kufika hapa Paris? Unaonekana kupafahamu vizuri”Aliuliza Josh na Hamza aliekuwa akiendelea kushambulia soseji zake aliishia kutingisha kichwa.

“Sio mbaya, ni tamu mno”Aliongea Hamza.

Upande wa Regina alijua Hamza alikuwa yupo vizuri kwenye kuongea kifaransa lakini hakujua kama pia alikuwa akilijua jiji la Paris vizuri.

“Huko square ndio wapi?”Aliuliza Regina.

“Tunaita Henry IV's Royal Square, mwanzoni kipindi cha mapinduzi paliitwa Parry Commune ila badae katika karne ya kumi na tisa jina lilibadilishwa na kuwa Place des Vosges”Aliongea Hamza kawaida kabisa.

“Hamza kweli unaonekana kuifahamu Paris na historia ya nchi yake”Aliongea Josh muda huo akijua sasa Hamza ambae alionekana kusinzia wakati wa kikao hakuwa mwepesi.

Regina alionekana kuvutiwa , ukweli ni kwamba maisha yake yalikuwa ni kusoma sana kwa ajili ya kurithishwa kampuni na hata baada ya kumaliza kusoma moja kwa moja alipewa kampuni kuongoza na hakupata muda wa kusafiri kwa ajili ya mapumziko.

Alikuwa na hela sana , lakini hakupata muda wa kuufurahia utajiri wake.Lakini bado alikuwa ni msichana mdogo na alitamani sana kusafiri, kupiga picha, kufanya shopping na kucheza. Kama Hamza alikuwa na uelewa wa maeneo mengi ya Paris aliona si ni fusa hio ya kumtembeza?.

“Kwasababu unaijua Paris vizuri unaonaje ukiwa Tour Guide wangu?”Aliongea Regina.

Hamza mara baada ya kusikia hivyo hamasa ilimvaa palepale na asingeweza kupinga kama Regina yupo tayari kuachana na kazi na kuamua kufanya matembezi.

“Wi.. namanisha Bosi hakuna tatizo kabisa , nitakutembeza maeneo yote kwanzia leo. Mimi ni Tour Guide mzuri na likija swala la kula bata sidhani kuna anenipiku”

“Kweli?”

“Usiwe na wasiwasi kabisa yaani hapa ni Mission Complete kabla ya kuanza”Aliongea Hamza kwa kujisifia huku akimalizia soseji yake.

Regina alijikuta akijawa na shauku kubwa lakini hakutaka kuonyesha waziwazi.

“Meneja Josh nitarefusha siku tatu za safari yangu hapa”Aliongea Regina.

Josh upande wake alikuwa kwenye majuto , alipanga kuwa Tour Guider kwa bosi wake ili kuongeza ukaribu wake na hata kunufaika lakini Hamza kaamua kumuibia nafasi yake , hakuwa na furaha hata kidogo.

Saa moja mbele waliweza kufika nje ya mgahawa uliofahamika kwa jina la T. Ambrosia .

“Mkurugenzi huu mgahawa ni maarufu sana wenye hadhi ya Michellin three Star. Nimetumia juhudi kubwa kuweza kufanya booking kwa ajili ya kupata nafasi kwa mwezi mzima. Chakula kinachopikwa hapa ni safi kabisa na cha kitamaduni zaidi. Wapishi wakubwa hapa ni baba na mtoto wake na wote wapo daraja la juu kabisa na wana uzoefu kwa zaidi ya miaka therathini”Aliongea Josh.

Regina mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akivutiwa . Ijapokuwa sio mtu wa kuchagua sana kuhusu vyakula lakini aina ya vyakula ambavyo maana yake imejificha katika historia na tamaduni ilimfanya avutike.

“Jina lake mbona fupi sana , linamaanisha nini?”Aliuliza Regina.

“Hata mimi sijui , labda tuwaulize wafanyakazi”Aliongea Josh lakini Hamza aliekuwa pembeni yake alijibu kwa kingereza.

“Katika ulimwengu wa simulizi za kigiriki kuhusu miungu kulikuwa na sehemu ambayo iliaminika kuwa na vyakula vyenye radha tofauti tofauti tamu bila ukomo na vinywaji vyake pia ambavyo viliwafanya miungu kuwa na maisha marefu. Sehemu hio iliitwa Ambrosia Paradise . Ndio maana mgahawa huu wakaupa jina la T. Ambrosia”Aliongea Hamza na kumfanya Regina na Josh kushangaa.

“Unaongea ukweli au unaongea pumba kutufurahisha”Aliuliza Regina.

“Kwanini niongee pumba wakati ni kweli?”

“Bwana Hamza wewe umejuaje , ushawahi kufika hapa kula?”Aliuliza Josh.

“Hapana , kuna mtu aliniambia”Aliongea.

“Basi twende tukaulizie kama ni kweli”Aliongea Josh.

Mara baada ya watatu hao kufika eneo la kuingilia wahudumu waliwasaidia kuvua makoti ya baridi kwa heshima kubwa na kisha yakakunjwa na kwenda kuhifadhiwa.

Josh kabla hata ya kuingia alimuuliza kwanza mhudumu kuhusu maana ya jina la mgahawa huo na alijibiwa kama Hamza alivyoongea.

Muda huo Josh alijikuta akijisikia vibaya , wakati Regina macho yake yakichuanua . Hakuwaza Hamza kweli alikuwa sahihi , lakini licha ya hivyo alijikuta akijawa na shauku ya kutaka kujua ni nani Hamza alimwambia hio stori.

Baada ya kutaja majina yao , mhudumu aliwachukua mpaka eneo maalumu kwenye siti zao.

Ingawa mapambo ya nje yalionekana rahisi, walipokaribia kuingia, taa kubwa za kioo, tapestry( Zulia za sufi za kuta) za kisasa kubwa na picha zenye muundo wa kifahari wa karne ya 18 wa rococo , zilikuwa za kupendeza na zenye mvuto. Zote zilionyesha hadhi kubwa ya kitamaduni.

“Huu mgahawa unapendeza mno .imenifanya nitamani kubadilisha mwonekano wa kule nyumbani na mapambo ya namna hii”Aliongea Regina ambae alionekana kuvutiwa mno na mapambo.

“Mkurugenzi nafahamiana na mfanyabiashara mmoja ambae anauza mapambo ya namna hii . Kama ukipenda nitaongea nae akutumie hio michoro na Tapestri”Aliongea Josh.

“Hio michoro ya mafuta na mazulia ya ukutani yatakuwa ghali mno kwa yanavyoonekana tu . Naamini mpaka kuufanya huu mgahawa kuonekana hivi ni hela nyingi zimetumika”Aliongea Regina

“Lakini mkurugenzi kwako wewe hela si hesabu tu?”Aliongea Josh na tabasamu.

“Meneja hivi kwanza unajua ni wapi hizi Tapestri zinatokea?”Aliuliza Hamza.

“Si Tapestri kama Tapestri kuna haja ya kujua zinapotokea?”Aliuliza.

“Hizo ni Aubusson Tapestri. Baada ya Karne nyingi kupita zimekwisha kuwa Antiques, Blanketi za kale kutoka Aubusson zilizosheheni tamaduni ya karne . Unadhani ni kitu ambacho unaweza kununua kwasababu tu una hela?”Aliongea Hamza.

Josh aliishia kushikwa na aibu tu . Angejuaje hayo yote sasa kama sio Hamza kumuonea? . Ijapokuwa alishawahi kuja kula hapo mara moja , lakini hakuwahi kuwaza mapambo hapo uhalisi wake ni wa kale mno.

Regina aliishia kumwangalia Hamza kwa macho ya maswali mengi na tanabahi, aliona tokea sekunde ambayo walitoka nje ya mipaka ya Tanzania , Hamza ni kama amefika nyumbani.

Muda huo wakati wakisubiria kwa ajili ya kuagiza chakula chao kuandaliwa , mwanaume mzungu alievalia suti na viatu vya kung’aa aliwasogelea.

Mzungu huyo alionekana kuwa ndio meneja wa mgahawa huo na alimwangalia Regina kwa tabasamu.

Lady, are you single?"Aliuliza yule bwana akimuuliza kama Regina hana mpenzi na swali lile lilimshangaza Regina kwa sekunde huku akimwangalia Hamza bila kupenda na kwasababu ya uwepo wa Josh alitingisha kichwa.

“Ndio , Kuna tatizo?”Alijibu hivyo Regina na kumfanya yule mzungu kutoa pumzi ya ahueni.

“Hongera kwako , Prince Mahmoud anaomba ujumuike nae kwa ajili ya chakula”Aliongea na muda huo alinyoosha kidole kuelekea chumba ambacho hakikuwa mbali sana . Kupitia dirishani alionekana mwanaume alievalia Kilemba cheupe na Regina mara baada ya kuangalia upande huo aliweza kumuona mwanaume akimpa ishara ya mkono huku akionekana kushikilia kinywaji mdomoni.

Katika mgahawa huo maarufu ilikuwa ni kawaida sana kukuta watu maarufu na kuntu wakipata chakula.

“Unaweza ukawa hufahamu , Prince Mahmoud ni mtoto wa tatu ndani ya familia ya kifalme nchini Saebia, ndio mmiliki wa Club kubwa ya mpira hapa Paris , na mara nyingi anafika hapa kwa ajili ya chakula. Ni mtu muungwana sana na wanawake wote wanaopata mafasi ya kukaa meza yake wanahesabika kuwa wenye bahati kubwa. Kwa urembo wako naamini Prince atakupendelea mno”

Ukweli haikuwa mara ya kwanza kwa meneja huyo wa mgahawa kufanya hivyo , unaweza kusema tofauti na kuridhisha wateja na chakula kitamu , lakini vilevile alikuwa kama dalali kwa mahitaji mengine wateja wake wanapomtaka kufanya hivyo.

Lakini Regina asingekubali , kwa maelezo hayo yote ni kama yalimfanya kutokumpa nafasi hata ya kumfikiria.

“Mwambie siko interested”

Hakutaka hata kujisumbua kuendelea kusikiliza kama alikuwa Prince au ana hela kiasi gani , hata kama angekuja mfalme mwenyewe asingemkubalia.

Meneja yule alijikuta akishangaa , kama vile ilikuwa mara ya kwanza kukutana na mwanamke Single ambae ni kipofu . Ilihali hata wale wanawake ambao walikuwa katika ndoa zao walipopata mwaliko hawakupoteza fursa zaidi ya kuvua pete zao za ndoa na kuzificha na kuwaacha waume zao.

“Dada fikiria kwa umakini juu ya hili , ijapokuwa Prince Mahomod ni mtu mkarimu na mwenye huruma , lakini asiporidhishwa na kitu anaweza kufanya vitu vya ajabu . Anachotaka ni kukaa na yeye kwenye meza moja tu na hakuna kitu kingine kitakachotokea”Alishauri Meneja.

“Mkurugenzi , Nasikia huyu Prince Mahmoud ana urafiki mkubwa na Waziri wa biashara na uwekezaji ndani ya serikali ya Mafuvu, kwa mpango wetu wa kufanya biashara hapa , kama tutamkasirisha sidhani itakuwa rahisi kwetu”Aliongea Josh.

Regina aliishia kukunja sura . Ni kweli alikuwa akijali sana kuhusu waziri wa biashara na uwekezaji wa Ufaransa kutokana na ndio mtu ambae anaweza kuamua biashara yake kuendelea ama kutoendelea hapo , lakini aliona ni kama alikuwa akidhalilishwa kwenda kumpa kampani mtu ambae hata hamfahamu kisa tu ana cheo cha Prince.

“Achana nae na mpotezee , mimi nipo hapa”Aliongea Hamza ambae alitoa tabasamu huku akimkonyeza Regina.

Regina mara baada ya kuona mwonekno wa utulivu wa Hamza , ingawa alikuwa na wasiwasi lakini aliishia kutingisha kichwa.

“Mwambie siji”

Meneja yule alishindwa kujizuia na kudharau ujinga wa Regina . Akiwa na sura iliokunjamana aliishia kugeuka zake na kwenda ndani ya chumba kile binafsi kuelezea.

Prince Mahmoud mara baada ya kuambiwa kilichoendelea , sura yake ilikunjamana na alionekana kumpa maelekezo mengine yule meneja ambae alionekana kutingisha kichwa kuyapokea.

Hamza na wengine waliona Mwanamfalme yule pengine alikuwa na busara, hivyo ameachana na wazo la kuwasumbua na palepale walijiandaa kwa ajili ya kuagiza chakula chao.

Regina alijua Hamza ni mzoefu hivyo alimpa kitabu akimwambia amsaidie kumwagizia. Hamza hakujali na alichukua nafasi hio na kisha akaongea na muhudumu.

"Etuvé-d-noix.-Sint-Jcqus-n-PRISINn-d - légums-à -l-truff-fr? "CHI …”

“Samahani Sir , hakuna zaidi. White Truffle zimeisha”Aliongea mhudumu na tabasamu la radhi.

Upande wa Regina aliekuwa akisikia kinyakyusa tupu , alionekana kuchanganyikiwa

“Ni aina gani ya chakula?”

“Mchanganyiko wa Scallops na mbonga za majani unaenda sawa kukiwa na White Truffle . Radha yake inakuwa nyepesi lakini tamu sana na inaendana na wewe sana sana, lakini eti wanasema Truffle zimeisha, sijui hata nini kinaendelea”Aliongea Hamza

“Tunaweza kuagizatu kingine kinachopatikana”Aliongea Regina na Hamza hakuona hata haja ya kuangalia orodha ya vyakula na alimpa maelekezo mengine yule mhudumu.

"Viande de bar avec de fines tranches de lys et du caviar.”Aliagiza lakini yule mhudumu alitingisha tena kichwa kukataa.

“Samahani , Cavier pia zimeisha”

“Nini!” Hamza palepale alihisi kuna kitu hakipo sawa.

“Kama hivyo hamna ni kipi mnacho?”

“Le serveur a dit : 'Seulement un vin de Bourgogne ? Qu'en est-il du vin rouge de Mosul du Manoir Demoux ?”Aliongea akimaanisha kwamba hapo ndani kinachopatikana ni mvinyo pekee wa aina hizo alizotaja.

Hamza aliishia kukunja ndita na kisha aligeuza uso wake na kumwangalia Prince Mahmoud kwenye kijichumba na palepale alimrushia mhudumu kile kitabu cha menu.

“Wewe sema tu tu kila kitu kimekwisha kununuliwa na yule mtu, si ndio?”

“Samahani sana kusema ni kweli kila chakula kimeununuliwa na Prince kasoro nilivyotaja..”Aliongea kwa kingereza na kumfanya Regina kuelewa.

“Inakuwaje Prince kuwa na tabia ya namna hii”Aliongea Regina akionekana kukasirika mno.“Kama ni hivyo haina haja ya kula tena , tuondokeni”Aliendelea kuongea

Joshua hakutegemea mambo yatafikia hatua hio na aliishia kuomba radhi akiwa na uso mchungu.

“Nisamehe Mkurugenzi , nilikosea kuwaleta hapa”Aliongea.

“Tuondoke! Kwanini tuondoke?”Aliongea Hamza huku mwonekano wake wa utulivu ukipotea na wa ukali kumvaa.

“Kwahio kama tusipoondoka tutaendelea kufanya nini hapa , tuendelee kunywa tu mivinyo . Prince ndio kafanya haya na anafahamaiana na vigogo wa serikali utaweza kumfanya nini?”Aliongea Regina akiwa hana furaha hata kidogo.

“Kwahio akiwa prince ndio nini , anathubutu vipi kunichokoza , halafu niondoke bila kufanya kitu”Aliongea Hamza huku akisimama na tabasamu la uovu likiwa limeupamba uso wake.

Regina mara baada ya kusikia hivyo , alikuwa na furaha kuona Hamza anamlinda lakini alikuwa na hofu Hamza atajiingiza kwenye matatizo.

“Hamza usikurupuke , hii sio nchi yetu na hatufahamiana na watu wengi..”

“Kwahio kwasababu sio nchi yetu tuache watuonee wanavyotaka?”Aliongea Hamza akigeuka wakati huo akitaka kwenda ndani ya kile chumba Lakini Hamza alimshika mkono.

“Usiende wewe vumilia tu , haina haja ya kujisumbua na mtu wa aina yake zaidi ya kupoteza muda wetu , ni swala la kumwelewa tu”Aliongea Regina

Hamza aliishia kusimama huku akijiambia ni kama anacheleweshwa , maana alipanga kwenda ndani na kumtia ngumi.

“Nataka kumrekebisha tu”Aliongea

“Hapana wewe una taka kwenda kumpiga , unajua itakuwaje baada ya hapo ?”

Regina alikuwa na wasiwasi mno , alijua kwa hela alizokuwa nazo huyo bwana haitakuwa ngumu kutafuta watu wa kuwaua . Lakini kwa wakati mmoja akiona Hamza anajikadiria kwa vigezo vya juu kudhania anaweza kutatua kila tatizo kwa kupigana.

“Hamza alichoongea mkurugenzi ni sahihi , usikurupuke kutaka kupigana na Prince sio swala rahisi . Mabodigadi wake wote pale wana bunduki”

Hamza aliishia kushindwa kufanya chochote baada ya kuona Regina anamzuia kutokana na kutokumjua yeye ni nani mpaka kutaka kuchukua hatua hio.Lakini hata hivyo aliona ni sahihi kwa Regina kuwa na wasiwasi.

Baada ya kuona Regina ameomba sana , aliamua kutulia huku akijiambia ni kwa ajili ya kumridhisha Regina tu ila baadae atamrudia.

“Sawa sitoenda , lakini lazima nipate chakula hapa hapa siwezi kuhangaika tena”Aliongea Hamza akiwa siriasi.

“Utafanyaje sasa kama wamekataa kutuhudumia , unapanga kumpiga na mhudumu?”Aliongea Regina huku akiwa na wasiwasi Hamza ataanzisha vurugu tena.

“Usiwe na wasiwasi , nina njaa hivyo sitoshindana nae kwasasa. Nataka kuongea na mmiliki mwenyewe wa mgahawa juu ya hiki kinachoendelea”Aliongea Hamza na kisha palepale alimwangalia yule mhudumu.

“Mathew na mtoto wake Bernard wapo wapi?”Aliuliza na mara baada ya mhudumu kusikia Hamza akiulizia hivyo alishangaa

“Sir , unafahamiana na Mzee Paco?”Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa.

Mathew na Bernard Paco , ni mtoto na baba na ndio wapishi na wamiliki wa mgahawa huo ambao pia ni maarufu sana ndani ya nchi hii ya Mafuvu.

“Kama una urafiki na mpishi wetu , kwanini hukuongea mapema?”Aliuliza Mhudumu yule akionekana bado haamini.

“Mbona unauliza maswali mengi ? Waambie watoke huko ndani na wakija itajulikana nafahamiana nao au lah”Aliongea Hamza.

“Wote hawapo leo . Raisi anapokea wageni kutoka nje ya nchi na aliwaomba kwenda Ikulu kwa ajili ya kusaidia swala zima la mapishi”Aliongea.

Kama mpishi wa kimataifa , ilikuwa kawaida mara nyingi kuitwa na watu wa serikali kwa ajili ya kuhudumia.

“Kumbe.. ndio maana naona baadhi ya vyakula vingi hapa ndani havivutii, kumbe ni wasaidizi wao ndio wapo . Anyway kama ni hivyo unaonaje ukiwapigia simu , mimi nitaongea nao mwenyewe”Aliongea Hamza na yule mhudumu alionekana kusita kidogo.

“Mimi siwezi kuwapigia labda niongee na Meneja . Subirini kidogo..”Aliongea mhudumu huku akienda kumuita Meneja.

Joshi alioneakna kushangazwa na jambo lile na alionekana hakuwa akiamini kabisa.

“Hamza unataka kusema unafahamiana na bosi wa hapa?”

“Ndio , mlivyoniambia niwaeleze jina la huu mgahawa nikawaambia , unadhani nani aliniambia maana yake? Alienielezea ni mmiliki wa hapa bwana Mathew Paco”

“Ndio maana ulikuwa sahihi sana kuhusu hii sehemu , kumbe unafahamiana na bosi”Aliongea Joshua huku furaha ikirudi.

“Kama ni hivyo basi lazima tupate chakula chetu hapa hapa bila tatizo”Aliendelea kuongea.

“Una urafiki pia na mpishi wa hapa . Mwanzoni ilikuwa mshonaji nguo na daktari na sasa hivi ni mpishi tena. Mbona inaonekana unafahamiana na kila mtu mzito ?”Aliongea Regina aliekuwa katika mshangao.

“Mimi ni mtu wa kujichanganya ndio maana”Aliongea Hamza akitoa tabasamu bila ya kuelezea zaidi.

Haikuchukua muda meneja alitoka akiwa na hali ya maswali kwenye sura yake

“Jina lako nani Sir?”Aliuliza Meneja.

“Naitwa Hamza Mzee”

“Sasa Mr Hamza kama kweli unafahamiana na bosi wetu , kwanini usimpigie simu mwenyewe?”Aliuliza Meneja.

Hamza mara baada ya kuambiwa vile alijifikiria kidogo na kujiambia kwa madaraja waliokuwa nayo Bernard na baba yake kwa vigezo vipi ahifadhi namba zao? Kawaida kama angetaka kuwasiliana nao angetumia watu wengine tu.Lakini Hamza hakuwa na muda wa kuelezea ukweli huo na akaaminika.

“Nilibadili simu na namba . Mpigie wewe kisha nipe niongee nae atanifahamu”Aliongea na meneja alionekana kusita . Lakini bado aliona sio vizuri kumdharau Hamza , kama anafahamiana na Bosi na ni marafiki itakuwaje kuhusu kibarua chake?.

“Okey , subiri kidogo”

Meneja palepale alitoa simu yake na kupiga namba flani na muda mchache tu ilipokelewa.

“Kuna nini?”Sauti ya mwanaume aliesikika kwa lugha ya kifaransa ilisikika.

“Samahani Mr Paco . Kuna mgeni hapa kajitambulisha kwa jina la Hamza , anasema ni rafiki yako ..?”

“Hamza , ni mtu kutoka nchi gani ? Sina urafiki na mtu huyo mimi,itakuwa anakudanganya ..”Aliongea Mr Paco lakini ni muda uleule Hamza alinyakua simu ile kutoka kwa Meneja.

“Ni mimi hapa..”Aliongea Hamza.

SEHEMU YA 177.

Lilikuwa neno moja tu na jepesi lakini lilifanya upande wa pili kuwa kimya kwa senduke kadhaa. Mathayo Paco ilionekana ni kama alikuwa kwenye mshangao au pengine hakusikia vizuri.

Baada ya kuisikia sauti ya Hamza ya kifaransa alijikuta akiwa katika kutafakari kwa sekunde kadhaa

“Oh! Mungu wangu ..” Mathayo alionekana kuhamasika mara moja huku akiongea kwa nguvu . na palepale alituliza sauti yake na kuiweka katika hali ya heshima.

“My- Prince umepata muda wa kuja kwenye mgahawa wangu , mbona kama naota vile? Kwa muda mrefu nilikuwa nikitamani hii siku ifike . ijapokuwa nimekupikia sana kule kisiwani , lakini sikupata fursa ya kukaribisha kwenye mgahawa wangu. Niseme tu kufika kwako kumetimiza moja ya ndoto yangu , nina furaha , nina furaha sana . Mimi na mtoto wangu tulitarajia sana hii siku …” Mathayo alionekana kama vile amefungwa betri jipya kwa namna alivyokuwa akiongea huku hata meneno yake yakikosa mtiririko , ili mradi tu kuwakilisha furaha yake.

Hamza upande wake alitamani kucheka kutokana na upande wa pili ulivyoonyesha kuchanganyikiwa

“Sawa nimekusikia , sio ndoto tena maana nimefika . Haraka hebu waambie hawa wafanyakazi wako nina njaa na nataka chakula sasa hivi”

“Sawa , lakini si unataka kula chakula nilichoandaa mimi? Nipo huku ikulu ila naweza kuongea tu na mheshimiwa na tutaweza kurudi mimi na mtoto wangu sasa hivi ..”

Kama kuna mtu angesikia maneno ya Mathayo angeshangaa mno . Wangeona ni kama mpishi huyo ameingiwa na wazimu wa ghafla kwa kutaka kuachana na swala la kumpikia raisi na kutaka kurudi haraka kumpikia Hamza.

Upande wa Hamza aliona ni kama usumbufu sasa ila aliishia kutingisha kichwa.

“Utachukua muda gai mpaka kufika hapa?”

“Mapema sanaa, Hatupo mbali sana naweza fika hapo ndani ya dakika ishirini”

“Haina ulazima sana maana tayari njaa imenishika . Hebu ongea kwanza na watu wako maana hawataki kunipa chochote”Aliongea Hamza na palepale alimkabidhi meneja ile simu.

Meneja mara baada ya kupokea simu ile na kuweka sikioni alianza kufokewa na Mathayo , akimuuliza kwanini hajamuandalia Hamza chakula kitamu.

Meneja alianza kujitetea kwa kumtaja Prince , lakini aliishia kuambiwa aachane na Prince na amhudumie kwa sahani ambazo zina saini yake kabisa.

Japo meneja hakuelewa sababu ya bosi wake kupaniki namna hio , lakini hakuthubutu kukataa kusikiliza maelekezo hayo , Baada ya kumuomba radhi Hamza haraka sana alienda kuwaagiza wengine kuandaa chakula.

Meneja na wahudumu walijikuta wakishikwa na shauku ya kumfahamu Hamza ni nani ,. Hawakuelewa mtu kama yeye anaweza kumfanya bosi wake kumpotezea Prince Mahmoud na kuhudumiwa yeye tena kwa sahani zenye sahihi ya mpishi.

Mara baada ya kuona swala hilo limeisha namna hio , Regina na Joshua walijikuta wakiona ni ajabn kweli , hususani Josh ambae alidhani alikuwa akiota.

“Shukrani sana kwako Mr Hamza , ningedhalilika usiku wa leo”Aliongea Josh.

“Usijali , kwa bahati nzuri nilianza kula hotdogs njiani , vinginevyo njaa ingeniua hapa”Aliongea Hamza huku akishika tumbo lake.

“Una uhusiago gani na Mathayo? Naona hajali kabiswa swala la uwepo wa Prince?”Aliuliza Regina bado akionyesha kuwa na wasiwasi.

“Usijali , anajua anachokifanya”Aliongea Hamza.

Haikuchukua muda jiko lote lilijaa ubize na msosi mmoja baada ya mwingine uliandaliwa kwa kupambwa kabisa.

“Haha… kuleni kabisa mshibe , msiwe na wasiwasi kuhusu malipo maana hakuna haja ya kulipa”Aliongea Hamza huku akionekana kutokujali kabisa namna anavyokula , mara nyingi chakula hiko cha kimagharibi kinaliwa kimagharibi pia.

Suala hilo la Hamza kuandaliwa chakula lilimfanya Mahmoud aliekuwa kwenye chumba chake binafsi kukasirika mno na palepale alimwita yule meneja.

“Meneja si nimekwambia nitalipia kila kitu kilichopo jikoni , kwanini bado mmewaandalia chakula?”Aliuliza kwa kingereza.

Your Royal Highness, because Mr. Paco and that gentleman are friends, we also provided them with additional dishes. But don't worry, you'll be able to buy a lot of ingredients. We'll make up for whatever we lack …”Aliongea Meneja akimaanisha kwamba kwasababu ya Hamza kufahamiana na Paco ndio maana wamewaandalia na ziada , ila asiwe na wasiwasi watamfidia.

“Mwanahramu wewe , ina maana huelewi ninachomaanisha? Nimekataa wasiandaliwe chakula cha aina yoyote. Inamaana Paco ameanza kunidharau kwa ajili ya yule mtu?”Aliongea Mahmuod.

“Kuhusu hilo hata mimi sina uelewa , nimepokea tu maagizo , pili yule bwana anafahamika kwa jina la Hamza , wote wanaonekana kuwa Watanzania”

“Yaani Mtanzania , nilidhania ni mtu mwenye cheo serikalini au tajiri? Ila kwasbabu mmeamua kunidharau na hamtaki kusikiliza maelekezo yangu basi msinilaumu kwa nitakachofanya”Aliongea na kisha palepale alichezesha vidole vyake

Nyuma yake wanaume wawili weupe waliojazia miili , wenye vipara na vifaa vya masikioni haraka sana walitembea kusogea alipokuwepo Hamza.

“Prince naomba usiwa na jazba , bado kuna wateja wengi wanaokula hapa”Aliongea kwa kuomba.

“Wasiwasi wa nini , kuna hela yoyote umepoteza? Hata kama ikitokea hivyo ntiafidia. Ila niache kwanza lazima leo nilale na yule mwanamke”Aliongea Mahmood na kisha palepale alichukua begi kutoka kwa msaidizi wake na alipolifungua ndani kulionekana vibunda vya hela za Euro na miche ya dhahabu na aliimwaga yote juu ya meza.

“Kama shida ni hela nadhani hizi zinatosha , kama hujaridhika naweza kukuingizia zingine kupitia benki , vingineyo nalipia hela ya kununua kabisa huu mgahawa”Aliongea Mahmood.

Meneja sura ilifubaa huku akiwa na mwonekano mchungu , nje kulikuwa na rafiki wa bosi wake na ndani alikuwa ni Prince wa Saebia , alijikuta akiwa kati na hakuna ambae alitaka kumkusea.Kwa mara ya kwanza maisha yake yanakuwa magumu sana kazini.

Muda huo Hamza aliweza kuona mabodigadi wawili wakisogelea .Aliishia kutabasamu tu huku akimwangalia Regina.

“Unaona sasa hatujawachokoza lakini hawataki kutuacha”

Regina alikuwa ashapiga zake vijiko kadhaa na mara baada ya kuona tukio hilo alijikuta akikunja sura .

“Kwanini huyu Prince yupo hivi , kama ni hivi tuondokeni tu”

“Unataka twende wapi? Hata kama ni uvumilivu una mipaka yake , kama sio wewe kunizuia muda ule ningeshalitatua hili tatizo mapema sana”aliongea Hamza na hakutaka kumpa nafasi ya pili Mahmood.

Mabodigadi wale wawili walikuwa wamefika tayari katika meza yao . Mmoja aliinua koti lake la suti na kuonyesha bastora ya Desert Eagle, huku mwingine akipiga ngumi meza yao.

“Prince wetu anamtaka huyu mrembo kwa ajili ya kula nae chakula”Aliongea kibabe kama vile na Regina alikuwa ni mali ya Prince.

“Sitaki”Aliongea Regina akionekana kukasiirika na palepale alishika mkoba wake.“Tuondoke”

Yule bodigadi mwenye kipara palepale alitoa bastora na kuiweka juu ya meza .

“Sio swala la wewe kuamua hili”

Regina mara baada ya kusikia vile uso ulibadilika palepale na alimwangalia Hamz akiwa wasiwasi.

Wateja waliokuwa wakipata chakula mara baada ya kuona tukio hilo,walijikuta wakiwa katika hali ya hofu . Na baadhi yao walikuwa washashikilia mikoba yao kwa ajili ya kuondoka.

Muda huo yule bodigadi aliekuwa ameshikilia bastora ghafla tu alitoa sauti ya maumivu.

Muda ule uma ilikuwa imepita juu ya kiganja cha bodigadi yule katika mkono ambao alikuwa ameshikilia bastora juu ya meza , huku uma ile ikipita hadi chini kutoboa na kufanya damu nyingi kuanza kumwagika zikichafua kitambaa cha meza.

Bodigadi yule mara baada ya kufanyiwa tukio lile alijitahidi kuvumilia maumivu na kuinua mkono mwingine kutaka kumpiga Hamza ngumi. Lakini ngumii ile kabla haijamfikia Hamza alishainua kisu na kuichoma na kile kisu kwa mara nyingine.

“Arghhhhhhh…”Kisu kile mara baada ya kupitia kwenye vidole vyake alipoteza fahamu kutokana na maumivu.

Mara baada ya tukio lile , bodigadi mwingine haraka sana alichomoa bastora yake na kutaka kumlipua Hamza , lakini Hamza sipidi yake ni kama radi kwani hata hakuelewa nini kilichotokea bastora hakuwa nayo tena.

Bodigadi yule alikuwa katika hali ya mshangao mara baada ya kugundua alikuwa amekwisha kupokonywa bastora , huku vidole vyake vikiuma mno. Ilionekana Hamza alikuwa ameuvunja mkono wake pia

Muda ule anainua macho kumwangalia Hamza alikutana na chuma ya baridi ikigusa paji lake la uso.

“Spidi yako ya kutoa siraha ni ndogo mno . Mtu kama wewe kuwa mlinzi nadhani Prince wenu anayo bahati mpaka sasa yupo hai”Aliongea Hamza huku akiwa anaendelea kutafuna chakula ma muda uleule alifyatua risasi nne.

“Bang , Bang , Bang , Bang “

Ijapokuwa Recoil ya aina hio ya bunduki ilikuwa na nguvu mno . ila Hamza aliishikilia na mkono mmoja tu bila ya kuyumba huku akifyatua kwa usahihi mkubwa.

Risasi zile zilikuwa kama moto wakati zikimpita yule Bodigadi na kwenda nyuma yake.

Bodigadi yule alikuwa katika hali ya kiwewe na aliishia kufumba macho yake tu . Lakini aligundua risasi zile zilipitia ubavuni kwake tu na hakuathirika nazo kabisa.

Hamza mara baada ya kumaliza kufyatua risasi zote , aliweka ile bunduki kwenye holder katika kiuno cha bodigadi.

Bodigadi aliishia kulegea na kujikalia chini , alikuwa na hofu kiasi kwamba sura yake ilianza kubadilika rangi.

Wazo la kuwa katika milimita moja umbali na kifo ni swala lililomtoa ndotoni.

Wageni wote waliokuwa wakipata chakula katika huo mgahawa waliishia kupiga makelele huku wakikimbilia nje na hata baadhi ya wahudumu pia, waliobakia ni wale waliokuwa majasiri pekee.

Regina upande wake alikuwa katika mshituko mkubwa. Hakuamini mtu ambae Hamza alikuwa akimfaytulia risasi ni Prince Mahmood tena ndani mgahawa wa nyota tatu ndani ya nchi ya watu.

Joshua upande wake alikuwa na hofu mno , aliishia kuweka mikono yake kichwnai akiwa amechuchumaa chini . Kama isingekuwa Regina kuwepo hapo angeungana na wengine kukimbia.

Hamza alitumia uma kumzimisha na bodigadi yule mwingine na kisha alianza kutembea kusogelea katika kile chumba alichokuwepo Mahmood.

Mara baada ya kuingia ndani aliweza kumuona bwana huyo akiwa amejificha chini ya meza.

Risasi alizofyatua Hamza ilikuwa ni kwa ajili ya kumuogopesha pekee na sio kumdhuru.

“Jitoe mwenyewe la sivyo nitakupasua”Aliongea Hamza kwa sauti nzito.

Mahmood alikuwa ameshikilia simu ya Iphone ilitengenezwa kwa madini Almasi na alikuwa ashawasiliana na mtu tayari kuja kuongeza nguvu.

Mara baada ya kumsikia Hamza akiongea , alijikuta akiwa hana jinsi na haraka sana alitoka.

“Unathubutu vipi kunifyatulia risasi , unajua mimi ni nani? Mimi ni mtoto wa tatu wa familia ya kifalme ,Prince Mahmoud Mohammed Bin Rashid….. arghhhh”

Hamza hakutaka taha kusikiliza jina lake lote na palepale aliinua mche wa Dhahabu na kumpiga nao mdomoni na kilichosikika ni sauti ya Khaa damu zilianza kumtoka na hata meno ya mbele yalionekana kupondeka.

Hajawahi kudhania hata katika ndoto atakuja kupigwa kwa kupondwa meno yake kwa kutumia dhahabu yake mwenyewe.

Mahmood aliishia kupiga yowe la maumivu huku akianza kuomba kuachwa.

“Naomba uniache , niachie , nipo tayari kukupa kiasi chochote cha fedha, nitakupa kila kitu”Aliongea

Alikuwa ni moja ya watoto pendwa ndani ya familia yake hivyo aliona kama hela anazo kwanini apitie mateso hayo ? Alijikuta akianza kujutia kuja ndani ya huo mgahawa bila mabodigadi wengi na kumchokoza kichaa kama Hamza.

Mara baada ya Regina , Josh , meneja na baadhi ya wahudumu waliobakia kuona tukio hilo walijikuta wakikosa neno.

“Hamza kwanini unampiga kiasi hicho?”Aliuliza Regina kwa wasiwasi.

“Kuna tatizo gani nikimpiga hivi , mtu haikuishia tu kutunyima kutokula chakula lakini pia akataka kukuchukua?”Aliongea Hamza.

“Nakwambia utajutia ulichonifanyia , Royal Guards hawapo mabali na hapa na kaka yangu pia amekuja Paris leo , lazima ataleta watu kunisaidia”

Mara baada ya meneja kusikia hivyo alijikuta akipagawa.

“Prince Maxim anakuja pia? Oh God .. what should we do?”

Regina aliishia kukunja ndita tu . licha ya kuwa mfanyabiashara lakini mara nyingi alikuwa akiangalia taarifa za habari , hivyo haikuwa ngumu kutokumfahamu mtu kama Maxim.

Crown Prince wa Saebia ndio huyo Maxim. Alikuwa akionekana sana kwenye vyimbo vya habari vya kimataifa na anasifika kwa kuwa na utajiri mkubwa sana ndani ya familia ya kifalme , alikuwa pia na madaraka ya kuongea kwa niaba ya nchi yake.

Watu wa aina hio walikuwa na ushawishi mkubwa sana kupitia hela zao , isitoshe hela zao zilikuwa na uwezo wa kuathiri mfumo mzima wa masoko ya fedha duniani.

Kwa kumlinganisha na Regina ambae alikuwan a trilioni kadhaa za kitanzania , hakuenea kabisa hata kwenye vidole vyake .

“Kwahio unahisi utaniogopesha , ngoja tuone huyo kaka yako uwezo wake ulivyo”Aliongea Hamza na kisha palepale alimshika Kola Mahmood.

“Kwahio unajiona kuwa tajiri ndio nini ? Kwamba kwasababu ya cheo chako unaweza kumpata mwanamke yoyote?”

“Wewe masikini hebu acha kunifanyia hivi , Kaka yangu atakufanya jambo baya sana”

“Simjali kabisa kuhusu kaka yako , lakini kwasasa nadhani unapaswa kupiga magoti na kumuomba huyu mwanamke msamaha”Aliongea Hamza na kisha palepale alimwinamisha kichwa chake chini kwa kumsukuma huku akimpiga na teke ambalo lilimfanya bila ya kupenda kupiga magoti kwa nguvu na kufanya kutokwa na damu.

Regina wa muda huo hakujua cha kufanya . ijapokuwa mwanzoni alikuwa na hasira lakini muda huo alikuwa na wasiwasi jambo baya linakwenda kumkuta Hamza.

“Hamza mwachie , sina hasira nae tena”Aliongea Regina.

“Hasira zako zimeisha , ila za kwangu bado! Mudi yangu ilikuwa vizuri mwanzo lakini huyu mtu kunifanya nisile chakula kwa utulivu ameniboa mno”Aliongea Hamza na palepale alimgeukia Meneja.

“Si umesema amenunua kila kitu ndani ya mgahawa huu ?”Aliuliza na Meneja bila kupenda aliishia kutingisha kichwa chake.

“Ndio , ndio”

Muda huo mgahawa ulitisha , maana Hamza ni kama kichaa kimempanda.Hata baada ya Prince kusema kaka yake na walinzi wake wengine wanakuja lakini Hamza hakuonekana kuwa na hofu na kuendelea kumletea fujo Mahmood.

“Kwasababu amenunua , sidhani itakuwa vizuri kuacha viharibike , Nenda kalete kila alichonunua hapa”Aliongea Hamza na kumfanya meneja kushangaa.

“Lakini vitu ni vingi sana”Aliongea kwa kusita.

“Wewe leta nyama iwe mbichi au imeiva , leta Cavier , Uyoga, matunda matunda , leta vyote hivyo vinavyobebeka kwa urahisi”Aliongea Hamza.

Ijapokuwa wahudumu wengine walikimbia , lakini wale wachache waliobaki , mara baada ya kusikia maagizo ya Hamza hawakupinga kwani haraka haraka walienda kuleta kama walivyoagizwa. Wakiogopa Hamza anaweza kuwakasirikia na kuwalipua pia.

Haikuchukua muda vitu vyote vya kuandaalia chakula vililetwa . Kulikuwa na kila aina ya nyama , Uyoga aina ya Truffles na Cavier za kutosha.

Wakati kila mmoja akishagnaa Hamza anataka kufanya nini na vitu hivyo, palepale aliokotoka pande la nyama mbichi na kulisindilia katika mdomo wa Mahmood .

“Kwasababu unapenda kununua kila kitu , sasa utakula kila kitu”Aliogea Hamza .

Mahmood mdomo wake ulikuwa umetapakaa damu na mara baada ya kuona pande la nyama mbichi kichefu chefu kilianza kumshika

“Lakini haijaiva”

“Lakini si ulinunua ikiwa mbichi?”Aliuliza Hamza huku kwa kumuogopesha zaidi alipiga ngumi ukutani na kufanya jengo lote kutetema kwa uzito na jambo hilo liliogopesha kila mmoja . Ijapokuwa Regina alijua na kuzoea nguvu za ajabu za Hamza lakini kwa watu kama Josh ilikuwa ni kama wanashuhudia mzimu.

Upande wa Meneja muda huo ni kama sasa akili yake inafunguka na kujua kwanini bosi wake Paco alimfokea kwa kutotii maagizo ya Hamza , ilionekana alikuwa akiogopa kipondo.

Endelea hapa :- SEHEMU YA 178
 
Good,,, umebarikiwa duniani hata mbinguni.
 
Viva Hamza🔥🔥 shukrani Sana Mr Hades/Pluto/Roma/Baba Lanlan/ mume wa warembo wengi! Ubarikiwe sana
 
Upande wa Meneja muda huo ni kama sasa akili yake inafunguka na kujua kwanini bosi wake Paco alimfokea kwa kutotii maagizo ya Hamza , ilionekana alikuwa akiogopa kipondo.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nimecheka sana hiki kipande cha mwisho cha meneja asante sana singano
 
Endelea kuinjoi Shunie , huko mbele kwa moto
 
Back
Top Bottom