Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Ila wabongo😅😅
Mmepewa link kbs ya kujimiminia venye mnataka lakn bado mnaweka MB za 2000 kuja kusoma kipande kimoja wakt ukilipia tokeni hyo 2000 unasoma mpk ujichokee 🙌🙌
Problem sio token na kujichokea kusoma.aweke no hapa pm ayapata token zake na atume link huko huko pm.process ya kule ni mambo privacy.
Na wengine hatuwezi kujiunga privacy zetu kwaajili ya hadithi tu.
Aseme hapa atapewa kilaini tu.
 
Naunga mkono hoja
 
Well said
 
Mkuu nani anajua Babu Kijana unatumia namba 06871513... au Hii ID yako ndio jina lako la NIDA? Kule huulizwi Id yako labda uamue kujitambulisha which is unnecessary.Wewe endelea kusubiri mwendelezo hapa utawekwa kwa udhamini wa wale wanaoniunga mkono.
 
SEHEMU YA 180.

Princess Airami Ingrid.

Hamza alikuwa amejichokea. Alikuwa amebembeleza watu wengi, lakini kwa Regina, ambaye ni mwepesi kukasirika, alishindwa kabisa kujua cha kufanya. Muda ambao aligeuka akitaka kuingia ndani kwa ajili ya kupumzika, palepale alisikia mlipuko mkubwa wa bomu na kumfanya ageuke haraka.

Mara baada ya kuangalia upande wa mbali kutoka hoteli hiyo, aliweza kuona moto ukiruka juu pamoja na moshi wake, na palepale alijua kabisa ni bomu. Hisia zake zilimwambia dhahiri kuwa lazima ni shambulizi la kigaidi. Hamza alikumbuka miaka miwili iliyopita wakati wakimbizi wengi walipoingia Ulaya, walivyosababisha matukio ya kigaidi. Alishawahi kushuhudia matukio kadhaa ya kigaidi kupitia taarifa za habari, lakini sasa alikuwa anaona ana kwa ana.

Hamza alijikuta akivuta pumzi ya baridi, akishikwa na wasiwasi kuhusu tukio hilo. Isitoshe, Regina alipaswa kukaa hapo Paris kwa siku kadhaa na alitarajia kushiriki katika mikusanyiko ya watu, jambo ambalo lilimfanya Hamza kuwa na wasiwasi zaidi. Palepale, Hamza aliamua kwenda kuangalia kilichokuwa kinaendelea, lakini kabla ya kuelekea huko, alikusudia kumuaga Regina.

Regina alikuwa anatoka bafuni na hakuweza kusikia kelele za mlipuko wa bomu nje. Aliposikia mlango ukigongwa, alijua Hamza amekuja kumbembeleza tena ili amsamehe.

"Nani?"

"Wife, ni mimi," aliongea Hamza kwa sauti. Regina, baada ya kusikia ni Hamza, furaha ilimshika. Alikuwa amevalia taulo pekee ambalo lilikuwa limemwacha sehemu za mwili wake wazi. Alisita kidogo akifikiria kuwa akifungua mlango akiwa katika hali hiyo, angeonekana kumtamanisha Hamza. Lakini baada ya kuwaza kidogo, aliona sio mbaya kama Hamza atafurahia uzuri wake.

Aliweka uso wa ukali na kusogelea mlango, kisha akaufungua.

"Nini tena?" aliuliza.

"Wife, endelea kupumzika. Hakikisha hutoki nje. Mimi naenda kuangalia kinachoendelea; kama kuna chochote, utanipigia simu," alisema Hamza, akimfanya Regina kushangaa.

"Wewe... Unaenda kuangalia nini?" Regina alijiuliza, akiwa hajui kama Hamza alikuja kwa ajili ya kumbembeleza au anaenda wapi usiku wote huu.

"Naenda kuangalia kilichosababisha mlipuko," aliongea Hamza.

"Mlipuko! Mlipuko gani huo?" aliuliza Regina, akionekana kuchanganyikiwa zaidi.

"Nazungumzia mlipuko uliotokea muda huu. Wife, usiwe na wasiwasi, hakuna kibaya kitakachotokea," Hamza alisema na akaondoka.

Regina, akiwa bado amevalia taulo, alibaki amesimama akiwa amebung’aa. Mara baada ya kuona Hamza ametoweka, alifunga mlango kwa hasira, akihisi maumivu na hasira kwa wakati mmoja, machozi yakianza kutiririka kwenye mboni za macho yake.

"Stupid zako, Hamza, ukafie huko huko usirudi."

*****

Hamza hakujua Regina alimhitaji sana usiku huo, na kitendo chake cha kuondoka bila ya kujielezea akaeleweka kilimkasirisha mno. Pengine mlipuko huo haukuwa ukimuhusu, lakini mazoea ya kutaka kujua kila hatari inayotokea machoni pake ndiyo ilimfanya kuwa na haraka na kutomzingatia Regina.

Licha ya kuwa usiku sana ndani ya jiji hilo la Parisi, kulikuwa na magari na watu kila mahali. Hususani kutokana na mlipuko huo, kundi kubwa la magari ya polisi yalikuwa yakielekea eneo la tukio na kufanya barabara kujaa ving’ora. Wafanyabiashara, raia na watalii walikuwa katika harakati za kuokoa uhai wao kwa kukimbia.

Hamza, ili kuepuka usumbufu na vikwazo, aliamua kuruka juu ya kuta na paa za baadhi ya nyumba kwa spidi kubwa sana. Alikuwa akikimbia kwa spidi kiasi kwamba ilikuwa ngumu kumuona.

Muda ule Hamza akiwa anakaribia kufikia eneo mlipuko ulipotokea, aliweza kuona tukio kushoto kwake ambalo lilimfanya asipuuzie.

Yalikuwa ni magari mawili meusi aina ya BMW 7s yakifukuzia gari aina ya Bentley katika barabara. Magari hayo matatu yalikuwa katika mwendo mkali mno, na wavuka barabara pamoja na baadhi ya madereva waliwapisha bila kupenda.

Suala la hatari ni kwamba katika BMW alionekana mwanaume aliyekuwa amevalia mavazi meusi akiwa ameshikilia bastola mkononi huku akilenga gari ile aina ya Bentley. Ndani ya Bentley kulikuwa na mwanaume mweupe mwenye kipara aliyeshikilia bunduki, na mara kwa mara alijitokeza dirishani na kushambulia zile BMW.

Uzoefu wa Hamza ulimwambia moja kwa moja watu waliokuwa katika gari za BMW walikuwa ni walinzi kama sio wanausalama, na mtu ambaye walikuwa wakimlinda alikuwa ndani ya ile Bentley, akiwa ametekwa.

Ile Bentley ilitengenezwa kwa muundo wa kutopitisha risasi, hivyo licha ya kujaribu kuishambulia haikupata athari zozote, na mbaya zaidi ni kwamba spidi ya ile Bentley ilikuwa ya juu mno kuliko zile BMW na kufanya kuwachwa umbali mrefu.

Yule mwanaume katika ile Bentley aliyeshikilia mtutu alikuwa na shabaha kali mno kwani risasi yake moja tu ilifanya gari moja ya wale walinzi ifuke moshi na kuserereka pembeni.

Muda ule Hamza akijiuliza atoe msaada au apotezee, yule mtu katika ile gari ya Bentley alikunja shati la mkono wake na palepale alionekana kuwa na tatoo ambalo chata lake Hamza alilitambua palepale.

"Sinagogu!!?" Hamza palepale aliweza kuona nembo ya Sanctuary of the Shadow, ambao waumini wake wengi walikuwa wakifahamika kwa imani za kiibada mbalimbali kama vile imani ya Ukweli uliovalishwa Sheria.

Hamza ilimshitua kwa sababu Sinagogu ndiyo walikuwa na makanisa maarufu Tanzania yaliyoenda kwa jina la Kanisa la Wabrazili.

Sasa Hamza kabla ya kufika Paris, rafiki yake Himidu alimuomba kufanya uchunguzi wa kugundua mashushushu waliopandikizwa ndani ya kitengo cha Malibu ambao walikuwa na muunganiko na Kanisa la Wabrazili kwa kushirikiana na watu wa Binamu.

Sasa Hamza mara baada ya kuona watu wa Sinagogu walikuwa mbele yake, ilikuwa kawaida kwake kutaka kwenda kuchunguza zaidi kile kinachoendelea. Lakini Hamza hakutaka kuwashitua watu wale kujua alikuwa akiwafuatilia. Aliona kama kweli atawaua watu wa Sinagogu, moja kwa moja atafukia nyayo zao na kushindwa kupata kile anachotaka.Hivyo, palepale aliona ni bora kuacha wafanikishe tu jaribio lao la utekaji.

"Tutututut! Plop, plop, plop!"

Ilikuwa ni mtutu wa bunduki kutoka kwa watekaji wale wakilenga gari ya BMW na haikuweza kuhimili zaidi kwani palepale iliserereka na kwenda kuvamia gari ya pembeni yake.

Mabodigadi wale walionekana kujeruhiwa na kutokana na hali za magari yao hawakuwa na uwezo tena wa kuendelea kufukuzia ile gari . Waliishia kujitoa kwenye gari zile wakiwa wanavunja damu nyingi.

Ijapokuwa Bentley ile ilipata michubuko ya risasi lakini haikuwa imeharibika kabisa na iliendelea kusonga kwa kasi ya hali ya juu kabisa.

Muda mchache mbele kundi la polisi walijitokeza kwa mbele wakizingira gari ile na kuifanya isiwe na nafasi ya kupita . Lakini kitu ambacho hawakuweza kukifahamu ni kwamba gari ile haikuwa na mtu ndani bali ilikuwa ikijiendesha yenyewe kwani wale watekaji walitoka muda mrefu wakiwa na mateka wao na kutokomea upande wa pili.

Yote hayo Hamza alikuwa akiyaangalia kwa mbali na baada ya mteka yule kushushwa na gari ile kuendelea na safari , hakuweza kumuona sura alietekwa ni nani kutokana na kuvalishwa mfuko mweusi kichwani.Metaka alionekana akiwa hajitambui na kupitia mavazi yake tu Hamza alitambua alikuwa ni mwanamke.

Wale mabodigadi wote walikuwa ni Wazungu , warefu kwenda hewani na waliojazia miili , walikuwa wamevalia miwani maalumu za kuwafanya kuona hata katika giza. Siraha zao walizokuwa wamefunga kiunoni zilikuwa za teknolojia ya juu.

Baada ya kutembea kwa mita kadhaa kutoka barabarani moja ya Gaidi alifungua ufuniko wa chemba na kuingia ndani na palepale gaidi mwingine alimtumbukiza yule mateka na kisha na yeye akaingia na kushikiza ule mlango wa chemba na kutokomea.

Yote hayo yalitokea ndani ya sekunde kumi tu na wakati polisi wakitoa maagizo ya dereva kushuka katika gari ile iliokuwa ikijiendesha kwa teknolojia ya akili mnemba upande wa watekaji na mateka walikuwa wamekwisha kupotea.

Hamza aliishia kuhema kwa mshangao na kujiambia hawa magaidi walikuwa vizuri mno na tukio hilo la utekaji lilionekana kupangwa vyema mno. Hususani pale magaidi walivyotoka nje ya gari na kuacha ijiendeshe yenyewe . Hamza hakuwahi kusikia uwepo wa gari aina ya Bentley ambayo ilikuwa na mfumo wa Selfdriving. Moja kwa moja aliamini pengine gari hio ilitengenezwa kwa kazi hio tu.

Hamza mara baada ya kuona watu wale wametokomea kwenye mtaro , na yeye hakutaka kuchelewa na palepale alifungua na kuzama ndani , lakini akitumia hatua nyepesi mno ili asije kushitukiwa.

Licha ya kuachwa umbali mrefu , Hamza alikuwa na uwezo wa kusikia sauti za hatua zao , Mtaro ulikuwa na harufu kali lakini hakujali.

Wale watekaji walibeba mateka yule na kutembea nae mpaka umbali mrefu kidogo na palepale walisimama na mmoja wa watekaji alitumia bunduki kugonga mfuniko wa chemba na haikuchukua sekunde chache mfuniko ule ulifunguliwa kwa juu.

Eneo hilo lilikuwa ni nyuma ya mgahawa na ilionekana ni sehemu iliogeuzwa jalala.

Mtu aliefungua ufuniko wa chemba alikuwa ni mwanaume mtu mzima mwenye masharubu na mvi nyingi na alikuwa amevalia sare za upishi.

“On a réussi ?” Aliuliza kwa kifaransa akimaanisha je wamefanikiwa.

“On va pas rater notre mission” Aliongea akimaanisha hawawezi kushindwa na misheni.

“Vizuri sana , usafiri upo tayari . Muingizeni mateka katika gari yetu ya mgahawa na ondokeni mkifuatisha ramani , Polisi hawatowasimamisha”Aliongea yule mpishi.

Wale majambazi wala hawakutoa jibu zaidi ya vitendo. Walimchukua yule mateka na kumuingiza nyuma ya gari na mmoja aliingia upande wa dereva na kuliondosha gari hilo katika huo mgahawa.

Baada ya kuondoka tu , yule mpishi alitoa simu yake na kufanya mawasiliano.

“Mr Blue , Mbweha na Fisi wameondoka hapa na mateka . Kila kitu kimeenda sawa , hakuna nyayo zilizoachwa nyuma… Sawa , nitaendelea kubakia hapa mgahawani na kukujuza kila baada ya muda”Aliongea yule mpishi.

Muda ule yule mpishi mara baada ya kuweka simu chini , ile anageuka akitaka kuziba chemba ile , alijikuta akishikwa na mshituko baada ya kuona mtu pembeni ya chemba akiwa na tabasamu pana usoni.

Mtu huyo alikuwa ni Hamza , ambae alikuwa akifuatisha majambazi wale katika mtaro huo wa maji machafu.

“Wewe ni nani?”Yule mpishi mwenye masharubu aliuliza kwa mshangao kwa lugha ya kifaransa.

“Mr Blueni nani kwa jamii ya WaSinagogu?”Aliuliza Hamza kwa kifaransa.

Yule bwana palepale muonekano wake ulibadilika mara moja na hali ya kimauaji ilimvaa. Lakini haraka sana aliificha nia yake na kutoa tabasamu bandia.

“Sir sijui unachokimaanisha . Mgahawa wetu tumeshafunga”

“Hilo gari la mgahawa Plate number zake ni 342 FN . Kama nikiwapigia simu polisi sasa hivi watafurahi kwa usamaria wema wangu. Au nasema uongo?”

Mara baada ya kusikia hivyo mpishi yule alijikuta wasiwasi ukimwingia na palepale alipiga magoti chini na kuanza kuomba.

“Sir nakuomba tafadhari .. walinilazimisha tu , mimi siwajui kweli”

Wakati huo akimshika Hamza mguu kabisa na kutoa kilio,, lakini dakika hio hio hali ya kimauaji ilimvaa mpishi huyo . Alionekana alikuwa akifanya maigizo na ile kuona amemfikia vizuri Hamza alichomoa kisu haraka kutoka kiunoni na kumlenga Hamza kwenye enka ya mguu wake.

Hamza alikuwa alishajua maigizo yake na kabla hata kisu kile hakijamfikia alishampiga teke la kichwani na kutokana na uzito wa teke lile shingo yake ilijikunja na alipoteza uhai palepale.

Hamza hakutarajia majibu hata hivyo kutoka kwa mtu huyo , hivyo kifo chake hakikumfanya kujutia . Hakutaka kujua Blue ni nani maana alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja jina hilo ni la msimbo.

Kilichomfanya Hamza kuwa na wasiwasi zaidi ni kwamba Sinagogu walionekana walikuwa na mtandao wa kitelijensia ndani ya Parisi hivyo ikimaanisha moja kwa moja walikuwa pia na kambi hapo. Hamza kuona hivyo alijiuliza inamaana watu hawa walikuwa kila taifa?.

Moja kwa moja hisia zake zilimwambia yoyote ambae anamiliki mtandao huo hawezi kuwa mtu wa kawaida , maana sio kitu ambacho kinaweza kukamilishwa na tajiri au mtu mwenye madaraka ya kawaida.

Hamza hakuendelea kupoteza muda na palepale kwa spidi kubwa alianza kuruka kupitia kwenye majengo yenye kimo kifupi na ndani ya dakika chache tu aliweza kuiona ile gari na kuendelea kuifuatilia.

Baada ya lisaa limoja gari ile ilikuja kusimama mbele ya kanisa pembezoni kabisa mwa jiji hilo la Paris.

Kanisa hili lilipatikana katika makazi ya watu , na nyakati hizo za usiku kulikuwa na ukimya mno.

Ndani yake mwanga ulikuwa hafifu mno na alionekana Padri ama mchungaji aliekuwa amesimama gizani akiwa amevalia miwani.

Hamza alienda kutua juu ya paa la kanisa hilo akiangalia kwa umakini wale majambazi wakimtoa yule mateka kwenye gari.

“Kwanini mmechelewa kwa dakika tano?”Aliuliza yule paroko kwa sauti nzito.

“Samahani sana Mr Blue , tuliendesha kwa kuzunguka ili kukwepa polisi”Aliongea jambazi mmoja.

“Acha kutafuta visingizio na hakikisha unafuata maelekezo wakati wa misheni. Ukifanya kila kitu kwa wakati polisi hawawezi kuonekana mbele yako”Aliongea Blue na kuwafanya wale majambazi wawili kutingisha vichwa wakionyesha kuelewa.

“Mleteni ndani”Aliongea Blue na wale majambazi waliitikia na kisha palepale walimbeba yule mateka na kumuingiza ndani ya kanisa.

Blue alingalia kulia na kushoto kuhakikisha hakuna aliekuwa anaewafuatilia na kisha aliingia ndani na kufunga mlango.

Hamza aliekuwa juu ya paa alikuwa akijiwazia na palepale alionekana sasa kugundua mtu aliefahamika kwa jina la Mr Blue alikuwa ni huyo paroko.Lakini mpaka hapo hakuamini pia bwana huyo ni Paroko.

Hamza alijiambia bado muda anao, haina haja ya kumshitua nyoka, hivyo alitafuta angle nzuri ya kusimama na kuangalia kupitia skylight(bati la kio) kama watu hao walikuwa wakifanya nini ndani ya kanisa.

Muda ule ndio aligundua nyuma ya madhabahu karibu na sanamu la Yesu kulikuwa na mlango wa siri.

Paroko Blue alionekana akiwaongoza wale majambazi kuingia kupitia mlango huo wa siri ambao uliwaongoza moja kwa moja kuingia katika vyumba vya chini ya ardhi.

Hamza aliishia kutoa tabasamu na kujiambia kuchagua kuwafuata ilikuwa busara kubwa kwa upande wake , kwani aliamini kanisa hilo linaonekana kubeba siri nyingi , aliamini lazima itakuwa ndio kambi ya wafuasi hao wa Sinagogu.

Hamza alisubiri mpaka alipohakikisha hakuna mtu aliebakia chini na kisha palepale alifungua kipande cha skylight na kwa wepesi kabisa aliruka mpaka chini.

Kupitia mbinu alizotumia Paroko Blue na yeye pia alitumia hizo hizo na kufungua mlango ule wa siri na kuingia ndani kwa kunyata akihakikisha hakuna anemshtukia.

Ile anakaribia kufika chini kabisa aliona eneo lote likipanuka kwa upana wake , huku likiwa limejengwa kwa kuta za mawe . Ilikuwa ni kama handaki la vita lakini ambalo limefanyiwa maboresho makubwa. Eneo hilo halikutisha hata kidogo na badale yake lilikuwa kavu , lenye joto na hali ya hewa nzuri.

Kuilichomshangaza Hamza zaidi ni kwamba kulikuwa na watu ndani ya eneo hilo na kwa mahesabu ya haraka haraka walifika hamsini kwenda sitini hivi , wote walikuwa wamevalia kofia mfano wa kepu za rangi nyekundu na makoti, wakiwa wamesimama huku wameshikilia mishumaa iliokuwa ikiungua moto.

Paroko Blue alikuwa amekwisha kuvua yale mavazi yake ya mwanzo na sasa alikuwa amevalia joho la rangi nyekundu lenye udarizi wa kamba za rangi ya dhahabu . Alionekana ndio kiongozi wa waumini hao kwani alikuwa akiongea maneno na wao walikuwa wakifuatisha.

“Ee Mfalme mkuu wa Sinagogu! Heshima na u tukufu twazielekeza kwako na kivuli chako na kithibitike kwetu!

Shukrani hutupa damu tamu kutuondolea dhambi zetu , Tuoshe katika uchafu, Kwa ajili yako Devasi , kwa ajili yako Jehanamu , Kwa ajili ya Utukufu wako . Tutakufuata milele. Ee Mfalme zipokee nafsi zetu …”

Mara baada ya kumaliza kutamka maneno yake , Blue aliinua bakuli la damu juu na waumini wote waliinua pia mabakuli yao.

“Tunakunywa damu hii kwa ajili yako mfalme”

“Kwa ajili yako mfalme Devasi”

Ndani ya eneo hilo la ardhini , mara baada ya wafuasi hao kupiga makelele kila mmoja alikunywa damu yake iliokuwa kwenye bakuri. Midomo yao yote ilikuwa imejaa damu lakini macho yao yalionekana kujawa na msisimko na fanaka kubwa.

Hamza aliekuwa akishuhudia hayo yote aliishia kukunja sura , mambo waliokuwa wakifanya watu hao ilikuwa ni nje ya matarajio yake.Aliona kabisa hilo halikuwa kundi la magaidi bali ni kanisa la kishetani.

Huyo mfalme wa masinagogu alikuwa na waumini wengi waliojaa imani kali zidi yake. Matokeo ya kugeuza akili na kuwafanya watu kufuatisha hivyo bila kulazimishwa halikuwa swala la kufanikisha ndani ya usiku mmoja . Alikuwa na uhakika kiilichokuwa kikiendelea hapo kilianza kwa miongo kadhaa.

Kilichomfanya Hamza kuwa na wasiwasi zaidi ni kwamba , ijapokuwa alikuwa mbali amejificha kwenye ukuta lakini alivyoangalia hali ya hapo ndani kupitia angle ndogo sana kuepusha kuonekana , karibia ya wafuasi hao wote sitini walikuwa wakitoa msisimko wa ajabu mno . Walionekana kuwa na nguvu za kiroho ambazo pia sio za kawaida.

Hamza aliona hata kama akianza kupigana nao , itabidi atumie nguvu nyingi sana na jitihada mpaka kufanikiwa kuwaua wote.

Muda ule aliacha kufikiria mara baada ya kusikia Blue akianza kuongea tena kwa shangwe.

“Leo ni siku muhimu ya kutambelewa na mfalme wa Sinagogu. Hatimae tumepiga hatua muhimu! Na kwa ajili ya kumpokea mfalme wetu tumefanikisha kumleta mrithi wa tatu wa familia ya kifalme . Moja ya mwanamke mrembo kuwahi kutokea duniani , Binti wa Kifamle,Princess Aira Ingrid, The Desires !”

Wafuasi hao mara baada ya kusikia kauli hio walijikuta wakianza kutoa vilio vya shangwe.

Hamza alijikuta akishangaa mno . Hakufikiri kundi hilo la washenzi mtu waliemteka ni Princes Airami Ingrid, Mtamaniwa

Ijapokuwa Hamza hakuwahi kumuona Princes Aira lakini alishawahi kusikia jina lake na hio yote ni kutokana na kuwepo kwa taarifa mbalimbali ambazo zilikuwa zikizungumzia uzuri wake kutoka kwa watu wa ulimwengu wa siri. Lakini licha ya sifa hizo hakuna mtu ambae alishawahi kuona sura yake na hata yeye Hamza hakuwahi kumuona kabisa , aliwahi tu kusikia uwepo wa Princess huyo.

“Usiku wa leo, mbele ya ulimwengu wote tutatumia damu ya kifalme kama kafara kwa Mfalme Mkuu Devasi”Aliongea Blue kwa sauti.

Hamza mara baada ya kusikia mbele ya ulimwengu , palepale alichunguza kwa umakini na kweli aliweza kuona kamera.

Alijiuliza inamana hao wendawazimu walipanga kumkausha damu Aira huku wakirekodi na kisha kutuma kwenye internet?.

Kama hilo lingefanyika kweli , basi ni dhahiri watu hao wa Sinagogu wangeenda kuwa maarufu mno.

Lakini hilo la umaarufu ni swala lingine , kitendo cha mwanafamilia huyo wa kifalme kutekwa ndani ya nchi ya Mafuvu ingeleta mgogoro mkubwa sana na raia wasingekubali na mfalme lazima angehitaji maelezo ya kina juu ya binti yake.

Mpaka hatua hio Hamza aliona kabisa jamii hio ya Sinagogu hawakuwa na hofu kabisa mpaka kufikia hatua hio na hakujua ni kipi kinachowafanya kujiamini kwa namna hio.

Hamza licha ya kwamba alishaachana kufuatilia mambo ya watu na kustaafu lakini asingeweza kuona jambo hilo la binti wa mfalme kuchinjwa linafanyika huku yeye akiangalia tu.

Hivyo palepale aliacha kujificha na kujitokeza . Waumini baadhi waliokuwa wamevalia kepu zao nyekundu mara baada ya kumuona Hamza walionekana kushangaaa mno na kushituka kwa wakati mmoja.

“Wewe ni nani na unafanya nini hapa??”

Hamza hakujali maswali yao na badala yake aliangalia katika madhahabu juu ya meza kubwa ya mawe alikuwa amelazwa mwanamke ambae alionekana kuwa katika hali ya kutokujitambua mbele ya Paroko Blue. Mwanamke huyo alikuwa ndio Princess Airami.

Hamza kuangalia kwa mbali tu , aliweza kujua kwanini watu hao walikuwa katika hamasa kubwa . Alijua sasa kwanini vyombo vya habari vilikuwa vikivumisha kwamba mwanamke huyo ndio mrembo kuwahi kutokea katika dunia nzima.

Alikuwa ni mwanamke mwenye nywele ndefu na nyingi za rangi ya kaharabu , rangi flani kama dhahabu iliokolea yenye chembe chembe za rangi nyekundu. Ni aina ya nywele za kizungu ambazo ni wazungu wachache sana wamebarikiwa nazo. Umbo la uso wake lilikuwa ni kama vile ni mchoro ambao ulihitaji lugha iliokomaa kuuelezea.

Koti alilokuwa amevaaa lilivuliwa na kubakishwa na shati la mtelezo la maua maua na sketi ya bluu na umbo lake la umisi kuonekana vizuri , ilimfanya hata Hamza ambae alikuwa mbali kuwa na uhakika na hisia zake mwanamke huyo alikuwa mrembo sana.

Hamza alikuwa ameona wanawake warembo wa aina tofauti tofauti lakini mwanamke kwa mwanamke huyo alikuwa na uhakika uzuri wake ulikuwa ni zaidi ya watu wawili aliokuwa akiwafahamu.

Upande wa mwanamke wa kizungu ambae alikuwa na mwonekano usiokuwa wa kawaida alikuwa ni Sally. Lakini kumfananisha na Aira ilikuwa ni kumkosea heshima princess huyo.

Hamza alijiambia alikuwa amefanya maamuzi sahihi kufuatilia watu hao , la sivyo mbingu si zingekuwa zinachekelea kuipokea nafsi ya mwanamke mrembo.

“Nyie watu mmetoa wapi ujasiri wote wa kufanya hivi?”Aliongea Hamza huku akitembea kupanda eneo la madhabahuni.

Aira alionekana bado alikuwa katika hali ya kutokuwa na fahamu kutokana na dawa alizowekewa.

“Mkamateni !!!”Aliongea Paroko Blue akiwapa ishara watu wake kufanya kazi ya kumshumbulia Hamza.
 
SEHEMU YA 181
Palepale wanaume waliojazia miili ambao pia walikuwa ni wafuasi wa sinagogu walitokeza mbele , wakiwa na visu mikononi mwao na haraka sana walianza kumshambulia Hamza..

Hamza aliishia kushika vile visu upande unaokata na kuvuta kwa nguvu lakini hakuonekana kuumia kabisa.

Kwa wakati mmoja alimpiga teke mwanaume yule na kisha alitumia kisu kile na kumkata mwingine shingo.

Ijapokuwa mbinu za mapigano za wafuasi hao zilikuwa sio za kawaida , lakini spidi yao ilikuwa ndogo mno kulinganisha na ya Hamza.

Hamza kila alipokwepa shambulizi aliweza kumuua mshambuliaji kwa urahisi kabisa na ndani ya sekunde chache tu watu kadhaa walikuwa wamedondoka chini wakiwa hawana uhai.

Mara baada ya kuona uwezo usiokuwa wa kawaida wa Hamza kupigana, Blue palepale alikamata bunduki aina ya AK-47 kutoka chini ya meza ya jiwe na kuanza kumlenga Hamza.

Hamza hakutaka risasi kumfikia , ingawa asingeweza kufa lakini zilikuwa zikiuma.

Alichokifanya alikimbia upande wa waumini wale na kufanya risasi zile ziue baadhi yao.

Kundi hilo la waumini walionekana hawakukiogopa kifo na walianza kumzingira Hamza wakitaka kumpiga.

Hamza aliishia kufyatua mateke akiwashambulia na kutengeneza njia ili kumfikia Blue, na alifanikiwa kutoka na kumpokonya paroko ile bunduki.

Hamza aliona ingekuwa kazi kuwaua kwa kutumia mikono yake na ili kuharakisha kazi aliona atumie bunduki hio.

“F*ck you zenu nyie wendawazimu msio na akili , kufaaaa!”aliongea Hamza na palepale alianza kuwafyatulia risasi na kufumba na kufumbua watu wengi ndani ya eneo hilo walidondoka chini.

Lakini baadhi ya waumini wakiungana na wale ambao walimteka Aira walionekana kuwa na bunduki zao pia na walianza kumshambulia Hamza.

Hamza alikuwa na wasiwasi risasi za bunduki zao zingemdhuru Aira hivyo alisogelea juu ya ile meza ya jiwe aliolazwa na kumsukumia upande mwingine chini na kisha alikimbia upande uliokuwa na wafuasi wengi na kuendeleza mashambulizi.

Waumini hao walikuwa ni kama vichaa , tofauti na kukimbia wote walikuwa wakimsogelea Hamza kama misukule na kumfanya Hamza kukosa jinsi na kuendelea kuwapasua vichwa na risasi.

Ndani ya dakika mbili eneo lote lilikuwa limejaa maiti na damu . Hamza aliishia kutoa pumzi ya masikitiko , ilipita muda mrefu kidogo mpaka kuuwa watu wengi kwa wakati mmoja kama siku hio , lakini hata hivyo alikuwa hana jinsi.

Watu hao hawakuwa katika akili zao , walikuwa wamegeuzwa kifikra na alijua kama wangetoka uraiani wangesababishia wenzao madhara.

Hamza mara baada ya kumalizana na wale wenye bunduki palepale alimsogelea Blue ambae uso wake bado ulionekana kuvimba . hakuwa na woga bali macho yake yalikuwa yamejaa chuki mno. Lakini Hamza hakumjali na palepale alimshika shingo kwa kumkwida.

“Jibu kila nitakachokuuliza la sivyo nitakugeuza maiti”Aliongea Hamza akiamini bwana huyo lazima atakuwa anajua baadhi ya siri za jamii hio ya wasinagogu.

Lakini mtu yule alionekana kabisa kutojali na palepale alitoa tabasamu la uvovu.

“Huwezi kupata chochote kutoka kwangu. Uishi milele mfalme wa masinagogu! Uishi milele Devasi…”

Hamza alishangazwa kwa sekunde na palepale ndio alipoweza kumuona Blue akitema damu huku mboni za macho yake zikizunguka na ndani ya sekunde kadhaa alipoteza pumzi.

Hamza aliishia kutupa chini mwili ule . Hakuamini bwana huyo atakunywa sumu kwa ajili ya kulinda umoja huo. Aliona watu wa Sinagogu kweli walikuwa ni hatari na kama mafunzo yao ni hayo aliamini hata kule Tanzania kuhusu makanisa ya kibrazili basi ni hatari pia kuendelea kuwepo.

Muda huo Hamza alivyogeuka aliweza kuona macho ya rangi ya bluu yalikuwa yakimwangalia kwa wasiwasi. Alikuwa ni Princess Airami ambae kwa macho yake tu alionekana kuwa katika hofu na kutia huruma.

“Princess Aira , haina haja ya kuwa na hofu . Kila kitu kipo sawa sasa”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.

Aira alionekana kuona ukarimu wa Hamza na palepale taratibu taratibu alisimama . Alionekana alishituka mara baada ya Hamza kumsukumia chini na makelele ya mirindimo ya bunduki ilikuwa ni ngumu kutokurejewa na fahamu..

“Wewe ni nani?”Aliuliza Aira kwa lugha ya kifaransa , huku macho yake yakionyesha kuwa na aibu kubwa . Wakati huo alipokuwa akiongea alikuwa ameegamia upande na hakuthubutu kumwangalia Hamza usoni.

Tofauti na wanafamilia wengi wa kifalme , ambao waliona kawaida sana kuonekana hadharani , lakini kwa Aira ilikuwa tofauti, alisifika kwa kuwa na aibu mno na ndio maana mara nyingi alipotokea katika kusanyiko alivaa Nikabu.

Aibu za Aira zilimfanya kumvutia Hamza . kwa uzuri wake usiokuwa wa kawaida na urefu wa mita moja nukta saba , ilikuwa ngumu sana kuona dosari katika uumbaji wake. Dosari pekee alioweza kuona ni kutokujiamini kwake.

“Jina langu naitwa Hamza , nilikuwa nikipita tu na kugundua umetekwa na ndio maana nikaja kukuokoa. Usikifirie sana kuhusu unachokiona”Aliongea Hamza.

“A.. amzha..”Alionekana kushindwa kutamka vizuri , hakuwahi kusikia jina hilo kabla na kama amelisikia pengine hakuwahi kulitamka.

“Amzah tupo wapi hapa?”Aliuliza kwa sauti ya unyonge.

Hamza mara baada ya kuulizwa swali hilo hata yeye mwenyewe alijishangaaa, wakati wa kuwafuatilia majambazi hakutilia umakini juu ya eneo walipo hivyo hakuwa na uelewa eneo hilo ni wapi.

“Princess , subiri tutoke nje , nikiona alama barabarani nitajua tupo wapi”Aliongea Hamza na kumfanya Aira kupepesa macho yake mazuri na baada ya sekunde kadhaa kupita alionekana kuanza kucheka.

“Princess ! mbona unacheka au nimekosea?”Aliuliza Hamza akiwa katika mshangao maana aliamini maneno yake hakuna alilosema likawa linachekesha.

“Hamna tu , samahani sio kama nakucheka bali ulivyojibu inachekesha , nilikuwa nauliza hapa ndani ni wapi? Kuna haja ya kuangalia alama za barabarani?”Aliuliza na Hamza palepale alijikuta akijidharau.

“Kumbe ulikuwa ukiuliza kuhusu hapa , Humu ndani ni chumba chini ya ardhi ndani ya kanisa , itakuwa ndio kambi ya hawa waumini.Tukiachana na hayo Princess , je unajua kuhusu wauamini wa Sinagogu? Nahisi sio kawaida kwa wao kukuteka , kuna sababu yoyote ambayo unaifahamu?”Aliuliza Hamza na Airami alitingisha kichwa kukataa.

“Nimefika hapa nchini kwa ajili ya kushiriki katika sherehe za kukata utepe , wakati nikitokea Airport kwenda hotelini nilihisi tu harufu nzuri ndani ya gari na nikapitiwa na usingizi”

Hamza alitingisha kichwa kuelewa , kwa maelezo hayo Hamza aliamini mlipuko ule wa bomu haukuwa ukihusiana na kutekwwa kwa Princess Aira bali ilikuwa ni kuwachanganya polisi kwakutengeneza machafuko.

“Princess nitakuondoa hapa kukurudisha , Umetekwa hivyo watu wengi watakuwa na wasiwasi juu yako”

Princess huyo mara baada ya kusikia hivyo alitngisha kichwa kukubali.

“Sawa , nadhani napaswa kukusumbua tena , Hamza”Aliongea akijitahidi kuita jina la Hamza kwa usahihi.

“Usijali kwangu ni swala dogo sana , kumuokoa mwanamke mrembo ni jukumu langu kama mwanaume , isitoshe pia wewe ni princess”

Aira mara baada ya kusikia hivyo alishikwa na aibu tena na aliishia kushika mikono yake huku akianza kumfuata Hamza kwa nyuma.

Wakati Hamza akiongoza kuitafuta njia ya kutokea , palepale alionekana kufikiria kitu na aligeuka na kumwangalia Aira.

“Princess , unaonekana kuwa jasiri mno , huogopi maiti zote hizo tulizopita?”Aliuliza na kumfanya Aira kushangaa kwa sekunde.

“Nilisahau”

“Umesahau?!”

“Ndio nimesahau kama kuna watu wamekufa pale”Aliongea akiwa ameinamisha kichwa chini akikwepesha macho yake na Hamza.

Hamza alijikuta akikosa usemi , aliona princess huyo ukilaza wake ulivutia mno , kilichomshangaza zaidi ni namna ambavyo alikuwa na aibu.

Hamza palepale alielewa kwanini mfalme Ingridi alikuwa akimficha binti yake katika macho ya watu. Kwa aibu hizo alimuonea huruma.

Mara baada ya kutoka nje ya kanisa hakukuwa na watu kuzunguka eneo hilo . Lakini kulikuwa na magari kadhaa yaliokuwa yameegeshwa kando ya barabara.

Hamza aliangalia mpangilio wa magari hayo na aliamini lazima magari hayo yatakuwa ni ya wale waumini, na kwa sababu alishawaua wote aliona magari hayo hayana mmiliki tena.

Hamza aliachana na magari ya kifahari na kutafuta gari ambalo lilionekana kuchakaaa na kisha palepale alivunja kioo na kufungua mlango kupitia ndani na mara baada ya kuingia ndani alianza kulazimisha gari hio kuwaka kwa kuchezesha nyaya.

Princess Aira ambae alikuwa akifuatisha nyuma nyuma alionekana kuwa na shauku kutokana na mambo aliokuwa akiyafanya Hamza.

“Hamza unataka turudi kwa gari?”Aliuliza.

“Ndio . Au unataka kupiga simu na kuwaambia upo salama?”Aliuliza Hamza.

“Hapana , kwasababu matatizo yamenitokea nikiwa katika gari ambayo imeandaliwa na walinzi nikifika Airport. Kuna uwezekano moja ya walinzi wangu ni msaliti. Nikipiga simu na kuwaambia nilipo ni sawa na kuwaambia waje kuniteka kwa mara ya pili, Au wewe unaonaje?”Aliuliza

Hamza mara baada ya kusikia hivyo alionekana kushangaa mno kuona alikuwa na uwezo wa kuchanganua mambo.

“Upo sahihi kabisa , unaonekana uko vuzuri kichwani Princess. Nilikudhania ni msichana mjinga”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kumfanya Aira kuangalia pembeni kutokana na aibu kumzidia.

“Hapana , nimejifikiria mimi mwenyewe , maana mpaka sasa sijui kwanini nimetekwa”

Hamza licha ya kumuita msichana mjinga , Aira alionekana kutojali kabisa.

Hamza kadri alivyokuwa akimwangalia Aira alivyo, alijiambia itakuwa furaha kubwa sana kwake akija kupata mtoto wa kike kama yeye hapo baadae.

“Princess , ingia sasa tuondoke”Aliongea Hamza akimfungulia mlango wa nyuma na Aira alitingisha kichwa na kuingia ndani.

“Hamza kwanini usingechagua Mercedenz benz au Audi naona yapo mengi , ila hii Renault imechoka mno”Aliuliza Aira.

“Kwasababu ni magari ya zamani pekee yanayowaka kwa kuchezesha nyaya , hayo unayosema bila funguo hayawezi waka”

“Oh! Wewe ni Agent au mwanajeshi? Una nguvu na uwezo zaidi ya walinzi wa baba yangu”

Muda huo Hamza alikuwa ashaondosha gari hilo mkabala na kanisa hilo na kuianza safari ya kurudi mjini Parisi.

“Mimi ni mtu wa kawaida tu ambae nikiona tukio la uovu linatendeka naonyesha uwezo wangu mdogo wa mapigano”Aliongea Hamza lakini maneno yake ambayo hayakuwa na maana ya moja kwa moja yalimfanya Aira kuonekana kuwa na shauku zaidi na kuanza kumuuliza Hamza maswali kama vile ni raia wa nchi gani , anafanya kazi gani na yupo Paris kwa ajili ya nini.

Ijapokuwa princess huyo alikuwa na aibu sana , lakini kitendo cha kukaa nyuma mbali na macho ya Hamza alionekana kuongea sana.

Hamza upande wake alijibu na kumwambia anatokea Tanzania nchi kutoka Afrika , kazi yake ni msaidizi wa bosi ndani ya kampuni na amekuja Parisi na bosi wake kwa ajili ya shughuli za kibiashara.

Hakuchoka kumjibu , alifurahishwa na namna anavyoongea na alikuwa akimtania hapa na pale , lakini Aira alionekana kukubali kila Hamza anachoongea akishindwa kujua Hamza alikuwa akitania tu na kumjibu uongo baadhi ya maswali. Lakini kutokana na kuongea kwao ilifanya safari yao kutochosha kabisa.

Kitu ambacho hawakufahamu ni kwamba ile wanaondoka tu katika kanisa lile , watu waliovalia mavazi ya suti walifika nje ya kanisa na kuingia ndani. Kiongozi wa watu hao alikuwa na chata la mfupa kwenye shingo yake na X na alionekana dhahiri alikuwa ni mwanachama wa umoja huo wa Sinagogu.

Ukweli ni kwamba ibada zote za Sinagogu duniani zilikuwa zikirekodiwa na kamera za siri na kusambazwa moja kwa moja makao makuu, hususani zile za kikafara , Hivyo uvamizi wa Hamza ulishuhudiwa lakini ilichukua muda kwa watu hao kufika katika kanisa hilo kuzuia kutokana na kuwa mbali.

“Pumbavu! Ni wapi huyu mtu katokea , amewezaje kumuokoa Princess Aira?”Aliongea kiongozi akionekana kukasirika mno “Tukiruhusu Princess kurudi Paris itakuwa ngumu kumteka tena”Aliendelea kuongea.

“Kiongozi nadhani nafasi bado tunayo , tunaweza kuwasiliana na wenzetu ili kuwazuia kwa mbele”Aliongea mwanaume aliekuwa pembeni.

“Lakini huyu mtu ni hatari mno . Wasiwasi wangu hata wakijaribu kumzuia wataishia kupoteza maisha tu”Aliongea mwingine.

“Tunamtaka Princess Aira kwa namna yoyote ile , haijalishi awe amekufa au yupo hai . Misheni yetu ni kuhakikisha tunamrekodi tukimdhalilisha na kisha kuposti mtandaoni … lengo kuu la hii misheni ni…”

“Bosi unajaribu kusema…”Wanaume wawili waliokuwa pembeni yake walianza kucheka kishetani . Walionekana kuelewa kiongozi wao anachomaanisha bila ya kuongea.

*****

Ndani ya gari la kizamani la kampuni ya Renault , Hamza alikuwa akiongea kwa furaha na Princess Airami.

“Hamza , Tanzania ni kuzuri eh? Nasikia kuna wanyama wengi wakubwa na wakali kama Simba na Tembo , nina miaka ishirini na mbili ila sijawahi kufika Bara la Afrika”Aliongea Aira kinyonge.

“Wewe ni Princess si una huru wa kwenda popote?”

“Hapana , nikisafiri kidogo tu baba anatuma watu wanirudishe nyumbani na kila ninapoenda nakosa uhuru kwasababu ya kuwa na walinzi wengi na itifaki nyingi za ki usalama”

“Kama ni hivyo , siku nyingine mwambiae baba yako nataka kwenda nchi inayoitwa Tanzania na utakuwa chini yangu”Aliongea Hamza kwa kujiamini.

“Kweli? Lakini baba ataweza kuamini kweli na kunikubalia?”

“Nitakuachia namba yangu ya simu ,Ukitaka kuja nitamwagiza mtu aongee na baba yako , nina uhakika atakuruhusu”Aliongea Hamza

“Unafahamiana na baba yangu?”Aliuliza Aira akioneakna kuwa katika mshangao na Hamza aliishia kutoa tabasamu tu.

“Ndio , wewe niamini mimi , nina uhakika baba yako ataelewa nikishaongea nae”Aliongea Hamza na kumfanya Aira kupepesa macho yake.

“Sawa mimi nakuamini Hamza kwasababu umeweza kuniokoa . Lakini nitajie namba yako”Aliongea na Hamza alimtajia namba yake na Aira alionekana kuirudia rudia kuhakikisha ilikuwa sahihi.

“Wakati wa kunipigia hakikisha unaweka code za Tanzania kwanza , ukipiga hivyo hivyo haitofanya kazi Au tumia Watsapp”Aliongea Hamza.

“Oh sawa , sijawahi kumpigia mtu nje ya nchi bado na simu yangu haipo hapa nitakwenda kujaribisha..”

Wakati wakiendelea na safari . Hamza aligundua Aira alikuwa ameacha kuongea na alionekana kumwemwesa midomo kama vile kuna kitu anachoongea lakini hakikuweza kusikika.

“Princess , unaongea nini?”Hamza hakuelewa lakini swali lake lilimfanya Aira kuona aibu.

Narudia rudia kukariri namba yako ya simu , sina mahali pa kuiandika , nikijikumbusha mara nyingi sitoisahau”

Hamza mara baada ya kusikia hivyo hakujua acheke ama alie , hakujua kama angekuwa siriasi hivyo kwenye kukariri namba yake tu.

“Princess , huna haja ya kupata tabu namna hio , nitakuandikia kwenye karatasi tukishafika Paris au nitakutumia namba yangu kupitia Email”Aliongea Hamza na kumfanya Aira kufurahi.

“Lakini sina Email , tukifika Parisi niandikie”Aliongea.

Sauti hio ya kumtoa nyoka pangoni ilimpagashiwa mno Hamza , alitamani kuruka nyuma na kufanya jambo , ashawahi kuwa na wanawake warembo wa kizungu wengi hapo kabla lakini Aria aliwazidi kila kitu.

Wakati wanafika nusu safari kuingia Paris , hatimae waliweza kuona gari ya polisi mbele yao . Gari hio ilikuwa imesimama na polisi walikuwa wakimuwashia taa nyekundu kumwashiria asimame.

Hamza palepale alihisi kuna kitu hakipo sawa na kujiuliza au amegundulika ameiba gari maana eneo hilo kusimamishwa ni kama ilikuwa kinyume sana.

Kwa uzoefu wa Hamza Trafiki wa Ulaya hawakuwa na ufanisi mkubwa nje ya mji mpaka kuweka kambi , hivyo aliona ni ngumu kuamini wapo hapo kwa ajili ya doria.

Hata hivyo Hamza hakutaka kuwaza sana na palepale alisimamisha gari pembeni na kushusha kioo.

“Afisa kuna tatizo?”Aliuliza na mzungu huyo trafiki alimwangalia Hamza bila ya hisia zozote na kisha macho yake yakatua kwa Aira nyuma ya gari.

“Tafadhari onyesha leseni yako”Aliongea.

“Hii gari ni ya rafiki yangu na leseni haipo ndani ya gari”Aliongea Hamza huku akijiambia kama kweli polisi hao walikuwa wakitaka kuona leseni yake , anatakchofanya ni kumpigia tu mtu na kutatua tatizo

Yule trafiki wa kifaransa aliishia kutingisha kichwa na kisha alimwambia Hamza asubiri kidogo.

Muda ule polisi alienda mpaka kwenye gari yao na kuungana na mwenzake kisha alionekana kuchukua kitu.

Mara baada ya kugeuka Hamza alijua palepale hali haikuwa shwari, Kwani polisi wote walionekana kuvaa Mask usoni za kujikinga na hewa chafu.

Muda ule Hamza akipanga kuchukua hatua, polisi wale wawili walirusha mabomu mawili ya gesi.

“F*ck! “Hamza alijikuta akitoa tusi baada ya kugundua polisi hao mpango wao ulikuwa ni kuwaua kwa sumu na kisha ndio wachukue maiti zao.

Bomu lile la gesi lilitoa moshi mzito ambao ulizingira gari yao na muda uleule wale polisi walichomoa bastora zao na kuanza kushambulia kioo cha mbele cha gari ya Hamza.

Kutokana na ukale wa gari hio hazikuhitajika risasi nyingi, moja tu ilitosha kusambaratisha kioo na kufanya moshi ule wa sumu kuingia ndani.
Kwa mwendelezo zaidi , tembelea tovuti yetu ya fasihinet.com kuendelea , kipande cha 182 na 183 ni bure kabisa nenda na link;- SEHEMU YA 182
 
Amani iwe nawe mkuu, shukrani sana
 
Singano jr mi na elimu yangu ya menkwa hii Wala bado sijaelewa,Kwa hii simulizi ya shetani hamza nimeisoma hapa hapa jukwaani na nimeishia hiyo sehem ya 182,nataka unielimishe process ya malipo uko fasihinet,mfano nikilipa Elfu 2 nasoma episode ngapi?.
 
Alafu Kaka singano nauliza tofauti za hawa wataalamu Roma na Hamza ni nini?
Roma alikuwa mvuna nishati za mbingu n aardhi na kupanda levo kwa mapigo ya radi , Roma alikuwa ni mtu aliekuwa modified kisayansi mwili wake na kuwa na uwezo usio na kawaida , Roma alikuwa sehemu ya miungu ya kigiriki aka Hades mungu wa kuzimu , vibe kutoka dayari nyingine ...Zipo sifa nyingi tu ..

HAMZA
Hamza mwili wake haujafanyiwa modification , Hamza alianza mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi lakini baada ya kumuua Mr Black ambae ni Master wake alipoteza nishati za mbingu na ardhi na ndio alipoanza kujifunza mbinu nyingine kinyume cha nishati za mbingu na ardhi .Hamza anaamini Binadamu tumeumbwa kuitawala asili na sio asili kututawala , hivyo anaamini nishati ya mazingira binadamu anaweza kuitumia kwa nna anavyotaka kwa kufungua vifungo vya kimwili.Hamza ni mwanasayansi , Hamza amelelewa na The odd ones(Code) na The Holy (coded)...
 
Back
Top Bottom